RIWAYA: Mume Gaidi

RIWAYA: Mume Gaidi

SEHEMU YA 54


Mara akashikwa bega, kugeuka nyuma ni Mwita akiwa na wanajeshi wengine watatu.
Patrick akashtuka hadi wale wakamshangaa kwani hakutarajia kuonana na Mwita kwa wakati huo ukizingatia ameshafanya mambo mabaya,
MWITA: Vipi Patrick mbona umeshtuka? Inamaana hukutarajia kukutana na mimi huku Mwanza?
PATRICK: Aah! Kumbe ulishakuja Mwanza!
MWITA: Patrick, umesahau jamani!! Si uliniambia mwenyewe kuwa nitangulie Mwanza? Na siku niliyoondoka nikakwambia, tangia hapo sijakupata tena hewani hadi nakuona leo.
PATRICK: Dah! Nilisahau bhana, kule nilipoenda hakuna umeme kabisa ndomana sikuwa hewani, nimechajia hapahapa Mwanza leo.
MWITA: Basi hawa ni wanajeshi wenzangu, wenyewe kikosi chao kipo huku Mwanza.
PATRICK: Basi vizuri kuwafahamu.
Patrick sasa akajisikia amani kidogo maana mwanzoni alidhania ameshtukiwa alichofanya.
MWITA: Sasa vipi kuhusu ile ahadi Patrick?
PATRICK: Ile ya kuhusu baba yako?
MWITA: Ndio.
Patrick akaamua kumuelekeza Mwita mahali alipoambiwa na Yuda ili yeye aendelee na mishe zake zingine kwanza, kwavile Mwita hakuwa mwenyeji mzuri wa Mwanza ikabidi aende na wale wenzie kule alipoelekezwa na Patrick.
Deborah na Pamela waliamua kuingia ndani ili kuongelea mambo mengine.
DEBORAH: Jamani hapa tumelia sana tena tumelia vya kutosha, hebu tuwashe na radio kwanza tujiliwaze na kupata habari tofauti tofauti.
PAMELA: Kweli kabisa Deborah ili tupunguze machungu yetu.
Deborah akainuka na kuwasha radio na muda huo huo wakasikia tukio la mauaji ya wanajeshi mkoani Singida.
PAMELA: Jamani majanga gani hayo?
DEBORAH: Zaidi ya majanga, ni binadamu gani mwenye roho mbaya kiasi hicho? Yani anachinja kama kuku!!
MARIUM: Ingekuwa Maiko yupo huko Singida ningesema ni yeye tu,
PAMELA: Kwanini Maiko na si mtu mwingine?
MARIUM: Kwasababu yeye ndio mwenye roho ya kinyama namna hiyo.
DEBORAH: Kwanza mimi ndio sielewi mwenzenu, kwanini Maiko kawa ndugu wa Adamu? Dah!
FAUSTA: Wote nadhani hilo swala haliwachanganyi, mimi mwenzenu ndio sielewi hata itakuwaje yani sielewi kabisa.
Maiko aliweka msiba mkubwa sana moyoni mwa wanawake hawa na hawataweza kumpokea kama mwanafamilia kwa aliyowatendea.
Tusa na Sele wakiwa Mwanza wanamuona Mwita na wenzie wakipita, Tusa anajibanza huku akimkumbatia Sele kwa nguvu kabisa.
Tusa hakutaka kumuachia Sele, alijikuta akiwaogopa wanaume wote kasoro Sele ambaye aliishi nae kwa kubembelezwa.
TUSA: Sele, nakuomba unirudishe kwa mama. Nataka nirudi nyumbani na mama yangu ili nikaishi tena na familia yangu.
SELE: Tulia Tusa, yote yana mwisho haya.
TUSA: Kwakweli Sele unanipenda na unateseka kwaajili yangu, tamaa imeniponza Sele. Nilidhani wanaume wote duniani ni Sele, kumbe kuna wakina Patrick, John, Maiko na Mwita. Sikulijua hilo, Sele una moyo wa kipekee, moyo wa tofauti. Nimeoza mimi Sele ila bado hutaki kuniacha, nanuka mimi ila bado upo karibu yangu.
Tusa alizidi kumkumbatia Sele huku machozi yakimbubujika.
Muda ambao Mwita na wenzie walipita mahali hapo ni muda huo pia Patrick nae alikatisha mahali hapo, wakina Mwita hawakuwaona Tusa na Sele ila Patrick aliwaona na kuwashangaa kilichowafanya wakumbatiane pale njiani, akaanza kuwafata pale walipo.
Mashaka aliumia sana moyo na kuendelea kumfatilia Maiko.
Akafika hadi mahali ambako Maiko alikuwa akifanya maongezi na mama yake na pacha wake pia.
Mashaka alifika na kuingia huku akiwa na hasira sana.
MASHAKA: Maiko, kitu ulichonifanyia nakwambia ipo siku utalipia.
Kuangalia pembeni akamuona dada yake bi.Rehema.
REHEMA: Hivi wewe Mashaka, mambo yako mangapi umeyalipia? Maovu uliyoyatenda unadhani yamesahaulika?
Mashaka akamuangalia sana dada yake hakutaka kuongea kitu cha zaidi ila akaondoka na kwenda kutafakari.
"Yani mimi ndio nikose kila kitu? Ila Maiko kwa maovu yake yote bado apate furaha ya maisha? Labda kama Mashaka nitakufa lazima nifanye kitu"
Mashaka alikuwa na hasira sana juu ya Maiko ukizingatia alikuwa anajua ndiye mwanae wa pekee.
Mwita alipelekwa na wanajeshi wenzie hadi mahali walipohisi ndio penyewe walipoelekezwa.
Mwita akagonga mlango, Maiko akajua Mashaka amerudi ikabidi ajiandae kwaajili ya kupambana.
Ila alipofungua mlango akamuona Mwita, naye Mwita akaingia ndani na kumwambia.
MWITA: Nimekutafuta sana baba, kwanini unanifanyia hivi?
MAIKO: Mmh!! Unanijua mimi vizuri?
MWITA: Nakujua ndio na picha zako ninazo baba.
MAIKO: Picha zangu? Alikupa nani?
MWITA: Alinipa mama, ngoja nikuonyeshe picha yake.
Mwita akatoa picha ya mama yake na kumkabidhi Maiko, akaitazama ile picha na kumkumbuka vizuri huyo mwanamke.
MAIKO: Kweli wewe ni mwanangu.
Maiko akamkumbatia Mwita, bi.Rehema na Adamu wakabaki wanashangaa tu. Ikabidi Maiko awatambulishe kwa ufupi.
Akawapatia na picha ya mwanamke aliyezaa nae.
MAIKO: Huyu ndiye mwanamke niliyezaa nae ila sikuwa naishi nae ilitokea tu tukampata huyo mtoto.
Maiko alificha ukweli wa mambo juu ya huyo mwanamke.
Bi.Rehema alipoangalia picha ya mwanamke huyo sura yake ilimjia vilivyo.
REHEMA: Mbona kama....., hebu ona na wewe.
Akamkabidhi na Adamu aitazame vizuri.
ADAMU: Mmh!! Ni huyu huyu mama.
Adamu na bi.Rehema wakajikuta wakitazamana kwa mshangao.
Tusa na Sele wala hawakumuona Patrick anavyowafata, Sele akasimamisha gari ya kukodi halafu wakapanda na kuondoka, Patrick nae akawafata kwa nyuma, yeye alikodi bodaboda.
Walienda moja kwa moja hadi karibia na nyumbani kwa Deborah wakashuka, wakawa wamesimama huku wakiongea, Patrick nae akashuka na kuwafata kwani wivu ulishamshika kwa jinsi alivyowaona.
Nia yake ni kujua kuwa kwanini walikuwa wamekumbatiana pale njiani.
 
SEHEMU YA 55


Nia yake ilikuwa ni kujua kuwa kwanini walikumbatiana pale njiani.
Patrick akawasogelea pale walipo, kumuona wakashtuka sana.
PATRICK: Mbona mmeshtuka?
SELE: Hatukutarajia kukuona hapa muda huu.
PATRICK: Vizuri sana, haya umetoka wapi na Tusa?
SELE: Nimetoka naye hospitali.
PATRICK: Inamaana humo ndani kwetu hakuna watu wote wa kwenda nao zaidi ya wewe?
SELE: Ndio tunafika leo Patrick, hali ya Tusa ilikuwa mbaya sana.
PATRICK: Hata kama, mlitakiwa kufika nyumbani kwanza. Hilo ni kosa la kwanza, haya na kwanini mlikumbatina njiani?
Ikabidi Sele amweleze walivyowaona wakina Mwita na Tusa akapatwa na uoga na kujificha.
PATRICK: Kwanini Tusa unamuogopa Mwita? Nipe sababu sasa.
Tusa huku akiogopa na kutetemeka,
TUSA: Alinibaka.
Sele alishtuka ila Patrick alishtuka zaidi na kumuuliza tena na jibu likawa lile lile.
PATRICK: Kwanini alikubaka? Kwani alikubakeje?
TUSA: Sijui ila alinipiga sana halafu akanibaka.
Hasira zikampanda Patrick na kuona Mwita nae ni sawa na Maiko.
Akataka kuondoka ila mama yake mdogo akamuona na kumuita.
"Patrick, Patrick"
Alikuwa ni mama yake mdogo ambaye ni Anna.
Deborah bado hakuridhishwa na hali ya kuwa ni Patrick ndiye aliyemkomboa Pamela.
FAUSTA: Ila Deborah hata mimi nimekombolewa na huyo kijana maana alisema kuwa nikifika hapa niseme ni yeye kanielekeza.
DEBORAH: Yani na wewe unamaanisha Patrick!!
FAUSTA: Ndio huyo huyo, kwakweli Deborah unastahili pongezi kwa kumpata mtoto wa aina ile.
Deborah alicheka machoni ila moyoni aliumia sana haswa akifikiria huo uhusiano wa Patrick na Maiko.
TINA: Hata na mimi ameniokoa Patrick.
DEBORAH: Kheee! Kumbe hadi wewe!!
TINA: Ndio, kwakweli yule Patrick ana moyo wa tofauti sana.
DEBORAH: Nyie wote mlitekwa halafu wote mmeokolewa na Patrick mbona nashindwa kuelewa hapa, je kuna mahusiano yoyote kati ya ho waliowateka na Patrick?
FAUSTA: Kwa hilo mi sijui labda utamuuliza mwenyewe siku akirudi.
Wakiwa wanaendelea na maongezi wakamuona Anna, Patrick, Tusa na Sele kwakweli hawakuamini kuwaona waliwafurahia sana na kuwakumbatia kwa furaha.
Deborah alifurahi sana kumuona mwanae.
DEBORAH: Jamani Patrick mwanangu, ulikuwa wapi siku zote baba?
PATRICK: Nisamehe mama, ni historia ndefu sana.
DEBORAH: Unanipa presha na mawazo mwanangu kwanini jamani?
PATRICK: Nisamehe mama.
Patrick hakupanga kabisa kurudi kwao muda huo kwani hakutaka kukumbana na lawama za mama yake.
Pamela alilia kwakweli kwa muonekano wa mwanae aliyekuwa amefifia na kukonda zaidi.
Huku Deborah kichwa kikikosa kumuelewa vizuri Patrick.
Akamgeukia na Anna kumuuliza.
DEBORAH: Na wewe Anna siku zote hizi ulikuwa wapi?
ANNA: Nilisafiri kidogo dadangu, nisamehe sikukuaga. Siku niliyoona umepata nafuu ndipo nilipoamua kuondoka.
Wote wakawa wanafurahi sana kasoro Patrick ambaye alikuwa na mawazo mengine kichwani huku wengine kama Pamela, Fausta na Tina wakimpa pongezi kwa kazi aliyowafanyia.
Maiko aliwaona mshangao walioupata wakina Adamu na mama yake.
MAIKO: Kwani vipi, mnamfahamu huyo??
Wakaamua kukataa kwa kujigelesha lakini ukweli ni kuwa walishamfahamu.
ADAMU: Hapana hata hatumfahamu.
MAIKO: Basi huyo mwanamke ndiye nilizaa nae huyu mtoto.
ADAMU: Na mbona huishi nae tena?
MAIKO: Ilitokea tu tukazaa ila haikupangwa kabisa.
ADAMU: Mmh!! Haya bhana.
Wakaamua kufanya mipango ya kwenda kwa kina Deborah tena kwani Adamu alimuhakikishia Maiko usalama wake na jinsi atakavyoongea na wakina Deborah ili kuwaelewesha kuhusu Maiko, laiti kama angejua aliyowatendea na jinsi wanavyomchukia hata asingejisumbua chochote.
Deborah akaamua kumuita mwanae pembeni ili kuzungumza nae.
DEBORAH: Umekuwa polisi siku hizi mwanangu?
Patrick akashtuka na kuhisi kuwa lazima kuna kitu mama yake amekishtukia, Patrick akakataa kwa ishara ya kichwa.
DEBORAH: Kama wewe sio Polisi, umewezaje kuwaokoa wote wale toka mikononi mwa watekaji?
PATRICK: Mama jamani, si nimewaokoa tu. Kwani kuna ubaya au nimefanya vibaya?
DEBORAH: Hakuna ubaya na wala hujafanya vibaya, nia yangu ni kujua una mahusiano gani na hao watekaji?
Patrick alikosa jibu la kutoa.
DEBORAH: Patrick mwanangu, nimekulea katika misingi mizuri ya dini. Sikuwa na uwezo mkubwa ila nilihangaika na maisha kwaajili yako mwanangu. Au nilifanya kosa kukulea Patrick? Mbona umebadilika sana mwanangu?
PATRICK: Nadhani mama katika maisha yako yote huwa hujutii kunizaa ila unajutia kunilea, kwanini mama kwanini? Kama usingenilea wewe unadhani angenilea nani mama? Wewe ni mama yangu wa pekee, nakupenda sana mama. Sijawahi juta kuwa mtoto wako ila nafurahia siku zote kuwa na mama kama wewe, kwanini nawe usijivunie kuwa na mimi jamani?
DEBORAH: Hivi kuna mzazi yeyote anayeweza kujivunia kuwa na mtoto jambazi?
PATRICK: Jambazi? Nani kakwambia hayo mambo mama? Umenilea mwenyewe na nimekuwa nawe siku zote na unanitambua vizuri, je umeshawahi kuniona nikitenda hayo matendo mama?
DEBORAH: Sijawahi kukuona, ila sikia Patrick lisemwalo lipo. Kwanini wasimtaje mtu mwingine kuwa jambazi wakutaje wewe Patrick? Na una mahusiano gani na Maiko?
Patrick akashtuka na kujua mama yake Tusa atakuwa ameshasema umbea tu, akajikuta akisema,
PATRICK: Wanawake bhana.
DEBORAH: Unamaana gani Patrick?
PATRICK: Sina maana yoyote mama wamekupa umbea tu. Ila nakuomba mama uniruhusu nitoke kidogo tu.
DEBORAH: Halafu utarudi au?
PATRICK: Nitarudi mama.
Mawazo ya Patrick yalikuwa ni kwa Mwita tu, alitaka amuwahi Mwita kule kule kwa Maiko kabla hajaondoka ili akamkomeshe kwa kumbaka Tusa.
Mashaka alitafuta kundi la watu ambao aliwalipa pesa na kufanya nao zoezi, nia ikiwa ni moja tu kupambana na Maiko pamoja na Patrick kwani alijua kwa vyovyote vile lazima Patrick nae atakuwa anaendelea kuwatafuta tu.
"Hapa lazima nijipange maana Maiko kanisaliti halafu Patrick nae si mtu mzuri lazima nikawasambaratishe tu."
Mashaka alikuwa na hasira sana za kuachwa mwenyewe, alimuona Maiko kuwa hamfai tena kwani amemsaliti na pia amemuumiza moyo wake.
Akawa yupo na vijana aliowanunua na kuwapa mazoezi kwaajili ya watu wawili nao ni Maiko na Patrick ila haswaa Patrick kwani ndio anayemsumbua mawazo yake.
Wale wanajeshi waliompeleka Mwita mahali alipo Maiko walishaondoka muda mrefu sana, wakati wanazunguka njiani wakakutana na Patrick.
PATRICK: Mwita yuko wapi?
MJESHI: Tumemuacha kulekule.
PATRICK: Basi sawa hakuna tatizo.
Patrick aliendelea na safari yake kwenda kumfata Mwita huku akiwa na hasira sana juu yake.
Adamu na Maiko na bi.Rehema kama walivyopanga wanaamua kuondoka kwenda kwa Deborah kama walivyopanga.
MAIKO: Jamani au twende na huyu mwanangu, kwavile ni mwanajeshi nadhani atatusaidia busara huko tuendako.
ADAMU: Itakuwa vizuri kwenda nae.
Wakiwa wanashuka kwenye ngazi za hoteli na Mwita ili waelekee kwenye gari, kufika tu mapokezi Mwita akakumbuka kuwa ameacha kofia na picha ya mama yake kwenye chumba cha Maiko anawaomba arudi kuvifata, Maiko anamkabidhi funguo na kumwambia akirudi aziache mapokezi na wao atawakuta nje wakimngoja, halafu Mwita akaenda huko chumbani.
Akiwa ameshachukua vile vitu anamsikia mtu anagonga akajua labda ni wahudumu wa hoteli ile.
Akafungua mlango na kukutana na Patrick mlangoni huku akiwa na jazba mno.
 
