Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,821
- 6,119
- Thread starter
- #41
RIWAYA; UKURASA WA GAIDI
NA;BAHATI MWAMBA.
SIMU; 0758573660.
SEHEMU YA SITA
Umakini uliongezeka usoni mwa Sajini.
“Taarifa zinasema mumeo hajaonekana zaidi ya miaka miwili, sasa yeye alikuwaje akamtafuta na anajua kabisa mumeo hayupo?” aAlisema Sajini Vengu.
“Sijui kama hawakuwa na mawasiliano kati yao katika miaka hiyo miwili na…” Remi hakumalizia kauli yake Sajini akamkatisha.
“Remi; mumeo tumeambiwa ni gaidi na haonekani sasa iweje Davis aseme hapatikani, hivyo unajua mumeo alipo sio?” Alihoji Sajini Vengu.
“Sijasema aliulizia mume wangu, bali nimesema pengine ndie alimaanisha afande” alisema Remi.
“Watch yo step madame!!” Alitahadharisha Sajini.
Remi akagwaya!!
Baada ya mazungumzo ya dakika kadhaa, Remi aliaga na kuondoka huku akimwacha Sajini akiwa amepata jambo jipya kuhusu mume wa Remi.
Remi alipanda gari lake na lengo lake alitaka arudi tena kule ofisini kwake, alitaka kufanya jambo ambalo alijua anaweza kubahatisha kulipata!
“Walioyafanya pale ofisini sina hakika kama kweli hawajaacha kosa moja, Hakuna mkamilifu” alisema Remi huku akiipita hospital ya mwananyamala, alikuwa anaelekea Mwenge zilipo ofisi zake. Hakutaka kuendelea kuhujumiwa, alitaka kukokotoa hesabu katikati ya hujuma na mitego.
Kitu kimoja hakujua madhara ya kile alichotaka kwenda kukifanya na kama angejua basi bora angeacha tu aendelee kushuhudia showtime alioahidiwa na bwana kitambi…
Hakika hakujua madhara yake kwa alichokusudia.
***
Jua lilikuwa linaelekea kuiachia dunia kiza; lilielekea magharibi.
Remi aliegesha gari lake pembeni kidogo mwa ofisi zake za utafiti wa mambo ya kale.
Eneo la ofisi zake lilikuwa lipo kimya na utepe wa njano ulikuwa umewekwa kwenye geti la kuingilia ndani ya ofisi zile.
Alitazama kushoto na kulia, kisha akaita kama kubahatisha tu ili ajue kama kuna askari atakuwa eneo lile.
Kukawa kimya!!
Akapiga hatua za mnato huku akiwa makini sana ili asije kuvuta jicho la mtu yeyote ambae alikuwa mitaa ile kufuatilia yeyote ambae angelifika pale nyakati zile.
Hakuona wala kuhisi jambo hilo eneo lile.
Akachukua funguo zake na kutia kwenye kitasa cha geti na likafunguka.
Akaingia!!
Akaelekea lilipokuwa gari la mwandishi Davis Minja lililokuwa limetelekezwa kabla haijafika kwenye maegesho.
Taa zilikuwa zimezimwa na eneo lote lilikuwa giza na kumezwa ukimya wa kifo.
Remi alitoa kurunzi ndogo kwenye mkoba aliokuwa ameubeba na kuanza kulitazama gari lile ambalo lilionekana kubondeka sehemu moja chini kidogo ya mlango wa kutokea dereva.
Remi aliinama na kugusa eneo lile na alichogundua ni kuwa mmbondeko ule ni wa chuma kilichobamiza pale kwa nguvu.
Zilifanyika harakati za la lazima kumchukua mwandishi yule.
Alisimama na kwa taratibu kabisa alianza kulizunguka gari lile ambalo hadi wakati huo lilionekana kupitia dhoruba kadhaa wakati likiwa njiani.
Remi hakuona cha maana zaidi katika lile gari,akaachana nalo.
Akaelekea mlango wa kuingilia ofisini kwake, akafungua na kuingia ndani taratibu huku akiangaza huku na huko.
