Sumve 2015
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 4,563
- 4,227
Mipu.mbavu tu, kwanza mtu kajitolea ye kalipia huko lakini bado wanataka kumpangia cha kufanya..mkuu story nyingi mbona zimeisha labda haujafuatilia ila story nyingi zimeisha ni arosto yako tu ya kutamani kusoma full kwa siku moja wapo watu humu nikiwemo mmoja wapo tumesoma story moja almost for 2 years na kumbe kulikuwa na possibility ya kuxoma yote kwa wiki kikubwa uvumilivu wak
Tunaomba msamaha mkuu kwa niaba ya hao wachache walokukosea, naomba utuletee mwendelezo plz..🙏🏼Naona kazi ya kujitolea inasababiswhwa navunjiwa heshima humu ndani nimeishia hapa kwa yoyote anayetaka story atawasiliana na mwandishi maana mimi sio mtunzi wa hiyo story
yeah ni kweli ucvunjike moyo kwa changamoto ndogo ndogoTunaomba msamaha mkuu kwa niaba ya hao wachache walokukosea, naomba utuletee mwendelezo plz..
Ina mana gan story ambayo hadi unasahau ilishia wap msieendekeze ujingamkuu story nyingi mbona zimeisha labda haujafuatilia ila story nyingi zimeisha ni arosto yako tu ya kutamani kusoma full kwa siku moja wapo watu humu nikiwemo mmoja wapo tumesoma story moja almost for 2 years na kumbe kulikuwa na possibility ya kuxoma yote kwa wiki kikubwa uvumilivu wak
Mipu.mbavu tu, kwanza mtu kajitolea ye kalipia huko lakini bado wanataka kumpangia cha kufanya..
Pumbavu aliyekuzaa shenzi ww kala hasara kwa kupata toto senge la mawazo embu onyesha ni mahali gani huyo anaeleta story kadhihakiwa ama kavunjiwa heshima kwa namna yoyote? Kajibiwa baada ya kusema kama mtu anataka mfululizo anaweza akatoa 5000 kwa mwandishi na atapewa stori yote, ndipo che mittoga alipouliza akituma mmoja itatumwa humu au kila mtu atoe hyo pesa? Hapo ndipo kudhalilishwa au kuvunjiwa heshima? Afuu we kima unakulupuka na kuita watu wapumbavu!! Acha uchoko wa mawazo finyu kaza fuvu hilo unefeli darasan hata fikra nazo za kuchanganua jambo unashindwa? Ulimuharibu mama yako bole njia yake na kumpa maumivu ya kutoa kiumbe dhaifu wa fikra!!Mipu.mbavu tu, kwanza mtu kajitolea ye kalipia huko lakini bado wanataka kumpangia cha kufanya..
Kaka tusimpe kichwa ni sehem gani kadhihakiwa au kudhalilishwa na kuvunjwa heshima yake?yeah ni kweli ucvunjike moyo kwa changamoto ndogo ndogo
🤝🤝🤝Au Brodre ni last born nini, ndo ameshasusa hivyo,, poa
Ndugu ulipaswa kujibu tu kama akitoa mtu itashushwa yote humu au private kuliko kuomba huruma za watu humu kisa hadithi tusipende kujiona muhim kwa vitu ambavyo havina faida sana zaidi ya kutufanya tusahau ugumu wa changamoto za hapa na pale tuNaona kazi ya kujitolea inasababiswhwa navunjiwa heshima humu ndani nimeishia hapa kwa yoyote anayetaka story atawasiliana na mwandishi maana mimi sio mtunzi wa hiyo story
Huwa sina muda wa kuargue na wapumuliwa visogoni, jitu huja unachokijua then unajitia ujuaji, kwani hujaona namba ya mwandishi? unashida nayo yote mtafute ulipie utumiwe kwa WhatsApp, swala la wewe kulipia itumwe humu na unajiona uko vizuri upstairs unaona inamake sense? kwanza kule kunamakubaliano ya kutokusambaza kazi baada ya kutumiwa, humu jamaa kafanya kujitolea tu kwa wasoweza kulipia, kuwa na akili.Ndugu ulipaswa kujibu tu kama akitoa mtu itashushwa yote humu au private kuliko kuomba huruma za watu humu kisa hadithi tusipende kujiona muhim kwa vitu ambavyo havina faida sana zaidi ya kutufanya tusahau ugumu wa changamoto za hapa na pale tu
Yeye anaeleta humu anacho kibali? Bao la baba yako bora angelimwaga njee tu na mama yako akatulia chali na kifo cha mende ukatoka kituko cha ulimwengu yaan macho na jasho la meno linakutoka kisa stori tu haya namba hyo umeona vipi umeshindwa kulipia mpaka unatafuta huruma ya kuletewa humu?senge wwHuwa sina muda wa kuargue na wapumuliwa visogoni, jitu huja unachokijua then unajitia ujuaji, kwani hujaona namba ya mwandishi? unashida nayo yote mtafute ulipie utumiwe kwa WhatsApp, swala la wewe kulipia itumwe humu na unajiona uko vizuri upstairs unaona inamake sense? kwanza kule kunamakubaliano ya kutokusambaza kazi baada ya kutumiwa, humu jamaa kafanya kujitolea tu kwa wasoweza kulipia, kuwa na akili.
