Riwaya: Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia

Riwaya: Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia

RIWAYA; URITHI WA GAIDI

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660


SEHEMU YA TISA




Remi alikuwa anatazamana na mwanamke waliepambana usiku ofisini kwake!!

Mwanamke yule akanyoosha vidole viwili kumwelekea Remi kisha akavipunga hewani mara mbili ishara ya mpigo wa bastola na kisha akavikunja vidole vyote na kubakiza kidole gumba kisha akakiinamishia chini ishara ya kuzika.

Remi aligwaya!!

Mwanamke yule akatoweka na Remi alishindwa hata kumfuata na punde tu kikasikika king’ora cha gari la polisi kikivuma kuelekea mitaa ile.

Moyo wa Remi ukapiga kite nguvu.
Macho yake akayageuza ulipo mwili wa Sajini.
Alijua ni nini kinafuata!

Remi hakutaka kuingia kwenye mikono ya dola kirahisi vile huku akiacha mengi yakiwa yana makandokando.

Haraka akaruka na kuingia ndani kwake na kama kichaa akaanza kupekua hovyo vitu vyake vya muhimu na alipopata alivyohitaji akavitia kwenye mkoba na kwa kutumia mlango wa stoo aliweza kutoka nje na kuacha askari polisi wakiingia ndani kwake kwa fujo na wasimuone bali walishuhudia mwili wa Sajini Vengu ukiwa umesambaratika chini bila uhai.

Askari polisi walifika na kuendelea na taratibu zao, ikiwemo kuchukua alama za vidole na kutathimini tukio kwa mazingira walioyakuta, kisha wakatafuta vitu kadhaa walivyodhani vinaweza kuwafikisha kwenye ushahidi wa kumtia hatiani mtu aliehusika na mauaji ya askari mwenzao.
Kikosi kizima cha maaskari kilikuwa kinaongozwa na Sajenti Kobelo wa kituo kikuu cha wilaya ya Kinondoni.

Sajenti Kobelo ndie aliepokea simu kwa mtu aliejitambulisha kuwa ni raia mwema na alimtaarifu kuna mauaji ya mtu kwenye nyumba ile ambayo wao wamo hadi wakati huo.

Sajenti Kobelo aliingia ndani mwa nyumba ile na kuanza kukagua kwa weledi wa hali ya juu sana bila kupuuzia kila alichokiona. Hatimae macho yake yaligota kwenye picha moja ya askari mmoja ambae alikuwa amechafuka vyeo kwenye mabega yake na moja kwa moja alijua kabisa nyumba ile ilikuwa inamilikiwa na afande yule.
Macho yake pia yalikutana na picha ya mwanamke mzuri mweusi ambae alikuwa na uzuri wa asili na ngozi ya kuvutia na pembeni ya mwanamke yule alikuwa amesimama bwana mmoja mrefu na sura lenye tabasamu na alipotizama vizuri aliona sura ya bwana yule ndio ililiokuwa kwenye picha ya yule askari mwenye vyeo vya kutisha.

Sajenti aliifuata picha ile na kuichukua kisha akaitazama kwa umakini sana na hapo alijiridhisha ya kuwa watu wale walikuwa ni mke na mume.
Akaitupa pembeni picha ile na ndipo alipoona maandishi kadhaa nyuma ya picha ile baada ya kuwa imeanguka kwa kujigeuza mbele nyuma.

“Showtime!!” maneno yalikuwa yameandikwa hivyo na chini ya maneno yale pia aliona maneno mengine yakiwa yameandikwa kwa herufi kubwa ila mwandiko ulionekana kuwa ni tofauti na ule aliouona katika maandishi ya mwanzo.

“MATHEMATICS”
Yalisomeka vile yale maandishi na kitu kimoja kilipita kichwani mwake; kwa nini iwe miandiko miwili kwenye picha moja na kwanini inaonekana kuwa kama ni majibizano fulani baina ya waandishi wale?

Hakukuwa na kumfafanulia,akasonya na kuendelea na ukaguzi wake.

Nyumba ile ni ya askari na kwanini askari mwingine auwawe kwenye nyumba hiyo hiyo!! Na kwanini hakuonekani kuwa na mmiliki wakati huo!

Sajenti Kobelo alichukua kitabu chake kidogo na kuandika andika mambo kadhaa kisha akarudisha mfukoni kitabu kile na kuanza kutazama upya sebule aliokuwamo!!

