Riwaya: SIN

Riwaya: SIN

mkuu story nyingi mbona zimeisha labda haujafuatilia ila story nyingi zimeisha ni arosto yako tu ya kutamani kusoma full kwa siku moja wapo watu humu nikiwemo mmoja wapo tumesoma story moja almost for 2 years na kumbe kulikuwa na possibility ya kuxoma yote kwa wiki kikubwa uvumilivu wak
Mipu.mbavu tu, kwanza mtu kajitolea ye kalipia huko lakini bado wanataka kumpangia cha kufanya..
 
Naona kazi ya kujitolea inasababiswhwa navunjiwa heshima humu ndani nimeishia hapa kwa yoyote anayetaka story atawasiliana na mwandishi maana mimi sio mtunzi wa hiyo story
Tunaomba msamaha mkuu kwa niaba ya hao wachache walokukosea, naomba utuletee mwendelezo plz..🙏🏼
 
mkuu story nyingi mbona zimeisha labda haujafuatilia ila story nyingi zimeisha ni arosto yako tu ya kutamani kusoma full kwa siku moja wapo watu humu nikiwemo mmoja wapo tumesoma story moja almost for 2 years na kumbe kulikuwa na possibility ya kuxoma yote kwa wiki kikubwa uvumilivu wak
Ina mana gan story ambayo hadi unasahau ilishia wap msieendekeze ujinga
Mipu.mbavu tu, kwanza mtu kajitolea ye kalipia huko lakini bado wanataka kumpangia cha kufanya..
Mipu.mbavu tu, kwanza mtu kajitolea ye kalipia huko lakini bado wanataka kumpangia cha kufanya..
Pumbavu aliyekuzaa shenzi ww kala hasara kwa kupata toto senge la mawazo embu onyesha ni mahali gani huyo anaeleta story kadhihakiwa ama kavunjiwa heshima kwa namna yoyote? Kajibiwa baada ya kusema kama mtu anataka mfululizo anaweza akatoa 5000 kwa mwandishi na atapewa stori yote, ndipo che mittoga alipouliza akituma mmoja itatumwa humu au kila mtu atoe hyo pesa? Hapo ndipo kudhalilishwa au kuvunjiwa heshima? Afuu we kima unakulupuka na kuita watu wapumbavu!! Acha uchoko wa mawazo finyu kaza fuvu hilo unefeli darasan hata fikra nazo za kuchanganua jambo unashindwa? Ulimuharibu mama yako bole njia yake na kumpa maumivu ya kutoa kiumbe dhaifu wa fikra!!
 
Naona kazi ya kujitolea inasababiswhwa navunjiwa heshima humu ndani nimeishia hapa kwa yoyote anayetaka story atawasiliana na mwandishi maana mimi sio mtunzi wa hiyo story
Ndugu ulipaswa kujibu tu kama akitoa mtu itashushwa yote humu au private kuliko kuomba huruma za watu humu kisa hadithi tusipende kujiona muhim kwa vitu ambavyo havina faida sana zaidi ya kutufanya tusahau ugumu wa changamoto za hapa na pale tu
 
Huwa sina muda wa kuargue na wapumuliwa visogoni, jitu huja unachokijua then unajitia ujuaji, kwani hujaona namba ya mwandishi? unashida nayo yote mtafute ulipie utumiwe kwa WhatsApp, swala la wewe kulipia itumwe humu na unajiona uko vizuri upstairs unaona inamake sense? kwanza kule kunamakubaliano ya kutokusambaza kazi baada ya kutumiwa, humu jamaa kafanya kujitolea tu kwa wasoweza kulipia, kuwa na akili.
 
Wakuu kwanza samahani kwa yaliyotokea kwa vile nilihidi kumaliza story ntaimaliza kwa ambao hawana muda wa kuisubiri wanaweza wasliana na muandishi tu. Tutarudi kwa utaratibu wetu kama kawaida. Siwezi leta watu wawili wakaharibia wengine.
 
Yeye anaeleta humu anacho kibali? Bao la baba yako bora angelimwaga njee tu na mama yako akatulia chali na kifo cha mende ukatoka kituko cha ulimwengu yaan macho na jasho la meno linakutoka kisa stori tu haya namba hyo umeona vipi umeshindwa kulipia mpaka unatafuta huruma ya kuletewa humu?senge ww
 
Wakuu kwanza samahani kwa yaliyotokea kwa vile nilihidi kumaliza story ntaimaliza kwa ambao hawana muda wa kuisubiri wanaweza wasliana na muandishi tu. Tutarudi kwa utaratibu wetu kama kawaida. Siwezi leta watu wawili wakaharibia wengine.
Hapo umeonesha ungwana kaka pia kwenye wengi kuna challenge zinatokeaga inabid ukubali ila niwie radhi kama kuna sehem unahisi nimekukwaza kwa namna moja ama nyingine.
 
SIN 86

Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)

Age ……………………………………………………18+

Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA

“U…u..me…kuj…a saa ngapi?”
“Dakika kumi zilizo pita. Ramani hiyo hapo mezani, pia nina masharti mapya”
“Mashrti gani tena?”
“Nimekuondolea kigezo cha kutembea na wasichana ambao ni bikra”
“Kweli?”
“Ndio, ila kigezo hicho kita ondoka mara baada ya kutembea na wasichana Bikra tisini na tisha kisha huyo wa mia moja ndio ata kuwa mke wako wa ndoa. Endapo uta shindwa kufanya hivyo au ukienenda kinyume na hivyo basi uta kufa. Nina imani ume nielewa?”
Evans akatingisha kichwa akimaanisha kwamba ame muelewa jini huyo ila kwa kweli hayo mashari aliyo pewa ni magumu sana kwa maana kwa upeo wake wa kawaida tu hawezi kufahamu mwanamke bikra ni yupi na yupi sio bikra.

ENDELEA

“Siku njema”

Jini huyo alizungumza na kupotea ndani ya chumba hicho. Evans akashusha pumzi huku akiwa amejawa na woga. Japo ana jaribu kuizoea hali hiyo ila kusema kweli, bado ina mtatiza. Evans akashuka kitandani na kufungua karatasi hizo zilizo chorwa michoro mikubwa ya kanisa ambalo ana hitaji kujengewa. Simu yake ikaanza kuita, akaitazama vizuri na kukuta ni namba ya daliali aliye wasiliana naye. Akaipokea simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.

“Umeamkaje Boss?”
“Salama tu habari ya wewe”
“Namshukuru Mungu. Sasa niambie upo wapi ili niweze kukupitia Boss wangu”
“Ahaa nipo hoteli ya KX Royol”
“Sawa nina fika hapo baada ya dakika kama ishirini”
“Nashukuru”
Evans akakata simu na kujilaza kitandani kidogo huku akijaribu kutafakari ni hatua gani ambazo ana weza kuzitumia kuhakikisha ana toa tenda katika kampuni ambayo ina weza kutengeneza kanisa hili katika ubora ulio mzuri. Evans akazikunja karatasi hizo na kuingia bafuni, akaoga haraka haraka kisha akajiandaa. Hazikupita hata dakika mbili simu yake ikaanza kuita.

“Ndio”
“Boss nimesha fika hapa chini”
“Sawa nina taoka sasa hivi”
Evans akatoka ndani hapo huku pesa zake zikiwa vizuri kwenye mfuko wa suruali. Akakabidhi funguo mapokezi wakasalimiana na dalali huyo na kuianza safari.

“Hivi huku Kigamboni maeneo ni mengi ehee?”
“Ndio yapo makubwa. Jambo la msingi ni pesa kaka”
“Okay kama pesa haisumbui kabisa”
Wakafika katika eneo kubwa la wazi ambalo lime kaa tambarere.
“Hili eneo ni kiasi gani”
“Eneo hili lote?”
“Ndio”
“Hili eneo kaka ni milioni mia mbili na hamsini?”
“Lote?”
“Ndio”
“Lina mmiliki mmoja au kuna wamiliki tofauti tofauti?”
“Hili eneo mmiliki ni mmoja kwa maana lipo chini ya serikali”
“Sawa basi nita hitaji kukamilisha taratibu za kulichukua”
Dalali huyo akamtazama Evans kwa maana muonekano wake hauendani kabisa na jinsi ya garama hizo anazo zisema ana zihimili.

“Hivi wewe una itwa nani kaka?”
“Evans”
“Evans nani?”
“Evans Shika”
‘Mmmm wasije wakawa ni baba na mwana wakanipotezea muda wangu hawa’

Daliali alizungumza kimoyo moyo huku akikumbuka sakata la tajiri mmoja nunua nyumba za zaidi ya bilioni tatu katika mnada huku mfukoni akiwa hana kitu kabisa.

“Sawa kaka, sasa ni lini una hitaji twende wilayani ili kupata hili eneo?”
“Hata leo”
“Leo hii hii?”
“Ndio”
“Sawa kaka hakuna shida”
Wakaingia kwenye gari na kuelekea katika ofisi za wilaya huku dalali akiendelea kuwa na mashaka mengi sana kwa Evans kwa maana haamini kama ana uwezo wa kununua eneo hilo ambalo ni matajiri wengi wamelitamani ila kutokana na kukosa pesa hizo wameshindwa kulinunua kabisa.

“Kaka pale una hitaji kujenga kiwanda nini?”
“Hapana ndugu”
“Una hitaji kujenga nini?”
“Kanisa!!?”
Dalali alishangaa huku macho yakimtoka.

“Ndio, mbona una shangaa”
“Kanisa eneo kubwa kama lile?”
“Ndio, nina taka kujenga kanisa ambalo kwa duniani litakuwa ni la pila au la tatu kwa ukubwa”
“Mmmm wewe ni mchungaji?”
“Mmmm ni nabii tu wa Mungu”
“Nabii!!?”
“Ndio”
“Ila mbona una onekana kijana mdogo sana. Una jua nime shazoea kuwaona wachungaji wakiwa na umri mkubwa mkubwa kama kina nabii Sanga na wengine”
“Ndio hivyo Mungu ame amua kuni fungulia na nita fungua kanisa ambalo maelefu ya watakuja kutoka duniani kote kuhakikisha kwamba wana sali pale”
“Sawa kaka, ila nisiwe mnafki, je una pesa ya kununua lile eneo au kuna kaujanja ujanja una taka kukafanya?”
“Pesa ipo mbona una mashaka, au ulihitaji nivae suti kali au niongee kibosi bosi ndio uamini kama nina pesa?”
“Hapana kwa maana nina mashaka sana juu ya jambo hili?”
“Una jua Watanzania wana amani kwamba mtu mwenye pesa ni yule mwenye kuvaa vizuri kuendesha gari zuri. Ngoja nikuambie siri moja, uta kuta mtu huo ana madeni chungu nzima au wengine magari ni ya mikopo, ila akionekana hivi una jua kabisa ana pesa. Ila wewe nenda usukumani huko au kwa wamasai. Utakuta mtu kavaa shuka lake, chini kapiga mabuti au sendeu. Ila cheki pesa yake aliyo kuwa nayo. Hivyo ina bidi ulitambua hilo”
Evans alizungumza kwa msisitizo ili kumtoa mashaka dalali huyo.

“Sawa kaka nime kuelewa”
Dalali huyo ili mbidi kuwa mpole kwa maana somo alilo pewa lime muingia kisawa sawa kichwani mwake. Wakafika katika ofisi za mkuu wa wilaya. Wakaonana na mkuu wa wiliya na wataalamu wa ardhi, wakakubaliana juu ya ununuzi wa eneo hilo.
“Kesho pesa zote nita zilipa”
“Sawa bwana Evans tuna kukaribisha sana”
“Nashukuru, ila nina omba namba ya benki”
Evans akakabidhiwa namba ya akaunti ya benki kisha wakaondoka ofisini hapo na dalali. Wakarudi hotelini na Evans akamlipa laki tatu dalali huyo ikiwa ni malipo ya mizunguko ya siku nzima, wakaagana kwa miadi ya kuonana naye kesho pale tu atakapo kuwa ame maliza kufanya malipo ya kiwanja hicho kwa njia ya benki.

***

“Mke wangu jana uliniambia kwamba una mpango. Hembu niambie ni mipango gani?”
Tomas alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Levina huku wakiendelea kupata kifungua kinywa.

“Pombe zime isha kichwani?”
“Ndio”
“Tomas nina imani hii sio mara ya kwanza kukueleza kwamba huwa sipendi mwanaume mlevi si ndio?”
“Nalijua hilo, ila si yalisha isha toka jana usiku?”
“Ndio ila nili hitaji nikueleze akili yako ikiwa ni nzima kama hivi”
“Sawa nime kuelewa mpenzi wangu, sinto rudia hili jambo”
“Poa. Mpango wako ulio kuwa ume upanga ni kumteka mtoto wa nabii Sanga si ndio?”
“Ndio”
“Jambo ambalo nilikuwa nime lifikiria ni kulipua gari la nabii Sanga ambalo siku ya harusi ata panda yeye na mke wake”
“Uta taka tuwaue haraka kiasi hicho?”
“Ndio, kifo hicho hakito hakito kuhusisha moja kwa moja, pili wata fanya uchunguzi ambao hauto kubaini kama wewe ndio ume husika. Kitu ninacho kichukia kwenye maisha yangu ni kuanza kutafutwa na polisi. Huwa sipendi kabisa kuingia katika kashfa kama hiyo na pia sinti penda nihusishwe kabisa katika mpango wako huo”
Levina alizungumza kwa msisitizo na kumfanya Tomas kushasha pumzi taratibu.

“Sasa hilo bomu tuta litega wapi ikiwa una ulinzi mkubwa?”
“Hilo ndio jambo la pekee la kulitafakari. Nipe siku ya leo niweze kugundua ni bomu la ina gani ambalo nita litengeneza kuhakikisha kwamba lina ingia ndani ya gari hilo”
“Sawa mke wangu nashukuru sana kwa kuwa nami katika huu mpango”
Levina akamtazama tu Tomas, kisha akanawa mikono yake na kusimama.

