Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bila kumsahau Wema kwenye I Do na Vicky madhahabu kwenye I was Wrong[emoji23] [emoji23] [emoji23] mambo ni [emoji91] [emoji91] [emoji91] [emoji91]Kwenye riwaya za Patrick kuna watu ukiwaangalia sifa zao zinafanana.
Jaji Elibariki kwenye peniela
Dr Marcelo kwenye Queen Monica
Na huyu Winnie
Hawa wote vihelehele vyao vinawaweka kwenye matatizo wenzao.
Can't Wait
"I do" na "I was Wrong" sijazisoma mkuu. Nkiliza hiiazisakaBila kumsahau Wema kwenye I Do na Vicky madhahabu kwenye I was Wrong[emoji23] [emoji23] [emoji23] mambo ni [emoji91] [emoji91] [emoji91] [emoji91]
Mimi naitafuta SERENA jamani kwenye chanzo changu haikufikaga mwisho, mwenye muendelezo wake plz!
Sent using Jamii Forums mobile app
Safi Sana mkuuI DIED TO SAVE PRESIDANT
Sehemu 69
awakute akina Steve akamlipa dereva
na kushuka na kuliona gari la akina
Steve likiwa limeegesha pembeni ya
barabara upande wa pili
wakimsubiri.Akavuka haraka
haraka,tayari akina Steve walimuona
na kumfungulia mlango akaingia
"We have to hurry" akasema
Elvis na Steve akawasha gari
wakaingia barabarani
"Nimezungumza na mkurugenzi
muda mfupi uliopita yuko njiani
anaelekea Yvona hotel na ninaamini
bado hajafika.Kutokea hapa hadi hotel
Yvona si mbali tutamuwahi kabla
hajafika huko" akasema Elvis
"Umemueleza tulichokigundua?
"Nimemueleza lakini anaonekana
kutonielewa.Hivi sasa anakwenda
Yvona hotel kuonana na Mbutolwe
ambaye amemtaka akaonane naye
pale.Ninajiuliza kama kuna jambo ambalo anataka kumueleza
mkurugenzi kuna njia zetu za
kuwasilisha taarifa za siri na si
kumuita mkurugenzi sehemu kama
zile.Nahisi huu ni mtego umeandaliwa
ili kumpata mkurugenzi.Tunatakiwa
kumuwahi kabla hajafika na kuhakiki
kama huu si mtego umewekwa ili
kumkamata.Kuna chochote
mmekipata kwa Juliana?" akauliza
Elvis
"Juliana amefanya uchunguzi
kuhusu mama yake na amegundua
kwamba anatumia majina tofauti
tofauti na ana vyeti vya kuzaliwa zaidi
ya vitano"
"Huyu mwanamke ni mhalifu
mkubwa wa kimataifa" akasema Elvis
"Kweli Elvis huyu lazima
anajihusisha na masuala ya kiuhalifu
na ndiyo maana anatumia majina
tofauti tofauti ili asijulikane.Tumempa kazi Juliana ya kuhakikisha
anafanikiwa kuipata simu au
kompyuta ya mama yake na ameahidi
kufanya kila awezalo kupata
mojawapo ya vitu hivyo kati ya simu
au kompyuta.Tukiachana na hilo la
Juliana tumepata pia mazungumzo
kati ya makamu wa rais na David "
akasema Steve na Omola akacheza ile
rekodi ya maongezi ya makamu wa
rais na David.Elvis akaisikiliza halafu
akairudia tena kwa mara ya pili
akashusha pumzi
"Dah ! akasema na kufuta jasho
usoni
"Makamu wa rais alipokea agizo
la kuniua kutoka kwa David ambaye
kwa mujibu wa maelezo yao kuna
watu wanashirikiana naye na ndiyo
maana akamweleza makamu wa rais
kuwa yeye hana wasiwasi hata kidogo
kama nimekufa ila washirika wake.Ni akina nani hao washirika wake ambao
wametaka mimi niuawe?akauliza Elvis
"Elvis kuna kitu tumekigundua
kutoka kwa Juliana.David na Elizabeth
wana mashirikiano,ni marafiki
wakubwa" akasema Steve
"Kama ni hivyo basi jibu
tumekwisha lipata.David naye
anashirikiana na akina Elizabeth
katika biashara ya silaha.Naye pia
yumo katika mtandao huu wa akina
Frank na ndiyo maana akamuomba
makamu wa rais niuawe.Tunatakiwa
pia kuchunguza kuhusu mipango yake
ya chini chini na makamu wa rais ya
kuwatumia wanasiasa hasa wa vyama
vya upinzani katika kusababisha
vurugu.Mkutano ambao umepangwa
kufanyika leo lazima utakuwa na
vurugu kwani hauna kibali cha jeshi la
polisi lakini wameendelea
kuwasisitiza wafuasi wao kuhudhuria kwa wingi mkutanoni leo.Nini kipo
nyuma ya haya
wanayoyafanya?akauliza Elvis
"Elvis kuna kitu kinanijia
kichwani,kama David ana
mashirikiano na akina Elizabeth na
Frank hudhani labda nao watakuwa
nyuma ya mkutano huu
wanauandaa?akauliza
"Siwezi kulipinga hilo lakini
kama wako nyuma ya harakati hizi za
kisiasa nini hasa lengo lao?Tuendelee
kuwachunguza na tutapata
majibu"akasema Elvis
"Kuna taarifa zozote kutoka kwa
Vicky hadi hivi sasa? akauliza Omola
"Mpaka sasa hakuna taarifa
zozote kutoka kwa
Vicky.Nimezungumza na mdogo wake
ambaye tayari amezinduka na
amenieleza mambo yaliyonishangaza
sana.Amenieleza kila kitu alichokifanya" akasema Elvis na
kunyamaza kimya kwa muda kisha
akasema
"Winnie hakukamatwa na akina
Frank bali alijipeleka yeye
mwenyewe"
"Yule binti ana wazimu !!!
akasema Steve kwa hasira
"Amekiri kwamba aliwaeleza
akina Frank kila kitu kuhusu sisi na
ndiyo chanzo cha Frank kuanza kuwa
na wasi wasi kuhusiana na mimi kuwa
hai"
"Kwa nini akafanya ujinga huo?
