I DIED TO SAVE MY PRESDENT
Sehemu 26
Saa kumi za alfajri tayari
Elvis alikwisha amka na kuanza
kujiandaa kwa safari .Akaenda
kumgongea mlango Doreen
akamuamsha ili ajiandae kwa
safari halafu akamfuata Graca
akamjulia hali na kumtaka
ajiandae kwani saa kumi na moja
juu ya alama wangenza safari ya
kurejea Dar.Elvis akarejea
chumbani kwake na kukaa
kitandani.Bado kichwa chake
kiliendelea kusongwa na mawazo
kutokana na maongezi ya jana na
Doreen
“ Sitakiwi kuliwaza sana suala hili linaweza kunipotezea
mwelekeo mzima wa shughuli
yangu ya sasa” akawaza halafu
akaitazama saa ya kutani
iliyoonyesha ilipata saa kumi na
moja kasoro dakika
kumi.Akafunga mlango na
kuelekea chumbani kwa Doreen
“ Tangulia garini ngoja
nikamchukue Graca” akasema
Elvis halafu akaelekea chumbani
kwa Graca akagonga na kuingia
ndani.Graca alikuwa amekaa
kitandani tayari alikwisha jiandaa
“ Pole na baridi ya Mbeya”
“ Dah ! Kuna baridi kali sana”
akasema Graca na wote
wakacheka
“ Graca its time to leave”
Graca akainuka na kuinua kibegi
chake kidogo halafu akamtazama
Elvis
“ Anything wrong Graca?
Akauliza Elvis baada ya kumuona Graca akimuangalia usoni kwa
wasiwasi
“ Your friend Doreen.Do you
trust her?
“ with my life” Elvis akajibu
“ Good” akajibu Graca halafu
wakatoka wakaelekea katika gari
la Doreen,Elvis akashika usukani
na safari ya kuelekea Dar es
salaam ikaanza
****************
Ni saa tano za asubuhi katika
jiji la Dare s salaam.Kijua ni kikali
kama kawaida ya jiji hili.Katika
kasri la aliyewahi kuwa waziri
mkuu wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania ndugu Daudi
sichoma ,gari zaidi ya nane
zimeegeshwa katika eneo la
maegesho.Utulivu ulikuwa
mkubwa sana kulizunguja kasri
hili na kama ilivyo kawaida ulinzi pia ulikuwa wa kutosha
Ndani ya kasri hili kulikuwa na
ukumbi wa mikutano ambamo
Daudi Sichoma alikuwa na
mkutano na wakuu wa vyama vya
siasa vya upinzani
kwanza alianza kwa kuwashukuru
wote kwa kufika kwao halafu
akaeleka katika mada.
“ Ndugu zangu nimewaiteni
hapa ili tujadili jambo muhimu
sana kwa mustakabali mzima wa
nchi yetu na kwa uhai wa vyama
vyenu vya upinzani.Nadhani nyote
mtakubaliana name kwamba kwa
siku za hivi karibuni vyama vya
upinzani vimepoteza sana nguvu
na taswira yake katika
jamii.Chama tawala kimezidi
kujiimarisha na kuwa na nguvu
sana.Msichangae kwa nini
ninajadili nanyi mambo kama
haya wakati mimi ni mwanachama
wa chama tawala.Naomba niweke wazi kwenu kwama mahusiano
yangu na chama changu si mazuri
hata kidogo hivi sasa.Nina
wapinzani wengi ndani ya chama
ambao wanajitahidi usiku na
mchana ili wanimalize
kisiasa.Mikakati mingi inapangwa
juu yangu ili kuweza kunididimiza
kisiasa na wamefanikiwa
kuniweka nje ya ulingo wa
siasa.Nimewavumilia sana na
nimefika mwisho.Sintavumilia
zaidi .Inanilazimu na mimi
nipambane nao na ndiyo maana
nimewaiteni hapa leo hii ili
kuwapeni mikakati na uwezo wa
kukidhoofisha chama tawala.”
Akasema David na kukaa kimya
akawaangalia wanasiasa wale
halafu akaendelea
“ Rais wa Marekani
amemaliza ziara yake ndefu
kuwahi kutokea hapa nchini.Ni
ziara ya kihistora na yenye mafanikio kwa serikali zote
mbili.Katika ziara hiyo mambo
mengi yamefanyika kama vile
uzinduzi wa miradi kadhaa
mikubwa ya maendelo .Pamoja na
yote makubwa yaliyofanyika
yenye maslahi makubwa kwa taifa
letu kuna mambo makubwa
mawili yaliyomleta rais huyu
mkubwa wa Marekani” Daudi
akanyamaza akanywa maji kidogo
nakuendelea
“ kwanza kabisa amekuja
kutafuta sehemu ambayo jeshi la
marekani litajenga kambi yake
kubwa kuwahi kuwekwa barani
afrika.lengo ni kuendeleza
mapambano dhidi ya vikundi vya
kigaidi ambavyo vimeonekana
kushamiri kila uchao katika eneo
hili la afrika mashariki kati na
kusini.tayari serikali ya Tanzania
imewaahidi kuwapatia eneo hilo ili
wejenge kambi kubwa ya kijeshi” Wanasiasa wale wakatazamana
usoni.Hawakuwa wakifahamu
kuhusu suala hili hivyo
lilionekana kuwastua
kidogo.Daudi akaendelea
“ jambo la pili na kubwa zaidi
ni kwamba hivi karibuni Tanzania
imegundua kiasi kikubwa cha
mafuta kiasi ambacho
kinasemekana kinaweza kulingana
au kuzidi kiasi chote cha mafuta
ya mashariki ya kati.Ugunduzi
huo umeifanya Tanzania kutolewa
