RIWAYA: Black star

RIWAYA: Black star

KARIBU KWA MAONI JUU YA RIWAYA HII. ILI NIPATE KUFAHAMIANA NANYI KWENYE JUKWAA HILI.

NIMETIMIZA SEHEMU YANGU KWENYE JUKWAA SASA FARASI KAFIKA SALAMA MWISHO WA SAFARI.

NASUBIRIA MWITIKIO WAKO ILI NIONE KAMA KITABU CHA PILI HADI CHA NNE KAMA MTAKIPOKEA.
MKIWA KIMYA NAMI NAKAA KIMYA. ITAKUWA HAMJANIELEWA KWENYE KITABU CHA KWANZA HIVYO CHA PILI HAMTONIELEWA KABISA.
Hii hapa
 
Black star 2: Astra 16







"Una mpango wa kufa na mimi?" Aliongea Hezoromo.



"Kufa na wewe! Nani kakwambia au kwasababu unaona Qi nyeusi ndio maana" alijibu Fahad.



"Hata kama hutaki kusema, najua kama unachoma damu kupata nguvu zaidi"



"Hapana hii sio damu inayounguwa, hizi ni hasira tu" alijibu na kujivuta akafyetuka kwa kasi na kumvaa Hezoromo. Hezoromo akamkwepa kurusha konde kali lililomkuta Fahad pasi na maandalizi. Akatupwa na kujigonga ukutani. "Koh, koh" akainuka na kukohoa kisha akatema funda kubwa la damu.



"Nikiendelea hivi hakuna uhakika wa kushinda, kweli niitumie saa hivi. Lakini bado hajaonesha kila kitu, nikiitumia na nikashindwa kumuwa kwa pigo moja basi itakula kwangu" alijisemea akojitahidi kudhibiti uwezo wake usicharuke.



"Hahahaha, aliesema ataniuwa anapambana na kifo kisichoepukika" Hezoromo aliongea na kumvaa Fahad. Fahad akamkwepa nankupuruzika, mikono yake ilikuwa kicheza huku na kule kuoangua mashambulizi makali sana.



"Hezoromo ikiwa hutaki kufa basi ni mida sahihi wa kutumia kila kitu ulichoficha" aliongea Fahad kama sehemu ya mtego wake. "Kwasababu mimi nimeshamaliza kupasha mwili, sasa nitakuonesha uwezo wangu halisi" aliendelea.



Mwili wake ukaanza kutetemeka, misuli yake ikatuna na kuwa kama iliopigwa msasa. Taratibu Qi yake nyeusi ikaanza kusafika na kuwa nyeupe kama chokaa na baada ya dakika chache ikabadilika na kuwa kama mvuke wa maji tu. Haikuwa na rangi yeyote ile.



"Kila msuli na mshipa wa fahamu katika mwili wangu unanambia nikimbie. Akili yangu yenyewe inanambia siwezi kushinda hapa, sina hata asilimia moja ya kushinda" alijisemea Hezoromo akihisi baridi ikatmbaa katika uti wake wa mgongo. Hali hiyo ikamfanya ashindwe hata kutembea, mwili uligoma kabisa kutoa ushirikiano.



Akang'ata ulimi kwa pembeni na kupeleka shoti ya maumivu katika kichwa chake. "Nilikuwa napanga kuishi kwa amani lakini naona hilo halitawezekana. Hatimae nimepata mtu wa kunitimizia ndoto yangu ya muda mrefu. Kabla hatujaendelea naweza kulifahamu jina lako" aliongea akiwa na tabasamu lenye kuonesha kiasi gani alikuwa amefurahi.



"Asura Fey, usijali njoo kwangu na kila kitu nitakuuwa bila huruma na kutimiza ndoto yako ya kifo" aliongea Fahad na kukunja ngumi, vidole vilivyokutana na kiganja sauti ya vyuma kugongana ilisikika.



"Una shukrani zangu" alijibu Hezoromo na Qi yake ikaongezeka kwa kasi. Mgongoni akachanika na kutoka mbawa kubwa lakini zilikuwa ni mifupa tu. Pembe zake zake zikaongezeka ukubwa na moto uliokuwa ukiwa katika ncha za pembe hizo ukabadilika na kuwa mweusi.



Mwili wake ukaongezeka ukubwa, makucha yale yakarefuka. Chini ya macho yake kukachanika na macho mengine yakatokea hapo.



"Grrrrr" akanguruma na kubonyea kidogo na kusababisha ardhi kuchimbika kabla ya kupotea. "Umeamuwa kuchoma maisha yako sio" aliongea Fahad na kuzunguka kwa kasi akivurumisha ngumi kali sana ya mkono wa kulia. Ni kama alijuwa wapi Hezoromo angetokea, ngumi hiyo ilivyokutana na sura ya Hezoromo ilitoa sauti mithili ya radi.



Ni kama vile muda ulisemama na ulipoanza kwenda tena Hezoromo alivurumishwa kilometa kadhaa kutoka alipotuwa.



"Ketouken" alinena neno hilo Fahad, nyota ndogo nyeusi ikatokea juu ya jicho la upande wa kushoto. "Naweza kuhimili hali hii kwa sekunde kumi tu" alijisemea na kurudisha mguu nyuma, akafanya kama anapiga hatua, akapotea akifuatiwa na mapande ya ardhi iliyopasuka baada ya kuondoka.



Hezoromo alinguruma tena kwa nguvu na kuchoma mbele. Wakakutana kati na Fahad katikati, kishindo kilichotokea baada ya wawili hao kukutana kilisababisha ardhi yote eneo hilo kupoteza muonekano wake.



"Muda wako umekwisha" aliongea Fahad na kuanza mashambulizi ya kasi. Hezeromo alishindwa kuyafata mashambulizi hayo kwa macho. Na kila shambulizi lilivyotuwa lilifuatiwa na upepo mkali sana.



"Ahsante Asura Fey, umetimiza ndoto yangu hatimae naweza kwenda kuonana na familia yangu. Kuwa makini na nguvu hiyo, itakuangusha nilipoangukia mimi" aliongea akiwa kakata tamaa kabisa.



