Riwaya: SIN

Riwaya: SIN

SIN 65


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188





ILIPOISHIA


“Tuna shukuru sana nabii Sanga na mama kwa kupokea ombi letu. Sasa yaliyo baki hapa ni vijana wao wenyewe wakutane, waridhiane na watuletee maamuzi yao walipo fikia basi sisi tuta yafanyia kazi”
“Sawa muheshimiwa, sisi tuta muandaa binti yetu kisha tuna mualika kijana wenu afike kuzungumza naye”
Nabii Sanga alizungumza kwa kujiamini ingali anatambua fika kwamba Julieth ana mahusiano na Evans na mbaya zaidi ni kwamba Julieth ameamua kuondoka nyumbani na kuanza maisha yake na Evans.


‘Lazima huyu panya nimuue kwa maana hawezi kuisukumia mbali bahati hii iliyo kuja kwenye familia yangu’


Nabii Sanga aliwaza huku akilini mwake akiiona sura ya Evans ambaye ana kisasi naye kikubwa sana.





ENDELEA


Wakamaliza kupata chakula cha mchana, kutokana raisi Mtenzi ana ratiba nyingine za kiofisi ikamlazimu kuagana na nabii Sanga kisha akandoka hapo nyumbani kwake.


“Tuna weza kuzungumza na Jery?”
“Ndio hakuna shaka kabisa”
Mrs Mtenzi akaondoka ndani hapo na baada ya muda akarudi akiwa ameongozana na mwanaye. Nabii Sanga na Jery wakatoka ndani hapa na kuanza kutembea kwenye bustani kubwa zilizopo katika eneo hilo la Ikulu.


“Mwanangu una mpenda?”
“Yaa nina mpenda sana mzee”
“Huwa siku zot nina ogopa kumuozesha mwanangu kwenye familia za aina hii alafu akanyanyasika hapo baadae”
“Hapana baba yangu. Nina apa kwa jina la Mungu wangu, huto jutiaa kuniozesha mwanao. Nitahakikisha ana kuwa na furaha kwenye maisha yake yote hadi kufa. Pia Julieth ana nitambua mimi vizuri kwani huwa sina mambo ya ajabu ni mwanaume ambaye nina jua nini maaa ya mwanamke”
“Aha…Nafurahi kusikia hivyo.”
“Pia nitakusaidia kwa baba kukupa japo nafasi katika serikali yake”
“Hapana bwana mimi ni mtumishi wa Mungu hivyo mambo ya siasa huwa siyawezi kabisa”
“Je mama akipewa nafasi ya mbunge mteuliwa hapo itakuwaje?”
“Mmmm labda nizungumze naye kwa maana siwezi kumsemea maamuzi yake”
“Basi zungumza na mama.”
“Mara ya mwisho kuzungumza na Julieth ni lini?”
“Masaa mawili yaliyopita?”
“Masaa mawili?”
“Ndio baba mbona una stuka?”
“No sijastuka”
“Yaa nimezungumza na tupo vizuri katika upande huo”
“Sawa mwanangu nimefurahi kuzungumza na wewe”
“Nashukuru sana mzee wangu”
Nabii Sanga na Jery wakarudi ndani na kuwakuta mrs Sanga na mrs Mtenzi wakizungumza na kucheka kwa furaha sana. Urafiki ulio anza kutengezwa kwenye familia hizi una zidi kukua baada ya pendekezo hilo la raisi mtenzi. Nabii Sanga na mke wake wakaaga na kuondoka eneo hilo la Ikulu huku wakiwa na furaha kubwa sana.


“Mume wangu itakuwaje?”
“Nini?”
“Umesahau kitu ambacho Julieth alikizungumza jana?”
Nabii Sanga akashusha pumzi huku akitafakari namna ya kumuingia Julieth ili kumuachanisha na Evans ambaye hana hata pesa.


“Siwezi kumuacha mwanangua aishie mikononi mwa yule Kenge. Hakikisha katika hili jambo una zungumza na mwanao na ana kuelewa vizuri la sivyo nita muua yule Kenge”
“Sawa mume wangu. Mimi mwenyewe nina tamani akubalien na hili ombi, unajua tukiziunganisha familia zetu ni biashara zetu nyingi sana tuna weza kuzifanya pasipo kufwatiliwa na mkono wa serikali wala kodi.”
“Hapo ume nena jambo la muhimu. Kuna ombi jengine ambalo nime ombwa na Jery”
“Ombi gani?”
“Anahitaji wewe uteuliwe kuwa mbuge wa viti maalumu?”
Mrs Sanga macho yakamtoka huku akimtazama mume wake kwa maana hiyo nayo ni bahati ambayo ita zidi kumuongezea cheo katika maisha yake.
“Mbona ume nitolea macho?”
“Mimi nipo tayari hata leo kuchaguliwa”
“Una iweza siasa?”
“Nitakwenda kuisoma huko huko Bungeni bwana”
“Sawa nitamjibu Jery. Pia alinieleza kwamba amezungumza na Julieth masaa mawili yaliyo pita hivyo hakikisha kwamba una zungumza na mwanao kwa kina”
“Usijali mume wangu, akikataa kuachana na huyo mjinga wake. Nitamuu yule kijana kwa mikono yangu mimi mwenyewe, sinto kubali mume wangu mikono yako iingie damu”
Nabii Sanga akamtazama mke wake, kisha akatabasamu kwa maana ana ifahamu kazi ya mke wake katika maswala ya kuwapoteza maadui zao.
***


“Siwezi kukaa hapa ni lazima nifanye jambo”
Magreth aliwaza kitu cha kufanya kwani kuendelea kulia hakuto msaidia jambo lolote kwenye maisha yake. Akaingi bafuni na kuoga kwa haraka, akatoka nyumbani kwake na kuiza safari ya kueleka nyumbani kwa nabii Sanga. Kutokana hapajui vizuri, ikamlazimu kuulizia watu wa mtaa ambao anaishi nabii Sanga. Akaelekekezwa nyumbani kwa nabii Sanga na akawasha gari na kuelekea katika nyumba hiyo. Akasimamisha gari lake katika jumba la kifahari la nabii Sanga. Akalitazama jumba hili kwa umakini kisha akapiga honi mara kadhaa na geti dogo likafunguliwa. Akatoka mlinzi akiwa ameshika bunduki.
“Habari yako kaka?”
Magreth alizungumza huku uso wake ukiwa umejawa na furaha ili mlinzi huyo asiwe na mashaka naye.


“Salama tu dada nikusaidie nini?”
“Mimi nina itwa Mage ni mgeni wa mrs Sanga”
“Ahaa una miahadi naye?”
“Nilizungumza naye ndio”
“Okay kwa sasa mama na mzee wametoka hivyo unge jaribu kuwasiliana nao”
“Mama aliniaeleza kwamba nifike hapa kwake na yeye ata nikuta hapa”
Magreth alidanganya. Mlinzi huyo akamtazam Magreth jinsi alivyo valia vizuri pamoja na kumiliki gari zuri la kifahari. Mlinzi akaamini kwa asilimia mia moja kwamba Magreth atakuwa ni mgeni wa mrs Sanga. Mlinzi huyo akampa ishara mwezake na akafungua geti hilo. Taratibu Magreth akaanza kuingiza gari hilo huku akianza kutazama ulinzi ulipo katika eneo hilo. Akapita katika geti la pili na kusimamisha gari lake katika magesho yaliyopo katika jumba hilo. Dada wa kazi akatoka na kumkaribisha Magreth ambaye alijitambulisha kwamba ni mgeni wa mrs Sanga.


“Unatumia kinywaji gani?”
“Mmmm ninaomba maji ya moto yasiyo na baridi”
“Sawa dada”


Mfanyakazi wa ndani akaondoka sebleni hapo, baada ya dakika kadhaa akarudi akiwa na glasi yenye maji. Hazikuisha hata dakika kumi na tano, nabii Sanga na mke wake wakafika nyumbani kwao. Furaha yao yote ikaisha mara baada ya kuliona gari la Magreth kwenye magesho ya magari yao.