Ningekuwa karibu ningemchapa
makofi kwa ujinga
alioufanya"akasema Steve
"Anasema kwamba alifanya haya
ili kumuokoa dada yake.Hakutaka
dada yake afany.........."
"Elvis tumefika" akasema Steve
na kukata kona akaingia Yvonahotel.Hakukuwa na magari mengi
eneo la maegesho.
"Kwa mujibu wa mkurugenzi ni
kwamba amepanga kuonana na
Mbutolwe chumba namba 83.Naamini
bado hajawasili.Mimi na Omola
tutakwenda kufanya uchunguzi katika
chumba hicho ili tuwe na uhakika nini
hasa kinacho..."
"Elvis" akaita Steve na
kumkatisha Elvis
"Mkurugenzi tayari amefika.Gari
lake lile pale na anashuka" akasema
Steve
"Oh my God,tumechelewa,lakini
hakijaharibika kitu tunakwenda ndani
na kumlinda mkurugenzi dhidi ya
chochote kitakachotokea.Omola
utabaki garini mimi na Steve
tunakwenda ndani kumfuata
mkurugenzi" akasema Elvis na
kuweka sawa silaha zake wakashuka na kutembea kwa tahadhari kubwa
kuelekea ndani
Meshack jumbo baada ya
kushuka garini akaingia ndani ya
hoteli na kuelekea mapokezi akauliza
chumba 83 kiko ghorofa ya ngapi na
kujibiwa kipo ghorofa ya
tatu.Akapanda lifti na kuelekea
ghorofa ya tatu.Milango ya lifti
ikajifungua ilipofika ghorofa ya tatu
akashuka na kuanza kukitafuta
chumba namba 83.
Steve na Elvis hawakupita
mapokezi wakapitia upande wa hoteli
na kupanda ngazi zinazoelekea
vyumbani wakiwa katika tahadhari
kubwa.Hawakutaka kutumia lifti ili
kuweza kuyasoma mazingira
yalivyokuwa.
"Mpaka sasa sijaona hatari
yoyote"akasema Steve wakipanda
ngazi kukitafuta chumba namba 83 Mimi bado ninaamini
mkurugenzi hayuko salama hadi pale
tutakapohakikisha yuko katika
mikono yetu" akasema Elvis
wakaendelea kupanda ngazi wakafika
ghorofa ya tatu.
Meshack Jumbo alipofika chumba
namna 83 akagonga mlango na sauti
kutokea ndani ikamruhusu
kuingia.Ilikuwa ni sauti aliyoifahamu
vyema ya Mbutolwe mmoja wa
wafanyakazi wa idara
yake.Akakinyonga kitasa na kuingia
ndani.Alipatwa na mstuko mkubwa
ambao hakuutarajia mara nyuma yake
wakatokea watu wawili wakiwa na
bastora na kumtaka asipige ukelele
wowote bali aingie ndani ya chumba
kimya kimya.Meshack Jumbo hakuwa
na ujanja akaingia ndani ya kile
chumba.Mwili ulimtetemeka kwa
alichokiona mle ndani Happy mtoto wa mwisho wa
Meshack alikuwa amefungwa katika
kiti akiwa na sare za shule.Meshack
alihisi mwili wote unamtetemeka kwa
woga.Nyuma ya Happy walikuwepo
watu wawili waliofunika nyuso zao
kwa kofia na kuacha macho
pekee.Pembeni alikuwepo Mbutolwe.
"Daddy help me !!akasema Happy
huku akilia.Meshack akapandwa na
hasira zilizochanganyika na woga
akamgeukia Mbutolwe.
"Mbutolwe what's the meaning of
this? akauliza kwa ukali na mmoja wa
wale jamaa akasogeza kiti na kwa
sauti ya ukali Mbutolwe akasema
"Sit !!
"I cant believe this.Mbutolwe ni
wewe kweli unayenifanyia hivi?
akauliza Meshack kwa hasira "Mzee Meshack hatutaki
kupoteza muda wako na wetu.Uko
hapa kwa jambo moja tu.The truth!!
"Before anything please let my
daughter go !! akasema Meshack
"Meshack hapa ulipo huna nafasi
ya kutoa amri bali utafanya kila
tutakachokuamuru sisi !! akasema
Mbutolwe
"What truth do you want?
"Is Elvis alive or not ? akauliza
jamaa mmoja aliyekuwa amevaa suti
nyeusi
"Who are you to ask me that?
akauliza Meshack na yule jamaa
akamsogelea na kumnasa kofi kali
lililompeleka hadi chini akamfuata na
kumsindikiza na teke la tumbo halafu
akawaamuru wenzake wamuinue na
kumuweka kitini.Damu zilikuwa
zinamtoka mdomoni Please dont hurt my dady!!
akalia Happy.Yule jamaa akamsogelea
Meshack na kumshika kidevu
akamuinua kichwa
"Ninapokuuliza unatakiwa
unijibu na si kuniuliza swali.Hapa
mimi ndiye mkuu hivyo unapaswa
kuniheshimu!! akasema yule jamaa
aliyekuwa na macho yaliyojaa ukatili
"Nataka utueleze Elvis yuko hai
au amekufa?Ni hilo tu ndilo tunalotaka
utujibu kisha tutakuachia wewe na
binti yako lakini kama utaendelea
kuwa kiburi you and your daughter
both will die" akasema yule
jamaa.Meshack hakujibu kitu.
