SIN 177
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
Website………………………………………………
www.storyzaeddytz.com
ILIPOISHIA
“Pale ndipo anapo ishi”
Mmoja wa wasichana huyo ambaye mkononi ameishika simu yake hiyo, alionyesha nyumba ya Magreth.
“Vipi signal ina onyesha yupo ndani?”
“Ndio”
“Ina bidi hii kazi tuifanye usiku huu huu na kama kurudi nchini Nigeria, ina bidi turudi usiku huu huu au una semaje?”
“Yaa hatuna muda wa kupotea”
Wasichana hao walishauriana huku kila mmoja akifungua pochi yake. Wakatoa vipande vipande vya bastola zilizo gawanyishwa kisha wakaanza kuziunga kwa uharaka na ndani ya muda mchache wakawa wamesha kamilisha zoezi hilo na wapo tayari kwa ajili ya kuielekea katika nyumba ya Magreth.
ENDELEA
Mwanga wa taa ya gari linalo kuja kwa mbali kidogo likawafanya kuzirudisha bastola zao kwenye pochi zao, huku wakilisindikiza gari hilo kwa macho ambalo, walijikuta wakistuka sana mara baada ya gari hilo la polisi kusimama kwenye geti la nyumba ya Magreth. Wakashuka askari sita wenye bunduki huku wakiwa wamevalia majaketi ya kuzuia risasi. Wasichana hao wakajibanza kwenye moja ya mti na kuendelea kutazama kinacho endelea.
Kengele ya getini ikamfanya Magreth kuichukua simu yake na moja kwa moja kuitazama upande unao rekodi kamera hizo za getini. Akastuka kidogo kuwaona askari hao wakiwa wamesimama hapo, akaingia chumbani kwake, akachukua bastola kisha akarudi sebleni. Akahesabu idadi hiyo ya askari polisi kisha akatoka nje huku bastola yake akiwa ameichomeka kiunoni mwake kwa nyuma.
“Nani?”
Magreth alizungumza huku akisikilizia jibu atakalo pewa na askari hao.
“Sisi ni jeshi la polisi tume agizwa na RPC Karata”
“Kufanya nini?”
“Kuimarisha ulinzi wenu”
Magreth akajifikiria kwa sekunde kadha akisha akafungua geti hilo. Akatazamana na askari huyo kwa sekunde kadha kisha askari huyo akatabasamu.
“Kwa jina nina itwa Emily ni kiongozi wa hichi kikosi hapa. Tume agizwa na RPC Karata kuimarisha ulinzi wa nyumba yenu”
Afande Emily alizungumza huku akimkabidhi Magreth kitambulisho chake cha kazi. Magreth akakipitia kitambulisho hicho kwa sekunde kadhaa kisha akamkabidhi.
“Okay so muna imarisha kwa usiku huu au?”
“Hapana ni jukumu endelelevu hadi pale tutakapo pangiwa mahala pengine, ila tuta kuwa tuna pokezana na askari wengine kila baada ya masaa kumi na mbili”
“Sawa karibuni ndani, naamini muna jua jinsi ya utendaji wenu wa kazi?”
“Ndio”
“Si muna linda eneo la nje ila si hadi ndani?”
“Yaa ni eneo la kuzunguka nyumba yako”
“Okay usiku mwema”
“Nawe pia dada”
Magreth akaingia ndani na kumuacha Emily akipanga vijana wake. Magreth akafunga mlango wa mbele wa kuingilia sebleni, akaichomoa bastola yake na kuiweka mezani kisha akaichukua simu yake na kutafuta RPC Karata.
“Kaka habari ya muda huu”
“Safi Mage aisee vijana wangu wamesha fika hapo nyumbani kwako?”
“Ndio, ila ni suprize kaka, vipi tena?”
“Nimepewa oder na raisi usiku huu wa kutuma vijana hapo kwenu kwa ajili ya kuwalinda”
“Ahaa…sawa sawa. Asante kwa hilo kaka”
“Nashukuru usiku mwema”
“Nawe pia”
Magreth akakata simu hiyo na kushusha pumzi nyingi. Akatembea hadi mlangoni mwa chumba cha Josephine akashika kitasa akajaribu kuusukuma mlango huo ila akasikia jinsi Josephine anavyo sali, hivyo akaona sio muda sahihi kwa yeye kumsumbua rafiki yake huyo.
***
“Tufanyaje”
Pili alimuuliza mwenzake huku wakitazama jinsi askari wanavyo jipanga katika geti la nyumba ya Magreth.
“Hata sijui tufanye nini rafiki yangu.”
