Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

SEHEMU YA 36


Vuai alikaa katikati na roara kwa mara alikuwa akijibenua huku na huku kwa nafasi ndogo ya hapo mbele iliyosababishwa na unene wa yule dereva. Wote walikaa kimya, ukisikika mlio wa gari tu.

Mara Marijani alikivunja kile kimya na kuanza kuzungumza na Vuai. “Huko tunakokwenda tunakuita ‘Dambwe’. Tunakuita hivyo kwa sababu ni pahala pa siri, hendi mtu ila aliyehusika tu, yaani, kama wewe. Unajua Vuai, serikali hii haitaki kutuona sisi wakulima tuldfanya jambo lo lote la kutunufaisha sisi. Wao wanataka daima tuwe watumwa wa mabwana shamba tu. Pindi wakibaini kwamba tunapo pahala ambapo tunaweza kujipatia maisha basi watafanya kila njia ili watuharibie. Ukifika huko utakutana na wenzako ambao watakuelekeza la kufanya. Watakuonyesha eneo la kuweza kuishi wewe na watakusaidia kujenga banda lako la kujisetiri.”

Vuai alinyamaza kimya ak’fikiri hayo maisha mapya anayokwenda kuishi huko Dambwe.

“Unajua,” Vuai alisema kwa ghafla kama mtu aliyekumbuka kitu alichokisahau.” zana zangu zote nimeziacha kule kwa Fuad, n’na jembe langu zuri na miundu miwili yote nimeinunua hivi karibuni, n’na koade nzuri ya muhogo na nilikuwa karibu nivune viazi vyangu. Vyote hivyo hakuniruhusu niondoke navyo.

“Sikiliza Vuai, hayo yote huna haja ya kufikiri. Hao utakaowakuta huko tunakokwenda yamewafika kama hayo au zaidi yake,” Marijani alimwambia Vuai.

Yule dereva alikuwa hasemi cho chote ameshughulika na usukani wa gari. Mara moja moja tu alikuwa akiguna wakati gia inapofanya matata kuingia.

“Lakini unajua Vuai, ijapokuwa utakuwa unaishi mbali na wale wenzako lazima ufanye kila njia uwe unakutana nao. Lazima, japo iwe kwa mwezi mara moja. uende Koani na uonane na wale ndugu zako. Fuad hataweza kukufanya cho chote hata akikuona huko,” Marijani aliongezea.

Walifuata barabara itokayo mjini kuelekea kaskazini ya kisiwa cha Unguja kwa muda mrefu na baadaye waliacha barabara kubwa na kufuata njia ndogo na baada ya mwendo wa kiasi cha nusu saa walifika huko Dambwe. Kwa muda hawakumwona mtu ye yote, labda kwa sababu kila mmoja alikuwa kondeni kwake. Jua lilikuwa limekwisha kutua na si desturi ya wakulima kukaa kondeni mpaka saa kama zile. Palikuwa na vibanda vidogo vidogo vya udongo vilivyoezekwa makuti na havikuwa pamoja. Vilitawanyika kimoja huku na kimoja kule. Konde za mpunga zilizostawi zilionekana kwa mbali na sehemu nyingine zilikuwa zimelimwa mazao mbali mbali.

Gari liliposimama Marijani alitoka nje akamwacha Vuai na yule dereva ndani ya gari. Baada ya kuingia kichakani na kupotea humo kwa muda mfupi alirejea amefuatana na mtu, mrefu, mwembamba, aliyejifunga shuka chafu. Tumbo lake lilikuwa wazi na miguu haikuwa na viatu. Alikuwa amcchomeka kisu kikubwa kiunoni kikiwa ndani ya ala iliyotengenezwa kwa bango la mpopoo. Marijani na yule mtu aliyefuatana naye walisimama mbali kidogo na lilipokuwa lile gari na baada ya mazungumzo mafupi Marijani alirejea peke yake.
 
SEHEMU YA 37


“Sasa Vuai sisi tutakuacha hapa na tutarejea mjini. Unamwona yule kijana niliyekuwa nikizungumza naye. Nenda pale na yeye atatengeneza kila kitu,” Marijani alimwambia Vuai huku akimfungulia mlango wa gari ili apate kutoka.

“Basi kwa heri, tutaonana na tutazungumza zaidi”.

Marijani aliingia ndam ya gari na hapo hapo gari liligeuzwa na kuanza safari ya kurejea mjini.

Vuai alifuatana na mwenyeji wake wakapita njia za ndani kwa ndani vichakani. Mara walitokea pahala paliposafishwa vizuri ambapo palikuwa na kibanda kama vile alivyoviona akiwa garini. Karibu na kibanda hicho palikuwa na mwembe mdogo na walipofika chini ya mwembe huo yule mwenyeji wa Vuai alimwomba mgeni wake amsubiri hapo. Aliingia ndani ya kibanda hicho na mara alitoka na mkeka akautandika na kumkaribisha Vuai akae.

Vuai alipokuwa amekaa chini ya mwembe zilimjia fikra mbali mbali nyingi. Alijiona hajui alipo wala hawaoni hao watu alioambiwa atawakuta pale. Hakujua maisha yangekuwaje pale lakini hata hivyo alikuwa na matumaini mazuri. Kwa vyo vyote yasingekuwa kama yalivyokuwa kwa Fuad.

Kiza kilikuwa kimeingia na bado mwenyeji wake hakutokea. Hata hivyo. hilo halikumtia wasiwasi. Alixuwa ana hakika kuwa atakuja tu bila ya shaka yo yote. Mara alisikia parakacha parakacha na mwenyeji wake alijitokeza kutoka kichakani na kuja pale alipokuwa.

“Umenisubiri muda mrefu enh?”

“Hapana kitu ndugu, mimi nahisi niko nyumbani tu,” Vuai alijibu.

