Six Man
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 253
- 892
- Thread starter
- #61
RIWAYA; MTITO WA RAIS
MWANDISGI; HALFANI SUDY
SIMU 0652 212391
Sehemu ya Kumi na Nne
Daniel na Martin wakachukua gari kuelekea nyumbani kwa Daniel Mwaseba.
***
Ulinzi katika nyumba ya Donald Tengo ulikuwa mkubwa sana. Kuibiwa kwa Kasiki yenye mipango yao iliyotekelezwa iligonga taa ya tahadhari kubwa sana kwao. Yeye mwenyewe alihama katika nyumba ile na kuhamia katika nyumba yake mpya huko Goba. Pale, aliacha vijana wa Bahari nyekundu ambao walikuwa tayari kumuua yeyote yule atakayejipendekeza.
Huko Goba, Donald Tengo na Balozi Rwekaza walikuwa sebuleni, nje ya nyumba hiyo kulikuwa na ulinzi mkubwa sana. Vijana wa Bahari nyekundu wasiopungua ishirini walikuwa wanazunguka nje ya nyumba huku na kule. Jukumu lao kuu lilikuwa ni kuhakikisha Donald Tengo na yeyote yule aliyopo mle ndani wanakuwa salama salmin.
Wakati huo, Donald Tengo alikuwa ameshika albamu ya picha waliyoipata nyumbani kwa Daniel. Alianza kuifunua na kuangalia picha mbalimbali zilizomo katika albam hiyo.
Picha ya tatu katika albamu hiyo ilimwacha mdomo wazi. Ilikuwa ni picha ikiyomuonesha Daniel Mwaseba akiwa na mtu aliyemtambua kama Salma Lungu!
"Kumbe huyu malaya anajuana na Daniel Mwaseba?" Donald Tengo alisema akishangaa.
"Nani?" Balozi Rwekaza aliuliza huku akimsogelea katika sofa alilokaa.
"Salma Lungu! Angalia hii picha" Donald alisema akimkabidhi ile albam Mzee Rwekaza.
"Khaa, huyu mwanamke kumbe ni nyoka!" Balozi Rwekaza alisema kwa wah'ka mkubwa.
Donald Tengo alijaribu tena kumpigia simu Salma Lungu. Bado simu yake ilikuwa haipatikani.
"Sasa nimeelewa, muda mrefu nilikuwa najiuliza Daniel alijuaje kuhusu mahali ilipokuwa Kasiki yangu ya siri. Sasa nimepata jibu, ni Salma ndiye aliyemwambia. Bila shaka Salma hakuja kwangu kwa bahati mbaya. Ulikuwa ni mpango wa Daniel Mwaseba. Kumbe Joan alikuwa sahihi. Salma, Salma omba nisikukamate Mwanaharamu wewe, nitakuvunja kila kiungo chako cha mwili!" Donald Tengo alisema kwa hasira.
Mara Joan alifika pale sebuleni akiwa na tarakilishi mpakato mkononi. Alikuwa anatembea kaishika mkono mmoja huku mkono mwengine akiendelea kubonyazabonyaza.
"Simu zenu zote zimedukuliwa!" Joan alisema huku akiwasogelea.
"Zimedukuliwa?" Mzee Rwekaza aliuliza kwa pupa.
"Ndio. Nilikuwa naangalia usalama wa simu zenu. Zote zimedukuliwa, najaribu kuzitoa hapa" Joan alisema huku akibonyaza tarakilishi yake.
Donald na mzee Rwekaza walibaki na mshangao.
"Nimefanikiwa. Sasa mko salama" Joan alisema.
"Unaweza kumjua mtu aliyezidukua simu zetu?" Donald Tengo aliuliza.
"Ni ngumu kujua. Mfumo alioutumia unamficha kabisa, huu ni mfumo wa kisasa sana ambao unamficha mtu aliyewadukua. Lakini la muhimu sasa mko salama" Joan alisema.
"Mdukuaji hajaweza kujua zile simu zetu tulizopiga kwa wajumbe?" Mzee Rwekaza aliuliza.
"Hapana, simu kwa wajumbe ninatumia simu maalum sio simu hii" Donald Tengo alisema.
"Joan angalia hii picha" Mzee Rwekaza alisema.
Joan aliiweka tarakilishi yake juu ya sofa na kuichukua ile picha. Mstuko mkubwa ulionekana alipoiangalia ile picha.
"Daniel yupo na Salma!" Alisema.
"Joan ninataka kujua ni nani huyu Salma Lungu!" Donald Tengo alisema.
"Katika mtandao hakuna taarifa zozote kuhusu Salma Lungu. Nilianza kumchunguza ile siku aliyofika hapa nyumbani. Na ndio maana nilimtilia shaka na kukuomba uachane nae" Joan alisema.
