SIN 107
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
“Nani wewe?”
Sauti nyororo ya kike kidogo ika mstua sana Magreth.
“Aha…mimi nina itwa Magreth naweza kuzungumza na mwenye simu?”
“Mimi ni mke wake hivyo una weza kuniachia maagizo yote nikampatia mume wangu kipenzi Evans”
Maneno ya mwanamke huyo yaka mnyong’onyeza sana Magreth na kujikuta akikata simu huku akiwa amekata tamaa kabisa ya kumpigia Evans. Haikuisha hata dakika mbili, meseji ikaingia kwenye simu yake, akaifungua mseji hiyo kutoka kwa namba ya Evans ambayo ilizidi kumnyong’onyeza Magreth kwa maana hakutaraji kama Evans ana weza kuwa na mke.
ENDELEA
“Mage mbona ume nyong’onyea?”
Levina alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake. Magreth hakujibu kitu chochote zaidi ya kuwa katika hali ya unyonge. Levina akaichukua simu ya Magreth na kuisoma meseji hiyo aliyo tumiwa.
‘Wewe malaya, achana na mume wangu. Kama alikujulisha uondoke Dar sio kwamba ana kupenda, tambua sasa hivi nina mimba ya Evans na nikisha jifungua nina funga naye ndoa hivyo kaa mbali na mume wangu’
“Huyu demu fala kweli”
Levina alizungumza kwa ukali huku akiachia msunyo ambao uka mstua Josephine ambaye ana endelea kuperuzi peruzi kwenye mitandao ya kijamii.
“Kuna nini?”
“Si kuna malaya wa Evan ana mtishia rafiki yetu”
“Ana mtishiaje?”
“Eti ana dai kwamba aache kumsumbua mume wake, hembu soma huo ujinga”
Levina akamrushia Josephine simu hiyo na akainyaka. Akasoma meseji hiyo kisha akamtazama Magreth ambaye ame tulia tuli, mithili ya mtu anaye sikilizia jambo fulani asilo lielewa kwa umakini sana.
“Jose lete hiyo simu”
Josephine akamrushia Levina simu ya Magreth. Levina akapiga tena namba ya Evans na ikapokelewa.
“Wewe malaya si nime kuambia usi mpigie mume wangu. Au una taka nikutafute nikuonyeshee ehee?”
“Sikiliza wewe mseng** uliye poteza muelekeo. Usijaribu kudili na watu usio wajua umeelewa wewe mwehu. Kama una taka tukutafute basi, mimi ndio nitakaye kutafuta na nita shuhulika na wewe. Sasa ole wako utume meseji zako za kijinga nita kuonyesha. Una hisi sisi wakijijini eheee, tumezaliwa Dar es Salaam na tume kulia Dar mbwa wewe”
Levina alizungumza bila hata ya kuwa na kituo. Simu ikakatwa, Levina akapiga tena, ikakata, akarudi kupiga tena na ikakatwa.
“Hii ndio dawa ya kushuhulika na machizi kama hawa”
Levina alizungumza na kumfata Magreth kumtazama tu.
“Lev kumbe una zungumza ehee?”
“Tena hap anime mstai tu kutokana upo wewe mtu wa Mungu, laiti ninge kuwa peke yangu, ninge mchamba huyu hadi ange ona dunia nzima ni chungu. Watu tume vurugwa, tuna mastress yetu na yeye ana tuleteea ujinga, na wewe Mage ujifunzage kujibu, sio kuambiwa hivyo kidogo una pooza kama ume chomwa ganzi bwana”
“Levina hujui ni jinsi hani ninavyo mpenda Evans, hujui ni jinsi gani nilivyo umia”
“Utaumia zaidi na zaidi, kutokana na ujinga wako. Pigania penzi lako acha ujinga wewe, ukikaa na kujifanya una jihisi mnyonge ndivyo utakavyo jikuta mwanaume aunaye mpenda akichukuliwa na uta baki uking’aa ng’aa macho”
Maneno ya Levina kidogo yakampa nguvu Magreth.
