Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Majuma 2 yaliyopita yalitawaliwa na mijadala ya ufisadi kutoka kwenye ripoti ya CAG kwa mwaka 2021/22. Sina haja ya kuingia ndani kuhusu ni nani wanahusika na ni fedha kiasi gani wamepiga.
Kwanza nawapongeza CAG na timu yake kwa kufanya kazi ILIYOTUKUKA. Inawezekana katika Taasisi za kujivunia nchini kwa sasa National Audit Office iliyo chini ya CAG ikawa ni ya pili kwa umahiri baada ya TPDF.
Ninachotaka kuwatahadharisha Watanzania wenzangu ni kwamba MSITEGEMEE makubwa yeyote kutoka hii TAASISI ya TAKUKURU kwa hao wanaotuhumiwa na CAG. Kwa kiasi kikubwa watuhumiwa wa ufisadi kwenye ropoti ya CAG ya 2021/22 watakwenda kugawana UFISADI na Maafisa wa TAKUKURU.
Wanaofikishwa Mahakamani na TAKUKURU ni wale wenye kesi za rushwa ndogo kama Mapolisi, Mahakimu, Manesi au Waalimu. Na hawa wanapokea kati Tsh 50,000 hadi Tsh 1,000,000.
Hawa wenye mabilioni wanagawana na maofisa TAKUKURU halafu ushahidi unavurugwa kwa kunyofoa nyaraka muhimu kwenye majalada au kupoteza jalada zima.
Kuna principle ya 'Quis custodiet ipsos custodes?' kwa Kiingereza who watches the watcher. Ni nani anayemchunguza TAKUKURU kwa Tanzania?
Ni wakati sasa Serikali kupitia Bunge likaweka chombo cha kuikagua TAKUKURU, kinyume cha hapo ni kutoitendea haki CAG na timu yake.
Au Serikali kupitia Bunge ibadili sheria ili CAG mwenyewe awafikishe Mahakamani watuhumiwa wake. Assuming kuwa anajengewa uwezo wa ku prosecute.
Tusijeshangaa hapo baadaye naye CAG akaacha kuripoti hizi kashafa kwa KUMALIZANA na watendaji huko huko, kwa kuwa kazi yake inaishia kuwatajirisha maafisa TAKUKURU.