Hapo umeonesha ungwana kaka pia kwenye wengi kuna challenge zinatokeaga inabid ukubali ila niwie radhi kama kuna sehem unahisi nimekukwaza kwa namna moja ama nyingine.Wakuu kwanza samahani kwa yaliyotokea kwa vile nilihidi kumaliza story ntaimaliza kwa ambao hawana muda wa kuisubiri wanaweza wasliana na muandishi tu. Tutarudi kwa utaratibu wetu kama kawaida. Siwezi leta watu wawili wakaharibia wengine.
Safi sana na hongera kwa ukomavu, watu wawili watatu wasiwe sababu ya kuwaharibia wengi.SIN 89
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 065707258 8(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
“Nashukuru sana, lengo la kukuita hapa ni kuomba ushirika wa kibiashara. Nina timu yangu ya wapishi nina omba sana uwa fundishe kupika chakula kama unacho kipika wewe nina imani uta kuwa ume tupa ujuzi mkubwa sana”
Magreth akatabasamu kwa maana japo yeye ana mgahawa, ila ukweli ni kwamba ana wateja wengi sana kwani wana penda mapishi yake.
“Kaka yangu hilo unalo lizungumza kwa namna moja ama nyingine ina wezekana au pia isiwezekane?”
“Kwa nini dada?”
“Kuna upishi wa kusomea na upishi wa kipaji. Mimi sikuwahi kuingia shuleni na kusomea mapishi, ila ni k……….!!”
Magreth akajikuta macho yakimtoka huku akijawa na mstuko mkubwa sana. Hakuamini macho yake kumuona Evans akikatiza mbele ya macho yake na akakaa kwenye kiti kingine huku akisubiria huduma ya wahudumu wa hoteli hiyo.
ENDELEA
“Ngoja nina kuja”
Magreth alizungumza hukua kinyanyuka kwenye kiti hicho. Akatembea hadi katika meza hiyo na kusimama mbele ya Evans.
“Evans”
Magreth aliita kwa mshangao, ila Evans akajitahidi sana kuwa kama mtu asiye mfahamu kwa maana kwa matatizo aliyo sababishiwa na mwana mke huyo yali vuruga sana ndoto zake za maisha.
“Evans ni wewe mume wangu?”
“Samahani dada, una zungumza na mimi?”
Evans akajitahidi kuibadilisha sauti yake ila haikumzuia Magreth kukaa kwenye kiti cha pembeni huku akimtazama Evans usoni mwake.
“Evans natambua kwamba nime kukosea na nina jua kuna mambo mengi sana ume yapitia. Ila nina kuomba unisikilize”
Magreth alizungumza kwa sauti ya unyonge na ya kubembeleza. Evans akashusha pumzi huku akimtazama Magreth.
“Samhani dada uta kuwa ume nifananisha”
“Hapana siwezi kukufananisha. Kwenye maisha yangu mtu wa pekee ambaye nina mfahamu sana ni wewe”
“Dada yangu nina kuomba unielewe mimi sio huyo mtu ambaye una mtafuta”
Evans mara baada ya kuzungumza maneno hayo akasimama na kuanza kuondoka eneo hilo. Magreth akamtazama jinsi anavyo tembea, moyo wake ukakataa kabisa kuamini anacho kizungumza Evans. Akanyanyuka kwa haraka na kuanza kumfwata kwa nyuma. Wakafika kwenye eneo la lifti.
“Umekuja hadi huku”
Evans alizungumzahuku akimtazama Magreth kwa macho ya hasira sana. Kabla hata Magreth hajazungumza jambo lolote, lifti hiyo ikafunguka, Evans akawahi kuingia na Magreth akamfwata kwa nyuma. Kila alama ambayo anayo Evans hata huyu mtu anayo.
“Wewe dada una kwenda wapi?”
Evans alizungumza kwa ukali sana huku akimkazia macho Magreth.
“Nahitaji kufahamu ukweli. Kama wewe sio Evans mimi nita kuacha uendelee na maisha yako na kama kweli wewe ni Evans basi nina hitaji kukuomba masamaha”
Magreth alizidi kuwa king’ang’anizi hadi Evans akajikuta akiminya kitufe cha gorofa anayo elekea. Walipo fika katikati ya gorofa ya pili, Magreth akaminya kitufe cha kuisimamisha lifti hiyo.
“Una taka kufanya nini?”
“Natambua tumboni kwako una jeraha la kuchomwa kisu nina kuomba niweze kukutazama. Endapo nita likuta jeraha hilo basi moja kwa moja wewe uta kuwa ndio Evans ila nisipo likuta basi nita shukuru kwa ushirikiano wako”
Kauli hiyo ya Magreth ikamstua sana Evans, akashusha pumzi huku akijifikiria kufungua tumbo lake.
