RIWAYA: Mume Gaidi

RIWAYA: Mume Gaidi

SEHEMU YA 71


Patrick alishangaa kumuona Tulo pamoja nao.
Akajiuliza wamemtoa wapi na kwanini wameongozana nae.
Kufika karibu Tulo nae akamuona Patrick na hofu ikamjaa, Patrick alimfata Tulo na kumkunja ikabidi Deborah ndio amtete Tulo.
DEBORAH: Patrick mwanangu muache kijana wa watu hajafanya lolote baya.
Patrick kwa heshima ya mama yake akamuachia Tulo ila akataka kupewa maelezo xa kutosha kuwa yule Tulo ni nani yao.
Walipoingia sebleni, Pamela alienda moja kwa moja mahali ambako mwanae alikuwa amekaa na kujiinamia na machozi, ikabidi ainuke nae na kwenda nae chumbani.
PAMELA: Tatizo ni nini mwanangu?
TUSA: Mama, Patrick ameniambia maneno ya fedheha na kuumiza sana.
PAMELA: Kivipi na amekwambiaje?
TUSA: Yani kweli yeye wa kuniambia mimi kuwa ni mwanamke niliyechakaa, eti nimeshachoka anaendelea nami kwa kunihurumia tu, kwakweli mama sitaweza kuishi tena na Patrick naomba myasitishe mahusiano yetu ikiwezekana anipe talaka yangu tu.
PAMELA: Mmh mbona pagumu sana hapo mwanangu!! Unadhani Patrick atakubali?
Mara Deborah naye akaingia mule chumbani na kuwauliza kinachoendelea na shida ya Tusa ni nini.
DEBORAH: Tusa jamani, kwanini tusiyasuluhishe tu haya ili muendelee kuwa pamoja?
TUSA: Mama zangu, kiukweli sijisikii kuwa na Patrick na kamwe sitajisikia kwahiyo matatizo na migogoro hii haita isha kamwe, ataendelea kunibaka na kunipiga. Nimechoka sasa, kama hamtaki kunisambaratisha nae nitajua cha kufanya.
PAMELA: Unamaana gani Tusa?
Deborah ikabidi amwombe Tusa aende sebleni kwanza ili wao waweze kujadili.
DEBORAH: Unadhani tufanyeje Pamela?
PAMELA: Mimi sijui, sijui kabisa mwanangu ana matatizo gani kwani nionavyo mimi Patrick ni mtu sahihi kwake cha muhimu ni kuelewana tu.
DEBORAH: Kwavile leo wote wapo, basi twende tukajadili ili kujaribu kuwapatanisha kwanza.
Wakakubaliana kwenda kufanya mazungumzo kwaajili ya kutatua tatizo baina ya Patrick na Tusa kwanza kabla ya chochote.
Bi.Rehema aliendelea kumuomba Mashaka kuwa akubali waende nae kwa Deborah, ila Mashaka aliendelea kukataa kufanya hicho ambacho anaambiwa na dada yake kwa kuhofia usalama wake na maisha yake.
MASHAKA: Dada, huko nitakutana na mtu mmoja anaitwa Patrick. Mtu huyo ni khatari sana dada yangu, anaweza hata kunichinja.
REHEMA: Wasiwasi wako tu ila Patrick si muuaji, yeye hupenda kusaidia watu walioko kwenye matatizo.
MASHAKA: Dada, nadhani humjui vizuri huyu Patrick na kwanini nakwambia kwamba ni mtu khatari. Patrick hafai kabisa, bora mimi chui unayenijua kuwa chui kuliko huyo Patrick. Amevaa ngozi ya kondoo kumbe ni chui mla watu.
REHEMA: Mbona sikuelewi Mashaka!!
MASHAKA: Unajua Patrick kaua watu wangapi? Unadhani atashindwa vipi kunimaliza na mimi? Patrick hujifanya kuokoa mmoja na kuangamiza zaidi ya kumi.
REHEMA: Mmh!! Ila hata hivyo pale hawezi fanya chochote ukizingatia mama yake yupo tena na wengi tu.
Rehema aliendelea kumuomba Mashaka hadi akakubali.
Mashaka akamwambia Rehema kuwa aende nae huko kwa Deborah.
Kufika karibu na nyumba ya Deborah, Rehema akashuka huku akimngoja Mashaka nae ashuke waweze kwenda ila alichofanya Mashaka ni kushusha kioo cha gari kisha akamuaga dada yake kuwa atakuja siku nyingine na kuondoka zake.
Mashaka bado alikuwa na hofu ya kukutana na Patrick kwani alijua ni jinsi gani Patrick alivynkuwa na hasira juu yake.
Pamela na Deborah wakarudi sebleni na kumuulizia Tusa ili waweze kuanza hicho kikao ila wakaambiwa kuwa Tusa ameenda dukani.
PAMELA: Ameenda peke yake?
PATRICK: Ndio, ila hakuna tatizo lolote.
Ndipo hapo wakakumbuka na kitu kingine kuwa bi.Rehema hayupo, wakamuuliza Sele ambaye alifika na Tusa mwanzoni naye akasema kuwa hawakumkuta.
Hofu ikawatawala kuwa mmama yule wa makamo atakuwa wapi.
Wakaji wanajiandaa kutafuta, bi.Rehema nae akawa anarudi, wakamshangaa na kumuuliza alipokuwa.
REHEMA: Nimekuja na Mashaka hadi hapa ila amekataa kuingia ndani na kuondoka.
Patrick akashtuka kusikia Mashaka ukizingatia Tusa nae alikuwa dukani.
PATRICK: Mmekutana na Tusa?
REHEMA: Hapana, hata hatujamuona.
Patrick bado hakuridhiwa kwani alimjua vizuri Mashaka kwa Tusa, ni kama vile simba kwa swala ikabidi atoke kwenda kumuangalia ila kwa bahati akamuona Tusa anarudi ndipo hapo aliporudi tena ndani.
Marium alikazana na lengo lake la kuonana na mganga wa jadi kwaajili ya mwanae, akaenda kwa mzee mmoja aliyeambiwa kuwa anahusika sana na mambo ya asili kumuulizia.
MZEE: Mwanao na huyo mwanamke hawawezi kuachana kabisa tena hawawezi kuachana kirahisi hivyo kama unavyodhani.
MARIUM: Vipi? Mwanangu amerogwa eeh!
MZEE: Kuna kitu kati yao ambacho walikifanya huko nyuma kabla, siku moja mdadisi mwanao.
MARIUM: Kitu gani hicho?
MZEE: Jaribu kumuuliza mwanao akwambie.
MARIUM: Je, kinaweza kutenguka na wakaachana? Nisaidie mzee, kiukweli yule binti hamfai kabisa mwanangu. Naomba unisaidie.
MZEE: Kuachana kwao labda mmoja afe ila la sivyo itabidi ukubali tu matokeo. Mwanao kampenda sana yule binti na yule binti nae kampenda sana mwanao na ndiomana anapata shida hata kukaa na kutulia na mwanaume mwingine hawezi anataka kurudi kulekule na kwa mwanao nae ndio hivyohivyo. Nadhani watakuwa wanajutia juu ya walichofanya ila ndio hivyo hakiwezi kutenguka.
MARIUM: Jamani mzee nisaidie, yule binti kachoka kashabakwa na wanaume hamsini kidogo sitapenda awe na mwanangu nakuomba unipe msaada wako.
MZEE: Labda ukajaribu kwingine ila kwa mimi imeshindikana.
Marium aliondoka akiwa amenywea sana ila akasema kuwa hawezi kukubali hadi pale atakapofanikiwa kumtenganisha Sele na Tusa ili wasikumbukane tena na Sele aweze kuoa mwanamke mwingine.
"wangapi wanaachana na kuoa na kuolewa na watu wengine tena mara nyingine ndoa hazidumu wanaoa tena na kuolewa tena na tena kwanini wao ishindikane? Sele lazima amuache yule mwanamke kwani hamfai kabisa kashachoka na kuchakaa, sijui Tusa alimpa limbwata mwanangu dah!! Limbwata lake kali sana ila lazima nitalitengua tu."
Maiko kuona mambo ya Mashaka hayaeleweki akapatwa na hisia kuwa huenda Mashaka amerudi tena Mwanza kwahiyo na yeye akaamua kufanya safari ya kwenda Mwanza kwani hakumuamini Mashaka hata kidogo, alihisi kuwa anaweza kuisambaratisha familia yake ndogo aliyoijua ukubwani.
Baada ya wote kukamilika, ikabidi wafanye mazungumzo ya kumpatanisha Patrick na Tusa, walizungumza mengi ila Tusa alionekana kulia na kujiinamia muda wote.
PATRICK: Jamani mimi sina tatizo, Tusa ni mke wangu na ninampenda. Ninachomuomba ni kuwa atulie na mimi tu, tatizo lake huyu Sele anamchanganya sana akili.
DEBORAH: Achana na hayo ya Sele Patrick, tuzungumzie haya kwanza. Sele ni muelewa na hawezi kuendelea kumfatilia mke wa mtu.
Deborah alimtetea Sele bila ya kujua kuwa Sele mwenyewe muda wote mawazo ni kwa Tusa.
PAMELA: Mi ninachoona Tusa atulie tu na Patrick.
ADAMU: Ngoja tumsikie na Tusa mwenyewe ana maoni gani.
TUSA: Mimi sitaki kuendelea kuishi na Patrick kwani matatizo baina yangu na yake hayataisha. Ingawa Patrick ni mume wangu ila nakiri wazi na mbele yenu kuwa simpendi.
FAUSTA: Jamani Tusa acha kuongea maneno makali kiasi hicho.
PATRICK: Mimi nampenda Tusa na pia nakiri wazi kuwa siwezi kuachana nae.
Wakaendelea kujadili na kumsihi Tusa awe na Patrick kwakuwa ni mumewe.
PATRICK: Nimefunga nae ndoa ya gharama sana, siwezi kuachana nae jamani. Tusa ni mke wangu cha msingi ni mumshauri kuwa atulie tu.
Tusa akainuka na kwenda jikoni.
PATRICK: Tusa ana kiburi sana na jeuri, mwambieni abadilike ili tujenge maisha yetu. Sipendi kurumbana nae kila siku wakati ni mke wangu.
PAMELA: Tumekuelewa Patrick, usijari Tusa nae atakuelewa tu.
Sele alipoona muda umepita bila Tusa kurejea akaamua kwenda jikoni na kumkuta Tusa chini, akamkimbilia na kumshika kisha akawaita waliokuwa sebleni.
Wote wakashangaa kumuona Tusa akitapatapa pale chini huku povu likimtoka mdomoni.
Tusa alikuwa amekunywa sumu.
 
SEHEMU YA 72

Wote wakashangaa kumuona Tusa akitapatapa pale chini huku povu likimtoka mdomoni.
Tusa alikuwa amekunywa sumu.
Pamela alipomuangalia mwanae pale chini akaangua kilio,
"Jamani mwanangu, mwanangu amekufa jamani"
Patrick akadakia na kuwaambia,
"Kweli nyie akili ni fupi, sasa kulia kutakusaidia nini?"
Patrick akainama na kumbeba Tusa begani kisha akaianza safari ya hospitali, wengine wakamfata nyuma tu.
Sele alikuwa kama vile kachanganyikiwa, alikazana kuomba kuwa Tusa apone na awe mzima.
Wengine wakaenda hospitali na wengine wakabaki nyumbani.
Pale hospitali wakaanza kumuhudumia Tusa na kugundua kuwa amekunywa sumu, ikabidi wafanye kazi yao ya kukata ile simu kwanza kisha kumuwekea dripu.
Daktari akawafuata ili azungumze nao ila Patrick akasogea na daktari pembeni ili azungumze nae yeye,
DAKTARI: Inaonyesha kuwa mgonjwa wenu amekunywa sumu.
PATRICK: Hilo tunalitambua labda useme lingine, kwani anaendeleaje?
DAKTARI: Maendeleo yake si mabaya, nadhani atapona.
PATRICK: Apone bhana ndio tunachokitaka.
DAKTARI: Mambo haya huhusiana na ripoti ya polisi sababu kujiua ni kosa kisheria na inahitajika mtuhumiwa awe chini ya ulinzi sasa.
PATRICK: Sawa nimekuelewa, kwahiyo unataka kufanya nini?
DAKTARI: Tunahitajika kuandika ripoti na kuipeleka polisi kabla hawajapata taarifa hii toka kwa wengine.
PATRICK: Wewe daktari unajipenda kweli?
DAKTARI: Ndio najipenda kwani vipi?
PATRICK: Kama unajipenda, tafadhari achana na hizo habari. Nyie muhudumieni akipona turudi nae nyumbani basi.
Daktari akashangaa kauli ya Patrick kwani yeye alikuwa anamuelezea kwaajili ya kupoozwa na vitu kama rushwa ila akashangaa jibu alilopewa na Patrick.
Yule daktari aliwafata madaktari wenzie wawili na wao wakaenda kumchungulia Patrick, daktari mmoja wapo alipomuona Patrick alishtuka sana kwani alikuwa ni yule daktari aliyetishiwa silaha na Patrick kwa kudai PF3.
DAKTARI 1: Dah! Kumbe ni yule jamaa, muacheni kama alivyo mafia yule.
DAKTARI: Kwani unamjua?
DAKTARI 1: Ndio namjua, kwanza pale usimuone vile anatembeaga na mguu wa kuku yule. Mi simo kabisa, kama mtaamua kuchonga kachongeni wenyewe tu.
DAKTARI 2: Hata mi mwenyewe namjua, akiamua kukupiga hutathubutu kuamka.
DAKTARI: Sasa kama anatumia ubabe kama huo, hajui kuwa sisi tunauwezo wa kumpoteza mgonjwa wake?
DAKTARI 1: Thubutu kama hujazikwa pamoja na huyo mgonjwa wake, jamaa yule ana machale balaa. Yule ni mafia nakwambia.
DAKTARI: Mmh! Jamani mi najipenda, naipenda kazi yangu na familia yangu naipenda, tuachaneni na mambo haya twendeni tukamuhudumie tu huyo mgonjwa.
Madaktari wakaamua kuendelea na kazi yao.
Pamela alijisikia kulia tu kwani uamuzi ambao mwanae ameuchukua uliwatisha sana, familia nzima ilijikuta ikiogopa.
Tusa akalazwa kwa takribani siku mbili ili kurejeshwa katika hali ya kawaida.
Anna alipopata habari ya Tusa ikabidi amfate dada yake Marium kwenda kumwambia na kumuuliza.
ANNA: Au kuna kitu umefanya dada yangu?
MARIUM: Kwanza mi mwenyewe hiyo habari ya Tusa kunywa sumu inanitisha na kunishangaza. Ni kweli sipendi Tusa awe na mwanangu ila siwezi kuwatenganisha kwa kifo bhana mdogo wangu.
ANNA: Basi hofu ikanishika, nilijua umeenda kwa hao waganga wako na kuwaomba wamuue maana watu hao nao wana njia nyingi kweli za kumaliza watu.
MARIUM: Itabidi twende tukamuone, haya sasa majanga ndiomana mwanangu Sele hajarudi kabisa. Yuda nae yupo kama mwizi mwizi vile haonekani nyumbani hata sijui anakuwa wapi siku hizi.
Ikabidi wajiandae na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwa Deborah wakijua labda Tusa ameshatoka.
Yuda ambaye alibaki na Tina pale nyumbani siku hiyo ambayo bi.Rehema naye aliomba kwenda hospitali kumuona Tusa.
Yuda akaamua kuutumia muda huo kuzungumza na Tina.
YUDA: Tina natumaini sasa matatizo yako yameisha, mimi swala langu kwako lipo palepale. Nataka kuwa na wewe.
TINA: Ingawa nimebakwa na unalijua hilo, bado wataka kuwa na mimi?
YUDA: Ndio Tina, nakupenda niamini hivyo Tina. Ukikubali kuwa na mimi nitakuoa Tina.
TINA: Mmh!! Hapana, bora niolewe na mwanaume ambaye hafahamu ukweli. Wewe Yuda unajua kila kitu lazima badae utanitusi kwa kejeli tu.
YUDA: Hapana Tina, siwezi fanya hivyo. Nimekuwa nikikufatilia kwa muda mrefu sasa. Uliniambia nitafute pesa kwanza, Tina utajiri ni majaaliwa ya mwenyezi Mungu nikubalie kwanza na tutafunga ndoa na kufanya sherehe kubwa uitakayo. Nikubalie Tina, nateseka mwenzio.
Tina akamuangalia sana Yuda na kushangaa kwanini bado ana moyo wa kutaka kuwa na yeye, Yuda nae akamsogelea vizuri Tina ili apewe jibu la uhakika.
YUDA: Tafadhari Tina nijibu nakupenda sana.
Tina akatikisa kichwa kama ishara ya kukubali.
Marium na Anna walipofika kwa Deborah wakaingia sebleni moja kwa moja bila hata ya kubisha hodi kwani walishapozoea.
Wakawakuta Tina na Yuda wamekaa mikao ya kihasara hasara, jambo la kwanza alilouliza Marium ni kuwa.
MARIUM: Nini kinaendelea kati yenu?
Yuda na Tina wakabaki kumtazama tu.
MARIUM: Mbona hamnijibu?
YUDA: Mama, kwasasa Tina ni mchumba wangu mtarajiwa.
MARIUM: Mmh!! Aliyenirogea wanangu kwakweli atakuwa amekufa.
Wakati wakiendelea kuzungumza, wale waliokuwa hospitali nao wakarejea, Tina akafurahi sana kumuona Tusa. Akainuka na kwenda kumkumbatia, kisha wote wakainuka na kusalimiana kisha kukaribishana.
Maiko aliingia jijini Mwanza akiwa na lengo moja tu la kumtafuta Mashaka kwani alijua kwa vyovyote vile atakuwa amekimbilia mkoa huo.
Nia yake kubwa ilikuwa ni kummaliza Mashaka popote pale atakapo muona atakuwa halali yake.
Tulo na Mwita nao wakazoeana kutokana na lile seke seke la kumpeleka Tusa hospitali. Wakajikuta wakiongea mambo mengi sana, wakati wenzao wamerudi nyumbani wao walielekea mjini kwa kupata vinywani na kuongea mambo mbalimbali.
MWITA: Unajua kinachonishangaza ni kwanini Patrick hataki kumuacha Tusa na kwanini Tusa hataki kuishi na Patrick.
TULO: Patrick ni gaidi bhana, hastahili kuishi na Tusa. Yule binti ni mpole sana halafu hajui kuzungumza, Patrick anatakiwa aishi na wale mabinti mcharuko ila Tusa hamfai. Na kama kumtesa dah!! Amemtesa sana, yule binti usimuone vile kateseka yule hadi kawa sugu.
MWITA: Sasa kwanini hataki kumuacha?
TULO: Pesa Mwita, Patrick amemgharamikia sana Tusa na ameshafanya mambo mengi mabaya kwaajili ya yule binti ndiomana hataki kumuacha ila sidhani kama anampenda tena sababu kama angempenda basi angemuacha apumue kwanza ila yeye kamng'ang'ania kama ruba.
MWITA: Na ilikuwaje hadi akamuoa?
TULO: Yote hayo ni mambo ya pesa, aliyesema pesa ni shetani hakukosea. Pesa ni mdudu mbaya sana kwani huharibu utu wa mtu kwa sekunde tu. Patrick anaumizwa na gharama zake juu ya Tusa, kule Arusha wanawake wengi wanampenda na kumuhitaji kwa sana ila yeye amekazana na Tusa tu. Labda kuna kitu cha ziada zaidi ya pesa kinachomvuta kwa Tusa.
MWITA: Mmh!! Khatari.
TULO: Ungemuona yule binti mwanzo kwakweli hata ungekuwa wewe ungemuhurumia kwa sasa. Alikuwa mzuri, mrembo na wa kuvutia. Ila sasa yupo kama wale misukule, dah anatia huruma. Ila Patrick mbabu na hashauriki sijui hata itakuwaje, labda atamuhurumia kwasasa baada ya kutaka kujiua.
MWITA: Basi itabidi Tusa akubali kutulia na Patrick.
TULO: Kwa mateso aliyopitia hawezi nakwambia, hata ingekuwa ni mimi ningekataa pia.
Walizungumza mengi, yale yote waliyoshindwa kuyazungumza mbele ya Patrick sasa waliyasema.
Nyumbani kwa Deborah waliona itakuwa vyema kwa Tusa kupata muda wa kupumzika kabla ya kuzungumza mambo yote yaliyojiri ila safari hii waliona kuwa itakuwa vyema kukaa karibu na Tusa ili kujua tatizo lake haswa ni nini hadi anakataa kiasi kile kuishi na Patrick. Ingawa alishawaeleza mambo mengi ila walihisi kuna kitu cha ziada ambacho Tusa anakificha.
DEBORAH: Jamani inatakiwa kila mmoja afunguke ili tujue jinsi ya kuokoa tatizo hili.
Wakakubaliana kuweka tena kikao cha familia ili wawekane sawa.
Mashaka nae aliendelea na mipango yake kama kawaida, wakati yupo mjini alionwa na Maiko.
Mashaka hakujua kama anafatiliwa.
Alirudi kwenye hoteli aliyofikia, alipoingia chumbani tu akasikia mtu akigonga mlango wa chumba kile.
 