Hawa naye alijibu.
“Au tuwashambulie?”
“Hapana hatujui wezetu wamejipanga nini na hatujui ni kwa nini askari wapo eneo hilo. Jambo la msingi, tutafute hoteli tulale na tujipange kwa ajili ya siku nyingine.”
Pili alijibu kwa suai ya upole kwa maana mpango wao ume vurugika. Wakatembea hadi bararaba ya lami, wakakodisha taksi na kumuomba dereva awapeleke kwenye hoteli yenye hadhi ya juu hapo Kigamboni. Moja kwa moja wakafikishwa kwenye moja ya hoteli, wakamlipa dereva taksi kisha wakalipia chumba kimoja katika hoteli hiyo kisha wakakabidhiwa kadi ya kufungulia mlango. Wakaingia kwenye chumba hicho na kuanza kukikagua vizuri, walipo jiridhisha hakina kamera za siri ambazo mara nyingi huwa zina kaa kwenye taa na kwenye kuta, wakaanza kufanya mazungumzo na viongozi wao walipo nchini Nigeria kwa kutumia mfumo wa video kupitia laptop ambayo yao.
“Kwa hiyo mkuu ita tubidi hii kazi ituchukue muda kidogo kwa maana muhusika nina ona amewekewa ulinzi wa askari polisi”
Hawa alizungumza huku akitazamana na mkuu wake huyo.
“Ina maana ana lindwa?”
“Ndio mkuu”
“Nina tambua kwamba mukia askari muta shindwa kutoka kwenye hiyo nchi. Hivyo hakikisheni kwamba muna tumia akili ya kiwango cha hali ya juu kabisa. Tume elewana”
“Ndio mkuu”
“Usiku mwema”
“Tuna shukuru mkuu”
Hawa akakata simu hiyo na kumgeukia Pili aliye simama pembeni yake.
“Hembu jaribu kuangalia detail za huyu binti kama ana safari yoyote, aliyo kata tiketi kupitia mtandao?”
Pili alizungumza na Hawa akainaza kazi hiyo mara moja. Uzuri ni kwamba wote wapo vizuri kwenye mambo tenkonolija. Wakaanza kupitia kwenye mashirika ya ndege moja baadaya jengine.
“Bingo”
Hawa alizungumza huku akijawa na furaha.
“Ume pata?”
“Yes ame booking kwenye ndege ya fly Emiraters na ana safari ya kwenda nchini Nigeria. Aisee ameturahisishia sana”
Pili naye akayatupia macho kwenye laptop hiyo. Akatabasamu mara baada ya kuona jina la Josephine.
“Vipi siti zipo kwenye hiyo ndege?”
“Ndio tuna weza ku booking na sisi”
“Basi fanya hivyo, tuna siku ngapi?”
“Leo na kesho”
“Basi itatuwia uraisi katika kuitekeleza kazi yetu. Huyu tuna mchoma sindano ya usingizi uwana wa ndege na hakuta atakaye fahamu kama tume mteja”
“Je kuna haja ya kuwaeleza wakubwa?”
“Hapana kwa manaa hatuhitaji msaada wao”
“Sawa”
Hawa na Pili wakautumiausiku mzima kuhakikisha wanalisoma jiji lote la Dar es Salaam kupitia googlemap. Walipo jiridhisha na jambo hilo wakapanda kitandani na kulala.
***
“Shikammoo baba ume amkaje??”
Julieth alizungumza na simu yake huku akiendelea kujiandaa kuvaa.
“Salama, nagitaji tuonane asubuhi hiii?”
“Wapi baba?”
“Popote au njoo nyumbani ndio salama zaidi”
“Mmmm sawa ngoja nimuombe mume wangu, kisha nita kujulisha”
“Sawa fanya hivyo”
Julieth akakata simu huku akimtazama Jery.
“Hei baby baba ana omba nikaonane naye kwake asubuhi hii”
“Kuna nini tena?”
“Wala sifahamu mume wangu. Vipi una nikubalie niende?”
“Yaa sina tatizo, je huyo baba yako mkwe vipi?”
“Nita muaga?”
“Sawa fanya hivyo, usije ukaondoka alafu akaanza kulalama, si unajua ukiwa ndani hapo mimi ndio nina mamlaka juu yako, ila ukienda huko ofisini yeye ndio bosi wako”
“Ni kweli”
Julieth akambusu Jery kwenye lipsi zake, kisha akajiandaa haraka haraka kisha akatoka ndani hapo na moja kwa moja akaelekea hadi ofisini kwa raisi Mtenzi, akamuaga juu ya wito huyo aliyo itiwa na baba yake mzazi.
