Riwaya ya Kijasusi; Mtoto wa Rais

Riwaya ya Kijasusi; Mtoto wa Rais

RIWAYA; MTOTO WA RAIS
IMEANDIKWA "NA HALFANI SUDY
Whatsapp 0652 212391

Sehemu ya Ishirini na Tano

Dokta Viran usiniangushe. Tukifeli katika hili tutakuwa tumefeli sisi na Taifa kwa ujumla. Mimi binafsi nimejipa kazi ya kuchunguza sababu ya kifo cha Aneth, na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wote walihusika. Naomba tusaidiane kuitafuta haki ya huyo binti. Kama ulivyonambia awali, Aneth hakuwa wa kuuwawa namna hiyo, sasa kauwawa. Usiruhusu wauaji watambe mtaani wakati tuna namna ya kufanya ili kuwatia katika mikono ya sheria." Daniel alilalama.

"Daah maneno yako yamenisikitisha sana. Ninaiona dhamira yako ya dhati katika kutafuta haki ya Aneth. Sasa kuna namna moja tu ya wewe kuiona maiti ya Aneth!"

"Njia gani hiyo?" Daniel aliuliza kwa hamu kubwa.

"Ni njia ngumu sana, lakini nd'o njia pekee kama unataka macho yako kuiona maiti ya Aneth. Maiti ya Aneth ipo katika chumba cha kuhifadhia maiti za watu maarufu. Nje kuna ulinzi wa askari wengi sana bila kusahau usalama wa Taifa. Kila daktari anayeenda kule anakaguliwa ipasavyo, na wanahakikisha ni daktari kweli. Njia pekee ya wewe kuingia katika chumba kile ni kufa!

"Unasemaje Dokta Viran?" Daniel alihamaki kwa nguvu.

"Nisikilize Daniel, kama kweli una nia ya kuiona maiti ya Aneth ni lazime ufe, ndipo upelekwe katika chumba ulipohifadhiwa mwili wa Aneth. Tunaweza kufanya hivi, tengeneza kifo chako kisha uletwe hapa. Mimi nitafanya juu chini maiti yako ipelekwe katika chumba ulipo mwili wa Aneth."

"Mfyuuuuuuuuu..." Daniel alipumua kwa nguvu. "Ni njia ngumu sana hiyo. Hakuna njia nyingine Dokta Viran?"

"Daniel ngoja nikwambie kitu kimoja, kifo cha Aneth kimegubikwa na utata mwingi sana. Wakati nimekwambia unipe dakika kumi na tano nitafakari kimetokea kitu cha ajabu sana hapa hospitali."

"Kitu gani kimetokea?" Daniel aliuliza.

"Alikuja askari aliyekabidhiwa kupeleleza kifo cha Aneth akitaka kwenda kuiona maiti ya Aneth. Lakini cha ajabu hata yeye amezuiliwa kuiona. Sasa fikiria, Polisi mwenye dhima na kesi hii amezuiliwa kuiona maiti ya Aneth, je wewe? Hivyo zaidi ya wewe kufa kifo bandia sidhani kama kuna njia nyingine ya kuiona maiti ya Aneth." Dokta Viran alisema kwa kirefu.

"Dokta hapo hospitali kuna monchwari nyingi. Na umesema mwili wa Aneth umewekwa katika chumba maalum. Sasa mimi nikifa nitawekwa katika chumba hicho?" Daniel aliuliza.

"Daniel hayo mengine niachie mimi. Ukiletwa mwili wako hapa nitajua ninafanyaje ukaingizwe katika chumba ulipo mwili wa Aneth."

"Sawa Dokta. Ngoja nione tunafanyaje. Nitakupigia kukutaarifu nitakapofikia." Daniel alikata simu.

Daniel alichukua nafasi ya kuwaeleza wakina Martin yote aliyoongea na Dokta Viran.

"Haiwezekani! Haiwezekani!" Hannan alikataa kwa nguvu." Hatuwezi kufanya mchezo wa hatari kama huo."

