Riwaya: Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia

Riwaya: Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia

RIWAYA; UKURASA WA GAIDI

NA;BAHATI MWAMBA.

SIMU; 0758573660.

SEHEMU YA SITA


Umakini uliongezeka usoni mwa Sajini.

“Taarifa zinasema mumeo hajaonekana zaidi ya miaka miwili, sasa yeye alikuwaje akamtafuta na anajua kabisa mumeo hayupo?” aAlisema Sajini Vengu.

“Sijui kama hawakuwa na mawasiliano kati yao katika miaka hiyo miwili na…” Remi hakumalizia kauli yake Sajini akamkatisha.

“Remi; mumeo tumeambiwa ni gaidi na haonekani sasa iweje Davis aseme hapatikani, hivyo unajua mumeo alipo sio?” Alihoji Sajini Vengu.

“Sijasema aliulizia mume wangu, bali nimesema pengine ndie alimaanisha afande” alisema Remi.

“Watch yo step madame!!” Alitahadharisha Sajini.

Remi akagwaya!!

Baada ya mazungumzo ya dakika kadhaa, Remi aliaga na kuondoka huku akimwacha Sajini akiwa amepata jambo jipya kuhusu mume wa Remi.

Remi alipanda gari lake na lengo lake alitaka arudi tena kule ofisini kwake, alitaka kufanya jambo ambalo alijua anaweza kubahatisha kulipata!

“Walioyafanya pale ofisini sina hakika kama kweli hawajaacha kosa moja, Hakuna mkamilifu” alisema Remi huku akiipita hospital ya mwananyamala, alikuwa anaelekea Mwenge zilipo ofisi zake. Hakutaka kuendelea kuhujumiwa, alitaka kukokotoa hesabu katikati ya hujuma na mitego.

Kitu kimoja hakujua madhara ya kile alichotaka kwenda kukifanya na kama angejua basi bora angeacha tu aendelee kushuhudia showtime alioahidiwa na bwana kitambi…

Hakika hakujua madhara yake kwa alichokusudia.

***

Jua lilikuwa linaelekea kuiachia dunia kiza; lilielekea magharibi.

Remi aliegesha gari lake pembeni kidogo mwa ofisi zake za utafiti wa mambo ya kale.
Eneo la ofisi zake lilikuwa lipo kimya na utepe wa njano ulikuwa umewekwa kwenye geti la kuingilia ndani ya ofisi zile.

Alitazama kushoto na kulia, kisha akaita kama kubahatisha tu ili ajue kama kuna askari atakuwa eneo lile.

Kukawa kimya!!

Akapiga hatua za mnato huku akiwa makini sana ili asije kuvuta jicho la mtu yeyote ambae alikuwa mitaa ile kufuatilia yeyote ambae angelifika pale nyakati zile.

Hakuona wala kuhisi jambo hilo eneo lile.
Akachukua funguo zake na kutia kwenye kitasa cha geti na likafunguka.

Akaingia!!

Akaelekea lilipokuwa gari la mwandishi Davis Minja lililokuwa limetelekezwa kabla haijafika kwenye maegesho.

Taa zilikuwa zimezimwa na eneo lote lilikuwa giza na kumezwa ukimya wa kifo.

Remi alitoa kurunzi ndogo kwenye mkoba aliokuwa ameubeba na kuanza kulitazama gari lile ambalo lilionekana kubondeka sehemu moja chini kidogo ya mlango wa kutokea dereva.
Remi aliinama na kugusa eneo lile na alichogundua ni kuwa mmbondeko ule ni wa chuma kilichobamiza pale kwa nguvu.
Zilifanyika harakati za la lazima kumchukua mwandishi yule.
Alisimama na kwa taratibu kabisa alianza kulizunguka gari lile ambalo hadi wakati huo lilionekana kupitia dhoruba kadhaa wakati likiwa njiani.

Remi hakuona cha maana zaidi katika lile gari,akaachana nalo.

Akaelekea mlango wa kuingilia ofisini kwake, akafungua na kuingia ndani taratibu huku akiangaza huku na huko.

Macho yake yakanasa mvurugano wa makablasha.

Kulipekuliwa!!

Saa ngapi na kwanini, hakujua!!

