Brodre
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 2,585
- 1,771
- Thread starter
- #81
SIN 49
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
“Ingekuwa ina pendeza zaidi kama ungeendelea kukaa na mke wako wa ndoa. Kuliko kupambana na vijana kwa ajili ya kugombania mabinti wadogo.”
Kauli hiyo ya RPC Karata ikaustua sana moyo wa nabii Sanga, akasimama na kumgeukia RPC Karata aliye achia tabasamu pana sana usoni mwake.
“Unasemaje wewe?”
Nabii Sanga aliuliza kwa dharua kubwa sana.
“Ni hivi. Acha kumdanganya mke wako kwa kutembea na binti mdogo kama Magreth. Tambua kwamba Magreth ana mchumba wake anaitwa Evans na ana mpenda sana na wewe unachunwa mjini hapa mzeee hahahaaaahahaaaa……..”
Nabii Sanga akaanza kuvimaba kwa hasira. Mrs Sanga machozi yakaanza kumwagika usoni mwake kwani jambo alilo kuwa ana lihisi kumbe hata RPC ana lifahamu tena kwa mapana.
ENDELEA
“Kijana una vuka mipaka, nitakupoteza”
Nabii Sanga alizungumza kwa hasira sana huku akimkazia macho RPC Karata.
“Hee!! Unanitisha ndani ya ofisini yangu na umesahau kwamba hapa ni wapi wewe? Upo kituo cha polisi na unaye zungumza naye hapa sio ispekta ni RPC wa mkoa mzima. Toka ofisini kwangu kabla majini yangu hayajabadilika na nikakusweka ndani. Sasa wewe nenda kajichanganye kama alivyo fanya mke wako katika kukuteka na majambazi wake mchwara. Alafu utajua kwamba hichi kiti sijakikalia bahati mbaya. Utafia jela na nikuambie jambo moja macho yangu yote yana waangalia nyinyi. Jichanganyeni”
RPC Katara alizunhgumza kwa kujiamini huku akimtazama nabii Sanga. Mrs Sanga akamshika mkono mume wake na taratibu wakaanza kuondoka eneo hilo.
“Huyu kijana amekuwa jeuri sana. Nitamuonyesha mimi ni nani?”
Nabii Sanga alizidi kuzungumza kwa hasira. RPC Karata mara baada ya kushuhudia gari la nabii Sanga likiondoka eneo hilo la polisi. Akatoa simu yake ya mkononi na kumpigia kijana wake anaye husika katika maswala ya upelelezi.
“Njoo ofisini kwangu”
“Sawa mkuu”
RPC Karata akarudi kwenye kiti chake na kukaa, huku akitafakari ni jinsi gani anavyo weza kumfwatilia nabii Sanga katika kila hatua atakayo piga. Kijana huyo mrefu na aliye valia nguo za kiraia, akaingia ofisini humo, akampigia saluti mkuu wake wa kazi, kisha akakaa kwenye kiti kilichopo mbele ya meza ya mkuu wake.
“Milinga kuna kazi hatari sana nina hitaji kukupatia kuanzia hivi sasa”
“Sawa mkuu. Ni kazi gani?”
RPC Karata akamgeuzia Milinga laptop yake na kumuonyesha video iliyo rekodiwa na kamera za barabarani katika eneo la Mwenge, zikionyesha jinsi gari ya mrs Sanga ikimgonga dereva bodaboda pamoja na abiria wake.
“Hiyo ni ajali ambayo ilisababishwa na mrs Sanga. Hawa watu wamekuwa wakitumia muamvuli wa dini katika kufanikisha mambo yao. Kama hapa unaweza kuona kwamba ana makosa makubwa sana, ila nimepewa oda kutoka ikulu ya kumuachia, ikiwa raia wa kawaida huwa ni lazima wakumbane na adhabu kali sana”
“Nahitaji kuanzia hivi sasa uwe karibu sana na hii familia. Ikiwezekana hata uokoke na utafute nafasi katika kanisa hilo. Hakikisha kwamba una fwatilia nyendo za nabii Sanga hatua by hatua”
“Sawa muheshimiwa. Ila nina weza kukuuliza swali?”
“Uliza tu”
“Hii kesi ina husiana sana na askari wa usalama wa barabarani. Je kuna jambo jengine tofuati na hili ambalo una hitaji nilifwatilie as person matter au ni kutokana na ajali na kupewa oda kutoka ikulu kumuachia huru?”