"Nenda kwa amani na roho yake ikapumzike mahala inapostahiki" aliongea Fahad akivuta mkono wake wa kulia nyuma kwa ajili ya kuamliza kazi.



Ngumi hiyo kali ikatuwa kifuani, hakuishia hapo. Akaizungusha na kusababisha meridian zote pamoja na dantian katika mwili wa Hezoromo kupasuka. "Nakuachia zawadi, ipo siku itakusaidia" aliongea Hezoromo mwili wake ukirudi na kuwa wa binadamu kabisa. Akamgusa Fahad kifuani, "hata mimi nilikuwa binadamu pia" hiyo ikawa kauli yake ya mwisho kabla mwili wake kusambaratika.



Vita ambayo haikudumu hata kwa saa moja, iliacha kumbukumbu katika vifua vya watu. Fahad akapiga goti moja chini, damu ilikuwa ikimtoka. Ile nyota ndogo iliyotokea juu ya jicho la kushoto ikafutika. "Nahisi nimejiamini sana" alijiongelea huku taratibu nuru ya macho ikianza kupotea.



Master Lu na Master Jerome wakatuwa na kumchukuwa na kuondoka nae kwa kasi. Moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Master Lu. Wakakimbilia kule bustanini na kumkuta Yuna akiwa kapoteza fahamu.



"Niekeni pembeni yake" aliongea Fahad. Wakamshuha na kumketisha kama alivyosema.



"Ondoke kabla utakaso wa radi haujaanza" aliongea na wao wakatii. Sekunde chache baada ya kuodoka, bila hata kuwepo kwa mawingu radi zikaanza kupiga. Ya kwanza ilimpata Fahad na baada ya hapo zikaanza kupiga kwa kasi na wingi. Hali hiyo iliendelea kwa karibu saa tatu.



Fahad akasimama na kumbeba Yuna, akatoka nae na kumkabidhi kwa baba ake. "Nimekuandalia chumba cha kupumzika" aliongea Master Lu.



"Hizo radi zilizopiga ni kwa ajili ya Yuna, mimi nilikuwa pale kumsaidia. Mzigo wangu ndio kwanza unafika, sijui nitatumia muda gani lakini kwa kuzingatia sheria za asili nilizovunja itakuwa muda mrefu" aliongea na kurudi bustanini.



Kwa siku tatu mfululizo radi zimekuwa zikisikika katika bustani hiyo. Katika siku ya pili hakuna aliyelala katika nyumba hiyo, Fahad alikuwa akipiga kelele kila radi ilivyotuwa. Baada ya siku hizo tatu kukawa kimya, na baada ya wiki moja mlago ukafunguliwa. Master Lu alipofikishiwa tu habari akatoka na kukimbilia huko.



Ila alipofika akapigwa na butwaa kama aliyowakuta hapo. "Master ni wewe au" aliongea akijaribu kufikicha macho.



"Ndio kwani vipi" alijibu Fahad akiwa haelewi kwanini wati hap walikuwa wanashangaa. "Kaleteni kioo" alitoa amri master Lu. Mfanyakazi mmoja akakimbia na kurudi na kioo.



Master Lu akakichukuwa na kukiweka mbele ya Fahad. Macho yakamtoka, mwili wake ulikuwa umetanuka kupita maelezo. Ulikuwa umevimba kisawasawa na nywele zake ndefu kukaribia mabegani. Na weusi wake ulikuwa uking'aa, hilo halikumshtuwa sana.



Kilichomfanya ajishangae zaidi ni kuwa ndevu nyingi sana. Zilikuwa nyingi kiasi cha kuwa kama mzinga wa nyuki. "Ondokeni" alitoa amri Master Lu, wafanya kazi wote wakaondoka. Akamuongoza Fahad mpaka katika chumba alichomtayarishia na kumuacha huko.



Fahad akajilaza kitandani kwa nia ya kuondolewa lakini kutokana na uchovu kuwa mwingi. Usingizi mzito ukamchukuwa basi na yeye mwenyewe kufahamu.

 
Black star 2: Astra 17







"Nilijuwa hutakuja tena" alisikia sauti akifumbuwa macho, "master" aliita Fahad akijiweka sawa. Kama kawaida mbele yake kulikuwa na kimeza kidogo. Juu ya kimeza hicho kulikuwa na kikombe chenye ya iliyokuwa ikutoa mvuke.



"Inaonekana tayari umefanikiwa kuvunja sheria za mazingira" aliongea Karakantha akigeuka.



"Kivipi, mbona sielewi"



"Unajuwa kuwa kucheza martial arts kwa kuchanganya na Qi ni kinyume na sheria asili za mazingira. Kwa kufanya hivyo unasababisha hasira kwa mama asili. Na ndio maana kila mcheza martial art ni lazima apitie utakaso wa radi, utakaso huwo una lengo la kuuwa lakini ukifanikiwa kupita bila kifo utakuwa na uwezo mkubwa sana"



"Anha"



"Baada ya utakaso uliupata wewe, umefanikiwa kuvuka tena mipaka ya martial art. Umehama kutoka daraja la Sutra na kuingia daraja Dharma. Hivyo sasa utaweza kujifunza ukurasa wa pili wa Ngome ya chuma" aliongea Karakantha.



"Ila si tayari nimeusoma"



"Ndio umeusoma lakini hujauelewa" alijibu.



"Kwa hiyo kuna maana ya zaidi niliyoelewa mwanzo"



"Ndio na pia unatakiwa kuhama na kuelekea ulimwengu mwengine. DoQi ya Astra haitakuwa tena na msaada kwako".



"Nilikuwa nina mpango wa kuhama hata hivyo"



"Kufika daraja la dharma umeweza kufungia bahari ya taaluma. Hivyo uelewa wako katika martial art pamoja na matumizi ya Qi umeongezeka. Bahari ya taaluma ni kama maktaba yako, majibu yote itakayohitaji utayapata katika bahari yako ya taaluma. Kwasababu imeitwa bahari usije ukadhani itakuwa na maji, imeitwa hivyo kwasababu bahari ni miongoni mwa viti viwili ambavyo mpaka leo hakuna anaiijua vizuri".