SEHEMU YA 73

Alipoingia chumbani tu akasikia mtu akigonga mlango wa chumba kile.
Mashaka akaenda kufungua huku akitarajia kuwa mgongaji atakuwa ni muhudumu wa hoteli ile.
Ila alivyofungua tu, Maiko alizama moja kwa moja ndani na Mashaka akamshangaa kuwa amejuaje kama yuko hapo.
MASHAKA: Umejuaje kama niko hapa?
MAIKO: Swali gani hilo? Nimekufatilia mwanzo mwisho.
MASHAKA: Najua umekuja kutimiza ahadi yako.
MAIKO: Ndio na leo sitazitaka hizo porojo zako.
MASHAKA: Maiko, hivi umejaribu kufikiria kuwa tumepoteza kazi ngapi, tumepoteza hela ngapi kwa huu upuuzi na ujinga? Hivi unajua kama ipo siku utakuwa masikini wa kutupwa sababu kwasasa unajua kutoa na si kuingiza. Fungua macho Maiko, ingawa ni mambo ya khatari ambayo tuliyafanya ila ndio mambo hayo yanayofanya tujidai na kutanua. Kila mmoja anafanya atakacho kwa pesa tuliyo nayo. Pata picha kama tungekuwa hatuna kitu.
MAIKO: Nina uhakika, kama tusingekuwa na kitu sasa ingesaidia sana kwani ingemaanisha kuwa hatufanyi kazi haramu, kazi ambayo imetuingizia pesa haramu na kazi hizo ndio zinazofanya tugombane sasa.
MASHAKA: Najua Maiko utanilaumu mimi kwa kazi zetu, na kama hivyo wataka kunimaliza. Ila jua kwamba wewe utamalizwa na Patrick kwani atakulaumu wewe siku zote. Umejipanga vipi kukabiliana na Patrick??
Maiko akaona kuwa Mashaka anamuwekea usiku tu, akajaribu kufikiria kuhusu swala la Patrick.
MASHAKA: Tena Patrick kama vile kwaajili yako, kumbuka kuwa wewe ndiye uliyemfundisha ujangili.
MAIKO: Ila mimi nilifundishwa na wewe.
MASHAKA: Atakuamini vipi, je kile kichwa ambacho Yuda alikikuta kwako ni mimi nimekufundisha? Hivi hujishangai Maiko kama wewe si binadamu wa kawaida?
MAIKO: Mimi ni mtu wa kawaida tu kama walivyo binadamu wengine.
MASHAKA: Unajua binadamu wa kawaida hawezi kulala hata usiku mmoja pembezoni mwa maiti? Wewe sasa, una vichwa vya marehemu wengi tu ndani kwako tena bila hofu nawe unalala kwenye nyumba hiyo hiyo. Mi huchukua viungo na kwenda kuviuza ila sio kwamba nitakaa navyo ndani kwangu kama wewe ufanyavyo Maiko. Sijui kama unaweza kusamehewa duniani na huko akhera, tena bila aibu unataka kujidai kuwa umebadilika kwa kuua tena! Unataka kuniua mimi, hayo si mabadiliko Maiko bali unajiongezea dhambi mbele za Mungu tu.
MAIKO: Kumbe hadi wewe unatambua uwepo wa Mungu? Ila bado sijaridhika, upo muda ambao kichwa chako hicho kitakuwa halali yangu.
MASHAKA: Na hakuna atakaye shangaa kwani kutunza vichwa vya marehemu ni kawaida yako.
Maiko alijifanya kupotezea ila maneno mengi aliyoambiwa na Mashaka yalimuingia sana. Akaamua kuondoka kwanza huku akijiuliza kuwa kwanini anasita kummaliza Mashaka wakati yeye akiamua kitu ameamua na huwa lazima akitekeleze kitu hicho.
Mwita na Tulo walilala kwa rafiki wa Mwita siku hiyo, mahali kule alipofikia Mwita kwa mara ya kwanza.
Mjeshi huyo aliyeitwa John ndiye aliyemuhabarisha Mwita juu ya kifo cha rafiki yake Hamisi.
MWITA: Inamaana Hamisi alikufa?
JOHN: Ndio, katika wale wajeshi sita waliouwawa kikatili na yeye alikuwa mmoja wao.
Mwita alisikitika sana kwani hakupata habari yoyote ukizingatia hakuwa na mawasiliano na watu wa Singida tangia siku aliyoondoka kwani aliacha na simu kabisa kwa kuhofia kutafutwatafutwa kabla hajampata baba yake.
Baada ya ile taarifa akaamua kuwasiliana na watu wa Singida, nao wakampa taarifa rasmi huku wakimwambia kuwa wamemtafuta sana kwa mahojiano ila hakupatikana kwani Hamisi alionekana mara ya Mwisho akienda nyumbani kwa Mwita na mwili wake ulitupwa mahali ambako si mbali sana na nyumbani kwa Mwita.
Alipokata simu akamgeukia John na kumuuliza.
MWITA: Inamaana Hamisi ameuwawa nyumbani kwangu?
JOHN: Itakuwa maana hata watu wanasema kuwa kwako ilisikika harufu ya damu ingawa damu hiyo haikuonekana.
Mwita akawa na maswali mengi sana kichwani mwake, akajikuta akimuhusisha Patrick kwenye yale matukio ila upande mwingine wa akili yake ukakataa kuwa si Patrick aliyefanya yale.
Maiko aliyawaza maneno ya Mashaka kwa kina na kujiuliza kama anastahili kutubu.
"Hivi nastahili kutubu kweli? Mungu atanisamehe kweli? Sijulikani Msikitini wala Kanisani, wapi nitaenda na kupokelewa mimi? Nawachukia Mashekhe na Wachungaji, nishawafanyia mengi mabaya. Sidhani kama nitasamehewa mimi binadamu ambaye sieleweki wala sina uelekeo. Nimewaumiza wanawake wengi sana, watoto wengi na sikuwa na huruma yoyote hadi nimewabaka na wanangu na kumuua baba yangu. Nitasamehewa kweli? Huyu Mashaka huyu nae anastahili kuuwawa tu, sio kila dhambi kunigeuzia mimi tu. Lazima auwawe ila je nikimmaliza itakuwa mwisho wa utajiri wetu? Ni kweli wanausalama watalijua hili swala la mauaji ambayo nimewahi kufanya? Wapi mimi, nimekuwa mtu mbaya sana"
Alikuwa akijilalamisha tu na kuamua jambo moja kwenda kuzungumza na Patrick alijua huyo lazima amlainishe na kujaribu kufanya kitu kizuri kwa wao na familia inayoonekana mbele yao.
Hali ya Tusa sasa haikuwa mbaya sana ila walipomuhoji bado aliendelea kuwa na msimamo wake uleule wa kukataa kuishi na Patrick, na Patrick nae alipohojiwa msimamo wake ukabaki uleule wa kuishi na Tusa.
Pamela alichanganywa kabisa na maamuzi ya Tusa kwani alijua wazi Tusa akiendelea na maamuzi yale basi umasikini unawanukilia yeye na mumewe kwani Adamu hakutaka kuona mwanae akiendelea kuteseka kisa pesa ambayo Patrick alimgharamia.
Kesho yake Mwita na Tulo waliondoka nyumbani kwa John, leo hii Mwita alivaa kijeshi.
Tulo alimuuliza Mwita kama wanauhusiano gani na ile familia ya kina Patrick, Mwita akamueleza kuwa baba yake ni Maiko kwakweli Tulo alishtuka sana.
TULO: Je, unajua kazi ambayo Maiko anaifanya?
MWITA: Sijui chochote, baba mwenyewe nimemfahamu ukubwani.
TULO: Wewe ni mwanausalama wa nchi hii Mwita, hata sijui itakuwaje ukigundua.
Mwita akajaribu kumdadisi Tulo ili amuelezee ila Tulo akapotezea kwa kumletea story zingine.
TULO: Unajua mimi nimecheza sana utotoni na Tina, halafu nimesoma nae tulikuwa kama dada na kaka ila kiukweli nampenda sana.
MWITA: Unampenda kimapenzi?
TULO: Ndio, tena sana.
MWITA: Je, umewahi kumwambia?
TULO: Hapana sijawahi ila hata yeye Tina inaonyesha kuwa ananipenda, nadhani napaswa kumwambia ukweli hisia zangu.
MWITA: Ndio mwambie ajue, chelewa chelewa utamkuta mwana si wako. Wasichana wengi ni wagumu kumuanza mtu kuwa wanampenda hubaki na yao moyoni, na wewe ukijigelesha anaweza fika mjanja na kukupiku. Changamka kijana.
Wakakubaliana kwenda kwa Deborah, huku Mwita akiwa na lengo la kuzungumza na Patrick ili amdadisi kuhusu vile vifo na Tulo nae akiwa na lengo la kuzungumza na Tina.
Deborah na Fausta ikabidi wazungumze na Patrick kujua ni gharama gani ambazo anazisema kuwa kamgharamia Tusa.
PATRICK: Mama, mahali tu nilitoa shilingi milioni kumi na tano.
FAUSTA: Milioni kumi na tano!! Walikuwa wanamuuza au?
DEBORAH: Mbona pesa ni nyingi sana?
FAUSTA: Ndiomana mdogo wangu Pamela hana usemi, pesa ni nyingi mno watairudishaje pesa yote hiyo? Tunapaswa kuzungumza juu ya hili jamani.
DEBORAH: Jamani Pamela anapenda pesa sana, yani mahali milioni kumi na tano? Mahali gani hiyo? Ndiomana pesa yako inakuuma mwanangu Patrick.
Ikabidi Deborah na Fausta waingie ndani kwa mazungumzo zaidi.
Patrick alizunguka nyuma ya nyumba yao, alipopiga jicho mbele akamuona Maiko.
"Amefata nini tena huyu firauni hapa?"
Maiko hakuja kwa shari bali alienda kwa utaratibu kabisa ili kuzungumza na Patrick ila Patrick alikuwa na chuki na hasira za wazi dhidi ya Maiko haswa kitendo cha Maiko kumchinja baba yao na wakina Yuda ambaye Patrick alimuona kama baba yake pia.
Patrick alizidi kupandwa na hasira kadri Maiko alivyosogea.
 
SEHEMU YA 74

Patrick alizidi kupandwa na hasira kadri Maiko alivyosogea.
Maiko nae aliendelea kumsogelea Patrick ila akaona mabadiliko ya Patrick usoni ikabidi aongee kabla hajamsogelea zaidi.
MAIKO: Tafadhari Patrick, sijaja kwa shari leo. Nina shida na mazungumzo na wewe Patrick. Nisogee hapo?
Patrick alimuangalia tu bila ya kumjibu chochote ila alitikisa kichwa kama ishara ya kukubali. Maiko nae akamsogelea zaidi ili apate kuzungumza nae.
MAIKO: Tafadhari Patrick naomba tumalize tofauti zetu.
PATRICK: Unajua wazi tofauti zetu haziwezi kuisha labda useme lingine.
MAIKO: Nataka tushirikiane kumuangamiza Mashaka.
Patrick akacheka sana, kisha akaondoka pale na kwenda mbele na kuingia ndani, Maiko akajikuta akibaki mwenyewe na kujiuliza kwanini Patrick amemcheka.
Maiko akiwa pale nje anamuona Mwita na Tulo wakifika pale.
Maiko akamshangaa Tulo kwa kumuona pale.
MAIKO: Kwani mnajuana?
MWITA: Tumejuana hapahapa, nadhani hii ni sehemu ya makutano.
MAIKO: Nadhani Tulo hapa umemfata rafiki yako Patrick, nafikiri pia itakuwa vyema kama utanisaidia kuzungumza nae.
TULO: Kuzungumza na nani, Patrick?? Hapana, namuogopa sana.
Ikabidi Maiko amuulize alichofanywa na Patrick.
MAIKO: Kwani amekufanyeje?
TULO: Nitakueleza tu usijari.
MWITA: Na mbona uliondoka bila ya kuniaga?
MAIKO: Dah!! Kuna kitu kilinichanganya bhana. Ila usijari.
Tulo alikuwa anamuelewa Maiko na anajua kuwa Maiko si mtu wa kuaga huwa anajiondokea tu.
Mwita akaingia ndani na Tulo akabakia pale nje na kumueleza kilichompata.
MAIKO: Dah! Na wewe zoba kweli, yani ulikubali kutumwa na Mashaka kwa Patrick!! Yeye mwenyewe kamshindwa.
TULO: Ndomana sijarudi Arusha hadi leo.
MAIKO: Hakuna tatizo, fanya kuwa karibu na Patrick huwezi jua, anaweza kukubali kuwa na sisi tena.
Wakaongea mawili matatu na Tulo kumfata Mwita ndani.
Fausta alimfata Adamu kwa lengo kumuuliza.
FAUSTA: Hivi kaka, unamuozesha mtoto kwa milioni kumi na tano kweli? Ulikuwa unamuuza au ni vipi?
ADAMU: Muulize mdogo wako maana posa hiyo aliipanga yeye.
FAUSTA: Na je mkafanyia nini?
ADAMU: Vitu vingi tu vya biashara ila nyingine tulikula.
FAUSTA: Ndio kipindi kile nini ambacho mlikuwa mkitanua? Kumbe mnatanulia pesa ya posa. Mtaweza kuilipa sasa maana mwananu kagoma kuishi na huyo mwanaume.
ADAMU: Tutailipa tu ila hasara yake itakuwa kubwa sana.
Pamela akawafata na kumuuliza mumewe.
PAMELA: Baba Tusa, tutailipaje hiyo pesa? Mi nadhani swala la muhimu ni kumuomba Tusa akubali tu kuishi na Patrick.
Pamela alikuwa hajielewi kabisa kwani hata alishindwa kuwaza namna ya kuipata hiyo pesa na kuirudisha.
Patrick alienda moja kwa moja kuzungumza na Tusa.
PATRICK: Hivi Tusa unajua kuwa unaipa familia yako umaskini kwa kuachana na mimi!!
TUSA: Umaskini kivipi sasa?
PATRICK: Wazazi wako unadhani watapata wapi pesa za kunilipa! Nimekutolea mahari kubwa sana Tusa. Ingekuwa laki tisa kushuka chini ningesamehe ila milioni kumi na tano!! Siwezi kuisamehe, hapa ni mimi kuendelea na wewe au wazazi wako kuilipa hiyo pesa.
TUSA: Bora wakulipe tu, sitaweza kuendelea kuishi na wewe. Mume gani nisiyetambua hata kazi yako? Bora tu tuachane.
PATRICK: Na utakula mapumba na huyo Sele wako asiyejielewa.
TUSA: Hata tusipokula poa tu.
Patrick alifanya kama vile kumtania Tusa huku akimpa maneno ya ukweli.
Marium aliamua kuondoka na familia yake ili waende kuzungumza vizuri.
SELE: Ila mama mi nitarudi tu badae.
YUDA: Hata mimi nitarudi.
Kwahiyo Mwita na Tulo hawakuwakuta watu hawa, Maiko hakutaka hata kuingia ndani aliendelea kubaki pale pale nje akitafakari mambo yake.
Mwita alitulia pale ndani akimngoja Patrick aliyekuwa chumbani ili apate kuzungumza nae.
Tulo nae alipomuona Tina amekaa mwenyewe akaona ni vyema kuzungumza nae.
Wakaongea mengi na stori za hapa na pale.
TINA: Kwani Tulo umekuja lini Mwanza?
TULO: Mbona kama wiki mbili zilizopita.
TINA: Na unalala wapi siku zote hizo?
TULO: Hotelini bhana.
TINA: Una hela za kuchezea eeh!!
TULO: Waswahili husema, tumia pesa ikuzoee. Pesa ninayo na raha ya pesa ni matumizi. Lini mtarudi Dar?
TINA: Hata sijui, vipi maisha lakini?
TULO: Yameninyookea kiasi, nina nyumba yangu. Gari mbili moja yangu na nyingine nitampa mwanamke nimpendaye.
TINA: Hongera sana, nani atapata hiyo bahati ya kukabidhiwa gari ya pili?
TULO: Unataka kumjua Tina? Tena si gari tu bali nitampa vitu vingi, kila akitakacho kwangu atapata.
TINA: Hebu nitajia huyo mwanamke ni nani na umempendea nini na kwanini umemchagua yeye na si mwinginewe.
TULO: Nampenda binti mmoja mzuri sana na anavutia, inaonyesha alipatwa na mikasa kidogo ila bado anavutia. Moyo wangu upo kwake na nitampa kila kizuri mbele yangu. Sitapenda alie, nitapenda kuona akitabasamu muda wote. Huyu binti nampenda sana.
TINA: Nitajie basi Tulo.
Tulo akaona kuwa asipoteze muda, akaanza kumueleza ukweli Tina juu ya hisia zake.
Tina akabaki kushangaa kuwa mwanamke mwenyewe ni yeye.
Maiko hakukata tamaa aliendelea kukaa pale pale nyuma akiingoja kauli ya Patrick kwani alijua wazi kuwa Patrick anamfanyia makusudi.
Maiko alijikuta akisinzia, ila alishtuliwa na ndoo ya maji aliyomwagiwa, kuangalia ni Deborah ndiye aliyeshika ndoo hiyo.
DEBORAH: Ondoka sasa hivi nyumbani kwangu sitaki kukuona shetani wewe.
MAIKO: Unanionea bure tu Deborah.
DEBORAH: Nani akuhurumie muuaji kama wewe, sitaki hata kukuona mbele ya macho yangu. Kama hao ndugu zako kutana nao hukooo ila sio hapa kwangu.
Ikambidi Maiko ajiongoze na kuondoka.
Mwita alikuwa akitafakari mambo mengi, haswaa mahali ambako wakina Patrick wanapatia pesa kwani hakuwaona hata mara moja wakienda kazini, huyo Maiko ndio kabisa hakueleweka ila alikuwa na pesa nyingi sana na hakuona shida kukodi gari kila anapokwenda. Kauli ya Tulo ikawa inatembea kichwani mwake kuwa je anajua kazi anayofanya baba yake, akajiuliza kuwa kazi hiyo inaendana vipi na usalama wake wa Taifa, kwakweli Mwita alikuwa na maswali mengi sana.
Patrick alipotoka ndani akaamua kutoka nae nje na kuzungumza nae.
MWITA: Unajua kuwa wale wanajeshi wenzangu wote waliotumika kumkamata Sele na tusa wameuwawa?
PATRICK: Kumbe wameuwawa, pole sana.
Mwita akashindwa kuelewa kwanini Patrick hana hata mshtuko.
MWITA: Hivi Patrick unafanya kazi gani?
PATRICK: Kamuulize baba yako kwanza ndipo uje kuniuliza na mimi.
Mwita alihisi kuwa lazima kuna kitu kinaendelea.
Patrick alionyesha chuki ya wazi kwa Mwita kwani huwa hapendi kuchunguzwa.
Marium alizungumza na watoto wake,
MARIUM: Hivi nyie wanangu mmerogwa jamani?
SELE: Kwanini mama?
MARIUM: Yani wote mnataka kuwa na familia ile iliyolaanika! Familia ambayo baba anambaka mwanae na kumpa mimba?
YUDA: Hatukuelewi mama?
MARIUM: Yuda mwanangu, yule Tina wa nini wewe? Hakufai yule mwanangu. Na wewe Sele, achana na Tusa si mwanamke wa kuishi nae yule.
SELE: Mama, nitakusikiliza vyote ila Tusa simuachi ng'ooo. Ananipenda ninampenda, najua ipo siku Mungu atatuweka pamoja. Haya mengine ni mapito tu.
YUDA: mama, nampenda sana Tina. Siwezi kumuacha mama.
MARIUM: Na mtawaacha tu labda mimi sio mama yenu.
Marium aliinuka kwa hasira na kusahau kuwa hata huyo Tina anayempinga ni mtoto wa rafiki yake kipenzi Fausta.
Mashaka akaamua kwenda tena nyumbani kwa Deborah ili akamuone dada yake bi.Rehema hadi akajishangaa kuwa kwanini amekuwa vile,
"Au ndio nataka kufa? Kwahiyo namuangalia angalia mara ya mwisho maana yeye ndiye ndugu yangu pekee aliyebaki.
Kufika kwa Deborah akamuona Fausta nje, kitu hiki kilimshtua Mashaka kwani hata hakujua kama Fausta anajuana na bi.Rehema.
Mashaka akabaki ameduwaa akimshangaa Fausta.
 
