Riwaya: Jina langu ni Pheady

Riwaya: Jina langu ni Pheady

12
Tulifika Musoma kwenye saa saba usiku na kukuta nyumba za wageni nyingi zimefungwa. Zilikuwa zimebaki nyumba za wageni za uswahilini ambazo kwa mji wa Musoma hazifai maana kuna mtindo wa polisi kupita na kuwaamsha watu wajitambulishe.
Kutokana na hali hio nilitafuta maegesho mazuri pembeni ya mji nikaegesha gari tukalala ndani ya gari kumalizia masaa yaliyobaki. Niliondoa pale gari alfajiri majira ya saa kumi na mbili Kikakika naye alikuwa macho, tulienda mpaka sehemu moja ya ziwani inayoitwa Mwigobhelo huko kuna wavua samaki na Kuna sehemu inaruhusiwa kuoga. Niliegesha gari hatua chache na kushuka kwenda ziwani kupiga mswaki na nilioga palepale ziwani, Kikakika yeye hakuweza kuoga kutokana na majeraha yake. Wakati namaliza kuoga na kutoka pale ziwani kulishapambazuka tu na watu walishaanza kuchakarika mitaani. Nilitekenya gari na kuliondoa kuelekea mjini, nilipofika mjini nilitafuta hotel nzuri iliyoanza kutoa huduma. Baada ya mitaa kukata mitaa miwili mitatu hivi nilipata hotel inayotufaa katika mtaa wa Nyasho, niliegesha gari pembeni tukashuka tayari kwa kwa kupata kifungua kinywa.

Ilipofika saa tatu tulishamaliza mipangilio yote ya hapa Musoma, Kikakika alipata tiketi ya ndege ambayo unaondoka saa tano na robo kwenda Dar kupitia Kilimanjaro. Wakati huo tulikuwa kwenye ofisi zetu za hapa Musoma zilizopo mtaa wa Kamnyonge. Tulikubaliana na Kikakika nimuache pale mimi niondoke, nilipata kijana mmoja kutoka ofisi za hapo Musoma ambaye alijitolea kunisindikiza na gari tulilokuja nalo alafu angerudi nalo Musoma ili lipelekwa Tabora. Tuliagana na Kikakika nilimuacha anasubili saa tano ifike naye aondoke.
Safari ilianza kuelekea Ukerewe, kutokana na udhoefu wangu wa kuendesha magari haikuchukua tulikuwa tumefika Kisorya sehemu ya kivuko inayotumia kivuko kuingia Ukerewe kutoka mkoani Mara, Ilikuwa ni muda wa saa tano na nusu. Tulikuta kivuko kikiwa sehemu ya Ukerewe hivyo ilibidi kusubiri kirudi ili tuweze kuvuka, niliingiza mkono mfukoni na kutoa shilingi elfu ishirini na kumpa yule kijana niliyekuwa nae alafu nikamwambia hapo panatosha anaweza kurudi na gari Musoma. Niliagana naye akageuza gari na kuondoka, mie niliendelea kusubiri na ilipofika saa sita na nusu tulikuwa tumeishavuka, nilipata usafiri wa gari ndogo ya abiria pale Rugezi iliyonipeleka mpaka nyumbani Nansio.