SEHEMU YA 56


Akafungua mlango na kukutana na Patrick mlangoni huku akiwa na jazba mno.
Alichofanya Patrick ni kumkunja Mwita na kuingia nae vizuri mule ndani.
Mwita akashtukia anapewa ngumi ya sura.
MWITA: Jamani Patrick, kwani nimefanyaje?
PATRICK: Unaweza kunipa sababu ya kumbaka Tusa wewe?
MWITA: Nisamehe Patrick sikukusudi.....
Kabla hajamaliza akashtukia kapigwa ngumi nyingine na mambo yakaanza kuwa ovyo ovyo mule ndani.
Nyumbani kwa Deborah walikuwa wakimshangaa Tusa tu alivyonyorodoka.
DEBORAH: Pole sana Tusa, kwakweli nakuhurumia sana.
TUSA: Asante mama.
DEBORAH: Umekonda sana yani mvuto wako umepotea kabisa.
TUSA: Najuta kuolewa mimi, kwasababu nisingeolewa yote haya yasingenipata. Ningeendelea kuishi kwa furaha na Sele wangu, tazama sasa sitaweza kuishi na Sele tena roho yaniuma sana kwani Patrick ananitesa mimi.
DEBORAH: Jamani kwani Patrick anakufanyaje Tusa?
Tusa akainama na kuanza kulia, Pamela ikabidi nae aongee ya kwake.
PAMELA: Deborah, ungemuona huyu mwanangu alivyokuwa mwanzo kabla hajaolewa na mwanao hakika ungemuhurumia kwenye hiyo ndoa.
DEBORAH: Namuona hapa kama huyu binti amechoka sana, anatia huruma kwakweli.
Tusa aliendelea kuinama na kulia kwa uchungu. Pamela akamvuta Tusa na kusogeza kichwa cha Tusa kifuani mwake huku kiganja cha mkono kikimgonga gonga Tusa mgongoni mwake. Akaanza kusema kwa uchungu,
PAMELA: Tamaa ndio iliyotufanya tukuozeshe mama, tusamehe sie mwanangu.
DEBORAH: Kwani mlitamani nini kwa Patrick?
PAMELA: Hii yote ni tamaa ya pesa Deborah, mwanao alitulaghai na pesa zake wala sikufikiria upendo wa Tusa kwa Sele nilichotazama ni pesa aliyonayo Patrick. Ni kweli Patrick ametusaidia sana ila najilaumu kwa kumuangamiza mwanangu na pia kumnyima Sele haki yake.
TUSA: (Akainua kichwa), mama hii ni zaidi ya kuangamizwa yani natolewa mimba nne ndani ya mwaka mmoja!!
DEBORAH: Mimba nne?? Umetolewajwe?
Tusa akainama huku akiendelea kulia kwa uchungu, kwakweli Debora nae akamuhurumia Tusa. Alimtazama tatizo lake kwa uchungu.
Mashaka aliendelea kujipanga na alipatana na kijana mmoja mkorofi sana aliyejulikana kwa jina la Mporipori.
Huyu kijana alimpa moyo Mashaka wa kufanikisha kazi hiyo.
MPORIPORI: Usijari mkuu, je ungependa tuanze na yupi?
MASHAKA: Nadhani tukianza na huyu Patrick itakuwa poa zaidi maana huyu nae anataka kuniharibia mipango yangu kabisa. MPORIPORI: Hiyo ni kazi ndogo sana kwetu, ila sie huwa tunamaliza kabisa.
MASHAKA: Nyie mmalizeni tu maana huyo Patrick sitaki hata kumuona kwenye macho yangu.
MPORIPORI: Usijari mkuu, yani hapa kwetu hiyo ni kazi ndogo kabisa. Kwani huyo Patrick anakundi?
MASHAKA: Yuko peke yake hana kundi lolote, nahitaji mshughulike nae vizuri.
Mashaka akawakabidhi picha ndogo ya Patrick iliyokuwa kwenye kitamburisho ili iwe rahisi kumpata.
Wakina Maiko walimngoja sana Mwita pale chini lakini hakurejea, Maiko akataka kumfata Mwita ila Adamu akamzuia na kumwambia.
ADAMU: Wewe baki na mama hapa, ngoja niende mimi.
MAIKO: Kwanini uende wewe sasa?
ADAMU: Nina maana yangu, baki na mama hapo.
Adamu hakutaka kubaki yeye kwa kuhofia kumpoteza mama yake kama alivyompoteza Fausta na Pamela pale alipokuwa amesimama nao.
Ikabidi yeye ndio akaangalie huko chumbani kuwa Mwita amepatwa na nini.
Kufika nje ya chumba akasikia kama watu wanarumbana akaamua kuingia ndani akakutana na mpambano wa hali ya juu akajikuta akistaajabu kile kitu kilichokuwa kimetokea kwani alimkuta Mwita akiwa amezidiwa kabisa na Patrick, ikabidi aingilie kati.
Patrick aliyekuwa na hasira bado akamshindilia ngumi ya nguvu muamuliaji ambaye ndiye Adamu halafu akampiga teke lililofanya arushwe hadi mlangoni.
Adamu aliugulia sana, Patrick akamuacha Mwita aliyekuwa hoi kwa mkong'oto na kumfata Adamu ili apambane nae.
Akamfata pale chini na kumkunja, akampiga ngumi ya kwanza na kutaka kumuongeza nyingine za mfululizo, ile anataka kumshindilia ngumi nyingine tu sura yake ikamjia kuwa ni baba yake na Tusa. Patrick alishusha ile ngumi na kumuacha pale chini kisha akatoka nje haraka na kuondoka kwani tayari alishaona kitumbua kimeingia mchanga sababu alimkong'ota baba mkwe bila hata ya kumuangalia vizuri kuwa ni nani.
Ikabidi aende mahali kupumzika ili afikirie kwanza.
Deborah akamchukua Tusa ili kumuhoji vizuri kuhusu Patrick, ila Anna akaona kuwa hali ya Tusa si nzuri.
ANNA: Huyu binti atakuwa amepungukiwa na damu.
DEBORAH: Eti eeh!!
ANNA: Si unaona macho yake yalivyo meupe sana, halafu angalia ngozi yake ilivyopauka na kubabuka. Mwacheni niende nae hospitali kwanza.
DEBORAH: Hayo mambo ya utaalamu wengine hatuyajui. Wewe mpeleke tu huko hospitali.
Ikabidi Anna amwambie Tusa ajiandae na kuondoka nae kwenda hospitali.
Adamu akainuka pale chini na kwenda kumsaidia Mwita kuinuka pale alipo halafu akamkongoja na kutoka nae hadi nje, Maiko akashangaa kuwaona vile.
MAIKO: Nini kimewakumba jamani?
ADAMU: Kweli Mwanza kuna majangili, kuna jamaa ametudunda huyo si mchezo.
MAIKO: Poleni sana, kwani imekuwaje?
ADAMU: Hata sielewi kabisa, ila Mwita ndo kama hivi hali yake sio nzuri kabisa.
MAIKO: Basi tumpelekeni hospitali.
ADAMU: Itakuwa vyema.
Mwita hakuweza hata kuongea kwani aliumizwa vibaya mno.
Adamu alikuwa akijifikiria tu kuhusu kijana aliyewapiga, sura yake ikamjia kichwani mara kwa mara ila hakujua ni nani. Akajiuliza vitu vingi kuhusu yule kijana, hadi akajikuta akiropoka.
"Nadhani atakuwa gaidi yule"
MAIKO: Nani huyo?
ADAMU: Dah! Yani yule kijana kanichanganya balaa. Yule kijana aliyetupiga atakuwa mafia tu.
Adamu hakuacha kumfikiria na sura ya Patrick haikuacha kumtoka usoni.
Mashaka na Mporipori wakiwa wanakatisha eneo fulani wakamuona Patrick njiani.
MASHAKA: Kijana mwenyewe ni yule pale.
MPORIPORI: Kumbe ni yule, ngoja nishuke nimfatie.
MASHAKA: Hapana, tuwaite na wale vijana watano usaidiane nao.
MPORIPORI: Haina haja, yule namdhibiti mwenyewe kwa dakika mbili tu.
MASHAKA: Ila kuwa makini.
MPORIPORI: Usijali bosi, mimi ndio Mporipori bhana.
Mporipori alijiaminia zaidi kwajinsi mwili wake ulivyojaa na misuli mingi kwahiyo alimuona Patrick ni kijana wa kawaida tu ukilinganisha na vijana wengine aliowahi kupambana nao.
Mporipori akashuka kwenye gari na kuanza kumfata Patrick alipo.
 
SEHEMU YA 57


Mporipori akashuka kwenye gari na kuanza kumfata Patrick alipo.
Mporipori akamsogelea Patrick kisha akamshika bega, Patrick akageuka kuona ni nani aliyemshika bega, alipoona ni mtu asiyemfahamu akaamua kuendelea na mawazo yake.
MPORIPORI: Oya dogo vipi, mbona una dharau?
Patrick akamshangaa Mporipori na kumuuliza.
PATRICK: Nina dharau unanijua?
MPORIPORI: Swala la kukujua mi halinihusu ila kwa kifupi mi naitwa Mporipori.
PATRICK: Aah kumbe!! Na mimi naitwa msitunisituni.
MPORIPORI: Naona una kiburi sana dogo.
PATRICK: Kwani wewe shida yako nini?
MPORIPORI: Shida yangu ni wewe.
PATRICK: Kivipi?
Kwavile sehemu yenyewe ilikuwa imetulia na si sehemu ya kupitiwa na watu sana, Mporipori akaona ile ni sehemu nzuri ya kumkomesha Patrick.
Wakati wakiendelea kuongea huku Patrick akimshangaa mtu huyu, Mporipori akaandaa kumi matata ya kumshindilia nayo Patrick, akainua kumi hiyo ili ampige nayo usoni ila kabla haijafika Patrick akaudaka ule mkono wa Mporipori.
Patrick hakutaka kupoteza muda, akampiga teke tumboni na kumshindilia na kiwiko mgongoni.
Mporipori akapatwa na hasira za kupigwa na mpambano ukaanza vizuri, Mporipori alipambana na Patrick kwaajili ya pesa ila Patrick aliamua kumalizia hasira zake zote za siku hiyo kwa Mporipori.
Patrick alimsukuma kwa nguvu Mporipori hadi akaanguka chini halafu akaruka juu na kumuangukia kwa kumkanyaga tumboni hadi Mporipori akatapika damu kwa mara ya kwanza, Patrick akamshika shingo na kumshambulia kwa ngumi za sura, kisha akamuuliza.
PATRICK: Nani kakutuma kwangu?
Mporipori alikuwa kimya kabisa.
PATRICK: Hunijibu eeh!! Sasa utanijua vizuri na utajua kwanini umetumwa badala ya muhusika kuja mwenyewe.
Mporipori alikuwa hoi kabisa.
Patrick akampigia simu Yuda kuwa ampelekee bodaboda yake.
Mwita akapelekwa hospitali na kwavile alikuwa na sare za jeshi haikuwa ngumu kumuhudumia.
Wakati Mwita akihudumiwa Maiko, Adamu na Rehema walikuwa mapokezi wakingoja kusikia anaendeleaje.
REHEMA: Huyo aliyewapiga lazima atakuwa jambazi tu.
ADAMU: Hata mimi nahisi ni hivyo yani hadi kichwa kinaniuma, sijawahi kumuona mtu anayepiga kiasi kile live. Dah ilikuwa ni mara yangu ya kwanza, yule kijana ni muuaji jamani.
REHEMA: Ila nani aliwasaidia?
ADAMU: Aliondoka yeye mwenyewe. Hata simjui kwakweli labda akipata nafuu huyo anaweza akawa anamjua.
Maiko alipatwa na hofu kuwa huenda kijana huyo ni Patrick ila akashindwa kuelewa uhusiano wa Patrick na Mwita na je wamefahamiana vipi.
Yuda akamfata Patrick mahali alipoelekezwa, Yuda akamshangaa yule Mporipori pale chini.
YUDA: Kaka umelikong'ota hili jitu?
PATRICK: Kwani unamjua?
YUDA: Namjua ndio, anaitwa Mporipori ni mkorofi na anaogopewa balaa.
PATRICK: Basi hakuna shida.
Patrick akachukua kamba na kuifunga kwenye boda boda halafu akaenda kumfunga Mporipori mikono, halafu akaenda kupanda kwenye bodaboda na kuanza kuendesha.
YUDA: Unataka kufanya nini kaka?
PATRICK: We ngoja hapohapo utaona tu.
Akaendesha ile bodaboda huku Mporipori akiburuzwa nayo.
Yuda aliendelea kumngoja, baada ya muda Patrick alirudi mwenyewe na bodaboda yake bila ya Mporipori, halafu akamwambia Yuda apande ili waondoke.
YUDA: Kwani umeenda kumfanyaje kaka?
PATRICK: Nimeenda kumuacha porini, yeye si ndio mporipori bhana basi kwake ni porini.
Ingawa Yuda alimchukia Mporipori ila hakufikiria kama Patrick atafanya alichofanya.
Mashaka alikimbia na gari yake baada ya kuona Mporipori anadundwa, ikabidi aende kuwatafuta wale vijana watano ili wakasaidiane na Mporipori.
Wakashangaa walipofika pale hawakuona mtu yeyote ila wakaona kama kuna kitu kilikuwa kimeburuzwa, wakaamua kufata ile alama ili wajue ni nini.
Wakamkuta Mporipori ametundikwa juu ya mti, kila mmoja alistaajabu na wote wakashangaa kuona Mporipori apigwe na mtu mmoja.
"Bosi unahakika kuwa huyo mtu alikuwa mmoja kweli?"
MASHAKA: Ndio ni mmoja ila ni mtu khatari sana.
Ikabidi wamshushe Mporipori aliyekuwa hajitambua na kachubuka mwili mzima sababu ya kuburutwa.
Yuda na Patrick wakiwa kwenye bodaboda wanamuona Anna akivuka barabara, wanaamua kusimamisha na kumfata.
YUDA: Vipi tena mamdogo?
ANNA: Bora hata nimewaona, hivi nilitaka kurudi nyumbani. Nilikuja na Tusa hospitali ila amelazwa.
PATRICK: Amelazwa?
ANNA: Ndio, amepungukiwa na damu. Inabidi aongezewe, sasa nilitaka kwenda nyumbani kuwaambia.
PATRICK: Haina haja mamdogo, mi nitamuongezea kwani damu yangu ni grupu o.
ANNA: Sawa basi twende hospitali, ila Yuda nenda nyumbani kawape taarifa.
Basi Patrick na Anna wakaenda hospitali na Yuda akarudi nyumbani.
Deborah na wenzie walibaki kustaajabu.
DEBORAH: Huko hospitali hawarudi jamani?
PAMELA: Hata na mimi nashangaa maana muda umepita sana.
DEBORAH: Hata tukisema tuwafatilie tutaenda hospitali gani?
PAMELA: Mmh!! Kazi ipo jamani.
Mara Yuda akafika na kuwapa taarifa kuhusu hali ya Tusa wote wakabaki wakishangaa tu.
Pamela na Deborah wakajiandaa kwaajili ya kwenda huko hospitali.
Adamu aliyekuwa na wenzie kumuangalia Mwita, akaamua awachomoke kidogo kwenda kuvuta sigara, hakupenda kuvuta mbele ya mama yake.
Kwahiyo akaenda upande mwingine wa hospitali hiyo, mara akaomuona Anna akikatisha nae akamshangaa na kujiuliza anafanya nini, ikabidi amuite kumuuliza.
Kila mmoja alimshangaa mwenzie, Anna akamueleza Adamu kuhusu Tusa, hapohapo Adamu akatupa na sigara chini akiwa na lengo la kwenda kumuona mwanae.
ANNA: Kwa bahati nzuri mumewe kajitolea kumtolea damu.
ADAMU: Nadhani huyo kijana atakuwa na roho nzuri sana.
Wakaenda hadi alipolazwa Tusa na pembeni alikuwepo Patrick.
Adamu alipomuona Patrick alijikuta akisema
"Mungu wangu!!!"
 
