Marilyn Monroe
Member
- Apr 2, 2020
- 80
- 167
RIWAYA: MKIMBIZI
MTUNZI: HUSSEIN ISSA TUWA
SEHEMU YA KWANZA
likuwa ni msafara wa watu watano, watatu kati yao, pamoja na mimi mwenyewe, tukiwa ni waajiriwa wa Idara ya Makumbusho ya taifa kitengo cha utafiti wa masalia ya kale. Wa nne alikuwa ni mpiga picha binafsi aliyeajiriwa kwa muda na Idara ya Makumbusho ya taifa maalum kwa shughuli iliyopelekea kwenye msafara huu, wakati mtu wa tano alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye alikuwa anafanya utafiti kwa ajili ya shahada yake ya pili hapo mlimani. Alikuwa anafanya utafiti juu ya masalia adimu ya viumbe vya zama za mwisho za mawe nchini Tanzania, na utafiti wake ulikuwa unawiana kabisa na dhumuni la msafara wetu.
Kutoka katika Idara ya Makumbusho ya taifa alikuwepo mtafiti wa mambo ya kale mwandamizi (ambaye ni mimi), mtafiti mkuu bwana Ibrahim Geresha ambaye ndiye alikuwa mkuu wa msafara na mkuu wangu wa kazi, pamoja na dereva wetu ambaye tangu niajiriwe katika Idara ya makumbusho ya taifa nimekuwa nikimjua kwa jina moja tu la Beka.
Mpiga picha wetu katika msafara huu alikuwa anaitwa Gilbert Kyaro, ambaye alipendelea zaidi kuitwa Gil, na alikuwa akipenda sana kusikiliza na kuimba nyimbo za Johnny Gil.Nadhani ndicho kitu kilichomfanya naye ajisikie kuitwa Gil.
Wakati gharama zote zilizotuhusu katika msafara huu zilikuwa zikilipiwa na idara ya Makumbusho ya Taifa, zile za bwana Ubwa Mgaya, kama nilivyokuja kumjua jina lake hapo baadaye, zilikuwa zikilipwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama sehemu ya fungu lake la utafiti.
Wakati Toyota Landcruiser ikitupeleka kwa kasi kuelekea kwenye eneo la tukio, nilikuwa na matarajio kuwa na hii itakuwa ni safari nyingine ya kuvutia na kunufaisha kama nilivyozoea. Sikuwa na sababu ya kutarajia vinginevyo.
Nikiwa nimehitimu kwa mafanikio makubwa mafunzo yangu ya shahada ya kwanza ya Utafiti wa mambo ya kale (Bachelor’s Degree in Archaelogy) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka mmoja uliopita, nilijihisi kuwa mwenye bahati sana kuweza kuajiriwa na Idara hii ya Makumbusho ya taifa kiasi cha mwezi mmoja tu baada ya kusherehekea kupata kwangu digrii hii adimu, nikiwa naelewa fika jinsi kazi zilivyokuwa ngumu kupatikana hapa nchini hata kwa wahitimu wa vyuo vikuu. Lakini nadhani hii ilitokana na fani niliyochagua kusomea, kwani ni fani ambayo haina upinzani mkubwa hasa hapa nchini.
Marafiki zangu wengi walinishangaa kutokana na uamuzi wangu wa kusomea fani hii, lakini kwa wakati ule nilikuwa nimo ndani ya penzi zito la profesa mmoja kijana wa pale Chuo Kikuu ambaye alinishawishi kuchagua fani hiyo akidai kuwa ilikuwa na nafasi nyingi za kwenda kujiendeleza nje ya nchi. Nilipofika mwaka wa pili nikamfumania mpenzi wangu huyo nyumbani kwake, akifanya mapenzi na mwanafunzi mwenzangu ambaye nilikuwa nikiishi naye chumba kimoja pale chuoni, tena sakafuni jikoni kwake wakiwa kama walivyozaliwa.
Nilichofanya ni kuwamwagia maji ya baridi kutoka kwenye jokofu lililokuwapo pale jikoni na kuwaacha wakitapa tapa pale sakafuni nami nikashika hamsini zangu. Matokeo yake penzi la profesa kijana likafa pamoja na ahadi ya kutoka nje ya nchi kwa masomo zaidi katika fani ya utafiti wa mambo ya kale.
Hapo tena ilikuwa haiwezekani kubadilisha masomo, hivyo nikaendelea tu na fani hiyo hiyo.
Baada ya kile kituko cha jikoni kwa profesa kijana, nilibadilishana chumba na msichana mwingine nami nikahamia chumba kingine nilicholazimika kuishi na msichana wa kipemba aliyekuwa akiswali swala tano kila siku, kitu kilichoonekana kumkera yule msichana aliyekuwa akiishi naye awali, ingawa kwangu halikuwa tatizo.
