Rita: Bora cheti kiandikwe baba mzazi hajulikani, kuliko jina lisilo asili

Kwenye suala hili RITA wapo sahihi kabisa.
 
Hii nimemkumbuka home boy...tulimbuluza shemeji yetu mahakamani kisa Mtoto kapewa baba mlezi..
Wakapelekwa kupima DNA...
Majibu DNA ilimkataa...
 
Kuna mtu huko ana kadi tatu za clinic majina tofauti na wala hajali, halafu unaweza kuta mwenye mimba ni msela ambaye hana time na hiyo mimba. Sometimes huwaga na jiuliza hivi wanawake huwaga wanawaza nini?
Baba hajulikani seriously?
Yaan mtoto anaitwa: Kimbembe Baba hajulikan? Hapa tumetatua tatizo au tunaongeza tatizo?
Hao wanalalamika watoto kupewa majina ya babu zao upande wa Mama kuna kitu walikosea.
Lakin Prof alishasema watz wengi ni social father and not biological father.....na sisi bodaboda tuna msemo wetu katika ndoa zenu kuna watoto wetu.
 
kwenye jamii zinazopenda sana watoto hii wala sio kesi.. nishiaona mara kibao usukumani kupewa u-bin wa babu mzaa mama
Kienyeji huko sawa kupeana majina hadi ya mababu sawa! Lakini unapokuja kuandikisha jina la mtoto Rita lazima unyooshe maelezo yako,hakuna ubabaifu,maana pale ndiyo tunasajili raia wa Tanzania, msije kutujazia mitoto ya ma foreigner kisa wanakimbilia kutumia majina ya kipewa tu!!
 
Hakuna Shida Yeyote Ile. Biblia Ipo Huru.
 
Fikra mgando hizo.. mzazi mmoja akiisha kuwa mbongo huyo ni raia as long hajazaliwa kwenye kambi ya wakimbizi.. akipewa ubin wa babu mzaa mama ni bora kuliko kumuita binadamu flan bin hajulikani
 
SAMAHANI Rita, ina maana huyu mwanamke mwenxangu ndani ya wiko moja ALIGAWA "papuu***" kwa mwanaume zaidi ya mmoja?
 
Maswali mazuri sana
 
Fikra mgando hizo.. mzazi mmoja akiisha kuwa mbongo huyo ni raia as long hajazaliwa kwenye kambi ya wakimbizi.. akipewa ubin wa babu mzaa mama ni bora kuliko kumuita binadamu flan bin hajulikani
Wwe ndiyo humjui baba wa mtoto, lakini Mama yake anamjua sana,sema tu kaamua kuwaficha nyie ndiyo maana anataka kutumia majina ya mababu zake badala ya majina ya baba yake halisi! Just for the record hata kama baba ni foreigner lazima tujuwe asili ya DNA zako,hata ukifanya jambo la ajabu tutasema huyu kwao ndiyo walivyo!!
 
Uislamu ushabainisha hili jambo mda mrefu tu kwa mfano mtoto wa nje ya ndoa ataitwa ubini wa mama ake

Mariam juma issa ni mzazi na mtoto ataitwa Abdallah mariam juma issa


Kwisha habari
Mkuu kwani Balozi Asha rose Mingiro ni jina la upande wa kike?
 
Kuna mtu huko ana kadi tatu za clinic majina tofauti na wala hajali, halafu unaweza kuta mwenye mimba ni msela ambaye hana time na hiyo mimba. Sometimes huwaga na jiuliza hivi wanawake huwaga wanawaza nini?
Wanawake wabawaza nani atamlea mtoto wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…