“Huyu malaya ameamua kuja kwamgu ehee?”
Mrs Sanga alizungumza kwa jazba hukua kifungua mlango wa gari hilo. Nabii Sanga naye akashuka kwa haraka kwenye gari hilo. Wakafika sebleni na kumkuta Magreth akiwa amekunja nne huku akiwatazama mrs Sanga na mume wake.
“Dada tupishe”
Mrs Sanga alimueleza mfanyakazi wake wa ndani. Akaondoka sebleni hapo na kuwaacha watatu.


“Umefwata nini ndani nyumbani kwangu?”
Mrs Sanga aliuliza kwa ukali sana.
“Hata hamukai, au niwakaribishe?”
“Zungumza ni kitu gani ambacho kimekuleta hapa nyumbani kwangu?”


Nabii Sanga alizungumza kwa ukali sana kwa maana moyo wake kwa sasa umejawa na chuki dhidi ya Magreth.
“Kuzungumza kwa hasira hakuto kusaidia kwa lolote kwa maana nimekuja kiamani na nina omba niondoke kiamani la sivyo muna fahamu ni kitu gani ambacho ninacho ambacho kina weza kuchafua upepo wa familia yenu, huduma yenu pamoja na taifa zima kwa ujumla. Nina imani kwa wapiga punyet** kwa video yako mrs Sanga utakuwa umewasaidia sana kupata ladha mpya katika shuhuli yao hiyo. Hivyo kaeni chini tuzungumze”
Magreth alizungumza kwa kujiamini kwa maana ana utambua udhaifu wa wazee hao. Taratibu nabii Sanga na mke wake wakaka kwenye masofa yaliyopo hapo sebleni kwao.
“Namuhitaji Evans wangu. Nabii Sanga nina imani kwamba una fahamu ni wapi alipo mume wangu”
“Hilo ndio lililo kuleta?”
“Ndio”


“Nashukuru sana Mungu umekuja kumtoa mzigo wako kwenye familia yangu kwa maana nilikuwa nina mpango wa kumua tena ningemuua vibaya sana. Ipo hivi, huyo Evans wako ana mahusiano na mwanangu wa kike Julieth na amemteka kabisa kimapenzi na mtoto wetu hadi amefika hatua ya kuondoka hapa nyumbani kwetu. Hivyo tuna ingia dili, una mchukua mjinga wako na sisi tuna mchukua mtoto wetu kwa maana hana hadhi ya kumuoa mtoto wetu”
Nabii Sanga alizungmza maneno yaliyo mstua sana Magreth pamoja na mke wake.


“Baba Julieth ume sema kwamba yule kijana ndio mpenzi wa huyu mwana haramu hapa?”
“Yaaa, ndio maana jana nilistuka sana kuioana picha yake mara baada ya kikamatwa. Hivyo mama tushirikiena katika hilo, ukajitahidi kumkatikia Evans wako viuno kitandani ili amsahau mwanangu na mwanangu arudi kwangu kwa maana inaonyesha kwamba ume shindwa kumpa vitu vitamu Evans hadi mwanangu akakupindua. Usipo jitahidi na Evans wako akaleta nyeg** zake kwenye familia yangu, nitamua kifo cha kinyama sana ambacho huto kaa ukisahau na wala sinto ogopa kutuchafua kwa video hizo kwa maana kipindi hicho na wewe utakuwa chini ya ardhi una liwa na funza.”
Maneno ya nabii Sanga yakaanza kumtoa machozi Magreth kwa maana hakuamini kama ipo siku Evans ana weza kuwa na mwanamke mwengine tofauti na yeye.
***


“Evans mume wangu kuna sehemu nina omba niweze kuelekea baadae kidogo mara baada ya kukurudisha hotelini?”
“Una kwenda wapi?”
“Kuna rafiki yangu ametoka Marekani hivyo alihitaji kuonana na mimi na amenisisitizia sana na nimejikuta nikishindwa kumkatalia”
“Ni wa kiume au wa kike?”
“Ni wa kike”
Julieth alidanganya kw amaana ana fahamu fika kwamba akisema ni rafiki wa kiume Evans atapoteza amani.


“Sawa sawa hakuna tabu”
Evans, J na Julieth wakapitia kwenye moja ya mgahawa. Wakapata chakula cha mchana kisha wakamrufisha J ofisini kwake. Wakaelekea hotelini walipo pangisha chumba. Julieth akamuacha Evans kisha akampigia simu Jery.
“Nipo free kwa sasa upo wapi?”
“Nipo Ikulu”
“Tuta onana wapi?”
“Tangulia Serena kuna chumba nime weka oder hivyo nikukute pale”
“Ni chumba namba ngapi?”
“Ukifika tu pale waambie wewe ni mgeni wa Jery Mtenzi”
“Sawa”
Julieth akakata simu na kushusha pumzi taratibu. Akaianza safari ya kuelekea katika hoteli hiyo yenye hadthi kubwa katika jiji la Dar es Salaam. Akafika hotelini hapo, akafika eneo la mapokezi na kumueleza muhudumu aliye mueleza kwamba yeye ni mgeni wa Jery Mtenzi. Muhudumu huyo akaomba waongozane na moja kwa moja akapoelekwa hadi katika chumba chenye hadhi ya kukaa maraisi wa nchi mbalimbali ambao wana tembelea nchi ya Tanzania. Nje ya chumba hicho akakuta walinzi wawili walio valia suti yeusi.


“Julieth yupo hapa”
Mlinzi mmoja alizungumza kwa kutumia kinasa saunti. Mlango ukafunguliwa na mlinzi aliyomo ndani ya chumba hicho na Julieth akaingia ndani na mlinzi huyo akatoka na wakamuacha Julieth peke yake.


“Umezidi kuwa mzuri”
Sauti ya Jery ikamstua sana Julieth na kujikuta akitazama pembeni ya chumba hicho na kumuona Jery aliwa amesimama huku amejawa na tanasamu pana usoni mwake.


“Ohoo Mungu wangu umenistua Jery”
“Kama kawaida yangu kukustua”
Wakakaumbatiana kwa furaha huku Jery akianza kumnyonya Julieth lipsi zake. Julieth hakuwa na pingamizi lolote.


“Umezidi kuwa mzuri Julieth”
“Hata wewe umekuwa handsome boy”
“Hahaa…..unakumbuka kipindi kile tupo shule hata kifuani manyoyo hayakuwa makubwa kama hivi”
“Hahaa ni kweli. Kwa nini hujanifahamisha kwamba una rudi Tanzania?”
“Nilihitaji kukufanyia suprize hivyo sikuona haja ya kukuambia. Isitoshe namba yako sikuwa nayo”
“Ila Jery una tabia mbaya sana. Kwanini kwa kipindi chote hicho huja nitafuta ikiwa uliniahidi kwamba ukifika nchini Marekani uta nitafuta na tutakuwa tuna wasiliana?”
Julieth alizungumza kwa suati ya upole na iliyo jaa mahaba huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Samahani mke wangu, nilicho kitarajia kukikuta kule ni tofauti kabisa. Kipindi cha mwazo mwazo wa masomo, tulikaa bila ya simu zaidi ya mwaka mmoja chuoni. Baada ya hapo tukaruhusiwa kuwa na simu ila nilipo kutafuta kwenye ile namba yako ya mwisho 01 sikuweza kukupata. Jana ndio niliweza kutafuta namba yako kupitia sorce zangu nikafanikiwa kuipata”
Jery alizungumza huku taratibu akimkaribisha Julieth katika meza aliyo andaa chakula kizuri pamoja na wyne ambayo Julieth ana ipenda sana.


