Brodre
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 2,585
- 1,771
- Thread starter
- #161
SIN 78
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
“Wanatupatia dili hilo ila wanacho kihitaji wao ni kujua ujuzi tunao tumia katika kutengeza chakula chetu kwa maana ni kitamu sana na endapo wakifahamu basi wana weza kumaliza mkataba na sisi na tukarudi katika maisha ya wateja wetu”
“Sasa niwajibu nini bosi”
“Waambie kwamba chakula chetu kina pikwa hapa. Atakaye hitaji kuja kula aje asiye hitaji kuja aondoke ndio maana nime fungua mgahawa. Sawa Juma?”
Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama Juma usoni mwake.
“Ndio bosi nime kuelewa”
Juma alijibu kwa unyonge kwa maana kile alicho kuwa ana kitarajia sicho alicho jibiwa na bosi wake.
ENDELEA
“Safi kama ume nielewa”
“Ila bosi nina kuomba uweze kufikiria mara mbili hili dili. Una jua wame tuambia wata tulipa kiasi gani kwa wiki?”
“Kiasi gani?”
“Dola laki moja, hivyo kwa mwenzi tuta kuwa na dola laki nne sawa na milioni mia nane za Kitanzania kwa wakati huu”
Magreth macho yakamtoka kwa maana kiwango hicho cha pesa ni kikubwa sana.
“Bosi haya ni maisha na hii ni bahati. Kuna makampuni mangapi yanayo pika chakula yameachwa na kufwata sisi kwenye mgahawa wetu. Hembu jaribu kulitazama hilo bosi.”
“Juma acha utani?”
“Sikutanii bosi nina kueleza ukweli. Hii ni namba ya mshauri wa balozi wa Marekeni, ameniachia leo baada ya kupata chakula chetu hapa”
Juma alizungumza huku akimuonyesha Magreth kadi ndogo yenye ndani ya mshauri huyo wa balozi wa Marekani nchini hapa Tanzania.Kadi hiyo imeandikwa jina la mshauri huyu, namba zake za simu na ofisi anayo ifanyia kazi na ina dhihirisha kweli ana fanya kazi katika ubalozi huyo wa Marekani.
“Wewe ni bosi wangu, natambua kwenye maisha yako siku zote una wazia kuwa tajiri mkubwa ili uweze kuwa katika orodha ya watu wenye pesa nyingi hapa Tanzania. Sasa huu ndio wakati wako kufanikiwa bosi”
Ushawishi wa Juma ukazidi kumuingia Magreth akilini mwake.
“Hembu niambie ilikuwaje kuwaje?”
“Kama unavyo jua hali halisi iliyopo hapa nchini. Raisi wa Marekani yupo hapa nchini. Wamarekani kwa sasa wapo wengi sana, hivyo walikuja hapa na wakaanza kupata chakula cha jioni. Walivutiwa sana na chakula chetu, wakazungumza biashara na mimi nami nimekuletea ili uwe muamuzi wa mwisho”
“Okay nime kubali, huyo muhisika ana hitaji tuonane naye lini?”
“Hata leo yupo tayari”
“Basi mpigie ili kama ni kuonana naye tuweze kukutana”
“Sawa”
Juma akampigia kiongozi huyo, ila simu yake haikuweza kupokelewa, akarudi kwa zaidi ya mara tatu ila majibu yakwa ni hayo hayo.
“Kama hapokei basi ata pokea baadae kwa maana nahisi wata kuwa kule kiwandani”
“Yaa ni kweli nime kumbuka”
“Alafu acha nikupe namba yangu ya benki pasa ikifikia mchana una kwenda kuzituma benki sawa”
“Sawa bosi”
Magreth akampatia Juma namba ya akaunti yake ya benki kisha akaelekea jikoni kumuandalia Josephine chakula cha jioni.
***
Nabii Sanga mara baada ya kutoka kwenye sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha magari nchini Tanzania. Wakaelekea katika mji wa Bagamoyo, wakapata chakula cha usiku katika hoteli moja ya kitalii ambayo nabii Sanga huwa ana penda sana kwenda kupata chakula akiwa katia mji huo.
“Chakula chao ni kitamu sana”
Julieth alizungumza huku akiendelea kula.
“Umekipenda ehee?”
“Ndio baba nime kipenda”
“Siku ya kwanza tulipo kuja hapa na baba yako nili mshawishi tuwachukue hawa wapishi wakatupike kule kwenye hoteli yetu”
“Ikawaje mama?”
“Walikataa. Wapishi wa hapa wana jali sana utu kulipo pesa”
“Mmmm labda muliwawekea dau dogo”
“Hapana tuliwapa ofa nzuri ila walishindwa kutuelewa, basi hatukuwa na namna”
“Bado muna wahitaji?”
“Ndio, una jua katika biashara yoyote ni lazima mtu uhakikishe kwamba una cheza rafu li mradi mambo yako yaweze kwenda”
“Ni kweli baba, ila nipeni siku kadha, nita washawishi na nita waondoa wote hapa”
Nabi Sanga akatoa simu yake iliyopo mfukoni na kuipokea.