Nabii Sanga akashusha pumzi taratibu, kutokana ana muamini sana kijana huyu Milinga.
“Una kumbuka kuna siku nilitolewa hapa na walinzi wa Ikulu na nikapelekwa Ikulu?”
“Ndio nina kumbuka?”
“Unakumbuka juu ya swala la yule kijana Tomas ambaye tulikuwa tuna mtafuta?”
“Ndio nina mkumbuka na hadi sasa hivi hatujamtia nguvuni.”
“Basi ishu ilikuwa hivi. Yule kijana alikuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mke wa nabii Sanga. Kutokana na utamu kolea wa mapenzi yao, walipanga njama za kumteka nabii Sanga na wakawatumia wale majambazi tulio waua”
“Nabii Sanga aliweza kulifahamu jambo hilo. Hivyo alinipa kazi ya kumuua Tomas na mimi ndio niliye mtorosha Tomas ndani ya kituo hichi pasipo hata askari yoyote kuweza kugundua. Nikiwa katika harakati ya kumuua, nabii Sanga alinipigia simu na nikiomba nimuachie huru.Ila kutokana na askari kugundua kwamba Tomas hayupo basi ilitubidi kuingia katika ule msako. Raisi Mtenzi unaifahamu historia yake vizuri, hivyo aliweza kujua fika mtu wa pekee aliye mtorosha muhalifu ni mimi. Raisi alinipa masaa ishirini na nne niwe nima mpata la sivyo nina stakiwa kijeshi”
“Ilibibidi kuwa muwazi kwa muheshimiwa raisi hivyo alinisamehe. Ila jambo baya sana alilo lifanya huyu mzee hakudhubutu hata kuniomba msamaha kwa kile kilicho tokea. Leo hii mara baada ya mke wake kuachiwa huru, ana nitisha na kuniambia kwamba ana nionyesha na ata hakikisha nina ondoka hapa Dar na kuepelekwa Kagera. Siwezi kuwa mwema zaidi ya hapo. Tafadhali hakikisha una nipatia siri zao nyeti kuhakikisha kwamba tuna muangusha”
“Sawa mkuu nime kuelewa. Nitaifanya kazi yako kwa asilimia mia moja”
“Nita shukuru, nina imani una fahamu ni wapi kwa kuanzia?”
“Ndio muheshimiwa hakuna tatizo”
Afande Milinga akaagana na RPC Karata na kutoka ofisini hapo, huku kichwani mwake akianza kupangilia mfumo mzima wa kazi yake jinsi utakavyo kwenda.
***
Julieth na Evans wakafika Mlimani City. Wakaingia katika duka la wauazaji wa bidhaa za apple. Dada aliye zungumza na Evans masaa mawili yaliyo pita akabaki akimshanga kwa jinsi alivyo fungwa bandeji hiyo mikoni mwake.
“Si ume toka hapa ukiwa mzima?”
“Wee acha tu dada yangu. Nimepata ajali hapo Mwenge”
“Jamani pole sana”
“Asante”
“Ni ajali ya nini?”
“Pikipiki”
“Umegongwa au?”
“Hapana nilikuwa kwenye pikipiki, tugagongwa na gari bwana”
“Pole sana kaka, yaani kweli binadamu tuna tembea na vifo mkonini”
“Wee acha tu”
“Simu yako si kama ile pale”
“Ndio”
Julieth akamnunulia Evans simu hiyo na Evans. Julieth akampigia simu baba yake ili kufahamu ni jambo gani linalo endelea.
“Tupo njiani tuna elekea nyumbani na mama yako”
“Sawa je gari langu vipi lime achiwa?”
“Sijafwatilia bwana mambo ya magari. Huyo mgonjwa wako ana endeleaje?”
“Amesha ruhusiwa hospitalini”
“Fidia ana taka nini?”
“Aha…sija zungumza naye kuhusiana na swala la fidia”
“Zungumza naye kisha urudi nyumbani sasa hivi”
“Sawa baba”
Julieth akakata simu, akamuomba Evans wakae kwenye mgahawa wa Samaki Samaki ili waweze kuzungumza mambo mawili matatu. Evans hakuwa na kipingamizi cha aina yoyote. Wakaagiza chakula na taratibu wakaanza kula.