Akazidi kuona namna upekuzi ulivyofanyika kwa fujo.

Walitaka nini hawa!

Alijiuliza bila kupata jibu.

Alizidi kuingia ndani ya vyumba kadhaa vilivyotumika kama ofisi.
Hali ilikuwa ni ile ile.

Kulipekuliwa.

Hatimae alielekea kulipokuwa na ofisi yake,kuna kitu alitaka kukifanya huko.

Alipotaka kuingiza ufunguo, alishangaa kukuta kupo wazi.

Nani kafungua ilihali aliacha kukiwa kumefungwa na hakuna mwingine ndani ya ofisi zile mwenye funguo za ofisi yake?

Alisita kuingia.

Aliendelea kusikilizia nje ya chumba kile cha ofisi yake bila kusikia lolote kutokea ndani.

Akasukuma mlango na kuingia.

Macho yake kwa kusaidiwa na mwanga wa taa ya kurunzi yake ndogo, yalielekea kulipokuwa na meza yake.

Napo aliona mtawanyiko wa karatasi kadhaa za utafiti ziliokuwa zimetupwa huku na huko bila mpangilio.

Alipita hadi kwenye kiti kilichokuwa nyuma ya meza na huko alitaka kuona kile kilichompelekea aende tena kwenye ofisi zile.

Akainama kwenye droo moja wapo ya meza, na kuifungua.

Akaona kifaa maalumu cha kuhifadhia matukio yanayochukuliwa na kamera zilizofungwa kwa siri maeneo mbalimbali katika ofisi ile.

Kwa namna zilivyokuwa zimefungwa ni wachache sana waliojua kuna kamera za siri eneo lile.

Akafungua sehemu ya kuhifadhia santuri ya mtambo ule.

Hamna kitu!!

Santuri ilikuwa imechukuliwa na alipojaribu kutafuta, hakuna alichoambulia zaidi ya kuona kunyofolewa kwa waya kadhaa ili kukata mawasiliano ya kamera na ule mtambo wa kuhifadhi data za kamera.

Remi aliinuka na kushika kiuno lakini mbele yake aligundua hakuwa peke yake tena ndani ya ofisi yake.

Mbele yake alisimama mtu aliekuwa amejiziba sura yake na kuvaa nguo nyeusi chini hadi juu na viganja vya mikono yake alikuwa amevificha kwa mipira maalumu mieusi.

Remi aligwaya!!

Hakutarajia kuona mtu yule katika mazingira yale.

Alitokea wapi, hakukuwa na wa kumjibu.

“Wewe ni nani na utafuta nini humu?” aliuliza kwa kitetemeshi Remi huku akili yake ikizunguka mara nyingi zaidi kujua atafanya nini kwa mtu yule ambae hakuonekana kuwa mwema kabisa.

“Nikuulize wewe, unafanya nini usiku huu wakati umefunga” yule mtu aliuliza huku akionekana kuwa makini sana na nyendo za Remi.

“Unatafuta hii?” aliuliza mtu yule huku akimwonesha Remi santuri.

Haswaa!!

Ndicho alichokuwa anakitafuta sasa anakiona mikononi mwa mtu ambae ni mvamizi wa ofisi zake na pia mtu yule alikuwa ni mwanamke mwenzie.

Remi alipandwa na gadhabu akaruka kutoka kule alikokuwa na kutua karibu na yule mwanamke mvamizi.

Akanyoosha mkono ili ampore lakini lilikuwa ni kosa, alijikuta akichezea ngumi safi katikati ya kifua na kumnyima pumzi kwa dakika mbili.
Lilikuwa ni pigo mujarabu lililopigwa makusudi na mtu anaejua kupigana.

Remi alipata tena pumzi zake, akataka kujiinua ila akajikuta anarudishwa tena chini kwa pigo safi lililoishia shingoni mwake na kumfanya ahisi anahitaji kunywa maji mengi ili kujiokoa na dhaham ya kukaukwa na koo.

“Uko wapi ukurasa wa Bombay?” aliuliza yule mwanamke huku akimwinamia Remi pale chini alipokuwa.
.
E bwana!!

Remi alitoa macho kama aliebanwa na haja kubwa ya kuhara katikati ya umati wa kariakoo.

“Ukurasa wa Bombay;ndio nini tena?” alihoji kwa tabu Remi.