“Ina kuwa ni jambo la ajabu sana pale unapo mg’ang’aniza mtu kufanya kitu asicho kipenda”
“Nalitambua hilo ila nina kuomba sana ufungue vifungo vya shali lako. Nipo chini ya miguu yako”
Evans akamtazama Magreth kwa sekunde kadha machoni mwake, kisha taratibu akaana kufungua vifungo vya shati lake.
Magreth macho yakamtoka, huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi. Eneo zima la kuanzi kifuani mwa Evans hadi tumboni mwake, lime jaa alama za majera makubwa makubwa. Evans akamalizia kuvua shati hilo na kugeuka na kumuonyesha Magreth majeraha mengine mgongoni mwake.
“Nina imani kwamba mtu anaye mtafuta sio mimi. Hivyo samahani sana”
Magreth akashindwa hata kuzungumza jambo la aina yoyote. Akaanza kungua kilio huku akikaa chini. Evans akaminya kitufe cha kuiruhusu lifti hiyo kuendelea kupanda juu huku akivaa shati lake.
“Dada una weza ukaondoka”
Evans alizungumza huku akimtazama Magreth aliye nyong’onyea kwa kushindwa kuona kile alicho kitarajia. Evans akatoka ndani ya lifti hiyo, akaanza kutembea kuelekea katika chumba chake. Magreth akajikaza taratibu huku akiminya kitufe cha kurudi chini. Evans alipo shuhudia lifti ina jifunga na kuanza kurudi chini, akaingia chumbani kwake kwa maana haijtaji Magreth kutambua chumba anacho kaa.
Taratibu Magreth akatoka nje la lifti hiyo, akaanza kutembea kwa unyonge, hakukumbuka hata kikao chake na meneja wa hoteli hiyo.
“Dada Magreth”
Maneja alimuita huku akimtazama usoni mwake.
“Mbona hivyo kuna tatizo”
“Tuwasiliane siku nyingine. Nina hitaji kupumzika sasa hivi”
Magreth alizungumza na kutoka nje ya hoteli hiyo, akaingi ndani ya gari lake. Machozi yakazidi kumbubujika, moyo wake bado una amini kwamba yule ni Evans ila kwa jinsi majeraha yalivyo mjaa mwilini mwake ana onekana amepitia mateso mengi sana yaliyo mpelekea kuwa katika hali kama hiyo.
“Kwa nini wame mtesa hivi mume wangu hadi hanikumbuki”
Magreth aliendelea kuzungumza huku akilia kwa uchungu sana. Akawasha gari lake na kuondoka hotelini hapo na kurudi nyumbani kwake.
“Una kwenda wapi”
Sauti hiyo ya kike ika mstua sana Evans ambaye ana kusanya kila kilicho chake ili kuondoka katika hoteli hiyo kwa maana hahitaji kabisa kuwa karibu na Magreth. Akageuka nyuma yake na kumkuta jini anaye muwezesha kwa kila jambo akiwa amesimaam kwenye moja ya kona ya chumba hicho.
“Nina hitaji kuondoka hapa hotelini”
“Kwa nini?”
“Yule mwanamke ana weza kurudi tena hapa na akanifanyia fujo mimi”
“Hawezi kurudi”
“Una uhakika gani?”
Dada huiyo akatabasamu huku akimtazama Evasn, akamsogelea Evans na kumshika mikono yake.
“Kama nime kupatia pesa za kutosha na nina kutoa kwenye hatua moja ya maisha na kwenda kwenye hatua nyingine una hisi nita shindwa kumzuia Magreth kurudi hapa?”
“Nime kuelewa”
Evans alizungumza huku akishushusha pumzi taratibu.
“Jambo la msingi hapa ni kuhakikisha kwamba una endelea na mapango ulipo mbeleni na wala usimfikirie huyo mwana mke tena. Umenielewa”
“Ndio”
“Endelea na mambo yako mengine. Usiku mwema”
“Ngoja mara moja?”
“Ehee?”
“Hivi huwa una kuwa karibu yangu kila mara au?”
“Ndio nina kufwatilia kila unapo kuwa na mimi ndio mlizi wako. Sawa”
“Haya”
Mwana dada huyo akapotea ndani hapo na kumuacha Evans peke yake.
***
Magreth akafika nyumbani kwake huku akiwa mnyonge sana. Akashuka kwenye gari lake na kuingia ndani, akamtazama rafiki yake Josephine aliye kaa sebleni hapo akitazama televishion.
“Mage upo sawa?”
Josephine aliuliza huku akimtazama Magreth anaye kaa kiunyonge kwenye moja ya sofa.
“Mage mbona uso wako ume jaa huzuni na umepoteza nuru ya furaha. Niambie kuna tatizo gani linalo kusumbua?”
“Nime kutana na Evans”
“Evans?”