"Nashukuru kwa msaada wako"



"Jingine ni kwamba mimi na wewe tutaonana tena tena ukifika daraja Qin"



"Kwani kuna madaraja mangapi baina ya Dharma na Qin"



"Yapo mengi ila makubwa ni mawili tu ambayo ni uzao na selestin"



"Nashukuru, mimi na wewe tutaonana tena pale wakati utakapofika".



******



Fahad akazinduka kutoka usingizini, akaangalia nje kupitia dirishani. Ulikuwa ni usiku mkubwa, akajizoazoa na kuelekea bafuni kwa ajili ya kufanya usafi wa mwili. Alipotoka tayari alishabadilika, ndevu nyingi zilizokuwepo kidevuni kwake hazikuwepo tena.



Nywele alikuwa kazifunga kwa juu na kutengeza kijimuinuko kidogo. Akakaa kitandani kwake na kufumba macho. Taratibu akijaribu kuelewa uwezo wake katika daraja la dharma unafanya kazi vipi. Asubuhi ikamkuta akiwa katika hali hiyo hiyo, mlango wake ukagongwa.



Akashuka kitandani na kwenda kufunguwa, "kaka mkubwa unaendeleaje" alikuwa Yuna. Alikuwa kabadilika kiasi baada ya kupitia utakaso wa radi.



"Mimi kama unavyoniona, niko vyema. Naona umefika darajanla sutra" aliongea na kutabasamu



"Yote haya ni kutokana na muongozo wako" alijibu na kuinamisha kichwa.



"Master Fahad habari ya asubuhi" sauti nzito ilisikika kutoka mbali kidogo, alikuwa ni Master Lu.



"Nzuri, ni matumaini yangu umepumzika vyema" alijibu.



"Wote tumepumzika vyema kwasababu ya msaada wako" alijibu na kucheka.



"Vipi Rahee anaendeleaje"



"Yule kijana ni mpambanaji sana, sema ndio hivyo hataweza tena kutumia Qi hivyo amepoteza uwezo wa kucheza Martial arts" alijibu na kuonekana akiwa na sonono.



"Master Lu katika huu ulimwengu kuna mengi ambayo hamyajui. Kuvunjika kwa dantian siyo mwisho wa kucheza Martial art, ikiwa tu meridian zake hazijaathirika basi ana uwezo wa kucheza Martial art ila tu itabidi aanze mwanzo" alifafanuwa.



"Kivipi?"



"Utaelewa lakini kwanza nahitaji unikusanyie watu wote ambao wako tayari kunifuata mimi. Sitamlazimisha mtu, nataka niwaachie zawadi kabla sijaondoka kuelekea ulimwengu wa juu zaidi"



Kauli hiyo ikawatia unyonge wote wawili lakini walijuwa tu kuwa siku hiyo itafika kutokana na uwezo wa mtu huyo. Master Lu akaondoka na kuelekea ofisini kwake, akaandika barua kadhaa na kuwapa vijana wake wazifikishe kwa wahusika.



Mchana kikundi kikubwa cha watu zaidi kumi kilikusanyika nyumbani kwa Master Lu.



"Nashukuru kwa kuitikia wito wangu japo ulikuwa ni wa muda mfupi. Ila si mimi niliwataka hapa leo bali ni master Fahad. Ana jambo anataka kuongea na nyinyi watu wema wa Astra" aliongea Master Lu na kumkaribisha Fahad.



"Nisizunguke sana, kama mtakuwa tayari nahitaji nyote muwe chini yangu" alianza kuongea Fahad na kuwafanya wengi kati yao wagune.



Akaendelea "kunifuata mimi kutakuwa na faida nyingi sana lakini hata usipoamua kunifata sitakulazimisha. Lakini kabla hamujafanya maamuzi nataka niwaambie kuwa katika myororo wa chakula basi watu wa Astra muko chini kabisa. Nikiwa na maana kuwa uwezo wenu ni mdogo sana. Ukiachilia Hezoromo ambae nimepambana nae kuna viumbe vina nguvu mara mia au elfu moja kuliko yeye" akanyamaza kidogo na kuwaangalia.



"Na hao wote macho yao yapo Astra, kwa miaka na miaka Astra mumekuwa shamba lao na ndio maana mnaona hata mukijitahidi vipi hamvuki daraja la Jin Dan. Wengi wenu hapa nikiwaangalia mnaonekana mumekwama katika daraja hilo kwa miaka mingi sana. Ni kwasababu, Qi unayoihifadhi ikifikia kiwango cha kuvunja mipaka husambaratika na kuwanufaisha hao".



"Kwasasa wamebakia nane na sijui lini wataamka, mimi sitakuwepo hapa kila siku kupigana vita yenu. Utafika muda mtahitajo mpambane wenyewe, na kwa uwezo ni kama ng'ombe tu munaosubiri kuchinjwa".



"Mimi nimeuona uwezo wako kwa macho yangu, hivyo nilikiwa nasubiri rasmi utangaze wale wanaopenda kukufata nami nifanye hivyo" aliongea Master Jerome na kusima. Akainamisha kichwa kama ishara ya heshima.



Waliobaki kuona hivyo nao wakasimama na kuinamisha vichwa. "Tumekubali kuwa chini yako, Master Fahad" kwa pamoja waliongea.



"Kwa muda wa mwezi mmoja, tutakuwa katika nyumba hii. Nitawaongoza mimi mwenyewe, na ndani ya muda wote mutafika daraja la Sutra. Na mtapitia utakaso wa radi, baada ya hapo nitawaacha na kuelekea kuelekea juu" aliongea na kukaa.



"Tukutane kesho asubuhi na kuingia katika utengo" aliongea Master Lu na wote wakatawanyika. Baada ya watu hao kuondoka Fahad akaomba apelekwe alipo Rahee kwa ajili ya kuongea nae.



Walimkuta akiwa amesimama anaangalia kupitia dirishani. Alionekana kunyongea sana, alikuwa ni mtoto ndani ya mwili asiyo uweza.



