Riwaya: To the End (Mpaka Mwisho)

Riwaya: To the End (Mpaka Mwisho)

SEHEMU YA KUMI: SPECTRE

To the end (mpaka mwisho) 11

Tariq Haji

0624065911

Baada ya roboti hilo kushushwa uwanjani, milango ikafungwa pamoja na ngao maalum zilizotengenezwa kwa nguvu ya sumaku (electromagnetic force field "EMFF"). Lengo la EMFF kuzuia mawimbi makali yenye madhara yatakayosababishwa na shughuli za mashine hiyo.

Mzee Rozalive na wengine wakapanda sehemu iliyokuwa juu na kukaa eneo ambalo lilitumika kuangalia majaribio hayo. Siyo wao tu, hata baadhi ya wafanyakazi wengine nao walikaa maeneo kama hayo wakitaka kushuhudia labda miujiza ingetokea. Maana wao walijaribu mbinu zote lakini Spectre hakuinua hata kidole.

"Kuna mtu anataka kujiaibisha leo"

"Hahaha, halafu nimesikia ni bwana mdogo hata bado unyevunyevu nyuma ya masikio yake haujakauka" "Fufu watu wengine hawajui kipi bora kwao"

Baadhi ya waangaliaji walikuwa wakinong'ona, hakuna alietaka kuamini kama roboti lililolala katika eneo hilo kwa miaka karibia mia na hamsini bila kuinua hata kidole kama lingetikisika.

Dakika tano, kumi, kumi na tano, bado kimya.

"Ah, hili pande la chuma labda lishakufa" aliongea profesa Bagani. Watu wote walikuwa kimya wakiliangalia roboti lililosimama uwanja bila hata kutikisika. Na kuna baadhi wakawa tayari wameanza kuonesha dharau.

Fwoooosh!!

Vitu kama maji vikatoka kwenye maungio ya Spectre, ukafuata mvuke mwingi mweupe. Watu wote wakatoa macho, hata wale ambao tayari walishaanza kuondoka wakasimama na kugeuka.

Vruuum!!!

Mashine ikanguruma na kusababisha mtetemeko ulisikika mpaka kwa waangaliaji, taratibu vyuma vya nje vya Spectre vikaanza kutikisika na kujipanga sehemu zake. Watu wakazidi kushangaa, roboti iliyolala miaka mia na hamsini imeamka mbele yao.

"Karibu, tafadhali ingiza jina lako" sautu ikasikika masikioni mwa Baston.

"Baston" alijibu.

"Karibu Baston", ghafla kiza kilichokuwa kimemzunguka baston kikatoweka na kujikuta amesimama katika eneo kubwa. Moja kwa moja alitambua kuwa eneo hilo liliitwa Emerald. Mbeke yake alikuwa mwanamke aliekuwa katika kombat ya jeshi "Spectre" aliita Baston.

Hakujibiwa ila mwanamkw huyo akapotea na baada ya hapo Baston akaona eneo kubwa. Ulikuwa ni uwanja ambao Spectre alikuwa amesimama. Tayari Baston na Spectre walishaungana na kuwa kitu kimoja.

"Kila kitu kimekamilika" alisikia tena sauti.

Baston akaanza kunyoosha viungo, na wakati huwo Spectre akaanza kunyoosha viungo.

Kah! Kah!

Sauti za vyuma zikasikika, sehemu ya mabega chuma kikafunguka. Bomba mbili zenye urefu wa mita moja zikatokea kila upande. Visu virefu vikachomoza chini ya viganja, pande zote mbili za kiuno kukafunguka zikaonekana bastola mbili.

Sehemu ya nyuma chini ya mgongo, kukikuwa na chuma kikichochongwa kama pochi. Kikafunguka, ikaonekana mipini mili meusi. Sehemu ya magoti nayo ikafunguka, vikaonekana vitu vyenye ncha kali. Wakati Baston alikuwa akiangalia silaha zote za Spectre. Akastaajabu sana, ni kweli katika kumbukumbu alizozirithi kwa Gilbot, Spectre alitajwa lakini hakukuwa na maelezo mengi sana.

Wakati huu ndio Baston akafahnu kuwa Spectre alitengezwa kwa kazi moja tu. Nayo ilikuwa ni kufanya mauaji, pia ikamfunukia kichwani kuwa Spectre alitengenezwa makhususi kwa ajili ya kamanda Dalia. Maana kila kiungo cha roboti huyo kilikuwa ni silaha ya mauaji.

Fwoooosh!!!

Sehemu ya pembeni ya kichwa karibu na masikio, pakafunguka na maji mengi yakatoka na kusababisha roboti zima kurowa. Baada ya sekunde chache mapovu yakaonekana yakijitemgeza katika mwili wa Spectre na baada dakika tatu mwili mzima ukawa umefunikwa na mapovu.

Maji yakatoka tena na povu lote likasafishwa kisha mvuke ukafuate na sekunde chache tu maji yakakauka. Sehemu ya kifua upande wa kushoto chini ya sehemu ilipoingua almasi ya damu kukafunguka, na chuma kidogo kikasogea mbeke. "Spectre" ndio lilisomeka katika chuma hicho.

Spectre alikuwa mweusi tii, weusi ambao haukung'ara ulipopigwa na jua bali ulinyonya mwanga wote uliotua katika chuma hicho na kukifanya kizidi kuwa cheusi.

Mashine ikazidi kunguruma na baada ya dakika mbili mngurumo wote ukapotea. Akaanza kutembea na kadri sekunde zilivyochanika ndivyo kasi ilivyoongezeka na mwisho akaanza kukimbia. Mara kadhaa alitikisika na kufannya miondoka ambayo ambayo haikuwa rahisi kwa roboti kufanya.

"Mungu wangu, lile roboti au binadamu" aliongea mtu mmoja akishika kichwa chake. Ila hakuna aliemsikia hata mmoja kila mtu alikuwa amepigwa na bumbuwazi la aina yake.

Ghafla Spectre akabiringitia na kutoa bastola, akafanya shambulizia na papo hapo akariudisha kupeleka mikono yake. Ile sehemu ya vusu ikafunguka, akatoa visu viwili na kushika kila kimoja katika mkono mmoja.

Akafanya mashambulizi ya kasi kama matano hivi akavizungusha na kuvirudisha katika pochi yake. Akarusha ngumi kadhaa kwa kasi mno, wengi hawakuona ila kwa wale wenye macho makali walishuhudia vitu vye ncha kali vikitoka pale ngumi zilipofika mwisho na kurudi mkono uliporudi nyuma.

Akazunguka mara kadhaa na kuachia mateke ambayo haya kuwa rahisi kwa roboti kufanya. Ila mateke hayo hayakuwa yakawaida tu. Kulikuwa visu vikali vilivyokuwepo kwenye visigino na vidole vya miguu.

Baada majaribio yote kukamilika, Spectre akasimama na moshi laini ukaonekana ukitoka katika mwili wa chuma hicho. Kwa wataalamu na magwiji wa vita waliokuwepo eneo hilo katika vichwa vyao kulikuwa na sentensi moja tu. "Kila pigo lilitoka kwa Spectre lilitoka na maana moja tu, kuuwa"

Walikuwa sahihi kwa asilimia thamanini lakini kiti ambacho hawakukifahamu. Spectre hakuwa tu roboti wa kufanya mauwaji bali mauaji ya halaiki. Spectre ilikuwa ni mashine iliyotengenezwa kuwa muwindaji. Hata baadhi ya Zestra wa ngazi za juu waliifahamu kazi ya Spectre. Kwao alikuwa ni shetani shuwaini asiye na huruma hata kidogo.

Baada ya nusu saa mashine ya kubebea roboti ikafika na kulibeba Spectre. Likarudishwa ndani, sehemu ya kifua ikafunguka. Baston akatoka akiwa karowa jasho mwili mzima, mwili wake wote ulikuwa umetutumka. Misuli ilikuwa imevimba na kufanya nguo aliyovaa kugandana na mwili kisawasawa.

Alipokanyaga tu ardhi akayumbayumba almanusura aanguke. Mishipa ya kichwa ilikuwa imevimba na kutweta kama mapigo ya moyo.

"Mbona umechoka sana" aliuliza profesa Bagani.

"Ngoja nipumzike kwanza nitaeleza kila kitu" aliongea

Baston kwa tabu vifuniko vya macho vikawa visito na hatimae akapoteza fahamu. Mzee Rozaliv akaita watu na kuwaagiza wampeleke chumba cha mapumziko.

Karibia wote walikuwa na maswali kedekede lakini hakukuwa na kuwapa majibu. Ni kweli kuna wakati marubani hupoteza fahamu baada ya kuendesha roboti. Ila hali hiyo huwa inakuja baada ya matumizi muda mrefu zaidi ya saa tatu. Lakini kwa Baston ilikuwa ni ajabu. Kwasababu yeye alikuwa katika roboti hilo kwa saa moja tu.

Hata hivyo hawakuwa na namna zaidi ya kumsubiri Baston aamke ndio wapate majibu. Kila mwenye swali alilieka swali lake pembeni na kuangalia mkanda (video) ya majaribio ya Spectre. Jopo la wataalamu lilikuwa limekusanyika katika ukumbi mdogo wakidadavua kila sekunde ya video hiyo.
 
To the end (mpaka mwisho) 12

Tariq Haji

0624065911

Saa mbili baadae.

Anaingia mtu katika ukumbi ambao wataalamu walikuwa wakiidadavua video ya majaribio ya Baston. Akaenda moja kwa moja mpaka alipo mzee Rozaliv na kumnong'oneza jambo. Baadaa ya kubalisha maneno mawili matatu, yule bwana aliefika akaondoka.

"Jamani Baston ameamka tayari, tusubiri dakika chache atakuja" aliongea kwa sauti ya wastan lakini kila mtu alisikia ndani humo. Dakika saba baadae mlango ukafunguliwa, Baston akaingia. Bado sura yake ilikuwa imepauka na uchovu ulidhihiri usoni mwake.

Wataalamu wote walikuwa wakimuangalia kama mbwa alieona mfupa. Kila mtu alikuwa na maswali kedekede na alihitaji majibu.

Baston akatembea mpaka mbele kabisa na kupanda jukwaani. Akavaa kama kidude kirefu kidogo sikioni na kukohoa kuhakikisha kilikuwa kinafanya kazi vyema.