“Sikuweza kujumuika na wazazi wako kula chakula cha mchana kwa ajili ya hili jambo.”
“Wait ume sema wazazi wangu?”
“Ndio kwani hawajakueleza kwamba leo walikuwa na mualiko ikulu?”
Julieth akakosa la kujibu kwa maana hajalala kwao na wala hafahamu chochote kinacho endelea kwa wazazi wake.
“Baba na mama yako walijikua kuzungumza na wazazi wangu kwa maana sasa hivi kilicho nirudisha nchini Tanzania ni wewe peke yako. Nimejuka kukuoa Julieth na baada ya hapo nina hitaji tuelekee nchini Marekani na tukaanzishe maisha yetu kwa pamoja”
Kauli ya Jery ikaustua sana moyo wa Julieth na kujikuta hata akishindwa kunyanyua glasi aliyo miminiwa wyne na Jery.


“Mbona kama ume stuka?”
“Mmm!!!?”
“Mbona kama ume stuka?”
“Jery swala la ndoa ni jambo zito?”
“Uzito wake upo wapi ikiwa familia zetu zina uwezo wa kipesa na isitoshe mimi na wewe tuna penda. Au hunipendi?”
Julieth akashusha pumzi kidogo huku macho yakimtoka.
“Ninakupenda sana Jery. Wewe ndio ulikuwa mwanaume wangu wa kwanza kuingia kwenye maisha yangu na uliweza kunivumilia kwa kila jambo. Kwanini niache kukupenda?”
Julieth alizungumza huku nafsi yake ikimsuta kwani ukweli ni kwamba moyo wake upo kwa Evans.


“Nina imani kwamba bikra yangu ume itunza na leo sinto kufanya kitu hadi pale tutakapo funga ndoa yetu na kuivunja bikra ambayo niliivumilia na kuitunza kwa kipindi chote tulicho kuwa pamoja.”
Jery alizungumza kwa furaha sana na kumfanya Julieth kujikaza tu katika kutabasamu ila ukweli ni kwamba hadi hapo alipo hana bikra na ni siku mbili tu zilizo pita Evans aliivunja bikra yake.


ITAENDELEA


Haya sasa, Jery bado ana amini kwamba Julieth ni bikra ikiwa Julieth sio bikra, itakuwaje siku akifahamu kwamab mchumba wake huyo ana mahusiao na kapuku mmoja ambaye hana hadthi ya kumiliki mtoto mzuri kama huyo? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 66.
 
SIN 66

Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)

Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188


ILIPOISHIA


“Ninakupenda sana Jery. Wewe ndio ulikuwa mwanaume wangu wa kwanza kuingia kwenye maisha yangu na uliweza kunivumilia kwa kila jambo. Kwanini niache kukupenda?”
Julieth alizungumza huku nafsi yake ikimsuta kwani ukweli ni kwamba moyo wake upo kwa Evans.


“Nina imani kwamba bikra yangu ume itunza na leo sinto kufanya kitu hadi pale tutakapo funga ndoa yetu na kuivunja bikra ambayo niliivumilia na kuitunza kwa kipindi chote tulicho kuwa pamoja.”
Jery alizungumza kwa furaha sana na kumfanya Julieth kujikaza tu katika kutabasamu ila ukweli ni kwamba hadi hapo alipo hana bikra na ni siku mbili tu zilizo pita Evans aliivunja bikra yake.





ENDELEA


“Kuna zawadi moja nime kununulia mke wangu, ila nitakupatia mara tu baada ya kufunga ndoa yetu”
“Zawadi gani?”
“NItakuambua siku tukifunga ndoa”
Gafla Julieth simu yake ikaanza kuita, akaitazama na kukuta ni namba ya baba yake. Akashusha pumzi na kuipoke.


“Yes Dady”
Julieth alizungumza kwa kuigiza kwani hata kumuita hivyo baba yake kwa madoido ni kumpumbaza Jery asiweze kuelewa chochote kinacho endelea.


“Upo wapi?”
“Mmmmm nipo some where dady”
“Sema up wapi kwa maana nina hitaji ufike hapa nyumbani haraka iwezekanavyo”
“Kuna nini baba?”
“Kuna tatizo, hivyo njoo sasa hivi”
Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo. Na kumfanya Julieth kuanza kutawaliwa na wasiwasi.


“Mpenzi wangu kuna nini?”
“Ba…baba anasema kwamba nyumbani kuna tatizo”
“Tatizo gani?”
“Sielewi mume wangu. Nahitaji kwenda sasa hivi”
“Basi acha nikupeleke”
“No acha niende tu”
“Hapana, wewe ni mke wangu na isitoshe nyumbani kwamba kuna matatizo. Siwezi kukuacha uende peke yake tena uendeshe gari ikiwa mimi nipo na nina walinzi kibao. Hivyo nyanyuka tuondoke”
Jery alizungumza kwa msisitizo huku akinyanyuka. Akaibeba pochi ya Julieth, akamshika mkono na wakaanza kutoka ndani hapo. Wakaongozana na walinzi wake hadi eneo la mapokezi.
“Funguo za gari lako zipo wapi?”
“Ndani ya hiyo pochi”
Jery akafungua pochi yake na kumkabidhi funguo hiyo mmoja wa walinzi wake. Wakaingia kwenye gari walizo kuja nazo hapo hotelini, huku mlinzi mmoja akiendesha gari la Jery na wakaondoka eneo hilo la hotelini.


***


“Sasa mwanangu ana kuja. Atakuletea huyu panya wako”
Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo mara baada ya kukata simu.


“Sio panya ni mume wangu”
“Una mume gani sasa pale?”
Nabii Sanga alizungumza kwa dharau huku akimtazama Magreth aliye lowana mashavu yake kwa machozi. Baada ya dakika ishirini, wakasikia mingurumo ya magari ikisimama nje hapo. Mrs Sanga akachungulia dirishani, akastuka sana mara baada ya kumuona Jery na Julieth wakishuka kwenye gari moja huku wakiwa wameongozana na walinzi wanao mlinda.


“Mungu wangu!!”
“Kuna nini?”
“Jery ana kuja na walinzi wake”
“Nini?”
Nabii Sanga kwa haraka akakimbilia naye dirishani na kuwaona Jery na Julieth wakija ndani hapo. Wakakaa kwenye masofa huku wakijikausha kana kwamba hakuna kitu chochote kinacho endelea. Julieth na Jery wakaingia ndani hapo, Magreth na Julieth wakashangaa sana kukutana hapa kwa maana Magreth kumbukumbu zake za mwisho alikutana na Julieth kwenye mgahawa wake akihitaji kupewa msaadawa kujua ni namna gani anaweza kufungua mgahawa kama wa kwake.


“Hi mom. Hi Dady”
Julieth alizungumza huku akimkumbatiana na mama yake, kisha akambusu baba yake shavuni.
“Jery karibu sana”
“Asanteni sana wazee wangu. Tumestuka sana yulipo sikia kwamba kuna tatizo hapa nyumbani?”
“Yaa ni kweli ni tatizo dogo tu lakifamilia.”
“Ahaa basi wazazi wangu nombeni mimi niondoke ili niwape nafasi ya kuzungumza”
“Mbona mwanangu una wahi hivyo?”
Mrs Sanga alizungumza huku akinyanyuka.
“Mama yangu ni vyema nikawapa nafasi ya kuyajadili mambo ya kifamilia na isitoshe nimekuja pasipo mualiko rasmi hivyo nitakuja siku nyingine rasmi hapa nyumbani”
Ucheshi wa Jery ukazidi kuwavutia nabii Sanga na mke wake. Jery akaondoka nyumbani hapo na walinzi wake.


“Huyu malaya amefwata nini hapa nyumbani kwetu?”
Julieth alizungumza kwa jazba kubwa huku akimtazama Magreth aliye jikuta akicheka kicheko cha kejeli.


