KERO RITA ni tatizo, wiki ya tatu sasa vyeti vya wanangu havijahakikiwa; nimelipa Tsh 12,000 kwa vyeti viwili lakini majibu sijapata

KERO RITA ni tatizo, wiki ya tatu sasa vyeti vya wanangu havijahakikiwa; nimelipa Tsh 12,000 kwa vyeti viwili lakini majibu sijapata

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Giltami

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Posts
1,038
Reaction score
1,623
Ndugu zangu,

Hii mamlaka ya RITA ni tatizo week ya tatu sasa vyeti vya wanangu havijahakikiwa nimelipa sh 12,000 kwa vyeti viwili tu lakini majibu cjapata na hawajitokezi kuelezea nini tatizo nakumbuka miaka mitatu nyuma tulihakiki vyeti kwa Tsh 2000.

Leo imefika 6000 lakini huduma zimekuwa tatizo hii nchi uwajibikaji ni mdogo sana kuna vijana wengi sana hawana kazi mnashindwa nini kuwapa kazi za muda wahakiki kama idadi ni kubwa?

Nawaambia makao makuu hatuta elewana mtamlipia mwanangu ada ya kusomea udaktari asipopata mkopo sababu yenu.

Soma majibu ya RITA; Madai ya kuchelewesha Vyeti, RITA yasema imepokea maombi 143,157, yaliyofanyiwa kazi ni 61.2%
 
RITA kuna Red Tape nyingi sana sijui kwanini Idara ya Matumbuzi haijasogea huko.
 
Wapo vijana wanaoweza kazi mkuu tatizo hata ukimuangalia mkurugenzi wa mamlaka unajua tu huyu kapitwa na wakati ifike mahali hizi ajira ziwe za mikataba kupima ufanisi wa watendaji.
 
Ndugu zangu,

Hii mamlaka ya RITA ni tatizo week ya tatu sasa vyeti vya wanangu havijahakikiwa nimelipa sh 12,000 kwa vyeti viwili tu lakini majibu cjapata na hawajitokezi kuelezea nini tatizo nakumbuka miaka mitatu nyuma tulihakiki vyeti kwa Tsh 2000.

Leo imefika 6000 lakini huduma zimekuwa tatizo hii nchi uwajibikaji ni mdogo sana kuna vijana wengi sana hawana kazi mnashindwa nini kuwapa kazi za muda wahakiki kama idadi ni kubwa?

Nawaambia makao makuu hatuta elewana mtamlipia mwanangu ada ya kusomea udaktari asipopata mkopo sababu yenu.
Poole ndo Bongo inatakiwa uewe mbele ya mda lasivyo tutalia Kila ciku
 
Ulipaswa utoe 12,000/= na 50,000/= ya walaji. Ungekipata siku hiyo hiyo.
 
Mimi nina mwezi sasa, ukienda instagram page yao ni malalamiko chungu nzima, number yao ya simu waliyotoa huwa haifanyi kazi. Tanzania kwa technologia bado saaaana!!!
 
Katika taasisi za serikali ambayo iko hovyo na hopeless basi ya kwanza ni hii.likurugenzi lake kwanza ni lizee sijui kwa nini halijastaafu mpaka leo,halina ubunifu wowote.
 
HIi ofisi ya kabidhi wasihi mkuu haijawahi kuwa bora. walitangaza kufanya application ya vyeti kwa mtandao, na watu tunalipa kwa mtandao, lakini hawafanyii kazi wakati pesa imeshachukuliwa. hivi kuna mtu alishawahi kupata cheti kwa njia hii kwa hawa watu?
 
Back
Top Bottom