“Ndio nime kutana naye na nimezungumza naye”
“Hapana Magreth, mbona nina sali sana juu ya hilo jambo ila simuoni. Inakuwaje huyo uliye kutana naye akawa Evans?”
“Yaani wee acha tu. Nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kwamba nina mueleza juu ya maisha yetu ya nyuma, ila alikataa katu katu na kusema kwamba yeye sio Evans”
“Mmmmm”
“Nilimuomba sana kuona jeraha la kisu katika tumbo lake. Alikubali na akavulia shati lake. Huwezi amini mwili wake umejaa alama za majeraha, mithili ya mtu aliye pigwa mijeledi. Isitoshe aliendelea kunisisitizia kwamba sio yeye”
“Wewe ume kunata naye wapi?”
“Kwenye hoteli hii iliyopo hapa wapi?”
“Ahaa hiyo hoteli ya hadthi ya nyota tano?”
“Ndio”
“Sasa ikawaje?”
“Nilimuruhusu aondoke kwa maana, kila sehemu ya mwili unayo mtazama ni yeye ila kwenye sauti kidogo ndio kuna utofauti na sikuweza kuona jeraha la siku, nahisi ni kutokana na kujaa alama hizi za mijeledi”
“Msikini, kama ata kuwa ni yeye basi hato kuwa na kumbukumbu zozote kuhusiana na wewe?”
“Ni kweli, nina imani kuna mateso mengi sana wamapatia.”
“Bado sijapata jibu, ni nani ambaye ana husika na kumteka kwake?”
“Sali rafiki yangu Mungu akufunulie katika hilo.”
“Nita sali leo usiku, ila nina kuomba sana usi panic katika hili jambo nina imani kwamba Mungu ata tusaidia kupata ufumbuzi”
“Amen”
Magreth akanyanyuka na kuingia chumbani kwake. Akawasha laptop yake na kuingia kwenye upande wa barua pepe. Akaanza kupitia picha za vazi lake analo lihitaji.
“Sanga lazima nidili na wewe”
Magreth alizungumza kwa msisitozo. Akajibu email hiyo na kuwaruhusu waendelee na utengenezaji wa vazi hilo. Kila muda akili yake ina mfikiri Evans aliye kutana naye hotelini. Akachukua simu yake, akaitafuta namba ya nabii Sanga, alipo ipata akampigia. Simu ya nabii Sanga ikaanza kuita kisha ikapokelewa.
“Una hitaji nini?”
“Natambua wewe ndio una husika na kumteka Evans wangu na umempatia kumbukumbua hadi akapoteza kumbukumbu zake juu yangu. Nina kuahidi kitu ambacho nita kufanyia Mungu mwenyewe ndio atakaye jua”
“Hivi wewe binti muuza maandazi una jiamini nini haswa hadi una kuwa ni mtu wa kunitisha tisha kisa hicho kiji vulana chako ehee?”
Nabii Sanga alizungumza kwa ukali sana.
“Aahaa una hisi ni kivulana si ndio?”
“Ndio ni kivulana. Ngoja nikuambie jambo moja sina muda mchafu na kuhangahika na hicho kijimasikini chako. Sasa hivi nina dili na ndoa ya binti yangu kama uta taka kadi wewe sema na sio kunipigia pigia kelele. Umenielewa?”
“Okay nime kuelewa”
Magreth alizungumza kwa hasira huku akimwagikwa na machozi usoni mwake. Akakata simu na kuirushia kitandani kwa hasira huku akipiga kelele za hasira.
“Mage Mage”
Sauti ya Josephine ilisikika akimuita Magreth kwa msisitizo. Josephine akaingia ndani hapo na kumkuta Magreth akilia kwa uchungu sana. Ikamlazimu Josephine kuanza kumbembeleza rafiki yake huyo kwa maana ana tambua ni magumu gani ambayo ana yapitia kwa kipindi hichi.
***
“Nani huyo baba?”
Julieth alizungumza huku akimtazama baba yake.
“Ni yule malaya”
“Nani?”
“Magreth ana dai sijui yule Evans ame poteza kumbukumbu zake kwa kuteswa”
“Ina maana yupo hai Evasn?”
“Nahisi hivyo kwamba yupo hai”
“Baba nina hitaji kumuua huyo kijana. Nahitaji kuhakikisha kwamba siri yangu ya usichana wangu haitoki kwa mtu yoyote. Endapo ikitoka, baba tuna poteza kila kitu na hatuto kuwa na ndo”
Julieth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama nabii Sanga usoni mwake.
“Achana naye kwa maana hato weza kufanya hivyo. Isitoshe kwamba akili yake kwa sasa haipo sawa”
“Baba!!!”
“Ndio, hatuna haja ya kushuhulika naye isitoshe daktari ame dhibitisha kwamba wewe ni bikra, huna haja ya kuendelea na kumfikiria”
“Sawa baba nime kuelewa
***
“Tusikilizane?”
Emmy mkuu mpya wa kitengo cha NSA alizungumza huku akiwatazama wanafunzi hao walio ingia kwenye chumba cha kufanyia kazi ya kuhakikisha wana chukua nafasi ya watumishi walio jiuzulu wa kitengo hicho cha NSA.
