Riwaya: To the End (Mpaka Mwisho)

Riwaya: To the End (Mpaka Mwisho)

To the end (mpaka mwisho) 20

"Nahodha Baston, tunaweza kukufuata" aliongea Cleyman, alipofika alipokuwa Baston.

"Mumewahi kupambana na Zestra daraja la komando" aliuliza.

"Hapana, sisi tutashighulika na hawa wengine tu"

"Hahaha! Hao wengine achieni watoto, nifuateni ninyi mnastahili mazuri zaidi" aliongea Baston. Nahodha Cleyman akasisimka kidogo, katika maisha yake hakuwahi kupambana na Zestra daraja la komando. Ilitambulika kwa wengine kuwa, malipo yalitokana na daraja la Zestra.

Hivyo wale Zestra wa kawaida, ambao walikuwa sawa na wanajeshi wakawaida tu. Walikuwa na malipo madogo, na mtu hakupata cheo chochote. Lakini haikuwa hivyo kuanzia daraja la komando. Daraja la komando lilikuwa gumu kwa wanajeshi wengi, hivyo kuuwa hata mmoja tu malipo yake yalikuwa makubwa sana na kulikuwa na uwezekano wa mtu kupanda daraja.

"Wanaumeeeee, mnataka kua"

"Aye" lilikuwa ni kundi la watu ishirini ukichanganya na nahodha wao, ila tokea walipojiunga na jeshi mpaka kuingia katika kundi la maveterani hawakuwahi kuuwa Zestra daraja la komando.

"Nyinyi tumieni mmifumo yenu mlioizoea, mimi nitakuwa nalishighulisha hili dudu. Kumbukeni, kila shambulizi mtakalolifanya, lifanywe na lengo la kuuwa. Mengine sitaki kuongea sana, najua mumekuwa vitani kwa muda mrefu hivyo mnaelewa cha kufanya" aliongea Baston.

Nahodha Cleyman na kikosi chake wakaanza mashambulizi, Baston yeye alikuwa akifanya mashambulizi makali katika maeneo ambayo yalikuwa ndio ni sehemu dhaifu kwa kiumbe huyo. Kuna wakati alichomekea na kulinda, kwa kufanya hivyo kazi ilipungua sana kwa wengine.

Hatimaye baada ya dakika arobaini na tano kupita, wakafanikiwa kumuua. Wakati wakivuta pumzi, ghafla hisia mbaya zikamfia Baston.

"Kimbieni kuelekea ngomeni, daraja la jenerali" aliongea kwa kelele na kufungua ngao maalum iliyotengezwa kwa chembechembe za itherium.

Boom!!!

Mlio mkali ukasikika, na Baston akarushwa mita kadhaa nyuma. Cleyman na wengine walikuwa vetarani wa kivita, hivyo ule ukwenzi mmoja tu ulitosha kuwafanya watii amri hiyo pasi na kufikiri.

"Nahodha Baston, vipi kuhusu wewe" aliongea Cleyman

"Naweza kuokoa maisha yangu, nyinyi endeleeni kurudi nyuma, mimi nitawalinda" aliongea Baston, wakati huwo misuli ya mwili mzima ikiwa imetuna.

Spectre alikuwa akirudi nyuma taratibu huku akihakikisha uslana wa roboti zilizotangulia. Haikuwa kazi rahisi, tayari ngao yake ilishapungua kwa asilimia sabini. Asilimia thalathini zilizobaki zilikuwa na uwezo wa kuzuia makombora mawili tu ya Zestra. Baada ya hapo Spectre angebakia uchi. Maana nyingine angekuwa na asilimia kubwa ya kupoteza maisha.

"Kwanini unarudi nyuma" swali lilitoka kwa Spectre

"Unadhani daraja la jenetali ni mchezo mchezo" alijibu Baston

"Hahaha, kama uwezo ndio huu na wewe huna tofauti na wengine, mashujaa walikuwa wanakwenda mbele tu. Kurudi nyuma ilikuwa ni baada ya ushindi. Mtu lazima awe msimamo, msimamo wako wewe ni kwenda mbele inapostahi na kurudi nyuma inapostahiki" alikejeli Spectre.

