HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,417
- 6,149
- Thread starter
- #361
I DIED TO SAVE PRESDANT
Sehemu 38
Elvis akatabasamu na
kumkumbatia Graca
“Thank you Elvis.We’re in this
together” akasema Graca na
kutoka mle chumbani mwa Elvis
“Graca ni mmoja wa watu
wanaonifanya nitumie kila uwezo
nilio nao kuufyekelea mbali
mtandao wa baba yake.Nitafanya
kila lililo ndani ya uwezo wangu
kuhakikisha anakuwa salama na
anayaanza upya maisha yake.Ni
binti mrembo sana na hafai kuishi
maisha ya aina hii
anayoishi.Nitamsaidia ili aweze
kuwa na maisha ya furaha kama
wengine” akawaza Elvis *******************
“Frank ! ..Frank !!
Vicky mwanamke kahaba
mwenye uzuri wa kipekee
alimtikisa Brigedia Frank aweze
kuamka.Frank akajigeuza kiuvivu
akamvuta Vicky na kumbusu
“Frank inakaribia saa tano
sasa.Huendi kazini leo? Akauliza
Vicky
“Leo ni siku yetu ya kufurahi
na ndiyo maana sitaki kwenda
kokote nataka nishinde nawe
tukiburudika na kujipongeza”
“C’mon Frank huu si wakati
wa masihara.Niko katika wakati
mgumu sana hivi sasa.Maisha
yangu yako hatarini na halafuunaingiza utani.Tuburudike na
nini katika matatizo haya
makubwa?Kwanza nataka
uniambie kuhusu hatima yangu
hapa.Mlinileta nije huku kujificha
lakini hamjaniambia nitakaa huku
hadi lini?Nimechoka kukaa
mafichoni.Nina mambo mengi ya
kufanya na siwezi kuendelea
kukaa huku wakati mambo yangu
yanaharibika.Tafadhali nieleze
mna mipango gani na mimi?
Mnanisaidiaje?
“Relax Vicky !! akasema Frank
“Relax ?!! How can I relax
while I’m stuck in here? I loose
millions in every single
minute.Frank I’m tired .I need to
get out of here.Mliniahidi kulishughulikia suala hili lakini
hakuna chochote mnachokifanya
na sasa umeamua kutumia nafasi
hii ya mimi kuwepo hapa
mafichoni kumaliza tamaa zako za
mwili”
“Relax Vicky.Jana nilikuja
nimechoka mno na sikupata nafasi
ya kukuhabarisha mambo
yanavyokwenda”
“Tulikuwa na nafasi ya
kuongea lakini hukutaka kunieleza
badala yake ukajielekeza kwenye
ngono”
“Tuachane na hayo Vicky.Kwa
ufupi ni kwamba yule jamaa
aliyekuwa anakufutilia tayari
amekwisha zimishwa na hakuna
tena kitisho kingine” Sura ya Vicky ikajenga
tabasamu
“Tafadhali usinitanie Frank”
“Sikutanii Vicky.Yule jamaa
tayari tumemuondoa jana”
“So I’m free to go now?
“Uko huru ila bado utaendelea
kubaki hapa hadi atakapozikwa ili
tuweze kujiridhisha kwamba
hakuna mtu mwingine
anayekufuatilia”
“Frank sioni sababu ya mimi
kuendelea kukaa hapa wakati yule
jamaa aliyekuwa ananifuatilia
amekufa.Sitaki kuendelea
kupoteza muda huku mambo
yangu yanaharibika.Ninaondoka
sasa hivi.Thank you Frank for this
wonderfull news” akasema VickyNot so fast pretty
angel.Nitakuruhusu utoke humu
pale nitakapohakikisha kuna
usalama wa uhakika.Wewe ni mtu
muhimu sana kwetu na ni jukumu
letu kukulinda” akasema Frank na
simu yake ikaita.Alikuwa ni
Pascal.Frank akainuka haraka
haraka na kujifunga taulo
“Excuse me,I need to take this
call” akasema na kutoka mle
chumbani
“Hallow Pascal” akasema
Frank
“Frank ni saa tano sasa za
asubuhi uko wapi?Nimeogopeshwa
na kimya chako.Mambo ni salama?
“Mambo salama.Nimeamka
hivi punde.Dah ! nilikuwa na usiku wa aina yake.Vicky ana uwezo
mkubwa wa kuburudisha”
“What ?!! You slept with her?
Pascal akauliza
“Yes and it was a wonderfull
night.Huyu mwanamke mambo
yake kitandani ni vigumu hata
kuyaelezea”
“You are doing a mistake
Frank.Tayari tumekwisha
kubaliana huyu mwanamke
auawe”
“We’re not going to kill her!!
Akasema Frank
“What ?!! Siamini kama kulala
naye kwa usiku mmoja
amekuchanganya kiasi cha
kubatilisha mipango yetu dhidi
yake.Mwanamke huyu ni hatari sana kwetu kwani tayari
anafahamu mambo yetu mengi ya
siri hivyo kumuweka hai ni
kuendelea kujihatarisha sisi
wengine”
“Pascal nimekwisha sema
kwamba hatutamuua tena.Tayari
nimebadili mawazo.Hana kosa
lolote na hastahili kuuawa”
“Frank hebu fungua macho
hivi sasa tuna mambo mazito ya
kufanya na huyo mwanamke
anaweza kuwa kikwazo kwani
tayari jamaa wamekwisha hisi kitu
kwake na ndiyo maana wakaanza
kumfuatilia”
“Usihofu kuhusu hilo
Pascal.That bastard is dead.hakuna tena wa kumsumbua
huyu malaika”
“Usijiamini sana Frank kwani
hujui Elvis alikuwa anashirikiana
na akina nani.Suluhu pekee hapa
ni kumuua huyo mwanamke ili
mambo yetu yaendelee kuwa siri”
“Pascal hilo halitawezekana
tena”
“Sawa Frank.Kama umeamua
hivyo mimi sina kipingamizi lakini
pale mambo yatakapoharibika
tafadhali usiniambie
sikukuonya.Tuachane na hayo vipi
kuhusu mpangilio wa siku ya leo?
Nini kinaendelea?
“Leo hatuna mambo mengi
zaidi ya kikao cha jioni ndiyo
maana unaona nimepumzika hadi mida hii.Nitakuja huko baadae
tutaonana .Endapo kuna lolote
utalipata kabla hatujaonana
nijulishe tafadhali”
“Nitakujulisha ila nina swali
moja.Vipi kuhusu kumsaka Graca?
Yule ndiye chanzo cha haya yote
yaliyotokea”
“Graca akapatikana tu kwani
nguzo yake tayari imekwisha
anguka.Mtu aliyekuwa
anamtegemea amlinde sasa
hayupo kwa hiyo lazima atakuwa
katika kutapa tapa afanye
nini.Nataka baadae tuhudhurie
msibani na tufanye utafiti kama
tutaweza kumuona Graca.lazima
tuhakikishe amepatikana haraka
iwezekanavyo”akasema Frank na kukata simu na mara akastushwa
na sauti ya mtu aliyekohoa nyuma
yake.Nusura aangushe simu baada
ya kugonganisha macho na Vicky
“Vicky !! akasema Frank kwa
mshangao
“Mnataka kumuua nani? Vicky
akauliza
“Uhhm….uh….hakuna
tunayetaka kumuua” Frank
akababika kujibu swali lile
“Nimesimama hapa mlangoni
kwa muda na nimekusikia kila
ulichokizungumza.Nieleze
tafadhali nani mnayetaka kumuua?