Macho yake yakanasa mvurugano wa makablasha.
Kulipekuliwa!!
Saa ngapi na kwanini, hakujua!!
Akazidi kuona namna upekuzi ulivyofanyika kwa fujo.
Walitaka nini hawa!
Alijiuliza bila kupata jibu.
Alizidi kuingia ndani ya vyumba kadhaa vilivyotumika kama ofisi.
Hali ilikuwa ni ile ile.
Kulipekuliwa.
Hatimae alielekea kulipokuwa na ofisi yake,kuna kitu alitaka kukifanya huko.
Alipotaka kuingiza ufunguo, alishangaa kukuta kupo wazi.
Nani kafungua ilihali aliacha kukiwa kumefungwa na hakuna mwingine ndani ya ofisi zile mwenye funguo za ofisi yake?
Alisita kuingia.
Aliendelea kusikilizia nje ya chumba kile cha ofisi yake bila kusikia lolote kutokea ndani.
Akasukuma mlango na kuingia.
Macho yake kwa kusaidiwa na mwanga wa taa ya kurunzi yake ndogo, yalielekea kulipokuwa na meza yake.
Napo aliona mtawanyiko wa karatasi kadhaa za utafiti ziliokuwa zimetupwa huku na huko bila mpangilio.
Alipita hadi kwenye kiti kilichokuwa nyuma ya meza na huko alitaka kuona kile kilichompelekea aende tena kwenye ofisi zile.
Akainama kwenye droo moja wapo ya meza, na kuifungua.
Akaona kifaa maalumu cha kuhifadhia matukio yanayochukuliwa na kamera zilizofungwa kwa siri maeneo mbalimbali katika ofisi ile.
Kwa namna zilivyokuwa zimefungwa ni wachache sana waliojua kuna kamera za siri eneo lile.
Akafungua sehemu ya kuhifadhia santuri ya mtambo ule.
Hamna kitu!!
Santuri ilikuwa imechukuliwa na alipojaribu kutafuta, hakuna alichoambulia zaidi ya kuona kunyofolewa kwa waya kadhaa ili kukata mawasiliano ya kamera na ule mtambo wa kuhifadhi data za kamera.
Remi aliinuka na kushika kiuno lakini mbele yake aligundua hakuwa peke yake tena ndani ya ofisi yake.
Mbele yake alisimama mtu aliekuwa amejiziba sura yake na kuvaa nguo nyeusi chini hadi juu na viganja vya mikono yake alikuwa amevificha kwa mipira maalumu mieusi.
Remi aligwaya!!
Hakutarajia kuona mtu yule katika mazingira yale.
Alitokea wapi, hakukuwa na wa kumjibu.
“Wewe ni nani na utafuta nini humu?” aliuliza kwa kitetemeshi Remi huku akili yake ikizunguka mara nyingi zaidi kujua atafanya nini kwa mtu yule ambae hakuonekana kuwa mwema kabisa.
“Nikuulize wewe, unafanya nini usiku huu wakati umefunga” yule mtu aliuliza huku akionekana kuwa makini sana na nyendo za Remi.
“Unatafuta hii?” aliuliza mtu yule huku akimwonesha Remi santuri.
Haswaa!!
Ndicho alichokuwa anakitafuta sasa anakiona mikononi mwa mtu ambae ni mvamizi wa ofisi zake na pia mtu yule alikuwa ni mwanamke mwenzie.
Remi alipandwa na gadhabu akaruka kutoka kule alikokuwa na kutua karibu na yule mwanamke mvamizi.
Akanyoosha mkono ili ampore lakini lilikuwa ni kosa, alijikuta akichezea ngumi safi katikati ya kifua na kumnyima pumzi kwa dakika mbili.
Lilikuwa ni pigo mujarabu lililopigwa makusudi na mtu anaejua kupigana.
