Riwaya: Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia

RIWAYA; URITHI WA GAIDI

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA KUMI NA TISA


***

Inspekta Kenge alikuwa katikati ya barabara huku akipiga mluzi usioeleweka masikioni mwake..

Mara akapigiwa honi na gari lililokuwa nyuma yake.

"unaendesha kama unaingia kwako bwana!!" Alilalama konda wa gari lililopiga honi na kumpita Inspekta.

Inspekta Kenge akajinunisha ndani ya gari, kisha akaongeza mwendo na kuanza kulifuata gari lile lililokuwa linapiga ruti za Mbagala hadi kawe.

Mbele kulikuwa kuna foleni!

Gari lilisimama na Kenge nae akasimamisha gari lake kisha akashuka kwa gadhabu na kumfuata dereva,akamshusha na kuanza kumsomea lisala.

"Hivi hujui kuona magari mengine ni ya serikali na waliomo ndio serikali yenyewe,au hujui sheria zinatukataza kukimbiza magari kwenye misongamano ya watu vyombo vingine vya usafiri"

Dereva akataka kujitetea; Kenge akamzuia.

"yani serikali inaongea na wewe unaongea, bado konda wako amenitukana, inamaana hukuona kuwa alieko kwenye gari ni Inspekta?"

Ebanaee!.

Dereva akagwaya!

Mara gari zikaruhusiwa kusogea na zilizposogea gari la Inspekta na lile la abiria havikusogea!

Bado waliendelea kulumbana,honi zilipigwa kwa fujo na magari yaliokuwa nyuma yao.

Inspekta mtata alirudi ndani ya gari lake baada ya kutupiwa chini kiasi cha pesa ya kununulia dawa ya kusafishia viatu vyake.

Inspekta Kenge alikuwa amevurugwa na mambo mengi siku hiyo ikiwemo suala la Remi kuhusika katika mauaji ya ofisa wa jeshi la polisi.

Kilichomchanganya zaidi ni kuona tangu aanze kazi yake amekuwa akipigiwa simu na kupewa maelekezo namna ya kufanya kazi yake.

Tangu lini nikaelekezwa mimi.

Kenge alipiga ngumi kwenye usukani na kusababisha mlio mkali wa honi huku yeye mwenyewe akiruka kwa msituko.

Alikumbuka namna alivyopokea simu na kupewa maelekezo ya kuandika kuhusu mkasa ule na aliahidiwa pesa ya kutakata endapo Remi angekubali kusaini maelezo yale.

Alijikuta anakunja sura kama kaonja kamasi za mtoto.

Alijikuta anamchukia Remi.

Kwa nini!

Kwa sababu Remi alikataa kusaini karatasi zile.

"Siwezi kusaini karatasi ulizoandika wewe na kamwe sitakaa nifanye hivyo, kama mtaniacha nifie humu sawa" Alikumbuka maneno ya Remi.

Remi kutokusaini inamaanisha yeye hatopata mpunga aliohadiwa na mtu anaempigiaga simu.

Alifyonza!

"Kile kipigo nilichompa nikirudi atatia adabu na kusaini mwenyewe" Alijisemea tena.

Kenge alihitaji kufanya jambo moja ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kuaminika kwa wakubwa wake.

Alihitaji kuwa karibu na ukweli zaidi kuliko uongo anaopangiwa kuufanya.

Mawazo yake yalimwambia anahitaji kukutana na mhariri wa gazeti la Chaupeku; gazeti la udaku ambalo kwa ufukunyuku wake alifanikiwa kujua ndilo lililosambaza picha na taarifa kwenye magazeti mengine.

Alihitaji kukutana na mhariri ili ajue yeye alizipataje hizo picha na ni nani alimtumia.

Kwake aliona ni silaha kubwa kujua pande mbili za mchezo ule.

Hatimae alifika kwenye ofisi zile na kushuka kwa madaha huku akirekebisha miwani yake usoni.

Wakati Kenge anafika ni wakati ambao mhariri alikuwa kwenye mazungumzo na Sajenti Kobelo na bado walikuwa katika ubishani.

Kenge aliingia.

Akamkuta Sajenti ambae hakuonekana kujali uwepo wake pale.

"Sajenti nashindwa kuelewa kwa nini hunipigii saluti" Alihoji Inspekta huku akivuta kiti na kukaa.