“Yaani malaya ni mama yako aliye tembea na Tomas, baba yako aliye tembea na mimi na wewe uliye tembea na mume wangu Evans hivyo naamini umesha jua nani ni malaya kati yenu na mimi”
“Magreth funga bakuli lako kumbuka kwamba hapa upo nyumbani kwangu”
“Haijalishi, ila twendeni kwenye point. Wewe nina imani huyu uliye kuja naye hapa ni mpenzi wako. Sasa ujije ukajikuta nina kuharibia kwake kwa maana sinto kuwa na huruma katika hilo”
Julieth akajawa na mshangao mkubwa sana mara baada ya kusikia Evans ni mume wake Magreth.
“Umekosea, Evans wangu sio mume wako”
“Muulize baba yako kwa maana yeye ndio aliye jaribu kumfukuza Evans wangu kwangu kwa kutumia bastola kutokana tu na wivu wake”
Julieth taratibu akaanza kupata picha taratibu. Evans alimuadisia kwamba mwanaume wa mwanamke ambaye akuwa ni mpenzi wake, alimfukuza nyumbani kwa mke wake kwa kutumia bastola. Machozi ya hasira na kinyongo cha kujiona ni mjinga yakaanza kumtiririka Julieth machoni mwake. Kitu kinacho mtia uchungu zaidi ni jinsi alivyo mkabidhi usichana wake mwanaume ambaye aliamini kwamba ni wa maisha yake yote.


‘Baba na Evans wameshea mwanamke mmoja ohoo Mungu wangu’


Julieth akanyanyuka na kukimbilia chumbani kwake na kuwafanya watu wote kujawa na mshangao. Mrs Sanga naye akanyanyuka na kukimbilia chumbani kwa Julieth, akamkuta akiwa amekaa kitandani huku akilia kwa uchungu.


“Mwanangu vipi?”
“Yaani baba na Evans wametembea na yule malaya pale eheee?”
Mrs Sanga akashusha pumzi kwa maana swali hilo lina uponda ponda sana moyo wake.


“Mama yaani nimetoa bikra yangua mbayo nilipanga kumpa Jery ila leo hii nime mpa yule mjinga. Ahaa……inaniuma mama”
Julieth alizidi kulia na kumfanya mrs Sanga kumkumbatia mwanaye huyo wa kike.


“Wanaume ni watu wabaya. Mwanangu huu ni wakati wa kufanya jambo juu ya maisha yako. Achana na huyo Evans, mtazame Jery ndio mwanaume sahihi kwenye maisha yako”
Mrs Sanga alizungumza kwa sauti ya upole hukua akimtazama Julieth usoni mwake. Julieth akajipangusha machozi yake kwa pamoja na kumkazia macho mama yake.


“Mama nina hitaji kumua Evans”
“Kwa nini?”
“Hawezi kunitoa bikra yangu na nikamucha hai ikiwa ni msaliti kwenye maisha yangu”
Mrs Sanga macho yakamtoka kisha baada ya muda akatabasamu kwani roho yake ya ukatili sasa ana anza kuiona ndani ya mwanaye huyo.


“Kamueleze huyo kunguni wako aniambie ni wapi alipo mume wangu. Nikamchukue la sivyo sinto ondoka hapa”
“Hivi wewe binti una jiamini nini, ikiwa mimi ndio nilikutoa kule uswahilini na kukupeleka kwenye maisha mazuri. Hivi una jua nina weza kukupokonya kila kitu”
“Hahaa hakuna tabu una weza kunipokonya. Ila kabla ya kunipokonya ulimwengu mzima utajua madhambi yako”
Nabii Sanga akafumba macho kwa sekunde kadha akisha akamatazama Magreth.
“Kitu unacho jaribu kukifanya wewe ni sawa na paya kuanzisha vita na panya ikiwa anatambau fika kwamba hana uwezo wa kuoambana na paka”
Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza hivyo akanyanyuka na kuondoka sebleni hapo na kuelekea chumbani kwa binti yake.
“Hei Julieth yupo wapi Evans?”
Nabii Sanga aliuliza huku akikaa pembeni ya binti yake.


“Baba”
“Naam”
“Ninawaomba munisamehe kwa yale niliyo yazungumza jana”
“Tume kusamehe kwa maana tuna jua ulikuwa hujui kinacho endelea”
“Ni kweli, ila baba nina hitaji kufanya jambo moja”
“Jambo gani?”
“Nataka kumuua Evans. Hawezi kunitoa usichana wangu na nikamuacha hai. Atakuja kuniharibia kwa Jery”
Nabii Sanga akamtazmaa mke wake huku akishindwa kutoa jibu sahihi.


“Kwa sasa yupo wapi?”
“Hotelini”
“Hoteli gani na yupo chumba namba ngapi?”
Julieth akakaa kimya kidogo kisha akamtazama baba yake.


“Yupo hoteli ya X Royal chumba namba elfu moja na tatu?”
“Sawa”
Nabii Sanga akanyanyuka na kutoka chumbani hapo. Akarudi sebleni na kumkuta Magreth akiwa amesimama.


“Yupo hoteli ya X Roya chumba namba elfu moja na tatu. Kaishi maisha ya amani na huyu kijana wako, sinto hitaji uingilie tena kwenye maisha yangu umenielewa”
Magreth akanyanyua begi lake, akamtazama nabii Sanga kwa sekunde kadhaa kisha akamsogelea.


“Endapo kuna jambo lolote litamtokea Evans au mimi, basi nita hakikisha watu wa kwanza kushuhulika nao ni wewe na familia yako. Umeona uwezo wangu kidogo tu, ila nina uwezo hata wa kupigana ana wanaume kumi wenye uwezo mkubwa na nikawapiga hiyo kuwa makini na mimi”
Magreth akampiga nabii Sanga busu la shavuni kisha akaondoka nyumbani hapo. Breki ya kwanza akasimama katika hoteli hiyo, akashuka na moja kwa moja akaingia kwenye lifti na kupandisha gadi gorofa ya nne. Akatembea kwenye kordo hiyo na akaona chumba namba elfu moja na tato. Akasimama malangoni hapo kwa sekunde kadhaa na kuanza kuminya kitufe cha kengele.


***


Evan mara baada ya kukaa dakika ishirini ndani ya chumba hicho, akatoka na kuingia kwenye mgahawa ulipo katika hoteli hiyo. Akaanza kunywa juisi huku akitazama mechi ya mpira pamoja na mashabiki wengine waliomo katika mgahawa huo.


‘Nina kwenda kuwa tajiri sasa’


Evans alizungumza huku akitengeneza picha za muono wa jumba walilo kubaliana yeye na Julieth kulinunua.


‘Sijui nimuambie aniadikishe jina langu?’


Evans alizidi kuwazia mafanikio hayo ambayoa amebakisha masaa kadhaa kabla ya siku hii ya keo kuisha.


“Habari yako kijana?”
Sauti ya mzee Mbogo ikamstua sana Evans aliye jikuta akimshangaa mzee huyo kwa maana hajawahi kumuona sehemu yoyote kwenye maisha yake.


“Salama. Shikamoo”
“Marahaba nina weza kukaa?”
“Ndio karibu”