"Muda unakwenda Meshack
answer me !! akasema yule jamaa kwa
ukali akimtikisa tikisa Meshack na
ghafla Meshack akamtemea mate
usoni.Yule jamaa akatoa kitambaa
akajipangusa halafu akamsogelea Meshack na kumvurumishia makonde
mfululizo hadi alipoanguka chini.
Steve na Elvis walifika ghorofa ya
tatu na kuanza kufuatilia namba za
vyumba.Kulikuwa na watu wawili
wamesimama nje ya chumba namba
83 na pembeni kidogo kulikuwa na
mwanamama akifanya usafi.
"Mkurugenzi yuko mle ndani na
wale jamaa pale nje wanalinda
usalama.Tutakachokifanya
tutakapokaribia pale utajifanya
umeteleza halafu utamgonga yule
mwanamama anayefanya usafi na
utaipiga teke ile ndoo yake ya maji
lengo ni maji yawarukie wale jamaa
wawili waliosimama nje ya mlango na
mimi nitamalizana nao ili tuweze
kupata nafasi ya kuingia ndani" Elvis
akamuelekeza Steve wakati
wakitembea katika varanda.Wale
jamaa waliokuwa wamesimama katika mlango wa chumba 83 wakawatazama
akina Elvis wakija na ghafla Steve
akafanya kama alivyoelekezwa na
Elvis.Akateleza na kumgonga yule
mama aliyekuwa anafanya usafi halafu
akaipiga teke ndoo ya maji
yakamwagika na kuwarukia wale
jamaa waliokuwa mlangoni.Kitendo
kile cha kumwagiwa maji machafu
kiliwakasirisha mno wale jamaa
wakamfuata Steve pale chni kwa
wepesi wa aina yake akachomoa
bastora na kumuelekezea.Wakati
Steve akimdhibiti yule jamaa
aliyemfuata pale chini,Elvis naye
akamdhibti yule mwingine aliyebaki
halafu akamuamuru yule
mwanamama aliyekuwa anafanya
usafi afungue chumba namba 82,kwa
haraka akafungua na wakawaingiza
ndani wale jamaaMeshack Jumbo yuko
wapi?akauliza Elvis kwa sauti
ndogo.Yule jamaa hakumjibu.
"Last chance where's Meshack
Jumbo? akauliza Elvis
"Simfahamu Meshack Jumbo"
akasema yule jamaa na ghafla bila
kutarajia Steve akaizinga bastora yake
iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti
na risasi mbili zikatoka kwa haraka
zikatua katika kichwa cha yule jamaa
akaanguka na roho ikamtoka.Yule
mwenzake macho yakamtoka pima
"Umeona kilichompata
mwenzako?Nawe sasa hivi utakwenda
kuzimu,tuonyeshe alipo Meshack
haraka sana" akasema Elvis na yule
jamaa huku akitetemeka akawaeleza
kwamba Meshack alikuwa katika
chumba kilichofuata.
"Steve get rid of that woman"
akasema Elvis na Steve akamshika yule mfanya usafi akamkaba na
kumpoteza fahamu.
Elvis akamuongoza yule jamaa
taratibu wakatoka ndani ya kile
chumba wakaenda chumba 83
akamuamuru afungue mlango.Yule
jamaa akakinyonga kitasa lakini
mlango ulikuwa umefungwa kwa
ndani
"Who's that?ikauliza sauti toka
ndani
"It's me Kendric" akasema yule
jamaa
"What do you want? ikauliza
sauti toka ndani
"Open the door.I have something
impotant to tell you" akasema yule
jamaa na mara mlango ukafunguliwa
na jamaa mmoja akatokeza
kichwa.Kufumba na kufumbua Elvis
aliyekuwa nyuma ya Kendric akaruka
teke kali akaupiga mlango ukafunguka na kumuangusha yule jamaa
aliyekuwa ameufungua.Kama vile
wamepeana ishara,Elvis akamvuta
pembeni yule jamaa aliyekuwa
amemtanguliza mbele halafu Steve
akajirusha ndani bastora yake ikiwa
mkononi.Alipokuwa anarukia ndani
aliwaona namna wale jamaa
walivyokuwa wamekaa mle ndani na
mara tu alipotua chini kwa kasi ya
umeme akaizinga bastora yake na
zikatoka risasi mfululizo zilizowapata
jamaa waliokuwa wamezifunika nyuso
zao kwa kofia wakaanguka chini
halafu akakipiga teke kiti alichokuwa
amefungwa binti wa Meshack Jumbo
kikaanguka chini.Kitendo kile
kikawastua wale jamaa wengine na
mmoja aliyekuwa karibu na mlango
akataka kuchomoka lakini akakutana
na Elvis aliyemtandika teke kali la uso
akaanguka chini halafu akampiga kichwa kizito Kendrik akaanguka chini
na kupoteza fahamu huku damu
ikimtoka puani.