“Uhm ! mwanangu Graca
alitoroka na kompyuta yenye siri
zangu nyingi na baada ya kufanya
uchunguzi tukabaini Graca amekuwa akishirikiana na Elvis
yule jamaa aliyekuwa
anakuchunguza.Kwa hasira
nilizokuwa nazo kwa kitendo kile
niliazimia kumtoa roho kwani
tayari ni mtu hatari sana
kwangu.Kwa sasa baada ya
kumuondoa Elvis sioni tena haja ya
kumuua Graca kwani tutampata
kirahisi tu”
Vicky akamtazama Frank kwa
sura yenye kuonyesha mashaka na
kuuliza
“Kweli?
“Kweli Vicky.Pascal alitaka
tumshughulikie Graca kwa haraka
mimi nikamwambia suala hilo
haliwezekani tena“Ok Frank lakini mimi
najiandaa niweze kuondoka.Siwezi
tena kuendelea kukaa hapa wakati
mtu aliyekuwa ananiwinda
amekwisha fariki”
“Vicky kama nilivyokueleza
kwamba usiharakishe sana
kuondoka hapa hadi kwanza
tujiridhishe kuhusiana na usalama
wako”
“Frank I’ll be fine.Nitaajiri
hata walinzi wa kunilinda usiku na
mchana kwani uwezo ninao lakini
siwezi kuendelea tena kukaa hapa”
Frank akamtazama Vicky na
kumshika mkono
“Kama umesisitiza unataka
kuondoka siwezi kukuzuia lakini
kabla ya kuondoka we must have a final round” akasema Frank.Vicky
akataka kugoma lakini Frank
ambaye mikono yake ilijazia
vilivyo akamuinua Vicky na
kumbeba hadi chumbani
akambwaga kitandani na bila
kupoteza wakati mtanange
ukaanza
******************
Waziri mkuu mstaafu David
Sichoma alikuwa katika kujiandaa
ili kuelekea hospitali kumjulia hali
kaka wa mke wake aliyepata ajali
ya gari pale mlango wa chumbani
kwake ulipogongwa.Mke wake
akaenda kuufungua akakutana na
mtumishi wao wa ndani ambaye alimweleza kwamba kuna simu
imepigwa kutoka kwa walinzi wa
getini wakidai kuna wageni wa
mzee
“Kuna wageni wako getini”
David akaambiwa na mkewe
“Ni akina nani hao?
Nimekwisha mueleza Imelda afute
miadi yote ya watu niliopaswa
kukutana nao asubuhi ya leo”
akasema David
“Onana nao yawezekana ni
watu muhimu” Mkewe akamshauri
na David akaelekeza wageni hao
waruhusiwe waingie ndani
“Dr makwa ! akasema David
kwa furaha baada ya Dr Makwa
Tusangira mwenyekiti wa chama
kikuu cha upinzani nchini akiwa ameongozana na watu wengine
wawili kuingia sebuleni
“Mheshimiwa David samahani
sana kwa kukuvamia bila kutoa
taarifa”
“Usijali Dr Makwa.karibuni
sana” akasema David na
kuwaongoza wageni wake hadi
bustanini kandoni mwa bwawa
kubwa
“Karibuni sana
jamani.Imekuwa vyema mmewahi
kwani mngechelewa kidogo
tusingeweza kuonana nilikuwa
najiandaa kwenda hospitali
kumjulia hali shemeji yangu”
akasema David
“Samahani sana mheshimiwa
kwa uvamizi huu,hata hivyo hatutachukua muda mrefu”
akasema Dr Makwa
Baada ya kuwaoneni
ninaamini kuna jambo la msingi
sana hivyo nimeahirisha safari
yangu ili tuendelee na maongezi
yetu” akasema David na mtumishi
akafika akiwa na vinywaji
akawahudumia.
“Mheshimiwa David” akasema
Dr Makwa
“C’mon Dr Makwa just call me
David.Haya mambo ya uheshimiwa
tumekwisha yaacha huko
serikalini” akasema David huku
akicheka
“Sawa David” akasema Dr
Makwa na baada ya sekunde
chache akaendelea Kabla sijaendelea mbele
naomba kwanza nifanye
utambulisho mfupi wa watu
nilioongozana nao.Nitaanza na
mheshimiwa Peter Jondau,yeye ni
mwenyekiti wa chama cha
maendeleo ya
wananchi.Anayefuatilia ni Dr
Kahigo Mlayela ambaye ni
mwenyekiti wa chama cha
Demokrasia na kazi.Hawa wote
wanaongonza vyama vikubwa vya
upinzani vyenye nguvu na wafuasi
wengi bila kusahau kuwa vyama
vyao pia vina wawakilishi bungeni”
“Ninafurahi sana kuwafahamu
waheshimiwa wenyeviti.Mimi
nanyi kwa sasa tutakuwa tukionana mara kwa mara”
akasema David
“Hata sisi tunafurahi pia
mheshimiwa David” Peter Jondau
na Dr Kahigo wakasema kwa
pamoja.
“Baada ya utambulisho huo”
Dr Makwa akaendelea
“Sasa nijielekeze katika suala
la muhimu lililotuleta hapa”
akanyamaza tena kidogo halafu
akaendelea
“Mr David,ulipokutana nasi
ulituachia kazi ya kufanya na leo
nina furaha kukueleza kwamba ile
kazi tumeikamilisha.Watu wetu
wamefanya kazi usiku na mchana
na wamekamilisha kila kitu” Oh ! That’s
wonderfull.Napenda sana kufanya
kazi na watu wenye kupeleka
mambo haraka haraka namna
hii.Ninaanza kupata picha ya
baraza langu la mawaziri
litakavyokuwa na watu
wachapakazi” akasema David na
wote wakaangua kicheko.Dr
Makwa akafungua mkoba wake
akatoa kitabu na kumkabidhi
David
“Ndani ya kitabu hiki kuna
mchanganuo mzima wa
operesheni mafuta yetu.Ni
mchanganuo mrefu utapitia
taratibu kila kitu kimewekwa
humo” Ahsante sana Dr
Makwa.Sipati neno zuri la kueleza
namna nilivyofurahishwa kwa jinsi
mlivyoitikia operesheni
hii.Nitapitia taratibu nione
mchanganuo ulivyo lakini kwa
sasa nahitaji kupata jumla ya fedha
zote za kugharamia operesheni
nzima itakuwa shilingi ngapi?