“Sawa msalimie sana mzee mwenzangu”
“Nashukuru”
Julieth akaondoka ikulu hapo na walinzi watatu. Haikuchukua muda mrefu akafika nyumba kwa wazazi wake, akamsalimiia mama yake kisha wakaelekea chumbani kwa baba yake kwa ajili ya mazungumzo hayo ambayo yana onekani ni mazungumzo ya siri sana.
“Ehee tuambie ni kitu gani kinacho endelea ikulu?”
“Hilo ndio mulilo niitia baba?”
“Ndio kwa maana tuna paswa kufahamu, tuna taka kuzipata hizo hadhina haraka iwezekanavyo na isitoshe, kesho kutwa nina safari ya kwenda nchini Nigeria kwa wale wakuu wangu wa mambo. Sasa ina bidi nikifika nipata nizungumze mazungumzo ya kunyooka na si kupindisha pindisha”
“Ni kweli mwangu anacho kizungumza baba yako. Una jua hili swala endapo tuka chelewa chelewa, basi nina tambua kwamba tuta poteza vitu vingi sana”
Julieth akashusha pumzi taratibu huku akiwatazama wazazi wake hao.
“Kwanza kinacho endelea kwa yule Josephine ni kwamba, kudi la Bokoharamu pamoja na Al-Shabab wame tuma wapelelezi wao ambao ni wasichaa kuja kwa ajili ya kumteka Josephine.”
“He kwa nini wata mteka?”
“Sijajua ila Josephine mwenyewe amesema hiyo ndio njia moja wapo ya kuweza kuwajua maadui zao. Sasa baba vipi una husika katika hili?”
“Aku ndio nina isikia habari hiyo kwako”
“Basi hiyo ndio hali halisi inayo endelea ndani ya ikulu. Ila hatujui ni wapi na lini ata tekwa Josephine na inavyo onyesha kuta kuwa na mpango madhubutu wa kumfany Josephine kuweza kujulikana ni wapi anapo pelekewa na watekaji hapo”
“Nina hisi kuna ishi kubwa sana nyuma ya hilo jambo, je una weza kuhisi ni nini kinacho endelea?”
“Hapana, ila kuna mpango wa Wamarekani waliweza kuufanya ili kuwaokoa wanajeshi wao na wakawatuma Makomandoo wanne, ila ile siri Josephine aliweza kuvumbua mbele ya Wamarekani hao na mwishowe wale makomandoo waliuliwa tulishuhudia kwenye tv live hivi huku makamu wa raisi wa Marekani”
“Duuu”
“Ndio, sasa hapo tunashindwa kupata dote kwa maana Marekeni na hao Al-Shabab na Bokoharamu ni vitu viwili tofauti.”
“Ni kweli, labda wame mpenda zaidi, huwezi jua na isitoshe ni makundi mawili yaliyo ungana kwa pamoja”
“Yaa ni kweli baba”
“Sasa mpango wa mimi kwenda Nigeria upo pale pale”
“Una rudi baada ya muda gani?”
“Sija jua, ila hadi hili swala niweze kulishuhulikia kwa maana Josephine hatuwezi kupambana naye kwa njia hizi za kawaida ni lazima kuhakikisha kwamba nina pambana naye kwa kutumia super natural power”
“Sawa baba, ila kuwa makini kwa maana sijui ni vitu gani ambavyo baba mkwe na Josephine wana vipanga wakiwa wao wawili”
“Hakuna shaka nipo makini. Ehee swala la bikra na mume wako lime fikia wapi?”
“Bikra gani?”
Mrs Sanga aliuliza kwa mshangao.
“Mume wake ameweza kujua kwmaba hiyo aliyo kuwa nayo ni bikra feki”
“Mungu wangu ime kuwaje mwangu?”
“Musiwe na hofu mama tumesha yamaliza hayo mambo na mume wangu”
“Una uhakika yame kwisha?”
“Ndio?”
“Baba yake hajui hilo?”
“Hapana hajalitambua hilo”
“Dooo ame jauje ikiwa yule dokta wa alisisitiza kwmaba bikra hiyo haina tofauti kabisa na bikra original?”