“Ndio”
“Munaweza kuja”
“Haya”
Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza maneno hayo ya mkato mkato akakata simu na kuirudisha mfukoni.
“Baba ni kina nani hao wana kuja?”
“Ni vijana wangu, wana kuja kutuchukua”
“Tuna kwenda wapi kwani?”
“Kwenye eneo ambalo ndio kikao leo kita fanyika kuanzia saa sita usiku. Tambua una kwenda kuwa mrithi wa mtandoa wetu, hivyo akili yako ina kupasa kuwa active zaidi ya hivi sasa”
“Sawa baba”
Majiria ya saa nne usiku, gari moja nyeusi aina ya BMW X5 ikafika katika eneo hilo la hoteli.
“Simu na vitu vyote vya mawasiliano tuviache kwenye gari”
Nabii Sanga alimuambi Julieth na mke wake. Wakaweka simu zao pamoja pochi zao ndani ya gari lao, kisha wakafunguliwa mlango na kijana mrefu aliye valia suti nyeusi na wakaingia katika gari hilo kisha wakaondoka hotelini hapo. Wakafika pembezoni mwa bahari na wakashuka kwenye gari hilo na wakapokelewa na vijana wengine wawili ambao nao wame valia suti nyeusi. Wakapanda kwenye boti ya ndogo na wakaanza safari.
“Mbona una tetemeka?”
Mrs Sanga alimuuliza Julieth aliye jikunyata.
“Baridi”
“Mpatie mwanangu koti”
“Sawa mkuu”
Kijana huyo akavua koti lake na kumkabidhi Julieth na akalivaa. Safari ya boti hiyo inayo kwenda kwa kasi, ikawachukua masaa mawili kufika katikati ya bahari na wakakuta meli moja kubwa ambayo ina lindwa kwa ulinzi mkali sana.
“Hii meli ni mali yetu mwanangu”
“Hii meli?”
“Ndio mwanangu”
Nabii Sanga alizungumza huku akitabasamu. Wakafika eneo la kushukia, wakapokelewa na vijana wengine ambao mikononi mwao wana bunduki. Vijana hao wakamsalimia nabii Sanga kwa kuinamisha kichwa chini. Julieth akazidi kushangaa uzuri wa meli hii kubwa na nzuri.
“Baba acha utani una taka kuniambia kwamba hii ni meli yetu?”
“Ndio mwanangu mbona huamini?”
“Na hawa watu?”
“Hawa ni walinzi wetu ambao ni wa siri sana na wana tulinda kwa siri sana ndio maana na umaarufu wangu wote huja wahi kuniona nikiongozana na walinzi kama watu wengine maarufu”
“Ahaaa…”
“Sisi na baba yako kuna mambo mengi ya siri ambayo taratibu utaanza kuyajua.”
Wakaingia katika chumba kimoja kilicho tengenezwa vizuri.
“Mkuu nguo zenu zipo tayari”
Dada mmoja mwenye asili ya Russian alizungumza huku akimtazama nabii Sanga usoni mwake.
“Nashukuru Lana”
Dada huyo akainamisha kichwa chake chini kisha akatoka ndani hapo.
“Badilisheni nguo haraka, kikao kina karibia kuanza”
Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza hivyo akatoka ndani hapo. Julieth na mama yake wakabadilisha nguo zao kwa haraka kisha nabii Sanga naye akaingia ndani ya chumba hicho na kuvaa nguo zoa ambazo ni suti nyeusi tupu. Wakaelekea katika ukumbi mkubwa ambao upo ndani ya meli hiyo. Julieth akashangaa sana kukuta watu wa mataifa mbalimbali, ambao mara baada ya kumuona nabii Sanga waka inamisha vichwa vyao chini ikwia ni ishara ya kumpa heshima. Mrs Sanga na mwanaye nao wakainamisha vichwa vyao chini wakiashiria kumpatia heshima kubwa nabii Sanga. Nabii Sanga mara baada ya kukaa kwenye kiti chake watu wote nao wakakaa. Kikao hicho cha siri ambacho kina wahusisha wauza madawa ya kulevya wakubwa sana kikaanza. Nabii Sanga akawatambulisha Julieth na akatangaza kwamba kuanzia hapo yeye ndio ata kuwa kiongozi wa muunganiko huo. Japo ni jambo la mshangazo kwa wengi, ila wote waka subiria kuona ni jinsi gani Julieth ata zungumza. Julieth akasimama na akapishwa kiti na nabii Sanga.
“Nita kuwa mara tatu na alicho kifanya baba yangu. Nita hakikisha tuna kuwa invisible na dunia nzima tuta itawala. Asanteni”
Julieth alizungumza kwa kujiamini hadi yeye mwenyewe akajishangaa. Watu wote wakaanza kupiga makofi kwa maana ujasiri alio uonyesha Julieth ume zaa imani kubwa kwa watu hao.