SEHEMU YA 58


Adamu alipomuona Patrick alijikuta akisema,
"Mungu wangu"
Akamuangalia kwa makini, Patrick nae akainamisha kichwa chini kumuona baba yake na Tusa.
Adamu akamgeukia Anna na kumuuliza tena,
ADAMU: Umesema yule kijana ni nani?
ANNA: Khee!! Kwani humjui? Yule ni mume wake Tusa anaitwa Patrick.
ADAMU: Hapana, yule ni jambazi.
Adamu akaangalia tena pale alipokuwepo Patrick ila hakumuona tena.
ANNA: Jambazi!! Kivipi?
ADAMU: Si unaona kakimbia.
ANNA: Hajakimbia bhana, utakuwa umemfananisha tu.
Adamu na Anna wakamsogelea Tusa pale kitandani ila hawakuweza kumuona Patrick alipoelekea ingawa nae alikuwa hapo kitandani mwanzoni tu wakati wanaingia walimuona.
Mashaka akawa na lile kundi lake wakimuhudumia Mporipori.
Timmy akaanza kuwaambia wenzie.
TIMMY: Jamani huyo Patrick nadhani amechokoza moto, hata tusimuachie yani kampiga Mporipori kiasi hiki!!
DANK: Hata na mimi nimechukia sana, hapa hata tusikubali.
MASHAKA: Kama mpo tayari kupambana nae basi nitawaelekeza cha kufanya au pa kumpata.
TIMMY: Huo ndio mpango mzima, halafu nitaenda kumkodi jamaa mmoja hivi anaitwa Jangili lazima atammaliza tu huyo Patrick.
DAVID: Nilijua tu Timmy lazima ulete habari za kumkodi mtu ila mimi huko simo.
DANK: Inamaana hutaki kulipa kisasi David?
DAVID: Nilipe kisasi kwa lipi?
TIMMY: Si kampiga Mporipori, huo unaotaka kufanya David ni uoga wa kike. Usituzingue wala nini. Hata ukikataa wewe hutupunguzii kitu.
Mpango ukaanza kupangwa sasa, mpango wa kumpata Patrick na kulipiza kisasi.
Sele alitoka kwao na kwenda nyumbani kwa Deborah kumuona Tusa.
TINA: Tusa yupo hospitali, amelazwa.
SELE: Duh! Hayo majanga sasa. Hebu nambieni na mie niende.
MARIUM: Ila usiku umeshaingia Sele bora uende kesho.
SELE: Yani mama nilale bila kumuona Tusa!! Hapana siwezi mama lazima nikamuone, nimetoka nyumbani kuja hapa kumuona halafu nilale bila kumuona, siwezi.
MARIUM: Huyo Tusa mwanangu atakuingiza kwenye matatizo jamani, wewe ni Tusa, Tusa na wewe. Kumbuka yule ni mke wa ndugu yako tayari.
SELE: Ndio Tusa kaolewa na Patrick, ila siwezi kuacha kumpenda Tusa kwakuwa yeye ndiye mwanamke nimpendae.
MARIUM: Mapenzi yatakuua wewe mwanangu dah!!
Sele hakusikiliza chochote zaidi ya kwenda kwenye hospitali aliyoambiwa.
Marium alibaki kumsikitia tu mwanae.
FAUSTA: Watoto hawasikii Marium, huwa tunawaacha wafanye watakavyo maana na wao washakuwa wakubwa.
MARIUM: Yani Fausta wee acha tu, wananipa presha hawa watoto balaa. Mji wenyewe huu ushaharibika halafu yeye anang'ang'ania kwenda hospitali usiku huu, bora hata wakina Deborah wapo na Yuda sasa yeye peke yake dah!!
Patrick alitoka nje ya hospitali kwanza kwavile hakuwa na la kumwambia mkwe wake huyo.
Deborah na Pamela na Yuda wakafika alipolazwa Tusa.
Wakamkuta Adamu mahali hapo.
DEBORAH: Hivi wewe mwanaume una akili?
ADAMU: Deborah sipendi matusi.
DEBORAH: Swali na jibu tofauti, sijakutusi hapa. Mama yuko wapi?
ADAMU: Unatakiwa uniulize kistaharabu sio unafokafoka tu.
PAMELA: Ila kweli Adamu, mama umempeleka wapi unajua unatuweka roho juu jamani.
ADAMU: Yule ni mama yangu mimi, nyie roho juu za nini?
Nesi akaingia wodini na kuwaambia kuwa muda wa kutazama wagonjwa umepita kwahiyo labda warudi kesho yake.
Ikabidi Yuda awarudishe Pamela na Deborah maana Anna alijitolea kulala na mgonjwa pale hospitali.
Wakina Deborah wakarudi nyumbani huku Pamela akiuliza,
PAMELA: Mbona mdogo wako amekataa nisibaki mimi na amebaki yeye?
DEBORAH: Anna anapenda sana kuhudumia wagonjwa hata usishangae mwaya.
Marium nae akawauliza kama wamemuona Sele.
MARIUM: Vipi mmekutana na Sele njiani?
DEBORAH: Hata hatujamuona kwani nae ameenda?
MARIUM: Ndio.
DEBORBH: Basi hatujamuona.
Marium akaingiwa na mashaka ikabidi amwambie Yuda ajaribu kuwasiliana na waliopo hospitali kama watamuona Sele.
Wanajeshi Singida nao waliendelea na upelelezi wa hali ya juu kuhusiana na vifo vya ajabu na gafla vya wanajeshi hao sita.
Upelelezi uliendelea ndani na nje ya mkoa ila walishindwa kumuhisi mtu yeyote. Safari hii wakaamua kufanya upelelezi wa kimya kimya ili waone kama watagundua chochote kuhusu yale mauaji ya aina moja.
Patrick alikuwa maeneo yale yale ya kuzunguka hospitali, hakuenda mbali ili apate urahisi wa kumuona Tusa.
Kwahiyo alikuwa akizunguka maeneo ya pale pale huku akitafakari mambo mbalimbali haswaa swala zima la Adamu kutaka kumuokoa Mwita, alijiuliza sana wamejuana vipi.
Sele nae hakuwa akipoteza muda kwani alifanya safari ya haraka haraka ili aweze kufika mapema hospitali ila kwa bahati mbaya bodaboda aliyokodi ilipoteza muelekeo na kuwafanya waanguke kwahiyo Sele alijikuta akiumia na kuchubuka, ila aliinuka pale na kuendelea na safari yake ya hospitali.
Alipofika ilikuwa muda umeenda sana, akakaribia eneo la hospitali ile anataka kuingia tu akashangaa mtu akimkaba roba kwa nyuma na kumwambia
"Nimekutafuta kwa muda mrefu sana wewe kijana"
Sele akashangaa kwani hajawahi kuwa na bifu na mtu yeyote katika maisha yake na ubaya ni kuwa hata ile sauti yenyewe hakuitambua kabisa.
Yule mtu alikazana kumkaba Sele.
 
SEHEMU YA 60


Patrick alifika pale akiwa amegubikwa na hasira kali kwani mama yake alimpenda sana.
Patrick aliwarukia juu na kuwapiga mateke wale watu wawili waliokuwa wamemshikilia Deborah, kitendo hicho kiliwafanya waanguke chini na wamuachie Deborah.
Anna na Pamela walikuwa wakitetemeka tu, Patrick akawafata pale chini na kuanza kuwapa kipondo tena kwa kumuinua mmoja juu na kumtupia kwa mwenzake, waliumia sana kwa kitendo hicho.
Wale waliokuwemo ndani ya gari wakataka kufungua mlango na kukimbia ile wanafungua mlango tu Patrick akabamiza mlango ule wa gari, akasikika Pamela akipiga kelele.
PAMELA: Kuna Tusa humo.
Patrick alimvuta Tusa aliyekuwa ameshikiliwa na Timmy, wakati Patrick akishughulika na wa kwenye gari, Sele nae aliendelea kushughulika na wapale chini ingawa nae tayari alikuwa na maumivu yake mengi tu.
Patrick alimpiga Timmy ngumi moja ya shingo iliyomfanya ahisi kama vile shingo inatoka na kujikuta akianguka chini na kumuachia Tusa, huyu mwingine alitaka kukimbia ila Patrick akamuwahi kwa kumpiga mtama wa nyuma uliomfanya aanguke kifudifudi halafu Patrick akainua mguu wake na kumpiga nao kwa nguvu mgongoni na kisha kumshindilia na ngumi, yule kijana alijikuta akitoa tu damu mdomoni.
Patrick akamgeukia Sele na kumwambia kuwa awachukue wakina Tusa awarudishe nyumbani.
Sele akaenda kuwafata kuwa waondoke ila Deborah akagoma, mwanae akamuomba aondoke, Deborah akakubali kwa shingo upande.
Sele akaondoka nao na kwenda kukodi gari, kufika njiani Deborah akang'ang'ania kushuka, Sele akamzuia ila ikashindikana ukizingatia Sele nae alikuwa ni mgonjwa kwahiyo hakuwa na nguvu kivile za kuweza kumzuia Deborah, ikabidi wamuache ashuke na wao kurudi nyumbani.
Mwita aliendelea vizuri kwasasa, ila Adamu nae aliendelea kumshangaa Mwita kuwa kwanini ameficha kuhusu huyo jambazi.
ADAMU: Hivi kwanini Mwita kwanini?
MWITA: Yule ni mtu wangu wa karibu sana siwezi kumteketeza ukizingatia yeye ndio aliyenionyesha baba yangu.
ADAMU: Ila alikupiga sana na mimi alinipiga.
MWITA: Msamehe bure tu, yule alikuwa na hasira na mimi.
ADAMU: Kwani umemfanyeje?
MWITA: Aah! Mambo ya ujana tu, vipi ile safari ipo au mmeihairisha?
ADAMU: Ipo, tena nimefurahi kuona binti yangu nae amesharuhusiwa kurudi nyumbani tukienda huko utamjua.
MWITA: Itakuwa vizuri kwakweli maana ndugu zangu siwajui kabisa.
Adamu akaamua kwenda kuongea tena na Maiko kuhusu ile safari.
Patrick aliendelea kutembeza dozi ya kichapo kwa wale vijana hadi akili ikawakaa sawa, akamshika Timmy na kumkaba ili ataje aliyewatuma. Mwanzoni Timmy hakutaka kusema ukweli ila kwa maumivu ikabidi aseme kuwa ni Mashaka.
PATRICK: Mashaka, Mashaka nadhani kuna kitu anahitaji kwangu. Haya niambie alipo Mashaka.
Timmy aliendelea kutetemeka huku akisema alipo Mashaka.
Wakati Patrick akiendelea kumuhoji Timmy, mara kijana mmoja pale chini aliinuka na kuchukua jiwe ili ampige nalo Patrick, ila Patrick akagundua kabla na kukwepa, na lile jiwe likaenda kumponda Timmy.
Patrick akamuacha Timmy na kwenda kumshughulikia aliyetupa jiwe, akampa teke la maana lililomfanya hadi apoteze fahamu.
Patrick akawakusanya na kuwaingiza kwenye gari, akachukua kiberiti ambacho huwa anatembea nacho halafu akafunua tanki la mafuta kwenye gari ili awashe moto ambao utawaua taratibu wakina Timmy ndani ya gari.
Ile anataka kuwasha tu akasikia sauti nyuma ikiita,
"Patrickkkkkkk........"
Patrick akageuka nyuma haraka na kukuta mtu amebeba kisu akitaka kumchoma, Patrick akapambana na mtu yule na kumchoma na kisu chake mwenyewe, kisa akamnyanyua na kumrushia kwenye gari walipo wenzie. Halafu akachukua kiberiti chake ili awashe moto.
Mara akamuona mama yake akimsogelea na kumuita kwa hofu.
DEBORAH: Patrick!!
PATRICK: Mama!!
DEBORAH: Mwanangu.
Halafu akamfata na kumkumbatia.
PATRICK: Mama unafanya nini hapa?
DEBORAH: Nimekufuata mwanangu, umepona kweli?
Deborah akawa anampapasa papasa mwilini Patrick kuangalia kama kweli amepona kwani ni yeye aliyepiga kelele ya kumshtua baada ya kuona mtu aliyeshika kisu nyuma ya Patrick.
PATRICK: Usijari mama yangu, mimi ni mzima.
Patrick akageuka ili achome lile gari, Deborah akamzuia.
DEBORAH: Tafadhari mwanangu tafadhari, najua wewe si muuaji. Ulichofanya kinatosha, naomba tuondoke baba. Nisikilize mwanangu.
Patrick alimuangalia sana mama yake aliyeonyesha kumpenda sana, akajikuta akifata pikipiki yake na kumpakia mama yake kisha akapanda na wakaanza safari ya kwenda kwao.
Mashaka aliyekuwa amewatuma vijana wake akashangaa kuona wamekawia kurejea, ndipo alipomtuma kijana aliyebaki David ili akawaangalie kuwa labda wamekwama njiani, ndio yule kijana aliyefika na kuchomwa na kisu chake mwenyewe.
Mashaka alitafakari sana kuona watu wake hawajarejea, akajiuliza maswali mengi bila ya majibu.
"Au wamekutana na Patrick? Inamaana Patrick ndio kawapiga vijana wote wale peke yake mmh!! Labda huyu Patrick si mtu jamani. Ila nitampata tu yani hadi biashara zangu zimesimama kwaajili yake!! Dah! Huyu Patrick ni hatari"
Mashaka aliwaza mengi sana kuhusu Patrick na namna ya kumpata.
Adamu akamueleza Maiko kuhusu ile safari ya kwenda kwa Deborah.
MAIKO: Tatizo langu kubwa ni moja tu kumdhibiti mtoto wa Deborah, je tutaweza?
ADAMU: Kwani ana nini huyo mtoto wa Deborah?
MAIKO: Inamaana humjui?
ADAMU: Simjui kwakweli na hata sijui kama Deborah ana mtoto.
MAIKO: Basi ana mtoto matata sana, mtoto asiye na shukrani kabisa. Ila tutaenda hivyo hivyo naamini busara za mama zitafanya kazi.
ADAMU: Kwavile umeamua kwenda kuwaomba msamaha basi itakuwa ni vizuri.
Wakapanga kuwa kesho yake ndio waende nyumbani kwa Deborah.
Patrick na mama yake walifika nyumbani, Deborah alikuwa akitafakari tu jinsi Patrick alivyokuwa anapigana, akajikuta akijisemea
"Au jambazi kweli?"
Kumbe Patrick alimsikia na kumuuliza
PATRICK: Nani jambazi mama?
DEBORAH: Mmmmh aaaah hata sijui ni nani nimejisemea tu, ni wale vijana waliotuteka.
Patrick aliona kama vile mama yake ana kiwewe tu. Akaenda chumbani kwake na kuendelea kutafakari kuhusu Mashaka. Ingawa alishajua alipo ila hakutaka kuondoka siku hiyo ili kuepusha kuhisiwa vibaya na mama yake.
Deborah hakuacha kutafakari yale mapigano ya Patrick.
Marium ilibidi aondoke na Sele ili akapate kutibiwa vizuri yale majeraha ya ajari aliyopata.
Patrick alikuwa chumbani kwake akitafakari vitu vingi hasa upendo wa mama yake kwake.
"Dah! Mama yangu ananipenda sana, sijui kwavile mimi ni mtoto wake wa pekee au ni mapenzi yake tu kwangu!! Nadhani hapa duniani ni mama tu anayenipenda"
Patrick alikuwa akijaribu kuangalia lile tukio la mama yake kurudi wakati anapambana, ingawa hakupenda kumuona mama yake pale ila kwa upande mwingine alifurahia kuona anapendwa vile na mama yake.
"Natamani Tusa nae angenipenda japo kidogo tu, najua hawezi fikia upendo wa mama basi hata angenipenda kidogo tu ningefurahi sana"
Mara akasikia mtu akigonga mlango wake.
Patrick akatoka na kumkuta Tusa mlangoni.
PATRICK: Tusa!!
TUSA: Asante sana Patrick kwa kuniokoa.
Patrick alitabasamu hadi hakuamini ile shukrani aliyoitoa Tusa.
Kama walivyopanga Rehema, Adamu, Maiko na Mwita walienda nyumbani kwa Deborah.
Wakashuka kwenye gari huku Maiko akiwa na tahadhari kubwa ya kukutana na Patrick.
Anna aliyekuwa anafagia, ile kuwaona tu macho yake moja kwa moja yalienda kugonga sura ya mtu mmoja tu, akajikuta akiangusha fagio chini na kusema kwa mshangao,
"Maiko!!"
Deborah aliyekuwa anatoka ndani akashangaa sana, kilichomshangaza ni kuwa Anna amemjulia wapi Maiko.
 