Mwenyeji wa Vuai aliingia ndani ya kile kibanda chake akatoka na taa ya kibatari mkononi. Aliiweka pembeni na kuja kukaa juu ya mkeka pamoja na Vuai.

“Unaitwaje mwonzangu?” aliuliza yule mtu.

“Mimi naitwa Vuai; na wewe je?”

“Mimi naitwa Kondo.” Palikuwa na kimya kidogo na mara Kondo akaanza mazungumzo.

“Basi karibu ndugu. Hapa ndipo tunapoishi na maisha yanakwenda kama kawaida. Usione kimya hapa, tupo wengi na pole pole utawajua wote. Wewe rafiki yangu ni mwanamapinduzi?” aliuliza Kondo.

Vuai hakuwahi kusikia kitu kama hicho na mara aliuliza, “Mwanamapinduzi wa kitu gani?”

“Ala, kwani yule kijana uliyekuja naye hakukueleza” Kondo aliuliza.

“Amenieleza mengi lakini hayo ya mapinduzi hakunieleza,” Vuai alijibu.

“Ikiwa yeye hakukueleza basi mimi nitakueleza,” Kondo alisema huku akincha mikono yake. “Sisi tuliopo hapa sote m wakulima tuliotukuzwa mashambani na mabwana shamba wenye kumiliki ardhi. Kabla ya kutufukuza walitutesa na kutuletea unyonge mkubwa na hivi sasa tupo hapa soto tumejikusanya pamoja, tunaishi kama ndugu, na azma yetu hasa ni kuipindua serikali ya kimwinyi ili tuwe na serikali itakayoleta maslahi na mabadiliko katika maisha ya wakulima na masikini wote katika nchi. Kuhusu jambo hili sisi tunaoishi bapa tumejitolea kufa na kupona; je, unasemaje Vuai?”

“Unafikiri jambo hilo linayumkinika?” aliuliza Vuai.

“Kwa nini lisiyumkinike; linayumkinika sana tena wala...”

Kabla hakumaliza mara mazungumzo yao yalikatwa na sauti ya kike iliyoita kutoka kule kibandani kwa Kondo:

“Bwana! Tayari.”

“Ala! Tayari siyo? Lete basi!” alisema Kondo.

Hapo tena alitoka mwanamke aliyejifunga shuka ya kaniki kifuani akiwa amebeba sinia iliyoonyesha nzito kwa vile alivyoichukua. Aliiweka ile sinia juu ya mkeka waliokalia Vuai na Kondo na ndani ya sinia hiyo mlikuwamo sahani ya ugali wa muhogo na bakuli la mchuzi wa nazi.

“Tuletee maji ya kunawa mikono basi!” aliamuru Kondo.

“Ntaleta.”

Yule bibi alirejea kule alikotoka. Kondo akamwambia Vuai, “Yule ni mama watoto wangu.”

Mara alitoka na sufuria ya maji na kumpa Kondo na wote wawili wakakosha mikono yao na kula. Kwa hakika Vuai alikuwa na njaa sana na alikula bila ya kutaka kuzungumza tena.
 
SEHEMU YA 38


Walipomaliza kula walibaki pale pale juu ya mkeka wakaendelea na mazungumzo waliyoyakatiza.

“Basi ndio hivyo ndugu; Lazima tupindue na kama hatukufanya hivyo basi tutaendelea kuteswa maisha yetu. Sisi sote tuliopo hapa ni wapinduzi na tuna mipango kamili iliyo madhubuti, si kama tutajifanyia mambo kijiendawazimu.”

“Mimi nimefukuzwa kutoka shambani kwa Fuad na huko nimewaacha wenzangu wengi na wote hawana uhakika wa maisha yao ya siku za mbele,” alisema Vuai.

“Najua, kwani hapa haletwi mtu isipokuwa amekwishafukuzwa shambani kwa bwana shamba. Tena waliokuwa hawana hakika ya maisha yao ya siku za mbele siyo hao waliokuweko huko ulikotoka wewe tu; wakulima wote nchini hawana hakika ya maisha yao ya siku za mbele na kwa sababu hii ndiyo tukaamua kupindua,” alisema Kondo.

“Mimi niko pamoja na nyinyi, kufa au kupona,” Vuai alisema.

“Barabara! Lete mkono ndugu,” alisema Kondo huku akiwa amefurahi kupata mwana mapinduzi mwenzao.

Usiku ule Vuai alikuwa mgeni wa Kondo. Alitengenezewa nafasi kibandani mwake na ilipatikana nafasi ndogo ya kuweza kujinyesha na saa zilipokuwa nyingi waliingia ndani na kulala.

Kama alivyoahidiwa, Vuai alisaidiwa kujenga banda lake la kuishi. Siku zilivyoendelea ndivyo alivyozoea maisha yake mapya. Alipata wenyeji. akajuana na jamaa wengine wanaoishi huko Dambwe. Alifahamishwa mipango zaidi kuhusu mapinduzi na mara kwa mara aliwaona wajumbe kutoka mjini wakija na miongoni mwao akiwa Marijani. Ycye alikuwa akija kutoa nasaha na kufahamisha yaliyokubaliwa na wakuu wa wakombozi wa wananchi.

Kama alivyonasihiwa na Marijani Vuai hakuwatupa wale wenzake huko Koani. Kila alipopata nafasi aliwatembelea na kuwajulisha wale aliowaamini mipango ya mapinduzi na jinsi ilivyokuwa ikiendelea.

Nchi ilikuwa imeharibika. Serikali ya kisultani ilizidi kuwakandamiza wafanyakazi na wakulima. Kila wakombozi wa wananchi walipofanya mikutano yao basi mikutano hiyo ilimalizika kwa wananchi kupigwa marungu na askari wa serikali ya Sultani, Magari yote yaliyotoka sehemu zote za mashamba kuja mjini ilibidi yapekuliwe katika vituo maalum vya polisi kabla hayajafika mjini.

