Riwaya: Kijijini kwa Bibi

Riwaya: Kijijini kwa Bibi

Kabinti kalokole kana taabu, kanamponza Ommy hivi hivi,Minja na yy hata simuelew elew
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE.

______________
ILIPOISHIA...
______________

Walipofika katika sehemu ambapo kulikuwa
kumetulia na kulikuwa na kapori kidogo, ni umbali
mdogo kutoka nyumbani kwav mganga
aliyewaagiza maiti, walisimamishwa na gari
ya polisi wa doria waliokuwa wanaimarisha ulinzi
kile kipindi cha usiku.

"mnaenda wapi?" askari mmoja akawauliza,

"nyumbani" Sajenti Minja akajibu huku wasiwasi
mwingi ukiwa umemtawala,

"huku juzi tulipishana na watu nao tulipowauliza
wakasema hivyo hivyo, kesho yake tukasikia
majambazi yamepavamia na kuiba mali za watu,
na nyie msije mkawa ni miongoni mwa hao
waarifu" Askari yule akamwambia sajent Minja
huku akiwa anawatilia mashaka,

"sisi hatuwezi kuwa majambazi, afande" Sajenti
Minja akajitetea

"hatuwezi kuwaamini, hadi tuwakague" yule
askari aliongea huku akimulika upande wa ndani
wa gari kwa kutumia tochi,

"Sisi ni watu safi" Sajenti Minja aliongea huku
ndani ya nafsi yake akiomba Askari wasikague
buti ya gari,

"Na huku kuna mini?" Askari mwingine aliongea
huku akifungua buti ya gari na kuwafanya wakina
Sajenti Minja waishiwe nguvu....

____________
ENDELEA....
____________

...."ebu toa lock ya buti" Askari yule akamuamrisha Sajenti Minja baada ya kufungua buti bila mafanikio.

Sajenti Minja akaona akifanya uzembe kidogo,
anaweza kuvuliwa nguo bila kutegemea, kwa
maana kwa Sajenti kama yeye kukutwa na maiti
ndani ya gari ni aibu kubwa.

"unajua unaongea nani?" sajenti Minja akamuuliza yule askari wa doria kistaharabu,

"haijalishi, kukujua wewe nani nadhani hakutasitisha kukukagua. fungua buti bwana" yule askari akaongea kwa ukali.

"Ngoja nikuoneshe kitambulisho changu" Sajenti Minja akatoa kitambulisho chake, akamtupia yule
askari,

"alafu inaonekana una jeuri sana kijana?, unamtupia nani likitambulisho lako?" yule afande
akawa anaongea huku akiwa anamfuata Sajenti Minja akiwa na gadhabu, alipomfikia, yule askari
akamtandika sajenti Minja kibao cha nguvu.

"haya okota likitambulisho lako na unipe mikononi, sio unirushie, umeona mi limbwa
eeh!?", yule askari wa doria akahoji kwa ukali mpaka mate yakamtoka,

Sajenti Minja akaona asilete mabishano wakati wanachelewesha kazi kwa mganga, akakubali kuwa mjinga, akakiendea
kile kitambulisho, akakiokota kisha akampatia yule askari wa doria.

Yule askari akakipokea,
akashtuka baada ya kukiangalia kwa nje, maana kilikuwa cha kipolisi, alipokifungua kwa ndani, akakisoma ndani, kisha
akammulika Sajenti Minja na tochi usoni, ghafla
akampigia saluti, wale askari aliokuwa ameongozana
nao, kuona hivyo, nao wakampigia saluti Sajenti Minja.

"samahani sana mkuu, mi sikujua kabisa" yule
askari wa doria aliongea huku sura yake
ikionesha kama anataka kulia kutokana na hofu aliyokuwa nayo,

"usijali, ndio kazi inatakiwa kufanywa hivyo" Sajenti Minja ndivyo alivyomjibu, kisha
akamuuliza, "bado unataka nifungue buti?"

"ha...hapa...hapana mkuu" yule askari wa doria akajibu kwa sauti iliyojaa kitetemeshi.

"Kwa hivyo mnaweza kuturuhusu twende?" Sajenti Minja aliwauliza,

"Nenda tu mkuu, samahani sana kwa usumbufu" Askari alijibu huku akimrudishia Sajenti Minja kitambulisho chake.

Sajenti Minja akakipokea kitambulisho chake na wakaingia ndani ya gari, kisha wakaendelea na safari yao.

"wajomba pale bila kutumia akili tulikuwa tunaumbuka" Sajenti Minja alianzisha maongezi baada ya kuondoka eneo walilosimamishwa,

"Mimi ndio nilikuwa nimekata tamaa kabisa" Omari nae akachangia,

"Mimi akili niliyokuwa nayo ilikuwa ni kutoka nduki tu" Kayoza aliongea na kufanya wenzake wacheke,

"bila ya kitambulisho, sasa hivi sijui tungekuwa
wapi?" Sajenti Minja akasema huku akiwa anaipaki gari nje ya nyumba ya mganga.

