I DIED TO SAVE PRESIDANT
Sehemu 65
Frank,Obi na vijana
walioongozana nao wakarejea tena
katika makazi ya akina Elvis na kukuta
mlango mdogo wa geti waliouacha
wazi ukiwa umefungwa.
"Mlango huu tuliuacha wazi
lakini umefungwa.Hii inaonyesha
hawa jamaa tayari wamekwisha rejea
na wako ndani" akasema Obi
"Wapange vijana haraka sana
muingie ndani na muwe waangalifu
sana.Jitahidini kuwadhibiti
ninawahitaji wote wakiwa hai"
akasema Frank na Obi akawapa
maelekezo ya kufanya vijana wake
halafu yeye na vijana wanne
wakarukia ndani na baada ya
kuhakikisha kuko shwari wakaelekea
katika mlango wa kuingilia sebuleni wakachungulia ndani hakukuwa na
dalili zozote za mtu licha ya taa
kuwaka.Akajaribu kukinyonga kitasa
mlango ulikuwa umefungwa kwa
funguo.Akawafanyia ishara vijana
wake wakae tayari akatoa funguo
bandia na kuufungua ule mlango na
kisha akaingia sebuleni akifuatiwa na
vijana wawili .Walikagua nyumba yote
lakini hakukuwa na mtu,akampigia
simu Frank
"Mkuu hakuna mtu ila
inaonekana walikuwa hapa muda si
mrefu kwani wamechukua vitu vyao
na kuondoka.Hakuna nguo wala
mabegi tuliyoyakuta wakati ule"
"Damn it !! akasema kwa hasira
Frank huku akiupiga usukani kwa
mikono yake.Akaegemea kiti na
kuzama mawazoni
"Sijawahi endeshwa na mtu
yeyote kama hivi sasa ninavyoendeshwa na hawa
jamaa.Lakini sikati tamaa lazima
watapatikana tu.Mimi huwa sichezewi
kiasi hiki.Watauona moto wangu"
akawaza Frank halafu akamgeukia
Winnie aliyekuwa amefungwa mikono
kiti cha nyuma
"Winnie ninakupa nafasi ya
mwisho ya kunionyesha mahala alipo
dada yako" akasema
"Frank nakuomba mzee uniamini
ninalokwambia.Dada na hao jamaa
niliokueleza wanaishi katika nyumba
hii.Tuendelee kusubiri lazima
watarudi" akasema Winnie.Frank
akatafakari halafu akatoa simu katika
droo ya gari na kumfungua Winnie
mikono akampa ile simu
"Simu yako hii nataka uiwashe na
uwasiliane na dada yako mwambie
kwamba uko hapa na akufuate mara
moja" akaamuru.Winnie akawasha simu ile na kuzitafuta namba za Vicky
akapiga lakini simu ya Vicky haikuwa
ikipatikana.Akapiga tena jibu likawa
lile lile simu ya Vicky haipatikani
"Endelea kujaribu kupiga kila
baada ya dakika kumi.Leo tutaendelea
kukaa hapa hapa hadi asubuhi.Lazima
tuwasubiri" akasema Frank na
kumpigia simu Obi akamtaka atoke
mle ndani na kuwapanga vijana pale
nje wawasubiri akina Elvis
"Uzima wako ni pale dada yako
atakapopatikana lakini kama
ukishindwa kusaidia katika kumpata
basi jihesabu wewe tayari ni mfu"
akasema Frank
"Frank nakuomba tafadhali
usiniue.Kama ningejua mahala
ambako dada anaweza kupatikana
ningewaeleza lakini sijui.Ninafahamu
mahala hapa kwani hata mimi nilikuwa nimefungiwa hapa" akasema
Winnie
" Salama yako ni kama watarejea
hapa lakini kama wasipoonekana
ninasikitika kwamba sintaendelea
kukuacha hai tena" akasema Frank
Masaa yalizidi kusonga bila ya
akina Elvis kuonekana pale
nyumbani.Taratibu kukaanza
kupambazuka na Obi akamfuata Frank
ambaye hakufunga ukope wake
akisubiri akina Elvis warejee
"Mkuu kumeanza kupambazuka
na hawa jamaa hawajareea hadi muda
huu tufanye nini? akauliza Onbi
"Tuondokeni ili watu wasije
wakapatwa na wasi wasi wakitukuta
hapa ila waache vijana wawili
waendelee kuchunguza na pindi
wakiwaona akina Elvis wamerejea
basi watujulishe mara moja.Huyu
msichana mtandoka naye.Hakikisheni mmempa kila aina ya mateso ili aseme
ukweli wake ni nani walimtuma
kwetu?Kama hata baada ya kuteswa
ataendelea kuwa mgumu wa
kusema,kill her"akasema Frank huku
akimtazama Winnie kwa macho
yaliyojaa hasira
"Sawa mkuu" akasema Obi na
kumshusha Winnie kutoka katika gari
la Frank akampakia katika gari lao
wakaondoka zao
*********************
Siku mpya ilianza na habari
kubwa iliyoliamsha taifa asubuhi hii ni
onyo la jeshi la polisi likiwaonya
wafuasi wa vyama vya upinzani
wasithubutu kuhudhuria mkutano
ulioitishwa na viongozi wao kwani
haukuwa na kibali.Hii ni habari kubwa
iliyoandikwa karibu na magazeti yote na kutangazwa na vituo vyote vya
redio na runinga.Wakati habari hii
ikitangazwa Elvis na Steve tayari
walikwisha amka na walikuwa
sebuleni wakitazama taarifa ya habari
kufuatilia kilichokuwa kinaendelea
nchini.
"Hakuna jipya haya yote ni ya
wanasiasa.Tuwaachie mambo yao na
sisi tuendelee na yetu.Nadhani ni
wakati wa kwenda kuanza kumfatilia
Irene Mwabukusi.Nimefikiria na
nimeona itabidi twende wote katika
kazi hii.Irene ana mahusiano na akina
Frank na hatujui yawezekana naye
akawemo katika mtandao wao na
hivyo akawa ni mtu mwenye ulinzi au
yawezekana Frank akatuma watu
kwenda kumuua endapo atagundua
kwamba tumezipata nyaraka zile za
kutolea mzigo bandarini.Watu hawa ni rahisi sana kuua ili mambo yao
yasijulikane" akasema Elvis
"Are you sure?Steven akauliza
"Yes I'm sure.Siwezi kukuacha
ukaenda huko peke yako ni hatari
sana.Wasiliana na Samira kama tayari
amekwisha fika kumchukua Omola
kumpeleka ikulu.Mimi ngoja
nikajiandae kwani siwezi kutoka bila
kubadili mwonekano wangu" akasema
Elvis na kutoka akarejea chumbani
kwake akajiandaa kwa ajili ya kutoka
kwenda kuanza kazi.