SEHEMU YA 61


Deborah aliyekuwa anatoka ndani akashangaa sana, kilichomshangaza ni kuwa Anna amemjulia wapi Maiko.
Deborah akamsogelea Anna na kumuuliza.
DEBORAH: Umemjulia wapi huyo mdogo wangu?
Anna alizidi kumuangalia Maiko kwa hasira hadi pale alipomuona Mwita akajikuta akimkimbilia na kumkumbatia,
ANNA: Jamani Frank, umemtolea wapi huyo shetani?
Frank nae akawa amemkumbatia Anna bila ya kusema chochote.
Deborah akaenda mlangoni kwake.
DEBORAH: Sidhani kama itakuwa busara kwa wewe Maiko kuingia humu ndani kwangu.
REHEMA: Hana nia mbaya Deborah, amekuja ili muweze kumsikiliza japo kidogo tu.
Deborah aliwaangalia sana na kuona kuwa hawajamuelewa tu, akaamua kuwaachia mlango wapite ili wajuane humo ndani.
Halafu Deborah akaamua kwenda kumuita Patrick ili aone kama kweli Patrick na Maiko wanaukaribu wowote.
Fausta na mwanae Tina siku hiyo walienda hospitali kwaajili ya uchunguzi wa hapa na pale, Fausta alitaka kujua maendeleo yake na kuonekana kuwa anaendelea vizuri na kumpima mwanae Tina, walifanya safari hii ya hospitali wakiwa wamesindikizwa na Yuda.
Tina nae alipopimwa akagundulika kuwa anaujauzito, Tina alishtuka sana na kuanza kulia, mama yake akawa anambembeleza.
TINA: Mama sitaki mimba ya kubakwa mimi sitaki kabisa.
FAUSTA: Nyamaza mwanangu, kumbe ulibakwa! Mbona hukusema mama?
TINA: Niliona aibu mama, nilibakwa na wanaume mashetani tena walinibaka kwa kupokezana. Mama sitaki hii mimba sitaki mama.
Yuda nae akasikia na kuwasogelea.
YUDA: Mimba? Nani ana mimba tena hapa?
Tina alizidi kulia na kushindwa kujielezea.
FAUSTA: Yani hapa ni tatizo juu ya tatizo jamani, sijui hata tufanyeje!
YUDA: Tina ana mimba au?
FAUSTA: Ndio, Tina ana mimba.
YUDA: Aaah!! Hapana kwakweli nasema hapana jamani yani.... Aaah! Hapana.
Tina alizidi kulia pale alipoinama.
FAUSTA: Mwanangu, haya mambo twende tukayajadili nyumbani hapa hospitali hatutaelewa cha kufanya. Twende nyumbani ili tuweze kupata maamuzi sahihi.
YUDA: Sikuzote nampenda Tina na sijawahi mlazimisha kufanya nae kitu chochote kumbe wenzangu walikuwa wanajibakia!! Aaah! Imeniuma sana.
FAUSTA: Najua kama inauma, ila turudi nyumbani kwanza jamani. Kwani mimba kitu gani bhana, cha muhimu kwasasa ni uhai. Twendeni nyumbani tukajadili.
Tina alijawa na machozi tu usoni, wakaamua wafanye safari ya kurudi nyumbani.
Marium alipotoka kumsindikiza mwanae Sele hospitali na kurudi nyumbani.
SELE: Mama, nataka kwenda kumuona Tusa.
MARIUM: Hivi mwanangu, unajua huyo mwanamke atakuu wewe!!
SELE: Hawezi kuniua mama tunapendana sana.
MARIUM: Hata kama mnapendana mwanangu, kuna kipindi kwenye mapenzi ni bora kusema inatosha sasa. Wanawake wangapi hapa mtaani wanakupenda mwanangu? Kuna wakina Sara na Maria, wanatamani hata leo utamke kuwa unawahitaji ila hawapati hiyo nafasi. Yani wewe na ndugu yako mnamng'ang'ania Tusa kama vile yeye ndiye mwanamke pekee duniani.
SELE: Mama, hao unaowasema wananipenda hawawezi kuwa kama Tusa. Nampenda sana Tusa na pia najua kuwa Tusa ananipenda, sina nia ya kumpora Tusa kwa Patrick kwasasa ila najua penzi la kweli halifi mama haijalishi nini kitatokea.
MARIUM: Penzi la kweli halifi labda kwa mwanamke na mwanaume wa kizungu ila sio sisi wenye ngozi nyeusi, tumeumbiwa tamaa na hatuna hiyo kitu mapenzi. Tusa angekupenda kweli asingekuwa na Patrick.
SELE: Inamaana wewe mama hukumpenda baba?
MARIUM: Mimi na baba yako tulipendana kweli ndomana tukadumu ila huyo Tusa hakupendi acha kujidanganya mwanangu.
Sele aliyatafakari maneno ya mama yake ila kwajinsi alivyokuwa anampenda Tusa yale maneno hayakumkaa kichwani hata kidogo.
SELE: Hivi mama unajua mimi nilimngoja sana Tusa, tangu anasoma hadi alipomaliza kama kunisaliti si angenisaliti kipindi kile jamani!
MARIUM: Hebu acha ulimbukeni wa mapenzi mwanangu, Tusa kashakuwa skrepa pale alipo. Mwanamke gani yule sasa, mimba nne ndani ya mwaka mmoja halafu wewe bado upo na msemo wa kumpenda!! Acha ujinga mwanangu, Tusa hakufai tena muachie tu Patrick maradhi yake yale. Yule Tusa pale alipo spana mkononi bora akae na Patrick atasaidiwa na pesa sasa kwako si atajifia tu? Acha kung'ang'ania mitumba iliyochoka mwanangu.
Sele akamuangalia sana mama yake halafu akaondoka, Marium akabaki akijisemea,
"Sijui karogwa jamani mwanangu mmh!! Mapenzi mabaya sana ukiyaendekeza."
Patrick alipokuwa akizungumza na Tusa pale mlangoni akaona itakuwa vyema sana kama wakikaa chumbani, kwahiyo akamuomba Tusa akae nae chumbani.
PATRICK: Kwanza pole sana Tusa kwa yote yaliyokupata, umebadilika sana Tusa yani umekuwa tofauti kabisa kama vile sio wewe niliyekuona facebook.
TUSA: Umenipitisha mapito ambayo sikuwahi kuyawaza maishani mwangu, umenifanya niwe mtu wa kilio na mateso. Nimebaki mwanamke picha tu ila si mwanamke kama nilivyotamani kuwa.
PATRICK: Naelewa Tusa ila yote hayo kwavile hukupenda kunielewa vile ninavyokupenda Tusa.
TUSA: Ubaya ni kuwa hata wewe hukupenda kunielewa kama sikupendi Patrick, umetumia nguvu nyingi na pesa nyingi sana kwaajili yangu Patrick ila kila nikitafakari yaliyopita nakuweka wewe kwenye kundi la wanaume wenye roho mbaya, ila kwasasa umenisaidia sana Patrick sinabudi.....
PATRICK: Hunabudi nini? Niambie Tusa, hunabudi kuniambia kuwa wanipenda?
Mlango wa Patrick ukagongwa ikabidi aende kufungua na kumkuta mama yake akigonga.
DEBORAH: Kuna wageni sebleni naomba twende ukaongee nao.
PATRICK: Nije na Tusa?
DEBORAH: Ndio njoo nae tena yeye anahusika zaidi.
PATRICK: Wageni gani hao mama?
DEBORAH: Nyie njoeni tu mtawaona.
PATRICK: Sawa mama tunakuja.
Ikabidi Patrick amwambie Tusa kuwa waende.
PATRICK: Halafu tutarudi kuzungumza vizuri sawa Tusa?
TUSA: Sawa, hakuna tatizo.
Patrick na Tusa wakatoka chumbani na kwenda sebleni.
Mashaka alikuwa na mawazo tu baada ya kuwakuta wale vijana wake wakiwa na hali mbaya sana, ikabidi aamue kusafiri na kwenda Arusha kuchukua baadhi ya vijana wao kwaajili ya Patrick.
Kule Arusha walimshangaa sana Mashaka kwani mawazo yalianza kumkondesha, Tulo ndio aliyempokea kwani ndio aliyeachwa kwenye himaya ya Maiko kwa muda.
TULO: Kwakweli tumeshangaa sana, kimya kirefu kwani huko Mwanza kuna tatizo gani?
MASHAKA: Mwanza hakuna tatizo ila Patrick amekuwa tatizo kubwa sana kwetu, Patrick ameua vijana wengi tu. Kwakifupi Patrick hafai, inabidi kujipanga kweli ili kwenda kupambana nae hata sijui Patrick amejifunzia wapi yale mambo ya mapigano.
TULO: Itakuwa China tu, ila Patrick inatakiwa tumuendee taratibu. Unajua yule jamaa ni jasiri sana halafu yupo kamili kila idara. Ngoja tufanye maamuzi ya taratibu tutampata tu.
MASHAKA: Tatizo muda, kazi nyingi zimelala kwaajili yake.
TULO: Hakuna tatizo, mi namjua Patrick vizuri niachie hiyo kazi kwa muda utaona majibu yake.
Mashaka akazungumza mengi na Tulo huku akiwaza hasara alizopewa na Patrick.
Patrick na Tusa walienda sebleni, Patrick ile anatokeza akabambana na sura ya Mwita, kuangalia pembeni anamuona Maiko halafu akamuona Adamu hapo akanywea na kurudi kwenye korido haraka.
TUSA: Mbona umerudi nyuma gafla?
PATRICK: Aaah! Hata sielewi.
TUSA: Twende bhana, hivi hadi wewe Patrick unakuwa na aibu kwa wageni? Twende bhana.
Patrick akaona njia bora ni kujifanya kuwa wote wale hawafahamu, kwanza aliona Maiko ni longolongo tu pale alitamani akutane nae kwenye anga zake amfundishe adabu.
Patrick na Tusa wakajitokeza, na kitendo cha kwanza ni Tusa kumkimbilia baba yake na kumkumbatia huku machozi yakimtoka ilikuwa ndio anamuona kwani kule hospitali wakati Adamu alienda kumtazama alikuwa amelala.
TUSA: Jamani baba, nimefurahi kukuona baba.
Patrick alikaa na kuwasalimia kama vile watu asiowajua halafu akainuka na kutoka nje, Deborah akawa anastaajabu kuona hali ile na kujiuliza kuwa inamaana hawajuani kweli na Maiko.
Wakati Patrick alipokuwa anatoka nje akakutana na Sele mlangoni wakasalimiana halafu Sele akaingia ndani.
Patrick alikaa pale nje akitafakari uwepo wa Maiko mule ndani na kitu gani akamfanye mara gafla akamuona Sele akitoka nje kwa jazba na kubeba jiwe, Patrick akashangaa kwani alimjua Sele vizuri kuwa si mtu wa hasira kiasi kile akaamua kumfatilia Sele ndani.
Lengo la Sele lilikuwa ni kumponda Maiko na lile jiwe kwani alijua wazi asingeweza kupambana nae kwa yale maumivu yake, akalishika lile jiwe kisawasawa na kulirusha mahali alipokuwa Maiko.
 
SEHEMU YA 62


Akalishika lile jiwe kisawasawa na kulirusha mahali alipokuwa Maiko.
Patrick akakimbia mbele gafla na kulidaka lile jiwe, Tusa nae akainuka pale alipokuwa amekaa na baba yake akawa anaongea kwa jazba.
TUSA: Patrick umelizuia kwanini hilo jiwe kumponda huyu shetani? Tena sikuwaona ni mashetani mawili yapo hapa, umezuia kwavile tabia zao na zako zinaendana?
Wakati Tusa alikuwa akizungumza hayo, Sele nae alikuwa amekazana kutaka kupambana na Maiko ila Patrick akawa anamzuia hata Maiko alishangaa leo kutetewa na Patrick.
PATRICK: Punguzeni hasira Sele na Tusa.
SELE: Unajua alichonifanya huyu Patrick? Unajua huyu alichonitenda?
PATRICK: Punguza hasira kwanza Sele tuzungumze, kumbuka hasira hasara.
TUSA: Yani unavyoongea Patrick kamavile na wewe ni mtu mwemaaa kumbe ndio walewale kasoro majina.
PATRICK: Tusa, usiwaze mabaya yangu tu, kumbuka na mema yangu.
TUSA: Katika wanaume ninaowachukia humu duniani ninyi watatu mnaongoza, siwapendi siwapendi siwapendi.
Tusa akatoka nje, Deborah akashangaa kuona Tusa ni muongeaji kiasi kile kwani mara nyingi huwa akimshuhudia anapolia tu. Patrick nae akaamua kutoka kumfata Tusa nje.
Deborah akamshika Sele mkono na kutoka nae nje pia.
Patrick akaamua kuzungumza na Tusa.
PATRICK: Tusa, nakuomba usinichukie. Mimi Patrick wa leo si Patrick uliyemfahamu kipindi kile nakupenda Tusa na sina roho mbaya kama unavyonifikiria na wala sina tena ushirika wowote na Maiko.
TUSA: Kama huna ushirika na Maiko mbona umemzuia Sele asimponde na jiwe?
PATRICK: Tusa, pale ndani si mahali sahihi pa kufanya hivyo. Sele angeweza kumuua Maiko na je angefunguliwa kesi ya mauaji si angefungwa maisha? Je, uko tayari kuona Sele akifungwa maisha?
TUSA: Inamaana Patrick unampenda Sele?
PATRICK: Ndio nampenda, Sele ni ndugu yangu siwezi kumchukia. Swala la Maiko ni dogo sana kwangu, hiyo kazi niachieni mimi.
TUSA: Sitapenda kuona Sele anafungwa sababu nampenda.
PATRICK: Hapo ndipo unapokosea Tusa, unatakiwa unipende mimi. Mimi Patrick ndio mumeo wa maisha.
Halafu Patrick akaenda kumfata Sele aliyekuwa ametolewa nje na Deborah.
Tusa alimuangalia Patrick na kuona kama mtu wa tofauti, akashangaa Patrick kumuhurumia mtu kufungwa, ila Tusa akajisemea,
"Sijawahi kuua katika maisha yangu ila huyo Maiko lazima nitamuua"
Anna aliyeachwa mule ndani na wale wageni.
ANNA: Kwakweli Maiko wewe ni shetani, hakuna binadamu atakayeweza kukupenda baada ya kugundua uyafanyayo. Najua wazi hata hao walioongozana na wewe hawakujui kuwa wewe ni mwanaume wa aina gani ila wakijua mambo yako watakuonea kinyaa.
ADAMU: Maiko, hebu tuweke wazi tafadhari ni mambo gani uliyoyafanya na iweje hadi binti yangu akuchukie?
Akatokea Deborah na kusema,
DEBORAH: Si binti yako tu anayemchukia, huyo Maiko unayemuona hapo mbele anachukiwa hadi na sisimizi nadhani ukimjua vizuri hata wewe mwenyewe utamchukia huyo shetani.
REHEMA: Mungu wangu, najua yote haya sababu ya kutokumlea mwanangu mimi mwenyewe, ona mambo yalivyo sasa.
PAMELA: Majuto ni mjukuu mama, huyo Maiko hapa Fausta bado hajarudi nae akirudi ana yake.
ADAMU: Hadi Fausta? Una matatizo gani Maiko? Ndugu yangu niliyekujua ukubwani, nini tatizo Maiko?
Maiko alikuwa ameinama tu kwa aibu.
Patrick akaenda kuzungumza pia na Sele.
PATRICK: Kwani yule jamaa umemjulia wapi Sele?
SELE: Kwanza ungeniachia yule mtu nimponde na jiwe, amekuwa akiniwinda muda mrefu sana. Yule ni adui yangu namba moja humu duniani.
PATRICK: Kwakweli mnanishangaza, hivi huyu Maiko ni mtu wa aina gani? Na kwanini ametenda matukio mengi ya ajabu kwa watu wengi?
SELE: Nina hasira nae sana, na siwezi kumsamehe hadi naingia kaburini.
Patrick alimtafakari sana Maiko ila alikosa jibu la kwanini Maiko amehusika kwenye matukio mengi ya ajabu.
Tina na mama yake walirudi huku macho ya Tina yakiwa yamejaa machozi.
Tusa ndiye aliyewapokea na kuwauliza kwanini Tina analia.
TINA: Nina mimba Tusa, tena mimba ya kubakwa. Naichukia Mwanza Tusa.
Tusa nae akajikuta akilia na kukumbuka mikasa yake yote ya mimba.
Ikabidi Patrick na Sele nao wawasogelee na kuamua kuingia nao ndani, Patrick alitaka kupata maelezo yakinifu juu ya uwepo wa Patrick mule ndani wakati anaonyesha kuwa ameshaumiza watu wengi.
TUSA: Pole sana Tina ndugu yangu.
Walipoingia ndani, Tina akamuona Maiko akamgeukia mama yake na kumwambia.
TINA: Mama, mwanaume mwenyewe aliyenibaka ni yule pale.
Wote wakamtazama Maiko na kumshangaa.
FAUSTA: Maiko, Maiko, Maiko yani umenibakia mwanangu? Hivi unajua kama umembaka mwanao shetani mkubwa wewe?
Fausta akaenda kumvaa Maiko mwilini, kukawa na varangati ndani ya nyumba kwani Fausta hakutaka kumuachia Maiko.
ADAMU: Haya makubwa sasa mi hata sielewi, yani Maiko umembaka Tina mtoto wetu dah!!
TUSA: Sio Tina tu hata mimi mwenyewe alinibaka.
PAMELA: Nini? Khe khe khe, Mungu wangu laana gani hii jamani!!
Wakajaribu kumtoa Fausta alipomshikilia Maiko ilikuwa ni kazi ngumu, ikabidi Maiko atumie nguvu zake mwenyewe na kutaka kukimbilia nje ila alikutana na Tusa mlangoni akiwa ameshika kisu na kumchoma nacho begani.
Damu nyingi zikamtoka Maiko ila akampushi Tusa na kutoka huku kisu kikiwa begani.
TUSA: Na bahati yako ningekubebea panga wewe.
Ikabidi Rehema nae atoke na kumfata Maiko aliyekuwa akivuja damu.
Tulo kama alivyomuahidi Mashaka akaamua kufunga safari kuelekea Mwanza ili kuweza kuonana na Patrick kwani Patrick alikuwa ni rafiki yake mkubwa sana kwahiyo alijua atampata tu.
Patrick bado alikuwa haelewi kitu, akaomba aelekezwe na Pamela akamwambia jinsi ilivyo ila bado hakuelewa.
PATRICK: Hii familia sasa imeanza kunichosha siielewi, siielewi, siielewi. Hivi inakuwaje mzazi hadi anashindwa kukaa na watoto wake hadi mambo kama haya yanatokea?
PAMELA: Sasa wewe Patrick unamlaumu nani?
PATRICK: Namlaumu huyo bibi, ila kiukweli familia ya Tusa imenichosha. Kwanza haieleweki. Familia haina mwanzo wala mwisho.
PAMELA: Usimlaumu Tusa tu, je wewe familia yako inaeleweka?
PATRICK: Ndio familia yangu inaeleweka na wote tunafahamiana sio kama familia yenu.
PAMELA: Kama inaeleweka mbona wewe na nduguyo kumgombea mke mmoja? Je ulifahamu kama Mwita ni mtoto wa Anna? Na je baba yako mzazi unamjua? Hata wewe familia yako haieleweki.
Kwenye swala la baba mzazi Patrick akawa ameguswa vilivyo na kuamua kumfata mama yake Deborah.
PATRICK: Mama, naomba na mimi leo unitajie baba yangu alipo sitaki mambo kama haya yatokee na kwangu. Sitaki kuwa na familia isiyoeleweka.
Deborah akajikuta akihema kwa nguvu na kuanguka.
 
