RIWAYA: Wivu-Beka Mfaume

RIWAYA: Wivu-Beka Mfaume

MTUNZI:BEKA MFAUME

SEHEMU YA MWISHO​

MLIO wa simu ndiouliomshitua kutoka usingizi! Alichukuliwa na usingizi bila yakujitambua alipokuwa amejilaza wakati akilia. Alishangaa kuionaasubuhi imeshafika na ndipo alipojitambua alikuwa amelala na lilegauni alilokuwa amepanga aende nalo Casino akiwa na Richard usikuuliopita. Kujiona ameamka akiwa na gauni hilo kukamtonesa kulikumbukazogo la usiku lililotokea hapo hotelini. Simu iliyokuwa ikiitailinyamaza, lakini sekunde chache baadaye ilianza kuitatena.

“Haloh,” Dina alisema baada ya kuipokea simu yachumbani kwake, kisha akapiga mwayo.

“Samahani,” sauti yakike ilisema kwenye simu. “Una mgeni wako hapa mapokezi.Amejitambulisha kwa jina la kachero Mussa.”

Ndipo fahamukamili zilipomrudia kuwa alikuwa na ahadi na kachero huyo asubuhihiyo.

“Naomba anipe dakika kumi za kujiandaa,” Dinaalisema kwenye simu. Kisha akamsikia msichana aliyepo kwenye simuakizungumza na mtu, akajua alikuwa akizungumza na kacheroMussa.

“Anasema utamkuta akikusubiri hapa mapokezi,”hatimaye msichana wa mapokezi alisema.

“Mwambie anisubirimgahawani, anaweza akaagiza kifungua kinywa kwa bili yangu,” Dinaalisema na kisha kukata simu.

Alitumia muda zaidi kuliko ulealiouahidi. Alikoga, kisha alijikwatua kwa vipodozi akiwa amekaakwenye stuli iliyopo mbele ya kioo cha kujiangalia wakati wa kuvaa.Moyo wake ulikuwa bado mzito kutokana na sintofahamu iliyokuwepo katiya John na Richard. Wote alitaka kujua taarifa zao zikoje. Kwa Johnni kwa ajili ya kujua kama amekwishakamatwa na polisi, na kwa Richardni kuhusu afya yake inavyoendelea baada ya upasuajialiyofanyiwa.

Kwa upande wa Richard angalau alikuwa namatumaini ya kuonana naye pindi atakapokwenda kumwona hospitaliatakapoongozana na kachero Mussa. Alikuwa na uhakika asingemkutakwenye hali ya kuruhusiwa kuzungumza na wageni kwa kuwa hali yake yakiafya ingekuwa bado haijatengemaa. Akaijenga taswira yaatakavyomwona Richard akiwa kitandani. Taswira hiyo akaijenga kwakumwona Richard akiwa hajarudiwa na fahamu kikamilifu kutoka kwenyemadawa ambayo angekuwa amepewa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.Alijua asingeweza kuzungumza naye zaidi ya kumwangalia na kishaangeondoka, lakini akajenga matumaini ya kuzungumza naye wakati wajioni atakavyorudi tena hospitali. Alikuwa na uhakika muda huo Johnangekuwa amerudiwa na fahamu kikamilifu.

Akapanga jioniatakapokuwa anarudi tena hospitali itamlazimu anunue maua na kadi yakumtakia Richard uponaji wa haraka.

Akiliona tatizo la Richardlikiwa halimwumizi sana kichwa, Dina alikiri tatizo la John ndilolililokuwa likimpa wakati mgumu. Alijiuliza kwa muda huo wa asubuhiJohn angekuwa wapi? Alijua John asingekuwa mpumbavu wa kuendeleakuwepo hotelini wakati akijua amefanya tukio ambalo limemwingizakutafutwa na polisi, lakini pia akajengwa na wasiwasi zaidi huendaJohn hakulala kabisa huko hotelini. Fikra hizo zikamfanya ayahisimachozi yakimlengalenga machoni baada ya kuifikiria hali ambayoangekuwa nayo John. Akaijenga taswira ya kumwona John akiwa kwenyewakati mgumu akiishi kwenye hali ya kukosa amani kutokana na woga wakukamatwa na polisi! Kwa mara nyingine, Dina alijisikia vibaya baadaya kujiona ndiye aliyeisababisha hali hiyo kwa John!

Wazo lakumpigia tena simu John likamrudia. Shinikizo la kutaka kumsaidia kwakumpatia pesa za kumsaidia kutoroka likaanza tena kuisumbua nafsiyake, aliamini kitendo hicho kingeweza kumwonyesha John kuwa yukopamoja naye kwenye tatizo hilo. Kwa upande mwingine, aliuona msaadahuo ungekuwa ni sehemu ya kumwomba John msamaha kwa kilekilichotokea!

Aliifuata simu yake iliyokuwa bado ipo kitandanina kumpigia John. Alipokuwa akisubiri simu hiyo ianze kuita upande wapili anakopiga, kimya hicho cha kusubiri pamoja na kwamba kilikuwa nicha muda mfupi, lakini kilimuweka kwenye wakati mgumu. Kilimjengeawoga wa kukabiliana na jibu kutoka kwenye simu kuwa, mtejaanayempigia hapatikani. Akaomba hilo lisitokee.

“Samahani,mteja unayempigia hapatikani, jaribu tena baadaye!” sauti kutokakwenye simu ilisikika.

Dina aliishiwa nguvu! Akaushusha chinimkono wake uliokamata simu, kisha akauinua juu uso wake uliokatatamaa. Alikuwa na uhakika John alikuwa amezima simu yake naasingeweza kumpata! Hakuhitaji kujiuliza ni kwa nini, yeyote angekuwakwenye mazingira kama aliyonayo John, angefanya hivyo. Akatamani Johnapate akili ya kuiwasha simu yake kisha ambipu japo mara moja.Alitamani iwe hivyo, lakini kwa hali halisi, ilikuwa sawa na mtumwenye kiu anayetamani kukiona kidimbwi cha maji jangwani!

Ghaflaakamkumbuka kachero Mussa, alikwisha kumsahau!

Kitendo chakumkumbuka kachero huyo kuwa alikuwa akimsubiri kikamtoa chumbaniharaka. Akamkuta akiwa anamalizia kifungua kinywa alichokiagiza.Kilikuwa ni kifungua kinywa kilichokamilika, kinachojulikana kwa jinala English Breakfast.

“Samahani kwa kukuweka sana,” Dinaalisema huku akivuta kiti na kukaa kwenye meza aliyokuwepoMussa.

“Usijali,” Mussa alisema huku akijifuta mdomo kwakitambaa cha mezani.
“Nashukuru kwa kifunguakinywa.”

“Usijali,” Dina alisema. Kisha aliagizia chaina vipande vya mikate ya kuokwa.

Dina alianza kunywa juisi nakusubiri chai aliyoiagiza.
“Hali ya Richard inaendeleaje?”aliuliza baada ya kumeza funda la juisi.

“Bado sijapatahabari zake,” Mussa alisema huku akijaribu kutoyatuliza machoyake.
“Nilipitia kituoni kujua kama kungekuwa na ripotiyoyote iliyoletwa na askari aliyekuwa akimlinda hospitali, hata hivyoalikuwa bado hajaiwasilisha. Nadhani askari mwenzake wa kuchukuanafasi yake atakuwa amechelewa kwenda kumtoa.”

“Na vipikuhusu John?”

“Kuna mtu mwenye jina lake amekamatwa janausiku na polisi,” Mussa alisema.
“Tutaanza kwenda hukoili ukamthibitishe kama ndiye yeye, kisha ndipo tutakapokwendakumwangalia Richard.”

Taarifa ya kukamatwa kwa Johnikampotezea Dina hamu ya chai aliyoiagiza!

“Nitakunywa chainitakaporudi!” Dina alisema huku akivuta nyuma kiti alichokalia nakusimama. Alijua asingeweza kuinywa chai ambayo angeletewa nahakutaka kachero Mussa alibaini hilo. “Twenzetu!” alimalizia kwakusema hivyo akiwa amekwishajitoa kwenye meza.

