SIN 47
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
“Ndio yapo hapa”
“Je tuna weza kuyasikia?”
“Muna hakika muna hitaji kuyasikia?”
“Ndio”
Levina akawatazama Julieth na mama yake, kutokana wame amaua kusikia mazungumzo yaliyo pita katika simu ya Magreth akaminya batani katika laptop yake na mazungumzo kati ya Magreth na nabii Sanga yakaanza kupenya taratibu masikioni mwao na kumfanya Julieth kushangaa sana huku mama yake akiwa ame fura kwa hasira kali sana ya kuibiwa mume wake na Magreth.
ENDELEA
“Wa…a…me…sema wana kwenda Bagamoyo?”
Mrs Sanga alizungumza huku akibabaika sana. Hakuweza hata kukaa kwenye kiti hicho, akanyanyuka na kuanza kuzunguka zunguka ndani ya chumba hicho huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi.
“Mama tulia basi, kufanya hivyo maana yake nini?”
Julieth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama mama yake usoni. Levina akatabasamu huku akimtazama mwana mama huyo kwani sasa ana zidi kumchanganya mwanamke huyo.
“Binti hembu jaribu kuitafuta namba ya mume wangu nataka kujua kwa sasa yupo wapi?”
“Hiyo ni kazi nyingine mama. Je uta nilipa?”
“Pesa sio shida. Wewe fanya kama nilivyo kueleza”
Levina akaitafuta namba ya nabii Sanga, haikuchukua muda sana akafanikiwa kufahamu ni sehemu gani nabii Sanga yupo.
“Mume wako yupo Bagamoyo kwa sasa”
“Na huyo malaya si yupo huko huko Bagamoyo?”
“Wapo eneo moja”
“Niamabie ni eneo gani wapo nahitaji kwenda sasa hivi”
Mrs Sanga alizungumza huku jasho likimwagika usoni mwake. Levina akachukua kikaratasi kidogo na kuandika jina la eneo walipo nabii Sanga na Magreth, pamoja na hoteli, kisha akamkabishi mrs Sanga kikaratasi hicho.
“Malipo yangu”
“Ni kiasi gani?”
“Hi kazi ya sasa niliyo kufanyia ni milioni mbili”
Mrs Sanga akahamisha kiasi cha milioni saba kwenye akauti ya Levina kisha akwaondoka eneo hilo huku mrs Sanga akitamani hata apae angani ili kufika eneo la Bagamoyo.
“Naomba funguo zako”
“Mama siwezi kukufa funguo ya gari ukaendesha. Acha niendeshe mimi mwenyewe”
“Usiniletee ujinga. Nipe funguo ya gari”
Mrs Sanga alimfokea sana Julieth ambaye hakuwa na jinsi zaidi ya kutii amri hiyo ya mama yake. Akamkabidhi funguo ya gari lake kisha wakaingia. Mrs Sanga akalirudisha nyuma gari hilo kwa kasi kisha akaliweka sawa. Safari ya kueleke Bagamoyo ikaanza huku akiwa katika mwendo wa kasi sana.
“Mama taa inashawaka ya orange punguza mwendo”
Julieth alimuambia mama yake, huku akizitazama taa za barabarani eneo hilo la Mwange. Hadi anakaribia kufika eneo la makutano ya taa hizo, tayari taa nyekundu ilisha waka kwa ishara ya kuwaashiria kwamba wasimame, na taa za upande wa kulia zikaruhusiwa. Mrs Sanga hakujali kuwashwa kwa taa hizo nyekundu na kujikuta akijitahidi kukatiza, ila gafla bodaboda aliye mpakiza abiria, tayari walishajaa mbele ya gari lao na kujikuta akiwabamiza kwa nguvu huku akifunga breki za gari hilo na kuzifanya tairi za gari hilo kuserereka kwa muda kisha gari likasimama huku mrs Sanga akiwa amejawa na hofu kubwa sana na tayari waendesha pikipiki wa eneo hilo pamoja na watu wengine wameanza kulisogelea gari hilo huku wakionekana kujawa na hasira kali sana.