Akaendelea "usiwe kama mnazi, unakwenda unapokwenda upepo, kuwa kama jabali haijalishi upepo unakwenda kwa kasi gani na upande gani, huyumbishwi". Kila neno lilitoka kwa Spectre lilimtia Baston hasira.

Pasi na mategeneo ya wengi, Baston akasimama kugeuka. Wengi wakapigwa na butwaa. "Sawa umeshinda, umefanikiwa kunitia ghadhabu. Nakwenda kupambana nae mpaka mwisho, ama nife mimi au aaunguke yeye" aliongea viini vyake vya macho vikiwa vyekundu mithili ya damu ya mzee.

Akazima ngao yake na kuchomoa visu vyake, taratibu vikaanza kuwa vyekundu. Macho ya Spectre yakabadilika rangi na kuwa mekundu.

Fwoosh!!!

Moshi mwingi ukatoka katika maungio ya roboti hilo, na mashine ikaenda katika ukimya. Hakukuwa na mngurumo wowote ule. Wakati huwo kulikuwa na mita kama mia tano baina ya Baston na adui yake.

"Twende asilimia mia moja", mishipa yake ikatuna na kuanza kusafirisha damu kwa wingi. Sehemu ya mabega ya Spectre ikafunguka na bomba mbili ndefu kiasi cha mita moja kasoro kidogo zikachomoza. Vyuma vya roboti hilo vikaanza kutikisika na kujipanga upya.

Mistari mikundu mingi ikaanza kuonekana katika mwili wa Spectre, rangi nyekundu hiyo ilionekana vyema japo wakati huwo ilikuwa kweupe. Yote hayo yalitokea kwa sekunde chache.

Grruuuuuuuuuu!!!

Zestra akanguruma na kuanza kukimbia alipo baston, kasi yake haikuwa kubwa sana lakini ilitosha kutuma ujume kuwa kiumbe hicho kilikuwa kimekasirika haswa.

Aaaaaaaaaaaaaahhhhh!!!

Baston nae akanguruma kabla ya Spectre kufyetuka, kasi yakw ilikuwa mara mbili ya Zestra. Mpaka hapo wengi wakajua kabisa kuwa Baston amewehuka. Itambulike kuwa hata wale wa kikosi cha makomando hawakuwa na uwezo wa kupambana Zestra wa daraja la Jenerali bila kuwepo zaidi ya watano.

"Baston unafanya nini?" alijisemea Shanequeen akikunja ngumi, jasho lilikuwa likimtoka. Hakuwa peke yake, wengi walikuwa kama yeye ila wao walihofia maisha tu isipokuwa Shanequeen alihofia kumpoteza mwanaume wake.

Haaaa!!!

Wengi wakamaka baada ya Baston kuamua kutumia visu, alikuwa anakwenda kwa vita ya karibu. Walipokaribia tu mdomo wa Zestra ukafunguka, muonzi mkali ukatoka. Baston akanesa kushoto na kuzunguka kwa kasi akitengeza alama ya nusu mwezi. Muonzi huwo ukamkosa kwa milimita chache sana.

Na kasi yake hiyo hiyo, akazunguka tena na kuachia teke kali sana lilitua katika mwili wa kiumbe huyo. Wote wawili wakarudi nyuma kwa kasi, ila pasi na mategemeo ya wengi kwamba Spectre angesimama.

Mgongo wa Spectre ukafunguka, bomba mbili nene kiasi zikaonekana.

Boom!!!

Moto ukatoka katika bomba hizo, zikalala kushoto. Spectre akasogea pembeni kidogo, mionzi mingine ikamkosa kwa sentimita kama moja hivu.

Fwooooooshhh!!

Moshi mweupe ukatoka katika zilw bomba zilizokuwa mabegani, mgongo wa Spectre ukajifunga. Baston akaendelea na kasi hiyo hiyo, visu viwili vyekundu mkononu. Akamavaa tena Zestra.