"Hannan, hata mimi najua tunataka kufanya kitu cha hatari sana. Lakini lazima tufanye. Lazima nife ili nikaingie mahali ilipo maiti ya Aneth. Hakuna njia nyingine yoyote ya kuiona maiti ya Aneth zaidi ya hiyo."

"Daniel, tunaweza kutumia njia nyingine kuwasaka wauaji wa Aneth na kuwapata. Sio lazima tutumie njia ya hatari kiasi hicho. Tunataka kufanya uchuro Daniel! Je ukifa kweli?"

"Nakubaliana na wewe Hannan." Daniel alisema "Tunaweza kutumia njia nyingine ili kuweza kuwanasa wauaji wa Aneth. Lakini, mimi kuna kitu ninataka kujua. Kwanini wazuie watu kuuona mwili wa Aneth. Kwanini wamzuie hata afisa wa jeshi la Polisi mwenye dhamana ya kupeleleza mauaji haya asiuone mwili wa marehemu. Kuna kitu! Na hiko kitu ndicho ninachotaka kwenda kukiona huko monchwari"

"Daniel..." Hannan aliita, machozi yalikuwa yamemlenga "Kwanini hauheshimu hisia za wengine? Kwanini hauheshimu hisia za watu wanaokupenda? Kwanini mara zote unajari hisia zako tu? Haujui kama maisha yako yana umuhimu na kwa watu wengine pia. Haujuii, haujuii. Usijari hisia zako tu." Hannan alianza kulia.

Daniel alikuwa anashangaa. Hannan aliongea maneno kwa hisia na uchungu mkubwa sana. Alikuwa katika mtihani, lipi afanye?

"Usilie Hannan." Daniel alimsogelea Hannan na kumshika bega. "Usiingize hisia binafsi katika kazi. Tupo hapa kwa ajili ya Taifa letu. Sisi ni vijana wazalendo kwa nchi yetu. Tumeapa kufa ili kuhakikisha nchi hii inakuwa salama. Tumeamua kuyaweka rehani maisha yetu kwa sababu ya mama yetu Tanzania. Najua tunaenda kufanya kitendo cha hatari sana, lakini lazima tukifanye kwa mustkabali wa nchi yetu. Mimi ninaenda kufa kifo cha bandia. Sifi kweli. Hivyo lazima hapa wote tukibariki kitendo hiki. Ili kifanikiwe, na kwa pamoja tufanikiwe. Tuwajue madhalimu hawa wa taifa letu, umenielewa Hannan?"

Hannan alipangusa mafua huku akitingisha kichwa. Alikubali. Aliubariki mpango huu wa Daniel Mwaseba.

"Ndugu zangu, kuna mwingine yeyote ana wasiwasi juu ya tunachoenda kukifanya?"

Watu wote walikuwa kimya. Walikuwa wamekubaliana na mpango wa kifo cha bandia cha Daniel Mwaseba.

***

Saa mbili baadae, mtandao wa kijamii ulichafuka tena. Ikiwa bado kifo cha Aneth kikitawala mtandaoni, ikafata taarifa nyingine ya kusikitisha sana.

'Mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel Mwaseba alikuwa ameuwawa na watu waliosadikiwa kuwa ni majambazi'

Habari hii ilisambaa mithili ya upepo wa Kimbunga. Kutokana na umaarufu wa Daniel, taarifa ya kifo chake ilifunika ile ya kifo cha Aneth.

Vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa vilitawaliwa na habari hii. Kenya iliandika. Uganda iliandika. Rwanda iliandika. Nigeria iliandika. Sudan iliandika. Burundi iliandika. Afrika yote ilizizima. Kifo cha Daniel Mwaseba kilikuwa ni alama ya umoja wa Bara la Afrika.

Nyumbani kwa Daniel, Hannan alikuwa analia isivyo kawaida. Ingawa alijua ni kifo bandia lakini kwake alihisi kama Daniel amefariki kweli. Hakuweza kuyadhibiti maumivu makubwa yaliyopo moyoni mwake. Lilikuwa ni pigo lililo juu ya uwezo wake.