"Habari za saa hizi, najua mlikuwa mnasubiri kwa hamu kutaka kujua nini kimetokea. Hivyo nitapokea maswaki mawili tu kwa kila mtu na si zaidi, bado nahitaji kupumzika" aliongea.

"Mimi ndio nitakuwa naongoza, ukiwa unaswali lolote tafadhali bonyeza kitufe kilichokuwa mbele yako" aliongea mzee Rozaliv na karibia watu wote wakabonyeza.

"Kwa waliobonyeza wataanza kuuliza, mpaka pale watakapokwisha watabonyeza wingine. Kumbukeni maswali ni mawili tu kama alivyosema Baston, hivyo kuwa makini na kile unachotaka kujua na sio kila swali" aliendelea. Akabonyeza sehemu katika meza yake na taa ikawaka eneo alilopo mtu mtaalamu mmoja.

"Ahsante, kwa ninavyofahamu ni kwamba karibia marubani wengi wamejaribu kuliendesha Spectre lakini bila mafanikio. Wewe umewaje?" aliuliza mtu huyo.

"Kwanza ifahamike kuwa marubani wengi wanaendesha maroboti ambayo hayana neurolink. Kuendesha kwao hakuna tofauti na mtu anayeendesha chombo cha usafiri" japo kauli hiyo iliwakera wengi lakini hakuna aliefungua mdomo.

Akaendelea "ili kuweza kuendesha Spectre ni lazima mtu atimiza mambo matatu. Moja awe na mwili madhubuti, mbili awe na uwezo wa kunyonya utherium usiopungua daraja B na tatu awe na akili madhubuti".

"Tunajua na kufahamu kwamba hakuna uhusiano wowote kati ya mwili, akili na utumiaji mashuhuri wa roboti, unachokisema hakileti maana, tufafanulie" aliuongea alieuliza swali.

"Spectre ni roboti kale zaidi ya miaka mia na hamsini nyuma, huenda ikawa lina miaka zaidi ya mia tatu. Teknolojia ya wakati ule ni tofauti na sasa. Kipindi cha sasa wengi tumezaliwa tukiwa tayari na uwezo wa kunyonya itheriuma lakini nyakati za kale binadamu walipitia majaribio mbali pamoja uhandisi wa kijenetiki kuhakikisha wanapata uwezo wa kunyonya nguvu asili ili kuweza kutumia roboti"

"Hivyo iliwabidi wengi wawe na mwili shupavu, madhubuti na mkakamavu kuweza kuhimili mikiki mikiki ya utumiaji wa maroboti, ila kwa sasa kinachoangaliwa ni uwezo wa mtu kuweza kuhifadhi na kunyonya itherium", hata kama muulizaji hakuridhika na majibu ila hakuwa na uwezo wa kuuliza swali jingine.

Mzee Rozaliv akabonyeza kitufe kingine iki kumpa nafasi muulizaji mwingine aulize maswali yake.

"Ahsante, katika maelezo yako ya mwanzo umesema ili rubani aweze kutumia Spectre ni lazima atimize mambo matatu. Unaweza kufafanua kwa kina?"

"Moja, mwili madhubuti. Nikiwa na maana awe na mwili usiopungua daraja B. Kutokana na mfumo aliotengenezewa Spectre, mtu yeyote mwenye uwezo wa kunyanyua chini ya kilogramu mia tano hatoweza kumudu kuendesha Spectre. Mfumo wa Spectre hauna msaada mkubwa kutoka AI ( artificial intelligence) tofauti na mifumo ya sasa ambayo kwa kiwango kikubwa rubani anasaidiwa na programu hiyo"

"What???"

Minong'ono ya hapa na pale ikazuka, kwa ufahamu wa kawaida ni kwamba mfumo wa kutumia vitufe katika riboti umekuja kuweka wepesi katika matumizi. Kwasababu rubanibakibonyeza tu sehemu basi roboti atainua mkonk au mguu. Na pia uwepo wa usukani umerahisisha katika kona, kuzunguka na kufanya miondoka mbali mbali na ndio maana kigezo cha mwili shupavu kikaondolewa.

Lakini kwa roboti za awali zote ilikuwa tofauti, kwasababu rubani aliunganisha ufahamu wake na kwenye mfumo wa ufahamu wa roboti. Hivyo kuifanya mashine hiyo kuwa kama mwili wake. Amri zote zilitoka moja kwa moja akilini mwake na roboti ilizifanya kama mwili wake. Hivyo ilikuwa ni lazima mtu awe na nguvu sana kufanikisha amri hizo.

"Mbili, akili komavu. Wataalamu waliipa jina la Battle Oriented Mind (BOM), akili ambayo inawaza vita na jinsi ya kushinda vita hiyo. Hiyo ilitokana na sababu ya kuwa, baada ya rubani kuingia vitani alitakiwa kudadavua na kupiga hesabu mwenyewe jinsi ya kushinda vita au kurudi salama ikiwa vita atashindwa"

"Tatu ni kuhusu itherium, hilo natumai nyote mnalifahamu kadri daraja linavyokuwa juu ndio bora zaidi", maswali yaliendelea huku Baston akijitahidi kujibu kadri ya uwezo wake. Ila mengi aliyajibuu kwa juu juu kwasababu kulikuwa na siri nyingi ambazo zilikuwa hajulikani. Ila wapo ambao wanazijua na hawako tayari mtu mwingine ajue, hivyo angehatariaha maisha yake.

Maswali na majibu yaliendelea kwa saa tatu na mwishoe kikao kikafikia tamati. Kutokea hapo kila atadadavua kwa vile alivyoelewa. Baston akaachana nao na kutoka ukumbini hapo, nyuma yake alifuata Malik na mzee Rozaliv akisukuma kiti cha mwanae.

"Baston, Shanequeen amenambia umehamia rasmi ukuta namba mbili. Ushapata sehemu ya kukaa?" aliuliza mzee

Rozaliv.

"Bado, ndio nimekusudia nikitoka hapa nikatafute"

"Kuna nyumba ndogo niliijenga muda mrefu sana ila kwasasa haina mtu, unaweza kwenda kukaa pale. Chukulia kama hiyo ni zawadi yangu kwa msaada ulompatia mwanangu" aliongea mzee Rozaliv akimrushia funguo. Ilikuwa ni kitendo cha ghafla na bila kufikiria Baston akaidaka.

"Ila... " alitaka kuongea jambo ila macho yake yalipokutana na Shanequeen akalimeza jambo hilo na kutabasamu.

"Nashukuru sana, Malik na wewe si ubakie huku huku" aliongea Baston.

"Kuna mambo mawili matatu ya kuongea na mzee Rozaliv, nitakutafuta baada ya kumaliza" aliongea Malik. Baston hakuwa na la kusema zaidi, akaagana nao na kutoka nje ya jengo hilo. Tayari gari ilikuwa ishaandaliwa, akapanda na kuelekea henga namba tano ambako alichukuwa begi lake na kuelekea huko ilipo hiyo nyumba.

Gari ikasimama nje ya geti kubwa jeusi, Baston akashuka na kuangalia nyumba hiyo aliyoambiwa ni ndogo.

"Hivi hawa watu ndogo kwao ina maana gani" alisimama nje na kujiulza. Mbele yake kulikuwa na nyumba yenye muundo wa zamani. Ilikuwa kubwa mara tano au sita ya nyumba yake ya zamani. Baada ya muda mrefu kupita akatoa ile funguo, ilikuwa imeambatanishwa na kadi ndogo.

Akagusisha sehemu katika geti hilo, likafunguka. Kwa mwendo wa taratibu akaelekea mpaka ulipo mlango wa mbele wa nyumba huyo na kuufungua. Almanusura macho yadondoke, alikaribishwa na ukumbi mkubwa wenye samani za kisasa. Karibia kila kitu ndani humo kilioneka kipya.

"Mimi hata sijuo tena udogo wa nyumba hii uko wapi" alijisemea na kufunga mlango.
 
_65018d6d-c351-4958-8828-8962dd466dbc.jpeg
 
To the end (mpaka mwisho) 13

Tariq Haji

0624065911

Mbele ya ukumbi huwo kulikuwa na ngazi ya mbao iliyozunguka mara. Akavuka na kupanda ngazi hizo, ghorofa ya kwanza ikaingia machoni mwake. Ilikuwa na vyumba vinne vilivyokuwa vijiangaliana. Mwisho kabisa ya koridoo kulikuwa na ngazi nyingine ikiyoelekea ghorofa ya tatu. Ghorofa hiyo ilikuwa na mlango mmoja tu ukiokuwa mita kama sita hivi kutoka ziliposhia ngazi.

Akauendea na kuufungua, kilikuwa ni chumba cha kulali, kilikuwa ni kubwa mno. Ndani humo kulikuwa na kila kitu cha msingi ili chumba kiitwe chumba cha kulalia. Baston akaweka begi lake chini na hakuendelea kustaajabu tena, alikuwa kashachoka kushangaa.

Kwasababu wakati huwo ulikuwa unakaribia mchana, na yeye akakumbuka kuwa hakula kitu. Akaingia bafuni na kuoga kisha akavaa nguo nyingine na kutoka chumbani. Akashuka ngazi mpaka chini, alipofika mlango wa kutokea nje akakumbuka kuwa usafiri wake ameuwacha henga namba tano. Akajikuta akiishiwa nguvu, ila akiwa anawaza afanye nini ghafla comlink yake ikawaka.

Ilikiwa simu inaingia, akaipokea.

"Baston, ukiwa unataka kutoka tumia gari iliyokuwepo katika sehemu ya kuhifadhia usafiri" alikuwa ni Shanequeen na baada ya kuongea maneno hayo akakata bila kumpa nafasi ya kujibu. Baston akazunguka na kutafuta eneo hilo, alipofika karibu ajikwae.

"Gari... " kulikuwa na gari tatu za muundo tofauti, ah!

Akaingia tu kwenye wapo na kuwasha kisha akaondoka. Hakutaka kuwaza tena kitu kingine chochote. Hapo ndio alifahamu kuwa kuna watu walikuwa na maisha ya kuchezea.

**************

Ukuta namba moja katika nyumba fulani.

"Anajua chochote kuhusu siri ya miaka miatatu" aliuliza mtu mmoja mzee sana.