Yule mwanamke alicheka kwa dharau.

“Unajifanya hujui ninachomaanisha siyo! Sasa leo utasema mwenyewe na sitaki niendelee kupata kazi ya kukufuata burebure kila mara” alitamba yule mwanamke.

Ndipo Remi alipopata jibu ni kwanini aliingiliwa nyumbani kwake usiku na kwanini alimuona mtu akiishia kichochoroni wakati wa alipokuwa akitoka nyumbani kwake.

“wewe ndo ulikuwa kwangu usiku?” alihoji Remi huku akipiga hesabu za kutoingia tena mikononi mwa bazazi yule wa kike.

“unalala kibwege mno kama ulietoka kupigwa bao nne na mumeo!” alikejeli yule mwanamke.

“Nakuuliza tena uko wapi ukurasa wa Bombay?” alihoji yule mwanamke.

“Sijui unachosema bwana!” alikoroma Remi huku akionekana kuchanganyikiwa kwa swala lile jipya.

Yule mwanamke akamfuata taratibu bila kusema neno.

Lakini gafla Remi aliinuka chini kwa kasi akiwa ameshika bastola mkononi mwake kumtupia risasi mbili yule mvamizi.

Patupu!

Yule mwanamke alikuwa ni mwepesi kama unyoya, akachumpa na kuangukia upande mwingine huku risasi zikimkosa sentimita chache kutoka alipokuwa.
Remi nae hakutaka kuzubaa akaendelea kutupa risasi kumwelekea yule mwanamke ambae alikuwa anaruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Mwanamke mvamizi akaona mambo yasiwe mengi akaamua kuumwaga na kutokomea na santuri.
Remi alimfuata nyuma kwa kasi lakini kasi yake haikuwa sawa na ile aliotumia mvamizi.
Hadi anafika nje hakuwa amemuona yule mwanamke wala kivuli chake.

Bastola ilimuokoa mikononi mwa mwanamke yule baradhuli mana kwa mapigano asingeweza hakuwa mjuzi wa upande huo.

Remi nae hakutaka kukawia pale, alitoka haraka na kuelekea getini, lakini akakumbuka kitu, haraka akarejea ilipokuwa gari ya mwandishi Davis Minja.

Akaanza kulikagua tena kwa umakini wenye haraka ya wasiwasi.

Aliona alichokitaka!!

Kwa kawaida aina ya magari ambayo yalitengenezwa na kampuni ya Toyota toleo la miaka ya karibuni, magari yote ya Harrie yalikuwa na kamera moja kwa nyuma na ndio aliotaka kuona kama ipo.

Alielekea kwenye milango ya mbele upande wa kushoto na kwa dhoruba moja la kitako cha bastola alifanikiwa kuvunja kioo na kuingiza mkono na kufyatua kabali ya mlango kisha akaingia na kufungua hapa na pale kwenye upande wa kushoto wa usukani na punde akatoka na kikanda kidogo kilichoenea kwenye kiganja na kuondoka nacho haraka.

Afunga geti kama alivyolikuta na kuelekea ilipokuwa gari yake..

Akazama ndani na kuwasha, mara sauti kavu ya kiume ikaunguruma nyuma yake.

“Tulia hivyo hivyo mwanamke” ilifoka sauti ya kavu na Remi alisikia mguso wa chuma kisogoni kwake.

Mkojo ukagusa nyeti zake tayari kwa kutoka,na tumbo likamuunguruma kwa woga.

**

Maoni yako tafadhali
 
RIWAYA : URITHI WA GAIDI

NA; BAHATI MWAMBA.

SIMU;0758573660

SEHEMU YA SABA




Alielekea kwenye milango ya mbele upande wa kushoto na kwa dhoruba moja la kitako cha bastola alifanikiwa kuvunja kioo na kuingiza mkono na kufyatua kabali ya mlango kisha akaingia na kufungua hapa na pale kwenye upande wa kushoto wa usukani na punde akatoka na kikanda kidogo kilichoenea kwenye kiganja na kuondoka nacho haraka.

Afunga geti kama alivyolikuta na kuelekea ilipokuwa gari yake..

Akazama ndani na kuwasha, mara sauti kavu ya kiume ikaunguruma nyuma yake.