"Yuko wapi huyu Binti?" Balozi Rwekaza aliuliza.
"Aliniaga anaenda kwa wazazi wake kijijiji lakini hadi sasa hajarudi. Nimegundua kwamba alikuwa anaondoka baada ya kumaliza kazi iliyomleta."
Joan aliichukua ile picha. Akaanza kuisachi katika mfumo maalum wa utambuzi wa picha. Majibu waliyoyapata kila mmoja alibaki mdomo wazi.
"Huyu mwanamke anajulikana kwa jina la Elizabeth Neville. Sio Salma Lungu kama alivyojitambulisha. Alikudanganya jina." Joan alisema huku akiitazama tarakilishi yake.
"Elizabeth Neville, ni nani?" Donald Tengo aliuliza.
Joan alianza kutafuta taarifa kuhusu Elizabeth. Baada ya dakika kumi ya kuzama katika mtandao wa majasusi alipata majibu.
"Elizabeth Neville ni Afisa wa Usalama wa Taifa!" Amanda alisema huku akimwangalia Donald Tengo.
"Afisa Usalama wa Taifa! Nilifanya kosa kubwa sana kumruhusu mwanamke yule aingie katika maisha yangu. Ona sasa, amepeleka taarifa muhimu sana kwa maadui zangu. Lazima tumsake huyo mwanamke alipe kwa alichotufanyia. Lazima tumsake huyo Malaya!" Donald Tengo alisema kwa hasira.
***
Wakina Daniel walifika nyumbani kwa Daniel. Hofu ilimpanda Daniel alipokaribia getini.
Geti lilikuwa wazi.
"Hapako sawa hapa" Daniel alisema.
"Bobby Bobby" Daniel alimwita mbwa wake lakini bado kulikuwa kimya. Akaichomoa bastola yake kiunoni. Akiwa na bastola mkononi alikuwa anasogea taratibu huku Martin akimfata kwa nyuma akiangaza huku na kule.
"Bobby" Daniel aliita tena huku akielekea katika banda la mbwa wake. Alipofika alimkuta Bobby akiwa amelala chini akichuruzika damu ya moto. Tundu la risasi bichi likionekana katika tumbo lake.
"Ameuwawa.." Daniel alisema kwa majonzi.
Sasa alielekea ndani kwake. Alizidisha tahadhari maradufu, bastola ikitangulia mbele. Huku Martin naye akiwa na bastola mkononi akiitembeza huku na kule. Walifika sebuleni, mlango nao ulikuwa wazi.
Walipofika sebuleni, walikuta kumetawanywa vibaya sana. Kila kitu hakipo sehemu yake. Kama hiki kilikuwa hapa, basi walikikuta pale.
"Martin, kwa walichokifanya hawa watu hawastahili msamaha hata kidogo" Daniel alisema akiificha hasira yake.
"Daniel tutoke nje!" Martin alisema kwa nguvu.
"Kuna nini?" Daniel aliuliza.
"Kuna hatari tutoke...." Martin alisema huku akikimbia na Daniel naye bila kufikiria alifata nyuma. Walivyofika nje tu mara ulisikika mripuko mkubwa sana. Nyumba ya Daniel ilianza kuwaka moto!
Wakati huo, wakina Daniel walikuwa wamerushwa mbali kwa kishindo cha bomu!
Baada ya kama dakika mbili kila mmoja aliinuka kutoka sehemu yake. Akiwa kachafuka vumbi.
"Tuondoke hapa" Daniel alisema baada ya watu kuanza kujaa. Walienda kimyakimya kwenye gari. Martin safari hii ndiye aliyeendesha.
"Wameteketeza nyumba yangu. Kuna vitu vyangu vingi sana vya thamani mle, wamenitia hasara sana" Daniel alisema kwa majonzi makubwa akijilaza kitini.
"Pole sana Daniel, la msingi tupo salama" Martin alisema huku akiwa makini na usukani.
"Martin, ulijuaje kama kumetegwa bomu mle ndani?" Daniel aliuliza akiwa katikati ya mawazo.
"Ni Hisia tu. Hisia za Martin. Ndio maana nikaitwa Martin Hisia"
"Ahsante sana Martin Hisia. Kwa mara nyingine tena hisia zako zimetuokoa katika hatari. Ila Martin naapa kuwasaka watu wote waliohusika kuichoma nyumba yangu. Hakuna atakayebaki salama, wameuchokoza moto mkali sana, katu hawataweza kuuzima. Naapa, hakuna jiwe litakalobaki juu ya jiwe. Nitayatawanya mawe yote!" Daniel alisema kwa uchungu.
Itaendelea...