SIN 36
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
“Ndio nina kupenda mpenzi wangu ndio maana nilikuwa tayari kuyatoa maisha yangu ili kukuokoa wewe uwe salama”
Kauli hiyo ya Evans ika uchoma sana moyo wa Magreth.
“Nina jambo lina niumiza sana moyoni mwangu natamani kukueleza ukweli, ila nina jikuta nina shindwa”
“Kuwa huru Magreth mimi nipo tayari kusikia ukweli na siku zote nina mpenda mtu mkweli na muwazi kwenye maisha yangu”
Magreth akajikuta akianza kulengwa lengwa na machozi kwani endapo ata mueleza Evans kwamba mali zote hizi na kila kitu walicho kivaa kimetokana na yeye kutoa penzi kwa nabii Sanga hakika itakuwa ni pigo kubwa sana kwa Evans ambaye alimdanganya kwamba mali hizo zime tokana na urithi wa pesa za marehemu baba yake.
ENDELEA
Magreth taratibu akashusha miguu yake mezani na kumgeukia Evans aliye jawa na hamu ya kuhitaji kufahamu ni kitu gani ambacho Magreth ana hitaji kumueleza.
“Yale yote niliyo kueleza juu ya hizi mali na pesa ninazo zimiliki ni uongo”
Magreth alizungumza kwa sauti ya upole sana huku akimtazama Evans usoni mwake.
“Ni uongo kivipi?”
“Sikurithi mali kutoka kwa baba yangu. Kwani baba yangu alikufa masikini mimi nikiwa na umri wa miaka nane”
“S…a….a….aaa hizi pesa zote ume tolea wapi?”
Evans alishikwa na kigugumizi huku mapigo ya moyo yakianza kumdunda taratibu. Macho yakamtoka huku akimtazama Magreth anaye mwagikwa na machozi.
“Niliuza kitu muhimu sana kwenye maisha yangu”
“Kitu gani Magreth”
Evans alizungumza hukua akijifuta jasho linalo mwagika kwa kitambaa.
“Evans niliyafanya yote haya ili kufika hapa nilipo”
“Sawa Magreth uliuza nini, tafadhali niambie”
“Niliuza usichana wangu kwa mwanaume ambaye sikuweza kumpanda. Mwanaume huyo ndio aliye nipatia pesa hizi zote na bado ana nipenda na kwa sasa yupo nje ya nchi ila ata rudi siku si nyingi. Ni mtu aliye ahidi endapo kwamba nita kuwa na mahusiano na mwanaume mwengine basi ata muua mwanaume huyo. Ile simu iliyo pigwa muda ule na nikaenda kuipokea pembeni ni yeye na ameniambia kwamba wiki ijayo ana rudi. Evans nina ogopa sana haya maisha, nina ogopa kukuingiza kwenye matatizo makubwa kwa maana mwanaume huyo nina mfahamu na hashindwi kukufanyia jambo baya. Naogopa Evans”
Magreth alizungumza hukua akilia kwa uchungu mkubwa sana. Evans mwili mzima ukazidi kumtetemeka. Woga ulio changanyikana na hasira ukazidi kuuvaa moyo wake.
“Kwa kuyatoa maisha yangu kwa ajili yako. Haya ndio malipo yake si ndio Magreth?”
Evans alizungumza huku akiendelea kutetemeka kwa woga.
“Hapana Evans sikuhitaji haya mambo yawe hivi. Mimi nina kupenda wewe”
“Acha unafki Magreth.”
Evans alizungumza kwa ukali sana huku akinyanyuka kwenye sofa hilo.
“Wewe una nileta humu ili niuwawe si ndio?”
