SIN 157
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
Jackline akakata simu huku akishuka kitandani.
“Kuna nini?”
“Nina tafutwa na vyombo vya usalama. Sasa sifahamu kwa nini wana nitafuta na sijui wame juaje jina langu hadi kunifwatilia na vyombo hivyo vina onyesha vina tokea hapa Tanzania. Sasa nina potea, kazi yako nita ifata, na wewe tembea kabla hujakamatwa. Tumeelewana mzee?”
“Ndi…ioo….o”
Nabii Sanga alijibu kwa kigugumizi kikali huku akishuka kitandani. Hapakuwa na mtu aliye kumbuka kuoga kwani hawajui ni nini kina fwata. Nabii Sanga akawa wa kwanza kuondoka hotelini hapo kisha akafwatila Jackline kuondoka usiku huo na kwenda anapo pajua yeye mwenyewe ili kujipanga zaidi kwa ajili ya kazi iliyo mleta nchini Tanzania.
ENDELEA
Nabii Sanga hadi ana fika getini kwake majira ya saa kumi usiku, bado yupo kwenye wasiwasi mkubwa sana wakuhisi ana fwatiliwa. Geti likafunguliwa na taratibu akaingia ndani huku akiwa katika mawazo mengi sana, akasimamisha gari lake kwenye maegesho ya hapo nyumbani kwake. Akatazama namba ya Jackline akatamani kumpigia simu ila akashindwa, kuhofia simu yake kudakwa na kuonekana ana husiana na Jackline ambaye wanavyo hisi ni kwamba amesha anza kutafutwa. Nabii Sanga akastuka mara ya kuhisikia kioo cha pembeni ya gari lake kikigongwa, akamuona Julieth ndio anaye gonga, taratibu akafungua lock ya mlango huo na Julieth akaingia.
“Vipi bado huja lala?”
“Yaa nilikuwa nina kusubiria wewe”
“Tena afadhali huja rudi kuna jambo nahitaji kufahamu”
“Jambo gani?”
“Nilikuwa na yule binti ambaye nina hitaji kumpatia kazi ya kumuua makamu wa raisi. Sasa kuna mtu wake amemualeza kwamba data zake zime weza kutazamwa kwenye mtandao na watafutaji wametokea hapa hapa nchini Tanzania. Hembu jaribu kudadisi kuna nini kinacho endelea ndani ya ikulu”
“Usiku huu ndio zime angaliwa?”
“Ndio”
“Kwani kuna mtu ambaye ana fahamu juu ya kuja kwake hapa nchini Tanzania?”
“Hapana ni mimi wewe na yeye?”
“Mmmmm sasa ni nani ambaye amemtazama?”
“Yaani hapa ndio tuna changanyikiwa na mbaya zaidi ni kwamba hao watu walio mtazama ni ngumu sana kuwa hack”
“Ohoo hiyo sasa ni shida nyingine. Kama wata kuwa ni NSA au IKULU basi ni ngumu sana kuingia kwenye database zao na kuhack na kufahamu ni kitu gani kinacho endelea.”
“Ndio maana nime kuambia hembu dadisi na ufahamu ndani ya ikulu. Ujue ni kitu gani kinacho endelea”
Julieth akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akijaribu kuwaza ni nani ambaye anaweza kumuamini ndani ya ikulu hiyo na akampatia mambo yanayo endelea.
“Kuna dogo ana itwa Simoni nime kuwa naye karibu siku hizi mbili tatu. Ngoja nimpigie”
“Fanya hivyo”
Julieth akaitafuta namba ya Samson na kuanza kumpigia.
“Dada habari ya usiku”
“Salama vipi upo ikulu?”
“Ndio nipo ikulu”
“Kuna nini kinacho endelea?”
“Hakuna kitu kinacho endelea mbona”
“Hakuna mtu anaye tafutwa?”
“Ahaa yupo kuna dada mmoja hivi ana itwa Jackline Odinga. Ni mkenya, ana tafutwa na chief staff pamoja na yule dada Magreth”
“Kwa kosa gani?”
“Sija jua kwa kweli?”
“Wame fikia wapi sasa?”
“Hili jambo kwa sasa, NSA ndio wanao shuhulika nalo, kwa sisi hapa limesha toka mikononi mwetu”
“Sawa nashukuru. Usiku mwema”
“Na wewe pia”
Julieth akakata simu huku akimtazama baba kwa maana aliweka loud speaker na nabii Sanga ameweza kusikia kila kitu kilicho zungumzwa.
“NSA endapo wata mkamata huyu binti kila jambo lina weza kuwa wazi”
“Kwani ni msichana ambaye hajiwezi kwenye kujilinda yeye mwenyewe?”