“Muda wa kazini ume fika. Una ratiba ya kwenda wapi?”
“Sina mke wangu”
“Hakikisha ukitaka kutoka una niambia”
“Sawa”
“Ila tafadhali nina kuomba usifanye kituko kama ulicho kifanya jana usiku”
“Usijali mke wangu, sinto rudia tena”
Levina akambusu Tomas mdomoni mwake kisha akaondoka eneo hilo. Tomas akaanza kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii, akastuka sana kumuona Magreth akitangazwa kama msichana mdogo ambaye ana weza kuja kuwa tajiri mkubwa afrika nzima.

“Huyu mshenzi huyu mshenzi bado ana mapenzi na huyu mzee?”

Tomas alizungumza huku akiendelea kitazama picha za Magreth akikabidhiwa tuzo na muwakilishi wa jarida kubwa duniani la linalo fwatilia wafanya biashara Forbes.

“Ina bidi nikutane naye”
Tomas alizungumza huku akielekea chumbani, akajiandaa haraka haraka na kumpigia simu Levina na kumpa taarifa ya kwenda kwenye mgajawa wa Magreth.

“Ni nini kina kupeleka huko”
“Nitakuambia mke wangu”
“Kuwa makini nini nina imani kwamba hakuna jambo la ajabu utakalo lifanya”
“Niamini mke wangu, nina jielewa na hakuna haja ya wewe kuni sisitizia kiasi hicho”
“Haya baadae nina wateja hapa”
“Poa”

Tomas akakata simu na kuingia kwenye gari na kuianza safari ya kuelekea ulipo mgahawa wa Magreth.

***

“Hongera sana bosi”
Kila mmfanyakazi wa Magreth hakusita kutoa pongezi zake kwa Magreth ambaye ame pokea tunzo hiyo kutoka kwenye jarida kubwa la Forbes.

“Nashukuru sana wote. Nina imani bila ya nyinyi na jitihada zenu kwa pamoja nisinge pata hii tuzo. Kusema kweli sikuwahi kufikiria ipo siku kama magazine kubwa kama hii ina weza kunifikiria kwamba hapa duniani kuna kajitu kama mimi”
Magreth alizungumza akiwa amesimama katikati ya wafanyakazi wake huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Bosi jitihada zako ndio zime kufikisha hapa sisi tuna fwata tu kile unacho tuelekeaza”

Juma alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.
“Nawashukuru sana tena sana. Tukimaliza kujenga mgahawa wetu basi nita toa zawadi kwa kila mmoja wenu”
“Ni zawadi gani hiyo bosi”
“Mmmm Anna ni mapema kuizungumza kwa sasa, ila tambueni hilo jukumu likiisha ni lazima niwapatie zawadi”
“Sawa”
“Sherehe ime kwisha, sasa tuendelee na kazi zetu”
“Sawa ila kuna waandishi wa habari wana omba kuzungumza nawe”
Juma alizungumza huku akimuonyesha waandishi wengi wa habari walio kusanyika hapo kupata dodoso za habari hiyo kwa maana ni watanzani wachache sana ambao wana weza kukumbukwa na jarida hilo kubwa la kibiashara. Magreth akawaalika wandishi hao kwenye moja ya meza na akaanza kuzungumza nao huku wakiendelea kumuhiji maswali na wengi wao wana penda kufahamu ni njia gani ambazo amezipitia hadi kutabiria kuja kuwa msichana mdogo, bilionea wa baadae.

“Marehemu mama yangu siku zote alikuwa ana nisisitizia katika juhudi na kuto kukata tamaa katika kutafuta. Niliamini kwenye mtaji wangu mdogo wa kuuza maandazi tena ya kutembeza mtaani, kutokana yalipendwa na watu wengi nilijitahidi kutengeneza kitu bora na nina mshukuru Mungu leo hii nipo hapa nilipo fika”

Magreth alizungumza huku akiruka baadhi ya vipengele katika safari hiyo kwa maana hayupo tayari kwamba aliotoa bikra yake kwa ajili ya kupata pesa zilizo muwezesha leo kufika katika mafanikio hayo. Mazungumzo ya waandishi wa bahari yakachukua nusu saa na yakaisha huku kila muandishi akitoka hapo akiwa na habari kamili.

Tomas akaangaza angaza katika eneo hilo la mgahawa, kisha akapata kiti na kukaa. Akawatazama waandishi wa habari walio mzunguka Magreth anaye endelea kuhojiwa.

“Kaka karibu sana. Una hitaji nini?”
“Maji ya moto chupa kubwa”
“Karibu”
Muhudumu huyo wa kike akaondoka eneo hilo, baada ya dakika moja akarudi akiwa na chupa hiyo ya maji.

“Samahani una weza kuniitia bosi wako”
“Hakuna shaka”
Muhudumu huyo akamfwata Magreth ambaye amemeliza kuzungumza na waandishi wa habari. Magreth akamfwata Tomas sehemu alipo kaa.

“Habari yako”
Magreth alizungumza huku akimkazia macho Tomas.

“Salama Magreth”
Magreth akastuka sana kwa maana sauti hiyo ni ya Tomas ambaye yeye ndio aliharibu dili zima la kutafutiwa aneo la mgahawa na nabii Sanga na pia yeye ndio muhusika mkuu wa kumteka nabii Sanga akishirikiana na mrs Sanga.

ITAENDELEA

Haya sasa Magreth ame kutana na Tomas ambaye kwa upende mmoja nia adui yake kwa maana bila yeye basi mahusiano yake na nbii Sanga hadi leo mke wake asinge jua? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose se hemu ya 87.
 
SIN 87

Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)

Age ……………………………………………………18+

Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA

Muhudumu huyo wa kike akaondoka eneo hilo, baada ya dakika moja akarudi akiwa na chupa hiyo ya maji.

“Samahani una weza kuniitia bosi wako”
“Hakuna shaka”
Muhudumu huyo akamfwata Magreth ambaye amemeliza kuzungumza na waandishi wa habari. Magreth akamfwata Tomas sehemu alipo kaa.

“Habari yako”
Magreth alizungumza huku akimkazia macho Tomas.

“Salama Magreth”
Magreth akastuka sana kwa maana sauti hiyo ni ya Tomas ambaye yeye ndio aliharibu dili zima la kutafutiwa aneo la mgahawa na nabii Sanga na pia yeye ndio muhusika mkuu wa kumteka nabii Sanga akishirikiana na mrs Sanga.

ENDELEA

“Tomas kwa nini ume weka sura bandia?”
Kauli ya Magreth ika mstua sana Toma kwa maana hakutarajia kama kuna mtu anaye weza kumfahamu au kutambua kwamba sura hiyo aliyo kuwa nayo ni ya bandia.
“Usistuke, nina imani kwamba huko ulipo pita hakuna aliye tambua kwamba hiyo sura uliyo ivaa ni ya bandia ehee?”
Magreth alizidi kumshindilia Tomas misumari ya moto moyoni mwake na kumfanya azidi kujawa na woga.

“Ume juaje?”
“Nime juaje nini?”
“Kwamba hii sura ni ya bandia?”
“Nina ujuzi wa mambo hayo toka nilipo kuwa mdogo, hivyo nina tambua sura halisi ya mtu na sura ya bandia”

Tomas akaka kimya huku akimtazama Magreth usoni mwake. Akapiga mafumba mawili ya maji kisha akaiweka mezani glasi hiyo.

“Ume ishi katika sura bandia kwa kipindi gani?”
Magreth alizungumza huku akimkazia macho Tomas.

“Toka nilipo kuwa nina tafutwa kwa kesi ambayo sikuifanya”
“Acha uongo. Ushahidi wa video yako ya ngono wewe na mrs Sanga ninayo na mimi ndio niliye rekodi pale ofisini mukifanya yetu na ubaya zaidi mulikuwa muna panga kuni kuniua na kumteka nabii Sanga”
Tomas akazidi kujawa na woga kwa maana Magreth amekuwa ni mtu aliye fahamu mambo mengi sana kuliko na alivyo kuwa ana tegemea.

“Natambua utakuwa una shangaa ni kwa nini niliweza kujua mambo hayo yote. Ila nime wasamehe, niambie ni kitu gani ambacho kimekuleta kwangu”
Tomas akashusha pumzi taratibu, huku akijitahidi kupambana na hali ya wasiwasi ambayo ina endelea kumkabili mwilini mwake.

“Hivi bado una mahusiano na nabii Sanga”
“Hapana, nina imani wewe uliweza kuvuruga kila kitu hivyo sina mahusiano naye”
“Sawa”
“Kwa nini ume uliza?”
“Nilihitaji kufahamu tu kwa maana nabii Sanga kuna mambo mengi mabaya alinifanyia”
“Hivi una hisi kutembea na mke wake tena ukawa una muingilia kinyume na maumbile ni jambo zuri. Pia nili weza kuona video yake alivyo kuwa ana kufanya na zote ninazo.”
“V…i…i..iii…d….e….o gani?”

Tomas alizungumza kwa wasiwasi mkubwa sana.

“Video ya yeye kukufi**”
Magreth alizungumza kwa sauti ya chini na kuzidi kuupa wakati mgumu moyo wa Tomas na akajikuta akijuta ni kwa nini ame kuja kuonana na Magreth kwa siku hiyo.

“Pole kwa maana nina imani wewe sio shoga hivyo aliweza kukusababishia maumivu kama uliyo kuwa una mpatia mke wake”
“Tafadhali Mage acha kuzungumzia hiyo mada”

Tomas alizungumza kwa ukali kidogo huku machozi ya hasira yakimlenga lenga usoni mwake. Magreth akaanza kucheka kwa kejeli huku akimtazama Tomas anaye hangaika kwa hasira kali.

“Ehee niambie kwa nini ume kuja kuonana nami. Au una taka nimchomeshe nabii Sanga kwako ili uweze kulipa kisasi?”
“Kwa lile alilo nifanyia nabii Sanga ina hitaji kumuua”
Magreth akajiweka vizuri kwenye kiti chake huku akitazama kulia na kushoto. Kauli hiyo haikuweza kusikiwa na watu wengine.
“Kumuua?”
“Ndio na hiyo ndio kazi iliyo nirudisha nchini Tanzania”
“Kwani ume tokea wapi?”
“Afrika Kusini”
“Sasa kama una taka kumuu, kwa nini una nieleza mimi ikiwa kwenye bifu lenu hilo mimi sihusiki”
“Nahitaji unisaidie jambo moja”
“Jambo gani?”
“Kumshawishi nabii Sanga kuonana naye ili nipate nafasi nzuri ya kumuua”
“Hahaaa huo mbona ni ushawishi wa kitoto sana. Una hisi kwamba namba ya mwisho ya atakaye kuwa ame mpigia kwenye simu yake si ita onekana ya kwangu. Wakifwatilia si wata nikamata, wakinikamata una hisi ni nini ambacho kina fwata? Ngoja nikuambie kitu kimoja, huyo nabii Sanga yeye ndio ame husika katika swala la kumuu mume wangu”
“Amemuua mume wako?”
“Ndio”
“Kwani ulisha olewa?”
“Huyo mume alitoka mbinguni. Unaulizaje maswali ya ajabu?”
“Okay sasa wewe una mpango gani?”
“Sina mpango wowote. Nimeamua kumsamehe ili niweze kuendelea na maisha yangu binafsi”
“Ahaaa Mage, hilo ni kosa kubwa sana kwenye maisha. Una msamehe vipi shetani ambaye ame kuulia mume wako. Pambana”
“Tomas sina moyo huyo na sitaki damu mikononi mwangu, kila jambo nina muachia Mungu sawa”
Magret alizungumza kwa msisitozo kwa manaa haitaji Tomas aweze kujua mpango wake.

“Sawa natambua wewe ni mlokole. Ila nilicho kuambia hapa funga kinywa chako na wala usije uka mueleza mtu yoyote na endapo uta muambia mtu mwengine nita kuua. Umenielewa?”
Tomas alizungumza kwa msisitizo.

“Sawa mkuu, kinywa changu nina kifunga zipu ziiiii”
Magreth alizungumza huku akionyesha ya kuufunga zipu mdomo kwake kwa vidole.

“Nashukuru, nina weza kupata namba yako”
“Ya nini?”
“Pale utakapo amua kubadilisha maamuzi yako ya kunisaidia katika mpango wangu basi nita kupigia”
“Okay”
Wakabadilishana nao zao.
“Nina imani kwamba ume nielewa kwamba sinto hitaji hili jambo liweze kutoka kwa mtu wa aina yoyote ile. Sawa”
“Ssawa mkuu, nikutakie kazi njema katika jitihada zako za kulipiza kisasi”
Tomas akamtazama Magreth kwa muda, akatoa noti ya shilingi elfu kumi na kuiweka mezani hapo kisha akaondoka, akaingia kwenye gari na kuondoka eneo hilo.

‘Tom Tom, una taka kuni haribia mpango wangu? Ila ukiingia kwenye kumi na nane zangu haki ya Mungu nita kuua’

Magreth alizungumza kimoyo moyo huku akitazama gari la Tomas jinsi tokomea barabarani.

***

“Baba”
“Naam”
“Hawa walinzi mimi wana nibana, nita shuhulika vipi na mipango ya biashara yangu”
Julieth alizungumza huku akimtazama baba yake usoni.

“Ila mwanangu, si mipango yako si ina kwenda vizuri?”
“Ndio ila nina taka kuhakikisha kwamba nina ona mzigo wangu. Japo nimetumia picha ila nahitaji kuuona kwa macho yangu mawili mzigo nilio fanikiwa kuiingiza nchini”
Julieth alizungumza huku wakiwa wamesimama na baba yake kwenye dirisha la chumbani kwake wakiwatazama walinzi wa serikali wakiendelea kuimarisha ulinzi katika jumba hilo.

“Kwa sasa ina bidi uwe mpole”
“Kivpi baba?”
“Ina bidi kusubiria uingie kwenye ndoa kisha ndio uendelee na mipango mingine. Tambua kwa sasa macho ya hawa walinzi yote yapo kwako”
“Sasa ita kuwaje juu ya huu mzigo?”
“Hakikisha una waambia waambia wausambaze mzigo kama kawaida”
“Sawa baba, ila lile swala la kuuwawa kwa askari kule baharini Jery alilizungumzia kipindi tulipo kuwa tuna kwenda kuchongesha pete.”
“Amesema upelelezi ume fikia wapi?”
“Hajazungumza ila amejawa na hofu ana hisi kwenye harusi yetu tuna weza kushambuliwa”
“Hakuna wa kutushambulia ikiwa sisi ndio tuna plan kila kitu”
“Sawa baba”
“Ila hakikisha huonyeshe dalili yoyote ya wewe kwamba una husika kwenye hilo jambo”
“Usijali baba”
Simu ya Julieth ukaanza kuita, akaifwata kitandani alipo iacha na kuipokea.