"Tulieni hivyo hivyo mlivyo"
akaamuru Steve lakini ghafla
Mbutolwe akaruka teke kali la haraka
lililompata Steve na kumpeleka
ukutani papo hapo yule jamaa
aliyekuwa anamuhoji Meshack
akamsogelea na kumtandika teke
lingine la mbavuni akaanguka chini
akigugumia kwa maumivu.Elvis
aliyekuwa nje akabiringika na kuingia
ndani akiwa na bastora mbili mkononi
na kuachia risasi zilizompata yule
kiongozi wao akaanguka
chini.Meshack Jumbo akapata nguvu
ya ghafla na kuinua kiti na kwa nguvu
zote alizokuwa nazo akampiga nacho
Mbutolwe kichwani akaanguka
chini.Akamfuata pale chini na kuanza
kumpiga na kiti kichwani na mchirizi wa damu ukaonekana mahala
alipoangukia Mbutolwe.Elvis
akamfuata
"Imetosha mzee.She's dead"
akasema Elvis halafu akamfuata Steve
aliyekuwa bado amelala chini
"Steve are you ok? akauliza
"Mshenzi yule amenipiga teke la
mbavu ninahisi maumivu makali sana
eneo hili la mbavu"
"Pole sana.Dr Philip atakuja
kukutazama but right now we need to
go" akasema Elvis na Steve akajitahidi
kusimama.Haraka haraka Elvis
akawavuta wale watu waliokuwa nje
akawaingiza ndani na kuufunga
mlango
"Ahsanteni sana vijana kwa
kuniokoa.Sikutegemea kabisa kama
ningeweza kuokolewa.Nilijua maisha
yangu na mwanangu yamefika
mwisho" akasema Meshack Jumbo Usijali mzee.Tumetimiza lile
tulilopaswa kulifanya.Steve wapekue
wote uone kama kuna chochote
chakuweza kutufaa" akasema Elvis na
Steve akaanza kuwapekua
"Imeniumiza sana hawa wawili
walioficha nyuso zao ni vijana
ninaowafahamu na mimi ndio
niliowapendekeza kuingia katika
kikosi cha walinzi wa makamu wa
rais.Kwa nini leo wame nifanyia
hivi?Ndio maana wameficha nyuso zao
kwa aibu ili nisiwatambue" akasema
Meshack Jumbo baada ya kuwavua
kofia walizovaa wale jamaa wawili
wakificha nyuso zao
"Usiwalamu sana mzee.Hawana
kosa lolote bali wanatekeleza maagizo
waliyopewa"akasema Elvis
"Who sent them?Who ever did
this to me must pay!! akasema na kumkumbatia mwanae aliyefunguliwa
kamba na Steve
"Wamekuumiza kokote hawa
washenzi?
"Hawa ni akina nani
baba?akauliza Happy huku
akitetemeka kwa mambo aliyoyaona
mle ndani
"Mzee tunatakiwa kuondoka
hapa mara moja" akasema Elvis na
Meshack akamshika mkono mwanae
wakatoka mle ndani wakaelekea chini.
"Mambo yameanza
kuharibika.Tayari wameanza kuwa na
wasi wasi kama kweli Elvis
amekufa.What happened?Kitu gani
kimewafanya waanze kuchunguza
kama amekufa?Waliofanya hivi lazima
ni mtandao wa akina Frank na
wenzake na kama ni hivyo basi familia
yangu itakuwa katika hatari
kubwa.Kama wameweza kumpata Happy na kumtumia ili kunilazimisha
niweke wazi kama Elvis amekufa au
mzima basi wanaweza wakaifuata
familia yangu nyumbani.I'll have to
protect my family" akawaza Meshack
akiwa garini baada ya kuondoka pale
Yvona hotel
"Elvis samahani sana kwa
kukupuuza.Ulijaribu kunionya
kuhusiana na hatari lakini sikuelewa
ni hatari gani.Niliamini niko salama na
hata nilipopata ujumbe kutoka kwa
Mbutolwe sikuwa na hata chembe ya
wasi wasi kwani ni mtu ambaye
ninamuamini sana.Aliponiita nilijua
kuna jambo amelipata anataka
kunieleza ndiyo maana nikawaacha
wageni nilikuwa nao nikawahi pale
Yvona hoteli kumbe ulikuwa ni
mtego.Mlifahamuje kama niko katika
hatari? akauliza Meshack Jumbo .Elvis
akamtaka Omola acheze ile rekodi ya makamu wa rais na David.Meshack
akaisikiliza na kushika mdomo kwa
mshangao
"Mambo haya ni vigumu
kuyaamini.David kumbe ndiye
anayetoa maelekezo haya kwa
makamu wa rais !! akasema Meshack
Jumbo kwa mshangao
"Ndiyo mzee.David amekuwa
anatoa maelekezo kwa Dr
Shafi.Tumegundua David ana
mashirikiano na Elizabeth na hii
inatufanya tuamini kwamba naye pia
yumo katika mtandao huu wa kuuza
silaha.Bado tunaendelea
kumchunguza makamu wa rais ili
tujue kama naye ana mahusiano
yoyote na mtandao huu wa akina
Frank.Tumegundua vile vile kwamba
makamu wa rais na David wako
nyuma ya mkutano wa vyama vya
siasa unaopangwa kufanyika leo licha ya jeshi la polisi kuupiga marufuku"
akasema Elvis na kumtaka Omola
aicheze ile rekodi ya makamu wa rais
na David wakizungumzia kuhusu
mkutano.Meshack akaisikiliza kwa
makini halafu akasema
"Kazi kubwa mmeifanya vijana
wangu.Haya ni mambo makubwa sana
mliyoyagundua.Hapa lazima kuna
jambo kubwa.Viongozi hawa
wakubwa kujihusisha na masuala
kama haya lazima kuna ajenda kubwa
nyuma yake"
"Kuna taarifa tumezipata
kwamba David ana mipango ya
kuwania urais na tunahisi labda
anataka kuwania urais kwa tiketi ya
upinzani na ndiyo maana ameanza
harakati zake chini chini"
"Anataka kuwania urais?!
Meshack akashangaa Kama ni hivyo basi yeye na Dr
Shafi wana lengo moja la kutaka
kujiunga na upinzani.Hilo si jambo
baya lakini wanatakiwa wafuate
taratibu na si kufanya mambo yao kwa
siri.Tuachane na mambo hayo ya
wanasiasa na tujikite zaidi katika
kuutafuta mtandao wa kuuza silaha
lakini kabla ya yote Elvis nahitaji
kuihamisha familia yangu na kuificha
sehemu salama.Watu hawa wanaweza
wakaitumia familia yangu kunitafuta
hivyo siwezi kuendelea kuiweka
familia yangu katika hatari.Nisaidie
tafadhali kwa hilo"
"Usijali mzee.Familia yako
itakuwa salama.Nina mtu ambaye
anaweza akaificha familia yako kwa
muda huu ambao tunaendelea
kupambana."
