Riwaya: Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia

Hiv huyu remi si ndiye yule mdada alietokea Rwanda akafikia nyegezi mwanza
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tuko pamoja kaka


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
RIWAYA; URITHI WA GAIDI

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA KUMI NA SITA



Mvamizi kwa kasi ya ajabu alitoa kitu mifukoni kwake na kupiga chini na kuzuka moshi mzito ambao ulimchanganya Kobelo na alichosikia ni sauti ya mgongano wa mtu na mlango na alioojaribu kufuata nyuma hakuna alichoambulia zaidi ya sauti za mgongano wa milango ya geti.

“ooh shit” alimaka Sajenti huku akirudi ndani na kuikwapua kompyuta kisha akatoka haraka eneo lile.

Kitu ambacho hakujua ni kuwa kompyuta ile ilienda kuzua utata.

Utata ambao ulizidi kuwa utata!!

***

Sajenti Kobelo alizidi kuona ugumu wa kazi ile hasa baada ya kupambana na mwanamke aliekuwa amejiziba uso wake kuanzia juu hadi chini.

“Alifuata nini nyumbani pale?” Alijiuliza bila kupata majibu na alizidi kuendesha gari kurejea nyumbani kwake.

“Kuna tatizo pahali kuhusu inshu hii” Alijisemea tena huku macho yake akiyatupa kwenye kompyuta mpakato iliokuwa kwenye kiti cha kushoto kwake.

Safari yake ilimfikisha nyumbani kwake na alishuka moja kwa moja alielekea ndani na kupitiliza hadi kwenye chumba kidogo kilichokuwa kimesheheni vifaa vingi vya mawasiliano.
Alikaa kwenye kiti kisha akachukua waya uliokuwa umeungwa kwenye umeme na kuchomeka kwenye kompyuta alioingia nayo mule ndani.

Akaiwasha na kuanza kupekuwa mafaili yaliokuwa yamehifadhiwa mule na hakuna la maana alilolipata.

Alipokuwa mbioni kukata tamaa akaona kwa chini kuna faili limeandikwa “REMI”

Akalifungua!!

Akakutana na maneno “inawezekana vipi?” kisha yakafuatia maneno mengine kwa chini “kwanini askari?” Alizidi kushuka na maneno mengine kadhaa ambayo yalikuwa na viulizo vingi.

Hatimae alifika kwenye ujumbe wa picha na kuufungua.

Video ile ilionesha gari likiwa linakimbia kwa kasi sana na ilivyoonesha picha zilizpigwa kutoka kwenye gari lililokuwa mbele na ilionekana ni mfukuzano uliokuwa baina ya gari zile.
Kuna kitu kilimshangaza kwenye gari ile iliokuwa nyuma ya gari la mbele.

Namba za gari!!

Namba alizoziona ni zile zile namba zilizokuwa kwenye gari aliloliona kule alikofia Sajini Vengu.

Aliguna!!

Kisha akachukua kalamu na kutaka kuandika ila akakumbuka karatasi alioichukua mfukoni mwa marehemu, akaitoa.

Alikutana na maneno yale yale ya viulizo na kisha kufuatiwa na namba za gari zilezile alizokuwa akizitazama kwenye picha mjongeo.

Video ilifika wakati ambao kuna tukio liliendelea ila kwa kuwa kamera ilikuwa inachukua kwa nyuma tu, hakuweza kuona ila alisikia purukushani kisha ikafuatiwa na mlipuko wa risasi na miguno na kisha akaona tena watu waliovalia sare za jeshi la polisi na kilichofuatia hapo ni video kuzima.

“ina maana polisi walihusika katika utekaji huu? Sasa kwa nini walitumia gari lenye namba sawa na za lile lililokuwa kwa Remi?”

Akaguna tena!!

Lakini kwanini Remi na Remi ni nani hasa?

Akajiuliza huku akihamia kwenye kompyuta kubwa iliokuwa mezani na kuiwasha kisha akawasha data na kuanza kuperuzi kuhusu Remi.

Alichokutana nacho ndicho kilichomshangaza.

Kweli Remi alikuwa ni mkimbizi ila alishatunukiwa uraia kwa ushujaa wake katika mkasa wa Congo sasa vije tena aitwe mkimbizi? Na vipi wale waliomtunuku nishani ya ushujaa wapo wapi wakati huu.

Aliguna tena na kisha akachukua kitabu chake na kurejea yale aliokuwa ameyaandika wakati alipokuwa anautazama mwili wa marehemu Vengu.