Wakashuka, kisha wakaenda hadi mlangoni kwa
mganga, wakabisha hodi, wakafunguliwa na
msaidizi wa mganga,

"sisi tulijua hamuwezi kuja tena, maana giza limekuwa kubwa sana" Msaidizi wa Mganga
aliwaambia baada ya kuwagundua,

"tulipata matatizo kidogo njiani, ila yameisha" Sajenti Minja aliongea huku akiwa anaingia ndani na nyuma yake wakina Kayoza wakimfuata.

"Sasa itabidi ifanyike ingawa tumechelewa kidogo" Mganga aliongea baada ya kuwaona,

"Itakuwa vyema sana" Sajenti Minja aliongea,

"Sasa huyo kijana mwenye tatizo inabidi asogee hapa tumfanyie mambo kidogo" Mganga aliongea huku akitandika kitambaa cheusi chini. Kayoza akasogea na kuambiwa Amalie kile kitambaa cheusi na mganga akaanza kufanya matambiko.

Baada mganga kumaliza matambiko madogo pale
nyumbani, wale wasaidizi wa mganga, walikuwa
wanne, wawili wakambeba yule maiti na wawili
wengine wakabeba vifaa vya uganga, hapo
ilikuwa saa sita na dakika zake za kutosha,
mganga akawa anaongoza msafara.

"Hizi sehemu zinatisha ila mnabidi mzizoee" Mganga aliwaambia wakina Sajenti Minja wakati wakiwa njiani,

"Hizi sehemu za kutisha nimeshazizoea sana, labda vijana wangu hapa ndio wageni" Sajenti Minja alijibu,

"Kwa hivyo mambo haya ya kutembea kwa waganga ushayazoea sana?" Mganga alimuuliza Sajenti Minja,

"Hapana, kwa masuala ya kiganga mi ndio mara yangu ya kwanza" Sajenti Minja alijibu,

"Sasa hata mazingira ya kutisha umeyazoeaje?" Mganga aliuliza,

"Kutokana na kazi zetu mzee wangu" Sajenti Minja alijibu,

"Kwani nyie mnafanya kazi gani?" Mganga aliwauliza,

"Hao vijana wangu wanasoma chuo, mimi ni muangaikaji tu wa sehemu mbalimbali katika kutafuta ridhiki" Sajenti Minja alijibu,

"Sasa kama huyu kijana mwenye matatizo yupo Chuo huko chuo anaishi vipi na chuo mzimu" Mganga alihoji,

"Matatizo matatizo tu na ndio maana tumemleta hapa" Sajenti Minja alijibu na ukimya ukatawala tena njiani.

Walitembea mda wa saa nzima hadi sehemu za makaburini.

" inabidi tuchague kaburi moja ambalo limetengenezwa vizuri na liwe la mwanamke" Mganga alitoa maelekezo na wale wasaidizi wake wakatawanyika kila mmoja na upande wake wakitafuta hilo kaburi zuri alilozikwa mwanamke.

"Naona hili hapa linafaa" Msaidizi mmoja wa mganga alipaza sauti na watu wote wakaelekea eneo alilopo.

Walipofika katika kaburi moja lililosakafikiwa
vizuri, Mganga alilidhika nalo baada ya kuona kila anachokihitaji kipo.

Mganga akawaamuru wasimame, kisha
akachukua kikapu cha uganga akatoa vifaa vyake
akavipanga kulizunguka lile kaburi,

"Were kijana njoo ulale hapa juu ya hili kaburi" Mganga alimwambia kayoza,

"Mi naogopa mzee" Kayoza aliongea huku akiwa na wasiwasi,

"We mpumbavu mini, ebu lala hapo kabla sijakuchapa makofi, we unafikiri utaponaje kama ukikahidi maneno ya mganga" Sajenti Minja aliongea kwa ukali, Kayoza akakubali kulala hivyo hivyo huku aakitetemeka.

Baada ya Kayoza kulala juu ya kaburi, mganga akammwagia madawa yake Kayoza kichwani, haikuchukua
hata dakika moja, Kayoza akapoteza fahamu na kulala kama maiti,

"Haya mchukueni huyo maiti na mumlaze pembeni ya huyo kijana" Mganga akawaamuru wasaidizi wake
wamchukue yule maiti na kumlaza pamoja na
kayoza, wasaidizi wakatekeleza agizo.

"Kazi ndiyo inaanza, sharti kubwa na la kuzingatia ni kwamba kazi itakapoanza haitatakiwa ionekane damu ya kitu chochote kile" Mganga aliongea,

"Hata ya mbu?" Sajenti Minja aliuliza kutokana na eneo like kuwa na mbu wengi,

"ndio, kama mbu atakung'ata hata usimuue, maana ukimuua ile damu yake inaweza kuwa tatizo kwetu" Mganga aliongea kwa msisitizo,

"Na ikionekana ni kipi kitachotokea?" Sajenti Minja aliuliza,

"Huu mzimu tunaoutoa hapa, nguvu zake zipo kwenye damu ya kila kiumbe, kwa hiyo damu itakapoonekana, mzimu atapata nguvu na kati yetu hapa hakuna atakayepona" Mganga alitoa Maelezo,

"Hilo litawezekana" Sajenti Minja alijibu,

"Na pia kama mtu ana kidonda ajitahidi akizibe kisionekane" Mganga alitilia mkazo,

"Basi kazi ifanyike tu, naona Maelezo yako yamejitosheleza" Sajenti Minja aliongea,

"Kwa hiyo hapa kazi inayofanyika ni kuutoa huu mzimu kutoka kwa kijana wenu na kuuingiza katika maiti alafu kazi itayofuata ni kuizika hivyo maiti pamoja na mzimu" Mganga alimaliza.