Taarifa za kifo cha Daniel Mwaseba zilipokelewa kwa furaha sana na maadui zake. Watu wasio penda amani ya dunia, wahalifu, wauzaji wa madawa ya kulevya. Wao kwao kifo cha Daniel kilikuwa ni jambo jema sana. Walishukuru kwakuwa mtu aliyekuwa anakwamisha mambo yao alikuwa amefariki.

Nyumbani kwa Donald Tengo ilikuwa ni furaha. Walipanga jioni wafanye sherehe kufurahia kifo cha Daniel Mwaseba. Furaha yao ilikuwa haina mfano. Maana kwasasa walikuwa wamepiga hatua nyingi sana mbele kukamilisha mipango yao.

Mwili wa Daniel Mwaseba ulipelekwa hospitali ya taifa ya Muhimbili. Hospitali ambayo ilikuwa inalindwa vibaya sana kwa kipindi hiko. Ingawa ilikuwa ngumu sana, lakini Dokta Viran alipambana mpaka mwili wa Daniel ulipelekwa katika chumba ulipohifadhiwa mwili wa Aneth.

Mpango uliopangwa, sasa ulikuwa katika utekelezaji. Daniel alikuwa amekubali kufanya jambo la hatari sana kwa maslahi ya nchi yake.

Nje ya chumba cha maiti, walikuwepo watu wengi sana. Wengi wakiwa ni watu kutoka katika vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama. Miongoni mwa watu hao alikuwepo Martin Hisia, ndugu wa pekee wa Daniel kwa wakati ule. Macho ya Martin yalikuwa hayatulii sehemu moja. Kila sekunde yakipepesa huku na kule. Yakimchunguza kila mtu yamwonaye. Akiwa pale nje, aliona mambo mengi yasiyokuwa ya kawaida. Hii ilimwaminisha kwamba kuna kitu cha ziada katika msiba huu.

Ni kitu gani hiko?.

Hapo ndipo kwa moyo wote, bila wasiwasi hata chembe alikubaliana na mpango wa Daniel Mwaseba. Ingawa kwake pia ilikuwa ngumu sana kukubaliana na mpango huu wa kifo bandia cha Daniel Mwaseba. Lakini ushawishi wa Daniel ulimfanya akubaliane nao. Kwake, ugumu ulikuwa ni vipi wazazi wa Daniel watachukulia taarifa za kifo cha mtoto wao? Vipi Chifu ataichukulia taarifa ya kifo cha Daniel? Raia je?. Lilikuwa ni jambo gumu kulikubali, lakini lilipaswa lifanywe. Alipokuwa pale alikiri kweli hii ndio ilikuwa namna pekee kuingia mle ndani kama alivyoshauri Dokta Viran. Hakukuwa na njia nyingine yoyote ile.

Martin akaanza kufanyia kazi mpango wa kifo cha Daniel. Alienda kwa Samson na kupanga namna ya kufanya ili Daniel aonekane ameuwawa na watu kutoka katika kikundi chao, lakini watambulike kama majambazi. Mpango ulienda sawa, risasi tatu zilipenya katika kifua cha Daniel Mwaseba, lakini zilikutana na kizuia risasi. Daniel alirushwa juu na kubwaga chini katika makutano ya barabara ya Keko! Wote walioona kitendo hiko waliamini kwamba Daniel alikuwa ameuwawa kweli!. Hapo ndipo taarifa za kuuwawa kwa askari zilisambaa kwa kasi, kabla ya baadae kusemekana askari huyo aliyepigwa risasi ni Daniel Mwaseba. Kutokea hapo, maiti ya Daniel ilipelekwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, ambapo Dokta Viran alisimamia kila kitu kuhakikisha mwili wa Daniel unapelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti alichomo Aneth.

Na kwasasa Daniel alikuwa ndani...