macho na mataifa makubwa na
ndiyo maana nimeona katika
kipindi hiki toka ilipogundua
mafuta kumekuwa na ziara
zisizokauka za viongozi mbali
mbali wa mataifa makubwa
akitembelea nchi yetu.Kutokana
na migogoro mingi kulikumbia
eneo la mashariki ya kati , bei ya
mafuta imepanda mara dufu
katika soko la dunia.Kutokana na migogoro hiyo mataifa makubwa
yameanza kupunguza utegemezi
wa mafuta ya kutoka mashariki ya
kati Ugunduzi wa mafuta
Tanzania umeleta matumaini
mapya kwa mataifa haya
makubwa yenye uchumi mkubwa
sana .Jambo lililomleta rais wa
marekani hapa nchini ni kuitaka
serikali ya Tanzania iruhusu
serikali ya marekani kuwekeza
katika sekta ya mafuta ya gesi na
mafuta nchini Tanzania na tayari
mikataba imekwisha sainiwa na
kwa maana hiyo sekta nzima ya
mafuta na gesi imeshikiliwa na
wamarekani.Makampuni yetu
hayana tena nafasi katika
uwekezaji huo mkubwa” akasema
David na wakuu wale wa vyama
vya siasa wakabaki wanatazamana
na minong’ono ikaanza kusikika
mle ndani.Wanasiasa wale
walionekana kustushwa sana na taarifa ile.David akafurahi moyon
kwani plani yake ilianza kufanya
kazi.Akakohoa kidogo na
kuendelea
“ Ndugu zangu nimewaiteni
hapa kwa makusudi kabisa
kuwaeleza haya yote kwani ni nyie
pekee wenye nguvu za kuyazuia
yasifanyike.Mtajiuliza mtawezaje
kuzuia mambo haya yasifanyike?
Ni kweli ni suala gumu kwa
sababu tayari serikali imekwisha
tiliana mikataba na serikali ya
marekani na hakuna namna
mtakayoweza kuitengua mikataba
hiyo lakini njia pekee hapa ni
kutumia umma kuishinikiza
serikali .Katika hilo kuna mambo
ambayo yanatakiwa yafanyike”
akanyamaza kidogo akanywa maji
na kuendelea
“ kwanza ni kuanzisha
kampeni kubwa sana nchi nzima
itakayojulikana kama mafuta yetu.Hii itakuwa ni kampeni
kubwa ambayo haijawahi kutokea
hapa nchini.Itakuwa ni kampeni
ya mkoa kwa mkoa,wilaya kwa
wilaya,kata kwa kata,kijiji kwa
kijiji,nyumba kwa nyumba na
hatimaye mtu kwa mtu.katika
kampeni hii wananchi wataelezwa
kwa kina serikali ilichokifanya
.Nawafahamu ninyi ni mahodari
wa kujenga hoja.Nataka mjenge
hoja ambazo zitaamsha hasira kwa
umma dhidi ya serikali kupinga
serikali itengue mikataba yote
iliyotiliana sahihi na serikali ya
Marekani .kampeni hii
itaambatana na maandamano
makubwa yasiyo na ukomo
.makundi makubwa ya vijana
yatachochewa kuandamana na
kuweka makambi katika viwanja
vya wazi.Maandamano hayo
yataambatana na vurugu kama
kuchoma matairi,kupiga mawe magari ya serikali kuchoma ofisi
na hivyo kuilazimisha serikali
kutumia nguvu nyingi katika
kuwatawanya makundi ya vijana
na katika mapambano hayo jeshi
la polisi litalazimika kutumia
nguvu kubwa kuwatawanya
waandamanaji na hivyo baadhi ya
raia watapoteza maisha na hivyo
itakuwa ni faida kwetu kwani
suala hili litaonekana katika
vyombo vya habari vya kimataifa
na hapo ndipo jumuia ya kimataifa
itakapoingilia katika suala hilo na
kuishinikiza serikali ya Tanzania
iachane na mipango yake serikali
italaumiwa kwa kukiuka haki za
binadamu na kwa kiasi kikubwa
wananchi hawatakuwa na imani
na serikali yao tena na endapo
utafanyika uchaguzi ninyi
mtakuwa na nafasi kubwa sana ya
kushinda uchaguzi mkuu.Nadhani
huu ni mpango mzuri sana.Nyie mnauonaje mpango huu? Akauliza
Daudi.wanasiasa wale
wakatazamana na nyuso zao
zikaonyesha
tabasamu.walionekana kuufurahia
mpango ule.kwa dakika kama nne
hivi walikuwa wakisemezana wao
kwa wao
“ ndugu zangu nadhani
itakuwa vyema kama nikaawacha
kwa muda ili mlijadili suala hili
kwa muda namna mnavyoweza
kulitekeleza.Nitarejea baada ya
muda mfupi” akasema Daudi na
kutoka nje akawaacha wanasiasa
wale wakijadiliana .
Akiwa nje ya ukumbi Daud
akachukua simu yake kazitafuta
namba za simu za Frank
akampigia
“ hallow David “ akasema
Frank
“ halow Frank habari yako?
Habari za toka jana? “habari nzuri daud.mambo
yanakwendaje?
“mambo yanakwenda vizuri
na nimekupigia kukutaarifu
kwamba tayari nimekwisha ianza
kazi.Hivi niongeapo tayari niko na
wakuu wa vyama vya
siasa.Nimeanza nao na hivi sasa
nimetoka nje nimewaacha
wakijadiliana”
“thats great news
David.Nilijua tu mpango huu bila
ya wewe katu hatuwezi kufanikiwa
.Umeonaje mwelekeo wa hao
wanasiasa?