Mzee Mbogo akaka katika kiti kichopo pembeni ya meza hiyo. Akaweka bahasha yenye rangi ya kaki, mezani hapo.
“Fungua ndani ya bahasha kuna zawadi yako”
“Samahani sana mzee. Una nifahamu mimi?”
Mzee Mbogo akatabasamu kidogo, akapiga fumba la maji aliyo fika nayo hapo mezani.
“Evans Richard Shika si ndio?”
“Nd….i…ioooo”
“Basi fungua ndani ya bahasha hiyo kuna zawadi yako”
Taratibu Evans akaichukua bahasha hiyo huku mikono ikimtetemeka mwili mzika. Akaifungua bahasha hiyo, picha ya kwanza kuitoa, ni picha yake na Julieth. Akastuka sana kwa maana picha hiyo ime pigwa wakiwa katika mgahawa ambao walikuwa wakipata chakula mchana wa siku ya leo. Akafungu picha ya pilis na kumshuhudia Julieth akiwa ameshika mikono na mwanaume mwengine ambaye hamtambui ni nani. Taratibu akatoa picha nyingine huku mapigo yake ya moyo yakizidi kumuenda kasi, akamshuhudia Julieth akiwa amekumbatiana na mwanaume huyo huku wakinyonyana lispi zao na nguo ambazo amevaa Julieth ndio nguo hizo hizo alizo ondoka nazo leo.
“Mzee ume zitoa wapi hizi picha?”
“Huyo binti anaitwa Julieth Sanga. Ni mtoto wa nabii mkubwa sana waha Tanzania, nabii Sanga nina imani kwamba una mfahamu. Pili huyo wa pembeni ni mwanaume wake anaitwa Jery Mtenzi, ni mtoto wa raisi Mtenzi aliyopo madarakani kwa sasa. Hivyo Evans kama ulikuwa na ndoto za kumuo huyo binti basi kaa naye mbali kwa maana kinacho fwata kwako ni kifo. Kwausalama wako ondoka kabisa ndani ya jiji la Dar es Salaam.”
Mzee Mbogo mara baada ya kuzumguza hivyo akaondoka huku vijana wake wanne wanao mlinda nao wakaanza kunyanyua kwenye meza walizo kuwa wamekaa na kuondoka naye na kumuacha Evans akiwa amenyong’onyea huku akihisi moyo wake ukichwanjwa chanjwa na viwembe kwani maumivu anayo yahisi hapo ni mara mbili ya maumivu aliyo sababishiwa na Magreth.


ITAENDELEA


Haya sasa, mambo yanazidi kunoga. Evans amefahamu ukweli juu ya mapenzi yaliyopo kati ya Julieth na Jery je ataondoka jijini Dar es Salaam? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose se hemu ya 67
 
SIN 67


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188





ILIPOISHIA


“Mzee ume zitoa wapi hizi picha?”
“Huyo binti anaitwa Julieth Sanga. Ni mtoto wa nabii mkubwa sana waha Tanzania, nabii Sanga nina imani kwamba una mfahamu. Pili huyo wa pembeni ni mwanaume wake anaitwa Jery Mtenzi, ni mtoto wa raisi Mtenzi aliyopo madarakani kwa sasa. Hivyo Evans kama ulikuwa na ndoto za kumuo huyo binti basi kaa naye mbali kwa maana kinacho fwata kwako ni kifo. Kwausalama wako ondoka kabisa ndani ya jiji la Dar es Salaam.”
Mzee Mbogo mara baada ya kuzumguza hivyo akaondoka huku vijana wake wanne wanao mlinda nao wakaanza kunyanyua kwenye meza walizo kuwa wamekaa na kuondoka naye na kumuacha Evans akiwa amenyong’onyea huku akihisi moyo wake ukichwanjwa chanjwa na viwembe kwani maumivu anayo yahisi hapo ni mara mbili ya maumivu aliyo sababishiwa na Magreth.





ENDELEA


Machozi yakaanza kumlenga lenga Evans huku akishuhudia jinsi matumaini ya mafanikio yakianza kuyayuka mithili ya barafu. Akatoa noti ya shilingi elfu tano na kuiweka chini ya glasi hiyo ya juisi ambayo imesalia kidogo. Akanyanyuka na kuishika bahasha hiyo mkononi mwake. Akaanza kupandisha ngazi za kuelekea gorofani, akafika kwenye kordo ya chumba alicho panga. Akastuka sana mara baada ya kumuona Magreth akiwa amesimama mlangoni kwake. Kwa haraka akarudi nyuma na kuanza kushusha ngazi huku woga mwingi ukiwa umemtalawala kwa maana ana amini kwamba Magreth ni lazima atakuwa ameambatana na nabii Sanga na kitendo cha kufika hapo ni kuhakikisha kwamba ana muangamiza. Kutokana mfukoni ana simu yake pamoja na wallet yenye kiasi cha shilingi laki tatu, hakuona haja ya kuendelea kurudi chumbani kwake. Akatoka nje na kusimamisha muendesha pikipiki, na akamuomba ampelekea katika stendi ya mabasi Ubungo.


Magreth akaendelea kuminya kitufe cha kengele hiyo, ila mlango haukufunguliwa. Baada ya dakika tano akamua kuelekea mapokezi.


“Habari yako dada”
“Salama”
“Ahaa una weza kuwasiliana na mgeni aliyopo katika chumba namba elfu moja na tatu?”


“Wewe ni nani yake?”
“Ni mgeni wake, alinieleza kwamba yupo hapa ila nimefika mlangoni hapo nimebisha hodi sana ila hajafungua”
“Muhudumu huyo akafunua daftari la wageni. Akatazama jina lililo andikwa katika chumba hicho.”
“Nahisi huyu kaka amepita hapa kama dakika saba hivi”
“Dakika saba ?”
“Ndio amepita hapa”
“Mrefu hivi, maji ya kunde?”
“Ndio dada”
“Amesema kwamba atarudi?”
“Hapana hajakabidhi hata fungua. Nahisi hajakwenda mbali sana ana weza kurudi”
“Sawa nina shukuru”
Magreth akatoka nje hoteli hiyo na kuanza kuangaza kila sehemu, ila hakuweza kuona dalili yoyote ya Evans. Akamfwata mlinzi wa geti.


“Shikamoo mzee”
“Marahaba”
“Kuna kijana hivi mrefu, maji ya kunde ametoka hapa kama dakika kadhaa zilizo pita je ameelekea uwepo gani?”
“Hivi, emekodisha pikipiki hapa na kuelekea kule”
“Asante”
Magreth akafuka upande wa pili wa barabara ambapo kuna kituo cha waendesha pikipiki.


“Habari zenu”
“Salama dada. Wapi una kwenda”
“Ahaa kuna kijana emetoka pale hotelini ni mrefu maji ya kunde, dakika kama kumi hivi amepanda pikipiki pale nje”
“Yaa nimeona, amepanda pikipiki ya Jose”
“Una weza kuwasiliana na huyo Jose na kumueleza ana elekea wapi?”
“Mmmm kwema sister?”
“Kwema ni mume wangu jamani yule nimegombana naye hivyo ameondoka kwa hasira”
Bodaboda hao wawili wakatazamana.


“Sister unajua hili tunalo fanya ni kukiuka sheria za kijiwe chetu. Tusije tukawa tuna mchomesha mchizi wetu”
Magreth akatoa elfu arobaini na kuwakabidhi vijana waha kila mmoja elfu ishirini.


“Nina waomba sana muweze kunisaidia kuwasiliana na huyo Jose ili nifahamu tu, niwapi ana elekea mume wangu”


Kijana mmoja akatoa mfukoni simu yake na kumpigia Jose.


“Oya kaka wapi hiyo?”
“Nina kwenda Ubungo stendi”
“Ahaa poa mwanangu”
“Fresh”


Kijana huyo akakata simu.


“Panda amekata simu anasema kwamba ana elekea Ubungo”
“Sawa nipeleke nipeleke”
Kijana huyo akamkabidhi Magreth kofia ya usalama kwa ajili ya kichwa chake kisha na yeye akavaa kofia hiyo na kuwasha pikipiki na kuondoka eneo hilo.
Njia nzima Evans akazidi kutafakari ni sehemu gani ambayo ana weza kwenda kutulia na kujipanga vizuri kama ni kurudi Dar es Salaam basi atarudi kwa siku nyingine akiwa na akili mpya.


“Oya hivi Ubungo kwa sasa nina weza kupata magari ya kuelekea Dodoma?”
“Kwa sasa ni uongo kaka. Ila labda upande gari kutoka hapa hadi Morogoro. Ulale Moro, au ubahatike kupata gari za kuelekea Dodoma za usiku”
“Eti ehee?”
“Ndio ila kwa urahisi zaidi una weza kupata gari za kuwahi Morogoro, Mbezi mwisho stendi”
“Sawa nipeleke Mbezi mwisho”


Kama walivyo kubaliana ndivyo jinsi safari ilivyo badilika na kuianza safari ya kuelekea Mbezi mwisho Stendi. Kutokana na pikipiki kuto kusimama kwenye foleni, ndani ya muda mchache wakafika Mbezi mwisho stendi na Evans akamlipa dereva huyo kiasi anacho kihitaji kisha akapanda kwenye gari aina ya costa na safari ya kutoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam ikaanza.


