Kijana wa Ifoza
JF-Expert Member
- Oct 31, 2025
- 1,180
- 2,302
⚠️ ANGALIZO LA MWANDISHI (DISCLAIMER)
Makala hii ni kazi ya sanaa ya kubuni (Fiction Story/Creative Writing). Mtunzi amebuni majina ya wahusika, matukio, na maeneo (ikiwemo nchi ya kufikirika ya Ugagagigikoko na mtawala Malkia Huihui) akivuta kumbukumbu zake za utotoni wakati akisoma vitabu vya kale vya waandishi mashuhuri kama Padri Alfons Loogman, hususan mfululizo wa vitabu vya masomo vya "Someni kwa Furaha". Majina haya yametokana na msukumo huo wa kifasihi kwa madhumuni ya kuburudisha, kuelimisha, na kushirikiana mawazo na jamii ya JamiiForums kama zilivyo hadithi nyinginezo za kubuni zinazochapishwa hapa jukwaani.
Uzi huu haujalenga, haujataja, wala hauhusiani na mtu yeyote, kiongozi yeyote wa sasa au wa zamani, wala nchi yeyote halisi iliyopo duniani. Kufanana kwa tukio, jina, au mwaka wowote na hali halisi ni sadfa tu ya kiugunduzi (coincidence) na kusiichukuliwe kama ukweli wa kihistoria au kisheria.
Katika nchi ya Ugagagigikoko, ukweli ni bidhaa ya anasa na uzalendo ni kosa la jinai; karibu kwenye kasri la Malkia Huihui, mahali ambapo sahani ya uongozi inasafishwa kwa nidhamu ya woga.
Safari ya nchi hii ilianza rasmi mwaka 1961 pale lilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa wakoloni, likiwa na ndoto ya kujenga jamii yenye usawa, utu, na heshima kwa mwanadamu.
Hata hivyo, hatua kubwa iliyokuja kuubadili mwelekeo wa kijiografia na kisiasa wa taifa hili ilitokea miaka michache baadaye. Baada ya nchi ndogo jirani kufanya mapinduzi ya damu mnamo Januari 1964, upepo wa hofu na taharuki ulitanda ukanda mzima. Miezi kadhaa baadaye katika mwaka huo huo wa 1964, viongozi wawili wakuu walikutana faragha, kwa siri kubwa na bila kuwahusisha wananchi wao wa kawaida.
Katika meza hiyo ya faragha, walifanya maamuzi mazito ya kuunganisha nchi zao mbili na kuzaa jamhuri mpya ya muungano—jamhuri ambayo leo hii inakabiliwa na dhoruba nzito. Lakini historia haikuwa na huruma; muda mfupi tu baada ya muungano huo, mmoja wa viongozi hao waasisi aliuawa kinyama kwa kupigwa risasi (assassinated), tukio lililoacha kovu lisilofutika kwenye mioyo ya raia.
Enzi za Weledi na Utendaji wa Kizalendo Licha ya changamoto na matatizo madogo madogo ya kiuongozi yaliyokuwepo wakati huo, serikali za awamu ile zilijengwa juu ya misingi thabiti ya weledi. Ofisi nyeti za serikali, kuanzia idara za usalama, uchumi, hadi diplomasia, zilikasimiwa mikononi mwa watu wenye weledi wa hali ya juu na usomi uliotukuka. Viongozi waliteuliwa kwa vigezo vya uwezo, nidhamu, na mapenzi mema kwa taifa, si kwa kujuana au sifa za kijinga.
Mabadiliko makubwa yalianza kutokea pale kizazi kile cha wakongwe na waasisi kilipoamua kung'atuka kwa hiyari na kuachia damu changa usukani. Tofauti na matarajio kwamba damu changa ingeleta ubunifu na kasi mpya, ndipo milango ya mmomonyoko wa maadili ilipofunguka rasmi katika nchi ya Ugagagigikoko.
Asili ya Nguvu za Malkia Huihui Katikati ya mmomonyoko huu ndipo unapoibuka utawala wa Malkia Huihui. Hakufika kwenye kiti cha enzi kwa bahati mbaya au kwa nguvu ya kijeshi. Hapo mwanzo, alijipenyeza ndani ya mfumo akitumia taswira ya weledi na weledi wa hali ya juu uliowahadaa wengi. Alionekana kama lulu kati ya damu changa.