"Sijavaa military fatigue" Sajenti alijibu kwa mkato.

Kenge akatabasamu kimajivuno.

"Nadhani unapaswa kunipisha, ni wakati wangu bwana mdogo" Alisema Kenge.

Sajenti akasimama na kuanza kuelekea mlangoni.

"Afu hii haipo mikononi mwako na ni kosa kisheria" Alisema Kenge huku akikaa..


Sajenti hakujibu akatoka.

Ndani ya ofisi walibaki mhariri mkuu na Inspekta Kenge.

Kenge alijawa na wivu baada ya kumkuta Sajenti akiwa ndani ya ofisi zile na ile aliitafsiri kama dharau na pia inaweza kumuondolea sifa kwa wakubwa wake endapo Sajenti atafanikiwa kujua ukweli kabla yake.

Akajikuta anataka kuhakikisha kama kweli Sajenti alikuwa pale ni kuhusu sakata lile.

Akauliza swali la kijinga tu.

"Huyu bwana mdogo alikuwa hapa kwa sababu gani eti"

"kazi yangu hainiruhusu kusema shida za wageni wetu kwa watu wengine" Alijibu mhariri ambae alikuwa ni kijana wa makamo tu na haiba ya upole.


Kenge alitabasamu!

"Naitwa Inspekta Kibe Kengeleo au wengi huniita Kenge nina maswali machache ndugu mhariri" Alijitambulisha Kenge..

Mhariri ambae kibao juu ya meza kilimtambulisha kama J Malao alitabasamu bila kutanabaisha dhamira yake ya kutabasamu.

"Jana habari kubwa ilikuwa ni mauaji, na gazeti lako lilikuwa la kwanza kupata picha na habari,naomba kufahamu ilitoka wapi habari ile ama mwandishi gani alieipata na wapi alikoitoa"

J Malao aligabasamu tena.

"Ni kinyume kabisa na maadili ya kazi yangu, na ndio mana unaona habari imeandikwa na mwandishi wetu" Alijibu J Malao.

Kenge aligafirika!

Mara simu ya J ikaita,akaipokea na kisha akasikiliza kidogo na kukata.

"Bwana afande, nadhani tunahitaji kutoka kidogo hadi nyumbani kwangu" Alisema J Malao huku akiinuka kwenye kiti.

Kenge bila kufikiri akasimama na kichwani akihisi huko waendako kuna taarifa anazozihitaji.

Kama alidhani kuna taarifa zinapatikana bure alikosea sana.

Kwa kuwa J Malao hakuwa na usafiri, basi iliwalazimu watumie gari la Inspekta Kenge.


Kenge hakutaka kujishugulisha na kujua alipoelekea Sajenti Kobelo baada ya kumkuta ofisini kwa mhariri.

Makazi ya J Malao yalikuwa ni mbezi mwisho.

Baada ya foleni ya hapa na pale hatimae gari la Kenge liliingia kwenye makazi ya J Malao na kwenda kupaki pembeni kidogo ya mlango wa kuingilia ndani kwa J.

Walishuka huku wakisema mawili matatu bila kugusia lililowapeleka pale.

Waliingia ndani na J alimkaribisha Kenge.

Nyumba haikuwa na samani za bei kubwa wala haikuonekana kuwa na hadhi kubwa licha ya kupangiliwa vyema muoenekano wake wa ndani.

"Chochote ambacho ungependa kutumia tafadhali" Alisema J.

Kenge alitikisa kichwa kukataa kisha akasema.

" Nadhani ni wakati sasa wa kupeana habari kuhusu swali langu"

J alitabasamu, na hilo lilimfanya Kenge ajue ni moja ya tabia za J Malao mhariri yule wa gazeti la Chaupeku.

"Sina hakika kama maelezo yangu yanaweza kukutosheleza afande" Alisema J

Kenge alikunja sura na kufanya azidi kuonekana kituko kwa sura yake isiokuwa na mpangilio maalumu wa muonekano.

J alielewa!

"Namaanisha maelezo sina bali nina kitu ambacho nahisi kinaweza kukusaidia kufika unakokutaka" Alisema J.

"Ok unaweza kunionesha tafadhali, nipo nyuma ya muda" Alisema Kenge.

"Nisubiri kwa dakika mbili tafadhali" Alisema J huku akinyanyuka na kuelekea chumbani kwake.

