RIWAYA; URITHI WA GAIDI
NA; BAHATI MWAMBA
SIMU; 0758573660
SEHEMU YA KUMI NA TATU
Akasimama huku akipiga hesabu za namna alivyokuwa amesimama mkwaruzaji.
“Aliposimama hapa, alitizama huku” Alisema Zedi huku macho yake yakielekea kule alikohisi msimamaji alisimama na kutazama.
Aliona!!
Macho yake yaliona mikwaruzo hafifu ukutani, akasogea na kuimulika kwa karibu zaidi.
“KEKERA” aliyanakili maneno yale kisha akaendelea kuchunguza ukutani pale na hatimae aliona tena maandishi mengine.
“Nü..Mďjust..fĺshai>”
Akayanakili tena maneno yale kisha akamstua Haji na wakapotea kwenye eneo lile na kurudi kwenye makazi yao ambayo yalikuwa katikati ya mji wa Mogadishu.
Saa moja badae iliwakuta wakiwa wametulia kwenye nyumba za viongozi wa serikali wakiwa ni kama walinzi wa viongozi wa ngazi za juu walioishi eneo lile ni hii ni baada ya kuhama kwenye hotel waliokuwa wakiishi tangu wafike Mogadishu. Makazi yao yalikuwa karibu na ubalozi wa Uturuki na hawakuwa mbali na Lido beach.
Waliweka mezani maneno walioyakuta kule kwenye gofu na yaliandikwa kwa code za kificho ili ambae atakutana nao na hahusiki basi asiweze kutambua kinachondelea.
Walianza na neno KEKERA.
Ndio ni kekera ila ila alimaanisha nini katika ujumbe huu” Alisema Haji huku akili yake ikizunguka kuhakikisha wanavunja code ile na kujua maana halisi ya ujumbe uliokusudiwa.
Zedi alikuna kichwa,hakujua ni nini sababu ila alijisikia tu kukuna kichwa.
Na kilichowachanganya ni kuwa ujumbe ulikuja kwa haraka sana tofauti na matarajio yao na hivyo kufanya kujua ya kuwa ujumbe ule ni wa muhimu sana.
Tatizo ni wa kuvunja fumbo.
Nywele ziliwasimama na ni lazima wafumbue ili wajue yaliomo.
Kazi ilikuwa ngumu hakika na muda ulizidi kusonga.
Ilipita zaidi ya nusu saa,hakuna mtu Kati yao aliekuwa ametongoa lau maana ya maneno yale.
Tunafanya nini sasa!? Zedi alimuuliza Haji.
Hebu tujaribu kudadavua hili neno la pili.
“Nü..Mďjust..fĺshai>”
Waliyapitia tena maneno yale kisha kwa pamoja walianza kukubaliana kitu kimojakimoja kilichoonekana kuwaletea maana.
Walianza na neno “físhai”
Walianza kulipindua pindua ili kuleta maana katika lugha inayoeleweka.
Hatimae jibu waIilipata.
“Bila shaka ukiliweka liwe jina la mtu intapendeza sana!!” Alisema Haji.
“Ok jaribu kulisuka liwe jina” Alisema Zedi huku sasa akiwa anatazama mikono ya Haji iliokuwa bize kuandika.
“Ona hii” Haji alimwonesha Zedi karatasi.
“Shafi’i” Zedi alilitamka lile jina.
“Yesi ni Shafi’I” alisisitiza Haji.
“Aisee!! Inaleta mana hii” alisema Zedi huku akitabasamu.
“Na kama ni jina basi hilo ni la kiislam na kama ndivyo,basi alitaka tujue kitu kuhusu huyu jamaa” Alisema Zedi.
“Na nionavyo huyu atakuwa ni Imamu na kama ni Imamu basi haya maandishia yaliosalia ni jina la Msikiti.
“Nü..Mďjust..