“Ana jiweza na yupo vizuri sana. Ila sijajua ni adhabu gani ambayo NSA wana weza kumpatia hadi akazungumza ukweli”
“Kama vipi wasiliana naye ili aweze kuondoka nchini usiku huu huu. Endapo ata kamatwa basi kila jambo lina weza kuharibika”
“Hapana huu mpango hauwezi kuishia hapa. Nilazima hiyo hadhina tuweze kuipata na lazima tuzigonganishe hizi hichi mbili kwa manufaa yetu binafsi. Jambo la msingi ita nilazimu kuhakikisha nina mkodisha muuaji mwengine wa pili kwa ajili ya kuifanya hiyo kazi”
“Wawili wamuue mtu mmoja?”
“Ndio kama mmoja akikamatwa basi mwengine akaitekeleze hiyo kazi na wasijuane kama wote wana ifanya kazi moja”
“Ila baba hao watu wako una waamini lakini kwa maana kama ni hivi tu wamesha jua kwamba Jackline ana tafutwa. Alafu huwa wana juaje kila kinacho pangwa kutokea”
“Ni Josephine”
“Josephine kivipi?”
“Umesahau kama ana maono ya kuona kila jambo lijalo. Kitu ambacho ana shindwa kukiona ni hii familia yetu na mipango yetu. Kama unavyo jua nguvu ninazo zitumia basi hato weza kuona chochote kwetu”
Julieth akashusha pumzi kwa sekunde kadhaa huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana moyoni mwake.
“Baba yule msichana ina bidi tushuhulike naye la sivyo ata kuja kugundua mimi ndio mvujishaji siri na endapo ata muambia raisi una hisi mimi nita kuwa wapi?”
“Hawezi kuona chochote kwetu”
“Baba ana onyeshwa na Mungu yule”
“Natambua, ila hawezi kuona chochote kwangu”
“Mmmm sawa”
Meseji ikaingia kwenye simu ya Julieth. Akaitazama kwa sekunde kadha.
‘Upo wapi’
Meseji hiyo ya Jery, ikamfanya kumtazama baba yake kwa sekunde kadhaa.
“Nina kwenda kulala, naona Jery ana nitafuta”
“Sawa kuwa makini”
Julieth akashuka kwenye gari hilo na moja kwa moja akelekea chumbani kwake. Akamkuta Jery akiwa amekaa kwenye sofa akimsubiria.
“Ume toka wapi mke wangu?”
“Kuzungumza na baba, ame rudi muda huu”
Julieth alizungumza kwa sauti ya upole. Taratibu Jery akamkalisha Julieth kwenye mapaja yake na kuanza kumtomasa maziwa yake.
“Baby mbona ume sahau ahadi tuliyo panga. Tusubirie mama azikwe”
Julieth alizungumza kwa sauti kimahaba.
“Nina hamu na wewe. Mama amesha kufa hakuna kitakacho badilika mke wangu.”
“Ndio najia hawezi kurudi duninia. Ila tumuheshimu kwa hata kwa hii nafasi yake ya mwisho”
Jery akamtazama Julieth kwa sekunde kadhaa kisha akamnyanyua na kusimama. Hakuzungumza kitu chochote zaidi ya kupanda kitandani na dhahiri moyo wake ume chafukwa na visababu hivyo anavyo vitoa Julieth.
“Baby najua ku……”
“Lala”
Jery alizungumza huku macho yake yakiwa yame tawaliwa na uwekundu ambao ulianza kumshangaza na kumuogopesha Julieth. Taratibu Julieth akavua nguo zake na kujilaza pembeni ya Jery huku akiwa na hofu kubwa sana. Hadi kuna pambazuka kila mtu hakuwa amepata usingizi, Jery akawa wa kwanza kushuka kitandani, moja kwamoja akaelekea bafuni na kujisaidia haja ndogo kisha akaoga na kurudi chumbani.
“Nahitaji kuelekea ikulu. Kama una fwatana na mimi sawa, kama una baki hapa kaa hapa”
“Mume wangu hiyo ndio salamu”
“Za asubuhi”
Jery alizungumza kwa ufupi huku uso wake ukiwa ume kunjiana ndita. Dhahiri ana onyesha kwamba ana hasira ya kile alicho nyimwa jana usiku.
“Mume wangu natambua kwamba nime kukwaza. Ila heshima ya mama ni muhimu”
“Yule ni mama yangu na sio mama yako. Mimi ndio nina uchungu kupita wewe umenielewa. Sasa mambo mengine yasiendelee kisa yeye amekufa. Mbona baba yangu ana fanya kazi za kiserikali kama kawaida, kwa nini asike wiki zote hizo toka mama amekufa akiwa ana lia lia tu eheee. Una nichukuliaje hivi Julieth, yaani usiku una niacha nikiwa nime lala una kwenda kupuyanga huko nje alafu una kuja kunipa porojo kama ulikuwa uan zungumza na baba yako si ndio?”