“Kazi yetu ni moja tu. Tuna hitaji kutafuta eneo ambalo ndio makao makuu ya kikosi cha kigaidi cha Al-Shabab ambao siku moja iliyo pita waliweza kuwashambulia askari wetu baharini na kuwaua vibaya sana kama hivyo munavyo ona kwenye hiyo video hapo”
Emmy alizungumza huku akiwaonyesha video hiyo wanafunzi hao ambao walibakisha mwenzi mmoja kabla ya kuhitimu katika kitengo hicho.
“Ina tupasa kuhakikisha tuna lipa kisasi kwa watu hao. Tuna masaa matano hadi asubuhi tuwe tumesha ikamilisha kazi hiy…….”
Kabla ya Emmy hajamalizia sentensi yake, computer zote ndani hapo zikaanza kuzima na kuwaka na ndani ya dakika moja zikazima moja kwa moja na hapakuwa na hata moja iliyo waka.
“Mkuu masaa hayo matano uliyo toa hayato tosha”
Kijana mmoja alizungumza huku akimtazama Emmy usoni mwake.
“Kwa nini?”
“Data zote zilizo kuwa zina hifadhiwa kwenye hizi computer zime futwa hivyo hatuwezi kufanya jambo la ina yoyote”
Emmy akajikuta akitukana kwa hasira kwa maana ana tambua ni lazima wafanyakazi walio ondoka ndio wame sababisha jambo hilo.
ITAENDELEA
Haya sasa data zote ambazo Emmy alikuwa ana zitegemea na vijana wake hao wapya zime futika je wata fanikiwa kuiendesha oparesheni hiyo, usikose se hemu ya 90.
OkKabla sijaanza naomba niwahakikishe kwamba hii story nimepewa ruhusa na mwandishi kupost humu. Kila siku ntakua napost na nawahakikishia story itaisha kabisa.
SIN 01
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
Kila mwanachuo ndoto zake ni kuweza kupata ajira nzuri sana kwa kile alicho kisomea kwa miaka mingi sana kipindi alipo kuwa chuoni. Ila mambo ni tofauti sana kwa kijana Evans Shika. Elimu ya Masters of Business Administration – International Business aliyo isoma katika chuo cha IFM, inamfanya azidi kutesaka sana katika swala zima la kutafuta ajira. Kila ofisi aliyo weza kupeleka maombi ya kuajiriwa, ana kataliwa na kujikuta ana zidi kukumbana na maisha magumu sana yaliyopo katika jiji la Dar es Salaa.
“Evans”
Lukas rafiki yake wa karibu alimuita huku akimtazama usoni mwake.
“Niambie kaka”
“Nina mazungumzo muhimu nahitaji kuongea na wewe. Kmaa unaweza kunipatia muda wako basi nakuomba tuzungumze”
“Sawa kama tuzungumze tu”
Evans alizungumza huku akikaa kitako kitandani na kumtazama Lukas aliye kalia stuli moja iliyomo ndani ya geto hilo.
“Lidya ni mjamzito na hapa ninavyo zungumza kwao wametambua hilo na baba yake ameamua kumfukuza”
“Mungu wangu….Sasa utafanya nini kaka?”
“Sina jinsi zaidi ya kumleta hapa kaka. Nilazima niishi naye kwa maana hakuna namna”
“Mmmm kaka sasa kweli tutaweza kuishi watatu geto moja!?”
“Ahaa kaka hatuta weza. Mimi naona kwa sasa uweze kujitafutia maisha mengine ndugu yangu. Usinifikirie vibaya au kuhisi kwamba nina kufukuza nyumbani kwangu. Hapana, ila shemeji yako ndio huyo ana kuja na kwakweli sikujipanga kabisa kuhimili maisha ya kuhudumia watu wawili.”
Maneno ya Lukas yakamstua sana Evans. Mapigo yake ya moyo yakaanza kumuenda kasi huku kijasho kikianza kumtiririka usoni mwake. Hakika toka alipo maliza chuo na kukosa ile mikopo ambayo wanapatia kwa ajili ya kujikimu, maisha yake yamekuwa magumu sana, kiasi cha kujikuta akipata hifadhi kwa rafiki yake Lucas ambaye naye kwa sasa amekabiliwa na majukumu mazito sana.
“Kaka wewe ni mwanaume. Ninakushauri, hembu jishikize kwenye vibarua vidogo vidogo japo upate vimiambili mia tatu vya kukukimu. Haya maisha ya kusema utafute kazi hizi ambazo mwisho wa siku unatoka hola, huoni kwamba una jicheleweshea malengo yako?”
Maneno ya Lucas hayakuweza kuleta matumaini wala faraja kwa Evan ambaye hatambui ni wapi atakapo kwenda. Kila akijaribu kulichanganua hili jiji la Dar es Salaam, hakika hana ndugu wa kuweza kuishi kwake.