Lakini wapi! Kila serikali ya Sultani ilivyozidi kukandamiza wakulima na wafanyakazi ndivyo nao walivyojiandaa na kutayarisha mipango ya kuipindua.

Huko Dambwe, akina Kondo walikuwa wakijiandaa kwa kukusanya kila silaha waliyoweza kipata. Hawakupata silaha za kisasa lakini bado waliamini kwamba kufanikiwa au kutofanikiwa kulitegemea watu zaidi kuliko silaha. Silaha walizokusanya zilikuwa ni mapanga, mashoka na zana nyinginezo wanazotumia wakulima katika kazi zao za kila siku.

ILIPITA miezi miwili hivi. Hata usiku romoja kama saa tano Vuai aliyekuwa amelala kibandani kwake alizindushwa na mlio wa gari kwa mbali. Kwa namna alivyousikia mlio ule alikuwa na hakika kwamba gari lile lilisimama; tena kwa muda mrefu. Hakulala tena. Baada ya saa mbili hivi alilisikia gari lile likitia moto tena na kuondoka. Alikuwa na hamu kubwa ya kutaka kujua ilikuwa m gari la nani. Kuja kule usiku ule ni jambo lisilokuwa la kawaida.

Alfajiri watu wote waliamka na wakati ulipofika kila mtu aliteremkia kondeni kwake. Kumbe wageni waliokuja na gari jana usiku walimjia Kondo. Walikuja kumpa habari muhimu kuhusu matayarisho ya mapinduzi na ilimbidi ampitie kila mmoja kondeni kwake na kumwarifu jun ya ‘ngoma’ kesho yake usiku nyumbani kwake. ‘Ngoma’ m msemo wao kwa siku kama hiyo wanapoarifiana juu ya mambo muhimu.

Usiku ulipofika wote walikusanyika chini ya ule mwembe mdogo mbele ya nyumba ya Kondo katika kiza.
 
SEHEMU YA 39

“Salamu zenu nyingi kutoka Kijangwani,” Kondo alianza kusema, “Wanasema, wakati umekaribia na siku haiko mbali. Mamao yote madhubuti na maboma yote mawili tutayakamata siku moja. Tutaanzia kwa silaha hizi hizi tulizonazo na tutamalizia kwa silaha tutakazonyakua toka kwao.”

Wote walimsikiliza Kondo kwa makini; hapana aliyesema kitu.

“Itakapofika siku yenyewe hasa, tutapata taarifa mapema ili tuweze kujitayarisha. Mimi sina zaidi. Nafikiri haina haja ya kukaa hapa kwa muda mrefu. Lakini, Vuai, n’na salamu zako kutoka kwa Marijani. Anasema ufanye kila njia ufike Koani ukawaarifu wale unaokutana nao na anasema hala hala usiache kwenda. Wenzetu wa sehemu nyinginezo pia watapelekewa habari kama tulivyoletewa sisi na siku ya siku itakapowadia sote tutakuwa pamoja.”

Kondo alimaliza hotuba yake na wote wakatawanyika kila mmoja akaenda kibandani kwake.

Vuai alielewa vizuri umuhimu wa jukumu alilopewa. Kwake yeye haikuwa shida kubwa kufanya safari ya kwenda Koani. Hakulazimika tena kungoja Fuad aende mjini kuuza karafuu kama alivyofanya alipokuwa akimfanyia kazi. Huku aliko aliweza kwenda atakako bila ya kuingiliwa na mtu ye yote. Kwa hiyo, siku ya pili asubuhi alianza safari ya kwenda Koani.

Alipanda gari ya kwanza ilotokea Mchangani na aliona bora kwanza apitie Kijangwani kuonana na Marijani kabla ya kuendelea pale na safari yake.

Alipofika pale hakukuta ghasia kama zile alizozoea kuzikuta kila alipokwenda. Palikuwa pamepooza kidogo ila kila baada ya muda aliingia mtu mmoja halafu akatoka hapo hapo kama kwamba alisahau kitu halafu akarudi kukichukua baada ya kukumbuka na kisha akaenda zake.

Vuai aliingia ndani ya ofisi ya Kijangwani akaufungua mlango wa ofisi ya Marijani kwa utaratibu bila ya kugonga. Alipochungulia alimkuta Marijani amekaa juu ya kiti, mikono yake miwili ameisimamisha juu ya meza na amekilaza kichwa chake katika viganja vya mikono yake. Alionekana kama mtu aliyetaka mapumziko mafupi baada ya kufanya kazi iliyomchokesha sana.

Mlio wa mlango uliokuwa ukifunguliwa taratibu ulimzindua na alipoinua kichwa alimwona Vuai amesimama mlangoni.

“Umeshakwenda Koani?” Marijani alimuuliza Vuai bila ya hata kumsalimu kama kawaida yake.

Marijani alikuwa amebadilika na hakutaka mzaha hata kidogo. Nguo zake zilikuwa zimechafuka na kidevu chake kilichozoea kunyolewa kila siku kilikuwa na ndevu changa za kiasi ya siku sita nivi.

“Nimeona bora nije kuonana na wewe kabla sijaenda huko Koani,” Vuai alijibu.

“Kwani Kondo hakukueleza kila kitu?” Marijani aliuliza tena akionekana kama hakupendezekewa na hatua aliyoichukua Vuai. “Lakini si vibaya,” Marijani aliukunjua uso wake kidogo na kuanza kuzungumza na Vuai kama kawaida yake ya siku zote. “Sasa wewe nenda Koani, wale ndugu unaoonana nao kila siku wambie kama alivyokwambia Kondo. Jambo moja tu zaidi, waulize kama washakusanya silaba. Tena fanya haraka mana’ake katika mipango yote tukikosea pamoja tu basi ujue tumeharibikiwa. Mambo yote lazima yafanyike kama yalivyopangwa. Sasa bora uende bila ya kupoteza wakati.”