“Kwa mujibu wa wataalamu
wetu waliofanya mchanganuyo
huu,operesheni nzima itagharimu
shilingi takribanmi Bilioni mia
tano na sabini” akasema Dr Makwa
akionekana kuwa na
wasiwasi.David akatabasamu na
kusema
“Safi sana.Hilo la fedha si
tatizo.Kiasi chote cha fedha mlichokiorodhesha
kitapatikana.Ninachohitaji
kufahamu ni namna mlivyojipanga
na lini operesheni itaanza”
“Baada ya kumaliza kufanya
mchanganuo wa kiasi cha fedha
tutakachokihitaji tumekaa na
kujadili kwa kina namna
tutakavyoendesha operesheni hii
na tumekubaliana yafuatayo”
akatulia kidogo halafu akaendelea
“Tayari tumekwisha wasilisha
maombi ya kufanya mkutano wa
hadhara siku ya jumapili lakini
bado hatujapewa jibu.Kama
hatutakuwa tumepata majibu toka
jeshi la polisi mpaka siku ya
ijumaa basi siku ya jumamosi
tutafanya mkutano na waandishi wa habari na kuwatangazia
wafuasi wetu wafike siku ya
jumapili kwa ajili ya mkutano wa
hadhara.Katika mkutano huo
tutaweka wazi kwa watanzania
kuhusu mambo yote ya siri
ambayo serikali ya Tanzania
imefanya na Marekani na
tutatangaza kuanza kwa
maandamano yasiyo na ukomo na
hapo ndipo mvutano na serikali
utakapoibuka”
“Dr Makwa” akaita David
“Dhumuni kuu la operesheji
hii ni kupandikiza chuki kwa
wananchi dhidi ya serikali na kisha
kusababisha kuibuka kwa
mapambano kati ya serikali na
wananchi.Katika maelezo yako sijasikia sehemu ya vurugu
zitakazolazimisha jeshi la polisi
litumie nguvu kubwa dhidi ya
waandmanaji.Yote mliyoyapanga
ni sahihi lakini kikubwa
ninachokihitaji mimi ni vurugu
zitakazoambatana na umwagikaji
wa damu.Nataka yafanyike mauaji
ya raia na dunia nzima ifahamu
kuhusu mauaji hayo na
kuishinikiza serikali iliyoko
madarakani iondoke.Nataka
kusikia namna mlivyojipanga
katika upande huo” akasema David
“Sikuwa nimemaliza maelezo
yangu David” akasema Dr Makwa
“Oh ! endelea mimi nilidhani
tayari umemaliza” Tunao mpango mzuri
kuhusiana na suala hilo Mr
David.Katika maandamano
tunayoyandaa kutakuwa na kundi
maalum la vijana ambao kazi yao
itakuwa ni kufanya uharibifu kama
vile kuchoma magari na ofisi za
serikali.Kingine tumeandaa
wadunguaji ambao watajificha
sehemu mbali mbali
kutakapofanyika maandamano na
pale vurugu zitakapopamba moto
wadunguaji hao wataua askari
kadhaa na askari watajua kwamba
ni raia ndio walioua askari hao na
hii itazidisha chuki na
kuwalazimisha kutumia nguvu
kubwa na kuua raia.Kuna watu
ambao watakuwa wakirekodi matukio yote haya na kisha
tutaionyesha dunia namna serikali
ya Tanzania inavyoua raia wasio
na hatia.Nakuhakikisha David
lazima serikali itaondoka
madarakani.Usihofu David
tumejipanga kikamilifu.Mambo
kama haya tuna uzoefu nayo
mkubwa na utafurahi
mwenyewe.Kilichokua
kinatushinda sisi kuyafanya ni
ukosefu wa fedha.Nakuhakikishia
anza maandalizi ya kwenda ikulu”
akasema Dr Makwa na tabasamu
kubwa likaonekana usoni pa David
kisha wakaendelea na majadiliano
ya kina kuhusiana na operesheni
mafuta yetu ******************
Steven na Ben walifanikisha
taratibu za kupata sehemu ya
kuzikia na shughuli ya uandaaji wa
kaburi ikaanza.Wakati shughuli
ikiendelea Steven akachepuka na
kusogea mbali kidogo mahala
kusiko na watu akaziandika
namna za Samira alizopewa na Ben
akapiga.Simu ikaita na
kupokelewa
“Hallow” ikasema sauti tamu
ya kike na Steven akaitambua sauti
ile ilikuwa ni ya Samira
“Hallo nani mwenzangu?
Samira akauliza tena
“hallow Summer baby”
akasema Steven Steven ?!! Sauti ya Samira
ikaonyesha mstuko mkubwa
“It’s me baby.Your king is
back” akasema Steven na kumsikia
Samira akiruka ruka kwa furaha
kubwa
“Bado siamini leo nimeisikia
sauti yako.Uko wapi Steven?
“I’m free now.Nimekupigia
kukujulisha hilo lakini naomba
usimueleze mtu yeyote kama
nimekupigia simu.Natamani sana
nikuone ila kuna kazi fulani
ninaifanya mida hii.Unaonaje
endapo tukaonana jioni ya leo kwa
chakula? I real miss you baby”
akasema Steven
“Ungejua nilivyo na hamu ya
kukuona Steven hata ungesema sasa hivi ningeacha kila kitu nije
nionane nawe.Wewe ni mtu
muhimu mno kwangu lakini kwa
vile umetaka tuonane jioni hakuna
tatizo.Tukutane wapi?
“Nimekuwa kifungoni kwa
miaka kadhaa kwa hiyo nikuachie
wewe uchague sehemu nzuri
tunayoweza kukutana”
“Sawa Steven nitakujulisha
baadae tuonane wapi.Steven kabla
hujakata simu naomba ufahamu
kwamba nilifanya jitihada nyingi
kufahamu mahala ulipokuwa
umefungwa lakini
sikufanikiwa.Laiti ningejua mahala
uliko ningekuja kila siku kukujulia
hali.Nimekuwa naiota hii ndoto ya
wewe kuwa huru kila siku na leo imekuwa kweli.Nakupenda sana
Steven”
“Mimi pia nakupenda
Samira.Tutaongea zaidi jioni
tutakapokutana” akasema Steven
na kukata simu halafu akashusha
pumzi
“Sasa moyo wangu nahisi wa
baridi baada ya kuisikia tena sauti
ya huyu malaika ambaye nikiwa
kifungoni kila siku nilikuwa
namuota.Sijui amenipa nini yule
mwanamke kwa sababu pamoja na
madhira yote yaliyonikuta kwa
sababu yale lakini bado
sikomi.Bado naendelea
kumpenda” akawaza na
kutabasamu Namkubali sana yule
mwanamuziki Diamond ambaye
ana wimbo mmoja unaitwa sikomi
ambao naweza kusema kwa kiasi
kikubwa unanihusu sana kwani
ninakumbana na mambo mengi
katika maisha yangu ya kimapenzi
lakini bado sikomi
kupenda.Nitakoma kumpenda
Samira pale uhai wangu
utakapotoka” akawaza Steven na
kurejea tena kaburini kuungana na
akina Ben katika maandalizi ya
kaburi
******************
Saa nane za mchana rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwa ameambatana na mke wake
waliwasili nyumbani kwa mama
yake Elvis uliko msiba wa
Elvis.Kulikuwa na umati mkubwa
wa watu.Rais akashuka garini
akapokewa na mjomba wa
marehemu na kutambulishwa kwa
ndugu wengine wa karibu wa Elvis
halafu yeye na mkewe
wakapelekwa kusaini kitabu cha
maombolezo na kisha wakaelekea
ndani kuwafariji wafiwa.Kwanza
mheshimiwa rais na mke wake
wakaingia katika chumba
alimokuwamo mama wa
marehemu wakamfariji halafu
wakapelekwa katika chumba
alimokuwamo Patricia mke wa
marehemu ambaye kwa muda mrefu amekuwa na ukaribu
mkubwa na familia ya rais kwani
ndiye anayemtibu mke wa
rais.Patricia aliangua kilio baada
ya kuwaona rais na mke wake.Mke
wa rais akaketi pembeni yake na
kumtuliza.Rais alitumia zaidi ya
dakika kumi kumfariji Patricia
halafu akatoka akaelekea sebuleni
akimuacha mke wake karibu na
Patricia akiendelea kumfariji
Rais akakutana na kamati ya
maandalizi ya mazishi ambayo
iliongozwa na Meshack Jumbo
mkurugenzi wa idara ya usalama
wa taifa.Rais na mke wake
walitumia zaidi ya saa mbili pale
msibani kisha wakaondoka.Watu
walikuwa wengi sana na kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo
watu walivyozidi
kuongezeka.Msiba ule uliwagusa
watu wengi sana
****************
Ni saa mbili za usiku,kiza
tayari kimeingia.Kila kitu ambacho
Elvis na na timu yake walipanga
kukifanya kilikwenda
vizuri.Maandalzi ya kaburi
yalikwenda vizuri.Kazi kubwa
ilikwisha fanyika na kulibaki
mambo machache ya
kumalizia.Upande wa jeneza tayari
kila kitu kilikwisha kamilika na
majaribio yalipofanyika yalitoa
matokeo mazuri. Baada tu ya kurejea nyumbani
Steven alitoa taarifa ya maendeleo
ya jukumu alilopewa halafu
akajiandaa haraka haraka kwa ajili
ya kwenda kukutana na
Samira.Hakuwa na mavazi mazuri
kwa ajili ya usiku huo hivyo
kumlazimu Elvis kumpatia suti
moja nzuri iliyomkaa
vyema.Hakumueleza chochote
Elvis kuhusiana na kukutana na
Samira bali aliaga kwamba kuna
sehemu muhimu anakwenda
Saa mbili na nusu usiku
Steven akaondoka katika makazi
yao akaelekea 360 garden mahala
walikopanga wakutane na Samira
“Jiji limebadilika
sana.Kumekuwa na sehemu nyingi za burudani.Kwa ujumla katika
kipindi hiki chote nilichokuwa
kizuizini nimepitwa na mambo
mengi lakini hayo hayana maana
kubwa kwangu kwani jambo
kubwa na la pekee ni kuonana na
Samira mwanamke ambaye
ninampenda kuliko wote na
ambaye niko tayari kwenda hadi
mwisho wa dunia kwa ajili ya
kumpata” akawaza Steven akiwa
njiani kuelekea mahala
atakapokutana na Samira
“Nimejaribu kutafakari
kuhusu mustakabali mzima wa
maisha yangu baada ya kutoka
kifungoni lakini bado sijapata jibu
maisha yangu yawaje.Bado
sijarejeshwa rasmi katika kazi yangu ya awali je nikirudishwa
niendelee nayo au nibadili maisha
yangu kama alivyonishauri Ben?