Kitu alichogundua ni kuwa kulikuwa kuna mtu mle ndani muda mfupi uliopita, na pia nyumba ile aliona imepekuliwa na mikono miwili zaidi na mkono mmoja alihisi ni mkono wa mtu mwenye haraka na mwingine ni mkono wenye kukagua kiweledi sana ni kama unaotafuta kitu cha muhimu sana.

Sajenti yule akaandika tena kwenye kitabu chake ambacho alikitoa tena mfukoni baada ya kuwa amekihifadhi.

Sajenti akatoka hadi nje na kukuta harakati kadhaa zikiwa zinaendelea na akarudi hadi kwenye maiti alioikuta pale.

Alieuwawa alikuwa ni ofisa aliemfahamu vizuri tu kwa kuwa waliwahi kuwa wote kituo kimoja kabla ya kusambaratika na kila mtu kupangiwa kazi kituo kingine.

Alimfahamu Sajini Vengu.

Akamfunua shuka jeupe alilokuwa amefunikwa na akatazama tundu lililoingiza risasi mwilini mwa Sajini Vengu.

Alilitizama tundu lile kwa dakika moja nzima kisha akatoa kitabu chake na kuandika kitu alichohisi kuona kwenye jeraha lile lililopelekea kifo cha Sajini.

Aliona risasi iliopenya pale ni kubwa na yenye nguvu na ndio maana iliacha tundu kubwa lakini haikutokea nyuma ya mgongo!

Kwa nini!

Kwa sababu silaha zote ndogo ili ziwe na nguvu ya kuacha tundu kubwa ni lazima bastola iwe karibu kabisa na eneo ilipopenya risasi na kisha huenda kufumua nyama za nyuma na kutokea nje hivyo kuacha jeraha kubwa nyuma kuliko mbele ilikoingilia.
Lakini risasi ile ambayo inaonekana ilipenya na kukwama baada ya kuwa imetoka umbali wa mita kadhaa na hivyo kupoteza nguvu baada ya kuwa imeingia kwenye nyama.

Alipata jibu kwa hesabu zake ndogo ya kuwa mpigaji hakuwa karibu na marehemu ila alikuwa mbali na mwili wa marehemu wakati akishambulia.
Pia risasi iliopenya haiwezi kuwa ya bastola hata kidogo.

Akanyanyuka na kitabu chake kisha akafunika mwili ule na kuwageukia askari waliokuwa nyuma yake.

Lakini tofauti na alivyotegemea kukuta askari wake pekee, alikutana pia na sura moja ngeni iliokuwa imejaa kwenye vazi safi la jeshi la polisi huku cheo chake kikijitanabaisha kuwa ni Inspekta na mkononi alikuwa na kablasha na pia kalamu nyeusi na usoni alikuwa amepachika miwani ya macho huku akiwa tabasamu la ajabu usoni, yani hakueleweka alikuwa atanataka kucheka ama kulia ama kupiga chafya!!

Inspekta yule hakuongea, alitoa simu mfukoni na kumpa Sajenti Kobelo.

Sajenti nae bila kuuliza akaipokea na kuiweka sikioni kisha kilichofuata ni kukunja sura huku akiitikia “ndio” na alipomaliza akamrejeshea Inspekta simu yake.

“Yah!! Ndo hivyo unapaswa kuniachia mimi kesi hii kuanzia sasa na wewe na watu wako mnapaswa kuondoka hapa haraka iwezekanavyo Sajenti.” Aliunguruma yule bwana.

“Sawa afande!!” alijibu Sajenti Kobelo na kuwapa ishara askari aliokuja nao, nao walianza kumfuata ili waondoke!!

“Aah; naitwa Inspekta Kibe Kengeleo kutoka makao makuu na wengi hupenda kuniita Kenge badala ya Kengeleo” Alijitambulisha Inspekta Kenge.

Sajenti alitoa tabasamu la pembeni na kuendelea na safari yake na askari wake.

**

Wakiwa kwenye gari wanarejea kituoni; Sajenti alitoa karatasi ndogo katikati ya kitabu chake kidogo na kuipitia.
Karatasi ile alikuwa ameichukua mfukoni mwa suruali aliokuwa amevaa marehemu Sajini Vengu.