“Kwa niniusingekunywa kabisa,” Mussa alishauri.
“Huwezi kujua,unaweza ukajikuta umechaelewa kurudi, ukarudi hapa mchana baada yashughuli ya huku na kule. Unajua mambo yetu ya kipolisi hayanadogo.”
“Mara nyingi sipendi kunywa chai asubuhi,” Dinaalidanganya.

“Nimekwishazoea kufanya kazi wakati wa asubuhibila ya kunywa chai.”

Mussa akataka kuongeza neno, lakinialisita baada ya kumwona Dina akiwa amekwishaupachika mkoba wakebegani na kutangulia kuondoka. Akaamua kuongozana naye. Wakapita kwamtunza fedha ambako Dina alilipa gharama za kifungua kinywaalichokula Mussa.

Wakati wakiwa wamekwishatoka nje ya hoteli,Dina alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu kimawazo. Alikuwa tayariamechanganyikiwa na habari za kukamatwa kwa John, lakini alipataugumu pale alipokuwa akijitahidi kuificha hali hiyo isionekane nakachero huyo anayeandamana naye.

Wakiwa kwenye gari, kacheroMussa hakuonyesha kuwa kwenye mdadi wa kuzungumza, sehemu kubwa yamwonekano wake alipokuwa akiliendesha gari, alionekana kuwa kwenyetafakuri iliyomtuliza. Ukimya ukajitokeza kati yao, Dina akaomba halihiyo iendelee kuwa hivyo, kwani naye alihitaji utulivu utakaomuwekakwenye kujiandaa jinsi atakavyokabiliana na John. Hakujua angeongeanaye nini wakati akiwa amesimamiwa na polisi, lakini kilichokuwakikimsumbua zaidi ni pale atakavyolijibu swali la kachero huyolitakalomtaka athibitishe mbele ya John kama huyo aliyekamatwa niJohn! Alikuwa na uhakika jibu la kukubali kumthibitisha Johnlingekuwa kama usaliti atakaokuwa amemfanyia John!

Siku mbili,tatu za nyuma alipokuwa kwenye gari akienda ofisini akiwa na Richard,Dina alikuwa akifurahia kuiangalia mandhari ya jiji hilo la Arushakila alivyokuwa akipita, lakini asubuhi hiyo, kwa mara ya kwanzatokea afike kwenye mji huo, Dina aliuona mji huo kama eneo asilotakakuliona kwenye maisha yake! Hali hiyo ilimfanya kukitumia kimyakilichowekwa na kachero Mussa kufumba macho yake wakati wote hukuakiusikilizia myumbo unaofanywa na gari wakati likipita kwenyemiinuko ya barabara au wakati likikata kona. Kibaya zaidi, hakutakahata kushuhudia kule anakopelekwa!

Alijikuta akifumbua machobaada ya kulisikia gari hilo limesimama na kisha likazimwa injini.Akajua wamefika! Lakini alipoyaangaza macho yake akashangaa kulionagari hilo likiwa limesimama nje ya hospitali ya Mount Meru.Akamwangalia kachero Mussa kama vile uangaliaji wake ungemfanya Mussaaujibu mshangao wake. Hata hivyo, Mussa hakuonekana kukijuakilichokuwa kinafanyika kwa Dina, yeye alikuwa ameinama akihangaikakuufungua mkanda wa kiti cha gari.

“Umeamua tuanze kwakumwangalia Richard?” Dina aliamua kuuliza. Mussa alishusha pumzikwa nguvu na kuangalia mbele ya kioo cha gari, akaonekana kama vilealikuwa akiwaangalia watu waliokuwa wakikatisha

mbele ya garihilo.
“Hapana!” alijibu bila ya kuacha kutazama mbele.Jibu hilo likamtia hofu Dina. Akawa na wasiwasi kuwa, maadam kamasiye Richard aliyewafanya waje hapo, basi atakuwa ni John! Dhanaikamjenga kuwa John atakuwa alikumbana na kipigo cha polisi baada yakukamatwa na majeruhi aliyoyapata ndio yatakuwa yamemfanya alazwehospitalini hapo.

“John amelazwa?” Dina aliuliza na sautiyake ilishindwa kuificha hofu aliyokuwa nayo huku akiwa badohajayabandua macho yake kumwangalia kachero Mussa.

“Amefariki!”Mussa alijibu kama vile alikuwa akizungumza peke yake. Akageuka nakumwangalia Dina aliyekuwa tayari amepigwa na mshangao usoni.Akaendelea, “Alipatikana kwenye chumba chake cha hoteli aliyofikiaakiwa amejinyonga!”

Shingo ya Dina ikalegea ghafla, mboni zamacho yake zikajibinua kuelekea juu!

* * * * *

Kitendocha Dina kuzirai mle ndani ya gari kulimfanya kachero Mussaachanganyikiwe baada ya kujaribu kuutingisha mwili wa Dina kwa lengola kumuamsha bila ya mafanikio. Akatambua kulihitajika huduma yakihospitali ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo. Akaufungua mlangowa gari na kuchomoka kwa kasi, akakimbilia idara ya mapokezi ambakoalijitambulisha cheo chake kwa mfanyakazi wa hospitali mwenye bejiiliyomwonyesha ni mtumishi wa mapokezi aliyekuwa anataka kuingiachumba cha mapokezi akitokea nje na kumweleza kilichomsibu.

“Kwahiyo huyo dada yuko kwenye gari yako?” mtumishi huyo aliuliza kwautulivu kama vile tatizo aliloambiwa halikuhitaji huduma yadharura.

“Ndiyo yupo kwenye gari yangu!” Mussa alisema nakuonekana akikosa utulivu.

“Subiri nikutafutie watu wakwenda kumchukua,” mfanyakazi yule wa mapokezi alisema. Akaanzakurudi alikotoka, lakini kabla hajachanganya hatua akatokea mtu, mtuhuyo akamfanya asimame, wakaanza kusalimiana na kitendo hichokiliwachukua takribani dakika moja kama vile hakukuwa na jambo ladharura alilotakiwa mtumishi huyo wa hospitalialishughulikie.

Kitendo hicho kikamchafua Mussa. Hasirailiyompanda kichwani ikamsukuma kutaka kumfokea mtumishi huyo wahospitali, lakini kabla hajafanya hivyo, akatokea mhudumu wa wagonjwaambaye ni mwanamke, akaitwa na yule mtumishi.

“Omba msaadawa mwenzako ili mfuatane na huyu bwana, ana mgonjwa wake yuko kwenyegari amezidiwa,” alisema yule mtumishi wa mapokezi.

Kitendohicho kikamfanya kachero Mussa azishushe hasira zake. “Utaandamanana huyu dada kwenda kumchukua mgonjwa wako,”
mtumishi wamapokezi alimwambia Mussa, kisha akaendelea kuzungumza na mtu wake nakuonekana amelimaliza tatizo hilo.

Muuguzi wa kike na wa kiumewalikisukuma kitanda cha magurudumu hadi kwenye gari alilokujanaloMussa, wakamtoa Dina na kumpakia kwenye kitanda na kumuwahisha kwenyechumba cha daktari huku Mussa akifuata nyuma yao.

* * * **

Dina alihifadhiwa kwenye chumba maalumu hadi aliporejewa nafahamu. Alirejewa na fahamu akiwa peke yake baada ya muuguzi wa kikeanayemwangalia akiwa ametoka nje. Dina hakutambua yuko wapi, lakiniakahisi kama yuko hospitali. Akafumba macho kujaribu kuvutakumbukumbu ya kutaka kujua ilikuwaje akawepo hapo. Harufu ya madawaya binadamu ikamhakikishia kuwa yuko hospitali, lakini akawa badohajaelewa alifikaje hapo. Akavuta tena kumbukumbu kutaka kujua maraya mwisho alikuwa wapi kabla ya kufika hapo. Akaikumbuka hoteli yaMasai Shield!

Kuikumbuka hoteli hiyo ikawa kama vileimemfungulia rejesho la kumbukumbu zilizokuwa zimepotea. Akaanzakukumbuka kimoja baada ya kingine…

Amefariki! hatimayeakaikumbuka kauli ya kachero Mussa alivyokuwa naye kwa mara ya mwishokwenye gari akimzungumzia John!
Muuguzi akaingia!

“Umeamka?”muuguzi aliuliza huku akionyesha tabasamu dogo akiwa amesimama kandoya kitanda alicholalia Dina.