"Rahee unaendeleaje" aliongea Fahad na kumshtuwa.



"Samahani sikuwa nimekuona" aligeuka na kujibu akiinamisha kichwa. Matone kadhaa ya machozi yakadondoka sakafuni.



Fahad akawapa ishara wengine waondoke, alitaka kuongea nae kwa usiri.



"Najua unapata mateso sana, ndani ya muda mchache umepoteza kila kitu" aliongea Fahad na kusimama pembeni yake. Yeye ndie alieonekana mdogo mbele kipande hicho cha mtu pamoja na kuwa na mwili mkubwa na wa kutisha.



"Sijamuua kaka ako lakini hataweza kucheza karate tena"



"Mimi na yeye hatuna tofauti" aliongea Rahee.



"Hapana, ipo tofauti kubwa sana. Wewe ni mkarimu sana na kama hutojali ningependa uwe mwanafunzi wangu. Nitakuongoza kuwa na kuliko yeyote katika ulimwengu wa Astra".



"Inawezekanaje wakati dantian yangu kuu imevunjwa".



"Nifuate katika safari yangu, utakuwa mmoja kati ya majenerali kumi na wawili mtakaokuwa mnapokea amri kutoka kwangu tu"



"Una maanisha nini kusema hivyo" aliuliza Rahee akionekana kutoelewa jambo analoongea Fahad.

 
Black star 2: Astra 18





"Ninapotoka, mimi ni mfalme na katika ngome yangu hakuna matabaka. Hakuna manyanyaso, mkono wa sheria ndio unaomuongoza kila mtu sio kama huku kwamba mwenye nguvu ndio mwenye msemo" aliongea Fahad.



"Hakuna sehemu kama hiyo katika ulimwengu wa martial arts, inajulikana kwa mapana na marefu kuwa katika ulimwengu huu, mwenye nguvu tu ndie mwenye kauli" alibisha Rahee.



"Nilijua haitakuwa rahisi kukuaminisha, acha nikuoneshe ngome yangu" aliongea Fahad na kumshika begani.



Ghafla wakajikuta wapo katikati ya umati mkubwa wa watu. Kila mtu alikuwa makini na kazi yake, walionekana pia watu mbali mbali wenyewe uwezo mkubwa lakini walikuwa wakitembea kwa adabu.



"Usijali hawatuoni hawa" aliongea Fahad, sekunde chache wakawa mbele ya jengo kubwa.



"Hapa ndio nyumbani kwangu, huyo anaetoka ni binti yangu. Anaitwa Zayaan, wanyuma yake ni mke wangu anaitwa Eunice. Kama wametoka hivyo basi mfalme anakuja" alifafanua.



"Mfalme yupi tena wakati wewe ndo umenambia kama ni mfalme" aliuliza Rahee.



"Mimi ni mfalme niliekabidhi taji kwa mwanagu, anaitwa Minhe. Baada ya mimi huyo bwana mdogo ndie anaefuata kuwa na uwezo mkubwa zaidi" aliongea.



Minhe akafika na kushuka farasi wake, akatembea kwa haraka mpaka mbele ya Eunice na kupiga goti. "Mama nimerudi" aliongea.



Kabla Eunice hajajibu kitu akasita na kugeuka upande aliyo Fahad. "Si umesema hawatuoni" aliongea Rahee.



"Minhe, Zayan na Master Fu pigeni goti na muinamishie vichwa tumebarikiwa na uwepo wa dalili za Asura Fey" aliongea.



Wote watatu wakafanya hivyo na kwa pamoja wakaongea, "ubarikiwe mtawala, endelea kutuangalia watu wako huko ulipo. Japo sisi hatuhisi uwepo wako lakini hatuna shaka na neno la malkia".



Fahad akasogea mbele kidogo na kukutanisha mikono yake. Alipoiachanisha akakunja nguvu kwa nguvu na kusababisha ngurumo. "Mpaka tutakapoonana tena" aliongea.



Rahee akafungua macho akihema, "inawezekanaje binadamu kufanya hivyo" aliongea akirudi nyuma.



"Nifuate mimi utajua tu" aliongea Fahad na kutabasamu.



Rahee akapiga magoti chini na kutaka kusujudu, Fahad akamuwahi na kumuinuwa. "Kuanzia leo utakuwa mdogo wangu, na ndugu hawapigiani magoti" aliongea.



Michirizi ya machozi ikatengeneza njia katika mashavu yake. Kwa Rahee kuitwa ndugu ni kumuacha huru na kifungo cha muda mrefu sana.



"Kama hutojali unaweza kunieleza historia yako kwa ufupi tu" aliongea Fahad.



****************



"Kwanza mimi ni mtoto wa hawara wa baba yetu" alianza kuelezea Rahee. "Baba etu ni mfanya biashara mkubwa tu, na sehemu kubwa ya maisha yake huwa ni njiani katika miji tofauti tofauti. Huyu mzee ana mahawara wengi sana na hilo hutokana kuwa mbali kwa muda mrefu sana".



"Hapa umetuona wawili tu lakini mi najua tupo zaidi ya ishirini na ni kwa wanawake tofauti. Ila mwanamke aliemuoa ni mmoja tu na ndie mama wa Gahena. Hivyo basi Gahena ni mrithi halisi wa mali zake na anaetambulika kisheria. Mimi amenichukuwa kwasababu tu alipata utabiri kutoka kwa mtu kuwa mwili wangu akiulea vizuri unaweza kuja kuwa msaada mkubwa sana kwa Gahena kama mcheza martial arts".



"Ndio na najua utakuwa na maswali mengi sana lakini huna haja ya kuyauliza kwasababu utapata tu majibu yake. Kutokana na asili ya martiala art ambayo Gahena alikuwa anajifunza, mwili wake ungefika wakati na kushindwa kuhimili kishindo. Hapo lingefanyika tambiko ambalo lingehamisha roho yake kutoka kwenye mwili wake na kuingia katika wangu mimi".