Klang!!!

Ni kama vile vyuma viwili vyenye kasi vilikutana na kusababisha mtikisiko mkubwa. Spectre akarudi tena nyuma kwa kasi.

Puhwak!!!

Baston akatpita damu, alihisi utumbo wake wote ukiparaganywa. Funda la pili la damu lilikuwa linakuja, akakaza shingo na kulirudisha tumboni. Laiti Zestra angejua kama alifanikiwa kumkasirisha Baston kiasi cha kutoka moshi kichwani, angekimbia.

Umbali wa mita thalathini kutoka alipo Zestra, Spectre alikuwa amesimama kama mlima. Ni kama vile alikuwa akimwambi "leo ni leo, afe punda afe muendesha punda, mzigo wa bwana lazima ufike".

Zestra akakita miguu yake chini, mdomo wake ukaanza kurefuka. Hata yeye mwenyewe alihisi kitisho kutoka kwa roboti hilo jeusi lenye mistari mekundu.

Vrrruuummmm!!!

Kwa mara nyingine tena mngurumo wa mashine ukasikia kutoka kwa Spectre. Waangaliaji wote wakajua kila upande ulikuwa unajipanga kufanya shambulizi ambalo lingeamua hatma ya pambano hilo.

Fyuuum!!

Ulisikika mlio mwemba kisha kimya kikatawala, bila matarajio waangaliaji wote wakabana pumzi. Mji mzima ulizizima, sauti ya upepo laini tu ndio iliyosikika.

Katuuum!!!!

Mlio mkali ukasikika ukifuatiwa na mtikisiko mkubwa na mwanga mkali, hakuna aliejua nini kimetokea lakini wengi waliomini pambano hilo lilikuwa limekwisha.
 
To the end (mpaka mwisho) 21

Baada ya dakika nzima kupita mwanga mkali ukaanza kutoweka, kwa mbali kikaonekana kivuli kikubwa kikiwa kimesimama. Upande wa kushto wa mwili wa juu wa kivuli hicho ulikuwa haupo, katika bega la kulia la kivuli hicho kulikuwa na kivuli kingine ambacho kilikuwa na umbile la mtu.

Wawili hao hawakuwa wengine isipokuwa Baston na Spectre, mtu na roboti lake. Imekuwa heshima kubwa sana kwa mimi kupambana upande kwa upande na wewe ila nasikitika inabidi ushirikiano wetu utamatikie hapa ilikuwa ni sauti iliotoka kwa kukata kata, ni wazi kabisa asilimia kubwa ya mfumo wa Spectre ulikuwa umeharibika.

Hata kwangu imekuwa heshima kubwa sana, wengine hawawezi kuelewa ila mimi naelewa alijibu Baston.

Ni wazi kwamba hakuna kiumbe anaeweza kukwepa makucha ya wakati, ingekuwa ni miaka mia tatu iliyopita shambulia la namna hii lisingeweza hata kuacha alama za michubuko katika mwili wangu ni wazi Spectre hakuwa tayari kutengana na Baston lakini kila kilichokuwa na mwanzo lazima kiwe na mwisho.

Najua hutaki kwenda bila kuaga sawa sawa, unaweza ukaounguza ukubwa wa visu. Nataka nikusindikze na roho kadhaa za Zestra. Ukikutana na Gilbot huko mwambie kama, ameacha uruthi nyuma hivyo apumzike kwa amani aliongea Baston na kuruka kutoka katika bega la roboti hilo na kutua ardhini kwa kishindo.

Visu ambavyo vilikuwa ardhini vikaanza kuoungua ukubwa, Baston akavibeba na kutikisa mikono kupima uzito wa visu ambavyo vilikuwa kama panga nyeusi. Rafiki fumbua macho yako na uwende kwa amani aliongea Baston na kutabasamu ambalo halikuwa tabasamu. Karibu mita mia kutoka alipo Baston, Cleyman na kikosi chake walikuwa wamesimama. Kamera zao zilifanikiwa kumvuta Baston karibu na kufanikiwa kuona tabasamu. Baridi kali mno ilitambaa katika migongo yao, kwa pamoja wote wakameza funda kubwa mate.