"Ouh ! hakika unajua
kujibadilisha mwonekano.Hakuna
yeyote atakayekutambua kwa
mwonekano huo" akasema Steve
aliyeingia chumbani wakati Elvis
akijiandaa.
"Vipi samira umewasiliana naye?
"Ndiyo.Yuko njiani hivi sasa
akielekea hotelini kwa Omola" Good.Inabidi tuzungumze pia na
Omola.Piga simu hotelini
wakuunganishe naye.Halafu itabidi
tutafute simu nyngine tatu kwa ajili ya
Omola,Vicky na Graca ili iwe rahisi
kuwasiliana" akasema Elvis na Steve
akapiga simu hotelini kwa Omola
akaunganishwa naye
"Hallo Steve habari yako?Elvis na
wengine wote hawajambo?
"Wote wazima kabisa.Vipi wewe
hali yako"akauliza Steve na kuiweka
simu katika sauti kubwa ili Elvis naye
aweze kusikia mazungumzo yale
"Hali yangu ni nzuri
kabisa.Imekuwa vizuri umewahi
kunipigia kwani nilikuwa na mpango
wa kuwapigia kuwajulisha kuwa ile
simu ya mdogo wake Vicky
imewashwa lakini inaonekana
amekuwa akizungushwa sehemu mbali mbali .Mpaka sasa bado wako
katika mzunguko." akasema
"Hallow Omola,Elvis hapa
ninaongea" akasema Elvis
"habari yako Elvis."
"Nzuri Omola.Kwa kuwa
unakwenda ikulu asubuhi hii tutahitaji
kuipata hiyo kompyuta yako ili
tuendelee kumfuatilia Winnie na
kufahamu mahala aliko.Jioni ya leo
tutakutana ili utupe mrejesho wa kazi
yako ya leo"
"Sawa Elvis.Mtaipataje?Mnakuja
huku hotelini kuichukua?akauliza
"Ndiyo tunakuja hapo muda si
mrefu.Tusubiri" akasema Elvis na
kukata simu
"Hizi ni habari njema kwa
Vicky.Inabidi afahamishwe ili aweze
kupata moyo kwamba mdogo wake
bado yuko hai" akasema Elvis na
kumalizia kupakia silaha zake katika kibegi kidogo wakatoka na kuelekea
katika chumba walimolala Vicky na
Graca,akagonga mlango na Graca
akaufungua.Macho yake yalionekana
bado amelemewa na usingizi.
"Elvis,karibuni.Habari za
asubhi?akasema Graca huku
akiyafikicha macho yake
"Umeamkaje?Akauliza Elvis
"Nimeamka vizuri."
"Nahitaji kuzungumza na Vicky"
"Vicky?! Graca akashangaa
"Ndiyo"
"Hakuwaaga?Graca akauliza na
akina Elvis wakatazamana
"Hapana.Ameondoka?
"Vicky ameondoka alfajiri
akasema kuna sehemu
anakwenda.Mimi nilikuwa na usingizi
sikumtilia maanani nikajua
atawajulisha." Where is she?akauliza Elvis na
kutoka nje wakalikuta gari lao lipo ila
geti lilikuwa wazi
"Inawezekana labda amekwenda
mahala kutafuta mahitaji ya hapa
nyumbani.Anyway atakaporejea
mwambie sisi tumetoka na asitoke
atusubiri hadi tutakaporejea"akasema
Elvis
"Mnakwenda wapi?
"Tunakwenda kufuatilia taarifa
muhimu kuhusiana na zile nyaraka
tulizozipata jana ofisini kwa
Frank.Usihofu utakuwa
salama.Hakuna anayefahamu mahala
hapa ila uwe makini.Mtu yeyote
akigonga geti usimfungulie kwanza
hakikisha umechungulia na
kumfahamu ni nani.Hatutakawia sana"
akasema Elvis
"Sawa Elvis .Halafu humu ndani
hakuna chochote cha kuandaa"Nadhani Vicky amekwenda
kushughulikia hilo lakini
tutakapokuwa tunarejea tutapita
supermarket na kununua mahitaji
yote yanayohitajika" akasema Elvis
kisha wakaingia garini na kuondoka
"She's very beautifull"akasema
Steve kwa utani
"Steve mambo hayo huu si
wakati wake.Tuna mambo makubwa
ya kujadili .,Kwa sasa tujiulize Vicky
amekwenda wapi?Mbona
hajatujulisha kama anatoka?akauliza
Elvis
"Hata mimi nimeshangaa ila
yawezekana ameona asitusumbue
kutokana na uchovu wa jana"akasema
Steve aliyekuwa katika usukani
"Lakini utaratibu wetu hauko
hivyo.Tuko katika kipindi cha hatari
kubwa na alipaswa atujulishe kuwa
anatoka na anakwenda wapi.Nitamkanya asirudie tena
kitendo hiki cha kuondoka bila kuaga
wenzake" akasema Elvis
"Vicky na mdogo wake
wanafanana tabia.Wote ni wabishi
sana"
"Ubishi wao hauna manufaa
yoyote kwetu zaidi ya kutuweka
katika matatizo.Tazama alichokifanya
Winnie.Ameondoka kwa kiburi lakini
ametua katika mikono ya akina
Frank"akasema Elvis na safari
ikaendelea kuelekea hotelini kwa
Omola.Walisimama katika duka la
kuuza simu Steve akashuka na
kwenda kununua simu tatu pamoja na
laini zake akarejea garini wakaendelea
na safari.
Walifika Maasai Hoteli alikofikia
Omola Steve akashuka na kumfuata
Omola chumbani kwake.Samira tayari alikwisha fika na alikuwa chumbani na
Omola
"Oh Samira kumbe tayari
umefika"akasema Steve
"Nimewahi sana kama
ulivyonielekeza."