"Kwa maana kuwa kipindi chote hichi wamekuwa wakinilea vizuri na kunipa matunzo ya hali ya juu kwasababu tu nilikuwa ni mfugo ninaesubiria kuchinjwa. Mi wala sikulijali hilo, kwasababu nilikuwa nikipenda Gahena kutoka moyoni na nilishajikubalisha kuwa ikiwa mwili wangu ungemfaa kuendelea na martial arts yake basi ningefanya hivyo bila kusita".



"Na ukweli ni kwamba zilikuwa zimebakia siku kidogo tu ili hilo litimie kabla ya yote haya kutokea. Lakini nina uhakika ugeni kutoka nyumbani utafika muda si mrefu kunichukuwa. Ni kweli umemtia ulemavu Gahena lakini ikiwa watafanya tambiko basi atarudi bila shida".



"Vipi kuhusu mamaako" aliuliza Fahad.



"Hata simkumbuko vizuri, inasemekana baba alimpa pesa nyingi sana ili kujivua ukaribu na mimi" alijibu.



"Unatamani kumuona"



"Nitamuonaje wakati hata sura yake siijui"



"Rahee kuna mambo huhitaji kukumbuka ili kuyajua, mama ako ndie aliekuleta ulimwenguni na ndie mtu wa kwanza kumuona baada ya kufumbuwa macho. Picha yake ipo sehemu katika akili yako, mimi naweza kuifanya na ukaiona" aliongea Fahad.



"Kweli?"



"Ndio lakini siwezi kukuahidi kama atakuwa hai ama laa, ila hata akiwa amekufa tunaouwezo wa kufika mpaka lilipo kaburi lake" aliongea.



"Kama inawezekana twende hata saa hivi".



"Usiwe na pupa, mimi na wewe tutaondoka baada ya mwezi mmoja. Kabla ya kuondoka kabisa Astra, tutamtafuta mama yako".



"Una maanisha nini kabla ya kuondoka kabisa Astra" aliuliza Rahee.



"Hivyo hivyo ulivyoelewa, kwa hali ilivyo sasa. Ulimwengu huu hauturuhusu kujifunza tunachokusudia. Hivyo tutaelekea ulimwengu wa juu zaidi. Lengo langu mimi ni mpaka kuvuka Yuggdrasil"



"Huko mimi sipajui lakini madhali nimeamua kukufata, nitaungana na wewe mpaka mwisho".



"Yugdrassil huwezi kufika, wewe zaidi utaishia Nirvana au Mythrill"



"Kadri unavyoongea ndivyo unavyozidi kunichanganya".



"Usijali, ukifika wakati utaelewa kila kitu", wakaendelea kuongea kwa muda mrefu kabla ya Fahad kuaga na kumuacha Rahee aendelee kupumzika.



Kama walivyokubaliana, siku ya pili mapema waliokubali kumfuta Fahad wa mafunzo. Hayakuwa rahisi hata kama walikuwa watu wazima.



Na kama alivyosema Rahee, baada ya wiki watu kutoka katika familia yao wakafika kumtaka arudi nyumbani lakini wakakumbana na Fahad. Wakaondoka wakiwa na majeruhi mengi basi na kupata mafanikio yoyote yale.



Hawakukoma lakino waliendelea kuja lakini jibu walilopata lilikuwa lile lile. Kipigo bila majibu, baada ya kipigo cha muda mrefu hatimae wakakoma kuja.



Fahad aliendelea kutoa mafunzo kwa matte hao wa Martial arts na ndani ya wiki ya tatu wakaanza utakaso wa radi.



Hatimae mwezi ulikatika kama upepo upitao, mlango wa bustanini ukafunguliwa. Wakatoka wakiwa wamechoka balaa, ila miili yao haikuwa kama walivyoongia.



Ni kama vile walirudi enzi zao za ujana, ya makunyanzi ya uzee yote yalitoweka. "Ahsante Master" waliongea kwa pamoja na kunamisha vichwa.



"Nataka kila mmoja wenu aanzishe shule ya Martial art na pia ziundwe sheria. Mfalme atachagua wenyewe, mimi siwezi kuingilia kati katika hilo. Kesho nitaondoka, nataka nikirudi nikute wanafunzi wa kutosha na wote wawe katika daraja la Sutra. nilivyowaeleza mnaweza kufika hata daraja la Dharma" aliongea.



"Tumesikia na tutatekeleza" waliitika kwa pamoja.



"Kaka mkubwa kama unaondoka na omba unichukue na mimi" aliongea Yuna baada ya kuwasili.



"Yuna kwasasa wewe ndie mwenye nguvu zaidi, nitakuwa na amani ikiwa nitaishi nikifahamu kuwa Astra imepata mlezi" aliongea Fahad.



Japo Yuna alitamani sana aunge safari lakini hakuwa na budi zaidi ya kukubali tu. "Mimi nikutakie safari njema, ikiwa hali itaruhusu tutaonana tena" aliongea na kunamisha kichwa kisha akaondoka.

 
Black star 2: Astra 19





"Natamani ungeendelea kuwepo lakini nafahamu fika kuwa huwezi kuendelea ukiwa huku" aliongea Master Jerome wakati akimuaga Fahad.



"Ni kweli ila nitarudi, japo sijui lini" alijibu na kumpa mkono. Master Jerome akaupokea na kutabasamu, alijitahidi kuficha machungu yake.



"Muna usafiri" aliuliza Raul.



"Hapana, ila tutafuta njiani"



"Kawaida huwa hakuna kiumbe ninaeshindwa kumuingiza katika himaya yangu lakini yupo mwewe mmoja wa ajabu sana katika msitu wa kusini. Ni mweusi na mwenye mkia mrefu sana. Huyu ndege ni mgumu sana na kitu kimoja nilichojifunza hakubali bwana ambae ni dhaifu kuliko yeye. Kwa maneno mengine, anataka kupigwa mpaka aitike amri na amtambue bwana wake" aliongea.



"Interesting!! Unaweza nipeleka" aliongea Fahad.



"Nitafurahi sana pia nitapata kuona pambano lako la mwisho" aliongea na kupiga mruzi. Mwewe mkubwa akatuwa.



"Master tunaweza kuja kushuhudia" aliuliza Master Lu.