Hata hivyo, mara baada ya kukamata hatamu za nchi, alirithi na kuuboresha ule mfumo mbovu wa "kujuana." Alitupa kando weledi wote aliouhubiri hapo awali na kuweka mbele utii kamili kwake binafsi. Kiti chake cha enzi kiligeuka kuwa sumaku inayovuta watu wasio na uwezo lakini wenye ndimi za sifa.
Saikolojia ya Kiutawala ya Kasri Kuu
Kisaikolojia, Malkia Huihui anaishi kwenye ulimwengu wa migongano ya ndani. Kwa nje, anajionyesha kama kiongozi mwenye tabasamu la huruma, mlinzi wa wanyonge, na mama wa taifa la Ugagagigikoko. Lakini nyuma ya pazia la tabasamu hilo, kuna hofu kubwa na ya kudumu ya kupoteza madaraka. Hofu hii inamfanya awe kiongozi asiyevumilia kabisa kukosolewa au kuhojiwa.
Amejenga mazingira ambapo sifa za genge la "Chawa" ndizo zinazomfanya ajione yuko salama. Anapenda kusikia akilinganishwa na miungu, na kila anayetoa ushauri wa kitaalamu na wa weledi anatafsiriwa moyoni mwake kama adui anayetaka kumpindua. Ukipishana kauli naye, ujue siku zako kwenye sahani ya uongozi zinahesabiwa.
Sauti za Wazalendo na Msukosuko wa akina Bulicheka
Katika mazingira haya ya kisaikolojia ya Malkia Huihui, idadi ndogo ya wataalamu na weledi waliobaki, ambao bado wanaamini katika uzalendo wa kweli na misingi ya utaifa (nationalism), wamejikuta kwenye wakati mgumu sana. Sauti kama za Bulicheka na mkewe Lizabeta—wasomi, walimu wa itikadi ya kale, na wataalamu waliolelewa kwenye misingi ya weledi—zimebaki kuwa maadui wakubwa wa utawala wa Kasri.
Bulicheka, kama mwalimu aliyewahi kushika hatamu za juu ndani ya mfumo, alianza kuona misingi inachezewa na Katiba ikidhulumiwa. Alipojaribu kupaza sauti yake kiweledi kuonya kuwa nchi inaelekea kuwa Banana Republic, dhoruba kali ilimshukia. Genge la Chawa wa Malkia lilimshambulia kwa propaganda kuwa "ametumwa na mabeberu wa baharini," akavuliwa nyadhifa zake zote, akavamiwa, na hatimaye kujikuta kwenye misukosuko mizito ya kiusalama iliyomwondoa machoni pa umma.
Mtikisiko huo haukuishia hapo. Hata wale wasomi wakubwa kama akina Dr. Lizabeta, ambao walikuwa wameshika nafasi nzito za juu kabisa kwenye sahani ya uongozi, hawakusalimika. Mara tu Lizabeta alipojaribu kuunga mkono sauti za wanaharakati zinazotaka mfumo wa haki na maridhiano ya Katiba mpya, alipishana kauli na Malkia Huihui. Ndani ya muda mfupi, siku zake kwenye sahani ya uongozi zilihesabiwa; alikabiliwa na shinikizo kubwa na dhoruba za kisiasa zilizomlazimisha kujiuzulu na kuondolewa kwenye korido za madaraka.
Genge la "Chawa" na Geuzi la "Banana Republic"
Nchi ya Ugagagigikoko ilianza kugeuzwa kuwa shamba la kuporwa na yeyote mwenye nguvu au ushawishi. Mfumo wa kupandisha watu vyeo ukabadilika kutoka kwenye sifa za kimasomo na kiutendaji, na kuwa mfumo wa kujuana, undugu, na urafiki. Leo hii, taifa limefika kwenye ukomo wa weledi (the death of meritocracy) na linaelekea kwa kasi kubwa kuwa nchi inayostahili kuitwa Banana Republic (Jamhuri ya Ndizi)—mahali ambapo sheria za nchi hazifuatwi kabisa na zinasokotwa kulinda maslahi ya wachache.
Kumezuka utamaduni mpya wa ajabu ambapo heshima kubwa haitolewi tena kwa usomi, ugunduzi, au utendaji uliotukuka. Badala ya usomi huo, kuwa CHAWA—kusifia viongozi bila utafiti, kupiga magoti, na kujipendekeza—ndiyo kigezo kikuu cha kupata nafasi kubwa serikalini na kwenye jamii. Elimu na weledi vimepoteza thamani; ulimi wa sifa za uongo umekuwa mtaji mkubwa wa mafanikio.