Dina hakujibu, kumbukumbuiliyomrejea ikaanza kumtoa machozi. Muuguzi akaingia kwenye kazi yakubembeleza. Juhudi zake zikafanikiwa kumtuliza Dina asilie kwasauti, lakini aliendelea kutokwa na machozi. Ghafla akataka kijiinua,akajilazimisha kujizoa zoa huku akionekana kukosa nguvu.

“Unatakakwenda wapi?” muuguzi alimwuliza.
“Nataka kukaa,” Dinaalijibu.

Muuguzi akamsaidia kumuinua, Dina akakaa kitandani namiguu yake ikaning’inia bila ya kukanyaga sakafuni. Baada ya kukaa,akabaki kimya.

“Unajisikiaje?” muuguzi aliuliza baada yakumwona Dina yuko kimya. “Naomba unipeleke nikamwone!” Dinaalisema bila ya kufafanua. Muuguzi akajua alichokimaanishaDina.

Taarifa za kujinyonga kwa John zilikuwa zikijulikana nabaadhi ya wauguzi, mmoja wa wauguzi hao alikuwa ni huyo anayemuuguzaDina kwenye chumba cha mapumziko ambaye pia alishiriki kumtoa Dinakutoka kwenye gari alipokuwa amezirai. Muuguzi huyo pia, alikuwa nataarifa zilizomjulisha kuwa, Dina ana mahusiano na John ingawahakuujua kwa undani uhusiano wao ulikuwa ni wa aina gani. Hivyo,kauli hiyo ya Dina kutaka kwenda kumwona anayetaka kumwona akawaameielewa vizuri kuwa, Dina alikuwa akitaka apelekwe chumba cha maitikumwona John!

“Mimi sina mamlaka ya kukupeleka,” muuguzialimwambia Dina. “Msubiri daktari akija umfahamishe, yeye ndiyemwenye mamlaka ya kukupeleka.”

Dina hakujibu. Alizubaa nakutulia bila ya kutikisika sehemu yoyote ya mwili wake, hakuonekanahata kupepesa macho yake. Muuguzi akabaki ameshangaa.

“Hivini kweli John amekufa?” Dina aliuliza na kuonekana kama amerudighafla kwenye uhai.

Swali hilo likamuweka muuguzi kwenyewakati mgumu. Akasita kujibu baada ya kukiri swali hilo lilikuwalimemchanganya. Lilikuwa gumu kulitolea jibu la haraka. “Kwani wewewamekwambiaje?” naye aliuliza.

“Nasikia amejinyo…”Dina hakuimaliza kauli yake, shingo yake ikalegea na macho yakekujipindua tena. Akaangukia ubavu!

Muuguzi akawahi kumdakaDina kabla hajaangukia chini kutoka kitandani. Akamlaza vizuri nakuirudisha miguu yake kitandani. Akajaribu kumtingisha huku akimuita.Baada ya kuona hakuna dalili yoyote ya kuitikiwa, akaamua kutoka mlechumbani kwa mwendo wa kasi, akaenda kumuita daktari!

* * * **

Mohsen aliwasili ofisini asubuhi, alikuwa badoakiendelea na majonzi ya kumkosa Dina tokea alivyoondoka kwendaArusha na alikuwa akiendelea kuumizwa na wivu kwa kujua yuko naRichard. Lile Jinamizi la kumkumbusha vitendo vya kimapenzialivyokuwa akifanya na Dina wakiwa humo ofisini lilikuwa likiendeleakumtesa. Alikuwa bado akimwona Dina kama vile yuko naye humo ofisini.Alijihisi kama anayechanganyikiwa kadri siku zilivyokuwa zikienda.Mazoea ya uwepo wao wa pamoja kwenye mapenzi ya muda mfupi yalimtesakana kwamba alikuwa kwenye mapenzi ya muda mrefu na msichanahuyo.

Pamoja na kuwa kwenye hali hiyo, lakini kila alipokuwaakimfikiria Dina ndivyo alivyokuwa akijilaumu kwa hatua aliyoichukuaya kumfuata John na kumbwagia mambo ambayo alikiri hayakupaswakujulikana na John kupitia kwake. Tukio hilo lilikuwa likimkoseshaamani baada ya kujiona alikuwa amekosea kuchukua hatua kama hiyo.Kitendo hicho kikamuweka kwenye mashaka kuwa, yote aliyokuwaamemweleza John yangeweza kumfikia Dina. Uwezekano wa John kwendakumweleza Dina na kisha kulitaja jina lake kuwa ndiye aliyemwambia,aliuona upo. Fikra hizo zikawa eneo jipya lililomkosesha amani kwamuda wote, hasa pale alipojiona angeonekana mshamba wa mapenzi namwanamume mmbeya!

Hofu hiyo ilimtia kwenye kiwingu kizito,iliyomwingizia majuto na kukiri upuuzi huo aliufanya kwa sababu yawivu wa kijinga! Fikra hizo za kukiri uhayawani wake zilimuwekakwenye wakati mgumu, ugumu ambao ulimjengea uhakika wa kujakumgharimu kwa gharama kubwa siku chache zijazo. Kwanza alikuwa nahakika ya kumpoteza Dina kama mpenzi wake ambaye tayarialikwishajikita moyoni mwake. Akakiri hilo litakuwa ni pigo kubwakwake na kumfanya aanze kuhisi kama vile hakutakuwa na maisha mengineikiwa atamkosa Dina. Lakini pia, kitendo hicho cha kupeleka umbeyakwa John alikiri kinaweza kumgharimu kwenye kazi yake! Alikuwa nauhakika Dina angeshikwa na hasira na angemshukia kama Mwewe nahatimaye angemshitaki kwa Richard! Richard angekuwa amepata sababu yakumfukuza kazi!

Akiwa kwenye lindi la mawazo asubuhi hiyo humoofisini kwake huku akiwaza jinsi atakavyompoteza Dina na kuipotezakazi yake, Mohsein alijikuta akipata wazo jipya. Wazo la kutakakurudi tena kwa John, safari hii kwa ajili ya kumpigia magoti!Alipanga aende kumsihi na kumrai asije akamtaja kwa Dina kuwa ni yeyendiye aliyeyazungumza maneno hayo. Hiyo ndio aliiona njia pekee yakuweza kumuokoa asikumbane na adhabu hizo mbili.

Akapanga mudawa kumfuata John kazini kwake. Akaona ni vyema kuitumia nafasi yaruhusa ya mchana inayotumika kwa ajili ya wafanyakazi kwenda kula,aitumie kwenda kumwona John! Akajiandaa kujipanga namna ya kumkabilikwa mara nyingine ya pili.

Ikiwa imebaki saa moja na usheemuda wa mapumziko kwa ajili ya chakula cha mchana ufike, taarifa zamsiba zikaja hapo kazini, taarifa zilizowashitua wafanyakazi wote wakampuni hiyo.

Lilikuwa tangazo la kufariki kwa Richard!

** * * *

Kifo cha Richard kilileta hisia tofauti kwawafanyakazi wa kampuni hiyo. Wapo waliofurahia kifo hicho kutokana naujivuni aliokuwa nao kijana huyo wakati wa uhai wake, wakazifichafuraha zao na kuunganika kwenye majonzi. Lakini pia walikuwepowalioguswa na kifo hicho kwa kukiri kuwa walikuwa wamempoteza mtuwanayemjua ambaye ni mfanyakazi mwenzao na huzuni ziliwagusa zaidikwa kumwona Richard amefariki akiwa bado ni kinda.

Mohseinyeye alikifurahia kwa sababu Richard alishakuwa adui yake,akakichukulia kifo hicho kwamba kitakuwa kimeondoa moja ya adhabumbili alizokuwa akizifikiria. Adhabu ya kufukuzwa kazi na Richard!Pamoja na kufurahia kwa upande huo, lakini upande wa pili ndiouliomfurahisha zaidi. Kifo cha Richard kingemuwezesha kulifaidi penzila Dina kwa wakati mwafaka, na ili kuliwezesha hilo, alitakiwakumkabili John hata kama ni kwa kutumia vitisho, kuhakikishahathubutu kumwambia Dina kwamba yeye aliupeleka umbeyakwake!