“Evans naomba uni elewe, mwanaume huyo sikujua kama ana weza kufanya haya aliyo ya fanya. Namuogopa Evans, amenitoa mavumbini na amenifanya niheshimike na kujulikana”
“Niachie unafki, kukutoa mavumbini kwako kwa hiyo una taka na mimi anirudishe mavumbini nikiwa mfu si ndio? Nashukuru kwa juhudi zako zote ulizo weza kunionyesha nilipo kuwa nimelela pale hospitalini. Sikuja na kiti kwenye hii nyumba ya mumeo. Acha nikatafute maisha yangu, nina mama yangu ana nitegemea kijijini nahisi ata shangaa na kuumia kuona mwanaye nitakufa eti kisa nimekutwa na mke wa mtu”
Evans alizungumza kwa hasira sana na kumfanya Magreth kujawa na hofu kubwa sana. Kwenye kipindi chote hicho hakuwahi kumuona Evans akiwa katika hali ya hasira kama hivyo.
“Eva…..”
“Kaa kimya mwanamke, ni heri ungenieleza ukweli toka nilipo kuwa hospitalini ninge jua ni jinsi gani nina pambana na hali yangu. Kuliko umesubiri nikuuingize moyoni mwangu alafu unakuja kunieleza ukweli. Hahaa…..hapa sio kwangu sijanunua hata hili kapeti nililo kaganya hapa, je nitaendelea kujiita mume wa mtu au mariooo? Siwezi kuishi maisha ya namna hiyo. Kwaheri, funguo za gari lako hizi hapa, simu uliyo ni nunulia hii hapa, pia ukihitaji nguo hizi ulizo ninunulia na viatu nita vua pia”
Evans aliendelea kuzungumza kwa hasira huku akimrushia Magreth funguo ya gari pamoja na simu. Magreth kwa haraka akasimama na kumfwata Evans anaye elekea mlangoni.
“Evans mimi nina kupenda wewe. Wewe ndio mume wangu, mwanaume wa maisha yangu”
“FUNGAAAAAAAAAA BAKULIIII LAKOOOO MAGEEEEEEEE. Usitake nikuueee kama nilivyo muua mzeee SHIKAAAAA………………..!!!”
Evans alizungumza huku macho yakiwa yamejaa uwekundu hadi Magreth akasitisha hatua za kumfwata. Maneno ya kumuua mzee Shika yakaanza kumrudia rudia Magreth kichwani mwake na kuzidi kumuogopesha.
“Kama niliweza kumuua baba yangu. Nawewe ninaweza kukuua hivyo achana na mimi kenge wewe.”
Evans mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo, akafungua mlango na kuubamiza kwa nguvu. Akatoka nje na kufungua geti dogo, akalibamiza na kutokomea gizani. Magreth akahisi nguvu zikimuishia miguuni mwake na taratibu akajikuta akikaa chini huku akilia kwa uchungu sana. Magreth akajikaza na kutoka nje ya geti la nyumba yake, akajaribu kuangaza kila sehemu kama ana weza kumuona Evans ila hakubahatika kumuona kabisa na kutokana ni usiku hakuweza kwenda mbali na nyumbani kwake, hii ni kutokana na woga. Akarudi sebleni huku akiwa na matumaini kwamba hasira za Evans zikiisha ata rudi.
***
Kundi kubwa la vijana nane wenye mapanga na marungu, wakavamia katika duka kubwa la jumla la mzee Hindu. Wakafanikiwa kumuweka mlinzi chini ya ulinzi mkali huku wakimfunga kamba na kupatia kipigo kizito almanusura waichomoe roho yake. Wakiwa katika harakati za kuvunja geti kubwa la duka hilo, gari mbili za polisi zilizopo kwenye doria, zikatiza eneo hilo na kusababisha vijana hao kuanza kutawanyika huku kila mmoja akipita njia yake. Polisi wenye silaha pamona na mbwa wakali wakaruka kwenye magari hayo hata kabla hayajasimama na wakaanza kuwafukuzia vijana hao ambao mpango wao ume vurugika. Evans akiwa na hasira zake akaona watu wawili wakija nyuma yake huku wakiwa spidi sana. Kutokana ni usiku na eneo alilipo lina tisha kidogo, akaona usalama wake ni kuanza kutimua mbio.