SEHEMU YA 75

Mashaka akabaki ameduwaa akimshangaa Fausta.
Fausta hakujua kama kuna mtu anayemuangalia, aliendelea na kazi zake pale nje kama kawaida.
Bi.Rehema nae akatoka ndani na kumfata Fausta pale nje huku akizungumza nae, yote hayo Mashaka alikuwa akiyashuhudia, alitamani kumuita bi.Rehema ila alishindwa kwasababu alijua Fausta angeshtuka.
Ila mara akamuona Fausta akiingia ndani na Rehema akiwa bado pale nje, akaamua kushusha kioo cha gari alilokuwa nalo na kumuita kwani vioo vyake vilikuwa vyeusi.
Bi.Rehema alipoangalia ile sauti ilipotokea akagundua ni kwenye lile gari na akagundua kama ni ya Mashaka, akaamua kumfata.
Alipofika Mashaka akamuomba azunguke ili aingie kwenye gari na kuzungumza nae, bi.Rehema akamwamuru Mashaka asogee ule upande mwingine na yeye akaye kwenye uskani kwani hakumuamini vizuri Mashaka alihisi kuwa huenda akaondoa gari, ila Mashaka akamuomba na kumsihi sana kuwa anahitaji kusogea nae kidogo tu ili wapate kuzungumza.
REHEMA: Na ukikiuka masharti je?
MASHAKA: Nifanye chochote utakachotaka kunifanya.
REHEMA: Mmh!! Naweza kukufanya chochote kweli mimi!!
MASHAKA: Usijari dada, kiukweli najutia makosa yangu ndomana ningependa tuzungumzie hili swala kidogo.
Bi.Rehema akakubali na kupanda kwenye ile gari ya Mashaka ambaye aliiondoa mahari pale.
Fausta alipotoka tena pale nje hakumkuta bi.Rehema, akamuangalia huku na kule bila ya kumuona.
Akamfata Pamela na kumuuliza.
FAUSTA: Hivi huyu mkweo ana matatizo gani?
PAMELA: Kwanini?
FAUSTA: Ni mara ya ngapi hii anaondoka bila ya kuaga jamani?
PAMELA: Inamaana hayupo?
FAUSTA: Ndio hayupo, yani aliniagiza ndani kuzungumza na Deborah kutoka nje nilhpomuacha hayupo tena.
PAMELA: Umejaribu kumuangalia na kule nyuma maana nyumba kubwa hii.
FAUSTA: Nimemuangalia kote hayupo sijui hata ameenda wapi.
Pamela nae akajaribu kuangalia huku na kule bila hata ya kumuona bi.Rehema.
PAMELA: Halafu akirudi hata huwa hasemi alipotoka.
FAUSTA: Labda kapata buzi mzee mwenzie.
Wakaanza kucheka kwa umbea.
Deborah alifikiria maneno aliyoambiwa na kuombwa na Fausta juu ya yeye kuzungumza na Patrick kuhusu Tusa.
Deborah akaamua kumuita tena mwanae ili kuzungumza nae.
DEBORAH: Mwanangu, me nadhani tuwaachie tu mtoto wao waende nae.
PATRICK: Yani mama kirahisi hivyo!!
DEBORAH: Sasa mwanangu unadhani itakuwaje jamani?
PATRICK: Mama, mimi nahitaji kuwakomesha hawa haswaa wazazi wa Tusa ili wazazi wenye tabia kama yao ya kupenda pesa na kufanya mabinti zao kama kitega uchumi waache.
DEBORAH: Ila anaeteseka ni Tusa mwanangu!!
PATRICK: Nataka wanilipe posa yangu, gharama zingine nitahesabu hasara ila wanilipe posa yangu tu. Si waliona fahari kumuozesha mtoto wao kwa milioni kumi na tano!! Sasa nataka wailipe tena sina masikhara kwa hilo, bora hiyo pesa uitumie mama yangu utakavyo ila sio wao. Wazazi wa Tusa hawana akili kabisa, na bora huyo baba yake Tusa si baba yangu maana akili zake fupi kama mchanga.
DEBORAH: Ila mwanangu si watakuwa maskini sasa?
PATRICK: Mama, binti yao si wamemfanya mtaji basi watapata pedeshee lingine litawajengea nyumba ila sidhani kama huyo Sele watamkubali na ukapuku wake.
DEBORAH: Patrick mwanangu umebadilika sana, sinabudi kukwambia ukweli wa maisha yako labda ukawa umefanana na ndugu zako tabia, haswaa baba yako nadhani utakuwa umefanana nae na sasa imeanza kujionyesha.
PATRICK: Inamaana mama wewe humjui baba yangu kabisaaa?
DEBORAH: Hivi karibuni utaujua ukweli tu maana Patrick niliyemnyonyesha ziwa langu na kumlea kwa kukimbizana ndani kwa fujo na utundu wake sidhani kama ni wewe. Kwakweli natamani arudi Patrick wangu yule wa zamani.
Deborah akamuacha Patrick na kutoka nje ya chumba na kwenda sebleni kwani machozi yalikuwa yakimlenga lenga.
Mashaka akaanza kuzungumza na bi.Rehema kuhusu Fausta.
MASHAKA: Fausta ni nani yako dada?
REHEMA: Khee swali gani hilo? Fausta ni mtoto wa baba wa wanangu pia ni dada wa mkwe wangu.
MASHAKA: Nadhani humjui Fausta vile ninavyomjua mimi, unamkumbuka Neema?
REHEMA: Neema yupi?
MASHAKA: Yule mtoto wa bamdogo aliyekuwa pacha wa baba yetu.
REHEMA: Sawasawa nimemkumbuka.
MASHAKA: Basi yule Fausta ana mdogo wake anaitwa Pamela na Neema ndio mama yao mzazi.
REHEMA: Kheee! Kumbe wale watoto ni ndugu zangu kabisa, Mungu wangu. Mbona ukoo wetu umesambaratika sana? Unajua huyo Pamela kaolewa na mwanangu mie!!
MASHAKA: Ndio mambo ya kutokufahamiana hayo, ila si mbaya sababu mtoto wa dada mkubwa na mdogo wameoana.
Halafu akawa anacheka,
REHEMA: Kinachokuchekesha sasa? Hebu nirudishe huko.
MASHAKA: Usipanic bhana dada yangu, nenda ukawaeleweshe ila mimi sikuja kuzungumza nawe kuhusu hilo.
REHEMA: Ulitaka kusema nini? Nirudishe bhana.
Mashaka akaendesha gari na kufika pale kwa Deborah kisha akamgeukia Rehema na kumwambia.
MASHAKA: Dada, usihangaike kumtafuta mchawi au mtu mbaya kwa kifo cha mzee Ayubu.
REHEMA: Unamaana gani?
MASHAKA: Aliyemuua mzee Ayubu si mwingine bali ni mwanao Maiko.
Mashaka akajihisi kupumua kwa kumtwisha Maiko mzigo wa lawama, bi.Rehema akahisi kuchanganyikiwa kwani ilikuwa ngumu kuamini kuwa mwanae angefanya ukatili wa kiasi kile kwa mzee Ayubu.
Bi.Rehema alishuka kwenye lile gari akiwa amenyong'onyea sana.
Tulo na Mwita wakaondoka tena kwana Mwita hakupata majibu mazuri toka kwa Patrick nao wakapanga kurudi tena.
MWITA: Vipi na wewe Tulo mbona unafuraha sana?
TULO: Mtoto anaonyesha kunielewa kabisa maana hata jibu la kunipa alikosa.
MWITA: Sasa umeamua vipi?
TULO: Tunavyoenda mjini hivi nitaenda kumnunulia zawadi nzuri sana, najua Tina ataipenda na atanipa jibu zuri na la uhakika.
MWITA: Na kuaminia bhana.
Tulo alikuwa na furaha kweli kwani aliamini kuwa lazima Tina atamkubalia tu.
Adamu alimfata mkewe Pamela kwani alishachoka kuishi pale Mwanza.
ADAMU: Unajua nimechoka, kwakweli tumekuwa mzigo kwenye mikono ya Deborah bora turudi kwetu tu.
PAMELA: Kwetu ambako una mpango wa kuuza nyumba ili kuweza kulipa posa ya mtoto? Mmh! Sikujua mambo yote haya kabla laiti ningejua nisingepanga mahari kubwa kiasi kile.
ADAMU: Majuto ni mjukuu mke wangu, hatuna la kufanya inabidi tu tukubaliane na halihalisi. Ninge ni kauli ya majuto na huja baada ya maji kumwagika.
PAMELA: Natamani kama vile siku zirudishwe nyuma, kwakweli hali ni mbaya.
Wakamuona bi.Rehema akirudi huku akiwa amenywea sana.
ADAMU: Nini tatizo mama?
REHEMA: Bora tukio hili angelifanya mtu yeyote duniani ila si mwanangu Juma. Kwanini lakini? Kwanini imekuwa hivi?
Wote wakamshangaa na kumuangalia tu.
Mashaka alijiona kafanikiwa kiasi fulani kwani alikuwa kashamvurugia Maiko kuwa tena karibu na bi.Rehema na alijua wazi kuwa lazima Maiko agome kubeba mzigo na atamtupia Patrick.
"Na hapo ndio patamu, maana Patrick anajifanya mwema sana. Ngoja tu na wao waumbuke na waogopwe na kujificha kama ambavyo mimi ninafanya"
Akaishia kwa kicheko cha kujipongeza.
Ilibidi Tina amueleze Tusa kuhusu Tulo kuwa anampenda.
TINA: Anaonyesha kunipenda kweli halafu anapesa tofauti na Yuda.
TUSA: Sikushauri kuwa nae, sidhani kama huyo Tulo atakuwa tofauti na Patrick. Wanaume wote ni sawa Tina.
TINA: Hapana bhana si sawa, Tulo kashajipanga kimaisha ana nyumba na magari. Nikiwa nae nitaishi maisha ya kifahari, sijawahi kufikiria kuwa na gari ila Tulo kasema atanipa. Unajua nikiwa nae nitaanza na mia tofauti na Yuda itabidi nianze nae na moja.
TUSA: Ngoja nikuulize Tina, unachoangalia wewe ni pesa ya mtu au upendo wa mtu kwako? Angalia Mapenzi Tina, pesa kitu gani bhana. Mi mwenzio nateseka hapa sababu ya pesa.
TINA: Jamani sasa nifanyeje?
TUSA: Akili kichwani mwako, wewe ni mtu mzima sasa na ushapitia mengi. Usifikirie nakuonea wivu la hasha, nakuhurumia Tina.
Tina akatulia akitafakari kauli ya Tusa kuwa aangalie mapenzi au pesa.
Maiko aliendelea kuhitaji kuzungumza na Patrick ingawa alimwagiwa maji na Deborah ila hakuacha kwenda kuchungulia nyumbani kwa Deborah maana alitambua wazi lazima kuna muda atakaosikiliza tu.
Akaamua kwenda tena nyumbani kwa Deborah.
Bi.Rehema alizunguka nyuma ya nyumba akitafakari aliyoambiwa, alikaa na kujiinamia.
Akatokea mtu na kumshika bega, kumtazama alikuwa ni Maiko.
 
SEHEMU YA 77

Muda huo Patrick nae ndio alikuwa amerudi nyumbani kwao.
Waliendelea kumjadili Patrick bila ya kujua kuwa yupo nje anawasikiliza wanavyosema.
DEBORAH: Nyie nani kawaambia kama Patrick ndiye aliyeua?
PAMELA: Wameambiwa na Maiko.
DEBORAH: Tatizo hamumjui Maiko vizuri, hata siwashangai.
REHEMA: Ila ni kweli, Patrick ndiye aliyeua.
Mara Patrick akaingia ndani na kufanya wote washtuke na kunyamaza.
PATRICK: Mnashangaa nini? Endeleeni kuongea.
Wakawa kimya tu wanatazamana bila ya kusema chochote.
PATRICK: Huwa sipendi kuishi na watu wanafki, kama nimefanya kitu niambie mwenyewe sio kukaa na kunijadili bila sababu za msingi. Semeni mnachosema juu yangu.
REHEMA: Hakuna chochote baba.
PATRICK: Hiyo ni nidhani ya uoga, mama nakuomba mara moja.
Ikabidi Deborah afatane na mwanae na kuwaacha wale wengine pale sebleni.
Bi.Rehema na wengine wakabaki kutazamana.
FAUSTA: (Akacheka), kweli nidhamu ya uoga yani hata wewe kaka umeshindwa kusema!!
ADAMU: Sijajiandaa bado, huyo kijana hatabiriki bhana.
PAMELA: Kwahiyo unamuogopa?
ADAMU: Hapana simuogopi.
FAUSTA: Mbona ulinyamaza sasa wakati wewe ndio mwanaume tunayekutegemea!
ADAMU: Dah! Haya mambo nyie acheni tu ila mi nadhani kuwa cha msingi ni kufata sheria juu ya swala hili.
PAMELA: Mmh!! Tutakuza mambo jamani, je tutayaweza? Hebu tufikirie kwanza.
REHEMA: Ila mi nadhani itakuwa bora kama tutaenda kuongelea nje maana humu ndani hapafai.
Wakaamua kutoka nje kwenda kuzungumzia hilo swala.
Patrick aliamua kuzungumza na mama yake.
PATRICK: Mama, kwanini mamkubwa ananisisitiza kuwa nisiachane na Tusa?
DEBORAH: Yule kashavurugwa mwanangu, kwa kifupi hata hajielewi.
PATRICK: Halafu mama wasisitizie hao watu, kuwa mi sipendi kusemwa semwa kama kuna tatizo wameliona basi wanifate mwenyewe sio kunisema pembeni.
DEBORAH: Usijari mwanangu.
Hata Deborah nae alishindwa kumuuliza mwanae kuhusiana na hiyo tetesi ya mauaji.
Tina na Tusa wala walikuwa hawaelewi kinachoendelea kwani wao walijifungia chumbani tu.
TUSA: Tina, leo Tulo anakuja. Jibu lako ni nini?
TINA: Hivi wewe Tusa huna habari zingine zaidi ya hizo? Nitaangalia kwanza akishakuja.
TUSA: Wanaume wana vishawishi vingi Tina, ni bora kuwa na jibu kabla hajafika.
TINA: Tusa, mi ni mkubwa sasa hakuna tatizo hata awe na vishawishi vya aina gani.
TUSA: Akikuletea zawadi hapo utakataa?
TINA: Kwani zawadi ina tatizo gani Tusa? Hakuna tatizo mdogo wangu niamini.
TUSA: Sawa ila nakuhurumia, je kwa mfano akifika Yuda na Tulo kwa muda mmoja utafanyaje?
TINA: Usijari Tusa, nitajua cha kufanya kama ikitokea hivyo ila najua haiwezi kutokea bhana.
Bado Tina alikuwa mgumu kuelewa.
Mashaka aliwanunulia pombe za kutosha Mwita na Tulo, wakanywa hadi kujisahau kabisa.
TULO: Itabidi ile safari yetu twende kesho Mwita.
MWITA: Sawa sawa hakuna tatizo.
Mashaka alikuwa akifurahia ushindi wake ila Mwita na Tulo hawakuelewa na waliendelea kunywa tu.
Usiku ulipofika ikabidi waende kulala hotelini, Mwita na Tulo wakalala hoteli ya karibu na Mashaka na kesho yake wakawa wakwanza kwenda kuzimua ile pombe kwa supu ili kuushtua mwili.
MWITA: Kwani Tulo unafanya kazi gani?
TULO: Kwanini?
MWITA: Tangu nimekufahamu, tunalala hoteli, kula vizuri na kukodi usafiri yaonyesha una pesa ya kutosha maana kila nikitaka kutoa pesa unanizuia na kutoa wewe. Hebu nihabarishe mwenzangu, kazi gani unafanya?
TULO: Aaah! Mi mchimba madini wewe, huko Arusha Mererani. Sisi ndio matajiri wadogo wadogo.
MWITA: Nadhani kazi yenu si ngumu ndomana hamna uchungu na pesa zenu. Inamaana unafanya kazi pamoja na Patrick maana na yeye aliniambia kuwa ni mchimba madini.
TULO: Ndio nafanya nae kazi moja, kazi yetu ukiwa unaanza ni ngumu sana ila ukiizoea inakuwa laini kama ugali na mrenda vile.
MWITA: Duh!! Haya bhana, si wengine tunahenyeka na serikali kwa mshahara kiduchu sana.
Mwita bado alikuwa na maswali kichwani mwake ila kidogo jibu la uchimbaji madini lilimridhisha kwani anajua jinsi gani madini yalivyo na pesa.
Yuda na Sele wakakaa na kujadili kauli ya mama yao.
YUDA: Unajua mama yetu utu uzima wake unampeleka vibaya sana, yani wanaume wakubwa kama sie ni wa kutuambia mwanamke anayefaa na asiyefaa kweli?
SELE: Mama kavurugwa bhana, mi badae nitaenda kwa mamdogo kusikilizia yale mambo ya Tusa na Patrick yameishia wapi.
YUDA: Kwahiyo hapo unatamani kweli Tusa apewe taraka!
SELE: Ndio ili nimpate kiurahisi.
YUDA: Bora hata mimi Tina uhakika kuliko wewe, nataka nikamnunulie Tina zawadi.
SELE: Zawadi gani?
YUDA: Yoyote nitakayopata, zawadi ni zawadi bhana.
SELE: Ila dah! Kwa huyo Tina hata mimi nakuhurumia, nakumbuka kipindi nipo na Tusa huyo Tina ndio alikuwa namba moja kumshawishi Tusa aachane na mimi. Yani Tina na mama yake Tusa wako sawasawa, wanapenda pesa balaa.
YUDA: Tina kabadilika bhana, si unakumbuka kipindi kile wakati namtongoza akaniambia nitafute pesa kwanza, mbona saivi hajaniambia? Inaonyesha kuwa ameshajifunza na kubadilika.
SELE: Kama kabadilika basi itakuwa vizuri.
Wote wawili wakajiandaa na kutoka.
Patrick alitulia kwao na kupanga cha kumfanya Maiko.
"Hivi mwanaume mzima kama Maiko bila hata aibu kuja kuwaambia hawa wasiojielewa eti Patrick kamuua mzee Ayubu. Hivi kweli mimi ningemuua mzee Ayubu bila ya yeye kunituma? Nadhani Maiko ananitafuta sasa. Na pia hawa nduguze hawamjui na hawanijui vizuri, sasa nitaenda kumchukua huyo Maiko wao na kumtoboa toboa mwili mzima mbele ya macho yao."
Patrick akaondoka nyumbani kwa lengo moja tu la kumpata Maiko.
Bi.Rehema akawaita tena watoto wake kujadili.
REHEMA: Hivi kweli tutakaa kimya hivi hivi bila kufanya chochote? Iko wapi haki ya mzee Ayubu?
PAMELA: Sasa mama tutafanyaje kwa unavyodhani?
REHEMA: Patrick achukuliwe hatua. Adamu acha kulala jamani wewe ni mwanaume unatakiwa usimame kwa hili.
ADAMU: Naona Deborah hatuamini, itabidi tumlete Maiko hapa aje kueleza.
FAUSTA: Jamani jamani naomba nitoe onyo, wengine hapa tuna aleji na huyo Maiko sasa mkija nae chochote nitakachofanya msinilaumu.
Halafu akainuka na kuondoka.
PAMELA: Achaneni na huyo kavurugwa, hebu tujadili wenyewe.
Wakaendelea kujadili yanayowasibu.
Fausta akaenda kuzungumza na Deborah.
FAUSTA: Wanavyojifanya wema utafikiri wao hawajawahi kutenda vitu vibaya.
DEBORAH: Kwani wao walifanya nini?
Fausta akaanza kumsimulia Deborah kuhusu kipindi kile cha yeye alivyokuwa mke wa Jumanne ambaye ndio huyo Adamu.
Stori aliyoambiwa ilimsisimua sana Deborah na kumfumbua macho na masikio na hata asijue itakuwaje pale ukweli wa mambo yote ukijulikana.
Kufika mjini, Yuda akaona viatu vizuri sana na kuamua kumnunulia Tina ili akamfurahishe.
Yuda na Sele wakaachana njiani kwani Sele alitaka kwenda kwanza kwa mama yao mdogo Anna halafu na Yuda akatangulia kwa Deborah.
Tulo na Mwita wakaenda nyumbani kwa Deborah, nia ya Tulo ni kuzungumza na Tina na kumkabidhi zawadi aliyomletea.
Tina alitoka sebleni akiwa na furaha ila Tusa alimuangalia kwa msononeko sana.
Wakati Tina akizungumza na Tulo pale sebleni, Yuda nae akaingia pale sebleni.
 