Haaaaaaaaaaaa!!!

Alipiga kelele na nguo yake ikaachanika na kuonesha kifua kilichojijenga kama matofali ya chuma, kwa ajili ya mashujaa wote alinguruma kwa nguvu na kufyetuka kama risasi.

Kwa ajili ya mashujaa wote Cleyman nae akanguruma na kulisukuma roboti lake mpaka katika kiwango cha juu kabisa mashine hiyoinayoweza kuhimili.

Kwa ajili ya mashujaa wote kikosi chake chote kikanguruma juu ya mapafu yao na kuzisukuma mashine mashine zao mpaka mwisho. Roboti ambazo zilionekana kuwa kama wafu wakati huwo zikapata uhai.

Vrruuuuuummm!!!!

Zikanguruma na kuanza kukimbia kuelekea alipo Baston, roho ya kivita ilikuwa imeamka katika miili ya watu hao, Binadamu mmoja na roboti ishirini kila walipopita waliacha mizoga. Baston alikuwa kama mungu wa vita alieshuka duniani na kuwapa watu hisia za kutaka kuabudu. Lakini hizo zilikuwa hisia tu, kila mtu alikuwa anaamini katika mungu wake.

Boom!!!

Booom!!

Booom!!

Milipuko ya hapa na pale ikaendelea kusikika, kwa zaidi ya dakika arobaini na tano, mti mmoja na roboti ishirini waliendelea kusababisha maafa kwa Zestra. Na kwa mara ya kwanza katika miaka mingi, hakuna Zestra aliefanitikiwa kutoroka chini ya kipigo cha maangamizi kutoka kwa watu hao. Mpaka wanafika katika eneo la mita mia mbili za ngome ndipo wakasimama, wote kwa pamoja wakageuka alipokuwa Spectre na kutoa saluti ya kuaga.

Kitu cha ajabu kilichotokea ni kwamba Spectre alijibu saluti hiyo kabla ya kusambaratika na kupotea hewa. Mwisho wa roboti hilo lililoishi kwa karibia miaka mia tatu ukawa umefika, lakini simulizi yake itabaki na kusimuliwa kizazi hadi kizazi. Zestra waliobakia walikuwa wakimalizwa na wanajeshi wengine.

Milango ya roboti ishirini ikafunguka, marubani wake wakashuka na kusimama mbele ya Baston kisha wakapiga saluti. Umetukumbusha enzi ambazo tulikuwa tunazurura katika uwanja wa vita bila sheria, pokea heshima zetu aliongea Cleyman.

Natamani hata mimi ningeishi katika wakati wenu, siku hizi wengi ni waoga alijibu Baston na kurudisha saluti hiyo. Vifunikio vyake vya macho vikaanza kuwa vizito, waaa! Akapiga miayayo na kufikicha macho. Alijitahidi kuyazuia macho yake yasifumbe lakini bila mafanikio.

Nahisi usiiiiingii.. hata hakumalizia akaanza kukoroma, alilala hali ya kuwa amesimama jambo ambalo liliwashangaza wengi. Na wala hakuwa akipepesuka, alikuwa kama jabali. Watu wa afya wakafika na machela na kumlaza kisha wakaondoka. Lakini Cleyman akafinya macho, alihsi kuna jambo halipo sawa lakini hakuwa na jinsi kwa sababu hilo lilikuwa nje ya uwezo wake.

************

Ndani ya jengo kubwa la hospitali ya kijeshi, Baston alikuwa amelazwa katika kitanda akiwa amebadilishwa nguo na kuvikwa gauni la wagonjwa. Madaktari wengi walikuwa wamemzunguka, walionekana kama simba waliozunguka kitoweo. Kila mmoja alitaka kujua siri zilizo katika mwili wa Baston zilizomfanya aweze kuoambana na Zestra bila kutumia roboti.