"Fanyeni munavyojisikia japo sidhani kama litakuwa pambano kivile. Ndege hawezi nipa tabu mimi" alijigamba Fahad na kupanda mgongoni mwa ndege huyo. Baada ya sekunde kadhaa wakafika wanyama wengine ambao ni vipando vya wengine na safari ikaanza.



Walisafiri kwa muda mrefu kabla ya kuanza kuuona msiti husika. Baada ya muda kidogo yule mwewe wa Raul akapunguza mwendo na kuanza kuzunguka eneo moja, ni kama aliekuwa akihofia jambo.



"Samahani lakini hawezi kuendelea zaidi ya hapa, anatambuwa kuwa eneo la mbele yake lipo chini ya kiumbe ambae ana nguvu kuliko yeye" aliongea Raul.



"Hakuna shida" alijibu Fahad na kusimama, "nisubirini" aliongea na kujiachia. Japo alijiachia kutoka juu sana lakini alipotiwa hata kishindo hakikusikika. Umbali kama wa kilometa mbili hivi kulikuwa na mlima mkubwa. Alipopiga hatuwa moja tu kuelekea ulipo mlima huwo akahisi tumbo likimcheza.



"Huyu ni mwewe kweli au" alijisemea na kupiga moyo konde na kuendelea kutembea. Milango yake yote ya hisia ilikuwa ikipiga kelele. Akili yake ilimwambia akimbie, kila msuli na mshipa wa fahamu mwilini mwake ulikuwa ukipiga kelele.



Sehemu fulani katika kilele cha mlima, kunaonekana pango kubwa. Macho yanafunguka katika kiza cha pango hilo. Kiumbe wa ajabu akatoka na kujitikisa kabla ya kufunguwa mbawa zake kubwa. Manyoya yake meusi yalionekana kuakisi mwanga vilivyo.



"Binadamu umefata nini huku" ilisikika sauti kali sana, Fahad alikuwa amesimama mita kadhaa mbele ya ndege huyo mwenye kutisha.



"Unaweza kuongea, umeishi miaka mingapi. Eh ngoja nirekebishe swali langu, umeishi miaka elfu ngapi" aliongea Fahad.



"Ohooo!! Unanisikia" sauti iliskika tena.



"Vizuri tu lakini hujanijibu swali langu"



"Nipige mpaka nikutii ndipo nitakwambia umri wangu" aliongea ndege huyo na kufunguwa mbawa zake. Kwa kasi ya ajabu akapotelea angani. Kitendo hicho kilisababisha upepo mkali sana na kumtupa Fahad mbali kutoka aliposimama awali.



Akasimama na kujiweka sawa, miguu yake ikatengeza vishimo. Alijizatiti kama mwamba wa goli, ndege yule akaanza kushuka chini kwa kasi. Mdomo wake wenye ncha kubwa ulikuwa mbele shingo ikinyooka kama kichwa cha mshare.



Alipokaribia Fahad akaweka mikono mbele na kumdaka kisha akageuka kwa kasi na kumbamiza chini. Alitoa ukwenzi mkali sana, "sijakwambia kumbe, mimi sipigi nadhalilisha" aliongea Fahad na kumrukia usoni. Akamshika manyoya na kuanza kumtandika makofi. Kila kofi lilifuatiwa na upepo mkali sana uliyosambaa eneo lote hilo.



Ndege yule alipapatua sana lakini hakuchomoka mikononi mwa Fahad. Alaipofanikiwa kumuangalia usoni, Fahad alikuwa akitabasamu huku akishusha makofi. Wakati huwo alijuwa kuwa ameingia choo cha kike, Fahad alikuwa ni tafsiri ya neno ukatili.



Fahad akaacha kupiga na kumuangalia machoni, "vipi umeridhika au niendelee kukusulubu" aliongea na kuramba midomo yake ya chini.



"Imetosha, nimekutambua kama bwana wangu" aliongea akijaribu kuinuwa mbawa zake kama ishara ya kusalimu amri.



"Nakuachia ila ukithubutu kufanya chochote, leo usiku nitakula nyama ya ndege" aliongea na kumuangalia machoni. Ndege huyo alitambua hatari aliyokuwa anakabiliana nayo.



"Sitafanya kitu kama hicho, mimi nimekutambuwa kama mmiliki wangu. Jina langu ni Gago, na nimetoka katika kabila la phonix weusi. Mpaka sasa nimeishi miaka zaidi ya elfu tano" aliongea.



"Mimi naitwa Fahad" alijitambulisha.



"Kama unataka tunaweza kuingia mkataba"



"Itakuwa jambo zuri lakini mkataba wangu mimi hautwakuwa wa bwana na mtumwa. Nataka tuingia mkataba wa sawa sawa" aliongea Fahad.



"Wewe ni binadamu wa kwanza kutaka mkataba wa namna hiyo na mnyama wa kiroho kama mimi"



"Mimi naamini katika usawa" alijibu Fahad.



Yule ndege akamdonoa Fahad mkononi na kuchukuwa damu kidogo. Mchoro mkubwa wa ndege huyo ukatokea mgongoni mwa Fahad. Baada ya hapo Fahad akapanda mgongoni mwa ndege huyo. Akafunguwa mbawa zake na kuelekea angani kwa kasi sana.



Yote hato yalikuwa yakiendelea huku wengine wakishugudia kwa mbali. Master Jerome na wenzake walimeza mate na kushukuru hawakuwa na uadui na Fahad. Japo alionekana kuwa mpole lakini alizungukwa asili ya kuuwa.



Gago alisafiri kwa kasi kwa kufuata maelekezo ya Fahad mpaka walipo wengine. Akatoa ishara washuke chini wote, nao wakafanya hivyo.



"Natumai mutaishi vyema mpaka pale tutakapokutana tena" aliongea Fahad. Wote wakainamisha vichwa, akampa ishara Rahee apande juu ya Gago kisha akampa amri. Akapaa na kupotelea angani. Na huwo ndio ukawa mwisho kwa watu Astra kumuona Fahad.