SEHEMU YA 63


Deborah alijikuta akihema kwa nguvu na kuanguka.
Ikabidi Patrick aanze kumpepea mama yake, Pamela nae akaenda kumsaidia hadi pale Deborah alipojisikia vizuri, akahitaji maji na Pamela akaenda kumletea.
PATRICK: Pole sana mama.
DEBORAH: Asante Patrick.
Pamela alipoyaleta yale maji, Deborah akayanywa na mengine kujimwagia kichwani.
Tusa nae akatoka ndani na kuwafata pale nje.
Patrick aliwaacha pale na kwenye nyuma ya nyumba yao kutuliza mawazo, alikuwa akifikiria kuwa kwanini mama yake hapendi kumwambia ukweli kuhusu baba yake.
PATRICK: Hii ni haki yangu, lazima niujue ukweli kama mtoto.
Kumbe Tusa alikuwa nyuma yake,
TUSA: Ukweli gani?
PATRICK: Ukweli kuhusu baba yangu, sitapenda familia yangu ikose uleleo kama familia yenu.
TUSA: Familia yetu haina uelekeo kivipi?
PATRICK: Familia yenu haieleweki, eti Maiko ni babako mdogo.
TUSA: Hapana, haiwezekani kabisa. Maiko hawezi kuwa ndugu yangu hata kidogo.
Patrick akajaribu kumuelekeza kama vile alivyoelekezwa ila Tusa akakataa kabisa, ikabidi aende ndani ili kupata ukweli wa mambo.
Rehema aliyekuwa ameongozana na Maiko akawa anajaribu kumshawishi Maiko ili warudi tena kwa Deborah na waweze kuweka mambo yote sawa.
MAIKO: Angalia mkono wangu ulivyojaa damu, unataka niende wakanichinje kabisa? Siwezi.
REHEMA: Sikia nikwambie, marumbano si mazuri kwa wanandugu. Tunatakiwa kukaa chini na kumaliza tofauti zote na kujuana, kwa mtindo huu unadhani utawajuaje ndugu zako wengine?
MAIKO: Mmh! Kurudi tena kule ni kujitakia kifo tu.
REHEMA: Hapana mwanangu, mimi mama yenu nipo.
MAIKO: Vipi baba, yuko wapi yeye? Maana nadhani itakuwa vyema nikianza kufahamiana na yeye kwanza.
REHEMA: Aliuwawa, tena alikufa kifo cha kikatili sana. Alikuwa anaishi Morogoro.
Maiko hofu ikamtanda kidogo kusikia kuwa baba yake aliuwawa tena ni Morogoro.
MAIKO: Aliitwa nani?
REHEMA: Walipendelea sana kumuita mzee Ayubu na Ayubu ndio jina lake.
Maiko akamuomba bi.Rehema warudi tena nyumbani kwa Deborah, nia yake ni kwenda kuzungumza na Patrick ili apate kujua ukweli.
Tusa aliingia ndani na kuanza kumwambia baba yake kuwa amwambie ukweli kuhusu Maiko.
Adamu akamueleza Tusa juu ya undugu wao.
Tusa akashangaa sana, kisha akamgeukia Mwita na kumuangalia tena baba yake.
TUSA: Usiniambie kuwa na huyu ni ndugu yetu.
ADAMU: Ndio ni ndugu yetu kwani ni mtoto wa Maiko.
TUSA: Baba, yani watu wote wameshindwa kuwa ndugu zetu zaidi ya hawa? Kwakweli siwapendi, siwataki na sitawakubali kamwe katika maisha yangu.
ADAMU: Mwanangu Tusa, hawa ni ndugu zetu tu hatuwezi kuwaepuka.
TUSA: Hao ni ndugu zako wewe na mama, mimi siwataki kabisa. Na laiti ungejua walivyonitenda hata usingewatetea hivyo.
Tusa akaenda chumbani, hakutaka tena kukaa pale sebleni kwani alihisi kuchanganyikiwa.
Anna alimuangalia Mwita kwa makini, kisha akamwambia.
ANNA: Natumai, matendo yako si sawa na matendo ya Maiko.
Mwita alikuwa kimya tu kwani aliona aibu kwa vitendo alivyowafanyia ndugu zake.
Fausta aliamua kumueleza Tina ukweli kuhusu Maiko, akamueleza kuwa Maiko ni baba yake.
Kwakweli Tina alilia sana na mama yake pia alilia.
PAMELA: Ila haya ni madhara ya kumficha mtoto kwa baba yake kwa kipindi kirefu.
FAUSTA: Hujui kitu wewe Pamela, unaongeaongea tu. Najua kwasababu hiki kilio ni kwangu ila kingekuwa kwako ungeyahisi maumivu yangu.
PAMELA: Basi yaishe jamani.
FAUSTA: Hujawahi umia kama hivi Pamela, mimi nimeumia. Inaniuma sana.
Tina kila alipoifikiria ile mimba alijikuta akizidi kulia zaidi na zaidi.
Patrick akaamua kumfata tena mama yake ili azungumze nae japo kidogo.
PATRICK: Ila mama nina haki ya kujua ukweli kuhusu mimi.
DEBORAH: Kweli unataka kuujua ukweli? Unataka kujijua wewe ni nani?
PATRICK: Ndio mama, nahitaji kujua.
DEBORAH: Nitakueleza ukweli, ila je ungependa nikueleze mbele ya nani?
PATRICK: Mbele ya wote wanaokufanya ulie kila unapokumbuka zamani, na mimi nitakuwa pembeni yako nikiyafuta machozi yako.
DEBORAH: Kweli mwanangu?
PATRICK: Kweli mama kwani natambua kama mimi ndio faraja yako.
DEBORAH: Basi......
Wakajikuta wakishangaa kumuona bi.Rehema na Maiko wakija, Patrick akajiandaa kumdhibiti Maiko kama ataleta fujo.
Maiko akashukuru kumuona Patrick pale nje kwani ndio ilikuwa shida yake iliyompeleka pale.
Akamuomba Patrick kwaajili ya mazungumzo, mwanzoni Patrick alikuwa anasita ila badae akakubali na wakasogea kuzungumza.
MAIKO: Samahani Patrick, eti yule mzee aliyeuliwa na kundi letu kule Morogoro aliitwa nani?
PATRICK: Kwani umekumbuka nini? Yule mzee tulimuua bila hatia, roho yangu inanisuda hadi leo. Aliitwa mzee Ayubu.
MAIKO: Mungu wangu, dah nimeshiriki kumuua baba yangu.
PATRICK: Baba yako? Nani baba yako?
MAIKO: Yule mzee Ayubu ni baba yangu mzazi, ndio nimejua leo. Dah! Mashaka amemaliza familia yangu.
PATRICK: Inamaana tulimuua babu yake na Tusa! Dah!
Patrick alihisi kutokuwa sawa kimawazo, muda huohuo Maiko akaondoka akiwa amenywea bila ya bi.Rehema kujua kama kaondoka kwani yeye alibaki kuzungumza na Deborah.
Patrick nae akapigiwa simu na rafiki yake kuwa aende mjini, Patrick akaondoka nyumbani na kwenda mjini ili kupunguza mawazo kidogo.
Tulo ndiye aliyempigia simu Patrick, na alikuwa mjini akimngoja.
Patrick alipofika walipokeana vizuri na kuongea hili na lile kama marafiki, wakaagiza na vinywaji wakawa wanakunywa huku wakiendelea na maongezi.
Simu ya Patrick iliita tena na alitakiwa kwenda kuongea mbali kidogo, kumbe huku nyuma Tulo akamuwekea Patrick madawa kwenye kinywaji chake.
Patrick aliporudi akakaa na kuinua kile kinywaji ili anywe ile kukifikisha mdomoni tu akasita na kushusha chupa chini, kisha akamtazama Tulo na kumuuliza.
PATRICK: Umeniwekea nini humu?
Tulo akabaki anashangaa kuwa Patrick kajuaje.
 
SEHEMU YA 65


Wakati amelala akatokewa na mzimu wa mzee Ayubu.
Patrick akaanza kutetemeka kwa hofu kwani ni kitu ambacho hakukitarajia kabisa. Ule mzimu ukamwambia,
"Usiogope Patrick, sijaja kulipa kisasi na siwezi kulipa kisasi juu yako"
Patrick alikuwa bado na hofu, akatamani kuongea ila akashindwa na ule mzimu ukaendelea kusema,
"Kuna mengi unayotakiwa kufahamu Patrick, rudi kwenu na usipendelee kulala porini"
Halafu ule mzimu ukatoweka, Patrick akashtuka pale alipokuwa amelala na kujikuta akikimbia sana, alikimbilia mahali hata asipofahamu.
Maiko alifika Arusha akiwa na lengo moja tu kukutana na Mashaka.
Alipofika nyumbani kwake, aliingia moja kwa moja ndani, alienda kuangalia lile friji analohifadhia vitu vyake na kujikuta akiingiwa na huruma na kujiuliza kwanini alikuwa vile alivyokuwa.
Alienda chumba kingine na kujiandaa namna ya kukabiliana na Mashaka, alikuwa na hasira sana juu ya Mashaka.
Patrick alijikuta akikimbilia sehemu ya mbali sana, kulipokucha alijishangaa pale alipokuwa, akarudisha akili yake vizuri kwanza.
"Hivi naota au ni nini? Iweje mtu aliyekufa akanitokea na kuongea nami? Mbona mambo haya ya ajabu jamani. Ni vitu gani ninavyotakiwa kufahamu au ni kuhusu baba yangu? Mbona sielewi sasa?"
Akajikuta akijiuliza maswali mengi bila ya majibu na alikuwa ameshajichokea kwa kukimbia sana.
Deborah aliendelea kuwa na mawazo ila hayakumsaidia chochote. Kwanza alimuwaza Patrick, pia akamuwaza Maiko kwani mahusiano ya Maiko na Patrick tayari yalishamchanganya.
Kitu kingine ni vipi Maiko aliweza kuwachanganya wanawake wote wale na kuwatesa vilivyo.
Ikabidi amfate Fausta na kwenda kumuuliza, Fausta akawaambia kuwa angependa kuwaelezea wote ili wajue kwanini anamchukia Maiko na hawezi kumsamehe kamwe katika maisha yake.
Adamu nae akawa makini kumsikiliza kwani hata yeye alihitaji kujua ukweli wa kwanini Maiko anachukiwa vile.
Fausta aliamua kuelezea kwanza jinsi alivyo kutana na Maiko na vitendo ambavyo Maiko alimfanyia.
"Nilikutana na Maiko nikiwa bado msichana na si mmama kama hivi.
Maiko alikuwa na pesa sana na kuniambia kuwa ananipenda, sikujua kama pesa yake ilitumika kumnunua mwanamke yeyote amtakaye. Alinilaghai kwa pesa yake na kujikuta nikiwa kama mtumwa wake wa mapenzi sababu ya pesa, kipindi hicho niliishi nae Morogoro kwani alinipangia nyumba kubwa sana ya kuishi. Pamela hakuwahi kumjua Maiko kwani Maiko hakuwa mkaaji sana wa pale, alikuwa akija leo basi ataondoka kesho.
Nikapata ujauzito, nilipomwambia akanishauri nitoe na kusema kuwa nikishatoa vile vipande nimwambie daktari aniwekee sehemu nzuri ili nije kumkabidhi yeye, nilijua ananitania. Hatahivyo nilikataa kutoa ile mimba kwani sikutaka kufanya kitendo kama nilichofanya na mdogo wangu Pamela hapo kabla. Sikutaka ile kitu ijurudie tena katika maisha yetu kwani tulishatenda dhambi tayari ya kukitoa kiumbe kisicho na hatia.
Siku hiyo nikiwa sijui hili wala lile, alikuja Maiko na mtu mwingine pale nilipokuwa naishi, machale yakanicheza, nikatoka nje kwa muda na kutokomea moja kwa moja, nilienda kuishi kwa baba mzee Ayubu kwa muda kwani mimba yangu ilishakuwa kubwa, kumbe kitendo kile kilimchukiza sana Maiko.
Siku niliporudi kwenye ile nyumba nilikuwa tayari nimeshajifungua watoto wawili mapacha Tina na Thomas. Nikajua kuwa labda Maiko alichukia mimba ila atafurahia watoto.
Nilipofika pale nilikuta barua nyingi sana alizoacha Maiko, tena aliacha na pesa nyingi tu mule ndani huku akisema kuwa alichukizwa na kitendo cha mimi kutoroka ila yupo tayari kunisamehe.
Nilipoona vile nikaamua kumtumia ujumbe kuwa nisharudi na tayari nimejifungua ila sikumwambia kama nimejifungua mapacha kwa lengo la kumfanyia surplise.
Siku hiyo ambayo siwezi kuisahau, alikuja mdogo wangu Pamela pale nilipokuwa naishi ambapo na yeye alikuwa na mimba ila changa, aliniomba aondoke kidogo na mtoto mmoja akakae nae kwake japo siku mbili akamchangamshe, sikumkatalia kwani nae aliishi Morogoro kwa kipindi hicho na alimchukua Tina kwani Tina alikuwa mwepesi wa kukubali kushinda Thomas ambaye alikuwa akilia kila alipochukuliwa kwangu.
Pamela alipoondoka tu, huku nyuma alikuja Maiko bila hata ya taarifa yoyote ile.
Alinikuta nikimvalisha Thomas ambaye nilitoka kumuogesha, kufika pale nilifurahi sana na kumkaribisha.
Alipokuwa ndani alimnyanyua mtoto na kumbeba, sikumkatalia kwavile alikuwa mwanae ila sikujua kama Maiko ni mtu katili kiasi kile alichofanya, aliniambia kuwa amekuja kumchukua mwanae, mimi nikashtuka sana na kumkatalia kwa kumwambia kuwa mtoto bado mdogo angoje akue kwanza.
Akaniangalia kwa dharau kisha akasema,
"Huyu mtoto umemkatalia tumboni hadi ametoka bado wamkatalia!!"
Sikumuelewa kuwa alikuwa na maana gani kusema vile, alikuwa na begi mgongoni akafungua na kutoa pesa nyingi kisha akaziweka mezani na kuniambia kuwa nimuachie mtoto aende nae ila nikagoma kwani pesa si mtoto, nikashangaa gafla akimuweka yule mtoto chini na kutoa kamba kwenye begi lake kisha kunifunga mikono na miguu huku akiniziba mdomo kwa zile solotepu kubwa ili nisiweze sema chochote, mwanangu Thomasi alikuwa akilia sana, Maiko alitoa kisu kwenye begi lake na kumchinja yule mtoto mbele ya macho yangu bila hata huruma kwakweli sikuamini kabisa, nilijihisi kama niko ndotoni.
Maiko ni mume gaidi, ana roho mbaya iliyopitiliza sijawahi kuifikilia maishani mwangu roho ya namna ile. Maiko ni shetani tena yule shetani mwenye mapembe saba.
Akaona ile kumchinja haitoshi, akamkatakata vipande na kuweka kwenye mfuko na kutumbukiza kwenye begi lake kisha akaniambia
"Hii ndio dawa ya kiburi chako, siku nyingine ukiambiwa kitu na mtu mwenye pesa kama mimi tekeleza"
akaondoka na kunifungia mlango kwa nje, nyumba yote ilinuka damu ya mwanangu.
Kwakweli siwezi kusahau, nililia sana hadi kupoteza fahamu, hata niliposhtuka bado sikuamini, sikuweza kwenda popote kwani alinifunga pale chini.
Nashukuru Mungu, kesho yake alikuja Pamela nyumbani pale ambapo nae alikuwa na funguo za ziada za mule ndani, hakuamini kuniona pale chini huku damu nyingi zikiwa zimeganda pale ndani.
Nilimsimulia kilichonikuta na tulilia sana na mdogo wangu, tulienda kutoa taarifa polisi ila haikusaidia chochote kwani Maiko ni mtu ambaye sikumfahamu ndugu, jamaa wala rafiki yake hata mmoja. Tuliamua kuamua kuondoka kabisa eneo lile na kuihama Morogoro, tangia hapo ilikuwa nikienda Morogoro basi naenda kwa mzee Ayubu tu.
Niliona Tanzania ya uchungu na ndio kipindi hicho nikasafiri na kukaa muda mrefu bila ya kurudi, mwanangu Tina alilelewa na Pamela mdogo wangu"
Habari ile iliwasikitisha sana, Deborah nae alijikuta akilia kwa uchungu na kukumbuka mambo ambayo na yeye yalimtokea hapo nyuma akiwa kwa Adamu na akiwa kwa Maiko pia.
DEBORAH: Maiko sio mtu jamani, Maiko ni shetani. Mama umeyasikia hayo?
Bi.Rehema alikuwa akilia tu bila kuamini kama mwanae wa kumzaa mwenyewe anaweza kufanya kitendo kama kile alichosimuliwa.
Adamu akajikuta akimchukia Maiko sasa kwa kitendo alichomfanyia Fausta na vile alivyoambiwa na Tusa kuwa alimbaka.
ADAMU: Mama, nadhani mwanao Juma sio huo Maiko. Nadhani tuendelee tu kumtafuta huyo pacha wangu, siwezi kuwa na ndugu mwenye roho mbaya kiasi hiki.
PAMELA: Kumbuka na matendo yako pia Adamu, nadhani wewe na yeye mmetofautiana ila kumbuka ulichonifanyia kipindi kile Adamu kama kilikuwa sahihi.
DEBORAH: Hii familia ina makubwa sana, na huyu Maiko ni mtu mbaya sana kwenye ukoo wenu.
Kila mmoja aliwaza chake juu ya Maiko kwani hakufikiriwa kuwa kama binadamu wa kawaida.
Patrick akiwa eneo asilolitambua, anaamua kuuliza watu alipo ili aweze kurudi kwao.
Anamuona kijana mmoja akiwa amesimama kamgeuzia mgongo, akaenda kumshtua ili amuulize. Yule kijana kugeuka alikuwa ni Mporipori, wakajikuta wakitazamana na Patrick.
Mporipori hakuweza kumtazama zaidi Patrick ila alianza kumkimbia ili kumkimbia Patrick kwa kuhofia kipigo, Patrick aliamua kumkimbilia Mporipori kwa nyuma kwani aliona kuwa yeye ndiye mtu pekee atakayemsaidia ukizingatia pale alipokuwa karibia watu wote waliongea kilugha na hawakujua kiswahili.
Maiko akiwa Arusha, aliwaulizia vibaraka wake alipo Mashaka. Akaelekezwa mahali ambapo Mashaka yupo. Maiko alikuwa na hasira na Mashaka kwa kumsababishia amuue baba yake mwenyewe, huku Mashaka akiwa na hasira ya kusalitiwa na Maiko.
Wakati Maiko akimfata Mashaka, kumbe Mashaka nae alikuwa akimngoja kwa hamu mahali hapo.
 