SEHEMU YA 78

Wakati Tina akizungumza na Tulo pale sebleni, Yuda nae alingia pale sebleni.
Tina akashtuka kumuona Yuda, Yuda nae akashangaa kuuona ukaribu wa Tulo na Tina.
Yuda akamtazama Tina na kuwa kama vile anamuuliza jambo fulani kwa macho, Tina akashusha macho chini.
Mara Tusa akatokea ndani na kumuona Yuda akiwa amesimama na mfuko wake mkononi, akamfata kwa mbwembwe.
TUSA: Wow, shemeji yangu wa ukweli. Karibu sana.
Akaenda na kumpokea ule mfuko na kuuchungulia,
TUSA: Mmh!! Shemeji, umeniletea zawadi nini?
Yuda akaushangaa sana uchangamfu ule wa Tusa kwani hajawahi kumuona akiwa hivyo kabla.
TUSA: Mbona hujibu shem? Karibu tukae.
Tusa akamshika mkono Yuda na kwenda kukaa nae palepale karibu na alipokaa Tina na Tulo.
Kwakweli Tina aliona kuharibiwa siku vibaya mno kwani yeye hakupanga kabisa kuwakutanisha watu wale wawili pale.
Yuda aliendelea kumuangalia Tina kwa umakini mkubwa huku Tusa nae akiendelea kumuongelesha, Tina alijionea aibu kwani alitambua anachofanya.
Tulo hakuelewa kinachoendelea, ikabidi amuulize Tina.
TULO: Mbona umebadilika gafla Tina?
TINA: Naombe twende tukazungumze nje.
TULO: Kwanini? Mbona sielewi jamani?
TINA: Utaelewa tu tukitoka nje.
Tulo akainuka, Tina nae akainuka na Yuda nae akainuka.
YUDA: Unaenda wapi Tina? Si unajua kuwa nimekufata wewe!
Tina alikaa kimya tu, Tulo nae akamgeukia Tina na kumuuliza.
TULO: Amekufata wewe kivipi?
TINA: Twende nje bhana tukazungumze.
Wakawa wanatoka nje, na Yuda nae akawa anawafata kwa nyuma.
Patrick alifanikiwa kumuona Maiko, alimkuta akiwa amelala mgongo wazi kwani alikuwa amebabuka sana mgongoni.
Patrick akacheka sana,
PATRICK: Vipi gaidi? Umemwagiwa tindikali nini?
MAIKO: Nimemwagiwa maji ya moto na mama yako.
PATRICK: (Akacheka), kazi nzuri sana aliyofanya mama yangu. Nitaenda kumpongeza.
MAIKO: Yani, Patrick umefurahi kiasi hicho!
PATRICK: Tena nimefurahi mno, nia yangu kwako ilikuwa ni kukumaliza leo ila nitangoja kwanza hayo maumivu yako yapoe halafu ndio nije kukuongeza na maumivu mengine. Kweli mama yangu anafaa jamani.
MAIKO: Sawa, ila nitapona tu.
PATRICK: Na ukipona utakuwa mikononi mwangu. Haya niambie, nani amekutuma kuwaambia kuwa mimi ndiye nimemuua mzee Ayubu?
MAIKO: Unanionea bure Patrick, sikuwa na nia ya kusema ila yote haya ameyaanzisha Mashaka. Huyu ndio mtu mbaya Patrick.
PATRICK: Hata kama, wewe hukutakiwa kunitaja mimi. Muone ulivyo na ushetani wako hadi unaua baba yako mzazi.
Patrick aliondoka na kwenda kumtafuta Mashaka kwani alijua kuwa huyu ndiye msumbufu namba moja.
Tina na Tulo wakatoka nje na Yuda nae akawafata.
YUDA: Nahitaji kujua kuna nini kinaendelea kati yenu wawili?
TULO: Ujue wewe kama nani?
YUDA: Mimi kama nani? Kivipi?
Tina akaona mambo yatamgeukia sasa, akaamua kukimbilia ndani na kumuacha Tulo na Yuda pale nje.
Tulo na Yuda wakaanza kurumbana.
YUDA: Tina ni mpenzi wangu, nakuomba ukae mbali nae.
TULO: Mimi ndiye mpenzi wake, wewe ndio unatakiwa ukae mbali nae.
Wakaanza kugombana na kupigana, Mwita akawaona na kuwafata.
MWITA: Acheni ujinga nyie, hebu angalieni mwanamke mwenyewe kawakimbia na kuwaona wapumbavu. Nyie mnaendelea kugombana wakati mnayemgombania katulia ndani.
YUDA: Huyu jamaa ni muharibifu tu na hajui wapi nimetoka na Tina.
TULO: Hata mimi pia hujui nilipotoka na Tina.
Mwita aliendelea kuwasihi waache kugombana ila hawakusikia.
Mara Deborah nae akatoka ndani na kukutana na yale marumbano kati ya Yuda na Tulo.
Ikabidi na yeye aingilie kati kwani hakujua wanagombea nini.
DEBORAH: Sitaki matatizo nyumbani kwangu, kwani mnagombea nini na nyie hapa? Semeni mnachogombea.
Ikabidi Mwita amueleze kuwa wale wawili wanamgombea Tina.
Deborah hakutaka majibishano, aliamua kumuita Tina mara moja.
Tina aliporudi ndani alimkuta Tusa anacheka.
TINA: Kinachokuchekesha ni nini sasa?
TUSA: Nilikwambia Tina, mshika mawili moja humponyoka dada.
TINA: Sasa ndio ucheke? Yani na wewe hujui madili kabisa sijui ukoje Tusa. Umenikera sana leo.
TUSA: Ndio ujipange sasa kumchagua mmoja. Kusuka au kunyoa?
TINA: Kwenda zako huko, huna lolote wewe. Yako yamekushinda, utaweza yangu wewe?? Huna ulijualo hapo ulipo.
Tina akakaa chini kwa hasira, mara akasikia anaitwa ila hakutoka kule nje, ikabidi Deborah aende ndani na kumshika Tina mkono na kutoka nae pale nje.
Tina alikuwa ameinamisha macho chini tu pale nje kwa aibu.
DEBORAH: Haya sasa, nataka utamke kwa mdomo wako mwenyewe. Wako ni Yuda au Tulo?
TINA: Sijui.
DEBORAH: Khee! Huna hata aibu, eti sijui. Inamaana hujui unampenda nani? Au hujui kama unampenda au la! Wewe ni waajabu sana. Hapa ni kusema tu wako ni yupi, na kama huwataki wote sema niwatimue hapa.
Tina akajifikiria sana, akafikiria mambo mengi na mtihani aliopewa hapo. Ikabidi achague moja kuliko kukosa vyote, alitaka amchague Tulo kwaajili ya pesa alizo nazo ila kauli ya Tusa ilimrudia sana kichwani mwake kuwa aangalie mapenzi ya kweli na si pesa, hivyo basi akaamua kumchagua Yuda.
Deborah akamuomba Tulo aondoke, Tulo aliumia sana moyo wake na kuamua kuondoka na Mwita, hakuamini kama Tina angemfanyia vile baada ya mambo yote aliyomuahidi.
Adamu na ndugu zake hawakuacha kumjadili Patrick, Deborah akawaomba sana na kuwasihi kuwa waache kumjadili Patrick.
DEBORAH: Naomba muache kumjadili Patrick, wakati familia yenu imelaaniwa.
REHEMA: Unamaana gani Deborah?
DEBORAH: Patrick nimempigia simu na amesema kesho anarudi, kesho nitaweka kikao na kuwaelezea jambo fulani najua wote mtastaajabu na kushangaa.
Hawakumuelewa Deborah, na wote wakawa wakijiuliza maswali kuwa ni jambo gani ambalo Deborah alihitaji kumwambia.
Mwita na Tulo walienda baa ili kujiliwaza kwa yale majanga yaliyomkuta Tulo siku hiyo.
Mwita alikaa karibu na Tulo ili kumchunguza zaidi kazi afanyazo ila Tulo hakulitambua hilo.
Mwita alianza kugundua mambo mengi sana kuhusu Tulo.
Patrick aliweka mtego wa kumnasa Mashaka, alimtegeshea mtego mdogo wa mtoto wa kike kwani Mashaka alipenda sana wanawake. Patrick akaona kuwa hiyo ndio itakuwa njia pekee ya kumpata Mashaka.
Patrick alitaka amshughulikie Mashaka na Maiko kwa mikono yake mwenyewe, bila ya kujua kuwa Maiko nae anampango huo huo na Mashaka.
Mashaka aliingia hotelini na binti yule bila kujua kuwa chumba alichoingia yupo Patrick.
 
SEHEMU YA 79

Mashaka aliingia hotelini na binti yule bila kujua kuwa chumba alichoingia yupo Patrick.
Mashaka hakuwa na habari wala nini, akashangaa akikabwa kwa nyuma na kuanza kufurukuta, alipogeuka mbele ana kutana macho kwa macho na Patrick, kwanza kabisa Mashaka hakuamini kama ni kweli yupo mikononi mwa Patrick au anaota.
Akataka kupambana na Patrick, ila akapewa ngumi moja ya kishindo na kutulia.
PATRICK: Na utulie hivyo hivyo, tunatoka hapa hotelini kuna mahali tunaenda. Ukileta papara tu, leo nitakumaliza.
Ikabidi Mashaka awe mpole kwani hakutaka kupoteza nguvu zake kupambana na Patrick ilihali anajua wazi kuwa atashindwa.
Patrick alitoka na Mashaka kimya kimya na kuingia nae kwenye gari ya Mashaka ambapo Dereva alikuwa ni Mashaka mwenyewe, alipeleka gari kulingana na alivyoelekezwa na Patrick.
Adamu akaitwa na mama yake ili wazungumzie swala la Deborah analotaka kuwaambia.
REHEMA: Eti, unafikiri Deborah ana jambo gani la kutuambia?
ADAMU: Kwakweli sijui mama, yani sijui chochote.
REHEMA: Au huyo Patrick ni mwanao?
ADAMU: Mama, Deborah kwangu hakuondoka na mtoto wala mimba. Kwakweli hata mi mwenyewe sijui huyo mtoto amezaa na nani.
REHEMA: Kama alikuficha je kumbe alikuwa na mimba yako?
ADAMU: Mama, kwajinsi ilivyokuwa Deborah angekua na mimba ningejua tu hata kama ingekuwa ya mwanaume mwingine. Deborah kwangu hakuondoka na mimba wala mtoto na nilipojaribu kumdadisi kuhusu baba wa mtoto wake alikuwa mkali sana, mi nahisi alibakwa baada ya kutoka kwangu ndomana yupo hivyo.
REHEMA: Sasa, anachosema kuwa amegundua kuhusu familia yetu ni kitu gani?
ADAMU: Mama, hata usijipe presha. Deborah ukimzoea ndo maneno yake hayo hayo. Mi sidhani kama anachaajabu kutueleza ila nia yake kubwa ni tuache kumzungumzia huyo jangili wake.
REHEMA: Na sasa je una mpango gani na huyo Patrick?
ADAMU: Ni kumfungulia kesi tu hata kama hatuna ushahidi, ila kiukweli mama yangu simpendi yule kijana balaa, namchukia sana kwani amenitesea sana mwanangu ila nashindwa kujielewa kwanini hadi sasa nashindwa kumchukulia hatua.
Adamu akawa anatafakari kitu cha kumfanya Patrick.
Patrick alienda porini na Mashaka, kulekule alipoenda na Tulo hadi akatokewa na mzimu wa mzee Ayubu. Sasa aliamua kwenda na Mashaka.
Alikwenda nae kimzobe mzobe kwani haikuwa rahisi kwa Mashaka kuingia porini.
Mashaka akaamua kutumia nguvu zake ili kuweza kupambana na Patrick ili pengine aweze kutoka mikononi mwake, na mpambano ukawa mkali sana.
Patrick alimdhibiti Mashaka kwa kumfunga kwenye mti, mwili wote wa Mashaka ulijazwa kamba alizofungwa na Patrick, kisha Patrick akamtazama na kuanza kumuongelesha.
PATRICK: Huwa sipendi kusumbuliwa, ungetulia hata yasingefikia yote haya.
Mashaka alimuangalia tu Patrick na kukosa cha kumjibu.
PATRICK: Haya bila papara wala vurugu, nahitaji unijibu haya maswali kwa ufasaha. Kwanini umesema kuwa mimi ndiye niliyemuua mzee Ayubu?
MASHAKA: Si kwamba nilikutaja wewe, Maiko ndiye aliyekutaja. Mimi nilisema kuwa Maiko ndiye aliyeua.
PATRICK: Na kwanini ulisema kuwa Maiko ndiye aliyeua? Ulitaka nini?
MASHAKA: Sikutaka chochote.
PATRICK: Na kwanini ulitoa oda ya kumuua mzee Ayubu ilihali unajua kuwa Maiko ni mwanae?
MASHAKA: Mimi sikujua kama Maiko ni mwanae, kwanza tambua kwamba nilichokuwa najua mimi ni kuwa Maiko ni mwanangu, jambo ambalo lilikuwa sivyo. Ayubu aliwahi kuwa bwana wa dada yangu Rehema, na baada ya kuachana kumbe akahamisha makombora kwa dada yangu mwingine ila nadhani hakujua hilo kama Neema na Rehema ni ndugu.
PATRICK: Kwahiyo umemuua kwasababu hiyo tu?
MASHAKA: Hapana, ila Ayubu alinichukulia mwanamke wangu ambaye alikuwa mama wa mwanangu niliyemdhania ndiye Maiko. Niliapa kwa Ayubu kuwa nitamlipizia kisasi, oda ya kumuua ilikuja kwa hitaji la biashara na hitaji binafsi la kulipa kisasi.
PATRICK: Hadi sasa umeua watu wangapi?
MASHAKA: Kwakweli sijui.
PATRICK: Huwezi kujua ndio, idadi yao ni kubwa sana. Hivi ni nani atakayekuelewa hayo uyasemayo Mashaka? Hivi wewe ni mtu kweli katika watu? Kumlipiza mtu kisasi ndio kumuua?
Mashaka aliendelea kumtazama Patrick huku akimsihi amfungue kwenye ule mti.
PATRICK: Kwa leo adhabu yako ni hiyo, utalala hapohapo mi naondoka. Nataka ufe taratibu ili ujue uchungu wa kifo.
Halafu Patrick akaanza kuondoka, jambo pekee ambalo Patrick hakulijua ni kuwa muda wote alikuwa anafatiliwa na Maiko kwa tahadhari kubwa sana.
Kesho yake Pamela na Fausta nao wakajadili na kusemezana.
FAUSTA: Unaonaje tukimwambia Tusa ukweli kuhusu kifo cha babu yake?
PAMELA: Unamaana tumwambie kuwa Patrick ndio kaua?
FAUSTA: Hapana, ila tumueleze kuwa babu yake alishakufa ili nae apate kujua.
PAMELA: Nadhani itakuwa ni jambo la busara maana Tusa hajui chochote kile.
Wakaamua kumuita Tusa ili kumwambia ukweli.
Baada ya mikasa kutulia ya wale vijana wawili yani Tulo na Yuda. Tina alijihisi kuwa ametua mzigo uliokuwa umemuelemea ingawa alikuwa na mawazo kiasi.
TUSA: Hujakosea Tina, uamuzi uliochagua ni sahihi na ipo siku utanishukuru kwa ushauri wangu.
TINA: Sawa ila nimepiga teke fuko la hela.
TUSA: Usimdharau Yuda, anakupenda sana. Naimani ataendelea kukujali na kukutunza. Hujapoteza kitu ila umechagua jambo jema.
TINA: Vipi na wewe hatma yako?
TUSA: Ushauri wako mbovu ndio ulioniponza, hilo fuko la hela unalosema ndio linalonitesa kwasasa.
TINA: Kwani Patrick anafanya kazi gani?
Mara Tusa akaitwa na mama yake.
Walimueleza Tusa kila kitu kuhusu kuuwawa kwa babu yake kasoro hawakumwambia aliyemuua.
Tusa akalia na kuomboleza sana kwani alimpenda sana babu yake hata ile safari ya kipindi kile yeye na Sele kwenda Morogoro alitaka waende kwa babu yake huyo.
Tusa aliona huo ni mkasa mwingine katika maisha yake, na kilichomuumiza zaidi ni kule kuambiwa kuwa aliuwawa kikatili.
Tulo alikuwa na machungu bado ya kukataliwa na Tina.
TULO: Unajua bado siamini kama kweli Tina kanikataa kwaajili ya kale kavulana!
MWITA: Inabidi ukubaliane na hali halisi kwamaana hakuna cha kufanya.
TULO: Cha kufanya kipo, lazima nimkomeshe yule kijana.
MWITA: Utamfanyaje sasa?
TULO: Wewe tulia tu, mimi ndio Tulo na atajuta kuzaliwa mwanaume na kunifahamu mimi.
Mwita alizidi kuingiwa na wasiwasi juu ya mwenendo wa Tulo na hakutaka kuachana nae, aliongozana nae kila mahali kupata taarifa tu.
Marium na Anna nao wakajiandaa na kwenda kwa Deborah kwani alishawaambia kuwa anawahitaji dada zake ili atakapoyasema aliyonayo moyoni wote wawepo.
ANNA: Deborah nae anatutisha!
MARIUM: Yani kama anataka kufa vile loh!
ANNA: Ile familia nayo iliyomzunguka pale ni balaa.
MARIUM: Ile familia ni nuksi wewe, ina majanga hakuna mfano.
Rehema aliamua kuwaida Pamela na Fausta na kuwaeleza kuwa wao ni ndugu zake kabisa kwani Neema ambaye ndiye aliyekuwa mama yao alikuwa ni ndugu wa damu na yeye kwani walikuwa ni watoto wa baba mkubwa na mdogo na baba zao hao walikuwa mapacha.
Wote wakabaki wakistaajabu.
FAUSTA: Inamaana tumeoana ndugu kabisa wa damu?
REHEMA: Huo ndio ukweli.
Wakati wanazungumza hayo, mara akatokea Tusa na kuwafata tena kwa maswali kuhusu kifo cha babu yake.
TUSA: Niambieni ukweli nani kamuua babu?
PAMELA: Hatujui mwanangu.
REHEMA: Hebu mwambieni ukweli mtoto.
PAMELA: Ukweli upi mama?
REHEMA: Kama aliyemuua babu yake ni Patrick.
TUSA: Patrick yupi?
REHEMA: Patrick mumeo.
Tusa hakuamini kabisa, mara Patrick nae akawa amerudi na kuingia ndani.
Tusa alivyomuona alinyanyuka na kukimbilia jikoni, kisha akachukua kisu na kumfata nacho Patrick kwa hasira.
 
