Riwaya: SIN

Riwaya: SIN

SIN 104


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188



ILIPOISHIA


“Mmmm haya mama”
Levina akafumba macho yake kwa sekunde thelathini kisha akayafumbua na kuwatazama Magreth na Josephine.


“Vipi mbona ume tukazia macho?”
Magreth alizungumza huku akimtazama Levina anaye onekana kukata tamaa. Baada ya sekunde kadhaa Levina akatabasamu kwa furaha.
“Kazi ime kamilika je naweza kuituma sasa”
Kauli hiyo ikawafanya Magreth na Josephine kukurupuka na kushuka kitandani kwa haraka na kumfwata kwenye meza aliyo kaa huku akiwa amesha andaa kidole chake kimoja kuminya batani ya kuiruhusu video hiyo ya ngono ya mrs Sanga na Tomas kuonekana kwenye tv za ukumbi wa send off.





ENDELEA


“No usiitume”
Josephine alizungumza huku macho yakiwa yame mtoka.


“Kwa nini?”
Levina aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.


“Huu sio muda wake. Ukifanya hivyo ni lazima wata jua ni wapi tulipo na kumbuka hao nao wana watu wenye ujuzi kama wako”
Josephine alizungumza kwa msisitizo huku akiwatazama Levina na Magreth.
“Hilo ndio nililo onyeshwa sasa hivi, niaminini katika hilo”
Levina akatoa kidole chake kwenye batani ambayo kama ange iminya, video hiyo inge onekana kwenye tv zote za ukumbi huo.
“Laiti kama unge jua jinsi nilivyo umiza kichwa wala usinge zungumza hivyo”
Levina alizungumza hukua akinyanyuka na kuingia bafuni.


***


“Tuna siku mbili za kujiandaa katika mpango wetu. Jiji la Dar es Salaam kwa sasa lina ulinzi mkali sana, ina tupasa kuwa makini sana”
Omary kiongozi wa kundi hio la watoto la Al-Shabab alizungumza huku akiwatazama wezake.


“Muda wa kujitoa muhanga ni saaa tisaa kamili alasiri. Maeneo ya kujitoa Muhanga yataongezeka, badala ya kuwa matatatu sasa yataongezeka na kuwa saba. Kariakoo, Stendi ya mbezi mwisho, Kimara mwisho kwenye stendi ya mabasi ya mwendo kasi. Stendi kuu ya mabasi Ubungo. Tazara, Central polisi na ndnai ya kanisa litakalo fungisha ibada. Tuna kwenda kufa, ila tuna kufa kwa faida, majina yetu yataandikwa mbinguni na mwneyezi Mungu ata tuandikia haki ya hichi tunacho kwenda kukifanya.”


Meneno ya Omary yakazidi kuongeza munkari kwa wezake ambao siku zote wame kuwa wakifundishwa na kuamini kwamba, unapo jitoa muhanga basi hiyo ina kuwa ni zawadi kubwa sana kwa mwenyezi Mungu.


“Kila mmoja ata kuwa na simu yake ya smart phone, simu hizi ni bomu kubwa ambalo lina weza kulipua eneo kubwa sana. Hakuna amabaye ana weza kufahamu kwamba simu hizi ni mabomu kwa maana hata mtu wa kawaida atakapo zitazama ana weza kupiga na kuongea na mtu mwengine kama kawaida”
“Naimani kila mmoja ana fahamu juu ya matumizi ya simu hizi, code zake ni 6616”
“Ndio”
“Tume kija Tanzani si kwa ajili ya kushangaa uzuri na magorofa yake. Tume kuja kulipiza kisasi kama vile walivyo fanya mauaji kwa ndugu zetu wapendwa. Watakao salia basi kazi yenu ni kuhakikisha kwamba muna shambulia watu kwa kutumia risasi. Tumelewana?”
“Ndio”
“Hapo kesho nita gawa majukumu kuhakikisha kwamba kila mtu ana tambu ni eneo gani ambalo ata fania kazi”
“Sawa sawa”
***


“Hii serikali bwana ina nichekesha?”
Mzee Mbogo alizungumza huku akiwatazama vijana wake wanao endelea kuhakikisha kwamba ulinzi una kuwa imara kwenye nchi nzima.


“Kwa nini mkuu?”
“Hadi sasa hivi kitengo cha NSA, hakijarudi hewani, yaani hapa nchi ulinzi wake ni imara huko mipakani ila ndani hakuna kitu”
“Ndio muheshimiwa, ila sisi si tupo?”
“Ndio tupo ila hakuna ambaye ana weza kuheshimu uwepo wetu”
“Wata heshimu uwepo wetu pale kutapo tokea tukio”
“Sawa ila hatuja ona dalili yoyote ya Al-Shabab?”
“Sidhani kama wana weza kufanya lolote, kama leo hii wame shindwa kufanya chochote kwenye hii send off iliyo jaza maelfu ya watu basi hawato weza kufanya chochote hata kwenye harusi”
“Sawa ila tusijiaminishe sana. Tuna paswa kuwa makini”
“Usijali muheshimiwa, timu yetu ime jipanga vizuri sana”
“Sawa nafurahi kusikia hivyo”
Mzee Mbogo akaondoka chumbani hapo na kuingia katika chumba chake cha kulala. Akawasha tv na kuendelea kuitazama send off ya mtoto wa nabii Sanga.
‘Binti ume mletea kijana wa watu matatizo ambayo hakuyatarajia kabisa’


Mzee Mbogo alizungumza huku akiendelea kumtazama Julieth ambaye amependeza kisawa sawa.


***


Watu wengi ndani ya ukumbi hususani wadada, wana hamu kubwa ya kumuona bwana harusi ambaye ana anza kutafutwa na Julieth. Julieth akiwa ameongozana na kaka zake, wakaanza kuzunguka ndani ya ukumbi huo kumtafuta Jery. Wakafanikuwa kumuona Jery akiwa amekaa kwenye moja ya meza iliyo zungukwa rafiki zake. Taratibu Julieth akamkumbatia Jery na kumpa busu moto moto. Akamvalisha saa iliyo tengenezwa kwa garama kubwa sana. Kila msichana aliye hudhuria ukumbini hapo, alihisi moyo wake kupata mstuko, uzuri wa Jery hakika uliweza kuwapagawisha wengi. Julieth na Jery wakarudi hadi eneo la mbele la ukumbi huo, waandishi wa habari na wapiga picha kila mmoja alihakikisha ana pata picha nzuri ya wawili hao.


Baada ya utambulisho wa pande zote mbili ulio fanywa na Jilieth na Jery, muda wa kupata chakula uka wadia kwa watu wote.
“Shemeji”
“Ndio”
“Dada yetu si una muoa alivyo mzuri?”
“Ndio shemeji”
Jery alijibu huku wakiwa wamekaa kwenye meza yao maalumu wakijipatia chakula.


“Tuna hitaji dada yetu awe mzuri zaidi ya hapa.”
“Musijali shemeji zenu. Nita mlinda, nita muheshimu, nita zidi kumpenda na nita hakikisha dada yenu ana kuwa na furaha kwenye kipindi chote cha maisha yake”
“Sawa yetu ni hayo tu. Isije uka tumia kigezo cha kusema mimi ni mtoto wa raisi hivyo nina uwezo wa kufanya chochote dada yetu, aisee tuta rudi Tanzania kwa ajili yako endapo ata tupatia mashtaka ya aina yoyote”


Kaka mkubwa wa Julieth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama Jery usoni mwake.
“Musijali, ila kwa nini musije kuwekeza Tanzania biashara zenu?”
“Hakuna pesa.Una jua Marekani kulu, kufanya biashara ni rahisi sana kuikuza kuliko Tanzania. Tanzania apa kwanza ukitazama sera za uwekezaji kidogo zime bada. Makodi ni mengi yaani yana katisha tamaa sana kwa wafanya biashara”
“Nita jaribu kuzungumza na baba ili alegeze kidogo kwenye hilo”
“Zungumza naye mambo yakiwa mazuri basi tuta kuja kuwekeza.”
“Nashukuru sana”
“Ila shemeji usisahau tuliyo kuambia. Dada yetu ndio mboni ya familia yetu, yupo peke yake na hatuna dada mwengine”
“Nime waelewa mashemeji zangu”
Wakamaliza kupata chakula hicho na wakarudi kujwaani. Sherehe ikaendeshwa hadi majira ya saa tano na nusu usiku ika malizika. Ulinzi uka zidi kuimarishwa, baada ya bibi harusi mtarajiwa kutoka ukumbini, uka wadia muda wa wazazi kutoka.


“Hakika nime ipenda sana sherehe ime kuwa nzuri na ime pendeza”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa furaha huku akipeana mkono na nabii Sanga.


“Nashukuru sana ndugu yangu”
“Nina imani muta tutunzia bibi harusi hadi siku yake ya ndoa”
“Ndio ndugu yangu”
“Basi acha sisi tuwahi ikulu. Muda ume kwenda”
“Tuna shukuru kwa kujitoa kwako muheshimiwa”
“Wala usijali muheshimiwa”
Raisi Mtenzi na mke wake, wakapeana mikono na nabii Sanga pamoja na mkewe, kisha wakaondoka eneo hilo. Nabii Sanga akaingia kwenye gari walilo panda wana familia yake.


“Baba hongera sana, sherehe ilikuwa bombastiki”
“Nashukuru sana wanangu, ehee nanyinyi lini kwa maana kama ni mdogo wenu ndio amesha anza hivyo?”
“Hata mimi nil wauliza ila naona hawajanipatia jibu la kueleweka”
“Baba tuta oa tu?”
“Llini kwa maana umri una kwenda. Wewe una miaka thelathini na mbili, mwenzio miaka ishirini na nane. Lini muna oa?”
Nabii Sanga alizidi kusisitizoia huku wakisubiria msafara wa raisi kondoka ukumbini hapo. Baada ya masafara kuondoka na waoa wakaanza kuondoka huku nao msafara wao ukisindikizwa na gari za askari, kuhakikisha bi harusi na familia nzima wana kuwa salama.


***


“Yaani hiyo kesho kutwa sijui kama tuta fanikiwa”
Levina alizungumza huku akiwa na hasira kidogo, juhudi zote alizo zifanya kwa siku nzima ya leo zime kuwa bure kabisa kwake.
“Levina ina bidi muda mwengine tumsikilize Josephine, huwezi jua kama tunge fanya vile ni jambo gani ambalo linge tokea. Hapa jambo la kufahanya ni kuhakikisha sote tuna kuwa salama na si kufanya ili mradi wa kufanya”
“Sawa nime walewa. Sherehe ndio hiyo ime isha na hakuna hata mende aliye leta shida kwenye eneo hilo”
Levina aliendelea kulalama huku akijifunika shuka,


“Muna onaje nika mtesa mrs Sanga kisaikolojia?”
“Kivipi?”
“Nikampigia simu na kumueleza juu ya mambo aliyo yafanya na nita mueleza kwamba nita ipost video hiyo kwenye mtandao”
“Magreth hilo sio wazo zuri kabisa kwa maana kwa sasa wata kusaka na wata kuua live live”
Levina alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake.


“Anacho kizungumza Levina ni kweli. Tusubirieni siku ya harusi nina imani kazi yetu ita kwenda vizuri”
“Haya”
Wakalala katika hoteli hiyo na siku iliyo fwata asubuhi na mapema wakaelekea katika nyumba wanayo ishi kwa muda.W


“Mpango wetu wa jumamosi kwenye harusi una kuwaje?”
Levina aliuliza huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Nipeni siku ya leo nikilala nikiamka kisha nita wapatia jibu”
Josephine aliwashauri wezake na wakakubalian ana wazo hilo, Siku hiyo nzima wakaitumia katika kutazama filamu ambazo wana zipenda.
“Juma upo wapi?”
“Kwenye mgahawa bosi”
“Tuletee chakula kama kawaida”
“Sawa bosi”
Magreth akakata simu na baada ya muda lisaa Juma akafika katika nyumba hiyo.
“Biashara zina kwendaje?”
“Ina kwenda poa bosi si una jua sisi ndio wauzaji bora wa chakula hapa mjini”
“Sawa Juma pesa uta ziingiza benki?”
“Tayari nimesha ziingiza za leo”
“Sawa nita angalia baadae”
“Haya bosi acha mimi nirudi ofisini”
Juma akapanda pikipiki yake na kuondoka eneo hilo.


“Huyu kaka ni mzuri jamani”
Josephine alizungumza na kuwafanya wezake wamtazame.
“Si nimeongea ukweli mbona muna nishangaa jamani”
“Mmmmmm umempenda hivyo”
“Jamani kwani kumsifia mtu ni kumpenda?”
“Mbona Levina hajamsifia?”
“Yaishe jamani kwa maana na nyinyi muki ng’ang’ania jambo basi hamuliachi”
“Ila sema kama ume mpenda nikuunganishe naye. Huyo ndio mtu ninaye muamini kupita watu wotte pale kazini kwangu”
“Hivi ana itwa Juma eheee?”
“Ndio una taka namba yake ya simu?”
Magreth alimuuliza Josephine swali la mtego.


“Muda bado, ukifika nita kuambia”
“Wewe chelewa chelewa uta kuta mwana sio wako”
Wakapata chakula cha usiku kisha kila mtu akaingia kwenye chumba chake cha kulala. Magreth hakupata usingizi kabisa kwa maana mtu anaye muwazia ni nabii Sanga. Josephine akaanza kusali huku akimuomba Mungu amuonyeshe ni mambo gani ambayo yana kwenda kutokea kwenye siku ya jumamosi. Josephine akajikuta akistuka sana huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana. Akaa akanyanyuka na kukaa kitandani huku akijaribu kutafakari kitu alicho kiona.


‘Ehee Mungu hichi ulicho nionyesha ni kweli?’


Josephine alizungumza huku akitetemeka kwa woga sana. Akaanza kuomba tena na akazidi kuonyeshwa zaidi mambo ambayo kwenye maisha yake hakuwahi hata siku moja kuonyeshwa. Josephine akanyanyuka kitandani hapo na kutoka chumbani kwake. Akawagongea Levina na Magreth na wakatoka kwenye vyumba vyao.
“Kuna nini mbona ume tustua?”
“Nimeona?”


Josephine alizungumza kwa wasiwasi huku jasho likimwagika usoni mwake.
“Umeona nini?”
Magreth aliuliza huku akianza kujawa na wasi wasi kwani toka amfahamu Josephine hakuwahi kumuona katika hali hiyo.


ITAENDELEA


Haya sasa, ni mambo gani ambayo Josephine ame onyeshwa hadi kufika hatua ya kumtisha sana? Usikose sehemu ya 105.
 
SIN 105


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188





ILIPOISHIA


‘Ehee Mungu hichi ulicho nionyesha ni kweli?’


Josephine alizungumza huku akitetemeka kwa woga sana. Akaanza kuomba tena na akazidi kuonyeshwa zaidi mambo ambayo kwenye maisha yake hakuwahi hata siku moja kuonyeshwa. Josephine akanyanyuka kitandani hapo na kutoka chumbani kwake. Akawagongea Levina na Magreth na wakatoka kwenye vyumba vyao.
“Kuna nini mbona ume tustua?”
“Nimeona?”


Josephine alizungumza kwa wasiwasi huku jasho likimwagika usoni mwake.
“Umeona nini?”
Magreth aliuliza huku akianza kujawa na wasi wasi kwani toka amfahamu Josephine hakuwahi kumuona katika hali hiyo.





ENDELEA


Josephine akazidi kutetemeka huku akiwa amejawa na kigugumizi kikubwa sana.


“Jose tuambie ume ona nini?”
“Nimeona siku…hiiyoo kabla ya harusi mji mzima wa Dar ukiwa ni jehanamu ya moto. Wadada, watoto, wazee watu wa kila aina wakiteketea kwa moto. Siku hiyo Dar es Salaam haito kuwa salama kwa mtu hata mmoja. Ninacho washauri rafiki zangu tuondokeni Dar es Salaam. Sijawahi kuona kitu kama hicho kwenye maisha yangu yote ya kuomba”
Levina na Magreth wakatazamana.