SEHEMU YA 66

Wakati Maiko akimfata Mashaka, kumbe Mashaka nae alikuwa akimngoja kwa hamu mahali hapo.
Maiko alipomuona Mashaka akamuangalia kwa jicho kali sana na kumuuliza.
MAIKO: Kwanini ulitoa oda ya kumuua mzee Ayubu?
MASHAKA: Ushajua kuwa Ayubu ni baba yako eeh!! Hata hivyo umemuua mwenyewe sababu mi nilitoa oda tu.
MAIKO: Shida yangu ni kujua, kwanini basi.
MASHAKA: Kwasababu nilikuwa simpendi, namchukia sana Ayubu.
MAIKO: Kwanini ulikuwa unamchukia?
MASHAKA: Kipindi yupo kwenye mahusiano na dadangu nilimkataza sana ila hakusikia hadi akampa mimba ndio wazazi wakaingilia kati halafu mi na yeye tushawahi kugombaniana mwanamke. Ila usisikitike sana, yule kaenda na sie tumebaki.
MAIKO: Hivi wewe Mashaka unajua umenipandikiza roho ya ajabu sana! Nimeua watu wengi kwaajili yako ila sasa sioni faida, nimeharibu familia yangu na kila kitu.
MASHAKA: Kuhusu familia hata mimi sina familia, nilikutegemea sana Maiko ila sikutegemea kama ungenisaliti.
Maiko alimuangalia sana Mashaka, alitamani amrarue ila aliona njia nzuri ni kumvizia kwani hapo Mashaka nae alikuwa na yake kwa Maiko.
Deborah na wengine wote wakawa wanasikitikia habari ya Fausta kwakweli iliwatisha na kuwasisimua sana, Deborah akafikiria mengi aliyotendewa na Maiko na kuona wote wana haki ya kumchukia Maiko.
Ikabidi wapange kikao cha familia kwajili ya kujadili kuhusu Maiko, ikabidi Deborah ampigie simu dada yake bi.Marium kuwa naye awepo kwenye kikao hicho ili aeleze alichotendewa na Patrick hadi kumchukia kiasi kile ambacho anamchukia.
Patrick aliendelea kumkimbilia Mporipori huku Mporipori nae akizidi kukimbia.
PATRICK: Tafadhari Mporipori simama, sina ubaya wowote na wewe.
Mporipori alikuwa na uoga sana juu ya Patrick, ikabidi asimame eneo lenye watu ili kama Patrick atahitaji kumdhuru basi wale watu waweze kumsaidia.
Patrick alimsogelea Mporipori na kumsalimia ila Mporipori alisita kuitikia.
PATRICK: Nisaidie ndugu yangu nimepotea.
MPORIPORI: Wewe unaomba msaada kwangu!!
PATRICK: Ndio Mporipori naomba unisaidie.
MPORIPORI: Ningekufa je kule porini angekusaidia nani?
PATRICK: Ndiomana hukufa Mporipori ili uweze kunisaidia.
Mporipori alimuangalia sana Patrick na kuamua kumuelekeza, ila akamueleza njia isiyo sahihi ili kumpoteza tu.
Walikaa kwenye kikao na kuanza kujadili matendo ya Maiko ambayo amewafanyia.
Rehema alikuwa makini kusikiliza huku moyo ukimuuma sana kama mzazi.
Anna aliamua kuelezea na yeye hadi kuzaa na Maiko.
"Kuna kipindi nilienda kuishi kwa baba yetu mdogo aliyekuwa akiishi Arusha, huko ndipo nilipokutana na Maiko alinipa kila nilichohitaji, kwakweli nikajikuta nikimpenda sana.
Nikapata ujauzito, Maiko alipojua akanichukua na kunipeleka kwa daktari ambapo nilitolewa ile mimba kinguvu. Tokea hapo sikutaka tena kuendelea na Maiko ila akanitishia kuwa nikiachana nae ataniua eti kisa nimeshakula vitu vyake vingi.
Nikapata mimba nyingine, sikutaka kumwambia nikawa kimya kabisa.
Sikuweza kuendelea kuishi pale kwa bamdogo na ile mimba na huku Mwanza niliogopa kurudi na mimba wala mtoto.
Sikuwa na mahali pa kwenda, kama ilivyo kawaida mimba haina siri, tumbo likakua na kufanya Maiko agundue kuwa mimi ni mjamzito, akanilazimisha niende nae kule tulipotoa ya Mwanzo nikagoma akanipiga sana na kusema atanitoa tena kwa nguvu, bahati nzuri nilipata upenyo na kutoroka.
Niliomba msaada kwa watu wa usafiri hadi nikajikuta naingia Tanga.
Niliteseka sana na ile mimba hadi nilijikuta nikijifungulia njiani ila walipita watu wema na kunisaidia kunipeleka hospitali.
Nilipotoka hospitali sikuwa na pa kwenda,
kulikuwa na watu flani waliojitolea kulea watoto wasio na baba, nikaamua kumpeleka huko mwanangu na kumuacha akiwa na miaka miwili, mimi nikarudi Mwanza, sikusema ukweli kwani nilimjua shangazi lazima angechukizwa na kitendo cha mimi kuzaa bila ndoa.
Mara ya pili kumuona mwanangu alikuwa na miaka kumi na tano, nilifurahi na kushukuru kwa kulelewa mtoto, hawakuwa watoto wengi walioamua kuwalea pale ila nashukuru katika hao wachache na mwanangu alikuwa mmoja wao.
Ni siku hiyo aliponiuliza kuhusu baba yake nami nikampa picha ya Maiko, nikamwambia angoje kwanza atakapo pambazuka vizuri akili ndio amtafute.
Nikarudi tena Mwanza na kukutana na Maiko, sikujua alifata nini Mwanza ila alinikamata na kuniteka huko alinipiga sana kwa kusema kuwa ananifundisha adabu kwa kumkatalia mtoto wake, alinidadisi sana alipo ila sikusema.
Nilirudi nikiwa nimetenguka mkono na mguu kwa kipigo chake, ndio toka siku hiyo sijaonana nae tena hadi siku aliyokuja hapa"
Deborah alimuangalia sana Anna bila kummaliza.
DEBORAH: Kumbe uliposema umevamiwa na majambazi huyo jambazi mwenyewe ndio Maiko!!
ANNA: Maiko ni jambazi kweli.
PAMELA: Jamani, ngoja niulize swali. Huyo Maiko yeye hizo mimba changa anaenda kufanyia nini?
DEBORAH: Maiko ni shetani na huo ni ushetani mmoja wapo aliokuwa akipenda kufanya.
FAUSTA: Mi naona huyu Maiko akija tena atujibu, watoto wetu wachanga huwa anawafanya nini. Anakula nyama au anauza?
Rehema alishindwa kuelewa kama mwanae Maiko ni mtu wa kawaida kweli.
Patrick alijikuta njia aliyoenda nayo sio kabisa yani, alijiona kuzidi kupotea.
Kwa bahati akaliona gari la mkaa akalisimamisha na kuomba lifti.
Nia yake ni kufika mahali ambapo atapata uelekeo wa maana wa kurudi nyumbani kwao.
Moyoni alikuwa akijilaumu sana kwani mbio za kuukimbia mzimu ndio zilizomponza.
Maiko akamnyemelea Mashaka akiwa na lengo moja tu la kummaliza, ila wakati anamnyemelea Mashaka alishtuka na kugundua kitu.
Hapo hapo akaanza kupambana.
Mashaka na Maiko walikuwa katika mpambano wa hali ya juu yani kufa na kupona.
Yuda nae aliamua kumsimulia Sele kuhusu kichwa cha baba yao.
SELE: Dah! Yule Maiko anastahili kufa kwakweli. Simpendi hakuna mfano, yani kumkata baba yetu kichwa dah!!
YUDA: Ndo hivyo, ila dawa ya moto ni moto. Yule nae tumkate kichwa tena kichwa chake tukiache kiliwe na kunguru.
Wakaamua kwenda kwa mama yao mdogo ili kuangalia kama Maiko kaja tena na safari hii wakajipanga kwa ajili ya kupambana nae.
YUDA: Hakuna kumuachia akimbie.
SELE: Nina hasira nae sana yule jamaa.
Baada ya Anna kuelezea yake, Tusa nae akaamua kufunguka mambo aliyofanyiwa na Patrick na Maiko alivyokuwa Arusha.
Wakati Tusa anasimulia kila mtu alipigwa na butwaa na kushangaa kuwa hata Patrick waliyemuamini nae kumbe hafai.
Muda huo Patrick nae alikuwa amefika nyumbani kwao, kusogelea mlango akawa anamsikia Tusa akisimulia.
 
SEHEMU YA 67


Muda huo Patrick nae alikuwa amefika nyumbani kwao, kusogelea mlango akawa anamsikia Tusa akisimulia.
Patrick roho ikamuuma sana kwani hakutaka mama yake ajue habari ile, akamuweka Tusa katika kundi la wanawake wapumbavu na wasio na akili, alibaki kusita pale mlangoni kwani hakujua sura yake itaangaliwa vipi atakapoingia ndani.
Akarudi nyuma na kutamani kuondoka hapo nyumbani kwao kwani vitendo alivyomfanyia Tusa wakati wapo Arusha hata yeye vilianza kumuumiza roho yake kwa sasa.
Akaanza kuondoka, wakati anapinda kona akakutana na Sele na Yuda ambao walikuwa wanakuja nyumbani kwao.
YUDA: Vipi Patrick?
PATRICK: Dah! Hakuna tatizo bhana, nyie nendeni tu.
YUDA: Ila mbona kama haupo sawa?
PATRICK: Aaah!! Ni Tusa bhana.
Sele kusikia vile hakutaka kuendelea kusikiliza ila alikimbia nakwenda moja kwa moja ndani kwani alihisi labda Tusa kapatwa na tatizo tena.
Patrick alizungumza kidogo pale na Yuda, halafu akaamua kuondoka.
Tusa aliendelea kuwaeleza namna ambavyo alitolewa mimba kinguvu na Patrick na jinsi ambavyo alikuwa akimfungia ndani hadi kubakwa na Maiko.
TUSA: Patrick alithubutu hata kuniingilia kinyume na maumbile bila ridhaa yangu.
DEBORAH: Mungu wangu, nini hiki!!! Yani Patrick ndio wa kufanya hayo mambo!! Dah.
Muda wote Deborah alionekana kusononeshwa tu na vitendo ambavyo aliambiwa kuwa Patrick amevitenda.
Tusa akaelezea pia alivyoteswa na wakina Maiko na kukombolewa na Patrick hadi kufika Mwanza.
Mara wakamuona Sele akiingia kwa kasi ya ajabu ndani.
MARIUM: Vipi na wewe?
SELE: Nilijua Tusa amepatwa na matatizo.
MARIUM: Kwanini?
SELE: Tumekutana na Patrick njiani anaondoka na akasema kuwa tatizo ni Tusa.
Deborah akashtuka sana na kujua kuwa kwa vyovyote vile lazima Patrick atakuwa amesikia mambo ambayo Tusa alikuwa akisimulia, ikabidi ainuke na kwenda nje ili akajaribu kumfatilia.
Wote mule ndani walibakia na mshangao kwani hawakuamini kama Patrick anaweza kufanya vitu alivyofanya kwa Tusa.
Ikabidi kikao kihairishwe na kupangwa tena kesho yake.
Pamela akamchukua mwanae Tusa na kwenda kuzungumza nae pembeni.
PAMELA: Pole sana mwanangu kwa yaliyokukuta.
TUSA: Asante mama, nimeshapoa.
PAMELA: Ila mwanangu tukiacha uovu wote huo ambao Patrick amekutendea ila inaonyesha anakupenda kwani alikukomboa.
TUSA: Hivi mama, kumbaka mtu ni upendo? Kumlazimisha atoe mimba ni upendo?
PAMELA: Sitayasemea hayo ila nadhani Patrick aliingiliwa na shetani wakati anayafanya hayo, Patrick anakufaa mwanangu usimchukie kiasi hicho. Yeye sio kama huyo Maiko wanayemsema.
TUSA: Mama, huyu Patrick hana cha kubadilika wala nini. Kama angebadilika basi asingenipulizia madawa wakati tuko hapa na kunibaka.
PAMELA: Inamaana hata wakati tuko hapa alikubaka?
TUSA: Ndio mama ila nilikaa kimya sikusema chochote.
Pamela alikuwa akitafakari mazuri na mabaya ya Patrick ili kuangalia wapi uzito umezidi.
Deborah akafata njia aliyopita Patrick bila ya mafanikio ya aina yoyote ile.
Deborah akaamua kurudi nyumbani kwake, alikaa chini na kumtafakari Patrick alivyokuwa wakati wa udogo wake.
"Alikuwa ni mtoto mchangamfu na mjanja, alikuwa mtundu sana ila ukimkataza anaelewa. Alipenda sana ibada, hakumchukia yeyote, alimpenda kila mtu. Alipokuwa na tatizo alinieleza, nilimpatia chochote alichotaka ilimradi afurahi. Kwanini Patrick umebadilika mwanangu!! Hivi hii ndio ahadi uliyoniahidi wakati mdogo kuwa utanisaidia!! Patrick, kwanini umebadilika baba?"
PAMELA: Usiwaze sana Deborah, kila mwanadamu na mapungufu yake na mara nyingine shetani hupitia kati.
DEBORAH: We acha tu Pamela.
PAMELA: Tusa ni mwanangu, na imeniuma sana kunielezea alichokuwa anafanyiwa na Patrick. Ila kwa upande mwingine Patrick ni mtu mwema, anahitaji kusamehewa tu ni shetani aliyempitia.
DEBORAH: Shetani mwenyewe si mwingine bali ni Maiko, huyu jamaa ndiye aliyemuharibu Patrick.
PAMELA: Ni kweli Deborah, Patrick si mtu mbaya.
Pamela aliendelea kumpa moyo Deborah.
Tulo aliyeachwa porini na Patrick, alipata msaada kutoka kwa wakata kuni kule porini. Walimuhurumia sana kwani alikuwa amevimba na kutokwa na damu sehemu nyingi sana.
Wale watu walimchukua na kumuhudumia ili aweze kupona na kurudi katika hali yake ya kawaida.
Maiko aliendelea kupambana na Mashaka hadi wakachoka wote wawili.
Maiko akamkaba Mashaka sasa, na Mashaka nae akawa anamzuia Maiko kumfanyia vile kwahiyo alikuwa amekazana kuitoa mikono ya Maiko. mashaka alikuwa akiongea kwa shida.
"Tafadhari Maiko naomba nikwambie kitu cha ukweli."
Maiko akaamua kumuachilia amsikilize, ila akachukua bastola yake na kumuelekezea Mashaka ili asikimbie.
MASHAKA: Nina mengi ya kuzungumza Maiko, unatakiwa uyajue mambo mengi sana. Ila je utajiri wote tuliousumbukia miaka yote mwisho wake ndio huu?
MAIKO: Huu utajiri si wa halali, na ubaya zaidi tumeua watu wengi sana wasiokuwa na hatia.
MASHAKA: Ni kweli, na je ukinimaliza mimi utakuwa umemaliza tatizo?
MAIKO: Sitaki maswali Mashaka, wee sema tu unachotaka kusema.
MASHAKA: Sawa mimi si baba yako Maiko ila pia ni mjomba wako. Kumbuka hilo kuwa mimi bado ni ndugu yako.
Maiko aliona Mashaka anataka kumpotezea muda tu.
Marium alipokuwa kwake akaamua kuongea vizuri na mwanae Sele.
MARIUM: Sele mwanangu, leo nimeamua kurudia tena Sele. Tusa hakufai.
SELE: Jamani mama, Mimi nampenda sana Tusa.
MARIUM: Hakufai mwanangu, Tusa amekuwa kopo tena kopo la jalalani hafai hata kidogo.
SELE: Mama, usiseme hivyo bhana.
MARIUM: Mimi ni mama yako Sele usije kusema kuwa hatukukwambia. Tusa ashaingiliwa na wanaume wengi sana, muachie huyo Patrick anayemng'ang'ania ila kwa wewe hakufai mwanangu.
SELE: Nampenda sana Tusa mama.
MARIUM: Sijui umerogwa wewe, hebu kaa chini nikusimulie kwanza aliyofanyiwa Tusa wakati yupo Arusha.
Marium akaanza kumueleza Sele yale mambo waliyosimuliwa na Tusa.
Patrick alikosa raha na kujiuliza kuwa kwanini Tusa ameamua kufanya vile, hakuelewa kwanini Tusa aliamua kuelezea mambo yao ya Arusha.
"Nitamuangaliaje mama mimi, mama atanionaje mwanae? Kuwa nimekuwa mtu mbaya!!"
Patrick alitafakari sana na kuamua kukodi chumba hotelini atacholala kwa siku hiyo huku akiendelea kutafakari jinsi ya kumueleza mama yake.
Akiwa hotelini amelala, mzimu wa mzee Ayubu ukamtokea tena.
 