***
Mara baada ya kupata kifungua kinywa, Evans akajiandaa kwa safari ya kwenda kuonana na mmoja wa wanachuo alio maliza nao kusoma. Evans akaichu simu yake inayo ita, akaipokea na kuiweka sikioni mwake.
“Niambie kaka”
“Vipi bado hujatoka?”
“Nipo njiani ndugu yangu ninakuomba unisubirie”
“Wahi ndugu yangu si unajua kwamba kuna ratiba nina hitaji kuiwahi mida ya saa sita hivi”
“Poa poa kaka”
Evans akakata simu na kumaliza kujianda, akachukua kiasi cha pesa na kuweka katika katika wallet yake. Kutokana Magreth ameondoka na gari lake, ikamlazimu Evans kukodisha pikipiki.
“Hadi Masaki ita garimu kiasi gani?”
“Hapo itakuwa ni elfu arobaini”
“Sawa nina omba helment”
“Lipo hili hili moja kaka”
“Sawa nina liomba nivae mimi. Ila si munapaswa madereva bodaboda si munatakiwa kuwa na helment mbili?”
“Ndio kaka ila vaa hili, tukifika hapo mbele nitawaomba jamaa maskani”
Muendesha pikipiki huyo akamkabidhi Evans kofia hiyo ngumu ya kujilinda kichwa pale kinapo pata tatizo kama ajali. Safari ikaanza kuelekea masaki, ila walipo kuwa njiani Evans akamuomba dereva huyo wapitie Mlimani City kuna jambo ambalo ana hitaji kulinunua.
Wakafanikiwa kufika Mlimani City na Evans akaingia ndani ya jengo hilo lenye maduka mengi. Akafika katika duka linalo uza bidhaa za kampuni ya apple. Akaulizia bei ya moja ya laptop.
“Basi nitakuja kuichukua by saa saba”
“Sawa kaka karibu sana”
Evans akatoka dukani hapo na kurudi alipo muacha muendesha pikikipi.
“Kaka kiasi kitaongezeka kidogo”
“Sawa hakuna shaka”
Wakaondoka eneo hilo, wakafika Mwenge na kusimama kwani taa za upande wao zimewazuia. Baada ya dakika moja taa za upande huo zikawaka. Dereva wa pikipiki akatia gia na kuondoka, kitendo cha kufika katikati ya eneo hili la makutano ya mataa hayo, gari moja ikawagonga, Evans akarushwa pembeni na kuanza kubingirika kwenye lami hiyo huku muendesha pikipiki akirushwa na pikipiki yake huku akivunjika vujika kwani yeye ndio amebamizwa vibaya sana na pikipiki hiyo. Evans akasimama huku akishangaa jinsi watu wanavyo zidi kujaa katika eneo hilo. Akatazama jinsi watu wanavyo mfwata muendesha pikipiku aliye laliwa na pikipiki yake huku hali yake ikizidi kuwa mbaya.
“Upo salama wewe?”
Jamaa mmoja alimuuliza Evans ambaye bado hajielewi. Kila anacho kiona katika eneo hilo ana ona kama ni filamu fulani.
“Mkalishe chini huyo hapo sio yeye”
Jamaa mmoja alizungumza, wakamshika Evans mkono na kumtoa katikati ya barabara hiyo na kumkalisha pembeni huku wakijaribu kumtazama kama ana majera ya aina yoyote.
“Oya una nijisiaje?”
“Nipo poa”
“Kweli?”
