Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE MY PRESDENT

Sehemu 26


Saa kumi za alfajri tayari
Elvis alikwisha amka na kuanza
kujiandaa kwa safari .Akaenda
kumgongea mlango Doreen
akamuamsha ili ajiandae kwa
safari halafu akamfuata Graca
akamjulia hali na kumtaka
ajiandae kwani saa kumi na moja
juu ya alama wangenza safari ya
kurejea Dar.Elvis akarejea
chumbani kwake na kukaa
kitandani.Bado kichwa chake
kiliendelea kusongwa na mawazo
kutokana na maongezi ya jana na
Doreen
“ Sitakiwi kuliwaza sana suala hili linaweza kunipotezea
mwelekeo mzima wa shughuli
yangu ya sasa” akawaza halafu
akaitazama saa ya kutani
iliyoonyesha ilipata saa kumi na
moja kasoro dakika
kumi.Akafunga mlango na
kuelekea chumbani kwa Doreen
“ Tangulia garini ngoja
nikamchukue Graca” akasema
Elvis halafu akaelekea chumbani
kwa Graca akagonga na kuingia
ndani.Graca alikuwa amekaa
kitandani tayari alikwisha jiandaa
“ Pole na baridi ya Mbeya”
“ Dah ! Kuna baridi kali sana”
akasema Graca na wote
wakacheka
“ Graca its time to leave”
Graca akainuka na kuinua kibegi
chake kidogo halafu akamtazama
Elvis
“ Anything wrong Graca?
Akauliza Elvis baada ya kumuona Graca akimuangalia usoni kwa
wasiwasi
“ Your friend Doreen.Do you
trust her?
“ with my life” Elvis akajibu
“ Good” akajibu Graca halafu
wakatoka wakaelekea katika gari
la Doreen,Elvis akashika usukani
na safari ya kuelekea Dar es
salaam ikaanza
****************
Ni saa tano za asubuhi katika
jiji la Dare s salaam.Kijua ni kikali
kama kawaida ya jiji hili.Katika
kasri la aliyewahi kuwa waziri
mkuu wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania ndugu Daudi
sichoma ,gari zaidi ya nane
zimeegeshwa katika eneo la
maegesho.Utulivu ulikuwa
mkubwa sana kulizunguja kasri
hili na kama ilivyo kawaida ulinzi pia ulikuwa wa kutosha
Ndani ya kasri hili kulikuwa na
ukumbi wa mikutano ambamo
Daudi Sichoma alikuwa na
mkutano na wakuu wa vyama vya
siasa vya upinzani
kwanza alianza kwa kuwashukuru
wote kwa kufika kwao halafu
akaeleka katika mada.
“ Ndugu zangu nimewaiteni
hapa ili tujadili jambo muhimu
sana kwa mustakabali mzima wa
nchi yetu na kwa uhai wa vyama
vyenu vya upinzani.Nadhani nyote
mtakubaliana name kwamba kwa
siku za hivi karibuni vyama vya
upinzani vimepoteza sana nguvu
na taswira yake katika
jamii.Chama tawala kimezidi
kujiimarisha na kuwa na nguvu
sana.Msichangae kwa nini
ninajadili nanyi mambo kama
haya wakati mimi ni mwanachama
wa chama tawala.Naomba niweke wazi kwenu kwama mahusiano
yangu na chama changu si mazuri
hata kidogo hivi sasa.Nina
wapinzani wengi ndani ya chama
ambao wanajitahidi usiku na
mchana ili wanimalize
kisiasa.Mikakati mingi inapangwa
juu yangu ili kuweza kunididimiza
kisiasa na wamefanikiwa
kuniweka nje ya ulingo wa
siasa.Nimewavumilia sana na
nimefika mwisho.Sintavumilia
zaidi .Inanilazimu na mimi
nipambane nao na ndiyo maana
nimewaiteni hapa leo hii ili
kuwapeni mikakati na uwezo wa
kukidhoofisha chama tawala.”
Akasema David na kukaa kimya
akawaangalia wanasiasa wale
halafu akaendelea
“ Rais wa Marekani
amemaliza ziara yake ndefu
kuwahi kutokea hapa nchini.Ni
ziara ya kihistora na yenye mafanikio kwa serikali zote
mbili.Katika ziara hiyo mambo
mengi yamefanyika kama vile
uzinduzi wa miradi kadhaa
mikubwa ya maendelo .Pamoja na
yote makubwa yaliyofanyika
yenye maslahi makubwa kwa taifa
letu kuna mambo makubwa
mawili yaliyomleta rais huyu
mkubwa wa Marekani” Daudi
akanyamaza akanywa maji kidogo
nakuendelea
“ kwanza kabisa amekuja
kutafuta sehemu ambayo jeshi la
marekani litajenga kambi yake
kubwa kuwahi kuwekwa barani
afrika.lengo ni kuendeleza
mapambano dhidi ya vikundi vya
kigaidi ambavyo vimeonekana
kushamiri kila uchao katika eneo
hili la afrika mashariki kati na
kusini.tayari serikali ya Tanzania
imewaahidi kuwapatia eneo hilo ili
wejenge kambi kubwa ya kijeshi” Wanasiasa wale wakatazamana
usoni.Hawakuwa wakifahamu
kuhusu suala hili hivyo
lilionekana kuwastua
kidogo.Daudi akaendelea
“ jambo la pili na kubwa zaidi
ni kwamba hivi karibuni Tanzania
imegundua kiasi kikubwa cha
mafuta kiasi ambacho
kinasemekana kinaweza kulingana
au kuzidi kiasi chote cha mafuta
ya mashariki ya kati.Ugunduzi
huo umeifanya Tanzania kutolewa
macho na mataifa makubwa na
ndiyo maana nimeona katika
kipindi hiki toka ilipogundua
mafuta kumekuwa na ziara
zisizokauka za viongozi mbali
mbali wa mataifa makubwa
akitembelea nchi yetu.Kutokana
na migogoro mingi kulikumbia
eneo la mashariki ya kati , bei ya
mafuta imepanda mara dufu
katika soko la dunia.Kutokana na migogoro hiyo mataifa makubwa
yameanza kupunguza utegemezi
wa mafuta ya kutoka mashariki ya
kati Ugunduzi wa mafuta
Tanzania umeleta matumaini
mapya kwa mataifa haya
makubwa yenye uchumi mkubwa
sana .Jambo lililomleta rais wa
marekani hapa nchini ni kuitaka
serikali ya Tanzania iruhusu
serikali ya marekani kuwekeza
katika sekta ya mafuta ya gesi na
mafuta nchini Tanzania na tayari
mikataba imekwisha sainiwa na
kwa maana hiyo sekta nzima ya
mafuta na gesi imeshikiliwa na
wamarekani.Makampuni yetu
hayana tena nafasi katika
uwekezaji huo mkubwa” akasema
David na wakuu wale wa vyama
vya siasa wakabaki wanatazamana
na minong’ono ikaanza kusikika
mle ndani.Wanasiasa wale
walionekana kustushwa sana na taarifa ile.David akafurahi moyon
kwani plani yake ilianza kufanya
kazi.Akakohoa kidogo na
kuendelea
“ Ndugu zangu nimewaiteni
hapa kwa makusudi kabisa
kuwaeleza haya yote kwani ni nyie
pekee wenye nguvu za kuyazuia
yasifanyike.Mtajiuliza mtawezaje
kuzuia mambo haya yasifanyike?
Ni kweli ni suala gumu kwa
sababu tayari serikali imekwisha
tiliana mikataba na serikali ya
marekani na hakuna namna
mtakayoweza kuitengua mikataba
hiyo lakini njia pekee hapa ni
kutumia umma kuishinikiza
serikali .Katika hilo kuna mambo
ambayo yanatakiwa yafanyike”
akanyamaza kidogo akanywa maji
na kuendelea
“ kwanza ni kuanzisha
kampeni kubwa sana nchi nzima
itakayojulikana kama mafuta yetu.Hii itakuwa ni kampeni
kubwa ambayo haijawahi kutokea
hapa nchini.Itakuwa ni kampeni
ya mkoa kwa mkoa,wilaya kwa
wilaya,kata kwa kata,kijiji kwa
kijiji,nyumba kwa nyumba na
hatimaye mtu kwa mtu.katika
kampeni hii wananchi wataelezwa
kwa kina serikali ilichokifanya
.Nawafahamu ninyi ni mahodari
wa kujenga hoja.Nataka mjenge
hoja ambazo zitaamsha hasira kwa
umma dhidi ya serikali kupinga
serikali itengue mikataba yote
iliyotiliana sahihi na serikali ya
Marekani .kampeni hii
itaambatana na maandamano
makubwa yasiyo na ukomo
.makundi makubwa ya vijana
yatachochewa kuandamana na
kuweka makambi katika viwanja
vya wazi.Maandamano hayo
yataambatana na vurugu kama
kuchoma matairi,kupiga mawe magari ya serikali kuchoma ofisi
na hivyo kuilazimisha serikali
kutumia nguvu nyingi katika
kuwatawanya makundi ya vijana
na katika mapambano hayo jeshi
la polisi litalazimika kutumia
nguvu kubwa kuwatawanya
waandamanaji na hivyo baadhi ya
raia watapoteza maisha na hivyo
itakuwa ni faida kwetu kwani
suala hili litaonekana katika
vyombo vya habari vya kimataifa
na hapo ndipo jumuia ya kimataifa
itakapoingilia katika suala hilo na
kuishinikiza serikali ya Tanzania
iachane na mipango yake serikali
italaumiwa kwa kukiuka haki za
binadamu na kwa kiasi kikubwa
wananchi hawatakuwa na imani
na serikali yao tena na endapo
utafanyika uchaguzi ninyi
mtakuwa na nafasi kubwa sana ya
kushinda uchaguzi mkuu.Nadhani
huu ni mpango mzuri sana.Nyie mnauonaje mpango huu? Akauliza
Daudi.wanasiasa wale
wakatazamana na nyuso zao
zikaonyesha
tabasamu.walionekana kuufurahia
mpango ule.kwa dakika kama nne
hivi walikuwa wakisemezana wao
kwa wao
“ ndugu zangu nadhani
itakuwa vyema kama nikaawacha
kwa muda ili mlijadili suala hili
kwa muda namna mnavyoweza
kulitekeleza.Nitarejea baada ya
muda mfupi” akasema Daudi na
kutoka nje akawaacha wanasiasa
wale wakijadiliana .
Akiwa nje ya ukumbi Daud
akachukua simu yake kazitafuta
namba za simu za Frank
akampigia
“ hallow David “ akasema
Frank
“ halow Frank habari yako?
Habari za toka jana? “habari nzuri daud.mambo
yanakwendaje?
“mambo yanakwenda vizuri
na nimekupigia kukutaarifu
kwamba tayari nimekwisha ianza
kazi.Hivi niongeapo tayari niko na
wakuu wa vyama vya
siasa.Nimeanza nao na hivi sasa
nimetoka nje nimewaacha
wakijadiliana”
“thats great news
David.Nilijua tu mpango huu bila
ya wewe katu hatuwezi kufanikiwa
.Umeonaje mwelekeo wa hao
wanasiasa?
“ Bila shaka watakubaliana
nami.Baada ya muda mfupi
nitarejea tena ndani ili kufahamu
wameamua nini” akasema David
“ Ok David .kazi nzuri
sana.Natumai kwa kupitia wewe
mpango wetu utafanikiwa
“ Ahsante kwa kuniamni na
kunishirikisha.Jioni ya leo nitakuwa na kikao na makamu wa
rais.Nimekwisha ongea naye na
kupanga kukutana naye jioni ya
leo.Nina hakika hata naye
atakubaliana na mpango
huu.Nitakupigia tena simu baada
ya kumaliza kikao na hawa
wanasiasa” akasema Daudi na
kukata simu
Mara tu baada ya kumaliza
kuongea naFrank simuni David
akarejea tena katika chumba cha
mikutano alikowaacha wanasiasa
wakijadiliana.
