THE SPIRIT THINKER
JF-Expert Member
- Sep 9, 2019
- 419
- 652
- Thread starter
- #61
To the end (mpaka mwisho) 20
"Nahodha Baston, tunaweza kukufuata" aliongea Cleyman, alipofika alipokuwa Baston.
"Mumewahi kupambana na Zestra daraja la komando" aliuliza.
"Hapana, sisi tutashighulika na hawa wengine tu"
"Hahaha! Hao wengine achieni watoto, nifuateni ninyi mnastahili mazuri zaidi" aliongea Baston. Nahodha Cleyman akasisimka kidogo, katika maisha yake hakuwahi kupambana na Zestra daraja la komando. Ilitambulika kwa wengine kuwa, malipo yalitokana na daraja la Zestra.
Hivyo wale Zestra wa kawaida, ambao walikuwa sawa na wanajeshi wakawaida tu. Walikuwa na malipo madogo, na mtu hakupata cheo chochote. Lakini haikuwa hivyo kuanzia daraja la komando. Daraja la komando lilikuwa gumu kwa wanajeshi wengi, hivyo kuuwa hata mmoja tu malipo yake yalikuwa makubwa sana na kulikuwa na uwezekano wa mtu kupanda daraja.
"Wanaumeeeee, mnataka kua"
"Aye" lilikuwa ni kundi la watu ishirini ukichanganya na nahodha wao, ila tokea walipojiunga na jeshi mpaka kuingia katika kundi la maveterani hawakuwahi kuuwa Zestra daraja la komando.
"Nyinyi tumieni mmifumo yenu mlioizoea, mimi nitakuwa nalishighulisha hili dudu. Kumbukeni, kila shambulizi mtakalolifanya, lifanywe na lengo la kuuwa. Mengine sitaki kuongea sana, najua mumekuwa vitani kwa muda mrefu hivyo mnaelewa cha kufanya" aliongea Baston.
Nahodha Cleyman na kikosi chake wakaanza mashambulizi, Baston yeye alikuwa akifanya mashambulizi makali katika maeneo ambayo yalikuwa ndio ni sehemu dhaifu kwa kiumbe huyo. Kuna wakati alichomekea na kulinda, kwa kufanya hivyo kazi ilipungua sana kwa wengine.
Hatimaye baada ya dakika arobaini na tano kupita, wakafanikiwa kumuua. Wakati wakivuta pumzi, ghafla hisia mbaya zikamfia Baston.
"Kimbieni kuelekea ngomeni, daraja la jenerali" aliongea kwa kelele na kufungua ngao maalum iliyotengezwa kwa chembechembe za itherium.
Boom!!!
Mlio mkali ukasikika, na Baston akarushwa mita kadhaa nyuma. Cleyman na wengine walikuwa vetarani wa kivita, hivyo ule ukwenzi mmoja tu ulitosha kuwafanya watii amri hiyo pasi na kufikiri.
"Nahodha Baston, vipi kuhusu wewe" aliongea Cleyman
"Naweza kuokoa maisha yangu, nyinyi endeleeni kurudi nyuma, mimi nitawalinda" aliongea Baston, wakati huwo misuli ya mwili mzima ikiwa imetuna.
Spectre alikuwa akirudi nyuma taratibu huku akihakikisha uslana wa roboti zilizotangulia. Haikuwa kazi rahisi, tayari ngao yake ilishapungua kwa asilimia sabini. Asilimia thalathini zilizobaki zilikuwa na uwezo wa kuzuia makombora mawili tu ya Zestra. Baada ya hapo Spectre angebakia uchi. Maana nyingine angekuwa na asilimia kubwa ya kupoteza maisha.
"Kwanini unarudi nyuma" swali lilitoka kwa Spectre
"Unadhani daraja la jenetali ni mchezo mchezo" alijibu Baston
"Hahaha, kama uwezo ndio huu na wewe huna tofauti na wengine, mashujaa walikuwa wanakwenda mbele tu. Kurudi nyuma ilikuwa ni baada ya ushindi. Mtu lazima awe msimamo, msimamo wako wewe ni kwenda mbele inapostahi na kurudi nyuma inapostahiki" alikejeli Spectre.
Akaendelea "usiwe kama mnazi, unakwenda unapokwenda upepo, kuwa kama jabali haijalishi upepo unakwenda kwa kasi gani na upande gani, huyumbishwi". Kila neno lilitoka kwa Spectre lilimtia Baston hasira.
Pasi na mategeneo ya wengi, Baston akasimama kugeuka. Wengi wakapigwa na butwaa. "Sawa umeshinda, umefanikiwa kunitia ghadhabu. Nakwenda kupambana nae mpaka mwisho, ama nife mimi au aaunguke yeye" aliongea viini vyake vya macho vikiwa vyekundu mithili ya damu ya mzee.