Demokrasia ya Picha na Mfumo wa Vyama Vingi
Historia ya kisiasa ya Ugagagigikoko ililazimika kubadilika miaka kadhaa nyuma pale ilipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa. Hata hivyo, mabadiliko haya hayakutokana na nia dhati ya kisiasa ya viongozi wake, bali ilikuwa ni shinikizo la lazima kutokana na upepo wa mabadiliko ya kidemokrasia yaliyokuwa yanatokea duniani kote. Ili kuonekana inaenda na wakati, nchi oliweka mfumo huo kama picha tu ya nje, huku Katiba Mama ikizuiwa katakata kubadilika ili kulinda utaratibu wa zamani.
Hadi leo hii, Ugagagigikoko bado inaongozwa na mfumo wa vyama vingi ulioridhia na kujikita kabisa kwenye muktadha, fikra, na misingi ya chama kimoja cha kikoloni. Mfumo huu chini ya Malkia Huihui unawafanya wapinzani wa kweli wenye nia thabiti ya kuleta mabadiliko wajione kama siyo raia wema, bali maadui wa taifa. Badala yake, nafasi na upendeleo vinatengewa kwa ajili ya "wapinzani wa kupangwa" au mamluki wanaotumika kuhalalisha igizo la demokrasia machoni pa jumuiya za kimataifa.
Mbinu za Kudhibiti Mihimili: Bunge na Vyombo vya Dola
Ili kuhakikisha mfumo huu wa vyama vingi vya picha hautikisiki, Malkia Huihui anatumia mbinu za kisayansi kudhibiti mihimili yote kama fimbo yake binafsi. Bunge la Ugagagigikoko limegeuzwa kuwa muhuri wa kupitisha matakwa ya serikali yake badala ya kuwa chombo cha kuisimamia. Wabunge wamekuwa washangiliaji wa miswada inayokandamiza wananchi, wakitazama maslahi yao ya matumbo kuliko viapo vyao.
Wakitazama Bunge likishona sheria kandamizi, Vyombo vya Dola navyo vimepewa jukumu jipya; badala ya kulinda raia na mali zao, vimegeuzwa kuwa silaha za kisiasa za kutesa, kutisha, na kuzima sauti yoyote inayojaribu kuamsha wananchi. Polisi na vyombo vya kiusalama vimekuwa virungu vya kulinda koti la kifalme la Malkia dhidi ya ukweli.
Kuminywa kwa Mhimili wa Nne (The 4th Estate)
Katika rasimu hii mpya ya uendeshaji wa Ugagagigikoko, Mhimili wa Nne wa Dola (Vyombo vya Habari) umeminywa koo kiasi cha kukata pumzi kabisa. Waandishi wa habari na vyombo vya utangazaji, ambao walipaswa kuwa kioo cha jamii na walinzi vya haki, wamewekwa chini ya ulinzi mkali wa kisheria na kiuchumi.
Kupitia sheria dhalimu za habari, faini kubwa, na vitisho vya kufungiwa, utawala wa Malkia Huihui umefanikiwa kuingiza hofu mioyoni mwa wanahabari. Waandishi wanaojaribu kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ufisadi au ukiukwaji wa haki wanatishiwa, wanatekwa, au kufutwa kazi. Mhimili huu sasa hivi umelazimishwa kuimba nyimbo za sifa (propaganda), ukifanya kazi ya kuwasafisha viongozi wasio na weledi na kuficha madhila yanayowapata wananchi wa kawaida.
Utawala wa Matajiri (Plutocracy)
Licha ya nguvu zote hizi za kifalme, Malkia Huihui hayuko peke yake; anashirikiana kwa karibu sana na genge la matajiri wakubwa wenye ukwasi wa kutisha. Hapa ndipo mbinu yake kuu ya kudhibiti inapoonekana: anawapa matajiri hawa ulinzi wa kibiashara, misamaha ya kodi ya upendeleo, na fursa za kupora rasilimali za Ugagagigikoko, na kwa kubadilishana, matajiri hao wanakuwa wafadhili wakuu wa mifumo yake ya kisiasa na kampeni za kudumisha utawala.
Maamuzi ya kisera na sheria za kodi vinatengenezwa kukidhi matumbo ya wenye fedha hawa, huku mwananchi wa kawaida akiachwa akitaabika. Kutoka kwenye nchi ya mfano wa maadili na uzalendo, Ugagagigikoko sasa imekuwa mateka wa mifumo isiyo na weledi, inayotawaliwa na upendeleo wa kujuana na usiri mkubwa unaoendelea kumnyonya mnyonge.