"Hapana, inaonekana anajua kuhusu roboti tu"

"Sawa ila tafuta vijana waendelee kumchunguza, nina wasiwasi huyu Baston si rahisi kama unavyodhani"

"Sawa babu nitafanya hivyo"

"Vizuri sana ila hakikisha vijana unaowatumia wanajua kazi yao, wasije wakakamatwa" "Usijali kuhusu hilo"

"Na vipi kuhusu Shanequeen"

"Asikupe wasiwasi sana, Edward amefanya kazi nzuri kilichobaki ni sisi kupeleka maneno tu. Nina uhakika baba ake hatokataa. Hakuna mzazi anaetaka binti yake awe hana maisha mazuri, kwasasa mzee Rozaliv hatokuwa na namna tena. Asipokubali itabidi aondoke ukuta namba mbili kwasababu hatokuwa na kitu chochote kinachomuhusisha na jeshi"

"Ila nimesikia amejiunga na henga namba tano"

"Hayo ni mawazo ya mfa maji tu, henga namba tano ni kongwe mno, na kujiunga kwake hakuna tofauti yeyote. Ndio kashakuwa mlemavu tena, njia pekee ni ya yeye kukubali kuwa mke wa fleet admiral (FA) ajae ambae ni kitukuu chako Edward. Ikiwa mambo yatakwenda vizuri ndani ya miaka kumi, Edward atafikia cheo cha Admiral. Moango wetu utakuwa umefikia nusu mpaka hapo"

"Sawa ni vizuri sana, unaweza kuenda" aliongea kizee huyo.

"Subiri habari nzuri tu" alijibu, akainuka na kuondoka akimuacha mzee huyo akiwa amekaa kizani. Wakati wote wakati wanaongea hawakuwa wamewasha taa.

****

Katika mgahawa uliokuwepo kwenye kona, watu wengi walikuwa wamekusanyika katika meza moja wakimuangalia kijana aliekuwa amemaliza karibia sahani kumi na tano za chakula.

"Samahani mteja, umefikia kiwango cha juu kabisa cha kupata huduma katika mgahawa wetu" aliongea muhudumu wa kike aliekuwa kasimama pembeni.

"Agghh! Kwani hamna chakula tena" aliongea Baston akimeza chakula alichokuwa nacho mdomoni.

"Hakuna" alijibu muhudumu na kuweka karatasi ya bili mezani, Baston akagusisha comlink yake katika kimashine alichokuwa nacho muhudumu huyo. Muhudumu akaandika kiwango cha pesa kinachotakiwa kulipwa. Kiwango hicho kikaktwa moja kwa moja kutoka benki.

Baston akainuka akionekana kuwa na majonzi, akapiga hatua ndogo ndogo kuelekea nje ya mgahawa. Akaelekea sehemu ya maegesho ulipo usafiri wake na kuondoka. Huwo ulikuwa ni mgahawa wa nne kufanya hivyo. Hata Baston mwenye hakuelewa njaa aliokuwa nayo imetoka wapi. Ni kweli ana desturi ya kula chakula kingi lakini hili lilikuwa la kawaida ukizingatia mazoezi magumu anayofanya.

Baada ua kutoka katika mgahawa huwo akaelekea Supermarket na kununua vitu kadhaa. Akavipakia katika na kurudi nyumbani kwake, alipofika tu akaingia jikoni na kuandaa chakula cha kutosha, akala mpaka akakosa nafasi ya kupumua. Akajitupa kwenye kochi na usingizi mzito ukamchukuwa.

"Mi nilikwambia atakuwa kalala" "Shhh, usiongee kwa nguvu ataamka" Fwoooosh!

Mara upepo ukawapita wote wawili, kivuli cha mtu kikazunguka na kumshika mmoja wao. Akapitisha mkono shingoni.

"Ukitikisika unakufa" sauti nzito ikasikika

"Baston!!" aliita Malik akiwasha taa, ila akashangaa kukuta bado Baston akiwa kafumba macho. Kwa maneno mengine bado alikuwa usingizini. Alichokifanya wakati huwo kimetokana na hisia zake kali za mabadiliko ya mazingira.

"Baston, mi Shanequeen" aliongea msichana huyo akitetemeka na uso wake ukiwa mwekundu.

"Shane.. " Baston akaita na kwa kasi ya umeme akaruka nyuma na kuweka umbali wa zaidi ya mita moja na kufumbua macho.

Malik alikuwa pembeni akitikisa kichwa, anajua kabisa kilichomshtua Shanequeen siyo kukabwa bali ni mgusano wa nyama zake za kiuno na Baston. Na sababu hiyo hiyo ndio iliyomfanya Baston aruke umbali mkubwa sana. Akiwa usingizini picha ya Shanequeen ilimjia kichwani na moja kwa moja umbile la mschana huyo likajichora.

"Samahani sijakusudia... " alikatishwa na teke kali sana lilitoka kwa Shanequeen. Baston akarudi nyuma na kuliacha lipite kisha akamazunguka akijaribu kukwepa mashambulizi yanayofuata.

"Samahani" aliongea huku akijitahidi kukwepa mashambulizi yote.

"Nifanye nini ili unisamehe"

"Simama hivyo hivyo" alinguruma Shanequeen.

Bang!!

Teke kali likatua kifuani mwa Baston na kumrusha nyuma nusu mita.

"Nyie malizaneni mimi naenda jikoni kuangalia kama kuna cha kupika" aliongea Malik akipiga tambwe ndefu kutafuta jiko lilipo.

"Umenisamehe" akiongea Baston kwa sauti ndogo akijaribu kumsogelea Shanequeen aliekuwa mbali kidogo na yeye.

"Simama hapo hapo, kuanzia hivi sasa ukae mita moja na mimi kila utakaponiona" aliongea Shanequeen lakini sauti haikuwa na hasira hata kidogo ndani yake. Baston akatikisa kichwa na kurudi nyuma, akakaa kwenye kochi. Kisha akamuonesha kocho jingine lililombali na yeye.

"Utakaa bila fulana mpaka saa ngapi", hapo Baston akakumbuka kama alipolala alivua fulana. Akaangaza kulia na kushoto kabla macho yake kutua alipokuwa amekaa Shanequeen kisha akatikisa kichwa kama vile mtu alieahindwa la kufanya.

"Nini?"

"Fulana yangu .... " Baston hakuona haja ya kuendelea maana angezua ugomvi mwingine. Akainuka na kuelekea chumbani kwake na kuvaa fulana nyingine kisha akarudi chini na kukaa alipokuwa mwanzo.

"Mbona mumekuja kimya kimya, si ungenijulisha hata kwa comlink" aliongea Baston.

"Tumekupigia sana lakini hukushika, na tulipofika tulibonyeza kengele sana lakini hakukuwa na jibu. Bahati nzuri mimi nilikuwa nimebeba funguo na kadi ya ziada. Baada ya Malik kunambia utakuwa umelala ndio nikaamua kutumia ufunguo huwo" alieleza Shanequeen.

"Ah! Nilikuwa nimechoka sana, si kawaida yangu kulala kama hivi" alijibu Baston akijichekesha.
 
Attachments

  • _b420141e-f704-41dd-aee9-53ce33344f96.jpeg
    _b420141e-f704-41dd-aee9-53ce33344f96.jpeg
    169.3 KB · Views: 13
SEHEMU YA TISA: TAALUMA ILIYOPOTOEA

To the end (mpaka mwisho) 10

Tariq Haji

0624065911

"Kushoto kwako ni Ranger PL6, ni aina ya roboti ambayo inahusika na mashambulizi. Japo uwezo wake wa kujilinda ni mdogo lakini linapokuja suala la mashambulizi linafanya mashambulizi makali na mazito. Lina uwezo wa kufanya mashambulizi ya masafa ya kati na marefu. Uwezo wake wa combat ya karibu ni mdogo"

"Mbele mwisho kabisa ni Doppa next gen, Doppa ni kizazi cha pili kutoka kizazi cha Doppa cha kwanza. Unaweza kusema ni Doppa alieboreshwa zaidi na ni All rounder. Ikiwa na maana anafanya mashambulizi na ulinzi ila nguvu ya mashambulizi ni kubwa kuliko ya ulinzi. Hivyo wanalitumia kama roboti la kufanyia mashambulizi".

"Nimeona mlangi umendikwa sector zero" aliongea Baston. Mzee Rozaliv akatabasamu na kuendea mlango huwo. Haukuwa mkubwa sana, akapitisha kadi sehemu, ukafunguka. Taratibu taa zikapata uhai na kumuliko eneo kubwa kiasi. Ndani humi kulikuwa na roboti chakavu mbali mbali ambazo kwa muonekano tu hazikuwa zimetengezwa na kampuni hiyi.

"Humu tunahifadhi roboti tunazohisi ni za kale, nyingi mimi nimezikuta tu" alifafanua Mzee Rozaliv. Baston akatupa macho yake mwisho kabisa. Yakatua kwenye roboti lililokuwa limeegemezwa ukutani. Lilionekana kuwa na vumbi jingi mno. Mzee Rozaliv akamuangalia Baston kisha akashusha pumzi kabla ya kuongea.

"Lile kule mwisho ni U01 (unknown 01), ni roboti namba moja kati ya mengi yaliyokuwemo humu. Lilikuwa ni roboti la kwanza kuletwa hapa na kutokana na maelezo katika kanzidata inasemekana lilipatikana miaka mia na hamsini iliyopita japo babu zangu waliamini lina miaka zaidi ya tajwa"

Baston akaliangalia kwa makini kisha taratibu akaanza kutembea kulifuata, alipofika akalishika shuka kubwa lililifunika na kulivuta. Chuma cheusi wa manane kilionekana, ni chuma ambacho kikizidi weusi kadri kikivyoakisi mwanga.

"Umesema limepatikana zaidi ya miaka mia na hamsini nyuma, mbona bado chuma chake kinaonekana kipya kabisa bila kuwa na dliki zozote za kuchakaa" alihoji Baston.

"Na hicho nduo kitemdawili kikubwa ambacho waliopita kabka yangu wameshindwa kukitatua, na inaonekana na mimi nitapita kama wao".

Baston akagusa chuma hicho na ghafla kumbukumbu za picha zikaanza kuonekana kichwani mwaka. Aliganda kwa dakika karibu tatu, hakuwa akisikia chochote.

"Baston" alizinduka baada ya kuguswa begani na Malik.

"Mr Rozalive mumewahi kujaribu kuliendesha?" aliuliza

"Ndio ila hakuna rubani aliefanikiwa, linawaka tu lakini halioneshi dalili zozote za uhai".

Baston akatabasamu na kuwageukia, akawaangalia kisha akatikisa kichwa akikumbuka msemo wa kale kuhusu afrika "Afrika ni nchi iliyokalia utajiri wake katika makalio".