Nilifika nyumbani na kuwakuta watoto wa kaka ambao huja kukaa pindi ninaposafiri kwa ajili ya usalama na usafi wa hapo kwangu. Walinipokea kwa furaha na kuniandalia chakula, wakati nakula ndipo wakati taarifa ya habari ilikuwa inasomwa, mara msomaji wa taarifa alisikika akisema; "Mwanza". Nilitega masikio kwa makini, "Nyumba moja ya mkazi wa Mwanza South aitwae Magesa imeungua moto usiku, maiti zipatazo tisa zimeonekana katika hiyo nyumba, Ikiwemo ya mwenye nyumba. Baada ya kufanyiwa uchunguzi imegundulika nane wameuawa kwa risasi na mmoja kauawa kwa kisu. Inaonekana mauaji hayo yalifanyika kabla ya nyumba kuwaka moto. Polisi wako mbioni kuwasa wauaji hao wakiongozwe na Ins.Bonifasi Mapambo. Taarifa hiyo iliishia hapo na kuendelea na habari nyingine.
Loo! Baada ya kusikia hivyo hamu ya chakula ilinitoka, kwani nilieleza iwapo mke wa Mzee Magesa ataulizwa kuhusiana na tukio hilo washukiwa wa kwanza tunaweza kuwa sisi kulingana na jinsi tulivyokuwa tunaingia pale na kutoka. Ila kitu kimoja hatufamu vizuri zaidi ya kuziona sura zetu kwa muda mfupi. Na kushukiwa kwetu kungetokana na mkewe Mzee Magesa kutokujua shughuri za sir za mmewe alizokuwa akifanya chini ya kivuli cha ofisi za kitapeli zinazojihusisha na biashara kumbe kumbe ziko chini ya kikosi cha wizi kiitwacho Cool Blood.
Nilitoka mezani na kusema nimeshiba, wale watoto wa kaka wakaja kufanya usafi wa meza, wakati huo nikaamua kupiga simu kwa yule msichana aitwae Mtuli ili niweze kufahamu iwapo mchumba wake naye yupo kwenye zile maiti zilizopatikana kwa Mzee Magesa. Kwani iwapo kumbukumbu zako ni nzuri utakumbuka tulijuana naye baada ya kumsikia akiongea juu ya Patrick kule Magnum Club, hivyo nikamuhisi vibaya na kuamua kukaa nae karibu. Sasa nilitaka kujua kama mchumba wake nae kafariki na nini Kinachoendelea kuhusiana na hilo tukio. Nilijua namna ya kumuuliza kijanja bila hata yeye kujua, nilizungusha namba za simu ya kazini kwake na ikiapokelewa.
"Hallo nani mwenzangu?" Ilisikika sauti upande wa pili.
"Samahani ndugu naomba kuongea na Mtuli." Nilisema bila kujitambulisha.
"Subiri." Ilisema sauti na kunyamaza. Baada ya sekunde kadhaa ilisikika sauti ya kike ikisema; "Mtuli hapa, nani mwenzangu?"
"Lyampili" nilimjibu kwa mkato.
"Habari za toka jana?" Aliuliza
"Safi tu, sijui unaweza kuwa na nafasi tuonane?" Nilimpiga swali la chenga kwani hakujua naongea toka Ukerewe.
"Tunaweza kuonana Lyampili, ila Kuna kitu kinanitatiza nataka kukifatilia kwanza. Kuna taarifa ya saa saba imeongelea mauaji na huenda mchumba wangu akawa miongoni mwa watu waliouawa. Hivyo nataka kuhakikisha kwanza, kwa hiyo samahani labda nipigie simu kesho hata kama itakuwa ni kweli nitamuachia mtu wa mapokezi ujumbe wa kukupa." Aliongea Mtuli kwa sauti ya pozi na tuo kama mtu asiyejali.
Baada ya maongezi ya hapa na pale tuliagana na kukata simu, yeye aliendelea kujua niko palepale Mwanza.

