RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA.
______________
ILIPOISHIA...
______________
Mida ya saa tano asubuhi, ndio sajenti Minja
alikurupuka, akaangalia simu yake, akukuta
missed call 12 za mkubwa wake wa polisi,
akawaamsha wakina Kayoza, kisha wakaenda
kujiswafi, wakatengeneza chai wakanywa.
Sajenti Minja akawarudisha wakina Kayoza kwa
mama Kayoza, kisha yeye akawa anaelekea
kituoni,
alipofika, akapaki gari lake kisha akawa anaenda
katika ofisi ya mkubwa wake, katika kolido ya
ofisi akapishana na askari watatu waliokuwa
wamemfunga pingu mzee mmoja ambae sura
yake haikuwa ngeni kwake yeye Sajenti Minja, ikabidi
ageuke amwangalie tena, na yule mzee nae
akageuka kumuangalia sajenti Minja, ndipo
sajenti Minja akamkumbuka, ni yule mzee mochwari na hapo pia ndipo yule mzee monchari akamkumbuka kuwa yule wanaepishana nae ndiye aliyemuuzia maiti na kumsababishia madhira Yale, Babu wa Monchwari akasimama huku akiwa bado amemgeuzia shingo Sajenti Minja ....
_____________
ENDELEA....
_____________
...yule babu wa mochwari akasimama, "vipi we mzee, songa mbele" askari mmoja akaongea kwa hasira.
"taratibu wanangu, nimemuona mtu kama aliekuja kununua ile maiti" yule babu akaongea kwa matumaini huku shingo yake akiitoa kwa Sajenti Minja na kuwageukia wale maaskari,
"yuko wapi?" askari mwenye hasira akauliza.
Yule babu akageukia ile sehemu aliyokuwepo sajenti Minja ili awaoneshe maaskari,
"kha!," yule babu akajikuta anashtuka kwa mshangao baada ya kutomuona tens Sajenti Minja,
"vipi babu?, tuoneshe haraka, unatuchelewesha" yule askari mwenye hasira akauliza huku amemtolea macho babu,
"alikuwepo pale" yule babu akasema huku akionesha lile eneo alilokuwepo Sajenti Minja.
"kwa hiyo hayupo?", yule askari mwenye hasira akahoji.
"alikuwepo pale", Babu akajitetea.
"hujanijibu bado, kwa hiyo hayupo" yule askari aliuliza tena huku akiwa na shauku ya kufanya kitu.
"ndio mwanangu" Babu akajibu kwa upole.
Bila kutegemea, babu alipigwa mtama mmoja mkali sana, akaangukia makalio.
"unatuchelewesha majumbani kwetu, hatujalala na wake zetu tokea juzi usiku" askari mwenye hasira aliongea huku akimnyanyua babu babu baada ya kumpiga mtama.
Sajenti Minja akacheka tu baada ya kushuhudia ule mtama aliopigwa babu kisha akaishia kujiuliza ni kwanini babu amekamatwa, akajiona mkosaji kwa kukimbia kwa maana yeye angeweza kuwa msaada wa babu, pia akaona alichokifanya kinaweza kubwa sahihi zaidi kwa kuwa huenda Babu atakuwa amekamatwa kutokana na kesi ile ya kuiba maiti, yaani inawezekana kabisa ndugu wa marehemu wamegundua kuwa wameibiwa, na mwisho akajisemea itabidi achunguze ni kitu kilichofanya mpaka yule babu awe katika mikono ya polisi.
"Vipi mbona una mawazo hivyo?" Askari mmoja aliyekuwa anatoka msalani alimuuliza Sajenti Minja aliyekuwa amezama katika bahari ya tafakuri,
"Ah, si unajua tena mawazo ni kawaida kwa binadamu" Sajenti Minja alijibu baada kushtuka kutoka katika lindi la mawazo,
"Wewe ni mgeni kituoni hapa? Maana sura yako sijawahi kuiona" Yule askari alimuuliza Sajenti Minja,
"Kabisa, inaelekea kila mtu anaefanya kazi hapa umemkariri?" Sajenti Minja aliuliza,
"Yaani wote, sisi ndio wakongwe wa hapa" Yule askari alijibu huku akitabasamu,
"Sawa bwana, mimi ndio nawasili muda huu kuja kuripoti kwa mara ya kwanza" Sajenti Minja aliongea huku nae akitabasamu,
"Bila shaka wewe ndiye Joel Minja?" Yule Askari aliuliza,
"Haswaa, umenijuaje?" Sajenti Minja aliuliza,
"Tuliambiwa Leo kuna ugeni wa askari mpelelezi kutoka Dodoma" Yule askari aliongea,
"Basi ndio huyo" Sajenti Minja aliongea,
"Umeshafika ofisini kwa mkuu?" Yule Askari aliuliza,
"Bado, yaani hapa ndo mahala pa kwanza kufika" sajenti Minja aliongea na wote wakacheka,
"Sasa ofisi ya mkuu unaijua?" Yule askari alimuuliza,
"Nitaijulia Wapi mimi?" Sajenti Minja alijibu,
"Sasa ungefikaje" Yule askari aliuliza,
"Ningefika tu, ila kwa kuwa nimekutana na wewe, mambo yatakuwa sawa" Sajenti Minja aliongea,
"Twende nikupeleke" Yule askari akaongea huku akitangulia mbele
Wakatoka katika eneo la chooni, akawa anaelekea katika ofisi ya mkubwa wake, walipofika yule askari aliyempeleka hakutaka kuingia, aliishia mlangoni na kuondoka zake na kumuacha Sajenti Minja mlangoni.