Lakini pamoja na upumbavu wake, profesa kijana hakukosea, kwani nilipata ajira haraka sana baada ya kumaliza masomo yangu, na baada ya kuajiriwa na idara ya makumbusho ya taifa nimekuja kuona kuwa hii hasa ndiyo fani inayonifaa kwani iliniweka njiani muda mwingi kwa safari kuelekea sehemu mbali mbali nchini kufanya tafiti nyingi tu kuhusiana na mambo ya kale na kukusanya mabaki ya kale kwa kuchunguzwa kitaalamu zaidi makao makuu ya idara, Dar es Salaam.
Ila kilichonipendeza zaidi katika kazi yangu hii ni pesa. Kwanza mshahara niliokuwa nikipokea ulikuwa ni mzuri sana, hasa kwa mtu niliyetoka chuoni kama mimi, ambaye hapo nyuma nimekuwa nikishambuliwa na FFU mara kadhaa nikiwa katika maandamano na migomo kugombea kuongezewa posho isiyotosheleza chochote wakati nipo chuoni. Zaidi ya hapo kulikuwa na posho nyingi zinazotokana na safari kama hizi za kikazi, ambazo huwa tunaziita per diem.
Na hivyo wakati mabaki ya kiumbe kisichojulikana yalipogunduliwa wiki chache zilizopita katika msitu fulani huko Manyoni katikati ya kanda ya kati ya Tanzania, kwa mara nyingine tena nikajikuta nikiwa safarini. “Manyoni Expedition” au “Msafara wa Manyoni” kama msafara wetu huu ulivyojulikana ulikuwa ni wa awali, uliotarajiwa kukamilika ndani ya wiki moja ambapo baada ya hapo ingeamuliwa iwapo kilichogundulika huko Manyoni ni kweli kilikuwa mabaki ya kiumbe hai wa kale basi ungekuwa ni mradi maalum ambao ungeweza kudumu kwa kadiri ya muda ambao ungehitajika ili kuukamilisha.
Na ikifikia hapo ndipo ningekuwa nazivuna per diem kama sina akili vizuri na wakati huo huo nikifanya kazi ninayoipenda.
Nikiwa nimetulia ndani ya Toyota Land Cruiser kuelekea Manyoni kupitia Dodoma, nilijifariji kuwa baada ya misuko suko na maisha magumu niliyolazimika kupitia wakati nikitafuta digrii yangu pale mlimani, sasa nilikuwa nafaidi nyakati nzuri kabisa katika maisha yangu.
Nyakati nzuri sana.
Nilisahau kabisa msemo tuliowahi kuambiwa na mhadhiri mmoja wakati tuko chuoni kuwa “Ni nyakati nzuri kabisa katika maisha ya binadamu ndizo zinazobadilika na kuwa nyakati mbaya kabisa bila ya kutarajia…”
It is always the very good times of one’s life that normally turns into one’s very bad times in no time…
Ni kwamba kama mtu akiwa katika maisha mabovu hakuna kibovu zaidi kitakachomkuta zaidi ya hicho, lakini akiwa kwenye maisha mazuri ndio ataona mabadiliko pale hali hiyo itakapotoweka.Na kwa kawaida maisha mazuri huwa hayadumu. Kwa wakati ule nilimuelewa sana mhadhiri yule, halafu nikasahau kabisa juu ya ukweli huu.
Sikuwa na sababu ya kuukumbuka tena, kwani tayari nilikuwa nimeshaingia kwenye raha ya maisha mazuri…mpaka hapo yalipokuja kunigeuka.
Tulisafiri kwa saa sita mpaka Dodoma ambapo tulilala kwenye hoteli moja ya bei nafuu kubania pesa zetu za safari kwa makubaliano kuwa tungeaza sehemu ya pili ya safari yetu asubuhi ya siku iliyofuata ili kukwepa jua kali libabualo la nusu jangwa.
Asubuhi ya siku iliyofuata, nikiwa msichana pekee katika msafara wetu, nilijiweka vizuri kwenye kiti changu cha dirishani nyuma ya kiti cha dereva na safari yetu kuelekea Manyoni ilianza. Nilipachika visikilizio masikioni na kuanza kusikiliza muziki wa Bongo Flava kutoka kwenye Walkman yangu ya CD na kuwaacha wasafiri wenzangu wakiburudika na muziki wao wa mayenu kutoka kwenye redio ya gari. Kadiri safari ilipoendelea huku Land Cruiser ikienda kwa kasi kupitia kwenye njia za vumbi na kona nyingi kuelekea kwenye lengo la safari yetu nikabaini kuwa bwana Ubwa Mgaya wa Chuo Kikuu alikuwa akinitupia macho ya mara kwa mara jambo ambalo lilianza kunikera.
Nikavaa miwani yangu ya jua na kuamua kuangalia nje ya dirisha.