“ ndugu zangu nadhani
mpaka sasa kuna jambo mtakuwa
mmekwisha lijadili “ akasema
David baada ya kuketi kitini
“ Tumejadiliana na
tumekubaliana na mawazo
yako.Hiyo ndiyo kazi ya vyama vya
upinzani,kuidhoofisha serikali
iliyoko madarakani.Tuko tayari
kwa ajili ya operesheni hiyo” akasema ndugu Makwa Tusangira
mwenyekiti wa chama kikubwa
cha upinzani Tanzania kwa niaba
ya wenzake
“ pamoja na kukubaliana
kuifanya operesheni hii lakini
kuna changamoto ya
kifedha.Kama ujuavyo vyama
vyetu vingi havina vyanzo vya
mapato zaidi ya kutegemea ruzuku
ya serikali kwa maana hiyo basi
uendeshaji wa vyama unakuwa
mgumu sana achilia mbali
operesheni kubwa kama hii.Pili
changamoto nyingine ni ya
kiusalama.Nina hakika kwamba
mara tu vuguvugu hili
litakaposhika kasi na kusambaa
mkoani ,serikali lazima
itawatafuta waasisi wa vurugu
hizo kwa hiyo lazima tutatiwa
nguvuni.Hizo ni changamoto
kubwa ambazo endapo tutazitafutia ufumbuzi basi
operesheni hii itakuwa na
mafanikio makubwa” akasema
Makwa.David akatabasamu na
kusema
“ kwanza kabisa niruhusuni
niwashukuru kwa kukubali
kwenu kuifanya operesheni hii
muhimu kwa taifa
letu.Changamoto hizo ulizozisema
ni changamoto ambazo lazima
tuzitafutie ufumbuzi wa
haraka.Kuhusu suala la fedha
nawaomba msiwe na wasi wasi
ninataka mkae na mtengeneze
bajeti ya kutosha kufanikisha
zoezi hili na mniletee.Pesa ipo ya
kutosha msihofu.Nileteeni vile vile
mchanganuo namna operesheni
itakavyofanyika nchi
nzima.Kuhusu suala la usalama
kwamba mnaweza kutafutwa na
kuwekwa kizuizini msiwe na
shaka na hilo pia.Baada tu ya kuuwasha moto na ukasambaa
nchi nzima nyie mtaondoka kwa
siri nchini na mtapewa hifadhi
nchi za nje na operesheni
itaendelea kuongozwa na vongozi
wa chini.Hakuna atakayegundua
kwamaba mmeondoka nchini na
mtaendeleza hareakati mkiwa nje
ya nchi.jambo lingine ambalo
nilisahau kuwaambieni ni kwamba
sambamba na harakati hizo
,tutavishawishi pia vyama vya
wafanyakazi kuendesha mgomo
wa wafanyakazi wa nchi nzima wa
umma na wa binafsi kushinikiza
serikali iliyopo madarakani
kuachia ngazi na hiyo itakuwa ni
fursa kwenu kuingia
madarakanibaada ya uchaguzi
kufanyika kwani tayari mtakuwa
juu kisiasa ” akasema Daud
Kikao kile kati yake na wakuu wa
vyama vya siasa kiliendelea hadi
ilipotimu saa kumi na moja za jioni ndipo kilipomalizika.wakuu
wale wa vyama vya siasa wote
nyuso zao zilikuwa zimetawaliwa
na tabasamu zito nahasa baada
ya kila mmoja kukabidhiwa
bahasha iliyotuna ambayo ndani
yake kulikuwa naiasikikubwa cha
pesa. Walipeana mikono
kupongezana kwa kikao kile
chenye manufaa makubwa kwao
na kisha wakaagana kwa miadi
ya kuonana naye tena baada ya
siku nne watakapokuwa tayari
wamekaa kikao na kutengeneza
bajeti ya operesheni nzima
*********************
Saa mbili za usiku
Elvis,Doreen na Graca wakawasili
jijini Dar e s salaam wakitokea
Mbeya.Ilikuwa ni safari ndefu
.Elvis ndiye aliyekuwa dereva siku
hii akimsaidia Doreen Welcome home Graca”
akasema Elvis .Graca
akatabasamu.uso wake
ukaonyesha furaha ya kurejea
tena ndani ya jiji hili halafu
akanyong’onyea baada ya
kukumbuka mambo yaliyomkuta
na kubwa zaidi lililomuogopesha
ni kuhusu usalama wake
Hatimaye wakawasili nyumbani
kwa Doreen.Graca aliyeonekama
kuchoka sana alipelekwa
chumbani kupumzika halafu
Doreen akarejea sebuleni
alikomuacha Elvis
“ Doreen ahsante sana kwa
msaada wako Bila wewe nina
hakika kazi yangu ya kumsafirisha
Graca ingekuwa ngumu sana”
akasema Elvis
Doreen akatasamu na kusema
“ Hupaswi kunishukuru
Elvis.Nimefanya kile
ninachopaswa kukifanya na nimefurahi kuwa sehemu ya
msaada kwako.”
“ Ahsante sana
Doreen.Mungu akubariki sana”
akajibu elvis na wote wakakaa
kimya
“ Elvis unakwenda kulala
nyumbani kwako usiku huu?
Akauliza Doreen.Alvis akanima
akafikiri kidogo na kusema
“ Natamani kama
ningekwenda nyumbani nikaonane
na mke wangu Patricia lakini
siwezi kufanya hivyo.Natakiwa
kumlinda Graca kwa kila namna
niwezavyo.Endapo watu
wanaomtafuta watagundua
kwamba Graca yuko hapa
hawatapoteza hata dakika moja
watafika na kuwadhuru wote
watakaowakuta.Sitaki hilo litokee
kwa hiyo nitalala hapa kuwalinda
wewe na Graca.Kuhusu sehemu
ya kulala usipate shida kabisanitalala hapa hapa
sofani.Nimekwisha zoea kukesha
macho” akasema Elvis
“ Elvis tafadhali usinielewe
vibaya kukuuliza vile.Nashukuru
kwa kuamua kulala hapa usiku
wa leo na kutulinda.Hapa ni
nyumbani kwako na siku zote
unamuda wowote.Nyumba yangu
ni kubwa na ina vyumba vya
kutosha vya kulala na endapo
ukipenda unaweza hata kulala
chumbani kwangu” akasema
Doreen na wote wakaangua
kicheko
“ Usijali Doreen hapa sebuleni
panatosha sana” akasema Elvis
“ Elvis tutaongea baadae kwa
sasa ngoja nikawaandalie chakula
cha usiku .Wakati naanda chakula
naomba nikupeleka chumbani
kwangu ukaoge na upumzike
kidogo kuondoa uchovu wa safari”
akasema DoreenUhhmmm Doreen kuna
jambo nataja
kukuomba.Ninaomba umpigie
simu Patricia na kumjulia hali ila
usimweleze chochote kuhusiana
na mimi kuwapo hapa kwako wala
safari ya Mbeya.”akasema Elvis
“ Sawa Elvis,nitampigia
.Twende chumbani ukaoge”
akasema Doreen na kumuongoza
Elvis hadi chumbani
kwake.Kilikuwa ni chumba
kikubwa na kizuri
“ Chumba chako kizuri sana
Doreen.Hongera sana”
“ Ahsante Elvis lakini
hakiwezi kuzidi kile cha Patricia.”
Akasema Doreen na kumfungulia
Elvis mlango wa bafu akamuacha
akioga na yeye akaelekea jikoni
kuandaa chakula cha usiku
Baada ya kumaliza kuoga
Elvis akarejea sebuleni.Kichwa
chake kilikuwa na mawazo mengi na mara akainga Doreen na
kumkuta Elvis pale sebuleni
“ Elvis ,mbona umetoka
chumbani ? unaogopa
nini?Unatakiwa upumzike safari
ilikuwa ndefu sana”akasema
Doreen.Elvis akatabasamu
“ Usijali Doreen,hata hapa
panatosha sana kupumzika.Vipi
umempigia simu Patricia?
“Ndiyo nimempigia na
anaendelea vizuri na hana tatizo
lolote”
“ Ahsante sana” akajibu Elvis
.Doreen akaendelea kumtazama
usoni
“ Mbona unanitazama hivyo
Doreen? Akauliza Elvis
“ uhhmm !! its nothing.Ngoja
na mimi nikaoge halafu
tutajumuika sote mezani kwa
chakula cha
usiku”akasemaDoreen nakuelekea
chumbani kwake kuoga.Kisha oga wote watatu wakajumuika katika
chakula cha usiku na baada ya
kumaliza kula wakaelekea
sebuleni
“ Graca pole sana na safari
ndefu “ akaanzisha maongezi
“ Ahsante sana Elvis.Pole
sana nawe Kuendesha gari umbali
ule mrefu si kazi ndogo”
“Ahsante ila mimi nimekwisha
zoea safari kama hizi” akajibu
Elvis
“ This is your house? Akauliza
Graca
“ hapana Graca hapa si
nyumbani kwangu.Hapa ni
nyumbani kwa Doreen’
“ wewe na Doreen ni
wapenzi?akauliza graca
“ hapana ,sisi si wapenzi bali
ni marafiki wakubwa.Mimi tayari
nina mke wangu anaitwa
Patricia”akasema Elvis
Graca akamtazama Elvis usoni na kusema
“kwa hiyo utaniacha hapa na
kwenda nyumbani kwako?Are you
sure I’m safe here? Elvis
akatasabamu kama kawaida
yakena kusema
“Usihofu Graca Sintaondoka
na kukuacha hapa peke
yako.Nilikuhakikishia usalama
wako kwa hiyo nitaendelea
kukulinda.Kuhusu usalama hapa
ni sehemu salama sana lakini
kesho tutahamia katika sehemu
salama zaidi ya hii .Kuna nyumba
ambayo nimeinunua maalum kwa
ajili yako na ndipo utakapoishi
hadi hapo tutakapofanya mpango
mwingine kuhusiana na maisha
yako kwa hiyo usihofu kitu
chochote”
Tabasamu kubwa likajengeka
usoni mwa binti yule mrembo kwa
maneno yaleya Elvis
“Ahsante sana Elvis kwa msaada wako mkubwa.katika
misha yangu sijawahi kukutana
na mtu mwenye moyo wa huruma
kama wewe”
“ Usijali Graca,ni jukumu
langu kukusaidia” akajibu Elvis
halafu kukawa kimya
“ mkeo anajua kwamba uko
hapa?akauliza Graca
“ hapana hafahamu”
“ kwa nini hujamwambia
.Dont you trust her?
“ I do trust her with my life
lakini kwa sasa siwezi kumweleza
chochote kuhusiana na suala
lako.Nitamfahamisha muda
ukifika”akasema Elvis
“ Ok Elvis nadhani kesho
tutakuwa na muda mzuri zaidi wa
kuongea.Kwa sasa nimechoka
sana naomba
nikapumzike”akasema Graca
akainuka na kuelekea chumbani
kupumzika.Baada ya dakika tano Doreen akaingia sebuleni
“ Elvis tayari nimekwisha
kuandalia chumba cha kulala
ukapumzike.Safari ilikuwa ndefu
sana “akasema Doreen
“Ahsante Doreen lakini
nitakaa hapa hapa sebuleni
kuhakikisha usalama wenu
usihofu kuhusu mimi.Hizi ni kazi
zangu na nimekwisha
zizoea.tafadhali nenda kalale
upumzike”
“hapana Elvis huwezi kukaa
hapa sebuleni peke yako usiku
kucha.Usalama hapa ni mkubwa
tu.Nyumba zote za hapa jirani
tumeweka walinzi kwa hiyo
usalama kuzunguka eneo hili ni
mkubwa”akasema Doreen
“ Doreen tafadhali usihofu.I’ll
be fine.Nenda kapumzike.Kesho
tutakuwa na siku ndefu
kidogo.Vipi kuhusu kazini kwako?
Hakuna tatizo ?akauliza Elvisa hakuna tatizo lolote
kazini.Nimekwisha omba ruhusa
ya siku kumi”akasema Doreen
“ ahsante sana,Sasa nenda
kapumzike”akasema Elvis huku
akiufungua mlango na kutoka nje
akaikagua nyumba yote
kuhakikisha iko salama halafu
akarejea sebuleni akazima kila
kitu kukawa na ukimya .
******************
Kumepambazuka na siku
mpya imeanza.Saa kumi na mbili
za asubuhi ilimkuta Elvis akiwa
macho.Usiku mzima hakuweza
kufumba macho akihakikisha
Graca na Doreen wanakuwa
salama.
“habari yako Elvis” Doreen
akamsalimu Elvis .
“ Ouh Doreen umeamkaje?
Akauliza Elvis huku akijinyoosha kwa uchovu
“ Pole sana kwa uchovu wa
usiku Elvis”
“usijali Doreen umeamka
salama lakini?
“ Niko salama kabisa Elvis”
“Nafurahi kusikia hivyo”
“ Elvis nadhani ungeenda
chumbani upumzike walau
kidogo.usiku mzima umekesha
hapa ukitulinda”
“ Ahsante sana Doreen lakini
huu si wakati muafaka wa
kupumzika.Dakika moja tu
inatosha sana kwa watu
wanaomtafuta Graca kuingia na
kumfanyia chochote.I cant let that
happen”akasemaElvis .Doreen
akamtazama kisha akasema
“basi twende ukaoge
tujiandae na siku ya leo”akasema
Doreen akamuongoza Elvis hadi
chumbani kwake.wakati Elvis
akiendelea kuoga Doreen akaenda kumuamsha Graca
Saa mbili za asubuhi wote
watatu wakajumuika mezani
wakapata kifungua kinywa .
“Graca ,tukitoka hapa
tunaelekea katika nyumba
ambayo utakuwa ukishi hadi hapo
tutakapokufanyia utaratibu
mwingine wa kwenda nje ya nchi
.Uwepo wako hapa nchini
unatakiwa uwe ni wa siri
kubwa”akasema Elvis wakiwa
mezani wakiendea kupata
kifungua kinywa
“ Ahsante sana Elvis.Lakini
nina swali nataka kuuliza”
“Uliza usihofu Graca”
“katika nyumba hiyo
unayonipeleka nitaishi na nani?
Nitaishi peke yangu?
Elvis na Doreen
wakatasamana,halafu Elvis
akasema
“ hapana hautakuwa peke yako,nitakuwa pamoja nawe.”
“Vipi kuhusu mkeo na
watoto?akauliza Graca
“ Usijali kuhusu
hilo,hakutakuwa na tatizo lolote.”
Akajibu Elvis
Waliendelea kupata kifungua
kinywa na walipomaliza wakaingai
katika gari la Doreen
wakaondoka.Breki ya kwanza
ilikuwa katika ofisi za kampuni ya
ulinzi ambako Amanda rafikiye
Doreen aliacha funguo za nyumba
aliyomuuzia Elvis.Doreen
akajitambulisha na akakabidhiwa
funguo kwani taarifa zake tayari
zilikuwepo pale ofisini.Kishapata
funguo safari ikaendelea kuelekea
katika jumba lile
“ wale jamaa wameniuliza
kama tutapenda kuingia mkataba
wa kuilinda nyumba ile kwani
mkataba wao na Amanda
umekwisha sitishwa.Sijawapa jibu nimewaambia wasubiri kwanza
tujadiliane”
“ Good.hakuna haja ya kuwa
na ulinzi.Graca nitamlinda
mwenyewe” akasema elvis.
Hatimaye wakawasili katika
jumba lile kubwa na la
kupendeza.Jumba lile lilikuwa
limezungukwa na ukuta mkubwa
wenye rangi yeupe na juu ya
ukuta kulikuwa na nyaya kwa ajili
ya usalama.
“wow ! what a wonderfull
place!! ELvis akasema kwa furaha
baada ya kuingia ndani ya jumba
lile na kuishuhudia mandhari
nzuri ya kupendeza.Katika
nyumba ile kulikuwa na vyumba
vinne vya kulala,sebule ,chumba
cha maongezi,maktaba,sehemu ya
kufulia,jiko,gereji ya gari na
chumba maalum kwa ajili ya
ibada.Elvis alifurahi mno kuipata
nyumba kama ile.Ingemfaa sana katika kazi zake
“Ahsante sana
Doreen.Nyumba hii ni nzuri sana
na inafaa.Ina kila kitu
ninachokihitaji”akasema Elvis.