“Tuwaambie watu tunao wapenda, hawatakiwi kuwa ndani ya mji kwa siku hiyo”
“Jose ulicho kiona ni kweli au?”


Levina aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao.
“Haki ya Mungu ni kweli, niaminini, tena nime fanya kuota mara mbili mbili. Laiti kama mungekuwa munaona kile ninacho ona mimi au nina weza kuki rekodi na kukiweka kwenye flash basi ninge waonyesha”
“Huo moto una tokea wapi?”
“Sijajua una tokea wapi, ila hiyo siku hali ya Dar es Salaama haito kuwa nzuri kabisa”
“Ehee Mungu watngu”
“Mage muambie Juma hiyo siku asifungue mgahawa na watu wote wafanyakazi wote watoke nje ya jiji la Dar es Salaam”
“Sasa nina anzia wapi kumuambia?”
“Wewe ndio bosi, muambie ni amri na sio ombi. Levina kama una wafanyakazi wako waambie wote waachane na siku hiyo. Tafadhali niaminini”
“Sawa tuta fanya hivyo”
“Nawaomba sana mufanya hivyo”
Usiku huo huo wakaanza kusambaza habari kwa watu wanao wapenda na kila waliye mpigia simu wali msisitizia siku hiyo waweze kutoka nje ya jiji la Dar es Salaam na walipo uliza ni kwa nini hawakuwaeleza ni kwa nini ila waliwasisitizia waondoke.


***


“Japo haito kuwa ni kisasi kile tunacho kihitaji ila siku hiyo ita kuwa ni siku ya kulia na kusaga meno kwa watu wote wenye mapenzi kwa familia ya nabii Sanga na raisi Mtenzi”
Jini Maimuna alizungumza huku akimtazama Evans aliye jilaza kitandani kwenye nyumba mpya yao mpya wanao endelea kuijenga.


“Ni kisasi gani hicho?”
“Siku hiyo kuta fanyika shambulizi moja kubwa sana na baya ambalo Tanzania halikuwahi kutokea”
“Shambulizi gani?”
“Siku kadhaa zilizo pita, raisi Mtenzi alishambulia kundi la Al-Shabab kima kosa. Vijana wa kundi hilo wame amua kulipiza kisasi. Hivyo siku hiyo wata ilipua Dar es Salaama kwenye maeneo yake muhimu sana na itakuwa ni siku ya kukumbukwa”
“Ehee Mungu wangu. Sasa hilo si lina weza likazuiliwa?”
“Hakuna ambaye ana weza kulizuia”
“Kwa nini ikiwa umesha nieleza?”
“Huo ni mpango ambao ume tolewa ili kuwa pigo kwa raisi Mtenzi. Kuna watu ambao ni muhimu sana kwenye serikali yake na hakupaswa kuwafukuza, ila yeye aliwafukuza, basi hayo yanayo kwenda kutokea ndio malipo yake ya kukosa ustamilizvu katika mipango yake.”
“Ila kuan raia ambao wana kwenda kufa pasipo sababu ya msingi”
“Ni lazima wafe”
“Ohoo Mungu wangu. Sasa ita kuwaje?”
“Jiji la Dar es Salaam lina kwenda kuwa moto.”
“Nina mpigia simu Mbogo na kumueleza juu ya hili jambo?”
“Hata ukimueleza hato weza kulizuia. Jambo ambalo una paswa kulifanya kwa sasa ni kumuambia ana paswa yeye na timu yake kuondoka katika jiji la Dar es Salaam tu. Akiwa mkaidi atakufa na watu wake, kwani mabomu ambayo yana kwenda kulipuliwa ni ya nyukilia na yametengenezwa kwenye ubora wa hali ya juu na hakuna ambaye ata jua mabomu hayo sehemu yalipo.”
“Ohoo Mungu wangu.


Evans alijikuta akikaa kitandani huku akihisi mwili wake kuishiwa na nguvu.


“Waambie watu unao wapenda kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam”
“Mage…..Magreth ndio wa kwanza”
Evans alizungumza huku akibabaika. Akaiwasha simu yake na kuiandika namba ya Magreth ambayo ana ifahamu kwa kichwa kuliko hata namba yake mpya.


“Shitiii namba yake ina tumika”


Evans alizungumza huku akizunguka zukunga ndani ya chumba hicho. Akapiga simu kwa mara nyingine na bahati nzuri ikaanza kuita.


“Halooo”
“Mage Mage”
“Evasn!!?”
Magreth alizungumza kwa mshangao.


“Ndio ni mimi sina muda wa kupoteza nisikilize kwa umakini”
“Ngoja kwanza upo wapi?”
“Sina muda wa kukueleza kwamba nipo wapi. Nahitaji kukueleza jambo moja na uliweke akilini. ONDOKA NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM, usijaribu kuhudhuria harusi ya Jery na Julieth. Sawa?”
Magreth akashangaa sana kwa maana taarifa hiyo hiyo ambayo wao wana ishambaza kwa watu, ime mfikia Evans”
“Kumbe hata wewe ume ipata taarifa yangu?”
“Nimeipata kivipi?”
“Mimi, nipo na rafiki zangu hapa wawili, Josephine na Levina, tuna wasisitizia watu kuondoka kwenye jiji la Dar es Salaam”
“Nyinyi mume muaje ikiwa wewe ndio mtu wa kwaza kukupa habari?”
“Mimi nina rafiki yangu ambaye ana uwezo wa kuona mambo yajayo na ndio ame niambia. Niambie upo wapi nikufwate mpenzi wangu.”
Magreth alizungumza huku akiwa na furaha. Kitendo cha kuambiwa na Evans kwamba yeye ndio mtu wa kwanza kumueleza habari hiyo, ana amini bado upendo wake una ishi moyoni mwa Magreth.


“Ame ona nini yeye?”
“Ameona jiji zima la Dar es Salaam likilipuliwa siku hiyo kabla ya harusi”
“Duuu sasa tuna fanyaje kuwaokoa watu zaidi ya hawa?”
“Sijajua, ndio hivyo tuna wapigia simu na kuwaambia waondoke jijini Dar es Salaam”
“Nimepata wazo. Kwanini musifungue page ya Facebook, Instargram na Twitter, muwahimize watu kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam.”
“Wazo hilo ni zuri, je tuna iitaje kwa maana tukifanya kazi hiyo serikali ina weza kutukamata na kutuambia kwamba tuna wapa hofu wananchi wake?”
Evans akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akitafakari majina ya page hizo yaitwaje.
“Nimepata jina”
“Jina gani?”
“Page zote ziiteni HARUSI YA JERY NA JULIETH NI HARAMU. MUSIHUDHURIE NA MUONDOKE JIJINI DAR ES SALAAM”


“Mmmmm jina ni refu sana ila lina weza kuleta matokea chanya”
“Ndio fanyeni hivyo”
“Hii ni namba yako?”
“Ndio”
“Sawa nita kupigia ngoja kwanza nifanye kazi hiyo”
Evans akakata simu huku akimtazama jini Maimuna aliye simama mbele yake. Akaingiza namba ya mzee Mbogo na kumpigia. Simu ya mzee huyo ikaanza kuita na baada ya muda ikapokelewa.


“Habari mzee”
“Salama, vipi Evans, mbona ume piga simu usiku huu saa tisa sasa”
“Ni kweli mzee ila nina maono ambayo nina hitaji kukueleza”
“Maono kutoka kwa wale malaika wako walio kupatia pesa zisizo na chanzo?”
“Ndio, ila nina kuomba unisikilize na wala usiyapuuzie”
“Haya una sekunde stini za kunishawishi juu ya maono yako”
Mzee Mbogo alizungumza kwa dharua kidogo kwa maana yeye ni mtu ambaye haamini sana kwenye mambo ya dini na siku zote ame kuwa akiamini akili yake na uhalisia wa maisha ana endana nao kwa kipindi alichopo.
“Al-Shabab wapo nchini Tanzania”
Mzee Mbogo akakurupuka kwa haraka na kukaa kitako kitandani.
“Una sema?”
“Kundi kubwa la Al-Shabab lipo nchini Tanzania na siku ya jumamosi ina kwenda kuilipua Dar es Salaam, katika muda mmoja na jiji lote lita geuka na kuwa moyo”
Mzee Mbogo akaka kimya huku akijaribu kuiamini maneno hayo ambayoa na yapa asilimia ishirini tu kwenye ufahamu wake wa akili kwamba ni ya kweli.
“Evans mimi na wewe tuna utani?”


“Sijawahi kukutania mzee wangu na hili ninalo kueleza ni ukweli kabisa na wala sio utani. Nime onyeshwa raisi Mtenzi alifanya shambulizi kwenye bandari ya Al-Shabab kimakosa pasipo kudhibitisha juu ya muhusika wa mauaji ya askari wake baharini. Ni kweli au uongo?”
“Hizo habari ni nani aliye kueleza?”
“Mungu”
Mzee Mbogo akatamani kuzungumza neno kali, ila akashindwa na kukizuia kinywa chake kisizungumze jambo baya lolote.


“Alikufukuza wewe na mshauri wake wa karibu, ikiwa nyinyi ndio watu muhimu sana kwenye serikali yake. Nina imani kwamba una jua hiyo hali na mimi wala sina mtu ninaye mjua ndani ya serikali zaidi yako. Al-Shabab wamekuja kulipiza kisasi kwa kufanya shambulizi ambalo toka kuumbwa mwa nchi ya Tanzania halijawahi kutokea. Mashambulizi hayo wata yafanya kwa mabomu ya nyuklia ambayo yana uwezo wa kulipua eneo kubwa sana na watu wengi sana wata kufa. Ninacho kushauri, usijaribu kuzuia hayo mashambulizi kwa maana wewe na timu yako muta kufa.”
Evans alizungumza kwa kujiamini sana. Jini Maimuna akamnyooshea dole gumba akimaanisha kwamba anacho kizungumza ni jambo sahihi.


“Timu yako ina kupenda ndio maana waliamua kufukuzwa na wewe. Waonyeshe upendo kwa kuondoka nao ndani ya jiji la Dar es Salaam na kama ni oparesheni zenu muta kwenda kuzifanyia nje ya jiji hilo. Huo ndio ujumbe wangu nilio ambiwa nikuambie wewe. Ukiuchukua na kuufanyia kazi ni heri kwako, ila ukiupuuzia na kuuacha, basi ita kuwa ni maumivu na kilio kwa watu wako. Asante na usiku mwema”
Evans akakata simu na jini Maimuna akajikuta akimkumbatia kwa nguvu na kumnyanyua kwa furaha.


“Ndio maana nilikuchagua wewe”
“Kweli?”
“Ndio, sija fanya makosa kukuchagua wewe”
Jiji Maimuna alizungumza kwa sauti ya furaha. Jinsi walivyo kumbatiana kwa nguvu, taratibu kukaanza kuamsha hisia za kimapenzi za Evans. Akausogeza mdomo wake karibu na limpsi za jini Maimuna, wakazikutanisha lipsi zao, kitendo cha Evans kunyonya lipsi za jini Maimuna, zikamfanya jini Maimuna kumuachia kwa haraka Evans na kurudi nyuma hatua chache.
“Vipi?”
“Siwezi kufanya mapenzi na binadamu na nikifanya naye basi nita poteza kila kitu ikiwemo nguvu zangu. Hivyo usijaribu kufanya kitu kama hicho siku nyingine. Sawa”
Jini Maimuna alizungumza kwa ukali kidogo huku akimtazama Evans usoni mwake.


“Nime kuelewa na nina omba unisamehe”
“Sawa”
***


Mzee Mbogo akaitazama simu yake kwa muda. Habari aliyo ambiwa na Evans kidogo ime mstua sana kwani kuna baadhi ya mambo ya siri ambayo kijana huyo hayafahamu, ime kuwaje ame yafahamu na ameyaelezea kwa usahihi kabisa pasipo kukosae jambo hata moja.


‘Hawa si ndio manabii wa Uongo hawa?’


Mzee Mbogo alijipa matumaini, ila nafsi yake moja ina endelea kumsisitizia kwamba alicho kizungumza Evans ni kitu cha ukweli kabisa. Mzee Mbogo akavaa suti yake nyeusi kisha akatoka ndani hapo, akaelekea kwenye ukumbi wa vijana wake na kuwakuta wakiendelea kufanya kazi.


“Mkuu kuna page zime funguliwa kwenye mitandao ya kijamii usiku huu, tuna ona zina kua kwa haraka sana na kupata wafuasi wengi kiasi cha kutuogopesha”
John alizungumza huku akimuonyesha mzee Mbogo page hizo tatu zilizo andikwa HARUSI YA JERY NA JULIETH NI HARAMU. MUSIHUDHURIE NA MUONDOKE JIJINI DAR ES SALAAM.


“Ni kina nani hao walio fungua page hizo?”
“Hatufahamu mkuu, tume jaribu kumtafuta muhusika wa hizo page ila hatuja mpata na inavyo onyesha kwamba mtu huyo ana high skill sana kwenye maswala ya mtandao”
Mzee Mbogo akashangaa sana kuona jinsi like za page hizo zinavyo panda kwa kasi. Katika dakika tano alizo ingia ndani ya chumba hicho, watu zaidi ya laki moja na nusu wama like page hiyo. Akaitazama saa yake na kukuta ina eleke saa kumi usiku.


“Muda huu watu wengi si wame lala?”
“Ndio muheshimiwa, ila ina imani kwambe wengi wame shinda macho kwa maana wametoka kwenye send off hivyo sidhani kama wata kuwa wame lala”
John alizungumza huku akimtazama mzee Mbogo usoni mwake.
“Tuna fanyaje mkuu”
“Mmmm”
“Tuna fanayaje ikiwa kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi watu wanavyo zidi kupande page hizo za Facebook, Twitter na Instergram?”
“Tusikilizane. Fungeni kila kitu chetu humu ndani. Kama una ndugu, jamaa rafiki una mpenda mupatie habari hiyo ya kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa maana sio salama kwetu sote”
John na wafanyakazi wengine wote wakajawa na mshangao wa bosi wao kutoa kaulio hiyo kila mtu ndani ya chumba hicho akatamani kufahamu ni kwa nini wana ambiwa waondoke jiji la Dar es Salaam ikiwa ulinzi ni mkali sana na wao wana ifanya kazi hiyo kuwalinda watu.


ITAENDELEA


Haya sasa, mzee Mbogo ame amua kuondoka na vijana wake, je ata wapa sababu gani ili waweze kumuamini ikiwa yeye ame elezwa utabiri ambao kwa kazi yake sio kitu cha kuaminika kabisa? Usikose sehemu ya 106.
 
SIN 106


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188



ILIPOISHIA


“Tuna fanyaje mkuu”
“Mmmm”
“Tuna fanayaje ikiwa kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi watu wanavyo zidi kupande page hizo za Facebook, Twitter na Instergram?”
“Tusikilizane. Fungeni kila kitu chetu humu ndani. Kama una ndugu, jamaa rafiki una mpenda mupatie habari hiyo ya kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa maana sio salama kwetu sote”
John na wafanyakazi wengine wote wakajawa na mshangao wa bosi wao kutoa kaulio hiyo kila mtu ndani ya chumba hicho akatamani kufahamu ni kwa nini wana ambiwa waondoke jiji la Dar es Salaam ikiwa ulinzi ni mkali sana na wao wana ifanya kazi hiyo kuwalinda watu.





ENDELEA


“Kwa nini mkuu?”
John aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.


