SIN 196
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
Website………………………………………………
www.storyzaeddytz.com
ILIPOISHIA
“Kwa kuonana pale ita kuwa ngumu. Niambie ofisini zenu zipo wapi ili nije?”
Josephine akamtazama Josephine kwa maana hadi sasa hawana ofisini na hiyo kazi wanayo izungumzia ni uongo.
“Ahaa kwa sasa nipo nje ya ofisini. Kama huto jali tukutane sehemu tofauti na ofisini”
“Poa basi tukutane Sinza, kwenye mgahawa mmoja una itwa AJ.”
“Poa nashukuru”
“Baada ya dakika kumi nita kuwepo hapo”
“Sawa nita fika hapo baada ya nusu saa”
Josephine mara baada yakukata simu wakakumbatiana na Josephine huku wakiwa wamejawa na furaha kubwa sana kwani leo rafiki yake ana kwenda kukutana na mwanaume ambaye ame mchanganya kimapenzi.
ENDELEA
“Nusu saa kutoka huku kigamboni hadi Sinza halitoshi kama tukitumia gari. Cha kufanya tutumie pikipiki”
Magreth alishauri na kwa haraka wakaanza kujiandaa na kisha wakaondoka nyumbani hapo. Kwa ujuzi wa Magreth na uwezo wake wa kuendesha pikipiki hiyo, wakafanikiwa kufika Sinza katika mgahawa walio elekezwa ndani ya muda mchache tofauti na vile walivyo weza kumuahidi Evans. Wakaingia kwenye mgahawa huo ambao kidogo ume jaa watu. Wakaangaza angaza na Evans akaonyoosha mkonono kuwaashiria kwamba wamuone.
“Yule pale”
Magreth alizungumza huku akiwa amejawa na furaha sana. Mapigo yake ya moyo yakamuanza kumuenda kasi huku hali tofauti ikimtawala mwili wake. Evans akasimama na wakaanza kusalimiana.
“Mimi nina itwa Josephine ndio tulizungumza kwenye simu n a huyu hapa ni rafiki yangu ana itwa Magreth”
Josephine alizungumza huku uso wake ukiwa ume jawa na tabasamu pana. Bumbuwazi lililo mkamata Magreth hakika likamfanya hadi Evans kuhisi kama ame fahamika kwa maana msichana huyo ana mfahamu vizuri sana.
“Mage”
Josephine alimgonga kidogo Magreth begani mwake, kwani Evans amenyoosha mkono kwa sekunde kadhaa pasipo Magreth kuupokea.
“Yeah habari”
Magreth alizungumza huku akishusha pumzi.
“Salama, nina itwa George. George Sanga”
Evans alizungumz akwa suati nzito ambayo ikazidi kumchanganya Magreth.
“Tuna shukuru kukufahamu”
Magreth alijibu huku wakiachiana mikono na Evans wanaye mfahamu kwa jina la George.
‘Kweli Mungu ana nipenda, yaani maandui zangu wamajileta wao wenyewe na mbaya hawajanifahamu’
Evans alizungumza kimoyo moyo huku akimtazama Magreth aliye jikuta akihisi aibu kwa kukodolewa macho hivyo na kujikuta akitazama chini.
Ehee niambieni, lengo la kuonana na mimi ni nini?”
Evans aliendelea kuzungumza kwa sauti ya kunguruma huku akimtazama Josephine.
“Ahaa…a.a..aaa”
Josephine naye alijikuta akijing’ata ng’ata kwa maana katika maisha yake siku zote huwa ana ogopa sana kuongopea.
“Vipi?”
“Ahaa kusema kweli ni jambo moja kaka yangu George. Nime tokea kukupenda sana, toka nilipo kuona pale jana Samaki Samaki, hakika ume weza kuuteka moyo wangu. Hapa nilipo nina jihisi mwili wangu kuishiwa nguvu kwa upendo wako”
Magreth alizungumz akwa kujiamini hadi Josephine macho yakamtoka kwa maana hakutajarijia kama Magreth ana weza kufunguka kwa namna hiyo. Evans akatabasamu huku akimtazama Magreth usoni mwake, muhudumu akafika mezani hapo.