Sajenti Minja akapiga hodi kisha akaingia, aliporudishia mlango, akampa heshima yake mkuu wa polisi,
"kaa hapo sajenti" Mkuu wa polisi wa shinyanga alimuelekeza sajenti Minja sehemu ya kukaa.
sajenti Minja akasogeza kiti, kisha akakaa.
"habari yako Minja" Mkuu wa polisi akamsalimia.
"nzuri tu, shikamoo mkuu" sajenti Minja akajibu.
"Marhaba, Leo ndio siku ya kwanza kuwasili kituoni hapa" Mkuu wake alimuuliza huku akiwa jibu analo kabisa,
"Naam mkuu" Sajenti Minja alijibu kikakamavu,
"Vizuri sana, na kilichokuleta huku nadhani unakijua" Mkuu wake aliuliza tena,
"Ndio mkuu" Sajenti Minja alijibu,
"Tukupatie Askari wa huku ili msaidiane au wewe una pendekezo Gani?" Mkuu wake alimuuliza,
"Naimani peke yangu nina uwezo wa kufanikisha" Sajenti Minja alijibu,
"Kwanini hutaki msaada?" Mkuu wake aliendelea kumbana,
"Kwa sababu hata niliyofikia katika upelelezi wa hii kesi ni hatua nzuri, sasa ukinipa mtu wa kusaidiana nae itakuwa kama tunaanza upya kwa kuwa atakuja na mipango, mbinu na mawazo tofauti kuhusu hii hii kesi" Sajenti Minja alijibu,,
"Lakini kumbuka umoja ni nguvu" Mkuu wake aliongea huku akitabasamu,
" hilo nalijua mkuu, nitapohitaji msaada nitakwambia" Sajenti Minja aliongea,
"Kesi unayoifuatilia umeishia nayo wapi?" Mkuu wake aliuliza,
"Kwa kweli hata niliyopiga ni ndogo sana, bado nahitaji mwanga zaidi ili hata nijue wa kumtia hatiani" Sajenti Minja aliongea,
"Sawa, basi hapa nna habari ambazo zinaweza kukupa mwanga kidogo" Mkuu wake aliongea na kumfanya Sajenti Minja atege masikio vyema,
"Habari zipi hizo mkuu?" Sajenti Minja aliuliza,
"leo asubuhi wasamalia wema walitoa taharifa za kuwepo watu wanne ambayo walikuwa wana alama ya kung'atwa shingoni na kitu kama mnyama mwenye meno makali, tulipoenda tuliweza kukuta watatu waliokuwa wamenyonywa damu makaburini, ila habari nzuri mmoja wapo amekutwa yuko hai, lakini hali yake sio nzuri, ni wa leo au wakesho muda wowote anaweza kufa", Mkuu wa Polisi aliongea huku akiangalia baadhi ya makabrasha yaliyopo mezani kwake,
Sajenti Minja alivyosikia habari ya watu kukutwa wakiwa wamekufa kwa kunyonywa damu eneo la makaburini, moja kwa moja akajua kuwa ni yule mganga na wasaidizi wake, ila habari ya mmoja kuwa hai ndio hakuipenda,
"ndio, nakusikia mkuu" sajenti Minja akajibu baada ya ukimya wa muda mfupi,
"Sasa kwa fikra zangu za haraka haraka haya mauaji nayafananisha na yanayofanywa na mtu unaemtafuta kwa maana hata wale watu waliokutwa wamekufa katika geti la mchungaji walikuwa hivyo hivyo na hizo alama shingoni" Mkuu wake alitoa maelezo,
"Nadhani kwa kuwa huyu mmoja yupo hai basi anaweza kutusaidia tukapata mwanga kidogo" Sajenti Minja aliongea huku moyoni akiwaza hata huyo mtu afe,
"Sasa hivi yupo sehemu ya wagonjwa mahututi amepumzishwa, jioni tutaenda kuongea nae" Mkuu wake aliongea,
"Litakuwa jambo jema sana" Sajenti Minja aliongea,
"sasa ni hivi tutatoka mimi na wewe hadi katika ofisi za akari wengine ili nikutambulishe, alafu jioni ndio tutaenda hadi hospitali ili tuchukuwe maelezo ya huyo aliebakia, maana anaweza kutupa pa kuelekea" mkuu wa polisi alimalizia kuongea huku akisimama,
"sawa mkuu" sajenti Minja akajibu.
Walitoka nje ya ofisi ya mkuu na kisha muda huo sajenti Minja akaanza kutembezwa katika ofisi za askari wa ngazi mbalimbali ili atambulishwe kwa wenzake hao, na kisha pia alizungushwa katika mazingira yote ya eneo like la Polish kwa ajili ya kupata kuyaona ili hata akitoka nje ajue duka linapatikana wapi? vyoo vinapatikana wapi na mambo mengine yanayolizunguka eneo lile.