“Eti”
“Nyoo eti nini, pigania penzi lako. Isitoshe ana dai kwamba yeye ni mjaumzito na hawajafunga ndoa, ni rahisi sana kumchukua mume wake. Fanya juhudi katika hilo”
“Sawa nisaidie kuitafuta namba ni wapi ilipo”
“Poa”
Levina akaanza kuitafuta namba ya Evans ni wapi ilipo kwa kutumia satelate ila jambo la kushangaza hakuweza kujua ni wapi ilipo na ina onyesha kwamba haijasajiliwa katika mtandao anao utumia.
***
“Wata jaribu kukutafuta, ila sinto hitaji uchanganye mapenzi na mipango yetu tuliyo kuwa nayo hivi sasa”
Jini Maimuna alizungumza huku akimtazama Evans usoni mwake.
“Sawa ila maneno uliyo wajubu nina imani yata muumiza sana”
“Ni heri aumie sasa kuliko kupoteza mipango yako.”
Jini Maimuna alizungumza huku akitazama gorofa linalo jengwa nyumbani hapo kwa kina Evans. Uwepo wa Maimuna katika eneo hakuna mtu mwengine anaye muona zaidi ya Evans yeye mwenyewe.
“Maimuna?”
“Bee”
“Hivi hatuwezi kuwasaidia watu wa Dar es Salama kesho waka ondokana na janga lililopo mbele yao”
“Hatuwezi”
“Kwa nini?”
“Una jua kuna mambo duniani yakitokea, mengina yana kuwa ni mpango wa Mungu na mengine yana kuwa ni mpango wa shetani”
“Kwa hiyo hilo la kesho ni mpango wa Mungu?”
“Hamsini kwa hamsini”
“Una maanisha nini?”
“Raisi wenu aliwatoa watu muhimu ambao walikuwa ni muhimili katika kukiongoza kichwa chake hususani kwenye maamuzi. Hilo linalo kwenda kutokea nia adhabu yake kwa kuwasaliti wezake na kufaya maamuzi ambayo hapo awali alipaswa kuwa mstamilivu”
“Ila kuna msamaha?”
“Msamaha uta patikana baada ya kupata adhabu anayo kwenda kuipata”
“Daa ina niuma sana kwa maana kuna watu ambao wata kufa bila ya hatia?”
“Ni kweli, ila kuna kipindi nchi ina takiwa kutoa kafara, ili mambo mengine yaende na iji jenge vizuri. Hilo linalo kwenda kutokea ni kafara na kuanzia hapo uta pata nguvu”
“Nani?”
“Wewe, uta pata nguvu na uta kuwa na ushawishi ambao hata wala walio kuwa wana kuchukulia poa basi wata kusujudia”
Jini Maimuna alizungumza maneno ambayo yakamfanya Evans kujisikia vizuri moyoni mwake kwani tamaa ya mafanikio ime sha mtawala moyoni mwake na sasa tayari amesha yaonja maisha ya utajiri na hataki kurudi tena kwenye umasikini.
***
“Muheshimiwa bado hatuja fanikiwa kumpata muanzilishi wa page hizo”
Kijana anaye shuhulika na mambo ya kimtandao alizungumza huku akimtazama raisi Mtenzi usoni mwake.
“Mume jaribu kuzi ripoti kwenye kampuni husika hizo page?”
“Ndio, tume jaribu kuwatumia maombi Facebook, Instergram na Twitter ili wazifunge page hizo ila hadi sasa hivi hatuja pokea majibu yoyote na kila dakika wafusi wana zidi kungezeka”
“Sawa, mukijibiwa uta kuja kuniambia. Sawa”
“Sawa muheshimiwa”
Kijana huyo akatoka ofisini hapo. Raisi Mtenzia akampia simu sekretari wake na akaingia ndani hapo.
“Niandalie kikao na mkuu wa mkoa. Meya wa jiji, mkuu wa majeshi pamoja na waziri wa mambo ya ndani. Nina hitaji kuzungumza nao baada ya lisaa moja wawe hapa”
“Sawa muheshimiwa raisi. Alafu mama yupo hapo nje ana hitaji kuonana na wewe”
“Mruhusu aingie”
“Sawa”
Sekretari huyo akatoka, akaingia mrs Mtenzi ambaye uso wake una onyesha kuto kuwa na furaha.