“There is one more thing’
akasema Doree
“ whats that? Akauliza Elvis
“ Kuna chumba cha chini kwa
chini kwa ajili ya usalama.Endapo
usalama ukiwa tete basi unangia
katika chumba cha chini”
Elvis akashindwa kujizuia
furaha yake na kujikuta
amemkubatia Doreen halafu
wakaelekea katika chumba
kikubwa cha kulala .katika ukuta
wa kile chumba kulikuwa na kifaa
Fulani mithili ya mita ya umeme
.Doreen akabonyeza namba
kadhaa na mara sehemu ya
sakafu ikafuguka .Wote wakabaki
na mshangao mkubwa.Kulikuwa
na ngazi za kushuka chini.Taratibu wakaifuata ngazi
ile na kukutana na varanda
ambalo mbele yake kulikuwa na
mlango ambao nao ulifunguliwa
kwa namba ,wakaingia katika
chumba kikubwa na kizuri chenye
kila kitu
“ I lovethis place” akasema
Graca
“ Doreen unastahli pongezi
kubwa .nyumba hii ni sahihi
kabisa kwa mimi kuishi.” Akasema
Elvis halafu wakarejea sebuleni
“ sasa Doreen kuna mambo
ambayo nataka uyafanye kwa siku
ya leo”
“ usijali elvis .I’m at your
service” akasema Doreen huku
akitabasamu
“ Nataka upite madukani
umfanyie Graca manunuzi
.Mnunulie nguo nzuri ,viatu
vipozodi na kila utakachoona
kinamfaa.Baada ya hapo ufanye pia manunuzi ya chakula na
vinywaji vya kututosha kwa wiki
mbili au zaidi.”akasemaElvis
akachukua kompyta ya Doreen na
kufungua akaunti yake
akapunguza shilingi milioni tatu
na kuzituma katika akaunti ya
Doreen
“ Elvis basi ngoja niwahi
nikaanze kufanya manunuzi
hayo.Nina hakika sintakawia
sana.Una mpango wa kutoka
baadae?
Elvis akafikiri kidogo na
kusema
“ Kama ikinilazimu kutoka
nitatumia gari la Amanda”
“ sawa .Amanda aliniambia
kwamba gari lake ni zima na
halina tatizo lolote”akasema
Doreen akachukua vipimo vya
Graca na kutoka mle
sebuleni.Elvis akamsindikiza hadi
garini “ Elvis are you sure you want
to live here? Akauliza Doreen
“ Itanilazmu kufanya hivyo
kwa kipindi hiki ambacho Graca
atakuwa hapa.Dhamana yote ya
usalama wake nimeibeba mimi
kwa hiyo natakiwa nimlinde kwa
kila namna kwani ndivyo
nilivyomuahidi”
“ Vipi kuhusu Patricia?
atakuelewa?
“ najua itakuwa ngumu
kwake kunielewa lakini sina
namna nyingine ya kufanya.Graca
anazo taarifa nyeti sana kwa hiyo
anatakiwa alindwe” akasema
Elvis.Doreen akamtazama usoni
na kusema
“ Una hakika taarifa hizo zina
umuhimu mkubwa kiasi cha
kukufanya ujitoe namna hii?
“ Doreen naomba usinielewe
vibaya lakini taarifa alizonazo
Graca ni za muhimu sana kwangu na nchi kwa jumla”
“Ok Elvis.Tutaonana baadae”
akasema Doreen na kuingia garini
akaondoka .Elvis akarejea
sebuleni alikomuacha Graca
“ Nyumba hii ni nzuri sana
.nani alikuwa akiishi hapa?
Akauliza Graca
“Kuna mzungu mmoja ndiye
aliyekuwa akiishi hapa na sasa
amerejea kwako”
“ Ni nyumba nzuri
sana.Nimeipenda” akasema Graca
“ hii ndiyo sehemu salama
ambayo nilikuahidi kwamba
utaishi.Hakuna mtu yeyote
atakayejua kama uko
hapa.Pamoja na usalama uliopo
lakini nitafunga pia kamera za
ulinzi kila kona ili kuzidisha ulinzi
zaidi.”
“ Ahsante sana Elvis kwa
namna ulivyojitahidi kunisaidia
Sijui nitakulipa kitu gani”akasemaGraca
“ Usiwaze sana kuhusu
kulipa.Nimefanya kile ambacho
ninapaswa kukifanya.”akasema
Elvis.Kikapita kimya cha sekunde
kadhaa Elvis akasema
“ Graca nimetimiza ahadi
yangu.Nilikuahidi kukutoa pale
hospitali afrika kusini na
kukupeleka sehemu salama.You
are safe now.Now it’s your turn to
tell me everything you know about
your father ”akasema Elvis
Graca akainama akazama
mawazoni halafu akainua kichwa
na kusema
“ Katika familia yetu
tulizaliwa watoto wawili tu mimi
na kaka yangu Edwin.Wakati bado
ninasoma Edwin akajiunga na
jeshi na kwa bahati mbaya
alifariki katika maozezi ya kijeshi
wakati wakipanda mlimaKilimanjaro kwa kuangukiwa na
mawe yaliyokuwa yakiporomoka
na kuwaponda yeye na wenzake
wawili ambao wote walipoteza
maisha.Nilibaki mimi peke
yangu.Maisha yetu yalikuwa
mazuri na hatukuwa na tatizo
lolote.Kila nilichokitaka nilikipata”
Akanyamaza akameza mate na
kuendelea
“ Siku moja ulitokea ugomvi
kati ya baba na mama.Sikujua
chanzo cha ugomvi huo lakini
nilisikia mama akimlalamikia baba
kwamba aachane na mambo yake
anayoyafanya.Sikujua ni mambo
gani hayo ambayo mama alimtaka
baba kuachana nayo.Nilidhani
labda ni mambo yao ya
wanandoa,yawezekana labda baba
akawa na mwanamke mwingine nje ya ndoa.Sikuwahi kumuuliza
mama sababu ya ugomvi
wao.Maisha yaliendela kama
kawaida lakini mama alionekana
kubadilika sana.Hakuwa katika
hali yake ya kawaida
niliyomzoea.Niligundua kuna
jambo lililokuwa
linamsumbua.Nilijaribu sana
kumdadisi aniambie ni kitu gani
kilichokuwa kinamsumbua lakini
hakunieleza chochote.Siku moja
baba aliwahi kuondokana
kusahau funguo za chumba chake
ambacho huingia yeye
pekee.Chumba hicho amehifadhi
vitu vyake muhimu zikiwemo
nyaraka zake nyingi.Mama aliingia
katika kile chumba na kuanza
kupekua,akatoka na mkoba
uliokuwa na kompyuta ndogo ndani yake.Akanipatia mkoba ule
na kunitaka niufiche mahala
ambako hakuna yeyote anayeweza
kuuona.Alinisisitiza sana kwamba
nisimuonyeshe mtu yeyote
.Niliuchukua mkoba ule na
kwenda kuuhifadhi kwa rafiki
yangu Salha.Kumbe katika kile
chumba cha baba kulikuwa na
kamera ndogo ambayo iliweza
kuchukua picha za kila anayeingia
mle chumbani wakati baba akiwa
hayupo na kumtumia baba moja
kwa moja katika simu yake kwa
hiyo baba aliweza kugundua
kwamba mama aliingia mle katika
ofisi yake na akachukua kompyuta
yake ndogo.” Akasema Graca
halafu akanyamaza kidogo na
kuendelea Jioni ya siku ile kulitokea
tena ugomvi mkubwa sana baba
akitaka mama arudishe kompyuta
yake ndogo aliyoichukua toka
ofisini kwake.Mama alikataa kata
kata kwamba hakuchukua
kompyuta ile lakini baba
akamuonyesha picha
zilizochukuliwa na kamera lakini
bado mama alikataa kwamba
hakuchukua ile
kompyuta.Nilitamani nimwambie
baba kwamba kompyuta yake
ninayo mimi ili kuumaliza ule
ugomvi lakini nikaogopa kwa
namna alivyokuwa
amekasirika.Nilikumbuka pia
kwamba mama aliniambia kwa
namna yoyote ile nisithubutu
kumpa mtu yeyote kompyuta ile
hadi hapo atakaponipa maelekezo yake” Graca akanyamaza kidogo
halafu akaendelea
“ wakiwa chumbani nilimsikia
mama akimtaka baba aachane na
biashara haramu alizokuwa
akifanya.Moja kwa moja akili
yangu ikanituma kwamba huenda
baba akawa anajishughulisha na
biashara ya madawa za kulevya na
ndiyo maana akawa na utajiri
mkubwa tofauti na kipato chake
anacholipwa kama
mwanajeshi.Baada ya siku hiyo
hakukuwa tena na maelewano
baina ya mama na baba kwani kila
mmoja alianza kulala chumba
tofauti na mwenzake.Niliendelea
kumdadisi mama chanzo cha
ugomvi wao na biashara haramu
ambayo baba anaifanya lakini
hakuwa tayari kuniambia bali alinisihi niendelee kuitunza
kompyuta ile kwani ndiyo yenye
kila kitu kuhusiana na
anachokifanya baba.Baada ya wiki
tatu alipata safari ya kwenda
Morogoro na akiwa njiani
alinitumia ujumbe mfupi kwamba
atakaporejea atanieleza kila
kitu.Hayo yalikuwa ni mawasiliano
yake ya mwisho kwani mama
hakurejea tena.Alipata ajali na
kufariki.Nina uhakika mkubwa
kwamba baba alihusika katika
ajali ile iliyosababisha kifo cha
mama kwani kabla sijapata taarifa
za kifo cha mama alinifuata na
kunitaka nimueleze mahala ilipo
kompyuta aliyonipa
mama.Nilikana kutofahamu
chochote lakini baba
akaninyang’anya simu na kunionyesha meseje niliyotumiwa
na mama.Nilijiuliza sana alijuae
kama mama alinitumia ujumbe
ule? Alinitolea vitisho vingi sana
lakini sikuogopa na niliendelea
kukana kupewa kompyuta na
mama.Jioniya siku ile ndipo
nilipopewa taarifa za kifo cha
mama.Niliumia sana”
akanyamaza kidogo na kufuta
machozihalafu akaendelea
“ Baada ya kumaliza msiba
alinifuata tena na kuendelea
kunitisha ili nimpatie ule mkoba
lakini bado niliendelea kukana
kupewa mkoba wowote na
mama.Vitisho vilipozidi ikanibidi
kwenda kuichukua kompyuta ile
kwa Salha na kuificha kwa mpenzi
wangu David.Niliamini kule
itakuwa salama.Kabla ya kuipeleka kwa David ilinilazimu
kwanza kuiwasha na kuangalia ni
kitu gani kilichokuwamo ndani
yake na nikastuka sana kwa
nilichokigundua” akasema Graca
“ Uligundua nini Graca?
Akauliza Elvis
“ Kupita kompyuta ile
niligundua kwamba baba
amekuwa akijishughulisha na
biashara ya kuuza silaha.Yeye na
wenzake wamekuwa wakifanya
biashara hii kwa muda mrefu na
ndiyo chanzo cha utajiri wake
mkubwa.Niligundua kwamba
silaha hizo wamekuwa wakiziagiza
toka nje ya nchi na kisha
huziingiza hapa nchini kama
silaha za jeshi la Congo na kisha
huzisafirisha kuzipeleka kwa
waasi wanaopigana na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
na kujipatia fedha nyingi
sana.Hiyo ndiyo biashara ambao
mama alikuwa akimkanya baba
kuacha kujihusisha nayo.” Graca
akanyamaza akainama chini.Elvis
akahisi shati lake linaanza kuloa
jasho.Ilikuwa ni taarifa yenye
kustusha sana.Graca akainua
kichwa halafu akasema
“ Siku moja usiku baba
akanikamata akanifungia katika
chumba kimoja akanitesa sana
akinitaka nimuonyeshe mahala
ilipo kompyuta yake.Alinipiga sana
usiku huo lakini sikumweleza
chochote.Alipoona nimegoma
kumpa jibu akaniacha.Alfajiri na
mapema nikawahi kwa David na
kumuomba anipe ile kompyuta
yake.Kumbe wakati naenda kwa David kuna watu walikuwa
wananifuatilia.Nikiwa chumbani
kwa David watu wale waligonga
mlango kwa nguvu ,David
akanipitishia dirishani nikakimbia
pamoja na kompyuta ile.Na
asubuhi ile ndio ulikuwa mwisho
wa mimi kuonana na David kwani
alikamatwa na kufunguliwa
shtaka la kumbaka mwanafunzi
yaani mimi” Graca akainama
akafuta machozi na kuendelea
“ Nilipotoka pale kwa David
nikaelekea moja kwa moja kwa
padre kalistus ambaye ndiye
paroko wa parokia yetu na
ananifahamu vyema.Aliponiona
katika hali ile alistuka sana lakini
sikumueleza chochote kuhusu
kilichonipata ,nilichomuomba kwa
wakati ule ni anihifadhie ile kompyuta na asijaribu kuifungua
ndani.Aliniahidi kufanya kama
nilivyomuomba halafu
nikaondoka.Ni hapo ndipo
nilipolazimika kujifanya mgonjwa
wa akili”
Graca akafuta machozi na
kuendelea
“Nilipelekwa hospitali ya
magonjwa ya akili na nikaanza
kudungwa sindano wakiamni
mimi nina matatizo ya akili.Baada
ya wiki moja nikapandishwa ndege
na kupelekwa afrika kusini katika
hospitali ile ulikonitoa” akasema
Graca.
“ Pole sana Graca.Simulizi
yako imenisikitisha sana
sana.Sikutegemea kama baba
yako anaweza kuwa na roho mbaya kiasi hicho.Nakupongeza
kwa ujasiri wako”
“ Ahsante sana Elvis.kwa sasa
najiona nimeutua mzigo mzito
sana na nimeufikisha sehemu
husika.Nilikuwa nikijiuliza sana
sehemu ambayo ninaweza kwenda
kuripoti kuhusu jambo hili lakini
nashukuru Mungu amekuleta
wewe .Tafadhali Elvis naomba
ulifanyie kazi jambo hili na
uhakikishe wahusika wote
wanachukuliwa hatua ukianzia na
baba yangu.” Akasema Graca
“ Graca ninashukuru sana
kwa kuniamini na kunieleza
mambo haya mazito.” Akasema
Elvis
“ Unayepaswa kushukuriwa
ni wewe kwani bila wewe
nisingeweza kuondoka palehospitali” akasema Graca kikapita
kimya Elvis akamtazama Graca na
kusema
“ Graca taarifa hizi
ulizonipatia ni taarifa nzito sana
na ninakuahidi kuzifanyia kazi
kiukamilifu.Maelfu ya raia wa
jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo
wamekuwa wakiuawa na waasi
ambao wanatumia silaha
wanazouziwa na Frank na kundi
lake.Lazima nihakikishe kwamba
wote wanaohusika na mtandao
huu wanatiwa hatiani na
wanahukumiwa kwa makosa
wanayoyafanya” akasema Elvis na
kunyamaza kifupi kisha akauliza
“ Ulisema kompyuta ile
uliipeka kwa padre?