“ Bila shaka watakubaliana
nami.Baada ya muda mfupi
nitarejea tena ndani ili kufahamu
wameamua nini” akasema David
“ Ok David .kazi nzuri
sana.Natumai kwa kupitia wewe
mpango wetu utafanikiwa
“ Ahsante kwa kuniamni na
kunishirikisha.Jioni ya leo nitakuwa na kikao na makamu wa
rais.Nimekwisha ongea naye na
kupanga kukutana naye jioni ya
leo.Nina hakika hata naye
atakubaliana na mpango
huu.Nitakupigia tena simu baada
ya kumaliza kikao na hawa
wanasiasa” akasema Daudi na
kukata simu
Mara tu baada ya kumaliza
kuongea naFrank simuni David
akarejea tena katika chumba cha
mikutano alikowaacha wanasiasa
wakijadiliana.
“ ndugu zangu nadhani
mpaka sasa kuna jambo mtakuwa
mmekwisha lijadili “ akasema
David baada ya kuketi kitini
“ Tumejadiliana na
tumekubaliana na mawazo
yako.Hiyo ndiyo kazi ya vyama vya
upinzani,kuidhoofisha serikali
iliyoko madarakani.Tuko tayari
kwa ajili ya operesheni hiyo” akasema ndugu Makwa Tusangira
mwenyekiti wa chama kikubwa
cha upinzani Tanzania kwa niaba
ya wenzake
“ pamoja na kukubaliana
kuifanya operesheni hii lakini
kuna changamoto ya
kifedha.Kama ujuavyo vyama
vyetu vingi havina vyanzo vya
mapato zaidi ya kutegemea ruzuku
ya serikali kwa maana hiyo basi
uendeshaji wa vyama unakuwa
mgumu sana achilia mbali
operesheni kubwa kama hii.Pili
changamoto nyingine ni ya
kiusalama.Nina hakika kwamba
mara tu vuguvugu hili
litakaposhika kasi na kusambaa
mkoani ,serikali lazima
itawatafuta waasisi wa vurugu
hizo kwa hiyo lazima tutatiwa
nguvuni.Hizo ni changamoto
kubwa ambazo endapo tutazitafutia ufumbuzi basi
operesheni hii itakuwa na
mafanikio makubwa” akasema
Makwa.David akatabasamu na
kusema
“ kwanza kabisa niruhusuni
niwashukuru kwa kukubali
kwenu kuifanya operesheni hii
muhimu kwa taifa
letu.Changamoto hizo ulizozisema
ni changamoto ambazo lazima
tuzitafutie ufumbuzi wa
haraka.Kuhusu suala la fedha
nawaomba msiwe na wasi wasi
ninataka mkae na mtengeneze
bajeti ya kutosha kufanikisha
zoezi hili na mniletee.Pesa ipo ya
kutosha msihofu.Nileteeni vile vile
mchanganuo namna operesheni
itakavyofanyika nchi
nzima.Kuhusu suala la usalama
kwamba mnaweza kutafutwa na
kuwekwa kizuizini msiwe na
shaka na hilo pia.Baada tu ya kuuwasha moto na ukasambaa
nchi nzima nyie mtaondoka kwa
siri nchini na mtapewa hifadhi
nchi za nje na operesheni
itaendelea kuongozwa na vongozi
wa chini.Hakuna atakayegundua
kwamaba mmeondoka nchini na
mtaendeleza hareakati mkiwa nje
ya nchi.jambo lingine ambalo
nilisahau kuwaambieni ni kwamba
sambamba na harakati hizo
,tutavishawishi pia vyama vya
wafanyakazi kuendesha mgomo
wa wafanyakazi wa nchi nzima wa
umma na wa binafsi kushinikiza
serikali iliyopo madarakani
kuachia ngazi na hiyo itakuwa ni
fursa kwenu kuingia
madarakanibaada ya uchaguzi
kufanyika kwani tayari mtakuwa
juu kisiasa ” akasema Daud
Kikao kile kati yake na wakuu wa
vyama vya siasa kiliendelea hadi
ilipotimu saa kumi na moja za jioni ndipo kilipomalizika.wakuu
wale wa vyama vya siasa wote
nyuso zao zilikuwa zimetawaliwa
na tabasamu zito nahasa baada
ya kila mmoja kukabidhiwa
bahasha iliyotuna ambayo ndani
yake kulikuwa naiasikikubwa cha
pesa. Walipeana mikono
kupongezana kwa kikao kile
chenye manufaa makubwa kwao
na kisha wakaagana kwa miadi
ya kuonana naye tena baada ya
siku nne watakapokuwa tayari
wamekaa kikao na kutengeneza
bajeti ya operesheni nzima
*********************
Saa mbili za usiku
Elvis,Doreen na Graca wakawasili
jijini Dar e s salaam wakitokea
Mbeya.Ilikuwa ni safari ndefu
.Elvis ndiye aliyekuwa dereva siku
hii akimsaidia Doreen Welcome home Graca”
akasema Elvis .Graca
akatabasamu.uso wake
ukaonyesha furaha ya kurejea
tena ndani ya jiji hili halafu
akanyong’onyea baada ya
kukumbuka mambo yaliyomkuta
na kubwa zaidi lililomuogopesha
ni kuhusu usalama wake
Hatimaye wakawasili nyumbani
kwa Doreen.Graca aliyeonekama
kuchoka sana alipelekwa
chumbani kupumzika halafu
Doreen akarejea sebuleni
alikomuacha Elvis
“ Doreen ahsante sana kwa
msaada wako Bila wewe nina
hakika kazi yangu ya kumsafirisha
Graca ingekuwa ngumu sana”
akasema Elvis
Doreen akatasamu na kusema
“ Hupaswi kunishukuru
Elvis.Nimefanya kile
ninachopaswa kukifanya na nimefurahi kuwa sehemu ya
msaada kwako.”