Taarifa endelevu za kifo cha Richard ziliendeleakuwasili kwa namna tofauti hapo kazini. Taarifa nyingine zikaletwakuwa, mzee Ken na mama yake Richard wanaondoka kwa ndege kuelekeaArusha asubuhi hiyo.

Baadaye zikaja taarifa za kipolisi kuwa,Richard aliuawa kwa kupigwa kisu kwenye ugomvi unaosadikika ulitokanana wivu wa mapenzi wa kumgombania mwanamke, lakini hazikumtajamwanamke mwenyewe. Hatimaye zikaja taarifa zenye mshitukozilizoeleza, polisi walikuwa wamethibitisha ugomvi uliosababisha kifocha Richard ulimhusisha mume mtarajiwa wa mfanyakazi mwenzake Richardanayeitwa Dina Nzasa, aliyetambulika kwa jina la John Sailas ambayebaada ya tukio la kumpiga kisu Richard aliamua kuchukua uamuzi wakujinyonga akiwa kwenye chumba cha hoteli aliyokuwa amefikia.Inasemekana John kabla ya kujinyonga aliacha barua yenye maelezo yakena polisi wamelithibitisha hilo kwa kusema kuwa, wanamtafuta mtummoja aliyetajwa kwenye barua hiyo kuwa ndiye anayeaminika ni chanzocha ugomvi huo. Polisi imekataa kulitaja jina la mtuhumiwa huyo kwasababu za kiusalama.

Taarifa hizo zikawa si njema kwa Mohsein!Kwanza hakuamini kama John alikwenda Arusha na moja kwa mojaakatambua kilichompeleka John Arusha ni zile taarifa alizokuwaamempelekea. Msala! aliwaza. Akajua mambo yamekwisha kuharibika nahofu yake ikawa ni barua iliyoachwa na John ambayo iko mikononi mwapolisi. Akawa na uhakika polisi watakuwa wakimtafuta yeye kwa kuaminibarua hiyo itakuwa imelitaja jina lake! Mohsein akawaamechanganyikiwa. Akapata wazo la kutoroka kabla ya polisi hawajafikahapo ofisini kumkamata!

Akatoka ofisini kwake, akawaagawafanyakazi wenzake aliokutana nao kwenye korido kuwa anakwenda kulachakula cha mchana.

Hakurudi tena kazini!

Siku ya piliasubuhi wakati wafanyakazi wakiwa kazini na wengine wakifuatiliamipango ya kuwasili kwa mwili wa Richard ambao taarifa za awalizilisema ungewasili kwa ndege siku inayofuata, ilipofika alasiri yasiku hiyo, taarifa nyingine za msiba zikawasili.

AlikuwaMohsein!

Taarifa hizo zilipokewa kama mchezo wa kuigizausiokubalika, hakuwepo aliyekuwa tayari kuziamini, hasa baada yataarifa hizo kudai, Mohsein alikutwa chumbani kwake akiwa amejinyongana kuacha ujumbe mfupi kwenye barua iliyoandikwa:

Wivuumeniponza!

Mohsein.

MISA

MISA ya kumwombeaJohn Sailas ilifanyika kwenye Kanisa Katoliki la Kimara Baruti baadaya siku ya arobaini tokea alipozikwa kwenye makaburi ya Kimara. Baadaya misa hiyo, wafiwa walikwenda makaburini kwa ajili ya kupandaMsalaba na kuweka mashada ya maua kwenye kaburi lake. Mmoja wawalioweka mashada hayo alikuwa ni Dina ambaye baada ya kuweka,akahisi hatia kwenye nafsi yake. Machozi yakaanza kumtoka na kiliocha kimya kimya kikafuata.
Ikabidi apewe msaada wa kuondolewa!

** * * *

Misa ya Richard ilifanyika siku nne tokea misa ya Johnilipofanyika. Misa yake ilifanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Peterlililopo Oysterbay. Dina alihudhuria misa hiyo akiongozana na wazaziwake, na wakati walipokuwa wakitoka Kanisani ili kujiandaa kwendakwenye makaburi ya Kinondoni alipozikwa Richard kwa ajili ya kupandaMsalaba, Dina akasikia akiitwa. Ilikuwa sauti ya kike iliyotoka nyumayake ikimuita kwa jina lake. Alipogeuka akamwona Judi aliyekuwaameandamana na kijana mmoja wa kiume.

“Hai Judi!” Dinaalisema na kusimama.

Ilikuwa ni mara yao ya pili kuonana tokeawalivyoonana kwa mara ya mwisho walipokutana kwenye msiba waRichard.

“Kutana na mchumba wangu,” Judi alimwambiaDina.
“Anaitwa Martin,”

“Nafurahi kukufahamu,” Dinaalisema huku akimpa mkono Martin. Kisha Judi akamtambulisha Martinkwa Dina.
“Martin, kutana na Dina, tulisoma pamoja kuanziakidato cha kwanza hadi cha nne kwenye shule ya Sekondari yaJangwani.”

Martin aliyekuwa bado akiliendeleza tabasamu lakeakasema, “Nami nafurahi kukufahamu.”

Baada ya Dina naMartin kusalimiana, Judi aliufungua mkoba wake na kutoa bahasha,akampa Dina.

“Nilihisi tungeonana huku Kanisani,” Judialisema.
“Nikapata wazo la kuja nayo hii kadi ilinikikuona nikupe. Mungu naye ametuwezesha tumeonana.”

Dinaaliipokea kadi aliyopewa ambayo ilikuwa ndani ya bahasha na kusema,“Ahsante.” Hakuhoji ni ya nini kwa sababu angeifungua na kuisomabaadaye.

Wakaagana.

Akiwa kwenye gari ndogo amekaanyuma pamoja na mama yake huku baba yake akiwa amekaa mbele nadereva, Dina aliifungua bahasha aliyopewa na Judi, akaichomoa kadi nakuisoma. Akagundua ilikuwa ni kadi ya mwaliko inayomwalika ahudhuriesherehe ya kufunga ndoa kati ya Judi na Martin!

Mchomo mkaliukapita na kuuchana moyo wa Dina, akaacha kuendelea kuisoma kadihiyo, akaamua kuangalia nje ambako watu wachache walikuwa wakitembeakando ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi na wakati huohuo magariwaliyokuwa wakipishana nayo yalisikika yakitoa mivumo ya kasi yamwendo. Macho ya Dina yalikuwa yamegubikwa na machozi yaliyomnyimanafasi ya kukiangalia kinachotokea barabarani.

Upepo uliokuwaukiingia kupitia dirisha lililokuwa upande aliokaa Dinauliyapeperusha machozi na kuyasambaza kwenye ncha za macho yakewakati gari hilo likiwa kwenye mwendo.

Akajifuta machozi yau pande mmoja wa jicho lake kwa kutumia kiganja cha mkono wake.

muuza ubuyu culbby @myln amina mabata sam II Analyse
 
Attachments

Last edited by a moderator:
RIWAYA: KIZUIZI.
MTUNZI: George IronMosenya

MUHTASARI

Penzi linathibitisha nguvu yake ya ajabu. Nguvu inayotikisa dunia na walimwengu ndani yake.
Sasa linajaribu kukabiliana na ukweli. ukweli unafungwa pingu, Pesa inasaidiana na penzi kuugalagaza ukweli.
Jose B Wa ukweli, kijana mpenda kujua mengi anaanzisha kile alichokiona ni kidogo tena cha kawaida sana. Anakivumbua KIZUIZI. Kizuizi ambacho kinahatarishanafasi ya bwana James kumvisha pete Happy!!
KIZUIZI kinageuzwa kuwa biashara halali, Biashara hii inageuka haramu tena ya kumwaga damu. Gharama ya Kizuizi inakuwa kubwa kuliko ilivyotarajiwa.
Kizuizi kinakuwa mpinzani wa pekee wa ukweli wa Penzi. Hatimaye penzi linapata mbabe wake lakini bado penzi halikubali kuangushwa.
Penzi linajijenga katika maadui na kuwafanya marafiki, linawatenga ndugu na kuwafanya maadui. ni penzi la maajabu, penzi lililojaa sintofahamu.
KIZUIZI kinalilazimisha penzi na pesa kuuachia UKWELIhuru lakini bado minyororo inakuwa migumu kufunguka. Damu inaendeleakumwagika.
Ni mpambano mkali wa kimya kimya, kizuizi kinatambaa,pesa na penzi vinasimama imara kukipinga.
Mpambano huu una matokeo mawili tu…ni aidha KIZUIZI kishinde na ukweli ufunguke kutoka katika pingu kisha amani itoweke ama UKWELI uendelee kukingwa na pesana penzi ili amani iendelee kuwepo.
Amani yenye mashaka.
Wakati maandalizi ya harusi kubwa ya kifahari yakipamba moto, bwana harusina bibi harusi mtarajiwa kila mmoja kwa wakati wake anaomba siku yaharusi isifike……

RIWAYA mahsusi kwa wewe uliye katika mapenzi, unatarajia kufunga ndoa na wewe mwenye mpango wa kuingia penzini.