“Evans, Evans”
“Naam kaka”
“Sijui umenielewa nilicho kuambia?”
“Yaa nimekuelewa kaka”
“Kuna ishu nyingi sana hapa mjini. Tazama mimi, ninaosha magari japo elimu yangu ni form four ila kidogo nina pata mia mbili mia tatu bro. Changamka hapa ni mjini usiamini sana kwenye maswala ya vyeti kaka.”
Evan taratibu akanyanyuka kitandani, akachukua begi lake la nguo pamoja na begi lake la mgongoni. Akafungua begi la mgongoni na kuhakikisha kwamba bahasha yenye vyeti vyake ipo salama. Alipo jiridhisha akalifunga na akalivaa mgongoni na kumtazama Lukas.
“Nashukuru kaka kwa kipindi chote ulicho weza kunivumilia kwa kukaa humu ndani. Nitaufanyia kazi ushauri wako”
“Nashukuru sana kaka. Kamata hii buku tano itakusaidia japo hata kwa chakula cha mchana huu na usiku”
Evans akautazaama mkono wa kulia wa Lukas unao mpatia kiasi hicho cha pesa. Kisha taratibu akaipokea na kuiweka mfukoni mwake.
“Asante kaka”
“Poa kaka ila nakuomba usinifikirie vibaya”
“Wala usiogope kaka, nimekuelewa na ninaelewa hali uliyo nayo ndugu yangu”
“Nashukuru sana kwa kuweza kulitambua hilo”
Lukas akanyanyuka kisha wakakumbatiana. Evans akatoka ndani ya chumba hichi. Akasimama eneo la nje la chumba hichi, akayatazama mazingira ya nyumba hii iliyopo, Tandale kwa tumbo. Taratibu akaanza kukatiza kwenye vichochoro vya nyumba hizi huku kichwani mwake akiwa na mawazo lukuki. Kila anavyo jaribu kumfikiria mama yake na mdogo wake wa kike walipo mkoni Kigoma, anashindwa kabisa kupata ujasiri wa kurudi kwao, kwani ufukara wa nyumbani kwao ndio umemfanya aweze kusoma kwa juhudi ili kujikomboa kwenye umasikini huo.
“Siwezi kurudi Kigoma”
Evans alizungumza mwenyewe huku akiendelea kukatiza kwenye vichochoro vilivyo jaa maji machafu, hii ni kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha kwenye jiji la Dar es Salaam. Evans akiwa katika chochoro moja, gafla akakutana na kundi kubwa la wahuni likiwa limebananisha dada mmoja aliye shika deli lililo jaa maandazi.
“Jamani maandazi yangu hayo ninauza musiyafanye hivyo”
Dada huyu alilalama huku akiwa amebananishwa ukutani, huku wahuni wengine wakiendelea kuyatafuna maandazi hayo bila hata ya kumuonea huruma.
“Tulia wewe. Kama hutaki tuyale tutakupa kifir** ambacho hujawahi kukipata toka uzaliwe”
Muhini mmoja alizungumza huku akimnyooshea panga la usoni dada huyo.
“Wewe mseng** una kodoa kodoa nini macho au unataka na wewe tuje kukupaku** hapo”
Muhuni mwengine alizungumza huku akimnyooshea Evans kisu. Katika maisha yake yote Evans amekuwa ni mtu ambaye hapendelei kushuhudia mwanamke ana nyanyasika mbele ya macho yake. Kushikwa shikwa kwa dada huyu, kukazirudisha kumbukumbu zake miaka kumi na mbili iliyo pita, kipindi akiwa na miaka kumi na mbili. Marehemu baba yake, alikuwa akimtesa sana mama yake na kumpa kipigo kizito mithili ya mwizi. Mzee Shika alisifika kwa ulevi na ubabe katika kijiji chao. Alikuwa ni mtu mwenye roho katili sana asiye jali utu wa mtu mwengine. Si mama yake tu aliye kuwa akishushiwa kipigo bali hata yeye mwenyewe alikuwa akibamizwa kisaswa sawa. Chuki na hasira juu ya mateso anayo yapata mama yake, yakatengeneza tabaka baya sanamoyoni mwa Evans dhidi ya baba yake.
Usiku wa siku moja kama kawaida, baba yake alirudi akiwa amelewa chakari. Kitendo cha mke wake kuchelewa kumfungulia mlango, ikawa ni kosa kubwa sana kwake. Alimkama mke wake na kuanza kumpiga bila ya huruma, huku mama Evans tumboni mwake akiwa ni mjamzito. Vilio vya mama yake akiomba msaada kwa watu vikamfanya Evans, kuvuta shoka alilo liweka chini ya kitanda chake na kutoka chumbani kwake huku akiwana hasira sana. Akaelekea kilipo chumba cha mama yake. Kwabahati nzuri akakuta chumba cha wazazi wake kikiwa wazi. Akaingia ndani na kumkuta mama yake akiwa amelala sakafuni huku akiendelea kushindiliwa mangumi ya uso na mzee Shika.