“Baada ya jumamosi ndio nita waeleza ni kwa nini tume ondoka Dar. Mwenye ndugu yake, jamaa rafiki, mpenzi, watoto. Nina wapa masaa sita hadi ina timia saa mbili kamili asubuhi tuwe tumesha ondoka jijini Dar es Salaam. Magari ya usafiri yapo lori zangu mbili zenye kontena mbili mbili zita beba hivi vifaa. Sasa muna weza kutawanyika”
Baada ya mzee Mbogo kuzungumza maneno hayo akaondoka ndani hapo na kuwaacha vijana wake wakiwa katika majadiliano ya kwa nini mkuu wao ame waambia hivi. John akamfwata mzee Mbogo ndani kwake.
“Mkuu samahani. Bado ume tuacha njia panda tueleze ni kitu gani ambacho kina kufanya uwaamini watu wa mitandao na wanao himiza watu kutoka nje ya jiji la Dar es Salaam.”
“John una niamini?”
“Ndio mkuu”
“Basi fanya hivyo.”
John akashindwa kuuliza swali jengine na akatoka ndani hapo. Mzee Mbogo akakusanya baadhi ya nguo zake pamoja na vitu vya muhimu na kuviingiza kwenye begi lake kubwa. John akawahimiza wafanyakazi wezake kutekeleza agizo la mkuu wao na kila mmoja akaelekea kwake huku wakiwajulisha watu wao wa karibu kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaa.


***


Mli wa simu inayo ita kwa mbali, ukaanza kusikika masikioni mwa Julieth aliye lala fofofo huku akiwa amechoka sana. Akaanza kupapasa pembeni ya mto wa wake na akaishika simu yake, akaitazama kwa sekunde kadhaa na kukuta ni namba ya rafiki yake anaye itwa Rebeca.


“Haloo”
“Julieth bado ume lala?”
“Ndio, vipi mbona asubuhi asubuhi hivi?”
“Amka shosti yangu na uingie kwenye facebook kumechafuka huko”
“Una maanisha nini?”
“Wewe ingia shosti yangu”
Julieth akakata simu na kuiweka pembeni. Akajilaza kidogo, ila nafsi yake ikamshawishi kuangalia ni nini hicho ambacho kimemfanya rafiki yake huko kupiga simu asubuhi hiyo. Akajilaza chali, na kuingia kwenye mtandao wa Facebook. Akastuka sana mara baada ya kukuta ukurasa unao hizimiza watu kutoka nje ya jiji la Dar es Salaam huku wakidai kwamba harusi yake na Jery ni haramu.


“Watu milioni kumi wame like?”
Julieth alizungumza huku mapigo ya moyo yakianza kumuenda spidi. Akajaribu kutafuta nani ni muhusika wa page hiyo ila akashindwa. Akashuka kitandani na kujifunga tenge na akatoka ndani hapo, akaelekea chumbani kwa wazazi wake, akagonga na baada ya muda mlango uka funguliwa na mama yake.
“Mama kuna tatizo”
“Tatizo gani?”
“Ona kilicho andikwa mtandaoni”
Julieth alizungumza huku akimuonyesha mama yake. Mrs Sanga akasoma jina la page hiyo.


“Sasa kinacho kuogopesha ni nini?”
“Mama watu wana seme kwamba ndoa yangu na Jery ni haramu watu waondoke Dar es Salaam alafu wewe una sema ni nini kinaniogopesha?”
“Ahaa hayo mambo ya mtandao mwanangu. Hembu achana nayo, kwenye kipindi kama hichi vitu hivi vita jitokeza vingi tu. Wewe una paswa kuangalia ndoa yako, sawa”
“Mama”
“Wewe achana na wapuuzi tu hao”
“Kuna nini?”
Nabii Sanga aliuliza huku naye akisimama mlangoni hapo.
“Eti ameona hii page facebook huko ndio ina mtatiza mwanao. Nabii Sanga akasoma jina la page hiyo, akaangalia idadi ya watu walio like.
“Mmmm kuna jambo hapa”
“Umeona baba ehee?”
“Ndio, watu milioni kumi, na page ime funguliwa usiku wa kuamki leo. Lazima kuna kamchezo ambako kana fanyika. Hembu ngoja niwasiliane na raisi?”
“Bora baba na wewe ufanye hivyo, mimi ngoja nimpigie Jery”
“Sawa’


Julieth akaitafuta namba ya Jery na kumpigia.


***


Jery akaitazama simu yake kwa sekunde kadhaa na kuipokea namba ya mke wake mtarajiwa.


“Umeamkaje mke wangu?”
“Vibaya baby, ume ona kwenye facebook jinsi watu wanavyo tuchafua kuhusiana na ndoa yetu?”
“Ndio nime ona mke wangu na sio facebook pekee, ila kuna Instergram pamoja na Twitter”
“Sasa tuna fanayaje mume wangu?”
“Watu wa I.T wa baba wana endelea kuhakikisha kwamba tuna mpata muhusika alite fanya huu ujinga”
“Mume wangu fanya hivyo basi kwa maana hili jambo lina niogopesha”
“Usiogope mke wangu. Hivi una weza uka hisi kwamba ni nani ambaye ana weza kuhusika na hili jambo?”
“Sina idea yoyote ya nani ambaye ana husika na hili swala”


“Sawa, jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba una tulia na usipokee pokee simu za watu wasio na maana hadi hili jambo litakapo wekwa chini ya uangalizi.”
“Sawa mume wangu”
“Nakupenda mke wangu na nipo kwa ajili yako na wala usijali katika hilo”
“Sawa mume wangu nina kupenda pia”
Jery akakata simu huku akimtazama baba yake.


“Sija mpokelea simu baba yake nina imani naye ata kuwa ana ulizia kuhusiana na jambo hilo hilo?”
“Ndio baba, wana wasiwasi sana”
“Ni kweli, ila sijui ni kwa nini hao watu wana wameanza kuiandama ndoa yetu”
“Nita muagiza mkuu wa mkoa kuzungumza na wananchi wake”
“Afanye hivyo basi baba kwa maana nina weza kukosa mke”
“Huwezi, hayo ni mambo ya kimtandao tu na hatuna budi katika kuyapuuzia.”
“Sawa, ngoja nika pumzike, kwa maana hili swala lime nifanya nikose usingizi”
Jery akatoka ofisini hapo na kuelekea chumbani kwake. Raisi Mtenzi, akampigia simu mkuu wa mkoa na kumuagiza ahakikishe ana toa angalizo kwa wachafuaji wa harusi ya mwanaye.


***


Magreth akapunguza mwendo wa gari lake na kulivuka tuta lililopo barabarani hapo. Akilini mwake mwote ana muwaza Evans wake.


“Jamani oneni”
Levina alizungumza huku akiwaonyesha wezake hao mahojiano ya mkuu wa mkoa yanayo ruka moja kwa moja kwenye vyombo vya habari.


“Ndugu zangu wana Dar es Salaam. Wengi wenu nina imani kwamba mume weza kuona uvumi ambao una zidi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Istergram na Twitter. Habari zina dai kwamba ndoa ya mtoto wa raisi wetu kipendi muheshimiwa mtenzi, kwamba ni harumu na watu waondoke ndani ya jiji la Dar es Salaam.”
“Kwa mtazamo wa haraka haraka, una weza kugundua huyu mtu aliuye fungua huu ukurasa ana tatizo la kiakili. Haiwezekani harusi ikufanye wewe mwananchi kuacha shuhuli zako au makazi yako na ukaondoka ndani ya jiji letu pendwa Dar es Salaam”


Mkuu wa mkoa alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana sana usoni mwake.


“Labd mimi nitoe angalizo kwa mtu aliye fungua page hizi. Mara moja nina hitaji azifute au wataalamu wetu wa mambo ya mtandao, wana endelea kumtafuta na endapo ata kamatwa basi tuta hakikisha kwamba ana shitakiwa kwa sheria za kimitandao, kama zinavyo elekeza.”


“Ulinzi wa jiji letu ni himara, kama ilivyo kuwa jana siku ya send off. Hapakuwa na tukio hata la kibaka kumwapua mtu simu. Hivyo ndugu zangu wana Dar es Salaam, nina waomba mukae majumbani mwenu na siku ya sherehe basi mujitokeze kwa wingi kanisani na barabarani kuwapungia mikono maharusi wetu wakiwa wame toka kanisani.”
“Nirudie tena, nina wahakikishia ulinzi kila raisin a hakuna haja ya nyinyi kujawa na wasiwasi. Nina wapenda sana wananchi wangu na asubuhi njema”
Mazungumzo hayo ya mkuu wa mkoa na waandishi wa habari yakaishia hapo.


“Huyu baba ata waponza wezake”
Josephine alizungumza huku akiwa amekaa siti ya nyuma ya gari hilo.


“Ni kweli, ila hatuna namna, watakao tusikia watusikie na wasio tusikia acha wajitokeze waka punge mikono barabarani”
Magreth alizungumza huku akiwa nyuma ya basi liendalo mkoani Dododma.
“Au tuwawekee sababu ya kitu kinacho kwenda kutokea Jumamosi?”
Josephine alishauri.


“Hakuna haja na hata tukiwawekea sababu hawato tuamini”
“Hivi Levina hawato weza kuhack na kujua ni wapi ulipo?”
“Hakuna anaye weza. Hii wata sumbuka na ime kula kwao”
Levina alizungumza huku akiifunga laptop yake. Safari ikazidi kuendelea huku wakizungumza mambo mbalimbali. Wakafika mkoani Morogoro majira ya saa tatu asubuhi. Wakakodisha chumba kimoja kwenye hoteli ya kifahari kwa ajili ya kusubiria matokeo ya nini kinacho kwenda kutokea Jumamosi.
***


Omary na wezake, wakaanza kujiuliza ni kina nani wanao himiza watu kuondoka jijini Dar es Salaam.


“Ila mkuu usiwe na wasiwasi. Mkuu wa mkoa alisha toa matumaini kwa wana nchi wake. Tuta kufa na wengi”
“Nahitaji leo hii, tusambaze simu hizi maeneo tofauti na jiji hili. Nahitaji tuhakikishe, tuna ichoma Dar es Salaama kama walivyo ichoma bandari yetu”
“Ila mkuu hapo nina ushauri”
“Ushauri gani?”
“Tunapo kwenda kuzisambaza hizi simu, tuna wapa watu au tuna zisambaza kwa mfumo gani?”
“Nilihitaji kwenda kuzidumbukiza kwenye maeneo mbalimbali kama mitaro mashino ya maji machafu na tuhakikishe ziwe on na pia tuhakikishe kwamba tume ziweka kwenye kirambo ili zisiharibike na maji”
“Sawa mkuu”
Omary akaanza kugawa simu hizo ambazo jina lake maarufu ni Nokia Obama au Nokia tochi. Simu hizo zime fungwa mabomu ambayo kwa muonekano wa macho ni madogo sana, ila kwa jinsi walivyo yaunda yana uwezo wa kusambaratisha eneo kubwa sana. Vijana hao wa kundi la Al-Shabab mara baada ya kugawana simu hizo wakatoka kila mmtu kwa wakati wake na wakaanza kusambaa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Wakafanikiwa kuzisambaza simu hizo katika maeneo muhimu ya jiji la Dar es Salaam kisha wakarudi kwenye handaki lao eneo hilo la Kariakoo kwa kusubiria siku ya kesho kufanya shambulizi moja litakalo kumbukwa na kila Mtazania kwenye maisha ya mbeleni.
***


Mzee Mbogo akaendelea kuongoza msafara wa magari ya wafanyakazi wake pamoja na familia zao. Wakafika Turiani Morogoro, kwenye mashamba makubwa ya mzee Mbogo, eneo analo lima zao la mpunga. Katikati ya mashamba hayo makubwa, ame jenga jumba kubwa la kifahari ambalo alikuwa ana ishi yeye na marehemu mke wake katika siku zao za mapumziko.


Akawakaribisha wafanyakazi wake ambao wame andamana na familia zao na wakaanza kufunga mitambo yao kwenye moja ya holi kubwa.


“Nawashukuru sana kwa kunisikiliza na kuja. Tuta kaa hapa hadi pale tutakapo jua hali halisi inayo endelea Dar es Salaam”
“Ila mkuu tume msikia mkuu wa mkoa kisisitiza kwamba hali ni shwari?”
“Ndio ila kumbukeni kwamba NSA hadi sasa hivi haijarudi hewani. Leo ni ijumaa na kesho ni Juma mosi, tuangalie ni nini kitakacho tokea kisha mambo yatakapo kuwa shwari basi tuta rudi Dar es Salaam. Najua wengi wenu mume zoea kuona magorofa, ila huku ni shamba muta ona mpunga na ndege wengi”
Mzee Mbogo aliwatania wafanyakazi hao na wakaanza kucheka. John akaanza kugawa majukumu yake kwa wezake huku akitenga wapishi ambao wata kuwa wana pokezana kupika.
***


“Mage mbona una onekana una mawazo sana?”
Josephine alimuuliza Magreth huku akimtazama usoni mwake.
“Nina muwazia sana Evans”
“Ila si ume pata namba yake ya simu?”
“Ndio ninayo”
“Mpigie na umuombe msamaha”
“Kwa niliyo mfanyia kweli ata nielewa?”
“Evans ni binadamu ana jua kuna makosa. Ata kusamehe tu rafiki yangu”
Magreth akamtazama Josephine kwa muda kisha akampigia Evans. Simu ya Evans ikaanza kuita na kuyafanya mapigo ya moyo kuanza kunda kasi sana. Simu ikakatika, akashusha pumzi na akapiga tena, simu hiyo ikaanza kuita tena.


“Haloo”
Magreth alianza kuzungumza mara baada ya simu hiyo kupokelewa.


“Nani wewe?”
Sauti nyororo ya kike kidogo ika mstua sana Magreth.


“Aha…mimi nina itwa Magreth naweza kuzungumza na mwenye simu?”
“Mimi ni mke wake hivyo una weza kuniachia maagizo yote nikampatia mume wangu kipenzi Evans”
Maneno ya mwanamke huyo yaka mnyong’onyeza sana Magreth na kujikuta akikata simu huku akiwa amekata tamaa kabisa ya kumpigia Evans. Haikuisha hata dakika mbili, meseji ikaingia kwenye simu yake, akaifungua mseji hiyo kutoka kwa namba ya Evans ambayo ilizidi kumnyong’onyeza Magreth kwa maana hakutaraji kama Evans ana weza kuwa na mke.


ITAENDELEA


Haya sasa ni meseji gani ambayo Magreth ame tumiwa kutoka kwenye namba hiyo ya Evans na kwa nini ime mnyong;onyeza? Usikose sehemu ya 107.
 
SIN 107


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188



ILIPOISHIA


“Nani wewe?”
Sauti nyororo ya kike kidogo ika mstua sana Magreth.


“Aha…mimi nina itwa Magreth naweza kuzungumza na mwenye simu?”
“Mimi ni mke wake hivyo una weza kuniachia maagizo yote nikampatia mume wangu kipenzi Evans”
Maneno ya mwanamke huyo yaka mnyong’onyeza sana Magreth na kujikuta akikata simu huku akiwa amekata tamaa kabisa ya kumpigia Evans. Haikuisha hata dakika mbili, meseji ikaingia kwenye simu yake, akaifungua mseji hiyo kutoka kwa namba ya Evans ambayo ilizidi kumnyong’onyeza Magreth kwa maana hakutaraji kama Evans ana weza kuwa na mke.





ENDELEA


“Mage mbona ume nyong’onyea?”
Levina alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake. Magreth hakujibu kitu chochote zaidi ya kuwa katika hali ya unyonge. Levina akaichukua simu ya Magreth na kuisoma meseji hiyo aliyo tumiwa.


‘Wewe malaya, achana na mume wangu. Kama alikujulisha uondoke Dar sio kwamba ana kupenda, tambua sasa hivi nina mimba ya Evans na nikisha jifungua nina funga naye ndoa hivyo kaa mbali na mume wangu’


“Huyu demu fala kweli”
Levina alizungumza kwa ukali huku akiachia msunyo ambao uka mstua Josephine ambaye ana endelea kuperuzi peruzi kwenye mitandao ya kijamii.


“Kuna nini?”
“Si kuna malaya wa Evan ana mtishia rafiki yetu”
“Ana mtishiaje?”
“Eti ana dai kwamba aache kumsumbua mume wake, hembu soma huo ujinga”
Levina akamrushia Josephine simu hiyo na akainyaka. Akasoma meseji hiyo kisha akamtazama Magreth ambaye ame tulia tuli, mithili ya mtu anaye sikilizia jambo fulani asilo lielewa kwa umakini sana.