Vuai alitoka. Alipofika Mikunguni tu alipata gari lililoendea Koani.
 
SEHEMU YA 40


Alipofika ilikuwa taabu kumpata mtu ye yote katika wenzake. Wote walikuwa wamo katika kumtumikia Fuad. Alijaribu kila rai akijichunga sana asionekane na Fuad akatia shaka fulani.

Vuai alikuwa mwenyeji shambani kwa Fuad kutokana na miaka mingi ya utumishi wake shambani mle. Alikijua kila kichaka. Alikwenda kila sehemu aliyojua angemwona mmoja wa wafanyakazi lakini hakufanikiwa. Alipokuwa amekwisha kata tamaa, na kidogo aketi chini apumzike kabla ya kuendelea zaidi, alimwona Mkongwe akitoka kisimani.

“Hebu ningojc nikuulize!” Vuai alimwambia.

Mkongwe alisituka, akinkiri Fuad anataka kumfanyia unyama wake. Lakini sauti iliyomwita haikufanana na yake. Alipogeuka kwa ghafla alimwona Vuai.

“He, Vuai masikini! Ulikuwa wapi?” Mkongwe aliuliza. Aliutua mtungi wa maji aliokuwa nao kichwani na kwenda kule aliko Vuai. “Ulikuwa wapi sikn zote hizi?” Mkongwe alimwuliza tena Vuai huku akimwonea huruma kubwa. Alimkaribia na kutaka kumkumbatia kwani hakufikiria kama angemwona tena.

“Samahani ndugu, huu si wakati wakuulizana maswala mengi. N’na haraka sana na tafadhali fanya kila njia uniitie Umari, na mwambie n’na haja naye muhimu sana. Mwambie namngojea hapo kibandani pake atanikuta ndani.”

Bila ya kutaka kuzungumza zaidi na Mkongwe, Vuai alikwenda zake.

Mkongwe alipigwa na mshangao kidogo lakini pale pale alijitwisha mtungi wake wa maji na alipokwisha kuutua mtungi ule alitoka akaenda kumtafuta Umari.

Alipomkuta tu, Mkongwe hakutaka kuzungumza naye kitu cho chote bali alimsogelea na kumnong’oneza, ‘Vuai anakwita; utamkuta kwako ndani,” huku akiangaza huku na huku asije Fuad akatokea na kuwakuta nale wanazungumza.

“Kaja? Lo!”

Umari ambaye alikuwa akipalilia migomba aliliweka jembe lake chini na bila ya kupoteza wakati alikimbilia kwake. Alipofika aliukuta mlango umesindikwa kidogo na Vuai amekaa juu ya kitanda cha mayowe kilichokuwa mle ndani.

“Je. kumezidi nini?” Umari aliuliza.

“Kwanza silaha mshakusanya.”

“Tayari lakini si nyingi; mambo unayajua tena.”

“Basi mambo yanakaribia. Jitayarisheni kwa wakati wo wote ule ingawa siku ikifika atakuja mtu kukwambieni mapema. Wape habari jamaa wote; siwezi kukaa tena. Kwa heri. Nisalimie wote.”

Pale pale Vuai alitoka na kuanza safari yake ya kurejea Dambwe. AIipitia Kijangwani kutaka kuonana na Marijani amwarifu yote lakini hakumkuta. Alirejea Dambwe na alipofika huko ilikuwa jioni.
 
SEHEMU YA 41


Mapinduzi yalikuwa yananukia. Huko mjini watu walikuwa hawazungumzi kitu tena - wakitazamana tu wanafahamiana. Huko Dambwe wote walikuwa wanajiandaa; wakingojea ujumbe tu kutoka mjini.

Ulipita mwezi mzima hakuwapitia mtu ye yote kutoka mjini lakini hata hivyo wakati wote walikuwa katika hali ya kuwa tayari.

Baada ya mwezi kupita, Idasi ya saa saba mcbana siku moja, liliingia gari kubwa la mizigo. Gari hili halikupata kuja pale na Vuai ambaye alikuwa karibu alikwenda kuona ni wageni gani waliokuja nalo. Gari lenyewe lilikuwa la serikali la kupakilia mizigo. Lilikuwa na rangi ya kijani na nyuma li wazi. Vuai alipokaribia alimwona Marijani akishuka kutoka mle garini na akionyesha kuwa ana haraka.

“Imekuwa kheri umetokeza! Yuko wapi Kondo?” Marijani aliuliza.

“Kondeni kwake.”

“Twende!”

Walifuatana mguu kwa mguu mpaka kondeni kwa Kondo na walimkuta anapiga matuta.

“Leo nimekuja kwa kazi muhimu sana,” Marijani alianza kusema. “Mambo tayari na silaha zote zinatakiwa ziwe zishafika mjini leo.”

“Leo?” Kondo aliuliza.

“Ndiyo leo. Tena sasa hivi kazileteni maana gari nimekuja nalo. Njiani askari wameshaanza kisiran’ chao na magari yote yanayotoka shambani yanapekuliwa. Sisi tumejitolea na askari yo yote atakayetusimamisha hatutasimama Kama mmoja atatufanyia matata basi tutamponda; haidhuru na liwe litakalokuwa.”

“Silaha ziko tayari twendeni tukazichukue,” alisema Kondo.

Wote watatu walifuatana na kwenda msituni mpaka sehemu moja palipokuwa pamewekwa lundo la makuti ya minazi.

“Ondoeni hayb makuti,” Kondo aliamuru.

Vuai na Marijani waliondoa makuti. Chini yake palikuwa na shimo kubwa na ndani yake mlikuwa na mapanga, visu, miundu na silaha nyinginezo. Walizichukua kidogo kidogo na kuzipeleka garini mpaka zikamalizika.