SEHEMU YA 80

Tusa alivyomuona alinyanyuka na kukimbilia jikoni, kisha akachukua kisu na kumfata nacho Patrick kwa hasira.
Tusa alikuwa amejawa sana na hasira dhidi ya Patrick, alikishika kile kisu kisawasawa na moja kwa moja alitaka akilengeshe kwenye kifua cha Patrick ila kabla hajafanya hivyo Patrick alimdaka mkono Tusa na kumpokonya kile kisu.
Tusa akaanza kumzenga zenga Patrick kwa maneno mengi makali, aliongea huku akilia na machozi kumtoka.
TUSA: Niue na mimi Patrick, naomba uniue kama ulivyoua hao tengine.
PATRICK: Kwani wewe mwanamke vipi? Una mashetani au?
Kisha Patrick akamsukumia Tusa pembeni na yeye akaelekea chumbani kwake, Tusa akaona kuwa ana kazi ya ziada kwa Tusa.
Maiko alienda moja kwa moja pale ambako Mashaka alipofungwa, Mashaka alishakata tamaa kwani hakuona msaada wowote ukizingatia ni porini.
Maiko alimwangalia na kumwambia.
MAIKO: Nimekuja kukusaidia kwa lengo na nia yangu moja kubwa sana.
Mashaka hakujali nia ya Maiko kwa muda huo ni nini ila alichojari ni kupatiwa huo msaada.
Yuda nae akajitahidi kumtafakari Tina ambaye alimshangaa tabia yake kwa muda mfupi kiasi kile.
SELE: Usiumize kichwa ndugu yangu, kuwa na Tina kunahitaji uvumilivu tu hata usiwe na wasiwasi.
YUDA: Uvimilivu si tatizo, tatizo ni kuwa hana msimamo bhana. Atakuwaje na mimi halafu anamkubali mwanaume mwingije.
SELE: Usijari, Tina yupo katika mabadiliko ya maisha yake na atakuwa kwenye mstari uliyonyooka tu hata usiwe na wasiwasi ndugu yangu.
Yuda alimpenda sana Tina na ndiomana alijitoa sana dhidi ya Tina.
Adamu alipoingia pale sebleni kwa Deborah akashangaa kubambana na kilio cha binti yake, na alipouliza akagundua ukweli kuwa binti yake analia kifo ch babu yake ambaye yeye ni baba yake.
Wote walikereka kwa kutambua uwepo wa muuaji ndani ya nyumba ila wote waliogopa sana hata kumgusa, ni Tusa pekee ndiye aliyejaribu kumsogelea mwilini Patrick.
Deborah naye alipofika akakutana na lile zogo, alipoambiwa.
DEBORAH: Mnanishangaza sana nyie binadamu msio na fadhila, sasa kumnywesha hiyo sumu ya unafki Tusa mnataka afanye nini? Nadhani mnataka amchukie zaidi ya vile anavyomchukia, ila sumu mnayoipandikiza mtainywa wenyewe.
ADAMU: Sasa hukupenda aujue ukweli?
DEBORAH: Ukweli mnaushahidi? Bora mie niliyeficha ukweli kwa muda mrefu nikingoja ushahidi ila Mungu si Athumani hatimaye ushahidi nimepata.
REHEMA: Tatizo Deborah hutaki kukubali kuwa unafuga maradhi ndani.
Ndugu wa Deborah wakawasili, nao ni Marium na Anna walikuja kwaajili ya kikao ambacho Deborah amewaitia.
Tina aliyekuwa chumbani akiendelea kujitafakarisha mwenyewe, aliamua kwenda sebleni aliposikia kuna kikao. Na alipoona majonzi ya Tusa akaamua kumbembeleza kwani wao walishaliaga na yakaisha.
TUSA: Kinachoniumiza ni kusikia kuwa Patrick amehusika.
TINA: Usiamini sana Tusa, hakuna mwenye ushahidi hata hivyo Patrick hawezi kufanya unyama ule.
Tina alizidi kumbembeleza Tusa na kumliwaza.
Deborah akamuita mwanae Patrick ili waweze kuzungumza.
PATRICK: Kwani kikao kinahusu nini? Kuachana mimi na Tusa? Kama kinahusu hivyo, mimi nasema hapana. Simwachi Tusa.
TUSA: (Kwa ukali), unaning'ang'ania mimi ndugu yako?
PATRICK: Nani umesikia anahaja na undugu na wewe na ukoo wako huo? Mi nakung'ang'ania kwa pesa yangu uliyopoteza toka nakufatilia, na kama kuna wa kumlaumu kwa hili basi mlaumu Maiko aliyekuwa akinishauri nitoe pesa nyingi sana kwako. Nadhani aliwajua ukoo wake kama mnapenda pesa.
PAMELA: Halafu sisi sio kwamba tunapenda pesa kama unavyofikiria.
PATRICK: Uliona wapi mzazi mwenye mapenzi mema na mwanae akamuozesha kwa posa ya milioni kumi na tano? Si uchizi huo, ukoo wenu umelaanika nyie.
DEBORAH: Mwanangu acha kabisa hayo marumbano, leo nataka kusema kitu ambacho nimekiweka moyoni kwa muda mrefu sana.
PATRICK: Nadhani itakuwa kuhusu baba yangu ila sidhani kama hawa wengine wanahusika.
ADAMU: Ni kweli hatuhusiki, hapa tuongelee mambo ya msingi. Kwanza kabisa kwanini mwanao kaua baba yetu na pia kwanini anaendelea kumtesa mtoto wetu.
DEBORAH: Hili jambo wote linawahusu na ndiomana nimewaita wote ili nipate kuwajuza na mjue kila kitu kilichotokea. Najua Adamu unapotezea sababu hutaki maovu yako ya nyuma yawe wazi, ila kosa dogo ulilotenda kipindi hicho cha nyuma leo ndio lililozua balaa, tafrani na mtafaruku katika maisha yenu.
MARIUM: Bora tu uelezee ulichotuitia Deborah, hayo unayoyaongea hayana msaada wowote kwenye hiyo familia iliyo laanika.
Adamu akachukia sana kwa hiyo kauli juu ya familia yake kuwa imelaanika.
ADAMU: Chunga kauli yako mwanamke.
MARIUM: Kauli yangu!! Kwani uongo? Familia gani kaka na dada wanazaa pamoja, halafu baba anabaka mwanae kama sio laana ni kitu gani?
Adamu alizidi kuchukia na kutamani kutoka kwenye kile kikao.
Mwita aliomba na ruhusa kazini kwaajili ya kuendelea kuchunguza mambo ambayo yanaonyesha kumpa utata mkubwa sana. Alihisi kuwa kuna kazi ambazo si halali zinazotendwa na Tulo pamoja na baba yake bwana Maiko.
Mwita aliendelea kuwa karibu na Tulo haswa kuhusu kisasi alichotaka kulipiza kwa Yuda. Mwita alitaka kujua kuwa Tulo atafanya kitu cha aina gani, akaandaa mtego wa kumkutanisha Tulo na Yuda bila ya Tulo kujua kama ni mtego tu.
Wakiwa tayari kuanza kikao baada ya marumbano ya hapa na pale kuhusu familia ya Adamu, gafla walisikia kelele nyingi nje kama vile mtu anakabwa. Kelele zile ziliwashtua na kuwafanya watoke nje kuangalia kuna nini.
Walipotoka nje walikuta damu nyingi sana imetapakaa pale nje ila hawakuona mtu yeyote.
Wote wakashangaa kuwa ni kitu gani.
 
SEHEMU YA 81

Wote wakashangaa kuwa ni kitu gani.
Marium ndio alikuwa wa kwanza kuuliza,
MARIUM: Mambo gani haya jamani?
DEBORAH: Hata sielewi ni kitu gani.
Adamu akainama na kuangalia ile damu,
ADAMU: Ila hii damu inaonyesha kuwa ni ya mtu.
PAMELA: Mtu gani sasa?
ADAMU: Sijui.
Patrick alikuwa kimya kabisa huku akitafakari mambo mbali mbali katika akili yake bila ya kupata jibu.
Alijiuliza vitu vingi bila ya majibu.
"Inamaana kuna mtu kauwawa hapa kwetu? Kama yupo je yuko wapi? Au ni mauzauza ya mzee Ayubu?"
Akakosa jibu, akawaacha wote pale nje na kurudi ndani.
Nao wakamshangaa Patrick kuonekana kamavile hajashtushwa na lile tukio, tena kamavile amelipuuzia na kuona halina maana au ni kitu cha kawaida.
REHEMA: Itakuwa anaelewa kilichotokea, wengine tunaumiza vichwa hapa wakati mwenzetu kashaelewa kilichotokea.
Tusa na Tina nao wakaamua kurudi ndani na kuwaacha wazazi wao pale nje kwani waliogopa kukutwa na makubwa pale nje.
DEBORAH: Sasa aliyeelewa ni nani?
REHEMA: Mwanao Patrick atakuwa anajua kila kitu.
DEBORAH: Naona unamchukia sana Patrick, ila ukweli utakapokuwa wazi najua utaona haya.
ADAMU: (kwa ukari), Sio maneno ya kumwambia mama yangu hayo.
DEBORAH: Wee mwanaume wewe tafadhari sana, mfokee mkeo sio mimi. Tena ukome kunikaripia, kumbuka hapa ni nyumbani kwangu, nina uhuru wa kufanya na kusema chochote ninachojisikia.
ADAMU: Siku hizi una kiburi sana wewe mwanamke.
DEBORAH: Ndio nina kiburi na jeuri pia.
FAUSTA: Jamani, msianzishe zogo lingine hapa. Kama vipi tukaendelee tu na kikao chetu.
PAMELA: Sasa nyinyi hizi damu mnaona tu ni kitu cha kawaida?
FAUSTA: Si kitu cha kawaida Pamela ila haina jinsi na hakuna la kufanya.
DEBORAH: Damu huwa ni kiashirio cha vitu vingi sana, pia najua inatukumbusha mambo mengi ya nyuma ama tuliyofanya au tuliyofanyiwa.
MARIUM: Sawa, basi turudini ndani.
Bi.Rehema akamvutia Adamu kwa pembeni wakati wengine wanarudi ndani.
Bi.Rehema akamuuliza tena Adamu kuhusu Deborah.
REHEMA: Kwani wewe na huyu mwanamke mna tatizo gani? Mliachana kwa mateke na ngumi nini?
ADAMU: Hapana mama, huyo mwanamke ni kisirani tu huwa hata sijui ana matatizo gani.
REHEMA: Au bado mnapendana?
ADAMU: Aaah mama!! Maswali gani hayo? Si unamuona mwanamke mwenyewe alivyo jeuri jamani.
REHEMA: Ndio kawaida ya wanawake wakipata mali, ila wewe vumilia mwanangu ili tuondoke hapa kwa usalama.
ADAMU: Sawa mama, hakuna tatizo.
Adamu akakubaliana na mama yake kutulia.
Tulo na Yuda wakakutana kama ambavyo Mwita amepanga mtego wa kuwakutanisha.
TULO: Niambie kidume, wewe si ndio unajifanya kidume.
YUDA: Sio najifanya, mimi ni mwanaume niliyekamilika.
TULO: Kumbe umekamilika eeh!!
YUDA: Ndio nii mwaname niliyekamilika na kujiamini sana.
TULO: Napenda sana wanaume wa aina yako.
Yuda hakutaka kuendelea kuwepo eneo lile na kuamua kuondoka hata kumshangaa aliyemuita pale bila kumuon.
Wakati Yuda anaondoka, akili ya Tulo ilishapanga kitu kingine juu ya Yuda.
Deborah na wengine wakataka kuanza kuzungumza yaliyowafanya waweke kikao humo ndani.
DEBORAH: Mbona hawarudi Adamu na mama yake?
Mara na wao wakarudi mule ndani na kukaa kwaajili ya mazungumzo.
PAMELA: Jamani mimi nina wazo, kabla ya kuanza kikao hapa wangetoka hao wanaume na kwenda kuangalia angalia nyumba nzima ili tujiamini kuwa tuko salama.
Patrick na Adamu wakajifanya kama vile hawajasikia kitu chochote kinachozungumzwa na Pamela kwani walikuwa kimya kabisa.
Pamela hakuna na imani na ile damu ukizingatia imeachwa pale nje, akapata wazo la kwenda kuifukia ile damu.
Kitu ambacho Maiko alikifanya hakuna aliyekijua kwa wakati huo ila Maiko mwenyewe alikuwa kama vile mtu aliyechanganyikiwa na hakujielewa kabisa kwa mambo aliyoyafanya.
Alidhani moyo utasawazika na kitu alichofanya, cha zaidi zaidi aliendelea kujiuliza kuwa kwanini amefanya alivyofanya.
Maiko alikuwa ndani ya gari, karibu kabisa na nyumbani kwa Deborah akatamani ajitokeze ili aongee anachotaka kusema ila alishindwa kwa kuona kuwa watamchukuliaje na kumuonaje.
Yuda akiwa anaondoka, akaamua kupita njia za mkato ili kurudi kwao.
Wakati anatembea sasa, mbele yake akazuiwa tena alizuiwa kwa kukabwa kwa nyuma.
Yuda akakukuruka sana, alipogeuka alikutana tena na Tulo, ila Tulo alikuwa tayari kwa mpambano safari hii.
Kwahiyo Tulo na Yuda wakaanza kupambana, kurushiana mateke, kupigana ngumi na kupimana mabavu. Kila mmoja alijifanya gangwe mbele ya mwingine.
Matukio yote haya yalikuwa yakishuhudiwa na Mwita aliyetumia mbinu za kijeshi kuwafatilia bila ya wao kujua.
Mpambano kati ya Yuda na Tulo ulikuwa mkali sana, Tulo akatoa bastola na kumnyooshea Yuda kwa lengo la kummaliza kabisa.
Mwita akashangaa kumuona Tulo na bastola, akajiuliza kwa raia wa kawaida kama Tulo atawezaje kumiliki bastola? Ana kibali gani cha kumiliki silaha kama ile?
Wakati Mwita akitafakari hayo, mlio mkari wa risasi ukasikika masikioni mwake "Paaaaaa"
Mwita akapatwa na mshtuko, huku moyo wake nao ukilia paaaa kwani ni yeye aliyeamua kuwakutanisha Yuda na Tulo siku hiyo ili ajue kile ambacho Tulo amepanga kumfanyia Yuda.
Sele aliyekuwa yupo ndani kwao, akapatwa hofu juu ya Yuda. Akahisi kuwa kuna kitu kibaya kimempata ndugu yake huyo.
Akaamua kumfatilia kwa njia aliyoondokea ili labda akutane nae njiani kwani hofu ilimjaa sana juu ya Yuda, ukizingatia hakuelewa kuwa Yuda aliitwa na nani kwani tangu alivyopigiwa simu na kuondoka hakurudi tena na wala hakuaga vizuri aendako.
Pamela alikuwa na uhitaji sana wa kutoka ili akaifukie ile damu kwani hakuona kuwa ni kitu kizuri wao kukaa na mazungumzo ndani wakati wanajua kuwa kuna damu imetapakaa nje ya nyumba ile.
Deborah hakutaka kujali sana kuhusu ile damu ila yeye alitaka kuendelea na maongezi yake aliyowaitia toka mwanzo.
DEBORAH: Nitapenda historia hii niieleze kwa makini ila sitahitaji swali lolote hadi pale nitakapohitimisha.
PATRICK: Kwani ni historia ya maisha yako au ni historia ya nini?
DEBORAH: Ni historia ya maisha yangu ila najua wengi itawagusa, na wengi wataelewa kile ambacho nitakieleza. Na huu ndio ukweli mtupu wa maisha yangu.
Pamela akaingilia kati wakati Deborah akiendelea kuzungumza.
PAMELA: Samahani kwa kukukatisha Deborah, ila nina ombi kidogo.
DEBORAH: Ombi gani? Hutaki niwataje majina yenu halisi kwenye stori hii.
PAMELA: Hapana sio hivyo, ombi langu ni jingine. Ila hata hivyo, unamaana unataka kuelezea yale yaliyopita zamani?
DEBORAH: Ndio, kwani kuna ubaya?
PAMELA: (Huku akisitasita), aaah hapana hakuna ubaya ila sidhani kama watoto wetu itawahusu.
DEBORAH: Itawahusu ndio, napenda wajifunze kuwa duniani kuna watu wa tofauti na umdhaniaye siye kumbe ndiye. Labda kama una lingine Pamela.
Pamela aliona Deborah anataka kumuumbua tu, jinsi yeye na Adamu walivyomsaliti ila hakuna jinsi ilimradi Deborah kaamua kuongea akaamua wamuache tu aongee.
PAMELA: Ila nilikuwa naomba nikafukie ile damu pale nje maana si kitu kizuri kuzungumza ndani wakati nje kukiwa na damu isiyoeleweka ni ya nini.
Deborah akamruhusu Pamela aende.
Pamela akatoka nje na muda huo huo akarudi ndani na kuwaambia kuwa ile damu haipo.
DEBORAH: Unamaana gani?
PAMELA: Ile damu haipo, sijaikuta pale ilipokuwa.
Deborah akaamua kwenda kuangalia mwenyewe.
 
SEHEMU YA 82

Deborah akaamua kwenda kuangalia mwenyewe.
Alipofika nje hakuona chochote na kurudi ndani.
DEBORAH: Ni kweli hakuna chochote, ile damu imepotea kweli.
Wote wakabaki kumtazama tu.
FAUSTA: Sasa hiyo damu inamaana gani? Kuja na kupotea?
DEBORAH: Kiukweli inakuwa ngumu kuelewa.
MARIUM: Mi nadhani tutoke nje na kutazama nyumba kwanza.
Wote wakakubaliana kutoka nje, wakati wananyanyuka, Patrick wala hakujishughulisha nae, aliendelea kukaa pale pale walipokaa.
Tusa nae akamvuta Tina na kumzuia kutoka nje ili waweze kujadili mambo yao.
Tina alikaa karibu na Tusa pale alipomwita.
TUSA: Unajua kwanini nimekuzuia?
TINA: Niambie kwanini, mi sijui.
TUSA: Nimeona wanajisumbua tu hakuna lolote, nadhani kuna mtu anawafanyia mchezo bila ya wao kujua.
TINA: Mmmh!! Kweli Tusa?
TUSA: Huo ndio ukweli wenyewe ila hao watu huwa hawashauriki, waache wajisumbue wakisharidhika na yao watarudi ndani.
Mara wakamuona Patrick akiinuka pale kwenye kochi na kuelekea chumbani kwake.
TINA: Na mbona Patrick yuko vile?
TUSA: Atakuwa ana mipango yake mibovu tu pale alipo, roho inaniuma sana tangu nisikie kuwa kamuua babu ila sina la kufanya kwamaana Patrick ana nguvu sana. Lakini nitalipa kisasi tu.
TINA: Mi nadhani kuwa yote tumuachie Mungu.
Wakamuona Patrick akirudi tena pale sebleni, wakaamua kunyamaza kwasasa.
Wakiwa pale nje na kujadili.
REHEMA: Ila mimi nawashangaa sana, tuatoka nje ila muhusika tunamuacha ndani.
DEBORAH: Tafadharini sana, mwacheni Patrick wangu. Maswala ya kumsemasema siyapendi.
PAMELA: Mmh!!
Wakajaribu kuzunguka zunguka ila hawakuona chochote na kuamua kurudi ndani.
DEBORAH: Nadhani tukaendelee na kikao chetu.
FAUSTA: Haya mambo yanachanganya sana hadi tunakuwa kama machizi kwa kufatilia kitu tusichokijua wala kukitambua.
Wakarudi tena ndani, kama walivyotoka ndivyo walivyorudi.
Mwita aliumia sana moyoni na kuinuka pale alipokuwa kisha akaanza kukimbilia eneo ambalo Yuda na Tulo walikuwa wakipambaniana.
Kufika pale akagundua kuwa ile risasi ambayo Tulo aliipiga ilikuwa ni risasi hewa kwani alipiga hewani na si mwilini kwa Yuda.
Mwita akaanza kumsihi Tulo asifanye chochote kwani bado alikuwa ameshikilia bastola mkononi.
Mwita alipoona Tulo ni mgumu kuachia bastola, akaamua kutumia mbinu zake za kijeshi kuipata na kusahau kuwa Tulo ni jasusi.
Sele alipofika eneo la tukio alishangaa sana kuona nduguye amenyooshewa bastola.
Wakati Mwita akiwa anapokonyana ile bastola na Tulo, Sele nae akatumia muda huo kukimbia na nduguye Yuda na kuamua kukimbilia nyumbani kwa mama yao mdogo Deborah.
Deborah akaanza kuzungumza tena pale sebleni.
DEBORAH: Jamani yaliyopita yamepita, hebu tuzungumze mengine yanayotuhusu sasa.
REHEMA: Ila nyumba yako ina maajabu sana Deborah.
DEBORAH: Ila maajabu yake hayawezi kufikia maajabu ya ukoo wenu.
ADAMU: Hivi Deborah huwezi ongea bila kutaja ukoo wetu?
DEBORAH: Lazima niutaje, ukoo wenu umeniharibia sana maisha. Umeniharibia mwanangu Patrick, mtoto niliyemkuza huku nikimtegemea kuwa ni faraja yangu na atakuwa nami katika shida na raha. Ila ukoo wenu umemuharibu Patrick na bado mnataka kumuandama kwa maneno mengi na chuki.
Wote wakawa wametulia wakimsikiliza Deborah anavyobwabwaja ya moyoni mwake.
ADAMU: Sema mama sema, leo ni siku yako ya kutoa ya moyoni.
Deborah hakuacha kuwaambia jinsi gani wanamkera pale wanapomuongelea Patrick kwa mabaya tu wakati Patrick anawahusu.
Mara Yuda na Sele wanaingia kwa Deborah huku wakihema juu juu.
Ikabidi waulizwe ni kitu gani kinachowafanya waheme vile, Yuda akaelezea kwa ufupi ilivyokuwa.
Mara gafla wakamuona Patrick akiinuka na kutaka kutoka, Deborah nae akainuka na kumzuia.
DEBORAH: Mwanangu, hiki kikao kinakuhusu wewe. Tafadhari usiondoke mwanangu, si wameshasema kuwa wamemuacha na Mwita? Basi hakuna kitakachoharibika maana Mwita ni mwanajeshi.
PATRICK: Ila mama umezidi kuzungusha mambo, baada utueleze yanayohusika wewe kitu kidogo unakatisha mada. Kama nitarudi kukaa basi utueleze yanayohusika kwa makini.
DEBORAH: Usijari mwanangu, hiki kikao kina umuhimu sana kwako na maisha yako kwa ujumla. Napenda ujue ukweli wote uliojificha katika maisha yangu na katika maisha yako, kuna siri kubwa sana kati yangu na yako unatakiwa kuijua Patrick. Sitaki uende popote bila ya kuijua siri hii mwanangu.
PATRICK: Sawa mama, nimekuelewa.
Wakarudi wote pale sebleni, na wengine wakiendelea kumpa pole Yuda kwa kilichotokea.
MARIUM: Mkiambiwa msikilize maneno ya watu wazima mnayapotezea.
Haya sasa, yakishawapata ya kuwapata ndo mnakupuka mliyoonywa kabla.
Marium alikuwa kama vile anawakumbusha wanae kwa kauli zake ya kuwa waachane na Tina na Tusa kwani watawaletea mabalaa.
Kikao kiliendelea sasa na Deborah kuanza kueleza yaliyojiri, kumbe huku nje Maiko alikuwa amekuja na mfuko tena mfuko uliokuwa unavuja damu, ilionyesha kuwa kuna kitu alikibeba ndani ya mfuko huo.
Maiko na mfuko wake alisogea hadi kwenye mlango wa nyumba ya Deborah, uleule mlango wa kuingia sebleni.
Maiko ndio alisimama hapo na mfuko wake.
 