“ Ndiyo.Nilimpa Padre kalistus
anitunzie” Nitahitaji kuipata kompyuta
hiyo ili niweze kukusanya taarifa
za kutosha kuhusiana na jambo
hili.Kwa maana hiyo itatutalzimu
kwenda kuichukua.usiwe na hofu
yoyote ukiwa na mimi” akasema
Elvis
“ Hakuna tatizo Elvis
tunaweza tukaenda.” akasema
Graca.Elvis akaelekea katika
chumba cha gari ambamo
kulikuwa na gari aliyoiacha
Amanda.Ilikuwa ni gari nzuri.
“ Wow ! what a nice car”
akasema Elvis huku
akitabasamu,akalikagua gari lile
na kuhakikisha liko vizuri.Akalitoa
nje kisha wakaondoka kuelekea
kwa padre Kalistus
*****************
 
I DIED TO SAVE MY PRESDENT

Sehemu 27

Ni saa tatu za asubuhi
Brigedia Frank akiwa amesimama
sebuleni kwake mkononi akiwa na
glasi ya pombe kali kama kawaida
yake.Mkono wa kushoto alikuwa
na sigara ikitoa moshi.
“ Najuta kwa nini Mungu
alinipa mtoto kama Graca.Yeye na
mama yake wote hawana faida
yoyote wangu zaidi ya hasara na
karaha.Graca akeshe akimuomba
Mungu wake nisimtie mikononi
mwangu.Aendelee kujificha hivyo
hivyo .Nikimpata safari hii sina
hakika kama nitamuacha hai.Na
huyu shetani Elvis kama kweli ni
yeye ndiye aliyemtorosha
mwanagu basi ninaapa
nitamuonyesha kazi.Safari hii
ameingia sehemu mbaya sana vijana wanasema ameingia choo
cha kike na nitamuonyesha mimi
ni nani” akawaza Frank na
kunywa funda kubwa la mvinyo
akavuta na sigara yake akapuliza
moshi halafu akachkua simu na
kumpigia Pascal
“ hallow Frank” akasema
Pascal baada ya kupokea simu
“ habari yako pascal?
“ Habari nzuri kuna habari
yoyote mpya?
“ David kanipgia simu
asubuhi na kunitaarifu kwamba
kikao chake na makamu wa rais
hakikuweza kufanikiwa kwani
makamu wa rais alipatwa na kikao
cha dharura kwa hiyo kikao chao
kitafanyika leo na kesho jioni
kutakuwa na kikao cha pamoja ili
kupeana taarifa za maendeleo katika majukumu
tuliyokabidhiana.Leo saa saba
mchana nitakuwa na kikao na
makamanda watano ambao
tulianza maongezi yetu jana lakini
hatukumaliza kwa hiyo baadae
tutaendelea.Taarifa zaidi
tutapeana kesho jioni katika
kikao.Vipi kuhusu Elvis? Umepata
taarifa zake zozote?
“ Mpaka sasa hivi sia taarifa
zozote za Elvis.Nimejaribu kufanya
uchunguzi kwa kupitia watu
wangu wa uwanja wa ndege na
Julius nyerere na
wamenihakikishia kwamba ni
kweli Elvis alipanda ndege ya
shirika la ndege la afrika kusini
na kuondoka nchini lakini
hakuna mahali kunakoonyesha
kwamba tayari amerejea nchini.Mara tu atakaporejea ama
atatumia njia ya ndege basi
nitataarifiwa mara moja.Vipi
kuhusu Graca kuna taarifa zozote
umepokea?
“ Hakuna taarifa zozote hadi
hivi sasa.Graca hajaonekana na
juhudi za kutafuta
zinaendelea.Nina hakika Elvis
ndiye aliyemtorosha na kumpeleka
kusikojulikana kwa sababu
anazozijua yeye.Nakuhakikishia
Pascal kwamba safari hii huyu
kijana amejiingiza mwenyewe
katika tanuru la
moto.Kitakachomkuta itakuwa ni
fundisho kwake na kwa wengine
wenye tabia kama yake na
kuingilia mambo yasiyowahusu”
“ Unadhani kuna jambo
ameligundua kuhusiana na sisi na ndiyo maana akaenda kuonana na
Graca?
“ Ninahisi hivyo.Ninahisi kuna
kitu atakuwa ameking’aza lakini
hana uhakika nacho na ndiyo
maana anatafuta uhakika
.Hatupaswi kumpa nafasi ya
kutuchunguza.Sisi ni mtandao
mkubwa na wenye nguvu na
hatuwezi kushindwa na mtu
mmoja na hasa katika wakati huu
ambao tuna mpango mkubwa
sana ulioko mbele yetu.Endelea
kufanya uchunguzi tujue mahala
alipo ili tumzimishe haraka sana”
akasema Frank
“ usijali Frank.Ninaendelea
kufuatilia kwa karibu sana suala
hili na ninakuhakikishia kwamba
katu Elvis hawezi kutuumiza
vichwa vyeti.Nitakuwa nakutaarifu mara kwa mara kila nitakapopata
taarifa za kuonekana kwa kenge
huyu”
“Ok Pascal .Tuwasiliane
baadae” akasema Frank na kukata
simu.Akanywa funda moja na
mara sura ya Graca ikamjia
akauma meno kwa hasira
“ Pone pone yako uendelee
kujificha huko huko ulikojificha
kwa sababu endapo utajitokeza tu
nitalifuta jina lako haraka sana
katika orodha ya walio
hai.Najilaumu sana kuwa na
mtoto kama wewe.I hate you !!
akasema kwa hasira halafu
akaenda ukutani akaitungua
picha kubwa ya Graca
“ Hustahili kuitwa mtoto
wangu.Wewe ni shetani mkubwa”
akasema kwa hasira halafu akaenda nje na kutupa picha ile
katika pipa la takataka
“ To me you are dead already
!! akasema Frank wakati akiitupa
picha ile ya mwanae
Mara tu baada ya Frank
kukata simu pascal akazitafuta
namba za simu za Arafa msichana
anayefanya kazi katika ofisi za
akina Elvis na kumpigia.Simu
ikaita bila kupokelewa,hakukata
tamaa akapiga tena na safari hii
ikapokelewa
“ Hallo Arafa” akasema pascal
“ pascal,Elvis
hajarudi,nitakufahamisha
atakaporejea” akasema sarafa na
kukata simu
“ Bastard !!!!..” akasema kwa
hasira pascal.Kitendo cha Arafa
kumkatia simu kilimkera sana Yawezekana akawa na
shughuli nyingi siku ya leo na
ndiyo maana amenijibu vile kwa
dharau”akawaza Pascal
*****************
Gari aina ya Toyota harrier
liliwasha taa ndogo ya njano ya
upande wa kulia ishara ya kukata
kona kuingia katika lango kuu la
kanisa la mt.Anthony wa padua na
kuelekea moja kwa moja katika
maegesho.Hakukuwa na magari
mengi siku hii mahala
hapa.mlango wa gari upande wa
dereva ukafunguliwa akashuka
Elvis halafu akazunguka upande
wa pili na kufungua mlango
akashuka Graca.Akasimama kwa
sekunde kadhaa akilitazamakanisa lile akatabasamu na kupiga
hatua kuelekea katika ofisi ya
parokia.Kabla ya kuelekea katika
ofisi kuu akaongoza hadi katika
ofisi ya katekista akabisha hodi na
kuruhusiwa kuingia,akakinyonga
kitasa na kujitoma ndani
akamuacha Elvis nje
akimsubiri.Mara tu alipoingia mle
ofisini mzee mmoja mwenye mvi
nyingi kichwani akapatwa na
mshangao mkubwa
“Graca !! akasema huku
akiinuka na kumkumbatia Graca
“Oh Graca,umerudi !! Mungu
mkubwa sana” akasema Yule mzee
aliyeonekana kumfahamu vyema
Graca
“Nimefurahi kukuona tena
mzee Abel” Akasema Graca na
kuketi kitini Ama kweli Mungu
anaweza.Nimekuwa
nakukumbuka sana katika
maombi yangu ya kila siku na
Mungu amesikia kilio chetu na leo
umerejea tena .Karibu sana.Vipi
hali yako? Akasema mwalimu Abel
“nashukuru sana mwalimu
Abel kwa sala na maombi
yako.Kwa sasa mimi ni mzima na
ninaendelea vizuri” akasema
Graca
“karibu sana Graca” mwalimu
Abel akamkaribisha tena
Graca.Kikapita kimya kifupi Graca
akasema
“Mwalimu Abel mimi si mkaji
sana nimepita hapa mara moja
kukusalimu lakini shida yangu
kubwa iliyonileta ni kuonana na
padre kalistus.Ninaweza kumpata? Padre kalistus yupo ila yuko
katika ibada.Wana mafungo ya
wiki mbili hapa parokiani lakini
ninaweza kukuitia.Subiri kidogo
hapa ofisini nikamuite” akasema
Mwalimu Abel huku akiinuka na
kabla hajafika mlangoni Graca
akamuita
“mwalimu Abel kuna jambo
lingine nataka kukuomba”
“Omba Graca” akasema
mwalimu Abel
“Ninaomba zaidi yako na
padre kalistus,asifahamu
mwingine yeyote kama niko
hapa.Nina sababu zangu za
kuomba hivyo”
“Usihofu kuhusu hilo
Graca.Hakuna atakaye fahamu
chochote .Nisubiri nikamuite
padre kalistus” Baada ya dakika kumi hivi
mwalimu Abel akarejea
“Padre kalistus ameelekeza
akukute katika ofisi yake.Twende
nikupeleke” akasema mwalimu
Abel na kumuongoza Graca katika
ofisi ya padre Kalistus na
kumuacha pale akimsubri.Zilipita
dakika kadhaa na padre akawasili
“Graca !! akasema padre na
Graca akasimama wakasalimiana
“Sikuamini mwalimu Abel
aliponieleza kwamba umekuja.Vipi
maendeleo yako? Vipi hali yako?
Pole na matatizo yaliyokukuta”
“Ahsanate sana
Padre.Nawashukuru sana kwa
kuniombea bila kuchoka na kwa
msaada mkubwa wa sala zenu
ninaendelea vyema” Pole sana Graca.Nilistushwa
mno niliposikia kuhusu matatizo
yaliyokupata.Nini hasa kilitokea?
Wote hapa hatuelewi ni kitu gani
hasa kilikupata kwa sababu kila
mtu anaongea analolifahamu”
“Padre,mambo yaliyonikuta ni
mengi sana na itachukua muda
kukueleza yote.Nitatafuta wasaa
nitakuja nikueleze kila kitu.Kwa
sasa nimepita kuuchukua ule
mkoba niliokupa unitunzie.Bado
unao?
“Ndiyo bado ninao na
nimeuhifadhi sehemu salama
kama ulivyoomba”akasema Padre
kalistus halafu akaenda chumbani
kwake na baada ya muda akareje
ana ule mkoba aliopewa na Graca. Mkoba wako huu hapa.Uko
salama kabisa na haujawahi
kufunguliwa”
“Ahsante sana baba
Padre.Nakuahidi nitakuja tena
siku nyingine kukusimulia mkasa
wangu”
“karibu sana Graca.Muda
wowote ukiwa na tatizo lolote
usisite kuja nasi tutakusaidia’
“Ahsante sana padre,wewe ni
baba yangu wa kiroho na nitakuja
kukueleza kila kitu ila kuna jambo
moja nataka kukuomba’
“Jambo gani?
“Naomba asifahamu mtu
yeyote kama nimefika hapa na
kama nilikupa mkoba unitunzie”
Padre kalistus akamtazama
Graca usoni na kuuliza Graca kuna kitu gani
kinaendelea?
“Nitakuja kukueleza baba
padre.Ahsante sana kwa
kunitunzia mkoba wangu”
akasema Graca na kutaka
kuondoka lakini padre akamzuia
na kumtaka apige magoti ambariki
na baada ya kubarikiwa akainuka
wakaagana na kutoka mle
ofisini,moja kwa moja akaelekea
mahala walipoegesha gari .Elvis
aliyekuwamo garini akashuka na
kumpokea Graca ule mkoba
akamfungulia mlango akaingia
wakaondoka.
“Elvis huo ndio mkoba wenye
kompyuta yenye ushahidi wa kila
kitu nilichokueleza.Huo mkoba ni
chanzo cha matatizo yangu yote
na sababu ya mama yangu kufariki.Tafadhali naomba wote
wanaohusika wakamatwe na
wachukuliwe hatua kwa uharamia
wanaoufanya.Ninakukabidhi
kompyuta hiyo nikiwa na imani
kwamba imefika katika mikono
salama”akasema Graca
“Ahsante sana
Graca.Nakuahidi hakuna yeyote
katika mtandao huu
atakayesalimika.Wote
watafikishwa mbele ya sheria
tukianzia na baba yako Frank”
“Ahsante Elvis.Tunaelekea
wapi?akauliza Graca
“ kwa sasa tunaelekea
nyumbani kwangu.Kuna vitu
ambavyo nahitaji kuvichukua”
akasema Elvis.
Safari ikawa ya kimya kimya
na baada ya saa moja hivi wakawasili nyumbani kwa
Elvis.Akapiga honi geti
likafunguliwa na mtumishi wa
ndani
“kaka Elvis ,karibu
sana.Shikamoo” akasalimia
“Marahaba Stella,hujambo?
‘Sijambo kaka pole na safari”
“Ahsante sana.Vipi likizo yako
ilikuaje? Wazee nyumbani
hawajambo?