Mganga akaanza kazi yake, alimwaga madawa
eneo lote, kisha akaanza kuongea lugha
anayoijua yeye, alifanya kwa nusu saa, kisha
likatokea dubwana la ajabu kwenye mwili wa
Kayoza, kila mtu alipata uoga isipokuwa mganga tu.

Sasa like dubwana likawa kama linavutwa kutoka kutoka kwenye mwili wa Kayoza, ila likawa
halitaki,
hiyo hali ilienda kama saa nzima, mganga
akaanza kuona mafanikio, lile dubwana lilishatoa
mwili mzima ikawa bado miguu, na mwisho hadi miguu ilitoka na likaanza kudumbukia katika ile maiti.

Mara ghafla panya akatokea
kichakani, alikuwa kama anakimbizwa na kitu,
akawa anaelekea kwenye miguu ya Omary, katika
jitihada za kumkwepa, Omary akajikuta anamkanyaga yule Panya,
damu ikaenea katika viatu vya Omari, mganga
aliliona lile tukio,
akajikuta anasema kwa sauti iliyokata tamaa

"tumekwisha...".

Na wakati huo huo mzimu ukachomoka kutoka katika mwili wa maiti na huku ukifoka kwa hasira kiasi kwamba ndege na wadudu waliolala maeneo Yale ya makaburini waliamka na kukimbia hovyo..............

******ITAENDELEA*******

*Je mganga atafanikiwa kuutuliza mzimu uliokuwa na hasira ya kudhuriwa au mzimu ndio utawamaliza wote waliotaka kumdhuru?

the Legend☆
Omary nayeeeeeh!!!! Shunie njoo umchukue shostito wako huku....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA.

______________
ILIPOISHIA...
______________
Mida ya saa tano asubuhi, ndio sajenti Minja
alikurupuka, akaangalia simu yake, akukuta
missed call 12 za mkubwa wake wa polisi,
akawaamsha wakina Kayoza, kisha wakaenda
kujiswafi, wakatengeneza chai wakanywa.
Sajenti Minja akawarudisha wakina Kayoza kwa
mama Kayoza, kisha yeye akawa anaelekea
kituoni,
alipofika, akapaki gari lake kisha akawa anaenda
katika ofisi ya mkubwa wake, katika kolido ya
ofisi akapishana na askari watatu waliokuwa
wamemfunga pingu mzee mmoja ambae sura
yake haikuwa ngeni kwake yeye Sajenti Minja, ikabidi
ageuke amwangalie tena, na yule mzee nae
akageuka kumuangalia sajenti Minja, ndipo
sajenti Minja akamkumbuka, ni yule mzee mochwari na hapo pia ndipo yule mzee monchari akamkumbuka kuwa yule wanaepishana nae ndiye aliyemuuzia maiti na kumsababishia madhira Yale, Babu wa Monchwari akasimama huku akiwa bado amemgeuzia shingo Sajenti Minja ....
_____________
ENDELEA....
_____________

...yule babu wa mochwari akasimama, "vipi we mzee, songa mbele" askari mmoja akaongea kwa hasira.
"taratibu wanangu, nimemuona mtu kama aliekuja kununua ile maiti" yule babu akaongea kwa matumaini huku shingo yake akiitoa kwa Sajenti Minja na kuwageukia wale maaskari,

"yuko wapi?" askari mwenye hasira akauliza.
Yule babu akageukia ile sehemu aliyokuwepo sajenti Minja ili awaoneshe maaskari,

"kha!," yule babu akajikuta anashtuka kwa mshangao baada ya kutomuona tens Sajenti Minja,

"vipi babu?, tuoneshe haraka, unatuchelewesha" yule askari mwenye hasira akauliza huku amemtolea macho babu,
"alikuwepo pale" yule babu akasema huku akionesha lile eneo alilokuwepo Sajenti Minja.
"kwa hiyo hayupo?", yule askari mwenye hasira akahoji.
"alikuwepo pale", Babu akajitetea.
"hujanijibu bado, kwa hiyo hayupo" yule askari aliuliza tena huku akiwa na shauku ya kufanya kitu.
"ndio mwanangu" Babu akajibu kwa upole.
Bila kutegemea, babu alipigwa mtama mmoja mkali sana, akaangukia makalio.
"unatuchelewesha majumbani kwetu, hatujalala na wake zetu tokea juzi usiku" askari mwenye hasira aliongea huku akimnyanyua babu babu baada ya kumpiga mtama.