***


Magreth na muendesha pikipiku huyo wakafika katika stendi kuu ya mabasi Ubungo.


“Una weza kunisubiria kaka”
“Pesa ita kuwa kubwa au unaweza kunilipa nauli ya kutoka kule hadi hapa”
“Ni kiasi gani?”
“Elfu kumi na tano”
Magreth akamkabidhi elfu ishirini na kuingia ndani ya kituo hicho kikubwa cha mabasi. Akaanza kuangaza macho huku na kule ila hakuweza kumuona Evans. Akajaribu kumpigia simu, ila jibu la kuto kupatikana kwa simu hiyo, likazidi kumchanganya Magreth. Magreth akaanza kumuuliza kila aliye ona ana weza kumfahamu Evans, ila kila mtu akakiri kwamba hamfahamu kabisa Evans. Baada ya dakika hamsini, Magreth akatoka ndani ya kituo hicho huku akiwa amechoka sana.


“Vipi ume mpata?”
“Hapana kaka”
“Ngoja basi nimcheki jamaa nimuulize ni wapi alipo mpeleka jamaa”
“Fanya hivyo, labda hakumleta Ubungo hapa stendi”
Kijana huyo akawasiliana na rafiki yake huyo aliye kuwa amembeba Evans.


“Kaka hivi yule abiria uliye ondoka naye pale hotelini umempeleka wapi?”
“Kwani vipi ndugu?”
“Nipo na mke wake hapa, ana mtafuta balaa. Wamegombana hivyo ameomba sana aweze kufahamu ni wapi alipo jamaa”
“Daa jamaa kwa sasa atakuwa anaitwafuta Kibaha kama si kuitafuta Kibaha basi atakuwa anainusa nusa Chalinze”
“Duu ana elekea wapi?”
“Dodoma, ila kutokana muda umekwenda, ana weza kulala Morogoro kisha kesho akaelekea Dodoma. Jamaa amepandia gari Mbezi Mwisho”
Muendesha pikipiku huyo akamtazama Magreth ambaye bado anaendelea kuangaza kila sehemu ya eneo hilo la Ubungo.


“Poa kaka”
Muendesha pikipiki huyo akakata simu na kumgusa Magreth bega.


“Sister jamaa amesha toka nje ya mji huu. Jamaa anasema kwamba alimpeleka stendi ya Mbezi mwisho na anadai kwamba jamaa ana elekea Morogoro na kesho ana sepa kwenda Dodoma”
Habari hiyo ikamyong’onyeza sana Magreth kwa maana haamini kwamba ndio ana kwenda kumpoteza Evans milele.


***


“Mkuu kuna habari nyeti nime ipata hapa”
Mlinzi wa karibu wa Jery alizungumza huku akimtazama usoni mwake.


“Habari gani?”
“Kuna rafiki yupo NSA. Amenitumia hizi picha kwenye simu ambazo zina muonyesha Magreth na mpenzi mwanaume mwengine”
Jery akakurupuka kwenye kiti alicho kikalia huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana.


“He….he….e…mbu nione”
Mlinzi huyo akamkabidhi Jery picha zinazo muonyesha Julieth na Evans wakiwa maeneo mbalimbali. Jery akahisi kifua chake kina kwenda kupasuka kwa maumivu ya wivu yaliyo ambatan ana hasira kali itokanayona kitendo hicho.


“Huyo jamaa ana fanya kazi gani?”
“Amemaliza chuo na hana kazi yoyote na hata leo hii kabla ya kuja hapa alikuwa naye”
“Nitafutie huyo kijana haraka iwezekanavyo na ikiwezekana mtekeni na nitahitaji kuonana naye. Jambo hili hakikisha baba halitambui. Umenielewa?”
“Ndio mkuu”
“Niandalie mazingira nina hitaji kwenda tena nyumbani kwa kina Julieth”
“Peke yako”
“Twende wote ila sinto hitaji ulinzi wa mtu mwengie yoyote”
“Sawa mkuu”


Jery akaendelea kuzipitia picha hizo, ambazo zilipigwa na mtu maalumu aliye wekwa na kitendo cha NSA kuhakikisha wana mfwatilia Evans popote pale anapo elekea. Richard akawakabidhi vijana wawili walipo chini yake kazi ya kumtafuta Evans, kisha akandaa mazingira ya kumtoa Jery eneo hilo la ikulu pasipo mlinzi mwengine yoyote kufanikiwa kufahamu. Wakafanikiwa kutoka ikulu na kuianza safari ya kuelekea nyumbani kwa nabii Sanga.


“Jery”
“Naam”
“Uta kwenda kumfanya nini Julieth?”
“Sijui hata nitamfanya nini. Ila ngoja tufike”
Jery alizungumza huku machozi yatokanayo na hasira yakimwagika taratibu usoni mwake.


***


“Mkuu nime mpoteza Evans”
Kijana aliye pewa kazi ya kumfwatilia Evans popote anapo kwenda alitoa ripoti kwa mzee Mbogo.
“Imekuwaje ume mpoteza?”
“Alikuwa kwenye pikipiki na mimi nipo kwenye gari hivyo foleni hapa Ubungo ndio ime sababishia nimempoteza.
“Hakikisha kwamba una mtafuta na kumpata. Umenielewa?”
“Sawa muu”
Kijana huyo akakata simu huku akiangaza kila sehemu hapo Ubungo na hakuweza kuona pikipiki aliyo kuwa amepanda Evans sehemu ilipo elekea. Mpelelezi huyo akasimamisha gari lake kwenye sheli iliyopo hapo eneo la Ubungo, akaanza kutafakari ni wapi ambapo Evans anaweza kuwa ameleelekea. Kwa bahati nzuri akamuona dereva pikipiki aliye kuwa amempakiza Evans akisamama hapo sheli na kuanza kuongeza mafuta kwenye pikipiki yake. Mpelelezi huyo akashuka kwenye gari lake na kumfwata muendesha pikipiki huyo. Akamuonyesha kitambulisho chake.


“Ume mpeleka wapi yule jamaa aliye ondoka naye pale hoteli ya X Royal”
Kijana huyo akaanza kuhisi abiria aliye kuwa amempakiza atakuwa ni muhalifu kwa maana si kwa kuuliziwa huko.


“A…aa nimempeleka Mbezi Mwisho stendi”
“Ana elekewa wapi?”
“Aliniambia kwmaba ana kwenda Dodoma. Ila kutokana ni jioni sasa hivi nilimshauri kulala Morogoro na kesho aweze kuelekea huko Dodoma”
Mpelelezi huyo akamtazama dereva huyo pipikipi na kumuamini kile alicho kizungumza.


“Amepanda gari gani?”
“Sijajua kwa maana mimi nilimshusha pale stendi na mimi nikaondoka zangu”
Mpelelezi huyo kwa haraka akarudi ndani ya gari lake na kuondoka eneo hilo na kuianza safari ya kuelekea mkoani Morogoro.


***


“Mama Jery akifahamu kwamba mimi sio bikra itakuwaje mama?”
Julieth alizungumza huku akilia kwa uchungu sana. Kabla ya mama yake kumjibu kitu chochote mlango ukafunguliwa na nabii Sanga akaingia ndani hapo.
“Jery amerudi na anahitaji kuonana nawe”
Julieth akastuka sana. Julieth kwa haraka akayafuta machozi yake na kujiweka sawa. Jery akaingia ndani hapo na kuwafanya nabii Sanga na mke wake kutoka ili kuwapisha waweze kuzungumza.