Kitu kimoja alichobaini ni kuwa Sajini alikuwa amendika namba za gari lililokuwa karibu na pale alipokuwa amepigiwa risasi lakini pia alikutana na maneno yalioandikwa kama kiulizo.

“Askari wanahusika vipi na utekaji?” ilisomeka hivyo katika karatasi ile.

Askari; utekaji!!

Aliyarudia maswali yale na hapo ikaja akili ya kuwa Sajini alikufa akiwa yupo kwenye kesi aliyokuwa anafuatilia.
Lakini kwa nini namba za gari lililokuwa pale ndizo zilizoko kwenye karatasi aliokuwa nayo marehemu na inaonekana ziliandikwa kabla ya umauti haujamkuta.

Hata! Haiwezekani!!

Sajenti alijikuta anatamani kuendelea kufuatilia kesi ile licha ya kuwa alipokea amri ya mkuu wake ya kuwa asifuatilie kesi ile na kumwachia Inspekta Kibe Kengeleo au Kenge kama alivyopenda kuitwa.

“Kenge!!” alirudia kulitaja hilo jina Sajenti Kobelo.

Sajenti alijiapiza ya kuwa hatoweza kuacha kesi ile bali ataifuatilia kimya kimya na hapo alikumbuka kitu.

Yawezekana kuna kablasha ambazo alikuwa anahifadhi mwenendo wa kesi yake nahitaji kuupata!


Alijiwazia Sajenti kisha akamwabia dereva ampeleke kituo cha Mwinjuma alikokuwa anafanyia kazi Sajini Vengu.

Gari ilielekea huko!!

***

Remi baada ya kukimbia nyumbani kwake, alielekea kwenye nyumba nyingine iliokuwa inamilikiwa na mumewe mitaa ya Moroco. Na alikuwa amekaa ndani na kufunga milango yote huku akilia kwa uchungu.

Simu zote alikuwa amezima na hakuna simu ilioingia ama kutoka na alifanya vile ili kukwepa yeyote ambae angelikuwa anamfuatilia kwa njia ya mtandao.
Alifuta machozi yaliokuwa yanamminika kama maji kisha akanyuka na kwenda kuuchukua mkoba wake ambao ulikuwa na vitu vingi alivyochukua wakati akitoka nyumbani kwake!

Akavimwaga chini vile vitu vyote, na alichokitaka alikiona.

Mkasi!!

Alihitaji kupunguza nywele zake ambazo alihisi ni mzigo mwingine usiokuwa wa lazima.

Alijikuta akimaliza zaidi ya saa zima kuzikata nywele kwa sababu kila mara alikuwa anakaa na kulifikilia swala lake lile na pia jinsi alivyomuona Sajini Vengu akivuta pumzi zake za mwisho!

Kwani ilikuwa lazima afe? Remi alijiuliza taratibu huku akivuta nywele na kuzikata.
.
Alikufa kwa sababu aligundua jambo au kwa kuwa wanahitaji kuniweka kubaya zaidi?

Remi bado hakupata jibu sahihi!!

Alimaliza kuzikata na kuziacha vile alivyotaka ziwe na kisha akataka kuurudisha kwenye mkoba na hapo macho yake yakaangukia kwenye kadi ndogo ambayo alipewa na Naibu Kamishina P Kagoshima.

Ilikuwa ni miongoni mwa vitu vilivyokuwa vimesambaa pale chini.

Akaikota na kuchukua simu ndogo ambayo hakuwa akiitumia sana.

Akaingiza namba zilizokuwa kwenye kadi ile na kupiga.

Simu iliita na kupokelewa punde.

“Ni mimi Remi!!” alisema Remi punde tu baada ya simu yake kupokelewa.


Kagoshima aliguna!

“Uko wapi wewe!!” Alihoji Naibu Kamishina.

“Nipo kwenye matatizo makubwa tafadhali naomba msaada wako”
Alisema Remi.

N. Kamishina Kagoshima alicheka sana kisha akasema…

“Wewe si ulisema hutakuja kuhitaji msaada wangu?” alihoji Kagoshima.

Remi hakujibu kitu.

“Nimesikia taarifa zako na kwa hili inabidi ujisalimishe jeshi la polisi ili kuepuka mambo mengi ambayo hayana mana” Alisema Kagoshima.

“Ni ngumu sana kwa mimi kujisalimisha kituoni, sijui adui yangu hivyo siwezi” Alijitutumua Remi.