“Ndio nipo sawa”
Evans akatoa simu yake mfukoni na kuitazama, akakuta kioo kikiwa kimepasuka kwa kuvunjika vunjika vibaya. Raia wenye hasira kali wakaendelea kuwalazimisha watu walio wagonga Evans na muendesha pikipiki huyo kushuka ndani ya gari huku wengine wakitishia kuvunja vioo vya gari hilo. Askari wa jeshi la kutuliza ghasia ambao walikuwa katika eneo la sheli katika makutano hayo, wakafika eneo la tukio na kuanza kuzungujmza na wananchi hao wenye hasira. Ila wananchi hao wakaonekana kuto kukubaliana na mazungumzo hayo ya askari. Askari mmoja akakoki bunduki yake aina ya SMG na kupiga risasi mbili hewani na wananchi hao wakaanza kutawanyika huku kila moja akiogopa milio hiyo. Askari hao wapatao nane, wakalizunguka gari hilo na askari mmoja akamuamrisha mwana mama anye endesha gari hilo kufungua.
Mrs Sanga wala hakuwa na nguvu ya kufungua mlango wa gari hilo. Julieth muda wote huo wameshikwa na bumbuwazi kiasi kwamba haelewi kinacho endelea.
“Mama fungua mlango”
Askari huyo alizungumza huku akipiga piga kioo cha gari hilo. Mrs Sanga akamtazama askari huyo, akashusha pumzi, kisha akaminya batani na kufungua lock za mlango huo.
“Mama shuka”
Askari huyo alizungumza kwa ukali sana. Mrs Sanga machozi yakaendelea kumwagika usoni mwake pasipo kuzungumza kitu chochote. Askari huyo akafungua mkanda wa siti wa mrs Sanga na kumshusha ndani ya gari hilo.
“Mpelekeni kule”
“Askari mmoja alizungumza huku akiwa amemshika kisawa sawa mrs Sanga. Baadhi ya watu walipo katika eneo hilo waliweza kumfahamu mrs Sanga. Mrs Sanga akapakizwa kwenye gari hilo la askari, huku askari mwengine akiingia kwenye gari la Mrs Sanga, wakampakiza Evans, huku dereva pikipiki akipakizwa kwenye gari jengine la msamaria mwema kuwahiswa hospitali. Askari huyo akafika hospitali ya Lugalo.
“Jamani hapa ni wapi?”
Julieth alistuka kutoka katika hali ya kuduwaa.
“Lugalo hapa”
Askari huyo alimjibu Julieth ambaye bado ana endelea kushangaa shangaa.
“Oya dogo shuka. Wewe demu, hii gari ipo chini ya ulinzi, kama ina wezekana shuka hapa nina ipeleka kituoni central”
“Kwani kuna nini kimetokea na mama yangu yupo wapi?”
“Kwani hukumuona mama yako ame gonga watu. Huyo jamaa ni mmoja wa watu walio gongwa. Oya dogo shuka kabisa”
Evans akafungua mlango wa gari hilo na kushuka. Wakaongozana na askari huyo hadi mapokezi, wakafungua jalada la matibabu na akamkabidhi Evans kwa daktari huyo kwa ajili ya matibabu.
“Samahani afande ahaa....mama yangu amepelekwa wapi?”
“Central polisi”
“Naweza kuongozana na wewe?”
“Itakulazimu kukaa na mgonjwa hapa na matibabu yote atakuwa juu yenu. Baada ya hapo njooni central polisi”
“Sawa samahani, ninaomba nichukue vitu vyangu ndani ya gari”
“Fanya haraka”
Julieth akachukua pochi yake pamoja na simu ya mama yake, kisha askari huyo akaingia ndani ya gari na kuondoka eneo hilo. Julieth akaitafuta namba ya baba yake na kumpigia simu.
***
Nabii Sanga, akamsukumia Magreth kitandani huku akiwa amejawa na usongo wa kuhakikisha kwamba ana ikata kiu yake ya mahaba kwa Magreth. Akaanza kuvua shati taratibu huku akimtazama Magreth aliye zidi kunona. Mlio wa simu ukamfanya nabii Sanga kuanchia msunyo mkali sana, kwani toka waingie hotelini hapo amesahau kuizima simu yake. Akaitoa mfukoni na kutaka kuizima, ila alipo ona jina la binti yake akashusha pumzi kidogo na kuipokea simu hiyo.