“Nyumbani wote wazima
wanawasalimu sana” akasema
Stella mtumishi wa ndani wa
akina Elvis ambaye alikuwa
amekwenda nyumbani kwao kwa
mapumziko na sasa amerejea
“Elizabeth naye hajambo?
Akauliza Elvis
“Ameondoka asubuhi ya leo
kuelekea Iringa” akasema Stella Sawa Stella mimi nilikuwa
na safari ya kikazi na nimerejea”
akasema Elivs na kuelekea
chumbani kwake.Akakitazama
chumba chake na kutabasamu
“Home sweet home” akasema
na kuchukua simu yake iliyokuwa
mezani akaiwasha na kuzitafuta
namba za Patricia akampigia
lakini simu ya Patricia haikuwa
ikipatikana
Nyuma ya kabati kubwa la
nguo kulikuwa na mlango
akalisukuma kabati na kuufungua
mlango akaingia katika chumba
kidogo.Hiki kilikuwa ni chumba
maalum ambacho huhifadhi vitu
vyake vya siri na huingia yeye na
Patricia pekee.Akakusanya vitu
alivyoona vinaweza kumsaidia
akapakia katika begi kubwa akarejea tena chumbani kwake
akachukua baadhi ya vitu vyake
akapakia katika begi lingine na
kutoka akakutana na Stella
“Kaka unasafiri tena?
Akauliza Stella na kumpokea Elvis
begi moja.
“Ndiyo nimepata safari
nyingine ya kikazi” akasema Elvis
kisha wakaongozana na Stella
hadi garini.Stella akastuka kidogo
baada ya kumuona Graca ndani
ya gari.Hakujua kama Elvis
alikuwa na mtu mwingine
garini.Elvis akapakia mabegi yake
garini na kumgeukia Stella
“Dada yako akirudi mwambie
nimerudi toka safari lakini
nimepata tena safari nyingine ya
kiazi” akasema Elvis akageuza gari
na kuondoka una nyumba nzuri sana
elvis” akasema Graca
‘Thank you” akajibu Elvis
halafu akachukua simu yake
akajaribu kumpigia tena Patricia
lakini bado simu haikuwa
ikipatikana,akaamua kuizima
kabisa simu
Waliwasili makazi mapya na
kukuta tayari Doreen amekwisha
rejea
“Nilipatwa na woga baada ya
kurejea na kukuta nyumba
tupu.Welcome home.Lunch is
ready” akasema Doreen na
kuwaongoza akina Elvis hadi
chumba cha chakula .Baada ya
kupata chakula Elvis akaendelea
na kazi ya kufunga kamera za
ulinzi na kuziunganisha na kompyuta yake na hivyo kuweza
kuona kila pembe ya nyumba ile.
*****************
Saa kumi na moja za jioni
Patricia akarejea nyumbani.Mara
tu baada ya kushuka garini
akakutana na sura yenye
tabasamu ya Stella
‘Shikamoo dada.Pole na kazi”
akasema Stella na kumpokea
Patricia mkoba
“Marahaba habari za hapa?
“Habari nzuri dada.Kaka Elvis
amerudi’
“Elvis amerudi?
“Ndiyo dada”
“Yuko ndani? Akauliza
Patricia kwa furaha Hapana amekwisha
ondoka.Alikuwa na haraka na
hakukaa sana.Aliingia ndani na
baada ya muda akatoka na mabegi
mawili akasema nikwambie
kwamba amekwisha rudi lakini
ameondoka tena”
“Alikuwa peke yake?
“Hapana ,hakuwa peke
yake.Alikuwa na msichana mmoja
ndani ya gari”
Patricia akasimama kwa
dakika moja akifikiria halafu
akachukua mkoba wake na
kuingia chumbani.
“Kwa nini Elvis hakunitaarifu
kama anarejea leo?Amekwenda
wapi tena?siku zote aondokapo
kama mimi sipo huwa anaacha
ujumbe mezani,mbona leo
hajaacha ujumbe wowote ?huyo msichana aliyekuwa naye garini ni
nani?”
Patricia akajiuliza maswali
mfululizo lakini akakosa
jibu.Akafungua chumba cha siri
cha Elvis na kukuta vifaa vingi
havipo.
“Huyu Elvis hii kazi yake
imeanza kunichosha.Kila mara
yuko kazini hana mapumziko
maalum.Sipati muda wa kutosha
wa kuwa naye,Oooh gosh!Sasa
ndo naanza kuuona ubaya wa kazi
hii aliyoichagua .Sijui ni kwanini
aliamua kuifanya kazi hii. Alikuwa
na uwezo mkubwa wa kuwa
daktari au mhandisi lakini
akachagua kuifanya kazi hii
ambayo inamnyima maisha
mazuri.I’m in hell right now and I
need him by my side but he’s away” akawaza patricia halafu
akachukua simu na kujaribu
kumpigia Elvis lakini simu yake
haikuwa ikipatikana.
“Where is he now? Huyo
mwanamke aliyekuwa
ameongozana naye ni nani? Wako
wapi muda huu na wanafanya
nini? Nashindwa kujizuia kuwa na
wivu.ninaelewa Elvis ananipenda
na hawezi kabisa kunisaliti lakini
kwa hali ilivyo hivi sasa anything
can happen” akawaza Patricia
halafu akaingia bafuni
kuoga.Kisha maliza kuoga akavaa
vizuri akajitazama katika kioo na
kuvuta pumzi ndefu
“I’m so pretty .Mungu
amenijalia uzuri wa kipekee lakini
kwa sasa uzuri wote huu hauna
faida yoyote kwangu.Sina thamani yoyote” akawaza Patricia halafu
akachukua mkoba wake
akamuaga Stella na kuingia garini
akaondoka
Mita kama mia mbili toka
aliache geti la nyumba yao simu
yake ikaita akatupia jicho
kutazama mpigaji alikuwa ni
mama mkwe wake yaani mama
yake elvis.Patricia akaguna na
kuitupa simu ile katika kiti cha
pembeni na kuiacha ikiendelea
kuita
“Huyu mama sitaki kupokea
simu yake anaweza akaniharibia
kabisa siku yangu kwa maneno
yake ya kejeli.Toka alipoanza
kuongelea masuala ya
mtoto,nimejkuta nikimchukia
sana.Nina wasi wasi anaweza hata
akaivunja ndoa yetu kamasintasimama imara” akawaza
Patricia.
Baada ya simu yake
kutopokelewa na Patricia mama
yake Elvis akaamua kupiga simu
ya mezani ambayo ilipokelewa na
Stella.Mama Elvis akamuuliza
Patricia
“Dada Patricia hayupo
.Ameondoka muda si mrefu sana”
akasema Stella
“Mume wake naye yupo?
akauliza mama Elvis
“Kaka Elvis amekwenda
safari”
“Mhhn ! Mama Elvis akaguna
kidogo na kuuliza tena
“Patricia amekwambia
anaelekea wapi?
“Hapana mama hajaniambia
anaelekea wapi” “Kwa namna alivyokuwa
amevaa wakati anatoka unadhani
amekwenda kazini?
“Sina hakika kama
amekwenda kazini kutokana na
mavazi aliyoyavaa.Ninafahamu
mavazi yake ambayo hupenda
kuvaa akienda kazini.Nina hakika
hajaenda kazini”
“ Sawa ahsante Stela”
akasema mama Elvis na kukata
simu
Patricia aliendelea na safari
yake mara ukaingia ujumbe katika
simu yake.Kwa kuwa alikuwa
barabarani alishindwa kuusoma
ujumbe ule.
Aliwasili Silvano hotel mahala
panapofanyika sherehe ya
kumkaribisha daktari bingwa wa
neva za fahamu toka Texas marekani anaitwa Dr Stephen
Washington.Daktari huyu bingwa
aliombwa na serikali kwa maombi
maalum ya serikali ya Tanzania ili
kuimarisha kitengo cha neva za
fahamu na alitarajiwa kuwepo
nchini kwa miaka minne
Toka amefika nchini yapata
wiki moja sasa amekuwa na
ukaribu mkubwa na Patricia
ambaye amemsaidia sana
kuyafahamu na kuyazoea
mazingira mapya ya kazi.Usiku
huu uongozi wa hospitali uliamua
kufanya sherehe ndogo ya
kumkaribisha rasmi
Patricia akaegesha gari na
kabla hajashuka akachukua simu
ili ausome ujumbe ule ulioingia
wakati akiwa
barabarani.Akausoma ujumbe ule akaegemea kiti huku machozi
yakimtoka.Akarudia kuusoma
tena ujumbe ule uliotoka kwa
mama mkwe wake ambao
ulisomeka hivi
“ Mumeo akitoka na wewe
unatoka.Hivyo ndivyo
ulivyofunzwa kwenu? Kaa jitulize
nyumbani muache mwanangu
akanitafutie mjukuu kwa wale
walio tayari kumzalia mtoto”
“Patricia alihisi kama kisu
kikali kimepenya na kuuchoma
moyo wake.Alihisi maumivu
makali ya moyo.Aliumizwa mno na
maneno yale mazito ya dharau na
kashfa.Alishindwa afanye nini
akabaki ameegemea kitu akilia
“Najuta kwa nini nilikubali
kuolewa na Elvis.Nilijua lazima
mambo kama haya yatajitokeza tu.Ee Mungu nisaidie nipe nguvu
ya kuhimili kipindi hiki kigumu
katika maisha yangu.Niko katika
majaribu makubwa.Sina jib.….”
Patricia akatolewa mawazoni na
mtu aliyegonga kioo cha
dirisha.Haraka haraka akafuta
machozi na kushusha kioo
“Samahani mama una tatizo?
Akauliza kijana aliyekuwa
amevalia sare za ulinzi
“Hapana sina tatizo” akajibu
Patricia na kupandisha kioo cha
gari akachukua mkoba wake na
kushuka akaelekea ukumbini
huku akihisi kushindwa kutembea
kutokana na miguu kuwa
mizito.Kabla ya kuingia ukumbini
akaenda katika chumba cha
wanawake akachukua poda na
kujipaka usoni.Hakutaka mtu yeyote agundua kama alikuwa
analia.Alijitazama katika kioo na
kujiona yuko sawa akaelekea
ukumbini.Tayari wengi wa wageni
walikwisha wasili akiwepo Dr
Stephen
Usiku huu Patricia alikuwa
mkimya sana na hakuonekana
kutaka maongezi na mtu yeyote
kitu ambacho si kawaida
yake.Pamoja na kumfahamu
patricia kwa mud amfupi,Dr
Stephen aligundua patricia
hakuwa sawa.
“Kuna tatizo lolote Dr
Patricia? akauliza Dr Steven
“Hapana hakuna tatizo”
akajibu Patricia na kwa mbali Dr
Steven akayaona machozi katika
macho ya Patricia Patricia akainuka na kwenda
katika chumba cha
wanawake.Bado machozi
yaliendelea kumtoka.Akajifuta
machozi na kurejea
ukumbini.Sherehe zikaanza.Dr
Steven alijiuliza maswali mengi
kuhusiana na tatizo
linalomsumbua Patricia
Wakati sherehe ikiendelea
wageni waliendelea kuburudika
kwa vinywaji mbalimbali Patricia
alikuwa akinywa mvinyo
mkali.Alitaka atulize
mawazo.Alitaka ayasahau
matatizo yake yote
aliyonayo.Hatimaye ukawadia
wakati wa kucheza muziki.Dr
Steven ambaye naye alikuwa
anatumia mvinyo akamshika
mkono Patricia na kumuomba wakacheze.Wakati wakicheza
muziki wa taratibu Patricia
akajikuta akipatwa na hisia za
ajabu akahisi kama anacheza na
Elvis na mara Dr Steven
akagundua Patricia alikuwa analia
“Patricia kuna tatizo gani?
Nini kinakuliza?akauliza Dr
Steven akijaribu kumbembeleza
Patricia
“Steven tafadhali naomba
uniondoe hapa.” Akasema huku
akilia.Dr Steven akahisi lazima
kuna jambo zito lililomsibu
Patricia.Akamshika mkono na
kumuongoza nje ya ukumbi
akampeleka katika bustani.Bado
patricia aliendelea kulia kwa
kwikwi
“Patricia tafadhali nieleze una
tatizo gani? Akauliza Dr Steven “Dr Steven siwezi kuvumilia
zaidi ya hapa !! akasema Patricia
“Nini kimetokea?Una tatizo
gani?Niambie tafadhali mimi ni
rafiki yako nitakusaidia” akasema
Dr Steven.Patricia akamtaka Dr
Steven ampeleke katika gari
lake.Steven akamshika mkono
akamuongoza Patricia kuelekea
katika gari lake akamfungulia
mlango akaingia.Patricia akampa
Dr Steven funguo za gari.
“Nikupeleka nyumbani?
Akauliza Dr Steven baada ya
kuwasha gari
“Tafadhali niondoe eneo hili
Steven.Nipeleke kokote.” akasema
Patricia.
“ Nyumbani kwako?
“Hapana sitaki kwenda
nyumbani kwangu.Nipeleke sehemu yoyote nikapumzishe
kichwa lakini si nyumbani
kwangu” akasisitiza Patricia.Dr
Steven akamtazama kwa sekunde
kadhaa kisha akaondoa gari
********************
Ukimya wa hali ya juu
ulitawala katika eneo zima
kulizunguka kasri la aliyewahi
kuwa waziri mkuu David
Sichoma.Licha ya ulinzi anaopewa
na serikali lakini David ana walinzi
wake maalum aliowakodisha toka
nje ya nchi kwa ajili ya kumlinda
wakisaidiwa na mbwa maalum
wawili wenye mafunzo.Kwa ulinzi
ulikuwa mkali sana eneo hili. Saa mbili na dakika ishirini
za usiku gari tatu zikawasili katika
makazi ya David.Geti kuu
likafunguliwa na gari zile
zikaruhusiwa kupita na kuelekea
sehemu ya kuegesha.Watu saba
wakashuka toka ndani ya gari
mbili na wote walivaa vifaa vya
mawasiliano masikioni .Baada ya
kuhakikisha eneo liko salama
mmoja wao akaufungua mlango
katika gari la kati kati akashuka
makamu wa rais mheshmiwa
Shafi Abdulkhareem Omar
akalakiwa na David.Walisalimiana
kwa furaha kubwa kisha David
akamuongoza makamu wa rais
kuelekea ndani akifuatana na
walinzi wake hadi katika sabule
kubwa .Makamu wa rais
akawaomba wasubiri hapo kwani alikuwa na maongezi ya faragha
na David.Wakaingia katika
chumba cha pembeni
kilichoonekana kama maktaba
kilichokuwa na mlango wa kioo
lakini maongezi hayakuweza
kusikika nje.