“ Ahsante sana
Doreen.Mungu akubariki sana”
akajibu elvis na wote wakakaa
kimya
“ Elvis unakwenda kulala
nyumbani kwako usiku huu?
Akauliza Doreen.Alvis akanima
akafikiri kidogo na kusema
“ Natamani kama
ningekwenda nyumbani nikaonane
na mke wangu Patricia lakini
siwezi kufanya hivyo.Natakiwa
kumlinda Graca kwa kila namna
niwezavyo.Endapo watu
wanaomtafuta watagundua
kwamba Graca yuko hapa
hawatapoteza hata dakika moja
watafika na kuwadhuru wote
watakaowakuta.Sitaki hilo litokee
kwa hiyo nitalala hapa kuwalinda
wewe na Graca.Kuhusu sehemu
ya kulala usipate shida kabisanitalala hapa hapa
sofani.Nimekwisha zoea kukesha
macho” akasema Elvis
“ Elvis tafadhali usinielewe
vibaya kukuuliza vile.Nashukuru
kwa kuamua kulala hapa usiku
wa leo na kutulinda.Hapa ni
nyumbani kwako na siku zote
unamuda wowote.Nyumba yangu
ni kubwa na ina vyumba vya
kutosha vya kulala na endapo
ukipenda unaweza hata kulala
chumbani kwangu” akasema
Doreen na wote wakaangua
kicheko
“ Usijali Doreen hapa sebuleni
panatosha sana” akasema Elvis
“ Elvis tutaongea baadae kwa
sasa ngoja nikawaandalie chakula
cha usiku .Wakati naanda chakula
naomba nikupeleka chumbani
kwangu ukaoge na upumzike
kidogo kuondoa uchovu wa safari”
akasema DoreenUhhmmm Doreen kuna
jambo nataja
kukuomba.Ninaomba umpigie
simu Patricia na kumjulia hali ila
usimweleze chochote kuhusiana
na mimi kuwapo hapa kwako wala
safari ya Mbeya.”akasema Elvis
“ Sawa Elvis,nitampigia
.Twende chumbani ukaoge”
akasema Doreen na kumuongoza
Elvis hadi chumbani
kwake.Kilikuwa ni chumba
kikubwa na kizuri
“ Chumba chako kizuri sana
Doreen.Hongera sana”
“ Ahsante Elvis lakini
hakiwezi kuzidi kile cha Patricia.”
Akasema Doreen na kumfungulia
Elvis mlango wa bafu akamuacha
akioga na yeye akaelekea jikoni
kuandaa chakula cha usiku
Baada ya kumaliza kuoga
Elvis akarejea sebuleni.Kichwa
chake kilikuwa na mawazo mengi na mara akainga Doreen na
kumkuta Elvis pale sebuleni
“ Elvis ,mbona umetoka
chumbani ? unaogopa
nini?Unatakiwa upumzike safari
ilikuwa ndefu sana”akasema
Doreen.Elvis akatabasamu
“ Usijali Doreen,hata hapa
panatosha sana kupumzika.Vipi
umempigia simu Patricia?
“Ndiyo nimempigia na
anaendelea vizuri na hana tatizo
lolote”
“ Ahsante sana” akajibu Elvis
.Doreen akaendelea kumtazama
usoni
“ Mbona unanitazama hivyo
Doreen? Akauliza Elvis
“ uhhmm !! its nothing.Ngoja
na mimi nikaoge halafu
tutajumuika sote mezani kwa
chakula cha
usiku”akasemaDoreen nakuelekea
chumbani kwake kuoga.Kisha oga wote watatu wakajumuika katika
chakula cha usiku na baada ya
kumaliza kula wakaelekea
sebuleni
“ Graca pole sana na safari
ndefu “ akaanzisha maongezi
“ Ahsante sana Elvis.Pole
sana nawe Kuendesha gari umbali
ule mrefu si kazi ndogo”
“Ahsante ila mimi nimekwisha
zoea safari kama hizi” akajibu
Elvis
“ This is your house? Akauliza
Graca
“ hapana Graca hapa si
nyumbani kwangu.Hapa ni
nyumbani kwa Doreen’
“ wewe na Doreen ni
wapenzi?akauliza graca
“ hapana ,sisi si wapenzi bali
ni marafiki wakubwa.Mimi tayari
nina mke wangu anaitwa
Patricia”akasema Elvis
Graca akamtazama Elvis usoni na kusema
“kwa hiyo utaniacha hapa na
kwenda nyumbani kwako?Are you
sure I’m safe here? Elvis
akatasabamu kama kawaida
yakena kusema
“Usihofu Graca Sintaondoka
na kukuacha hapa peke
yako.Nilikuhakikishia usalama
wako kwa hiyo nitaendelea
kukulinda.Kuhusu usalama hapa
ni sehemu salama sana lakini
kesho tutahamia katika sehemu
salama zaidi ya hii .Kuna nyumba
ambayo nimeinunua maalum kwa
ajili yako na ndipo utakapoishi
hadi hapo tutakapofanya mpango
mwingine kuhusiana na maisha
yako kwa hiyo usihofu kitu
chochote”
Tabasamu kubwa likajengeka
usoni mwa binti yule mrembo kwa
maneno yaleya Elvis
“Ahsante sana Elvis kwa msaada wako mkubwa.katika
misha yangu sijawahi kukutana
na mtu mwenye moyo wa huruma
kama wewe”
“ Usijali Graca,ni jukumu
langu kukusaidia” akajibu Elvis
halafu kukawa kimya
“ mkeo anajua kwamba uko
hapa?akauliza Graca
“ hapana hafahamu”
“ kwa nini hujamwambia
.Dont you trust her?