Kenge alingojea sebuleni.

Ilikuwa ni dakika mbili; zikaongezeka na kuwa dakika kumi na hatime nusu saa; J hakutokea.

Kenge aliona kama ni dharau anafanyiwa.

Akaanza kuita!

Aliita midomo mitatu bila kupokea majibu na kwa kuwa alikuwa na asili ya kuwehuka kwa muda, basi hakutaka kudadisi, akanyanyuka na kumfuata huko huko chumbani.

Akasukuma mlango.

Dimbwi la damu!!

Kenge akaruka juu kwa woga na badala ya kuruka kurudi alikotoka; yeye aliruka kuvuka mwili wa J Malao na kusogea kitandani.

Eeh!!

Alibwata kwa mshangao!

Mlango ulifungwa na alipotupia macho alikutana na pande la mtu likiwa na bastola mkononi yenye kiwambo cha kuzuia sauti.

E bwana eeh!

Kenge alidata; chini kunamaiti na mlangoni kasimama mtu mwenye bastola na sio mtu tu bali ni jitu lenye sura isio na masihara hata chembe.
 
Tuko pamoja mzazi na kazi imekaa kizazi sana unanirudisha kuleeee kwa tiga mumba mkimbizi

*real is not real fake is not fake*
 
Daaah.!! Unanifanya hadi mapigo ya moyo yaende mbio broo mwendo wa mabasi ya mwendo kasi kila nisomapo mstari kwa msitari, hongera sana, kweli Kenge kakutana na likengee lenzieee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
safi sana riwaya nzuri lakini jifunze kutumia kiswahili fasaha, usitumie sana lugha za mtaani za kihuni, hakika utakuwa mwandishi nguli, tamathali za semi, methali, zinaongeza ladha
 
Nahitaji sana ushauri kama huu
Ahsante sana komredi
na kuongezea mkuu jina la riwaya limekuwa refu mno mpaka linaboa ungetafuta jina fupi linalobeba ujumbe wa riwaya kwa mfano ingekuwa mimi kutokana na mahangaiko anayopitia remi ningeita hii riwaya "REMI" ingependeza zaidi au "OPERATION SOMALIA"
 
na kuongezea mkuu jina la riwaya limekuwa refu mno mpaka linaboa ungetafuta jina fupi linalobeba ujumbe wa riwaya kwa mfano ingekuwa mimi kutokana na mahangaiko anayopitia remi ningeita hii riwaya "REMI" ingependeza zaidi au "OPERATION SOMALIA"
Jina ni fupi mbona!! Inaitwa URITHI WA GAIDI. title ya uzi ni kuvutia wasomaji tu ila sio jina la riwaya
 
Ďrdďdđfďėďďrfd Ffffr

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIWAYA; URITHI WA GAIDI

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA ISHIRINI


Kenge alibaki akimtizama yule bwana ambae alikuwa anachezesha shingo yake ambayo ilikuwa inatoa mlio kama mvunjiko wa kijiti kikavu.

Kenge alitazama vyema bastola ya jitu lile ikiwa imeenea vyema kwenye mikono yake. Kenge akapiga hesabu ni jinsi gani ataweza kuvuka maiti iliomiguuni mwake na kumfanyia shambulizi bwana yule ambae hakujua wepesi wake.

Kenge akajionya!

Akatabasamu kinyonge, hakuwa na namna.
Alitegemea jitu lile lipokee tabasamu lake kirafiki ila ndio kwanza alikutana na macho makali yaliokuwa mbali na mzaha.

"Fanya kile unachoelekezwa, tofauti na hapo unajitakia matatizo tu" Lilionya jitu lile.

Kenge akatikisa kichwa kukubaliana nae na hapo hakutaka kukaa mule, akavuka maiti ya J na kutaka kulipita jitu lile.

Kosa!

Kenge alijikuta akirudishwa nyuma kwa nguvu baada ya kupigwa kofi usoni lililoubganisha midomo na uso kiujumla.

Kenge alitoa mguno kama mbwa koko.

Kenge akagadhibika!

Kenge hajawahi kupenda dharau na akichukia huwa haoni ukubwa wa mtu ama uwezo wa mtu; Kenge aliona Katdharauliwa na jitu lile.