“Tulia hivyo hivyo mwanamke” ilifoka sauti ya kavu na Remi alisikia mguso wa chuma kisogoni kwake.

Mkojo ukagusa nyeti zake tayari kwa kutoka,na tumbo likamuunguruma kwa woga.

“Ulifuata nini huku usiku huu?” sauti iliokuwa nyuma yake ilisaili.

Remi kwa haraka haraka aliitambua sauti ile ni ya Sajini Vengu.

Akashusha pumzi na kuitowesha hofu.

“Kuna kitu cha muhimu sana nilikuja kukichukua ambacho najua hakuna aliekumbuka kukichukua kati yenu” Alijibu Remi.

Sajini akapiga kimya kidogo.

“kwa hiyo unadhani tutakuwa hatukufanya uchunguzi vizuri?” Alisaili Sajini.

“Mnaweza kuwa mmefanya vizuri,ila ni ngumu kukifikia hiki ambacho nilikuja kukichukua” Alijibu Remi.

Sajini Vengu aliguna huku akitoa bastola kuchwani kwa Remi.

“Kitu gani hicho” aliuliza Sajini.

Mkanda wa kuhifadhi matukio yanayorekodiwa na kamera za siri za hapa ofisini”

Sajini alikaa sawa baada ya kusikia habari hiyo.

“Uko wapi sasa huo mkanda na unahisi utakuwa umerekodi vyema tukio lililotokea hapa?” Alisaili kwa kimuhemuhe Sajini.

Remi alitikisa kichwa kwa masikitiko kisha akasema…

“Wakati naingia, sikujua ndani kuna mtu nae alikuwa na lengo kama langu hivyo amenipiga na kuondoka na rekodi hiyo”

“Ooh shiit! Sasa ndo nini?” alihoji bila kujua Sajini.

“Yawezekana mi na wewe hatujajua nguvu inayotumika na hawa waliofanya hiki kitendo mana wanawahi kila sehemu tunayoifikia” alisema Remi na hapo Sajini akamtupia jicho la kiulizo katikati ya kiza kilichowatenganisha.

“Lakini nikuukize sasa; kwa nini unaingilia jeshi la polisi katika kazi zake?” alihoji Sajini.

“Kwa sababu mi ni mtuhumiwa wa hili tukio, lakini pia mume wangu ambae sijui aliko nae anahusishwa katika haya, hivyo nina kila sababu ya kujitahidi kulisaidia jeshi ili niepukane na hii dhahama” alijitetea Remi.

“Lakini hii ni hatari kwako, kufanya haya unayoyafanya na inaweza kukugarimu hadi uhai” Sajini alitahadharisha.

Remi alipiga kimya.

“ok una lolote la kunambia?” alivunja ukimya Sajini.

Remi akawasha taa za mle garini na kumgeukia Sajini.

“Hii inaweza kukupa mwanga katika kesi hii na mimi mkanitoa rasimi katika sakata hili ambalo hakika sijui linapotaka kunipeleka” Remi alisema huku akimpa Sajini kanda ndogo iliokuwa mkononi mwake.

Sajini aliichukua na kuitazama, na alitambua ni rekodi ya mienendo ya gari aliopewa.

Sajini akashika kitasa cha mlango wa gari na kutoka.
Alipokwisha kukanyaga chini, akaenda hadi upande wa dereva na kumtazama Remi.

“Ni heri zaidi ungekaa mbali na sakata hili na uache jeshi lifanye kazi yake bila kuingiliwa na wewe ambae unaweza kuharibu upelelezi.

Alisema Sajini na kugeuka kupotelea vichochoroni alikokuwa ametokea wakati akimfuatilia Remi.

Remi nae akaitia moto gari yake na kurejea nyumbani kwake kinondoni.

***

Wakati inatimia mida ya saa nne ahsubuhi kwa saa za Africa mashariki; kuna mambo mawili yalitokea kwa makusudi au ni bahati mbaya tu ilikuwa imesababisha yale yote.