“Ahaa baba ameniuliza kama kuna fidia ya aina yoyoye ambayo una weza kudai ili tukupatie”
“Hapana usijali. Kutokana simu yangu ime rudi hakuna tatizo”
“Kweli”
“Ndio Julieth”
Evans alizungumza huku akiendelea kuudadisi uzuri wa Magreth.
“Aha samahani Evans hapa mjini una jishuhulisha na shuhuli gani?”
“Nimemaliza chuo, nilipata matatizo ya kuvamiwa na vibaka na wakaniibia vyeti vyangu vyote”
“Aisee pole sana”
“Nashukuru”
“Sasa una ishije hapa mjini kama huna kazi?”
“Nimejishikiza kwa msichana mmoja ambaye ni mpenzi wangu. Japo ame nieleza kwamba ana mpenzi wake. Ila bado nina endelea kutafuta tafuta maisha si unajua wana wake muda wowote wana badilika”
“Ni kweli, sasa ina huyo mwanamke mpenzi wake yupo wapi?”
“Hajanieleza, japo ana kiri kwamba ana nipenda. Ila ndio hivyo maisha yake hayo ame tengenezewa na mwanaume wake”
“Pole sana Evans na ume somea maswala gani?”
“Nimesomea mambo ya biashara”
“Ahaa ngoja kuna kampuni ya usafirishaji nina hitaji kuifungua mwezi huu. Basi nita kupa nafasi ya umeneja”
“Kweli?”
“Haki ya Mungu. Nimeagizia roli ina ya Benz zipatazo hamsini. Zitakuwa zina chukua mizigo bandarini, kupelekea nje ya nchi”
“Aissee hongera sana. Je nina weza kukuuliza swali?”
“Uliza tu”
“Pesa zote hizo umezitoa wapi ikiwa una onekana ni binti mdogo”
“Wazazi wangu ni mabilionea. Wana pesa nyingi sana, hivyo waliniuliza ni mradi gani ambao ningependa kufanya. Nikaona ni heri nifungue biashara hiyo. Gari hizo zipo baharani na zina tokea nchini Ujerumani”
“Nashukuru kukutana na wewe na nina kuahidi kwamba nita simamia kampuni yako na itwa kwenda vizuri sana”
“Sawa kikubwa ni kujituma. Japo mmi ni mwanafunzi ila ni mfwatiliaji mzuri sana katika maswala ya pesa”
“Sinto kuangusha.”
“Kesho kama uta pata muda. Tukutane ili niweze kukupatia pesa ambayo una weza kupangisha nyumba ya kwako mwenyewe. Hapa nina fikiria endapo mwanaume huyo ata kuja kukukuta ndani ya nyumba ya demu wake ita kuwaje? Au hilo hujawahi kulifikiria?”
“Nimelifikiria ila mwanamke huyo ameniambia kwamba yupo tayari kupoteza kila kitu ili mradi awe na mimi?”
“Si kwa dunia ya sasa hivi. Ana kudanganya sana huyo mwamke, hakuna mtu ambaye ata kubali kuishi katika maisha ya umasikini kisa mwaume. Hapana amekuingiza cha kike na tena na kutafutia matatizo makubwa sana”
Maneno ya Julieth kidogo yakaanza kumpa wasiwasi Evans.
“Ila sijui lakini, ila kwa asilimia kubwa ya wanawake wa hapa mjini, hususani wale ambao wana wana pata wanaume wa kuwawezesha, wana mambo mawili. Yupo tayari kukufanya wewe kuwa kaka yake pale atakapo kuwa na mwanaume huyo au kukuacha kabisa. Kuwa makini sana Evans”
“Nimekuelewa dada yangu”
“Sawa muda wangu ni mdogo, acha niondoke hapa, niwahi nyumbani na pia nifanye taratibu za kulitoa gari langu polisi”
“Sawa nina shukuru kwa muda wako”
Julieth akafungua pochi yake na kutoa laki moja na kumkabidhi Evans.
“Kodisha taksi ikufikshe nyumbani. Angalia usije ukapanda pikipiki ukapata tena matatizo”
“Nina shukuru sana”
Wakaagana na Evans akaanza safari ya kurudi kigamboni, huku Julieth akirudi nyumbani kwa baba yake. Evans akajifikria kwa muda na kuona hakuna haja ya kurudi nyumbani muda hao. Moja kwa moja akaelekea kwenye mgahawa wa Magreth. Kwa bahati nzuri akamkuta Magreth aliye jawa na mshangao mara baada ya kumuona mume wake akiwa katika hali hiyo.