Baada ya kumaliza kufanya kazi hiyo, wote watatu walisimama pembeni mwa lile gari. Vuai alimtazama yule dereva akamtambua kuwa ni yule yule aliyomleta pale Dambwe kwa lile gari dogo bovu mara ile ya kwanza baada ya kutoka kwa Fuad

“Sasa sikilizeni vizuri mipango ya kesho; mana’ke kesho ndiyo siku ya siku,” Marijani alisema. “Kesho patapigwa magoma ya kienyeji hapo Kisiwandui na wakulima na wafanyakazi wote wanatakiwa wafike kwenye magoma hayo. Madhumuni yenyewe siyo kupiga magoma, ni kuweza kuwapata wanamapinduzi wote kutoka sehemu mbali mbali za mashamba na kuja mjini. Ndiyo sababu tumeona bora tupigishe magoma ili watakapokuwa wakija mjini magoma yawe ndiyo kis’ngizio. Baada ya magoma hayo kwisha. wote wale wanaohusika wataarifiwa ni wapi watazikuta silaha zao. Usiku huo huo tutaanza mapinduzi kwa kulichukua boma la askari wa serikali ya kisultani hapo Mtoni. Mipango yote kuhusu jinsi boma hilo litakavyochukuliwa imekwisha tayarishwa na mtaambiwa huko huko mjini.” Marijani aliendelea na maelezo yake
 
SEHEMU YA 42


“Tumefahamu sawa sawa na tutawaarifu wenzetu wote,” Kondo alisema.

“Basi sasa kwa herini na tunatumai m’shajiandaa na kwamba nyote mtafika hapo Kisiwandui kesho usiku. Angalia msifuatane nyote pamoja, au sivyo, maaskari pale Mwera watawatilia shaka. Njooni mmoja mmoja au wawili wawili.” Marijani aliwatahadharisha.

Marijani alikuwa ametulia na hakuwa na wasi wasi hata kidogo. Uso wake ulidhihirisha imani yake kuwa mapinduzi yatafanikiwa.

“Basi kwa herini tutaonana kesho. Kondo utapofika Kisiwandui usiwe na haja ya kuonana na mtu yo yote pale. Kila kikundi kina mtu wa kukifahamisha mipango yote na mimi ndive nitakayekuwa na dhamana ya kukifahamisha mipango yote kikundi cha huku Dambwe.” Marijani alimgeukia Vuai na kumwambia, “Wewe utawatafuta wale jamaa wa Koani uwapashe habari za mipango yote. Wamekwishapashwa habari za ngoma na iliyobaki ni kuwajulisha wale wanaohusika kazi zao ngoma ilakapoiva.”

Baada ya kumaliza hapo, Marijani aliingia ndani ya lile gari na hapo hapo lilitiwa moto na kuondoka mbio.

Kwa bahati hawakusimamishwa pale Mwera. Walipita bila ya taabu yo yote. Gari lao likiwa limesheheni mapanga na mashoka. Walikwenda moja kwa moja mpaka Wengiwape na wakazitia silaha zote ndani ya kijumba kidogo.

Kila kitu kilikuwa lazima kifanywe bila ya kuacha alama yo yote ambayo ingemfanya mtu kutia shaka. Kwa hiyo, pale Wengiwape palipoteremshiwa silaha palikuwa na watu maalum ambao walipewa kazi ya kuzifagia alama za mipira ya ile motokaa kutoka pale nyumbani mpaka kufika barabarani. Kazi hiyo ilifanywa mara moja baada ya lile gari kuondoka.

Siku ile ilikuwa ya kujiandaa kwa kila mwanamapinduzi po pote pale alipo. Huko mjini cheti cha ngoma kilikuwa kimeshakatwa na banda kubwa lishajengwa. Kila mtu alikuwa anajiandaa kuja ngomani, tena ngomani kweli. Siku ile ilikuwa siku ya wakulima na wafanyakazi, siku walipoamua kuleta mabadiliko katika maisha yao kwa kuondoa dhuluma ya kame.

Tokea asubuhi wakulima kutoka sehemu mbali mbali za mashamba walianza kuteremkia mjini wengine kwa magari wengine kwa miguu. Wengine walikuwa wanakuja ngomani kweli; wanamapinduzi tu ndio waliojua vizuri mwisho wa ngoma ile.

Si wanamapinduzi wote waliotakiwa wafike hapo ngomani na kwa hivyo baadhi ya wanamapinduzi walipata amri ya kukaa katika nyumba maalum mpaka utakapofika wakati.

Usiku huo asiyekuwa na mwana alibeba jiwe. Mamia ya wakulima walifika magomani, waliokuwamo na wasiokuwamo. Waliokuwamo walijua vizuri nini kilichowapeleka mjini na wasiokuwamo walikwenda ngomani.

Kisiwandui ilikuwa inang’ara siku hiyo kwa mataa ya umeme. Hewa ya hapo ilichafuka kwa vumbi lililokuwa likitimuliwa na wacheza ngoma. Lilikuwapo ‘gombesugu’, yalikuwapo ‘maumbwa, ‘gonga’ na ngoma nyingine za kienyeji. Mchanganyiko wa ngoma namna mbali mbali ziliizokuwa zikipigwa hapo ulisababisha kelele kubwa. Watu walistarehe kwa ngoma mpaka saa sita ya usiku.

Baada ya kuvunjika ngoma, taratibu watu walianza kupungua ngomani pale. Akina mama walikuwa wanakimbilia majumbani kupika daku. Waliwacha nyuma yao nuru ya mataa ya umeme iliyokuwapo ngomani pale na kujitosa ndani ya kiza cha vichochoro vya ng’ambo kwa safari za mitaani kwao kulikojaa vijumba vya udongo vilivyosongamana kwa kujengwa bila ya mpango. Misitu na vichaka vilivyokuwapo katika sehemu hiyo waliyokuwa wakiishi wafanya kazi wa Unguja, makaburi yaliyotapakaa katika takriban kila pembe ya sehemu hiyo pamoja na imani ya hadithi mbali mbali za kubuni juu ya mashetani, wanga na wachawi walizokuwa nazo watu - hayo yote yaliwafanya wakimbilie makwao mbio usiku ule kwa khofu wasiyokuwa na hakika nayo.
 