“Baba kuna matatizo makubwa sana”
Kauali hiyo ya Julieth aliyo itoa pasipo hata salamu, ikamstua sana nabii Sanga.
“Matatizo gani?”
“Yaani hapa ninapo kuambia mama ameshikiliwa na polisi na amepelekwa central polisi.”
“Ameshikiliwa na polisi!! Amefanya kosa gani?”
Kauli hiyo ikamfanya Magreth kukaa kitandani huku akimtazama nabii Sanga ambaye tayari ana onekana kama kuchanganyikiwa.
“Amegonga muendesha pikipiki pamoja na abiria wake”
“Ohoo Mungu wangu. Hao alio wagonga wapo hai au wamekufa?”
“Mmoja nipo naye hapa Lugalo, ila huyu kidogo hali yake inaridhisha. Ila huyo muendesha pikipiki sijamuona kabisa”
“Umesema mama yako amepelekwa kituo gani?”
“Central”
“Nina kuja hapo Lugalo sasa hivi”
“Sawa baba, ila kamtoe mama”
“Sawa, ila acha nije hapo”
Nabii Sanga akakata simu na kuirudisha simu yake mfukoni. Akaanza kufunga vifungo vya shati lake.
“Mume wangu kuna kitu gani kinacho enelea?”
“Mke wangu ame gonga muendesha pikipiki pamoja na abiria wake”
“Ohoo Mungu, sasa ina kuwaje?”
“Tuondoke tu, kwa leo imeshindikana mke wangu. Ule mfuko wa zawadi nilio kupa upo wapi?”
“Nimeuwacha ndani ya gari”
“Twende”
Nabii Sanga na Magreth wakachukua kila walicho ingia nacho. Wakaingia ndani ya gari hilo, nabii Sanga akafungu mfuko huo na kutoa boksi la cheni hizo zenye thamani kubwa sana ya pesa.
“Waooo baby asante sana”
“Usijali mke wangu ni zawadi ndogo tu hiyo. Utaendelea kupata vitu vingi sana ukiwa na mimi”
“Nashukuru sana”
Wakaondoka eneo hilo huku nabi Sanga akianza kutafuta namba ya RPC Karata, akampigia na simu ikapokelewa.
“Naona umenitafuta mara baada ya matatizo yangu kuisha si ndio?”
Kauli ya RPC Karata kidogo ikampa kigugumiza nabii Sanga cha kuzungumza jambo ambalo anahitaji kumueleza kiongozi huyo wa jeshi la polisi kwa mkoa huu wa Dar es Salaam.
“Samahani ndugu yangu. Nina jambo moja ambalo ndio limenifanya nikupigie. Nimesikia mke wangu ameletwa hapo kituoni kwako. Ningependa kujua ni utaratibu gani una fwata?”
“Utaratibu ulipo hapa ni kwamba mke wako atapelekwa moja kwa moja Segerea na katika hili mzee wangu, tafadhali usinihusishe kabisa katika jambi hili kwa maana sinto kusaidia chochote na habari mbaya iliyopo sasa hivi. Yule bodaboda aliye gongwa na mke wako ame fariki dunia hivyo jiandae kifikra mke wako ana shikiliwa pia kwa kosa la mauaji. Nakutakia siku njema”
RPC Karata akakata simu na kumfanya nabii Sanga kuanza kujawa na wasiwasi mwingi sana huku mapigo yake ya moyo yakianza kumuenda kasi sana.
ITAENDELEA
Haya sasa Mrs Sanga ameshikiliwa kwa kosa la mauaji, RPC Karata amekataa kutoa msaada wa kumsaidia mrs Sanga nini kitatokea? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 48.