Ameniahidi kunipa mtaji wa
biashara ili niweze kuachana na
kazi hii ya ujasusi,ni wazo zuri
lakini naona kama moyo wangu
hauko tayari kwa hilo kwani kazi
hii tayari iko damuni.Hata hivyo
nitapata jibu baadae baada ya
kuimaliza operesheni hii
muhimu.Nina mambo mengi ya
kufanya kuyatengeneza upya
maisha yangu.Kifungo hiki
kimenipotezea kabisa uelekeo
mzima wa maisha yangu.Sina
sehemu yoyote ya kuanzia.Kila
nilichokuwa nacho kimekwisha
chukuliwa na ndugu zangu ambao hawakujua niko wapi na lini
nitarejea” akaendelea kuwaza Ben
huku safari ikiendelea hadi
alipofika 360 garden na kuegesha
gari.kwa mbali muziki wa bendi
ulisikika.Kulikuwa na bendi
maalum iliyokuwa ikiburudisha
wateja usiku huu.
Kabla hajashuka garini
akampigia simu Samira na
kumjulisha kwamba tayari
amekwisha wasili pale mahala
walikopanga wakutane.Samira
akamwambia kwamba amekaribia
sana kufika hapo hotelini na
amsubiri eneo la maegesho.Steven
akatoka na kukaa nje ya
gari.Baada ya dakika tano gari la
kifahari aina ya mercedece benz lenye rangi nyeusi liliingia katika
eneo la maegesho na toka ndani ya
gari lile akashuka mwanamke
mmoja mwenye umbo dogo na
aliyevaa vazi fupi ambalo liliacha
sehemu kubwa ya mapaja yake
wazi.Alikuwa ni mwanamke
mwenye uzuri wa kipekee kabisa.
“Samira !! akasema Steven
akiwa amebaki mdomo wazi kama
mtu aliyeshuhudia jambo kubwa la
kushangaza.Mwanamke yule
alikuwa anapiga hatua za kunyata
kama vile hataki kukanyaga ardhi
“baby Summer ! akaita Steven
na Samira akageuza shingo yake
akamuona Steven amesimama
mbele ya gari lake.Akatoka mbio
na kwenda kumkumbatia kwa nguvu.Steven akamuinua na
kumuweka mikononi mwake
wakapeana mabusu mazito
“Steven ! siamini kama leo hii
nimekilaza tena kichwa changu
katika kifua chako” akasema
Samira huku akibubujikwa na
machozi
“Its ok summer baby.Please
don’t cry.I’m here .Your king is
back” akasema Steven na
kumbembeleza Samira akamfuta
machozi na kumbusu
“Steven nashindwa kujizuia
kuangusha machozi.Kupotea
kwako ni jambo ambalo liliniumiza
sana na kunipa donda ambalo
niliamini halitakuja kupona hadi
nitakapoingia kaburini.lakini leo hii kidonda changu kimepona na
sijui niseme nini zaidi ya
kumshukuru Mungu kwa jambo
hili kubwa alilotufanyia.Steven
nakupenda sana sana na sipati
maneno mazuri ya kueleza ni
namna gani ninakupenda”
akasema Samira na kuanza tena
kumwaga machozi
“Usilie samira.Nafahamu hali
gani uliyokuwa nayo lakini sasa
nimerejea na atakayeweza
kututenganisha ni Mungu
pekee.Futa machozi malaika
wangu huu ni wakati wetu wa
kufurahi” akasema Steven huku
akimfuta machozi Samira
akamshika mkono wakaanza
kuongozana kuelekea ndani.Muhudumu akawapokea na
kuwapeleka katika meza yao
ambayo Samira alikwisha weka
oda tangu mapema.
“Nimefurahi sana kuonana
nawe baby summer.Umezidi
kupendeza.Maisha yako
yanakwendaje? Akauliza Steven na
Samira akatabasamu
“Ninamshukuru Mungu
maisha yangu yanakwenda vizuri
licha ya misuko suko
niliyoipitia.Mathew nimepitia
mambo mengi sana magumu
wakati ulipotoweka.Kabla
hatujaendelea mbele zaidi
tafadhali nieleze ulikuwa wapi?
“Nilikuwa kizuizini sehemu
fulani hapa hapa dar es salaam.Nilizuliwa jambo kwamba
nimetoa siri za nchi kwa majasusi
wa nchi za nje na nikawekwa
kizuizini lakini sikuwahi
kufunguliwa mashitaka hadi
nilipokuja kutolewa siku ya jana”
“Oh masikini Steven.Naomba
nikuweke wazi kwamba mambo
yote yaliyokutokea mimi ndiye
niliyesababisha”
“Usijali Samira ninayafahamu
hayo yote hivyo naomba usijihisi
una hatia”
“Ninayo hatia Steven.kama si
mimi wewe usingeingia katika
matatizo haya”
“Samira wakati mimi na wewe
tunaanza mahusiano yetu tayari
ulikuwa katika mahusiano na yule kigogo wako na nilikuwa
nikifahamau kwamba siku moja
yanaweza kunipata mambo kama
haya kwani nilikuwa nimeingia
katika anga za mtu mwenye nguvu
kwa hiyo angeweza kunifanya
chochote hivyo usijilaumu.Vipi
kuhusu yule mzee wako yuko wapi
sasa hivi?
“Yule kigogo wangu ni kweli
alikuwa ananipenda sana na
alijitapa kwangu kwamba
amekukomesha na kwamba
sintakuona tena.Kwa bahati nzuri
naweza kusema yule mzee
alipatwa na mstuko wa moyo
akafariki dunia hivyo siko naye
tena” akasema Samira na wahudumu wakafika wakaandaa
meza
“Steven karibu chakula
mpenzi wangu.” Samira
akamkaribisha Steven chakula
wakaanza kula huku wakiendelea
na maonegzi yao.Walizungumza
mambo mengi kuhusiana na
maisha yao na ilipofika saa tano za
usiku Steven akamtaka Samira
waondoke.