Jiandae kuifatilia...

Wakati wa kuisubiri tuendelee na riwaya ya sitaisahau facebook, moderator kaihamishia MMU

RIWAYA: Sitaisahau Facebook

amina mabata sam II Analyse muuza ubuyu culbby
 
Habari wanajukwaa, kuna softcopy kadhaa nnazo za hadithi tofauti nkaona si vibaya ku-share ikizingatia watunzi wake wameziweka public hivyo kutohesabika kama wizi wa kazi za watu au kuharibu mapato.. Kila siku nitaweka sehemu moja, watakuwepo ambao wameshazisoma lakini pia kutakua na wengi ambao hawajahi kuzisoma,
Habari
 
MTUNZI:BEKA MFAUME

SEHEMU YA MWISHO​

MLIO wa simu ndiouliomshitua kutoka usingizi! Alichukuliwa na usingizi bila yakujitambua alipokuwa amejilaza wakati akilia. Alishangaa kuionaasubuhi imeshafika na ndipo alipojitambua alikuwa amelala na lilegauni alilokuwa amepanga aende nalo Casino akiwa na Richard usikuuliopita. Kujiona ameamka akiwa na gauni hilo kukamtonesa kulikumbukazogo la usiku lililotokea hapo hotelini. Simu iliyokuwa ikiitailinyamaza, lakini sekunde chache baadaye ilianza kuitatena.

Haloh, Dina alisema baada ya kuipokea simu yachumbani kwake, kisha akapiga mwayo.

Samahani, sauti yakike ilisema kwenye simu. Una mgeni wako hapa mapokezi.Amejitambulisha kwa jina la kachero Mussa.

Ndipo fahamukamili zilipomrudia kuwa alikuwa na ahadi na kachero huyo asubuhihiyo.

Naomba anipe dakika kumi za kujiandaa, Dinaalisema kwenye simu. Kisha akamsikia msichana aliyepo kwenye simuakizungumza na mtu, akajua alikuwa akizungumza na kacheroMussa.

Anasema utamkuta akikusubiri hapa mapokezi,hatimaye msichana wa mapokezi alisema.

Mwambie anisubirimgahawani, anaweza akaagiza kifungua kinywa kwa bili yangu, Dinaalisema na kisha kukata simu.

Alitumia muda zaidi kuliko ulealiouahidi. Alikoga, kisha alijikwatua kwa vipodozi akiwa amekaakwenye stuli iliyopo mbele ya kioo cha kujiangalia wakati wa kuvaa.Moyo wake ulikuwa bado mzito kutokana na sintofahamu iliyokuwepo katiya John na Richard. Wote alitaka kujua taarifa zao zikoje. Kwa Johnni kwa ajili ya kujua kama amekwishakamatwa na polisi, na kwa Richardni kuhusu afya yake inavyoendelea baada ya upasuajialiyofanyiwa.

Kwa upande wa Richard angalau alikuwa namatumaini ya kuonana naye pindi atakapokwenda kumwona hospitaliatakapoongozana na kachero Mussa. Alikuwa na uhakika asingemkutakwenye hali ya kuruhusiwa kuzungumza na wageni kwa kuwa hali yake yakiafya ingekuwa bado haijatengemaa. Akaijenga taswira yaatakavyomwona Richard akiwa kitandani. Taswira hiyo akaijenga kwakumwona Richard akiwa hajarudiwa na fahamu kikamilifu kutoka kwenyemadawa ambayo angekuwa amepewa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.Alijua asingeweza kuzungumza naye zaidi ya kumwangalia na kishaangeondoka, lakini akajenga matumaini ya kuzungumza naye wakati wajioni atakavyorudi tena hospitali. Alikuwa na uhakika muda huo Johnangekuwa amerudiwa na fahamu kikamilifu.

Akapanga jioniatakapokuwa anarudi tena hospitali itamlazimu anunue maua na kadi yakumtakia Richard uponaji wa haraka.

Akiliona tatizo la Richardlikiwa halimwumizi sana kichwa, Dina alikiri tatizo la John ndilolililokuwa likimpa wakati mgumu. Alijiuliza kwa muda huo wa asubuhiJohn angekuwa wapi? Alijua John asingekuwa mpumbavu wa kuendeleakuwepo hotelini wakati akijua amefanya tukio ambalo limemwingizakutafutwa na polisi, lakini pia akajengwa na wasiwasi zaidi huendaJohn hakulala kabisa huko hotelini. Fikra hizo zikamfanya ayahisimachozi yakimlengalenga machoni baada ya kuifikiria hali ambayoangekuwa nayo John. Akaijenga taswira ya kumwona John akiwa kwenyewakati mgumu akiishi kwenye hali ya kukosa amani kutokana na woga wakukamatwa na polisi! Kwa mara nyingine, Dina alijisikia vibaya baadaya kujiona ndiye aliyeisababisha hali hiyo kwa John!

Wazo lakumpigia tena simu John likamrudia. Shinikizo la kutaka kumsaidia kwakumpatia pesa za kumsaidia kutoroka likaanza tena kuisumbua nafsiyake, aliamini kitendo hicho kingeweza kumwonyesha John kuwa yukopamoja naye kwenye tatizo hilo. Kwa upande mwingine, aliuona msaadahuo ungekuwa ni sehemu ya kumwomba John msamaha kwa kilekilichotokea!

Aliifuata simu yake iliyokuwa bado ipo kitandanina kumpigia John. Alipokuwa akisubiri simu hiyo ianze kuita upande wapili anakopiga, kimya hicho cha kusubiri pamoja na kwamba kilikuwa nicha muda mfupi, lakini kilimuweka kwenye wakati mgumu. Kilimjengeawoga wa kukabiliana na jibu kutoka kwenye simu kuwa, mtejaanayempigia hapatikani. Akaomba hilo lisitokee.

Samahani,mteja unayempigia hapatikani, jaribu tena baadaye! sauti kutokakwenye simu ilisikika.

Dina aliishiwa nguvu! Akaushusha chinimkono wake uliokamata simu, kisha akauinua juu uso wake uliokatatamaa. Alikuwa na uhakika John alikuwa amezima simu yake naasingeweza kumpata! Hakuhitaji kujiuliza ni kwa nini, yeyote angekuwakwenye mazingira kama aliyonayo John, angefanya hivyo. Akatamani Johnapate akili ya kuiwasha simu yake kisha ambipu japo mara moja.Alitamani iwe hivyo, lakini kwa hali halisi, ilikuwa sawa na mtumwenye kiu anayetamani kukiona kidimbwi cha maji jangwani!

Ghaflaakamkumbuka kachero Mussa, alikwisha kumsahau!

Kitendo chakumkumbuka kachero huyo kuwa alikuwa akimsubiri kikamtoa chumbaniharaka. Akamkuta akiwa anamalizia kifungua kinywa alichokiagiza.Kilikuwa ni kifungua kinywa kilichokamilika, kinachojulikana kwa jinala English Breakfast.

Samahani kwa kukuweka sana, Dinaalisema huku akivuta kiti na kukaa kwenye meza aliyokuwepoMussa.

Usijali, Mussa alisema huku akijifuta mdomo kwakitambaa cha mezani.
Nashukuru kwa kifunguakinywa.

Usijali, Dina alisema. Kisha aliagizia chaina vipande vya mikate ya kuokwa.