“Serikali haishindwi kukutia nguvuni ili ujibu tuhuma zako Remi. Anyway unataka msaada gani kutoka kwangu.” Alihoji Kagoshima.

“Nahitaji kuonana na wewe!”

“Sasa nitaonana vipi na mtuhumiwa wa matukio makubwa!”
Alisema Kagoshima.

Remi aliguna tu.

“Sawa!! Naomba tuonane Panda hotel chumba namba 10,ila itabidi wote tusaidiane” alisema Kagoshima.

“Nikusaidie nini upande wangu” Alihoji Remi huku fikira fulani zikipita kichwani mwake.

“Ni mapema sana kusema ila lazima ujue ili nikusaidie lazima ujitoe” alisisitiza Kagoshima.

Toba!!

Remi alishika midomo yake huku akisikia utulivu wa hali ya juu kutoka upande wa pili.
“Sawa!!” alijibu Remi na kukata simu.

Naibu Kamishina P Kagoshima alitabasamu tabasamu fulani la ushindi.

“Namkula na kumfunga!! Mtoto safi huyu” Alisema Kagoshima akiwa peke yake ofisini kwake.

Je Remi atakubali kuliwa ili asaidiwe? Na vipi picha alizopigwa zina kazi gani? Sajenti Kobelo je atatimiza adhima yake? Na vipi kuhusu Kenge?

Ungana nami jioni!!
 
Kudos najua umebnwa kwan hujawahi kuwa na tabia hii ya kututafuna kwa arosto
 
Hapo mwisho sijaelewa.. "NA VIPI PICHA ALIZOPIGWA ZINA KAZI GANI?"... Kwenye story sjaona sehemu alipopigwa picha remi au nimejichanganya!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kapigwa picha na yule mwanamke waliepambana nae kule ofisini kwake. Angalia episode iliyopita
Hapo mwisho sijaelewa.. "NA VIPI PICHA ALIZOPIGWA ZINA KAZI GANI?"... Kwenye story sjaona sehemu alipopigwa picha remi au nimejichanganya!


Sent from my iPhone using JamiiForums

Not strong will survival but remnants are strong
 
RIWAYA; URITHI WA GAIDI

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA KUMI



ma.

Remi aliguna tu.

“Sawa!! Naomba tuonane Panda hotel chumba namba 10,ila itabidi wote tusaidiane” alisema Kagoshima.

“Nikusaidie nini upande wangu” Alihoji Remi huku fikira fulani zikipita kichwani mwake.

“Ni mapema sana kusema ila lazima ujue ili nikusaidie lazima ujitoe” alisisitiza Kagoshima.

Toba!!

Remi alishika midomo yake huku akisikia utulivu wa hali ya juu kutoka upande wa pili.
“Sawa!!” alijibu Remi na kukata simu.

Naibu Kamishina P Kagoshima alitabasamu tabasamu fulani la ushindi.

“Namkula na kumfunga!! Mtoto safi huyu” Alisema Kagoshima akiwa peke yake ofisini kwake.

**

Mida ya saa mbili na nusu usiku ilimkuta Remi akiwa Pamba hotel na tayari alikuwa amekwishaingia ndani ya chumba namba kumi na alikuwa anatazamana na sura yenye ujivuni mwingi.

“Unakunywa wine?” alihoji Kagoshima.

“Hapana!” alijibu kwa mkato Remi.

Kagoshima alivuta funda moja la wine kisha akafinya midomo yake huku macho yake yakimtizama Remi.

“Ni kwamba hujawahi kunywa kabisa au ni leo tu” Alihoji tena Kagoshima.

“Sijawahi kunywa” Remi alijibu.

“Ooh sawa!! Na inakuwaje mrembo kama wewe unakosa kunywa lau hata tone la kileo?” Alihoji Kagoshima huku akigida tena funda la wine nzuri alioipenda.

Remi hakusema kitu.

“Mumeo Haji Makame hakika alifaidi sana kuwa na mwanamke mzuri kama wewe” Alisema tena Kagoshima.

“Afande nadhani tungelizungumza zaidi kilichotuleta hapa moja kwa moja” Alisema Remi huku akijitahidi kuzuia jaziba zilizoanza kumzonga kwa aina ya maongezi yale.

Kagoshima alitabasamu kifedhuli.