“Tunaelekea wapi? Samira
akauliza
“Kwa sasa sina makazi rasmi
kama
nilivyokueleza.Nimehifadhiwa na
rafiki yangu hivyo tuelekee kwako
kama hakutakuwa na tatizo lolote”
akasema Steven
Sent using Jamii Forums mobile app
Sehemu 38
Elvis akatabasamu na
kumkumbatia Graca
“Thank you Elvis.We’re in this
together” akasema Graca na
kutoka mle chumbani mwa Elvis
“Graca ni mmoja wa watu
wanaonifanya nitumie kila uwezo
nilio nao kuufyekelea mbali
mtandao wa baba yake.Nitafanya
kila lililo ndani ya uwezo wangu
kuhakikisha anakuwa salama na
anayaanza upya maisha yake.Ni
binti mrembo sana na hafai kuishi
maisha ya aina hii
anayoishi.Nitamsaidia ili aweze
kuwa na maisha ya furaha kama
wengine” akawaza Elvis *******************
“Frank ! ..Frank !!
Vicky mwanamke kahaba
mwenye uzuri wa kipekee
alimtikisa Brigedia Frank aweze
kuamka.Frank akajigeuza kiuvivu
akamvuta Vicky na kumbusu
“Frank inakaribia saa tano
sasa.Huendi kazini leo? Akauliza
Vicky
“Leo ni siku yetu ya kufurahi
na ndiyo maana sitaki kwenda
kokote nataka nishinde nawe
tukiburudika na kujipongeza”
“C’mon Frank huu si wakati
wa masihara.Niko katika wakati
mgumu sana hivi sasa.Maisha
yangu yako hatarini na halafuunaingiza utani.Tuburudike na
nini katika matatizo haya
makubwa?Kwanza nataka
uniambie kuhusu hatima yangu
hapa.Mlinileta nije huku kujificha
lakini hamjaniambia nitakaa huku
hadi lini?Nimechoka kukaa
mafichoni.Nina mambo mengi ya
kufanya na siwezi kuendelea
kukaa huku wakati mambo yangu
yanaharibika.Tafadhali nieleze
mna mipango gani na mimi?
Mnanisaidiaje?
“Relax Vicky !! akasema Frank
“Relax ?!! How can I relax
while I’m stuck in here? I loose
millions in every single
minute.Frank I’m tired .I need to
get out of here.Mliniahidi kulishughulikia suala hili lakini
hakuna chochote mnachokifanya
na sasa umeamua kutumia nafasi
hii ya mimi kuwepo hapa
mafichoni kumaliza tamaa zako za
mwili”
“Relax Vicky.Jana nilikuja
nimechoka mno na sikupata nafasi
ya kukuhabarisha mambo
yanavyokwenda”
“Tulikuwa na nafasi ya
kuongea lakini hukutaka kunieleza
badala yake ukajielekeza kwenye
ngono”
“Tuachane na hayo Vicky.Kwa
ufupi ni kwamba yule jamaa
aliyekuwa anakufutilia tayari
amekwisha zimishwa na hakuna
tena kitisho kingine” Sura ya Vicky ikajenga
tabasamu
“Tafadhali usinitanie Frank”
“Sikutanii Vicky.Yule jamaa
tayari tumemuondoa jana”
“So I’m free to go now?
“Uko huru ila bado utaendelea
kubaki hapa hadi atakapozikwa ili
tuweze kujiridhisha kwamba
hakuna mtu mwingine
anayekufuatilia”
“Frank sioni sababu ya mimi
kuendelea kukaa hapa wakati yule
jamaa aliyekuwa ananifuatilia
amekufa.Sitaki kuendelea
kupoteza muda huku mambo
yangu yanaharibika.Ninaondoka
sasa hivi.Thank you Frank for this
wonderfull news” akasema VickyNot so fast pretty
angel.Nitakuruhusu utoke humu
pale nitakapohakikisha kuna
usalama wa uhakika.Wewe ni mtu
muhimu sana kwetu na ni jukumu
letu kukulinda” akasema Frank na
simu yake ikaita.Alikuwa ni
Pascal.Frank akainuka haraka
haraka na kujifunga taulo
“Excuse me,I need to take this
call” akasema na kutoka mle
chumbani
“Hallow Pascal” akasema
Frank
“Frank ni saa tano sasa za
asubuhi uko wapi?Nimeogopeshwa
na kimya chako.Mambo ni salama?
“Mambo salama.Nimeamka
hivi punde.Dah ! nilikuwa na usiku wa aina yake.Vicky ana uwezo
mkubwa wa kuburudisha”
“What ?!! You slept with her?
Pascal akauliza
“Yes and it was a wonderfull
night.Huyu mwanamke mambo
yake kitandani ni vigumu hata
kuyaelezea”
“You are doing a mistake
Frank.Tayari tumekwisha
kubaliana huyu mwanamke
auawe”
“We’re not going to kill her!!
Akasema Frank
“What ?!! Siamini kama kulala
naye kwa usiku mmoja
amekuchanganya kiasi cha
kubatilisha mipango yetu dhidi
yake.Mwanamke huyu ni hatari sana kwetu kwani tayari
anafahamu mambo yetu mengi ya
siri hivyo kumuweka hai ni
kuendelea kujihatarisha sisi
wengine”
“Pascal nimekwisha sema
kwamba hatutamuua tena.Tayari
nimebadili mawazo.Hana kosa
lolote na hastahili kuuawa”
“Frank hebu fungua macho
hivi sasa tuna mambo mazito ya
kufanya na huyo mwanamke
anaweza kuwa kikwazo kwani
tayari jamaa wamekwisha hisi kitu
kwake na ndiyo maana wakaanza
kumfuatilia”
“Usihofu kuhusu hilo
Pascal.That bastard is dead.hakuna tena wa kumsumbua
huyu malaika”
“Usijiamini sana Frank kwani
hujui Elvis alikuwa anashirikiana
na akina nani.Suluhu pekee hapa
ni kumuua huyo mwanamke ili
mambo yetu yaendelee kuwa siri”
“Pascal hilo halitawezekana
tena”
“Sawa Frank.Kama umeamua
hivyo mimi sina kipingamizi lakini
pale mambo yatakapoharibika
tafadhali usiniambie
sikukuonya.Tuachane na hayo vipi
kuhusu mpangilio wa siku ya leo?
Nini kinaendelea?
“Leo hatuna mambo mengi
zaidi ya kikao cha jioni ndiyo
maana unaona nimepumzika hadi mida hii.Nitakuja huko baadae
tutaonana .Endapo kuna lolote
utalipata kabla hatujaonana
nijulishe tafadhali”
“Nitakujulisha ila nina swali
moja.Vipi kuhusu kumsaka Graca?
Yule ndiye chanzo cha haya yote
yaliyotokea”
“Graca akapatikana tu kwani
nguzo yake tayari imekwisha
anguka.Mtu aliyekuwa
anamtegemea amlinde sasa
hayupo kwa hiyo lazima atakuwa
katika kutapa tapa afanye
nini.Nataka baadae tuhudhurie
msibani na tufanye utafiti kama
tutaweza kumuona Graca.lazima
tuhakikishe amepatikana haraka
iwezekanavyo”akasema Frank na kukata simu na mara akastushwa
na sauti ya mtu aliyekohoa nyuma
yake.Nusura aangushe simu baada
ya kugonganisha macho na Vicky
“Vicky !! akasema Frank kwa
mshangao
“Mnataka kumuua nani? Vicky
akauliza
“Uhhm….uh….hakuna
tunayetaka kumuua” Frank
akababika kujibu swali lile
“Nimesimama hapa mlangoni
kwa muda na nimekusikia kila
ulichokizungumza.Nieleze
tafadhali nani mnayetaka kumuua?