“Yes baby”
“Upo wapi mke wangu?”
“Nipo home mume wangu”
Nabii Sanga akatoka ndani hapo ili kumuacha huru mwanaye aendelee na kuzungumza na simu hiyo.

“Nime kumiss mke wangu, yaani nina tamani hata masaa yaende kasi sana ili siku yetu ya harusi iweze kufika”
“Usijali mume wangu, mimi ni wako na siku hiyo ya harusi nina hamu uni fanye hadi nichanganyikiwe”
“Mmmmm baby una nipagawisha. Usija ukanifanya nitoroke nije huko kukupa mambo”
“Hahaa usitoroke bwana mume wangu”

Julieth alizungumza huku akiwa amelala kifudi fudi kitandani kwake huku akiinua inua miguu yake kwa nyuma.

“Ehee niambie shela lako tayari limesha malizwa kushonwa?”
“Wameniambia kesho wata kuwa wame maliza na wata lileta”
“Sawa mke wangu. Vipi ume kula?”
“Mmm bado ila nita kula”
“Fanya ule mke wangu, si unajua nataka siku ya harusi shavu liwe dodo”
“Hahaa sitaki kuwa kibonge bwana”
“Sawa mke wangu, kuna daktari jioni hii nita onana naye ni rafiki yangu, hivyo nina omba ruhusu malikia wangu”
“Hahaaa usijali mume wangu. Nenda ila kuwa makini si una jua watu wanavyo iangalia kwa jicho la husda ndoa yetu”
“Ni kweli ila nina walinzi wa kutosha”
“Sawa mume wangu, jioni njema”
“Nawe pia”

Julieth akakata simu, akaichukua simu yake nyingine ambayo ana itumia kwa ajili ya kuwasiliana na vijana wake wanao shuhulika na maswala ya usambazaji na madawa hayo ya kulevya.

“Ndio mkuu”
“Muna weza kuanza kazi”
“Sawa”
Julieth akakata simu na kuirudisha katika droo ndogo ya kitanda chake kisha akatoka ndani hapo.

***

“Mbongo masaa ishirini na nne yamekwisha ripoti yako ni ipi?”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa njia ya video call kwa kutumia computer yake iliyopo mezani kwake.

“Mkuu bado upelelezi una endele”
“Sawa una endelea ila si Al-Shabab si ndio walio husika?”
“Nina shindwa kukupa jibu la moja kwa moja muheshimiwa ila tuna mashaka kwamba wao wana weza kuhusika”
“Una mashaka au ni wao.”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa msisitizo na kumfanya mzee Mbogo mkuu wa kitengo cha NSA, kutingisha tu kichwa.

“Sasa nina hitaji mutume vikosi kuhakikisha kwamba muna kwenda kushambulia kikosi hicho kuanzia huko Somalia na upande mzima wa bahari ambapo wamejificha”
“Sawa muheshimiwa raisi, ila una onaje tuka ishirikisha serikali ya Somalia?”
“Wao walivyo waua askari wetu walishirikisha serikali yao?”
“Hapana mkuu”
“Basi fanya hivyo nahitaji ndani ya masaa ishirini na nne mengine hilo jambo liwe lina matokea mazuri. Umenielewa Mbogo”
“Sawa muheshimiwa nita tuma timu ya vijana wangu wanne wata kwenda huko”
“Fanya hivyo na nita hitaji kuifwatilia hiyo oparesheni mubashara sawa”
“Sawa muheshimia”
“Na nina taka ianze usiku wa leo”
“Nime kuelewa muheshimiwa raisi”
“Sihitaji makosa yoyote kutokea kwenye hiyo oparesheni ya siri. Peleka vijana wenye uwezo sawa”
“Nime kuelewa muheshimiwa raisi, kazi ita anza ndani ya masaa mawili yajayo”
“Sawa”

Raisi Mtenzi akakatisha mazungumzo hayo na kutoka ofisini kwake kwa maana muda wa kukaa ndani ya ofisi hiyo ume kwisha.
***

“Mkuu tuna fanya nini sasa”
Msaidizi wa mzee Mbogo aliuliza mara baada ya kukata simu hiyo ya raisi Mtenzi.

“Raisi ame panic”
“Ni kweli ila ume muahidi kutuma vijana katika oparesheni hii, sasa ita kuwaje?”

“Siwezi kutuma mtu yoyote kwenda kwenye oparesheni ambayo haija kamilika uchunguzi wake. Sinto taka vijana wangu wafe kizembe kama hao walio tumwa huko na kufa kijinga”
“Ila muheshimiwa si uta kuwa ume kiuka amri ya raisin a matokeo yake si una yafahamu?”
“Ndio nina yafahamu nipo tayari kuachishwa kazi ila sinto fanya kitu nje yauwezo wa kitengo changu”
Mzee Mbogo alizungumza huku akimtazama msaidizi wake huyo ambaye amejawa na wasiwasi mkubwa sana kwa maana kuenenda kinyume na amri ya raisi ni kosa moja kubwa katika kitengo chochote cha usalama kwa maana wote wapo chini ya raisi Mtenzi.

ITAENDELEA

Haya sasa mzee Mbogo mkuu wa kitengo cha NSA ame kataa kutuma vijana wake kwenda kwenye oparesheni anayo ing’ang’aniza raisi Mtenzi je ni kitu gani ambacho kita tokea? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose se hemu ya 88.
 
SIN 88

Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)

Age ……………………………………………………18+

Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA

“Ni kweli ila ume muahidi kutuma vijana katika oparesheni hii, sasa ita kuwaje?”

“Siwezi kutuma mtu yoyote kwenda kwenye oparesheni ambayo haija kamilika uchunguzi wake. Sinto taka vijana wangu wafe kizembe kama hao walio tumwa huko na kufa kijinga”
“Ila muheshimiwa si uta kuwa ume kiuka amri ya raisin a matokeo yake si una yafahamu?”
“Ndio nina yafahamu nipo tayari kuachishwa kazi ila sinto fanya kitu nje yauwezo wa kitengo changu”
Mzee Mbogo alizungumza huku akimtazama msaidizi wake huyo ambaye amejawa na wasiwasi mkubwa sana kwa maana kuenenda kinyume na amri ya raisi ni kosa moja kubwa katika kitengo chochote cha usalama kwa maana wote wapo chini ya raisi Mtenzi.

ENDELEA

“Sawa mkuu”
“Nenda kaendelee kusimamia upelelezi na usimueleze mtu yoyote juu ya mawasiliano haya”
“Sawa”
Baada ya msaizidi wake kutoka. Mzee Mbogo akaingia upane wa kuandika barua kwenye computer yake. Taratibu akaanza kuandika barua ya kujizulu, ili hata kama ikitokea raisi Mtenzi ata kasirika basi iwe rahisi kwa yeye kuachia madaraka ya kitengo hicho haraka iwezekanavyo. Mzee Mbogo akaanza kukusanya vitu vyake muhimu ndani ya ofisi hiyo. Kisha akaelekea katika chumba kikubwa cha mawasiliano.

“Nina omba tusikilizane”
Mzee Mbogo alizungumza na wafanyakazi zaidi ya hamsini wa kitengo hicho wakaacha kazi wanazo zifanya na kumtazama mkuu wao, ambaye kwa miaka zaidi ya thelathini ame kuwa akifanya kazi katika kitengo hicho.

“Naamini wote muliweza kushuhudia juu ya tukio la kushambuliwa kwa askari wetu. Halikuwa tukio zuri kwetu wala katika nchi yetu.”
Mzee Mbogo alizungumza kwa sauti ya upole ila yenye kusikika kwa kila mtu katika chumba hicho kikubwa.

“Hadi sasa hivi hatuja fanikiwa kujua ni nani ambaye ana husika katika tukio hili, si ndio”
“Ndio mkuu”
“Kazi yetu ni kuhakikisha nchi ina kuwa salama. Haiongezi adui zaidi ni kupunguza adui. Nina tambua hadi sasa hivi hatujakamilisha upelelezi wetu na ni ngumu kumshuku mtu yoyote katika hii kazi. Hivyo nina waomba muhakikishe kwamba muna ifanya kazi hii kwa umakini wa hali ya juu na ikiwezekana apatikane muhusika sahihi. Muna weza kuendelea na kazi zetu”

Mzee Mbogo alizungumza kwa hali ya mafumbo na hakutaka kuwapa presha ya aina yoyote wafanyakazi wake. Wafanyakazi wakaendelea na kazi ya kuendelea kuhakikisha kupitia teknolojia ya satelate basi wana weza kubainisha ni nani ambaye ndio muhusika. Mzee Mbogo akaendelea kuzunguka zunguka ndani ya ofisi hiyo huku kwa mara kadha macho yake yapo kwenye saa ya ukutani kwa maana ana tambua kwamba raisi Mtenzi ni mtu ambaye ana kwenda na muda na huwa hapendi masihara hata kidogo kwenye kauli zako. Majira ya saa mbili na dikaki mbili, mmoja wa wafanyakazi akamsogelea.

“Mkuu raisi yupo kwenye simu namba moja”
“Sawa nina shukuru”
Mzee Mbogo, akasogelea meza yenye simu ya mezani. Akanyanyua mkonga wa simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.

“Ndio muheshimiwa raisi”
“Nime kaa hapa na wakuu wa majeshi tuna subiri oparesheni hiyo ianze”
Mzee Mbogo akashusha pumzi taratibu, akawatazama vijana wake ambao kila mtu yupo bize na computer yake.

“Samahani muheshimiwa raisi, hatuwezi kutuma timu kwa leo usiku kwa maana hatujui tuna kwenda kumkamata nani”
Raisi Mtenzi akaka kimya kama sekunde hamsini hivi.
“Hivi umesha anza kuzeeka?”
“Hapana muheshimiwa. Ila upelelezi wa timu yangu bado una endelea na endapo tuta fahamu basi nita tuma timu kwenda kuwakamata wahalifu”
“Mbogo una nitambua vizuri si ndio?”
“Ndio muheshimiwa”
“Basi kuanzia hivi sasa huna kazi na sio mkuu tena kwa kitengo cha NSA. Nafasi yako sasa hivi nina tuma mtu ana kuja kuichukua ndani ya kitengo hicho. Laiti kama unge kuwa sio mzee basi nigekusweka ndani, ila kwa heshima yako chukua kila kilicho chako na utoke ndani ya kitengo sasa hivi. Tumeelewana”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa msisitizo sana.

“Ndio nime kuelewa muheshimiwa raisi.”
Simu ikakatwa na mfanyakazi anaye shuhulika na maswala ya mawasiliano macho yakamtoka sana kwa maana ame sikia kila kitu. Akanayanyuka kwenye kiti chake huku akijikaza sana kwa maana ame ishiwa nguvu kabisa za miguu yake. Akamtazama bosi wake ambaye kwa kipindo chote ame kuwa akifanya naye kazi kwa amani na upendo. AKamsogelea huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Mkuu nilicho kisikia ni ukweli au kuna jambo tofauti na hilo?”
“Ulicho kisikia ni kweli?”
“Tuna fanya nini sasa mkuu. Katikati ya upelelezi una fukuzwa kazi”
“John tuliza hasira. Lazima upelelezi uendelee”
“Hapana mkuu, hii sio sawa. Huu ni uonevu”
“Nime kuelewa John rudi kwenye kiti chako. Sio ombi ni amri”
Kijana huyo mwembamba taratibu akaanza kurudi hadi kwenye kiti chake. Mzee Mbogo aka tembea hadi kwenye ngazi ambazo akisimama eneo hilo, kila mtu ana muona.

“Tusikilizane”

Wafanyakazi wote wakamgeuka yeye na kumtazama.

“Dakika tatu au tano zilizo pita nime pokea simu kutoka ikulu.”
Mzee Mbogo akaka kimya huku akiwaonea huruma vijana hao ambao wote ame wakuza katika kazi hiyo.
“Simu imetoka moja kwa moja kwa raisi Mtenzi……….”
Mzee Mbogo akainamisha kichwa chake chini, akatoa kitambaa mfukoni mwake na kujifuta machozi kisha akawatazama vijana wake hao ambao wote walisha aanza kujawa na wasi wasi kwa maana hawajawahi kumuona mkuu wao akiwa katika hali kama hiyo.
“Nimefukuzwa kazi”
Minong’ono ikaanza kuzuka ndani ya chumba hicho huku kila mmoja akiwa haelewi ni nini kimepekelea mkuu wao kufukuzwa kazi, ikiwa amebakisha mwaka mmoja kabla ya kustafu kwake. Mzee Mbogo akanyoosha mkono wake wa kulia juu kidogo na wafanyakazi wote wakaa kimya.
“Sababu ya kufukuzwa ni kwamba masaa ishirini na nne niliyo pewa juu ya kuwatafuta watu walio husika na wanajeshi hao yamepita na mbaya zaidi ni kwamba nime kataa kutuma timu kwenda Somalia, kushambulia Al-Shabab ambao hatuna uhakika nao kama wao ndio wame husika kwenye lile tukio”
“Ahaaa….mkuu hiyo sio sawa”
Kijana mmoja aliropoka huku akiwa amejawa na jazba. Mlango wa chumba hicho uka funguliwa, akaingia mwana mama mmoja mrefu huku akiwa amevalia suti nyeupe na nyuma yake ame ongozana na walinzi wanane.

“Director Mbogo. Naitwa Emmy nina imani kwamba ume pata taarifa zangu”
Mwana mama huyo alizungumza huku akimpa mkono mzee Mbogo.