"Kabla hatujaondoka niliahidi nitamtafuta mamaako" aliongea Fahad wakiwa angani. Kisha akamsogelea Rahee na kumshika sehemu ya paji la uso. Akafumba macho na kuanza kutafuta alama za mwanamke huyo katika kumbukumbu za Rahee.



Baada kama dakika akamuachia na kumuangalia usoni kwa huzuni. "Nini?" Aliuliza Rahee.



"Mama yako ameshafariki, ila nitakupeleka angalau ukalione kaburi lake" aliongea Fahad na kugeuka mbele. Akatoa maelekezo kwa Gago nae akabadilisha upande na kuelekea alipoelekezwa kwa kasi sana. Japo alikuwa akipaa kwa kasi lakini iliwachukuwa nusu siku mpaka kufika mahali alipolazwa mwanamke huyo.



Ndege yule akatuwa, Fahad na Rahee wakashuka kuelekea kuelekea lilipo kaburi. "Nyinyi ni akina nani" walisikia sauti yenye mikwaruzo. Ilikuwa ni bibi kizee, alionekana chumvi sana.



"Samahani mimi naitwa Rahee na nimekuja kumuona mama yangu" aliongea Rahee.



"Mjukuu wangu, ni wewe kweli" aliongea bibi huyo akimsogelea Rahee na kumgusa usoni. Michirizi ya machozi ikajichora katika mashavu ya bibi huyo.



"Ungewahi kidogo badi ungemkuta mama yako akiwa katika saa zake za mwisho" aliongea bibi huyo. "Kwani amefariki lini" aliuliza Rahee.



"Wiki moja nyuma, ila sio kufariki. Mama yako ameuwa kwa sumu, sijui huko ulikosana nini na baba yako. Ametuma wauwaji waje kuchukuwa uhai wa mama yako. Alipambana nao sana lakini walifanikiwa kumchoma sindano yenye sumu. Japo aliwawa lakini na yeye hakuwa na siku. nyingi za kuishi".



"Mpaka anakufa alikuwa anaamini kabisa ipo siku utakuja, hivyo ameacha kitana chake kama sehemu ya urithi wako" aliongea bibi huyo kwa majonzi.



 

Attachments

  • _19a2d3d6-8b5e-475b-a7f8-38ece6023221.jpeg
    _19a2d3d6-8b5e-475b-a7f8-38ece6023221.jpeg
    276 KB · Views: 16
Kuna kazi wengi hamjaipitia hii hapa



.
.
 
Black star 2: Astra 20





Akaelekea katika nyumba iliyo karibu na karibu na kurudi akiwa na kifurushi mkononi.



"Amenambia ukifika wakati utafahamu kwanini amekuachia kitana tu kama sehemu ya urithi wako. hayo ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho" aliongee kizee huyo na kumkabidhi Rahee kile kifurushi.



Rahee akasogea lilipo kaburi hilo na kupiga magoti. Machozi yalikuwa yakimtoka. Fahad akawaacha wawili hao, yeye akaelekea alipo Gago na kupanda mgongoni.



"Fahad, hivi wewe ni kiumbe wa aina gani" aliuliza Gago.



"Kwanini unauliza wakati unaona kabisa mimi ni binadamu".



"Binadamu, utawadanganya wote lakini sio mimi Gago. Ulishaacha kuwa binadamu siku nyingi sana, uwezo wako halisi umeshavuka mipaka ya binadamu" aliongea ndege huyo.



"Sasa wewe unadhani mi ni nani"



"Hata sijui ila ipo siku nitajua tu ikiwa tutaendelea kuwa pamoja" aliongea Gago.



"Master tuondoke" alifika Rahee na kuongea



"Umeridhika?"



"Ndio japo nasikitika nimechelewa sana, ila ipo siku watalipa walionitenda hivi" alikuwa na hasira sana.



"Hiyo siku itafika lakini si ndani ya muda mfupi ujao"



"Haijalishi, ikiwa nitakuwa hai tu hata kama ni miaka elfu moja au mbili nitarudi kwa ajili ya kulipa kisasi" akiongea macho yake yalikuwa makavu na yenye kutoa hali ubaridi fulani hivi.



Fahad akatabasamu na kumpa ishara apande, wakaaga na ndege huyo akapotelea angani.



"Gago, unajua mlango wa kuelekea Sekai" aliongea Fahad.



"Una maanisha unataka kuvuka" aliuliza Gago kwa mshangao.



"Ndio, nataka kuelekea Sekai. Astra hapanifai tena kuendelea kufanya mafunzo yangu"



"Itakuwa safari ndefu na yenye hatari nyingi lakini, kwa kasi yangu na uwezo wako. Tutatumia angalau miezi mitatu kuvuka katika koridoo ya muda" aliongea.



"Si mbaya, twende" aliongea Fahad.



"Shikeni vizuri, nitaongeza kasi mpaka kupasua anga kisha tutaingia katika koridoo ya muda. Baada ya hapo nitasafiri kwa kasi ya radi mpaka tutakapofika" aaliongea Gago na kuanza kuongeaza kasi. Alipaa kuelekea juu zaidi.



Taratibu mwili wake ukaanza kutoa radi, kasi yake iliongezeka na kuwa kali sana. Fahad na Rahee ilibidi walale kabisa katika mgongo wa ndege huyo. Gago alipiga ukwenzi mkali sana, ghafla anga ikapasuka na kuwa kama mlango. Akaingia katika mlango huwo, ambao ndani ya kulikuwa na koridoo kubwa iliyokuwa na giza totoro.



Baada ya kuingia tu ni kama vile alikuwa hatembei kabisa, ni kama muda ulikuwa umesimama.



"Fahad tumia Qi kutengeza chumba kutuzungunguka" aliongea na Fahad nae akafanya hivyo. Gago akaongeza mpaka kufikia kasi ya radi. Mwili wake haukuonekana kabisa.



Baada ya miezi mitatu, Sekai.



Anga ikapasuka na Gago akatoka akiwa kasi kupita maelezo. Akaanza kupunguza kasi huku akishuka mpaka akakanyaga ardhi. Fahad na Rahee wakashuka na kukaa kitako. Gago akaanguka kabisa kutokana na uchovu, Fahad nae akafuata. Wote wawili walikuwa wamechoka sana, Rahee kwasababu hakuwa amefanya kazi yeyote alikuwa sawa.