Itaendelea...
 
mkuu tuongezee japo kimoja basi
 
RIWAYA; MTOTO WA RAIS
IMEANDIKWA NA HALFANI SUDY
SIMU 0652 212391

Sehemu ya Ishirini na Sita

Na kwasasa Daniel alikuwa ndani...

Wakati hayo yakipita katika kichwa cha Martin Hisia, ndipo alipomwona yule mzee. Martin aliacha kuwaza na kuanza kumwangalia mzee Kizito. Mzee waliyekuwa wanamtafuta kwa udi na uvumba leo alikuwa mbele yake. Tena mita chache tu kutoka mahali alipokuwa amesimama.

"Leo nitakula naye sahani moja. Siku zinaenda na Aisha anahitaji dawa za kumfanya aendelee kuishi. Lazima nimfatilie mtu huyu ili usiku tukavamie nyumbani kwake. Lazima tumsaidie Salum Taiwan, namuonea huruma sana kwa aliyopitia" Martin aliwaza kipindi hiko macho yake ya kipelelezi yakiwa hayabanduki kwa Mzee Kizito.

Kizito alikuwa amesimama peke yake, mita kama kumi na tano toka mahali alipo Martin Hisia. Yeye alikuwa pale kwa lengo moja tu, kuthibitisha ukweli wa taarifa ya kifo cha Daniel Mwaseba. Akiwa mahali aliposimama, mara uliingia ujumbe katika simu yake. Aliitoa simu yake mfukoni, na kuanza kuusoma. Ulikuwa ujumbe mfupi kutoka kwa Donald Tengo, na ulikuwa unasomeka hivi.

'Simu ya Aneth imewashwa katika nyumba moja huko Tabata. Andaa watu mwende'

Naye akaujibu..

'Kwanini wasiende jeshi la Polisi. Tutumie Polisi wetu kisha tutawapoteza hao watu wakiwa Gerezani'

Baada ya sekunde chache, alijibiwa.

'Polisi kwa sasa hapana, bado hatujamweka mikononi mwetu Mpelelezi wa kesi hii. Vijana wa Bahari nyekundu nd'o wanapaswa kwenda. Pia ingependeza kama Polisi wetu wangeenda endapo tungemjua mmiliki wa hiyo nyumba na kaipata vipi simu ya Aneth. Tunawahitaji hao watu kwa mahojiano kwa maana kuna majibu tunayataka kutoka kwao'

Baada ya kuusoma, Kizito akautuma mwengine.

'Sawa nimekuelewa, kwahiyo hii kazi ya hapa niachane nayo'

'Achana nayo, Taarifa tulizozipata ni kuwa Daniel Mwaseba hajafariki kweli. Ni mchezo tulichezewa.'

'Aisee kumbe, ngoja nielekee huko Tabata'

'Kazi njema, nitakupa uelekeo ukiwa njiani'

Baada ya majibizano hayo Kizito akaanza kuondoka. Alielekea mahali alipopaki gari yake na kuingia ndani yake. Kitu ambacho alikuwa hakijui ni kuwa, Martin Hisia alikuwa nyuma yake. Akikanyaga kila mahali ambapo alitoa mguu wake.

Safari ya Kizito kwanza ilielekea Mikocheni, kambini kwa vijana wa Bahari nyekundu. Aliongeza nguvu ya vijana mahiri sita. Baada ya kutoka Mikocheni alielekea Tabata tayari kwenda kufanya uvamizi katika nyumba aliyoambiwa na Donald Tengo. Magari manne nyuma yake kutoka katika magari yao, ndipo kulikuwa na gari la Martin Hisia. Martin alikuwa akifatilia kwa umakini sana gari la kina gari la kina Kizito.

Gari la kina Kizito lilipofika katika makutano ya taa za TAZARA lilikata kushoto. Njia iliyokuwa inaelekea Ubungo, kupitia Tabata. Hapo ndipo hisia za Martin zilipohisi. Alihisi kitu, alihisi jamaa walikuwa wanaelekea nyumbani kwa Daniel Mwaseba, ambapo ni maskani yao kwa sasa.