Jery alizungumza kwa kufoka hadi mishipa ya shingo na mikononi mwake ikanza kuvimba na kuonekana vizuri tu. Julieth kwa kweli hakuweza kuamini kama ipo siku Jery ata kuja kumfokea kiasi hicho.
“Haki ya Mungu mume wangu jana usiku nilikwenda kuzungumza na baba. Muulize”
“Hivi una hisi mimi ni mjinga si ndio. Nisikilize wewe, mimi sio mpumbavu nitoke hapa niende kumuuliza baba mkwe wangu, eti jana ulikuwa una zungumza na mke wangu. Ata nichukuliaje, au una hisi mimi ni mtoto wa mikaa kumi na mbili si ndio”
Jery alizidi kukoroma huku akimsogelea Julieth aliye jikuta akianza kurudi hadi akafika ukutani. Jery akaichukua simu ya Julieth.
“Toa password”
“Baby mambo gani ya kushikiana simu”
“Nimesema toa password?”
Macho ya Jery yalijawa uwekundu mithili ya mtu aliye vuta bangi kwa siku ya kwanza. Julieth mwili mzima ukaanza kumtetemeka, akatoa neno hilo la siri na Jery moja kw amoja akaelekea upande wa simu zilizo pigwa.
“Huyu Samson ndio mume wako ambaye saa tisa usiku una toka hapa na kwenda kuzungumza naye nje si ndio”
“Ohoo Mungu wangu. Samson sio mpenzi wangu mume wangu kuna….kuna”
Julieth alijikuta akishindwa kumalizia sentensi yake kutokana na kujua kwamba endapo ata elezea ni kitu gani ambacho alizungumza na Samson usiku basi ita mlazimu kutoa maelezo marefu na endapo Jery ata mbana kwa maswali basi ataweza kugundua jambo.
“Kuna nini?”
“Ni mfanyakazi wa pale ikuku”
“Kwa hiyo siku hizi umesha anza kuwa na namba za wafanyakazi wa ikulu wa kiume si ndio?”
“Mume wangu, huniamini?”
“Nisikilize Julieth, nilikuoa uwe mke wangu na sikukuoa uwe na urafiki na watu wa ikulu”
“Ila nilikuwa nina muuliza maswala ya kazi tu”
“Saa kumi usiku una muuliza maswala ya kazi. Kwani maasaa yote ulishindwa kumuuliza si ndio, sasa nisikilize kama ni kazi hiyo uliyo pewa na baba yangu. Basi nina kwenda kumuambie akutoea na wiki ijayo tuna ondoka na kuelekea Marekani”
Jery mara baada ya kuzungumza hivyo akairusha simu ya Julieth kitandani. Akamalizia kufunga vifungo vya shati lake vizuri na kutoka ndani hapo huku koti lake la suti akiwa amelishika mkononi. Julieth akajihisi kama dunia ime badilika na kumuendea katika njia ambayo hakuitarajia kuipata. Tabasamu la Jery ambalo kila siku alikuwa ana liona usoni mwake, leo lime potea, tena asubuhi na mapema kabisa. Julieth kwa haraka akatoka nje, kitando cha kutoka akashuhudia gari walailo jia likitoka getini huku likiwa lime baki gari moja la walinzi wa ikuku.
“Hei mume wangu ame ondoka?”
Julieth alimuuliza mmoja wa walinzi.
“Ndio ame ondoka na walinzi kadhaa na wametangulia ikulu. Ametuambia ukimaliza kukaa hapa turudi nawe ikulu”
Julieth akahisi kama kuchanganyikiwa kila neno la kwenda Marekani linavyo mrudia kichwani mwake. Akapandisha gorofani kwa haraka na kugonga chumbani kwa baba yake. Nabii Sanga akafungua mlango huo huku akionekana kujawa na usingizi kwa maana usiku wa jana alikuwa na shuhuli pevu ya kumburudisha Jackline.
“Baba Jery ame ondoka”
“Ame kwenda wapi?”
“Amerudi ikulu, tume gombana asubuhi ya leo”
“Mume gombana? Nini chanzo?”
“Nilimkatalia kufanya chochote na nilimuambia kwamba hadi tusubiri mazishi ya mama yake yaishe. Sasa ndio ame kasirika na amekagua simu yangu na kukuta nina zungumza na Samson na mbaya zaidi ana sema kwamba ata kwenda kumuambia baba yake anitoe kwenye hii kazi na wiki ijayo tuna elekea nchini Marekani kuishi huko”
Nabii Sanga kusikia neno la kuondoka kuelekea nchini Marekani likaumaliza usingizi wote ulio mjaa machoni kwa maana mwanaye huyo ndio kiungo kikubwa sana cha kufanikisha mambo yake machafu huku akijivunia siri nzito za serikali na kuamua kuzibadilisha kama apendavyo yeye.