“Wasikilize wageni wangu”
“Muna tumia nini dada zangu”
“Mimi nina omba Safari ya baridi”
Magreth alizungumza kwa kujikaza.
“Safari!!?”
Josephine aliuliza kwa mshangao kwa maana toka amfahamu Magreth hajawahi kumuona siku hata moja akiwa ana kunywa kilevi chochote. Evans naye macho yakamtoka kwa maana na mtambua vizuri Magreth na kuhitaji kunywa huko pombe kuna kitu kinacho endelea kwenye kichwa chake.
“Nisikilize dada, tuletee Cocacola mbili, hiyo safari achana nayo”
“Hapana Josephine nina hitaji kunywa?”
“Hapana, ingekuwa tume kuja na gari hapo sawa ninge kuruhusu kunywa. Ila tumekuja na ile tukutuku, mimi siwezi kuiendesha bwana”
Josephine alionyesha wasiwasi wake upo wapi.
“Mletee Cocacola”
Evans alimbidi kuingilia kati jambo hilo.
“Sawa, je muna tumia chakula gani?”
“Tuta kuambia tukuhitaji”
Josephine alijibu na muhudumu huyo akaondoka na baada ya muda akarudi akiwa na chupa mbili za Cocacola pamoja na glasi mbili zenye tishu ndani. Baada ya muhudumu kuondoka maongezi yakaendelea.
“Ume niambia una nipenda kwa namna gani?”
Evans akajifanya kama vile haijui kitu alicho ambiwa kina maanisha nini.
“George nina imani kwamba uta kuwa una nishangaa sana. Ila mimi sio wale wanawake malaya, mimi nime zungumza kitu kilichopo moyoni mwangu. Nina kupenda sana George, nilisha wahi kumpenda mwanaume kama hivyo, ila Mungu hakupenda niwe naye hivyo tuliachana. Ila wewe toka nilipo kuona, moyo wangu uliweza kustuka sana, tafadhali Geogre naomba unielewe”
Maneno ya Magreth yakamfanya Josephine kufumba macho yake kwa maana badala ya rafiki yake kutongoza sasa ni wakati wa yeye kutongoza na jambo hilo ni aibu kubwa sana kwa wanawake wengi wa Kitanzania.
“Una jua mimi siwajui nyinyi ni kina nani, muna jishuhulisha na nini. Niliwaona tu jana pale mgahawani, sasa ukiniambia hayo maneno nina weza kupata mashaka. Isije mukawa ni watu mulio tumwa na watu wasio kulikana na mukaniteka”
“Hahaaa hapana kaka yangu. Mimi ni chief staff ikulu”
Josephine alizungumza hukua akichomoa kitambulisho chake kwenye pochi na kumpatia Evans, aliye kisoma kwa sekunde kadhaa.
“Waoo hongera sana. Kumbe nipo na mshauri mkuu wa raisi hapa?”
“Ndio, huyu rafiki yangu ana husika kwenye maswala ya usalama zaidi”
“Una taka kuniambia Magreth ni usalama wa taifa?”
“Hapana, kwa maana hana kitambulisho hicho. Ila ana dili sana na mambo ya kiusalama. Endapo huko mbele tukizidi kuwa marafiki uta zidi kumfahamu vizuri”
Macho ya Magreth hayakusita kutazama macho ya Evans na kujikuta akianza kuyafananisha macho hayo na macho ya mpenzi wake Evans.
“Magreth”
Evans aliita.
“Beee”
“Huyo mpenzi wako, ilikuwaje ukaachna naye?”
“Ni story ndefu sana, ila nikiwa vizuri siku nita kusimulia mambo yote yalivyo kuwa”
“Mmmm sawa, hakuna shaka. Kutokana mimi nina kaa hoteli kwa sasa kwa maana nime kuja hapa Dar kwa mambo ya kibiashara, nita tafuta siku ya kukaa na wewe, tuzungumze mambo mengi sana”
Simu ya Evans ikaanza kuita, akaitazama kwa sekunde kadhaa na kukuta ni Leila.
“Samahani jamani”
Evans alizungumza huku akisogeza kiti nyuma na kusimama, akatoka nje ya mgahawa huo na kuipokea simu hiyo.