“Mume wangu ni daktari mama hivyo vitu kama hivyo nina hisi wana visoma huko Marekenia”
“Duu, ume niogopesha mwanangu. Una jua kutoka kwenye familia hile kabla ya mipango haijakamilika ni swala zito”
“Ndio hivyo mama”
“Alafu Julieth nilipokea simu kutoka Ujerumani yale malori yako yamesha fika bandarini, sasa sijajua kama uta yatoa au kuyaacha hapo bandarini”
“Hilo swala la hiyo kampuni kwa sasa niwe muwazi sinto kuwa na muda wa kulisimamia, labda nizungumze na mume wangu”
“Jaribu kumshirikisha kwa maana mumesha kuwa mwili mmoja”
Mrs Sanga alishauri.
“Sawa nitaongea na yeye. Kuna jengine jamani kwa maana kukaa mbali na ikulu ndio kukosa mengi”
“Hakuna jengine?”
Julieth akaagana na wazazi wake kisha akarudi ikulu.
***
“Ume kuja kufanyaje Jery asubuhi yote hii?”
Shani alimuuliza Jery aliye simama mkangoni mwa nyumba anayo ishi.
“Nina hitaji kuzungumza na wewe”
Jery alizungumza huku akiingia ndani. Shani hakuwa na uwezo wa kumzuia zaidi ya kumkubalia kwa maana siku hiyo hajakwenda kazini.
“Una kunywa nini?”
“Niandalie kahawa”
“Sawa”
Shani akaondoka sebleni na kumuacha Jery akitazama vitu vilivyopo ndani hapo. Jery akachukua moja ya picha iliyopo juu ya meza ya tv. Akaitazama kwa sekunde kadha akisha akairudishia hapo. Simu yake ikaanza kuita, akaitoa mfukoni na kukuta ni Julieth ndio anaye piga. Akaipoke na kuiweka sikioni mwake.
“Honey, ndio nipo njiani nina rudi ikulu”
“Ahaa ume shama maliza kuzungumza na wazazi?”
“Ndio tume maliza.”
“Sawa, sasa mimi nime toka mara moja kuna mambo ambayo nime kuja kuyafwatailia”
“Sawa mume wangu hakuna shaka, kuwa makini”
“Nashukuru”
“Nakupenda sana mume wangu”
“Nina kupenda pia”
Shani aliweza kuyasikia mameno hayo ya Jery ambayo kidogo yakauumiza moyo wake kwa maana bado moyo wake una mpenda sana Jery.
“Ni wife”
Jery alijitetea huku akiirudisha simu yake mfukoni mwake na kukaa kwenye sofa. Shani akaweka kikombe hicho cha kahawa mezani, akamimina maji ya moto kutoka kwenye chupa ya chai kisha akachanganya na unga wa kahawa hiyo, akakoroga kidogo, kisha akaonja ikiwa kama ishara ya kumdhibitishia Jery kwamba hakuna sumu yoyote.
“Mimi sio raisi uka hisi kila kitu ninacho paswa kula lazima kionywe”
“Hahaa, nimesha zoea hivyo na isitoshe wewe ni mwanaye kwa hiyo lolote litakalo tokea, mimi ndio nita husika mojak wa moja”
“Sawa, sogea hapa”
Jery alizungumza huku akimvuta Shani karibu yake. Mkono wake mmoja akaupitiasha kiunoni mwa Shani na kuanza kumtomasa kiuno hicho kilicho jaa shanga.
“Jery stop it”
Shani alizungumza huku akiutoa mkono huo wa Jery kwa maana akiendelea kumtomasa huko ana weza kupandwa na ashiki na kujikuta wakifanya mapenzi.
“Nikuulize swali?”
“Ndio”
“Una nipenda?”
“Ndio Jery nina kupenda, ila umesha wahiwa na baba yako alisha niambia kwamba niachane na wewe. Kusema kweli nina kuogopa sana Jery na hata kuja kwako hapa nimepoteza amani kabisa”
“Hayo ya baba wewe achana nayo. Kitu nilicho kuwa nina hitaji kukijua ni hicho tu kwamba una nipenda au laa. Sasa nina ombi moja kwako”
“Ombi gani?”
“Nina hitaji unizalie mtoto haraka iwezekanavyo. Endapo uta fanya hivyo basi nita kuwa nipo tayari hata kuivunja ndoa yangu kwa ajili ya familia yangu hiyo mpya”
Maneno ya Jery yakamfanya Shani kutokwa na macho. Taratibu akanyanyuka kwenye sofa hilo huku uso wake ukiwa umejaa mikunjo ya hasira jambo ambalo lilimshangaza Jery.
****************************************************************************************************************
****
ITAENDELEA
Haya sasa, Kwa nini Shania mekasirika mara baada ya kuambiwa maneno hayo, je ata mkubalia Jery ombi hilo au ata likataa kwa kumuhofia raisi Mtenzi?. Usikose sehemu ya 178.