“ I do trust her with my life
lakini kwa sasa siwezi kumweleza
chochote kuhusiana na suala
lako.Nitamfahamisha muda
ukifika”akasema Elvis
“ Ok Elvis nadhani kesho
tutakuwa na muda mzuri zaidi wa
kuongea.Kwa sasa nimechoka
sana naomba
nikapumzike”akasema Graca
akainuka na kuelekea chumbani
kupumzika.Baada ya dakika tano Doreen akaingia sebuleni
“ Elvis tayari nimekwisha
kuandalia chumba cha kulala
ukapumzike.Safari ilikuwa ndefu
sana “akasema Doreen
“Ahsante Doreen lakini
nitakaa hapa hapa sebuleni
kuhakikisha usalama wenu
usihofu kuhusu mimi.Hizi ni kazi
zangu na nimekwisha
zizoea.tafadhali nenda kalale
upumzike”
“hapana Elvis huwezi kukaa
hapa sebuleni peke yako usiku
kucha.Usalama hapa ni mkubwa
tu.Nyumba zote za hapa jirani
tumeweka walinzi kwa hiyo
usalama kuzunguka eneo hili ni
mkubwa”akasema Doreen
“ Doreen tafadhali usihofu.I’ll
be fine.Nenda kapumzike.Kesho
tutakuwa na siku ndefu
kidogo.Vipi kuhusu kazini kwako?
Hakuna tatizo ?akauliza Elvisa hakuna tatizo lolote
kazini.Nimekwisha omba ruhusa
ya siku kumi”akasema Doreen
“ ahsante sana,Sasa nenda
kapumzike”akasema Elvis huku
akiufungua mlango na kutoka nje
akaikagua nyumba yote
kuhakikisha iko salama halafu
akarejea sebuleni akazima kila
kitu kukawa na ukimya .
******************
Kumepambazuka na siku
mpya imeanza.Saa kumi na mbili
za asubuhi ilimkuta Elvis akiwa
macho.Usiku mzima hakuweza
kufumba macho akihakikisha
Graca na Doreen wanakuwa
salama.
“habari yako Elvis” Doreen
akamsalimu Elvis .
“ Ouh Doreen umeamkaje?
Akauliza Elvis huku akijinyoosha kwa uchovu
“ Pole sana kwa uchovu wa
usiku Elvis”
“usijali Doreen umeamka
salama lakini?
“ Niko salama kabisa Elvis”
“Nafurahi kusikia hivyo”
“ Elvis nadhani ungeenda
chumbani upumzike walau
kidogo.usiku mzima umekesha
hapa ukitulinda”
“ Ahsante sana Doreen lakini
huu si wakati muafaka wa
kupumzika.Dakika moja tu
inatosha sana kwa watu
wanaomtafuta Graca kuingia na
kumfanyia chochote.I cant let that
happen”akasemaElvis .Doreen
akamtazama kisha akasema
“basi twende ukaoge
tujiandae na siku ya leo”akasema
Doreen akamuongoza Elvis hadi
chumbani kwake.wakati Elvis
akiendelea kuoga Doreen akaenda kumuamsha Graca
Saa mbili za asubuhi wote
watatu wakajumuika mezani
wakapata kifungua kinywa .
“Graca ,tukitoka hapa
tunaelekea katika nyumba
ambayo utakuwa ukishi hadi hapo
tutakapokufanyia utaratibu
mwingine wa kwenda nje ya nchi
.Uwepo wako hapa nchini
unatakiwa uwe ni wa siri
kubwa”akasema Elvis wakiwa
mezani wakiendea kupata
kifungua kinywa
“ Ahsante sana Elvis.Lakini
nina swali nataka kuuliza”
“Uliza usihofu Graca”
“katika nyumba hiyo
unayonipeleka nitaishi na nani?
Nitaishi peke yangu?
Elvis na Doreen
wakatasamana,halafu Elvis
akasema
“ hapana hautakuwa peke yako,nitakuwa pamoja nawe.”
“Vipi kuhusu mkeo na
watoto?akauliza Graca
“ Usijali kuhusu
hilo,hakutakuwa na tatizo lolote.”
Akajibu Elvis
Waliendelea kupata kifungua
kinywa na walipomaliza wakaingai
katika gari la Doreen
wakaondoka.Breki ya kwanza
ilikuwa katika ofisi za kampuni ya
ulinzi ambako Amanda rafikiye
Doreen aliacha funguo za nyumba
aliyomuuzia Elvis.Doreen
akajitambulisha na akakabidhiwa
funguo kwani taarifa zake tayari
zilikuwepo pale ofisini.Kishapata
funguo safari ikaendelea kuelekea
katika jumba lile
“ wale jamaa wameniuliza
kama tutapenda kuingia mkataba
wa kuilinda nyumba ile kwani
mkataba wao na Amanda
umekwisha sitishwa.Sijawapa jibu nimewaambia wasubiri kwanza
tujadiliane”
“ Good.hakuna haja ya kuwa
na ulinzi.Graca nitamlinda
mwenyewe” akasema elvis.
Hatimaye wakawasili katika
jumba lile kubwa na la
kupendeza.Jumba lile lilikuwa
limezungukwa na ukuta mkubwa
wenye rangi yeupe na juu ya
ukuta kulikuwa na nyaya kwa ajili
ya usalama.