“Jose lete hiyo simu”
Josephine akamrushia Levina simu ya Magreth. Levina akapiga tena namba ya Evans na ikapokelewa.


“Wewe malaya si nime kuambia usi mpigie mume wangu. Au una taka nikutafute nikuonyeshee ehee?”
“Sikiliza wewe mseng** uliye poteza muelekeo. Usijaribu kudili na watu usio wajua umeelewa wewe mwehu. Kama una taka tukutafute basi, mimi ndio nitakaye kutafuta na nita shuhulika na wewe. Sasa ole wako utume meseji zako za kijinga nita kuonyesha. Una hisi sisi wakijijini eheee, tumezaliwa Dar es Salaam na tume kulia Dar mbwa wewe”
Levina alizungumza bila hata ya kuwa na kituo. Simu ikakatwa, Levina akapiga tena, ikakata, akarudi kupiga tena na ikakatwa.
“Hii ndio dawa ya kushuhulika na machizi kama hawa”
Levina alizungumza na kumfata Magreth kumtazama tu.
“Lev kumbe una zungumza ehee?”
“Tena hap anime mstai tu kutokana upo wewe mtu wa Mungu, laiti ninge kuwa peke yangu, ninge mchamba huyu hadi ange ona dunia nzima ni chungu. Watu tume vurugwa, tuna mastress yetu na yeye ana tuleteea ujinga, na wewe Mage ujifunzage kujibu, sio kuambiwa hivyo kidogo una pooza kama ume chomwa ganzi bwana”
“Levina hujui ni jinsi hani ninavyo mpenda Evans, hujui ni jinsi gani nilivyo umia”
“Utaumia zaidi na zaidi, kutokana na ujinga wako. Pigania penzi lako acha ujinga wewe, ukikaa na kujifanya una jihisi mnyonge ndivyo utakavyo jikuta mwanaume aunaye mpenda akichukuliwa na uta baki uking’aa ng’aa macho”
Maneno ya Levina kidogo yakampa nguvu Magreth.
“Eti”
“Nyoo eti nini, pigania penzi lako. Isitoshe ana dai kwamba yeye ni mjaumzito na hawajafunga ndoa, ni rahisi sana kumchukua mume wake. Fanya juhudi katika hilo”
“Sawa nisaidie kuitafuta namba ni wapi ilipo”
“Poa”
Levina akaanza kuitafuta namba ya Evans ni wapi ilipo kwa kutumia satelate ila jambo la kushangaza hakuweza kujua ni wapi ilipo na ina onyesha kwamba haijasajiliwa katika mtandao anao utumia.


***


“Wata jaribu kukutafuta, ila sinto hitaji uchanganye mapenzi na mipango yetu tuliyo kuwa nayo hivi sasa”
Jini Maimuna alizungumza huku akimtazama Evans usoni mwake.
“Sawa ila maneno uliyo wajubu nina imani yata muumiza sana”
“Ni heri aumie sasa kuliko kupoteza mipango yako.”
Jini Maimuna alizungumza huku akitazama gorofa linalo jengwa nyumbani hapo kwa kina Evans. Uwepo wa Maimuna katika eneo hakuna mtu mwengine anaye muona zaidi ya Evans yeye mwenyewe.
“Maimuna?”
“Bee”
“Hivi hatuwezi kuwasaidia watu wa Dar es Salama kesho waka ondokana na janga lililopo mbele yao”
“Hatuwezi”
“Kwa nini?”
“Una jua kuna mambo duniani yakitokea, mengina yana kuwa ni mpango wa Mungu na mengine yana kuwa ni mpango wa shetani”
“Kwa hiyo hilo la kesho ni mpango wa Mungu?”
“Hamsini kwa hamsini”
“Una maanisha nini?”
“Raisi wenu aliwatoa watu muhimu ambao walikuwa ni muhimili katika kukiongoza kichwa chake hususani kwenye maamuzi. Hilo linalo kwenda kutokea nia adhabu yake kwa kuwasaliti wezake na kufaya maamuzi ambayo hapo awali alipaswa kuwa mstamilivu”
“Ila kuna msamaha?”
“Msamaha uta patikana baada ya kupata adhabu anayo kwenda kuipata”
“Daa ina niuma sana kwa maana kuna watu ambao wata kufa bila ya hatia?”
“Ni kweli, ila kuna kipindi nchi ina takiwa kutoa kafara, ili mambo mengine yaende na iji jenge vizuri. Hilo linalo kwenda kutokea ni kafara na kuanzia hapo uta pata nguvu”
“Nani?”
“Wewe, uta pata nguvu na uta kuwa na ushawishi ambao hata wala walio kuwa wana kuchukulia poa basi wata kusujudia”
Jini Maimuna alizungumza maneno ambayo yakamfanya Evans kujisikia vizuri moyoni mwake kwani tamaa ya mafanikio ime sha mtawala moyoni mwake na sasa tayari amesha yaonja maisha ya utajiri na hataki kurudi tena kwenye umasikini.


***


“Muheshimiwa bado hatuja fanikiwa kumpata muanzilishi wa page hizo”
Kijana anaye shuhulika na mambo ya kimtandao alizungumza huku akimtazama raisi Mtenzi usoni mwake.
“Mume jaribu kuzi ripoti kwenye kampuni husika hizo page?”
“Ndio, tume jaribu kuwatumia maombi Facebook, Instergram na Twitter ili wazifunge page hizo ila hadi sasa hivi hatuja pokea majibu yoyote na kila dakika wafusi wana zidi kungezeka”
“Sawa, mukijibiwa uta kuja kuniambia. Sawa”
“Sawa muheshimiwa”
Kijana huyo akatoka ofisini hapo. Raisi Mtenzia akampia simu sekretari wake na akaingia ndani hapo.
“Niandalie kikao na mkuu wa mkoa. Meya wa jiji, mkuu wa majeshi pamoja na waziri wa mambo ya ndani. Nina hitaji kuzungumza nao baada ya lisaa moja wawe hapa”
“Sawa muheshimiwa raisi. Alafu mama yupo hapo nje ana hitaji kuonana na wewe”
“Mruhusu aingie”
“Sawa”
Sekretari huyo akatoka, akaingia mrs Mtenzi ambaye uso wake una onyesha kuto kuwa na furaha.
“Mume wangu nina pata simu za usumbufu. Watu wana niuliza kwa habari hizi za kuondoka jijini Dar hadi nina pata hofu”
“Mke wangu usimjibu mtu yoyote juu ya mambo hayo. Tambua kwamba nchi ipo kwenye hali ya usalama na hili ndio jiji letu na ulinzi ni mkali sana”
“Sawa mume wangu. Je hawa wananchi wanao hoji na kuulizana maswali huko kwenye mitandao ya kijamii tuna watuliza vipi?”
“Nchi yetu ni ya kidemokrasia. Kila mtu ana uhuru wa kuzungumza anacho jisikia, ili mradi asienende kinyume sheria za nchi. Jambo la msingi ni wewe kuhakikisha kwamba una tuliza akili na kesho harusi ipo kama kawaida, hakuto kuwa na hata panya wa kukatiza mtaani. Umenielewa mke wangu”
“Sawa mume wangu”
“Njoo”
Mrs Mtenzi akasimama kutoka kwenye kiti alicho kalia na kuzunguka meza ya mume wake na kusimama pembeni yake. Taratibu raisi Mtenzi akasimama na kumshika kiuno mke wake.


“Tambua kwamba mimi ndio raisi. Nina jukumu la kuilinda nchi yangu na watu wake, huwa una jua nikizungumza nina maanisha. Hivyo maneo ya kimtandao yasikuumize kichwa, sawa mama watoto”
“Sawa mume wangu”
Raisi Mtenzi akambusu mke wake mdomoni kisha akamuachia.
“Wewe nenda kazungumze na wageni wetu, nikitoka ofisini nita jumuika nanyi”
“Sawa mume wangu”
“Nina kupenda”
“Nina kupenda pia”
Mrs Mtenzi akambusu mumewe shamvuni kisha akatoka ndani hapo. Akapisha na sekretari mlangoni.
“Muheshimiwa, nimesha wajulisha na wana kuja”
“Sawa wakifika wote waambie nikutane nao kwenye ukumbi namba moja”
“Sawa muheshimiwa”
Raisi Mtenzi akashusha pumzi taratibu, akaichukua simu yake na kuanza kutazama kutazama kurasa ya Intergram ambayo ina wahimiza watu kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam na ndoa ya Jery na Julieth ni haramu. Simu ya mezani ya raisi Jery ikaanza kuita, akaitazama kwa sekunde kadhaa kisha akachukua mkonga wa simu na kuiweka sikioni mwake.


“Halooo”
“Habari muheshimiwa raisi”
“Una hitaji nini The Brain?”
“Natambua kwamba ume nitoa nje ya nafasi ya ushauri. Ila nina imani kwamba una weza kuona ni mambo gani ambayo yana endelea kunywe mtandao si ndio”
“Ndio”


“Hapa nilipo nami nipo kwenye harakati za kuondoka jiji la Dar es Salaam. Ukiachilia mbali kwamba wewe ni raisi au bosi wangu, ila wewe ni rafiki yangu na pia ni mdogo wangu. Nitakueleza ukweli, uwe una penda ua hupendi,ila huu ni ukweli. Hili ambalo una ona lina endelea kwenye mitando ya kijamii, sio jambo la kulipuuzia hata kidogo. Fukua fukua ili uone ni kipi kipo nyuma ya pazia, nina imani kwamba uta kuwa una watafuta waanzilishi wa kurasi hizi kwa ajili ya kuwakamata. Ila jambo moja Chinas, una paswa kuwa na busara, waulize ni kitu gani ambacho kina wafanya wahimize watu kuondoka jiji la Dar es Salaam na endapo uta pata sababu uta jua ni njia gani utatue, ila ukiendelea kuwa mbabe mdogo wangu. Hata mimi sijui ni nini kita tokea, ndio maana nina hamasika na mimi kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam. Nikutakie ndoa njema ya vijana wako”
Simu ikakatwa na kumfanya raisi Mtenzi kuishusha simu hiyo chini taratibu. Jambo hili ambalo hapo awali alilichukulia kama mzaha sasa lina anza kumkaa akilini mwake vizuri. Raisi Mtenzi akampigia simu mr THE Brain.
“Ndio muheshimiwa”
“Nahitaji uje ikulu sasa hivi?”
“Muheshimiwa uta nisamehe kwa maana na mimi nina ondoka Dar es Salaam”
“Tafadhali nina kuomba sana ugahiri hiyo safari nina kuomba uje ikulu sasa hivi”
Mr the Brain akaka kimya kwa sekunde kama thelathini.
“Sawa nina kuja ila nita kaa lisaa moja, kisha nita endelea na safari yangu”
“Nashukuru kwa kuitikia wito wangu”
Raisi Mtenzi akakata simu yake kisha akampigia simu makamu wa raisi ambaye yupo nchini China kwa ziara ya kikazi.
“Habari muheshimiwa”
“Salama, kuna jambo linalo endelea kwenye mitandao ya kijamii. Je ume fanikiwa kuliona?”
“Ndio muheshimiwa, nime jaribu kuomba msaada kwa serikali hii kujaribu kutusaidia kuwapata waanzilishi wa page hizo”
“Wame semaje?”
“Wana lishuhulikia muheshimiwa, ila sija taka kuwaambia kwamba kitengo chetu cha NSA, kina tatizo”
“Kazi nzuri ndugu yangu”
“Watakapo fikia basi nita kujulisha muheshimiwa”
“Sawa sawa”
Sekretari akagonga na raisi Mtenzi akamruhusu kuingia ndani kwa ishara.


“Muheshimiwa wageni wote wamesha fika”
“Sawa twende ila wasiliana na mr the Brain na umuambie aje kwenye ukumbi namba moja”
“Mr the Brain ame rudi kazini?”
“No nime muita kwa ajili ya hili jambo”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Raisi Mtenzi akaingia ndani ya ukumbi huo na kuwafanya viongozi alio waita hapo kusimama kwa heshima. Alipo kaa kwenye kiti chake na yeye akakaa.
“Nime waita hapa wa ajili ya hili swala linalo endelea kwenye mitandao ya kikamii. Wana nchi bado wana hofu kwenye hili, je kuna hata mmoja wenu ambaye ana weza kuwaza au kufikiria ni kitu gani ambacho kita kwenda kutokea?”
“Muheshimiwa kwa upande wangu najaribu kutafuta sababu ya hawa watu au mtu kufungua hizo kurasa, ila nina shindwa kupata jibu la uhakika katika hili.”


Mkuu wa mkoa alizungumza, mlango ukafunguliwa na akaingia mr the brain akawasalimia watu wote, kisha akatafuta kiti na kukaa.
“Nashukuru kwa kuja ndugu yangu”
“Usijali muheshimiwa”
“The Brain swala tunalo jadili ni kuhusiana na hili jambo la wananchi kuhimiza kuondoka jiji la Dar es Salaam nawe ni mmoja wapo ya watu walio kuwa wana ondoka jijini. Tuambie una maoni gani juu ya jambo hili?”
“Muheshimiwa nchi ipo kwenye shambulizi na eneo ambalo lime pangwa kutoka kwa mashambulizi hayo ni jiji la Dar es Salaam”
Mr the Brain alizungumza kwa kujiamini na kuwafanya viongozi wote kustuka.
“Shambulizi gani na nani ambaye ana kwenda kuishambulia nchi?”
“Dakika tano kabla sija ingia hapa ndani, nilikuwa nina zungumza na mr Mbogo uliye mfukuza kwenye kitengo cha NSA. Yeye na timu yake wamesha ondoka jijini Dar es Salaam na ameniambia kwamba kesho kwenye harusi ya mwanao. Kundi la Al-Shabab ambalo uli lishambulia kima kosa wata fanya shambulizi, hivyo muheshimiwa, haijulikani ni wapi na wapi wata shambuli na wala kati yetu hakuna anaye fahamu ni saa ngapi wanavyo shambulia. Kiufupi muheshimiwa, kesho haito kuwa siku nzuri kwako na taifa kwa ujumla”
Maneno ya mr the Brain yaka wafanya viongozi wote macho kuwatoka, huku raisi Mtenzi mapigo ya moyo yakianza kumuenda kasi sana kwani wamebakisha muda mchache sana kabla ya harusi ya kijana wake kufanyika.


ITAENDELEA


Haya sasa raisi Mtenzi ana pata habari ya jiji zima kushambuliwa na muda walio nao ni mchache, je wata fanikiwa kuzuia mashambulizi ya kundi hilo la Al-Shabab? Usikose sehemu ya 108.
 
SIN 108


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188





ILIPOISHIA


“Dakika tano kabla sija ingia hapa ndani, nilikuwa nina zungumza na mr Mbogo uliye mfukuza kwenye kitengo cha NSA. Yeye na timu yake wamesha ondoka jijini Dar es Salaam na ameniambia kwamba kesho kwenye harusi ya mwanao. Kundi la Al-Shabab ambalo uli lishambulia kima kosa wata fanya shambulizi, hivyo muheshimiwa, haijulikani ni wapi na wapi wata shambuli na wala kati yetu hakuna anaye fahamu ni saa ngapi wanavyo shambulia. Kiufupi muheshimiwa, kesho haito kuwa siku nzuri kwako na taifa kwa ujumla”
Maneno ya mr the Brain yaka wafanya viongozi wote macho kuwatoka, huku raisi Mtenzi mapigo ya moyo yakianza kumuenda kasi sana kwani wamebakisha muda mchache sana kabla ya harusi ya kijana wake kufanyika.





ENDELEA


Macho ya viongozi wote yapo kwa raisi Mtenzi ambaye jasho la uso lime anza kumtiririka. Akilini mwake akakumbuka jinsi mzee Mbogo alivyo kuwa ame kataa kabisa kufanya shambulizi kwa Al-Shabab pasipo kuwa na kidhibitisho kwamba wao ndio wame husika katika shambulizi la kuwaua askari wake wa majini.