Mosi; wakati kunapambazuka, tayari Sajini Vengu alikuwa ameshapata rekodi zilizorekodiwa na kuhifadhiwa ndani ya kifaa alichokuwa amepewa na Remi usiku uliopita.
Lakini kuna kitu kilimchanganya zaidi Sajini.
Rekodi ilionesha vizuri gari lililokuwa nyuma ya gari la mwandishi Davis Minja na pia liliendelea kurekodi hadi wakati linasimama na watu waliokuwa kwenye gari la nyuma walishuka.

“Military fatigue!” alijuliza Sajini huku akijitahidi kuzikuza sura za watu wale bila mafanikio.

“Sasa polisi anahusika vipi tena na utekaji?” alijiuliza Sajini bila kupata wa kumjibu.
Akaguna na kuzinakili pembeni namba za gari lililokuwa linafuatilia mwandishi Davis Minja.

Sajini akachukua simu na kupiga pahali kisha akahitaji kujua mmiliki wa gari ile.

Na hilo ndilo lililomkuta saa nne hiyo ahsubuhi akiwa na taharuki ya kutoelewa mambo yalivyo.

Eti gari lililotumiwa na watekaji linamilikiwa na Haji Makame.

Ebana ee!

Ajabu hii!!

Inakuwaje tena gari linalomilikiwa na Haji Makame lihusike na utekaji?

Mambo yalimchanganya Sajini na alishindwa kupambanua vyema kabisa.

Akili yake ilimwambia bado Remi anaweza kuwa anahusika, lakini kama anahusika kwanini utekaji na mauaji afanyie ofisini kwake?

Hata!!

Haiwezi kuwa rahisi hivyo,kuna tatizo sehemu na kilichomchanganya zaidi ni yale mavazi ya jeshi la polisi waliokuwa wamevaa watekaji.

Alihitaji kupata jibu litakalo mpunguzia msongo wa mawazo kuhusu matukio yale yaliokuwa yanazidi kuchukua sura mpya.

Alichukua simu na kumpigia Remi..

**
Upande mwingine pia ndani ya saa nne ile kulikuwa kuna jambo la pili lenye kumchanganya pia.

Remi hakuwa ametaka kutoka nje kwa siku hiyo,alikuwa amekaa kwenye meza akipangilia hesabu zake namna anavyoweza kutatua jambo lile bila papara na pia alikuwa anagojea simu ya Sajini kuhusu alichokiona kwenye rekodi aliompa.
Mawazo yake yakiwa bado yapo kwenye lindi la ukungu,aliamua kuchukua simu janja yake na kuperuzi hapa na pale.
Wakati anawasha data tu, akapokea ujumbe kwa njia ya whatsapp na ulitoka kwa mmoja wa wafanyakazi wake.

Aliufungua na kukutana na link mbili alizokuwa ametumiwa.

Akafungua!!

Link ya kwanza ilimpeleka kwenye tovuti ya mamlaka ya ukusanyaji kodi na mapato nchini. Ambapo alikutana na majina ya wadaiwa sugu wa kodi nchini yaliokuwa yametolewa na mamlaka hiyo.

Jina lake na kampuni yake lilikuwa miongoni mwa majina ya mwanzo kabisa katika orodha.

Hilo halikumstua sana japo lilikuwa geni kufanywa na mamlaka ile.

Link ya pili ndio iliokuwa na wahaka mkubwa katika fikira za Remi.

Aliifungua na kumpeleka kwenye tovuti ya mtandao wa matukio na habari muhimu wa Jamii forums.

Kichwa cha habari cha habari ile kilisomeka hivi:

“Mkimbizi anaeishi kinyemela nchini;aibuka kuwa mdaiwa sugu wa kodi katika kampuni yake inayofanya kazi kinyemela nchini.”
Remi aliufungua uzi ule na kuusoma.
Ndani alikutana na habari ndefu iliohusu wasifu wake na kampuni yake ambayo wasajili wa makampuni walikaririwa wakisema hawajui chochote kuhusu hiyo kampuni, lakini pia licha ya kuwapo kinyemela inahitajika kulipa kodi kwa muda wote ilipokuwapo na mbaya zaidi watu wa uhamiaji nao walikiririwa wakisema wanamtafuta mmiliki wa kampuni hiyo athibitishe uraia wake.
Baada ya hapo yalifuatia maoni mengi ya wanachama wa mtandao ule ambao kila mmoja alisema lake.

Remi alijikuta akilowa jasho mwili mzima huku moyo ukiongeza kasi ya udundaji wake.