"Ahsante sana." akasema Steve
na kumgeukia Omola
"Omola huyu atakayekuwa
dereva wako wa leo na siku zote
anaitwa Samira ni mpenzi wangu
hivyo jisikie amani uko katika mikono
salama"akasema Steve na Omola
akatabasamu
"Nafurahi kukutanana naye
Samira ni mrembo sana.Una bahati
sana kumpata mrembo kama huyu"
akasema Omola halafu akachukua
kompyuta yake na kumkabidhi Steve
na kumuelekeza namna programu ile
inavyofanya kaziHii programu ni mpya kabisa na
CIA ndiyo shirika la kwanza la ujasusi
duniani kuanza kuitumia programu hii
.Japo zipo programu nyingine kama hii
ambazo zinaendelea kutumika lakini
hii ni mwisho wa yote.Ni programu ya
kisasa mno" akasema Omola na
kuendelea kumuelekeza Steve mambo
kadhaa kuhusiana na programu ile
"Ahsante Omola tutaonana
jioni.Tutakuja kukuchukua hapa
hapa.Nadhani kila kitu kuhusiana na
Ikulu Vicky amekwisha
kuelekeza"akasema Steve
"Ndiyo Steve kila kitu nimekwisa
elekezwa na hakuna tatizo
lolote.Mambo yote yatakwenda sawa"
"Nakutakia kila la heri" akasema
Steve na kuanza kupiga hatua
kuondoka halafu akakumbuka kitu
"Nimesahau.Hii hapa ni simu
yako ambayo utakuwa unaitumia ukiwa hapa Tanzania.Ndani ya simu
hii kuna muda wa maongezi wa
kutohja na kuna namba zetu Elvis,ya
kwangu na Vicky.Muda wowote
ukitaka kuwasiliana nasi usisite
kufanya hivyo" akasema Steve na
kumkabidhi Omola simu kisha
akaondoka.Alirejea garini
alikomuacha Elvis
"Sasa mambo yamekaa
vizuri.Kompyuta ya Omola hii hapa"
akasema Steve na kumkabidhi Elvis
kompyuta ile na kumuelekeza
kuhusiana na programu ile
inayotumika kumfuatilia Winnie.
"Kwa mujibu wa programu hii
kwa sasa wako katika mtaa wa
viwandani na anaonekana anaendelea
na safari.Kwa mwendo anaokwenda
nao inaonyesha yuko katika
gari.Anakwenda wapi huku?Anyway
tuendelee kumfuatilia tutajua mwisho wake.Twende tukamtafute kwanza
Irene" akasema Elvis na Steve
akaondoa gari huku Elvis akiendelea
kumfuatilia Winnie
"Wamesimama.Nayafahamu
maeneo haya ni maeneo ya viwanda
na si maeneo ya makazi"akasema Elvis
Steve alifuata maelekezo
yaliyokuwepo katika nyaraka zile za
kutolea mzigo bandarini kuhusu
mahala ilipo kampuni ya Pendeza
Co.Ltd na kufika bila taabu.
"We're here" akasema Steve
akimwambia Elvis ambaye bado
alikuwa ameelekeza akili yake yote
katika kompyuta akimfuatilia Winnie
"Good.Ni duka kubwa na zuri"
akasema Elvis akilikodolea macho
duka lililokuwa mbele yao likiwa na
maandishi makubwa Pendeza Co.Ltd
wakaenda katika maegesho Elvis mimi ninashuka na kuingia
ndani wewe baki hapa hapa ndani ya
gari.Nitamaliza kila kitu
mwenyewe.Kama ukiona hatari
yoyote huku nje nitaarifu haraka sana"
akasema Steve na kushuka akaangaza
angaza kama ilivyo kawaida ya
majasusi kuhakiki usalama halafu
akaanza kupiga hatua kuelekea
ndani.Tayari duka limekwisha
funguliwa na hakukuwa na wateja
wengi asubuhi hii.Mle ndani
akawakuta akina dada watatu
wamesimama wakipeana
michapo,akawasogelea
"Habari zenu akina dada"
akawasalimu kwa uchangamfu
mkubwa
"habari nzuri kaka,habari yako"
"Nzuri kabisa.Nawaona na nyie
mko vizuri.Sura zenu zinanionyesha
hivyo" akasema na wale akina dada wakatabasamu na kufurahia
uchangamfu wake
"Karibu kaka .Tukusaidie
nini?akauliza dada mmoja baada ya
kumuona Steve kama si mnunuzi
"Nina shida na madam Irene.
Nimemkuta au nimewahi
sana?akauliza huku akiwatolea
tabasamu
"Bosi aje saa hizi?Umewahi
sana."
"Saa ngapi anaweza kuja?
"Kuanzia saa nne ndio muda
wake.Ila yupo msaidizi wake unaweza
kumuona huyo naye akakusaidia shida
yako" akasema mmoja wa wale akina
dada
"Hapana nina shida na madam
Irene pekee.Nitakuja tena baadae
kwani maagizo niliyopewa ni kwamba
nionane naye mwenyewe" akasema
Steve na kuwaaga wale akina dada akaanza kupiga hatua
kuondoka.Alipokaribia kufika
mlangoni akageuka na kurudi
"Naombeni mnielekeze kwake ili
nimfuate huko huko" akasema Steve
na kuelekezwa nyumbani kwa
Irene.Akaondoka na kurejea garini
"Irene bado hajafika hapa ila
nimeelekezwa nyumbani
kwake.Twende tumfuate kwani
wanasema huwa anachelewa sana
kufika hapa" akasema Steve huku
akiwasha gari wakaondoka maeneo
yale
"Kuna maendeleo yoyote kwa
Winnie? akauliza
"Inaonekana amesimama.Hili ni
eneo la viwanda na sijui anatafuta nini
huku.Tumalizane kwanza na Irene
halafu tutaenda kumtafuta Winnie"
akasema Elvis Walifika katika nyumba Steve
aliyoelekezwa kuwa ni nyumbani kwa
Irene Mwabukusi.Ilikuwa ni nyumba
kubwa ya ghorofa moja.
"Ni hapa tumefika.Jumba
lenyewe linaonyesha ni mtu
anayejiweza sana" akasema Steve na
kuendesha gari taratibu hadi karibu
na geti akashuka na kwenda
kubonyeza kengele ya geti.Baada ya
dakika moja dirisha dogo lililokuwa
pembeni ya geti likafunguliwa na
msichana mmoja akajitokeza.
"Karibu.Nikusaidie nini?
"ahsante sana.Nahitaji kuonana
na madam Irene"
"Una miadi naye?
"Hapana sina miadi naye ila nina
shida naye ya dharura nimemfuata
ofisini kwake nikaelekezwa kumfuata
hapa nyumbani"
"Nimwambie unaitwa nani? Walifika katika nyumba Steve
aliyoelekezwa kuwa ni nyumbani kwa
Irene Mwabukusi.Ilikuwa ni nyumba
kubwa ya ghorofa moja.
"Ni hapa tumefika.Jumba
lenyewe linaonyesha ni mtu
anayejiweza sana" akasema Steve na
kuendesha gari taratibu hadi karibu
na geti akashuka na kwenda
kubonyeza kengele ya geti.Baada ya
dakika moja dirisha dogo lililokuwa
pembeni ya geti likafunguliwa na
msichana mmoja akajitokeza.