“Mage aisee ume jikaza kwa kweli”
“Yaani wee acha, sijui hata ujasiri niliutolea wapi”
“Una jua hadi nilihisi tumbo lilikuwa lina niuma, ulipo kuwa una zungumza yale maneno”
“Kupenda kubaya rafiki yangu, yaani huyu kaka amenichanganya kwa kweli. Alafu nime gundua jambo moja kwake”
“Jambo gani?”
“George ana macho kama ya Evans. Yaani hayana utofauti kabisa, kilicho na utofauti ni sura zao”
“Ndio ujitahidi kutulia naya rafiki yangu. Si una jua wanaume jinsi walivyo, huyu ukimletea itikadi za kina nabii Sanga ita kula kwako”
“Yaani we acha akinikubalia, haki ya Mungu nina mbebea ujauzito”
“Ohoo!!”
“Haki ya Mungu vile, lazima nimbebee ujauzito”
“Kazi kweli kweli”
Josephine alizungumza huku akimtazama Evans aliye simama nje akiendelea kuzungumza na simu hiyo.
“Hakikisha una kuwa makini”
“Usijali mume wangu, jioni si tuna weza kuonana kwa maana nikirudi kutoka kwa rafiki yangu, nita kuandalia chakula kizuri sana”
“Usijali, tuta wasiliana”
“Nashukuru kwa wito wako. Nina kupenda pia?”
“Nami pia nina kupenda”
“Haya lunch njema”
“Asante”
Evans akakata simu na kuirudisha mfukoni mwake. Akarudi ndani na kukaa kwenye kiti chake.
“Jamani munaonaje tukaagiza chakula”
“Ni kweli”
Josephine aliunga mkono. Evans akamuita muhudumu na wakaagiza chakula kisha wakaanza kula taratibu, huku kwa mara kadhaa Evans na Magreth wanayagonganisha macho yao na kujikuta wakitabasamu. Kumbukumbu za Evans zikaanza kurudi nyuma kama mkanda wa video. Akakumbuka kichochoro alicho mkuta Magreth akiwa ana sumbuliwa na vibaka huku akiwa ameshika deli lililo jaa maandazi mkononi mwake. Akakumbuka jinsi alivyo anza kupambana na wahuni hao, hadi ikapeleka kuchomwa kisu.
Akakumbuka kipindi walipo kuwa wakishirikiana kuuza mgahawa na Magreth huku akiamini kwamba ndio mpenzi wa maisha yake yote, ila mambo yakabadilika mara baada ya kumjua nabii Sanga kwa upande wa pili ambao ndio wa chui, kwani laiti inge kuwa sio Magreth basi ile siku waliyo kutwa kitandani basi risasi ambayo inge toka kwenye bastola ya nabii Sanga inge kuwa halali yake.
***
Leila moja kwa moja akaelekea kwa rafiki yake Caro, mara baada ya kupewa ruhusa ya kwenda huko na Evans. Umbea ambao rafiki yake Caro alimueleza kwamba ana hitaji kumuambia akifika tu nyumbani kwake, hakika ume mfanya ajitahidi kuwahi nyumbani hapo. Akaribishwa vizuri na Caro na wakakaa sebleni
“Ehee rafiki yangu, mbona ume rudi haraka haraka”
“Yaani wee acha tu shosti yangu. Katika safari zangu zote nilizo wahi kutoka nje ya nchi hii safari ya wakati huu ilikuwa na mikosi pia ikawa na baraka kubwa”
“Ehee nipe mchapo shosti yangu. Ila ngoja kwanza, shemeji yupo?”
“Mmmm shemeji yako ame toka, amekwenda kutazama zake mpira. Ana sema sijui Manchester inacheza huko, hivyo ame toka juu juu”
“Hapo sawa kwa maana nisije nika teleza hapa mambo yakawa sio mambo bure”
“Yaa ni kweli. Acha sasa niendelee”
“Ehee niambie”
Leila alizungumza huku akikunja nne kabisa, ili kusika umbea huo.
“Bwana si tuliondoka hapa Tanzania kwa ndege ya Fly Emirates?”