Dina alianza kunywa juisi nakusubiri chai aliyoiagiza.
Hali ya Richard inaendeleaje?aliuliza baada ya kumeza funda la juisi.

Bado sijapatahabari zake, Mussa alisema huku akijaribu kutoyatuliza machoyake.
Nilipitia kituoni kujua kama kungekuwa na ripotiyoyote iliyoletwa na askari aliyekuwa akimlinda hospitali, hata hivyoalikuwa bado hajaiwasilisha. Nadhani askari mwenzake wa kuchukuanafasi yake atakuwa amechelewa kwenda kumtoa.

Na vipikuhusu John?

Kuna mtu mwenye jina lake amekamatwa janausiku na polisi, Mussa alisema.
Tutaanza kwenda hukoili ukamthibitishe kama ndiye yeye, kisha ndipo tutakapokwendakumwangalia Richard.

Taarifa ya kukamatwa kwa Johnikampotezea Dina hamu ya chai aliyoiagiza!

Nitakunywa chainitakaporudi! Dina alisema huku akivuta nyuma kiti alichokalia nakusimama. Alijua asingeweza kuinywa chai ambayo angeletewa nahakutaka kachero Mussa alibaini hilo. Twenzetu! alimalizia kwakusema hivyo akiwa amekwishajitoa kwenye meza.

Kwa niniusingekunywa kabisa, Mussa alishauri.
Huwezi kujua,unaweza ukajikuta umechaelewa kurudi, ukarudi hapa mchana baada yashughuli ya huku na kule. Unajua mambo yetu ya kipolisi hayanadogo.
Mara nyingi sipendi kunywa chai asubuhi, Dinaalidanganya.

Nimekwishazoea kufanya kazi wakati wa asubuhibila ya kunywa chai.

Mussa akataka kuongeza neno, lakinialisita baada ya kumwona Dina akiwa amekwishaupachika mkoba wakebegani na kutangulia kuondoka. Akaamua kuongozana naye. Wakapita kwamtunza fedha ambako Dina alilipa gharama za kifungua kinywaalichokula Mussa.

Wakati wakiwa wamekwishatoka nje ya hoteli,Dina alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu kimawazo. Alikuwa tayariamechanganyikiwa na habari za kukamatwa kwa John, lakini alipataugumu pale alipokuwa akijitahidi kuificha hali hiyo isionekane nakachero huyo anayeandamana naye.

Wakiwa kwenye gari, kacheroMussa hakuonyesha kuwa kwenye mdadi wa kuzungumza, sehemu kubwa yamwonekano wake alipokuwa akiliendesha gari, alionekana kuwa kwenyetafakuri iliyomtuliza. Ukimya ukajitokeza kati yao, Dina akaomba halihiyo iendelee kuwa hivyo, kwani naye alihitaji utulivu utakaomuwekakwenye kujiandaa jinsi atakavyokabiliana na John. Hakujua angeongeanaye nini wakati akiwa amesimamiwa na polisi, lakini kilichokuwakikimsumbua zaidi ni pale atakavyolijibu swali la kachero huyolitakalomtaka athibitishe mbele ya John kama huyo aliyekamatwa niJohn! Alikuwa na uhakika jibu la kukubali kumthibitisha Johnlingekuwa kama usaliti atakaokuwa amemfanyia John!

Siku mbili,tatu za nyuma alipokuwa kwenye gari akienda ofisini akiwa na Richard,Dina alikuwa akifurahia kuiangalia mandhari ya jiji hilo la Arushakila alivyokuwa akipita, lakini asubuhi hiyo, kwa mara ya kwanzatokea afike kwenye mji huo, Dina aliuona mji huo kama eneo asilotakakuliona kwenye maisha yake! Hali hiyo ilimfanya kukitumia kimyakilichowekwa na kachero Mussa kufumba macho yake wakati wote hukuakiusikilizia myumbo unaofanywa na gari wakati likipita kwenyemiinuko ya barabara au wakati likikata kona. Kibaya zaidi, hakutakahata kushuhudia kule anakopelekwa!

Alijikuta akifumbua machobaada ya kulisikia gari hilo limesimama na kisha likazimwa injini.Akajua wamefika! Lakini alipoyaangaza macho yake akashangaa kulionagari hilo likiwa limesimama nje ya hospitali ya Mount Meru.Akamwangalia kachero Mussa kama vile uangaliaji wake ungemfanya Mussaaujibu mshangao wake. Hata hivyo, Mussa hakuonekana kukijuakilichokuwa kinafanyika kwa Dina, yeye alikuwa ameinama akihangaikakuufungua mkanda wa kiti cha gari.

Umeamua tuanze kwakumwangalia Richard? Dina aliamua kuuliza. Mussa alishusha pumzikwa nguvu na kuangalia mbele ya kioo cha gari, akaonekana kama vilealikuwa akiwaangalia watu waliokuwa wakikatisha

mbele ya garihilo.
Hapana! alijibu bila ya kuacha kutazama mbele.Jibu hilo likamtia hofu Dina. Akawa na wasiwasi kuwa, maadam kamasiye Richard aliyewafanya waje hapo, basi atakuwa ni John! Dhanaikamjenga kuwa John atakuwa alikumbana na kipigo cha polisi baada yakukamatwa na majeruhi aliyoyapata ndio yatakuwa yamemfanya alazwehospitalini hapo.

John amelazwa? Dina aliuliza na sautiyake ilishindwa kuificha hofu aliyokuwa nayo huku akiwa badohajayabandua macho yake kumwangalia kachero Mussa.

Amefariki!Mussa alijibu kama vile alikuwa akizungumza peke yake. Akageuka nakumwangalia Dina aliyekuwa tayari amepigwa na mshangao usoni.Akaendelea, Alipatikana kwenye chumba chake cha hoteli aliyofikiaakiwa amejinyonga!

Shingo ya Dina ikalegea ghafla, mboni zamacho yake zikajibinua kuelekea juu!

* * * * *

Kitendocha Dina kuzirai mle ndani ya gari kulimfanya kachero Mussaachanganyikiwe baada ya kujaribu kuutingisha mwili wa Dina kwa lengola kumuamsha bila ya mafanikio. Akatambua kulihitajika huduma yakihospitali ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo. Akaufungua mlangowa gari na kuchomoka kwa kasi, akakimbilia idara ya mapokezi ambakoalijitambulisha cheo chake kwa mfanyakazi wa hospitali mwenye bejiiliyomwonyesha ni mtumishi wa mapokezi aliyekuwa anataka kuingiachumba cha mapokezi akitokea nje na kumweleza kilichomsibu.

Kwahiyo huyo dada yuko kwenye gari yako? mtumishi huyo aliuliza kwautulivu kama vile tatizo aliloambiwa halikuhitaji huduma yadharura.

Ndiyo yupo kwenye gari yangu! Mussa alisema nakuonekana akikosa utulivu.

Subiri nikutafutie watu wakwenda kumchukua, mfanyakazi yule wa mapokezi alisema. Akaanzakurudi alikotoka, lakini kabla hajachanganya hatua akatokea mtu, mtuhuyo akamfanya asimame, wakaanza kusalimiana na kitendo hichokiliwachukua takribani dakika moja kama vile hakukuwa na jambo ladharura alilotakiwa mtumishi huyo wa hospitalialishughulikie.

Kitendo hicho kikamchafua Mussa. Hasirailiyompanda kichwani ikamsukuma kutaka kumfokea mtumishi huyo wahospitali, lakini kabla hajafanya hivyo, akatokea mhudumu wa wagonjwaambaye ni mwanamke, akaitwa na yule mtumishi.

Omba msaadawa mwenzako ili mfuatane na huyu bwana, ana mgonjwa wake yuko kwenyegari amezidiwa, alisema yule mtumishi wa mapokezi.

Kitendohicho kikamfanya kachero Mussa azishushe hasira zake. Utaandamanana huyu dada kwenda kumchukua mgonjwa wako,
mtumishi wamapokezi alimwambia Mussa, kisha akaendelea kuzungumza na mtu wake nakuonekana amelimaliza tatizo hilo.

Muuguzi wa kike na wa kiumewalikisukuma kitanda cha magurudumu hadi kwenye gari alilokujanaloMussa, wakamtoa Dina na kumpakia kwenye kitanda na kumuwahisha kwenyechumba cha daktari huku Mussa akifuata nyuma yao.