Nilikaa chumbani kwangu huku nikitafakari maisha yanavyokwenda, ghafla nilipata wazo na kuwaita watoto wa kaka waliokuwa uani. Niliwambia usiku inabidi wakalale kule makwao pamoja na kuwa haikuwa kawaida yangu kuwaambia. Niliamua kuwaambia kutokana na akili yangu ilivyonituma, niliendelea kupumzika mpaka ilipotimia saa kumi na moja. Nilitoka kwenda kuwasalimia ndugu na jamaa huku nikiwaacha watoto wa kaka wakiandaa chakula cha jioni. Nilipotoka katika matembezi yangu ya jioni nilikuta chakula tayari, tukala wote na baada ya chakula ilikuwa imetumia kwenye saa mbili usiku. Niliondoka na wale watoto wa kaka mpaka kwao, niliwaacha pale kwao ambapo ni Boma road na kuteremka chini alafu nikakata kushoto na kwenda kupata kinywaji kidogo katika bar iitwayo Bondeni Bar. Ilikuwa saa tano na kitu nilipojisikia tosha na kwenda kulala.

Nilishtuka toka usingizini huku jasho likimtoka kutokana na ndoto mbaya niliyokuwa naota, Nilipostuka nilihisi halufu ya petrol puani mwangu. Hapo machale yalinicheza na kuchukua hisia za tahadhari kwani sikuwa na chombo kinachotumia petrol nyumbani kwangu. Nilitoka kitandani taratibu na kuanza kunyata kuelekea mlango wa kutokea chumbani. Kabla sijaufikia nilisimia mchakacho wa kitu nikasita na kutega sikio vizuri. Nyumba yote ilikuwa giza Mimi nilitumia udhoefu kwani mtu kwake. Wakati nasikilizia nilisikia nyayo zinazotembea kwa mbali nikajua Ipo kazi huenda Patrick na wenzake wapo hapa. Niliendelea kwa tahadhari mpaka mlangoni. Niliweka sikio kwenye tundu la funguo lakini sikusikia chochote pale sebuleni.mlango wa chumba changu ulikuwa unaelekea sebuleni. Nilitoka pale mlangoni na kunyata mpaka sehemu ya dirishani, nilipofika pale dirishani harufu ya petrol ikasikika kwa nguvu puani mwangu. Nikajua kuna hatari ya kuchomwa moto hapa, nikapiga hesabu za haraka haraka na kuamua kwenda kufungua mlango, nilirudi mlangoni na kutembeza funguo taratibu kwenye kitasa, nilifanikiwa bila kelele yoyote hapo nilianza kuuvuta polepole wakati huo nikiwa nimelala chini pembeni ya mlango huku bastola mkononi mmoja na mkono mwingine ukifungua mlango. Mlango ulibaki wazi Mimi nikasotea tumbo kidogo na kuchungulia sebuleni, pamoja na kuwa ilikuwa giza lakini mimi pale ni kwangu hivyo najua mpangilio wa pale, niliona kivuli kisicho cha kawaida kwenye dirisha la pale sebuleni. Niliendelea kutembelea tumbo na kuwa sebuleni nyuma kochi nikatulia, kile kivuli kilichokuwa sehemu ya dirisha kikawa kimetoweka nikajua kuna mtu kwa nje, nilijisogeza kwa tumbo mpaka nyuma ya kochi jingine lililokuwa na dirisha la siri kwa chini. Nyumba hii niliijenga kwa kuweka tahadhari ya kuvamiwa kama hivi.

Nilifungua lile dirisha kwa tahadhari, lilipofunguka tu nikakutana na harufu Kali ya petrol, nilitoa kichwa kwa makini na kuchungulia nje. Sikuamini macho yangu, nilishikwa na butwaa kwani niliona moto ukisafiri kwa kasi kuelekea kwenye mlango wa nyuma ya nyumba. Kutahamaki naona mlipuko mkubwa sana, nilifungua lile dirisha haraka kwani tayari moto ulishatanda sehemu zote kuzunguka nyumba huku paa likianza kuungua. Moshi ulinikereketa nikajihisi kufa, palepale nilifungua dirisha na kuamua kujitosa kwenye moto huko nje nikaonane na kifo mbele kwa mbele kuliko kufa kibwege nikiwa ndani. Nilijirusha kupitia pale dirishani kwa kasi ya ajabu na kuangukia upande wa nje hatua kama saba kutoka usawa wa ukuta wa nyumba. Nilipotua chini nikasikia mlipuko mkubwa alafu nikasikia maumivu makali kifuani na hapo fahamu zikanitoka.

Nilipokuja kuzunguka nilijikuta niko kwenye hospital ya wilaya ya Ukerewe. Niliangaza macho na kumuona muuguzi aliyekuwa karibu yangu huku amekaa kwenye kiti. Aliniona nilivyozinduka akanisogelea na kuniinamia alafu akaniuliza; "Vipi unajisikiaje?"
"Ninajisikiaje? Au nashangaa nimefikaje hapa?" Nililopoka kwa hasira nadhani kichwa changu hakikuwa sawa.
" Sikiliza kaka, usishangae, wewe umepatwa na ajali ya moto usiku, bahati nzuri watu wakawahi kukuokoa wakati umezimia ndio wakakuleta hapa." Alisema yule muuguzi huku nilimuangalia kwa makini.
"Je baada ya hapo hakuna kilichotokea tena?" Nilimuuliza huku nikimkazia macho. Nilishamtambua nae alinitambua kutokana na kuwa tunaishia mtaa mmoja. "Walikuja hapa polisi baada ya kuwa umefikishwa hapa na wamekupiga picha na kusema Kuna tukio kama hili limetokea Mwanza hivyo walitaka picha yako ikatambuliwe na mama mmoja ayewajua wahusika wa tukio." Alisema yule muuguzi. Hapo kengele ya hatari ililia akilini mwangu.
"Je baada ya hapo hawajarudi tena?" Nilimuuliza tena yule muuguzi.
Walisema watarudi saa nne baada ya meli kutoka kwanza kuwa imewasili, nimesikia wakimuambia daktari asikuruhusu mpaka awasiliane nao kwanza.' alimaliza kueleza.