Remi alipata tena pumzi zake, akataka kujiinua ila akajikuta anarudishwa tena chini kwa pigo safi lililoishia shingoni mwake na kumfanya ahisi anahitaji kunywa maji mengi ili kujiokoa na dhaham ya kukaukwa na koo.
“Uko wapi ukurasa wa Bombay?” aliuliza yule mwanamke huku akimwinamia Remi pale chini alipokuwa.
.
E bwana!!
Remi alitoa macho kama aliebanwa na haja kubwa ya kuhara katikati ya umati wa kariakoo.
“Ukurasa wa Bombay;ndio nini tena?” alihoji kwa tabu Remi.
Yule mwanamke alicheka kwa dharau.
“Unajifanya hujui ninachomaanisha siyo! Sasa leo utasema mwenyewe na sitaki niendelee kupata kazi ya kukufuata burebure kila mara” alitamba yule mwanamke.
Ndipo Remi alipopata jibu ni kwanini aliingiliwa nyumbani kwake usiku na kwanini alimuona mtu akiishia kichochoroni wakati wa alipokuwa akitoka nyumbani kwake.
“wewe ndo ulikuwa kwangu usiku?” alihoji Remi huku akipiga hesabu za kutoingia tena mikononi mwa bazazi yule wa kike.
“unalala kibwege mno kama ulietoka kupigwa bao nne na mumeo!” alikejeli yule mwanamke.
“Nakuuliza tena uko wapi ukurasa wa Bombay?” alihoji yule mwanamke.
“Sijui unachosema bwana!” alikoroma Remi huku akionekana kuchanganyikiwa kwa swala lile jipya.
Yule mwanamke akamfuata taratibu bila kusema neno.
Lakini gafla Remi aliinuka chini kwa kasi akiwa ameshika bastola mkononi mwake kumtupia risasi mbili yule mvamizi.
Patupu!
Yule mwanamke alikuwa ni mwepesi kama unyoya, akachumpa na kuangukia upande mwingine huku risasi zikimkosa sentimita chache kutoka alipokuwa.
Remi nae hakutaka kuzubaa akaendelea kutupa risasi kumwelekea yule mwanamke ambae alikuwa anaruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Mwanamke mvamizi akaona mambo yasiwe mengi akaamua kuumwaga na kutokomea na santuri.
Remi alimfuata nyuma kwa kasi lakini kasi yake haikuwa sawa na ile aliotumia mvamizi.
Hadi anafika nje hakuwa amemuona yule mwanamke wala kivuli chake.
Bastola ilimuokoa mikononi mwa mwanamke yule baradhuli mana kwa mapigano asingeweza hakuwa mjuzi wa upande huo.
Remi nae hakutaka kukawia pale, alitoka haraka na kuelekea getini, lakini akakumbuka kitu, haraka akarejea ilipokuwa gari ya mwandishi Davis Minja.
Akaanza kulikagua tena kwa umakini wenye haraka ya wasiwasi.
Aliona alichokitaka!!
Kwa kawaida aina ya magari ambayo yalitengenezwa na kampuni ya Toyota toleo la miaka ya karibuni, magari yote ya Harrie yalikuwa na kamera moja kwa nyuma na ndio aliotaka kuona kama ipo.
Alielekea kwenye milango ya mbele upande wa kushoto na kwa dhoruba moja la kitako cha bastola alifanikiwa kuvunja kioo na kuingiza mkono na kufyatua kabali ya mlango kisha akaingia na kufungua hapa na pale kwenye upande wa kushoto wa usukani na punde akatoka na kikanda kidogo kilichoenea kwenye kiganja na kuondoka nacho haraka.
Afunga geti kama alivyolikuta na kuelekea ilipokuwa gari yake..
Akazama ndani na kuwasha, mara sauti kavu ya kiume ikaunguruma nyuma yake.
“Tulia hivyo hivyo mwanamke” ilifoka sauti ya kavu na Remi alisikia mguso wa chuma kisogoni kwake.
Mkojo ukagusa nyeti zake tayari kwa kutoka,na tumbo likamuunguruma kwa woga.
**
Maoni yako tafadhali