SEHEMU YA 43


Ulikuwa usiku wa kuamkia Januari 12, na watu walikuwa wamo katika kumi la mwanzo la mwazi wa Ramadbani. Wanamapinduzi wote walikuwa wanaelewa vizuri dhamana waliyokuwa nayo siku ile. Kutoka ngomani kila mmoja wao alishika njia yake, kuelekea kwenye mkutano ‘Wengiwape’.

Chonjo alikuwa wa mwanzo kufika penye kijumba kilichofichiwa silaha. Alimkuta Pongwe amejibanza pembeni ya kijumba kile tumbo wazi kama mtu aliyekuwa akivizia kitu na panga lake mkononi. Alipomwona tu Chonjo, Pongwe aligutuka na kuuliza kwa sauti ya ukali, “Nani wewe?”

“Mimi”

“Wewe nani? Huna jina?”

“Mimi Chonjo”

Pongwe alimjongelea Chonjo taratibu na alipofika karibu naye alimwuliza kwa sauti ya chini. “Wengine wako wapi?”

“Watakuja sasa hivi. Nenda kanitafutie panga zuri uniletee.”

“Nenda kachague mwenyewe.”

Kijumbani humo mlikuwa kiza totoro. Miembe na mizambarau mikubwa iliyokizunguka kijumba hicho ilikizidisha kiza hicho. Chonjo aliingia ndani, akajaribu kuyalazimisha macho yake apate kuona katika kiza kile lakini yalikataa katakata. Aliutia mkono ndani ya suruali yake ya khaki na kutoa kibiriti. Aliwasha kijiti cha kwanza lakini mara kilizimika kwa upepo uliopepea ghafla kutoka uani.

“Ala, wewe namna gani bwana! Usiwashe kibiriti; hapatakiwi mwangaza hapa!” kwa sauti ya hamaki Pongwe alimwambia Chonjo. “Ingia hicbo chumba cha mkono wa kushoto vita vyote vimo humo.”

Chonjo alipapasapapasa mpaka akaugusa mlango wa chumba alichoelekezwa. Alisukuma ule mlango akaingia chumbani humo na kunyemelea kidogo kidogo. Bila ya kutumainia alikwaa chungu ya silaha zilizokusanywa humo. Alipotaka kuinama na kuchagua silaha aliyopenda katika kiza kile alimsikia Pongwe akizungumza na mtu mwingine. Chonjo aliinuka na kutaka kusikiliza ni mtu gani yule lakini mara alimsikia mtu yule akiingia ndani. Mara moja alijua kuwa yule alikuwa mwanamapinduzi mweazake. Aliinama tena na kuanza kuchagua silaha. Yule mtu naye aliingia chumbani mle na aliposikia parakacha parakacha aliuliza, “Je nani mwenzangu?”

“Mimi Chonjo. Je, wewe nani?”

“Mimi Marijani. Upesi chagua silaha; wengine wanakuja sasa hivi. Na tutapotimia tutakwenda zetu; wakati ushakuwa mkubwa.”

Kila mtu alichukua panga ambalo alilihisi zuri na kutoka nje.

Wanamapinduzi waliendelea kuja mmoja mmoja. Kila aliyefika alichukua silaha aliyoipata, mwenye panga, mwenye rungu, mwenye shoka na wote baadaye walijikusanya mbele ya kijumba kile. Pongwe aliingia ndani na kuvaa shati. Na baada ya wote kutimia Marijani alianza kutoa amri.

“Ndugu, saa ya kitendo imefika. Sasa sote tunaelekea Mtoni, kufa na kupona - lakini mambo yote tuyabadili leo. Haya, safari ndugu.”

Ilikuwa kiza totoro. Hali ya hewa ilikuwa shwari na miti imetulia tulii. Ari ya kimapinduzi ilikuwa imetawala ndani ya nyoyo za akina Shomari na wenzake.
 
SEHEMU YA 44


Walipita njia za porini kwa hadhari. Hapana aliyekuwa akizungumza na mwenzake mpaka walipolikaribia boma. Walipofika hapo Shomari alitoa shauri, “Sasa sote tulaleni chini. Tutatambaa mpaka tuzifikie seng’enge. Kundi moja litabujumu kutokea mlango wa mbele wa boma na kundi jingine litahujumu kwa upande wa pili.

Bomani kulikuwa kimya. Askari wa jeshi la Sultani walikuwa wamelala. Mataa makali ya umeme yalimulika kila pembe bomani hapo. Mlangoni mbele ya boma palikuwa na askari mmoja aliyekuwa akishika zamu. Alikuwa akiranda huku na huku na bunduki yake mkononi.

Wanamapinduzi walitambaa mpaka wakazifikia seng’enge na walipofika hapo walitulia tulii wakingojea amri ya kushambulia.

Kikundi kimoja kilinyemelea kwa kutambaa maguguni mpaka wakafika karibu na alipo yule mlinzi. Alisituka kidogo aliposikia parakacha parakacha lakini pale pale alilia komba na hapo wasiwasi ulimtoka na kufikiri parakacha parakacha ile ilikuwa ni yule komba aliyckuwa akichupia minazi. Lakini hakwenda hata hatua mbili alijishtukia amevamiwa na kutiwa kabari na kabla hajawahi kupiga kelele alishindiliwa kisu eha shingo na kuanguka chini kimya. Alikufa hapo hapo.

Hapo tena ulisikika ukelele Wa Marijani - “Tayari ndugu!”