"Karibu.Nikusaidie nini?
"ahsante sana.Nahitaji kuonana
na madam Irene"
"Una miadi naye?
"Hapana sina miadi naye ila nina
shida naye ya dharura nimemfuata
ofisini kwake nikaelekezwa kumfuata
hapa nyumbani"
"Nimwambie unaitwa nani? Mwambie Lukas ninatoka
kampuni ya kusafirisha mizigo ya
Shamsi " akasema Steve na yule
msichana akaondoka na baada ya
dakika tatu akarejea na kufungua geti
na akawakaribisha ndani akina
Steve.Walikaribishwa katika sebule
nzuri sana yenye samani za
kupendeza.
"Karibuni .Mama amesema
mumsubiri hapa atakuja muda si
mrefu" akasema yule msichana na
kuondoka akawaacha akina Elvis peke
yao
"Kuna watu hapa duniani
hawafahamu nini maana ya shida
wanaishi kama vile wako katika sayari
nyingine" akasema Steve kwa sauti
ndogo wakiwa pale sebuleni
wakimsubiri Irene lakini Elvis
hakumjibu kitu macho yake yalikuwa
katika kompyuta akiendelea kumfuatilia Winnie.Baada ya dakika
tano mama mmoja mnene mwenye
umri wa kati ya miaka arobaini hadi
arobaini na tano akatokea.Kwa mavazi
aliyokuwa amevaa ilionyesha wazi
kuwa alikuwa amekwisha jiandaa
tayari kwa kutoka kwenda katika
shughuli zake.
"Karibuni" akasema yule mama
.Steve na Elvis wakasimama
kumsalimu
"Madam Irene
shikamoo."akasema Steve huku
akimfuata na kumpa mkono kana
kwamba wanafahamiana hali
iliyomfanya Irene naye atabasamu na
kufurahia uchangamfu ule wa Steve
"Habari nzuri sana .Karibuni"
akasema huku akipeana mkono pia na
Elvis halafu wote wakaketi
"Samahani kwa kukusumbua
madam Irene tumefika dukani wakatuambia kwamba utachelewa
kufika ikabidi tukufuate hapa
nyumbani" akasema Steve
"Karibuni sana ila sina hakika
kama tunafahamiana.Mmeseam
mnatokea kampuni gani?akauliza
Irene
"Hapana hatufahamiani ila
tumekutafuta kwa ajili ya
mazungumzo ya kibiashara.Sisi tuna
kampuni yetu ya usafirishaji ....."
akasema Elvis na kuinuka akachomoa
makaratasi kutoka katika mfuko wa
koti na kumfuata Irene pale alipokuwa
amekaa kwa dhumuni la
kumuonyesha zile karatasi.Mara tu
alipoketi kitini akainua koti lake na
bastora ikaonekana.Irene akastuka
sana na kugeuka haraka na Steve naye
akainua koti lake ikaonekana bastora
na akamfanyia ishara ya kukaa kimya.Macho yakamtoka pima.Kwa
sauti ndogo Elvis akamwambia
"Usipige kelele wala
kutaharuki,inuka na tuongozane hadi
katika gari.Ukithubutu kupiga kelele
au kufanya chochote tunakufumua
kichwa chako.Now let's go!! akaamuru
Elvis huku akisimama na Irene naye
akasimama,Steve akaichukua
kompyuta yao wakaanza kuondoka
mle ndani.Walitembea kana kwamba
hakuna tatizo lolote.Sura ya Steve
ilionyesha tabasamu muda wote na
hakuna yeyote ambaye angehisi kuwa
Irene alikuwa ametekwa.Walifika
katika gari la akina Elvis Steve
akamfungulia mlango wa nyuma
akaingia kisha nao wakaingia garini na
kuondoka.
********************** I have to do anythng I can to get
Winnie back.Hawa jamaa akina Elvis
hawana uchungu kama nilio nao mimi
na ndiyo maana hawaonyeshi juhudi
zozote za kutaka kumtafuta
Winnie.Siwezi kumuacha ndugu yangu
wa damu akiendelea kuteswa bila
kufanya jitihada zozote za kumuokoa.I
must do something" akawaza Vicky
baada ya kuondoka katika nyumba
walikohamia.Alikuwa anatembea kwa
miguu na kwa mbali akaiona piki piki
inakuja,akapunga mkono na piki piki
ile ikasimama akamuelekeza dereva
ampeleke katika kituo cha
taksi.Dereva akaendesha kwa
mwendo wa kasi na kwa muda wa
dakika nane wakafika katika kituo cha
taksi akashuka na kuchukua taksi
iliyompeleka moja kwa moja
nyumbani kwake.Kitu cha kwanza alipofika nyumbani ni kuuliza walinzi
kama Winnie amefika pale akaelezwa
kwamba hajafika akaingia ndani
haraka haraka na kuwasha simu yake
akazitafuta namba za Frank na
kumpigia.
"Vicky!! ikasema sauti ya Frank
kwa mshangao
"Frank where are you?akauliza
Vicky
"Where are you? Frank naye
akauliza
"Niko hapa nyumbani
kwangu.Frank we need to talk"
"We need to talk?Frank akauliza
"Yes we need to talk"akasema
Vicky na Frank akavuta pumzi ndefu
akauliza
"What do you want?
"I want Winnie back!!
Badala ya kujibu Frank akaangua
kicheko kisha akasema You want me to free
Winnie,surrender yourself to me and
I'll let her go" akasema Frank
"Where are you now?
"You want to kill me too?akauliza
Frank
"Frank I only want Winnie,
nothing else"
"If you want Winnie back stay
where you are" akasema Frank na
kukata simu
Vicky alihisi kutetemeka kwa
ndani,alikuwa anaogopa
"Mwili unanitetemeka kwa woga
lakini sina namna nyingine lazima
nifanye hivi ili Winnie awe huru.Ni
bora kama nikiteswa mimi kuliko
Winnie hana kosa lolote.Sijui nini
kitatokea akina Elvis wakigundua
kwamba nimefanya hivi,lakini wao
ndio chanzo cha haya yote.Kama
wasingeniingiza katika mpango wao wa kumuua Pascal haya yote
yasingenikuta.Nadhani ni wakati
muafaka wa kuachana na hizi kazi na
kuendelea na shughuli zangu
nyingine.Kuendelea kuzifanya ni
kuendelea kumuweka hatarini ndugu
yangu Winnie" akawaza Vicky.