SEHEMU YA 68


Akatokewa na mzimu wa mzee Ayubu.
Patrick akaanza kuogopa tena ingawa alikuwa ndotoni.
"Usikimbie kwenu Patrick, rudi nyumbani ukakabiliane na tatizo. Kukimbia tatizo sio suruhisho la tatizo, unatakiwa ulikabili tatizo"
Halafu akapotea, Patrick aliogopa sana na kushtuka, akaamua kukaa sasa pale kitandani akijadili na akili yake.
"Kwanini huyu mzee anapenda kunitokea? Je, anataka nikaseme ukweli kuwa nahusika na kifo chake mmh!! Mama yangu je atanionaje??"
Patrick akajiuliza sana ila akaona itakuwa vyema kama kesho yake atarudi tena kwao.
Tangu siku Mwita alipoona wanafamilia wameamua kukaa kikao na kujadili maovu ya watu, akajua lazima na yeye atajadiliwa kwahiyo aliamua kuondoka pale kwa Deborah.
Mwita nae aliona ukoo wake haufai ukizingatia kila shutuma zilimuhusu baba yake mzazi, akaona sasa hali si shwari kabisa ukizingatia yeye ni mwanausalama na mambo aliyofanya babaye ni makubwa sana.
Alijikuta akienda kulala hotelini kwa muda ila kumbe alipanga hoteli moja na aliyopanga Patrick.
Deborah aliendelea kumuwaza mwanae Patrick, alijikuta akitokwa na machozi kwani alihisi labda Patrick ameondoka moja kwa moja na hatorudi tena kutokana na yale maneno, kwani alimjua mwanae ni mtu wa hasira sana haswa akihisi mama yake amemchukia.
Debora akawa anajisemea,
"Nakupenda mwanangu, rudi nyumbani"
Pamela aliyekuwa pembeni alimsikia na kumfata.
PAMELA: Atarudi tu Deborah, hata usiwe na shaka. Ukizingatia Patrick ni mtu mzima sasa.
DEBORAH: Mtoto ni mtoto Pamela, haijalishi ukubwa wake. Patrick amekuwa mwanangu kwa muda sasa, nimepata nae tabu na shida ila sikumtupa kwani nilimuona kama vile ni faraja yangu kwa kipindi kile kigumu cha maisha yangu.
PAMELA: Sawa Debo, ila atarudi tu. Unapataje mashaka kwa mtoto mkubwa kama Patrick jamani!!
DEBORAH: Pamela hujui uchungu wa kupoteza mtoto ndugu yangu, ukiujua uchungu huo utasema.
PAMELA: Inamaana hata uchungu wa kuzaa si uchungu?
DEBORAH: Kuzaa ni kuchungu sana ila unafarijika pale kuona uchungu wa kuzaa kwako umefutwa na mtoto uliyempakatia. Kupotelewa na mtoto inauma sana, kufiwa ndio kabisa asikwambie mtu. Hata nawashangaa wanawake wenzetu wanaotupa vitoto walivyovizaa wenyewe.
PAMELA: Ugumu wa maisha hufanya hiyo kitu, hakuna mwanamke anayependa kumtupa mtoto wake.
Pamela nae akawa anatoa machozi.
DEBORAH: Inamaana unawatetea watoa mimba na watupa watoto? Nadhani utakuwa umepitia humo kwenye ujana wako ndomana machozi yanakutoka. Kupenda usichana wakati ushakuwa mama ni kubaya sana, ukishakuwa mwanamke hunabudi kuwa mama.
PAMELA: Na kwa wale wasiozaa je!
DEBORAH: Sikia Pamela, haijalishi mtoto umemzaa au hujamzaa ila ukimlea kiukamilifu na kwa mapenzi mema mtoto yule atakupenda tena atakupenda kushinda hata mama yake mzazi. Mama mlezi naye ni mama, mwanamke yeyote anatakiwa kuwa mama kwa mtoto aliyembele yake. Kubagua watoto ndio kunakofanya tusiheshimiane wakubwa kwa watoto, ila ukijiweka kama mama mbele ya mtoto yeyote itakufanya uweze kumsaidia hata pale anapopatwa na tatizo wakati wowote hata kama mama yake mzazi hayupo.
PAMELA: Umenifundisha kitu Deborah, ningempenda Sele kama mwanangu na kumwelewa basi yote haya yasingetokea. Ila nilimdharau sana na kumchukia.
DEBORAH: Hunabudi kumuomba msamaha hata kama ni mtoto kwako kwani chuki na dharau si kitu kizuri mbele ya mwanadamu mwenzio.
Pamela akakubaliana na Deborah kuwa kesho yake atamuita Sele ili aweze kuzungumza nae na kumuomba msamaha.
Kesho yake wakati Patrick anatoka kwenye chumba chake, Mwita nae alikuwa anatoka.
Wakajikuta wapo wote kwenye ngazi wanashuka, wakaangaliana na kusalimiana.
PATRICK: Natumaini yale yaliyotokea kati yetu yameisha.
MWITA: Yote yameisha Patrick.
Kwa kuonyesha kuwa yameisha, ikabidi waende mahali kukaa na kupata supu pamoja kama kifungua kinywa.
MWITA: Unajua nini Patrick, hakuna kitu kinachoniuma kama kumtendea vile Tusa. Nilikaa mule ndani hata kumtazama Tusa mara mbili mbili sikuweza na kumbe Tusa ni dada yangu dah inaniuma sana.
PATRICK: Mara nyingi watu hufanya mambo bila kufikiri, kama baba yako nae Maiko, alikuja kwangu na kumbaka Tusa kwa lengo la kunikomesha mimi kumbe alikuwa akimtesa mwanae nadhani hata yeye hilo swala linamuumiza.
MWITA: Ni kweli, hata mimi nilifanya vile kwa lengo la kumpiku Sele kumbe namtesa dada yangu.
PATRICK: Unajua mimi mwanzoni kabisa wakati namfahamu Tusa kupitia mtandao wa facebook, nilikuwa naona jamaa yake anafaidi sana ukizingatia Tusa alikuwa haachi kumtaja Sele kila unapojaribu kutupia ndoano kwake ndomana nikatumia gharama kubwa sana kumpata Tusa. Ila badae nilitekwa na mapenzi, nilitaka Tusa anione mimi kama huyo Sele aliyekuwa akimtajataja ndomana nikafanya kila njia kumuweka Tusa karibu bila kujua kama zile njia zilimuathiri Tusa kiasi gani na bila kujua kama Sele aliyetajwatajwa ni ndugu yangu.
MWITA: Mmh!! Sasa ulivyogundua kuhusu Sele ulichukua hatua gani?
PATRICK: Sikia Frank, Tusa nilishafunga nae ndoa kwahiyo hata nilipogundua kuwa Sele ni ndugu yangu na kuwa mimi na yeye tumegombea mwanamke mmoja sikuwa na la kufanya kwakweli na kumuacha Tusa siwezi ukizingatia nishamuharibu sana.
MWITA: Sasa Sele yeye anaichukuliaje hiyo hali?
PATRICK: Muda mwingine anakubaliana nayo na muda mwingine anahitaji kurudiana na Tusa hata namshangaa utafikiri wanawake wameisha duniani! Kwakweli mtindo wa kumgombea mwanamke mmoja siupendi ila namgombea Tusa sababu nishamuharibu na kumuumiza sana.
MWITA: Mmh! Khatari, je Tusa anakupenda sasa?
PATRICK: Haijalishi ananipenda au hanipendi ila mimi ni mume wake tu.
MWITA: Ila usisahau kwamba Sele naye anamgombea Tusa sababu wanapendana.
PATRICK: Aaargh! Tuachane na habari hizo bhana, ngoja tuzungumze mengine ya maana.
Wakakubaliana kurudi nyumbani ili kuweza kukabiliana na kile ambacho kinatokea.
Mashaka alimuomba Maiko karatasi na peni ili aweze kuandika anachotaka kuandika.
Maiko akamkabidhi daftari kabisa.
MAIKO: Haya, andika humo hayo matapishi yako.
MASHAKA: Usijari Maiko, mimi leo naandika ila kesho wewe utasema.
MAIKO: Sina cha kusema mimi.
MASHAKA: Utayasema tu maovu yako yote uliyoyatenda, mimi leo nitaandika maovu yangu yote niliyoyatenda na kwanini nimeyatenda. Ila wewe utasimama na kuyasema maovu yako kwani mengi yapo wazi na ubaya ni kuwa karibia wote uliowatendea wanakujua. Nakuhurumia sana Maiko.
MAIKO: Jihurumie wewe na nafsi yako, tena usiendelee kujiongelesha nisije nikafyatua huo ubongo wako, endelea kuandika hapo.
Muda wote Maiko alikuwa ameshika bastola kwani alikuwa na uchungu sana na Mashaka haswa kwa kitendo cha yeye kutumwa kwenda kumuua baba yake mwenyewe.
Sele alimuaga mama yake kuwa ameitwa na Pamela kwaajili ya mazungumzo.
MARIUM: Mwanangu narudia tena kukwambia, swala la wewe kurudiana na Tusa lipoteze kabisa. Tusa si mwanamke wa kuoa tena.
SELE: Jamani mama!
MARIUM: Ndio hivyo. Tusa ni kopo mwanangu hafai kabisa. Sitaki kabisa umuoe huyo binti, sitaki umrudie hata kama Patrick akisema mrudiane. Tafuta mwanamke mwingine atakayekufaa lakini sio Tusa.
Sele akaondoka nyumbani kwao na kuelekea nyumbani kwa Deborah.
Tulo alipopata unafuu aliwashukuru sana wale watu waliomsaidia na kuomba kurudi mjini ili aweze kurudi kwao Arusha.
Alifika mjini salama na kuanza safari ya kwenda stendi kukata tiketi ya kurudi Arusha kwani aliona mji wa Mwanza haumfai tena.
Tusa na Tina walichukuzana siku hiyo ili kwenda magengeni kutafuta udongo ambao Tina alikuwa akiuhitaji kwa sana.
Wakiwa njiani wakakutana na Tulo aliyeonyesha akimtambua Tina.
TULE: Kheee Tina!!
Mara gafla Tina akapatwa na kizunguzungu na kuanguka.
 
