KERO RITA Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma hawajibu wananchi mitandaoni wala kusuluhisha changamoto zetu

KERO RITA Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma hawajibu wananchi mitandaoni wala kusuluhisha changamoto zetu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Taaisis ya Rita kitengo cha mtandao na Habari kinakabiliwa na tuhuma za kutojibu wateja wao mitandaoni hasa wale wanao omba usaidizi kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa sasa nchini Taasisi ambazo ziko chini ya serikali zimekuwa zikitoa huduma mbovu kwa wateja wake kwa kiasi ambacho kinakatisha tamaa kwa wateja wake

Kumekuwa na malalamiko mengi juu ya taasisi ya Rita tanzania kitengo chake cha habari na mawasiliano kushindwa kuhudumia wateja wake kwa wakati na kusababuisha usumbufu

Nilipewa ushahidi na ndugu yangu wa karibu alituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii ili kuomba usaidizi lakini hakujibiwa hadi leo na hakuna kitu chochote kimefanyika.alisema kuwa alikuwa anaulizia kuwa .kusaidiwa lakini hakupata mrejesho tangu atume hadi leo”

lakini ukitazama mda anatuma ujumbe admini alikuwa anamaliza kluweka chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii wa Instgram.

Pia nimejitahidi kufuatilia swala hili baada ya kwenda kwenye ukurasa rasmi wa rita tanzania na kugundua kuwa kumekuwa na watu wakichapisha malalamiko yao kwenye upande wa comment wakawa hawajibiwi jambo ambalo linatoa taswira mbaya kwa taasisi kama Rita hasa ususani kitendo cha habari na mawasiliano

Naomba RITA kupitia kitengo cha mawasilino kwa umma kuanza kuwajibu wateja wao kwani kufanya hivyo kutaweza wateja wao kupata huduma bora zaidi.

======

Soma pia:

1) DOKEZO - Mkurugenzi wa RITA shughulikia kero ya Huduma kuchelewa na majibu mabaya ya Maafisa wako

2) KERO - √ - RITA badilikeni, toeni majibu ya uhakiki wa vyeti kwa wakati
 
Back
Top Bottom