Shetani wa hasira na ujasiri, akamjaa Evans moyoni mwake. Akanyanyua kishoka hicho na kumpiga nacho baba yake usogoni na kikazama karibia nusu, na kusababisha damu nyingi sana kuanza kutapakaa ndani ya chumba hicho.
“Evan..s mwanangu umeniua”
Mzee Shika alizungumza huku akianguka chini na kupoteza uhai wake hapo hapo. Kofi zito alilo pigwa dada huyo muuza maandazi likamtoa Evans kwenye dibwi zima la mawazo. Akashuhudia jinsi wahuni hao wanavyo mchania nguo dada huyo huku wengine wakimshika shika maeneo ya siri pamoja na maziwa yake.
“MUACHENIII NIMESEMA”
Evans alizungumza kwa ujasiri na sauti ya juu. Wahuni hao wapatao sita, wakamtazama kwa sekunde kadhaa, kisha wakaanza kuangua kicheko cha dharau na kejeli.
“Mchekini huyu matak** ametokea wapi?”
Muhini mmoja alizungumza huku akianza kumsogelea Evans. Taratibu Evans akaweka begi lake chini na kujiandaa kwa lolote ambalo linaweza kujitokeza. Muhuni huyu aliye shika kisu mkononi mwake, akamvamia Evans, ila Evnas, hakuwa mjinga wala mzembe. Akamtandika ngumi nzito ya kichwa na kumfanya jamaa huyu kupepesuka na kuanguka chini. Wezake wakajawa na hasira na wakagairi zoezi la kumbaka mwana huyo. Wakamvamia Evans kwa pamoja na kuanza kupambaba naye. Wingi wao ukamfanya Evans ashindwe kabisa kuwakabili, wakamtembezea kichapo huku mmoja wao akimkita kisu cha tumboni na kumfanya Evans kuanguka chini.
“Oya mwana umeua. Msala msala huu.”
Mmoja wao alizungumza mara baada ya damu nyingi zilizo toka tumboni mwa Evans kumrukia mwilini mwake. Wakanza kuchanguka huku wakibeba mabegi yake yote mawili ya Evans, wakiamini kwamba ndani ya mabegi hayo wana weza kupata chochote kitu.
Mwana dada huyo akaanza kupiga kelele za kuomba msaada kwa watu kwani Evans anaendelea kutokwa na damu nyingi sana mwilini mwake. Wasamaria wema wakajitokeza na kuanza harakati za kumpa msaada Evans ambaye tayari amepoteza fahamu zake. Evans akafikishwa kwenye hospitali ya mwana nyamala.
“Amefanyaje?”
Nesi mmoja aliuliza huku akiwatazama watu hawa alio mleta hapa hospitalini.
“Amevamiwa na wahuni”
Dada muuza maandazi alijibu huku jasho na machozi yakimwagika.
“Muna pf3 ya askari?”
“Hatuna dada, tunaomba mutusaidie”
“Sasa hatuwezi kumtibu mgonjwa aliye vamiwa bila ya kibali kutoka polisi. Akitufia hapa hamuoni kwamba itakuwa ni hatari kwetu.”
“Dada nipo chini ya miguu yako nakuomba mumpokee. Nipo tayari kwenda kuitafuta hiyo sijui pp3 polisi. Ila nakuomba mumtibu huyu kijana”
Dada muuza maandazi alizungumza huku akimpigia nesi huyu magoti. Ushawishi wa watu wengine walio msaidia Evans, ukaulainisha msimamo wa nesi huyu na kujikuta akikubaliana nao na kuwaomba wahakikishe kwamba wana tafuta kibali cha matibabu kutoka polisi.
“Nashukuru nashukuru sana dada”
Dada muuza maandazi alizungumza huku akitoka baru ndani ya hospitali hii na kuelekea kituo cha polisi. Akafanikiwa kufika polisi na kuelezea hali nzima ya tukio lilivyo tokea.
“Mgonjwa yupo wapi?”
Afande Mwahila aliuliza huku akimtazama dada huyu.
“Mwanayamala hospital”
“Unaitwa nani dada?”
“Naitwa Magreth”
“Hao vijana walitumia silaha gani kuwashambulia?”
“Visu na mapanga”
“Hao ni panya road. Wanarudi tena ehee?”
Askari mwengine alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake. Magreth hakuweza kujibu jambo lolote zaidi ya kukaa kimya. Akaandikiwa ruhusa hiyo na kurudi hospitali ya Mwananyamala. Akamkabidhi nesi hati hiyo na matibabu ya Evans yakazidi kuendelea.
“Sasa mgonjwa amepoteza damu ya kutosha. Benk yetu ya damu hapa hospitalini ime kwisha. Kama unaweza kumchangia japo chupa moja itakuwa ni vizuri sana kwani kwa sasa mgonjwa yupo kwenye chumba cha upasuaji”
“Nipo tayari nesi”
“Basi jaza hii fomu hapa majina yako matatu. Kisha nifwate”
Magreth akasoma fomu hiyo ya kuchangia damu. Alipo ridhishwa na maelezo yaliyo andikwa kwenye fumo hiyo akajaza kilicho hitajika kisha akafwatana na nesi hiyo. Magreth akapimwa HIV na kwa bahati nzuri akakutwa yupo salama.
