Black star 2: Astra 20
Akaelekea katika nyumba iliyo karibu na karibu na kurudi akiwa na kifurushi mkononi.
"Amenambia ukifika wakati utafahamu kwanini amekuachia kitana tu kama sehemu ya urithi wako. hayo ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho" aliongee kizee huyo na kumkabidhi Rahee kile kifurushi.
Rahee akasogea lilipo kaburi hilo na kupiga magoti. Machozi yalikuwa yakimtoka. Fahad akawaacha wawili hao, yeye akaelekea alipo Gago na kupanda mgongoni.
"Fahad, hivi wewe ni kiumbe wa aina gani" aliuliza Gago.
"Kwanini unauliza wakati unaona kabisa mimi ni binadamu".
"Binadamu, utawadanganya wote lakini sio mimi Gago. Ulishaacha kuwa binadamu siku nyingi sana, uwezo wako halisi umeshavuka mipaka ya binadamu" aliongea ndege huyo.
"Sasa wewe unadhani mi ni nani"
"Hata sijui ila ipo siku nitajua tu ikiwa tutaendelea kuwa pamoja" aliongea Gago.
"Master tuondoke" alifika Rahee na kuongea
"Umeridhika?"
"Ndio japo nasikitika nimechelewa sana, ila ipo siku watalipa walionitenda hivi" alikuwa na hasira sana.
"Hiyo siku itafika lakini si ndani ya muda mfupi ujao"
"Haijalishi, ikiwa nitakuwa hai tu hata kama ni miaka elfu moja au mbili nitarudi kwa ajili ya kulipa kisasi" akiongea macho yake yalikuwa makavu na yenye kutoa hali ubaridi fulani hivi.
Fahad akatabasamu na kumpa ishara apande, wakaaga na ndege huyo akapotelea angani.
"Gago, unajua mlango wa kuelekea Sekai" aliongea Fahad.
"Una maanisha unataka kuvuka" aliuliza Gago kwa mshangao.
"Ndio, nataka kuelekea Sekai. Astra hapanifai tena kuendelea kufanya mafunzo yangu"
"Itakuwa safari ndefu na yenye hatari nyingi lakini, kwa kasi yangu na uwezo wako. Tutatumia angalau miezi mitatu kuvuka katika koridoo ya muda" aliongea.
"Si mbaya, twende" aliongea Fahad.
"Shikeni vizuri, nitaongeza kasi mpaka kupasua anga kisha tutaingia katika koridoo ya muda. Baada ya hapo nitasafiri kwa kasi ya radi mpaka tutakapofika" aaliongea Gago na kuanza kuongeaza kasi. Alipaa kuelekea juu zaidi.
Taratibu mwili wake ukaanza kutoa radi, kasi yake iliongezeka na kuwa kali sana. Fahad na Rahee ilibidi walale kabisa katika mgongo wa ndege huyo. Gago alipiga ukwenzi mkali sana, ghafla anga ikapasuka na kuwa kama mlango. Akaingia katika mlango huwo, ambao ndani ya kulikuwa na koridoo kubwa iliyokuwa na giza totoro.
Baada ya kuingia tu ni kama vile alikuwa hatembei kabisa, ni kama muda ulikuwa umesimama.
"Fahad tumia Qi kutengeza chumba kutuzungunguka" aliongea na Fahad nae akafanya hivyo. Gago akaongeza mpaka kufikia kasi ya radi. Mwili wake haukuonekana kabisa.
Baada ya miezi mitatu, Sekai.
Anga ikapasuka na Gago akatoka akiwa kasi kupita maelezo. Akaanza kupunguza kasi huku akishuka mpaka akakanyaga ardhi. Fahad na Rahee wakashuka na kukaa kitako. Gago akaanguka kabisa kutokana na uchovu, Fahad nae akafuata. Wote wawili walikuwa wamechoka sana, Rahee kwasababu hakuwa amefanya kazi yeyote alikuwa sawa.
"Fahad kuanzia hapa mutatembea kwa miguu, nahitaji angalau miezi minne ya kupumzika" aliongea Gago ma taratibu manyoya yakaanza kusambaratika. Ule mchoro mgongoni kwa Fahad ukakolea rangi.
"Unapumzika katika mwili wangu" aliongea Fahad.
"Ndio, sisi wanyama wa kiroho huwa tunapumzika katika miili ya kiumbe ambae tumeingia nae mkataba. Na pia nitatumia Qi yako wakati wote wa mapumziko" aliongea Gago.
"Pumzika, umefanya kazi kubwa sana" aliongea Fahad na sekunde chache sauti ya Gago ikapotea. "Ameshalala" alijisemea na kuegemea mti.
"Rahee nahitaji kupumzika kidogo" aliongea Fahad na wala hakusubiri jibu akapitiwa na usingizi.
Wiki moja baadae.