Mara tu alipomaliza kuzungumza
na Vicky simuni,Frank akampigia Obi
"Obi nimepigiwa simu muda si
mrefu na Vicky anataka kujisalimisha
ili kumuokoa mdogo wake"
"Unamuamini?akauliza Obi
"Bado sijamuamini yawezekana
huu ukawa ni mtego wanataka
kuutumia hivyo waache vijana wawili
hapo mlipo waendele kumchunga
Winnie halafu wewe na wengine wote
mjipange kwenda kumchukua Vicky
nyumbani kwake.Nataka apotezwe
fahamu ili asifahamu mahala
anakopelekwa.Chukueni kila aina ya tahadhari ili kuhakikisha kwamba
hakuna mtu yeyote anayewafuatilia
kwani kuna uwezekano mkubwa watu
hawa wanaomtumia wakamtanguliza
kama chambo ili waweze kunipata
kirahisi kama walivyofanya kwa
Pascal.Umenielewa Obi?
"Nimekuelewa mzee"
"Vipi kuhusu wale vijana
tuliowaacha katika ile nymba kuna
ripoti yoyote wametuma?
"Nimezungumza nao muda si
mrefu na mpaka sasa hakuna mtu
yeyote aliyefika pale nyumbani"
"Ok sawa wasiondoke waendelee
kubaki hapo hapo ili tujue ni nani
anaishi hapo" akasema Frank na
kukata simu akainuka na kwenda
kuchukua chupa ya mvinyo
akaimimina katika glasi na kuanza
kunywa huku uso ake ukiwa umejaa
hasira Hatimaye umekuja
mwenyewe.Wewe ndiye mwenye
majibu ya maswali yangu yote.Sipati
picha mateso nitakayokupa Vicky"
akawaza huku akiendelea kugugumia
mvinyo kwa fujo
***********************
Imekuwa ni kawaida ya Patricia
kutokupata usingizi usiku na badala
yake huanza kupata usingizi mida ya
alfajiri.Akiwa katika usingizi mzito
asubuhu akasikia simu yake
ikiita,akajiinua kivivu na kuichukua
akatazama mpigaji alikuwa ni
Meshack Jumbo.Haraka haraka
akaipokea
"Shikamoo mzee Jumbo" Marahaba Patricia,habari za
asubuhi?
"Nzuri kabisa mzee wangu"
"Patricia nimekupigia
kukujulisha kuwa leo hii utahama
hapo kwa akina Juliana.Kuna nyumba
nimekutafutia maeneo ya Peninsula ni
nzuri ambayo utaishi hapo kwa muda
wakati tunakutafutia makazi ya
kudumu.Tumeona tukuondoe hapo
kwani panaonekana si mahala salama
kwa wewe kuendelea kuishi hasa kwa
wakati huu ambao tunafanya
uchunguzi wa lile suala la
Juliana.Ninakwenda kukamilisha
taratibu za malipo asubuhi hiyo na
jioni ya leo kila kitu kitakuwa tayari
kwa wewe kuhamia hapo"akasema
Meshack
"Mzee Jumbo nakushukuru sana
kwa kunijali.Hata hivyo nakuomba
usisumbuke mzee wangu kutafuta nyumba kwani kuna sehemu
nitakwenda kuishi yenye usalama
zaidi.Rais na mke wake wameniomba
nikaishi nao ikulu hadi hapo
nitakapokuwa nimeweza kujitegemea
tena.Wale wazee wananipenda sana
na wananichukulia kama sehemu ya
familia yao hivyo usihofu kuhusu mimi
mzee Jumbo nitakuwa salama"
"Hilo ni jambo zuri sana
wamelifanya kwani pale ikulu kuna
ulinzi na usalama wa kutosha
sana.Hata hivyo bado nitaendelea
kufuatilia nyumba hii ili pale
utakapoondoka ikulu uweze kuwa na
sehemu ya kuanzia.Patricia najua
wewe ni mgumu sana kukubali vitu
hasa kutoka kwa watu wenye
mahusiano na Elvis lakini nakuomba
usikatae hili ninalotaka kulifanya kwa
ajili yako.Elvis nilimpenda kama
mwanangu na kwa sasa hayupo tena na jukumu la kukulea ninalibeba
mimi hivyo ninaanza kwa kukutafutia
makazi.Muda wowote ukichoka kuishi
ikulu utakwenda kuishi katika hiyo
nyumba niliyokutafutia"
"Ahsante sana mzee
Jumbo.Ninashukuru kwa hilo" akajibu
Patricia huku akitabasamu
"Ni lini unahamia Ikulu?
"Nimepanga kwenda ikulu baada
ya msiba wa hapa kumalizika.Nataka
nishiriki nao katika mazishi ya baba
yao ndipo niondoke.Ni watu wema
sana kwangu hivyo siwezi kuondoka
kabla msiba haujamalizika"
"Patricia ninakushauri ufanye
haraka sana kwenda ikulu kwani kuna
viashiria vinatuonyesha mahala hapo
si salama kwa wewe kuendelea
kuwepo hivyo itakuwa vyema kama
utahamia ikulu leo hii hii.Hata ukiwa
kule utaendelea kuwatembelea na kuungana nao katika msiba lakini
kitendo cha kuendelea kuishi hapo si
salama"
"Mzee Jumbo ahsante sana kwa
ushauri wako nitaufanyia kazi japo
Juliana atasikitika sana kama
nikiondoka na kumuacha peke yake"
"Hautamuacha peke yake Patricia
bado utakuwa na muda wa kwenda
kuungana nao katika msiba
tunachohitaji sisi ni kukuondoa tu
hapo"
"Nimekuelewa mzee
wangu.Nitafanya kama ulivyoelekeza
nitawasiliana na mama mke wa rais
nitamjulisha kuwa nitahamia kwao
leo"
"Good.Thank you very
much.Usimweleze mtu yeyote hata
Juliana kuwa unaondoka kwao kwa
sababu za kiusalama.Waeleze kwamba
rais amesisistiza uende ukaishi nao na wewe huwezi kumkatalia" akasema
Meshack Jumbo akaagana na Patricia
"Analolisema Meshack ni jambo
la kweli.Familia hii ya akina Juliana
inaonekana inawindwa sana na mimi
kuendelea kuishi hapa kunaweza
kuniweka matatani.Ngoja niondoke
zangu nikaishi ikulu sitaki tena
matatizo zai......."Patricia akatolewa
mawazoni na simu ya Dr Washington
"Habari za asubuhi Dr
Washington"
"Habari yangu nzuri,hofu yangu
kwako.Umeamka salama?
"Nimeamka salama kabisa."