“wow ! what a wonderfull
place!! ELvis akasema kwa furaha
baada ya kuingia ndani ya jumba
lile na kuishuhudia mandhari
nzuri ya kupendeza.Katika
nyumba ile kulikuwa na vyumba
vinne vya kulala,sebule ,chumba
cha maongezi,maktaba,sehemu ya
kufulia,jiko,gereji ya gari na
chumba maalum kwa ajili ya
ibada.Elvis alifurahi mno kuipata
nyumba kama ile.Ingemfaa sana katika kazi zake
“Ahsante sana
Doreen.Nyumba hii ni nzuri sana
na inafaa.Ina kila kitu
ninachokihitaji”akasema Elvis.
“There is one more thing’
akasema Doree
“ whats that? Akauliza Elvis
“ Kuna chumba cha chini kwa
chini kwa ajili ya usalama.Endapo
usalama ukiwa tete basi unangia
katika chumba cha chini”
Elvis akashindwa kujizuia
furaha yake na kujikuta
amemkubatia Doreen halafu
wakaelekea katika chumba
kikubwa cha kulala .katika ukuta
wa kile chumba kulikuwa na kifaa
Fulani mithili ya mita ya umeme
.Doreen akabonyeza namba
kadhaa na mara sehemu ya
sakafu ikafuguka .Wote wakabaki
na mshangao mkubwa.Kulikuwa
na ngazi za kushuka chini.Taratibu wakaifuata ngazi
ile na kukutana na varanda
ambalo mbele yake kulikuwa na
mlango ambao nao ulifunguliwa
kwa namba ,wakaingia katika
chumba kikubwa na kizuri chenye
kila kitu
“ I lovethis place” akasema
Graca
“ Doreen unastahli pongezi
kubwa .nyumba hii ni sahihi
kabisa kwa mimi kuishi.” Akasema
Elvis halafu wakarejea sebuleni
“ sasa Doreen kuna mambo
ambayo nataka uyafanye kwa siku
ya leo”
“ usijali elvis .I’m at your
service” akasema Doreen huku
akitabasamu
“ Nataka upite madukani
umfanyie Graca manunuzi
.Mnunulie nguo nzuri ,viatu
vipozodi na kila utakachoona
kinamfaa.Baada ya hapo ufanye pia manunuzi ya chakula na
vinywaji vya kututosha kwa wiki
mbili au zaidi.”akasemaElvis
akachukua kompyta ya Doreen na
kufungua akaunti yake
akapunguza shilingi milioni tatu
na kuzituma katika akaunti ya
Doreen
“ Elvis basi ngoja niwahi
nikaanze kufanya manunuzi
hayo.Nina hakika sintakawia
sana.Una mpango wa kutoka
baadae?
Elvis akafikiri kidogo na
kusema
“ Kama ikinilazimu kutoka
nitatumia gari la Amanda”
“ sawa .Amanda aliniambia
kwamba gari lake ni zima na
halina tatizo lolote”akasema
Doreen akachukua vipimo vya
Graca na kutoka mle
sebuleni.Elvis akamsindikiza hadi
garini “ Elvis are you sure you want
to live here? Akauliza Doreen
“ Itanilazmu kufanya hivyo
kwa kipindi hiki ambacho Graca
atakuwa hapa.Dhamana yote ya
usalama wake nimeibeba mimi
kwa hiyo natakiwa nimlinde kwa
kila namna kwani ndivyo
nilivyomuahidi”
“ Vipi kuhusu Patricia?
atakuelewa?
“ najua itakuwa ngumu
kwake kunielewa lakini sina
namna nyingine ya kufanya.Graca
anazo taarifa nyeti sana kwa hiyo
anatakiwa alindwe” akasema
Elvis.Doreen akamtazama usoni
na kusema
“ Una hakika taarifa hizo zina
umuhimu mkubwa kiasi cha
kukufanya ujitoe namna hii?
“ Doreen naomba usinielewe
vibaya lakini taarifa alizonazo
Graca ni za muhimu sana kwangu na nchi kwa jumla”
“Ok Elvis.Tutaonana baadae”
akasema Doreen na kuingia garini
akaondoka .Elvis akarejea
sebuleni alikomuacha Graca
“ Nyumba hii ni nzuri sana
.nani alikuwa akiishi hapa?
Akauliza Graca
“Kuna mzungu mmoja ndiye
aliyekuwa akiishi hapa na sasa
amerejea kwako”
“ Ni nyumba nzuri
sana.Nimeipenda” akasema Graca
“ hii ndiyo sehemu salama
ambayo nilikuahidi kwamba
utaishi.Hakuna mtu yeyote
atakayejua kama uko
hapa.Pamoja na usalama uliopo
lakini nitafunga pia kamera za
ulinzi kila kona ili kuzidisha ulinzi
zaidi.”