Martin alichukua simu yake. Akatafuta harakaharaka kwenye orodha ya majina, akaiona namba akiyoitafuta, namba ya Hannan. Akabofya kitufe cha kijani cha kupigia huku akiwa makini na usukani.

"Nambie Martin, vipi mmefanikiwa?" Hannan aliuliza kwa pupa alipopokea simu ya Martin.

"Hannan nisikilize kwa umakini. Kwasasa nipo hapa TAZARA namfatilia yule jamaa, lakini cha kushangaza nimemwona anafuata uelekeo wa huko nyumbani kwetu"

"Nani Martin? Anakuja huku kwetu kapajuaje?" Mfululizo wa maswali ulimtoka Hannan.

"Usiwe na wasiwasi Hannan, Kizito anakuja huko nyumbani. Tupo katika foleni hapa. Sasa fanya hivi, wakusanye watu wote hapo, katika chumba cha mateso kuna kabati jeusi. Lisukume pembeni hilo kabati, kisha chukua rimoti nyeupe ipo juu ya runinga. Ukifika mahali ulipotoa kabati bonyaza kitufe chekundu cha hiyo rimoti, kipo upande wa kushoto kwa juu. Ukuta utafunguka. Ingieni humo mjifiche. Mkifika ndani bonyaza kitufe cha kijani, ukuta utajifunga. Naamini mtakuwa salama maana kuna kila kitu ndani ya chumba hiko cha siri. Humo kuna chakula cha kuwezesheni kula hata mwezi"

"Mart.."

"Fanya hivyo Hannan! Sio muda wa maswali huu.." Martin alisema kwa ukali na kukata simu.

Hannan alitekeleza maagizo, alienda katika chumba walichokuwemo kina Candy, akawachukua. Na kwenda kuwaweka mahali alipoambiwa na Martin. Akaenda chumbani kwa Salum na Aisha, nao akawapeleka katika chumba cha siri. Akawafuata wakina Karim waliokuwa sebuleni.

"Jamani nimepigiwa simu na Martin. Kasema tunakuja kuvamiwa, yatupasa kujificha kwa muda" Hannan alisema kwa pupa.

"Kujificha? Sisi ni wapambanaji. Kwanini tusipambane badala ya kujificha" Leonard alikataa.

"Inaonesha wapo wengi. Inaweza kuwa ngumu kwetu kupambana" Hannan alisema.

"Sisi ni watoto wa Samson. Tumekamilika katika kupambana na maadui wa aina zote. Ngoja tukuoneshe kazi" Karim alisema bila wasiwasi wowote.

Mara simu ya Hannan iliita. Alikuwa ni Martin.

"Tupo karibu sana na hapa nyumbani. Vipi umefanikiwa kufungua ukuta"

"Nimefanikiwa Martin. Nimewaficha wakina Salum. Lakini kina Leonard wamekataa, wamesema wanataka kupambana nao" Hannan alisema.

"Kuna watu kumi na moja wenye silaha ndani ya Noah. Wataweza kupambana nao kweli?" Martin aliuliza.

Mara, Leonard alipora simu kutoka kwa Hannan. Leonard alisema neno moja tu.

"Tutapambana!" Akakata simu.

Baada ya Leonard kukata simu. Alianza kuwapanga vizuri watu wake. Ni kweli waliamua kupambana na vijana wa Bahari nyekundu.

"Amini, utapanda juu ya ule mti, utadungua kila mtu atakayejipendekeza katika upande wako. Amani utapanda katika ule mti mwengine, jukumu lako ni kama la Amini, kumdungua yeyote yule utakayemwona katika upande wako. Leonard na mimi tutabana humu ndani, ninajua tutawachezesha kindumbwendumbwe tutakavyo" Karim alisema.

Harakaharaka, vijana walichukua nafasi zao. Wakiwasubiri vijana wa Bahari nyekundu.