“Muheshimiwa raisi”
Mkuu wa mko alimuuia raisi Mtenzi, ila hakuitika.


“Muheshimiwa”
“Mmmmm!!!”
“Tuna fanyanye mkuu”
Waziri wa mambo ya ndani aliuliza huku akimtazama raisi Mtenzi usoni mwake.


“The Brain ulizingumza na na…na na nani?”
“Mbogo?”
“Ndio muda gani?”
“Kwa sasa zita kuwa ni dakika kumi zilizo pita”
“Yeye amepata wapi hizo habari?”
“Hakuniambia sorce ya habari yake, ila kama unavyo fahamu. Mbogo ni mtu mzuri sana kwenye maswala ya upelelezi muheshimiwa. Isitoshe kwa sasa yupo nje ya serikali yako hivyo ana weza kuwa na vyanzo vingi vya habari nyeti kama hizo ndio maana aka nieleza kama rafiki yake”
“Una weza kumpigia simu”
“Alafu nimuambie nini?”
“Aje hapa ikulu”
“Kabla sija mpigia ila ukweli muheshimiwa ni kwamba hayupo ndani ya jiji la Dar es Salaam”
“Wewe mpigie simu”


Raisi Mtenzi alizungumza kwa msisitizo huku akiwa na wasiwasi mwingi sana moyoni mwake. Mr the Brain, akampigia simu mzee Mbogo.
“Ndugu yangu umesha anza safari?”
“Hapana, nipo ikulu sasa hivi na nipo na raisi. Nime mfikishia ile habari ambayo ume niambia na ame kuomba uweze kuja ikulu”
“Najua ume weka loud speeker si ndio?”
“Ndio”
“Raisi ana nisikia vizuri si ndio?”
“Ndio ana kusikia”
“Ngoja niwe muwazi, siwezi kurudi Dar es Salaam kwa sasa hivi. Pia siwezi kufanya kazi kwenye serikali ambayo haiwezi kunisikiliza. Mimi nime kuwa professional kwenye hii kazi sasa una kwenda mwaka wa arobaini na tano. Nime fanya kazi na maraisi wa awamu kama nne hivi na wote waliheshimu mawazo yangu na hapakuwa na kitu chochote kilicho weza kutokea katika serikali zao.”
“Muheshimiwa raisi nilikuwa nipo very disappointed kwa maamuzi uliyo yafanya kwenye kundi la Al-Shabab. Ningekuwa sija kushauri hapo kweli unge sema nina makosa. Ila nime kushauri na nikaenenda kinyume ana oder yako ya kuwashambulia, ila ulicho kifanya ni kunifukuza kwenye nafasi ambayo nilihitaji kustafu kwa heshima, ila ile siku nilistafu kwa kudhalikishwa mbele ya wafanyakazi wangu ambao wote wame amua kuungana na mimi kwa manaa kilicho fanyika hakikuwa sawa. Una yule binti uliye mkabidhi kitengo cha NSA. Muambie ahakikishe ana tafuta ni wapi Al-Shabab watakapo fanyia mashambulizi yao. Ila kwa mimi kurudi tena kazini siwezi hata mukiniua siwezi kutoa ujuzi wangu, ni heri kufa kuliko kudharualiwa. Kama nime zungumza maneno mabaya nina kuomba uni samehe muheshimiwa raisi”
Mzee Mbogo alizungumza kwa msisitizo na uchungu mkali sana. Viongozi wote wakatazamana na nyuso zao waka zidurisha kwa raisi Mtenzi ambaye amekaa kimya huku mikono iki mtetemeka.
“Ila Mbogo ndugu yangu, hapa tuna angalia taifa na si kumuangalia raisi alifanya vipi. Ita kuwaje wana mama, watoto, wazee wakafa kwenye mashambulizi hayo?”
“Ndio maana kume anzishwa page za kuwasisitiza watu waondoke jiji la Dar es Salaam. Japo sifahamu ni kina nani ambao wame anzisha page hizo. Ila ukweli ni kwamba lengo na nia ya hao watu ni kuwaomba watu wasihudhurie harusi ya mtoto wa muheshimiwa kwani kuna asilimia kubwa kwa Al-Shabab kufanya mashambulizi huko. Hivyo msaada wangu ndio huo nilio wapa wa kuwafafanulia hali halisi inayo kwenda kutokea. Baada ya hapo pambeneni na hali zenu, siku njema”
Mzee Mbogo akakata simu na kila kiongozi aliyopo hapo, akaanza kupata tumbo joto. Kila mmoja akaanza kuiwazia familia yake. Wapo walio tamani kupiga simu hapo hapo kwa familia zao ili waambie waondoke Dar es Salaam, ila kutokana na kumuogopa raisi, ikawabidi kuvumilia wasiwasi unao watafuna kwenye mioyo yao.


“Muheshimiwa tuna subiri maamuzi yako. Tuna fanyaje?”
Mr the Brain alizungumza huku akimtazama raisi Mtenzi.


“Waziri wa mambo ya ndani”
“Ndio muheshimiwa”
“Zungumza na askari wako. Wape maagizo ya kufanya msako nyumba hadi nyumba. Wahakikishe wana wakamata Wasomali wote, awe mwamke, mwanaume au mtoto wa kisomali. Wote wakamatwe na wahojiwe asiye zungumza apigwe risasi afe”
“Sawa muheshimiwa, ila kwenye hilo swala la kuwaua kidogo hapo tuna weza kukiuka haki za kibinadamu muheshimiwa?”
“Nimesema waueni wote. Maswala ya haki za binadamu nita jibu mimi na sio nyinyi ume nielewa?”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa kufoka.


“Ndio mkuu nime kuelewa”
“Wewe mkuu wa majeshi. Hakikisha jiji zima na mipaka yake una mwaga wanajeshi wako. Endapo ata onekana mtu wa kutiliwa shaka, basi hakikisheni kwamba muna waaua”
“Sawa muheshimiwa”
“Mkuu wa mkoa nataka, narudi tena nataka wananchi wote wanao ondoka jijini kisa uvumi wa kimitandao. Wazuiwe na wasiingie ndani ya huu mkoa. Wale walio toka wasiingie ndani ya huu mkoa, ume nielewa?”
“Ndio muheshimiwa nime kuelewa”
“Chinas”
Mr the Brain alimuita raisi Mtenzi jina lake na kuwafanya viongozi wote kumshangaa kwani kumuita raisi jina lake halisi pasipo kutanguliza cheo au heshima yake ni kosa.
“Ume niita kwa ajili ya kukushauri si ndio?”
“Ndio”
“Basi nina kuambia ukweli. Maagizo yote uliyo yatoa kwa hawa viongozi wako yana makosa. Waziri wa mambo ya ndani pekee tu ndio aliye jitahidi kuuliza swali, ila kutokana na ukali wako ata kwenda kuwavisha Polisi wa watu joho la dhambi wazizo husika. Usitake kuigeuza nchi Sodoma na Gomora na Mungu ata tuhukumu kwa moto. Nikiwa kama mshauri wako nina pigana na wewe kwenye kila agizo ulilo wapatia hawa viongozi wako. Sio kila Msomali aliyopo ndani ya nchi yetu ni gaidi na pia na sio kila Mtanzania aliyopo ndani ya hii nchi ni mwema na nchi yake.”
“Acha kunihubiria Brain. Nenda kwenye ushauri wako nini tufanye kama hizo njia hapo una hisi kwamba hazipo sawa”
Raisi Mtenzi alizidi kuzungumza kwa hasira.
“Ushauri wangu ni kwamba. Askari na jeshi, wahakikishe wana pita mtaa kwa mtaa wakiwa na vipimo vyao vya kutafuta mabomu pamoja na mbwa wenye utambuzi wa kunusu mabomu. Hayo mambo ya kuua na kumwaga damu kwa kweli yata iweka nchi katika sifa mbaya na hata hiyo serikali yako haito pendwa.”
“Ni kweli muheshimiwa alicho kizungumza mr brain”
Mkuu wa mkoa alizungumza kwa sauti ya unyonge huku akimtazama raisi Mtenzi.


“Basi kafanyeni hivyo alivyo zungumza bwana Brain na muwe muna nipatia ripoti kila baada ya dakika kumi na tano”
“Sawamuheshimiwa”
Viongozi hao wakatoka ndani hapo huku kila mmoja akiwa na wasiwasi na mashaka makubwa sana juu ya familia yake.


“Mtenzi ni lini uta acha kufanya maamuzi ya hasira?”
“Ndivyo nilivyo”
“Badilika na kama una chindwa uta ipeleka nchi shimoni. Mimi nina ondoka zangu kazi njema”
“Hutaki kuhudhuria harusi ya kijana wangu?”
“Duu ndugu yangu hadi sasa bado una fikiria kuhusiana na ndoa ya kijana wako. Hembu fikiria ni shambulizi gani linalo kwenda kutokea. Kumguka wewe ndio raisi wa hii nchi. Ume nielewa?”
“Sawa”
Bwana the Brain aka nyanyuka, akatembea hadi mlangoni kisha akasimama. Akageuka na kumtazama raisi Mtenzi jinsi alivyo jawa na unyonge mwingi sana. Hali aliyo kuwa nayo raisi hakika ika mtia simanzi na huruma ika mtawala. Ukiachilia kwamba utendaji wao wa kazi wa pamoja, ila ni marafiki wa kipindi kirefu sana, mr the Brain akarudi na kukaa kwenye kiti chake.
“Nilihisi kwamba una weza kumuomba msamaha Mbogo, ili arudi madarakani, ila kumbue huna hata huo mpango”
“Siwezi kumuomba msamaha”
“Kwa nini?”
“Wewe una nijua kwamba siwezi kumuomba mtu msamaha. Mimi ni raisi na ana paswa kuniheshimu?”
“Kumbuka kwamba ukiachilia mbali kwamba wewe ni raisi, ila wewe pia ni binadamu. Unakosea na una paswa kumuomba msamaha kila mtu unaye mkosea”
“Siwezi badilika ndugu yangu. Nilibadilika kidogo tu pale alipo niaombea Sanga, ila kwa sasa siwezi badilika”
“Mmmm haya. Sinto ondoka nita kusaidia kwenye kukushauri kwa maana niki kuacha peke yako, nita shangaa nchi ikianguka hivi hivi”
“Una hofu na uwezo wangu wa kuongoza?”
“Tena sana. Afadhali pale mara ya kwanza nilikuwa nina uhofia kidogo ila kwa sasa, nina uhofia sana tena sana”
Raisi Mtenzi akamtazama mr the Brain kwa macho makali sana kisha akasimama na kutoka ndani ya ofisi hiyo pasipo hata kuaga na kumfanya mr the Brain kutabasamu tu kwa maana ana tambua tayari raisi Mtenzi amesha karisika.


***


“Ulinzi nina ona ni mkali sana huko nje, hivyo tusiwe na wasiwasi wowote”
Nabii Sanga alimuambia ndugu zake na ndugu wa wake zake walio fikia nyumbani kwake kwa ajili ya kushuhudia harusi ya binti yao.


“Shemeji tuna shukuru kwa taarifa kwa maana tulisha jawa na wasiwasi.”
“Ni kweli shemeji, ila muna jua kwamba mambo haya ya kimitandao siku hizi huwa yana tatizo. Kila mtu ana kuwa ana post kile anacho jisikia. Ila musiwe na mashaka kabisa. Muheshimiwa ame nihakikishia usalama wa hali ya juu”
Nabii Sanga aliendelea kuwafariji wageni hao. Mrs Sanga akasimama mara baada ya simu yake kuanza kuitwa, moyo wake uka stuka sana mara baada ya mtu anaye mpigia ikiwa aime andikwa unknown number. Akatoka nje na kusimama eneo ambalo hakuna ambaye ana msikia mazungumzo hayo.
“Haloo”
“Habari yako mrs Sanga”
Sauti mbaya inayo kwaruza kwarudha na nzito ilisikika na kumfanya mrs Sanga kuishusha simu yake kutoka sikioni na kuitazama vizuri namba hiyo.
“Nani wewe?”
Mrs Sanga alizungumza kwa ukali mara baada ya kuirudisha sikioni mwake.
“Natambua hunijiu ila mimi nina kujua. Ume muua Tomas kwa kumchoma sindano ya sumu, machungu ambayo ulinipatia moyoni mwangu hakika siwezi kukuacha uka sherekea sherehe ya huyo msichana wako”
Mrs Sanga akahisi tumbo likimvuruga, akahisi haja kubwa ikimbana kisawa sawa, ila hakuwa na la kufanya zaidi ya kuendelea kumsikiliza.


“Mimi ndio niliye fungua page zote za kuikashifu harusi ya mwanao. Sasa nina kwenda kuiweka video yako ya ngono kwenye kurasa zote. Dunia nzima ita kwenda kuona jinsi ulivyo kuwa una fir** ofisini kwa mume wako. Hahahahaahahaaaaaaaaa”
Sauti hiyo mbaya ilicheka na kumfanya mrs Sanga kutetemeka mwili mzima. Mrs Sanga akajikuta akikaa kwenye kiti kilichopo kwenye moja ya kibanda. Mrs Sanga akamshuhudia mume wake, akija eneo hilo huku akionekana kuwa ni mtu mwenye mashaka.
“Mrs Sanga”
“Be…e.e..e.e..e..e.ee”
Nabii Sanga akaka kiti cha pembeni huku akimtazama mume wake.
“Naona mume wako ame kuja hapo”
Mrs Sanga akazidi kustuka na kuangaza kila eneo la nyumba yao huku akihisi kwamba mtu anaye zungumza naye yupo ndani ya jumba lao.
“Usipate shida ya kunitafuta. Ila nina waona jinsi mulivyo kaa, weka simu yako loud speaker”
Mrs Sanga akaiweka simu yake loud speaker huku mikono yote ikitetemeka.


“Ifikapo saa mbili kamili usiku nina kwenda kuipandisha video hiyo kwenye kurasa sangu zote. Una onaje wakwe zako wakijua kwamba wewe kahaba”
Nabii Sanga kwa haraka akaikwapua simu ya mke wake na kuiweka karibu yake.
“Wewe ni nani ambaye una mtishia mke wangu kirahisi rahisi”
“Hahahahahahaaaaa nabiii Sangaaa. Nawe nina dhambi zako nyingi sana, dhambi za kumf** mwanaume mwenzako Tomas. Isitoshe mke wako aka muuua. Hahahaaaaaaaa nina kwenda kuwadhihirishia dunia kwamba nyinyi sio watumishi wa Mungu bali ni watenda DHAMBI namba moja duniania. Hahahahahaaaahahahahaaaa, subirini na muoneeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee. Hahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa!!!”
Mtu mwenye sauti hilo baya alizungumza huku akicheka kwa dharuau na akaikata simu na kuwacha nabii Sanga na mke wake mapigo yao ya moyo yakiwaenda kasi sana kwani ubaya ni kwamba simu hiyo haijakuja na namba na wala hawajui ni nani aliye wapiga.


ITAENDELEA


Haya sasa hali ime kuwa tetee kwenye familia za pande zote mbili. Familia ya bwana harusi ina hofu na kushambuliwa na AL-Shabab na familia ya bi harusi wa hofo ya video zoa za ngono kurushwa kwenye mitandao ya kijamii ni nini kita tokea? Usikose sehemu ya 109.
 
SIN 109


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188





ILIPOISHIA


“Wewe ni nani ambaye una mtishia mke wangu kirahisi rahisi”
“Hahahahahahaaaaa nabiii Sangaaa. Nawe nina dhambi zako nyingi sana, dhambi za kumf** mwanaume mwenzako Tomas. Isitoshe mke wako aka muuua. Hahahaaaaaaaa nina kwenda kuwadhihirishia dunia kwamba nyinyi sio watumishi wa Mungu bali ni watenda DHAMBI namba moja duniania. Hahahahahaaaahahahahaaaa, subirini na muoneeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee. Hahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa!!!”
Mtu mwenye sauti hilo baya alizungumza huku akicheka kwa dharuau na akaikata simu na kuwacha nabii Sanga na mke wake mapigo yao ya moyo yakiwaenda kasi sana kwani ubaya ni kwamba simu hiyo haijakuja na namba na wala hawajui ni nani aliye wapiga.