"Fahad kuanzia hapa mutatembea kwa miguu, nahitaji angalau miezi minne ya kupumzika" aliongea Gago ma taratibu manyoya yakaanza kusambaratika. Ule mchoro mgongoni kwa Fahad ukakolea rangi.



"Unapumzika katika mwili wangu" aliongea Fahad.



"Ndio, sisi wanyama wa kiroho huwa tunapumzika katika miili ya kiumbe ambae tumeingia nae mkataba. Na pia nitatumia Qi yako wakati wote wa mapumziko" aliongea Gago.



"Pumzika, umefanya kazi kubwa sana" aliongea Fahad na sekunde chache sauti ya Gago ikapotea. "Ameshalala" alijisemea na kuegemea mti.



"Rahee nahitaji kupumzika kidogo" aliongea Fahad na wala hakusubiri jibu akapitiwa na usingizi.



Wiki moja baadae.



Fahad anaamka na kujinyoosha, "nimelala vizuri sana" alijisemea na kuangaza kulia na kushoto. Alishangaa kuona miti inatembea, "umeshaamka" aliongea Rahee aliekuwa mbele.



"Tuko wapi na nimelala kwa muda gani" aliulizs



"Tupo kwenye gari ya farasi, nimepata bahati. Kilikuwa kuna msafara unapita karibu yetu. Nimeomba msaada na wamekubali" aliongea Rahee.



"Hujanijibu nimelala kwa muda gani" aliuliza tena.



"Umelala kwa wiki moja nzima" aliongea Rahee.



"Anha, waulize kama wanapoelekea kuna chama cha wawindaji" aliongea. Rahee akawauliza wenyeweji na baada ya muda kidogo akamgeukia Fahad.



"Wamesema wanapoelekea hakipo ila mji unaofata baada ya hapo wamesema kipo" aliongea.



"Basi sawa", safari ikaendelea kwa ukimya na baada ya siku mbili wakawasili ambapo msafara huwo ulikuwa unaishia. Fahad na Rahee wakashuka na kushukuru kisha wakaaga na kuanza safari ya kuelekea huko kilipo chama cha wawindaji.



"Wamesema huwo mji unaitwaje" aliuliza Fahad.



"Zingi, ngome ndogo kusini mwa ngome hii" alijibu. Waliendelea na safari usiku na mchana, kuna wakati walilala porini. Hatimae baada ya siku kumi na tano wakawasili Zingi.



Getini kulikuwa na mstari mkubwa sana, "ukitaka kupita kupita onesha kibali chako" aliongea mlinzi mmoja. Fahad hakuwa na haraka, ilipofika zamu yake akatoa kibali chake.



"Cha kwako kiko wapi" aliulizwa Rahee.



"Huyu ni mwanafunzi wangu, sheria za chama zinaniruhusu kuwa na mwanafunzi mmoja ambae atakuwa anatumia kibali changu" aliongea Fahad kwa utaratibu. Yule mlinzi akajifanya kama hajasikia, Fahad akaongiza mkono mfukono na kutoa tael moja ya dhahabu. "Fanya kama hujamuona" akajifanya kama anamsalimia na kumkabidhi ile tael.



"Ohoo, unaweza kupita" aliongea mlinzi huyo baada ya kupokea rushwa hiyo kisha akageuka upande mwingine. "Ahsante" aliongea Fahad na kumgeukia Rahee akampa ishara amfuate. Wakaingia ndani ya mji huo na kulakiwa umati mkubwa wa watu uliokuwa umeshughulika na purukushani za hapa na pale.



Wakaulizia lilipo jengo la wawindaji, wakaelekea huko baada ya kupata maelezo. Walipoingia tu ndani ya jengo hilo wakakutana na macho makali ya wawindaji yakiwaangalia.



Wengi wao walionekana kuwadharau kutokana na mafazi yao kuchakaa. Wengi wa watu waliokuwemo humo walikuwa wanang'aa na mavazi ya kumeremeta.



Fahad wala hakujali, akaelekea mpaka mapokezi. "Sura yako ni ngeni hapa, sema kazi yako" aliongea mtu wa mapokezi.



"Nahitaji kuonana na kiongozi wa chama" aliongea Fahad.



"Kiongozi wetu hawezi kuonana tu na kila mtu" alijibu na kumuangalia Fahad kwa macho makali.



"Kijana kama huna kazi ondoka" alisikia sauti kutoka nyuma ikifuatiwa na kushikwa bega.



"Toa mkono wako mchafu katika bega langu" aliongea na kuushika mkono huo. Akaanza kutoa, yule bwana alieshika akajifanya ana nguvu sana. "Ukiendelea kuwa mbishi nitakuadhibu" aliongea yule bwana.



"Hivi ndivyo munavyokaribisha watu, bila kuulizia vibali vyao" aliongea akiendelea kuukaza mkono wake. Taratibu yule bwana akaanza kukunja ndita, alihisi mifupa yake ya kiganja ikivunjika.



"Kuna virugu la kazi gani" sauti nzito ilisikika ikitokea mlango uliokuwa mbele na eneo hilo.



"Huyu kijana amefika na kuanza kufanya vurugu" aliongea mtu wa mapokezi.



"Lakini bwana wangu sie alieanza" alijibu Rahee.



"Samahani naweza kuona kibali chako" aliongea aliefika. Fahad akaingiza mfukoni na kutoka kibali chake cha dhahabu. Akakiweka mezani, "damn, cha dhahabu" aliongea mtu wa mapokezi na kuanza kung'ata kucha.



"Pumbavu sana wewe, mara ngapi nakwambia kabla hujamhukumu, ulizia kibali kwanza" aliongea na kumgeukia Fahad. "Samahani huyu kijana bado mgeni, mimi naitwa Fang Shi na ni kiongozi wa tawi hili. Tunaweza kwenda kuongelea hili jambo ofisini" aliongea.

 
Back
Top Bottom