Mmoja wao akachukuwa sindano na kutaka kuchukuwa damu, sindano hiyo ilipogusa mwili wa Baston ikapinda na alipolazimisha ikakatika. Wakatoa macho!! Akachukua sindano nyingine ambayo ilikuwa stadi zaidi lakini matokeo yakawa yale yale. Walijaribu kila aina ya sindano lakini hakuwa sindano iliyofanikiwa kuacha hata mchumbuko katika mwili wa Baston.

Madaktari hao hawakuwa tayari kushindwa, wakachuku mashine maalum inayotumika kutobole mifupa drili, nayo ikazunguka mpaka msumari ukawa butu lakini haikupenya katika ngozi ya Baston. Wakaishiwa pozi na kuangaliana, hawakujua nini kinaendelea kwa sababu hawakuwahi kukutana na hali kama hiyo.

Inaonekana mwili wake uko katika hali ya ulinzi, hakuna kitakachokuwa mpaka pale atakapoamka

Lakini unadhani atakubali akiamka

Lazima akubali ikiwezekana tutamtoa jeshini na kumuingiza maabara awe sampuli

Hehehe!!! Hata asipokubali, itabidi tu aingie maabara. Sampuli kama hii ni vyema ikaishi maabara kwa ajili ya mafanikio ya binadamu wote

Madaktari hao walikuwa walijadiliana na kuweka sababu nyingi ila lengo lao kubwa lilikuwa ni kumfanya awe chambo katika kukata kiu yao. Jambo ambalo hawakulitambua ni kwamba Baston alikuwa akisikia mazungumzo yao yote japo alikuwa katika usingizi mzito.

Kumbuka siri zote ulizojifunza usizitoe mpaka pale utakapokuwa na uwezo wa kujilinda na kuwalinda wale walio karibu yake, akakurupuka kutoka ungizini na kujikuta ndani ya chumba kilichokuwa na rangi nyeupe.

Mwilini alikuwa amevisha gauni jeupe, moja kwa moja akagundua kuwa alikuwa maabara, sekunde chache baada kuamka mlango ukafunguliwa. Watu wanne wakaingia wakiwa ndani ya mavazi meupe na kusimama mbele yake. Mmoja wao akapita mbele na kuweka karatasi na kalamu katika meza iliyookuwemo humo.

Kuanzia hivi sasa, umevuliwa madaraka yote ya kijeshi. Unatakiwa utoe ushirikiano kwa asilimia mia moja katika ndaki ya sayansi na tiba. Huu ni mkataba, unatakiwa uweke sahihi yako aliongea mtu huyo. Baston akaibeba ile karatasi na kuichana kisha akawaangalia na kuachia tabasamu ambalo liliwaambia mnakijua kifo nyinyi au mnadhani siwezi kuwachambua. Madaktari wote wakarudi nyuma bila kutegemea, waliisikio mioyo yao ikidunda katika masikio yao, na hiyo ilikuwa ni kama ishara ya kifo kwao.
 
Nakubali kazi zako mkuu
 
ajili ya kubadili nguo.

To the end (mpaka mwisho) 23

Tariq Haji

0624065911

Nusu saa baadae

Mlangp mkubwa wa kuingilia katika ukumbi wa mikutano ulifunguliwa, akatangulia Shanequeen akiwa katika vazo tofauti na lile alilokuwa nalo mwanzo. Kichwani alikuwa na kofia aina ya kapelo yenye kipaa kifupi. Sehemu ya mbele ya kofia hiyo kulikuwa na duara kubwa. Ndani ya duara hilo kulikuwa na herufi K.

Pande zote mbili za duara hilo kulikuwa na mistari miwili mirefu na watatu ulikuwa nusu. Katika mabega yake kulining'inia koti lililokaribia vifundo vya miguu. Katika pande zote mbili za mabega yake kulikuwa na kama kiraka cheusi kilichoshonwa kwa ustadi wa hali ya juu. Katika upande wake wa kushoto kulining'inia medani mbili za dhahabu na moja ya shaba katika shati aliyoivaa.