“Hata maongezi ya aina hii pia ndio yamenifanya nikubali kuonana na wewe japo wewe ni mtuhumiwa wangu” Alisema Kagoshima huku akitikisatikisa miguu yake aliokuwa ameibebanisha.

“Nadhani ulipaswa unisikilize shida yangu kisha utumie cheo chako kusimama katika haki na si uelekeo unaotaka tuelekee afande” Alisema tena Remi.

Kagoshima alicheka kwa sauti kisha akasema…
“Kwanza nikiwa mitaa hii huwa siruhusu kuitwa afande, na pia mwanadamu ni mwanadamu tu haijalishi ni yapi anakutana nayo ila hisia zinabaki kuwa pale pale” Alisema Kagoshima huku akiwa sasa ameifumbata mikono yake pamoja na kuikunja usawa wa kinywa chake.

“Kabla sijakwambia shida yangu naomba unambie unalenga nini” Alihoji Remi.

“Hakuna nacholenga zaidi ya mahusiano na wewe kisha nitajua namna ya kukusaidia” Alijibu Naibu Kamishina Kagoshima.

Remi alihisi mwili ukipitiwa na upepo baridi mithili ya pumzi za panya kwenye kidole cha mguu.

“Ila si wajua mi ni mke wa mtu?” Alihoji Remi.

“He is no more,hayupo tena na ni kama amekutelekeza tu huku akiwa amehamia na kuwa gaidi” Alisema kwa kebehi Kagoshima.

Remi alikunja ndita na kushusha pumzi ili kujaribu kuzuia gadhabu zilizoanza kumpanda.

“Lakini utawezaje kuwa na mahusiano na mkimbizi ambae habari zake zimetapakaa kote nchini ama ni vipi utakuwa na mtuhumiwa wa utekaji na mauaji?” Lilikuwa ni swali muhimu sana ambalo Remi aliuliza.

Kagoshima akacheka kisha akasema
“Lakini usasahu mi ni nani katika nchi hii”

“Sawa! Lakini usisahau ya kuwa cheo ni dhamana na nyakati hazidumu pia ila hatia ama tuhuma zinaishi milele na zaweza ibuliwa wakati wowote” Alisema Remi.

Kagoshima aliingiwa vyema na maneno yale nae akaamua kuhamisha mada.

“Anyway naomba unambie kilichofanya ukahitaji tukutane hapa”

“Nimegairi, kwa sababu ili unisaidie utanidai ngono” Remi alitamka wazi wazi mbele ya Kagoshima.

“Hapana,yote ni mapenzi yangu tu nilionayo kwako tangu siku ya kwanza niliokuona hivyo kuhusu tuhuma ni nje ya haya” Alijitetea Kagoshima.

Remi akasimama kwa lengo la kutoka ndani ya chumba kile, lakini kwa wepesi wa hali ya juu alijikuta akidakw mkono na mikono imara ya Kagoshima.

Vipi mrembo mbona unaenda tukiwa hatujamalizana” Alihoji Kagoshima.

“Kwani wataka tumalizaneje?” Alihoji huku akitetemeka.

“Aah kwani mi nimekwambiaje?”

“Lakini wajua utahukumiwa kwa kutaka kulala na mtuhumiwa?” Alihoji Remi.

Kagoshima akatoa macho kwa gadhabu na kumnasa kibao kikali Remi.

“Mimi sijawahi kataliwa wewe..iweje wewe unipe kebehi?” Alihoji kwa gadhabu Kagoshima.

Remi alijishika shavu lake lililokuwa linachonyota kwa ukali wa banzi alilopigwa.

“sasa naita maafande wakukamate”

Remi alinyoosha mikono na kumwambia..

“funga pingu, na unipeleke kituoni, matatizo yangu sio fursa kwa mafisi”

Kagoshima akaishia kumtazama Remi na asimmalize kwa ujasiri aliomuonesha.

Remi hakuwa mwanamke wa kutishika kwa vitisho vidogo; Remi tangu anakuwa hadi anafika hapo alipo ameshuhudia mengi kuliko hilo alilotaka kufanyiwa na Kagoshima.

Remi hakuteteleka kamwe. Remi alijali utu wake na kumvulia nguo Kagoshima ilikuwa ni kama kuutupa utu wake na kumdhalili mumewe.