“Ndio japo sija ambiwa ni nani ambaye ana kuja kuchukua nafasi yangu”
“Ni mimi. Tusikilizane, kwa nijina nina itwa Emmy kuanzia hivi sasa mimi ndio nita kuwa director wa hicho kitengo na nina waomba muendane na kasi yangu kwa maana mimi ni mchapa kazi sana”
Kila mmfanyakazi hakupendezwa na ujio wa mwana mama huyo.
“Mzee wangu walinzi wangu wana weza kukuongoza hadi ofisini kwako. Ukachukua kila kitu chako na kuondoka katika jengo hilo. Una dakika thelathini za kufanya hivyo”
Mwana mama huyo alizungumza huku akiitazama saa yake ya mkononi.
“Huwezi kumpelekesha bosi wetu hivyo”
Kijana mmoja alizungumza kwa hasira huku akimsogelea mwana mama huyo.

“Samahani una sema?”
“Ume nisikia, sihitaji kurudia”
“Hahaaa wewe ni nani kwani?”
“Mimi ndio msaidizi wake”
“Ohoo basi na wewe kama una taka kuondoka na bosi wako, nenda”
“Sawa”
John akamtazama mzee Mbogo, kila mmfanyakazi akahisi kunyong’onyea kwa maana watu wawili tegemezi ndani ya ofisi yao ndio hao wana ondoka.
“Nisikilizeni, kama kuna mtu ana hitaji kuondoka zake nani ya ofisi hii. Basi njia ni yeupe, ila nina imani wote muna tambua madhara ya kuondoka kwako kwa maana huto pata hata shilingu moja ya malipo yako kwa maana uta kuwa ume jiachisha kazi wewe mwenyewe.”
Wafanyakazi hao wa kike na wakiume wakaanza kutazamana. Mfanyakazi mmoja baada ya mwangine akaanza kukusanya kila kilicho chake na kuungana na mzee Mbogo na wakaondoka ofisini hapo. Emmy akashusha pumzi huku akitazama meza jinsi zilivyo nyeupe.

“Mkuu tuna fanya nini ikiwa wameondoka wote”
“Usijali waacheni wafwate mkumbo. Nina mpigia raisi”
Emmy akatoa simu yake mfukoni na kumpigia raisi Mtenzi, simu ya raisi Mtenzi ikapokelewa.

“Ndio Emmy”
“Muheshimiwa raisi, huwezi amini wafanyakazi wote wame acha kazi na wameondoka hapa ofisini kisa tu bosi wao ame ondoka”
“Nini?”
“Ndio muheshimiwa. Tuna fanya nini?”
“Weka timu mpya au na wewe una shindwa kujiongoza?”
“Nime kuelewa je hawa wafanyakazi walio ondoka tuwafanye nini?”
“Si wameacha wenyewe, acha waondoke zao ila kwa sasa nina taka hiyo oparesheni iweze kuendelea”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Emmy akakata simu kisha akapiga simu kwenye chuo cha kitengo hicho na akaagiza timu ya vijana hamsini wenye uwezo mkubwa katika maswala ya mawasiliano kufika hapo mara moja.

“Jamani tambueni muna familia na nyinyi bado ni vijana wadogo. Mukiacha hivi kazi muta kwenda kufanya nini huko mtaani?”
Mzee Mbogo alizungumza kwa upole huku akiwa amesimama katikati ya kundi la wafanyakazi wake hao.
“Mkuu tuta tambua hilo, ila heshima ni kitu cha bure sana kwenye maisha yetu. Ume fanya kazi na zaidi ya serikali tatu, ina kuwaje huyo raisi ana kufukuza tena kwenye oparesheni ambayo sisi hatuhusiki”
“Ni kweli, ila ina bidi mubaki kazini”
“Hatuwezi kufanya kazi ya yule mwana mama muheshimiwa. Kwako pale una ukumbi mkubwa sana, una weza kufungau ofisi ya kwako peke yako na kuanzisha kampuni yako na sisi tukawa chini yako”
“Ni kweli hilo ni wazo zuri mkuu”
“Nita walipa nini vijana wangu”
“Tupo tayri kufanya kila aina ya kazi ili mradi kuhakikisha kwamba tuna pata pesa za kutukidhi sisi na familia zetu”
“Alilo lizungumza dada Alima hapo ni jambo zuri muheshimiwa. Tafadhali nina kuomba uweze kufanya hivyo”
“Sawa nime wasikia, basi kutokana muda ume kwenda, nina waomba muende kupumzika kisha kesho saa mbili muje pale nyumbani kwangu”
“Sawa muheshimiwa”
Wafanyakazi hao kila mtu akaingia kwenye gari lake na kuondoka ofisini hapo.

***

Simu ya Magreth ikaanza kuita, akapunguza mwendo wa gari lake kisha akaitoa kwenye pochi. Akaitazama namba hiyo itakayo katika kampuni nchini Thailand alio wapa oder ya kutengenea nguo ambazo ana mpangow a kuzitumia kwenye kazi ya kumteketeza nabii Sanga.

“Haloo madam Magreth”
Sauti ya kike ilisikika.
“Haloo habari yenu”
“Salama, japo sijui Swahili vizuri ila naweza ongea nawe”
“Sawa nafurahi kusikia hivyo”
“Tuma jumbe katika barua pepe yako hivyo una weza fungu na kuona ukamilisho wa kwanza wa nguo yako kisha tuta kutumia tena awamu ya pili na ya tatu”
“Sawa, nita ingia kwenye email yangu baada ya lisaa kama moja hivi kisha nita jibu”
“Hakuna matata”
“Asante”
Mwana dada huyo akakata simu na kumfanya Magreth ajawe na shahuku kubwa sana ya kuhitaji kuiona nguo yake hiyo. Foleni ya magari iliyopo mbele yake, hakika akatamani hata ange kuwa na piki piki yake. Simu yake ikaita tena, akaitazama na kukuta ni namba ya mmoja wa mameneja wa hoteli KX Royol, ambaye alimuahidi wata onana saa tatu usiku kwa ajili ya mazungumzo ya kibishara.

“Kaka yangu nisa mehe sana kwa kuchelewa”
“Usijali dada nili kuwa nina kukumbushia tu”
“Nakumbuka, nina fika hapo hotelini kwako, nipo kwenye foleni hivyo nina kuomba uweze kunivumilia”
“Sawa nina kusubiria”
“Asante”
Magreth akakata simu. Baada ya sakika ishirini na tano akafika katika hoteli hiyo yenye hadhi kubwa kwa eneo hilo la Kigamboni. Akasimamisha gari lake eneo la maegesho, akampigia meneja huyo na akamueleza ni eneo gani alipo.
“Pole sana kwa foleni dada yangu”
“Nashukuru sana, hoteli yenu ni nzuri sana”
“Kidogo tume jitaidi, tuna shukuru”
“Niimeitikia wito kaka yangu”
“Nashukuru sana, lengo la kukuita hapa ni kuomba ushirika wa kibiashara. Nina timu yangu ya wapishi nina omba sana uwa fundishe kupika chakula kama unacho kipika wewe nina imani uta kuwa ume tupa ujuzi mkubwa sana”
Magreth akatabasamu kwa maana japo yeye ana mgahawa, ila ukweli ni kwamba ana wateja wengi sana kwani wana penda mapishi yake.
“Kaka yangu hilo unalo lizungumza kwa namna moja ama nyingine ina wezekana au pia isiwezekane?”
“Kwa nini dada?”
“Kuna upishi wa kusomea na upishi wa kipaji. Mimi sikuwahi kuingia shuleni na kusomea mapishi, ila ni k……….!!”
Magreth akajikuta macho yakimtoka huku akijawa na mstuko mkubwa sana. Hakuamini macho yake kumuona Evans akikatiza mbele ya macho yake na akakaa kwenye kiti kingine huku akisubiria huduma ya wahudumu wa hoteli hiyo.

ITAENDELEA

Haya sasa Magreth kwa mara nyingine ame muona Evans je ni yeye au ana mfananisha? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose se hemu ya 89.
 
SIN 89

Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)

Age ……………………………………………………18+

Simu………………………………………………… 065707258 8(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA

“Nashukuru sana, lengo la kukuita hapa ni kuomba ushirika wa kibiashara. Nina timu yangu ya wapishi nina omba sana uwa fundishe kupika chakula kama unacho kipika wewe nina imani uta kuwa ume tupa ujuzi mkubwa sana”
Magreth akatabasamu kwa maana japo yeye ana mgahawa, ila ukweli ni kwamba ana wateja wengi sana kwani wana penda mapishi yake.
“Kaka yangu hilo unalo lizungumza kwa namna moja ama nyingine ina wezekana au pia isiwezekane?”
“Kwa nini dada?”
“Kuna upishi wa kusomea na upishi wa kipaji. Mimi sikuwahi kuingia shuleni na kusomea mapishi, ila ni k……….!!”
Magreth akajikuta macho yakimtoka huku akijawa na mstuko mkubwa sana. Hakuamini macho yake kumuona Evans akikatiza mbele ya macho yake na akakaa kwenye kiti kingine huku akisubiria huduma ya wahudumu wa hoteli hiyo.

ENDELEA

“Ngoja nina kuja”
Magreth alizungumza hukua kinyanyuka kwenye kiti hicho. Akatembea hadi katika meza hiyo na kusimama mbele ya Evans.

“Evans”

Magreth aliita kwa mshangao, ila Evans akajitahidi sana kuwa kama mtu asiye mfahamu kwa maana kwa matatizo aliyo sababishiwa na mwana mke huyo yali vuruga sana ndoto zake za maisha.

“Evans ni wewe mume wangu?”
“Samahani dada, una zungumza na mimi?”
Evans akajitahidi kuibadilisha sauti yake ila haikumzuia Magreth kukaa kwenye kiti cha pembeni huku akimtazama Evans usoni mwake.

“Evans natambua kwamba nime kukosea na nina jua kuna mambo mengi sana ume yapitia. Ila nina kuomba unisikilize”
Magreth alizungumza kwa sauti ya unyonge na ya kubembeleza. Evans akashusha pumzi huku akimtazama Magreth.

“Samhani dada uta kuwa ume nifananisha”
“Hapana siwezi kukufananisha. Kwenye maisha yangu mtu wa pekee ambaye nina mfahamu sana ni wewe”
“Dada yangu nina kuomba unielewe mimi sio huyo mtu ambaye una mtafuta”
Evans mara baada ya kuzungumza maneno hayo akasimama na kuanza kuondoka eneo hilo. Magreth akamtazama jinsi anavyo tembea, moyo wake ukakataa kabisa kuamini anacho kizungumza Evans. Akanyanyuka kwa haraka na kuanza kumfwata kwa nyuma. Wakafika kwenye eneo la lifti.

“Umekuja hadi huku”
Evans alizungumzahuku akimtazama Magreth kwa macho ya hasira sana. Kabla hata Magreth hajazungumza jambo lolote, lifti hiyo ikafunguka, Evans akawahi kuingia na Magreth akamfwata kwa nyuma. Kila alama ambayo anayo Evans hata huyu mtu anayo.

“Wewe dada una kwenda wapi?”
Evans alizungumza kwa ukali sana huku akimkazia macho Magreth.

“Nahitaji kufahamu ukweli. Kama wewe sio Evans mimi nita kuacha uendelee na maisha yako na kama kweli wewe ni Evans basi nina hitaji kukuomba masamaha”
Magreth alizidi kuwa king’ang’anizi hadi Evans akajikuta akiminya kitufe cha gorofa anayo elekea. Walipo fika katikati ya gorofa ya pili, Magreth akaminya kitufe cha kuisimamisha lifti hiyo.

“Una taka kufanya nini?”
“Natambua tumboni kwako una jeraha la kuchomwa kisu nina kuomba niweze kukutazama. Endapo nita likuta jeraha hilo basi moja kwa moja wewe uta kuwa ndio Evans ila nisipo likuta basi nita shukuru kwa ushirikiano wako”
Kauli hiyo ya Magreth ikamstua sana Evans, akashusha pumzi huku akijifikiria kufungua tumbo lake.

“Ina kuwa ni jambo la ajabu sana pale unapo mg’ang’aniza mtu kufanya kitu asicho kipenda”
“Nalitambua hilo ila nina kuomba sana ufungue vifungo vya shali lako. Nipo chini ya miguu yako”
Evans akamtazama Magreth kwa sekunde kadha machoni mwake, kisha taratibu akaana kufungua vifungo vya shati lake.

Magreth macho yakamtoka, huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi. Eneo zima la kuanzi kifuani mwa Evans hadi tumboni mwake, lime jaa alama za majera makubwa makubwa. Evans akamalizia kuvua shati hilo na kugeuka na kumuonyesha Magreth majeraha mengine mgongoni mwake.

“Nina imani kwamba mtu anaye mtafuta sio mimi. Hivyo samahani sana”
Magreth akashindwa hata kuzungumza jambo la aina yoyote. Akaanza kungua kilio huku akikaa chini. Evans akaminya kitufe cha kuiruhusu lifti hiyo kuendelea kupanda juu huku akivaa shati lake.
“Dada una weza ukaondoka”
Evans alizungumza huku akimtazama Magreth aliye nyong’onyea kwa kushindwa kuona kile alicho kitarajia. Evans akatoka ndani ya lifti hiyo, akaanza kutembea kuelekea katika chumba chake. Magreth akajikaza taratibu huku akiminya kitufe cha kurudi chini. Evans alipo shuhudia lifti ina jifunga na kuanza kurudi chini, akaingia chumbani kwake kwa maana haijtaji Magreth kutambua chumba anacho kaa.

Taratibu Magreth akatoka nje la lifti hiyo, akaanza kutembea kwa unyonge, hakukumbuka hata kikao chake na meneja wa hoteli hiyo.
“Dada Magreth”
Maneja alimuita huku akimtazama usoni mwake.
“Mbona hivyo kuna tatizo”
“Tuwasiliane siku nyingine. Nina hitaji kupumzika sasa hivi”
Magreth alizungumza na kutoka nje ya hoteli hiyo, akaingi ndani ya gari lake. Machozi yakazidi kumbubujika, moyo wake bado una amini kwamba yule ni Evans ila kwa jinsi majeraha yalivyo mjaa mwilini mwake ana onekana amepitia mateso mengi sana yaliyo mpelekea kuwa katika hali kama hiyo.