“Jery”


Julieth alizungumza huku akitabasamu. Jery akaufunga mlango huo kwa ndani na kumshika Julieth kwa hasira sana na kumsukumia kitandani. Kitendo hicho kika mstua sana Julieth na katika maisha yake yote hakuwahi kumuona Jery akiwa amekasirika kwa kiasi hicho.


“Kabla sijakuoa nina hitaji kufahamu, je wewe ni bikra au si bikra?”
Swali la Jery likamstua sana Julieth pamoja na mrs Sanga aliye simama mlangoni hapo akihitaji kusikia ni kitu gani Jery ana zunugmza na mwanaye kwa maana alipo weza kumuona Jery aligundua kwamba amekasirika sana.


ITAENDELEA


Haya sasa, ni kitu gani ambacho Julieth ata kwenda kumjibu Jery ikiwa ukweli ni kwamba hana bikra? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose se hemu ya 68
 
SIN 68


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188





ILIPOISHIA


“Jery”


Julieth alizungumza huku akitabasamu. Jery akaufunga mlango huo kwa ndani na kumshika Julieth kwa hasira sana na kumsukumia kitandani. Kitendo hicho kika mstua sana Julieth na katika maisha yake yote hakuwahi kumuona Jery akiwa amekasirika kwa kiasi hicho.


“Kabla sijakuoa nina hitaji kufahamu, je wewe ni bikra au si bikra?”
Swali la Jery likamstua sana Julieth pamoja na mrs Sanga aliye simama mlangoni hapo akihitaji kusikia ni kitu gani Jery ana zunugmza na mwanaye kwa maana alipo weza kumuona Jery aligundua kwamba amekasirika sana.





ENDELEA


Julieth akapatwa na bumbuwazi, akatamani kuzungumza ila mdomo wake ukakosa uwezo kabisa wa kuzungumza.


“ZUNGUMZAAAA”
Jery alizungumza kwa ukali sana huku akimkazia macho Julieth ambaye mwili mzima una mtetemeka kwa woga.
“Mimi ni bikra Jery”
Julieth aliongopea ili kuepukana na kipigo ambacho ana weza kukipokea kutoka kwa Jery ambaye amefura kama Mbogo aliye jeruhiwa na muwindaji. Mrs Sanga naye mapigo yake ya moyo yakazidi kumuenda kasi hadi akatamani kuingia ndani humo, ila akaona sio jambo zuri kuingilia mazungumzo ya watoto. Jery akatoa simu ya mlinzi wake, akamuonyesha Julieth picha alizo pigwa akiwa na Evans.


“Unaweza kunipa maelezo juu ya huyu mtu”
Julieth akatamani ardhi ipasuke na immeze kwani limekuwa ni jambo la haraka sana kwa Jery kufahamu mahusiano yake na Evans ambaye amepanga kumuua.


“Huyo kijana ana itwa Evans”
“Ni nani yako?”
“Majuzi hapa mimi na mama tulikuwa tuna alekea Bagamoyo. Ia tulipo fika pale mataa na ya Mwenge tuli mgonga muendesha pikipiki akiwa amempakiza abiria ambaye ndio huyo kijana”


Jery akashusha pumzi kwa nguvu huku akijaribu kuiweka sawa hasira yake.


“Baada ya kumgonga ikawaje?”
“Dereva alifariki pale pale ila huyo kijana alifanikiwa kupona. Ili kumuweka sawa asiende kutufugulia kesi mahakamani ilinibidi niwe naye karibu sana.”
“Ina maana huna mapenzi na huyu kijana?
“Sina mapenzi naye na una nijua jinsi nilivyo na msimamo na maisha yangu. Siwezi kukutana na mwanaume tu alafu nikawa naye kwenye mahusiano”
Julieth alizungumza kwa kujiamini sana. Kujiamini kwake kuka ufaifanya hasira ya Jery taratibu kuanza kushuka huku akianza kumuamini Julieth.


“Una nihakikishia kwamba sio mpenzi wako kabisa?”
“Ndio na hizi picha aliye zipiga ana malengo mabaya na sisi. Hivi una hisi miaka yote minne uliyo kaa Marekani bila ya kuwasiliana na mimi una hisi kwamba nilikuwa nina jiachia jiachia eheee?”
“Hapana mpenzi wangu. Una jua ni lazima niwe na wivu na wewe. Na swala la kuto kuwasiliana nawe mbona tulisha lizungumza”


Jery alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Julieth usoni mwake.
“Ndio hivyo huyo kijana mimi sina mahusiano naye kabisa na wala usihisi kwamba nina weza kukusaliti wewe na kama ni zawadi yako ya bikra utaipata ukisha nioa”
“Nashukuru sana mpenzi wangu. Nina kupenda sana mke wangu”
“Nina kupenda pia mume wangu”
Jery na Julieth waka kumbatiana kwa sekunde kadhaa kisha, taratibu wakaanza kunyonyana lipsi zao huku wakizama katika hisia nzito za kimapenzi. Jery akataka kuingiza kiganja chake cha mkono wa kulia katika suruali aliyo vaa Julieth ila Julieth akakiwahi kiganja hicho kwa maana kina weza kwenda kushika kitumbua chake na hilo lina weza kumpelekea Jery kufahamu kwamba mke wake sio bikra tena.


“No baby, muda haujafika”


“Oho sory nimejisahau mke wangu”
“Usijali natambua una hamu na mimi”
“Ni kweli je upo tayari kuolewa na mimi?”
“Ndio mume wangu nipo tayari”
Jery akajawa na furaha ya ajabu sana. Hata mrs Sanga ambaye muda wote alikuwa amesimama hapo mlangoni pasipo Jery wala Julieth kufahamu, naye alijawa na furaha kubwa sana. Baada ya mazungumzo ya hapa na pale, Jery akaaga na kurudi zake ikulu.


“Mama nitafanya nini ikiwa nime mdanganya Jery kwamba nina bikra?”
“Wala usijali kuna bikra za kutengeneza nita hakikisha una ipata hiyo na hato weza kufahamu kama bikra yako alisha tolewa”
“Nashukuru sana mama yangu ukinisaidia katika hilo”
“Ehee na huyo kichaa una mshuhulikia lini kwa maana ikitokea aka weka pingamizi katika ndoa yenu kanisaini ita kuwaje?”
Julieth taratibu akashusha pumzi huku akimtazama mama yake.


“Nisaidie katika hilo kwa maana Jery amekuja na picha za ushahidi nikiwa na kijana huyo”
“Kweli?”
“Ndio mama sijui nita fanya nini?”
“Nita kuambi nini cha kufanya kwa maana sasa hivi yule malaya wake atakuwa amekwenda kumchukua hotelini”
“Nani?”
“Si umemueleza baba yako ni hoteli gani alipo Evans hivyo utambue kwamba ni lazima atakuwa amemuambia Magreth ni wapi alipo huyo kunguni wake.”
“Mama siwezi kukubali Magreth ampate Evans”
“Kwa nini ikiwa una hitaji kumua?”
“Ndio ila sitaki awe na huyo Mage”
Julieth alizungumza huku akinyanyuka kitandani hapo.


“Sasa una kwenda wapi?”
“Nina kwenda hotelini”
“Hembu rudisha makalio yako hapa. Acha ujinga wewe, kumbuka upo kwenye kipindi gani. Kama Jery amesha kuonyesha picha upo na huyo mwenda wazimu wako ni lazima utambue kwamba una fwatiliwa na kama una fwatiliwa basi ina kupasa kuwa makini. Umenielewa?”
Mrs Sanga alizungumza kwa msisitizo na kumfanya Julieth kuwa mpole kwa maana hasira aliyo iona kwa Jery hatamani tena kuiona kwenye maisha yao ya ndoa.



***


Amani ikazidi kupotea moyoni mwa Evans, njia nzima ana tafakari ni kitu gani ambacho kina weza kumkuta kwa kujihusisha kimanusiano na Julieth, mtoto wa nabii Sanga. Akazitoa picha kwenye bahasha aliyo achiwa na mzee Mbogo. Akaanza kutazama picha moja baada ya nyingine.