“Mume wangu nina pata simu za usumbufu. Watu wana niuliza kwa habari hizi za kuondoka jijini Dar hadi nina pata hofu”
“Mke wangu usimjibu mtu yoyote juu ya mambo hayo. Tambua kwamba nchi ipo kwenye hali ya usalama na hili ndio jiji letu na ulinzi ni mkali sana”
“Sawa mume wangu. Je hawa wananchi wanao hoji na kuulizana maswali huko kwenye mitandao ya kijamii tuna watuliza vipi?”
“Nchi yetu ni ya kidemokrasia. Kila mtu ana uhuru wa kuzungumza anacho jisikia, ili mradi asienende kinyume sheria za nchi. Jambo la msingi ni wewe kuhakikisha kwamba una tuliza akili na kesho harusi ipo kama kawaida, hakuto kuwa na hata panya wa kukatiza mtaani. Umenielewa mke wangu”
“Sawa mume wangu”
“Njoo”
Mrs Mtenzi akasimama kutoka kwenye kiti alicho kalia na kuzunguka meza ya mume wake na kusimama pembeni yake. Taratibu raisi Mtenzi akasimama na kumshika kiuno mke wake.
“Tambua kwamba mimi ndio raisi. Nina jukumu la kuilinda nchi yangu na watu wake, huwa una jua nikizungumza nina maanisha. Hivyo maneo ya kimtandao yasikuumize kichwa, sawa mama watoto”
“Sawa mume wangu”
Raisi Mtenzi akambusu mke wake mdomoni kisha akamuachia.
“Wewe nenda kazungumze na wageni wetu, nikitoka ofisini nita jumuika nanyi”
“Sawa mume wangu”
“Nina kupenda”
“Nina kupenda pia”
Mrs Mtenzi akambusu mumewe shamvuni kisha akatoka ndani hapo. Akapisha na sekretari mlangoni.
“Muheshimiwa, nimesha wajulisha na wana kuja”
“Sawa wakifika wote waambie nikutane nao kwenye ukumbi namba moja”
“Sawa muheshimiwa”
Raisi Mtenzi akashusha pumzi taratibu, akaichukua simu yake na kuanza kutazama kutazama kurasa ya Intergram ambayo ina wahimiza watu kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam na ndoa ya Jery na Julieth ni haramu. Simu ya mezani ya raisi Jery ikaanza kuita, akaitazama kwa sekunde kadhaa kisha akachukua mkonga wa simu na kuiweka sikioni mwake.
“Halooo”
“Habari muheshimiwa raisi”
“Una hitaji nini The Brain?”
“Natambua kwamba ume nitoa nje ya nafasi ya ushauri. Ila nina imani kwamba una weza kuona ni mambo gani ambayo yana endelea kunywe mtandao si ndio”
“Ndio”
“Hapa nilipo nami nipo kwenye harakati za kuondoka jiji la Dar es Salaam. Ukiachilia mbali kwamba wewe ni raisi au bosi wangu, ila wewe ni rafiki yangu na pia ni mdogo wangu. Nitakueleza ukweli, uwe una penda ua hupendi,ila huu ni ukweli. Hili ambalo una ona lina endelea kwenye mitando ya kijamii, sio jambo la kulipuuzia hata kidogo. Fukua fukua ili uone ni kipi kipo nyuma ya pazia, nina imani kwamba uta kuwa una watafuta waanzilishi wa kurasi hizi kwa ajili ya kuwakamata. Ila jambo moja Chinas, una paswa kuwa na busara, waulize ni kitu gani ambacho kina wafanya wahimize watu kuondoka jiji la Dar es Salaam na endapo uta pata sababu uta jua ni njia gani utatue, ila ukiendelea kuwa mbabe mdogo wangu. Hata mimi sijui ni nini kita tokea, ndio maana nina hamasika na mimi kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam. Nikutakie ndoa njema ya vijana wako”
Simu ikakatwa na kumfanya raisi Mtenzi kuishusha simu hiyo chini taratibu. Jambo hili ambalo hapo awali alilichukulia kama mzaha sasa lina anza kumkaa akilini mwake vizuri. Raisi Mtenzi akampigia simu mr THE Brain.
“Ndio muheshimiwa”
“Nahitaji uje ikulu sasa hivi?”