“Kwa nini wame mtesa hivi mume wangu hadi hanikumbuki”
Magreth aliendelea kuzungumza huku akilia kwa uchungu sana. Akawasha gari lake na kuondoka hotelini hapo na kurudi nyumbani kwake.
“Una kwenda wapi”
Sauti hiyo ya kike ika mstua sana Evans ambaye ana kusanya kila kilicho chake ili kuondoka katika hoteli hiyo kwa maana hahitaji kabisa kuwa karibu na Magreth. Akageuka nyuma yake na kumkuta jini anaye muwezesha kwa kila jambo akiwa amesimaam kwenye moja ya kona ya chumba hicho.

“Nina hitaji kuondoka hapa hotelini”
“Kwa nini?”
“Yule mwanamke ana weza kurudi tena hapa na akanifanyia fujo mimi”
“Hawezi kurudi”
“Una uhakika gani?”

Dada huiyo akatabasamu huku akimtazama Evasn, akamsogelea Evans na kumshika mikono yake.

“Kama nime kupatia pesa za kutosha na nina kutoa kwenye hatua moja ya maisha na kwenda kwenye hatua nyingine una hisi nita shindwa kumzuia Magreth kurudi hapa?”
“Nime kuelewa”

Evans alizungumza huku akishushusha pumzi taratibu.
“Jambo la msingi hapa ni kuhakikisha kwamba una endelea na mapango ulipo mbeleni na wala usimfikirie huyo mwana mke tena. Umenielewa”
“Ndio”
“Endelea na mambo yako mengine. Usiku mwema”
“Ngoja mara moja?”
“Ehee?”
“Hivi huwa una kuwa karibu yangu kila mara au?”
“Ndio nina kufwatilia kila unapo kuwa na mimi ndio mlizi wako. Sawa”
“Haya”
Mwana dada huyo akapotea ndani hapo na kumuacha Evans peke yake.

***

Magreth akafika nyumbani kwake huku akiwa mnyonge sana. Akashuka kwenye gari lake na kuingia ndani, akamtazama rafiki yake Josephine aliye kaa sebleni hapo akitazama televishion.
“Mage upo sawa?”
Josephine aliuliza huku akimtazama Magreth anaye kaa kiunyonge kwenye moja ya sofa.
“Mage mbona uso wako ume jaa huzuni na umepoteza nuru ya furaha. Niambie kuna tatizo gani linalo kusumbua?”
“Nime kutana na Evans”
“Evans?”
“Ndio nime kutana naye na nimezungumza naye”
“Hapana Magreth, mbona nina sali sana juu ya hilo jambo ila simuoni. Inakuwaje huyo uliye kutana naye akawa Evans?”
“Yaani wee acha tu. Nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kwamba nina mueleza juu ya maisha yetu ya nyuma, ila alikataa katu katu na kusema kwamba yeye sio Evans”
“Mmmmm”
“Nilimuomba sana kuona jeraha la kisu katika tumbo lake. Alikubali na akavulia shati lake. Huwezi amini mwili wake umejaa alama za majeraha, mithili ya mtu aliye pigwa mijeledi. Isitoshe aliendelea kunisisitizia kwamba sio yeye”
“Wewe ume kunata naye wapi?”
“Kwenye hoteli hii iliyopo hapa wapi?”
“Ahaa hiyo hoteli ya hadthi ya nyota tano?”
“Ndio”
“Sasa ikawaje?”
“Nilimuruhusu aondoke kwa maana, kila sehemu ya mwili unayo mtazama ni yeye ila kwenye sauti kidogo ndio kuna utofauti na sikuweza kuona jeraha la siku, nahisi ni kutokana na kujaa alama hizi za mijeledi”
“Msikini, kama ata kuwa ni yeye basi hato kuwa na kumbukumbu zozote kuhusiana na wewe?”
“Ni kweli, nina imani kuna mateso mengi sana wamapatia.”
“Bado sijapata jibu, ni nani ambaye ana husika na kumteka kwake?”
“Sali rafiki yangu Mungu akufunulie katika hilo.”
“Nita sali leo usiku, ila nina kuomba sana usi panic katika hili jambo nina imani kwamba Mungu ata tusaidia kupata ufumbuzi”
“Amen”
Magreth akanyanyuka na kuingia chumbani kwake. Akawasha laptop yake na kuingia kwenye upande wa barua pepe. Akaanza kupitia picha za vazi lake analo lihitaji.

“Sanga lazima nidili na wewe”
Magreth alizungumza kwa msisitozo. Akajibu email hiyo na kuwaruhusu waendelee na utengenezaji wa vazi hilo. Kila muda akili yake ina mfikiri Evans aliye kutana naye hotelini. Akachukua simu yake, akaitafuta namba ya nabii Sanga, alipo ipata akampigia. Simu ya nabii Sanga ikaanza kuita kisha ikapokelewa.

“Una hitaji nini?”
“Natambua wewe ndio una husika na kumteka Evans wangu na umempatia kumbukumbua hadi akapoteza kumbukumbu zake juu yangu. Nina kuahidi kitu ambacho nita kufanyia Mungu mwenyewe ndio atakaye jua”

“Hivi wewe binti muuza maandazi una jiamini nini haswa hadi una kuwa ni mtu wa kunitisha tisha kisa hicho kiji vulana chako ehee?”
Nabii Sanga alizungumza kwa ukali sana.

“Aahaa una hisi ni kivulana si ndio?”
“Ndio ni kivulana. Ngoja nikuambie jambo moja sina muda mchafu na kuhangahika na hicho kijimasikini chako. Sasa hivi nina dili na ndoa ya binti yangu kama uta taka kadi wewe sema na sio kunipigia pigia kelele. Umenielewa?”
“Okay nime kuelewa”
Magreth alizungumza kwa hasira huku akimwagikwa na machozi usoni mwake. Akakata simu na kuirushia kitandani kwa hasira huku akipiga kelele za hasira.

“Mage Mage”
Sauti ya Josephine ilisikika akimuita Magreth kwa msisitizo. Josephine akaingia ndani hapo na kumkuta Magreth akilia kwa uchungu sana. Ikamlazimu Josephine kuanza kumbembeleza rafiki yake huyo kwa maana ana tambua ni magumu gani ambayo ana yapitia kwa kipindi hichi.
***

“Nani huyo baba?”
Julieth alizungumza huku akimtazama baba yake.

“Ni yule malaya”
“Nani?”
“Magreth ana dai sijui yule Evans ame poteza kumbukumbu zake kwa kuteswa”
“Ina maana yupo hai Evasn?”
“Nahisi hivyo kwamba yupo hai”
“Baba nina hitaji kumuua huyo kijana. Nahitaji kuhakikisha kwamba siri yangu ya usichana wangu haitoki kwa mtu yoyote. Endapo ikitoka, baba tuna poteza kila kitu na hatuto kuwa na ndo”
Julieth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama nabii Sanga usoni mwake.

“Achana naye kwa maana hato weza kufanya hivyo. Isitoshe kwamba akili yake kwa sasa haipo sawa”
“Baba!!!”
“Ndio, hatuna haja ya kushuhulika naye isitoshe daktari ame dhibitisha kwamba wewe ni bikra, huna haja ya kuendelea na kumfikiria”
“Sawa baba nime kuelewa
***

“Tusikilizane?”
Emmy mkuu mpya wa kitengo cha NSA alizungumza huku akiwatazama wanafunzi hao walio ingia kwenye chumba cha kufanyia kazi ya kuhakikisha wana chukua nafasi ya watumishi walio jiuzulu wa kitengo hicho cha NSA.

“Kazi yetu ni moja tu. Tuna hitaji kutafuta eneo ambalo ndio makao makuu ya kikosi cha kigaidi cha Al-Shabab ambao siku moja iliyo pita waliweza kuwashambulia askari wetu baharini na kuwaua vibaya sana kama hivyo munavyo ona kwenye hiyo video hapo”
Emmy alizungumza huku akiwaonyesha video hiyo wanafunzi hao ambao walibakisha mwenzi mmoja kabla ya kuhitimu katika kitengo hicho.
“Ina tupasa kuhakikisha tuna lipa kisasi kwa watu hao. Tuna masaa matano hadi asubuhi tuwe tumesha ikamilisha kazi hiy…….”
Kabla ya Emmy hajamalizia sentensi yake, computer zote ndani hapo zikaanza kuzima na kuwaka na ndani ya dakika moja zikazima moja kwa moja na hapakuwa na hata moja iliyo waka.
“Mkuu masaa hayo matano uliyo toa hayato tosha”

Kijana mmoja alizungumza huku akimtazama Emmy usoni mwake.
“Kwa nini?”
“Data zote zilizo kuwa zina hifadhiwa kwenye hizi computer zime futwa hivyo hatuwezi kufanya jambo la ina yoyote”
Emmy akajikuta akitukana kwa hasira kwa maana ana tambua ni lazima wafanyakazi walio ondoka ndio wame sababisha jambo hilo.

ITAENDELEA

Haya sasa data zote ambazo Emmy alikuwa ana zitegemea na vijana wake hao wapya zime futika je wata fanikiwa kuiendesha oparesheni hiyo, usikose se hemu ya 90.
 
Safi sana na hongera kwa ukomavu, watu wawili watatu wasiwe sababu ya kuwaharibia wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla sijaanza naomba niwahakikishe kwamba hii story nimepewa ruhusa na mwandishi kupost humu. Kila siku ntakua napost na nawahakikishia story itaisha kabisa.