‘Julieth nina kuchukia ume yayumbisha maisha yangu’


Evans alizungumza kimoyo moyo huku machozi ya hasira yakimwagika usoni mwake. Safari ikazidi kusonga mbele hadi wakafika katika stendi ya Msavu mkono Morogoro. Evans akashuka kwenye gari huku akishangaa shangaa magari mengi yaliyopo kwenye stendi hiyo kubwa.


“Oya mambo vipi”
Evans alimuambia muuza maji vinjwaji kwenye boksi aliye simama pembeni yake.


“Poa kaka”
“Nina omba Coca take away”
“Poa ni buku”


Evans akatia noti ya shilingi elfu mbili na akachukua na pakti ya biskuti ya elfu moja.


“Oya hapa kuna gari za kwenda Dodoma usiku huu?”
“Ahaa hapana kaka mabasi yoyote yamesha pita kaka”
“Duu hapa hoteli nina weza kupatia wapi?”
“Zipo loge nyingi tu kaka”
“Nielelekeze”
“Njoo nikuonyeshe”
Muuza vinywaji huyo alizungumza huku wakisogea katika eneo ambalo wana weza kuona gorofa moja la hoteli.


“Kwenye lile gorofa pale una weza kupata vyumba kaka”
“Shukrani sana ndugu”
“Hapa chukua bodaboda ata kupeleka hadi pale”
“Poa”
Evans akaagana na muuza vinywaji huyo kisha akakodisha pikipiki iliiyo mpeleka hadi kwenye hoteli hiyo. Kwa bahati nzuri akafanikiwa kupata chumba. Usiku mzima Evans hakupata usingizi kabisa, maneo ya mzee Mbogo yakaendelea kujirudia kichwani mwake.


‘Mtoto wa raisi. Daaa kwa nini Julieth ali nipumbaza kiasi hichi hadi nika muamini sana?’


Evans aliendelea kuwaza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.


‘Mimi ni mwanaume, nilazima nihakikishe nina pambana kwenye haya maisha na kuanzi hivi sasa sinto mpenda mwanamke wa aina yoyote. Nitakuwa nina chapa ilale tu’


***


Mpelelezi anaye amfwatilia Evans, akafika mkono Morogoro majira ya saa saba kasoro usiku. Akasimamisha gari karibu na stendi ya mabasi. Akawafwata waendesha pikipiki walipo eneo hilo.


“Waskaji mambo vipi?”
“Safi kaka”
“Aisee gari za kuelekea Dodoma hapa za mwisho huwa zina pita saa ngapi?”
“Mmmm saa nne hivi zikichelewa sana zina pita hapa saa tano kaka”
“Ahaa sawa nina shukuru”
“Poa poa”
Mpelelezi huyo akarudi ndani ya gari lake na kuanza kupiga mahesabu ya gari la abiri likitoka Dar es Salaam hususani costa zinazo simama simama barabarani, akagundua kwamba costa aliyo ipanda Evans ni lazima itakuwa ime chelewa kufika Morogoro hivyo ame kosa usafiri wa kuondoka Morogoro hapo.


‘Ata kuwa wapi huyu jamaa’


Mpelelezi huyo alijiuliza huku akitazama majengo ya gorofa yaliyopo katika mji huo. Kabla hajapata jibu akapokea simu bosi wake Mzee Mbogo.


“Habari mkuu”
“Upo wapo?”
“Nimefika Morogoro usiku huu”
“Sasa tume nasa video za CCTV kamera zilizopo hapo kwenye hiyo stendi. Dakika arobaini na nne Evans aliondoka hapo”
“Muheshimiwa una weza kunitumia hiyo video?”
“Ndio”
“Nashukuru sana”


Simu ikakatwa, hazikuisha hata dakika mbili, video hiyo ikaingia kwenye simu yake. Akamshuhudia Evans akishuka kwenye moja ya costa. Akamshuhudia akizungumza na kijana wa maji huku akinunua soda pamoja na biskuti. Akaendelea kuitazama video hiyo na kumuona kijana huyo akimuelekeza Evans sehemu ya kwenda na Evans akatoka nje ya stendi hiyo na kupanda pikipiki na kuondoka eneo hilo. Mpelelezi huyo akarudi sehemu ya maelekezo anayo pewa Evans na kijana muuza maji.


‘Akiwa upande ule pale, akielekezwa kule sehemu aliyo fikia ni ile pale’


Mpelelezi huyo alijikuta akitabasamu mara baada ya kugundua ni wapi Evans ameelekea.


‘Kazi imekwisha sasa’


Mpelelezi huyo alizungumza huku akiwasha gari lake. Akafika hotelini hapo na moja kwa moja akaelekea mapokezi. Akamasalimia muhudumu huyo wa kiume kisha akamuonyesha video inayo muonyesha Evans.


“Huyu kijana amefika hapa hotelini kwenu?”
Muhudumu akaitazama video hiyo, kisha akamtazama mpelelezi huyo.


“Ahaa kwa nini una muulizia?”
“Ni rafiki yangu”
“Basi acha niwasiliane naye ili nifahamu kama una miahadi naye”
“Hapana. Wewe niambie ni chumba kipi alichopo ili niweze kuingia na kuonana naye”
“Utaratibu wa kazi yangu hausemi hivyo. Isitoshe sasa hivi ni usiku na nina ogopa sana endapo ikatokea mteja akauwawa ndani ya hoteli yetu, ita tutia matatizoni”
“Mimi sio muaji ila ni mlinzi wake”
“Mlinzi wake? Nitaamini vipi?”
“Amini hilo”
“Ndio uniaminishe, siwezi kuamini tu maneno”
Mpelelezi huyo akashusha pumzi huku akimtazama muhudumu huyo. Akatoa kitambulisho chake na kumkabidhi muhudumu huyo ambaye mara baada ya kukisoma, akajikuta akianza kutetemeka.


“Haya nipelekea chumbeni kwake”
Muhudumu huyu hakuwa na namna zaidi ya kukubaliana na mpelelezi huyo. Wakafika katika chumba cha Evans, mpelelezi huyo akampa ishara muhudumu huyo kungonga na akatii agizo hilo.


Evans akastuka sana mara baada ya kusikia mlango ukigongwa. Akatazama saa ya ukutani inamuonyesha ni saa saba kasoro usiku. Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda kasi huku wasiwasi mwingi ukimtawala. Taratibu akashuka kitandani.


“Nani?”
Evans alizungumza huku akijibanza mlangoni.


“Room service”
“Muda huu una hitaji nini?”
“Tuna utaratibu wa kukagua wateja wetu kila usiku”
Evans akaanza kupata mashaka kwa maana amelala latika mahoteli makubwa na ya kifahari kuliko hata hoteli hii ila hajawahi kukutana na utaratibu wa aina kama huo.
“Nita kuamini vipi kama wewe ni room service”
“Mimi ndio yule niliye kupa chumba pale mapokezi. Ume sahau sauti yangu?”
Evans akaka kimya kwa sekunde kadhaa, akaikumbuka sauti ya kijana, akaufungua mlango huo. Kwaharaka mpelelezi huyo akaingia ndani hapo na kumstua sana Evans kwa maana alicho kitegemea ni tofauti kabisa na hichi anacho kiona.
“Wewe ni nani?”
“Vaa nguo zako sasa hivi na tuondokea, eneo hili sio salama”
Mpelelezi huyo alizungumza huku akikimbilia dirishani, akachungulia na kushuhudia kundi kubwa la watu walio valia suti nyeusi, wapatao ishirini, wakishuka katikamagari mawili aina ya Toyota VOXY. Mpelelezi huyo akachomoa bastola yake na kuwafanya Evans na muhudumu huyo kustuka sana.


ITAENDELEA


Haya sasa, watu hao ni kina nani na kwa nini wana kuja hotelini hapo na wameagizwa na nani kufika hapo hotelini na wana mtafuta nani? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose se hemu ya 69
 
Back
Top Bottom