ENDELEA


“Mume wangu tuna fanyaje?”
Mrs Sanga aliuliza huku aklengwa lengwa na machozi usoni mwake.


“Sijui mke wangu tuna fanya nini na mbaya zaidi ni kwamba aliye piga ame tumia private number na hatuwezi kumjua.”
“Ehee Mungu ni aibu gani hii inayo kwenda kutukumbuka”
Mrs Sanga alizungumza kwa unyonge mkubwa sana huku akiifikiria aibu atakayo ipata kwa mamioni ya watu walio likes page hizo.


***


Levina akaachi kicheko kikali hukua kigongesheana mkono na Josephine. Mtindo alio utumia wa kutengeneza sauti ya ajabu ambayo hakika ana amini ime mzuzua mrs Sanga na mume wake.


“Hiyo saa mbili uta ziweka video zao kwenye hiyo page?”
Magreth aliuliza kwa upole hukua kiwatazama wezake.
“Kesho kama munavyo jua, mambo yanaweza kuwa sio mambo Dar. Jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba tuna vuna pesa zao kabla mambo hayajawa mabaya”
“Hapo Levina ume nena jambo. Alafu uile mzee ana pesa nyingi sana”
Magreth alitilia msisitizo jambo hilo.
“Kwa hiyo tuna fanyaje?”
“Nina fungua akaunti nje ya nchi.”
“Nchi gani?”
“Canada”
“Una weza kufungua akaunti ukiwa nchi tofauti”
Josephine aliuuliza huku akiwa na mshangao.


“Ndio tuna fungua kwenye mtandao.”
“Basi fanya hivyo”


Levina akaianza kazi hiyo na ndani ya dakika hamsini, akawa amekamilisha taratibu zote za kibeki huku akitumia baadhi ya vitambulisho feki vya Frank ambavyo alikuwa ame mtengenezea.


“Jamani mambo tayari je tuna wachukulia kiasi gani?”
“Mmmm kwa haraka haraka nabii Sanga ana weza kuwa na utajiri wa kiasi gani?”
Josephine aliuliza huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Yule mshenzi ana pesa nyingi sana. Tuwapige dola milioni mia”
“Mmmmm dola milioni 10 kweli si nyingi sana?”
Josephine alizungumza kwa sauti ya upole.
“Awe nazo asiwe nazo lazima atoe. Tena dola milion 15, kila mmoja ana chukua milioni 5, aisee wakizitoa hizo tuna kuwa tupo level nyingine za kimaisha jamani”


Magreth alizungumza kwa msisitizo.


“Kwa hiyo niwapigie tena”
“No watumie kila mmoja video yake kwenye simu yake, si haito onekana namba ehee?”
“Ndio namba haito onekana”
“Sawa fanya hivyo kisha baada ya dakika tano una wapigia”
Levina akamtumia nabii Sanga na mrs Sanga video zao na zote zikaonekana kufunguliwa katika wakati mmoja.
“Naona wata kuwa wana haha sasa hivi”
“Ndio, tuwape muda wa kutazama madhambi yao”
Magreth alizungumza huku akilini mwake akianza kufikiria kiasi hicho cha pesa ambacho ni kikubwa sana.


“Wapigie sasa”
Magreth alizungumza. Levina akaiunganisha simu yake na mfumo ambao una toa sauti mbaya na za kutisha. Simu ya mrs Sanga aikaanza kuita na baada ya sekunde tano ikapokelewa.


“Nina ona mume pata zawadi zenu sasa?”
Levina alizungumz akwa sauti yake ya kawaida, ila kwa upande wa mrs Sanga ana isikia sauti nzito yenye mikwaruzo na ina tisha.
“Ndio tuambie ni nini tuna paswa kufanya Kama una taka pesa zungumza”
“Hahaaaa una hisi pesa zina weza kurudisha uhai wa Tomas?
“Nakuomba unisikilize wewe mtu. Kama una fanya haya mambo kwa ajili ya pesa ni heriuka zungumza, una nielewa. Usitake kutu black mail mimi na mke wangu kwa ajili ya shida zako.”
Nabii Sanga alizungumza kwa sauti kali sana.


“Mzee usiwe jeuri sana kwa maana tuna weza kuishusha hiyo heshima yako uliyo jitengenezea kwa muda mredu ndani ya dakika moja tu tuna iharibu”
“Sawa sawa, sema una hitaji nini?”
“Kabla haijafika saa mbili usiku nina hitaji kwenye akaunti yangu kuwe na kiasi cha dola milioni 15”
“Dola milioni 15?”
“Ndio. Sasa chagua pesa au heshima yako ya mke wako na familia yako kwa ujumla. Kumbuka kuna waumini wako wanao kusujudia na kukuona wewe ni mwema sana, kumbe ni mtu mwenye dhambi kuliko hata mtengeneza dhambi shetani. HahahaaahahHAHA”
Levina alizungumza kwa kujiamini sana kisha akakata sim hiyo.
“Hapo ume wakomesha. Sasa watumie hiyo akaunti namba na jina”
Magreth alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Josephie akafanya kama vile alivyo agizwa na wote wakaka mkao wa kusubiria mamilioni ya pesa ambayo endapo wata yapata basi maisha yao yana kwenda kubadilika kwa asilimia kubwa sana.
***


“Milioni 15 dolar ni nyingi sana mke wangu. Mimi siwezi kuzitoa”
“Mume wangu, heshima tuliyo nayo sio sawa na hiyo pesa. Piga picha hizi video zikiwa mtandaoni una hisi kwamba ni nani ambaye ata kanyaga pale kanisani kwetu”
“Nina waza kitu”
“Kitu gani?”
“Magreth ndio mtu wa pekee amabaye ana hizi video na yeye ndio aliye tuambia kuhusiana na kufa kwa Tomas na yeye ndio mtu wa pekee ambaye ana tishia juu ya hizo video. Nina imani yeye ndio ana fanya huu mchezo”
“Sawa mume wangu. Kama ni yeye je tuna fanyaje, ikiwa hatujui ni wapi alipo na wala hatujui ata fanya nini hiyo saa mbili, ikiwa sasa hivi yame baki maaa sita hadi ifike saa mbili usiku”
“Nita kuambia”
Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza hivyo akanyanyuka na kuondoka eneo hilo na kumuacha mke wake akiwa katika wakati mgumu sana. Nabii Sanga akaingia chumbani kwake huku akiwa amejawa na hasira kali sana. Akilini mwake ana muwazo Magreth ni kwa nini ana msumbua kwa kiasi hichi.


‘Wewe malaya lazima nita kuua’


Nabii Sanga alizungumza huku hasira ikiwa imemtawala kisaswa sawa. Akachukua funguo ya gari lake aina ya Toyota Land Cruiser V8. Akaanza kushuka kwenye gari na akakutana na mtoto wake wa kwanza.


“Baba mbona speed speed wapi tena”
“Kuna swala nina kwenda kulishuhulikia mara moja.”
Nabii Sanga alijibu kwa ufupi kisha akaendelea kushuka kwenye ngazi hizo. Akatoka nje na kuanza kutembea kuelekea kwenye gari lake. Mke wake akamfwata kwa haraka.


“Una kwenda wapi mume wangu?”
“Nina kwenda kwenye mgahawa wa yule malaya na nikimpata hakika nina muu”
“Twende wote”
“Ingia kwenye gari sasa, acha kushangaa shangaa”
Wote wakaingia kwenye gari, kitendo cha nabii Sanga kuwasha gari lake tu, simu yake ikaanza kuita, akaitoa mfukoni na kukuta ni watu wanao wasumbua. Akaipokea na kuweka loud speker.
“Sanga Sanga, una kwenda wapi?”
Sauti hiyo ilizungumza na kumfanya nabii Sanga na mke wake kuanza kuangaza angaza kila eneo la nyumba yao.
“Nina kwenda kukutafutia pesa unazo hitaji?”
“Nyuso zenu zime jaa hasira. Sidhani kama una kwenda kutafuta pesa”
“Kwani wewe una taka tutabasamu ili iweje?”
Nabii Sanga alizungumza kwa kufoka sana.
“Hahaaaaahahaaa nabii Sanga Sanga Sanga, usinifokee kabisa. Haya nenda katafute hizo pesa”
Simu hiyo ikakatwa na kuwafanya nabii Sanga kuzidi kushangaa.


“Huyu mshenzi yupo hapa ndani”
Nabii Sanga akizungumza huku akitazama tazama watu waliopo hapo kwao.
“Ndio hata mimi nina hisi hivyo kwa maana ame juaje kwamba tumeingia ndani ya gari?”
Nabii Sanga akashuka ndani ya gari na kuanza kumtazama ndugu na jamaa walipo eneo hilo. Kila mmoja ana onekana kuwa yupo bize. Nabii Sanga akaingia sebleni na kuwaangalia wageni ila wote wana onekana kuwa bize na mambo yao. Akarudi kwenye gari alipo muacha mke wake.


“Kila mtu namuona yupo bize na mambo yake”
“Hembu twende kwanza kwenye mgahawa wa yule mpuuzi”


Wakaondoka nyumbani hapo na wakafika katika mgahawa na Magreth. Jambo la kushangaza wakakuta mgahwa huyo ukiwa ume fungwa na hakuna mtu hata mmoja.


“Umamini mke wangu kwamba ni Magreth”
“Ndio, kama ingekuwa sio yeye tunge mkuta hapa. Ila ana fanya makosa kisha ana kimbia”
“Tuna fanyaje mke wangu?”
Nabii Sanga aliuliza kwa sauti ya upole huku akiwa amejichokea.


“Tumpatie hizo pesa alafu najua ni jinsi gani ya kuzirudisha”
“Sawa mke wangu, ila dola milioni 15 ni nyingi sana. Hapo tuna zungumzia billions of shilingis baby”
“I know honey. Ila ita tulazimu kulinda heshima yetu. Ona hizi video zikienda hewani ita kuwaje. Kesho tutatazamwa vipi na jamiii. Ukiachilia mbali jamii, je watoto wetu wata tuangalia vipi mume wangu. Tupo kwenye bad position.”


Nabii Sanga akashusha pumzi huku kitafakari kutoa kiasi hicho cha pesa. Japo wana pesa nyingi sana zaidi ya dola million 100 ambazo ni pesa halali, ila kwenye akaunti zao za siri ambazo zina ingiza pesa zipatikanazo na biashara haramu, ni nyingi zaidi ya pesa zao halali.”
“Hili swala kama lingekuwa sio la aibu, ninge mshirikisha raisi”
“Ni kweli, ila hatuwezi kumshirikisha yule ni mkwe wetu laiti akijua sisi tuna tabia kama hizi nina imani ata leta ukinzani katika ndoa ya mtoto wetu”
“Haki ya Mungu kama ingekuwa sio harusi ya binti wetu hakika nisinge toa hii pesa”
“Ndio hivyo mume wangu. Alafu kabla ya kuwapa pesa hizo ina bidi watuhakikishie kwamba wana futa video zetu na hawazitumii kama chanzo cha kutuchafua tena”
“Yaani ukisikia kucheza kamari ndio leo”
Nabii Sanga alizungumza huku akiwasha gari lake na kuondoka eneo hilo.


***


Polisi wakisaidiana na wanajeshi wakazidi kusambazwa mitaani huku wakiwa na vifaa vya kutafuta mabomu pamoja na mbwa walio funzwa uwezo wa kutambua bomu. Msako huo ukazidi kuwashangaza wananchi wengi, kila mmoja alijawa na swali lake ambalo halikuwa na jibu. Msako huo haukuweza kuza matunda yoyote kwa maana wengi wao wana hisi kwamba mabomu hayo ni makubwa au ya kutega kama yaliyo zoeleka. Ripoti ya msako huo ikatolewa kwa waziri wa mambo ya ndani naye akawasiliana raisi Mtenzi na kumueleza hali ya usalama iliyopo ndani ya jiji zima.
“Kwa hiyo hakuna bomu lolote?”
“Ndio muheshimiwa, vijana wangu wamefanya kazi ya mtaa kwa mtaa na hakuna ambaye ameweza kukuta hata kipisi cha bomu”
“Kazi nzui sana waziri kwa hiyo kesho harusi ya vijana wangu iendelee kama kawaida”
“Nina kuhakikishia muheshimiwa ulinzi uta kuwa ni asilimia mia moja. Furaha itawale ndani yako muheshimiwa na kama ni hawa Al-Shabab nina kuhakikishia muheshimiwa, tuta kwenda kuwa bamiza endapo tu wana onyesha nyuso zao”
“Basi kazi nzuri sana.”


“Nashukuru muheshimiwa”
Raisi Mtenzi akakata simu huku akiwa na furaha kubwa sana moyoni mwake. Hofu na mashaka ikamuisha kabisa. Akatoka ofisini kwake na kuelekea katika nyumba anayo ishi ndani ya ikulu hiyo hiyo. Akakuta shamra shamra za maandalizi ya harusi zikiwa zina endelea kama kawaida.


“Baba vipi ume fanikiwa kufahamu ni kina nani wanao eneza upuuzi?”
Jery aliuliza huku akiwa na wasiwasi mkubwa sana.


“Wala usijali katika hilo. Wewe jiandae kesho una chukua mke wako”
“Nashukuru sana baba”
“Usijali mwanangu”
Raisi Mtenzi akamkumbatia kidogo Jery kisha akamfwata mama yake mzazi ambaye ame zeeka sana na akaka pembeni yake na wakanza kuzungumza kilugha.


***


Levina, Magreth na Josephine kila muda macho yao wana yatupia kwenye saa zao. Kila mmoja ana ona saa mbili usiku ni mbali. Kila mmoja wao ameingiwa na tamaa ya utajiri na hakuna hata mmoja wao ambaye ana fikiria umakisikini tena.
“Zime baki dakika ishirini kufika saa mbili na hawajatuma chochote”
Levina alizungumza huku akiwatazama wezake.
“Labda tuwapigie tena na kuwasisitizia”
Josephine alishauri.
“Hapana tusiwapigie endapo wapipo tuma. Ikifika saa mbili kambili Levina uta zipandisha video zao zote kwenye mtandao. Sisi tutakosa pesa na wao wata kosa heshima, na sidhani kama raisi na familia yake akiwaona wakwe wezie ata kubali kuwaozesha”
Magreth alizungumza kwa msisitizo kutokana yeye ndio kiongozi wao hapakuwa na mtu aliye pinga wazo hilo kwani lengo lao la toka mwanzoni ni kuhakikisha kwamba wana ichafua heshima ya nabii Sanga na mkewe.


ITAENDELEA


Haya sasa umesalia muda mchache kabla ya kufika saa mbili kamili usiku na pesa walizo kuwa wana zihitaji hakuja ingia kiasi chochote kwa nini nabii Sanga ame chelewa kutuma pesa hizo, kuna mpango gani ana uwazia? Usikose sehemu ya 110.
 
SIN 110


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188



ILIPOISHIA


“Zime baki dakika ishirini kufika saa mbili na hawajatuma chochote”
Levina alizungumza huku akiwatazama wezake.
“Labda tuwapigie tena na kuwasisitizia”
Josephine alishauri.
“Hapana tusiwapigie endapo wapipo tuma. Ikifika saa mbili kambili Levina uta zipandisha video zao zote kwenye mtandao. Sisi tutakosa pesa na wao wata kosa heshima, na sidhani kama raisi na familia yake akiwaona wakwe wezie ata kubali kuwaozesha”
Magreth alizungumza kwa msisitizo kutokana yeye ndio kiongozi wao hapakuwa na mtu aliye pinga wazo hilo kwani lengo lao la toka mwanzoni ni kuhakikisha kwamba wana ichafua heshima ya nabii Sanga na mkewe.