“Yes,hebu igeuze hiyo u iwe a kisha tukiivunja tuseme hilo ..Mďjust. alimaanisha Masjid na hii “Nü..” inamaanisha nuur kwa sababu hapo juu ya u kuna doti mbili ikimaanisha hizo ni u mbili hivyo basi tunaweza kuusoma kama “Masjid nuur” Alisema Haji.
Zedi alitabasamu kiushindi.
“Kwa hiyo anamaanisha tumtafute Imamu Shafi’I kwenye msikiti wa Masjid nuur” Alisema Zedi.
“Lakini tunamtafuta kwa uzuri ama ubaya” Alihoji Haji.
“Haiwezi kuwa uzuri mana hapa Somali tupo sisi tu katika hii suicide mission na hakuna mwingine, hivyo huyo ni mbaya” Zedi alitanabaisha hisia zake.
Walikubaliana katika hilo.
Wakarudi tena kwa neno “KEKERA”
“kwani kesho ni siku gani?” Aliuliza Haji
“Alhamis” Alijibu Zed.
“Rais wa Kenya anahutubia si ndio” alihoji tena Haji na Zedi akaitikia.
“Basi tuliweke hili neno kama Kesho kenya Rais” Alifafanua Haji.
Zedi akaruka juu na kupiga mluzi wa nguvu kisha akaachia bonge la mtusi kuashiria kuwa anakubaliana na wa mawazo ya Haji.
“Sasa nimeelewa alichomaanisha bwana, yani mbali na kumtafuta Imamu Shafi’I; inatakiwa pia tujue kesho kuna tukio lingine kwenye hotuba ya Rais wa Kenya hapa Somalia” Alisema Zedi.
“sasa ana maana gani” Alihoji Haji huku akijikuna kichwa.
“He need to rescue the president” Alisema Zedi.
“Yah hilo linaweza kuwa ndilo wazo lake, lakini sasa hajasema litatokea tukio gani nyakati hizo” Alionesha mashaka Haji.
“Hawa ni magaidi na magaidi siku zote huwa wana njia mbili za kutekeleza mashambulio yao. Kwanza ni kwa kutumia collar bomb, hapa ni kujitoa muhanga na njia ya pili ni kwa kutumia wadunguaji” Alisema Zedi.
“Sasa hapa watatumia njia gani?” Aliuliza Haji.
“Ndo kazi yetu kujua ila nadhani wanaweza kutumia mdunguaji kwa sababu kujitoa muhanga mazingira yatakuwa hayawaruhusu.
Haji aliguna huku akikaa karibu na kompyuta lengo alitaka kujua ni wapi hasa mkutano wa Rais wa Kenya utafanyikia.
Aliwasha data na kuanza kuperuzi habari zinazohusu ziara hiyo.
“Watakuwa katikati ya mji kwenye ukumbi wa hoteli ya Lamada.” Alisema Haji huku akiendelea kuchezesha vidole vyake.
“Pale ni rahisi sana shambulio kufanyika kwa sababu ya majengo yaliozunguka hotel ile” Alisema Zedi.
“Hapa tukimtafuta mdunguaji tutachelewa, ila inabidi tuweke taharuki dakika chache baada ya hotuba kuanza” Alishauri Haji.
“Hatuwezi jua nafasi gani wanatumia ili kutekeleza tukio lao,hivyo inabidi tujue tunavuruga vipi mkutano huo kabla haujaanza” Alisema Zedi.
“So!” Alihoji Zedi.
“Tupange fake bomb, lile litazua taharuki na viongozi wataondolewa kabla ya kufanyika tukio”
“ooh sawa kamanda” Alisema Haji huku akiinuka na kuchukua chupa ya soda iliokuwa mezani kisha akachukua shati lake na kuiviringisha juu yake na alipomaliza alichukua kinyundo kidogo ambacho hutembea nacho kwenye begi akaanza kuiponda.