"Ahsante sana Elvis." akasema
Meshack ana Elvis akachukua simu yake akampigia Doreen akamueleza
kwamba kuna watu atawapeleka pale
kwake kwa ajili ya kujificha.Doreen
hakuwa na kipingamizi hivyo moja
kwa moja wakaelekea nyumbani kwa
Meshack Jumbo kuiondoa familia
yake.
****************
Alipotoka nyumbani kwa
Elizabeth Frank alielekea moja kwa
moja mahala alikopelekwa Vicky.
"Sikutegemea kabisa kama
mambo yangeharibika namna
hii.Katika wakati ambao mipango yetu
imeanza kwenda vizuri ndipo
vinapoibuka vikwazo ambavyo
hatukuvitarajia kabisa.Lakini haya
yote yamesababishwa na Graca.Pone
pone yake aendelee kujificha lakini
endapo nitafanikiwa kumpata sintakuwa na huruma naye hata
kidogo.Tayari amekwisha ingia katika
orodha ya maadui zangu na
nitamfanya kama ninavyowafanya
maadui zangu wengine.Nitamuua
kikatili sana.Sioni sababu ya kuwa na
mtoto kama yule ambaye hana faida
yoyote kwangu.Yeye ndiye
aliyeniingiza katika haya matatizo
yote.Kama asingejiunga na Elvis na
kumpa siri zangu mida hii ningekuwa
nimetulia ninakula mvinyo nikijiandaa
kuwa waziri wa ulinzi." Frank akahisi
mwili unamsisimka alipomkumbuka
Elvis,akakunja sura kwa hasira
"Huyu ndiye chanzo cha matatizo
haya yote.Je ni kweli yuko hai? Winnie
hakuonekana kama anasema uongo
lakini mtu pekee ambaye alipaswa
kutoa ukweli kuhusiana na Elvis
kuonekana ni Vicky ambaye yeye
ameleta hadithi nyingine kabisa.Nilitegemea kumtesa mdogo
wake mbele yake ili kumfanya
afunguke lakini naye amechukuliwa
na watu wasiojulikana.Je ni nani hawa
waliomchukua Winnie?Wamejuaje
kama yuko pale?akajiuliza
"Lazima ni watu wataalamu sana
walioweza kufahamu mahala
alipofichwa Winnie na nina hakika
Vicky atakuwa anafahamu kila
kinachoendelea.Nimepewa hadi saa
kumi na mbili kuhakikisha amesema
yote.Nitampa mateso makali na
ataongea kila kitu" akaendelea
kuwaza Frank
Aliwasili katika nyumba
alimokuwamo Vicky.Obi na vijana
wake walikuwa wameimarisha ulinzi
"Kila kitu kinakwenda vizuri
hapa? akauliza Frank baada ya
kushuka garini na kupokewa na Obi Kila kitu kinakwenda vyema
mkuu.Wale vijana wetu tayari
tumewahifadhi kimya kimya bila
familia zao kufahamu chochote kwani
wanaweza wakafanya uchunguzi na
sisi tukajiweka matatani"
"Good.Waelekeze vijana wako
waimarishe ulinzi nataka nimtese
mwenyewe huyu Vicky na leo ataeleza
kila kitu" akasema Frank na kuelekea
ndani katika chumba alimowekwa
Vicky.Akamtazama kwa hasira halafu
akavua koti na kulitupa chini
"Vicky naomba unisikilize
vizuri.Safari hii nimekuja kikazi hivyo
sitaki kupotezewa muda wangu
nawe.Nitakuuliza swali moja tu na
endapo utashindwa kunijibu basi
sintakuwa na huruma nawe hata
kidogo" akasema Frank
"Frank nimekwisha kueleza
kwamba siwezi kuzungumza nawe jambo lolote bila ya kumuona kwanza
mdogo wangu Winnie.Bring Winnie
here and we'll talk" akasema Vicky
"Vicky inaonekana bado
hujanifahamu vyema na leo
nitakuonyesha upande wangu wa pili
ambao bado haujaufahamu
vyema.Utanisamehe sana kwa hilo"
akasema Frank
"Unapoteza muda wako Frank
huwezi kupata chchote toka kwangu
hadi nimuone mdogo wangu Winnie"
akasema Vicky
"Tutaona" akasema Vicky na
Frank akamuita Obi
"Andaa kila kitu niwekee hapo
mezani" akasema na Obi akatoka
"Vicky sipendi nikuumize
naomba kwa mara ya mwisho
uniambie wako wapi wale watu
waliokuteka? Yuko wapi Elvis? Frank nimechoshwa na hilo
swali lako.Mara ngapi nikwambie
kwamba siwafahamu hao watu !!
akasema Vicky kwa ukali.Obi akarejea
akiwa na sanduku la chuma akaliweka
mezani na kuanza kutoa vifaa mbali
mbali vya kutesea akavitandaza
mezani
"Mfunge mikono mning'nize
katika kamba" akasema Frank na Obi
akamshika Vicky mikono akaifunga na
kumning'iniza
"Good.Muondoe hizo nguo
zote"akaamuru Frank.Obi akazivua
nguo za Vicky akabaki mtupu.Frank
akachukua fimbo yenye mikia sita
iliyofungwa vyuma vyenye makali
nchani mwake akamsogelea Vicky na
kwa kutumia nguvu akamchapa na
fmbo ile mgongoni,vile vyuma vyenye
makali vikazama katika nyama na Frank akavuta kwa nguvu vikamchana
chana Vicky mgongo
"Aaaaaggghhhhhhh!!!!!!!! Vicky
akapiga ukelele mkubwa.Frank
hakujali akamchapa tena na kuongeza
maumivu zaidi huku Vicky akiendelea
kupiga kelele na damu kumtoka
"Where is Elvis?! akauliza Frank
"I..I..I dont know...." akajibu
Vicky.Frank akamchapa tena kwa
nguvu na ile fimbo lakini Vicky
hakutamka chochote.