Fahad anaamka na kujinyoosha, "nimelala vizuri sana" alijisemea na kuangaza kulia na kushoto. Alishangaa kuona miti inatembea, "umeshaamka" aliongea Rahee aliekuwa mbele.
"Tuko wapi na nimelala kwa muda gani" aliulizs
"Tupo kwenye gari ya farasi, nimepata bahati. Kilikuwa kuna msafara unapita karibu yetu. Nimeomba msaada na wamekubali" aliongea Rahee.
"Hujanijibu nimelala kwa muda gani" aliuliza tena.
"Umelala kwa wiki moja nzima" aliongea Rahee.
"Anha, waulize kama wanapoelekea kuna chama cha wawindaji" aliongea. Rahee akawauliza wenyeweji na baada ya muda kidogo akamgeukia Fahad.
"Wamesema wanapoelekea hakipo ila mji unaofata baada ya hapo wamesema kipo" aliongea.
"Basi sawa", safari ikaendelea kwa ukimya na baada ya siku mbili wakawasili ambapo msafara huwo ulikuwa unaishia. Fahad na Rahee wakashuka na kushukuru kisha wakaaga na kuanza safari ya kuelekea huko kilipo chama cha wawindaji.
"Wamesema huwo mji unaitwaje" aliuliza Fahad.
"Zingi, ngome ndogo kusini mwa ngome hii" alijibu. Waliendelea na safari usiku na mchana, kuna wakati walilala porini. Hatimae baada ya siku kumi na tano wakawasili Zingi.
Getini kulikuwa na mstari mkubwa sana, "ukitaka kupita kupita onesha kibali chako" aliongea mlinzi mmoja. Fahad hakuwa na haraka, ilipofika zamu yake akatoa kibali chake.
"Cha kwako kiko wapi" aliulizwa Rahee.
"Huyu ni mwanafunzi wangu, sheria za chama zinaniruhusu kuwa na mwanafunzi mmoja ambae atakuwa anatumia kibali changu" aliongea Fahad kwa utaratibu. Yule mlinzi akajifanya kama hajasikia, Fahad akaongiza mkono mfukono na kutoa tael moja ya dhahabu. "Fanya kama hujamuona" akajifanya kama anamsalimia na kumkabidhi ile tael.
"Ohoo, unaweza kupita" aliongea mlinzi huyo baada ya kupokea rushwa hiyo kisha akageuka upande mwingine. "Ahsante" aliongea Fahad na kumgeukia Rahee akampa ishara amfuate. Wakaingia ndani ya mji huo na kulakiwa umati mkubwa wa watu uliokuwa umeshughulika na purukushani za hapa na pale.
Wakaulizia lilipo jengo la wawindaji, wakaelekea huko baada ya kupata maelezo. Walipoingia tu ndani ya jengo hilo wakakutana na macho makali ya wawindaji yakiwaangalia.
Wengi wao walionekana kuwadharau kutokana na mafazi yao kuchakaa. Wengi wa watu waliokuwemo humo walikuwa wanang'aa na mavazi ya kumeremeta.
Fahad wala hakujali, akaelekea mpaka mapokezi. "Sura yako ni ngeni hapa, sema kazi yako" aliongea mtu wa mapokezi.
"Nahitaji kuonana na kiongozi wa chama" aliongea Fahad.
"Kiongozi wetu hawezi kuonana tu na kila mtu" alijibu na kumuangalia Fahad kwa macho makali.
"Kijana kama huna kazi ondoka" alisikia sauti kutoka nyuma ikifuatiwa na kushikwa bega.
"Toa mkono wako mchafu katika bega langu" aliongea na kuushika mkono huo. Akaanza kutoa, yule bwana alieshika akajifanya ana nguvu sana. "Ukiendelea kuwa mbishi nitakuadhibu" aliongea yule bwana.
"Hivi ndivyo munavyokaribisha watu, bila kuulizia vibali vyao" aliongea akiendelea kuukaza mkono wake. Taratibu yule bwana akaanza kukunja ndita, alihisi mifupa yake ya kiganja ikivunjika.
"Kuna virugu la kazi gani" sauti nzito ilisikika ikitokea mlango uliokuwa mbele na eneo hilo.
"Huyu kijana amefika na kuanza kufanya vurugu" aliongea mtu wa mapokezi.
"Lakini bwana wangu sie alieanza" alijibu Rahee.
"Samahani naweza kuona kibali chako" aliongea aliefika. Fahad akaingiza mfukoni na kutoka kibali chake cha dhahabu. Akakiweka mezani, "damn, cha dhahabu" aliongea mtu wa mapokezi na kuanza kung'ata kucha.
"Pumbavu sana wewe, mara ngapi nakwambia kabla hujamhukumu, ulizia kibali kwanza" aliongea na kumgeukia Fahad. "Samahani huyu kijana bado mgeni, mimi naitwa Fang Shi na ni kiongozi wa tawi hili. Tunaweza kwenda kuongelea hili jambo ofisini" aliongea.