Dakika kumi baadae ule unga alikuwa anaujaza kwenye chupa nyingine na kisha alichukua njiti za kiberiti nazo pia alizisaga na kumchanganya ndani ya chupa iliokuwa na unga wa chupa iliosagwa kisha akachukua wine nyekundu iliokuwa kwenye jokofu na kuimimina mle na alichukua pia kiasi kidogo cha soda ya pepsi na kuweka kisha alianza kutikisa kwa nguvu na ilipoleta fukuto akafunika na kizibo kwa juu kisha akagongelea ili kuziba vizuri.
“ewaa,sasa huo mlio wake, bomu la nyukilia likasome kibada dadeki” Haji alijigamba.
“Hongera komredi mana naona unakamilisha taharuki” zedi alisema huku akicheka na kukaa kitandani.
“Zedi; hatuna muda wa kupoteza, ngoja tumsake huyu Imamu na msikiti wake” Alisema Haji huku akirudi tena kwenye kompyuta na kuendelea kutafuta jina la Masjid nuur.
Ukapita ukimya kidogo.
“Huu msikiti upo karibu na Casapoplare road na kilomita moja nyuma pia kuna shule ya msingi ya Imamu Shafi’I” Alisema Haji huku vidole vyake vikifanya kazi ya kusonta kwenye kioo cha kompyuta ambapo kulikuwa kuna ramani ya eneo lile.
“Jamaa inaonekana yupo vizuri mfukoni” Alisema Zedi.
“Tutajua mbivu na mbichi akijaa kwenye kumi na nane zetu” Alisema Haji.
Waliendelea kusoma ramani ile ili wajue mazingira ya kumtafuta Imamu Shafi’I.
Usiku nao ulizidi kuwa mkubwa!.
***
Honda na kundi la wapiganaji walipokewa katika misitu ya Ganigani kulikokuwa na kambi yao kubwa. Misitu ile ilikuwa juu ya vilima vya Ganigani na asilimia kubwa mji wa Mogadishu ulionekana vyema kuanzia pale.
Eneo lile lilikuwa ni la kimkakati kwao kwa sababu ya za kiusalama.
Mahema mengi na vidungu vilitamalaki eneo kubwa sana la kambi ile.
Wapiganaji wengi walikuwa ni watoto chini ya miaka kumi na saba lakini kwa mazoezi makali waliokuwa wanapitia walionekana kuwa ni wakubwa kuliko umri wao.
Sozi alimvuta mkono Honda na kuelekea nae kwenye hema moja lililokuwa pembeni kidogo ya kimlima.
“Hii ndo nyumba yako, maisha yetu unayajua hivyo vumilia, siku za furaha zinakaribia” Alisema Sozi.
Honda alitabasamu.
“Kwani kule Saadan kulikuwa ni kwa nani na kwanini kambi isiwe kule?” Alihoji Honda
“Hata mimi sijui ile nyumba ni ya nani, na sijawahi kuona mmiliki wake,lakini pia haiwezi kuishi mjini na hakuna usalama kabisa kule” Alisema Sozi na kisha akagongesha mikono na Honda na kuondoka kwenye hema lile.
Honda alibaki peke yake,alizunguka kila pahali kukagua na alipohakikisha kila kitu kiko sawa akaelekea kwenye godoro la sufi lililokuwa limewekwa juu ya kichanja.
Akajaribu kulala, alikutana na vumbi kubwa sana likitimka.
Akaguna.
Akalitoa godoro lile na kulipigapiga ili kupunguza vumbi.
Isa nae akaingia!!
“Inabidi uzoee na ndio maisha yetu yalivyo” Alisema Isa.
Honda hakujibu!
“Sasa hapa kuna jukumu kubwa la kufanya kesho na jukumu lenyewe ni kumwondoa mtu anaetusumbua hapa Somali ikiwa na yeye ana nchi yake, Kesho atakuwa hotel Lamada na vijana watu wameshafanya ukaguzi wa kutosha na hali ya ulinzi ni kubwa sana hivyo tumeona bora tutumie wadunguaji ambao watakaa jengo hili na hili” Alisema Isa huku akimwonesha Honda ramani aliokuwa ameshikilia mkononi.