“karibu sana mheshimiwa
Shafi” akasema David
“Ahsannte sana
David.Nimefurahi sana kukutana
nawe tena usiku huu.Maisha
yanakwendaje?Naona mambo si
mabaya toka uachane na mambo
ya siasa mwenzetu unazidi kuwa
kijana badala ya kuzeeka”
Kauli ile ya makamu wa rais
ikamfanya David aangue kicheko
kikubwa
“Usemayo yanaweza kuwa na
ukweli Shafi.Toka nimeachana na siasa hizi za majitaka
nimeeleekeza nguvu zote katika
kuimarisha afya yangu.Ninakula
vizuri na kufanya mazoezi ya
kutosha na ndiyo maana unaniona
nimenawiri namna hii.Vipi huko
serikalini mnaendeleaje?
“Huko ni kama kawaida.Siku
ikiisha salama unashukuru
Mungu lakini kwa kuwa
tumechagua wenyewe kuingia
katika siasa hatuna budi
kukubaliana na kila linalojitokeza”
“Vipi kuhusu mahusiano yako
na rais yanakwendaje?
Yameimarika siku hizi?David
akauliza
“kwa kweli mpaka leo mimi na
mheshimiwa rais bado hatuna
mahusiano mazuri kitu ambacho
kinaifanya kazi yangu kuwa ngumu sana.Ninafikikiria baada
ya kumaliza kipindi
changu,ninataka niachane kabisa
na siasa niishi kama wewe”
“Pole sana
mheshimiwa.Mambo kama hayo
katika ulingo wa siasa
hayakosekani”
“Nalifahamu hilo” akajibu
makamu wa rais halafu kikapita
kimya kifupi na makamu wa rais
akasema
“David nilikuwa na kikao
usiku huu lakini nimekiahirisha
hadi kesho asubuhi ili nije
kuonana nawe kama
ulivyonisisitiza .Naamini una
jambo la muhimu sana uliloniitia
hapa” akasema makamu wa rais
“Kwanza kabisa nakushukuru
sana mheshimiwa kwa kuitika wito.Ni heshima ya pekee umenipa
na nina hakika kufika kwako hapa
leo haujapoteza muda
bure”akasema David
“Mr Shafi ,nimekuita hapa
kwa ajili ya kuongelea suala zito
linalohusu maslahi mapana ya
nchi yetu na mustakabali mzima
wa maisha yetu ya kisiasa”
Akanyamaza tena na
kumtazama makamu wa rais
aliyekuwa kimya akimsikiliza
halafu akaendelea
“Hivi majuzi tumepokea ugeni
mzito wa rais wa marekani.Ni
ugeni wa kihistoria
sana.Sambamba na lengo la rais
huyo kuja kusaidia miradi kadhaa
ya kimaendeleo lakini kuna
mambo makubwa mawili
yaliyomleta.Nina hakika unayafahamu mambo hayo ni
mambo gani kwani hata katika
maamuzi yake nawe umeshiriki”
akasema David na kumstua
kidogo Shafi
“Ina maana tayari umekwisha
fahamu mambo yaliyofanyika
katika ujio ule wa rais wa
marekani? makamu wa rais
akashangaa
“Mr Shafi dunia ya sasa
inazidi kuwa ndogo kwa hiyo
hakuna kitu chochote
kinachoweza kufanyika bila
kujulikana.Taarifa zote ninazo
kuhusiana na mikataba ya mafuta
,gesi na suala la ujenzi wa kambi
kubwa ya kijeshi ya jeshi la
marekani hapa nchini”
“Mambo yote haya
umeyapataje? Akauliza Shafi Usishangae Mr Shafi.Mimi ni
mtu mwenye vyanzo vingi vya
taarifa .Tuachane na
hayo.Nimekuita hapa ili tuweze
kujadili masuala ya msingi sana
yanayohusiana na namna hayo
niliyokueleza” akasema David na
kutulia kidogo halafu akaendelea
“Juzi tulipata ugeni wa watu
wawili toka nchi za mashariki ya
kati zenye kuzalisha mafuta kwa
wingi duniani na ambazo uchumi
wake mkubwa unategemea
mafuta.Watu hao walitumwa kama
wawakilishi wa serikali na
makampuni makubwa ya mafuta
toka eneo la mashariki ya
kati.walitumwa hapa Tanzania
kufuatia kikao kilichofanyika
baina ya nchi zinazotegemea
mafuta kwa uchumi na wakuu wa makampnuni makubwa ya
mafuta.Katika kikao hicho
walijadili hali ya biashara ya
mafuta duniani na tishio la
biashara hiyo baada ya
makampuni ya marekani
kuruhusiwa kufanya uwekezaji
mkubwa katika sekta ya mafuta
nchini Tanzania.Hofu kubwa
iliyonayo mataifa ya mashariki ya
kati ambayo uchumi wake mkuu
unategemea mafuta kwani kiasi
cha mafuta ni kwamba kiasi cha
mafuta kilichogunduliwa Tanzania
ni kikubwa sana na endapo
marekani itakuwa ndiye mwekezaji
pekee wa mafuta hayo hapa
Tanzania kuna hatari kubwa sana
soko la mafuta ya mashariki ya
kati kuyumba sana na hivyo
kuhatarisha chumi zao.Kwa sasa sera ya marekani ni kupunguza
utegemezi wa mafuta ya kuitoka
nje hasa mashariki ya kati kwa
hiyo uwekezaji watakaoufanya
Tanzania utaifanya marekani na
washirika wake ambao ni
wanunuzi wakubwa wa mafuta
hayo wasihitaji tena mafuta
kutoka mashariki ya kati na hivyo
bei ya mafuta kushuka na chumi
za nchi za mashariki ya kati
kuyumba.Baada ya majadiliano
marefu umefikia uamuzi kwamba
jambo hili ni hatari kwa mataifa ya
kiarabu.Hii ni vita mpya kati ya
marekani na mataifa ya kiarabu
yanayozalisha mafuta.kwa mantiki
hiyo basi mataifa hayo yameazimia
kupambana na marekani kwa kila
namna wanayoweza ili
kuhakikisha kwamba mpango wao wa kuwekeza katika sekta ya
mafuta Tanzania haufanikiwi”
akatulia akamtazama makamu wa
rais na kuendelea
“Wajumbe hao waliotumwa
Tanzania wametukabidhi sisi kazi
hiyo ya kuhakikisha kwamba
jambo hilo halifanikiwa”
Kimya kikatawala mle
chumbani.Baada ya dakika moja
makamu wa rais akauliza .
“Nimekusikiliza vizuri David
lakini bado sijakuelewa
vizuri.Mataifa hayo ya kiarabu
yanataka ninyi mfanye nini?
Mtawezaje kulifanikisha hilo
wanalolitaka?
“Kikubwa wanachokitaka ni
sisi kuhakkisha kwamba mpango
huo wa makampuni makubwa ya
mafuta ya marekani kuwekeza Tanzania haufanikiwi na badala
yake makampuni ya kiarabu ndiyo
yapewe nafasi hiyo ya kuwekeza
katika sekta ya mafuta hapa
Tanzania na hivyo kuendelea
kulitawala soko la mafuta
duniani.Kingine wanachokitaka ni
kuhakikisha kwamba mpango wa
serikali ya marekani kutaka
kujenga kituo kikubwa cha kijeshi
hapa Tanzania halifanikiwi”
Makamu wa rais akainama na
kufikiri kwa muda halafu akinua
kichwa na kusema
‘Bado umeniacha gizani
David.Jambo hili linawezaje
kuzuiwa? Tayari mikataba
imekwisha sainiwa na hakuna
namna ya kuweza
kuitengua.Suala hili haliwezekani”
akasema Shafi. Linawezekana kabisa Mr
Shafi’ akasema David
“Inawezekanaje David?
“kwa kuiangusha serikali
iliyopo madarakani”
Kauli ile ilimstua mno
makamu wa rais.Akasimama na
kumtazama David kwa hasira na
kusema
“Sikutegemea kama katika
dunia hii ya leo bado kuna watu
wenye mawazo ya kijinga kama
yako David.Siamini macho yangu
David !! Ni wewe kweli !! akasema
makamu wa rais kwa mshangao
mkubwa
“Nmeshangaa sana.Sikujua
kama unaweza ukawa na mawazo
ya kipumbavu namna hii.Nilidhani
umeniitia jambo la maana kumbe
ni huu ujinga.Ahsante kwa kunipotezea muda wangu”
Akasema makamu wa rais na
kuinuka akataka kuondoka.
“Mr Shafi calm down
.tafadhali usiondoke.Naomba
uendelee kunisikiliza” Akasema
David
“Siwezi kukaa hapa na
kuusikiliza upuuzi wako
huu.Ninakuonya David usijaribu
kabisa kufanya hicho
unachofikiria kukifanya wewe na
wenzako” akasema makamu wa
rais
“Naomba unisikilize mr
Shafi.Nipe dakika tano tu na
utaamua nini cha kufanya”
akasema David huku akiushika
mkono wa makamu wa rais na
kumsihi aketi.Shafi akaketi.
 
I DIED TO SAVE MY PRESDENT

Sehemu 28


Haya niambie hicho
unachotaka kuniambia” akasema
Shafi kwa ukali.
“Hata mimi nilipoingizwa
katika mpango huu nilistuka zaidi
yako na nilihamaki kama wewe
lakini baada ya kutulia na
kusikiliza kwa makini nilielewa na
nikauona umuhimu wa mpango
huu na mwishowe nikaamua
kushiriki” akasema David na
kumtazama David
“Shafi sisi ni wanasiasa na
tunafahamiana
vyema.Tunafahamu nia zetu na
nini tumefuata katika siasa.Kila
mwanasiasa lengo lake kubwa ni
kupata madaraka ya juu kabisa ya
uongozi.Ilikufikia malengo yake
kila mwanasiasa anatumia kila mbinu ili aweze kufikia malengo
yake”
Akatulia na kumtazama Shafi
ambaye alionekana kuanza
kupunguza hasira na kumsikiliza
David
“Shafi wewe si mgeni wa
mambo machafu yanayofanyika
katika ulingo wa siasa.Siasa zetu
zimejaa mambo mengi machafu na
sina haja ya kuyasema kwani
unayafahamu.Mimi nimekuwa
waziri mkuu na wewe ni makamu
wa rais unafahamu vyema nini
ninaongelea” David akatulia
akamtazama makamu wa rais na
kuendelea
“Shafi ninakufahamu vizuri
sana.Kwa muda mrefu umekuwa
ukiasisi kwa siri harakati za
Zanzibar ijiondoe katika serikali ya muungano na iwe dola huru.Nina
fahamu wewe ndiye uliye nyuma
ya vuguvugu linaloendelea hivi
sasa kutaka Zanzibar ijiondoe
kutoka katika serikali ya
muungano.Ninazo taarifa zote
kuhusu ushiriki wako katika suala
hili” akasema David
“David unathubutuje
kunitamkia maneno hayo ya
kipuuzi? Mimi ni makamu wa rais
wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania ni mtu mwenye
dhamana kubwa na kamwe siwezi
kwenda kinyume na katiba ya
jamhuri ya muungano wa
Tanzania niliyoapaa kuilinda”
akasema kwa ukali Shafi
“Shafi naomba upunguze
jazba ndugu yangu na tuongee
vizuri tuelewane.Nadhani mimi unanifahamu vizuri na
unafahamu vile vile kwamba haya
nikwambiayo ni ukweli
mtupu.Hata hivyo tuachane na
hayo mambo na tujielekeze katika
jambo la msingi” akasema David
na kumtazama Shafi ambaye
alionekana kuanza kushusha
jazba
“Shafi nafahamu lengo lako
kubwa ni kuitawala Zanzibar na
ndiyo maana unafanya harakati za
chini chini ili Zanzibar
ijitenge.Kwa uhalisia suala la
Zanzibar kujitenga na kuwa dola
huru ni gumu sana na njia pekee
ya kuhakikisha kwamba hilo
linawezekana ni kwa kutumia njia
ya mapinduzi.Shafi huu ndio ule
muda uliokuwa unausubiri wa
kutimiza lengo lako la kuiongozaZanzibar huru.Endapo utaungana
nasi na tukafanikiwa kuiondoa
serikali ya jamhuri ya muungano
madarakani mimi ndiye
nitakayekuwa rais wa Tanzania na
bila kuchelewa tutauvunja
muungano na wewe utakuwa rais
wa Zanzibar iliyo huru.Sina
hakika kama utakuwa tayari
kuiachia fursa hii iliyojitokeza
itakayokusaidia kutimiza malengo
yako.Ni wakati wako wa kuamua
kama utapenda kushirikiana nasi”
akasema David.Shafi akainama
akafikiri kwa muda wa kama
dakika moja hivi halafu akatoa
pakiti la sigara akawasha moja na
kuvuta kisha akasema
“Mpango wenyewe
mmeupangaje? Nani na nani wanashiriki katika huo mpango
wenu?
David akatabasamu na
kukohoa kidogo akamueleza Shafi
namna mpango mzima
ulivyoandaliwa na maendeleo
yake.Alipomaliza maelezo yale
Shafi akajikuta anatabasamu
“Sawa David.Nimekuelewa na
nimeuelewa mpango
mzima.Nitashirikiana nanyi lakini
kwa masharti.Baada ya mipango
yote kwenda vizuri nitaomba
nialikwe katika kikao cha
wahusika wote ili na mimi nipate
nafasi ya kuzungumza nao”
akasema Shafi
Mazungumzo yaliendelea hadi
saa saba za usiku walipoagana na
makamu wa rais akarejea katika
makazi yake******************
Saa mbili za usiku baada ya
kumaliza kupata chakula cha
usiku Elvis akamuomba Graca
aende chumbani kwake
kupumzika kwani alionekana
kuchoka sana.Sebuleni pale
wakabaki Elvis na Doreen
wakitazama runinga
“Elvis mlienda wapi mchana
na Graca? Akauliza Doreen
“Kuna mahala Graca
alinipeleka”
‘Tayari amekwisha kueleza
kile ambacho aliahidi kukueleza?