* * * **

Dina alihifadhiwa kwenye chumba maalumu hadi aliporejewa nafahamu. Alirejewa na fahamu akiwa peke yake baada ya muuguzi wa kikeanayemwangalia akiwa ametoka nje. Dina hakutambua yuko wapi, lakiniakahisi kama yuko hospitali. Akafumba macho kujaribu kuvutakumbukumbu ya kutaka kujua ilikuwaje akawepo hapo. Harufu ya madawaya binadamu ikamhakikishia kuwa yuko hospitali, lakini akawa badohajaelewa alifikaje hapo. Akavuta tena kumbukumbu kutaka kujua maraya mwisho alikuwa wapi kabla ya kufika hapo. Akaikumbuka hoteli yaMasai Shield!

Kuikumbuka hoteli hiyo ikawa kama vileimemfungulia rejesho la kumbukumbu zilizokuwa zimepotea. Akaanzakukumbuka kimoja baada ya kingine

Amefariki! hatimayeakaikumbuka kauli ya kachero Mussa alivyokuwa naye kwa mara ya mwishokwenye gari akimzungumzia John!
Muuguzi akaingia!

Umeamka?muuguzi aliuliza huku akionyesha tabasamu dogo akiwa amesimama kandoya kitanda alicholalia Dina.

Dina hakujibu, kumbukumbuiliyomrejea ikaanza kumtoa machozi. Muuguzi akaingia kwenye kazi yakubembeleza. Juhudi zake zikafanikiwa kumtuliza Dina asilie kwasauti, lakini aliendelea kutokwa na machozi. Ghafla akataka kijiinua,akajilazimisha kujizoa zoa huku akionekana kukosa nguvu.

Unatakakwenda wapi? muuguzi alimwuliza.
Nataka kukaa, Dinaalijibu.

Muuguzi akamsaidia kumuinua, Dina akakaa kitandani namiguu yake ikaninginia bila ya kukanyaga sakafuni. Baada ya kukaa,akabaki kimya.

Unajisikiaje? muuguzi aliuliza baada yakumwona Dina yuko kimya. Naomba unipeleke nikamwone! Dinaalisema bila ya kufafanua. Muuguzi akajua alichokimaanishaDina.

Taarifa za kujinyonga kwa John zilikuwa zikijulikana nabaadhi ya wauguzi, mmoja wa wauguzi hao alikuwa ni huyo anayemuuguzaDina kwenye chumba cha mapumziko ambaye pia alishiriki kumtoa Dinakutoka kwenye gari alipokuwa amezirai. Muuguzi huyo pia, alikuwa nataarifa zilizomjulisha kuwa, Dina ana mahusiano na John ingawahakuujua kwa undani uhusiano wao ulikuwa ni wa aina gani. Hivyo,kauli hiyo ya Dina kutaka kwenda kumwona anayetaka kumwona akawaameielewa vizuri kuwa, Dina alikuwa akitaka apelekwe chumba cha maitikumwona John!

Mimi sina mamlaka ya kukupeleka, muuguzialimwambia Dina. Msubiri daktari akija umfahamishe, yeye ndiyemwenye mamlaka ya kukupeleka.

Dina hakujibu. Alizubaa nakutulia bila ya kutikisika sehemu yoyote ya mwili wake, hakuonekanahata kupepesa macho yake. Muuguzi akabaki ameshangaa.

Hivini kweli John amekufa? Dina aliuliza na kuonekana kama amerudighafla kwenye uhai.

Swali hilo likamuweka muuguzi kwenyewakati mgumu. Akasita kujibu baada ya kukiri swali hilo lilikuwalimemchanganya. Lilikuwa gumu kulitolea jibu la haraka. Kwani wewewamekwambiaje? naye aliuliza.

Nasikia amejinyoDina hakuimaliza kauli yake, shingo yake ikalegea na macho yakekujipindua tena. Akaangukia ubavu!

Muuguzi akawahi kumdakaDina kabla hajaangukia chini kutoka kitandani. Akamlaza vizuri nakuirudisha miguu yake kitandani. Akajaribu kumtingisha huku akimuita.Baada ya kuona hakuna dalili yoyote ya kuitikiwa, akaamua kutoka mlechumbani kwa mwendo wa kasi, akaenda kumuita daktari!

* * * **

Mohsen aliwasili ofisini asubuhi, alikuwa badoakiendelea na majonzi ya kumkosa Dina tokea alivyoondoka kwendaArusha na alikuwa akiendelea kuumizwa na wivu kwa kujua yuko naRichard. Lile Jinamizi la kumkumbusha vitendo vya kimapenzialivyokuwa akifanya na Dina wakiwa humo ofisini lilikuwa likiendeleakumtesa. Alikuwa bado akimwona Dina kama vile yuko naye humo ofisini.Alijihisi kama anayechanganyikiwa kadri siku zilivyokuwa zikienda.Mazoea ya uwepo wao wa pamoja kwenye mapenzi ya muda mfupi yalimtesakana kwamba alikuwa kwenye mapenzi ya muda mrefu na msichanahuyo.

Pamoja na kuwa kwenye hali hiyo, lakini kila alipokuwaakimfikiria Dina ndivyo alivyokuwa akijilaumu kwa hatua aliyoichukuaya kumfuata John na kumbwagia mambo ambayo alikiri hayakupaswakujulikana na John kupitia kwake. Tukio hilo lilikuwa likimkoseshaamani baada ya kujiona alikuwa amekosea kuchukua hatua kama hiyo.Kitendo hicho kikamuweka kwenye mashaka kuwa, yote aliyokuwaamemweleza John yangeweza kumfikia Dina. Uwezekano wa John kwendakumweleza Dina na kisha kulitaja jina lake kuwa ndiye aliyemwambia,aliuona upo. Fikra hizo zikawa eneo jipya lililomkosesha amani kwamuda wote, hasa pale alipojiona angeonekana mshamba wa mapenzi namwanamume mmbeya!

Hofu hiyo ilimtia kwenye kiwingu kizito,iliyomwingizia majuto na kukiri upuuzi huo aliufanya kwa sababu yawivu wa kijinga! Fikra hizo za kukiri uhayawani wake zilimuwekakwenye wakati mgumu, ugumu ambao ulimjengea uhakika wa kujakumgharimu kwa gharama kubwa siku chache zijazo. Kwanza alikuwa nahakika ya kumpoteza Dina kama mpenzi wake ambaye tayarialikwishajikita moyoni mwake. Akakiri hilo litakuwa ni pigo kubwakwake na kumfanya aanze kuhisi kama vile hakutakuwa na maisha mengineikiwa atamkosa Dina. Lakini pia, kitendo hicho cha kupeleka umbeyakwa John alikiri kinaweza kumgharimu kwenye kazi yake! Alikuwa nauhakika Dina angeshikwa na hasira na angemshukia kama Mwewe nahatimaye angemshitaki kwa Richard! Richard angekuwa amepata sababu yakumfukuza kazi!

Akiwa kwenye lindi la mawazo asubuhi hiyo humoofisini kwake huku akiwaza jinsi atakavyompoteza Dina na kuipotezakazi yake, Mohsein alijikuta akipata wazo jipya. Wazo la kutakakurudi tena kwa John, safari hii kwa ajili ya kumpigia magoti!Alipanga aende kumsihi na kumrai asije akamtaja kwa Dina kuwa ni yeyendiye aliyeyazungumza maneno hayo. Hiyo ndio aliiona njia pekee yakuweza kumuokoa asikumbane na adhabu hizo mbili.

Akapanga mudawa kumfuata John kazini kwake. Akaona ni vyema kuitumia nafasi yaruhusa ya mchana inayotumika kwa ajili ya wafanyakazi kwenda kula,aitumie kwenda kumwona John! Akajiandaa kujipanga namna ya kumkabilikwa mara nyingine ya pili.

Ikiwa imebaki saa moja na usheemuda wa mapumziko kwa ajili ya chakula cha mchana ufike, taarifa zamsiba zikaja hapo kazini, taarifa zilizowashitua wafanyakazi wote wakampuni hiyo.

Lilikuwa tangazo la kufariki kwa Richard!