"This is not working" akasema
Frank akiwa amejawa na hasira baada
ya kumuona Vicky ameloa damu mwili
mzima lakini hakuwa ametamka
chochote.Akaenda mezani
akachukukua chupa fulani na
kuibonyeza ikatoa maji akammiminia
Vicky mwilini akatoa ukelele mkubwa
sana kwa maumivu makali
aliyoyasikia Tell me where is Elvis?!!
akauliza Frank kwa ukali lakini Vicky
hakumjibu akaendelea kutoa ukelele
wa maumivu.Frank akamwagia tena
lakini licha ya maumivu makali
aliyoyahisi na kuuona mwili wote
unawaka moto hakuthubutu kutamka
chochote
"Huyu ni mwanamke wa aina
gani anayeweza kuvumilia mateso ya
namna hii?Hata wanaume hawawezi
kuvumilia mateso ya aina hii.Haya
maji pekee ya maumivu yanatosha
kabisa kumfungua mtu yeyote aliye
mgumu kufunguka na akasema kila
kitu.Hata hivyo nitaendelea kumtesa
na atasema kila kitu" akawaza Frank
akachukua kifaa chakukatia vyuma na
alipomkaribia akagundua Vicky
hakuwa na fahamu
"C'mon wake up !! akasema na
kumnasa Winnie kofi zito Nataka nikuondoe hizi nyeti
zako kwani ndiyo sababu ya wewe
kuendelea kuwa hai mpaka
sasa.Nilikuwa na mipango ya kukuua
lakini ni hizi nyeti zilizonifanya
nibadili mawazo baada ya kuonja
utamu wake.Nitakuondoa kiungo
kimoja kimoja hadi utakaposema kile
ninachokitaka" akasema Frank na
kumuangalia tena Vicky ni kweli
hakuwa na fahamu.Akamuita Obi na
kumtaka amfungue amuweke
kitandani azinduke.Damu ilikuwa
imeacha kutoka kufuatia yale maji ya
maumivu makali aliyomwagiwa.
"Mkuu taratibu usije ukamuua
kwani tunamtegemea sana kupata
taarifa muhimu.Akikushinda nipe
mimi kazi hiyo na atasema tu"
akasema Obi
"Nitamalizana naye mimi
mwenyewe leo.Lazima atasema kila kitu.Nitampa mateso ya kila aina na
atasema tu!! Hakikisha anazinduka
haraka"akasema Frank na kutoka mle
chumbani.
"Mwanamke wa aina gani
huyu?Mateso haya yote niliyompa
hajathubutu kusema chochote?Mateso
haya hata wanaume huwa
wanashindwa kuyavumilia lakini bado
amefumba mdomo wake.Sikutegemea
kama angeshindwa kusema kitu baada
ya kumwagiwa yale maji ya
maumivu.Amenishangaza mno ujasiri
wake.Au anasema kweli?Kama ndiyo
nani basi mkweli kati yake na
Winnie?Kwa nini Winnie anitafute
kunieleza maneno yale ambayo kwa
asilimia kubwa ninaamini ni ya kweli
halafu anatokea Vicky na kudai kuwa
maneno yale hayakuwa ya kweli?I'm
confused lakini huyu Vicky leo lazima
atanieleza ukweli" akawaza Frank akiwa ananawa mikono akifuta damu
iliyomtapakaa mikononi
Obi alimfungua Vicky akamlaza
kitandani na kumfungua kamba zote
akaanza kumpepea ili azinduke
"Dah ! Kwa kuwa ni kazi tu ndiyo
maana ninamtesa lakini kama si hivyo
kamwe nisingeweza kumtesa
mwanamke mzuri kama
huyu.Ukimtazama akiwa mtupu
unaweza pata uchizi wa ghafla na
uzuri wa kipekee sana"akawaza Obi
akimtazama Vicky kwa
matamanio.Taratibu akampapasa
Vicky mapajani
"Frank amemuumiza
sana.Mrembo kama huyu hastahili
kuumizwa namna hii" akawaza Obi
akiendelea kuyapapasa mapaja ya
Vicky ambayo licha ya kwamba
yalikuwa yameloa damu lakini bado
yaliendelea kuvutia.Ghafla kukatokea jambo ambalo Obi hakuwa
amelitegemea kabisa.Vicky aliinuka
ghafla na kwa nguvu akamrukia Obi
akampiga kichwa kilichomfanya Obi
aone nyota akajibamiza ukutani.Vicky
akaruka toka kitandani kwa lengo la
kumfuata Obi lakini tayari Obi
alikwisha jua dhamira ya Vicky
akainua chupa iliyokuwa karibu
akairusha lakini Vicky akaiona
akaikwepa.Obi akajirusha mzima
mzima na kumvaa Vicky wote
wakaanguka chini kisha akaanza
kumshindilia makonde mazito.Mara
Vicky kwa kutumia miguu yake
akamkaba Obi kabali na kumuangusha
chini.Obi akajitahidi kujitoa katika
kabali ile lakini Vicky kwa kutuima
nguvu zake zote alizobaki nazo
akahakikisha Obi hachomoki.Obi
akatambua kwamba Vicky alikuwa
vizuri na kama angefanya mzaha angeweza kupoteza
maisha.Akanyoosha mkono na
kuushika mguu wa meza iliyokuwa na
vifaa vya kutesa akaivuta na meza ile
ikaanguka na vifaa vile kutawanyika
chini,akaokota kisu na kutaka
kumchoma nacho Vicky lakini kwa
jicho kama la tai akauona mkono wa
Obi ukiwa na kisu ukimuelekea
sehemu za kifuani akauzuia kwa
mkono wake wa kushoto halafu kwa
kutumia mkono wa kulia akachukua
chupa iliyoanguka karibu yake
iliyokuwa na kimiminika akampulizia
Obi usoni na akasikia akitoa ukelele na
akaangusha kile kisu akakiokota na
kukizamisha tumboni mwa
Obi.Akaitoa miguu yake shingoni kwa
Obi halafu kwa hasira akakizamisha
kile kisu kwa mara nyingine kifuani
kwa Obi mahala ulipo moyo na Obi
akaanza kutapa tapa akikata roho.Vicky akajiegemeza ukutani
akitweta.