Kweli alikuwa ameingia kwenye hujuma na wale watu waliendelea kumpa show waliomuahidi.

Remi alishindwa kujua ni kwanini kapokonywa uraia wake na kutangazwa kama mkimbizi, lakini pia ni kuhusu umiliki wa kampuni yake ambayo alikuwa ameisajili kikamilifu na kodi alilipa bila kukwepa.

Dah!!

Remi alichanganyikiwa hakika.

Ilianza ya mume wake kuitwa gaidi na sasa yeye ni mkimbizi halali sio tena mkimbizi aliejificha kwa kivuli cha kupewa uraia baada ya kufanya makubwa katika mkasa ulioandikwa kama Mpango wa Congo.

Alibaki akijuliza kama nchi hii ilistahili kumlipa ubaya wa aina hii hata baada ya kufanya mengi mazuri ili kuikomboa na watu dhalimu na majahili.

Remi alikuwa amehujumiwa hakika.

Lakini kama alijipanga kukukabiliana na hujuma zile, alikuwa anakosea na hakujua ndo kwanza hujuma zilianza.

Kwa kuwa usilojua ni sawa na usiku wa kiza kinene.

Remi hakujua yajayo hakika!!


ITAENDELEA LEO!!
 
RIWAYA; URITHI WA GAIDI

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA NANE



Ilianza ya mume wake kuitwa gaidi na sasa yeye ni mkimbizi halali sio tena mkimbizi aliejificha kwa kivuli cha kupewa uraia baada ya kufanya makubwa katika mkasa ulioandikwa kama Mpango wa Congo.

Alibaki akijuliza kama nchi hii ilistahili kumlipa ubaya wa aina hii hata baada ya kufanya mengi mazuri ili kuikomboa na watu dhalimu na majahili.

Remi alikuwa amehujumiwa hakika.

Lakini kama alijipanga kukukabiliana na hujuma zile, alikuwa anakosea na hakujua ndo kwanza hujuma zilianza.

Kwa kuwa usilojua ni sawa na usiku wa kiza kinene.

Remi hakujua yajayo hakika!!

**

Akiwa bado hajui afanye nini na kichwa kinamzunguka kwa taarifa zile; Simu yake ilitetema.

Akaangalia namba ya mpigaji.

Sajini!!

Ilisomeka hivyo.
Akaipokea huku akiwa bado hajapata sauti walau ya kusema heloo!!

“Uko wapi hivi sasa?” Aliuliza Sajini baada ya kubaini simu yake imepokelewa.

“Nipo nyumbani!” alijibu Remi.

“Ok! Hii namba ya gari(akitaja namba) unaifahamu?” aliuliza Sajini Vengu.

Remi alishusha pumzi nyingi kwa mkupuo kisha akakaa sawa kwenye sofa, alihisi kuna habari nyingine mbaya zaidi.

Na ndivyo ilivyokuwa..

“Ndio, naifahamu. Ni namba za gari la mume wangu Haji” alisema Remi huku akingoja Sajini upande wa pili ajibu.

Sajini nae alipumua kwa nguvu na kusema.

“ile kanda ulionipa, nimeifanyia kazi na kufanikiwa, lakini gari lilofanya utekaji ni lenye namba hizo nilizokutaji”

“unasemaa!!” Remi alimaka kwa mshangao.

Na haraka akakimbilia dirisha lililokuwa upande wa pili kutoka alipokuwa na kusukuma kidogo kioo na kutazama nje kulikokuwa kunapakiwa magari ya mume wake na lake pia.

Magari yote matatu yalikuwepo na mawili kati ya matatu yalikuwa yamefunikwa kwa turubai jeusi kwa juu.

“Are you there?” alihoji kimombo Sajini Vengu huku akijistukia kama yupo sahihi ama la.

“aah hii inakuwaje afande!!” alihoji tena Remi.

“Nikuulize wewe, hii imekaaje” Alimrudishia mpira Remi.

Remi alikuna kichwa kwa kuchanganyikiwa.

“Afande; gari lenye hizo namba lipo hapa kwangu na hakuna ambae amewahi kulitumia tangu mume wangu aondoke nchini” alijibu Remi.

