Riwaya: Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia

Riwaya: Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia

Tuko pamoja mzee
RIWAYA; URITHI WA GAIDI

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA ISHIRINI


Kenge alibaki akimtizama yule bwana ambae alikuwa anachezesha shingo yake ambayo ilikuwa inatoa mlio kama mvunjiko wa kijiti kikavu.

Kenge alitazama vyema bastola ya jitu lile ikiwa imeenea vyema kwenye mikono yake. Kenge akapiga hesabu ni jinsi gani ataweza kuvuka maiti iliomiguuni mwake na kumfanyia shambulizi bwana yule ambae hakujua wepesi wake.

Kenge akajionya!

Akatabasamu kinyonge, hakuwa na namna.
Alitegemea jitu lile lipokee tabasamu lake kirafiki ila ndio kwanza alikutana na macho makali yaliokuwa mbali na mzaha.

"Fanya kile unachoelekezwa, tofauti na hapo unajitakia matatizo tu" Lilionya jitu lile.

Kenge akatikisa kichwa kukubaliana nae na hapo hakutaka kukaa mule, akavuka maiti ya J na kutaka kulipita jitu lile.

Kosa!

Kenge alijikuta akirudishwa nyuma kwa nguvu baada ya kupigwa kofi usoni lililoubganisha midomo na uso kiujumla.

Kenge alitoa mguno kama mbwa koko.

Kenge akagadhibika!

Kenge hajawahi kupenda dharau na akichukia huwa haoni ukubwa wa mtu ama uwezo wa mtu; Kenge aliona Katdharauliwa na jitu lile.

Akaachia ngumi nzito alioamini inaujazo wa kulitetemesha jitu lile lililokuwa limejaa kimazoezi.

Ngumi yake iliishia shingoni mwake na tofauti na matarajio yake, aliona jitu lile likichezesha tu shingo yake na kuweka bastola pembeni.

Ebanaee!!

Kenge alinywea gafla huku akijitahidi kujichekesha ili kutengeneza urafiki bandia.

Cheko lake halikusaidia!

Kenge alishikwa ukosi wa shati yake kisha akabebwa na kunyanyuliw juu kama karatasi na kutupwa kitandani ambapo alidunda mara moja na kuangukia chini.

Kenge alilia kama mbweha!

Kenge akataka kujizoa chini, ila hakufanikiwa alishikwa shati lake usawa wa mgongo kisha akanyanyuliwa tena na kutupwa kwenye kabati la nguo na kwenda nalo chini huku akisikia mvunjiko wa vioo vya kabati lile nae akitoa mguno kama mtoto anaeugulia maumivu ya bakora.

Jitu liliunguruma kwa gadhabu huku likimtizama anavyojinyanyua chini bila mafanikio.

Kenge alijitahidi kunyayuka na hatimae alifanikiwa na kukaa kitako.

Alilishuhudia jitu lile likienda kuokota bastola yake chini na kisha likamnyooshea huku uso ukiwa mbali na masihara.

Kenge aligwaya!

Jitu lile likaondoa kitunza usalama huku likianza kukenua meno kifurahia kifuatacho. Kenge hakuwa na namna zaidi ya kungojea hukumu, nguvu zake hazikuwa kitu mbele ya baunsa yule.

Mara likatokea tukio ambalo Kenge haelewi hadi leo hii lilitokeaje ila alikuja kushangaa jitu lile likijibwaga chini na kuacha bastola yake ikisambaratika chini huku ikitoa milio ya risasi bila mpangilio.
Na ndani hawakuwa wawili tena bali walikuwa ni watatu na watatu alivyoingia ndio ilimshangaza Kenge.

Alikuwa ni Sajenti Kobelo ambae alikuwa nje ya chumba kile akifuatilia kwa makini sauti za humo ndani.
Sajenti alikuwa nyuma ya msafara wa J Malao na Inspekta Kenge; na pia alifanikiwa kusogea hadi karibu na mlango na yote yaliotokea mle ndani aliyanasa vyema kabisa na sasa alikuwa ameingilia mpango wa jitu ambalo lilitaka kutoa uhai wa Inspekta kama lilivyotoa uhai wa mhariri J Malao.

Jitu lilishangaa kikumbo lilichopigwa na mtu mwenye mwili mdogo kuliko wake.

Hata!

Halijawahi kuangushwa na mwili mdogo, likajinyayua na kusimama kisha likaunguruma kwa gadhabu na kwenda kumvaa Kobelo.

Likaambulia patupu! Kobelo alikuwa mwepesi kubaini hila zake, akaepa na kusimama pembeni kisha akaruka mtindo safi wa kuambatanisha miguu yake na kulisukumia dhoruba ile lile baunsa ambapo alilipiga mbavuni.

Baunsa likaenda chini tena ila safari hii lilimwangukia Kenge na kuwa juu yake.
Kenge akaguna kwa maumivu na uzito wa baunsa lile ambalo wakati huo lilikuwa linajitikisa ili kujiinua.

Kenge akaona linamwelemea, akatumia mbinu ya kitoto kabisa, akalitekenya.
Baunsa likasimama kwa gadhabu ya kutekenywa likaachia kwenzi mujarabu ilioenda kutua utosini mwa Kenge na kumzubaisha kwa sekunde kadhaa.