"I need to get out of
here.!!akawaza na mara akasikia hatua
za mtu akainuka na kuchukua kisu
alichokitumia kumuulia Obi akaenda
kujificha pembeni ya mlango.
"Ob.............." akasema mtu
aliyeufungua mlango na kwa kasi ya
umeme Vicky akaurusha mkono
wenye kisu akimlenga usoni yule
jamaa ambaye kwa sauti alimtambua
ni Frank lakini alikiona kitendo kile na
akaupiga mkono ule wenye kisu
kikaanguka halafu akamvuta Vicky na
kumpa ngumi nzito iliyompeleka chini
na ndipo alipoweza kuona kile
kilichokuwa kimefanyika mle
chumbani.Obi alikuwa amelalia
dimbwi la damu hakuwa na uhai
tena.Frank akatetemeka kwa hasira Umemuua Obi?!!! akaulizia huku
akitoa bastora yake kwa lengo la
kumfuata Vicky pale chini alipokua
ameanguka na ghafla bila kutegemea
Vicky akamkata ngwala na Frank
akaanguka mzima mzima kama
furushi akagongesha kichwa
sakafuni.Vicky akainuka ili aweze
kumkabili lakini Frank akaokota kisu
na kukirusha kikamchoma Vicky
begani na wakati akijaribu
kukichomoa Frank akasimama na
kumtwisha tena ngumi nyingine
iliyompeleka Vicky sakafuni na bila
kupoteza muda Frank akamfuata pale
chini na kumkalia juu akaanza
kumvurumishia makonde mazito.
"Who are you ?Leo utanieleza
wewe ni nani.Hakuna aliyewahi
kupambana na Obi akabaki hai!!!
akasema Frank.Vicky akakiona kile
kisu alichochomwa begani kikiwakimeanguka karibu naye akakiokota
na kukizamisha mbavuni mwa Frank
"Aaaghhh!!! Frank akapiga
ukelele mkubwa na Vicky akaitumia
nafasi hiyo akamsukuma
akaanguka.Mwili wa Vicky haukuwa
na nguvu,akajizoa zoa ili kumkabili
Frank ambaye alikua chini akigugumia
kwa maumivu.Mara Frank akaiona
bastora yake ikiwa karibu akaiokota
na kugeuka huku damu ikimtiririka na
kumnyooshea Vicky
"Stay where....yo..you...are...."
akasema akiwa katika maumivu
makali na damu ikiendelea kumtoka
mahala alipochomwa kisu
"Frank put the gun
down"akasema Vicky
"I'm going to kill y...." kabla Frank
hajamaliza sentensi yake Vicky
akaruka na kuupiga teke ule mkono
uliokuwa na bastora ikaanguka akaokota kifaa cha kukatia vyuma
akakiwasha na bila kupoteza hata
sekunde moja akakipitisha katika sikio
la kushoto la Frank na
kuliondoa.Frank akatoa ukelele
mkubwa.Vicky akiwa bado na hasira
akakipitisha kifaa kile katika goti na
kuukata mguu.
"Aaagghhh..!!!! akapiga ukelele
wa maumivu.
"Wewe hasa ndiye niliyekuwa
nakutafuta.Leo nimekupata na ni
zamu yako kwenda kuungana na wale
ambao wameuawa kwa sababu ya
silaha ambazo wewe na mtandao
wako mmekuwa mnaziuza kwa
waasi.Ni wakati wenu wa kulipa uovu
wenu!! akasema Vicky akamtazama
Frank kwa hasira halafu akaliondoa
tena sikio lingine la Frank kwa
kutumia kile kifaa Mtu katili sana wewe na tayari
umekwisha ua watu wengi.Unastahili
kufa kifo cha maumivu makali
mno.Sintakuacha hai" akasema Vicky
huku Frank akihangaika pale chini na
hakuweza kuzungumza tena lakini
sura yake iliyokuwa imeloa damu
ilionyesha alikuwa kaika maumivu
makali mno.
"Unastahili kufanyiwa ukatili
huu!!! akasema Vicky akiwa amejawa
hasira na kukishika kiganja cha mkono
akakikata halafu akachukua ile chupa
yenye maji ya kuongeza maumivu
akamwagia sehemu zile alizomkata na
Frank akajinyonga nyonga kwa
maumivu makali aliyoyapata.