Waliingia ndani ya boma kama umeme. Baada ya muda mchache walilikamata boma na kufungua chumba cha silaha. Askari wa serikali ya kisultani hawakuwa na moyo wa kupigana. Baada ya kuona kishindo tu walitimka na kukimbia.

Baada ya masaa machache tu boma la Ziwani nalo pia lilitekwa. Na baada ya hapo, hatua kwa hatua, wanamapinduzi walianza kuvikamata vituo muhimu na klkundi kimoja kikaelekea kwenye kituo cha radio.

Kiza kilikuwa kimeutawala usiku wa siku ile na vivuli vya miembe mikubwa mikubwa iliyoizunguka Raha Leo nzima vilizidisha kiza kile kukawa kweusi tititi.

Mbele ya jumba kubwa la manjano lililozungukwa kila pembe na vibanda vya udongo vilivyoezekwa makuti, koplo Paulo na askari mwenzake walikuwa wamezama katika soga lililowaza kuvunja machofu ya ulinzi wa usiku kucha wa kituo cha radio kilichokuwemo ndani ya jumba hilo.

“Basi nikamfata toka Kidongochekundu mpaka Miembeni,” Koplo Paulo aliendelea na soga lake.

“Enhe!”

“Kila nikimwuliza hali hanijibu, kila nikimwuliza hali hanijibu, Shoti ananukia kama jini.”

“Enhe!”

Halafu nikajiuliza mwenyewe moyoni. mwanamke huyu anaringa nini hasa?”

“Enhe!”

“Nilivyomwona hanijibu nikaona bora nimkaribie zaidi na nilipofika karibu yake nikamshika mkono.”

“Enhe!”

“Nilipomgusa tu alinigutua mkono wangu. E, mwanamke anaringa yule, lakini mwa...... “Mara koplo Paulo aliyakata mazungumzo na kurejesha kiti alichokua amekalia nyuma. Alionyesha amestuka sana na bila ya kusema chochote au kumwambia mwenzake lolote alikupuka mbio.

Yule mwenzake Koplo Paulo alibabaika na alipogeuka nyuma aliona kundi la watu linamkaribia. Alianza kujiuliza na kujijibu, “Nikimbie? Ah, hata nikikimbia sitofika popote. Nipigane nao? Ah, hata nikipigana nao wataniua bure. Bora nijisalimishe.”

“Nani wewe?” iliuliza sauti moja kutoka katika kundi lile kwa ukali.

“Mimi askari!”

“Unafanya nini hapa?”
 
SEHEMU YA 45


“Nipo kazini!”

“Aa, msipoteze wakati bwana! Mchinjeni tu!” ilisema sauti nyingine kwa hamaki zaidi kuliko ile sauti ya kwanza.

“Ngojeni, msimwue bure, ngojeni kwanza,” alisema mwingine kwa sauti ya kuamrisha.

Yule askari alikwisha fadhaika haelewi kinachotokea Alihisi amekabiliwa oa mauti na alikata tamaa kabisa kwani kundi lililomzunguka lilikuwa m kundi la watu waliokasirika kila mmoja na silaha mkononi. Bahati yake nzuri kiza cha usiku ule kilificha mandhari ya kutisha ya watu wale ambao nguo zao zilijaa damu na nyuso zimezungukwa na manywele na madevu yasiyoshughulikiwa kwa muda wa siku nyingi sana.

“Wewe nani?” iliuliza sauti katika kundi.

“Mimi askari.”

Pale pale alitoka mtu katikati ya kundi lile na kumpiga kofi hata akaona vimurimuri badala ya shangwe lile lililomzunguka.

“Ebo, sisi tunakuuliza wewe nani tokea saa ile wewe umeshika askari, askari. jina lako nani?”

“Mcha, Mcha Hamadi.” alijibu mbio mbio huku bado maruirui ya kofi alilopigwa yanamtaabisha.

“Ah, Mcha, mwacheni, hawezi kufanya tabu, mlinzi mwenye funguo yuko wapi?”

“Yuko pale! Nyumba ile!” alijibu Mcha huku sauti inamtetemeka kwa hofu na wasiwasi, miguu inamtetemeka, nywele zimemsimama.

“Haji, nenda kachukue funguo halafu..wengine watakwenda kumlafuta fundi mitambo, nani anajua anakokaa?”

“Mimi nakujua! Twendeni nikupelekeni!” Mcha aliruka na kusema haraka haraka.

“Twende, sisi tutakuchukua kwa amani lakini ukijaribu kuleta shari njiani utakiona cha mtema kuni,” ilisema sauti moja kutoka katika kundi lile la watu waliokuwa tayari kufanya chochote kile, kizuri au kibaya.

Kundi lile lilijigawa sehemu mbili, kundi moja lilibaki Raha leo na kundi jingine likafuatana na yule askari na kukiandama kiza cha usiku ule. Mcha bila ya hata kujua njia aliyoipita alijishtukia ameshafika mbele ya nyumba ya fundi wa mitambo, “anakaa hapa, ngojeni nimgongee dirisha.”

“Ngoja kijana, usiwe na pupa, sisi tunamjua zaidi kuliko wewe,” ilisema sauti moja kwa utulivu.

Dirisha liligongwa, kabla ya aliegongewa dirisha hajafungua, dirisha la nyumba ya pili lilifunguliwa na ilisikika sauti ikiuliza, “Nani ana......”

Kabla hajamaliza kusema alilolitaka risasi ya ghafla iliyotoka katika bunduki mojawapo ya watu waliokuwemo kundini mle ilipiga pale pale ilipotokea ile sauti na sauti hiyo haikusikika tena.

“Mwamba!” iliita sauti moja.

“Hallo!” alijibu Mwamba aliyeonyesha yu macho.

“Tayari!”

“Tayari sio? Nakuja.”