SEHEMU YA 83

Maiko ndio alisimama hapo na mfuko wake.
Akatamani kugonga ule mlango ila akasita, akatamani kuingia bila ya hodi napo akasita.
Aliposikilizia kwa makini alimsikia Deborah akianza kuelezea historia ya maisha yake.
Ikabidi akae chini akiwangoja wamalize kuzungumza yale maongezi yao ili na yeye apeleke vyake.
Mwita alimshikilia Tulo na sasa alitumia kazi yake ya usalama wa taifa, hakutaka tena kuleta mambo ya urafiki.
MWITA: Tulo, unamiliki silaha kwa misingi ipi?
TULO: Maswali gani ya kuniuliza hayo bhana?
Mwita akaona hapa itakuwa longolongo, akaamua kujitoa kupambana na Tulo ili kumpeleka kituoni na maswali yale akayajibie kituoni kama wengine wafanyavyo.
Deborah alianza kwa umakini kabisa kuwaelezea na alipenda wote wapate kuelewa na kutambua ilivyokuwa toka mwanzo. Alitaka kueleza kila kitu kilivyokuwa hadi kilivyo sasa kwani yeye alijiona kama kiungo kikubwa cha katikati kwenye yale marumbano ya familia.
"Katika familia yetu ya watoto watatu yani mimi, dada yatu Marium na mdogo wetu Anna.
Wazazi walifariki na kutuacha tukiwa bado wadogo, shangazi yetu ndiye aliyechukua jukumu la kutulea sisi.
Tulikaa kwa shangazi huku tukimtegemea kwa kila kitu, kipindi hicho alikuwa akiishi hapa hapa Mwanza.
Nilipokuwa binti, alikuwa baba mdogo, ambaye ni mdogo wake na baba yetu mzazi, akamuomba shangazi anichukue mimi ili ampunguzie mzigo kidogo wa kulea, na alinichagua mimi kwavile nilikuwa mchangamfu sana na niliweza kumudu maisha mbalimbali.
Bamdogo alikuwa akiishi Arusha, hapo ndipo nikapata safari ya kutoka nje ya Mwanza na kwenda Arusha.
Kwa mara ya kwanza niliingia Arusha na kuona ni mji wa tofauti kidogo na Mwanza ambako nilikuzoea.
Bamdogo hakuwa mtu wa shida kwa kifupi alikuwa na pesa za kutosha hata nikamshangaa kwanini amechagua kunilea mimi tu wakati uwezo wa kutulea wote na ndugu zangu alikuwa nao.
Kwakweli niliyafurahia maisha ya Arusha haswaa pale nyumbani kwa bamdogo.
Kulikuwa na kijana aliyekuwa na urafiki na bamdogo, kijana huyo alikuwa anakuja mara kwa mara nyumbani kwa bamdogo, na huyu kijana ndio Maiko.
Alionyesha kuvutiwa sana na mimi kwani kila alipokuwa akija kwa bamdogo alikuwa anabeba zawadi mbalimbali na kuniletea, ila mimi sikuvutiwa nae wala sikumpenda. Nikamuona kama sehemu ya familia tu.
Kuna kipindi bamdogo alinituma nimpelekee mzigo wake Dar es salaam, alinikatia tiketi nami nikasafiri na kwenda huko.
Nilikaa Dar es salaam kwa muda wa wiki moja, nilifikia nyumbani kwa rafiki wa bamdogo yani kule nilikopeleka mzigo.
Nikiwa Dar es salaam, siku moja kabla ya safari yangu ya kurudi Arusha, nilimuomba mtoto mmoja wa ile familia niliyofikia anipeleke baharini ili nami nikashangae maji ya bahari kidogo kabla sijarudi Arusha.
Tukiwa baharini, akatokea kijana aliyejitambulisha kwetu kwa jina la Jumanne, kijana huyu alionyesha kuvutiwa sana na mimi kwani alimuomba nafasi ya kuzungumza na mimi yule mtu niliyekuwa nae kule baharini. Na yule dada akatupisha kidogo tuzungumze.
Jumanne akaanza kwa kunipa sifa kedekede na kunitongoza nikafurahia kwavile hata mimi nilivutiwa nae ila sikumuonyesha moja kwa moja kuwa namkubali, tukaongea ya hapa na pale ila nikakumbuka kuwa kesho yake natakiwa nisafiri na kurudi Arusha, nilipomwambia yule kaka alisikitika sana ila akaniomba nimuelekeze ninapoishi huko Arusha, sikukataa kumuelekeza kwavile nilivutiwa nae, nikamuelekeza kila kitu ila sikuwa na imani kama anaweza kufika Arusha kwaajili yangu tu.
Kesho yake kama ilivyopangwa, nikasafiri na kurudi Arusha.
Nilipokuwa Arusha, sura ya Jumanne haikuweza kutoka machoni mwangu. Ingawa nilimuona kwa siku moja tu ila moyo wangu ulimpenda sana ila sikufikiria kama Jumanne na yeye amenipenda kiasi kile nilichompenda mimi.
Ilikuwa hata akipita mtu mwingine mwenye jina hilo na kuitwa nilikuwa nashtuka mimi, hii yote ni jinsi gani Jumanne aliingia vizuri kwenye akili na mawazo yangu.
Siku zilipita bila barua wala mawasiliano yoyote kutoka kwa Jumanne na kipindi hicho ilikuwa simu ni kitu cha nadra sana labda zile za mezani ambayo pia namba yake nilimpa ila sikuwahi kuitwa kuwa kuna mtu ananipigia.
Nilijua Jumanne ameshanisahau kama kawaida ya wanaume ilivyo, anakukumbuka akikuona machoni tu, ukiwa mbali naye kumbukumbu juu yako anapoteza.
Ikabidi nianze kujilazimisha taratibu ili niweze kumsahau Jumanne.
Nikiwa nimetulia ndani, wazo la Jumanne likanijia tena kichwani, nikajikuta nikipiga kichwa changu kwa ulimbukeni wa kufikiri huku nikijilaumu kuwa kwanini namfikiria huyo Jumanne muda wote.
Alikuja mtoto wa bamdogo na kunishtua na huyu ndiye aliyekatisha mawazo yangu, akaniambia nje kuna mgeni wangu ananiningoja. Nikachukia sana kwani nilihisi kuwa huenda akawa Maiko kwani na yeye siku zingine alikuwa anafanya hivyo ili apate wasaa wa kuzungumza na mimi, nilitamani nisiende ila nikaamua kwenda ili nijue huyo Maiko kaja na mpya gani maana kama kumkataa nilishamkataa sana hadi kuchoka sasa.
Nilipofika nje nilimuona mtu kasimama chini ya mti halafu amegeuzia mgongo getini kwetu, nikajiuliza mgeni mwenyewe ndio yule au ni nani, nikarudi tena ndani kumuuliza mdogo wangu, akanielekeza alivyovaa ndipo nikajua kuwa mgeni mwenyewe atakuwa ni yule.
Nikatoka na kumfata pale chini ya mti, nikamgusa bega ili nimuulize kuwa ameniitia nini, kugeuka ni Jumanne.
Kwanza kabisa sikuamini macho yangu, nilijihisi kama vile naota. Nilijikuta nikimkumbatia kwa furaha, na kitu cha kwanza alichosema,
"Umeamini kuwa kweli nakupenda Deborah?"
Nikaitikia kwa kichwa tu kwani sikuamini kama Jumanne alifunga safari ya kutoka Dar kuja Arusha kwaajili yangu.
Tukaongea mengi sana pale chini ya mti, hadi alipoondoka na kuniahidi kuja tena kesho.
Penzi langu na Jumanne lilikua siku hadi siku, Jumanne alikaa Arusha kwa muda wa mwezi mmoja, akaniambia kuwa anapenda niwe mke wake ili niweze kurudi nae Dar kuishi wote kama mke na mume, nilifurahia sana na ndoto yangu kubwa ikawa kuwa mke wa Jumanne siku zote za maisha yangu.
Nilimuamini sana Jumanne kwani si kitu rahisi mtu kufunga safari ndefu vile kwaajili ya mwanamke tu wakati wanawake wapo wengi.
Usumbufu wa Maiko ulinikera sana, sikutaka hata kumuona mbele ya macho yangu, kumbe Maiko alimwambia bamdogo kuwa anataka kunioa na kuishi na mimi.
Bamdogo akaanza kunilazimisha kuwa niolewe na Maiko ila mimi nikakataa katakata, nikamwambia bamdogo kuwa nina mchumba na yupo tayari kunioa, bamdogo hakutaka hata kunisikia kuhusu huyo mchumba. Bamdogo akaniambia kuwa,
"ukiolewa na mtu mwingine tofauti na Maiko, ujue huna radhi na mimi"
Nilimuomba sana bamdogo anikubalie kuolewa na mtu nimtakae ila bamdogo alikataa kabisa, sikujua cha kufanya ili niweze kuolewa na kuishi na Jumanne.
Jumanne alikuwa na nia ya kunioa kweli kwani alitafuta watu wa karibu kule Arusha ili wazungumze na bamdogo nae apate kibali cha kuja kujitambulisha ila bamdogo hakutaka hata kumuoa Jumanne.
Hakukuwa na la kufanya kwani bamdogo alizidi kung'ang'ania kuwa mimi niolewe na Maiko, wakati Jumanne amerudi Dar nikakubaliana nae kuwa nitatoroka kwa bamdogo na kwenda Dar kuishi nae halafu tutaenda kujitambulisha kwa shangazi Mwanza.
Bamdogo aliendelea kunilazimisha kuolewa na Maiko ndipo nilipoamua kufanya nilichodhamiria, nikapanda gari na kutoroka kwenda Dar kwa Jumanne.
Tukiwa njiani, akapanda mdada aliyekaa jirani na mimi, alijitambulisha kwangu kwa jina la Pamela.
Tukajikuta tukipiga stori nyingi sana na kuzoeana gafla hadi tunafika Dar es salaam.
Kwa bahati nzuri, alipokuja Jumanne kunipokea sababu nilimpa taarifa tukajikuta na yule mdada tukienda nae mtaa mmoja.
Niliishi na Jumanne kama mke na mume, baada ya muda tukapanga safari na kwenda Mwanza kwa shangazi, nilipomuelezea shangazi hakupinga bali alitupa baraka zote na taratibu za posa zikafanyika hapo nyumbani kwa shangazi.
Mimi na Jumanne tulirudi Dar na kuishi kwa amani sasa kwani tulishatambulika kwa ndugu zetu.
Nikapata ujauzito, mtu pekee na rafiki wa karibu alikuwa ni Pamela. Alionekana kunisaidia kwa mambo mengi sana kipindi changu chote cha ujauzito hadi kujifungua.
Nilipojifungua, mume wangu alifurahi sana na nilijifungua mtoto mzuri wa kike aliyeitwa Jasmine.
Bibi yake na Jumanne alifurahi sana kumuona Jasmine na akasema amekuwa hai muda wote akingoja kumuona mjukuu atakayefanana nae, na Jasmine alifanana kweli na bibi huyo.
Jumanne alimpenda sana mtoto wetu.
Siku chache baada ya kujifungua niliona tabia ya Jumanne imebadilika, nilihisi huenda ana mwanamke mwingine nje.
 
SEHEMU YA 84

Siku chache baada ya kujifungua, niliona tabia ya Jumanne imebadilika. Nilihisi huenda ana mwanamke mwingine nje.
Nikajaribu kumshirikisha swala hili rafiki yangu Pamela ili anisaidie kwa mawazo, akaniambia kuwa ni kawaida ya wanaume kuwa kama alivyo Jumanne kwa wengi huwa wanachukizwa na harufu za watoto wakiwa bado wachanga.
Nikashindwa kuelewa kuwa inakuwaje Jumanne achukizwe na harufu ya mtoto wetu? Sikuona harufu mbaya kwa mtoto kusema hadi yeye achukizwe na kubadilika kitabia.
Ilikuwa tofauti na nilivyozoea, Jumanne alikuwa anarudi usiku sana na mara nyingine analala huko huko bila taarifa yoyote ile.
Kukikucha, Pamela anakuja nyumbani kwangu tunaongea mengi na kufanya vingi pamoja. Jioni anaondoka, hata kama siku hiyo Jumanne kawahi kurudi ila anapoondoka Pamela nae alikuwa anaondoka na kutokomea huko huko.
Kwakweli sikumfikiria vibaya Pamela, nilimuamini sana kwani alikuwa mtu wa karibu yangu akinisaidia mambo mbali mbali, nilimuelezea yote yaliyonisibu, naye alikuwa mstari wa mbele kunifariji na kunibembeleza.
Mtoto wangu aliendelea kukua na kuzidi kupendwa na watu wengi, kwani alikuwa ni mtoto mzuri na anayependa kucheka muda wote. Kila mtu alimpenda Jasmine.
Mara nyingi Pamela alifika nyumbani kwangu ili tu amuone Jasmine wangu, ila bado tabia ya Jumanne ilizidi kunishangaza, nilishindwa hata kuelewa ni shetani gani aliyemkumba na kuchukua upendo wote aliokuwa akinipenda.
Baada ya miezi kadhaa nilimuona Pamela akibadilika, na kwavile hata mimi nilishawahi kuwa mjamzito nikaweza kugundua mapema kuwa naye ni mjamzito ila nilipomuuliza alipinga kuwa hana ujauzito.
Siku zikapita na hali yake ikazidi kubadilika, sasa ilionyesha wazi kuwa ni mjamzito, nikamuuliza tena ila hakunijibu chochote aliniaga na kuondoka na hakurudi kwangu tena, nikaja kusikia habari kwa majirani kuwa Pamela amesafiri yuko Morogoro na anaishi huko kwa sasa.
Nikashangaa sana kuwa kwanini ameondoka bila hata ya kuniaga, nikahisi labda hakutaka nijue kama anasafiri au basi alisahau kuaga.
Maisha yaliendelea hivyo hivyo nikiwa na mwanangu Jasmine, baada ya miezi mitatu Jumanne akaniaga kuwa anasafiri anaenda Morogoro kikazi, nikamuomba twende wote na mtoto wetu ila aligoma.
Lakini nilishukuru kwa kuagwa maana mara nyingine huondoka bila ya kutoa taarifa yoyote ile.
Hakukuwa na mawasiliano kati yangu mimi na Jumanne, kwani sikuwa na simu ya kuweza kuwasiliana nae chochote. Nilingoja barua zake au apige simu kwa jirani ila haikuwa hivyo, Jumanne alikuwa kimya kabisa kama vile hajaacha mtu nyumbani.
Mwanangu Jasmine, alipenda sana kubebwa na pia aliwahi kuongea na kutembea.
Ikitokea jirani amwambie Jasmine njoo nikubebe mgongoni, mwanangu hakusita bali alienda na kubebwa hadi pale mtaani wakamtunga jina na kumuita "cha mgongo" kwavile alikuwa anapenda sana kubebwa mgongoni.
Wengi walimpenda Jasmine kwa utundu wake na uzuri wake.
Siku moja nikiwa ndani napika, mwanangu Jasmine akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu alitembea toka pale jikoni hadi nje, nikajua mwanangu yupo kucheza na wenzie pale upenuni kwani pale kulikuwa na watoto wengine na wote walipenda kucheza na mwanangu Jasmine. Kwavile mwanangu alikuwa mtundu, alipotoka nje niliona afadhari ili nipike haraka haraka nikamchukue na kumpa maziwa.
Na kweli nilipika haraka haraka, nilipotoka nje kwenda kumchukua mwanangu sikumuona, ikabidi niwaulize watu wa pale kuwa mwanangu kaenda wapi, mtoto mmoja wa miaka saba akanijibu kuwa Jasmine amechukuliwa na Vero mtoto wa mama mwenye nyumba kasema anaenda nae dukani.
Nikajikuta roho ikiniuma gafla na kujiuliza kwanini hakuja kuchukua ruhusa kwangu mwenye mtoto.
Nikamfata mama Vero na kumwambia kuwa tabia ya mwanae Vero kumchukua mwanangu Jasmine bila taarifa yoyote sijaipenda. Mama yake akasema kuwa akirudi atamsema Vero.
Muda ulipita bila ya Vero kurudi na mwanangu, hofu ikanitanda na uoga kunishika kuwa Vero atakuwa wapi na mwanangu maana kama ni dukani wangekuwa wamesharudi.
Ikabidi niende maduka ya karibu kuwatizama ila sikuona dalili yoyote ya uwepo wa Vero, nikamfata tena mama Vero kumwambia kuwa Vero hajarudi na mwanangu hadi muda huo.
Mama yake nae akashangaa kuwa Vero atakuwa amepitia wapi hadi hajarudi kumrudisha mtoto ila akanipa matumaini kuwa Vero atarudi tu huku akifoka kuwa akirudi atamsema sana kwa kuchukua mtoto bila taarifa na kutokomea nae.
Kufika jioni ndio tunamuona Vero akirudi tena peke yake bila ya mwanangu Jasmine. Kwakweli nilipatwa na mshtuko sana, ikabidi tumuulize Vero amemuacha wapi mtoto akawa anakataa kuwa hajaondoka na mtoto wakati watu wengi walimuona akiondoka nae, tulimuuliza sana ila akagoma kusema kwakweli sikuweza kuvumilia.
Nilienda moja kwa moja kituo cha polisi na kuwaeleza kila kitu kuhusu upotevu wa mwanangu, nilihisi kuchanganyikiwa kabisa.
Polisi walifika pale tunapoishi na kumkamata Vero ili akaonyeshe mahali alipompeleka Jasmine.
Mwanzoni alikuwa anagoma ila polisi wakampiga sana na mwisho wa siku akakubali kutupeleka.
Jamani hili swala ulisikie kwa mwenzio tu, usiombe likutokee maishani mwako.
Vero alitupeleka katikati ya migomba, mwili wa mtoto mdogo ulikuwa umelala chini hauna ngozi. Mwanangu Jasmine alichunwa ngozi, ooh mwanangu mimi sijui aliliaje jamani sijui alihangaika vipi mtoto mdogo kama yule tena malaika wa Mungu, sijui alilia kilio gani mwanangu Jasmine.
Kumchunguza vizuri alikuwa amekatwa sehemu za siri, ni ukatili gani huu jamani kwa mtoto mdogo kama Jasmine. Sijui mwanangu aliwakosea nini hadi wakamfanya vile walivyomfanya.
Uchungu nilioupata hauelezeki, ni uchungu wa milele. Kila nikikumbuka mwili wa mwanangu Jasmine machozi hunitoka, najihisi kulia muda wote sijui mwanangu aliwakosea nini. (Deborah aliinama na kulia kwa muda, Patrick akasogea na kumbembeleza mama yake. Kisha akaendelea kusimulia mkasa mzima)
Sikuwa na ndugu Dar es salaam, Jumanne nae hakuwepo. Rafiki wa karibu niliyemtegemea hakuwepo, nani wa kunifariji Deborah nani wa kunifuta machozi muda huo. Nilikuwa na maumivu makubwa sana.
Mwili wa mwanangu ulipelekwa hospitali kwa uchunguzi kisha tukarudishiwa kwenda kuzika, majirani walinisaidia sana ila sikuona umuhimu wao, nilichotaka ni mwanangu Jasmine tu.
Walinisaidia na kufanikisha maziko ya mwanangu Jasmine, kilichoendelea hapo ni maumivu, uchungu na kilio nilitamani ardhi ipasuke na kunimeza kabisa ili nisiwepo katika uso wa nchi.
Vero alishikiliwa na polisi kwa uchunguzi ambapo alisema kuwa kuna vijana walimpa pesa na kutaka kupelekewa mtoto ila hao vijana hawakujulikana ni wakina nani.
Ulipita mwezi mzima bila Jumanne kurudi na mimi niliendelea na maumivu yangu.
Vero nae aliachiwa na polisi kwa kigezo kuwa wamempima na kumuona kuwa hana akili nzuri yani akili yake inakuja na kupotea. Roho iliniuma sana kumuona aliyehusika na kifo cha mwanangu akidundika mtaani.
Siku aliyorudi Jumanne jambo la kwanza ilikuwa ni kumuulizia Jasmine kuwa yuko wapi.
Nilitokwa na machozi tu bila ya kuwa na maelezo ya kuhusu Jasmine. Majirani walimuita Jumanne na kumueleza ilivyokuwa.
Jumanne aliporudi ndani nilijua atakuja kunifariji na kuomboleza wote, ila alikuja kwa maneno makali sana tena kwa kufoka.
"wewe mwanamke ni mpumbavu sana, huna akili kabisa wewe. Umemuachia mwanangu mpaka kauwawa? Hujui kulea kabisa wewe. Na kwa kiburi chako ukamzika mwanangu bila ruhusa yangu! Sijapata kuona mwanamke mpumbavu kama wewe. Kwakweli najilaumu na kujuta sana kwa uamuzi wangu wa kuishi na mwanamke mpumbavu kama wewe. Itabidi nianze kujifikiria upya kuoa mwingine"
Muda wote nilikuwa nalia tu mule chumbani.
Jumanne hakutaka hata kunisogelea, akaniambia kuwa anaondoka tena na hatarajii kurudi wala nini, alichoniomba ni kufungasha vyangu na kuondoka ili atakaporudi asinikute.
Roho iliniuma sana pale Jumanne alipoondoka kweli, nikaamua kufanya kitu cha kijasiri, kulipa kisasi japo kidogo tu.
Nikatoka nje na kumuita Vero kwa upendo kabisa huku nikimchekea kuwa kuna kitu nataka anisaidie ndani na bahati nzuri pale nje hapakuwa na mtu yeyote zaidi yake.
Alipokuja sikumlazia damu, nilimponda kichwani na kitu kizito akaanguka chini na kupoteza fahamu, kisha nikachukua upanga na kukata miguu yake kwani ile ndio iliyomtembeza kumpeleka mwanangu kuuwawa, sikujali kusema hana akili nzuri wala nini.
Baada ya hapo nikajiandaa kutoka sasa kwaajili ya kutoroka.
 