Ilikuwa jioni sana tulipoingia Manyoni mjini na kuamua kupata malazi katika nyumba yoyote ya wageni tutakayoiona, ambayo ilitokea kuwa ni nyumba kubwa ya vyuma sita isiyokuwa na umeme na choo cha shimo ambacho pia hutumika kama bafu, na mama mwenye nyumba mcheshi sana. Ilibidi tufanye zamu kutumia choo na bafu na kwa msisitizo wa bwana Ubwa Mgaya nikapewa nafasi ya kuwa wa kwanza kutumia huduma hiyo. Nilipotoka bafuni nikajibwaga kitandani chumbani kwangu kwa lengo la kujipumzisha kabla ya kupata mlo wa jioni, lakini nilipofumbua macho ilikuwa alfajiri ya siku iliyofuata.
Kama jinsi taratibu zinavyotaka, tuliripoti ofisini kwa mkuu wa wilaya, ambaye alitokea kuwa ni mwanamke wa makamu mwenye sura ya kuvutia na tabasamu la kutia moyo. Kwa kuwa alikuwa na taarifa ya ujio wetu, hatukupoteza muda pale ofisini kwake. Baada ya mkuu wa msafara bwana Ibrahim Geresha kututambulisha na mpiga picha wetu Gilbert Kyaro au Gil kutupiga picha ya pamoja tukiwa na mkuu wa wilaya, tulipewa wenyeji wawili kutoka kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ambao ndio wangetuongoza kuelekea huko kulipoonekana hayo mabaki ya kiumbe cha kale kisichojulikana.
Kwa mara nyingine tena tukaingia kwenye Land Cruiser yetu na safari ya kuelekea msituni ikaanza, tukiwa tuna watu wawili zaidi na zana zetu za kazi zilizojumuisha mahema, machepeo maalum, vifaa vya kupikia, chakula cha kuweza kutosha kwa wiki nzima na mabegi yetu binafsi. Tukiwa njiani nilianza urafiki na mpiga picha wetu Gil huku nikibaini kuwa bwana Ubwa Mgaya sasa hakuwa akinitupia macho ya wizi tena bali alikuwa akinikodolea macho wazi wazi kama mvulana ambaye amebaleghe halafu akamwona msichana wa ndoto zake.
Niliamua kutomtilia maanani na kujaribu kuelekeza akili yangu kwenye kazi iliyopo mbele yetu.
Laiti ningejua kilichokuwa kikitusubiri huko mbele.
--
Katika siku yetu ya tatu tukiwa msituni ndipo tulipofanikiwa kufanya ugunduzi tulioukusudia. Ugunduzi wa masalia ya kiumbe hicho cha kale yaligundulika umbali wa kilometa zipatazo mbili kutoka eneo ambalo masalia hayo yalionekana kwa mara ya kwanza na wachimba madini walioshindwa kufanikiwa katika lengo lao la kupata madini waliyoyakusudia na kuambulia kufukua mabaki ya kiumbe hicho.
Zilikuwa ni siku tatu za kazi ngumu lakini ya kufurahisha kwani tulikuwa tukicheka na kutaniana huku tukichimba na kutambaa ardhini tukipima aina za udongo na kulinganisha na aina ya mabaki yaliyogunduliwa hapo awali.Tulichimbua aina mbali mbali za mifupa na kujaribu kuipima kitaalam kugundua aina ya kiumbe kilichobakiza mifupa hiyo.Wakati tukiwa katika harakati zetu hizo, Gil naye alikuwa katika harakati za kupiga picha vitu tulivyokuwa tunavichimbua kutoka ardhini na sisi wenyewe tukiwa katika pozi mbalimbali za kazi. Alikuwa anatumia kamera ndogo aina ya Sony ambayo ilinivutia sana.
Gil alinielekeza ni wapi ningeweza kuipata nami nikaweka dhamira kuwa nikirudi tu ustaarabuni nitainunua. Ilikuwa ni kamera iliyoweza kupiga picha za video na wakati huo huo kupiga picha za kawaida. Wakati wa kupiga picha za video, mtumiaji hakutakiwa kuiweka jichoni mwake muda wote, kwani ilikuwa na kiji-runinga kidogo pembeni ambacho mtumiaji aliweza kuwaona watu aliokuwa akiwapiga picha kupitia pale kwenye hicho kijiruninga. Kwa hakika ilinivutia sana na mara kadhaa nilipokuwa najipumzisha katikati ya kazi, Gil alikuwa akinielekeza namna ya kuitumia na nilivutiwa zaidi na mikanda yake ya kurekodia picha za video ambayo ilikuwa midogo sana kuliko hata ile mikanda ya kaseti za redio.