“Uhm ! mwanangu Graca
alitoroka na kompyuta yenye siri
zangu nyingi na baada ya kufanya
uchunguzi tukabaini Graca amekuwa akishirikiana na Elvis
yule jamaa aliyekuwa
anakuchunguza.Kwa hasira
nilizokuwa nazo kwa kitendo kile
niliazimia kumtoa roho kwani
tayari ni mtu hatari sana
kwangu.Kwa sasa baada ya
kumuondoa Elvis sioni tena haja ya
kumuua Graca kwani tutampata
kirahisi tu”
Vicky akamtazama Frank kwa
sura yenye kuonyesha mashaka na
kuuliza
“Kweli?
“Kweli Vicky.Pascal alitaka
tumshughulikie Graca kwa haraka
mimi nikamwambia suala hilo
haliwezekani tena“Ok Frank lakini mimi
najiandaa niweze kuondoka.Siwezi
tena kuendelea kukaa hapa wakati
mtu aliyekuwa ananiwinda
amekwisha fariki”
“Vicky kama nilivyokueleza
kwamba usiharakishe sana
kuondoka hapa hadi kwanza
tujiridhishe kuhusiana na usalama
wako”
“Frank I’ll be fine.Nitaajiri
hata walinzi wa kunilinda usiku na
mchana kwani uwezo ninao lakini
siwezi kuendelea tena kukaa hapa”
Frank akamtazama Vicky na
kumshika mkono
“Kama umesisitiza unataka
kuondoka siwezi kukuzuia lakini
kabla ya kuondoka we must have a final round” akasema Frank.Vicky
akataka kugoma lakini Frank
ambaye mikono yake ilijazia
vilivyo akamuinua Vicky na
kumbeba hadi chumbani
akambwaga kitandani na bila
kupoteza wakati mtanange
ukaanza
******************
Waziri mkuu mstaafu David
Sichoma alikuwa katika kujiandaa
ili kuelekea hospitali kumjulia hali
kaka wa mke wake aliyepata ajali
ya gari pale mlango wa chumbani
kwake ulipogongwa.Mke wake
akaenda kuufungua akakutana na
mtumishi wao wa ndani ambaye alimweleza kwamba kuna simu
imepigwa kutoka kwa walinzi wa
getini wakidai kuna wageni wa
mzee
“Kuna wageni wako getini”
David akaambiwa na mkewe
“Ni akina nani hao?
Nimekwisha mueleza Imelda afute
miadi yote ya watu niliopaswa
kukutana nao asubuhi ya leo”
akasema David
“Onana nao yawezekana ni
watu muhimu” Mkewe akamshauri
na David akaelekeza wageni hao
waruhusiwe waingie ndani
“Dr makwa ! akasema David
kwa furaha baada ya Dr Makwa
Tusangira mwenyekiti wa chama
kikuu cha upinzani nchini akiwa ameongozana na watu wengine
wawili kuingia sebuleni
“Mheshimiwa David samahani
sana kwa kukuvamia bila kutoa
taarifa”
“Usijali Dr Makwa.karibuni
sana” akasema David na
kuwaongoza wageni wake hadi
bustanini kandoni mwa bwawa
kubwa
“Karibuni sana
jamani.Imekuwa vyema mmewahi
kwani mngechelewa kidogo
tusingeweza kuonana nilikuwa
najiandaa kwenda hospitali
kumjulia hali shemeji yangu”
akasema David
“Samahani sana mheshimiwa
kwa uvamizi huu,hata hivyo hatutachukua muda mrefu”
akasema Dr Makwa
Baada ya kuwaoneni
ninaamini kuna jambo la msingi
sana hivyo nimeahirisha safari
yangu ili tuendelee na maongezi
yetu” akasema David na mtumishi
akafika akiwa na vinywaji
akawahudumia.
“Mheshimiwa David” akasema
Dr Makwa
“C’mon Dr Makwa just call me
David.Haya mambo ya uheshimiwa
tumekwisha yaacha huko
serikalini” akasema David huku
akicheka
“Sawa David” akasema Dr
Makwa na baada ya sekunde
chache akaendelea Kabla sijaendelea mbele
naomba kwanza nifanye
utambulisho mfupi wa watu
nilioongozana nao.Nitaanza na
mheshimiwa Peter Jondau,yeye ni
mwenyekiti wa chama cha
maendeleo ya
wananchi.Anayefuatilia ni Dr
Kahigo Mlayela ambaye ni
mwenyekiti wa chama cha
Demokrasia na kazi.Hawa wote
wanaongonza vyama vikubwa vya
upinzani vyenye nguvu na wafuasi
wengi bila kusahau kuwa vyama
vyao pia vina wawakilishi bungeni”
“Ninafurahi sana kuwafahamu
waheshimiwa wenyeviti.Mimi
nanyi kwa sasa tutakuwa tukionana mara kwa mara”
akasema David
“Hata sisi tunafurahi pia
mheshimiwa David” Peter Jondau
na Dr Kahigo wakasema kwa
pamoja.
“Baada ya utambulisho huo”
Dr Makwa akaendelea
“Sasa nijielekeze katika suala
la muhimu lililotuleta hapa”
akanyamaza tena kidogo halafu
akaendelea
“Mr David,ulipokutana nasi
ulituachia kazi ya kufanya na leo
nina furaha kukueleza kwamba ile
kazi tumeikamilisha.Watu wetu
wamefanya kazi usiku na mchana
na wamekamilisha kila kitu” Oh ! That’s
wonderfull.Napenda sana kufanya
kazi na watu wenye kupeleka
mambo haraka haraka namna
hii.Ninaanza kupata picha ya
baraza langu la mawaziri
litakavyokuwa na watu
wachapakazi” akasema David na
wote wakaangua kicheko.Dr
Makwa akafungua mkoba wake
akatoa kitabu na kumkabidhi
David
“Ndani ya kitabu hiki kuna
mchanganuo mzima wa
operesheni mafuta yetu.Ni
mchanganuo mrefu utapitia
taratibu kila kitu kimewekwa
humo” Ahsante sana Dr
Makwa.Sipati neno zuri la kueleza
namna nilivyofurahishwa kwa jinsi
mlivyoitikia operesheni
hii.Nitapitia taratibu nione
mchanganuo ulivyo lakini kwa
sasa nahitaji kupata jumla ya fedha
zote za kugharamia operesheni
nzima itakuwa shilingi ngapi?