“Ndiyo amekwisha nieleza”
“Good” akajibu Doreen na
ukimya utawala “Doreen” akaita Elvis na
kuuvunja ukimya
“Unasemaje Elvis?
“Nataka nikushukuru kwa
dhati kabisa kwa namna
ulivyojitolea
kunisaidia.Umenisaidia msaada
mkubwa .Ahsante sana”
Doreen akatabasamu na
kusema
“Elvis kama nilivyokuahidi
kwamba siku yoyote na muda
wowote mimi niko tayari
kukusaidia kwa msaada wowote
unaouhitaji.Usihofu kuomba
chochote toka kwangu”
“Ahsante sana Doreen”
Kikapita kimya cha sekunde
kadhaa Doreen akasema
“Elvis kwa muda gani
unategemea kukaa hapa? Swali lile likaonekana gumu kidogo kwa
Elvis akafikiri kidogo na kusema
“Sifahamu ni kwa muda gani
lakini hadi hapo
nitakapokamilisha zoezi la
kumtafutia Graca makazi ya
kudumu nje ya nchi.Kwa hali
ilivyo Graca hatakiwi kuishi hapa
nchini kabisa.Ninafikiria
kumfanyia mpango wa kumpeleka
Marekani akaishi kule.Nitaanza
kulishughulikia suala lake
kuanzia kesho”
“Unadhani unafanya vizuri
kutomshirikisha Patricia ili ajue ni
kitu gani kinachoendelea hivi
sasa?
“Nafahamu sifanyi vizuri
lakini sina namna nyingine ya
kufanya.Suala ninaloshughulikia ni zito na hapaswi kufahamu
chochote”
“Nafahamu hilo Elvis lakini
huoni kama utakuwa unauumiza
sana moyo wake ?
“Nafahamu ataumia na hata
mimi ninaumia pia lakini sina
namna nyingine ya
kufanya.Lazima niishi hapa kwa
muda ili kumlinda Graca ambaye
amenipa taarifa nzito sana na pili
kulishughulikia suala zito kwa
mustakabali wa taifa.Leo mchana
nilifika hadi nyumbani kwangu
nikajaribu kumpigia simu Patricia
lakini simu yake haikuwa
ikipatikana.Niliacha maagizo kwa
mtumishi wetu wa ndani
amfahamishe kwamba tayari
nimerejea toka Afrika kusini lakini
nimekwenda katika kazi nyingine.Tafadhali naomba
usimueleze Patricia chochote au
hata kumuonyesha mahala nilipo”
akasema Elvis.Doreen
akatabasamu na kuuliza
“Elvis you are so handsome
and intelligent.Kwa nini
usiachane na kazi hii kwani
hufanani nayo kabisa.Kazi hizi
zinahitaji mtu uwe na moyo
mgumu na mwenye uwezo wa
kuua muda wowote .Elvis una
moyo wa huruma ,una sura nzuri
ya upole na ulipaswa kuwa daktari
na si kazi hii.Please think twice
about this job.If you cant do it for
yourself doit for Patricia.Wewe
ndiye mfariji wake mkuu na
angependa awe nawe kila wakati
lakini kazi hii inakufanya uwe
mbali naye hata kwa nyakati zile anazokuhitaji sana” akasema
Doreen .Elvis akatabasamu na
kusema
“Wewe si mtu wa kwanza
kuniuliza swali kama hilo.Wengi
wananiuliza lakini kazi hii
nimeipenda mwenyewe na
ninafurahia kuifanya.lakini ni kazi
yenye changamotokubwa kwani
inanifanya nisimuamini mtu
yeyote hata mke wangu na
inaniweka mbali na familia na
hata mke wangu.Najua anateseka
kwa hilo lakini sina namna
nyingine”
“Sawa nimekuelewa Elvis”
Akasema Doreen halafu kikapita
kimya kifupi akasema
“Elvis leo nitalala hapa.Sitaki
kuondoka kuwaacha peke yenu” Usihofu Doreen we’ll be
ok.Umefanya kazi kubwa na sasa
unapaswa uende ukapumzike”
‘Nitapumzika hapa hapa leo”
akasisitiza Doreen.Elvis
akamtazama kana kwamba
ameshangazwa kwa kitendo kile
cha Doreen kuamua kulala pale
“Mbona unaniangalia hivyo
Elvis? Hutaki nilale hapa?
“si hivyo Doreen.Nyumba hii
ni kubwa na ina vyumba vya
kutosha.Jisikie huru.lakini vipi
usalama nyumbani kwako?
“Usijali kuhusu nyumbani
kwangu.Siku zote ni salama lakini
binafsi najihisi ni salama zaidi
nikiwa hapa na ninyi.Tukiachana
na hayo Elvis kuna jambo nataka
nikuombe”
“Omba Doreen” Nataka na mimi nije niishi
hapa na ninyi.”
Elvis akatabasamu na
kusema
“Are you serious?
“Yes I’m serious.Elvis kwa
sasa hata mimi najiona siko
salama.Tumesafiri safari ndefu
toka Mbeya .Vipi kama kuna watu
walikuwa wanatufuatilia?Naomba
tafadhali uniruhusu nikae hapa
pamoja nanyi ili nijihakikishie
usalama” akasema Doren.Elvis
akamtazama halafu akasema
“Uko sahihi.Samahani sana
Doreen kwa kukuingiza katika
matatizo makubwa.Sin..” Kabla
hajamaliza sentensi yake Doreen
akamsogelea na kumzika mdomo
kwa kidole chake. Shhhhh !!! don’t be sorry.”
Akasema Doreen.
“I’m going to bed” akasema na
kuinuka akaenda katika chumba
alichokuwa amekiandaa kwa ajili
yake.Elvis naye akainuka akaeleka
katika chumba cha maktaba
ambacho aliamua kukitumia kama
ofisi yake.Akaushika mkoba ule
aliopewa na Graca akaufungua na
ndani yake kulikuwa na kompyuta
ndogo.Akaiweka mezani na
kuitazama.
“Kazi imeanza” akasema huku
akiichomeka kompyuta ile katika
umeme na kuiwasha halafu
akaanza kufungua faili moja moja
kuangalia kilichomo
Ilimchukua zaidi ya saa tatu
kumaliza kupitia mafaili yote
yaliyokuwamo katika kompyuta ile.Uso wake ulikuwa unatoa
kijasho chembamba.Akainuka na
kuelekea jikoni akachukua chupa
ya maji ya kunywa
Katika kompyuta ile Elvis
alikutana na mambo mengi.Ni
kweli kulikuwa na biashara
iliyokuwa ikiendelea baina ya
baadhi ya maafisa wa jeshi na
waasi wa C201 wanaopigana na
serikali Kongo.Kwa miaka ya hivi
karibuni kundi hili la waasi
limeonekana kuwa hatari sana
kiasi cha kuilazimisha jumuiya ya
kimataifa kutuma kikosi maalum
cha wanajeshi wake kwenda
kuungana na jeshi la kongo
kupambana na waasi hao
Kupitia kompyuta ile,Elvis
aligundua kwamba kuna mtandao
mkubwa unaowahusisha watu wa ndani na nje ya nchi ambao kwa
pamoja wamekuwa wakifanya
biashara ya silaha na waasi hawa
na kuvuna pesa nyingi ikiwemo
madini ambayo waasi
hubadilishana na silaha
Hakukuwa na majina kamili
ya wahusika wakuu wa mtandao
huu lakini katika kumbu kumbu
za barua pepe ambazo Frank
alizihifadfhi katika kopmyuta hii
zilionyesha alikuwa akifanya
mawasilianio na mtu mmoja
aliyeitwa Deusdedith m.m.Huyu
ndiye aliyeonekana kupewa taarifa
za mara kwa mara na
Frank.Wakati mwingine ilionekana
mtu huyu akitoa maelekezo nini
kifanyike.Barua pepe nyingine
toka kwa Frank kwenda kwa
Deusdedith zilikuwa zikionyesha kiasi cha malipo walichopokea
baada ya mauzo ya silaha na mara
nyingine kiasi cha madini
kilichopatikana kwa kubadilisha
na silaha.Viambatanisho vya
miamala ya fedha vilionyesha
kwamba malipo yalikuwa
yakifanyika kupitia benki moja
iliyopo Uswisi.Ilionyesha kuna
watu waliokuwa wakikifadhili
kikundi hiki cha waasi cha C201
toka nje ya Congo
Kitu kingine alichokigundua
Elvis ni kwamba silaha hizo huja
nchini kama silaha za jeshi la
Congo na husafirishwa kama vile
zinakwenda Congo lakini huishia
katika mikono ya waasi.
“Watu hawa wana roho za
kinyama sana.Hawana ubinadamu
hata kidogo.Kitendo cha kuwauzia silaha waasi hawa ni kitendo
kisichovumiliwa kwani wamekuwa
wakizitumia silaha hizi katika
mauaji ya raia wasio na
hatia.Miezi miwili iliyopita
tumezika wanajeshi wetu watatu
waliouawa na waasi hawa kwa
silaha hizi hizi zinazouzwa na
akina Frank.Kibaya zaidi hata
ndani ya jeshi la Congo kuna watu
ambao wanahusika na biashara
hii.Hili ni jambo zito mno”
akawaza Elvis
“Graca ni msichana shujaa na
anastahili kupongezwa kwa
kitendo chake cha ushujaa
alichokifanya.Bila yeye katu jambo
hili lisingefahamika na ndugu zetu
wa Congo wangeendelea kuteseka
na kuuawa kila uchao.Mateso yote
aliyoyapata hayatakwenda bure.Lazima wale wote
wanaohusika na biashara hii
haramu wafikishwe mbele ya
sheria.Ninaapa sintaulaza mgongo
wangu kabla ya wahusika hawa
wote kukamatwa na kufikishwa
mbele ya sheria.” Akawaza huku
akiendelea kupitia kumbu kumbu
za mawasilianoya Frank
Katika barua pepe moja
iliyotoka kwa Deusdedith m.m
alimwelekeza Frank kuna mtu
ambnaye ameona anaweza akafaa
katika mpango wao wa kumuua
kanali Norman Sulayi ambaye
alianza kuonekana kuwa hatari
kwao.Alimtumia namba za simu za
mtu huyo ambaye alimtaja kama
kahaba alyekubuhi aitwaye
Victoria mapenzi.Alimtaja kuwa ni
kahaba ambaye amekuwa akitumiwa na vigogo na watu
matajiri kwani gharama zake ni
kubwa na ni mwanamke mzuri
sana.Elvis alistushwa na taarifa ile
“Kanali normal alikufa katika
mazingira tata mno.Mpaka leo
sababu ya kifo chake
haijajulikana.Sasa nimepata picha
halisi inaonekana naye alikuwamo
katika mtandao huu na
walionekana kutofautiana hivyo
wakaona ni vyema kama
wakimuua.Na walimuua kwa
kumtumia kahab huyu …dah
!Mtandao huu unaonekana hatari
mno.Huyu Deus ni nani?
Akajiuliza Elvis
“Lazima nihakikishe watu
hawa wanafahamika” akachukua
simu yake akaziandika namba za
simu za Victoria mapenzi na kupiga.simu ikaita lakini
haikupokelewa,akapiga tena na
safari hii ikapokelewa
“hallow” ikasema sauti nzuri
ya mwanamke upande wa pili
“Hallow habari yako.Naongea
na Vicky?
“Ndiyo.Wewe ni nani?
“Naitwa Robin.” Elvis
akadanganya
“Unahitaji nikusaidie nini
Robin usiku huu? Kama ni
huduma usiku huu wa leo sina
nafasi labda kesho”
“Vicky sihitaji huduma ya
mwili lakini kuna mambo Ambayo
nataka nizungumze
nawe.Nitakulipa vizuri sana”
“Mambo gani hayo? Akauliza
Vicky “Siwezi kukwambia simuni
hadi tutakapoonana ana kwa ana”
“sawa.Tuonane kesho saa
tatu kamili katika hoteli yangu
inaitwa Angel Vicky
hotel.Umesema unaitwa Robin?
“Ndiyo.naitwa Robin”
“Sawa Robin,ukifika
utajitambulisha mapokezi na
utaletwa moja kwa moja ofisini
kwangu.Nitawapa taarifa
zako.Kumbuka ni saa tatu kamili
juu ya alama.Ukichelewa zaidi ya
hapo sintakuwa na muda na wewe
kwani nina watu wengi wa
kuonana nao” akasema Vicky na
kukata simu
“Natumai kupitia kahaba
huyu ninaweza kupata kitu cha
kunisaidia kumfahamu huyu Deus
ni nani.Yeye anachokijali ni fedha kwa hiyo kwa kutumia fedha
ninaweza kupata mambo mazuri
toka kwake” Akawaza Elvis na
kuendelea na kazi yake
“Ndiyo maana Frank alikuwa
radhi kumuona mwanae akiteseka
na alikuwa tayari hata kumtoa
uhai wake kwa sababu ya nyaraka
hizi muhimu muhimu.” Akawaza
Elvis na alipotazama saa yake
tayari ilikuwa ni usiku wa
manane.Akaizima kompyuta ile na
kuelekea chumba cha kulala.
*****************
Dr Steven aliendesha gari
taratibu huku akijiuliza kitu
kilichomsibu Patricia.Toka amefahamiana naye hakuwahi
kumuona akiwa katika hali
hii.Siku zote Patricia alikuwa
mcheshi na mwenye furaha lakini
hali aliyokuwa nayo usiku huu
ilimtia hofu sana Dr Steven na
kumpa hamu ya kutaka kufahamu
kile kilichomsibu rafiki yake huyu
mkubwa hapa Tanzania ili aone
namna ya kumsaidia
“Lazima Patricia amepatwa na
jambo zito sana .Kwa muda huu
mfupi niliofahamiana naye
nimegundua ni mwanamke jasiri
lakini kitendo cha kumuona
akiangusha machozi usiku huu
kimenistua sana.Kwa nini mrembo
huyu amwage mwachozi?Nini
kimemsibu? akawaza Dr.Steven
Hakulifahamu vyema jiji la
Dar hivyo alikuwa anaendesha taratibu huku akijaribu kuangaza
angaza akitafuta hoteli nzuri
ambayo angempeleka Patricia
kupumzika
“Angel Vicky hotel” Dr Steven
akalisoma bango kubwa pembeni
ya barabara.