Chini alivaa suruali nyeupe, iliofanana na shati yake na miguuni alikuwa na viatu vyeusi. Alitembea kikakamavu mpaka alipofika karibu na jukwaa. Hakupanda, badala yake akasimama pembeni na kufunguka mguu.

"Dragon Soul Komando Baston" akaongea kwa sauti ya juu, mlango ukasukumwa. Kimya kikatawala kiasi ambacho hata kama sindano ingeanguka basi ingesikilikana. Wote walibana pumzi na wala hakuna aliethubutu kuiachia.

Koh!

Koh!

Koh!

Hatua za taratibu zikasikika, zilikuwa nzito na zenye kufanana. Baada ya sekunde mbili akaonekana Baston akiwa katika vazi lake jipya baada ya kupandishwa cheo. Kichwani alikuwa na kapelo iliyofanana na ile ya Shanequeen lakini yake ilikuwa ilikuwa na mistari mitatu iliofanana kwa urefu na yenye rangi ya dhahabu.

Mabegani kwake lilining'inia koti lililokuwa na kiraka cheusi katika pande zote mbili. Isipokuwa vilikuwa vya dhahabu na upande wa kushoto iling'inia kamba nene ya dhahabu iliozunguka chini ya kwapa. Katika shati lake upande wa kushoto kifuani kuling'inia medani tatu za dhahabu.

Chini alivaa suruali lakini mkanda wake ulikuwa wa dhahabu, viatu vyeusi vilivyodariziwa na mistari kadhaa ya dhahabu. Alipofika jukwaani akapanda na nyuma yake akafuata Shanequeen. Aliposimama na kuwaangalia watu waliokaa, wote wakasimama na kutoa heshima.

Baston akaipokea heshima hiyo na kuwarudishia kisha akawapa ishara ya kukaa. Shanequeen alikuwa amesimama pembeni yake.

"Hili vazi kwa wengi linaweza kuwa lina maana kubwa mno, lakini kwangu si chochote si lolote. Wanaoliona lina maana ni kutaka kujionesha kuwa na cheo kikubwa. Mimi leo nimelivaa kwasababu ni wajibu lakini halijabadilisha jambo. Nina uhakika ipo siku wengi wenu mtalivaa pia" aliongea.

Watu wote waliokuwa wanamsikiliza walimuangalia kwa mshangao, nani aliekuwa hataki kuonekana amepiga hatua katika jeshi. Lakini kauli ya Baston ilitosha kuwaeleza kuwa yeye hakujali kabisa umuhimu wa vazi hilo.

"Kabla hatujaendelea nataka watu wote mtambue uwepo wa maveterani kati yetu, watu hawa wamepambana bega kwa bega na mimi Baston na wameonesha ukomavu wa hali ya juu sana. Kwa hilo tu mimi Baston nawapa heshima kutoka katika kina cha moyo wangu" alipomaliza akafunga mguu na kutoa saluti.

Cleyman akasimama japo hakutaka lakini alijuwa kuwa Baston aliipandisha thamani yao mbele ya watu wengi. Maveterani hawakuwa na umuhimu sana katika ngome hiyo, kwa wengi walikuwa ni wanajeshi walioshindwa kupanda cheo baada ya kutumikia jeshi kwa muda mrefu hivyo kuonekana kuwa ni watu wa kiwango cha chini zaidi. Na watu wengi waliwadharau.

"Cleyman, kama kuna jambo unataka kusema ni wakati wako kwasababu maongezi yatakayofuata yatakuwa ni ya wahusika tu" aliongea Baston, sauti yake ilikuwa na kina kama kisima cha kale kisichoonekana mwisho wake.