“Kwa mujibu wa wataalamu
wetu waliofanya mchanganuyo
huu,operesheni nzima itagharimu
shilingi takribanmi Bilioni mia
tano na sabini” akasema Dr Makwa
akionekana kuwa na
wasiwasi.David akatabasamu na
kusema
“Safi sana.Hilo la fedha si
tatizo.Kiasi chote cha fedha mlichokiorodhesha
kitapatikana.Ninachohitaji
kufahamu ni namna mlivyojipanga
na lini operesheni itaanza”
“Baada ya kumaliza kufanya
mchanganuo wa kiasi cha fedha
tutakachokihitaji tumekaa na
kujadili kwa kina namna
tutakavyoendesha operesheni hii
na tumekubaliana yafuatayo”
akatulia kidogo halafu akaendelea
“Tayari tumekwisha wasilisha
maombi ya kufanya mkutano wa
hadhara siku ya jumapili lakini
bado hatujapewa jibu.Kama
hatutakuwa tumepata majibu toka
jeshi la polisi mpaka siku ya
ijumaa basi siku ya jumamosi
tutafanya mkutano na waandishi wa habari na kuwatangazia
wafuasi wetu wafike siku ya
jumapili kwa ajili ya mkutano wa
hadhara.Katika mkutano huo
tutaweka wazi kwa watanzania
kuhusu mambo yote ya siri
ambayo serikali ya Tanzania
imefanya na Marekani na
tutatangaza kuanza kwa
maandamano yasiyo na ukomo na
hapo ndipo mvutano na serikali
utakapoibuka”
“Dr Makwa” akaita David
“Dhumuni kuu la operesheji
hii ni kupandikiza chuki kwa
wananchi dhidi ya serikali na kisha
kusababisha kuibuka kwa
mapambano kati ya serikali na
wananchi.Katika maelezo yako sijasikia sehemu ya vurugu
zitakazolazimisha jeshi la polisi
litumie nguvu kubwa dhidi ya
waandmanaji.Yote mliyoyapanga
ni sahihi lakini kikubwa
ninachokihitaji mimi ni vurugu
zitakazoambatana na umwagikaji
wa damu.Nataka yafanyike mauaji
ya raia na dunia nzima ifahamu
kuhusu mauaji hayo na
kuishinikiza serikali iliyoko
madarakani iondoke.Nataka
kusikia namna mlivyojipanga
katika upande huo” akasema David
“Sikuwa nimemaliza maelezo
yangu David” akasema Dr Makwa
“Oh ! endelea mimi nilidhani
tayari umemaliza” Tunao mpango mzuri
kuhusiana na suala hilo Mr
David.Katika maandamano
tunayoyandaa kutakuwa na kundi
maalum la vijana ambao kazi yao
itakuwa ni kufanya uharibifu kama
vile kuchoma magari na ofisi za
serikali.Kingine tumeandaa
wadunguaji ambao watajificha
sehemu mbali mbali
kutakapofanyika maandamano na
pale vurugu zitakapopamba moto
wadunguaji hao wataua askari
kadhaa na askari watajua kwamba
ni raia ndio walioua askari hao na
hii itazidisha chuki na
kuwalazimisha kutumia nguvu
kubwa na kuua raia.Kuna watu
ambao watakuwa wakirekodi matukio yote haya na kisha
tutaionyesha dunia namna serikali
ya Tanzania inavyoua raia wasio
na hatia.Nakuhakikisha David
lazima serikali itaondoka
madarakani.Usihofu David
tumejipanga kikamilifu.Mambo
kama haya tuna uzoefu nayo
mkubwa na utafurahi
mwenyewe.Kilichokua
kinatushinda sisi kuyafanya ni
ukosefu wa fedha.Nakuhakikishia
anza maandalizi ya kwenda ikulu”
akasema Dr Makwa na tabasamu
kubwa likaonekana usoni pa David
kisha wakaendelea na majadiliano
ya kina kuhusiana na operesheni
mafuta yetu ******************
Steven na Ben walifanikisha
taratibu za kupata sehemu ya
kuzikia na shughuli ya uandaaji wa
kaburi ikaanza.Wakati shughuli
ikiendelea Steven akachepuka na
kusogea mbali kidogo mahala
kusiko na watu akaziandika
namna za Samira alizopewa na Ben
akapiga.Simu ikaita na
kupokelewa
“Hallow” ikasema sauti tamu
ya kike na Steven akaitambua sauti
ile ilikuwa ni ya Samira
“Hallo nani mwenzangu?
Samira akauliza tena
“hallow Summer baby”
akasema Steven Steven ?!! Sauti ya Samira
ikaonyesha mstuko mkubwa
“It’s me baby.Your king is
back” akasema Steven na kumsikia
Samira akiruka ruka kwa furaha
kubwa
“Bado siamini leo nimeisikia
sauti yako.Uko wapi Steven?
“I’m free now.Nimekupigia
kukujulisha hilo lakini naomba
usimueleze mtu yeyote kama
nimekupigia simu.Natamani sana
nikuone ila kuna kazi fulani
ninaifanya mida hii.Unaonaje
endapo tukaonana jioni ya leo kwa
chakula? I real miss you baby”
akasema Steven
“Ungejua nilivyo na hamu ya
kukuona Steven hata ungesema sasa hivi ningeacha kila kitu nije
nionane nawe.Wewe ni mtu
muhimu mno kwangu lakini kwa
vile umetaka tuonane jioni hakuna
tatizo.Tukutane wapi?
“Nimekuwa kifungoni kwa
miaka kadhaa kwa hiyo nikuachie
wewe uchague sehemu nzuri
tunayoweza kukutana”
“Sawa Steven nitakujulisha
baadae tuonane wapi.Steven kabla
hujakata simu naomba ufahamu
kwamba nilifanya jitihada nyingi
kufahamu mahala ulipokuwa
umefungwa lakini
sikufanikiwa.Laiti ningejua mahala
uliko ningekuja kila siku kukujulia
hali.Nimekuwa naiota hii ndoto ya
wewe kuwa huru kila siku na leo imekuwa kweli.Nakupenda sana
Steven”
“Mimi pia nakupenda
Samira.Tutaongea zaidi jioni
tutakapokutana” akasema Steven
na kukata simu halafu akashusha
pumzi
“Sasa moyo wangu nahisi wa
baridi baada ya kuisikia tena sauti
ya huyu malaika ambaye nikiwa
kifungoni kila siku nilikuwa
namuota.Sijui amenipa nini yule
mwanamke kwa sababu pamoja na
madhira yote yaliyonikuta kwa
sababu yale lakini bado
sikomi.Bado naendelea
kumpenda” akawaza na
kutabasamu Namkubali sana yule
mwanamuziki Diamond ambaye
ana wimbo mmoja unaitwa sikomi
ambao naweza kusema kwa kiasi
kikubwa unanihusu sana kwani
ninakumbana na mambo mengi
katika maisha yangu ya kimapenzi
lakini bado sikomi
kupenda.Nitakoma kumpenda
Samira pale uhai wangu
utakapotoka” akawaza Steven na
kurejea tena kaburini kuungana na
akina Ben katika maandalizi ya
kaburi
******************
Saa nane za mchana rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwa ameambatana na mke wake
waliwasili nyumbani kwa mama
yake Elvis uliko msiba wa
Elvis.Kulikuwa na umati mkubwa
wa watu.Rais akashuka garini
akapokewa na mjomba wa
marehemu na kutambulishwa kwa
ndugu wengine wa karibu wa Elvis
halafu yeye na mkewe
wakapelekwa kusaini kitabu cha
maombolezo na kisha wakaelekea
ndani kuwafariji wafiwa.Kwanza
mheshimiwa rais na mke wake
wakaingia katika chumba
alimokuwamo mama wa
marehemu wakamfariji halafu
wakapelekwa katika chumba
alimokuwamo Patricia mke wa
marehemu ambaye kwa muda mrefu amekuwa na ukaribu
mkubwa na familia ya rais kwani
ndiye anayemtibu mke wa
rais.Patricia aliangua kilio baada
ya kuwaona rais na mke wake.Mke
wa rais akaketi pembeni yake na
kumtuliza.Rais alitumia zaidi ya
dakika kumi kumfariji Patricia
halafu akatoka akaelekea sebuleni
akimuacha mke wake karibu na
Patricia akiendelea kumfariji
Rais akakutana na kamati ya
maandalizi ya mazishi ambayo
iliongozwa na Meshack Jumbo
mkurugenzi wa idara ya usalama
wa taifa.Rais na mke wake
walitumia zaidi ya saa mbili pale
msibani kisha wakaondoka.Watu
walikuwa wengi sana na kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo
watu walivyozidi
kuongezeka.Msiba ule uliwagusa
watu wengi sana
****************
Ni saa mbili za usiku,kiza
tayari kimeingia.Kila kitu ambacho
Elvis na na timu yake walipanga
kukifanya kilikwenda
vizuri.Maandalzi ya kaburi
yalikwenda vizuri.Kazi kubwa
ilikwisha fanyika na kulibaki
mambo machache ya
kumalizia.Upande wa jeneza tayari
kila kitu kilikwisha kamilika na
majaribio yalipofanyika yalitoa
matokeo mazuri. Baada tu ya kurejea nyumbani
Steven alitoa taarifa ya maendeleo
ya jukumu alilopewa halafu
akajiandaa haraka haraka kwa ajili
ya kwenda kukutana na
Samira.Hakuwa na mavazi mazuri
kwa ajili ya usiku huo hivyo
kumlazimu Elvis kumpatia suti
moja nzuri iliyomkaa
vyema.Hakumueleza chochote
Elvis kuhusiana na kukutana na
Samira bali aliaga kwamba kuna
sehemu muhimu anakwenda
Saa mbili na nusu usiku
Steven akaondoka katika makazi
yao akaelekea 360 garden mahala
walikopanga wakutane na Samira
“Jiji limebadilika
sana.Kumekuwa na sehemu nyingi za burudani.Kwa ujumla katika
kipindi hiki chote nilichokuwa
kizuizini nimepitwa na mambo
mengi lakini hayo hayana maana
kubwa kwangu kwani jambo
kubwa na la pekee ni kuonana na
Samira mwanamke ambaye
ninampenda kuliko wote na
ambaye niko tayari kwenda hadi
mwisho wa dunia kwa ajili ya
kumpata” akawaza Steven akiwa
njiani kuelekea mahala
atakapokutana na Samira
“Nimejaribu kutafakari
kuhusu mustakabali mzima wa
maisha yangu baada ya kutoka
kifungoni lakini bado sijapata jibu
maisha yangu yawaje.Bado
sijarejeshwa rasmi katika kazi yangu ya awali je nikirudishwa
niendelee nayo au nibadili maisha
yangu kama alivyonishauri Ben?