Nyakati za jioni tulipenda kukaa kuzunguka moto na kupata mlo ambao mimi nilijitolea kuwa nawapikia wenzangu na kuongea juu ya mambo mbalimbali kabla ya kila mtu kuingia kwenye hema lake kulala. Ni katika nyakati hizi za jioni baada ya kazi wakati siku moja bwana Ubwa Mgaya aliponiuliza iwapo nilikuwa nimeolewa, wakati huu ikiwa tumezoeana kidogo. Nilimjibu kwa kumwonesha pete yangu ya uchumba ambayo ilikuwa kidoleni mwangu.
“Oh! Aa-Okay…I mean, Hongera sana…” Alijibu kinyonge huku akionesha wazi kuwa alikuwa amekatishwa tamaa.
Nikamshukuru kama kwamba sikuelewa kitu.
--
Ilipofika siku ya nne ilikuwa tayari imethibitika kuwa “Manyoni Expedition” ilikuwa imefanikiwa kwani tuligundua mabaki mengi sana yaliyofanana na yale yaliyogundulika hapo awali ambayo mpaka hapo hatukuwa na namna ya kujua ni ya kiumbe wa aina gani mpaka hapo tutakapoyafikisha Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi. Kwa hali hii, mapema siku iliyofuata tulianza kufungasha virago vyetu tayari kwa safari yetu ya kurudi Dar.
Kwa hiyo wakati wenzangu wanafungasha mahema na vifaa vyetu vya kazi na kupikia, nilimwomba Gil kamera yake ili nijifurahishe kwa kupiga picha mbalimbali za wanyama wadogowadogo pale porini ambao walikuwa wengi. Gil alitoa mkanda wa video aliokuwa amerekodi picha zetu za kazi na akaniwekea mkanda mwingine.
“Haya nenda kachezee huo.” Alisema kwa utani na sote tulicheka. Nilichukua ile kamera na kukimbia porini zaidi kutafuta wanyama wa kuwapiga picha. “Msiniache jamani eenh!” Niliwapigia kelele wenzangu.
“We’ ukisikia honi ujue safari iko tayari!” Ibrahim Geresha alinipigia kelele. Nami nikamnyooshea ishara ya dole gumba kumuashiria kuwa nimemuelewa.
Mara nikaona kundi la tumbiri ambalo lilinivutia na nikaanza kuwapiga picha kwa kutumia ile video kamera ya Gil wakiruka kutoka tawi moja la mti kwenda jingine. Mara nikaona digidigi wakikimbizana nami nikawageukia wao na kamera yangu. Nilikuwa najisikia raha sana. Muda si mrefu likapita kundi kubwa la nyani wakubwa sana ambao kidogo walinitisha kwani nilisikia kuwa nyani wa aina hii huwa wakiona mwanamke msituni lazima wambake. Hivyo nilijificha kwenye kichaka huku nikiwarekodi kwenye video kamera niliyokuwa nayo hadi walipopotea.
Nilijitoa kutoka kwenye kichaka nilichokuwa nimejificha na nilianza kurudi kwa wenzangu taratibu huku nikiangaza huku na huko kutafuta viumbe vingine vya kuvutia wakati ghafla niliposikia mngurumo kama wa ndege kwa mbali lakini ukizidi kuja karibu kila sekunde. Nilitazama juu lakini sikuona kitu kutokana na miti iliyojishona sana juu yangu. Nilianza kurudi tena kwa wenzangu, lakini ile sauti ilikuwa inaongezeka na kuanza hata kupeperusha matawi ya miti iliyokuwa karibu kwa upepo nami nikawa na hakika kabisa kuwa ile ilikuwa ni ngurumo ya helikopta. Niliangaza huku na huko nikijaribu kuitafuta ile helikopta bila mafanikio. Nikaamua kurudi kwa wenzangu.
Nilipokuwa naanza kugeuka ili nirudi kule kwa wenzangu, ghafla helikopta ilijitokeza juu ya uzio wa vilele vya miti iliyokuwa ikinikinga. Bila ya kujua ni kwa nini au ni nini kilichonifanya nichukue hatua hiyo, nilijibanza haraka nyuma ya mti na kuanza kuitazama ile helikopta kubwa wakati ikizunguka kwa madaha mara mbili juu ya eneo lile na kuanza kuteremka taratibu na kwa makelele kwenye ukingo wa msitu ambako katika kuranda randa kwangu sikuweza kufika. Nilijiuliza hii helikopta itakuwa inatafuta nini huku porini katika muda huu. Kwa siku zote nne tulizokuwa tumepiga kambi pale msituni hatukuona harakati zozote za binadamu isipokuwa zile za kwetu tu, ambazo zilikuwa ni za muda tu, hivyo wote tulikubaliana kuwa eneo lile halikuwa na harakati nyingi zaidi ya zile za tumbiri na digidigi.
ITAENDELEA KESHO SAA MOJA ASUBUHI.