Sajenti Minja akacheka tu baada ya kushuhudia ule mtama aliopigwa babu kisha akaishia kujiuliza ni kwanini babu amekamatwa, akajiona mkosaji kwa kukimbia kwa maana yeye angeweza kuwa msaada wa babu, pia akaona alichokifanya kinaweza kubwa sahihi zaidi kwa kuwa huenda Babu atakuwa amekamatwa kutokana na kesi ile ya kuiba maiti, yaani inawezekana kabisa ndugu wa marehemu wamegundua kuwa wameibiwa, na mwisho akajisemea itabidi achunguze ni kitu kilichofanya mpaka yule babu awe katika mikono ya polisi.

"Vipi mbona una mawazo hivyo?" Askari mmoja aliyekuwa anatoka msalani alimuuliza Sajenti Minja aliyekuwa amezama katika bahari ya tafakuri,

"Ah, si unajua tena mawazo ni kawaida kwa binadamu" Sajenti Minja alijibu baada kushtuka kutoka katika lindi la mawazo,

"Wewe ni mgeni kituoni hapa? Maana sura yako sijawahi kuiona" Yule askari alimuuliza Sajenti Minja,
"Kabisa, inaelekea kila mtu anaefanya kazi hapa umemkariri?" Sajenti Minja aliuliza,
"Yaani wote, sisi ndio wakongwe wa hapa" Yule askari alijibu huku akitabasamu,
"Sawa bwana, mimi ndio nawasili muda huu kuja kuripoti kwa mara ya kwanza" Sajenti Minja aliongea huku nae akitabasamu,

"Bila shaka wewe ndiye Joel Minja?" Yule Askari aliuliza,
"Haswaa, umenijuaje?" Sajenti Minja aliuliza,
"Tuliambiwa Leo kuna ugeni wa askari mpelelezi kutoka Dodoma" Yule askari aliongea,
"Basi ndio huyo" Sajenti Minja aliongea,
"Umeshafika ofisini kwa mkuu?" Yule Askari aliuliza,
"Bado, yaani hapa ndo mahala pa kwanza kufika" sajenti Minja aliongea na wote wakacheka,
"Sasa ofisi ya mkuu unaijua?" Yule askari alimuuliza,
"Nitaijulia Wapi mimi?" Sajenti Minja alijibu,
"Sasa ungefikaje" Yule askari aliuliza,
"Ningefika tu, ila kwa kuwa nimekutana na wewe, mambo yatakuwa sawa" Sajenti Minja aliongea,
"Twende nikupeleke" Yule askari akaongea huku akitangulia mbele

Wakatoka katika eneo la chooni, akawa anaelekea katika ofisi ya mkubwa wake, walipofika yule askari aliyempeleka hakutaka kuingia, aliishia mlangoni na kuondoka zake na kumuacha Sajenti Minja mlangoni.

Sajenti Minja akapiga hodi kisha akaingia, aliporudishia mlango, akampa heshima yake mkuu wa polisi,
"kaa hapo sajenti" Mkuu wa polisi wa shinyanga alimuelekeza sajenti Minja sehemu ya kukaa.
sajenti Minja akasogeza kiti, kisha akakaa.
"habari yako Minja" Mkuu wa polisi akamsalimia.
"nzuri tu, shikamoo mkuu" sajenti Minja akajibu.
"Marhaba, Leo ndio siku ya kwanza kuwasili kituoni hapa" Mkuu wake alimuuliza huku akiwa jibu analo kabisa,
"Naam mkuu" Sajenti Minja alijibu kikakamavu,
"Vizuri sana, na kilichokuleta huku nadhani unakijua" Mkuu wake aliuliza tena,
"Ndio mkuu" Sajenti Minja alijibu,
"Tukupatie Askari wa huku ili msaidiane au wewe una pendekezo Gani?" Mkuu wake alimuuliza,
"Naimani peke yangu nina uwezo wa kufanikisha" Sajenti Minja alijibu,
"Kwanini hutaki msaada?" Mkuu wake aliendelea kumbana,
"Kwa sababu hata niliyofikia katika upelelezi wa hii kesi ni hatua nzuri, sasa ukinipa mtu wa kusaidiana nae itakuwa kama tunaanza upya kwa kuwa atakuja na mipango, mbinu na mawazo tofauti kuhusu hii hii kesi" Sajenti Minja alijibu,,

"Lakini kumbuka umoja ni nguvu" Mkuu wake aliongea huku akitabasamu,

" hilo nalijua mkuu, nitapohitaji msaada nitakwambia" Sajenti Minja aliongea,

"Kesi unayoifuatilia umeishia nayo wapi?" Mkuu wake aliuliza,

"Kwa kweli hata niliyopiga ni ndogo sana, bado nahitaji mwanga zaidi ili hata nijue wa kumtia hatiani" Sajenti Minja aliongea,