** * * *

Kifo cha Richard kilileta hisia tofauti kwawafanyakazi wa kampuni hiyo. Wapo waliofurahia kifo hicho kutokana naujivuni aliokuwa nao kijana huyo wakati wa uhai wake, wakazifichafuraha zao na kuunganika kwenye majonzi. Lakini pia walikuwepowalioguswa na kifo hicho kwa kukiri kuwa walikuwa wamempoteza mtuwanayemjua ambaye ni mfanyakazi mwenzao na huzuni ziliwagusa zaidikwa kumwona Richard amefariki akiwa bado ni kinda.

Mohseinyeye alikifurahia kwa sababu Richard alishakuwa adui yake,akakichukulia kifo hicho kwamba kitakuwa kimeondoa moja ya adhabumbili alizokuwa akizifikiria. Adhabu ya kufukuzwa kazi na Richard!Pamoja na kufurahia kwa upande huo, lakini upande wa pili ndiouliomfurahisha zaidi. Kifo cha Richard kingemuwezesha kulifaidi penzila Dina kwa wakati mwafaka, na ili kuliwezesha hilo, alitakiwakumkabili John hata kama ni kwa kutumia vitisho, kuhakikishahathubutu kumwambia Dina kwamba yeye aliupeleka umbeyakwake!

Taarifa endelevu za kifo cha Richard ziliendeleakuwasili kwa namna tofauti hapo kazini. Taarifa nyingine zikaletwakuwa, mzee Ken na mama yake Richard wanaondoka kwa ndege kuelekeaArusha asubuhi hiyo.

Baadaye zikaja taarifa za kipolisi kuwa,Richard aliuawa kwa kupigwa kisu kwenye ugomvi unaosadikika ulitokanana wivu wa mapenzi wa kumgombania mwanamke, lakini hazikumtajamwanamke mwenyewe. Hatimaye zikaja taarifa zenye mshitukozilizoeleza, polisi walikuwa wamethibitisha ugomvi uliosababisha kifocha Richard ulimhusisha mume mtarajiwa wa mfanyakazi mwenzake Richardanayeitwa Dina Nzasa, aliyetambulika kwa jina la John Sailas ambayebaada ya tukio la kumpiga kisu Richard aliamua kuchukua uamuzi wakujinyonga akiwa kwenye chumba cha hoteli aliyokuwa amefikia.Inasemekana John kabla ya kujinyonga aliacha barua yenye maelezo yakena polisi wamelithibitisha hilo kwa kusema kuwa, wanamtafuta mtummoja aliyetajwa kwenye barua hiyo kuwa ndiye anayeaminika ni chanzocha ugomvi huo. Polisi imekataa kulitaja jina la mtuhumiwa huyo kwasababu za kiusalama.

Taarifa hizo zikawa si njema kwa Mohsein!Kwanza hakuamini kama John alikwenda Arusha na moja kwa mojaakatambua kilichompeleka John Arusha ni zile taarifa alizokuwaamempelekea. Msala! aliwaza. Akajua mambo yamekwisha kuharibika nahofu yake ikawa ni barua iliyoachwa na John ambayo iko mikononi mwapolisi. Akawa na uhakika polisi watakuwa wakimtafuta yeye kwa kuaminibarua hiyo itakuwa imelitaja jina lake! Mohsein akawaamechanganyikiwa. Akapata wazo la kutoroka kabla ya polisi hawajafikahapo ofisini kumkamata!

Akatoka ofisini kwake, akawaagawafanyakazi wenzake aliokutana nao kwenye korido kuwa anakwenda kulachakula cha mchana.

Hakurudi tena kazini!

Siku ya piliasubuhi wakati wafanyakazi wakiwa kazini na wengine wakifuatiliamipango ya kuwasili kwa mwili wa Richard ambao taarifa za awalizilisema ungewasili kwa ndege siku inayofuata, ilipofika alasiri yasiku hiyo, taarifa nyingine za msiba zikawasili.

AlikuwaMohsein!

Taarifa hizo zilipokewa kama mchezo wa kuigizausiokubalika, hakuwepo aliyekuwa tayari kuziamini, hasa baada yataarifa hizo kudai, Mohsein alikutwa chumbani kwake akiwa amejinyongana kuacha ujumbe mfupi kwenye barua iliyoandikwa:

Wivuumeniponza!

Mohsein.

MISA

MISA ya kumwombeaJohn Sailas ilifanyika kwenye Kanisa Katoliki la Kimara Baruti baadaya siku ya arobaini tokea alipozikwa kwenye makaburi ya Kimara. Baadaya misa hiyo, wafiwa walikwenda makaburini kwa ajili ya kupandaMsalaba na kuweka mashada ya maua kwenye kaburi lake. Mmoja wawalioweka mashada hayo alikuwa ni Dina ambaye baada ya kuweka,akahisi hatia kwenye nafsi yake. Machozi yakaanza kumtoka na kiliocha kimya kimya kikafuata.
Ikabidi apewe msaada wa kuondolewa!

** * * *

Misa ya Richard ilifanyika siku nne tokea misa ya Johnilipofanyika. Misa yake ilifanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Peterlililopo Oysterbay. Dina alihudhuria misa hiyo akiongozana na wazaziwake, na wakati walipokuwa wakitoka Kanisani ili kujiandaa kwendakwenye makaburi ya Kinondoni alipozikwa Richard kwa ajili ya kupandaMsalaba, Dina akasikia akiitwa. Ilikuwa sauti ya kike iliyotoka nyumayake ikimuita kwa jina lake. Alipogeuka akamwona Judi aliyekuwaameandamana na kijana mmoja wa kiume.

Hai Judi! Dinaalisema na kusimama.

Ilikuwa ni mara yao ya pili kuonana tokeawalivyoonana kwa mara ya mwisho walipokutana kwenye msiba waRichard.

Kutana na mchumba wangu, Judi alimwambiaDina.
Anaitwa Martin,

Nafurahi kukufahamu, Dinaalisema huku akimpa mkono Martin. Kisha Judi akamtambulisha Martinkwa Dina.
Martin, kutana na Dina, tulisoma pamoja kuanziakidato cha kwanza hadi cha nne kwenye shule ya Sekondari yaJangwani.

Martin aliyekuwa bado akiliendeleza tabasamu lakeakasema, Nami nafurahi kukufahamu.

Baada ya Dina naMartin kusalimiana, Judi aliufungua mkoba wake na kutoa bahasha,akampa Dina.

Nilihisi tungeonana huku Kanisani, Judialisema.
Nikapata wazo la kuja nayo hii kadi ilinikikuona nikupe. Mungu naye ametuwezesha tumeonana.

Dinaaliipokea kadi aliyopewa ambayo ilikuwa ndani ya bahasha na kusema,Ahsante. Hakuhoji ni ya nini kwa sababu angeifungua na kuisomabaadaye.

Wakaagana.

Akiwa kwenye gari ndogo amekaanyuma pamoja na mama yake huku baba yake akiwa amekaa mbele nadereva, Dina aliifungua bahasha aliyopewa na Judi, akaichomoa kadi nakuisoma. Akagundua ilikuwa ni kadi ya mwaliko inayomwalika ahudhuriesherehe ya kufunga ndoa kati ya Judi na Martin!

Mchomo mkaliukapita na kuuchana moyo wa Dina, akaacha kuendelea kuisoma kadihiyo, akaamua kuangalia nje ambako watu wachache walikuwa wakitembeakando ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi na wakati huohuo magariwaliyokuwa wakipishana nayo yalisikika yakitoa mivumo ya kasi yamwendo. Macho ya Dina yalikuwa yamegubikwa na machozi yaliyomnyimanafasi ya kukiangalia kinachotokea barabarani.

Upepo uliokuwaukiingia kupitia dirisha lililokuwa upande aliokaa Dinauliyapeperusha machozi na kuyasambaza kwenye ncha za macho yakewakati gari hilo likiwa kwenye mwendo.

Akajifuta machozi yau pande mmoja wa jicho lake kwa kutumia kiganja cha mkono wake.

muuza ubuyu culbby @myln amina mabata sam II Analyse
Mkuu nimeona unasema unazo soft copy nyingi, kama unayo ile inaitwa MZEE BEKA part 1 ya huyohuyo gwiji nayo weka hapa
 
Back
Top Bottom