Mwamba alifungua mlango wa nyumba kwa haraka na kutoka nje. Vunge la fungilo lilikuwa mfukoni mwake na kutoka hapo walifululiza moja kwa moja mpaka kwenye kituo cha radio.

Zogo lilizidi na makundi ya watu yalianza kumiminika Raha Leo kila mmoja silaha mkononi. Mwamba alipousogelea mlango wa kituo cha radio macho ya watu wote waliokuwa na hasira za siku nyingi yalimwangalia yeye. Mwamba alilifungua lango kubwa lililochongwa kwa nakshi nzuri na bila ya kujali chochote alifululiza moja kwa moja mitamboni. Watu watatu walokuwa na bunduki za aina ya ‘Mark 4’ walimfuata nyuma yake.
ITAENDELEA
 
ITAENDELEA KESHO.....

Kula kibao cha Oliver Mtukudzi - Todii.... 2002 hiyo
 
SEHEMU YA 46

Ijapokuwa alfajiri ilikuwa ishaanza kubisha hodi, kiza kilichochanganyika na mwanga mdogo kilimlazimisha Mwamba kuwasha taa na baada ya kufanya hivyo alianza kuchokora mitambo iliyokuwemo ndani ya chumba cha matangazo. Mara alibinya kifungo kile, akabinya swichi hii. Mara alichomoa waya na kuupachika pengine halafu aliingia na mmoja wa wale watu mpaka kwenye chumba cha kusemea na kumweka juu ya kiti, “Sasa sema,” alimwambia.

“Ndugu wananchi, serikali ya Ki-Sultani tushaipindua, tunawaomba wananchi wawe watulivu. Tunawataka askari wote wa Sultani wajisalimishe na wote wale wenye silaha wazisalimishe silaha zao kwa wanamapinduzl.”

Baada ya tangazo hilo matangazo kem kem yalifuatia. Ilipofika asubuhi mapinduzi yaliendelea.

Hiyo ilikuwa kweli ni siku ya siku. Wanamapinduzi waliranda katika kila pembe ya kisiwa cha Unguja wengine kwa miguu wengine kwa magari waliyoyateka. Waliuranda mji wa Unguja kila mmoja bunduki mkononi, kwani sasa haikuwa mapanga ‘na mashoka tena. Walipigana kila walipolazimu kupigana na vikosi vya serikali ya Ki-Sultani na vibaraka wao.

Mapigano makali yalitokea hapo penye kituo cha polisi cha Malindi. Wanamapinduzi walipigana kishujaa kabisa na askari wa serikali ya Ki-SuItani, ambao walikuwa na kinga nzuri ya kujificha. Wakati wa mapigano ndani ya kituo hicho waliweza kuwaona wanamapinduzi waliokuwa wametawanyika katika uwanja uliokuwa wazi kabisa mbele ya kituo hicho. Wengi katika wanamapinduzi waliteketezwa hapo. Lakini bila ya kujali kifo, wanamapinduzi hao walisonga mbele, na baada ya mapigano ya muda mrefu, walikiteka kituo hicho.

Kwa Sultani mambo yalikuwa ya moto. Yeye na watu wake kwa mara ya kwanza iliwabidi waende mbio huku majoho na makanzu yakiwazonga miguuni. Walikimbia huku wakipita wakianguka. Bahati yao waliwahi kutoroka katika meli iliyokuwa bandarini, wao na baadhi ya wafuasi wao.

Mjmi na mashamba mambo yote yalimalizika wakati wa magharibi. Radio ya Mapinduzi ilitangaza kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar iliyoongozwa na Chama cha Afro-Shirazi - wakombozi wa wananchi.

Serikali ya Ki-Sultani iliyowapa kila haki na uwezo mabwana shamba na mabepari ilipinduliwa, kwa mara ya kwanza katika historia ya visiwa vya Unguja na Pemba, ikaundwa serikali inayoongozwa na wakulima na wafanyakazi.

MWEZI mmoja baada ya kufaulu kwa mapinduzi serikali mpya ilitangaza kutaifishwa kwa ardhi yote na baada ya muda ilianza kugawiwa miongoni mwa wakulima. Wasiwasi uliochanganyika na chuki ulimjaa Fuad.

“Wallahi shamba langu hawalichukui!” Fuad alianza kusema peke yake.

Wakati wote Fuad alikuwa ameghadhibika. Lakini hivi sivyo alivyokuwa kama vile akimghadhibikia Mkongwe au mfanyakazi wa shambani mwake, la. Ghadhabu hii ilikuwa pia na woga mkubwa, na kwa hiyo, ilimkera sana moyoni.

Masikini Kijakazi hakujua nini kimetokea nchini ila kuwa wakati wote Bwana Fuad alikuwa asnekasirika na mnyonge. Kijakazi alimwonea huruma sana na alitamani kumsaidia na kumtoa katika shida aliyokuwa nayo lakini ndiyo hakuwa na uwezo.

“Siku nyingi anatafuta mchumba; labda hajapata mchumba anayemtaka?” Kijakazi alijiambia kimoyomoyo.

Asubuhi moja kama saa mbili na nusu magari mawili yalisimama mbele ya mlango wa nyumba ya Fuad. Watu watatu kutoka katika kila gari walishuka wakapiga hodi na Fuad aliyekuwa amekaa ukumbini peke yake alitoka kuja kuwaona wageni hao.

“Tumekuja tunataka kuonana na wewe,” mmoja wao alisema.

“Mnataka kuonana na mimi. Tafadhali, karibuni; piteni ndani!” Fuad alijibu huku akijidai kujichekesha kicheko kil’chochanganyika na chuki.

Kijakazi aliyekuwa amesimama kwa mbali aliweza kuwaona watu hao wakiongea na Fuad lakini hakujua wakiongea kitu gani.

Fuad aliwakaribisha wote ukumbini na kuwataka wakae juu ya viti.
 
Back
Top Bottom