Vijana hao waka mpita kwa maana wana mazoezi mazuri tu ya kukimbia mithili ya mwana riadha maarufu duniani Hussein Bolt. Polisi ambao nao wapo kwenye spidi, wakaanza kukaribia Evans ambaye naye ana anakimbia kuelekea wanapo kwenda vijana hao. Askari mrefu na anaye kimbia kuwapita wezake, akafanikiwa kumfikia Evas na njia pekee ambayo aliona ita msaidia kumzuia Evans ni kumtandika teke kwa nyuma na teke hilo likafanikiwa kuifikia miguu ya Evans na uifanya igongane na kuanguka vibaya sana.
“Mfungeni pingu huyo”
Askari huyo aliwaambia wezake watatu walipo nyuma yake huku yeye akizidi kukimbizana na vijana hao wawili. Askari wawili, wakamvamia Evans anaye jitahidi kua kunyanyuka chini hapo, wakamlaza kifudi fudi na kuirudisha mikono yake kwa nyuma na kumfunga pingu.
“Jamani mimi kosa langu ni nini?”
Evans alilalama, ila askajibiwa kwa kutandikwa teke la mbavu na kumfanya agugumie kwa kutoa maumivu makali sana. Wakamnyanyua, huku wakimzaba ngumi na makofi mfululizo. Wakafika eneo walipo simamisha defender zoa mbili na kukuta vijana wengine sita wakiwa wame kamatwa tayari na wapo chini ya ulinzi mkali sana.
“Panda panda”
Evans akasukumiwa kwenye gari hilo na kuchanganywa na waizi hao.
“Jamani mimi sijui ni nini kinacho endelea. Muna nionea tu”
Evans alilalama hukua kilia kwa uchungu sana. Hapakuwa na askari aliye weza kumsikiliza wala kujali kilio chake. Askari huyo mrefu na mwenye nguvu akarudi eneo hilo huku akiwa amewaswega vijana hao wawili suruali zao maeneo ya makalioni. Akawasukumia kwa wezake ambao wakaanza kuwashambulia kwa mateka na makofi huku wakiwapandisha kwenye gari hizo.
“Wajinga sana hawa watoto. Badala ya kufanya kazi kwa juhudi wame kuwa mijizi”
Askari huyo alizunguma huku akihema kwani shuhuli aliyo ifanya si ndogo kwa kweli. Askari kadhaa wakabaki katika eneo hilo la tukio huku wengine wakiondoka na kundi hilo la vijana hadi central Polisi. Wakawashusha huku wakiwatandika virungu, huku Evans naye akijikuta akipata dhahama hiyo.
“Panga mstari mmoja”
Askari huyo mrefu alizungumza na hapakuwa na kijana hata mmoja aliye goma kufwata amri hiyo kwani kipigo walicho kipata si kidogo.
“Chuchumaa weweeee. Munataka kuingia kwa kutembea hapa ni kanisani kwani?”
Vijana wote wakachuchumaa. Wakaanza kurukishwa kichura chura huku wakiingizwa katika kituo hicho kikubwa cha polisi. Wakingizwa katika sero ya kwao peke yao wakisubiri utaratibu mwengine.
“Afande mimi sihusikia”
Evans aliendelea kuwaomba askari hao.
“Alafu wewe kaa kimya, si ulikuwa una kimbizana na hawa wezako. Tena ukiendelea kupiga piga kelele tuta kuvunja”
Askari huyo alizungumza kwa ukali na kumfanya Evans kukaa kwa kuogopa kuvunjwa.
“Sasa ole wenu nisikie kelele, tutapiga risasi mmoja baada ya mwengine”
Vitisho hivyo vya askari vikawafanya vijana hao kukaa kimya huku malengo yao na ndoto zao walizo kuwa wana zipanga kuhusiana na kupata mali zilizomo dukani humo, zikiishia katika chumba hicho chenye giza tototo.
***
Hadi kuna pambazuka, Magreth hakuweza kupaona uwezo wa Evans. Wasiwasi na woga ukazidi kumjaa kwani kuondoka kwa Evans haukuwa kwa amani.