Moja kwa moja niliona jinsi askari wasivyotumia weledi yaani unamtilia mtu wasiwasi alafu humuwekei ulinzi hata wa kisiri. Hapo nilifikiri kwa haraka na kuona mahali nilipo pananuka mauti au kifungo. Nilihisi mwanamke anayedaiwa kuwajua wahusika atakuwa mkewe Mzee Magesa ambaye anafikiri ni sisi hivyo sura yangu akiiona ataitambua. Niliiangalia saa yangu ambayo kwa kawaida huwa na lala nimeivaa nayo ilinionyesha saa tatu asubuhi. Kitu cha kwanza nilichowaza ilikuwa ni kulipa kisasi kwa Patrick na wenzie kwanza kabla sijakamatwa na polisi. Hapo nilipata wazo la kutoroka pale hospital na kutafuta usafiri utakaonipeleka Mwanza kwa siri ili nikalipe kisasi changu kwa Patrick. Wakati nikiwa kwenye mawazo hayo ndugu zangu watatu wakawa wameingia wodini na kuanza kunisemesha; "Vipi unaendeleaje?" Aliuliza mmoja wao.
"Ndio namaliza kuzinduka sasa hivi ila sihisi maumivu zaidi ya sehemu hizi za kifua zilizofungwa bandage." Nilieleza.
"Unajua hiyo inatokana na kipande cha bati la moto kilichokuangukia kifuani wakati nyumba ilipolipuka." Alieleza ndugu yangu mmoja alafu mwingine akaingilia na kusema; "Kaka, tumeacha polisi wanakagua mabaki ya nyumba yako lakini walionekana kushika kitu walichodai ni bastola nadhani wanaweza kuwa njiani kuja kukuhoji." Alisema. Wakati huo uliongeza mapigo na kusahau maumivu niliyonayo kifuani na kujihisi mzima, nisingeweza kukaa pale kusubiri pingu za polisi kabla ya kulipa kisasi kwa Patrick.

"Hayo ni mawazo yao, watakuja nitawaelimisha." Nilijibu hoja ile kana kwamba sina wasiwasi. "Naomba unionyeshe sehemu ya kujisaidia" nilimuambia muuguzi. Wakati huo akili ilishaanza kufanya kazi kwa haraka, hiyo Ilikuwa ni mbinu, aikujali kuwaacha ndugu zangu pale maana ilikuwa ni kwa usalama wangu.
Wakati nanyanyuka kitandani na kuanza kumfuata muuguzi aliyekuwa mbele yangu tayari kuniongoza njia mara mlango wa wodi ulifunguka wakaingia askari wanne, wawili wakiwa kiraia na wawili wakiwa na gwanda. Kati ya wenye gwanda mmoja alikuwa na nyota mbili wakati mwingine alikuwa na v na ameshikilia bunduki ana pingu, nikajua sasa kazi maana serikali Iko mbele yangu. Niliwatupia macho kama sina habari nao, mmoja wao alikuwa akichezea funguo za gari. Nilianza kuvuta hatua kumfuata yule muuguzi, "Simama hapo ulipo" nilipewa amri baada ya kuwa nimewakaribia huku yule muuguzi akiwa ameishawavuka. Nilisimama na yule muuguzi akawa amesimama kwa nyuma yao huku wale ndugu zangu wakiwa wamesimama kwenye kitanda nilichokuwepo.
"Unakwenda wapi?" Niliulizwa swali wakati huo nikiangalia kwa dirishani na kuona Land Rover ya polisi ikiwa imeegesha nje huku hakuna mtu ndani yake, nikajua dereva ndie yule mwenye funguo.
"Naenda kujisaidia." Nilijibu huku nikifikiria kitu cha kufanya. "Hatuna Imani na wewe hivyo inabidi uwe chini ya ulinzi." Alisema yule askari mwenye nyota mbili. "Weka pingu huyo" alimalizia usemi wake kwa kumuamuru yule askari mwenye V aliyekuwa na bunduki pamoja na pingu. Nilijifanya mnyonge na kupeleka mikono yangu mbele nikiwa tayari kuwekwa pingu. Yule askari alifanya kosa kuiacha bunduki ikininginia begani huku mikono yake akiileta kwangu kunifunga pingu. Kama umeme niliruka na kumshika juu ya kichwa na chini ya kidevu huku miguu miwili nikiisambaza kwa wale waliovaa kiraia na kuwapata barabara sehemu za vichwa wakaanguka chini. Yule askari aliyetaka kuniweka pingu alianguka chini akiwa kazimia kwa mshituko wa shingo. Kutahamaki yule mwenye nyota mbili alipokea teke la shingo huku nikiinama kumtoa bunduki yule mwenye V aliyezimia. Wote walikuwa chini, wanashtuka kujipapasa ili watoe bastola zao wanakuta mie Pheady nimesimama huku nikiwa na bunduki nzito mikononi. Wote waligwaya na kuanza kusotea matako kurudi nyuma, kitendo hicho hakikuchukua zaidi ya sekunde therathini kiasi kwamba wote waliokuwa mle wodini walikuwa bado na butwaa.
"Weka hapo funguo alafu usogee nyuma hatua tatu" nilimwambia yule aliyekuwa ameshika funguo za gari. Alifanya kama nilivyosema, nilizisogelea zile funguo na kuziokota kwa tahadhari. Niliwaamuru walale kifudifudi huku nikingiza risasi chemba tayari kwa shambulizi. Nikarudi nyuma kinyumenyume na kutoka mlangoni, nilipotoka tu nikakimbia na kuwahi walipoegesha gari lao. Nilifungua mlango huku bunduki ikiwa tayari kwa lolote mkononi. Niliingia ndani ya gari na kuwasha likaitika, wakati naweka gia ndipo wale askari wakajitokeza na kuanza kurusha risasi lakini walikuwa wamechelewa. Nichomoa magazine kwenye bunduki na kutupa nje bunduki na magazine yake huku gari likipata moto. Nilikata kona kutoka barabara inayotoka hospital na kuelekea kulia katika barabara iendayo Ilangara na kuacha barabara iendayo Nansio mjini. Pamoja na kufungwa bandage sehemu zilizoungua na moto lakini sikusikia maumivu makali kivile. Akili zilishasafiri hazikuwazia maumivu bali zilikuwa na uchungu wa maisha yaani uhai na uhuru sio maumivu ya sehemu ya mwili tu. Nikifikiria kulipa kisasi kwa watu walionifanyia unyama nyumbani kwangu kabla ya sijawekwa chini ya ulinzi wa polisi. Nilijua sitaweza kuishi iwapo wao wako hai maana daima watakuwa mwiba kwangu hata kama sheria itaniacha huru wao watautafuta uhai wangu. Hivyo nilitaka niwahi kuwatoa roho kabla sijaanza kusakwa na polisi kwa udi na uvumba. Nilisema moyoni mwangu kuwa wataipata habari yangu na hata kama ni kuniua watabaku na kumbukumbu kali vichwani mwao.