“Muheshimiwa uta nisamehe kwa maana na mimi nina ondoka Dar es Salaam”
“Tafadhali nina kuomba sana ugahiri hiyo safari nina kuomba uje ikulu sasa hivi”
Mr the Brain akaka kimya kwa sekunde kama thelathini.
“Sawa nina kuja ila nita kaa lisaa moja, kisha nita endelea na safari yangu”
“Nashukuru kwa kuitikia wito wangu”
Raisi Mtenzi akakata simu yake kisha akampigia simu makamu wa raisi ambaye yupo nchini China kwa ziara ya kikazi.
“Habari muheshimiwa”
“Salama, kuna jambo linalo endelea kwenye mitandao ya kijamii. Je ume fanikiwa kuliona?”
“Ndio muheshimiwa, nime jaribu kuomba msaada kwa serikali hii kujaribu kutusaidia kuwapata waanzilishi wa page hizo”
“Wame semaje?”
“Wana lishuhulikia muheshimiwa, ila sija taka kuwaambia kwamba kitengo chetu cha NSA, kina tatizo”
“Kazi nzuri ndugu yangu”
“Watakapo fikia basi nita kujulisha muheshimiwa”
“Sawa sawa”
Sekretari akagonga na raisi Mtenzi akamruhusu kuingia ndani kwa ishara.
“Muheshimiwa wageni wote wamesha fika”
“Sawa twende ila wasiliana na mr the Brain na umuambie aje kwenye ukumbi namba moja”
“Mr the Brain ame rudi kazini?”
“No nime muita kwa ajili ya hili jambo”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Raisi Mtenzi akaingia ndani ya ukumbi huo na kuwafanya viongozi alio waita hapo kusimama kwa heshima. Alipo kaa kwenye kiti chake na yeye akakaa.
“Nime waita hapa wa ajili ya hili swala linalo endelea kwenye mitandao ya kikamii. Wana nchi bado wana hofu kwenye hili, je kuna hata mmoja wenu ambaye ana weza kuwaza au kufikiria ni kitu gani ambacho kita kwenda kutokea?”
“Muheshimiwa kwa upande wangu najaribu kutafuta sababu ya hawa watu au mtu kufungua hizo kurasa, ila nina shindwa kupata jibu la uhakika katika hili.”
Mkuu wa mkoa alizungumza, mlango ukafunguliwa na akaingia mr the brain akawasalimia watu wote, kisha akatafuta kiti na kukaa.
“Nashukuru kwa kuja ndugu yangu”
“Usijali muheshimiwa”
“The Brain swala tunalo jadili ni kuhusiana na hili jambo la wananchi kuhimiza kuondoka jiji la Dar es Salaam nawe ni mmoja wapo ya watu walio kuwa wana ondoka jijini. Tuambie una maoni gani juu ya jambo hili?”
“Muheshimiwa nchi ipo kwenye shambulizi na eneo ambalo lime pangwa kutoka kwa mashambulizi hayo ni jiji la Dar es Salaam”
Mr the Brain alizungumza kwa kujiamini na kuwafanya viongozi wote kustuka.
“Shambulizi gani na nani ambaye ana kwenda kuishambulia nchi?”
“Dakika tano kabla sija ingia hapa ndani, nilikuwa nina zungumza na mr Mbogo uliye mfukuza kwenye kitengo cha NSA. Yeye na timu yake wamesha ondoka jijini Dar es Salaam na ameniambia kwamba kesho kwenye harusi ya mwanao. Kundi la Al-Shabab ambalo uli lishambulia kima kosa wata fanya shambulizi, hivyo muheshimiwa, haijulikani ni wapi na wapi wata shambuli na wala kati yetu hakuna anaye fahamu ni saa ngapi wanavyo shambulia. Kiufupi muheshimiwa, kesho haito kuwa siku nzuri kwako na taifa kwa ujumla”
Maneno ya mr the Brain yaka wafanya viongozi wote macho kuwatoka, huku raisi Mtenzi mapigo ya moyo yakianza kumuenda kasi sana kwani wamebakisha muda mchache sana kabla ya harusi ya kijana wake kufanyika.
ITAENDELEA
Haya sasa raisi Mtenzi ana pata habari ya jiji zima kushambuliwa na muda walio nao ni mchache, je wata fanikiwa kuzuia mashambulizi ya kundi hilo la Al-Shabab? Usikose sehemu ya 108.