SIN 01
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188

Kila mwanachuo ndoto zake ni kuweza kupata ajira nzuri sana kwa kile alicho kisomea kwa miaka mingi sana kipindi alipo kuwa chuoni. Ila mambo ni tofauti sana kwa kijana Evans Shika. Elimu ya Masters of Business Administration – International Business aliyo isoma katika chuo cha IFM, inamfanya azidi kutesaka sana katika swala zima la kutafuta ajira. Kila ofisi aliyo weza kupeleka maombi ya kuajiriwa, ana kataliwa na kujikuta ana zidi kukumbana na maisha magumu sana yaliyopo katika jiji la Dar es Salaa.
“Evans”
Lukas rafiki yake wa karibu alimuita huku akimtazama usoni mwake.
“Niambie kaka”
“Nina mazungumzo muhimu nahitaji kuongea na wewe. Kmaa unaweza kunipatia muda wako basi nakuomba tuzungumze”
“Sawa kama tuzungumze tu”
Evans alizungumza huku akikaa kitako kitandani na kumtazama Lukas aliye kalia stuli moja iliyomo ndani ya geto hilo.
“Lidya ni mjamzito na hapa ninavyo zungumza kwao wametambua hilo na baba yake ameamua kumfukuza”
“Mungu wangu….Sasa utafanya nini kaka?”
“Sina jinsi zaidi ya kumleta hapa kaka. Nilazima niishi naye kwa maana hakuna namna”
“Mmmm kaka sasa kweli tutaweza kuishi watatu geto moja!?”
“Ahaa kaka hatuta weza. Mimi naona kwa sasa uweze kujitafutia maisha mengine ndugu yangu. Usinifikirie vibaya au kuhisi kwamba nina kufukuza nyumbani kwangu. Hapana, ila shemeji yako ndio huyo ana kuja na kwakweli sikujipanga kabisa kuhimili maisha ya kuhudumia watu wawili.”
Maneno ya Lukas yakamstua sana Evans. Mapigo yake ya moyo yakaanza kumuenda kasi huku kijasho kikianza kumtiririka usoni mwake. Hakika toka alipo maliza chuo na kukosa ile mikopo ambayo wanapatia kwa ajili ya kujikimu, maisha yake yamekuwa magumu sana, kiasi cha kujikuta akipata hifadhi kwa rafiki yake Lucas ambaye naye kwa sasa amekabiliwa na majukumu mazito sana.
“Kaka wewe ni mwanaume. Ninakushauri, hembu jishikize kwenye vibarua vidogo vidogo japo upate vimiambili mia tatu vya kukukimu. Haya maisha ya kusema utafute kazi hizi ambazo mwisho wa siku unatoka hola, huoni kwamba una jicheleweshea malengo yako?”
Maneno ya Lucas hayakuweza kuleta matumaini wala faraja kwa Evan ambaye hatambui ni wapi atakapo kwenda. Kila akijaribu kulichanganua hili jiji la Dar es Salaam, hakika hana ndugu wa kuweza kuishi kwake.
“Evans, Evans”
“Naam kaka”
“Sijui umenielewa nilicho kuambia?”
“Yaa nimekuelewa kaka”
“Kuna ishu nyingi sana hapa mjini. Tazama mimi, ninaosha magari japo elimu yangu ni form four ila kidogo nina pata mia mbili mia tatu bro. Changamka hapa ni mjini usiamini sana kwenye maswala ya vyeti kaka.”
Evan taratibu akanyanyuka kitandani, akachukua begi lake la nguo pamoja na begi lake la mgongoni. Akafungua begi la mgongoni na kuhakikisha kwamba bahasha yenye vyeti vyake ipo salama. Alipo jiridhisha akalifunga na akalivaa mgongoni na kumtazama Lukas.
“Nashukuru kaka kwa kipindi chote ulicho weza kunivumilia kwa kukaa humu ndani. Nitaufanyia kazi ushauri wako”
“Nashukuru sana kaka. Kamata hii buku tano itakusaidia japo hata kwa chakula cha mchana huu na usiku”
Evans akautazaama mkono wa kulia wa Lukas unao mpatia kiasi hicho cha pesa. Kisha taratibu akaipokea na kuiweka mfukoni mwake.
“Asante kaka”
“Poa kaka ila nakuomba usinifikirie vibaya”
“Wala usiogope kaka, nimekuelewa na ninaelewa hali uliyo nayo ndugu yangu”
“Nashukuru sana kwa kuweza kulitambua hilo”
Lukas akanyanyuka kisha wakakumbatiana. Evans akatoka ndani ya chumba hichi. Akasimama eneo la nje la chumba hichi, akayatazama mazingira ya nyumba hii iliyopo, Tandale kwa tumbo. Taratibu akaanza kukatiza kwenye vichochoro vya nyumba hizi huku kichwani mwake akiwa na mawazo lukuki. Kila anavyo jaribu kumfikiria mama yake na mdogo wake wa kike walipo mkoni Kigoma, anashindwa kabisa kupata ujasiri wa kurudi kwao, kwani ufukara wa nyumbani kwao ndio umemfanya aweze kusoma kwa juhudi ili kujikomboa kwenye umasikini huo.
“Siwezi kurudi Kigoma”
Evans alizungumza mwenyewe huku akiendelea kukatiza kwenye vichochoro vilivyo jaa maji machafu, hii ni kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha kwenye jiji la Dar es Salaam. Evans akiwa katika chochoro moja, gafla akakutana na kundi kubwa la wahuni likiwa limebananisha dada mmoja aliye shika deli lililo jaa maandazi.
“Jamani maandazi yangu hayo ninauza musiyafanye hivyo”
Dada huyu alilalama huku akiwa amebananishwa ukutani, huku wahuni wengine wakiendelea kuyatafuna maandazi hayo bila hata ya kumuonea huruma.
“Tulia wewe. Kama hutaki tuyale tutakupa kifir** ambacho hujawahi kukipata toka uzaliwe”
Muhini mmoja alizungumza huku akimnyooshea panga la usoni dada huyo.
“Wewe mseng** una kodoa kodoa nini macho au unataka na wewe tuje kukupaku** hapo”
Muhuni mwengine alizungumza huku akimnyooshea Evans kisu. Katika maisha yake yote Evans amekuwa ni mtu ambaye hapendelei kushuhudia mwanamke ana nyanyasika mbele ya macho yake. Kushikwa shikwa kwa dada huyu, kukazirudisha kumbukumbu zake miaka kumi na mbili iliyo pita, kipindi akiwa na miaka kumi na mbili. Marehemu baba yake, alikuwa akimtesa sana mama yake na kumpa kipigo kizito mithili ya mwizi. Mzee Shika alisifika kwa ulevi na ubabe katika kijiji chao. Alikuwa ni mtu mwenye roho katili sana asiye jali utu wa mtu mwengine. Si mama yake tu aliye kuwa akishushiwa kipigo bali hata yeye mwenyewe alikuwa akibamizwa kisaswa sawa. Chuki na hasira juu ya mateso anayo yapata mama yake, yakatengeneza tabaka baya sanamoyoni mwa Evans dhidi ya baba yake.
Usiku wa siku moja kama kawaida, baba yake alirudi akiwa amelewa chakari. Kitendo cha mke wake kuchelewa kumfungulia mlango, ikawa ni kosa kubwa sana kwake. Alimkama mke wake na kuanza kumpiga bila ya huruma, huku mama Evans tumboni mwake akiwa ni mjamzito. Vilio vya mama yake akiomba msaada kwa watu vikamfanya Evans, kuvuta shoka alilo liweka chini ya kitanda chake na kutoka chumbani kwake huku akiwana hasira sana. Akaelekea kilipo chumba cha mama yake. Kwabahati nzuri akakuta chumba cha wazazi wake kikiwa wazi. Akaingia ndani na kumkuta mama yake akiwa amelala sakafuni huku akiendelea kushindiliwa mangumi ya uso na mzee Shika.
Shetani wa hasira na ujasiri, akamjaa Evans moyoni mwake. Akanyanyua kishoka hicho na kumpiga nacho baba yake usogoni na kikazama karibia nusu, na kusababisha damu nyingi sana kuanza kutapakaa ndani ya chumba hicho.
“Evan..s mwanangu umeniua”
Mzee Shika alizungumza huku akianguka chini na kupoteza uhai wake hapo hapo. Kofi zito alilo pigwa dada huyo muuza maandazi likamtoa Evans kwenye dibwi zima la mawazo. Akashuhudia jinsi wahuni hao wanavyo mchania nguo dada huyo huku wengine wakimshika shika maeneo ya siri pamoja na maziwa yake.
“MUACHENIII NIMESEMA”
Evans alizungumza kwa ujasiri na sauti ya juu. Wahuni hao wapatao sita, wakamtazama kwa sekunde kadhaa, kisha wakaanza kuangua kicheko cha dharau na kejeli.
“Mchekini huyu matak** ametokea wapi?”
Muhini mmoja alizungumza huku akianza kumsogelea Evans. Taratibu Evans akaweka begi lake chini na kujiandaa kwa lolote ambalo linaweza kujitokeza. Muhuni huyu aliye shika kisu mkononi mwake, akamvamia Evans, ila Evnas, hakuwa mjinga wala mzembe. Akamtandika ngumi nzito ya kichwa na kumfanya jamaa huyu kupepesuka na kuanguka chini. Wezake wakajawa na hasira na wakagairi zoezi la kumbaka mwana huyo. Wakamvamia Evans kwa pamoja na kuanza kupambaba naye. Wingi wao ukamfanya Evans ashindwe kabisa kuwakabili, wakamtembezea kichapo huku mmoja wao akimkita kisu cha tumboni na kumfanya Evans kuanguka chini.
“Oya mwana umeua. Msala msala huu.”
Mmoja wao alizungumza mara baada ya damu nyingi zilizo toka tumboni mwa Evans kumrukia mwilini mwake. Wakanza kuchanguka huku wakibeba mabegi yake yote mawili ya Evans, wakiamini kwamba ndani ya mabegi hayo wana weza kupata chochote kitu.
Mwana dada huyo akaanza kupiga kelele za kuomba msaada kwa watu kwani Evans anaendelea kutokwa na damu nyingi sana mwilini mwake. Wasamaria wema wakajitokeza na kuanza harakati za kumpa msaada Evans ambaye tayari amepoteza fahamu zake. Evans akafikishwa kwenye hospitali ya mwana nyamala.
“Amefanyaje?”
Nesi mmoja aliuliza huku akiwatazama watu hawa alio mleta hapa hospitalini.
“Amevamiwa na wahuni”
Dada muuza maandazi alijibu huku jasho na machozi yakimwagika.
“Muna pf3 ya askari?”
“Hatuna dada, tunaomba mutusaidie”
“Sasa hatuwezi kumtibu mgonjwa aliye vamiwa bila ya kibali kutoka polisi. Akitufia hapa hamuoni kwamba itakuwa ni hatari kwetu.”
“Dada nipo chini ya miguu yako nakuomba mumpokee. Nipo tayari kwenda kuitafuta hiyo sijui pp3 polisi. Ila nakuomba mumtibu huyu kijana”
Dada muuza maandazi alizungumza huku akimpigia nesi huyu magoti. Ushawishi wa watu wengine walio msaidia Evans, ukaulainisha msimamo wa nesi huyu na kujikuta akikubaliana nao na kuwaomba wahakikishe kwamba wana tafuta kibali cha matibabu kutoka polisi.
“Nashukuru nashukuru sana dada”
Dada muuza maandazi alizungumza huku akitoka baru ndani ya hospitali hii na kuelekea kituo cha polisi. Akafanikiwa kufika polisi na kuelezea hali nzima ya tukio lilivyo tokea.
“Mgonjwa yupo wapi?”
Afande Mwahila aliuliza huku akimtazama dada huyu.
“Mwanayamala hospital”
“Unaitwa nani dada?”
“Naitwa Magreth”
“Hao vijana walitumia silaha gani kuwashambulia?”
“Visu na mapanga”
“Hao ni panya road. Wanarudi tena ehee?”
Askari mwengine alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake. Magreth hakuweza kujibu jambo lolote zaidi ya kukaa kimya. Akaandikiwa ruhusa hiyo na kurudi hospitali ya Mwananyamala. Akamkabidhi nesi hati hiyo na matibabu ya Evans yakazidi kuendelea.
“Sasa mgonjwa amepoteza damu ya kutosha. Benk yetu ya damu hapa hospitalini ime kwisha. Kama unaweza kumchangia japo chupa moja itakuwa ni vizuri sana kwani kwa sasa mgonjwa yupo kwenye chumba cha upasuaji”
“Nipo tayari nesi”
“Basi jaza hii fomu hapa majina yako matatu. Kisha nifwate”
Magreth akasoma fomu hiyo ya kuchangia damu. Alipo ridhishwa na maelezo yaliyo andikwa kwenye fumo hiyo akajaza kilicho hitajika kisha akafwatana na nesi hiyo. Magreth akapimwa HIV na kwa bahati nzuri akakutwa yupo salama.
“Sasa unaweza kuchangia damu”
Nesi huyo alizungumza huku akianza taratibu za kutoa kiasi cha damu mwilini mwa Magerth.
“Ila mgonjwa atapona ehee?”
“Tuombe Mungu kwani kwa sasa yupo kwenye chumba cha upasuaji, madaktari wandelea na kazi ya kumuhudumia.”
“Ehee jehova, shusha muujiza wako mgonjwa aweze kupona. Damu ya Yesu kristo ikamuangazie”
Magreth alijikuta akipiga maombi na kumfanya nesi huyu kumshangaa.
“Mgonjwa ni nani yako?”
“Ni mpita njia”
“Mpita njia tu ndio una muombea hivyo. Mimi nilidhani ni kaka yako au ndugu yako kumbe mpita njia?”
Maneno ya nesi huyu yakauumiza moyo wa Magreth, ila hakuhitaji kumjibu chochote zaidi ya kuendelea kumlilia na kumuomba Mungu wake kimoyo moyo.
Madaktari wakazidi kujitahidi kwamba wana fanya upasuaji wa kukitoa kisu alicho chomwa Evans tumboni mwake. Upasuaji huo ukafanikiwa kuisha salama ndani ya masaa mawili. Evans akapelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi huku akiwa hajitambui kabisa.
“Nina weza kumuona mgonjwa wangu dokta?”
Magreth aliuliza swali huku akiwa amesimama nje ya chumba cha wagonjwa mahututi.
“Hapana kwa sasa huwezi kumuona kwani hali yake haijawa sawa”
“Ila anaweza kupona?”
“Hilo ni jambo la kumuomba Mungu, ila kwa sisi tumeweza kuikamilisha kazi yetu. Hatua inayo fwata ni hatua ya Mungu”
Dokta Mkama alimjibu Magreth kwa sauti ya upole huku akimtazama usoni mwake.
“Nashukuru”
“Nifwate ofisini kwangu”
Dokta Mkama na Magreth wakaongozana hadi ofisini na wakaka kwenye viti vilivyomo ofisini humo..
“Mgonjwa wako ana itwa nani?”
Magreth akaka kimya huku akimtazama dokta Mkama.
“Mbona kimya”
“Ahaa…simfahamu mgonjwa”
“Humjui? Mbona ume muhangaikia kwa kiasi kikubwa sana ikiwa mtu umtambui?”
“Bila ya huyu kaka mimi sasa hivi wala nisinge kuwa nimekaa mbele yako na kujibu maswali unayo niuliza. Alijitolea kupamabana na kundi la wahuni wa Panya Road, ili kuweza kuyaokoa maisha yangu.”
Magreth alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Okay nimekuelewa. Je upo tayari kubeba garama za kutibiwa kwa mgonjwa au kuna namna nyingine labda ya kuwasiliana na ndugu zake, wakakusaidia?”
Magreth akaka kimya huku akitafakari. Kwaufupi maisha yake naye ni magumu sana, biashara ya kutembeza maandazi mtaani ndio inayo mfanya aweze kuishi katika jiji hili la Dar es Salaam. Japo na uzuri wa kipekee alio barikiwa na Mungu, ila haitaji kuutumia uzuri wake huo kuwa kigezo cha kujipatia kipato kwa njia ya umalaya wa kujiuza.
“Nakusikiliza upo tayari tukuandike wewe ndio msimamizi wa mgonjwa huyu”
Magreth akamtazama daktari Mkama kisha akamuitikia kwa kutingisha kichwa, akimaanisha kwamba ame kubaliana nahilo.
“Sawa nitakuandikia garama zote hapa ambazo tumeweze kuzitumia katika kumuhudumia mgonjwa wako. Na tutakupigia bei ya yeye kulala ICU kwa siku moja”
“Sawa dokta”
Magreth akakaa kimya huku akimtazama dokta Mkama jinsi anavyo endelea kucharaza kwa peni karatasi iliyopo mezani mwake. Dokta Mkama alivyo maliza kuiandika karatasi hiyo, akaipitia kwa kuisoma kama kila alicho kiandika ni sahihi kisha akamkabishi Magreth. Taratibu Magreth akatupia macho yake kwenye karatasi hiyo. Moyo ukampasuka, kwani garama iliyo andikwa kwenye karatasi hiyo ni kubwa na toka kuzaliwa kwake hajawahi kumiliki kiasi hicho cha pesa .
ITAENDELEA
Haya sasa mambo ndio yameanza? Evans hali yake ni tete kitandani. Msaada wake wa mwisho ni Magreth ambaye naye uwezo wake ni duni, je ni wapi Magreth atakapo weza kupata kiashi hicho kikubwa cha pesa?Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 02
Ok
 
SIN 90

Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)

Age ……………………………………………………18+

Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA

“Ina tupasa kuhakikisha tuna lipa kisasi kwa watu hao. Tuna masaa matano hadi asubuhi tuwe tumesha ikamilisha kazi hiy…….”
Kabla ya Emmy hajamalizia sentensi yake, computer zote ndani hapo zikaanza kuzima na kuwaka na ndani ya dakika moja zikazima moja kwa moja na hapakuwa na hata moja iliyo waka.
“Mkuu masaa hayo matano uliyo toa hayato tosha”

Kijana mmoja alizungumza huku akimtazama Emmy usoni mwake.
“Kwa nini?”
“Data zote zilizo kuwa zina hifadhiwa kwenye hizi computer zime futwa hivyo hatuwezi kufanya jambo la ina yoyote”
Emmy akajikuta akitukana kwa hasira kwa maana ana tambua ni lazima wafanyakazi walio ondoka ndio wame sababisha jambo hilo.

ENDELEA

“Rudisheni basi hizo data. Una shangaa shangaa nini?”
Director Emmy alizungumza kwa kufoka sana na kumfanya kijana huyo kutingisha kichwa akimaanisha kwamba ana kwenda kuifanya kazi hiyo.

“Nitengenezee kahawa”
Emmy alimuambia mlinzi wake na akatoka ndani hapo. Vijana hao wakaendelea kufanya kila linalo wezekana na wakafanikiwa kurudisha mfumo mzima ambao ulikuwa ume futwa.