"Hili roboti linaitwa Spectre (specta)" alianza kuongea "na lilitambuka kama Spectre the hunter, ni moja miongoni mwa maroboti wachache sana waliotengenezwa na kuonyesha makucha ya kipekee vitani. Rubani wake aliitwa Kamanda Dalia, alikuwa mwanamke pekee katika kikosi cha mstari wa mbele".

"Sifa kubwa ya Kamanda Dalia ilikuwa ni kuwinda Zestra, vitani hakutulia mstari wa mbele bali aliingia katikati ya kundi la Zestra na kuwawinda. Alikuwa ni kama simba mfalme wa porini, hakusikiliza amri ya mtu mwengine yeyote. Sifa zakw zilifika mbali mno, hata katika ulimwengu wa Zestra alitambulika vyema".

"Ila jwa bahati mbaya alikufa kwa ugonjwa usiojulikana na tokea siku hiyo hakuna mtu mwingine aliewezesha kuendesha Spectre na hivyo likapotea katika wakati" alipomaliza kauli hiyo, mtikisiko mdogo ukasikika.

Macho ya Spectre yakafunguka na rangi nyekundu ikaonekan, "kwanini una sonono" aliuliza Baston akiingalia mashne hiyo machoni.

"Dalia hakufa kwa ugonjwa, alichomwa sindano ya sumu" mara akasikia sauti katika kichwa chake. Hali kama hiyo ilitokea alipokutana na Gilbot, roboti zote mbili zilikuwa na akili ya kwao.

"Unataka kurudi vitani?"

"Ndio, nitarudi endapo utanisikiliza ombi langu"

"Ombi gani"

"Nataka aliehusika na kifo cha Dalia ahukumiwe ili kupoza roho ya rafiki yangu".

"Ila ni miaka mingi sana imepita, sidhani kama mtu huyo atakuwa hai mpaka sasa"

"Hhhmf!! Atakuwa hai tu kwasababu sio mtu wa kawaida baki ni zao kati ya binadamu na Zestra"

Maongezi hayo yalifanyika kupitia njia maalum ya kimawazo, hakuna sauti iliyotoka. Wengine walikuwa wakimuona Baston akiliangalia roboti hilo bila kuongea jambo.

"Nitakuchukuwa vitani, sijui kama nitaweza kufikia kiwango cha Kamanda Dalia, ila nina uhakika utaishi vizuri siku zako za mwisho. Na kuhusu kifo chake, usijali nitahakikisha nachimba siri zote. Hata mimi nina mashaka kuwa katika safu ya uongozi wa juu wa binadamu kuna wavamizi ambao wameweza kupata vyeo baada ya kuvaa sura za binadamu"

Chozi jicho la kushoto la Baston likachuruzika, wote wakashangaa.

"Hivi mnaamini baada ya mida flani kupita hata roboti anatengeneza hisia" aliongea akiwaangalia.

"Hayo ni maneno tu ila hawayajawahi kuthibitishwa" alijibu profesa Ashdawi.

"Ni kwasababu marubani wengi wanachukulia roboti kama mashine za kivita tu, wanakosa muunganiko wa hisia. Profesa Bagani najua unafahamu ninachokiongea. Silaha kubwa kwa binadamu ni hisia zake na ndio maana tukatofautiana na jamii nyingi"

"Hapana si kweli" alijibu profesa Ashdawi kabla ya profesa Bagani kuongea

"Ni kweli anachokiongea Baston, silaha kubwa ya binadamu ni hisia zake lakini pia hisia hizo hizo zinaweza kuwa chanzo maangamizi yake. Mfano kwanini mwanajeshi anakwenda vitani, ni kwasababu anajua kutokwenda kwake kunaweza kukawaangamiza walio nyuma yake. Lakini sioni muunganiko kati ya hisia hizo na kwanini roboti hilo wengi wamwshindwa kuliendesha" alifafanua profesa Bagani.

"Mr Rozaliv natumai katika ukusanyaji wako wa vito mbali mbali umepata almasi ya damu" aliuliza Baston.

"Ndio"

"Unaweza ukaichonga" aliongea Baston na kutoa vipimo vyote.

"Kwanini"

"Kwasababu Spectre lilikuwa roboti la kwanza na la pekee kutumia moyo" alijibu. Hapo sasa Mr Rozaliv akashtuka, kichwani alikuwa na swali siku zote alipoangalia upande wa kushoto wa roboti hilo. Kuliko na shimo ambali halikuwa likielezeka.

Papo hapo akagisa comlink yake na kutafuta namba kisha akapiga, akatoa maelekezo yote kisha akakata. Baada ya nusu saa akafika mtu akiwa na chombo fulani na kumkabidhi. Mr Rozaliv akatoa almasi ya dhahabu ambayo tayari ilishachongwa na kumrushia Baston.

Nae akapanda mpaka katika kifua cha Spectre na kuitumbukiza, kisha akaponyeza sehemu na mlango wa kuingilia eneo la rubani ukafunguka, akaingia. Mr Rozalive akabonyeza sehemu na mlango mkubwa ukafunguka. Ndani ya chumba hicho kulikuwa na mashine kubwa ya kubebea roboti, ikalibeba Spectre na kulipeleka eneo la majaribio. Ulikuwa ni uwanja mkubwa sana uliokuwa umezungukwa na kuta ndefu mno.

Akiwa ndani humo Baston akaangalia muundo wa cockpit, akaangalia kushoto na kulia kisha akabonyeza kitufe fulani. Kofia kubwa ya chuma ikashuka na kuingia kichwani mwake.

Neural connection initiated

Loading data to the new pilot

Taarifa nyingi zikaanza kuingia katika ubongo wa Baston, ikikuwa shughuli yenye maumivu mno. Lakini alivumilia kwasababu wakati huwo huwo alikuwa akirithi taaluma ya kamanda Dalia pamoja na baadhi ya kumbukumbu zake ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika roboti hilo.

********
 
SEHEMU YA KUMI: SPECTRE

To the end (mpaka mwisho) 11

Tariq Haji

0624065911

Baada ya roboti hilo kushushwa uwanjani, milango ikafungwa pamoja na ngao maalum zilizotengenezwa kwa nguvu ya sumaku (electromagnetic force field "EMFF"). Lengo la EMFF kuzuia mawimbi makali yenye madhara yatakayosababishwa na shughuli za mashine hiyo.

Mzee Rozalive na wengine wakapanda sehemu iliyokuwa juu na kukaa eneo ambalo lilitumika kuangalia majaribio hayo. Siyo wao tu, hata baadhi ya wafanyakazi wengine nao walikaa maeneo kama hayo wakitaka kushuhudia labda miujiza ingetokea. Maana wao walijaribu mbinu zote lakini Spectre hakuinua hata kidole.

"Kuna mtu anataka kujiaibisha leo"

"Hahaha, halafu nimesikia ni bwana mdogo hata bado unyevunyevu nyuma ya masikio yake haujakauka" "Fufu watu wengine hawajui kipi bora kwao"

Baadhi ya waangaliaji walikuwa wakinong'ona, hakuna alietaka kuamini kama roboti lililolala katika eneo hilo kwa miaka karibia mia na hamsini bila kuinua hata kidole kama lingetikisika.

Dakika tano, kumi, kumi na tano, bado kimya.

"Ah, hili pande la chuma labda lishakufa" aliongea profesa Bagani. Watu wote walikuwa kimya wakiliangalia roboti lililosimama uwanja bila hata kutikisika. Na kuna baadhi wakawa tayari wameanza kuonesha dharau.

Fwoooosh!!

Vitu kama maji vikatoka kwenye maungio ya Spectre, ukafuata mvuke mwingi mweupe. Watu wote wakatoa macho, hata wale ambao tayari walishaanza kuondoka wakasimama na kugeuka.

Vruuum!!!

Mashine ikanguruma na kusababisha mtetemeko ulisikika mpaka kwa waangaliaji, taratibu vyuma vya nje vya Spectre vikaanza kutikisika na kujipanga sehemu zake. Watu wakazidi kushangaa, roboti iliyolala miaka mia na hamsini imeamka mbele yao.

"Karibu, tafadhali ingiza jina lako" sautu ikasikika masikioni mwa Baston.

"Baston" alijibu.

"Karibu Baston", ghafla kiza kilichokuwa kimemzunguka baston kikatoweka na kujikuta amesimama katika eneo kubwa. Moja kwa moja alitambua kuwa eneo hilo liliitwa Emerald. Mbeke yake alikuwa mwanamke aliekuwa katika kombat ya jeshi "Spectre" aliita Baston.

Hakujibiwa ila mwanamkw huyo akapotea na baada ya hapo Baston akaona eneo kubwa. Ulikuwa ni uwanja ambao Spectre alikuwa amesimama. Tayari Baston na Spectre walishaungana na kuwa kitu kimoja.

"Kila kitu kimekamilika" alisikia tena sauti.

Baston akaanza kunyoosha viungo, na wakati huwo Spectre akaanza kunyoosha viungo.

Kah! Kah!

Sauti za vyuma zikasikika, sehemu ya mabega chuma kikafunguka. Bomba mbili zenye urefu wa mita moja zikatokea kila upande. Visu virefu vikachomoza chini ya viganja, pande zote mbili za kiuno kukafunguka zikaonekana bastola mbili.

Sehemu ya nyuma chini ya mgongo, kukikuwa na chuma kikichochongwa kama pochi. Kikafunguka, ikaonekana mipini mili meusi. Sehemu ya magoti nayo ikafunguka, vikaonekana vitu vyenye ncha kali. Wakati Baston alikuwa akiangalia silaha zote za Spectre. Akastaajabu sana, ni kweli katika kumbukumbu alizozirithi kwa Gilbot, Spectre alitajwa lakini hakukuwa na maelezo mengi sana.

Wakati huu ndio Baston akafahnu kuwa Spectre alitengezwa kwa kazi moja tu. Nayo ilikuwa ni kufanya mauaji, pia ikamfunukia kichwani kuwa Spectre alitengenezwa makhususi kwa ajili ya kamanda Dalia. Maana kila kiungo cha roboti huyo kilikuwa ni silaha ya mauaji.

Fwoooosh!!!

Sehemu ya pembeni ya kichwa karibu na masikio, pakafunguka na maji mengi yakatoka na kusababisha roboti zima kurowa. Baada ya sekunde chache mapovu yakaonekana yakijitemgeza katika mwili wa Spectre na baada dakika tatu mwili mzima ukawa umefunikwa na mapovu.