Akaachia ngumi nzito alioamini inaujazo wa kulitetemesha jitu lile lililokuwa limejaa kimazoezi.

Ngumi yake iliishia shingoni mwake na tofauti na matarajio yake, aliona jitu lile likichezesha tu shingo yake na kuweka bastola pembeni.

Ebanaee!!

Kenge alinywea gafla huku akijitahidi kujichekesha ili kutengeneza urafiki bandia.

Cheko lake halikusaidia!

Kenge alishikwa ukosi wa shati yake kisha akabebwa na kunyanyuliw juu kama karatasi na kutupwa kitandani ambapo alidunda mara moja na kuangukia chini.

Kenge alilia kama mbweha!

Kenge akataka kujizoa chini, ila hakufanikiwa alishikwa shati lake usawa wa mgongo kisha akanyanyuliwa tena na kutupwa kwenye kabati la nguo na kwenda nalo chini huku akisikia mvunjiko wa vioo vya kabati lile nae akitoa mguno kama mtoto anaeugulia maumivu ya bakora.

Jitu liliunguruma kwa gadhabu huku likimtizama anavyojinyanyua chini bila mafanikio.

Kenge alijitahidi kunyayuka na hatimae alifanikiwa na kukaa kitako.

Alilishuhudia jitu lile likienda kuokota bastola yake chini na kisha likamnyooshea huku uso ukiwa mbali na masihara.

Kenge aligwaya!

Jitu lile likaondoa kitunza usalama huku likianza kukenua meno kifurahia kifuatacho. Kenge hakuwa na namna zaidi ya kungojea hukumu, nguvu zake hazikuwa kitu mbele ya baunsa yule.

Mara likatokea tukio ambalo Kenge haelewi hadi leo hii lilitokeaje ila alikuja kushangaa jitu lile likijibwaga chini na kuacha bastola yake ikisambaratika chini huku ikitoa milio ya risasi bila mpangilio.
Na ndani hawakuwa wawili tena bali walikuwa ni watatu na watatu alivyoingia ndio ilimshangaza Kenge.

Alikuwa ni Sajenti Kobelo ambae alikuwa nje ya chumba kile akifuatilia kwa makini sauti za humo ndani.
Sajenti alikuwa nyuma ya msafara wa J Malao na Inspekta Kenge; na pia alifanikiwa kusogea hadi karibu na mlango na yote yaliotokea mle ndani aliyanasa vyema kabisa na sasa alikuwa ameingilia mpango wa jitu ambalo lilitaka kutoa uhai wa Inspekta kama lilivyotoa uhai wa mhariri J Malao.

Jitu lilishangaa kikumbo lilichopigwa na mtu mwenye mwili mdogo kuliko wake.

Hata!

Halijawahi kuangushwa na mwili mdogo, likajinyayua na kusimama kisha likaunguruma kwa gadhabu na kwenda kumvaa Kobelo.

Likaambulia patupu! Kobelo alikuwa mwepesi kubaini hila zake, akaepa na kusimama pembeni kisha akaruka mtindo safi wa kuambatanisha miguu yake na kulisukumia dhoruba ile lile baunsa ambapo alilipiga mbavuni.

Baunsa likaenda chini tena ila safari hii lilimwangukia Kenge na kuwa juu yake.
Kenge akaguna kwa maumivu na uzito wa baunsa lile ambalo wakati huo lilikuwa linajitikisa ili kujiinua.

Kenge akaona linamwelemea, akatumia mbinu ya kitoto kabisa, akalitekenya.
Baunsa likasimama kwa gadhabu ya kutekenywa likaachia kwenzi mujarabu ilioenda kutua utosini mwa Kenge na kumzubaisha kwa sekunde kadhaa.

Baunsa halikuwa na shida na Kenge; likajiinua tena kwa jaziba na kumwendea kwa pupa Kobelo.

Kobelo alielewa anapambana na jitu lenye nguvu, yeye alitumia akili tu ili awe bingwa wa pambano lile.

Akaruka hadi juu ya kitanda kisha akafanya kunesa kidogo na kwenda juu kisha akakunja goti na kushuka kulikabili baunsa lile.

Mbinu ilitiki.

Goti likatua kichwani mwa baunsa na kumsambaratisha chini kama kiroba cha mavi ya kuku, likabweka kama taahira.

Bahati mbaya bado ilikuwa kwa Kenge.