"Sawa, basi hapa nna habari ambazo zinaweza kukupa mwanga kidogo" Mkuu wake aliongea na kumfanya Sajenti Minja atege masikio vyema,

"Habari zipi hizo mkuu?" Sajenti Minja aliuliza,

"leo asubuhi wasamalia wema walitoa taharifa za kuwepo watu wanne ambayo walikuwa wana alama ya kung'atwa shingoni na kitu kama mnyama mwenye meno makali, tulipoenda tuliweza kukuta watatu waliokuwa wamenyonywa damu makaburini, ila habari nzuri mmoja wapo amekutwa yuko hai, lakini hali yake sio nzuri, ni wa leo au wakesho muda wowote anaweza kufa", Mkuu wa Polisi aliongea huku akiangalia baadhi ya makabrasha yaliyopo mezani kwake,
Sajenti Minja alivyosikia habari ya watu kukutwa wakiwa wamekufa kwa kunyonywa damu eneo la makaburini, moja kwa moja akajua kuwa ni yule mganga na wasaidizi wake, ila habari ya mmoja kuwa hai ndio hakuipenda,
"ndio, nakusikia mkuu" sajenti Minja akajibu baada ya ukimya wa muda mfupi,
"Sasa kwa fikra zangu za haraka haraka haya mauaji nayafananisha na yanayofanywa na mtu unaemtafuta kwa maana hata wale watu waliokutwa wamekufa katika geti la mchungaji walikuwa hivyo hivyo na hizo alama shingoni" Mkuu wake alitoa maelezo,
"Nadhani kwa kuwa huyu mmoja yupo hai basi anaweza kutusaidia tukapata mwanga kidogo" Sajenti Minja aliongea huku moyoni akiwaza hata huyo mtu afe,

"Sasa hivi yupo sehemu ya wagonjwa mahututi amepumzishwa, jioni tutaenda kuongea nae" Mkuu wake aliongea,

"Litakuwa jambo jema sana" Sajenti Minja aliongea,

"sasa ni hivi tutatoka mimi na wewe hadi katika ofisi za akari wengine ili nikutambulishe, alafu jioni ndio tutaenda hadi hospitali ili tuchukuwe maelezo ya huyo aliebakia, maana anaweza kutupa pa kuelekea" mkuu wa polisi alimalizia kuongea huku akisimama,
"sawa mkuu" sajenti Minja akajibu.

Walitoka nje ya ofisi ya mkuu na kisha muda huo sajenti Minja akaanza kutembezwa katika ofisi za askari wa ngazi mbalimbali ili atambulishwe kwa wenzake hao, na kisha pia alizungushwa katika mazingira yote ya eneo like la Polish kwa ajili ya kupata kuyaona ili hata akitoka nje ajue duka linapatikana wapi? vyoo vinapatikana wapi na mambo mengine yanayolizunguka eneo lile.
Baada ya Mkuu wake kuridhika aliamua na kumpeleka katika ofisi ambayo Sajenti Minja ataitumia muda wote ambao atakuwepo pale na kisha wakaagana huku wakikumbushiana kuwa jioni ni lazima waende hospitali kumuona huyo mtu aliyebakia ya wenzie kunyonywa damu, Sajenti Minja hakupenda kabisa hyo safari ila hakuwa na la kufanya, ilibidi atimize matakwa ya kazi yake.

************************

Jioni ilifika haraka sana kwa upande wa Sajenti Minja, alitamani hata isifike kabisa.
Mkubwa wake alimpitia na wakatoka eneo la kituoni.
Baada ya kutoka kituo cha polisi, sajenti Minja na mkuu wake wakafunga safari hadi hospitali, njia nzima sajenti Minja alikuwa anatetemeka, alijua fika kuwa anaenda kuumbuka mbele ya mkuu wake,
"vipi Minja, mbona unatetemeka sana?" mkuu wa polisi akauliza.
"leo nimeamka na homa, kwa hiyo sijisikii vema kabisa" sajenti Minja alidanganya.
"itakuwa malaria, tukifika itabidi upime kabisa" mkuu wa polisi alimshauri Sajenti Minja.

Gari ilipofika, sajenti Minja na Mkuu wa polisi wakatelemka kisha wakawa wanaelekea sehemu ilipo wodi za wagonjwa mahututi, walitumia dakika mbili mpaka kufika katika chumba ambacho alilazwa yule msaidizi wa Mganga ambae alikuwa amenusurika na kifo, ila chumba kilikuwa kitupu,

"Eh, mbona hayupo, ameshakufa nini?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akitoa macho kuangaza bila mafanikio. Kwa upande wa Sajenti Minja hiyo habari ilikuwa nzuri, alijikuta anatabasamu waziwazi mbele ya Mkuu wake,

"Mbona unacheka, unafurahia kumpoteza shahidi?" Mkuu wake alimuuliza kwa mshangao,
"Hapana mkuu, nacheka unavyopeleka imani yako katika kifo wakati hata hujaenda kuuliza kwanza kwa madaktari" Sajenti Minja alijitetea kwa njia ya uongo,