Gari aina ya Noah ilipaki mita chache kutoka katika nyumba ya Daniel Mwaseba. Kutokana na nyumba kujitenga kidogo na nyumba nyingine iliwapa urahisi kupanga na kwenda kutekeleza walichopanga. Mzee Kizito ndiye aliyewaongoza vijana kumi wa Bahari nyekundu katika operesheni hii.

Martin, alikuwa amepaki gari yake mbali kidogo na ile nyumba ya Daniel. Moyoni mwake hakukubaliana hata kidogo na mpango huu wa kina Karim. Aliiona hatari ya kupambana na watu wale. Idadi yao na silaha walizozibeba zilimwogopesha sana. Lakini kubwa zaidi, alikuwa anamhitaji Kizito akiwa hai ili awasaidie kupata dawa za mtoto Aisha.

Baada ya dakika mbili za maelekezo, vijana wa Bahari nyekundu walielekea nyumbani kwa Daniel. Vijana watano walizunguka kwa nyuma, huku vijana sita akiwemo na Kizito wakipita kwa mbele. Mahali lilipokuwa geti.

Itaendelea..
 
RIWAYA; MTOTO WA RAIS
IMEANDIKWA NA HALFANI SUDY
SIMU 0652 212391

Sehemu ya Ishirini na Saba

Baada ya dakika mbili za maelekezo, vijana wa Bahari nyekundu walielekea nyumbani kwa Daniel. Vijana watano walizunguka kwa nyuma, huku vijana sita akiwemo na Kizito wakipita kwa mbele. Mahali lilipokuwa geti.

***

Amani aliyekuwa juu ya mti aliliona kundi lile la watu likielekea getini. Na bunduki zao mkononi. Akaona ule ndio muda muafaka. Akakoki bunduki yake. Akamlenga kijana mmoja aliyekuwa anakaribia kuligusa geti.

Akafyatua!

Ilimpata!

Kijana alisukumwa nyuma kwa nguvu na kujibwaga chini kama mzigo usiohitajika tena. Kichwa kilikuwa pese'pese kwa nguvu ya risasi. Kijana hakuthubutu kusema neno lolote lile. Atasema nini wakati alikuwa ameiaga dunia.

Shambulio lile la ghafla likawastua wakina Kizito. Hawakutegemea hata kuwahiwa namna ile. Lakini, liliwafanya wajipange vizuri

"Kuna Mdunguaji! Laleni chini.." Kizito akawatahadharisha wenzake.

Yeye na wengine watatu walilala chini. Lakini kwa bahati mbaya kwao, mmoja alichelewa. Hilo ilikuwa hasara kwake na faida kwa Mdunguaji. Kifua chake kinene kilididimizwa risasi kutoka katika bunduki ya Amini. Naye alitupwa kwa nguvu hatua kadhaa nyuma. Safari hii Kizito alikuwa makini, wakati akilala chini aliona mahali risasi ilipotokea.

Juu ya mti.

Akiwa pale chini alijipanga vizuri. Akakoki bastola yake vizuri. Sasa akaanza kuitafuta nafasi ya kumwonesha Mdunguaji yeye ni nani?. Amini naye alibaki kimya. Kwa jinsi jamaa walivyolala nje ya ukuta hakuweza kuwaona. Hivyo alitulia huku bunduki yake ikielekea getini.

"Mdunguaji yupo juu ya mti upande wa kulia" Kizito aliwaambia wenzake kwa kunong'ona.

"Inabidi tutumie ujanja kum.." Kizito hakumaliza kuongea. Wakasikia mlio wa bunduki. Wakajua na upande wa wenzao nako kumekucha.

"Wanashambuliwa" Kizito alisema kwa hamaki.

'Paaa!' Mlio wa risasi ukasikika tena na ukelele mdogo. Katika hesabu yake akajua watu wake wawili wameuwawa.
Kizito kwa kutambaa alianza kuuzunguka ukuta kuelekea upande wa kulia. Ukuta ulimsaidia kumkinga, hakuonwa na macho ya Amini. Kizito alitambaa mpaka pembeni ya nyumba. Usawa ulipokuwa mti alimwona adui akiwa kampa mgongo. Hapo ndipo mahali alipokuwa anapataka.