"Nina jambo nataka kuongea, baada ya ya kujadiliana na wenzangu wote tulioshirikia katika vita siku ya nyuma. Tumefikia maamuzi ya kuomba kujiunga na henga namba tano. Hata kama itakuwa hatutakwenda vitani, ni kwa mara ya kwanza ametokea mtu na kutuchukulia kama binadamu na sio vyambo. Na kwa niaba ya wenzangu, pokea hii saluti" aliongea Cleyman na kufunga mguu. "Mnajua kwa kufanya hivyo mtapoteza mafao yenu yote mliyotakiwa kuyapata baada ya kukamilisha kazi ya juzi?" Baston aliipokea saluti ile na kisha akatupa swali.

"Mafao yana faida gani ikiwa bado katika macho ya wengi tunaonekana kama wanyama tu. Hatutaki mafao sisi, furaha yetu ni kumfuata mtu ambaye atazifanya damu zetu zichemke na mtu hiyo si mwingine isipokuwa wewe"

"Vyema, baada ya leo nitawapa siku tatu za kuagana na familia zenu. Mtahamia katika henga namba tano na kuungana na wengine. Ila niseme mambo ya muhimu mapema, kwanza inabidi mkubali kama umri wenu umeenda. Hivyo ni wachache sana wataweza kuvuka kiunzi hichi na kufika mbali. Pili kwangu mimi hakuna tofauti kati ya veterani na mwanajeshi wa kawaida, kifurushi ni kile kile kama kwa wengine"

"Tatu hamtakuwa faida juu ya wengine, nyote mtakuwa ndugu katika jeshi, hakutakuwa na tofauti kati ya umri. Hakutakuwa na utofauti katika uwezo. Hakutakuwa na madaraja ya chochote kile, narudia kwangu mimi. Nyinyi

na wengine nyote mtakuwa sawa"

"Sisi tunataka tukufuate wewe, sheria zako zitakuwa lazima kwetu hivyo hatutakuwa na lawama zozote" aliongea Cleyman.

"Sawa, sasa nataka niongee mambo machache"

"Moja; ndani ya wiki mbili tutapokea roboti ishirini na nne. Kati ya hizo ishirini na nne mbili tayari zina wamiliki. Ishirini na mbili zitakazobaki zitakuwa na wachache miongoni mwenu. Ikumbukwe roboti hizo ni maalum kwa watu watakaokuwa wanaenda vitani. Na hazitatolewa kwa kujuana, kutakuwa na mashindano maalum na washindi watapata nafasi ya upendeleo ya kuchagua roboti lake"

"Mbili; kila mtu anatakiwa ajitathmini nafasiba anayoiweza vizuri ili kusudi kila mtu awe na nafasi sawa na mwingine. Natumai nafasi zote zinatambulika na sifa za wenyewe nafasi hizo pia"

"Tatu, miezi mitatu kutoka sasa, isipokuwa walw ambao watakuwa hawahusiki moja kwa moja na uwanja wa vita. Wote waliobaki tutakwenda nje ya ngome kwa ajili ya maoezi yatakayodumu kwa zaidi ya mwaka na nusu" "Nne; kundi la madaktari na wale wa mipango baada ya miezi mitatu nyote mtakwenda katika vyuo husika kwa ajili kusoma. Makundi haya mawiki mtatakiwa mjifunze na kukuza taaluma yenu kwa kasi sana. Huenda ikawa hamuendi uwanjani lakini vifo vingi vitakavyotokea, mtaulizwa nyie"

"Tano na mwisho kabisa, baada ya kikao hichi wale wa kikundi cha ukusanyaji mtabakia" alimaliza kuongea na hakuna alieuliza swali lolote. Baada ya dakika ukumbi wote ukawa mtupu isipokuwa watu wachache waliosimama mbele ya Baston kikakamavu.

Watu kumi na nane na kundi la intelijensia walikuwa wamesimama, nyuso zao zikionesha wasiwasi. Kwasababu hakuna aliefahamu kwanini waliambiwa wabakia. Swali hilo lilikuwa katika kila kichwa cha mmoja wao. Lakini wote hao hawakuwa wakitambua uwepo wa mtu mmoja aliekuwa na umbile dogo. Alikuwa mbele yao lakini ni kama alikuwa hayupo kabisa.
 
Fupiii😭😭😭
 
Back
Top Bottom