"Kweli bwana, ebu twende tukaulize" Mkuu wake aliongea huku akielekea upande zilizopo ofisi za madaktari na huku Sajenti Minja akiendelea kuomba wakifika waambiwe yule bwana amekufa.
Baada ya sekunde kadhaa walitokea sehemu zilipo ofisi za madaktari, ila kwa bahati nzuri hata kabla hawajaingia ndani, walikutana na Daktari ambae ndiye anayesimamia matibabu ya msaidizi wa Mganga,

"Ooohoo kamanda umeshawasili?" Daktari aliongea huku akimpa mkono Mkuu wa polisi,

"Vipi kuna wema kweli? mbona mgonjwa wetu hayupo kule katika wodi aliyokuwepo asubuhi?" Mkuu aliuliza huku akionesha wasiwasi,

"Wema upo, tens mkubwa sana" Daktari alijibu huku akicheka,

"Hapo kidogo umenipa nguvu, haya niambie huo wema" Mkuu aliongea huku akiwa bado yupo makini kumsikiliza Daktari,

"Mgonjwa wako amepata nafuu na hata kuongea anaongea" Daktari alitoa habari zilizokuwa nzuri kwa Mkuu wa polisi ila hizo hizo habari zilikuwa mbaya sana kwa Sajenti Minja,

"Mmempeleka wapi sasa?" Mkuu wa Polisi aliuliza,

" yuko katika wodu ileee" Daktari aliongea huku akiwaelekeza kwa kidole katika wodi ambayo amehamishiwa msaidizi wa Mganga.

Sajeni Minja na Mkuu wa Polisi baada ya kumshukuru Daktari wakawa wanaelekea kwenye wodi aliyokuwamo yule msaidizi wa mganga huku Sajenti Minja mapigo yake ya moyo yakiongezeka kasi.

wakaingia ndani ya wodi, kisha wakawa wanaelekea kwenye kitanda cha yule msaidizi wa mganga, hapo Sajenti Minja moyo ulikuwa unamkimbia ajabu, akatamani hata sura yake ibadilike au akatamani hata yule msaidizi wa Mganga awe amepoteza kumbukumbu zake, lakini haikuwa hivyo.

Walipofika katika kitanda cha yule msaidizi wa mganga, wakakuta kalala huku kawapa mgongo, yule mkuu wa polisi akamshika bega kwa lengo la kumuasha, yule msaidizi wa Mganga akageuza sura na macho yake yakagongana na macho ya Sajenti Minja........

******ITAENDELEA******

*je Msaidizi wa Mganga atalopoka na kumtaja sajenti Minja kama ni mtu mmoja wapo kati ya wale waliomsababishia matatizo?

the Legend☆
Kwa mara ya kwanza "nimeonekana mwehu mbele za watu..."

Viboko alivyokula minja...nimejikuta nacheka pekee yangu kwa sauti kubwa sana!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI.

______________
ILIPOISHIA...
______________
"Kwani hatuwezi kununua mboga nyingine zaidi ya maziwa" Sajenti Minja aliuliza,

"Mbona tunaweza kununua hata maharage au nyama, tatizo tukiinjika mpaka viive si utakuwa umeshakufa na njaa yako?" Mama Kayoza aliongea,

"Kweli Dada, basi nyie wahini, maana njaa niliyonayo ni ya hatari...

______________
ENDELEA......
_______________
baada ya wakina kayoza kutoka, Sajenti Minja na dada yake waliendelea na maongezi yao.

"afadhali umekuja mwenzangu, maana mjomba ako kanichachamalia hapa", Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja

"kachachamaa na nini tena?"Sajenti Minja akauliza,

"eti anadai tuko kimya katika kufuatilia matatizo yake", Mama Kayoza akajibu,

"kuna askari niliongea nae jana, akaniambia kuna mtaalam wa jadi ana uwezo mkubwa wa kusaidia watu", Sajenti Minja alimwambia dada yake

,"kwa hiyo ulimwambia una ndugu yako ananyonya damu?", mama Kayoza aliuliza kwa mshtuko,

"kwani mi sina hakili mpaka nimwambie hivyo?, nilimdanganya natokewa na mauzauza kila nikitaka kulala", Sajenti Minja akamjibu dada yake,

"ataweza kweli kumtibia kayoza?", Mama kayoza akamtupia mdogo wake swali jingine,

"dada nawe kwa maswali!, tutajua uko uko kama ataweza au lah", Sajenti Minja alimjibu dada yake,

"lini mtaenda uko", mama Kayoza akauliza tena

"nafikiri kesho, kama nitapata nafasi", Sajenti Minja alijibu

"haya bwana, wacha nikakutayarishie chakula jikoni", mama kayoza aliongea huku akinyanyuka kwenye kochi,

"hayo ndo mambo sasa, kama kuna pilipili niwekee", Sajenti Minja alisema na kumfanya mama kayoza ahangue kicheko.

"Sasa hiyo pilipili utaiweka katika maziwa?" Mama Kayoza aliuliza huku akicheka,

"Nitaitafunia tu na ugali" Sajenti Minja alijibu,

"Ngoja nikutafutie kama ntaipata" Mama Kayoza aliongea huku akiingia jikoni.