"Ni hicho pekee ninachohitaji
kukisikia kutoka katika mdomo wako
kwamba unaendelea vyema" akasema
Dr Washington na halafu ukimya
ukapita
"Patricia utanisamehe kwa hili
lakini nina hamu sana ya kukuona.Nafahamu bado una
machungu mazito ya kifo cha mumeo
lakini naomba kama utaniruhusu
nikutembelee nije nikujulie
hali.Nataka nikufariji ana kwa
ana.Toka yalipotokea matatizo haya
hatujaonana na hii inanipa wakati
mgumu sana hata katika kutenda kazi
zangu.Kila wakati picha yako inakuja
kichwani kwangu.Nahitaji nikuone
Patricia,tafadhali nielekeze mahala
ulipo ili nikutembelee" akasema Dr
Washington.Patricia akavuta pumzi
ndefu na kusema
"Dr Washington hata mimi
nimekukumbuka sana na ningependa
kuonana nawe ila mazingira niliyomo
kwa sasa hayaruhusu mimi na wewe
kuonana.Tuendelee kuwasiliana
simuni na siku moja tutaonana tena"
akasema Patricia Nimekuelewa Patricia ila bado
nina swali moja.Utarudi tena
kazini?akauliza Dr Washington na
Patricia akachukua muda kidogo
kujibu
"Bado sijajua nini nitakifanya
kama nitarejea tena kazini au
vipi.Nitakujulisha maamuzi
nitakayochukukua kwani maisha
yangu tayari yamebadilika sana na
hayatakuwa kama yale niliyoishi
wakati niko na mume wangu.Dr
Washington ahsante kwa kunijulia
hali tutawasiliana siku nyingine"
akasema Patricia na kukata simu
tayari machozi yalikuwa yanamtoka
"Machozi haya ya kumlilia Elvis
hayatakauka kamwe.Elvis alikuwa ni
sehemu kubwa ya maisha yangu.Kuna
nyakati ninaomba utokee muujiza na
nimuone tena mume wangu mbele
yangu lakini haiwezekani.Elvis is gone.Kuna nyakati hata mimi
ninatamani kama ningekufa ili
nikaungane na mume wangu huko
aliko kwani naamini maisha yangu
yatakuwa magumu sana bila yeye"
akawaza Patricia na kujilaza tena
kitandani
*********************
Dr Makwa Tusangira na waziri
mkuu mstaafu David walikuwa mezani
wakipata kifungua kinywa kwani Dr
Makwa alilala hapa nyumbani kwa
David kwa hofu ya kukamatwa na
polisi baada ya kutangaza kufanyika
kwa mkutano wa hadhara uliopigwa
marufuku na jeshi la polisi.Wakiwa
mezani wakiendelea kupata kifungua
kinywa pamoja na maongezi mbalimbali simu ya Dr Makwa ikaita
akaipokea haraka
haraka.Akazungumza kwa dakika
zaidi ya kumi na mtu aliyempigia
halafu wakaagana huku uso wake
ukiwa na tabasamu kubwa
" Nilikuwa nazungmuza na
familia yangu tayari wamevuka mpaka
wa Namanga na wameingia Kenya.Ni
hao tu waliokuwa wananipa wasi
wasi.Ahsante sana David kwa msaada
wako mkubwa wa kuiondoa familia
yangu.Sitaki ipate misuko suko ya aina
yoyote" akasema Dr Makwa
"Dr Makwa siku zote familia
huwekwa mbele.Ningekushangaa sana
kama ungeacha familia yako hapa
Tanzania wakati unafahamu fika kuwa
machafuko makubwa yanakwenda
kutokea.Leo inazinduliwa rasmi safari
ya kuelekea ikulu.Hakikisha tafadhali kila kitu kinakwenda vizuri hatuhitaji
uzembe wa aina yoyote ile"
"Usihofu David kila kitu
kinakwenda vyema na hakuna uzembe
wowote utakaotokea.Tumejipanga
vizuri.Frank alifanya vyema sana
kuhakikisha tunapokea pesa jana na
zimetusaidia mno katika maandalizi
na matunda yake utayaona" akasema
Dr Makwa kisha wakaendelea na
mikakati mingine huku simu ya Dr
Makwa ikiita kila wakati akiwasiliana
na watu mbalimbali kuhusiana na
maendeleo ya mipango yao
****************
Steve aliendesha gari hadi karibu
na daraja ambalo ujenzi wake ulikuwa
umesimama akaegesha pembeni. "I'm going out.Endelea naye"
akasema Steve na kushuka akafungua
mfuniko wa injini na kujifanya
anatengeneza
"Irene naomba nisikilize kwa
makini sana.Hatuna tatizo nawe ila
kuna mambo tunataka kuyafahamu
kutoka kwako hivyo nakuomba uwe
mkweli kwa kila nitakachokuuliza."
akasema Elvis
"Ninyi ni akina nani?Mnataka
nini?Niambieni ni kiasi gani cha pesa
mnahitaji niwalipe but please don't
hurt me" akasema Irene huku macho
yake yakilengwa na machozi
"Hatuhitaji pesa Irene ila
tunachohitaji ni taarifa.Wewe ndiye
mmiliki wa kampuni ya Pendeza
Co.Ltd?
"Ndiyo.Hiyo ni kampuni yangu"
akajibu Irene Unaimiliki wewe mwenyewe
kwa asilimia mia moja au kuna mtu
mwingine unashirikiana naye?
"Hii ni kampuni yangu kwa
asilimia mia moja.Hakuna mtu
mwingine ninayeshirikiana naye"
"Are you sure?
"Yes I'm sure"
"Irene ninarudia tena kuuliza
kwamba kuna mtu yeyote
unayeshirikiana naye katika kumiliki
kampuni hii?
"Hakuna mtu mwingine,mmiliki
ni mimi peke yangu"
"Unaifahamu kampuni inaitwa
McLorien?
"Ndiyo ninaifahamu.Hao ni
washirika wangu wa biashara
.Wanatuuzia mzigo wa nguo na vatu
kutoka Marekani na Ulaya"
"Mara ya mwisho ilikuwa lini
kupokea mzigo kutoka kwao? Ni miezi kadhaa imepita"
"Mingapi?
"Miezi kama mitano au sita hivi"
"Hakuna mzigo wowote
umepokea kutoka katika kampuni hii
wiki tatu zilizopita?
"Hapana hakuna mzigo wowote
tumepokea"
"Are you sure?