Gari lilikuwa linaenda kwa kasi sana, mie nilijisahau kwenye mawazo huku nikizidi kukanyaga mafuta, nilikuja kushituka kwenye mawazo na kurudisha akili barabarani wakati napanda mlima wa kijiji cha Mahande kutoka Kijiji cha Namagondo, sikujua huko nyuma nimepitaje, nilipumua pumzi ndefu na kupunguza mwendo alafu nikapachika gia namba tatu. Nilijua kwa hali ya jiografia ya Ukerewe wale askari wasingewahi kuja kunifukuzia. Nilipiga mahesabu ya muelekeo wangu kwa wakati huo na kuamua kwenda kuiacha ile gari katika kijiji cha Igala kuna kipori kidogo nitaiingiza kwenye kichaka na kuitelekeza hapo, alafu nikatishe kwa mguu au nikodi baiskeli inipeleke Kijiji cha Bukondo kilicho kando ya ziwa ambacho hakipo mbali na hapo Igala.

Huko Bukondo kulikuwa na rafiki yangu ambaye kwao ni huko, tulisoma naye, yeye akiwa anatokea familia ya wawindaji. Hivyo Wakati wa likizo nilikuwa napenda kumtembelea na kujifunza mbinu za uwindaji kwa kutumia mishale. Baadae nilikuwa mjuzi kama yeye, tulipendana sana kipindi cha masomo yetu, tulikuja kuachana baada ya masomo na kuingia kwenye pilika pilika za maisha. Tukaja kuonana tena tumeishakuwa watu wazima, yeye kwa wakati huo alikuwa akifanya biashara ya magendo kwa kutoa au kupeleka bidhaa Kenya au Uganda kwa kutumia mitumbwi ya injini. Uhusiano wetu ulikuwa mzuri mpaka sasa na alijua shughuri zangu kwa undani.