SEHEMU YA 85

Baada ya hapo nikajiandaa kutoka sasa kwaajili ya kutoroka.
Nilichukua mkoba wangu uliokuwa na baadhi ya nguo na vitenge kisha nikaubeba, nikachungulia nje bado niliona kupo kimya, nikatumia mwanya huo kutoka na kuondoka.
Nakumbuka njiani nilikutana na mama Vero akiwa anarudi nyumbani, alinishangaa kwa zile harakati nilizokuwa nazo, akaniuliza "vipi unasafiri?"
Nilimjibu hapana naenda kumpelekea nguo rafiki yangu mmoja hivi, akauliza tena kuwa mbona naenda usiku, nikamjibu kwavile mchana huwa yupo kazini.
Nikaenda hadi kituoni na kupanda daladala ila kiukweli sikujua pa kuelekea ila nilitaka kujificha kwani nilijua kwamba wakijua tu kuwa nimemkata mtu miguu lazima nitafunguliwa kesi bila kujali maumivu yangu na mimi juu ya mwanangu.
Sikuwa na pesa ya kuweza kufika Mwanza, kwakweli sikujua cha kufanya.
Kufika njiani na lile daladala nikashuka, yani nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, sina pa kuelekea, sina ndugu Dar es salaam na hakuna wa kunisaidia.
Nikawa natembea bila ya kuelewa ninakoelekea, nikaona bonde, nikadhani itakuwa vyema nikienda kupumzika pale bondeni.
Kulikuwa na mti wa mwembe pale karibu na bonde, nilienda na kukaa chini ya ule mti kama vile najikinga jua wakati ulikuwa ni usiku.
Wakati nimekaa pale chini ya mti nikiwa na mawazo yangu ya pa kwenda, mara gafla nikasikia sauti ya mtoto akilia, nilidhani ni mawenge yangu juu ya Jasmine ila kadri nilivyokaa ndivyo sauti ya kitoto ilivyozidi.
Nikainuka na kuangaza huku na kule kuwa labda kuna mtu anapita na mtoto, ila eneo lile halikuwa na njia wala nini.
Ikabidi niangalie ni wapi sauti inatokea, wakati natafuta tafuta nikaona kitoto kidogo sana kimetupwa, kilikuwa kidogo kweli kimeviringishwa kwenye khanga.
Roro ya uchungu ikanishika, nikamuinua yule mtoto, nikachukua baadhi ya vitenge vyangu kumkinga na baridi. Alikuwa mdogo sana, nadhani alitoka kuzaliwa na mama yake kuamua kumtupa labda sababu ya ugumu wa maisha.
Nikakaa nae chini, alikuwa bado analia nikajua kuwa ana njaa pia.
Nikachukua ziwa langu ambalo bado lilikuwa linaendelea kutoa maziwa kwani Jasmine alikufa wakati bado sijamuachisha kunyonya. Nilipokamua chuchu yangu na kuona inatoa maziwa, nikamnyonyesha mtoto yule.
Alinyonya na kutulia, nikanyanyuka pale chini na kuendelea na safari, na sasa nilikuwa naenda kituo cha mabasi ya mikoani ili nikaombe japo msaada wa safari.
Nilikuwa naomba msaada kwa mtu yeyote aliyembele yangu huku nikimwambia kuwa nimetelekezwa na mume na kuachiwa mtoto mchanga yule niliyembeba.
Wengi walinionea huruma na kunipa pole za mdomo tu, ndipo nikakutana na huyu mzee mmoja hivi aliyejitambulisha kwangu kwa jina moja la Patrick.
Nikamuelezea tatizo langu, akanihurumia sana, akaniambia nisijari atanisaidia nifike niendako kwakuwa nilimwambia nataka kurudi kwetu Mwanza kutokana na kutelekezwa huko na mume.
Mzee huyo aliniambia kuwa kesho yake mapema yeye na familia yake wanasafiri wanaenda Sindida kwa usafiri binafsi kwahiyo nitasafiri nao kisha atanisafirisha kwenda Mwanza.
Akanipakia kwenye gari yake na kwenda nae kwake maeneo ya kimara.
Usiku kucha sikulala maana mtoto alikuwa ananisumbua sana, muda mwingi nilikuwa nambembeleza kwa kuhofia kuwakera walioko mule ndani ya ile nyumba.
Alfajiri na mapema safari ikaanza, na tulifika Singida usiku kutokana na ubovu wa barabara kipindi hiko.
Yule mzee alinitafutia nyumba ya kulala wageni na nikalala humo na mwanangu kwani yule mtoto alishakuwa mwanangu kwasasa, sikutaka kumpoteza kabisa, sikutaka atoke mikononi mwangu na kama kufa basi nilikuwa tayari afie mikononi mwangu ila namshukuru Mungu, yule mtoto alikuwa ni mkakamavu licha ya misukosuko ila bado alihimili vishindo vya dunia.
Asubuhi na mapema, yule mzee alikuja kunifata na kwenda kunipakia magari yaendayo Mwanza, kisha akanipa pesa kiasi ya kunisaidia nilimshukuru sana kwani si rahisi mtu kukusaidia hivyo wakati hakufahamu.
Safari ya kwenda Mwanza ikaanza, mawazo yangu ni vile ambavyo shangazi atanipokea, sikujua atanichukulia kwa njia gani ila nilienda tu.
Tuliingia Mwanza kwenye mida ya saa moja usiku napo ni kutokana na barabara mbona na kuharibika haribika kwa gari nililopanda na mvua iliyonyesha siku hiyo.
Nilienda moja kwa moja hadi nyumbani kwa shangazi, nikiwa mlangoni kabla sijaingia ndani nilimsikia shangazi akizungumza.
"watoto wa kuokota sio watoto kabisa, mtoto akishatupwa na wazazi wake ujue ana laana hafai kabisa. Kwakweli mimi mtu yeyote akileta mtoto wa kuokota humu ndani, nitaenda kumtupa jamani. Sitaki kabisa watoto wa kuokota"
Kwanza kabisa nilishtuka na kujiuliza shangazi amejuaje, ila sikuelewa mazungumzo yao yalihusu nini hadi shangazi kusema vile ila nikajipa moyo na kusema kuwa lazima niendelee na ileile stori ya kutelekezwa ili shangazi amuhurumie mwanangu.
Nikaingia ndani, wote wakashangaa kuniona kwani hakuna aliyetarajia kuniona kwa wakati ule.
Shangazi akauliza kwa hamaki,
"mbona gafla jamani!! Kwema huko kweli?"
Nilikuwa nalia tu, nikamwambia shangazi kuwa Jumanne kanifukuza na kunitelekeza na mtoto yule, nilijua shangazi atanielewa ila shangazi hakunielewa na hakutaka kunielewa kabisa.
"Kwa mila za kwetu, kijana anapochoka kuishi na binti inabidi aje yeye mwenyewe kukukabidhi kwetu. Kingine nimekuozesha bila mtoto halafu wewe unanirudia na mtoto kwa misingi ipi?? Haiwezekani kabisa na siwezi kukupokea, bora hata ungekuwa peke yako ila na mtoto hapana. Itabidi tu urudi kwa mumeo, leo utalala hapa ila kesho sitaki kukuona. Rudi tu kwa mumeo."
Nililia sana, nilimkumbuka baba na mama. Kweli mzazi ni mzazi, sidhani kama wazazi wangu wangekataa kunipokea kiasi kile.
Sikuwa na raha kabisa, niliwaza tu niende wapi na yule mtoto.
Wazo likanijia kuwa niende Arusha kwa bamdogo, nikamuombe msamaha labda atanipokea.
Kesho yake, nikaondoka nyumbani kwa shangazi walijua narudi Dar ila nilienda Arusha kwa bamdogo.
Mwili wangu ulikuwa unanuka sana, sikuwahi kuoga tena toka nitoke Dar kwa kuhofia kumuacha mtoto chini na kupatwa matatizo.
Kufika Arusha nyumbani kwa bamdogo, huko ndio ilikuwa balaa zaidi. Bamdogo hakutaka hata kuniona, akanifukuza kama mbwa huku akisema nitakula jeuri yangu. Bamdogo aliongea mengi sana kuwa alinikataza kuolewa na Jumanne ila kiburi changu kimeniponza.
Nilikaa nje ya nyumba ya bamdogo, chini ya ule mti ambao Jumanne alisimama kwa mara ya kwanza aliponifata Arusha kwa bamdogo.
Nilikumbuka mengi sana na kulia sana, nilijiuliza maswali mengi kuwa upendo ule wa Jumanne alionipenda Mwanzo uko wapi, maana aliniacha kabisa, hakunitaka tena wala kunitamani. Nililia sana wala sikufikiria kama Jumanne aliyenipenda kiasi kile angenitenda vile.
Mara akaja mtu na kunishika bega, kumuangalia alikuwa ni Maiko.
Akanishika mkono, akanipakiza kwenye gari yake na kunipeleka nyumbani kwake.
Kufika kwake, akaniambia nisijari. Atanilea, atanitunza mimi na mwanangu nisiwe na shaka yoyote.
Nilifurahi sana kupata msaada ila sikujua kitu kimoja, kumbe Maiko alikuwa na mpango wake kabambe juu ya yule mtoto.
 
SEHEMU YA 86

Kumbe Maiko alikuwa na mipango yake iliyojificha juu ya mtoto.
Sikujua mipango yake mwanzoni, mi niliendelea kulea na kumuhudumia mwanangu.
Kuna kipindi Maiko alikuwa anasafiri safiri ila kitu kilichonishangaza nyumbani kwa Maiko kwani kuna chumba kimoja ambacho huwa anaingia na kutoka yeye mwenyewe.
Hakuna aliyeruhusiwa kuingia kwenye kile chumba zaidi ya yeye mwenyewe. Nilihisi labda hutunza baadhi ya mali zake humo ndomana hapendi watu waingie ingie.
Sikujua kazi rasmi ya Maiko, ila badae nikagundua kuwa anafanya kazi za magendo.
Maiko alikuwa akimtamani sana yule mtoto na kunitamkia wazi wazi kuwa anamtamani, sikujua anamtamani kwa lipi ila aliniambia.
"mtoto huyu asingekuwa shupavu ungesikia mengine hapa, ila nadhani atanifaa sana kwenye biashara zangu huyu"
Kumuelewa moja kwa moja ilikuwa ngumu kuwa alikuwa na mipango gani hadi kusema kuwa ningesikia mengine.
Mwanzoni nilipoamua kumuhoji kuwa anafanya kazi gani, aliniuliza.
"kwani hapa huli, hunywi, huvai?"
Nilibakia kumuangalia tu kwani alikuwa ni mtu wa ajabu kupita maelezo.
Huku nikijisemea kuwa naishi na mtu nisiyejua kazi yake, kumbe alikuwa anangoja mtoto akue kidogo ili mimi na mwanangu tuingie humo kwenye kazi yake hiyo haramu.
Mtoto alipofikisha mwaka mmoja, ndipo aliponiambia kuwa mimi nahitajika kusafiri ili kufata mzigo wa biashara, sikujua ni mzigo gani na sikuweza kukataa kwani niliishi kwake na kula kwake.
Nikamuomba niwe nasafiri na mtoto, mwanzoni alikataa ila badae akakubali.
Sikupenda kufanya safari ya mbali na kumuacha mwanangu nyuma, mwanangu niliyeamua kumpa jina la Patrick kutokana na mzee Patrick kunisaidia na kunifadhili. Nilipenda Patrick nae akiwa mkubwa awe na moyo wa kusaidia watu kama huyo mzee.
Nilianza kusafiri rasmi kwaajili ya biashara hiyo, kumbe biashara yenyewe ilikuwa ni ya madawa ya kulevya ambapo nilitakiwa kumeza, kisha nikirudi nayatoa kwa njia ya haja.
Nilikataa kazi hiyo ila Maiko akanitisha na kuniambia kuwa siwezi kukataa wakati washanifikisha eneo la tukio na sina pa kwenda kwani popote nitakapoenda atakuwa ananifatilia.
Nikakubali na kufanya hiyo kazi ya kubeba madawa tumboni mwangu.
Nikawa mtumwa wa Maiko tayari ukizingatia sina pa kwenda na mwanangu.
Kuna kipindi alikuwa anapenda kutembea sana na mtoto hadi nikapatwa na wasiwasi, kumbe alikuwa akifanya nae ile ile biashara, alimuweka madawa ya kulevya sehemu za siri kisha kuzunguka nae na kuyasambaza kwa wenzie.
Alikuwa anambebesha mzigo mkubwa sana, usipojua unaweza ukahisi kuwa labda mtoto amevishwa nepi ila haikuwa hivyo.
Maiko ni mwanaume katili sana, alikuwa anajua mtoto hana simile na kukojoa alichokuwa akikifanya ni kumfunga solotepu pale pa kutolea haja ndogo kisha kumbebesha madawa yake hayo.
Nilipomuhoji akanieleza ukweli, niliumia sana na kujaribu kumkataza ila hakutaka kunisikiliza.
Hii siri ya kumbebesha mtoto madawa ni mimi tu niliyekuwa naijua, moyo wangu uliumia sana kwa yale mateso ambayo Maiko alimpa mwanangu, yani mzigo wake ukitua tu basi mwanangu atakoma katika usambazaji.
Mtoto huyu sikumzaa ila aliniuma hakuna maelezo, nikamwambia na kumuomba Maiko aache kumtesa mwanangu ila napo alikataa.
Ikabidi nimuombe kuwa yale madawa anayombebesha mwanangu basi niwe nayabeba mimi mwenyewe na kuyasambaza, akaniambia kuwa mimi wanaweza wakanigundua, ikabidi tutafute njia mbadala.
Kwavile mwanangu alikuwa akimbebesha sehemu za siri basi nilimuomba mimi niyabebe kwenye matiti yangu, tukajaribu kufanya hivyo na kufanikiwa kuyasambaza kwani hakuna aliyejua kama kwenye matiti zangu zaidi ya sidiria kuna kingine nilikuwa nabeba.
Ila Maiko hakupenda mimi kumzuia mtoto kubeba yale madawa pia, ila nilimuomba tungoje akue.
Akasema wakati tukingoja akue itabidi mimi nibebe mzigo mkubwa zaidi tumboni wakati wa kusafirisha kwani mtoto nae angehusika ila kwavile nilimkatalia itabidi nibebe mimi mwenyewe.
Mzigo wa madawa niliokuwa naubeba ulikuwa mkubwa sana, haikuwezekana tena kutoa kwa njia ya haja bali walikuwa wakinifanyia operesheni ndogo kuyatoa.
Tumbo langu liliharibika sana kwa ile biashara, nilitamani kutoroka ila je nikitoroka nitaenda wapi? Sikuwa na pa kwenda ndio kitu pekee kilichonikalisha nyumbani kwa Maiko kwani nilijua kuwa shangazi hawezi kunikubali na mtoto hata iweje.
Niliendelea kupata mateso tu pale nyumbani kwa Maiko huku nikiyavumilia kwa kungoja mwanangu akue kidogo hata nitakapoamua kufanya nae maisha ya kuzurula mitaani iwe rahisi.
Ukiacha biashara ya madawa, Maiko alikuwa akifanya biashara nyingine ambayo kwa kipindi hiko sikuijua.
Mimi niliendelea tu kuwa kontena la madawa ya kulevya hata mwili nao ukawa umeshazoea ile hali.
Nilifanya ile biashara kwa muda mrefu sana.
Kuna kipindi Maiko alitoka kidogo na kusahau funguo wa kile chumba chake, nikaenda kufungua na kuangalia.
Nilichokiona kiliniumiza sana, viungo vya binadamu wakubwa kwa watoto, ngozi, sehemu za siri huku vichwa baadhi vya watu alikuwa ameviweka kwenye friji, niliogopa sana nilijiuliza huyu Maiko ni mtu wa aina gani.
Uchungu ulinishika pale nilipoona ngozi za watoto wadogo, moja kwa moja nilimuhusisha Maiko na kifo cha mwanangu, machozi yalinitoka sana ila bado sikupata tafsiri ya Maiko kuwa ni binadamu wa aina gani, kukaa na viungo vya watu ndani tena bila uoga wa aina yoyote ile.
Nilipotoka mule ndani akili yangu ilivurugika sana ila nikasema kuwa sitakubali hadi pale nitakapoondoka kwenye ile nyumba, nilitamani kulipa kisasi kwa Maiko ila sikujua nitaanzia wapi.
Maiko aliporudi alihisi kuwa kuna kitu nimegundua, nikakataa na kumwambia sijui chochote.
Akanipiga sana ili nimwambie ukweli, nimweleze kile nilichogundua kuhusu yeye ila bado nilikataa kwani nilijua kusema kwangu ukweli ndio kujiandalia kuuwawa na Maiko.
Baada ya kile kipigo nikaamua kubeba mwanangu na kutoroka ila Maiko alinitafuta hadi kunipata kisha mi na mwanangu akaturudisha nyumbani kwake.
Akanipiga tena sana zaidi ya pale mwanzo huku akinipa onyo kuwa nisithubutu kutoroka kwani nitakapofanya hivyo tena ataniua.
Mimi na mwanangu tukawa watumwa wa Maiko, alitutesa sana na kutuonea. Kosa dogo nilikuwa napewa kipigo cha haja huku akisema kuwa ananilipizia kwa kumkataa mwanzoni wakati ananitongoza.
Nakumbuka siku nyingine niliyojaribu kutoroka, Maiko aliponikamata akanifunga mikono na miguu kisa akachukua kisu na kukiweka kwenye moto, kikishika moto vya kutosha akawa ananibandika nacho mwilini, maumivu niliyokuwa nayapata kwakweli hayasimuliki.
Nilijuta kuzaliwa, nilijuta kumfahamu Maiko haswa nikikumbuka kifo cha mwanangu na yeye ndiye msababishaji kwani alikuwa anauza viungo vya binadamu.
Alimchukua Patrick mwanangu na kumfunga kwenye mti, kichwa chini miguu juu.
Mtoto alilia sana na mimi niliumia sana ila Maiko hakuwa mwanaume mwenye huruma hata kidogo, yeye ni ukatili tu na ukatili na yeye.
Baada ya adhabu hiyo, akanihakikishia wazi kuwa nikijaribu tena kutoroka basi kifo kinaniita tena akasema kuwa ataniua taratibu kwa kunichinja, ikabidi niwe mpole nifanye vile anavyotaka yeye.
Nilikuwa kama mke kwenye nyumba yenye mume gaidi, alinilazimisha kufanya kile anachotaka yeye hapakuwa na ladha ya mapenzi bali ni mateso tupu.
Kila alipotaka mapenzi ilikuwa ni lazima anipige kwanza, mwili wangu ulikuwa kama ngoma huku tumbo likiwa kontena la madawa ila nikajisemea kuwa yote mapito, niliamini ipo siku Mungu atasikia kilio changu na kunitoa kwenye mikono ya Maiko.
Nilifanya kila anachotaka kufanya, mengine hayaelezeki. Kwakweli Maiko alinitesa sana.
Ndipo safari hii niliondoka na huyo wa kuitwa Mashaka ili nikabebe mzigo mwingine, kufika huko nae akanibaki na kunifanya vibaya vibaya kisha kuniwekea ule mzigo nirudi nao Tanzania.
Nikiwa na mwanangu pembeni huku tumeongozana na mlinzi ambaye Maiko alitupa ili tusiweze kutoroka. Nilisema sasa inatosha.
Niliamua kufanya kitu kingine cha khatari katika maisha yangu.
 