"Sema siku hizi umekuwa mswahili kweli Dada yangu" Sajenti Minja aliongea huku akitabasamu,

"Kwanini unasema hivyo?" Mama Kayoza aliuliza huku akisimama,

"Naona nawe unakubali tu tumpeleke mwanao kwa waganga sio kama zamani ulivyoshikilia msimamo wako wa kanisani" Sajenti Minja alimwambia Dada yake,

"Ujue Mungu hana njia moja ya kukupa mafanikio, unatakiwa upitie njia nyingi lakini ukimuamini yeye tu na sio vitu vingine" Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja,

"Sawa mama mchungaji, inabidi na wewe ujenge kanisa lako sasa" Sajenti Minja alimwambia Mama Kayoza,

"Ebu kwenda zako uko, kwanza ulivyosema mchungaji umenikumbusha awa wendawazimu waliofuata maziwa, mbona wamechelewa hivyo?" Mama Kayoza aliuliza,

"Wana mambo mengi wale vijana, usikute wanamnyatia yule binti wa mchungaji" Sajenti Minja aliongea kwa utani huku akicheka,

"Acha uwendawazimu wako, watoto wa mchungaji wana maadili wewe" Mama Kayoza aliongea,

"Sio wote, kama yule binti mcharuko niliekutana nae juzi ni bure kabisa, bora angeishi uswahilini tu" Sajenti Minja aliongea huku akicheka,

"Kwani ana kosa gani? Si alikuwa anaenda polisi kusema habari za ukweli" Mama Kayoza aliongea huku akitabasamu,

"We si ni mlokole? Nenda na wewe polisi kaseme hizo hizo habari kuwa mwanao muuaji" Sajenti Minja alimwambia Mama Kayoza,

"Mtoto anauma bwana, mtoto mwenyewe ndio huyo huyo mmoja kama roho" Mama Kayoza aliongea huku akicheka,

"Nenda jikoni bwana, maana story zimezidi mpaka unasahau kuwa mimi njaa inaniuma" Sajenti Minja alimwambia Dada yake,

"Hata baba, usije ukanifia bure kwa njaa" Mama Kayoza aliongea huku akielekea jikoni.

*********************

Baada ya mkuu wa polisi kurudi ndani, alimpgia simu askari mwingine na kumwambia amrudishe rumande Babu wa mochwari,

"jamani nitakaa huku mpaka lini, nina mke na watoto mimi",Babu wa mochwari aliongea huku machozi yakimtoka,

"usijali mzee wangu, upepelezi utakamilika hivi karibuni", Mkuu wa polisi alimjibu Babu wa mochwari kwa huruma.

"Mwanzo askari wako waliniambia nikiri kosa ili niachiwe, nikakiri kosa kuwa ni kweli mwili umeibwa, lakini hawajaniachia, naambulia kipigo tu mpaka viungo vinateguka" Babu wa monchwari alilalamika,

"Mzee ujue upelelezi sio kitu cha kukurupuka tu, inahitajika muda mrefu wa kuchunguza na kujiridhisha na jibu la kile kilichopelelezwa, na hapo sasa ndipo sisi tutaachana na wewe na kesi yako itakuwa mahakamani" Mkuu wa polisi alimuelewesha Babu wa monchwari,

"Mahakamani tena?, si nitafungwa jamani mie?" Babu wa monchwari aliuliza huku akilalamika,

"Sasa sisi hatutaki ufungwe, na ndio maana tunaendelea kukuhifadhi ili utusaidie kumpata huyo aliyeichukua hiyo maiti" Polisi alimwambia Babu wa monchwari,

"Sasa mbona sioni juhudi zozote ukizifanya kumtafuta huyo mtu na nilishawahi kumuona eneo hili huyo mtu mwenyewe" Babu wa monchwari aliongea na kumfanya Mkuu wa polisi ashtuke kidogo,

"Alikuwa anafanya nini na kwa nini hukuwaambia Askari?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akimshangaa,

"Kitu ninachokishangaa ni kwamba alipotea ghafla, inawezekana kabisa yule bwana si mtu wa kawaida, atakuwa mshirikina tu" Babu wa monchwari aliongea,

"Kumbe ukimuona kwa sura unamjua vizuri tu?" Mkuu wa polisi aliuliza,

"Vizuri sana tu, hata akiwa mbali namtambua" Babu wa monchwari aliuliza,

"Ulivyomuona alivaaje, au alivaa kiaskari?" Mkuu wa polisi alimdadisi Babu wa monchwari,

"Hajavaa kiaskari, na kwanza hawezi kuwa askari yule, ana ndevu kabisa" Babu wa monchwari alijibu,

"Basis usijali babu, tunaendelea kufuatilia" Mkuu wa Polisi aliongea,

Kisha yule askari aliepigiwa simu aliingia na kisha akamchukua Babu wa mochwari na kumrudisha rumande.