“Madam, tumerudi hewani”
“Safi, haya nahitaji kazi ianze kutafuta ni wapi yalipo makazi ya Al-Shabab ndani ya Somali na hata nje ya Somalia”
“Sawa madam”
Vijana hao wenye ujuzi mkubwawakendelea kuifanya kazi hiyo huku wakiwa makini sana. Ndani ya lisaa limoja wakafanikiwa kuona moja ya bandari bubu ikiwa inamilikiwa na kikundi hicho cha kigaidi cha Al-Shabab.

“Madam hii bandari ipo chini ya Al-Shabab”
“Safi, hembu vuta karibu hivyo video”
Emmy alizungumza na kijana huyo anaye shuhulika na maswala ya kuendesha ndege hiyo ndogo isiyo na rubani(drone) ambayo ina kamera yenye uwezo wa kurekodi kila jambo. Emmy akachukua simu ya mezani na kumpigia raisi Mtenzi.

“Muheshimiwa raisi kuna video tuna ituma hapo una weza kuitazama”

“Sawawa, naiangalia”
Emmy akakata simu na kuituma video hiyo ikulu kwa raisi Mtenzi.

***

“Una kwenda wapi mume wangu?”
Mrs Mtenzi alizungumza mara baada ya kumuona mume wake akishuka kitandani na kuanza kuvaa nguo ikiwa nib ado usiku

“Kuna oparesheni ina ongozwa hivyo nina hitaji kwenda kuisimamia”
“Mmmm sawa mume wangu”
Mrs Mtenzi alizungumza huku akimuonea huruma mume wake kwa maana kazi hiyo ni ya mateso sana, japo ni kiongozi wa nchi ila ana fanya kazi mara mbili na hata wafanyakazi wa kawaid. Raisi Mtenzi mara baada ya kumaliza kujiandaa katoka ndani hapo na kukutana na Jery sebleni.

“Huja lala?”
Raisi Mtenzi alimuuliza Jery.

“Hapana Dany kuna hii filamu nina imalizia kuitazama. Vipi wewe una kwenda wapi?”
“Tume gundua kwamba wale walio shambulia askari wetu ni Al-Shabab na hapa nina kwenda kutazama jinsi gani oparesheni inavyo endeshwa.”
“Al-Shabab ndio waliwashambulia?”
Jery aliuliza kwa mshangao mkubwa sana.

“Ndio mwanangu”
“Sawa baba”
Jery alizungumza kwa upole, baba yake akatoka ndani hapo. Akaungana na walinzi wake wawili ambao kazi yao ni kumlinda muda wowote ule. Wakaingia ndani ya chumba cha kuongozea oparesheni zote za kijeshi.

“Muheshimiwa raisi, video iliyo ingia sasa ni hiyo hapo”
Msimamizi mkuu wa oparesheni hizo alizungumza huku akimtazama raisi Mtenzi ambaye moja kwa moja akaa kwenye kiti chake. Akaanza kuitazama video hiyo iliyo rekodiwa kutoka juu angani ikionyesha jinsi bandari hiyo iliyopo chini ya kundi la Al-Shabab jinsi inavyo lindwa.

“Mkuu tuna uwezo wa kuishambulia kutokea juu, je uta turuhusu kufanya hivyo?”
“Ngojeni kwanza, niunganisheni na Emmy”
Hazikupita hata dakika mbili Emmy akaonekana katika moja tv iliyopo ndani hapo.

“Ndio muheshimiwa raisi”
“Hii video mume irekodi muda gani?”
“Kama dakika sana zilizo pita”
“Drone bado ipo eneo hilo?”
“Ndio muheshimiwa”
“Muna uhakika eneo hilo ni eneo sahihi la ngome ya Al-Shabab?”
“Ndio muheshimiwa”
“Hembu fanyeni upelelezi wa kutosha ili tufahamu kina biashara gani zinazo endelea eneo hilo”
“Sawa meheshimiwa”
Upelezi wa angani ukaendelea kufanyika huku wakishuhudia wana jeshi wa kikundi hicho cha Al-Shabab wakishusha wakishusha maboksi kwenye moja ya meli kubwa iliyo simamishwa eneo hilo.

“El del clasico?”
Raisi Mtenzi alisoma meli hiyo jinsi ilivyo andikwa.
“Hii meli ime tokea nchi gani?”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akiwatazama vijana wake.
“Ngoja niitafute”
Kijana mmoja alizungumza, akaitafuta meli hiyo na ndani ya muda mfupi akafanikiwa kufahamu imetokewa wapi.

“Meli hii imetokea ufarasa, ina milikiwa na tajiri mmoja De Rose Jr. Tajiri huyo ana shuhulika na maswala ya uuzaji wa madawa ya kulevya pamoja na silaha”
Kijana huyo alizungumza kwa kujiamini na kumfanya raisi Boaz kushusha pumzi.
“Kwa nini hajakamatwa kipindi chote hicho?”
“Ana tafutwa na nchi kubwa kama Marekani, Ufaransa wenyewe pamoja na Uingereza. Amekuwa akisaidia sana vikundi vya kigaidi kama Al-Shabab, Al-quida na Islamic state”
Kijana huyo alidi kutoa maelezo huku picha ya mmiliki wa boti hiyo ikionekana katika tv kubwa iliyomo hapo ndani.

“Ni wakati wa kuvuruga kila kitu”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akimtazama Emmy anaye onekana kwenye tv.

“Sawa muheshimiwa raisi”
Amri hiyo ya raisi Boaz, ikafanya Emmy kutoa maagizo kwa vijana wake anaye endesha drone hiyo, ambayo ina beba mabomu yenye uwezo wa kulipua eneo kubwa. Ndani ya muda mchache eneo hilo la bandari likaanza kulipuka huku likiteketeza meli hiyo pamoja na bandari nzima. Kila mtu ndani ya chumba hicho alishangilia kwa maana ni kazi iliyo leta mafanikio ndani ya muda mchache sana.

“Hongera sana muheshimiwa raisi”
Kila mmoja alimpongeza raisi Mtenzi.

”Nina imani mume fanya kazi kubwa sana. Muna weza kwenda kupumzika sasa”

Raisi Mtenzi alitoa ruhusa hiyo kwa vijana wake ambao ni zaidi ya masaa thelathini wapo ndani ya chumba hicho. Raisi Mtenzi akatoka ndani hapo na kurudi ndani kwake.

“Vipi kazi ime kwisha?”
Jery alimuuliza baba yake huku akimtazama jinsi anayo kaa kwenye moja ya sofa.

“Yaa tume fanya shambulizi la anga”
“Kwa hiyo mume waua?”
“Ndio tume waangamiza wote. Unajua nchi yangu huwa haipendi maswala hayo ya kigaidi, ila endapo mtu ata tushambulia, hakika hatuwezi kukaa kimya ni lazima tulipize”
“Daa ila baba kazi yako kweli ni ngumu, hivi ilikuwaje ukaacha uaskari na kuamua kuingia kwenye siasa?”
“Ni wito mwanangu. Hata wewe huko mbeeni una weza kuacha udaktari na ukaingia kwenye siasa. Marehemu babu yenu alikuwa ni mmoja wa wana siasa wazuri sana, hivyo ile damu yake ya uongozi bado ipo ndani yangu.”
“Ila baba kazi hii ni ngumu sana?”
“Ndio ni ngumu kwa maana unaongoza watu wanao jitambua na wasio jitambua hivyo kila mmtu ana mapungufu yake. Jambo la msingi ni kuhakikisha mtu una kuwa makini kwenye kila kitu unacho kifanya”
“Sawa baba, ila endapo Al-Shabab wakaamua kurudisha mashambulizi ita kuwaje?”
“Ndio ita kuwa ndio mwisho wao kwa maana tuta wafutilia mbali kwenye ramani ya dunia”
“Sawa vipi huyo mwenzako ana endeleaje?”
“Yupo safi tuna subiri tu siku yetu ya harusi”
“Safi sana, ila mwanangu pale ume weza kuchagua chombo”

“Kweli baba?”
“Yaa yule binti ni mzuri kila idara, jambo la msingi hakikisha una muheshimu na kumjali. Endapo uta poteza hivyo vigezo, ata tokea mjinga mjinga mmoja ata mchukua”
“Weee baba endapo atatokea mtu kufanya huo uzembe lazima afe”
“Mmm mimi nime kupa tu tahadhari. Usiku mwema”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akinyanyuka, akatoka ndani hapo na kumucha Jery sebleni akiendelea kutazama filamu yake.

***

Vilio na maumivu ya vikazidi kutanda kwenye bandari ndogo hiyo iliyopo kunisi mashariki mwa nchi ya Somalia. Mabomu yaliyo shambulia eneo hilo dakika ishirini zilizo pita, yame sababisha hasara kubwa sana kwenye eneo hilo huku idadi kubwa ya wana mgambo hao wa kikundi cha Al-Shabab wakipoteza maisha yao. Baadhi ya walio salia ni wale wachache walio wahi kujiursha kwenye maji.

“Mkuu tume shambuliwa”

Mmoja wa anamgambo walio salimika alizungumza kwa kutumia simu ya upepe huku akiwa ana elea elea ndani ya maji hayo.

“Imekuwaje?”
Mkuu wa kikosi hicho alizungumza kwa ukali sana.

“Hatujui, ni mashambulizi ya anga”
“Shiti”
Simu hiyo ikakatwa. Mkuu wa kikosi hicho aliyopo katika mji wa Mogadishu pamoja na mmiliki wa meli hiyo bwana De Rose Jr.
“Kuna nini kilicho tokea?”
De Rose Jr aliuliza huku akimtazama bwana Abuu Mohamed Mohamed aliye fura kwa hasira.

“Bandari yangu ya Rassini ime shambuliwa kwa anga”
“Nini? ina maana na meli yangu pia ime shabuliwa?”
“Sijapata habari acha niulize”
Abuu Mohamed Mohamed, akawasha redio yake ya upepo.

“Nahitaji kujua meli ya tajiri ipo salama. Over”
“Mkuu kila kitu kime shambuliwa. Over”
“Ina maana hakuna kilicho salia. Over”
“Ndio mkuu hakuna, yaani idadi kubwa ya watu wame kufa. Over”
Bwana De Rose Jr, mwili mzima ukaanza kumtetemeka kwa hasira kwa maana meli yake hiyo ime beba itu vingi sana tena vyenye thamani kubwa. Mwili mzima ukabadilika rangi na kutawaliwa na uwekundu, hata vinywaji walivyo kuwa wana kunywa havikuwa na thamani tena kwao.
Upande wa Bwana Abuu Mohamed Mohamed naye akazidi kujawa na hasira, ndevu nyingi zilizo mjaa usoni mwake zikazidi kuifanya sura yake kuwa mbaya akiwa katika hali ya hasira.

“Nahitaji kwenda Rassini sasa hivi nikaone meli yangu?”
De Rose Jr alizungumza kwa ukali sana.

“Unahisi ukienda sasa hivi una weza kuwa salama. Ehee?”
Abuu Mohamed Mohamed alifoka kwa hasira sana.

“Sijali, unajua ndani ya meli kuna nini kule?”
“Sijui ila kumbuka sasa hivi tupo kwenye wakati mgumu wa kushambuliwa. Wewe una maadui na mimi nina maadui una hisi ita kuwaje endapo tukajitoa sura zetu, si tuta uwawa?”
Abuu naye alizungumza kwa kufoka na ujasiri wa hali ya juu na kumfanya bwana De Rose Jr kutulia huku akitafakari ni jambo gani la kufanya kwa maana na yeye ana tafutwa karibia dunia nzima.

“Ina tupasa kutambua aliye fanya shambulizi hili ni nani”
Bwana De Rose Jr alizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo ya hasira.

“Wewe una wataalamu wengi, jaribu kuangalia ni nani ambaye ana husika na kuharibu bandari na meli yako”
Bwana De Rose Jr akamtazama Abuu Mohamed Mohamed kwa sekunde kadhaa kisha akatoa simu yake mfukoni na kumpigia kijana wake mmoja.
“Ingia ndani na laptop yako”
Akakata simu na kijana huyo akaingia ndani hapo.

“Meli yetu na bandari vime shambuliwa nahitaji kufahamu ni nani alite tushambulia.

“Sawa mkuu”
Kijana huyo kwa haraka akaitoa laptop yake kwenye begi lake la mgongoni, akakivaa miwani yake kubwa kidogo kisha akaianza kazi hiyo ya kutafuta mashambulizi hayo ya anga yametokea nchi gani. Haikuwa kazi rahisi sana kwake, ila kazidi kujitahidi kuhakikisha kwamba ana pata jibu sahihi la shambulizi hilo.

“Bado”
Bwana De Rose Jr aliuliza.

“Bado kidogo mkuu”
Kijana huyo alizungumza huku akizidi kujitahidi kuhakikisha ana pata jibu. Baada ya lisa moja la kuhangaika, kijana huyo akafanikiwa kupata jibu la ni wapi bomu hilo limetokea na akajikuta akistuka sana.

“Vipi umpata?”
“Ndio mkuu”
Bwana De Rose Jr na Abuu Mohamed Mohamed, wote kwa pamoja wakamsogelea kijana huyo na macho yao yote wakayapeleka katika kioo cha laptop hiyo.

“Drone iliyo shambulia eneo la bandari pamoja na meli yetu, imetokea nchini Tanzania na oparesheni hii imeendeshwa na serikali ya Tanzania”
Bwana De Rose Jr pamoja na bwana Abuu Mohamed Mohamed, wote wakajawa na mshangao kwa maana wote wawili hawana ugomvi wowote na serikali ya nchi ya Tanzania.

ITAENDELEA

Haya sasa bwana De Rose Jr pamoja na Abuu Mohame Mohamed, wamampata adui ambaye hawaja mkosea ni nini wata fanaya, usikose se hemu ya 91.
 
SIN 91

Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)

Age ……………………………………………………18+

Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA

“Vipi umpata?”
“Ndio mkuu”
Bwana De Rose Jr na Abuu Mohamed Mohamed, wote kwa pamoja wakamsogelea kijana huyo na macho yao yote wakayapeleka katika kioo cha laptop hiyo.