Maji yakatoka tena na povu lote likasafishwa kisha mvuke ukafuate na sekunde chache tu maji yakakauka. Sehemu ya kifua upande wa kushoto chini ya sehemu ilipoingua almasi ya damu kukafunguka, na chuma kidogo kikasogea mbeke. "Spectre" ndio lilisomeka katika chuma hicho.

Spectre alikuwa mweusi tii, weusi ambao haukung'ara ulipopigwa na jua bali ulinyonya mwanga wote uliotua katika chuma hicho na kukifanya kizidi kuwa cheusi.

Mashine ikazidi kunguruma na baada ya dakika mbili mngurumo wote ukapotea. Akaanza kutembea na kadri sekunde zilivyochanika ndivyo kasi ilivyoongezeka na mwisho akaanza kukimbia. Mara kadhaa alitikisika na kufannya miondoka ambayo ambayo haikuwa rahisi kwa roboti kufanya.

"Mungu wangu, lile roboti au binadamu" aliongea mtu mmoja akishika kichwa chake. Ila hakuna aliemsikia hata mmoja kila mtu alikuwa amepigwa na bumbuwazi la aina yake.

Ghafla Spectre akabiringitia na kutoa bastola, akafanya shambulizia na papo hapo akariudisha kupeleka mikono yake. Ile sehemu ya vusu ikafunguka, akatoa visu viwili na kushika kila kimoja katika mkono mmoja.

Akafanya mashambulizi ya kasi kama matano hivi akavizungusha na kuvirudisha katika pochi yake. Akarusha ngumi kadhaa kwa kasi mno, wengi hawakuona ila kwa wale wenye macho makali walishuhudia vitu vye ncha kali vikitoka pale ngumi zilipofika mwisho na kurudi mkono uliporudi nyuma.

Akazunguka mara kadhaa na kuachia mateke ambayo haya kuwa rahisi kwa roboti kufanya. Ila mateke hayo hayakuwa yakawaida tu. Kulikuwa visu vikali vilivyokuwepo kwenye visigino na vidole vya miguu.

Baada majaribio yote kukamilika, Spectre akasimama na moshi laini ukaonekana ukitoka katika mwili wa chuma hicho. Kwa wataalamu na magwiji wa vita waliokuwepo eneo hilo katika vichwa vyao kulikuwa na sentensi moja tu. "Kila pigo lilitoka kwa Spectre lilitoka na maana moja tu, kuuwa"

Walikuwa sahihi kwa asilimia thamanini lakini kiti ambacho hawakukifahamu. Spectre hakuwa tu roboti wa kufanya mauwaji bali mauaji ya halaiki. Spectre ilikuwa ni mashine iliyotengenezwa kuwa muwindaji. Hata baadhi ya Zestra wa ngazi za juu waliifahamu kazi ya Spectre. Kwao alikuwa ni shetani shuwaini asiye na huruma hata kidogo.

Baada ya nusu saa mashine ya kubebea roboti ikafika na kulibeba Spectre. Likarudishwa ndani, sehemu ya kifua ikafunguka. Baston akatoka akiwa karowa jasho mwili mzima, mwili wake wote ulikuwa umetutumka. Misuli ilikuwa imevimba na kufanya nguo aliyovaa kugandana na mwili kisawasawa.

Alipokanyaga tu ardhi akayumbayumba almanusura aanguke. Mishipa ya kichwa ilikuwa imevimba na kutweta kama mapigo ya moyo.

"Mbona umechoka sana" aliuliza profesa Bagani.

"Ngoja nipumzike kwanza nitaeleza kila kitu" aliongea

Baston kwa tabu vifuniko vya macho vikawa visito na hatimae akapoteza fahamu. Mzee Rozaliv akaita watu na kuwaagiza wampeleke chumba cha mapumziko.

Karibia wote walikuwa na maswali kedekede lakini hakukuwa na kuwapa majibu. Ni kweli kuna wakati marubani hupoteza fahamu baada ya kuendesha roboti. Ila hali hiyo huwa inakuja baada ya matumizi muda mrefu zaidi ya saa tatu. Lakini kwa Baston ilikuwa ni ajabu. Kwasababu yeye alikuwa katika roboti hilo kwa saa moja tu.

Hata hivyo hawakuwa na namna zaidi ya kumsubiri Baston aamke ndio wapate majibu. Kila mwenye swali alilieka swali lake pembeni na kuangalia mkanda (video) ya majaribio ya Spectre. Jopo la wataalamu lilikuwa limekusanyika katika ukumbi mdogo wakidadavua kila sekunde ya video hiyo.

To the end (mpaka mwisho) 12

Tariq Haji

0624065911

Saa mbili baadae.

Anaingia mtu katika ukumbi ambao wataalamu walikuwa wakiidadavua video ya majaribio ya Baston. Akaenda moja kwa moja mpaka alipo mzee Rozaliv na kumnong'oneza jambo. Baadaa ya kubalisha maneno mawili matatu, yule bwana aliefika akaondoka.

"Jamani Baston ameamka tayari, tusubiri dakika chache atakuja" aliongea kwa sauti ya wastan lakini kila mtu alisikia ndani humo. Dakika saba baadae mlango ukafunguliwa, Baston akaingia. Bado sura yake ilikuwa imepauka na uchovu ulidhihiri usoni mwake.

Wataalamu wote walikuwa wakimuangalia kama mbwa alieona mfupa. Kila mtu alikuwa na maswali kedekede na alihitaji majibu.

Baston akatembea mpaka mbele kabisa na kupanda jukwaani. Akavaa kama kidude kirefu kidogo sikioni na kukohoa kuhakikisha kilikuwa kinafanya kazi vyema.

"Habari za saa hizi, najua mlikuwa mnasubiri kwa hamu kutaka kujua nini kimetokea. Hivyo nitapokea maswaki mawili tu kwa kila mtu na si zaidi, bado nahitaji kupumzika" aliongea.

"Mimi ndio nitakuwa naongoza, ukiwa unaswali lolote tafadhali bonyeza kitufe kilichokuwa mbele yako" aliongea mzee Rozaliv na karibia watu wote wakabonyeza.

"Kwa waliobonyeza wataanza kuuliza, mpaka pale watakapokwisha watabonyeza wingine. Kumbukeni maswali ni mawili tu kama alivyosema Baston, hivyo kuwa makini na kile unachotaka kujua na sio kila swali" aliendelea. Akabonyeza sehemu katika meza yake na taa ikawaka eneo alilopo mtu mtaalamu mmoja.

"Ahsante, kwa ninavyofahamu ni kwamba karibia marubani wengi wamejaribu kuliendesha Spectre lakini bila mafanikio. Wewe umewaje?" aliuliza mtu huyo.

"Kwanza ifahamike kuwa marubani wengi wanaendesha maroboti ambayo hayana neurolink. Kuendesha kwao hakuna tofauti na mtu anayeendesha chombo cha usafiri" japo kauli hiyo iliwakera wengi lakini hakuna aliefungua mdomo.

Akaendelea "ili kuweza kuendesha Spectre ni lazima mtu atimiza mambo matatu. Moja awe na mwili madhubuti, mbili awe na uwezo wa kunyonya utherium usiopungua daraja B na tatu awe na akili madhubuti".

"Tunajua na kufahamu kwamba hakuna uhusiano wowote kati ya mwili, akili na utumiaji mashuhuri wa roboti, unachokisema hakileti maana, tufafanulie" aliuongea alieuliza swali.

"Spectre ni roboti kale zaidi ya miaka mia na hamsini nyuma, huenda ikawa lina miaka zaidi ya mia tatu. Teknolojia ya wakati ule ni tofauti na sasa. Kipindi cha sasa wengi tumezaliwa tukiwa tayari na uwezo wa kunyonya itheriuma lakini nyakati za kale binadamu walipitia majaribio mbali pamoja uhandisi wa kijenetiki kuhakikisha wanapata uwezo wa kunyonya nguvu asili ili kuweza kutumia roboti"

"Hivyo iliwabidi wengi wawe na mwili shupavu, madhubuti na mkakamavu kuweza kuhimili mikiki mikiki ya utumiaji wa maroboti, ila kwa sasa kinachoangaliwa ni uwezo wa mtu kuweza kuhifadhi na kunyonya itherium", hata kama muulizaji hakuridhika na majibu ila hakuwa na uwezo wa kuuliza swali jingine.

Mzee Rozaliv akabonyeza kitufe kingine iki kumpa nafasi muulizaji mwingine aulize maswali yake.

"Ahsante, katika maelezo yako ya mwanzo umesema ili rubani aweze kutumia Spectre ni lazima atimize mambo matatu. Unaweza kufafanua kwa kina?"

"Moja, mwili madhubuti. Nikiwa na maana awe na mwili usiopungua daraja B. Kutokana na mfumo aliotengenezewa Spectre, mtu yeyote mwenye uwezo wa kunyanyua chini ya kilogramu mia tano hatoweza kumudu kuendesha Spectre. Mfumo wa Spectre hauna msaada mkubwa kutoka AI ( artificial intelligence) tofauti na mifumo ya sasa ambayo kwa kiwango kikubwa rubani anasaidiwa na programu hiyo"

"What???"

Minong'ono ya hapa na pale ikazuka, kwa ufahamu wa kawaida ni kwamba mfumo wa kutumia vitufe katika riboti umekuja kuweka wepesi katika matumizi. Kwasababu rubanibakibonyeza tu sehemu basi roboti atainua mkonk au mguu. Na pia uwepo wa usukani umerahisisha katika kona, kuzunguka na kufanya miondoka mbali mbali na ndio maana kigezo cha mwili shupavu kikaondolewa.

Lakini kwa roboti za awali zote ilikuwa tofauti, kwa sababu rubani aliunganisha ufahamu wake na kwenye mfumo wa ufahamu wa roboti. Hivyo, mashine hiyo kuwa kama mwili wake. Amri zote zilitoka moja kwa moja akilini mwake na roboti ilizifanya kama mwili wake. Hivyo ilikuwa ni lazima mtu awe na nguvu sana dini amri hizo.