***
Jery mara baada ya kushuka kwenye gari moja kwa moja akaelekea nyumbani kwao na kumkuta mfanyakazi wa kike anaye safisha ndani hapo akifanya usafi.
“Bab yupo wapi?”
“Yupo ofisini”
Jery akalirusha koti la suti kwenye sofa na kutoka ndani hapo. Akafika ofisini kwa baba yake, hakuhitaji hata kumsalimia sekretari wake na akapitiliza moja kwa moja ofisini na kumkuta raisi Mtenzi akiwa na kikao pamoja na Julieth, Magreth na mr the Brain.
“Baba nahitaji tuzungumze”
Jery alizungumza huku akihema kwa hasira. Raisi Mtenzi akamtazama mwanaye huyo kwa sekunde kadhaa na hali hiyo ya hasira kali aliyo nayo mara ya mwisho kumuona nayo ni kipindi alipo kuwa na umri wa miaka saba.
“Samahani jamani nina omba mutupishe kidogo”
Josephine na wezake wakatoka ofisini hapo na kumuacha Jery na baba yake.
“Vipi mwanangu. Mbona una hasira sana?”
“Huyu mwanamke baba nina hitaji umtoe kwenye nafasi uliyo mpatia”
Raisi Jery macho yakamtoka kwa maana ni suprize hiyo anayo ambiwa.
“Kwa nini nimtoe ikiwa hata wiki moja hajamaliza”
“Baba Julieth ni mke wangu. Mimi ndio mwenye mamlaka naye, nahitaji kuondoka naye na kwenda kuishi Marekani na sihitaji kuishi naye hapa Tanzania”
“Heiii cool down”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti chake. Akamshika Jery mkono na kumkalisha kwenye moja ya sofa kisha na yeye akakaa kwenye sofa la mbele yake huku akimtazama.
“Niambie ni nini ambacho kime tokea hadi ume kuwa hivyo”
Jery akameza fumba la mate huku akisikilizia mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi.
“Endapo ata endelea kuifanya hii kazi baba nita muua siku.”
“Heee!! Kwa nini?”
“Moja ana weka kazi mbele kuliko mimi. Mwanamke gani ambaye toka nimuoe hatujawahi kufanya mapenzi. Mimi nina hamu ya kuwa naye alafu yeye ana niletea stori za mama sijui hadi tumzike. Wewe mbona una fanya kazi zako na hukuwahi kulala ndani na kusema hufanyi kazi kisa mama amekufa ehee?”
Jery alizungumza kwa hasira hadi mwili mzima ukaanza kumtetemeka. Ugonjwa wa hasira ambao hapo awali Jery alikuwa nao sasa, unaanza kumrudia akiwa katika hali ya utu uzima jambo ambalo lilimfanya raisi Jery kuanza kujawa na woga pamoja na wasiwasi.
“Ni lini nita itoa hiyo bikra yake au aliolewa na mimi ili aje kunipumbaza pumbaza. Baba muambie nita muua mimi sitaki ujinga na kuna mjinga mmoja hapa ikulu ana mahusiano naye, jana usiku ame mpigia simu ikiwa ameniacha mimi kitandani nikiwa nime lala, alafu ametoka nje kwenda kuzungumza naye na nina mpigia simu yake ina tumika. Si umalaya huo, saa kumi usiku ana zungumza na nani kwenye simu”
Jery aliendelea kufoka huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Ana itwa nani huyo aliye wasiliana naye saa kumi usiku?”
“Fala mmoja nime kuta ame msave Samson”
“Nita dili na hilo jambo mwanangu. Nenda kalale sawa”
Raisi Jery alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Jery uso wake ulio jaa ndita za hasira.
“Sawa”
Jery akasimama huku akihema kwa jazba akatoka ofisini hapo na moja kwa moja akaelekea nyumbani kwao na kumkuta mfanya kazi akiwa ameinama huku akiweka kitambaa cha mezani vizuri. Kigauni cha mfanyakazi huyo kidogo kwa nyuma kina onyesha mapaja yake yaliyo mfanya Jery kumsogelea na kumshika kiuno chake na kumfanya mwana dada huyo kustuka huku akiruka kwa woga mkubwa sana.
**
ITAENDELEA
Haya sasa, haya sasa Jery ameanza kuumwa na ugonjwa wake wa hasira. Je baba yake ata fanya kama vile alivyo elezwa na mwanaye aweze kumtoa katika kazi Julieth na endapo Julieth akitolewa kwenye hiyo kazi ni nini wata fanya kuipata hadhina hiyo wanayo ihitaji? Usikose sehemu ya 158.