Ameniahidi kunipa mtaji wa
biashara ili niweze kuachana na
kazi hii ya ujasusi,ni wazo zuri
lakini naona kama moyo wangu
hauko tayari kwa hilo kwani kazi
hii tayari iko damuni.Hata hivyo
nitapata jibu baadae baada ya
kuimaliza operesheni hii
muhimu.Nina mambo mengi ya
kufanya kuyatengeneza upya
maisha yangu.Kifungo hiki
kimenipotezea kabisa uelekeo
mzima wa maisha yangu.Sina
sehemu yoyote ya kuanzia.Kila
nilichokuwa nacho kimekwisha
chukuliwa na ndugu zangu ambao hawakujua niko wapi na lini
nitarejea” akaendelea kuwaza Ben
huku safari ikiendelea hadi
alipofika 360 garden na kuegesha
gari.kwa mbali muziki wa bendi
ulisikika.Kulikuwa na bendi
maalum iliyokuwa ikiburudisha
wateja usiku huu.
Kabla hajashuka garini
akampigia simu Samira na
kumjulisha kwamba tayari
amekwisha wasili pale mahala
walikopanga wakutane.Samira
akamwambia kwamba amekaribia
sana kufika hapo hotelini na
amsubiri eneo la maegesho.Steven
akatoka na kukaa nje ya
gari.Baada ya dakika tano gari la
kifahari aina ya mercedece benz lenye rangi nyeusi liliingia katika
eneo la maegesho na toka ndani ya
gari lile akashuka mwanamke
mmoja mwenye umbo dogo na
aliyevaa vazi fupi ambalo liliacha
sehemu kubwa ya mapaja yake
wazi.Alikuwa ni mwanamke
mwenye uzuri wa kipekee kabisa.
“Samira !! akasema Steven
akiwa amebaki mdomo wazi kama
mtu aliyeshuhudia jambo kubwa la
kushangaza.Mwanamke yule
alikuwa anapiga hatua za kunyata
kama vile hataki kukanyaga ardhi
“baby Summer ! akaita Steven
na Samira akageuza shingo yake
akamuona Steven amesimama
mbele ya gari lake.Akatoka mbio
na kwenda kumkumbatia kwa nguvu.Steven akamuinua na
kumuweka mikononi mwake
wakapeana mabusu mazito
“Steven ! siamini kama leo hii
nimekilaza tena kichwa changu
katika kifua chako” akasema
Samira huku akibubujikwa na
machozi
“Its ok summer baby.Please
don’t cry.I’m here .Your king is
back” akasema Steven na
kumbembeleza Samira akamfuta
machozi na kumbusu
“Steven nashindwa kujizuia
kuangusha machozi.Kupotea
kwako ni jambo ambalo liliniumiza
sana na kunipa donda ambalo
niliamini halitakuja kupona hadi
nitakapoingia kaburini.lakini leo hii kidonda changu kimepona na
sijui niseme nini zaidi ya
kumshukuru Mungu kwa jambo
hili kubwa alilotufanyia.Steven
nakupenda sana sana na sipati
maneno mazuri ya kueleza ni
namna gani ninakupenda”
akasema Samira na kuanza tena
kumwaga machozi
“Usilie samira.Nafahamu hali
gani uliyokuwa nayo lakini sasa
nimerejea na atakayeweza
kututenganisha ni Mungu
pekee.Futa machozi malaika
wangu huu ni wakati wetu wa
kufurahi” akasema Steven huku
akimfuta machozi Samira
akamshika mkono wakaanza
kuongozana kuelekea ndani.Muhudumu akawapokea na
kuwapeleka katika meza yao
ambayo Samira alikwisha weka
oda tangu mapema.
“Nimefurahi sana kuonana
nawe baby summer.Umezidi
kupendeza.Maisha yako
yanakwendaje? Akauliza Steven na
Samira akatabasamu
“Ninamshukuru Mungu
maisha yangu yanakwenda vizuri
licha ya misuko suko
niliyoipitia.Mathew nimepitia
mambo mengi sana magumu
wakati ulipotoweka.Kabla
hatujaendelea mbele zaidi
tafadhali nieleze ulikuwa wapi?
“Nilikuwa kizuizini sehemu
fulani hapa hapa dar es salaam.Nilizuliwa jambo kwamba
nimetoa siri za nchi kwa majasusi
wa nchi za nje na nikawekwa
kizuizini lakini sikuwahi
kufunguliwa mashitaka hadi
nilipokuja kutolewa siku ya jana”
“Oh masikini Steven.Naomba
nikuweke wazi kwamba mambo
yote yaliyokutokea mimi ndiye
niliyesababisha”
“Usijali Samira ninayafahamu
hayo yote hivyo naomba usijihisi
una hatia”
“Ninayo hatia Steven.kama si
mimi wewe usingeingia katika
matatizo haya”
“Samira wakati mimi na wewe
tunaanza mahusiano yetu tayari
ulikuwa katika mahusiano na yule kigogo wako na nilikuwa
nikifahamau kwamba siku moja
yanaweza kunipata mambo kama
haya kwani nilikuwa nimeingia
katika anga za mtu mwenye nguvu
kwa hiyo angeweza kunifanya
chochote hivyo usijilaumu.Vipi
kuhusu yule mzee wako yuko wapi
sasa hivi?
“Yule kigogo wangu ni kweli
alikuwa ananipenda sana na
alijitapa kwangu kwamba
amekukomesha na kwamba
sintakuona tena.Kwa bahati nzuri
naweza kusema yule mzee
alipatwa na mstuko wa moyo
akafariki dunia hivyo siko naye
tena” akasema Samira na wahudumu wakafika wakaandaa
meza
“Steven karibu chakula
mpenzi wangu.” Samira
akamkaribisha Steven chakula
wakaanza kula huku wakiendelea
na maonegzi yao.Walizungumza
mambo mengi kuhusiana na
maisha yao na ilipofika saa tano za
usiku Steven akamtaka Samira
waondoke.
“Tunaelekea wapi? Samira
akauliza
“Kwa sasa sina makazi rasmi
kama
nilivyokueleza.Nimehifadhiwa na
rafiki yangu hivyo tuelekee kwako
kama hakutakuwa na tatizo lolote”
akasema Steven
Sent using Jamii Forums mobile app