‘Jamani upo wapi Evans wangu’
Magreth alilala na ana shindwa kumpigia simu kwa maana simu ya Evans ipo sebleni hapo. Magreth akajifikiria kwa muda kisha akaingia chumbani kwake. Akaoga na kubadilisha nguo zake, akafunga nyumba yake na kuingia kwenye gari lake ambalo kwa sasa ana weza kuliendesha vizuri. Akaaanza safari ya kuelekea ofisini kwake huku akijipa matumaini ya kumkuta Evans ofisini kwake. Foleni kubwa ya barabarani ika mfanya Magreth kutumia zaidi ya masaa mawili kufika ofisini kwake. Akafika ofisini na kuwakuta vijana wake wakifanya usafi wa mgahawa huo mkubwa. Akasalimiana na wafanyakazi wake hao.
“Evans mume muona asubuhi hii?”
“Hapana bosi”
“Hajafika?”
“Ndio, mimi ndio wa kwanza kufika hapa ila sija muona”
“Ohoo Mungu wangu ata kuwa wapi huyu mwanume?”
Magreth aliwaza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana.
“Kwani bosi jana si uliondoka naye?”
“Ndio niliondoka naye ila tulipishana kauli usiku na aliondoka kwa hasira. Sasa ijajua ni wapi ame kwenda.”
“Jaribu kumpigia simu yake?”
“Sim aliacha nyumbani ndio maana nina pata wakati mgumu sana kumtafuta”
“Ila kama aliondoka kwa hasira basi zikiisha ata rudi. Si ana marafiki wengi hapa Dar?”
“Ndio anao ila hajawahi kunitambulisha?”
“Usijali bosi ata rudi”
Magreth alipewa matumaini na mfanyakazi wake huyo wa kike aitwaye Anjelina. Wakaanza kazi ya kuandaa vifungua vinywa kama kawaida kwani mgahawa huo una fanya kazi kuanzia asubuhi hadi usiku. Wateja wakaanza kumiminika hadi wakajikuta wengine wakikosa nafasi za kukaa. Wingi wa wateja uka mfanya Magreth kuwa bize sana na hata wazo la kumfikiria Evans akaliweka kando.
Mapishi ya Magreth yakazidi kuwapagawisha wateja wengi ambao kila mmoja alijikuta akimwaga sifa kedekede kwa Magreth.
“Mimi nina kula chakula kwenye migahawa mingi hapa Kinondoni na Dar kwa ujumla ila chakula chako kipo very amaizing”
Mwana dada huyo ambaye ni mteja alimsifia Magreth hukua akihesabu noti za shilingi elfu kumi kumi sita na kumkabidhi Magreth, kwani chakula na vinywaji walivyo kula na wezake vime fika kiasi hicho cha pesa.
“Nashukuru sana”
“Yaani nina kuambia uta kuwa top in dar. Mungu akikubariki huko mbeleni, fungua hata hoteli au ongeza ukubwa wa eneo hili”
“Nitalifanyia kazi wazo lako”
“Hivi muna pika vyakula kwenye maharusi?”
“Mmmm kutokana ndio kwanza tuna anza bado hatujaanza kupika, ila tukipata oda ya uhakika basi tuta pika”
“Sasa chukua namba yangu nawe nipe yako. Mwezi ujao, mdogo wangu wa mwisho ana funga ndoa. Nitapenda chakula tutakacho kula ukumbini kifikie hapa”
“Karibuni sana”
“Nashukuru, tena tuta kulipa vizuri sana. Yaani ume nikamata Mage”
“Nashukuru sana, una itwa dada nani?”
“Vivian”
“Sawa nita kusave kwa jina hilo”
“Sawa, leo usiku nitakuja na familia yangu yote hapa, tuje kupata chakula cha usiku na baada ya hapo nita washawishi juu ya kukupa tenda ya kutupikia kwenye harudi ya dogo”
“Karibuni sana na nina imani kwamba hamto jutia kwa nini mulinipa nafasi”
“Sawa acha nirudi ofisini kwangu”
“Karibu sana”
Magreth akazidi kujawa na furaha na usongo wa kufanya vizuri kwenye mapishi yake. Kwajinsi watu wanavyo zidi kuingia na kutoka kwenye mgahawa wa Magreth ukaanza kuwafanya wamiliki wengine wa migahawa na mahoteli ya karibu naye kuingiwa na kinyongo cha chuki, kwani wateja wao walio kuwa wana wategemea wote wame hamia kwa Magreth.