“ Ahsante sana Elvis kwa
namna ulivyojitahidi kunisaidia
Sijui nitakulipa kitu gani”akasemaGraca
“ Usiwaze sana kuhusu
kulipa.Nimefanya kile ambacho
ninapaswa kukifanya.”akasema
Elvis.Kikapita kimya cha sekunde
kadhaa Elvis akasema
“ Graca nimetimiza ahadi
yangu.Nilikuahidi kukutoa pale
hospitali afrika kusini na
kukupeleka sehemu salama.You
are safe now.Now it’s your turn to
tell me everything you know about
your father ”akasema Elvis
Graca akainama akazama
mawazoni halafu akainua kichwa
na kusema
“ Katika familia yetu
tulizaliwa watoto wawili tu mimi
na kaka yangu Edwin.Wakati bado
ninasoma Edwin akajiunga na
jeshi na kwa bahati mbaya
alifariki katika maozezi ya kijeshi
wakati wakipanda mlimaKilimanjaro kwa kuangukiwa na
mawe yaliyokuwa yakiporomoka
na kuwaponda yeye na wenzake
wawili ambao wote walipoteza
maisha.Nilibaki mimi peke
yangu.Maisha yetu yalikuwa
mazuri na hatukuwa na tatizo
lolote.Kila nilichokitaka nilikipata”
Akanyamaza akameza mate na
kuendelea
“ Siku moja ulitokea ugomvi
kati ya baba na mama.Sikujua
chanzo cha ugomvi huo lakini
nilisikia mama akimlalamikia baba
kwamba aachane na mambo yake
anayoyafanya.Sikujua ni mambo
gani hayo ambayo mama alimtaka
baba kuachana nayo.Nilidhani
labda ni mambo yao ya
wanandoa,yawezekana labda baba
akawa na mwanamke mwingine nje ya ndoa.Sikuwahi kumuuliza
mama sababu ya ugomvi
wao.Maisha yaliendela kama
kawaida lakini mama alionekana
kubadilika sana.Hakuwa katika
hali yake ya kawaida
niliyomzoea.Niligundua kuna
jambo lililokuwa
linamsumbua.Nilijaribu sana
kumdadisi aniambie ni kitu gani
kilichokuwa kinamsumbua lakini
hakunieleza chochote.Siku moja
baba aliwahi kuondokana
kusahau funguo za chumba chake
ambacho huingia yeye
pekee.Chumba hicho amehifadhi
vitu vyake muhimu zikiwemo
nyaraka zake nyingi.Mama aliingia
katika kile chumba na kuanza
kupekua,akatoka na mkoba
uliokuwa na kompyuta ndogo ndani yake.Akanipatia mkoba ule
na kunitaka niufiche mahala
ambako hakuna yeyote anayeweza
kuuona.Alinisisitiza sana kwamba
nisimuonyeshe mtu yeyote
.Niliuchukua mkoba ule na
kwenda kuuhifadhi kwa rafiki
yangu Salha.Kumbe katika kile
chumba cha baba kulikuwa na
kamera ndogo ambayo iliweza
kuchukua picha za kila anayeingia
mle chumbani wakati baba akiwa
hayupo na kumtumia baba moja
kwa moja katika simu yake kwa
hiyo baba aliweza kugundua
kwamba mama aliingia mle katika
ofisi yake na akachukua kompyuta
yake ndogo.” Akasema Graca
halafu akanyamaza kidogo na
kuendelea Jioni ya siku ile kulitokea
tena ugomvi mkubwa sana baba
akitaka mama arudishe kompyuta
yake ndogo aliyoichukua toka
ofisini kwake.Mama alikataa kata
kata kwamba hakuchukua
kompyuta ile lakini baba
akamuonyesha picha
zilizochukuliwa na kamera lakini
bado mama alikataa kwamba
hakuchukua ile
kompyuta.Nilitamani nimwambie
baba kwamba kompyuta yake
ninayo mimi ili kuumaliza ule
ugomvi lakini nikaogopa kwa
namna alivyokuwa
amekasirika.Nilikumbuka pia
kwamba mama aliniambia kwa
namna yoyote ile nisithubutu
kumpa mtu yeyote kompyuta ile
hadi hapo atakaponipa maelekezo yake” Graca akanyamaza kidogo
halafu akaendelea
“ wakiwa chumbani nilimsikia
mama akimtaka baba aachane na
biashara haramu alizokuwa
akifanya.Moja kwa moja akili
yangu ikanituma kwamba huenda
baba akawa anajishughulisha na
biashara ya madawa za kulevya na
ndiyo maana akawa na utajiri
mkubwa tofauti na kipato chake
anacholipwa kama
mwanajeshi.Baada ya siku hiyo
hakukuwa tena na maelewano
baina ya mama na baba kwani kila
mmoja alianza kulala chumba
tofauti na mwenzake.Niliendelea
kumdadisi mama chanzo cha
ugomvi wao na biashara haramu
ambayo baba anaifanya lakini
hakuwa tayari kuniambia bali alinisihi niendelee kuitunza
kompyuta ile kwani ndiyo yenye
kila kitu kuhusiana na
anachokifanya baba.Baada ya wiki
tatu alipata safari ya kwenda
Morogoro na akiwa njiani
alinitumia ujumbe mfupi kwamba
atakaporejea atanieleza kila
kitu.Hayo yalikuwa ni mawasiliano
yake ya mwisho kwani mama
hakurejea tena.Alipata ajali na
kufariki.Nina uhakika mkubwa
kwamba baba alihusika katika
ajali ile iliyosababisha kifo cha
mama kwani kabla sijapata taarifa
za kifo cha mama alinifuata na
kunitaka nimueleze mahala ilipo
kompyuta aliyonipa
mama.Nilikana kutofahamu
chochote lakini baba
akaninyang’anya simu na kunionyesha meseje niliyotumiwa
na mama.Nilijiuliza sana alijuae
kama mama alinitumia ujumbe
ule? Alinitolea vitisho vingi sana
lakini sikuogopa na niliendelea
kukana kupewa kompyuta na
mama.Jioniya siku ile ndipo
nilipopewa taarifa za kifo cha
mama.Niliumia sana”
akanyamaza kidogo na kufuta
machozihalafu akaendelea
“ Baada ya kumaliza msiba
alinifuata tena na kuendelea
kunitisha ili nimpatie ule mkoba
lakini bado niliendelea kukana
kupewa mkoba wowote na
mama.Vitisho vilipozidi ikanibidi
kwenda kuichukua kompyuta ile
kwa Salha na kuificha kwa mpenzi
wangu David.Niliamini kule
itakuwa salama.Kabla ya kuipeleka kwa David ilinilazimu
kwanza kuiwasha na kuangalia ni
kitu gani kilichokuwamo ndani
yake na nikastuka sana kwa
nilichokigundua” akasema Graca
“ Uligundua nini Graca?