"Mbili, akili komavu. Wataalamu waliipa jina la Battle Oriented Mind (BOM), akili ambayo inawaza vita na jinsi ya kushinda vita hiyo. Hiyo ilitokana na sababu ya kuwa, baada ya rubani kuingia vitani alitakiwa kudadavua na kupiga hesabu mwenyewe jinsi ya kushinda vita au kurudi salama ikiwa vita atashindwa"

"Tatu ni kuhusu itherium, hilo natumai nyote mnalifahamu kadri daraja linavyokuwa juu ndio bora zaidi", maswali yaliendelea huku Baston akijitahidi kujibu kadri ya uwezo wake. Ila mengi aliyajibu kwa juu juu maarifa na siri nyingi ambazo hajulikani. Ila wapo ambao wanazijua na hawako tayari mtu mwingine ajue, hivyo angehatariaha maisha yake.

Maswali na majibu yaliendelea kwa saa tatu na mwisho kikao kikafikia tamati. Kutokea hapo kila atadadavua kwa vile alivyoelewa. Baston akaachana nao na kutoka ukumbini hapo, nyuma yake alifuata Malik na mzee Rozaliv akisukuma kiti cha mwanae.

"Baston, Shanequeen amenambia umehamia rasmi ukuta namba mbili. Ushapata sehemu ya kukaa?" aliuliza mzee

Rozaliv.

"Bado, ndio nimekusudia nikitoka hapa nikatafute"

"Kuna ndogo niliijenga muda mrefu sana ila kwasasa haina mtu, unaweza kwenda kukaa pale. Chukulia kama hiyo ni zawadi yangu kwa msaada ulompatia mwanangu" aliongea mzee Rozaliv akimrushia funguo. Ilikuwa ni kitendo cha ghafla na bila bala Baston akaidaka.

"Ila... " alitaka kuongea jambo ila macho yake yalipokutana na Shanequeen akalimeza jambo hilo na kutabasamu.

"Nashukuru sana, Malik na wewe si ubakie huku huku" aliongea Baston.

"Kuna mambo mawili matatu ya kuongea na mzee Rozaliv, nitakutafuta baada ya kumaliza" aliongea Malik. Baston hakuwa na la kusema zaidi, akaagana nao na kutoka nje ya jengo hilo. Tayari gari ilikuwa ishaandaliwa, akapanda na kuelekea henga namba tano ambako alichukuwa begi lake na kuelekea huko ilipo hiyo nyumba.

Gari ikasimama nje ya geti kubwa jeusi, Baston akashuka na kuangalia nyumba hiyo aliyoambiwa ni ndogo.

"Hivi hawa watu wadogo kwao ina maana gani" alisimama nje na kujiulza. Mbele yake na yenye nyumba muundo wa zamani. Ilikuwa kubwa mara tano au sita ya nyumba yake ya zamani. Baada ya muda mrefu kupita akatoa ile funguo, ilikuwa imeambatanishwa na kadi ndogo.

Akagusisha sehemu katika kupata hilo, likafunguka. Kwa mwendo wa taratibu akaelekea mpaka ulipo mlango wa mbele wa nyumba huyo na kuufungua. Almanusura macho yadondoke, alikaribishwa na ukumbi mkubwa wenye samani za kisasa. Karibia kila kitu ndani humo kilioneka kipya.

"Mimi hata sijuo tena udogo wa nyumba hii uko wapi" alijisemea na kufunga mlango.
 
To the end (mpaka mwisho) 13

Tariq Haji

0624065911

Mbele ya ukumbi huwo kulikuwa na ngazi ya mbao iliyozunguka mara. Akavuka na kupanda ngazi hizo, ghorofa ya kwanza ikaingia machoni mwake. Ilikuwa na vyumba vinne vilivyokuwa vijiangaliana. Mwisho kabisa ya koridoo kulikuwa na ngazi nyingine ikiyoelekea ghorofa ya tatu. Ghorofa hiyo ilikuwa na mlango mmoja tu ukiokuwa mita kama sita hivi kutoka ziliposhia ngazi.

Akauendea na kuufungua, kilikuwa ni chumba cha kulali, kilikuwa ni kubwa mno. Ndani humo kulikuwa na kila kitu cha msingi ili chumba kiitwe chumba cha kulalia. Baston akaweka begi lake chini na hakuendelea kustaajabu tena, alikuwa kashachoka kushangaa.

Kwasababu wakati huwo ulikuwa unakaribia mchana, na yeye akakumbuka kuwa hakula kitu. Akaingia bafuni na kuoga kisha akavaa nguo nyingine na kutoka chumbani. Akashuka ngazi mpaka chini, alipofika mlango wa kutokea nje akakumbuka kuwa usafiri wake ameuwacha henga namba tano. Akajikuta akiishiwa nguvu, ila akiwa anawaza afanye nini ghafla comlink yake ikawaka.

Ilikiwa simu inaingia, akaipokea.

"Baston, ukiwa unataka kutoka tumia gari iliyokuwepo katika sehemu ya kuhifadhia usafiri" alikuwa ni Shanequeen na baada ya kuongea maneno hayo akakata bila kumpa nafasi ya kujibu. Baston akazunguka na kutafuta eneo hilo, alipofika karibu ajikwae.

"Gari... " kulikuwa na gari tatu za muundo tofauti, ah!

Akaingia tu kwenye wapo na kuwasha kisha akaondoka. Hakutaka kuwaza tena kitu kingine chochote. Hapo ndio alifahamu kuwa kuna watu walikuwa na maisha ya kuchezea.

**************

Ukuta namba moja katika nyumba fulani.

"Anajua chochote kuhusu siri ya miaka miatatu" aliuliza mtu mmoja mzee sana.

"Hapana, inaonekana anajua kuhusu roboti tu"

"Sawa ila tafuta vijana waendelee kumchunguza, nina wasiwasi huyu Baston si rahisi kama unavyodhani"

"Sawa babu nitafanya hivyo"

"Vizuri sana ila hakikisha vijana unaowatumia wanajua kazi yao, wasije wakakamatwa" "Usijali kuhusu hilo"

"Na vipi kuhusu Shanequeen"

"Asikupe wasiwasi sana, Edward amefanya kazi nzuri kilichobaki ni sisi kupeleka maneno tu. Nina uhakika baba ake hatokataa. Hakuna mzazi anaetaka binti yake awe hana maisha mazuri, kwasasa mzee Rozaliv hatokuwa na namna tena. Asipokubali itabidi aondoke ukuta namba mbili kwasababu hatokuwa na kitu chochote kinachomuhusisha na jeshi"

"Ila nimesikia amejiunga na henga namba tano"

"Hayo ni mawazo ya mfa maji tu, henga namba tano ni kongwe mno, na kujiunga kwake hakuna tofauti yeyote. Ndio kashakuwa mlemavu tena, njia pekee ni ya yeye kukubali kuwa mke wa fleet admiral (FA) ajae ambae ni kitukuu chako Edward. Ikiwa mambo yatakwenda vizuri ndani ya miaka kumi, Edward atafikia cheo cha Admiral. Moango wetu utakuwa umefikia nusu mpaka hapo"

"Sawa ni vizuri sana, unaweza kuenda" aliongea kizee huyo.

"Subiri habari nzuri tu" alijibu, akainuka na kuondoka akimuacha mzee huyo akiwa amekaa kiazani. Wakati wote wakati wanaongea hawakuwa wamewasha taa.

****

Katika mgahawa uliokuwepo kwenye kona, watu wengi walikuwa wamekusanyika katika meza moja wakimuangalia kijana aliekuwa amemaliza karibia sahani kumi na tano za chakula.

"Samahani mteja, umefikia kiwango cha juu kabisa cha kupata huduma katika mgahawa wetu" aliongea muhudumu wa kike aliekuwa kasimama pembeni.

"Agghh! Kwani hamna chakula tena" aliongea Baston akikula chakula alichokuwa nacho mdomoni.

"Hakuna" alijibu muhudumu na kuweka karatasi ya bili mezani, Baston akagusisha comlink yake katika kimashine alichokuwa nacho muhudumu huyo. Muhudumu akaandika kiwango cha pesa kinachotakiwa kulipwa. Kiwango hicho kikaktwa moja kwa moja kutoka benki.

Baston akainuka akionekana kuwa na majonzi, akapiga hatua ndogo kuelekea nje ya mgahawa. Akaelekea sehemu ya gari ulipo usafiri wake na kuondoka. Huwo ulikuwa ni mgahawa wa nne kufanya hivyo. Hata Baston mwenye hakuelewa njaa aliyokuwa nayo imetoka wapi. Ni kweli ana desturi ya kula chakula kingi lakini hili lilikuwa la kawaida ukizingatia mazoezi magumu anayofanya.

Baada ua kutoka katika mgahawa huo akaelekea Supermarket na kununua vitu kadhaa. Akavipakia katika na kurudi nyumbani kwake, alipofika tu akaingia jikoni na kuandaa chakula cha kutosha, akala mpaka akakosa nafasi ya haki. Akajitupa kwenye kochi na usingizi mzito ukamchukuwa.

"Mi niliwambia atakuwa kalala" "Shhh, usiongee kwa nguvu ataamka" Fwoooosh!

Mara upepo ukawapita wote wawili, kivuli cha mtu kikazunguka na kumshika mmoja wao. Akapitisha mkono shingoni.

"Ukitikisika unakufa" sauti nzito ikasikika

"Baston!!" aliita Malik akiwasha taa, ila akashangaa kukuta bado Baston akiwa kafumba macho. Kwa maneno mengine bado alikuwa usingizini. Alichokifanya wakati huo kimetokana na hisia zake kali za mabadiliko ya mazingira.

"Baston, mi Shanequeen" aliongea msichana huyo akitetemeka na uso wake ukiwa mwekundu.

"Shane.. " Baston akaita na kwa kasi ya umeme akaruka nyuma na kuweka umbali wa mita moja na kufumbua macho.

Malik alikuwa pembeni akitikisa kichwa, anajua kabisa kilichomshtua Shanequeen siyo kukabwa bali ni mgusano wa nyama zake za kiuno na Baston. Na hiyo ndiyo iliyomfanya Baston aruke umbali mkubwa sana. Akiwa usingizini picha ya Shanequeen ilimjia kichwani na moja kwa moja umbile la mschana huyo likajichora.

"Samahani sijakusudia... " alikatishwa na teke kali sana lilitoka kwa Shanequeen. Baston akarudi nyuma na kuliacha lipite kisha akazunguka akijaribu kukwepa matokeo yanayofuata.

"Samahani" aliongea huku akijitahidi kukwepa yote.

"Nifanye nini ili unisamehe"

"Simama hivyo hivyo" alinguruma Shanequeen.

Bangi!!