Kizito akanyanyuka taratibu akifichwa na ukuta. Wakati huo, Amini alikuwa makini na kule getini. Akisubri wale jamaa wafanye tena kosa awaadhibu. Kumbe kosa alilifanya yeye.

Kizito alilenga vizuri shabaha, akaachia risasi iliyotua katikati ya mgongo wa Amini. Amini aliporomoka kule juu kama furushi.

Baada ya kumuua Amini, Kizito alitambaa na ukuta kuelekea nyuma ya nyumba. Alijua kule nako kutakuwa na Mdunguaji mwengine aliyewashambulia lile kundi lingine. Alipokaribia kuumaliza ukuta alinyanyuka kwa juu kidogo. Aliuona mti mwingine. Akajua Mdunguaji lazima atakuwa katika mti huo. Akabonyea chini kidogo akiiweka sawa bastola yake, akaibusu, baada ya kama sekunde kumi alinyanyuka tena huku akiachia risasi moja.

Alimpata!

Amani alidondoka chini kama embe bivu baada ya kupatwa na risasi ya kichwa. Kizito alitambaa vilevile kuelekea upande wa geti.

"Jaribu kufungua geti" Kizito alisema alipowakaribia wenzake.

Kijana mmoja alijaribu kufungua geti. Hakuweza, lilikuwa limefungwa.

Wakati huo, Martin Hisia alikuwa amejibanza katika kona moja mita kadhaa. Aliwashuhudia wakina Kizito wakiwa wamejilaza pale getini. Na masikio yake yalisikia makelele ya watu baada ya mlio wa bunduki. Martin aliona ule ni muda muafaka wa kufanya kitu ili kuokoa maisha ya wenzake.

Martin alianza kunyata taratibu kuelekea nyumbani kwa Daniel. Ilikuwa bahati yake kwakuwa alisaidiwa kujificha katika miti iliyokuwepo eneo lile. Kwa kasi akatoka mti aliokuwepo na kuufata mti mwingine.

Lakini hakufika. Kwani ukitaka afike wapi?.

Ghafla, alikwapuliwa na risasi ya bega na kutupwa chini. Mlio wa risasi hiyo ukawastua wakina Kizito. Waliacha kutafuta namna ya kuingia ndani na kugeuka nyuma. Walimwona mtu akigalagala chini kama kambale. Hakuna aliyejua yule mtu alikuwa ni nani?.

"Hapa sio salama. Tuondokeni.." Kizito alisema kwa pupa.

"Wakina John je?" Kijana mmoja aliwaulizia wenzake waliozunguka kule nyuma.

"Ni wanaume wale, watajua cha kufanya" Kizito alisema huku akichukua hatua. Kwa mwendo wa tahadhari alielekea mahali walipoliacha gari lao. Na wenzake wakimfata nyuma. Mikono yenye bastola ikiyumba huku na kule kwa namna ya ajabu, kuhakikisha usalama wao.

Walifika garini salama.

Kizito aliwasha gari na kuling'oa kwa kasi. Njiani ilikuwa kimya. Hakuna aliyetegemea kama watakutana na upinzani wa aina ile. Walihisi ni misheni ndogo lakini walikuwa wamepoteza watu wanne huku watu watatu wakiwa hawaijui hatma yao.

"Sijaelewa hata kidogo kitu gani kimetokea?" John aliipata sauti yake wakiwa garini.

"Jamaa walikuwa wamejipanga kisawa'sawa. Bila shaka walikua wanafaham juu ya ujio wetu" Kizito akatoa maoni yake.

"Wamejuaje sasa?" Sengo aliuliza.

Hakuna aliyemjibu, kwani hakukuwa na aliyekuwa na jibu sahihi la kujibu. Angetokea wapi?.

Itaendelea...
 
Back
Top Bottom