“Sasa unaweza kuchangia damu”
Nesi huyo alizungumza huku akianza taratibu za kutoa kiasi cha damu mwilini mwa Magerth.
“Ila mgonjwa atapona ehee?”
“Tuombe Mungu kwani kwa sasa yupo kwenye chumba cha upasuaji, madaktari wandelea na kazi ya kumuhudumia.”
“Ehee jehova, shusha muujiza wako mgonjwa aweze kupona. Damu ya Yesu kristo ikamuangazie”
Magreth alijikuta akipiga maombi na kumfanya nesi huyu kumshangaa.
“Mgonjwa ni nani yako?”
“Ni mpita njia”
“Mpita njia tu ndio una muombea hivyo. Mimi nilidhani ni kaka yako au ndugu yako kumbe mpita njia?”
Maneno ya nesi huyu yakauumiza moyo wa Magreth, ila hakuhitaji kumjibu chochote zaidi ya kuendelea kumlilia na kumuomba Mungu wake kimoyo moyo.
Madaktari wakazidi kujitahidi kwamba wana fanya upasuaji wa kukitoa kisu alicho chomwa Evans tumboni mwake. Upasuaji huo ukafanikiwa kuisha salama ndani ya masaa mawili. Evans akapelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi huku akiwa hajitambui kabisa.
“Nina weza kumuona mgonjwa wangu dokta?”
Magreth aliuliza swali huku akiwa amesimama nje ya chumba cha wagonjwa mahututi.
“Hapana kwa sasa huwezi kumuona kwani hali yake haijawa sawa”
“Ila anaweza kupona?”
“Hilo ni jambo la kumuomba Mungu, ila kwa sisi tumeweza kuikamilisha kazi yetu. Hatua inayo fwata ni hatua ya Mungu”
Dokta Mkama alimjibu Magreth kwa sauti ya upole huku akimtazama usoni mwake.
“Nashukuru”
“Nifwate ofisini kwangu”
Dokta Mkama na Magreth wakaongozana hadi ofisini na wakaka kwenye viti vilivyomo ofisini humo..
“Mgonjwa wako ana itwa nani?”
Magreth akaka kimya huku akimtazama dokta Mkama.
“Mbona kimya”
“Ahaa…simfahamu mgonjwa”
“Humjui? Mbona ume muhangaikia kwa kiasi kikubwa sana ikiwa mtu umtambui?”
“Bila ya huyu kaka mimi sasa hivi wala nisinge kuwa nimekaa mbele yako na kujibu maswali unayo niuliza. Alijitolea kupamabana na kundi la wahuni wa Panya Road, ili kuweza kuyaokoa maisha yangu.”
Magreth alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Okay nimekuelewa. Je upo tayari kubeba garama za kutibiwa kwa mgonjwa au kuna namna nyingine labda ya kuwasiliana na ndugu zake, wakakusaidia?”
Magreth akaka kimya huku akitafakari. Kwaufupi maisha yake naye ni magumu sana, biashara ya kutembeza maandazi mtaani ndio inayo mfanya aweze kuishi katika jiji hili la Dar es Salaam. Japo na uzuri wa kipekee alio barikiwa na Mungu, ila haitaji kuutumia uzuri wake huo kuwa kigezo cha kujipatia kipato kwa njia ya umalaya wa kujiuza.
“Nakusikiliza upo tayari tukuandike wewe ndio msimamizi wa mgonjwa huyu”
Magreth akamtazama daktari Mkama kisha akamuitikia kwa kutingisha kichwa, akimaanisha kwamba ame kubaliana nahilo.
“Sawa nitakuandikia garama zote hapa ambazo tumeweze kuzitumia katika kumuhudumia mgonjwa wako. Na tutakupigia bei ya yeye kulala ICU kwa siku moja”
“Sawa dokta”
Magreth akakaa kimya huku akimtazama dokta Mkama jinsi anavyo endelea kucharaza kwa peni karatasi iliyopo mezani mwake. Dokta Mkama alivyo maliza kuiandika karatasi hiyo, akaipitia kwa kuisoma kama kila alicho kiandika ni sahihi kisha akamkabishi Magreth. Taratibu Magreth akatupia macho yake kwenye karatasi hiyo. Moyo ukampasuka, kwani garama iliyo andikwa kwenye karatasi hiyo ni kubwa na toka kuzaliwa kwake hajawahi kumiliki kiasi hicho cha pesa .
ITAENDELEA
Haya sasa mambo ndio yameanza? Evans hali yake ni tete kitandani. Msaada wake wa mwisho ni Magreth ambaye naye uwezo wake ni duni, je ni wapi Magreth atakapo weza kupata kiashi hicho kikubwa cha pesa?Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 02