SEHEMU YA 69


Mara gafla Tina akapatwa na kizunguzungu na kuanguka.
Ikabidi Tulo na Tusa waanze kumpa huduma ya kwanza.
Baada ya kumpatia huduma ya kwanza Tina akazinduka ila kabla hawajafanya chochote akazimia tena.
Ikabidi waombe msaada wa kumuwaisha hospitali, walipofika hospitali ikabidi Tusa aamue kwenda nyumbani ili kutoa taarifa ya kuanguka na kuzidiwa kwa Tina.
Akaamua kumuacha Tulo pale hospitali akiendelea kutoa maelezo huku yeye akichukua uamuzi wa kuwahi nyumbani kutoa taarifa ingawa hakumuelewa Tulo vizuri.
Sele alikuwa amefika nyumbani kwa Deborah kwaajili ya wito ambao ameitiwa na Pamela.
Aliwakuta wote kasoro Tina na Tusa.
Baada ya salamu akaamua kumuulizia Tusa kwanza.
SELE: Kwani Tusa yuko wapi?
PAMELA: Tusa katoka kidogo na Tina, ila ngoja tuzungumze yetu hapa.
SELE: Ila mama, mmewaacha vipi watoke peke yao wakati wote ni wagonjwa wale?
PAMELA: Tusa kapona bhana.
Mara wakamuona Tusa akirudi mwenyewe, mama yake akamuuliza kwa mshtuko alipomuacha Tina, ikabidi awaeleze ilivyokuwa na Tina alipo, wakashangaa kusikia yale maelezo.
Wakaamua kwenda huko hospitali kuona anaendeleaje. Ikabidi waondoke nyumba nzima kasoro bi.Rehema ambaye waliona kuwa itakuwa ni vyema kumuacha nyumbani.
Walipofika pale hospitali ambapo Tusa alimuacha Tina na Tulo hawakuwakuta wote wawili.
Hofu ikawatawala sasa, Tusa ndio hakuelewa chochote.
Wakajaribu kuulizia ila hawakupa jibu la maana.
FAUSTA: Tusa, una uhakika kweli kuwa Tina umemuacha hospitali hii?
TUSA: Ndio, nilimuacha hapa na kijana mmoja hivi aliyeonyesha kumjua Tina vizuri.
PAMELA: wewe huyo kijana unamfahamu?
TUSA: Hapana mama simfahamu.
PAMELA: Mbona unaakili mbovu mwanangu? Si unajua kuwa hapa Mwanza kuna watekaji! Iweje unamuacha mwenzio na mtu usiyemfahamu. Kama kamteka je?
TUSA: Unanilaumu bure mama, mimi nilichanganyikiwa.
PAMELA: Kuchanganyikiwa gani huko, yani Tusa hauko makini kabisa wewe.
Fausta nae akahisi kuchanganyikiwa kabisa kwa kutotambulika mwanae alipo, lawama zote zikamuendea Tusa.
SELE: Mnamkandamiza Tusa bure tu wakati mnatambua kuwa na yeye alikuwa hoi siku chache tu zilizopita.
PAMELA: Hata kama ila ana wajibu wa kutupa maelezo ya kutosha juu ya alipo Tina.
Walikuwa wakibishana tu bila ya maelewano kwani hakuna aliyeelewa alipoenda huyo Tina.
PAMELA: Na huyu Tusa anatuletea kiwingu tu bora arudi nyumbani na sisi tuendelee kumtafuta huyo Tina.
DEBORAH: Sele, basi wewe ndio urudi na Tusa nyumbani ngoja sie tujaribu kuulizia hospitali zote za hapa.
Sele akaamua kuondoka na Tusa.
Adamu ndiye aliyebaki na wale wanawake watatu katika kumtafuta Tusa
Mashaka na Maiko waliendeleza yale majibizano yao huku Mashaka akiendelea kuandika ule ujumbe wake, alipomaliza akauweka pembeni na Maiko akaenda kuuchukua ikawa muda huo huo ambapo Mashaka akamgeuka Maiko na kumpokonya ile bastora kisha akamdhibiti yeye.
MASHAKA: Ila mimi sina nia ya kukumaliza kama wewe ambavyo unataka kufanya.
MAIKO: Nia yako nini wewe?
MASHAKA: Nia yangu ni kukudhibiti ili niweze kufanya yangu.
Alipomaliza kunena hayo Mashaka alitoka kinyumenyume na kuondoka.
Na safari yake ilikuwa ni kurudi tena Mwanza, nia yake ni kuonana na dada yake tena kabla ya kufanywa chochote na Maiko au Patrick.
Aliamua kufanya safari ya haraka kwa kutumia usafiri wa ndege, kwavile alikuwa na pesa bado kwahiyo haikuwa tatizo kwake katika swala la kusafiri na ndege.
Yuda na yeye aliondoka kwao kama alivyofanya Sele ila yeye alienda mjini kwa mambo yake tu.
Ndipo alipomuona Tina akiwa anakokotwa na kijana mwingine ila alipomuangalia vizuri akamtambua kuwa yule ni mfanyakazi wa Maiko na Mashaka kwahiyo aliamua kumfatilia nyumanyuma ili ajue wanapoelekea.
Tusa na Sele walirudi nyumbani, Deborah aliamua kuwa Tusa arudi na Sele kwaajili ya usalama wa Tusa kwani aliona akili ya Tusa kuwa kama akili ya mtu aliyechanganyikiwa.
Walipofika nyumbani ikabidi Sele amuhoji vizuri kwanza.
SELE: Tusa, una uhakika kuwa hospitali mliyompeleka Tina ndio ile?
TUSA: Mara ngapi niseme jamani? Nashangaa hamniamini, nishawaambia kuwa kweli ni hospitali ile.
SELE: Tusa, usifikirie vibaya bhana ni kwamba tunahitaji uhakika tu. Sina nia ya kukukandamiza wala nini.
Tusa akashangaa kuona bi.Rehema hatoki ndani kuwauliza ikabidi aende kumuangalia ila alimtazama kote bila ya mafanikio.
TUSA: Sele, simuoni bibi. Atakuwa ameenda wapi?
Sele nae akaingia ndani kumsaidia Tusa kumtafuta bi.Rehema ila hakuwepo.
SELE: Au ameenda dukani?
TUSA: Dukani kufanya nini? Huwa haendagi.
SELE: Mmh! Atakuwa wapi sasa?
TUSA: Labda kweli ameenda dukani, hebu tungoje kidogo kama atarudi.
Ikabidi wavute subira kidogo kuangalizia kama bi.Rehema atarudi.
Wakina Deborah ikabidi wagawane katika kumtafuta Tina, ikabidi wawili waende upande huu na wawili upande mwingine.
DEBORAH: Nadhani itakuwa vyema kama Adamu ukifatana na Fausta halafu mimi nikifatana na Pamela. Ila uwe makini sana safari hii.
Wakiwa wanaendelea kujadili, Fausta akamuona kijana ambaye alikuwa anamfahamu na kuanza kumuita.
FAUSTA: Tulo, Tulo.
Tulo akageuka na kutazama nani anamuita kwani safari yake ilikuwa ni kuingia ndani ya hospitali hiyo.
Tulo akamfata muitaji na kuwasalimia.
FAUSTA: Khee! Unafanya nini huku?
TULO: Tena bora nimekuona mama, nilipokuwa njiani nilikutana na Tina na mwenzie mmoja hivi ila Tina akaanguka...
Fausta hakungoja amalize, aliamua kumuuliza haraka.
FAUSTA: Yuko wapi huyo Tina?
TULO: Yupo hospitali ya chini hapo.
Ikabidi waanze safari ya kwenda nae huko hospitali.
DEBORAH: Sasa mbona Tusa alituonyesha hospitali ile?
TULO: Ni kweli tulifikia pale na Tusa akaja kuwaambia ila huduma pale ni mbovu, kuna mtu akatushauri twende pale chini kwahiyo nimempeleka Tina pale na kashafanyiwa vipimo ndio nikaja huku kumuangalia Tusa kama amerudi ili nimpe taarifa.
PAMELA: Hakuna tatizo ili mradi tumewapata.
Wakaenda hadi kufika hospitali.
Patrick na Mwita wakaongea mengi na kukubaliana kurudi nyumbani.
MWITA: Kama ulivyosema Patrick, kukimbia sio muafaka bora kurudi tu na kukabiliana na tatizo.
PATRICK: Ndio hivyo, bora kuwa nyumbani kwanza mengine yataeleweka tukifika.
Wakachukua usafiri na kwenda nyumbani.
Anna nae aliamua kwenda nyumbani kwa Marium ili kuzungumza nae kuhusu mambo yanayojiri.
ANNA: Hivi unaelewa kinachotokea kweli dada yangu?
MARIUM: Hata sielewi yani sielewi kabisa na huyo mwanangu Sele ndio ananichanganya zaidi.
ANNA: Kwani amefanyaje?
MARIUM: Nahisi amerogwa maana kule sio kupenda jamani, atakuwa amerogwa tu.
ANNA: Acha imani mbaya dada, amroge nani bhana?
MARIUM: Amerogwa na ule ukoo, kwanza haueleweki halafu yeye amekazana kung'ang'ania itabidi nimtafute mganga wa jadi nikaulizie kwanini mwanangu yuko vile.
ANNA: Utajisumbua tu dadangu, mapenzi hayaingiliwi na wala hayashauriki.
Ila Marium hakutaka kabisa kukubaliana na dhana kuwa yale ni mapenzi tu, alihisi lazima kutakuwa na kitu cha ziada.
Tusa akawa anajilalamisha kwa Sele kuwa lazima lawama zote atapewa yeye tu.
TUSA: Yani na huyu bibi asiporudi, basi mimi tu ndio nitaonekana mbaya siku zote utadhani mimi ndio mpangaji wa haya.
SELE: Usijari Tusa, yote haya yatapita na wote watarudi nyumbani.
TUSA: Ila Sele unajua kuwa mimi sistahili tena kuwa na wewe? Ila pia sitaki kuwa tena na Patrick.
SELE: Achana na hizo habari kwanza Tusa. Mimi bado nakupenda na nitakupenda siku zote za maisha yangu ila kwasasa sinabudi kukubaliana na ukweli kuwa wewe ni mke wa ndugu yangu.
TUSA: Roho inaniuma sana, najiona mkosaji siku zote sijui kwanini mimi. Ila kwa yote bado wewe unaonyesha kunipenda na kunijari.
Tusa akaenda na kumkumbatia Sele, muda huo Patrick na Mwita nao wanaingia ndani.
 
SEHEMU YA 70


Tusa akaenda na kumkumbatia Sele, muda huo Patrick na Mwita nao wanaingia ndani.
Patrick aliwatazama kwa jicho kali sana na wote wawili wakashtuka.
PATRICK: Mnashtuka nini? Endeleeni.
Sele na Tusa wakabaki kutazamana tu.
PATRICK: Hivi Sele, kwanini hupendi kunielewa? Nikikufanya chochote nitakuwa nimekuonea? Je upo tayari kufa kwa mapenzi?
Sele akabaki kimya huku akimsikilizia Patrick ambaye teyari alishakuwa na hasira.
Patrick akamsogelea Sele na kumpiga ngumi moja ambayo ilimpeleka hadi chini, Tusa akamfata Sele pale chini na kumuinua.
SELE: Halafu wewe jamaa sio kabisa yani huulizi wala nini unafikia kupiga tu sio vizuri bhana.
PATRICK: Sio vizurh eeh!! Haya Tusa muachie huyo mtu wako.
Tusa akabaki amemshika mkono Sele tu, sasa Patrick akaongea kwa ukali.
PATRICK: Nimesema muachie.
Tusa akatetemeka na kwenda pembeni.
Patrick akataka kumpiga tena Sele, Mwita akamsihi asifanye hivyo.
SELE: Mwache anipige bhana si kashazoea kutumia mabavu bila hata ya kujua nini tatizo.
PATRICK: Unajua Sele nitakuumiza wewe, sipendi tugombane ila wewe ndio unahitaji tugombane. Kuanzia leo, sitaki kukuona karibu na Tusa, hiyo ni amri na wala sio ombi.
Halafu Patrick akaenda chumbani kwake na kumuacha Mwita, Sele na Tusa pale sebleni.
Tina alipokuwa pale hospitali alipopelekwa na Tulo, baada ya Tulo kuondoka Tina akafatwa na Yuda.
YUDA: Tuondoke mahali hapa, hapakufai. Yule mkaka aliyekuleta ni mfanyakazi wa wakina Maiko.
TINA: Hapana Yuda, yule Tulo ni mtu mzuri tu na amekwenda kuwaita ndugu zangu.
YUDA: Tina, mi namjua yule hafai kabisa. Ni mtu mbaya, ni mfanyakazi wa wakina Maiko. Tuondoke hapa.
TINA: Hapana Yuda. Yule si mtu mbaya.
Yuda hakuelewa kuwa Tina anamjulia wapi Tulo na kwanini anamkatalia kile ambacho yeye anamwambia kuwa anamjua huyo Tulo.
YUDA: Ila basi kwa usalama wako tumuombe nesi akuweke sehemu nyingine ya mapumziko kwa muda, halafu mimi nitakuwa hapa kuangalia kama akija na ndugu zako niwalete.
TINA: Wasi wasi wako tu Yuda, ila ngoja tufanye usemacho.
Wakamuomba nesi naye akambadilisha chumba cha mapumziko.
Tulo alipofika pale alipomuacha Tina hawakumkuta na wote kushangaa.
ADAMU: Michezo gani ambayo mnatufanyia jamani!!
TULO: Jamani nilimuacha humu kweli, ngoja tuwaulize manesi.
Tulo akaenda kuuliza manesi na huku akafika Yuda na kuwaambia alipo Tina, ilibidi Fausta aulize kuwa tatizo ni nini.
YUDA: Sio mtu mzuri yule.
Wote wakabaki wanatazamana.
Yuda akaanza kuwaongoza alipo Tina na wao kumfuata ila Tulo nae alipowaona akaamua kuwafuata.
Bi.Rehema ambaye alikuwa mikononi kwa Mashaka sasa akakumbuka kuwa mara ya mwisho alikuwa nje.
MASHAKA: Sina nia mbaya dada, ila shida yangu ni kukiri kila jambo ambalo nilitenda kabla.
REHEMA: Kama nia yako ni nzuri, mbona ukaniteka sasa?
MASHAKA: Sikutaka wanione kwanza, najua wapo wenye hasira kali sana na mimi ingawa hawajawahi kuniona nikitenda huo uovu.
REHEMA: Hebu niweke wazi nijue, mwanangu tangia ameondoka pale nilipofikia hajaja tena je uko nae?
MASHAKA: Yeye yupo Arusha, mimi nataka nikiri mbele yako dada. Wewe ni ndugu yangu pekee uliyebaki, wote wameteketea sababu yangu.
REHEMA: Mmh!! Nitaweza kukusikiliza mwenyewe kweli mambo makubwa kama hayo ya kuteketeza ndugu wote? Naomba twende tukazungumze na hawa wachache waliobaki, kila mwanadamu ana haki ya kusamehewa najua hata wewe utasamehewa.
MASHAKA: Sidhani kama itakuwa rahisi hivyo.
REHEMA: Usijari mdogo wangu, kwani mimi umenifanyia mangapi mabaya na makubwa? Mbona nimekusamehe sasa, usiwe na shaka wote watakusamehe.
Bi.Rehema alikuwa akimvuta Mashaka kwa maneno ili aweze kuwa karibu nao ila kiukweli bado alikuwa na hasira kali sana dhidi ya Mashaka.
Wakaenda na kumuona Tina aliyekuwa katika mapumziko, wakati wanazungumza nae mara Tina akaanza kulalamika tumbo linamuuma, kuja kuinuka akawa amelowa damu.
Ndipo manesi wakaitwa na kuanza kumshughulikia huku ndugu zake wakiwa nje.
Badae wakaja kuambiwa kuwa mimba ya Tina imetoka, walimuhurumia Tina ila ile ikawa ni habari njema kwani aibu ambayo ingepatikana kwa mtoto ingekuwa ni kubwa sana.
DEBORAH: Kweli Mungu mkubwa, bora tu hiyo mimba imetoka.
FAUSTA: Ndio afadhari, nadhani sasa mwanangu ataishi kwa amani.
Wakatulia kungoja muda ambao Tina ataruhusiwa ili warudi nae nyumbani.
Patrick alitoka tena sebleni na kuhitaji kuzungumza na Tusa hivyo Sele na Mwita wakaamua kutoka nje kwani Tusa aligoma kwenda kuzungumza na Patrick chumbani kwake.
PATRICK: Hivi wewe Tusa unataka upendwe vipi? Unajua mambo mangapi nimefanya kwaajili yako? Hivi kweli mema yangu yote huyakumbuki? Yani wewe unakumbuka mabaya tu!
TUSA: Sio hivyo Patrick.
PATRICK: Hivi kweli isingekuwa hivyo, ungethubutu kukaa na umati wote ule humu ndani huku ukizungumza mabaya yangu? Ukafurahi sana kuzungumza maneno yale ulitaka wanione vipi?
Tusa alikuwa kimya tu kwani alikosa cha kujibu.
PATRICK: Eti alikuwa ananilazimisha mapenzi, sijui aliniingilia kinyume. Sasa hayo yanawahusu nini? Hata kama nilikulazimisha mapenzi wewe ni mke wangu na nina haki ya kupata penzi toka kwako.
TUSA: Una haki ndio ila si kwa kunilazimisha.
PATRICK: Hivi wewe Tusa lini umekubali kwa hiyari yako kunipa penzi? Lini? Ningekuwa nangoja ukubali haja zangu ningemalizia wapi wakati wewe upo! Halafu swala la kinyume unajua kabisa chanzo kilikuwa ni nini, hivi ni mwanaume gani atakayeweza kuishi na mkewe bila ya kufanya chochote ndani? Wewe ungekuwa mke au picha tu?
TUSA: Na kunitoa mimba kinguvu je?
PATRICK: Tumia akili Tusa, uliondoka na mimba yangu ukaenda na kuitoa halafu unakuja kwangu na mimba ya mwanaume mwingine ukitegemea mimi nilee! Mi sio mpumbavu kiasi hicho, ungekuwa hujawahi kutoa kweli hilo lingekuwa tatizo langu ila ulishatoa mimba kabla ulitegemea nini?
TUSA: Na kunipiga je?
PATRICK: Mwanamke yeyote jeuri dawa yake ni kipigo tu, Tusa wewe ni jeuri na kiburi. Ulitaka nikulee kama yai kuwa utavunjika? Kwangu ukileta ujeuri utasubiri dawa yako ya kipigo.
TUSA: Na kunifungia ndani je?
PATRICK: Na ule urembo wako wa kipindi kile ningekuachia vipi utembee nje? Ulitaka wajanja wa Arusha waniibie eeh!! Kwasasa nikienda nawe siwezi kukufungia ndani tena kwanza umeshachoka na huna urembo tena na mvuto wako wa mwanzoni wote umepotea. Tena ushukuru Mungu kuwa mimi bado nakujali mwanamke uliyechoka kama wewe.
Tusa alijisikia vibaya sana na machozi yakawa yanamtiririka kuona kuwa Patrick anaona kila alichomfanyia mwanzoni ni sawa.
PATRICK: Tena ngoja nikwambie, hata huyo Sele anayekufata hapa usifikiri ni mapenzi bali anakufata kwa kukuhurumia tu.
TUSA: Kwani mimi kosa langu ni nini jamani?
PATRICK: Kosa lako ni tamaa, tamaa ya mali, magari na pesa na tamaa waliyonayo wazazi wako haswaa mama yako.
Tusa akawa analia huku akikumbuka mambo ya nyuma, alimkumbuka Sele ambapo alipokuwa analia alikuwa akimbembeleza ila Patrick hakuwa hivyo na wala hakufanya hivyo.
TUSA: Kweli Patrick wewe una roho mbaya, hivi ni mwanaume gani wewe usiyejua hata kubembeleza jamani? Hata siku moja hujawahi kunifuta machozi halafu unadai unanipenda mmh!!
PATRICK: Wewe Tusa huwa unalia ujinga wako, kwahiyo mimi huwa nakuacha ulie hadi pale utakapotosheka utanyamaza.
TUSA: Hadi mamako humfanyia hivyo?
PATRICK: Mama haliagi ujinga wewe. Akilia basi ni mambo ya maana sio kama wewe unayelia ujinga ujinga.
Tusa akazidi kujiona mpumbavu.
Patrick akainuka na kutoka nje huku Tusa akiwa analia pale ndani.
Walipokuwa nje wale walioenda hospitali nao walikuwa wanarudi.
Patrick alishangaa kumuona Tulo pamoja nao.
 
Back
Top Bottom