SEHEMU YA 88

Kuna kitu ambacho nimekigundua na kitu hicho ndio kilichofanya niwaeleze kila kitu kuhusu maisha yangu.
Patrick amenisumbua kwa kipindi kirefu sana kutaka kumjua baba yake akadiriki kuniambia kuwa hata kama nilibakwa nimueleze ukweli ajue kwani yeye ni kijana mkubwa sasa.
Hakujua ni ugumu gani naupata katika kumueleza ukweli.
Nakumbuka swala la Patrick kutaka kumjua baba yake lilianza baada ya kifo cha shemeji yangu yani mume wa Marium aliyeuwawa gafla kabisa na tukamzika kiwiliwili bila kichwa, nilishangaa sana siku ambayo Maiko amefika hapa kisha dadangu akamvamia, kumbe Maiko ndiye aliyemuua shemeji. Bado sijajua huyu Maiko alikuwa na maana gani kufanya kama alivyofanya.
Ingawa Patrick nilimsomesha kwa shida ila sikumnyima uhuru, nilimruhusu kufanya chochote kinachopendeza machoni mwa watu na kumpendeza Mungu.
Mwanangu alitamani sana kuanza kazi, alishachoka kukaa nyumbani na mimi ukizingatia nilikuwa simjibu swali la alipo baba yake.
Ningemjibu vipi wakati hata mama yake simjui? Ningemwambia vipi vitu vya kuumiza kiasi hiki?
Nilimvumilia sana licha ya maneno makali aliyoongea kwangu kuhusu baba yake, kweli kuna umuhimu kwa mtoto kuwajua wazazi wake, je ningemueleza kuwa hata mimi si mama yake mzazi angejisikiaje? Kwakweli nimevumilia sana, Patrick alikuwa ni msumbufu sana katika kumjua baba yake.
Patrick alipopata kazi Arusha kwanza kabisa nilimkatalia asiende kwa kuhofia kuwa angekutana na Maiko kwani Maiko ni mtu mbaya sana na niliogopa kuwa atamfundisha tabia mbaya mwanangu ila Patrick aling'ang'ania sana kuwa lazima aende kwani kazi ndio hitaji lake kwasasa.
Nilitamani mwanangu apate kazi sehemu nyingine tu ila si Arusha.
Kitu kikubwa nilichomsisitizia Patrick ni kuwa asioe bila kuja kunitambulisha huyo mwanamke kwanza, nilihofia vitu vikubwa viwili yani kukutana na familia ya Jumanne na pia kukutana na familia ya Maiko.
Sikutaka kabisa Patrick kujihusisha na familia hizi mbili kwamaana kwa upande wangu sikuhisi kama angejenga familia njema na hizi familia mbili. Ingawa si vizuri kumchagulia mtoto mchumba ila kwa Patrick kutokana na historia za nyuma nilipenda kama ataamua kuoa basi huyo mwanamke atokee Mwanza au atoke kwenye familia tutakayotambulishana kwanza.
Patrick akiwa Arusha, mwanzoni alikuwa akiwasiliana sana na mimi tena sana hadi mara nyingine niliweza kugundua kuwa kuna kitu anatamani kuniambia ila anashindwa ila mawasiliano hayakukatika mpaka siku aliyorudi tena Mwanza na gari yake mwenyewe kunisalimia.
Aliporudi tena Arusha mambo yalibadirika sana, mawasiliano yangu na Patrick yalikuwa hafifu mno.
Haikuwa kama ilivyokuwa mwanzo, kuna kitu nilikihisi kama mama. Patrick hakuwa mwanangu wa kumzaa ila kuna kitu kikubwa sana ambacho kimeniunganisha na Patrick, siku zote sikuacha kumpenda Patrick kama mwanangu naye hakuacha kunipenda kama mama yake.
Hali ile ya mawasiliano hafifu kati yetu iliniumiza sana, mara ukimpigia hapatikani mara sijui nini nilijikuta nikiwa na mawazo tu juu ya mwanangu kipindi hicho.
Siku nilipokuta kuwa kuna namba ngeni imenipigia ila sikupokea kwakuwa nilikuwa nje nikifanya usafi, nilichukua simu na kupiga akapokea mtoto wa kike huku akilia kuwa yeye ni mke wa Patrick.
Nilipata mpasuko mkubwa sana moyoni, yani Patrick anaoa bila hata ya kunishirikisha? Anaoa kimya kimya kama vile nimemkosea kitu gani?
Ni kipindi hicho nilichomsisitiza Patrick amlete huyo mwanamke hapa nyumbani kwangu.
Siku waliyokuja sijui hata walipatwa na majanga gani huko ila nilishtuka sana kumuona huyo binti, machozi yalinitiririka.
Jamani Tusa amefanana sana na mtoto wangu Jasmine yani wamefanana, sura ya Jasmine ilikuwa hivyo hivyo kama sura ya Tusa, utafikiri Jasmine wangu amekua. Nilitoa machozi sana kumuona kumbe binti mwenyewe alifika na matatizo yake tayari. Alishaharibiwa haribiwa kila kitu na mwanangu Patrick, ila Tusa mwenyewe alikuwa akilia tu huku akihofia kusema ukweli.
Nilimsisitiza Tusa kuwajua wazazi wake kwani nilihisi lazima kuna mahusiano ya karibu kati ya Tusa na mwanangu Jasmine, na wala sikukosea.
Alipofika Pamela na kusema kuwa yeye ni mama yake Tusa, moja kwa moja nikajua baba wa Tusa lazima atakuwa Jumanne.
Katika kumuuliza Pamela ni kweli alikuwa Jumanne ila alibadili jina na kujiita Adamu, sawa sawa ni Adamu kweli sijui alibadili kwa misingi ipi labda hakutaka kukumbuka yaliyopita.
Tangu familia ya Tusa imefika hapa mambo yamekuwa shaghala bhaghala mala limetokea hili mara lile yani mambo hayaeleweki kabisa hadi pale nagundua kuwa Jumanne na Maiko ni mapacha mmh kweli kuna siri nzito hujificha kati ya mtu na mtu.
Pamela alinieleza kitu kilichonishtua sana na pale Fausta naye alivyonieleza nimegundua kuwa wazazi wa Patrick wanatokea humohumo kwenye familia ya Tusa.
Haya sasa Pamela na Fausta kazi kwenu kutambua kati yenu ni nani mama mzazi wa Patrick? Na nyie ndio mtamwambia Patrick je baba yake ni Adamu au Maiko au kuna mwingine. Mimi sina la ziada yangu ni hayo tu. Nadhani sasa nitakuwa huru na mawazo hata kama nikifa nitakufa kwa amani"
Wote walikuwa wakilia na kuomboleza, Patrick alizidi kumkumbatia mama yake huku akisema,
"mama, simtaki mama mwingine nakutaka wewe tu. Wewe ndiye mama yangu mzazi, simtaki mwingine mama"
Patrick alikuwa akitokwa na machozi tu, huku Pamela na Fausta nao wakilia tu kwa yaliyopita na kujilaumu sana.
Adamu nae alipatwa na mshituko usio na maelezo kwani nae alihusika humohumo, si Tusa wala Tina walioacha kulia. Tusa alilia sana kwani kwa vyovyote vile ametembea na kaka yake iwe ni mtoto wa Pamela au Fausta.
Wote walilia mule ndani kama vile kulikuwa na msiba.
Bi.Rehema ndio hakuwa na hali kabisa, alihisi kama vile dunia ikimzomea na kumng'ong'a.
Maiko naye na mfuko wake pale nje alipatwa na mshangao mkubwa sana kusikia kuwa Patrick ni mtoto anayewahusu katika familia yao.
Aliinuka na mfuko wake ili kujumuika na wote wa ndani. Hakujali chochote kwani mengi yalishaharibika.
 
SEHEMU YA 89

Hakujali chochote kwani mengi yalishaharibika.
Maiko hakutaka kuendelea kusubiri pale nje, alitaka aingie ndani ili wawezo kumuona. Kuku akijisemea:
"Liwalo na liwe"
Hakutaka hata kujua Patrick ni mtoto wa nani kwani alihisi kwa vyovyote vile Patrick anaweza kuwa mtoto wake au wa Adamu.
Maombolezo yaliendelea mule ndani kwani wengi walijihisi kama vile wanaota au wameamka toka usingizini.
Tusa na Tina nao waliwasogelea mama zao.
TUSA: Mama tafadhari, Patrick si kaka yangu jamani.
Pamela alizidi kulia kwani maelezo hakuwa nayo ya kutosha.
Bi.Rehema akadakia kusema,
"Jamani, tuambieni basi huyo Patrick ni mtoto wa nani na kwanini mlimtupa ili tuweze kuokoa jahazi hili."
Mara Maiko akaingia ndani na mfuko wake na kuwafanya wote washtuko kwani matendo ya ajabu waliyoelezwa juu ya Maiko walihofia na wao kudhuruka.
Maiko alisimama katikati yao huku akizungumza.
MAIKO: Jamani, mazungumzo yote nimeyasikia. Deborah amewaeleza matukio ya ukweli tena ukweli mtupu, hakuna alichowaongopea. Mimi kweli ni mwanaume wa ajabu nisiyefaa katika jamii inayonizunguka"
Wote wakashtuka na kumuangalia tu kwani ilikuwa ni vitu vya kushangaza na ajabu.
Tulo alibanwa sana kule kwenye kituo cha polisi ila aligoma kusema.
Badae ikabidi Mwita aende kuzungumza nae tena.
MWITA: Tulo, ukweli humuweka mtu huru. Ni bora useme ukweli tu.
TULO: Ukweli humuweka mtu huru?? Hujielewi wewe, kuna ukweli wa kumuweka mtu huru ila ukweli mwingine unafanya ufungwe maisha. Siko tayari kufungwa, siko tayari kuozea jela.
MWITA: Sina nia mbaya Tulo, ninachotaka ni wewe kubadilika.
TULO: Unahitaji mimi kubadilika? Kabla hujanibadili mimi unatakiwa ukawabadili ndugu zako kwanza.
MWITA: Kivipi? Mbona sikuelewi?
TULO: Mimi ni rafiki tu ila kumbuka kuwa mapinduzi huanza ndani kwanza. Mimi Tulo kuna kazi naifanya inayoniingizia pesa na kunifanya nionekane tayari. Ila kazi yangu mimi sio kubwa sana kama ya baba yako Maiko, tena pia kuna ndugu yako Patrick. Nenda ukaanze na hawa kwanza kisha ndio urudi kwangu.
Mwita alimshangaa sana Tulo, kwani alikuwa tayari hata kufa kwaajili ya kuficha ukweli halisi.
Mwita akaona itakuwa vyema kama akimtafuta baba yake bwana Maiko na nduguye Patrick kuwahoji kidogo na kama akishindwa basi atumie nguvu ya dola.
Mwita aliondoka pale polisi na kuanza kuelekea kwakina Patrick kwanza kwani Maiko hakuwa na mahali pa kusema kuwa utamkuta moja kwa moja ndiomana Mwita alienda moja kwa moja kwakina Patrick.
Alipofika akasikia kuna mtu akizungumza ndani huku wengine wakisikika na vilio vya chini kwa chini.
Mwita akategesha masikio yake kujua kuna nini ila matone ya damu yalimshangaza sana pale nje na akajua tu kuwa mule ndani kuna matukio yasiyo ya kawaida, akategesha sikio dirishani ili kujua kinachoongelewa.
Maiko aliendelea kuongea bila ya kuogopa kitu chochote na bila kujali kama anawatisha watu waliopo mule ndani.
"Jamani, sijapenda kuwa kama hivi nilivyokuwa leo. Roho inaniuma sana, nimepoteza maisha ya watu wengi mno. Kinachoniuma zaidi ni kifo cha baba yangu, roho imeniuma sana kwa kummaliza baba yangu kisha viungo vyake kuvipatia kwa pesa nyingi za kutosha.
Sikuwahi kumuona wala kumjua baba yangu, nilikuwa natoa oda tu. Kwa mama naye nilishapotezwa, sikuweza tena kukutana na mama yangu ila laiti kama ningekutana na mama kama Deborah nina hakika ningekuwa na chembe kidogo ya huruma.
Jinsi Patrick alivyompa shida Deborah wakati mdogo sikufikiria kabisa kama Patrick si mtoto mzazi wa Deborah.
Mateso mengi ambayo Deborah ameyapata ni sababu ya Patrick, roho imeniuma sana kuona kumbe Patrick ni sehemu ya familia yangu.
Nilichukizwa sana kumuona Deborah ana mtoto tena mtoto mwenyewe ni kutoka kwa mwanaume aliyeng'ang'ania kuolewa naye na kuniacha mimi.
Nilikuwa namfanyia mambo mengi ya ajabu ili kumfanya Deborah ajutie kitendo cha kuolewa na mume mwingine na pia ajutie kutelekezwa na mtoto ambaye alikuwa hataki kumuweka chini.
Nakiri wazi kumuua mume wa huyo dada (akionyesha kidole kwa Marium ambaye alikuwa ameangalia chini tu akikumbuka mumewe alivyouwawa kwani kila amuonapo Maiko hukumbuka kifo cha mumewe.)
Nikweli nilimchinja, ila sababu kubwa ni kuwa nilimuona na Deborah kipindi hiko nikimsaka Deborah kwa lengo la kurudisha alivyovichukua kwangu, kweli nimeamini pesa haina mwisho.
Mimi nina pesa nyingi sana, kwa pesa aliyochukua Deborah wala sio ya kuniathiri ila nilimsaka kwa kila njia aweze kunilipa mali zangu.
Ndipo siku hiyo nilipomuona ameongozana na huyo mwanaume na kwa vyovyote vile nilijua kuwa lazima yule atakuwa mwanaume wake na nikapanga kumkomesha.
Nikaanza kumfatilia yule mwanaume, siku niliyomkuta alikuwa nje nikamfata na kumuuliza mahusiano yake na Deborah akanijibu kuwa ni shemeji yake nikahisi ananificha tu. Nikamuuliza alipo Deborah akagoma kusema, nikamvizia anapoelekea.
Aliingia kwenye chumba, nami nikaingia kwa njia za panya hakuona kama nimeingia.
Nikamuona amekaa na yule dada (akimuonyesha tena Marium) ila sikufikiria kama ni mumewe kwani walikuwa wamekaa mbali mbali, nikajitokeza mule ndani, nikambamiza na gongo nililobeba yule mwanaume akaanguka chini, mwanamke akataka kupiga kelele na kukimbia, nikamuwahi kwa kumpiga na gongo nae akazimia kisha nikachukua kisu changu na kumchinja na kuondoka na kichwa chake.
Kwakweli nilifanya tukio la ajabu sana kwa yule baba, kichwa chake nikakitunza na ninacho hadi leo nyumbani mwangu nilitaka siku Deborah akija kwangu aje kukishuhudia.
Kijana yule pale aitwaye Yuda nae pia alikuwa mfanyakazi wangu (wote wakashangaa kusikia kuwa Yuda nae yu chini ya Maiko.)
Niligombana nae baada ya kuona kile kichwa ndani kwangu kumbe alikuwa ni baba yake. Nisamehe sana Yuda ila ndio ishatokea tayari.
Tukiacha yote hayo niliyofanya kwa hiyari yangu ila mengi nilishinikizwa na mtu mmoja aitwae Mashaka.
Mashaka ni mtu mbaya sana, alinijengea kuwa na roho mbaya kupita maelezo na nimefanya mengi mabaya kwa ajili yake, yeye ndiye alikuwa shinikizo kubwa kwangu.
Najua mimi hamnielewi kama mlivyomuelewa Deborah wakati anawaelezea, mimi nishachanganyikiwa kwa mengi mabaya niliyofanya. Sina amani tena moyoni mwangu.
Kisasi changu kimemrudia Mashaka, ngoja niwaambie nilichomfanya Mashaka. Kabla ya yote, ngoja niwaonyeshe hivi vitu."
Maiko aliingiza mkono kwenye mfuko wake wa suruali kisha akatoa barua na kuiweka mezani kisha akasema,
"Hakikisheni mnaisoma hiyo barua"
Kisha akainua ule mfuko wake, akaingiza mkono na kutoa kitu.
Kilikuwa ni kichwa cha Mashaka, Maiko alikuwa amemuua Mashaka.
Kila mmoja alianza kupiga kelele mule ndani na kuogopa.
 
Back
Top Bottom