Teke kali likatua kifuani mwa Baston na kumrusha nyuma nusu mita.

"Nyie malizaneni mimi naenda jikoni kuangalia kama kuna cha kupika" aliongea Malik akipiga tambwe ndefu kutafuta jiko lilipo.

"Umenisamehe" akiongea Baston kwa sauti ndogo akijaribu kumsogelea Shanequeen aliekuwa mbali kidogo na yeye.

"Simama hapo hapo, kuanzia sasa ukae mita moja na mimi kila utakaponiona" aliongea Shanequeen lakini sauti haikuwa na hasira hata ndani yake. Baston akatikisa kichwa na kurudi nyuma, akakaa kwenye kochi. Kisha akamuonesha kocho lililombali na yeye.

"Utakaa bila fulana mpaka saa ngapi", hapo Baston akakumbuka kama alipolala alivua fulana. Akaangaza kulia na kushoto kabla macho yake kutua alipokuwa amekaa Shanequeen kisha akatikisa kichwa kama vile mtu aliehindwa la kufanya.

"Nini?"

"Fulana yangu .... " Baston hajaona haja ya kuendelea maana angezua ugomvi mwingine. Akainuka na chumbani kwake na kuvaa fulana nyingine kisha akarudi chini na kukaa alipokuwa mwanzo.

"Mbona mumekuja kimya kimya, si ungenijulisha hata kwa comlink" aliongea Baston.

"Tumekupigia sana lakini hukushika, na tulipofika tulibonyeza kengele sana lakini hakukuwa na jibu. Bahati nzuri mimi nilikuwa nimebeba funguo na kadi ya ziada. Baada ya Malik kunambia utakuwa umelala ndio nikaamua kutumia ufunguo huo" alieleza Shanequeen.

"Ah! Nilikuwa nimechoka sana, si kawaida yangu kulala kama hivi" alijibu Baston akijichekesha.
 
To the end (mpaka mwisho) 14

Tariq Haji

0624065911

Wakati wakiendelea na maongezi, Malik alifika na nyungu kubwa iliyojaa chakula na kuiweka mezani.

"Umealika watu au?" aliuliza Shanequeen, Malik akatabasamu na kumgeukia Baston kisha akamkonyeza.

"Niseme au nisiseme" Basto aliifahamu sentensi hiyo katika kichwa hali ya kuwa Malik hakuisema kwa mdomo. Wawili hao wamekuwa na urafiki wa muda mrefu kiasi kwamba walijuana nje ndani.

"Baston huwa anakula zaidi ya mara nne kwa siku" aliongea Malik. Kwa namna moja ama nyingie Shanequeen alihisi kuna kitu hakipo sawa lakini kila alivyojaribu kukitafuta hakukipata akaamua achana nacho kwa wakati huwo.

Wakapata chakula huku wakipiga soga za hapa na pale mpaka karibia saa tano usiku.

"Shanequeen nenda ukapumzike, unajua imebaki miezi miwili tu mpaka mwaka mpya wa kujiunga na jeshi utakapoanza. Henga namba tano ina vitu vikongwe tupu, tunahitaji vitu vipya. Mimi nina kiasi kadhaa natumai kitatosha kwa kuanzia" aliongea Baston.

"Hakuna haja ya kuumiza mfuko wako kila kitu kimeshashighulikiwa tayari" aliongea Malik.

"Najua itakuwa haitoshi lak... " akanyamaza na kuwaangalia wengine waliokuwa wanamuangalia na matabasamu makubwa usoni.

"Unadhani kazi yangu nini?" aliongea Malik akijipiga piga kifuani kama sokwe, Baston akabaki anatikisa kichwa. Malik alikuwa amekosa haya kabisa.

Baada ya maongezi wakaagana na Shanequeen akaondoka, haikuwa kazi ngumu kwa kwasababu alipokuja hapo alikuja na gari yake. Walipohakikisha kashaondoka, Basto akarudi mezani na kutia chakula tena.

"Dooooh! Yaani natamani arudi saa hivi akukute unavyofakamia" aliongea Malik na kucheka sana. Baston wala hakumjali, aliendelea kufakamia mpaka njaa yake ilipokata.

"Wuuuh!! Afadhali sasa" alijisemea akichezea tumbo lake lililowamba kama ngoma inayopashwa.

"Unaweza kukaa hapa, hii nyumba kubwa mno kwa peke yangu" aliongea Baston akiegemea kochi.

"Ah mi ntatafuta sehemu nyingine ya kukaa, huku ni mbali mno na mara kwa mara ntakuwa nahitajika The Hub"

"Kwanini"

"Kwasasa wewe ndio mwenye kiwango kikubwa cha hisa

katika project mpya ambayo tumekubaliana na mzee Rozaliv. Project zero"

"Ah ushaanza kunichanganya, hebu tumia lugha rahisi" aliongea Baston akionesha dalili za kuchukia. Biashara kwake ni jambo ambalo limemtia kushoto tena mbali, kwake jeshi na vitu ndio vitu pekee anavyojali. "Nakwamabiaje wewe unashikilia asilimia thalathini na moja ya mafao yote yatakayokisanywa mwisho wa mwezi. Katika hizo asilimia kumi na sita zitachukuliwa na mzee Rozaliv kama sehemu ya malipo yake kuhusiana na kuing'arisha henga namba tano" Gruuuuruuuu!!!

Malik akamuangalia Baston ambayo alikuwa kashalala na kukoroma juu. Akamuamsha na kumsindikiza chumbani kisha akatafuta chumba kingine na kuupitisha usiku.

Siku ya pili mapema asubuhi, wote wawili wakatoka na kuelekea henga namba tano ambako tayari baadhi ya watu walishafika kwa ajili ya kufunga vifaa vipya na kufanya marekebisho ya kina katika henga hiyo. Kazi hiyo ilichukuwa karibu mwezi mzima kutokana na kuwa henga hiyo ilikuwa kongwe mno.

"Wiki mbili kutoka sasa ni wakati watu wapya kujiunga na jeshi" aliongea Shanequeen.

"Ndio"

"Tuweke vigezo gani vya kujiunga, ni wazi hatuwezi kuchukuwa kila mtu"

"Hakuna haja ya kuweka vigezo vya kujiunga, ila baada kukubali kujiunga tutafanya mchujo wa ndani. Ila niamini, hatutapata watu wengi, na kwa taarifa nilizozipata hivi karibuni ni kwamba, kuna kikundi kidogo cha wahuni kimekuwa kikitupaka matope"

"Edward"

"Ila usijali, hao wachache watakaojiunga ukiachilia mbali sifa mbaya tunazopewa watakuwa wanatosha. Pia watu wote wanaruhusa kubadilisha henga baada ya kujiunga ndani ya miezi miwili"

Shanequeen akabaki anamkodelea macho Baston, alijaeibu kumsoma bila kuambulia jambo. Ni kama vile alikuwa anaangalia ndani ya kiza kinene.

Wiki mbili baadae.

Kipindi hicho huwa ni kipindi ambacho ukuta namba mbili kunakuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu. Kwasababu watu hutoka maeneo mbali mbali kwa ajili ya kujiunga na jeshi. Henga namba tano ilikuwa mtaa namba tisini, tofauti na kwengine mtaa huo haukuonekana kuwa na watu wengi.

Baston alichukuwa jukumu la kusambaza vipeperushi maeneo mbali mbali. Udahili huwo ulichukuwa wiki mbili nzima nzima kabla ya kuruhusu wadahiliwa kuelekea katika henga husika.

Henga nyingi zilieka vigezo maalum vya kujiunga henga hizo. Kwa mfano henga ambayo ilikuwa inaongozwa na Edward ilitaka wote wanaotaka kujiunga na henga hiyo kuwa uwezo wa daraja B kwenda juu wa kunyonya itherium. Katika vipeperushi vyao waliweka ahadi mbali mbali. Kama vile watakaojiunga watafanikiwa kupata dawa maalum ambayo itawasaidia kuongeza daraja moja juu.

Kwa kufanya hivyo karibia kundi kubwa la watu wenye daraja B walijiunga na henga namba moja. Kila henga iliweka vigezo vyake na faida atakazozipata mtu pindi atakapojiunga na henga hizo isipokuwa henga namba tano tu. Hakukuwa na kigezo chochote cha kujiunga wala hakukutajwa faida atakayoipata ipata mtu pindi atakapojiunga. Chini kabisa ya vipeperushi kulikuwa na sentensi moja tu "yajayo yanafurahisha".

Pia katika kipindi hichi kulikuwa na mfumo wa wanajeshi kuhama kutoka henga moja kwenda nyingine. Na hili lilisababisha wizi wa hali ya juu. Mwanajeshi yeyote ambae alionekana kuwa na kipaji aliwindwa na henga mbali mbali na kuahidiwa mambo makubwa. Wapo walioweza kujizuia ila wengi walivutiwa na kuhama.

Hatimaye wiki mbili za udahi zikaisha na siku ilikua ni siku ya kuripoti katika habari husika mtu aliochagua. Ila mpaka inafika saa sita hakuna hata roho moja iliyokanyaga henga namba tano. Shanequeen alikuwa akizunguka huku na kule, wasiwasi ulikuwa rohoni. Ila alipomuangalia Baston alihisi hasira, mtu huyo alikuwa ametulia akipata sharubati. Hakuonekana kuwa na wasiwasi wa aina yeyote.

Pale Shanequeen alipotaka kutoa donge lake kooni tu, mlango ukasukumwa na vivuli vya watu wawili vikaonekana.

"Wewe mi nilikwambia ni hapa ukajifanya unajua sana, sasa tumezunguka karibia saa nzima"

“Kwenda zako huko, umenambia wakati gani.

Nilipokwambia tuulize wapita ukajiona una akili nyingi"

"Inaweza kuwa mi sina akili nyingine, lakini si kilaza kama wewe"

"Unasema nini wewe", wawili hao wakavamiana na kuanza kutwangana makonde. Ilikuwa ni pata shika nguonika, makonde waliotwangana yalikuwa mazito. Shanequeen alitaka kwenda kuwaamua ila Baston akainua mkono kumuashiaria asifanye hivyo.

Wakati wawili hao wakiendelea kutwangana, watu wengine wakafika na kuwakwepa. Wakaingia ndani, Shanequeen akawapokea na kuwaelekeza sehemu ya kukaa. Mpaka wakati huwo tayari walishafika watu ishirini.