Hata!! Hilo asingeweza kulifanya kamwe, huku akiwa hajui kama kukubali kudhalilishwa inaweza kuwa bado ni hasara, akachezewa na bado akaingizwa kwenye hatia!!.

Remi akaona bado afande amepigwa na butwaa,akavua mkoba wake na kuutupia kwenye sofa kisha akaanza kuvua T-shirt aliokuwa amevaa akaitupa pembeni na kubaki na braa kisha akaanza kufungua zipu ya suruali yake.

Dah!!

Kagoshima akabaki akiwa amebutwaika bila kujua lengo la Remi.

Kagoshima akamdaka mikono Remi wakati akianza kuishusha suruali yake.

“Sasa nini mana yake?” Alihoji Kagoshima.

“Nimekwambia wapigie wanikamate umeshindwa, sasa nataka nikuvulie nguo unifanye unavyotaka ili roho yako iridhike,shida yako si mwili wangu?” Alizungumza kwa jaziba Remi huku akifanya jitihada za kujinasua mikononi mwa Kagoshima.

“Ni kweli nakuhitaji ila unanishangaza kidogo kwa…”

“sio nakushangaza ila wewe ndie wanishangaza, hakuna haki inayopatikana kwa kuhongana mwili ndani ya Pamba hotel” alifoka Remi.

Kagoshima aligwaya na aliona amekosea mbinu, ikabidi awe mpole.

“Tafadhali naomba uvae nguo zako na uende” Alisema Kagoshima huku akirudi kukaa kwenye sofa lililokuwa mle ndani na kubaki akimtizama Remi akishugulika kuvaa nguo zake.

Remi alipokwisha kuvaa akadaka mkoba wake na kutoka nje.

Alipofika tu nje ya chumba akapumua kwa ahueni huku akitikisa kichwa kwa kushindwa kuamini kama kweli amejinasua mikononi mwa baradhuli yule anaetaka kutumia matatizo yake kujistarehesha.

“Kagoshima mtu mwenye tamaa nyingi sana” Alijisemea Remi huku akitokomea mbali na hotel ile.

Kagoshima nae alibaki akiwa amenuna na asiamini kilichomkuta kutoka kwa mwananke yule.

Akatoa tusi zito na kujitupa kitandani huku akimalizia kutuma ujumbe kwa kimada wake aende kumsindikizia usiku wake ulioharibiwa na Remi.

Usiku ukapita na ikaja ahsubuhi yenye mauzauza yake.

***
Ahsubuhi ilimkuta Sajenti Kobelo akiwa na gazeti mkononi mwake huku akiwa kwenye foleni akielekea mwananyamala.

Kurasa ya mbele ya gazeti lile ilikuwa imepambwa na picha kubwa ya Remi akiwa ameinama kutazama maiti iliokuwa chini huku kichwa cha habari kikisomeka “Balaa la mkimbizi laondoa uhai wa polisi” huku maneno ya pembeni yaliosindika picha zile yakisema “ni yule aliekwepa kulipa kodi na kuishi nchini kinyemela, aua askari aliefuatilia kesi yake…”

Sajenti akalikunjua kwa ndani na kuanza kusoma yaliondikwa kuhusu sakata lile.

Alipomaliza akarudi kutazama tena picha ile.

“Mbona hajaonekana kuwa na bastola au silaha yoyote? Lakini kama sie ni nani muuaji na aliepiga picha ni nani na alijuaje kuna mauaji tena ndani ya jumba lenye uzio?”

Akiwa anajiuliza hayo akapigiwa honi na gari lililokuwa nyuma yake kuashiria atembeze gari foleni inasogea!!

Kichwani mwake maswali yalikuwa ni mengi kuliko majibu.

Ahsubuhi ile radio mbali mbali zilikuwa zinatangaza vichwa vya habari vya magazeti mbali mbali huku ikionekana habari kubwa ni ya mauaji ya ofisa wa jeshi la polisi.

Remi pia ambae hakuwa na usiku mzuri pia alikuwa ameamka na habari zake zilizoonekana kutikisa ahsubuhi ile.

Remi aliishiwa nguvu na kubaki akiwa anachuruzikwa na machozi sambamba na kamasi.

Remi alijuta kuijua Tanzania; na bado hakujua kiini cha yale yote na nini hatima ya mchezo ule na kwanini alilengwa yeye.

Hakika alitatizika!.
 
Back
Top Bottom