***********************

Wakina kayoza walipofika kwa Mchungaji Wingo, walimkuta Binti wa mchungaji anafagia fagia

"karibuni", Binti wa mchungaji aliwakaribisha alipowaona,

"asante, za hapa?", Omari alijibu alafu akamjulia hali,

"poa my husband, Kayoza mambo?", baada ya kujibu salamu ya Omari, binti wa mchungaji akamgeukia Kayoza,

"poa, kuna maziwa ya mtindi?" Kayoza akamjibu kwa mkato, kisha akasema kilichompeleka,

"yapo, mnataka kiasi gani?" Binti Mchungaji akauliza,

"nusu lita" Kayoza alijibu huku akimpatia pesa, Binti wa mchungaji akachua hela kisha akaingia ndani kuwapimia maziwa.

"kaka uko siriazi, hutaki hata kucheka nae", Omari alimwambia kayoza huku akijichekesha

"boya sana huyu demu", Kayoza aliongea akiwa na chuki za wazi kwa binti wa mchungaji.

Baada ya dakika tano binti wa mchungaji alitoka, akawapa maziwa

,"Omari baki, kuna kitu kizuri nataka kukwambia", Binti wa mchungaji alisema,

"nibaki?, kwani ndani uko na nani?", Omari alimuhoji Binti wa mchungaji,

"niko peke yangu, wote wameenda mjini, ila baba kaenda kanisani", ndivyo alivyojibu,

"Boy we tangulia, mimi ninakuja" Omary alimwambia Kayoza,

"Sasa nikifika peke yangu mama si ataniuliza?" Kayoza alihoji,

"Utajua namna ya kumdanganya, ila hata sitochelewa" Omary aliongea,

"Poa, jitahidi kuwahi bwana" Kayoza aliongea huku akianza kuondoka.

"Twende ndani basi" Binti Mchungaji alimwambia Omary huku akimvuta mkono,

"Huogopi?" Omary aliuliza huku akijatahidi kutosogea zaidi ya pale alipo,

"Twende ommy, utaniudhi ujue" Binti Mchungaji aliongea sauti ya kudeka na kumfanya Omary alegeze msimamo,

"Una hatari sana" Omary aliongea huku akipiga hatua kumfuata binti mchungaji

"Twende usiogope, awa hawarudi sasa hivi" Binti Mchungaji aliongea huku akifungua mlango wa chumbani kwake,

"Bora ungenipeleka sebuleni, huku ndio pabaya kabisa" Omary aliongea huku akiingia katika chumba cha Mchungaji,

"Kelele bwana, kaa hapo mimi nakuja sasa hivi" Binti Mchungaji aliongea huku akimkalisha Omary kitandani,

"Uwahi basi" Omary aliongea wakati Binti Mchungaji akitoka,

"Nakukuja sasa hivi, kuna kazi naenda kuimalizia chap chap" Binti Mchungaji aliongea na kisha akatoka nje baada ya kuurudishia mlango, Omary akabaki chumbani peke yake huku macho yake yakitalii katika kila kona ya chumba kile cha Binti Mchungaji.

Baada ya Binti mchungaji kumaliza kazi, akaenda kujisafi mwili, kisha akarudi chumbani kwake na kufunga mlango kwa ndani,

"we mtoto huogopi?, Omari alimuuliza huku akiwa na sura ya wasiwasi, Binti wa mchungaji badala ya kujibu, yeye akaitoa ile khanga aliyotokanayo kuoga na kubaki mtupu kama alivyozaliwa, Omari akili ilimruka na uoga wote ukamtoka, bila kutarajia akamvuta binti wa mchungaji kitandani, na kuamia katika ulimwengu mwingie.

Mchungaji Wingo aliporudi nyumbani kwake, akakuta mlango wa mbele uko wazi, video sebuleni inawaka, akamuita binti yake, lakini hakupata jibu, akaamua aende akamuangalie chumbani kwake, alipokaribia mlango wa chumba cha binti yake, alisikia mlio wa kitanda cha binti yake kikilalamika kwa fujo,

"mh..", mchungaji Wingo aliguna...

*******ITAENDELEA*******

*haya sasa Mchungaji anakuta utata katika chumba cha mwanaye, je nini kitatokea?

*Sajenti Minja amepata habari za kuwepo kwa mganga mwingine kiboko, je huyo mganga atamponesha Kayoza?

the Legend☆
Hatimahe nimefika ukingoni. Aiseeeh huyu Kireo ni fundi sana.....honestly anajua.

Asante sana legend, kwa kushare nasi haya maudambu udambu.....much blessing to you.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatimahe nimefika ukingoni. Aiseeeh huyu Kireo ni fundi sana.....honestly anajua.

Asante sana legend, kwa kushare nasi haya maudambu udambu.....much blessing to you.

Sent using Jamii Forums mobile app
Amen. Tuko pamoja mkuu.
Jamaa anajua, aliwahi kusema hii ndio ilikua ni riwaya yake ya kwanza kabisa kuitunga

the Legend☆
 
Back
Top Bottom