“Ndio nakumbuka siku ile ulipo toka kukata tiketi ulipita pale kazini kwangu”
“Ewalaa. Ebwana, safari ilipo anza si ndege ikapata ajali”
“Weeee!!?”
Leila alishangaa sana.
“Ndio, ila cha kumshukuru Mungu iliangukia ziwani na watu wote tuka toka salama”
“Ehee ikawaje sasa?”
“Tukasafirishwa na ndege za kijeshi hadi katika kiwanja cha Congo kusubiria hali ya hewa ikae vizuri. Sasa tukiwa pale uwanjani, si nikakutana na nabii Sanga”
Leila akastuka kidogo ila akazuia mstuko wake.
“Ehee?”
“Bwana nikaanza kuzungumza naye. Nashukuru Mungu hakuwa na mke wake wale walinzi wake. Tukaanza kuzoeana na tukaenda Nigeria pamoja. Yaani nika sema hii ndio nafasi simuachii yule mzee kwa maana ana pesa ya kufa mtu”
“Kama kawaida yako?”
“Yaani, sikujali ni mtumishi wa Mungu au nani, yaani nilicho kifanya ni kumtega hadi akaingia laini. Mtoto nilimpa mauno yule mzee, yaani nikaenda mbali hadi nikampa ***”
“Weee acha utani?”
“Haki ya Mungu vile. Mzee kamla bata wangu”
“Hakuanza kukuombea kama una mapepo?”
“Nyoo aanzie wapi kwa mfano. Ila mzee kumbe naye yupo vizuri bwana, damu bado ina mchemka, yaani alinila bata hadi nikaanza kuomba poo mimi. Ila shosti yangu ni siri haya ninayo kuambia”
“Wala usijali, mimi na wewe damu damu, siri yako siri yangu, yangu ya kwako”
“Ni hapo tu ninapo kupendea shosti yangu. Yaani mzee alinipa dola elfu hamsini, sawa na milioni mia na usheee”
“Wacha wee”
“Yaani nikanunua bidhaa zangu baada ya hapo nikarudi naye, ndege kanilipia. Hapa nilipo yaani nasubiria simu yake. Yaani akiniita mafichoni basi nita hakikisha nina kwenda kumpa show za kizaramo hadi yeye mwenyewe aninunulie nyumba au kunijengea”
“Ila kuwa makini, si una jua ana mke na mtoto wake yule aliye olewa na mtoto wa raisi?”
“Nalijua hilo shosti yangu”
“Basi usije uka jikuta una tekwa na watu wasio julikana. Ita kula kwako”
“Usijali rafiki yangu, nipo makoni tena sana. Ila mchele ndio huo shosti yangu. Yaani nilijitahidi kuubania moyoni mwangu, ila nimeshindwa kabisa nime ona nikuambie ndugu yangu”
‘Laiti unge jua ninacho muwazia huyo nabii Sanga wala usinge zungumza hivyo Caro rafiki yangu’
Leila alizungumza kimoyo moyo huku akimtazama Caro aliye jawa na furaha kubwa sana.
“Pia kuwa makini shemeji asijue?”
“Hawezi kujua, si unajua hapa mimi ndio mume, yaani huyu nikimpa pesa tu hata kama ana hasira basi zina mnyeyu…….”
Caro akajikuta akikatisha sentensi yake huku akitazama namba ngeni iliyo ingia kwenye simu yake. Akaipokea na kuiweka simu sikioni mwake.
“Ni mimi upo wapi?”
Sauti ya nabii Sanga ilisikika na kumfanya Caro kujawa na tabasamu pana sana usoni mwake kiasi cha kumfanya Leila kumshangaa kwa maana hatambui ni kwa nini simu huyo aliyo pigiwa ime mfurahisha kiasi hicho.
****************************************************************************************************************
****
ITAENDELEA
Haya sasa, Caro ame toa siri ambayo nabii Sanga alimuambia asiweze kumueleza mtu yoyote na huyo aliye mueleza ni miongoni mwa watu walio pewa kazi na Evans ya kujua nyendo za nabii Sanga, je ita kuwaje? Usikose sehemu ya 197.