Baunsa alidondoka karibu na alipokuwa Kenge ambae alikuwa bado amezubaa na kwenzi ya baunsa.

Baunsa hakutaka kupigwa peke yake nae akamchapa kibao Kenge wote wakiwa chini; Kenge akarejewa na fahamu ila akakabiliana na maumivu ya shavu lake, akaachama ili upepo umwingie kinywani kumpunguzia maumivu.

Baunsa akaachana na Kenge akamvaa tena Kobelo; safari hii Kobelo hakupiga hesabu zake vyema akajikuta akijaa mikononi mwa baunsa kisha akapigwa kichwa matata pajini mwa uso wake na kuona nyota za rangi ya nyeusi.
Baunsa halikumwachia, likamnyanyua na kumtupia ukutani na kumwacha Kobelo akigugumia kwa maumivu ya dhoruba ile.

Baunsa akamfuata pale chini.

Kosa!

Kobelo kwa utalamu wa hali ya juu akaserereka kutoka alipo na kumvaa baunsa miguu mwake kisha akajiweka pembeni na kumwacha baunsa akienda chini kwa kupiga magoti na Kobelo akawa kama anainuka chini na kuacha mkono mmoja chini kisha akaachia mateke mawili kwa mpigo wa tofauti ya sekunde moja kila teke moja lilipotua shingoni mwa baunsa. Baunsa hakuwa na namna alienda tena chini kama zigo la karanga mbichi.

Bahati mbaya kwa Kenge; Baunsa akamwangukia kwenye mguu uliokuwa umejeruhiwa na vioo vya kabati..

Kenge akapiga ukunga kama bikira.

Hakuna aliemjali na Baunsa akataka kuinuka ila alichelewa alijikuta akijaa kwenye kabali ya miguu ya Kobelo ambae alimpiga kabali ya kumrukia huku amekunja miguu na alipotua alitua na shingo ya Baunsa na akapiga soti ya kubinuka, miguu ilibinuka na shingo la ulisikika mlio mmoja tu wa kuvunjika kwa kitu kikavu.

Baunsa alitikisika mara moja na kutulia.

Habari yake iliisha.

Kobelo akamfuata Kenge ambae alikuwa bado ameshika mguu kwa maumivu.

"Pole afande!!" Alisema Kobelo.

"Lakini sikukuita uje kunisaidia ujue" Alijitutumua Kenge kwa maumivu.

"Hata mimi najua, vipi umeumia" Aliuliza Kobelo.

"aah! Afande haumiagi ujue, afu ungechelewa kidogo ningemtoa nyongo huyu baunsa uchwara" Kenge alijitapa.

Kobelo alitabasamu tu na kutazama pembeni ambapo aliona mwili wa J ukiwa umelelala katikati ya dimbwi la damu.

Akaachana na Kenge ambae alikuwa anajitutumua kibwege.
Akaugeuza na kufanya kitendo cha haraka sana ambacho Kenge hakuona.

Alikwapua simu janja mfukoni mwa J na kuifutika mfukoni mwake na kuendelea kuipekuwa maiti taratibu.

"Wewe bwana mdogo acha kazi isiokuhusu, niache nimpekue mwenyewe, kesi hii ipo kwangu na sijui unaingilia kwa masilahi ya nani" Kenge alifoka.

Kobelo alijiinua taratibu bila kusema neno na kuanza kuondoka mle ndani.

"wee! tulia hapo hapo unamwachaje mkubwa wako akiwa kama hivi, ndivyo ulivyofunzwa chuoni?" Alifoka Kenge.

Kobelo alicheka tena na kumgeukia Kenge.

"Afande si useme unaogopa hilo jabali lililolala hapo? Usijali halitaamka fanya taritibu askari wengine waje hapa afande" Alisema Kobelo huku akilinyooshea kidole baunsa liliokuwa limelala bila uhai.

"Mh nani aogope, mimi au" Kenge Aliuliza kibwege tu.

Kobelo alitabasamu na kufungua mlango wa chumba na kutoka huku akiamini kabisa Kenge atadanganya watu ya kuwa yeye ndie alieliuwa lile baunsa.

Akapepea kuendelea na hamsini zake na huku nyuma Kenge akapiga simu kituoni kuomba msaada wa maaskari zaidi katika eneo lile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…