“Inaonekana ni hoteli nzuri
ambayo Patricia anaweza
akapumzika ngoja nimpeleke
hapa” akawaza Dr Steven
akapunguza mwendo wa gari na
akaingia katika hoteli ile iliyokuwa
na mandhari ya kuvutia mno
“Hapa panaweza kukufaa
kupumzika usiku wa leo? Dr
Steven akamuuliza Patricia
wakiwa katika maegesho ya
magari
“Ndiyo
panafaa.Ninachokihitaji mimi ni kuwa mbali na nyumbani tu”
akasema Patricia halafu
wakashuka na kuelekea hotelini
wakapatiwa chumba namba 102
ghorofa ya tano.Baada ya kuingia
katika chumba hicho,Patricia
akaelekea bafuni,akajitazama
katika kioo machozi yakamtoka
“Sikutegemea kama siku moja
nitaumizwa kiasi hiki.Uko wapi
Elvis? Laiti ungekuwepo
ungenifariji na mateso haya
niyapatayo.Kwa mara ya kwanza
leo toka tumeoana ninaiona
nyumba yangu chungu na
ninalala nje.Maneno yale ya mama
yameniumiza mno.I’m deeply hurt
and I need someone to comfort
me” akawaza Patricia halafu
akajifuta machozi na kurejea
chumbani akaketi sofani“Ungependa kutumia kinywaji
chochote nikuagizie Patricia?
Akauliza Dr Steven
“naomba mvinyo wowote
tafadhali’ akasema Patricia na Dr
Steven akapiga simu akaomba
waletewe mvinyo
“Patricia toka nimefika hapa
Tanzania wewe ndiye uliyenipokea
na kunisaidia nimeyafahamu na
kuyazoea mazingira kwa
haraka.Ni furaha yangu kukutana
na mtu kama wewe ambaye ni
rafiki wa kila mtu ,usiyekaukiwa
tabasamu usoni lakini usiku wa
leo nimestuka kukuona
ukilia.Nimeogopa na nimejiuliza
maswali mengi kulikoni ukawa
katika hali hii?Kitu gani
kimekusibu?Tafadhali naomba
unieleze Patricia nini kimekupata? Una tatizo gani? Niko hapa
kukusaidia nieleze tafadhali”
akasema Dr Steven
Mvinyo ukaletwa Patricia
akamimina katika glasi akanywa
na kumtazama Dr Steven kisha
akasema
“Siku ile nilisimama mbele ya
Altare ya Mungu na mbele ya
mashahidi nikaulizwa kama
nitakuwa tayari kusimama imara
na kuvumilia katika taabu na
shida,furaha na huzuni nikajibu
kutoka moyoni kwamba nakubali
.Sikujua kama ningekutana na
kipindi kigumu katika maisha
yangu ya ndoa kama
ninachokabiliana nacho sasa”
akasema Patricia Nini kimetokea katika ndoa
yako Patricia?Umekwaruzana na
mumeo? Akauliza Dr Steven
“Hapana sijakwaruzana na
mume wangu.Elvis ananipenda
mno na kamwe hatuwezi
kukwaruzana”
“Nini basi kimekupata hadi
ukawa katika hali hii? Akauliza Dr
Steven
Patricia akafikiri kidogo na
kusema
“Mimi na mume wangi mpaka
leo hatujabahatika kupata
mtoto.Hilo limekuwa ni tatizo
kubwa sana kwa ndugu za mume
wangu.Wamekuwa wakinitolea
maneno machafu ya kejeli na
kuniumiza sana.Nyumba yangu
kwa sasa naiona chungu ndiyo
maana nimeamua kuja hapa hotelini kupumzika na kutuliza
akili yangu”
“Pole sana.Kwa nini mpaka
leo hamjabahatika kupata mtoto?
Akauliza Steven.Patricia
akamueleza kila kitu kuhusu
historia yake na kwa nini hawezi
kupata mtoto.Dr Steven akaguswa
sana na histotia ile ya patricia
akamsogelea akamkumbatia
kumfariji
“Pole sana Patricia.Historia
yako imenigusa sana hata
mimi.Ndugu za mumeo hawapaswi
kukutenda hivi.Mnaonaje endapo
wewe na mumeo mkawaeleza hali
halisi kwamba hamuwezi kupata
mtoto? Akauliza Dr Steven
“Hilo ni kosa tulilolifanya toka
mwanzo kutokuwaeleza
ukweli.Laiti kama tungewafahamisha ukweli
kusingekuwa na matatizo haya
yote” akasema Patricia .Baada ya
muda Dr Steven akauliza
“Mumeo yuko wapi? Alitakiwa
awe nawe katika kipindi kigumu
kama hiki”
“Yuko safarini kikazi.Ana
safiri mara kwa mara .Muda wake
wa kukaa nyumbani ni mdogo
sana na ndiyo maana umeona leo
nimeshindwa kuvumilia kukaa
nyumbani mwenyewe nimeamua
nije nipumzike mbali na
nyumbani.” akasema Patricia na
kumtazama Dr Steve
“Steven umewahi kuhisi
upweke hadi ukajiona kama uko
peke yako duniani?
“Ndiyo.Nimewahi kupitia
kipindi kigumu kama hicho cha upweke mkubwa pale mke wangu
Laura alipofariki kwa ajali ya
ndege miezi miwili tu baada ya
kufunga ndoa.Nilihisi dunia nzima
imenitenga .Ilinichukua muda
mrefu kidogo kurudia katika hali
yangu ya kawaida kwa hiyo
ninaelewa hali unayokabiliana
nayo kwa sasa” akasema Dr Steve.
Ukapita ukimya na baada ya
muda akauliza
“Patricia unataka nikusaidie
nini katika jambo hili
linalokuumiza?Niko tayari
kukusaidia kitu chochote hata
kama ni kwenda kuzungumza na
mama mkwe wako niko tayari”
akasema Dr Steven
“Ahsante sana Steven lakini
ninachokihitaji ni kuufanya usiku
wangu wa leo kuwa mzuri.Kwa masaa haya machache nataka
niyasahau mateso yangu”
akasema Patricia na kumkumbatia
Dr Steven akambusu.Alionekana
kulemewa na kilevi na hakujali
alichokuwa anakifanya.
“Patricia una hakika unataka
kufanya hivi? Akauliza Dr Steven
kwa wasi wasi
Patricia hakujbu kitu
akaendelea kumbusu Steven huku
akimfungua vifungo vya
shati.Tayari alikwisha dhamiria
kufanya kitendo kile na Dr
Steven.Mara moja Dr Stene naye
mashetani yake yakaamka
akaanza kutoa ushirikiano.
“Kama kwa kufanya hivi
nitakuwa namsaidia kuyapooza
machungu yake ya moyo ngoja
nimsaidie” akawaza Dr Steven **********************
Saa kumi na mbili za asubuhi
ilimkuta Elvis akiwa tayari
ameamka.Macho yalikuwa mazito
kutokana na kulala kwa muda
mchache.Taratibu akajizoa zoa
pale kitandani akanywa maji kisha
akapiga magoti na kumshukuru
Mungu kwa siku mpya na
kumuomba amuongoze kumlinda
katika kazi ngumu iliyoko mbele
yake.Hakusahau pia kumuombea
mke wake Patricia ili aweze kuwa
salama hasa katika kpindi hiki
ambacho atakuwa mbali naye
kutokana na kazi nzito
inayomkabili.Alipomaliza kufanya
maombi yale akachukua simu
yake akaiwasha na kumpigia simumke wake Patricia lakini bado
simu yake haikuwa
ikipatikana.Kichwa chake kikajaa
mawazo mengi
“Nina hakika atakuwa
salama.Yawezekana atakuwa
ametingwa na kazi nyingi”
akawaza Elvis na kuelekea moja
kwa moja katika chumba cha
Graca akabonyeza kengele ya
mlangoni,mlango
ukafunguliwa.Uso wa Graca
ulikuwa na tabasamu kubwa
“Elvis karibu.Habari za
asubuhi?
“Habari nzuri sana
Graca.Umeamkaje?Samahani kwa
kukuamsha”
“Usijali Elvis.Nimekwisha
amka kitambo nilikuwa natazama
runinga.Umemkaje wewe? “Nimeamka salama.Endelea
kupumzika nimepita kukujulia
hali na kukutaarifu kwamba
baadae nitatoka kuna mahala nina
kwenda utabaki hapa na Doreen”
“Sawa Elvis.Kwa sasa nina
amani kwani tayari mzigo wote
nimekwisha utua kwako.”
Akasema Graca na kumfanya Elvis
atabasamu kisha akaelekea katika
chumba alicholala Doreen.Mlango
ulikuwa wazi lakini Doreen
hakuwemo chumbani.Akaelekea
jikoni na kumkuta Doreen akiwa
katika harakati za kuandaa
kifungua kinywa.
“Habari za asubuhi Doreen”
Elvis akamsalimu
“Nzuro Elvis.Umeamkaje?
“Nimeamka salama kabisa”
akasema Elvis aliyekuwa akimkodolea macho Doreen
ambaye alikuwa amevaa gauni
fupi sana na kuyaacha mapaja
yake meupe yaonekane.Doreen
akageuka na kukuta akitazamwa
na Elvis
“Mbona unaniangalia namna
hiyo Elvis? Akauliza Doreen.Elvis
akatabasamu kidogo na kusema
“Nategemea kutoka asubuhi
hii kuna sehemu
ninakwenda.Kuna jambo nataka
unisaidie”
“Sema chochote Elvis
nitakusaidia” akasema Doreen
huku akitabasamu
‘Nimejaribu kumpigia simu
Patricia asubuhi ya leo lakini bado
simu yake haipatikani.Naomba
baadae unisaidie kumtafuta na
uhakikishe yuko salama na kamwe usimweleze chochote
kuhusu kinachoendelea”
“sawa Elvis nitafanya hivyo”
“Ahsante Doreen” Akasema
Elvis na kwenda kujiandaa.
“Ilipotimu saa moja na robo
tayari alikuwa amejiandaa akapata
kifungua kinywa kisha akaondoka.
Kabla ya kwenda kuonana na
Vick kama walivyokubaliana
usiku,Elvis akapita kwanza ofisini
kwao ili kutoa taarifa kwa
mkurugenzi wake kwamba
amekwisha rejea toka safari.Saa
mbili na dakika nane akawasili
katika jengo la idara yao.Tayari
wafanyakazi wengi walikwisha fika
na kila mmoja alitaka kusalimiana
na Elvis kwani alipendwa na kila
mmoja.Alisalimiana nao haraka haraka halafu akaelekea kwa
mkurugenzi wake
“Karibu sana Elvis.Pole na
safari” akasema mzee Meshack
Jumbo mkurugenzi wa idara ya
ujasusi Tanzania baada ya Elvis
kuingia ofisini kwake
“Ahsanate sana mzee”
akasema Elvis.
“Vipi safari yako ilikuwa na
mafanikio? Akauliza
“Ndiyo mzee Ilikuwa na
mafanikio makubwa sana.Kila kitu
kimekwenda kama nilivyotarajia”
“Good.nadhani sasa ni wakati
wa kunieleza nini hasa
unachokichunguza” akasema mzee
Meshack
“mzee nilikuahidi kukueleza
kila kitu pindi nitakaporejea lakini
naomba kwa sasa unipe nafasi ili nikaonane na mtu mmoja muhimu
sana katika jambo hili ambaye
nimeahidiana kuonana naye saa
tatu kamili asubuhi hii.Mara tu
baada ya kuonana naye nitakuja
hapa kukueleza ni jambo gani
ninalolifuatilia.Kwa ufupi tu ni
kwamba ni jambo kubwa na zito”
akasema Elvis.Mzee Meshack
Jumbo akamtazama kwa makini
halafu akasema
“Sawa Elvis.Nenda kaonane
na huyo mtu na ukioshaonana
naye urudi hapa.Nitakusubiri
kutaka kulifahamu suala hilo”
akasema mkurugenzi
“Ahsante mzee” akasema Elvis
na kutoka huku akiitazama saa
yake.Hakutaka kuchelewa miadi
yake na Victoria .Wakati akielekea
katika gari lake akasikia mtu akimuita.Akageuka na kukutana
na Sofia
“Sofia ! akasema Elvis
“Elvis kuna kitu nimesahau
kukwambia.Kuna mtu mmoja
anaitwa Pascal ni mfanyakazi wa
idara ya usalama wa taifa
amekuwa ananipigia simu
kukuulizia na akadai kwamba
kuna jambo anataka
kukueleza.Nadhani ingekuwa
vyema kama ungeonana naye”
“Ahsante sana Sofia kwa
taarifa hizo.Nitalishughulikia
suala hilo” akasema Elvis na
kuingia garini
“Tayari Pascal amekwisha
fahamu kwamba ninahusika kwa
namna Fulani kupotea kwa
Graca.Mapambano yameanza”
akawaza Elvis akiwa garini kuelekea Angel Vicky hotel
kuonana na Victoria kahaba
anayetajwa kuwa na utajiri
mkubwa
Saa tatu kasoro dakika
kumi,tayari alikuwa analitazama
jengo la ghorofa saba ambalo juu
yake kulikuwa na maandishi
makubwa Angel Vickly hotel.Ni
moja kati ya hoteli nzuri jijini Dar
es salaam.
“Hoteli nzuri sana hii.Ni kweli
kazi ya ukahaba ndiyo
imemuwezesha Vick kumiliki
hoteli kubwa namna hii? Hapana
lazima kuna kazi nyingine
anaifanya na kazi ya ukahaba
atakuwa anaitumia kama mwavuli
kuficha kazi zake nyingine
zinazompatia fedha nyingi.Kuna
ulazima wa kumfanyia uchunguzi
 
Nimeianza leo hii story, upo vizuri Mkuu

Endelea kushusha vitu Mkuu
 
Back
Top Bottom