***
Habari ya kuvunjwa na kuibwa kiwango kikubwa cha pesa katika benki ya Standar Chartered iliyopo Sandton South Afrika ikaanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ndani ya nchi hiyo na nje ya nchi hiyo.Vituo vikubwa vya habari duniani kama CNN, BBC na Al Jazirah zikaitangaza habari hiyo huku wakidai majambazi walio fanya kazi hiyo ni watu wenye uwezo mkubwa sana wa akili na wameweza kuisoma ramani ya benki hiyo kwa kipindi kirefu sana. Wapelelezi kutoka katika vitengo mbalimbali katika nchi ya Afrika kusini, wakaanza kushirikiana kwa pmoja ili kuhakikisha kwamba wana pata japo hata alama za vidole vya waizi hao ili mradi waweze kumtambua japo mmoja wao amabaye ana weza kusababisha wengine kuweza kupatikana.
Kazi ya upelelezi wao haikuweza kuzaa matunda ya aina yoyote kwani hakuna hata alama ya kidole iliyo weza kuachwa.
‘Bado tuna endelea na upelelezi na tuna wahakikishia watu kwamba ni lazima tuta watia nguvuni majambazi hao’
Ngosha akazima tv kubwa iliyopo sebleni hapo huku akiangua kicheko cha dharau hadi Tomas akabaki akiwa ana mshangaa.
“Mbona una cheka”
“Namcheka huyu kamishina wa polisi.”
“Kwa nini una mcheka?”
“Hii si mara yake ya kwanza kuzungumza jambo hilo. Unajua katika kipindi chote ambacho vijana wangu wana kuwa wana fanya matukio ya wizi wa mabeki, huwa hakuna mpelelezi hata mmoja anaye weza kupata ushahidi wa aina yoyote na huwa wana ishia kusema kwamba watatutia nguvuni ila hakuna kitu”
“Ni kwa nini wanashindwa kupata ushahidi wowote?”
“Ndio maana kuna ile kambi ya siri kule. Nina imani Scooby doo alikufundisha vizuri. Umakini na kiwango ambacho tuna kitazama kwa wana timu yanagu ni umakini. Tazama mume kwenda, mume iba na hakuna uzembe ulio fanyika. Huo ndio umakini ninao uzungumzia”
“Sawa sawa hapo nime kuelewa”
“Ehee lini una kwenda kumuona mwanao. Sasa hivi una una takiwa kutengeneza mazingira kwa mwanao”
“Ni kweli kaka inabidi leo niende kwa yule mwanamke”
“Una uhakika kwamba yule jamaa yake huto weza kumkuta?”
“Sijajua, ila kutokana simpendi sina haja ya kuwa na wivu naye. Ile sherehe uliyo zungumza ita fanyika saa ngapi?”
“Leo hii, boti tayari ipo tayari na ndani ya boti tuta kuwa na wanawake mia moja walivalia bikini tu na sidiria”
“Weeee!!”
Tomas alishangaa huku akihisi udenda una mtoka.
“Ndio hiyo kaka hiyo ina itwa SEX PARTY, yaani wewe una jikamatia umtakaye, una kula mzigo, una chukua mwengine una kula mzigo. Yaani kwa wewe ambaye una ugwadu wa kukaa porini nina imani wata kukoma”
“Yaani kaka nina tamani hiyo sherehe ianze hata sasa hivi”
“Je kwenda kuiona familia yako?”
“Siku nyingine tuta kwenda ila nataka kwenda kushuhudia kwa macho yangu hiyo Patry na nitakacho wafanya hao wasichana hakika wata simuliana”
Tomas alizungumza kwa msisitizo huku shetani wa ngono akiwa tayari amesha mtawala ufahamu wake wa akili na mwili mzima.
ITAENDELEA
Haya sasa Tomas ana ingia kwenye ulimwengu wa starehe. Evans amekamatwa na polisi akidhaniwa ni muhalifu je atafanikiwa kutoka? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 37.