ENDELEA


Levina akajifikiria kwa sekunde kadha akisha akanyaua simu yake na kumpigia kumpigia nabii Sanga.


“Unwa fanya nini Levina”
Magreth aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.


“Pesa ni muhimu kwetu. Mambo ya heshima zao sisi hayatuhusu ni lini sii tuta kuwa na pesa nyingi ni lini nasi tuta heshimika na kuwa watu wenye hadthi ndani ya hii nchi hii?’


Maswali mfululizo ya Levina yakamfanya Magreth kukaa kimya na kumuacha afanya kile anacho hisi kwamba ni sahihi. Simu ya nabii Sanga ikapokelewa.


“Naamini mume jianda kwa nyeti zenu kuonakena hadhariani”
Levina alizungumza kwa msisitizo.
“Hiyo pesa ipo na tupo kwneye hatua za kuzituma. Ila hatuwezi kuzituma pasipo wewe kutu hakikishia kufuta video hizo kwa maana muna weza kuzitumia siku nyingine kudai pesa, sasa uta uwani mchezo wa kitoto”
Levina akawatazama wezake. Magreth akazungumza bila ya kutoa sauti na Levina akamuambia.


“Nyinyi muna taka tuwadhibitishie vipi kwamba tuna zifuta video hizo?”
“Nina hitaji kuonana nawe ili kama ni kuzifuta basi uta zifuta mbele yangu na mke wangu”
Matakwa ya nabii Sanga yakazidi kumbada Levina, akakosa cha kujibu zaidi ya kuwatazama wezake, Magreth akachukua simu ya Levina na kumfanya Levina kushangaa.


“Saa tisa kamili usiku tukutane katika fukwe za koko beach. Hakikisha una kuja na mke wako enapo uta kuja na mtu zaidi ya mmoja basi viche vyenu kesho ita kuwa ni zawadi za maharusi wenu”
Magreth mara baada ya kuzungumza hivyo akakata simu.


“Tuna rudi Dar es Salaam”
Levina alizungumza huku akichukua funguo ya gari lake juu ya meza.
“Dar!!?”
Josephine alizungumza huku macho yakiwa yamemtoka.
“Ndio hau hamjanisikia”
“Ila Levina Dar si mabomu yana lupika?”
“Munataka pesa au hamtaki pesa?”
Josephine na Levina wakatazamana.


“Tuna taka”
Levina akajibu kwa sauti ya upole.
“Tuondokeni”
Magreth alizungumza hukua kitangulia mlangoni. Levina na Josephine kila mtu akachukua kilicho chake na wakatoka ndani hapo huku wakiwa na wasiwasi na mashakama mengi sana. Wakaingia kwenye gari huku kila mmoja akitamani kumuuliza swali Magreth ila wana hofia kwa maana ana onekana kukasirika.
“Fungeni mikanda kwa maana spidi nitakayo tembea nayo kuna mawili, tuwahi kufika Dar es Salaam au tuwahi kufika mbiguni. Tumeelewana?”
Magreth aliuliza kwa ukali kidogo. Levina akajikuta akihamia siti ya nyuma alipo Josephine, akajifunga mkanda wa siti na safari ikaanza huku Magreth akihakikisha kwamba ana fanya kila liwezekanalo, ana tumia masaa mawili au mawili na nusu kufika Dar es Salaam wakitokea Morogoro.


***
“Nilikuambiaje mke wangu. Hawa watu wana taka pesa na ni lazima wangepiga simu”
Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama mke wake.
“Sasa wana hitaji tukutane koko hiyo saa tisa mume wangu si hatari?”
“Ndio ni hatari, ila ina tubidi tuwaambie vijana wetu. Hatuwezi kwenda sisi kama sisi”
“Sasa vijana ukiwaambia si lazima watatumia njia ya baharini kuja huku. Je ulinzi ulio imarishwa, ita kuwaje mume wangu”
“Ila yupo Tyson acha niwasiliane naye”
“Huyo si alishindwa kumpata Evans je hao watu wengine kwelia ata weza kuwapata?”
“Namuamini Tyson na isitoshe jambo la Evans liliingiliwa na watu ambao hatuwajui”
“Sawa mpigie”
Nabii Sanga akampigia Tyson, simu ikapokelewa.
“Ndio muheshimiwa”
“Upo Dar es Salaam”
“Ndio”
“Kuna kazi, ikiwezekana tuonane muda huu”
“Wapi?”
“Niambie nikufwate”
“Nipo Kimara kwa sasa”
“Sogea hadi Ubungo”
“Sawa mkuu”
Nabii Sanga akakata simu. Wakatoka chumbani kwao na mke wake, wakaingia kwenye gari na kuoandoka, wakafika Ubungo sheli, Tyson akashuka kwenye gari lake na kuingia kwenye gari la nabii Sanga ambalo vioo vyake ni vyeusi kasoro tu kioo cha mbele.
“Habari yako Tyson”
“Salama mkuu, heshima yako. Mama heshima yako”
“Nashukuru”
Mrs Sanga alijibu huku wote wakiwa wame mgeukia nabii Tyson aliye kaa siti ya nyuma.
“Nina imani una mualiko wa harusi ya binti yangu?”
“Ndio mkuu na kesho Mungu bariki ni lazima nifike”
‘Sawa, ila kabla ya kesho kufika, tume pata mtihani kidogo. Kuna watu wana tupigia simu za vitisho wana hitaji pesa nyingi sana na sisi hatuna mpango wa kuwapatia hizo pesa. Wana hitaji tukutane nao koko bichi mida ya saa tisa kamili usiku. Nahitaji ufanye jambo, tuna hitaji udungue huyo mtu na nahitaji kumjua kwa maana ana ifanya siku yangu nzima kuenenda vibaya”
“Sawa mkuu hilo swala lina wezekana. Malipo nina imani kwamba yata kuwa ni makubwa”
“Siwezi kukuangusha kwenye hilo”
“Sawa saa tisa kasoro usiku nita fika pale. Nita jiweka sehemu ambayo sio rahisi kwa huyo mtu kuniona”
“Hakuna shaka tuta onana huo muda”
“Sawa sawa muheshimiwa”
Tyson akashuka kwenye gari hilo, akaingia kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo.
“Kazi ime kwisha mke wangu twende tuka ungane na familia yetu”
Nabii Sanga alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana moyoni mwake. Wakandoka eneo hilo na kurudi nyumbani kwao.


***


“Hakuna hata simu yetu moja iliyo okotwa na askari hivyo kesho mpango wetu upo pale pale. Ifikapo kesho saa tisa kamili alasiri Dar es Salaam yote ita geuja na kuwa tanuri la jehanamu”
Omary alizungumza kwa furaha kwa maana walikuwa wakiufwatilia msako wa wanajeshi pamoja na mbwa wao kuhakikisha wana tafuta kama kuna mabomu yoyote yale yaliyo tegwa ardhini. Omary na wezake usiku huo waka utumia katika kusoma baadhi ya dua za kujikabidhi mikononi mwa mwenyezi Mungu kwani wana amini kwamba jambo wanalo kwenda kulifanya kesho lita kuwa ni jambo la kishujaa na wata kubukwa sana kwenye familia zao miaka na miaka.
Walipo maliza kusoma dua hizo, wakaanza kula vyakula vizuri ambao mwenyeji wao aliwaandalia, ikiwa ndio vyakula vyao vya mwisho mwisho kula wakiwa hai.
“Najua kwamba kesho tuna kwenda kufa si ndio”
“Ndio”
“Mwenyezi Mungu ata tupokea na tuna ingia peponi tukiwana furaha sana”
Omary alizungumza kwa msisitizo huku furaha ikiwa ime mtawala.


“Kesho nina hitaji kila mmoja uso wake uwa na furaha. Kesho ni siku yetu ya ushindi, je tupo pamoja”
“Ndio tupo pamoja”
Vijana hao walishangilia kwa furaha sana kana kwamba kesho wana kwenda kucheza fainali za kombe la dunia.
***


Majira ya saa sita Magreth akasimamisha gari lake mbele ya nyumba amba yake ya Kigamboni. Levina na Josephine wakamshukuru Mungu kwa kufika salama eneo hilo kwa maana spidi aliyo kuwa ana tembea nayo Magreth barabarani hakika haikuwa ya kawaida. Kitu kilicho wasaidia ni foleni ya magari kidogo ndio ime wafanya wasiende mwendo wa kasi sana.
“Levina nahitaji uchukue gari lako. Tuna ondoka hapa”
“Kumbe hatuingii ndani?”
“Kwani kuna kitu cha kuchukua tofauti na gari lako?”
“Hakuna”
“Basi chukua gari lako na tuna elekea nyumba ya kule”
“Sawa”
Levina akashuka kwenye gari, akaingia ndani hapo, moja kwa moja akapitiliza hadi chumbani alicho kuwa naa kaa. Akachukua fungua ya gari lake akatoka nje na kukuta Josephine akiwa tayaria mesha fungua geti kubwa. Levina akaingia kwenye gari lake na kulitoa ndani hapo. Magreth akafunga nyumba yake, kisha wakaondoka eneo hilo. Wakafika katika nyumba iliyopo pembezoni mwa habari na imejitenga na nyumba nyingi.
“Ehee tume rudi Dar tuna mpango gani Mage”
Levina alizungumza huku akifunga mlango wa gari lake.
“Nifwateni”
Magreth alizungumza na wakaingia kwenye banda kubwa la gereji iliyopo nyumbani hapo. Magreth akafunua turubai kubwa lililo ifunika pikipiki yake ambayo ni kubwa.


“Waooo hii pikipiki ni ya nini?”


Josephine alizungumza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana
“Ni yangu na nimpya kabisa”
“Duu hizi pikipiki hivi bongo zimesha ingia?”
“Tanzania nzima tupo watu wawili tu ambao tuna mikili hizi pikipiki. Sasa pointi yangu ni kwamba nina kwenda mimi mwenyewe Coco kwa kutumia hii pikipiki. Nahitaji wewe Levina unisaidie kwenye jambo moja, sihitaji kuitumia sauti yangu hii, je una uwezo wa kuibadilisha sauti yangu na ikawa kama sauti uliyo kuwa una zugumza na hawa viajuza?”
“Sauti kubadilishwa ina wezekana.”
“Kweli?”
“Ndio, kuna mfumo fulani hivi una tumika, na kuna viji plasta vina tumika kubadilisha sauti, huwa una vifunga hapa shingoni. Sasa vipo nyumbani kwangu”
“Sasa hivi ni saa saba kasoro, tuna weza kwenda kuvichuku”
“Hakuna noma”
Wakaingia kwenye gari la Levina na kuondoka nyumbani hapo. Wakafika nyumbani kwa Levina na wakaingia ndani wakiwa na tahadhari kubwa kwani toka Levina aondoke nyumbani kwake hapo leo hii ndio ana rudi. Walipo hakikisha kwamba kuna usalama wa kutosha wakawasha taa za ndani.
“Njooni huku”
Levina alizungumza huku akielekea chumbani kwake. Wakaingia katika chumba hicho, Levina akaminya moja ya batani na kitanda chake kikaanza kusogea pembeni.


“Heee kitanda mbona kina sogea”
Josephine aliuliza kwa mshangao.


“Usishangae”
Levina alijibu huku akiwa amejawa na tabasamu. Mlango wa siri ambao upo chini ya kitanda hicho ukafunguka. Wakaanza kushuka kwenye ngazi na wakaingia katika chumba kilichopo ardhini.
“Karibuni, katika chumba hichi ndipo ninapo fanya kazi zangu za kutengeneza sura za bandia pamoja na mambo mengine mengine kama vyeti vya bandia hati za bandi na kadhalika”
“Ahaa hongera”
Josephine alizungumza kwa furaha sana.
“Magreth ni sauti ya aina gani ambayo una hitaji uwe una zungumza nayo?”
“Nzito yaani kama uliyo kuwa ana isikia nabii Sanga”
“Sawa”
Levina akawasha laptop yake na kumuomba Magreth azungumze neno lolote na akalirekodi, akaanza kuitengeneza sauti hiyo. Mara baada ya kumaliza kuifanya kazi hiyo, akamuwekea Magreth kiji plasta shingoni mwake eneo la koromeo.


“Sema mama”
“Mama”
Magreth na Josephine wakajikuta wakishangaa kwa maana sauti yake ime kuwa nzito.
“Hichi kiplasta ume weka nini?”
“Ni utaalamu, ukikibandua, sauti yako ina rudi kuwa ya kawaida. Ila ukikiacha basi sauti yako ina kuwa nzito.”
“Hapa nahitaji nirushe ndege ndogo isiyo na rubani, ambayo ita kuwa ina kufwatilia kila unapo kwenda”
“Ipo wapi?”
Levina akafunua kitambaa kilicho ifunika ndege hiyo ambayo ni ndogo ila ina urefu wa futi nne.


“Hii ina uwezo wa kuzunguka kila eneo la nchi na nje ya nchi hii na nina weza kuiendesha nikiwa sehemu yoyote ile”
“Ume itengeneza wewe?”
Josephine aliuliza.
“Ndio, nime itengeneza mimi. Pia ina uwezo wa kwenda juu usawa wa ndege hizi kubwa zinapo pita. Kiufupi ni nzuri nime ifanyia majaribio kama mara nne hivi na ime fanya vizuri”
“Hapo rafiki yangu uta kuwa ume nisaidia sana kwa mana ninavyo mjua nabii Sanga ni lazima ata jaribu kutafuta msaada wa pembeni. Endapo ata fanya hivyo, ina bidi unipe taarifa nihakikishe nina anza na hao ambao wana msaidia, kisha baada ya hapo nina dili naye”
Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akiwatazama wezake hao.
“Sasa Mage, je ikiwa hivyo uta muua nabii Sanga na mke wake?”
Swali la Josephine kikamfanya Magreth kujifikiria kwa muda kisha akashusha pumzi na kumtazama Josephine kisha akatingisha kichwa akimaanisha hato fanya hivyo na kuwafanya wezake wamshangae kwa maana kama ni nafasi ya kumuua nabii Sanga na mke ndio hiyo hapo.
ITAENDELEA


Haya sasa kwa nini Magreh ana kataa kumuua nabii Sanga ikiwa leo hii wana kwenda kuonana akiwa na mke wake.? Usikose sehemu ya 111.
 
SIN 111


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188



ILIPOISHIA


“Ndio, nime itengeneza mimi. Pia ina uwezo wa kwenda juu usawa wa ndege hizi kubwa zinapo pita. Kiufupi ni nzuri nime ifanyia majaribio kama mara nne hivi na ime fanya vizuri”
“Hapo rafiki yangu uta kuwa ume nisaidia sana kwa mana ninavyo mjua nabii Sanga ni lazima ata jaribu kutafuta msaada wa pembeni. Endapo ata fanya hivyo, ina bidi unipe taarifa nihakikishe nina anza na hao ambao wana msaidia, kisha baada ya hapo nina dili naye”
Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akiwatazama wezake hao.
“Sasa Mage, je ikiwa hivyo uta muua nabii Sanga na mke wake?”
Swali la Josephine kikamfanya Magreth kujifikiria kwa muda kisha akashusha pumzi na kumtazama Josephine kisha akatingisha kichwa akimaanisha hato fanya hivyo na kuwafanya wezake wamshangae kwa maana kama ni nafasi ya kumuua nabii Sanga na mke ndio hiyo hapo.





ENDELEA


“Kwa nini sasa usiwaue?”
Levina aliuliza kwa mshangao.


“Nataka kuwatesa kwa maumivu ya moyo kama niliyo kuwa nina pitia mimi. Nitakapo ridhika na mateso hayo basi uta kuwa ni wakati wa wao kufa”
Josephine akajikuta akiangua kicheko sana kwa maana jinsi sauti ya Magreth ilivyo badilika hakika ina chekesha.