Baunsa halikuwa na shida na Kenge; likajiinua tena kwa jaziba na kumwendea kwa pupa Kobelo.

Kobelo alielewa anapambana na jitu lenye nguvu, yeye alitumia akili tu ili awe bingwa wa pambano lile.

Akaruka hadi juu ya kitanda kisha akafanya kunesa kidogo na kwenda juu kisha akakunja goti na kushuka kulikabili baunsa lile.

Mbinu ilitiki.

Goti likatua kichwani mwa baunsa na kumsambaratisha chini kama kiroba cha mavi ya kuku, likabweka kama taahira.

Bahati mbaya bado ilikuwa kwa Kenge.

Baunsa alidondoka karibu na alipokuwa Kenge ambae alikuwa bado amezubaa na kwenzi ya baunsa.

Baunsa hakutaka kupigwa peke yake nae akamchapa kibao Kenge wote wakiwa chini; Kenge akarejewa na fahamu ila akakabiliana na maumivu ya shavu lake, akaachama ili upepo umwingie kinywani kumpunguzia maumivu.

Baunsa akaachana na Kenge akamvaa tena Kobelo; safari hii Kobelo hakupiga hesabu zake vyema akajikuta akijaa mikononi mwa baunsa kisha akapigwa kichwa matata pajini mwa uso wake na kuona nyota za rangi ya nyeusi.
Baunsa halikumwachia, likamnyanyua na kumtupia ukutani na kumwacha Kobelo akigugumia kwa maumivu ya dhoruba ile.

Baunsa akamfuata pale chini.

Kosa!

Kobelo kwa utalamu wa hali ya juu akaserereka kutoka alipo na kumvaa baunsa miguu mwake kisha akajiweka pembeni na kumwacha baunsa akienda chini kwa kupiga magoti na Kobelo akawa kama anainuka chini na kuacha mkono mmoja chini kisha akaachia mateke mawili kwa mpigo wa tofauti ya sekunde moja kila teke moja lilipotua shingoni mwa baunsa. Baunsa hakuwa na namna alienda tena chini kama zigo la karanga mbichi.

Bahati mbaya kwa Kenge; Baunsa akamwangukia kwenye mguu uliokuwa umejeruhiwa na vioo vya kabati..

Kenge akapiga ukunga kama bikira.

Hakuna aliemjali na Baunsa akataka kuinuka ila alichelewa alijikuta akijaa kwenye kabali ya miguu ya Kobelo ambae alimpiga kabali ya kumrukia huku amekunja miguu na alipotua alitua na shingo ya Baunsa na akapiga soti ya kubinuka, miguu ilibinuka na shingo la ulisikika mlio mmoja tu wa kuvunjika kwa kitu kikavu.

Baunsa alitikisika mara moja na kutulia.

Habari yake iliisha.

Kobelo akamfuata Kenge ambae alikuwa bado ameshika mguu kwa maumivu.

"Pole afande!!" Alisema Kobelo.

"Lakini sikukuita uje kunisaidia ujue" Alijitutumua Kenge kwa maumivu.

"Hata mimi najua, vipi umeumia" Aliuliza Kobelo.

"aah! Afande haumiagi ujue, afu ungechelewa kidogo ningemtoa nyongo huyu baunsa uchwara" Kenge alijitapa.

Kobelo alitabasamu tu na kutazama pembeni ambapo aliona mwili wa J ukiwa umelelala katikati ya dimbwi la damu.

Akaachana na Kenge ambae alikuwa anajitutumua kibwege.
Akaugeuza na kufanya kitendo cha haraka sana ambacho Kenge hakuona.

Alikwapua simu janja mfukoni mwa J na kuifutika mfukoni mwake na kuendelea kuipekuwa maiti taratibu.

"Wewe bwana mdogo acha kazi isiokuhusu, niache nimpekue mwenyewe, kesi hii ipo kwangu na sijui unaingilia kwa masilahi ya nani" Kenge alifoka.

Kobelo alijiinua taratibu bila kusema neno na kuanza kuondoka mle ndani.

"wee! tulia hapo hapo unamwachaje mkubwa wako akiwa kama hivi, ndivyo ulivyofunzwa chuoni?" Alifoka Kenge.

Kobelo alicheka tena na kumgeukia Kenge.

"Afande si useme unaogopa hilo jabali lililolala hapo? Usijali halitaamka fanya taritibu askari wengine waje hapa afande" Alisema Kobelo huku akilinyooshea kidole baunsa liliokuwa limelala bila uhai.

"Mh nani aogope, mimi au" Kenge Aliuliza kibwege tu.

Kobelo alitabasamu na kufungua mlango wa chumba na kutoka huku akiamini kabisa Kenge atadanganya watu ya kuwa yeye ndie alieliuwa lile baunsa.

Akapepea kuendelea na hamsini zake na huku nyuma Kenge akapiga simu kituoni kuomba msaada wa maaskari zaidi katika eneo lile.

*real is not real fake is not fake*
 
Kazi nzuri sana mkuu.
Huyu kenge kweli kenge haswa.
 
Kenge kala kichapo, halafu bado kiburi kwa bwana mdogo, Sajini Kobelo. Halafu mhusika Mkuu (Steering) yupo Jella bibie Remi aka mkimbizi.
 
Kudo ongeza speed mkuu tafadhali story kali sana sema speed eroo
 
Back
Top Bottom