"Yes I'm sure" akajibu Irene kwa
kujiamini
"Good.Unamfahamu
Frank?akauliza Elvis na swali lile
likamstua Irene akababaika
"Frank?..akauliza
"Frank yupi?akauliza tena
"Brigedia Frank"
Irene akawaza halafu akasema
"Hapana simfahamu mtu huyo"
"Are you sure?Elvis akauliza Yes I'm sure"akajibu Irene.Elvis
akamtazama kwa sekunde kadhaa na
kusema
"Irene wewe ni dada yangu na
nilikuonya toka awali kwamba
unieleze ukweli mtupu kwa yale
nitakayokuuliza lakini wewe
unanidanganya.Umeniudhi kwa
kuniambia uongo na mimi huchuia
sana mtu anaponieleza uongo"
"Sijakudanganya kaka yangu
simfahamu mtu huyo anaitwa brigedia
Frank"akasema Irene.Elvis akashusha
kioo cha gari na kumuita Steve
akamtaka aingie garini waondoke
"Mnanipeleka wapi?
"Nilikupa nafasi ukaichezea sasa
ni wakati wetu wa kuutafuta ukweli
kwa kutumia nguvu.Hatukutaka
kutumia njia hii lakini
umetulazimisha" Mtaniumiza bure kaka zangu
mimi simfahamu huyo Frank
nawaomba mniamini
tafadhali"akasema Irene.Steve
akawasha gari wakaondoka.Mara tu
walipoingia barabarani Elvis akatoa
karatasi mfukoni akazikunjua na
kumuonyesha Irene
"Hizi ni nyaraka za kutolea mzigo
bandarini ambazo zinaonyesha kuwa
wiki tatu zilizopita umepokea mzigo
wa viatu kutoka kwa kampuni ya
McLorien"
Irene macho yakamtoka mdomo
ikamtetemeka hakujua aseme
nini.Nyaraka zile zilieleza kila kitu
"Umekataa kwamba hujapokea
mzigo wowote kutoka kwa kampuni
ya Mclorien kwa miezi mitano au sita
lakini nyaraka zinaonyesha umepokea
mzigo wiki tatu zilizopita.kwa nini umetudanganya? akauliza Elvis na
Irene akamtazama kwa woga akasema
"Samahani kaka..Samahani
sana.Naombeni tuzungumze"
"Mazungumzo ni kutueleza
ukweli tu.Unamfahamu Frank?
"Hapana simjui Fr....."kabla
hajamalizia sentensi yake Steve
aliyekuwa katika usukani akageuka
kwa kasi ya ajabu na kumnasa kibao
kikali usoni
"Don't lie to us !! akasema na
kuendelea kuendesha
"Jamani naombeni msiniumize
simfahamu Frank"akasema Irene
"Nyaraka hizi tumezitoa katika
ofisi yake.Kwa nini
usimfahamu?Tueleze haraka
mahusiano ya Frank na kampuni
yako"akasema Elvis Nimekwisha waeleza kaka
zangu kwamba simfahamu kabisa
huyo Frank!! akasema Irene
"Unazidi kunipa hasira
Irene.Ninakupa nafasi ya mwisho
utueleze unamfahamu Frank? akauliza
Elvis
"Jamani naombeni mniamini
kwamba simfahamu Frank" akasema
Irene.
"Steve naomba vifaa vyangu"
akasema Elvis na Steve akafungua
droo ya gari na kumrushia kiboksi
kidogo akakifungua akatoa koleo
ndogo na kuukamata kwa nguvu
mkono wa Irena akakibana kidole kwa
koleo na Irene akapiga kelele kwa
maumivu makali aliyoyapata
"Tell me the truth! akasema Elvis
lakini Irene aliendelea kulia.Elvis
akamnasa kibao kikali halafu
akaukamata tena mkono wake na kukibana kidole kingine kwa koleo
lakini bado Irene aliendelea kushikilia
msimamo wake wa kutokumfahamu
Frank.Elvis akazidi kukasirika
akamshika kwa nguvu na kumlaza
katika kiti halafu akachukua kisu
kidogo
"Ninakwenda kuliondoa jicho la
kwanza na kama utaendelea kuwa
mbishi nitaliondoa jicho la
pili.Akasema na kumkandamiza Irene
kichwa na kukipeleka kisu sehemu ya
chini ya jicho na Irene akaanza kuhisi
kitu chenye nya kali kikiichana ngozi
yake
"Basi !! basi !! nitawaeleza
ukweli!! Usinimize tafadhali
nitakueleza kila kitu!! akasema Irene
na Elvis akamuachia.Tayari damu
ilikwisha anza kutoka sehemu ya
chini ya jicho la kulia.Irene akavuta pumzi haraka haraka hakuamini
kilichotaka kumtokea.
"Nataka majibu haraka sana"
akasema Elvis.Wakati haya yakitokea
gari lilikuwa katika mwendo mkali na
hakuna yeyote aliyeweza kuona
kilichokuwa kinaendelea ndani kwani
vioo vyote vilikuwa na rangi nyeusi
halafu Steve alifungua mziki kwa sauti
kubwa.
"Irene naomba usinipotezee
muda wangu.Nipe majibu haraka
sana"akasema Elvis
"Nitakueleza kaka angu ila
naomba msiniumize.Nitawaeleza kila
kitu"akasema Irene na kumtazama
Elvis kwa woga halafu akaendelea
"Frank ndiye mmiliki wa
kampuni hii ya Pendeza Co.Ltd"
akasema na kunyamaza kidogo
akafuta damu na kuendelea Hakutaka kujulikana kama
anamiliki hii kampuni hivyo
akanitumia mimi ili niwe kama
mmiliki wake lakini ukweli yeye ndiye
mwenye kampuni.Frank hajihusishi
na lolote katika kampuni hii zaidi ya
kuagiza mzigo na kutukabidhi."
"Frank ndiye huagiza mzigo?
"Ndiyo.Mimi humpelekea orodha
ya bidhaa tunazozihitaji na yeye
huagiza kutoka nje na baadae huja
kutukabidhi kwa ajili ya kuuza"
"Wiki tatu zilizopita kontena
zaidi ya kumi za viatu zimetolewa
bandarini.Mmeupokea mzigo
huo?akauliza Elvis na Irene
akababaika
"Irene answer me!! akafoka Elvis
"Tulipokea jozi chache za viatu
kwani bado havijapakuliwa katika
makontena.Upakuzi utakapokamilika basi tutaupata mzigo wote" akasema
Irene
"Mnasubiri upakuzi?Mnapakulia
wapi mzigo wenu mkiutoa bandarini?
"Mzigo unapokuja ni Frank
ambaye hushughulikia kila kitu na
kisha huenda kuupakua na ndipo
hutuletea kwa ajili ya kuuza.Mahala
anapopakulia hata mimi sipafahamu
na sijawahi kumuuliza kwani shida
yangu mimi ni kupata mzigo
pekee.Wakati mwingine mzigo huwa
unakuja kwa ajili ya maduka yetu
yaliyoko nchini jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo na Burundi."