Akazima ngao yake na kuchomoa visu vyake, taratibu vikaanza kuwa vyekundu. Macho ya Spectre yakabadilika rangi na kuwa mekundu.
Fwoosh!!!
Moshi mwingi ukatoka katika maungio ya roboti hilo, na mashine ikaenda katika ukimya. Hakukuwa na mngurumo wowote ule. Wakati huwo kulikuwa na mita kama mia tano baina ya Baston na adui yake.
"Twende asilimia mia moja", mishipa yake ikatuna na kuanza kusafirisha damu kwa wingi. Sehemu ya mabega ya Spectre ikafunguka na bomba mbili ndefu kiasi cha mita moja kasoro kidogo zikachomoza. Vyuma vya roboti hilo vikaanza kutikisika na kujipanga upya.
Mistari mikundu mingi ikaanza kuonekana katika mwili wa Spectre, rangi nyekundu hiyo ilionekana vyema japo wakati huwo ilikuwa kweupe. Yote hayo yalitokea kwa sekunde chache.
Grruuuuuuuuuu!!!
Zestra akanguruma na kuanza kukimbia alipo baston, kasi yake haikuwa kubwa sana lakini ilitosha kutuma ujume kuwa kiumbe hicho kilikuwa kimekasirika haswa.
Aaaaaaaaaaaaaahhhhh!!!
Baston nae akanguruma kabla ya Spectre kufyetuka, kasi yakw ilikuwa mara mbili ya Zestra. Mpaka hapo wengi wakajua kabisa kuwa Baston amewehuka. Itambulike kuwa hata wale wa kikosi cha makomando hawakuwa na uwezo wa kupambana Zestra wa daraja la Jenerali bila kuwepo zaidi ya watano.
"Baston unafanya nini?" alijisemea Shanequeen akikunja ngumi, jasho lilikuwa likimtoka. Hakuwa peke yake, wengi walikuwa kama yeye ila wao walihofia maisha tu isipokuwa Shanequeen alihofia kumpoteza mwanaume wake.
Haaaa!!!
Wengi wakamaka baada ya Baston kuamua kutumia visu, alikuwa anakwenda kwa vita ya karibu. Walipokaribia tu mdomo wa Zestra ukafunguka, muonzi mkali ukatoka. Baston akanesa kushoto na kuzunguka kwa kasi akitengeza alama ya nusu mwezi. Muonzi huwo ukamkosa kwa milimita chache sana.
Na kasi yake hiyo hiyo, akazunguka tena na kuachia teke kali sana lilitua katika mwili wa kiumbe huyo. Wote wawili wakarudi nyuma kwa kasi, ila pasi na mategemeo ya wengi kwamba Spectre angesimama.
Mgongo wa Spectre ukafunguka, bomba mbili nene kiasi zikaonekana.
Boom!!!
Moto ukatoka katika bomba hizo, zikalala kushoto. Spectre akasogea pembeni kidogo, mionzi mingine ikamkosa kwa sentimita kama moja hivu.
Fwooooooshhh!!
Moshi mweupe ukatoka katika zilw bomba zilizokuwa mabegani, mgongo wa Spectre ukajifunga. Baston akaendelea na kasi hiyo hiyo, visu viwili vyekundu mkononu. Akamavaa tena Zestra.
Klang!!!
Ni kama vile vyuma viwili vyenye kasi vilikutana na kusababisha mtikisiko mkubwa. Spectre akarudi tena nyuma kwa kasi.
Puhwak!!!
Baston akatpita damu, alihisi utumbo wake wote ukiparaganywa. Funda la pili la damu lilikuwa linakuja, akakaza shingo na kulirudisha tumboni. Laiti Zestra angejua kama alifanikiwa kumkasirisha Baston kiasi cha kutoka moshi kichwani, angekimbia.
Umbali wa mita thalathini kutoka alipo Zestra, Spectre alikuwa amesimama kama mlima. Ni kama vile alikuwa akimwambi "leo ni leo, afe punda afe muendesha punda, mzigo wa bwana lazima ufike".
Zestra akakita miguu yake chini, mdomo wake ukaanza kurefuka. Hata yeye mwenyewe alihisi kitisho kutoka kwa roboti hilo jeusi lenye mistari mekundu.
Vrrruuummmm!!!
Kwa mara nyingine tena mngurumo wa mashine ukasikia kutoka kwa Spectre. Waangaliaji wote wakajua kila upande ulikuwa unajipanga kufanya shambulizi ambalo lingeamua hatma ya pambano hilo.
Fyuuum!!
Ulisikika mlio mwemba kisha kimya kikatawala, bila matarajio waangaliaji wote wakabana pumzi. Mji mzima ulizizima, sauti ya upepo laini tu ndio iliyosikika.
Katuuum!!!!
Mlio mkali ukasikika ukifuatiwa na mtikisiko mkubwa na mwanga mkali, hakuna aliejua nini kimetokea lakini wengi waliomini pambano hilo lilikuwa limekwisha.