“Kuna nini kimekupata mume wangu”
Evans akamuelezea Magreth hali halisi ya tukio lilivyo tokea. Hakumuelezea kukutana na Julieth kwani ana imani kwamba kupitia msichana huyo basi ana weza kupata msaada mkubwa sana utakao mtoa kimaisha.
“Basi twende nyumbani uka pumzike”
“Wewe si upo kazini mpenzi wangu?”
“No ila hali yako sio nzuri, twende nyumbani sasa hivi uka pumzike”
Magreth alizungumza kwa msisitizo. Evans hakuwa na pingamizi lolote zaiid ya kukubaliana na mke wake huyo. Magreth akaacha majukumu yote ya kuendesha mgahawa huo kwa Juma, kisha yeye na Evans wakaondoka na kuianza safari ya kuelekea nyumbani kwao Kigamboni.
***
Nabii Sanga akafika nyumbani kwake huku akiwa amejawana hasira kali sana. Akapitiliza hadi chumbani kwake, akafungua shelf ya kuhifadhia nyaraka zake muhimu pamoja na bastola yake. Akachukua bastola yake na kuichomeka kiunoni kwa nyuma.
“Una kwenda wapi mume wangu?”
Mrs Sanga alizungumza huku akimtazama mume wake aliye fura kwa hasira.
“Sitaki maswali ya kipumbavu. Wewe hujaona udhalilishanji nilio pewa na yule kijana”
“Mume wangu, nakuomba uzuie hasira yako. Kumbuka kwamba wewe ni mtumishi wa Mungu mbele ya macho ya watu. Itakuwaje pale watu wakisikia kwamba ume fanya mauaji?”
“Sijali mimi, nita hakikisha kwamba nina mfundisha adabu. Ninakwenda na nikirudi hapa ninataka unipe majibu ya wapi ulikuwa unakwenda hadi uka gonga mtu. Umenielewa wewe mwanamke”
Nabii Sanga alizungumza kwa msisitozo huku akimtazama mke wake. Mrs Sanga hakuwa na uwezo wa kumzuia mume wake. Nabii Sanga, akafungua kabati linalo hifadhia kofia zake, akachukua moja ya kofia na kutoka ndani humo. Akabadilisha gari na kutumia gari aina ya BMW X6 ambayo ni mara chache sana amekuwa akiitumia. Kilicho mkasirisha nabii Sanga si dharau za RPC Karata, ila kitu kinacho muumiza moyoni mwake ni kuhusiana na mahusiano ya Magreth na Evans kijana ambaye alimsaidia hospitalini kwa kumlipia matibabu mara baada ya kuchomwa kisu na wahuni wa mtaani.
‘Lazima nimuue huyu ngedere. Hawezi kunichukulia mwanamke wangu ninaye mpenda’
Nabii Sanga alizungumza huku akizidi kuongeza mwendo wa gari lake.Akafika nyumbani kwa Magreth, akalisimamisha gari lake katika moja ya dula la karibu na nyumba hiyo. Akashuka na kuanza kutembea hadi getini kwa nyumba ya Magreth. Akatoa funguo za geti hilo na kufungua, akaingia ndani. Ukimya wa nyumba hiyo haukumuogopesha nabii Sanga. Akafungua mlango wa mbele wa nyumba, akaingia na kuufunga kwa ndani.
Nabii Sanga moja kwa moja akaeleka chumbani kwa Magreth na kuingia ndani,kitu kilicho mshangaza na kumuumiza roho yake ni kukuta nguo za mwanaume.
“Huyu malaya ana ujasiri gani wa kuishi na mwanaume ikiwa kila kitu hapa ni mali yangu?”
Nabii Sanga alizidi kuzungumza kwa hasira kali sana. Akaichomoa bastola yake na kukaa kitandani hapo huku akimsubiria Magreth na Evans kwa hamu sana.
ITAENDELEA
Haya sasa nabii Sanga anawasubiria Magreth na Evans wafike nyumbani hapo, je itakuwaje wakirudi ikiwa hawatambua uwepo wowote wa nabii Sanga? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 50.
Tuonane kesho