“una hakika gari hilo silo lililofanya haya?” alisaili Sajini.

“Hakika silo, mana hili gari lipo hapa limepaki kwa muda murefu sana bila kutamika”

Sajini aliguna kisha akasema.

“Usitoke hapo nyumbani nakuja kulikagua hilo gari na pia tuzungumze kitu fulani hivi kinachoweza kutupa mwanga japo inategemeana na ushirikiano wako” Alisema Sajini na kukata.

Wakati Sajini anakata simu, kuna upande mwingine nao ulikuwa unaweka chini simu na kutafarakari yale alioyasikia kutoka kwa Remi na Sajini Vengu.

“Vengu anataka kumshirikisha nini huyu mwanamke?” alijihoji yule bwana ambae wakati huo alikuwa amesimama akiangalia dirishani huku mikono akiwa ameifumbata kwa nyuma.

“Bado mapema sana kuruhusu makosa” alijisemea tena, huku mara hii akiingiza mkono mfukoni na kutoka na simu ngingine ndogo ambayo kwa kuitazama tu haiukuendana na hadhi yake.

Yule bwana kwa kutumia simu hiyo akapiga mahali..

**

Remi ndani kwake hakukulika, aliona ni kama anaenda kutumbukia kwenye shimo refu lisilo na mwisho wa kina chake, huku mara kwa mara akihisi atavamiwa na maaskari muda wowote na kumkamata.

Hakika aligwaya!!

**

Akiwa bado yupo njia panda huku akimsubiri Sajini Vengu; Remi akapata wazo na kuelekea chumbani kwake ambako alichukua kompyuta mpakato yake na kuiwasha kisha akaingia upande wa kuandika email na kuutuma kwa akaunti ya mumewe.

Aliamini kama ni mzima basi ipo siku ataufungua na kusoma na atajua kilicholendelea wakati yeye akiwa hayupo.

Akarejea sebuleni na ni wakati huo aliposikia mlango ukigongwa kwa kengele maalumu ilioko nje ya geti.

Alienda kufungua na alimkuta Sajini Vengu akiwa na usafiri wa pikipiki! Akaingia ndani ya ua kisha moja kwa moja walielekea kulipokuwa na maegesho ya magari ya nyumba ile.

“Kama unavyoona, gari hili hapa na lina hizo namba ulizozitaja,lakini tizama lilivyo,je waona limeingia barabarani hivi punde?” alisema Remi huku akifunua turubai lililokuwa limezifunika gari mbili za kampuni moja ila matoleo tofauti.

Sajini aliyatizama magari yale kwa makini na kweli aliona zile namba alizoziona kwenye picha iliorekodiwa na kamera maalumu kwenye gari alilokuwamo mwandishi Davis Minja.

Gari halikuonekana kuwa na dalili yoyote ya kutumika siku za hivi karibuni.

Sajini aliinama hadi kwenye uvungu wa gari ili kusikia kama gari linapumua kuashiria limetumika karibuni, ila alikutana na ukimya ambao ulimhakikishia hakukuwa na matumizi ya injini ya gari lile.

“Sasa mambo yanazidi kuwa makubwa Remi; na hadi sasa hakuna mwelekeo tuliopiga licha ya kujitahidi sana. Kwa akili za kawaida inamaana inatakiwa nikuweke chini ya ulinzi ili usaidie jeshi katika utata huu, lakini kwa askari makini huwezi kufanya hivyo ila utatakiwa kujua sababu zaidi ya kumweka huyo mtu chini ya ulinzi.” Alisema Sajini huku akijipangusa mchanga kwenye viganja vya mikono yake.

“Remi;unaweza kunambia mumeo alikuaga anaenda wapi na kwanini hajarudi?” Aliuliza Sajini.

Siwezi kujua kwa nini hajarudi ila wakati anaondoka alinambia anaenda Pakistani kwenye kozi maalumu” alijibu Remi.

“mh!! Sasa kwanini hajarejea na huku ofisi zinakana kuwa na mtu wa aina hiyo? Unahisi nini hapo?” alihoji Sajini huku akiwa makini sana kusikia jibu la Remi.

“Siwezi jua sababu ni nini, ila mambo ni mengi muda hauruhusu kujadili hayo ambayo yameanzia ndani ya uongozi, kwa sasa nadhani tunapaswa kujadili hili linalonihusu moja kwa moja afande!” Alisema Remi.