Baada ya Mkuu wake kuridhika aliamua na kumpeleka katika ofisi ambayo Sajenti Minja ataitumia muda wote ambao atakuwepo pale na kisha wakaagana huku wakikumbushiana kuwa jioni ni lazima waende hospitali kumuona huyo mtu aliyebakia ya wenzie kunyonywa damu, Sajenti Minja hakupenda kabisa hyo safari ila hakuwa na la kufanya, ilibidi atimize matakwa ya kazi yake.
************************
Jioni ilifika haraka sana kwa upande wa Sajenti Minja, alitamani hata isifike kabisa.
Mkubwa wake alimpitia na wakatoka eneo la kituoni.
Baada ya kutoka kituo cha polisi, sajenti Minja na mkuu wake wakafunga safari hadi hospitali, njia nzima sajenti Minja alikuwa anatetemeka, alijua fika kuwa anaenda kuumbuka mbele ya mkuu wake,
"vipi Minja, mbona unatetemeka sana?" mkuu wa polisi akauliza.
"leo nimeamka na homa, kwa hiyo sijisikii vema kabisa" sajenti Minja alidanganya.
"itakuwa malaria, tukifika itabidi upime kabisa" mkuu wa polisi alimshauri Sajenti Minja.
Gari ilipofika, sajenti Minja na Mkuu wa polisi wakatelemka kisha wakawa wanaelekea sehemu ilipo wodi za wagonjwa mahututi, walitumia dakika mbili mpaka kufika katika chumba ambacho alilazwa yule msaidizi wa Mganga ambae alikuwa amenusurika na kifo, ila chumba kilikuwa kitupu,
"Eh, mbona hayupo, ameshakufa nini?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akitoa macho kuangaza bila mafanikio. Kwa upande wa Sajenti Minja hiyo habari ilikuwa nzuri, alijikuta anatabasamu waziwazi mbele ya Mkuu wake,
"Mbona unacheka, unafurahia kumpoteza shahidi?" Mkuu wake alimuuliza kwa mshangao,
"Hapana mkuu, nacheka unavyopeleka imani yako katika kifo wakati hata hujaenda kuuliza kwanza kwa madaktari" Sajenti Minja alijitetea kwa njia ya uongo,
"Kweli bwana, ebu twende tukaulize" Mkuu wake aliongea huku akielekea upande zilizopo ofisi za madaktari na huku Sajenti Minja akiendelea kuomba wakifika waambiwe yule bwana amekufa.
Baada ya sekunde kadhaa walitokea sehemu zilipo ofisi za madaktari, ila kwa bahati nzuri hata kabla hawajaingia ndani, walikutana na Daktari ambae ndiye anayesimamia matibabu ya msaidizi wa Mganga,
"Ooohoo kamanda umeshawasili?" Daktari aliongea huku akimpa mkono Mkuu wa polisi,
"Vipi kuna wema kweli? mbona mgonjwa wetu hayupo kule katika wodi aliyokuwepo asubuhi?" Mkuu aliuliza huku akionesha wasiwasi,
"Wema upo, tens mkubwa sana" Daktari alijibu huku akicheka,
"Hapo kidogo umenipa nguvu, haya niambie huo wema" Mkuu aliongea huku akiwa bado yupo makini kumsikiliza Daktari,
"Mgonjwa wako amepata nafuu na hata kuongea anaongea" Daktari alitoa habari zilizokuwa nzuri kwa Mkuu wa polisi ila hizo hizo habari zilikuwa mbaya sana kwa Sajenti Minja,
"Mmempeleka wapi sasa?" Mkuu wa Polisi aliuliza,
" yuko katika wodu ileee" Daktari aliongea huku akiwaelekeza kwa kidole katika wodi ambayo amehamishiwa msaidizi wa Mganga.
Sajeni Minja na Mkuu wa Polisi baada ya kumshukuru Daktari wakawa wanaelekea kwenye wodi aliyokuwamo yule msaidizi wa mganga huku Sajenti Minja mapigo yake ya moyo yakiongezeka kasi.
wakaingia ndani ya wodi, kisha wakawa wanaelekea kwenye kitanda cha yule msaidizi wa mganga, hapo Sajenti Minja moyo ulikuwa unamkimbia ajabu, akatamani hata sura yake ibadilike au akatamani hata yule msaidizi wa Mganga awe amepoteza kumbukumbu zake, lakini haikuwa hivyo.
Walipofika katika kitanda cha yule msaidizi wa mganga, wakakuta kalala huku kawapa mgongo, yule mkuu wa polisi akamshika bega kwa lengo la kumuasha, yule msaidizi wa Mganga akageuza sura na macho yake yakagongana na macho ya Sajenti Minja........
******ITAENDELEA******
*je Msaidizi wa Mganga atalopoka na kumtaja sajenti Minja kama ni mtu mmoja wapo kati ya wale waliomsababishia matatizo?
the Legend☆