"Inatosha" alinguruma Baston, sauti yake ilikuwa kali sana ikiambatana na tambwe ndefu mno. Mpaka neno inatosha linafikia mwisho tayari alishafika walipo wawili hao. Akawashika na kuwatenganisha kisha akawabeba wote wawili kama vitoto vya paka na kuwapeleka kwenye viti. "Niache, nimesema niache. Nataka nimuue huyu punda" alifoka mmoja wao na kukunja ngumi, kwa kutumia uwezo wake wote akamtandika Baston ya kifua.

Klang!!!

Aaaah!! Alipiga ukwenzi mkali sana huku akiangalia kiganja chake, "bibie kuwa makini, utavunja mkono" aliongea Baston na kuwaweka kwenye viti.
 
Mkuu uliishia kipande cha 13 kwaiy leo tumeanzia 14 na kuendela maana hiko cha 10 ulikiruka kwaiyo wakati unakiweka ndo kikabahatika kuwa cha mwisho kweny post yako hivyo kama kuna uwezekano endelea endelea kidogo maana hapo tuna kipande kimoja tu
 
  • Thanks
Reactions: 511
SEHEMU YA TISA: TAALUMA ILIYOPOTOEA

To the end (mpaka mwisho) 10

Tariq Haji

0624065911

"Kushoto kwako ni Ranger PL6, ni aina ya roboti ambayo inahusika na mashambulizi. Japo uwezo wake wa kujilinda ni mdogo lakini linapokuja suala la mashambulizi linafanya mashambulizi makali na mazito. Lina uwezo wa kufanya mashambulizi ya masafa ya kati na marefu. Uwezo wake wa combat ya karibu ni mdogo"

"Mbele mwisho kabisa ni Doppa next gen, Doppa ni kizazi cha pili kutoka kizazi cha Doppa cha kwanza. Unaweza kusema ni Doppa alieboreshwa zaidi na ni All rounder. Ikiwa na maana anafanya mashambulizi na ulinzi ila nguvu ya mashambulizi ni kubwa kuliko ya ulinzi. Hivyo wanalitumia kama roboti la kufanyia mashambulizi".

"Nimeona mlangi umendikwa sector zero" aliongea Baston. Mzee Rozaliv akatabasamu na kuendea mlango huwo. Haukuwa mkubwa sana, akapitisha kadi sehemu, ukafunguka. Taratibu taa zikapata uhai na kumuliko eneo kubwa kiasi. Ndani humi kulikuwa na roboti chakavu mbali mbali ambazo kwa muonekano tu hazikuwa zimetengezwa na kampuni hiyi.

"Humu tunahifadhi roboti tunazohisi ni za kale, nyingi mimi nimezikuta tu" alifafanua Mzee Rozaliv. Baston akatupa macho yake mwisho kabisa. Yakatua kwenye roboti lililokuwa limeegemezwa ukutani. Lilionekana kuwa na vumbi jingi mno. Mzee Rozaliv akamuangalia Baston kisha akashusha pumzi kabla ya kuongea.

"Lile kule mwisho ni U01 (unknown 01), ni roboti namba moja kati ya mengi yaliyokuwemo humu. Lilikuwa ni roboti la kwanza kuletwa hapa na kutokana na maelezo katika kanzidata inasemekana lilipatikana miaka mia na hamsini iliyopita japo babu zangu waliamini lina miaka zaidi ya tajwa"

Baston akaliangalia kwa makini kisha taratibu akaanza kutembea kulifuata, alipofika akalishika shuka kubwa lililifunika na kulivuta. Chuma cheusi wa manane kilionekana, ni chuma ambacho kikizidi weusi kadri kikivyoakisi mwanga.

"Umesema limepatikana zaidi ya miaka mia na hamsini nyuma, mbona bado chuma chake kinaonekana kipya kabisa bila kuwa na dliki zozote za kuchakaa" alihoji Baston.

"Na hicho nduo kitemdawili kikubwa ambacho waliopita kabka yangu wameshindwa kukitatua, na inaonekana na mimi nitapita kama wao".

Baston akagusa chuma hicho na ghafla kumbukumbu za picha zikaanza kuonekana kichwani mwaka. Aliganda kwa dakika karibu tatu, hakuwa akisikia chochote.

"Baston" alizinduka baada ya kuguswa begani na Malik.

"Mr Rozalive mumewahi kujaribu kuliendesha?" aliuliza

"Ndio ila hakuna rubani aliefanikiwa, linawaka tu lakini halioneshi dalili zozote za uhai".

Baston akatabasamu na kuwageukia, akawaangalia kisha akatikisa kichwa akikumbuka msemo wa kale kuhusu afrika "Afrika ni nchi iliyokalia utajiri wake katika makalio".

"Hili roboti linaitwa Spectre (specta)" alianza kuongea "na lilitambuka kama Spectre the hunter, ni moja miongoni mwa maroboti wachache sana waliotengenezwa na kuonyesha makucha ya kipekee vitani. Rubani wake aliitwa Kamanda Dalia, alikuwa mwanamke pekee katika kikosi cha mstari wa mbele".

"Sifa kubwa ya Kamanda Dalia ilikuwa ni kuwinda Zestra, vitani hakutulia mstari wa mbele bali aliingia katikati ya kundi la Zestra na kuwawinda. Alikuwa ni kama simba mfalme wa porini, hakusikiliza amri ya mtu mwengine yeyote. Sifa zakw zilifika mbali mno, hata katika ulimwengu wa Zestra alitambulika vyema".

"Ila jwa bahati mbaya alikufa kwa ugonjwa usiojulikana na tokea siku hiyo hakuna mtu mwingine aliewezesha kuendesha Spectre na hivyo likapotea katika wakati" alipomaliza kauli hiyo, mtikisiko mdogo ukasikika.

Macho ya Spectre yakafunguka na rangi nyekundu ikaonekan, "kwanini una sonono" aliuliza Baston akiingalia mashne hiyo machoni.

"Dalia hakufa kwa ugonjwa, alichomwa sindano ya sumu" mara akasikia sauti katika kichwa chake. Hali kama hiyo ilitokea alipokutana na Gilbot, roboti zote mbili zilikuwa na akili ya kwao.

"Unataka kurudi vitani?"

"Ndio, nitarudi endapo utanisikiliza ombi langu"

"Ombi gani"

"Nataka aliehusika na kifo cha Dalia ahukumiwe ili kupoza roho ya rafiki yangu".

"Ila ni miaka mingi sana imepita, sidhani kama mtu huyo atakuwa hai mpaka sasa"

"Hhhmf!! Atakuwa hai tu kwasababu sio mtu wa kawaida baki ni zao kati ya binadamu na Zestra"

Maongezi hayo yalifanyika kupitia njia maalum ya kimawazo, hakuna sauti iliyotoka. Wengine walikuwa wakimuona Baston akiliangalia roboti hilo bila kuongea jambo.

"Nitakuchukuwa vitani, sijui kama nitaweza kufikia kiwango cha Kamanda Dalia, ila nina uhakika utaishi vizuri siku zako za mwisho. Na kuhusu kifo chake, usijali nitahakikisha nachimba siri zote. Hata mimi nina mashaka kuwa katika safu ya uongozi wa juu wa binadamu kuna wavamizi ambao wameweza kupata vyeo baada ya kuvaa sura za binadamu"

Chozi jicho la kushoto la Baston likachuruzika, wote wakashangaa.

"Hivi mnaamini baada ya mida flani kupita hata roboti anatengeneza hisia" aliongea akiwaangalia.

"Hayo ni maneno tu ila hawayajawahi kuthibitishwa" alijibu profesa Ashdawi.

"Ni kwasababu marubani wengi wanachukulia roboti kama mashine za kivita tu, wanakosa muunganiko wa hisia. Profesa Bagani najua unafahamu ninachokiongea. Silaha kubwa kwa binadamu ni hisia zake na ndio maana tukatofautiana na jamii nyingi"

"Hapana si kweli" alijibu profesa Ashdawi kabla ya profesa Bagani kuongea

"Ni kweli anachokiongea Baston, silaha kubwa ya binadamu ni hisia zake lakini pia hisia hizo kwa kuwa chanzo cha maangamizi yake. Mfano kwanini mwanajeshi anakwenda vitani, ni maana anajua kutokwenda kwake kutekeleza kukawaangamiza waliookoa nyuma yake. Lakini sioni muunganishi kati ya hisia hizo nanini. roboti hilo wengi wamwshindwa kuliendesha" alifafanua profesa Bagani.

"Mr Rozaliv natumai katika wakati wako wa vitu mbali mbali umepata almasi ya damu" aliuliza Baston.

"Ndio"

"Unaweza ukaichonga" aliongea Baston na kutoa vipimo vyote.

"Kwanini"

"Kwasababu Specter walikuwa roboti la kwanza na la pekee kutumia moyo" alijibu. Hapo sasa Mr Rozaliv akashtuka, kichwani alikuwa na swali siku zote alipoangalia upande wa kushoto wa roboti hilo. Kuliko na shimo mbali halikuwa likielezeka.

Papo hapo akagisa comlink yake na kutafuta namba kisha akapiga, akatoa yote kisha akakata. Baada ya nusu saa akafika mtu akiwa na chombo fulani na kumkabidhi. Mr Rozaliv akatoa almasi ya dhahabu ambayo tayari ilishachongwa na kumrushia Baston.

Nae akapanda mpaka katika kifua cha Specter na kuitumbukiza, kisha akaponyeza sehemu na mlango wa kuingilia eneo la rubani ukafunguka, akaingia. Mr Rozalive akabonyeza sehemu na mlango mkubwa ukafunguka. Ndani ya chumba hicho chumba na mashine kubwa ya kubebea roboti, ikabeba Specter na kulipeleka eneo la ujumbe. Ulikuwa ni uwanja mkubwa sana uliokuwa umezungukwa na kuta ndefu mno.

Akiwa ndani humo Baston akaangalia muundo wa cockpit, akaangalia kushoto na kulia kisha akabonyeza kitufe fulani. Kofia kubwa ya chuma ikashuka na kuingia kichwani mwake.

Muunganisho wa Neural umeanzishwa

Inapakia data kwa majaribio mapya

nyingi zikaanza kuingia katika ubongo wa Baston, ikikuwa shughuli yenye maumivu mno. Lakini alivumilia wakati huo huo alikuwa akirithi taaluma ya kamanda Dalia pamoja na baadhi ya kumbukumbu zake ambazo zimehifadhiwa katika roboti hilo.

********
kumi hii hapa
 
Back
Top Bottom