***
Siku zikazidi kusonga mbele na hali ya Evans ikazidi kuimarikia. Kwa wiki tatu na siku mbili alizo kaa nyumbani kwa mzee Msese, zika mfanya afahamu mambo mengi sana katika milima hiyo. Siku kadhaa Evans aliweza kuondoka na mzee Msese kwenye milima kutafuta dawa kwa ajili ya wateja mbalimbali wanao fika katika milima hiyo kwa ajili ya kutibiwa.
“Evans”
Kwa mara ya kwanza Evans alishangaa baada ya mzee huyo kumuita jina lake. Siku zote wame kuwa wakizungumza kwa kupitia Dada ambaye ana fahamu lugha ya kiswahili na kiruguru.
“Ndio mzee wangu.”
“Kwenye maisha yako ume kuwa ni mtu wa kudhulumiwa haki zako si ndio?”
“Ndio mzee kumbe una weza kuzungumza kiswahili?”
“Ndio nina tambua tena vizuri sana.”
“Kwa nini kipindi hicho chote ume kuwa ukizungumza kiruguru?”
“Nilihitaji kukujua vizuri na sasa nina kujua vizuri sana”
Mzee Msese alizungumza huku akimtazama Evans usoni mwake.
“Ahaa”
“Ndio. Nyota yako ni kubwa sana na ndio inayo kufanya uweze kuwa na ulinzi mkubwa kiasi kwamba hadi mamba walishindwa kukutafuna kwenye ule mto. Nimekaa kwenye hii milima sasa ni mwaka wa stini na sita, sijawahi kuona binadamu wa kawaida anaye ingia kwenye ule mto pale na kushindwa kumtafuna mtu”
“Mmmmm”
“Ni kweli, wewe ndio binadamu wa kwanza kabisa kutoka ukiwa pale salama na tena mamba waliweza kukaa mbali na wewe. Nita kufanyia dawa ambayo nyota yako isiweze kuchukuliwa na watu wabaya”
“Sawa mzee wangu. Na nyota huwa zina chukuliwaje?”
“Ni mambo ya kitaalamu hayo mwanangu. Ila leo twende nika kuonyeshe kitu”
Mzee Msase alizungumza. Wakandoka nyumbani hapo na Evans na wakaelekea kwenye milima mikubwa kabisa iliyopo jirani na wanapo ishi.
“Mzee wangu hivi huku milimani kuna watu wana ishi?”
“Hapana, huku ni sisi tu ndio tuna ishi tena tuna ishi kutokana kukubaliwa na mizimu ya milima hii”
“Kuna mizimu?”
Evans alizungumza kwa mshangao mkubwa sana.
“Ndio achilia mizimu peke yake, ila kuna hadi majini wakubwa wana ishi humu. Ndio maana binadamu wa kawaida akiingia humu hawezi kutoka”
“Mmmm mzee wangu una niogopesha.”
“Usiogope kwa maana kuna habari nzuri kwako”
“Habari gani?”
“Mizimu ime weza kukukubali ndio maana una ishi kwa amani na furaha ndani ya msitu huu. Ila inge kuwa sio hivyo unge kuwa umesha potwezwa siku nyingi sana.”
“Mmmm”
Evans alizungumza huku akizidi kumfwata mzee Msese. Wakafika katika moja ya pango kubwa.
“Tuna ingia humu ndani, ila kabla ya kuingia ina bidi ujichane kidogo kwenye mkono wake na umwage damu yako hapa chini”
Maneno ya mzee Msese yaka mstua sana Evans na kujikuta akizidi kujawa na woga.
“Kwa nini?”
“Humu ndani kuna utajiri wako, ila una lindwa na majini na wewe ndio mtu wa pekee unaye weza kuchukua hadihina hiyo.”
Evans macho yakamtoka, akatazama kisu anacho pewa na mzee Msese kisha taratibu akakipokea huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana kwani hakutarajia kama safari hiyo inaweza kufika hapo walipo fika.
“Mzee ume sema kwamba humu ndani kuna majini?”
“Ndio kuna majini na hakuna mtu aliye wahi kuingia humo ndani.”
“Hata wewe hujawahi kuingia ndani humo?”
“Ndio sijawahi kuingia. Ila wewe ndio una pawa kuingia na ukitoka humo hakika wewe ume kuwa tajiri”
Evans akazidi kushangaa huku akiwa na wasiwasi mwingi sana.
“Evans huu ni utajiri wako ingia ndani humo”
Mzee Msese alizidi kumshawishi Evans. Evans akafikiria maisha aliyo pitia kutoka kwa Magreth hadi Julieth. Katika mahusiano hayo yote hakuweza kuambulia hata biashara ya kuuza machungwa.
‘Liwalo na liwe ni lazima niwe tajiri’
Evans alizungumza kimoyo moyo kisha akajikata kiganja chake cha mkono wa kulia kisha akaanza kumwaga damu eneo alilo onyeshwa na mzee Msese na taratibu akaanza kuingua ndani ya pango hilo ambalo lina giza totoro.
ITAENDELEA
Haya sasa Evans ameingia ndani ya pango hilo je ata kuwa tajiri kama alivyo ambiwa na mzee huyo msese.? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose se hemu ya 79.