“Bado mumeo anahusika sana tu na inawezekana yote haya lengo ni yeye na ndivyo wanakutumia wewe ili atoke aliko aje!” Alisema Sajini.

Wazo lile lilionekana kumuingia Remi; lakini ikabaki swali moja kichwani mwake, ni nani yupo nyuma ya haya na ni nani aliemteka Davis au nae anahusikaje katika haya!

“Anyway,kuna mambo ambayo wewe hupaswi kuyajua ila kuna mkono mrefu katika hili na nimeanza kuingiwa na hofu hata mimi” alisema Sajini huku akiegemea kwenye gari na kuifumbata mikono yake kifuani pake.

“Kila ninakopita hawa jamaa wamefanya usafi wa kutokuhusishwa na tukio hili” alisema Sajini.

Remi aliguna tu!!

“Hakuna mtu yeyote unaehisi anahusika katika sakata hili au kutuongoza katika mkasa huu?” alihoji Sajini.

Remi alitatizika na alitaka kumtaja bwana kitambi ila alijikuta anasita tu kufanya hivyo na akaishia kutikisa kichwa kuashiria hajui lolote hadi wakati huo.

Sajini akatoka kwenye gari na kuanza kujongea,, lakini hakufanikisha dhamira yake hiyo ya kujongea bila kumpa taarifa Remi ya kile alichotaka kufanya, kama ni kuondoka ama kufanya kitu gani.

Sajini alijikuta akipaa juu na kudondokea kwenye gari alilokuwa ameegemea huku upande wake wa kushoto usawa wa moyo ukiwa na tundu kubwa la risasi na damu ilikuwa inamwagika kama bomba la maji lililotoboka.
Sajini koo lilimkauka na alishindwa hata kutamka kitu chochote alibaki akiwa amemkodolea macho Remi ambae alikuwa ameshikwa na mshangao mkubwa kwa kile kilichokuwa kinatokea mbele yake!!

Hakujua risasi ilikotokea na muuaji alikuwa amepiga kutokea wapi. Kwanini alimuua sajini wakati ambao yuko kwa Remi.

Hakika ulikuwa ni mtihani mwingine tena kwa Remi na hakujua atajinasua vipi katika hujuma ile.
Hesabu zake bado hazikuzaa matunda katika awamu ya pili ya showtime.

Alipiga hatua za aste aste na kufika pale alipoangukia Sajini Vengu; akainama na kuweka vidole vyake kwenye shingo ya Sajini ili kujua kama bado anapumua ili ampeleke hospital lau awahi kuokoa maisha yake, ila alikuta tayari mishipa imeanza kupoa na haidundi tena.

Ni wakati akinyanyuka ndipo alipohisi mwanga mkali wa kamera ukimmlika usoni. Haraka akageuka na kutizama kule alipohisi umetokea na kweli upande wa geti dogo alisimama mwanamke aliekuwa amevaa mavazi meusi juu hadi chini na kufunika uso wake na kubakiza macho tu.

Mwanamke yule begani mwake alikuwa amening’iniza silaha kubwa ya kudungulia na mkononi mwake akishika kamera kubwa sawa na za waandishi wa habari.

Remi alikuwa anatazamana na mwanamke waliepambana usiku ofisini kwake!!

Mwanamke yule akanyoosha vidole viwili kumwelekea Remi kisha akavipunga hewani mara mbili ishara ya mpigo wa bastola na kisha akavikunja vidole vyote na kubakiza kidole gumba kisha akakiinamishia chini ishara ya kuzika.

Remi aligwaya!!

Mwanamke yule akatoweka na Remi alishindwa hata kumfuata na punde tu kikasikika king’ora cha gari la polisi kikivuma kuelekea mitaa ile.

Moyo wa Remi ukapiga kite nguvu.
Macho yake akayageuza ulipo mwili wa Sajini.
Alijua ni nini kinafuata!

Remi matatani jama!!


***


ITAENDELEA KESHO JIONI.
 
Remi alijua nini kitafuata baada ya kusikia ving'ora vya gari la polisi.Usiombe serikali itekwe na genge la wahuni
 
Back
Top Bottom