Akauliza Elvis
“ Kupita kompyuta ile
niligundua kwamba baba
amekuwa akijishughulisha na
biashara ya kuuza silaha.Yeye na
wenzake wamekuwa wakifanya
biashara hii kwa muda mrefu na
ndiyo chanzo cha utajiri wake
mkubwa.Niligundua kwamba
silaha hizo wamekuwa wakiziagiza
toka nje ya nchi na kisha
huziingiza hapa nchini kama
silaha za jeshi la Congo na kisha
huzisafirisha kuzipeleka kwa
waasi wanaopigana na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
na kujipatia fedha nyingi
sana.Hiyo ndiyo biashara ambao
mama alikuwa akimkanya baba
kuacha kujihusisha nayo.” Graca
akanyamaza akainama chini.Elvis
akahisi shati lake linaanza kuloa
jasho.Ilikuwa ni taarifa yenye
kustusha sana.Graca akainua
kichwa halafu akasema
“ Siku moja usiku baba
akanikamata akanifungia katika
chumba kimoja akanitesa sana
akinitaka nimuonyeshe mahala
ilipo kompyuta yake.Alinipiga sana
usiku huo lakini sikumweleza
chochote.Alipoona nimegoma
kumpa jibu akaniacha.Alfajiri na
mapema nikawahi kwa David na
kumuomba anipe ile kompyuta
yake.Kumbe wakati naenda kwa David kuna watu walikuwa
wananifuatilia.Nikiwa chumbani
kwa David watu wale waligonga
mlango kwa nguvu ,David
akanipitishia dirishani nikakimbia
pamoja na kompyuta ile.Na
asubuhi ile ndio ulikuwa mwisho
wa mimi kuonana na David kwani
alikamatwa na kufunguliwa
shtaka la kumbaka mwanafunzi
yaani mimi” Graca akainama
akafuta machozi na kuendelea
“ Nilipotoka pale kwa David
nikaelekea moja kwa moja kwa
padre kalistus ambaye ndiye
paroko wa parokia yetu na
ananifahamu vyema.Aliponiona
katika hali ile alistuka sana lakini
sikumueleza chochote kuhusu
kilichonipata ,nilichomuomba kwa
wakati ule ni anihifadhie ile kompyuta na asijaribu kuifungua
ndani.Aliniahidi kufanya kama
nilivyomuomba halafu
nikaondoka.Ni hapo ndipo
nilipolazimika kujifanya mgonjwa
wa akili”
Graca akafuta machozi na
kuendelea
“Nilipelekwa hospitali ya
magonjwa ya akili na nikaanza
kudungwa sindano wakiamni
mimi nina matatizo ya akili.Baada
ya wiki moja nikapandishwa ndege
na kupelekwa afrika kusini katika
hospitali ile ulikonitoa” akasema
Graca.
“ Pole sana Graca.Simulizi
yako imenisikitisha sana
sana.Sikutegemea kama baba
yako anaweza kuwa na roho mbaya kiasi hicho.Nakupongeza
kwa ujasiri wako”
“ Ahsante sana Elvis.kwa sasa
najiona nimeutua mzigo mzito
sana na nimeufikisha sehemu
husika.Nilikuwa nikijiuliza sana
sehemu ambayo ninaweza kwenda
kuripoti kuhusu jambo hili lakini
nashukuru Mungu amekuleta
wewe .Tafadhali Elvis naomba
ulifanyie kazi jambo hili na
uhakikishe wahusika wote
wanachukuliwa hatua ukianzia na
baba yangu.” Akasema Graca
“ Graca ninashukuru sana
kwa kuniamini na kunieleza
mambo haya mazito.” Akasema
Elvis
“ Unayepaswa kushukuriwa
ni wewe kwani bila wewe
nisingeweza kuondoka palehospitali” akasema Graca kikapita
kimya Elvis akamtazama Graca na
kusema
“ Graca taarifa hizi
ulizonipatia ni taarifa nzito sana
na ninakuahidi kuzifanyia kazi
kiukamilifu.Maelfu ya raia wa
jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo
wamekuwa wakiuawa na waasi
ambao wanatumia silaha
wanazouziwa na Frank na kundi
lake.Lazima nihakikishe kwamba
wote wanaohusika na mtandao
huu wanatiwa hatiani na
wanahukumiwa kwa makosa
wanayoyafanya” akasema Elvis na
kunyamaza kifupi kisha akauliza
“ Ulisema kompyuta ile
uliipeka kwa padre?
“ Ndiyo.Nilimpa Padre kalistus
anitunzie” Nitahitaji kuipata kompyuta
hiyo ili niweze kukusanya taarifa
za kutosha kuhusiana na jambo
hili.Kwa maana hiyo itatutalzimu
kwenda kuichukua.usiwe na hofu
yoyote ukiwa na mimi” akasema
Elvis
“ Hakuna tatizo Elvis
tunaweza tukaenda.” akasema
Graca.Elvis akaelekea katika
chumba cha gari ambamo
kulikuwa na gari aliyoiacha
Amanda.Ilikuwa ni gari nzuri.
“ Wow ! what a nice car”
akasema Elvis huku
akitabasamu,akalikagua gari lile
na kuhakikisha liko vizuri.Akalitoa
nje kisha wakaondoka kuelekea
kwa padre Kalistus
*****************