“Sawa kama ume amua kufanya hivyo kwa maana sisi tuna kusikiliza wewe. Sasa hivi ni saa nane ina kubidi ukaonane naye”
“Ni kweli, tuondokeni”
Levina akasaidia na Josephine kubeba vifaa vyake ambavyo ana amini kwamba vita wasaidia katika kazi hiyo. Wakafika katika nyumba ambayo kwa sasa wana isha. Magreth akaanza kujiandaa na kuivaa nguo yake hiyo inayo mfunika mwili mzima na eneo la machoni line tengenezwa na miwani ngumu ambayo haipitishi risasi yoyote. Miwani hiyo ina uwezo wa kumsaidia Magreth kuona hata kwenye giza nene. Magreth akachukua upanga wake mrefu ambao ume chomekwa kwenye kibebeo chake. Akavaa kibebeo cha upanga huo mgongoni mwake. Cheni yake ndefu yenye kisu kilicho jikunja mbele kidogo akaizungusha kuinoni mwake na kuifunga vizuri. Akabeba silaha ndogo ishirini zenye umbo la nyota.


“Magreth hii ni kifaa cha mawasiliano, kivae sikioni mwako. Tuta kuwa tuna wasiliana na nita kupatia taarifa ya kula kitu ambacho uta pitia sawa”
“Sawa”
Magreth akafungua vizipu vya nguo hiyo na kuivua eneo la kichwani mwake kisha akavaa kifaa hicho na kuirudishia nguo hiyo.


“Hii ndio simu ambayo ina video zao na na namba zao. Hakikisha kwamba una wakabidhi na wana futa wao wenyewe”
“Pesa”
“Mimi nipo online, mukifika pale muta kubaliana muingiziane hicho kiwango cha pesa kisha pesa zikiingia huku uta wapatia hiyo simu wazivute au waende nayo kabisa”
“Hakuna kitu kinacho onyesha kwamba ni wewe ndio mmiliki wa hiyo simu?”
“Hakuna”
“Ila jamani kama wakifiria kwmaba hizo video zita kuwa kwenye simu nyingine ita kuwaje?”
Josephine alitoa wazo hilo na kuwafanya wajifikirie kwa sekunde kadhaa.


“Wata amini hivyo hivyo, hatuna muda wa kujieleza sana kwao”
“Sawa kama ni hivyo”
Magreth akaaingiza simu hiyo mfukoni. Akafungua sanduku lenye vifaa vyake, akachukua bastola moja pamoja na magazine iliyo jaa risasi, akaichomeka magazine hiyo na kuichomeka hiyo kwenye mfukoulipo kwenye paja la mguu wa kushoto. Uzuri wa nguo hiyo ime tengenezwa na viatu vyake maalumu ambavyo vime unganishwa na suruali ya chini.


“Kuwa makini Mage”
Josephine alizungumza kwa sauti ya upole”
“Usijali”
Wakatoka nje, Magreth akapanda kwenye pikipiki yake, Josephine akafungua geti na Magreth akaondoka eneo hilo. Levina akawasha ndege yake hiyo ndogo inayo endeshwa bila rubani, akairukisha hewani na ilipo fika kimo fulani akarudi ndani kwa haraka na kuanza kuiongoza kwa kupitia laptop yake na kila eneo ambalo Magreth ana pita wana liona vizuri kwa maana ndege hiyo ina mfwatilia.


***


Raisi Mtenzi akamimina wyne kidogo kwenye glasi yake na kuanza kunywa taratibu akiwa amekaa eneo la kupumzikia ndani ya ikulu. Jery kutokana na kiweru weru cha ndoa, siku hiyo naye hakupata usingizi kabisa, akatoka chumbani kwake na katika kukatiza katiza akamuona baba yake akishusha mvinyo huo taratibu. Akatembea hadi eneo hilo na kukaa.


“Baba huja lala?”
“Yaa sija lala bado vipi una fanya nini nje usiku huu?”
“Yaani baba hapa akili yangu yote ina muwaza Julieth”
“Haha yule ni wako. Ila una jua hiyo hali yako ina nikumbusha kipindi hicho ambacho nili kuwa nina muoa mama yako. Usiku ule wa kuamkia harusi, kwa kweli sikuweza kupata hata lepe la usingizi”
“Wee!!”
“Haki ya Mungu vile, yaani ile siku nilijikuta nikiwa katika wakati wa kuwaza ita kuwaje kanisani. Ila nina mshukuru Mungu nilimuoa mama yako akiwa bikra kabisa”
“Duuu kwa hiyo mimi na wewe tume pata bahati ya kuoa wana wake bikra?”
“Yaa ni bahati kwa kweli hususani kwenye hii dunia yenu ya sasa iliyo jaa mitandao ya kijamii ya kila aina”
“Ni kweli. Ehee baba nipe experience yako kwenye ndoa ilikuwaje?”
“Mmmm mama yako jambo la kwanza ambalo lime nivutia kweke ni kwamba ana nisikiliza na kunitii. Mwanamke akiwa ana kusikiliza wewe mume ndani na kutii kile unacho zungumza basi huyo ni mwanamke mzuri. Hata kama ata kuwa ana pinga kauli yako basi ana ipinga kwa unyenyekevu ambao akikuambia wewe mwaume kweli una jikuta una kubaliana naye”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa suati ya upole. Akapiga fumba la wyne hiyo.


“Chuku glasi unywe na wewe”
Jery akanyanyuka na kuelekea jikoni, akachukua glasi na kurudi eneo hilo. Baba yake akamiminia kiasi hicho cha wyne na wakaendelea na mazungumzo.


“Kipindi nilipo kuwa nina jiunga na jeshi la polisi, nilikuwa kijana mmoja machachari sana. Nilikuwa nina ruka sarakasi sana kwa hiyo mabinti wengi walinipenda sana pale chuoni. Aisee nili wachinja”
“Hahahaaaa”
Jery alicheka kwa furaha sana kwani toka azaliwe hajawahi kuzungumza na baba yake mazungumzo kama hayo.
“Haki ya Mungu vile, yaani niliwachinja, sema nilikuwa nina akili sana. Sikuwahi kukamatwa hata siku moja na mkufunzi yoyote pale chuoni. Hadi nina maliza na kupewa ajira, nika endelea kuwatafuna hadi nilipo kuja kumpata mam yako na akaniwekea mkazo nisi mle hadi tufunge ndoa, hapo ndipo nilipo weza kuyaelewa maana ya mapenzi na toka nimuoe mama yako sikuwahi kutoka nje ya ndoa yangu”
“Kweli?”
“Haki ya Mungu vile, nami nina kuasia usiruke ruke, magonjwa ni mengi na si una jua kwamba haya jali kama wewe ni mtoto wa raisi au ni dokta”
“Yaa nalitambua”
“Wewe kaa na yule binti, isitoshe ni mzuri na amekamilika kila idara. Ila angalizo moja, asikupande kichwani, endapo uta ona ana dalili fulani ya kukupanda kichwani, mtulize kwa ukali au hata kumtandika makofi mawili matatu. Ila ukisema kwamba uwe mpole na mnyonge mwanamke ata kupanda kichwani”
“Usijali baba nita kuwa kiongozi bora wa familia yangu”
“Sawa, unajua japo kumpiga mwamke sio jambo zuri. Ila kwa hichi kizazi chenu kwa kweli usipo mlamba makofi kadha ana weza kupeleka puta”


“Nime kuelewa baba”
rais akamtazama Jery ambaye ndio mwanaye wa pekee kwani kwenye maisha yake ame bahatika kupata watoto wawili wa kime na mtoto wake wa kwanza alikuwa ni jambazi na akaagiza polisi wake kipindi ni RPC kumuu ili kuli tawanyisha kundi hilo la kihalifu lililo kuwa lina pora magari na mali za watu katika mkoa wa Kagera.
***


Majira ya saa tisa kasoro usiku nabii Sanga na mke wake wakaanza safari ya kuelekea Coco beach. Safari yao haikuwachukua umbali mrefu kwa maana hawapo mbali sana na beach hiyo. Wakafika karibu beach hiyo, nabii Sanga akampigi simu Tyson.


“Vipi sisi ndio tuna karibia”
“Mimi nimesha fika eneo la tukio n anime jitegea sehemu ambayo nina weza kuona kila kitu”
“Sawa hakikisha una mtandika risasi ya mguu, nina imani kwamba hato kuwa na uwezo wa kunikimbia”
“Hakuna shaka muheshimiwa”
Nabii Sanga akakata simu huku akimtazama mke wake usoni. Akaliendesha gari lake taratibu hadi kwenye maegesho ya beach hiyo. Akazima taa za gari hilo na hawakushuka kabisa.
“Mume wangu nahisi kuogopa”
“Usiope mke wangu, huyu mjinga lazima nimuue leo”


“Sawa mume wangu”
Wakaendelea kukaa ndani ya gari huku wakiendelea kuangaza angaza eneo hilo wakisubiria kuonana na mtu aliye ahidi ana naye kufika eneo hilo.


“Punguza mwendo”
Sauti ya Levina ilisikika vizuri kabisa masikioni mwa Magreth ambaye tupo kasi na pikipiki yake hiyo, taratibu Magreth akapunguza mwendo kasi wa pikipiki hiyo.


“Ume ona nini?”
“Ngoja kwanza nivute kwa ukaribu eneo hilo”
Levina alizungumza huku akilivuta eneo zima la coco beach kwa ukaribu kwa kutumia kamera iliyo fungwa kwenye ndege hiyo.


“Hei nime ona mtu”
Levina alizungumza huku akiwa amehamaki.


“Wapi?”
“Eneo la mashariki mwa beach. Tena mtu huyu ana bunduki….Ohooo Mungu wangu, ana onekana ni mdunguaji”
“Okay ngoja nifanye jambo”
Magreth akasimamisha pikipiki yake kwenye moja ya mti ambao upo mbali kido na beach hiyo.


“Umesema kwamba yupo eneogani?”
“Hapo ulipo ni upande wako wa kulia. Songa mbele uta tokea nyuma yake”
“Poa”
Magreth akaanza kukimbia pembezoni mwa barabara. Akamuona Tyson kwa mbali kidogo akiwa amelala kwenye moja ya jiwe kubwa huku bunduki yake akwia ame ielekezea eneo la beach hiyo. Magreth akajibanza kwenye moja ya mti, akatoa simu yake na kumpigia nabii Sanga.
“Upo wapi?”
Sauti ya Magreth alikuwa ni mbaya hadi nabii Sanga akaitazama simu yake mara mbili.
“Tumesha fika beach hapa jitokeze”
“Nime waona”
Magreth akakatasimu na kusubiria kwa sekunde kadhaa. Nabii Sanga kwa haraka akampigia simu Tyson.
“Amesha vika jiandae”
“Sawa mkuu”
Magretha akashuhudia jamaa huyo akishusha simu yake sikioni na kuiweka pembeni huku akiongeza umakini wa kuangalia eneo zima la beach. Magreth akakimbia kwa kasi kabla hajafika eneo la karibi na alipo Tyson, Tyson akageuka kwa haraka kwani hata yeye ana machale ya hali ya juu. Akachomoa bastola yale, ila kabla haja fyatua risasi tayari Magreth alisha rusha teka lililo ipiga basola hiyo pembeni.


Uharaka wa Magreth uka mshangaza sana Tyson ambaye akajipanga kwa kupigana kwa mkono kwa mkono kuhakikisha kwamab ana mkabili mtu huyo aliye valia mavazi ya ajabu.


“Una nafasi ya kuondoka eneo hili na ukamuachia nabii Sanga kisanga chale la sivyo nita kuua”
Sauti nzito na yenye mikwaruzo, ikamshangaza sana Tyson kwani katika ujasusi wake wote hajawahi kukutana na mtu anaye fanania hivyo.
“Una hisi kwamba nina kuogopa?”
Tyson alizungumza huku akijiandaa kufanya shambulizi. Magreth akamtazama Tyson kwa umakini, usimamaji wake kati kupigana akajua kabisa kwamba ana weza kumuhimili.


“Mage una muweza?”
Levina aliuliza huku yeye na Josephine wakifwatilia mtanange huo moja kwa moja kupitia laptop yake. Tyson akaanza kurusha ngumi mfululizo. Magreth akazikwepa ngumi hizo, huku naye akituma makombora ya nguvu ambayo mengi yalimpata Tyson mwilini mwake.
“Nina kupa nafasi ondoka”
“Siwezi kupigwa na kiumbe cha ajabu kama wewe”
Kauli hiyo Tyson ilio jaa dharau ndani yake, ikamfanya Magreth kuchomoa mnyororo wake huo, mrefu, Tyson akiwa katika kushangaa jinsi Magreth anavyo zungusha zungusha myororo huo mkononi mwake, akastukia myororo huo ukizunguka shingoni mwake. Mgreth akamvuta Tyson kwa karibu na kumfanya ajitahidi kutoa myororo huo ila akajikuta akishindwa. Magreth akaivunja shingo ya tyson kwa kutumia mnyororo huo Tyson taratibu akafariki. Magreth akautoa mnyororo huo huku akimtazama Tyson ambaye ame ingilia vita ambayo haimuhusu.


Magreth akapiga hatua mbili mbele kisha akasimama, akautazama mwili wa Tyson, akachomoa upanga wake ambao una kata pande zote mbili. Akakishika kichwa cha Tyson na kukikata na upanga huo, Levina na Josephine wakastuka sana hawakuamini kama Magreth ana roho ya kikatili namna hiyo. Magreth akatazama eneo la fukwe hiyo na akaona gari la nabii Sang na mke wake. Akaanza kukimbia kwa umakini huku mkono wake wa kushoto ukiwa ume bebe kichwa cha Tyson. Alipo fika eneo la karibu la gari hilo, akachomoa nyota nne na kuanza kuzirusha kwenye tairi la moja la mbele na tairi moja la nyuma na kusababisha gari hilo kuanza kupungua upepo hali iliyo wastua sana nabii Sanga na mke wake.


“Nini hicho mume wangu?”
Mrs Sanga aliuliza huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana.
“Nahisi gari lime pata pancha.”
Nabii Sanga alizungumza huku akichomoa bastola yake kiunoni, akaifunga kiwambo cha kuzuia risasi. Gafla wakastukia kioo cha upande wa nabii Sanga kikigongwa kidogongwa, hali ya hofu ikawatawala nabii Sanga na mke wake. Gafla wakamuona mtu aliye valia mavazi meusi yaliyo mfunika hadi uso wake akiwa amesimama upande huo wa nabii Sanga. Magreth akagonga kioo tena, na kuwafanya nabii Sanga na mke wake kuchachawa.
“Mume wangu washa gari tuondoke”
Mrs Sanga alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Nabii Sanga akajaribu kupeleka mkono wake kwenye batani ya kuwashia gari lake, gafla kioo cha upande wa nabii Sanga kikavunjwa na kuwafanya wachanganyikiwe, nabii Sanga akajaribu kufyatua risasi, iliyo tua kifuani mwa Magreth, ila haikuweza kumdhuru Magreth kwani nguo alizo zivaa haziingizi risasi. Magreth kwa haraka akafungua mlango wa gari hilo na kuwafanya nabii Sanga na mke wake kupiga makelele ya woga.
“KIMYA”
Sauti nzito ya Magreth ikawafanya nabii Sanga na mke wake kuacha kupiga kelele na kukaa kimya huku haja ndogo ikaanza kumtoka.


“Muna hisi huyu mtu ana weza kupambana na mimi?”
Magrerth alizungumza huku akikirushia kichwa cha Tyson ndani ya gari na kikatua mapajani mwa mrs Sanga mstuko walio upata wa kukiona kichwa cha Tyson ndani ya gari lao kika mfanya mrs Sanga kuzimia kwani hawakutarajia kama Tyson ambaye walikuwa wame mpa kazi hiyo ame uwawa kikatili namna hiyo.


ITAENDELEA


Haya sasa nabii Sanga na mke wake wamepewa suprize iliyo pelekea mrs Sanga kuzimia je ni kitu gania ambacho Magreth ata wafanya ikiwa walipanga kumuua? Usikose sehemu ya 112.
 
Back
Top Bottom