"Mna maduka mengine Congo na
Burundi?
"Ndiyo tuna maduka mengine
mawili makubwa nchini Congo na
Burundi" akasema Irene. Namna gani huwa mnayatoa
makontena yenu bandarini? akauliza
Elvis na Irene akabaki kimya
"Irene usitake kuniudhi
tena.Nitakuondoa jicho lako sasa
hivi"akasema Elvis kwa ukali na Irene
huku akionyesha woga mkubwa
akasema
"Frank ndiye anayesimamia
utoaji wa makontena bandarini lakini
ninavyofahamu kuna watu huwa
wanatusaidia katika utoajia
makontena hayo"
"Mnapotoa makontena hayo
hupita katika mtambo maalum wa
kuchunguza na kuoa kilichomo ndani?
akauliza Steve
"Hapana hayapiti huko"
"Kwa nini?akauliza Elvis na Irene
akabaki kimya
"Kwa nini?akauliza tena lakini
Irene akabaki kimya Irene nataka majibu.Kwa nini
makontena yenu hayapiti katika
ukaguzi?akauliza Elvis lakini Irene
hakufumbua mdomo wake.Kufumba
na kufumbua akajikuta amenaswa kofi
kali sana lililomuangusha kitini na
damu ikaanza kutoka mdomoni.Elvis
akamkandamiza tena kichwa na
kukipeleka kisu jichoni
"Wait !!! wait !!.akasema Irene
"Irene tafadhali naomba usicheze
nami kabisa.!! Answer my questions !!
akasema Elvis
"Mizigo yetu haipiti katika
ukaguzi kwa sababu Frank hudai kuna
mizigo yake huwa anaipakia ndani ya
mzigo huo wa nguo au viatu ambayo
hataki ijulikane na ndiyo maana
mizigo haipiti katika ukaguzi"
"Ni mzigo gani huwa anaupakia
ndani ya makontena hayo ya viatu? Hajawahi kunieleza.Hiyo ni siri
yake mwenyewe na ndiyo maana
hushughulikia mizigo yote yeye
mwenyewe"
"Nani mshirika wake mkubwa
katika biashara zake ukiacha wewe?
"Frank ana marafiki wengi
wakubwa anaoshirikiana nao katika
mambo mbali mbali lakini katika
biashara hii ni mimi pekee
ninayeshirikiana naye"
"Nani unayemfahamu ambaye
anashirikiana naye kwa karibu zaidi?
"Ni Pascal ambaye ameuawa juzi"
"hakuna mwingine?
"Frank anafahamiana na watu
wengi hivyo sijui yupi anashirikiana
naye katika jambo gani ila huyo Pascal
ndiye muda mwingi walikuwa
wote.Huyo ndiye rafiki yake kubwa
ninayemfahamu"akasema Irene.Elvis akamtazama kwa muda halafu
akasema
"Tutakuacha uende zako ila
usimweleze Frank chochote juu yetu
sisi.Ukifanya hivyo you'll
die.Umenielewa Irene? akauliza Elvis
"Nimewaelewa na nitafanya
kama mlivyonielekeza,sintamwambia
Frank" akasema Irene na Elvis
akamuelekeza Steve aegeshe gari
karibu na hoteli 66.Palikuwa na taksi
nyingi pale Steve akashuka
"Get out of the car.Chukua taksi
na uende nyumbani!! akasema
Elvis.Irene akashuka kwa woga Steve
tayari alikwisha mtafutia gari
akamfungulia mlango na kumtaka
dereva ampeleke Irene mahala
atakapomuelekeza na dereva wa taksi
akamuuliza Irene mahala anakotaka
apelekwe akamuelekeza
wakaondoka.Steve alipohakikisha taksi ile imepotea kabisa akaingia
garini kisha nao wakaondoka
"Kwa nini umemuacha
aende?Steve akauliza
"Hana msaada tena kwetu.Tayari
amekwisha tueleza kile
tunachokitafuta hivyo hakuna haja ya
kuendelea kumshikilia.Kwa maelezo
yake ni wazi ndani ya makontena hayo
ndimo hupakiwa silaha ndiyo maana
hayapiti katika ukaguzi.Hapa
inaonyesha kuna mtandao uko
bandarini na ndiyo maana imekuwa
rahisi kwao kutoa mizigo yao bila
wasiwasi wala kukaguliwa.Hizi ni
taarifa nzuri sana
tumezipata.Makontena hayo huja
kama mzigo wa nguo na viatu kisha
hutolewa bandarini na halafu
husafirishwa kwenda Congo na
Burundi kama viatu na huko ndiko
huuziwa waasi.Haya ni mafanikio makubwa sana tumeyapata lakini
bado tunahitaji kuchimba zaidi na
kufahamu Frank anashirikiana na
akina nani katika biashara hii?Lengo
ni kuhakikisha mtandao wote
tunaung'oa.Hakuna
atakayesalia"akasema Elvis
"Nakubaliana nawe Elvis
kwamba sasa tumepata picha ya
kueleweka kuhusiana na biashara ya
silaha anayoifanya Frank.Nguvu
kubwa sasa tuielekeze katika
kumchunguza Frank ili tuufahamu
watu anaoshirikiana nao"
"Tunapaswa kufanya uchunguzi
pia bandarini kujiridhisha namna
makontena hayo yanavyotolewa na
tufahamu ni akina nani wanahusika
katika jambo hilo.Vile vile tusubiri
taarifa kutoka kwa Omola ili tufahamu
kuhusiana na kampuni ya
McLorien.Irene nimemuachia huru makusudi kabisa kwani naamini
atamueleza Frank na akipata taarifa
hizi atastuka sana na ataanza kutafuta
namna ya kujihami na sisi tutampata
kirahisi.Kwa sasa tuendelee
kukusanya vielelezo kuhusiana na hii
biashara.Bado hatuna ushahidi wa
kutosha kwamba ndani ya makontena
hayo kuna silaha" akasema Elvis
"Nimekupata vyema Elvis.Vipi
kuhusu Winnie?akauliza Steve
"Oh tumemsahau kabisa Winnie"
akasema Elvis na kuichukua kompyuta
"Bado inaonyesha yuko pale
pale.Tuelekee eneo la mtaa wa
viwanda.Huko ndiko aliko"
"Anafanya nini huko? akauliza
Steve
"Yawezekana amefichwa huko
kwani wale jamaa hawataweza
kumuachia hadi wahakikishe
wamempata dada yake"akasema Elvis na gari likasimama katika taa kabla ya
kuingia katika barabara ya Chaguso.
Sent using
Jamii Forums mobile app