Ilikuwa saa saba nilipofika kwa huyo rafiki yangu, iyo ilikuwa baada ya kufanya kama akili yangu ilivyonituma. Niliwakuta wakiwa kwenye chakula cha mchana, walinikaribisha kwa furaha sana hasa rafiki yangu na mkewe ambao ndio walikuwa wakinifahamu haswa. Walinikaribisha kwenye chakula nami nikajumuika nao kama zilivyo mila na desturi zetu. Baada ya chakula rafiki yangu alinichukua kutoka pale na kwenda kwenye chumba kimoja kilichokuwa pembeni ya nyumba ambacho alikitumia kama sebule yake kwa watu maalumu. Nilishangaa kidogo nilipoingia ndani ya sebule ile, kwani kulikuwa na vitu cha kitamaduni tupu(asili) kuanzia viti na Mapambo mpaka na ngozi za wanyama aliowahi kuwaua. Viti vilitengenezwa kwa ngozi ya kiboko. Ukutani kulitundikwa pinde za kila aina kuanzia ndogo mpaka zile kubwa vilevile mshale ilikuwa aina mbalimbali. Visu vidogo kwa vikubwa vilivyotengenezwa kwa aina tofautitofauti navyo vilining'inia ukutani huku vikiwa kwenye ala zake. Kweli palipendeza kwa macho.
"Vipi? Karibu uketi" alisema baada ya kuona nimesimama huku nikiangaza macho.
"Asante rafiki yangu, lakini hapa umeniacha hoi." Nilisema alafu wote tukacheka. Nilisogea kwenye kiti nikakata, yeye hakujua tatizo nililokuwa nalo, baada ya kuona silaha zile nilishafikiria kupata silaha pale pamoja na usafiri wa kunipeleka Mwanza haraka na kwa siri. Baada ya kuwa tumekaa na kutaniana kidogo kuhusiana na maisha yetu ya zamani ndipo nilikata mzizi wa fitina kwa kumueleza kinaga ubaga matatizo yangu na kuniomba anipatie vijana na mtumbwi wa injini wanivushe usiku kwenda Mwanza alafu aniruhusu nichague siraha nitakazo pale ndani. Alikuwa akinisikiliza kwa makini wakati namuelezea na baada ya kumaliza maelezo yangu alikaa kimya kwa sekunde kadhaa huku kainama chini, aliponyanyua kichwa na kunitazama nilimiona macho yamembadilika na kuwa mekundu.
"Sikiliza Pheady, kila kitu uatakacho kilicho ndani ya uwezo wangu utapata na kukuvusha nitakuvusha mimi mwenyewe. Ila kitu kimoja, wewe afya yako sio nzuri maana umeumizwa na moto hivyo huwezi kuwakabili hao watu peke yako. Alafu mimi sina siraha ya moto zilizopo ni za kiasili tu kama unavyoziona. Alimaliza kuongea huku akinyanyua uso na kutazama kutani mwa chumba kulikotanda siraha za asili.
Nilimuambia kuhusu afya yangu asijali maana ni mbabuko wa ngozi ya juu tu ya kifua wala haizuii misuli kufanya kazi, kwani mpaka sasa sijisikii maumivu zaidi ya kusikia mbano wa bandage, vilevile silaha zilizomo humo zingenifaa bila tatizo sikuwa na haja ya kuwa na bunduki mie ni mpiganaji hivyo chochote kwangu ni siraha muhimu ni umahili wa kuitumia. Nilimaliza usemi wangu wakati rafiki yangu akionyesha tabasamu la simanzi.
"Sawa, tusubiri usiku nitakupeleka" alisema yule rafiki yangu.

Ilikuwa saa nne za usiku wakati nilipokuwa tayari kwa kuanza safari ya Mwanza, tulikuwa watu watatu kwenye ile safari, rafiki yangu alikuwa na kijana wake aliyeshika usukani wa injini. Ile ingine ilikuwa na uwezo wa kutumia saa mbili kufika Mwanza. Nilibeba siraha nilizoweza kuzitumia na kuziweka kwenye mtumbwi. Baada ya safari kama ya masaa mawili tulifika Mwanza, injini ilielekezwa kandokando ya milima ya Kigoto alafu ikazimwa. Tukaanza kuambaaambaa kandokando ya ziwa kwa kutumia kasia huku nikiangalia kwa makini nchi kavu.
 
👍👍
 
Hii umeweka kwa ajili yangu??

Safi Sana..

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Nimecomment kabla ya kuisoma.
 
Haahaa umenifurahisha kaa mkao wa kula mpaka chakula kiishe
 
Naash nash ama kweli mvumilivu hula mbivu pamoja saana kiongozi
 
Back
Top Bottom