“Huyu binti hakuuwa bwana!!” Alijikatalia peke yake.

Hili tundu sio la mpigo wa bunduki ndogo” Alijisemea tena huku akiwa anazidi kupitia hiki na kile kuhakikisha anapata picha kamili ya tukio lilivyokuwa.

Bado nafsi yake ilimwambia Remi hawezi kuwa mhusika.

Akakumbuka kitu

Alikumbuka kachumbari ya jina la Remi.

Remi Haji Makame!

Akalitaja tena lile jina na kuliandika kwenye kompyuta na kufuta lile la Remi na kubaki Haji Makame.

Ex soldier? Alijiuliza baada ya kuona tovuti moja ikimtaja kama ni mwanajeshi zamani, lakini pia alitajwa kama aliwahi kuwa askari polisi wa cheo cha juu na hivi sasa hatambuliki baada ya kuwa anajihusisha na ugaidi na sasa anatafutwa na serikali ya marekani.

Mmh!! Inawezekana vipi hii! Alijiuliza tena.

Mambo yalizidi kumchanganya.

Haji tayari alikuwa ameshafutwa katika utumishi na alinasibishwa kama mtu hatari.

Hapo akawa amepata jibu ya kuwa Haji alikuwa ni mume wa Remi na walioana miaka kadhaa nyuma.


Alihitaji kumpata Remi.

Alichukua namba za simu zilizokuwa zimeandikwa kwenye vitabu vya Vengu na kuzipiga ila hazikuwa zikipatikana.

Alishusha pumzi nyingi na kuzishusha, hakujua aanzie wapi kudadavua jambo lile.

Wanataka nini kwa huyu mwanamke?

Alikumbuka kitu, akatoka na kuelekea kwenye gari lake na kuchukua gazeti lililokuwa limeandika habari za mauaji ya Vengu.

Alikuwa anatafuta mwandishi wa habari ile ila kama kawaida katika habari kama hizo huwa kunakuwa na neno “Na mwandishi wetu”

Alifyonza!!

Akapiga tena namba iliompigia kumpa taarifa ya mauaji ya Vengu; nayo haikupatikana.

Alirudi tena kwenye sifuri.

Akaigemea kiti na kushika kichwa huku akitizama kompyuta yake.

Hakupata jibu!!

Akainuka na kurejea tena kwenye kitabu chake, akarudia kusoma baadhi ya mambo alionukuu kutoka kwenye kablasha la Vengu kule kituoni.

Akasoma tena muda uliokisiwa kutumika katika utekaji na mauaji ofisini kwa Remi.

Akafikiria kwa zaidi ya dakika sita bila kupata cha kumuongoza katika sakata lile.

Mara akawaza jambo ambalo hakuwa na hakika nalo, akachukua simu yake na kutafuta namba fulani kisha akapiga.

“nambie kipanga!!” Sauti ya kike ilipokea kwa uchangamfu.

“Acha zako Habiba” Alisema kwa masihala Kobelo.

“Aah kipanga; vipi leo tena mmepigana na shoga angu?” Alihoji huku akicheka.

Yalikuwa ni masihala ya Habiba na Kobelo.

“aah umekariri tu, sikia leo naomba unisaidie jambo fulani hivi” Kobelo alisema.

Habiba aliguna kisha akasema
“Shida gani tena naweza kukusaidia mimi?” Alihoji Habiba kwa mshangao kidogo.

“Hivi inawezekana kupata mawasiliano ya mtu akiwa hayuko kwenye eneo alillopo wakati huo” Alisema Kobelo.

“Sijakwelewa kipanga”

“Ok yani namaanisha unaweza kujua mawasiliano ya simu katika eneo fulani hata kama akiwa ametoka kwenye hilo eneo?” Alifafanua Kobelo.

“eeh mbona rahisi tu” Alijibu Habiba.

“Sasa subiri kidogo nitakutaarifu kwa ujumbe mfupi sasa hivi unisaidie hiyo kazi”

“Sawa”

Kobelo akakata simu na kuanza kutafuta anuani ya ofisi za Remi na alipozipata akazituma kwa Habiba huku akiambatanisha na ujumbe mfupi wa maneno.

“Nitafutie mawasiliano yaliokuwa karibu na eneo hilo au ndani ya eneo hilo mida ya alfajiri”

Kama alijua kupokea jibu lile na kulifanyia kazi ni kazi nyepesi, alikosea sana Sajenti Kobelo.

**+
 
Bomba sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…