“Vipi una uhakika una wadunguaji makini?” Alihoji Honda.
“Ninao vijana sita ni hodari sana kwa kazi hiyo” Isa alijibu.
“Good!!” Aliitikia Honda.
Isa aliondoka kwenye hema lile ili kumwacha Honda apumzike mana usiku ulikolea na mvua ilianza kunyesha.
Honda alipobaki peke yake, alitoa ile risasi alioikuta kwenye furushi la risasi zingine.
Akaifungua kichungi chake na ndani alikutana na kidude kidogo mithili ya kadi ya simu ila kilikuwa kinavibonyezeo kama viwili hivi na pia kulikuwa kuna kikaratasi chembamba kilichokuwa na maneno machache ya kiingereza.
“Press when you meet flamingo” Alijua ni kwanini alipewa kidubwasha kile kwa njia ile.
Alitafuna kikaratasi kile kisha akachukua kikasha cha risasi na kukifunga na kurudisha mfukoni huku kidubwasha kile akikipachika ndani ya nywele zake ndefu alizokuwa amezikata mtindo wa afro.
Kitu ambacho hakujua ni kuwa wakati analazimisha kikae sawia kwenye nywele alikibonyeza bahati mbaya na kilianza kusoma mawimbi.
Sozi alikuwa amelala na Isa pia alikuwa amelala.
Ila kuna mtu hema fulani hakuwa amelala na ni mwiko kwake kulala.
Mtu huyu alikuwa ni mtaalamu wa mawasiliano na kazi yake alihakikisha ananasa mawimbi ya radio yoyote ambayo ingelikuwa inasogelea kambi yao kwa sababu makomando ili wavamie ni lazima wawe na vifaa vya mawasiliano na pia alikuwa ndie anaeunganisha mawasiliano yote ya kambi nzima na watu waliokuwa nje ya kambi ambao ni viongozi wao.
Kifaa kimoja kilianza kukoroma kuashiria kuna muunganiko wa mawimbi rasimi na yasio rasimi.
Bwana yule akakifuatilia kifaa kile nacho kiliendelea kukoroma na kila alipojaribu kufuatilia mwelekeo wa mawimbi alipata ugumu kwa sababu ya mvua kubwa ya radi na miungurumo iliathiri utendaji wa kifaa kile.
Aligwaya!!
Ilimaanisha kufeli kwake ni kuangamiza kambi nzima.
Akavaa nguo za kuzuia mvua, akachukua kurunzi na kisu kisha akanyofoa kifaa kile na kutoka nje huku taratibu akiendelea kufuatilia mawimbi yale.
Honda alikuwa amelala chali huku mawazo lukuki yakipita kichwani kwake na utulivu wa mwili kwake ilikuwa ni afueni ili achanganue mambo.
Baada ya dakika nyingi za kuwaza hili na lile, taratibu usingizi ukaanza kujenga kibanda kichwani pake.
Mara muungurumo mkubwa wa radi ukarindima.
Usingizi ulikata.
Lakini akili yake ilimwambia kuna kitu cha ziada amekisikia wakati wa ngurumo ile.
Akatega sikio vyema.
Wakati wa mtiririko wa mvua “tatatatata……!” kuna sauti nyingine aliisikia katikati ya mtiririko ule.
Akatega tena!!
“tatatata.. ti..tatatata..ti..”
Ile ti,ilimwashia kengele ya tahadhari.
“hakuna mlinzi anaeweza kutembea katikati ya mvua kubwa hii” Alijisemea!!
Ndipo alipoamka na pia akahisi kitu kikiwaka na kuzima kichwani kwake.
Akakitoa kifaa kile na kukibonyeza kikaacha kumweka.
“tatatata…ti….tatatata..ti..”
Bado aliendelea kusikia sauti ile na sasa ilizidi kukaribia kwenye hema lake.
Roho ikamdunda!!
****
ITAENDELEA KESHO JIONI.