“Drone iliyo shambulia eneo la bandari pamoja na meli yetu, imetokea nchini Tanzania na oparesheni hii imeendeshwa na serikali ya Tanzania”
Bwana De Rose Jr pamoja na bwana Abuu Mohamed Mohamed, wote wakajawa na mshangao kwa maana wote wawili hawana ugomvi wowote na serikali ya nchi ya Tanzania.

ENDELEA

“Una uhakika ni Tanzania!!?”
Bwana De Rose Jr aliuliza kwa mshangao mkubwa sana.

“Ndio mkuu nina uhakika wa asilimia mia moja na zaidi”

“Abuu una bifu lolote na Tanzania?”
“Hapana sina sijawahi kufanya shambulizi lolote kwenye nchi hiyo. Sasa nina shindwa kujua kwa nni imekuwa hivyo”
“Ila raisi wa Marekani si alikuwepo kule miezi ulio pita?”
“Ndio”
“Kuna mkono wa Mmarekani kwenye hili tukioa”
“Kama kuna kumkono wa Mmarekani ni lazima tulipieze kiasi?”
“Wakuu hapa Wamarekani hawahusiki, hili jambo limefanywa na serikali ya Tanzania wao peke yao na hawajashirikiana na hata nchi yoyote”
“Ni lazima tulipize kisasi na kisasi tutakacho kifanya wata juta kwa nini wameivuruga bandari yangu.”
“Ni kweli Abuu ila kama wame weza kutushambulia kwa anga ina bidi kuwa mkini sana kwa maana nina imani kwamba wata kuwa wame jikua vizuri kwenye maswala ya ulinzi kwa kutumia tecnolojia”
Bwana De Rose Jr alizungumza huku akimtazama Abuu Mohamed Mohamed usoni mwake.

“Ni kweli. Kijana hembu fwatilia Tanzania kuna tukio gani ambalo lina kwenda kutokea katika siku hizi za karibuni?”
“Dakika moja”
Kijana huyo mwenye asili ya kihidi alizungumza huku akiendela kuminya minya batani za laptop yake.

“Mwezi ujao tarehe tisa kuna harusi ya mtoto wa raisi Chinas Mtenzi, ana muoa mtoto wa nabii Sanga, mmoja wa watumishi wa Mungu wakubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki”
“Harusi ya nini tuna taka tukio kibwa ambalo tukipiga, tuna piga kweli”
Bwana De Rose Jr alizungumza huku akimtazama kijana wake.

“Hapana hilo hilo tulio la harusi ndio la kuonyesha kwamba sisi hatupendi kochokozwa. Hilo jambo la shambulizi ni lazima liwe lime idhinishwa na raisi. Hakuna kitengo cha ulinzi kinacho weza kufanya kazi pasipo kupata idhini ya raisi.”
“Eti ehee?”
“Ndio, kama ni raisi ame idhinisha basi ni lazima ata lipa kwa hili. Nita hakikisha kwamba wana lipa kwa hili jambo”
Abuu Mohamed Mohamed alizungumza kwa sauti ya msisitizo na wakakubaliana na bwana De Rose Jr kuhakikisha wana fanya tukio kubwa kwenye harusi ya mtoto wa raisi Mtenz.

***

“Hei amka”
Evans akakurupuka kitandani. Akamtazama jini ambaye ni mwana dada ambaye kwa sasa ndio mtu wake wa karibu.

“Begi hilo hapo lina pesa dola milioni moja. Nenda benki kaweke na kufungua akaunti, Weka hiyo pesa kisha lipia ile ardhi”
“Sawa, ila nikiulizwa hizi pesa nime toa wapi?”
“Hakuna mtu wa kukuuliza ikiwa benki wao wanacho hitaji ni pesa na sio kuuliza maswali watu”
“Ila dola milioni moja kwetu ni bilioni of shilingis”
“Evans tamuba kwamba upo na nani na hiyo pesa imetoka wapi. Fanya kama niliyo kuambia. Umenielewa?”
“Nimekuelewa. Ila nahitaji kufahamu jina lako?”
“Halito kusaidia kitu ila kitakacho kusaidia ni wewe kufwata utaratibu na kile nilicho kueleza sawa”
“Sawa mkuu”
“Badae”
Jini huyo akapotea ndani hapo. Evans akafungua begi hilo na hakuamini kuona pesa hizo nyingi za kimarekani ambazo kwenye maisha yake yote hajawahi kuzimiliki. Akatoka nje ya hoteli hiyo, akakodisha taksi na kuelekea moja kwa moja kwenye benk Bacrays. Akafungua akaunti na kuweka kiasi hicho chote cha pesa. Baada ya kukamilisha hatua hizo za kibenki akalipia kiasi hicho cha kuinunua ardhi, akampigia dalali na akafika benki hapo na moja kwa moja wakaelekea katika ofisi za mkuu wa wilaya. Evans akajaza fomu za umiliki wa eneo hilo na akakabidhiwa hati yake kuonyesha yeye ndio mmiliki.
“Nashukuru sana”
“Tunashukuru sana na wewe kwa maana tuna penda wawekezaji wa ndani kama wewe”
Mkuu wa Wilaya alizungumza kwa furaha. Dalali akaingiziwa kiasi chake kama kazi yake aliyo ifanya. Evans akaelekea kwenye moja ya show room za magari, akanunua gari ndogo aina ya Toyota ist.

“Kata nisaidia kwenye mizunguko yangu”

Evans alizungumza na muuzaji huyo huku wakikabidhiana pesa za malipo. Evans akarudi hotelini na kuanza kuperuzi kwenye mitandao huku akitafuta kampuni ya utengenezaji wa majengo makubwa. Akafanikiwa kupata kampuni mbili, moja ikiwa ina tokea nchini China na nyingine ikiwa ina tokea nchini Ujerumani.

Akaendelea kupitia sifa za makampuni hayo makubwa ambao yana fanya kazi nzuri za kujenga majengo makubwa na imara duniani.

“Kampuni hiyo ya kijerumani ndio nzuri”
Sauti ya dada huyo ambaye ni jini ika mstua sana Evans.

“Mbona una kuwa una stuka stuka sana au bado huja zoea?”
“Kuzoea nime zoea, ila sio kwa kunistusha hivyo”
“Ahaa sawa. Wasiliana nao na uwatumie picha za huo mchoro mukubaliane bei kisha watakuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuanza kazi”
“Je nina paswa kuwalipa kwanza?”
“Hapana hakuna hajaya kuwalipa kwanza. Waje waone eneo kisha ndio maswala ya kulipana yata anza”
“Sawa”

“Kesho nahitaji ununue nyumba uilete familia yako hapa Dar es Salaam”
“Nita fanya hivyo mkuu”
“Siku nje”
Jini huyo akaondoka na kumfanya Evans ajifikirie kwa muda kisha akanakili namba za mawasiliano za kampuni hiyo kisha akaanza kuwasiliana nao.

***

“Magreth acha kuwa mnyonge. Huja kula chochote toka asubuhi. Nakuomba rafiki yangu, kunywa hata huu uji wa maziwa basi”
Josephine alizungumza kwa sauti ya kumbembeleza huku akimtazama Magreth aliye kaa kitandani kwake huku akionekana kujawa na mawazo mengi sana.
“Mage”
“Mmmm”
“Kula kidogo rafiki yangu”
“Jose sijisikii kula chochote”
“Najua hujisikii kula ila kunywa huu uji nilio kuandalia. Uta pata vidonda vya tumbo rafiki yangu”
Josephine aliendelea kuzungumza kwa unyonge wa hali ya juu. Taratibu Magreth akachukua bakuli hilo la uji, akaanza kunywa taratibu huku akimtazama Josephine aliye anza kutabasamu.
“Usiku uliiomba?”
“Ndio”
“Ume pata nini?”
“Sijapewa jibu la aina yoyote, laiti kama ninge pata jibu basi ninge kueleza”
“Mmmmm sawa”
“Leo huto kwenda kazini?”
“Hapana, nahiaji kufikiria baadhi ya mambo”
“Mambo gani rafiki yangu”
“Nita kuambia rafiki yangu kichwa changu kikikaa sawa”
“Haya ngoja nikiache”
Josephine akashika gongo lake linalo msaidia katika kutembea, akatoka ndani hapo. Magreth akaweka bakuli hilo la uji mezani kisha akashuka kitandani. Akaitafuta namba ya Tomas kwenye simu yake kisha akampigia, simu ya Tomas ikaanza kuita kisha ikapokelewa.

“Upo wapi?”
“Nyumbani vipi ume badilisha mawazo yako?”
“Hapana, sinto weza kuifanya kazi hiyo”
“Sawa”
Magreth akata simu, akaoga haraka haraka, akajiandaa na kutoka ndani hapo.
“Wapi una kwenda”
“Kuna sehemu nina elekea”
Magreth akaingia kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi sana. Akafika kwenye nyumba yenye vifaa ambavyo ana amini ata vitumia katika kazi yake. Akavua shatu alilo kivaa na akabaki na siridi pamoja na suruali. Akachukua upanga mrefu na taratibu akaanza kufanya mazoezi ya kuutumia upanga huo. Hasira na roho ya kisasi kiliyo jaa moyoni mwake, ikamfanya Magreth kuzidi kufanya mazoezi hayo kwa nguvu zake zote. Magreth akaendelea kufanya mazoezi ya vifaa tofauti tofauti, huku kila anavyo zidi kujifua ndivyo jinsi anayo iona sura ya nabii Sanga mbele yake.

“Lazima nikuue”
Magreth alizungumza huku akicheza na cheni ndefu ambayo kwa mbele ina kisu kikali sana ambacho kime jikunja kidogo. Mazoezi yake yakachukua masaa mawili na nusu, alipo hakikisha ame tosheka, akafungia vifaa hivyo kwenye sanduku lake kisha akaondoka eneo hilo.

***

“Aisee jana baba kawachakaza Al-Shabab”
Jery alizungumza kwa furaha huku akiwa na Julieth kwenye moja ya bustuni katika jumba la nabii Sanga.
“Kivipi?”
“Juzi si nilikuambia kuna askari wame vamiwa na kuuwawa?”
“Ndio?”
“Jana usiku baba ame amelipiza kisasi kwa kuwashambulia, yaani hapa nina amani aisee”
Jery alizidi kumsifia baba yake pasipo kujua kwamba wamecheza pata potea.
“Duuu mpe hongera sana baba”
“Usijali zime fika mke wangu”
“Ila Jery mume wangu, una jua hupaswi kuniona hadi siku ya harusi”
“Ahaa wapi, tambua siwezi kukaa pasipo kukuona wewe mke wangu”
“Nallijua hili, tume bakisha wiki mbili tu mume wangu. Kuanzia hapo nita kuwa ni wa kwako daima”
“Nalitambua hilo, vipi baba na mama wapo ndani?”
“Wame toka mara moja, si una jua siku zime baki chache hivyo wana kuwa wapo bize bize sana”
“Ahaa tuna weza tuka toka leo”
“Hapana Jery, sipaswi kutembea tembea mume wangu”
“No baby kuna sehemu nahitaji kukupeleka?”
“Wapi?”
“Wewe twende”

Julieth akajifikiria kisha akakubaliana na ombi hilo. Wakaondoka eneo hilo huku walinzi wakiendelea kuhakikisha wana kuwa salama.

“Niambie mume wangu tuna kwenda wapi?”
“Wewe twende”
Julieth ika mbidi kuwa mpole tu. Simu ya Jery ikaanza kuita, akaitoa mfukoni mwake na kukuta ni simu ya mama yake.

“Mom”
“Upo wapi?”
“Nina kwenda Kigamboni mara moja mama yangu”
“Kufanya nini tena Jery”
“Mama nipo na Julieth tuna kwenda kupata chakula cha mchana”
“Sawa kuwa makini”
“Usijali mama yangu”
“Kumbe tuna kwenda kupata lunch”
“Yes kuna chakula maalumu nime kianda kwa ajili yako”
“Mmmm sasa kwa nini hukunieleza?”
“Nime ona nikufanyie suprize mke wangu”
Wakafika katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano. KX Royal. Walinzi kumi wakashuka kwenye gari zoa mbili na wakaimarisha ulinzi, walipo hakikisha eneo hilo lipo salama mmoja, wao akafungua mlango wa gari alilo panda Jery na Julieth. Wakashuka kwenye gari hilo, wakaingia ndani ya hoteli hiyo na moja kwa moja wakaelekea katika eneo walipo andaliwa chakula hicho.

“Waoo ume juaje nina kipenda hichi chakula”
Julieth alishangaa sana mara baada ya chakula hicho kilicho kiitwacho kishumba kuwekwa hapo mezani.
“Yaa nilijua tu utakuwa ume kimiss hichi chakula”
“Ni kweli mume wangu, nina miaka mingi sana sija kila”
Julieth alizungumza huku akiwa amejawa na uchu wa kula chakula hicho.
“Samahani huruhusiwi kuingia eneo hili”
Mmoja wa walinzi alimuambia Evans ambaye ana hitaji kuingia katika eneo la mgahawa wa hoteli hiyo.
“Ahaa samahani kwani kuna nini?”
Evans aliuliza huku akitazama tazama eneo la ndani, akashangaa sana kuona eneo zima la mgahawa huo kukiwa na watu wawili tu, mwanaume na msichana huko watu wengine wote wakiwa hawapo. Evans akamkazia macho msichana huyo aliye mpa mgongo. Mlio wa simu ya Evans uka mfanya Julieth kugeuka nyuma kwa maana hata simu yake ina mlio wa aina hiyo. Macho ya Evans yakagongana na macho ya Julieth na kumfanya astuke kidogo kwa maana Julieth anavyo tambua kwamba Evans amepoteza kumbukumbu zake mara baada ya mateso makali aliyo patiwa na watu ambao hadi sasa hajaweza kuwafahamu.

ITAENDELEA

Haya sasa Julieth ame muona Evans na Evans ame muona Julieth amaye yupo na mume wake aliye tuma vijana wake kumtesa ni nini kita endelea? Usikose sehemu ya 92.
 
Back
Top Bottom