"Unastahili kuyapata maumivu
makali kabla hujafa.Maumivu kama
haya ndiyo wanayoyapata ndugu zetu
wa huko Congo ambao maisha yao
yamekuwa magumu kwa sababu yako wewe na wenzako" akasema huku
akimtazama Frank aliyekuwa amelalia
dimbwi la damu
"Natamani nikukate kiungo
kimoja kimoja ili ufe kwa maumivu
makali sana lakini hautaweza kuishi
tena.Ninakuacha ufe taratibu na hii ni
salamu kwa wenzako wote wajiandae
tunakuja" akasema Vicky na kuiokota
bastora ya Frank
"Umenitesa sana bazazi wewe na
ulikuwa na lengo la kuniua lakini
wewe ndiye utalayetangulia mbele za
haki na ukajibu maswali kwa roho za
watu zilizotolewa kutokana na silaha
mnazouza"akasema Vicky halafu
akampekua Frank na kumkuta na
simu mbili moja ikiwa ni ile ya kwake
"Ouh thanks God" akasema na
kuiwasha ilikuwa na chaji kidgo sana
na mda wowote
ingezima.Akamtazama Frank ambaye alikuwa anatapa tapa pale chini
akionekana hatakuwa na muda mrefu
wa kuishi
"Nguvu zimeniisha na siwezi
kuendelea kupambana tena na hawa
jamaa kwani inaonekana wako
wengine huko nje.I need help.I have to
call Winnie" akawaza Vicky halafu
akazifafuta namba za Winnie
akapiga.Simu ikaita na kupokelewa
"Hallow dada " akasema Winnie
na Vicky akashusha pumzi
"Winnie uko wapi? Are you safe?
"Dada niko salama.Niko hapa
kwa akina Elvis.They saved my
life.Wewe uko wapi dada? akauliza
Winnie huku machozi yakimtoka
"Oh thak God .Nilikuwa na wasi
wasi sana na usalama wako.Winnie
uko karibu na akina Elvis?
"Hapana wametoka wote niko na
Graca pekee.Uko wapi dada?akauliza Winnie "Winnie I'm in trouble and I
need help.Nahitaji msaada wa akina
Elvis haraka sana" akasema Vicky
"Where are you ?Nielekeze nije
hapo nikuchukue haraka sana"
akasema Winnie
"Not you Winnie.I need Elvis and
Steve people who can fight" akasema
Vicky
"Nisubiri kidogo nimuulize Graca
kama ana mawasiliano ya akina Elvis"
akasema Winnie na kutoka akamfuata
Graca akamuuliza kama ana
mawasiliano na akina Elvis
"You want to run again? akauliza
Graca
"Graca please its Vicky.She's
stuck some where and she needs
help.Kama una mawasiliano na akina
Elvis nipe nizungumze nao tafadhali"
akasema Winnie Oh.Elvis amenipa simu mpya
ambayo nitakuwa naitumia katika
kuwasiliana nao ngoja nimpigie"
akasema Graca na kuchukua simu
yake iliyokuwa na namba mbili tu za
Steve na Elvis akampigia Elvis
"Graca" akasema Elvis baada ya
kupokea simu
"Elvis kuna jambo limetokea
hapa muda si mrefu na linahitaji
msaada wenu"
"Jambo gani?
"Vicky amepiga simu na anahitaji
msaada wa haraka sana"
"Vicky?Yuko wapi? akauliza Elvis
na Graca akampa simu Winnie
" Elvis its me Winnie.Vicky
amenipigia muda si mrefu katika simu
yangu na amenieleza kwamba yuko
mahala na anahitaji msaada wenu wa
haraka." Sawa Winnie naomba unipe
namba zake za simu niwasiliane naye"
akasema Elvis na Winnie akampa
namba za Vicky na bila kupoteza
muda akampigia Vicky
"Hallo Vicky,where are you?
What happened to you? akauliza Elvis
"Elvis listen tome.Simu yangu
inakaribia kuisha chaji na sifahamu
mahala nilipo hivyo naomba mtumie
ile programu ya Omola aliyotumia
kumtafuta Winnie kunitafuta na kujua
mahala nilipo.I'm in great danger so
please help me" akasema Vicky
"Sawa Vicky.Stay where you are
and we'll be there very soon.Please
make sure you are safe" akasema Elvis
na kukata simu akamfuata Omola
"Omola Vicky amepiga simu na
yuko katika hatari anahitaji msaada
wetu.Tumia ile programu yako
uliyotumia kumtafutia Winnie ili tujue mahala aliko Vicky" akasema Elvis na
bila kuchelewa Omola akawasha
kompyuta yake na kuanza kuitafuta
simu ya Vicky
"Nimeipata" akasema na
kumuonyesha Elvis mahala alipo
Vicky.Elvis akamfuata Meshack Jumbo
"Mzee sisi tunahitaji
kuondoka.Tumepata taarifa Vicky
yuko katika matatizo na anahitaji
msaada.Utaongozana na Steve hadi
kwa Doreen ili ahakikishe nyote mko
salama.Usihofu kuhusu familia yako
itakuwa salama.Ninamuamini Doreen"
akasema Elvis
"Usijali Elvis,ahsante sana kwa
kila kitu"akasema Meshack Jumbo
halafu Elvis akamfuata Steve
"Steve Vicky amepiga simu muda
si mrefu yuko katika matatizo na
anahitaji msaada.Mimi na Omola
tunakwenda huko.Tayari Omola amekwisha pata mahala aliko
Vicky.Wewe utaongozana na Meshack
Jumbo kuelekea kwa Doreen.Make
sure they are all safe.Ukiwafkisha
salama utamchukua Meshack Jumbo
na kumleta kule kwenye kambi yetu
ila familia yake itaendelea kukaa pale
kwa Doreen hadi mambo
yatakapomalizika" akasema Elvis
"Sawa Elvis.Endapo mtahitaji
msaada usisite kunijulisha nami
nitakuja mara moja" akasema Steve
na Elvis akamfuata Doreen
"Doreen mimi ninaondoka kuna
sehemu ninakwenda mara
moja.Tafadhali hakikisha familia hii
inakuwa salama.Muda wowote ukihisi
hatari nijulishe haraka" akasema Elvis
na bila kupoteza muda akaingia garini
na Omola wakaondoka kumfuata
Vicky
Sent using Jamii Forums mobile app