Riziki mafungu saba: Kijana muuza kashata aliyegeuka mfanyabiashara mwenye mafanikio

Riziki mafungu saba: Kijana muuza kashata aliyegeuka mfanyabiashara mwenye mafanikio

Mnamo mwaka 2018, kuna kijana mstaarabu sana aliyeishia darasa la tano ambaye nilifahamiana naye kupitia mwalimu mmoja aliyekuwa amepanga nyumbani kwetu. Huyu kijana alikuwa anamletea mwalimu kashata siku za wikendi, hivyo mara nyingi alikuwa ananikuta nyumbani.

Kijana huyu alikuwa na haiba ya ucheshi na alikuwa mchangamfu mno. Baada ya kuendelea kuja pale kwa muda mrefu, tukawa tumezoeana mpaka tukabadilishana namba za simu. Alionekana kunipenda ila hakuwahi kuniambia, na hata kama angeniambia, nisingemkubalia kwa sababu tulipishana sana kielimu na hakuwa na hadhi ya kuwa na mimi.

Baada ya mwaka mmoja kupita, yule mwalimu aliyezoea kuletwa kashata alimpigia simu kijana huyo akihitaji mzigo wa kashata. Kijana yule alimwambia kwamba kwa sasa hawezi kuuza kashata kwani ameacha kazi hiyo na anauza mkaa maeneo ya Buguruni.

Tangu mwaka 2019 mpaka leo, sikuwahi kuwa na mawasiliano naye na sikuwahi kumtafuta licha ya yeye kupoteza namba yangu.

Jioni moja mida ya saa kumi na moja, nikiwa natokea mjini nimekaa kule juu kwenye pantoni nikiwa nawaangalia watu waliokuwa wanazozana chini, nilitupa jicho kwenye gari moja aina ya Toyota Lumion. Nilimuona yule kijana muuza kashata akiwa kwenye usukani. Nilishuka haraka nimuangalie vizuri kama ni yeye. Naam, ni yeye!

Tulishuka kwenye pantoni na akaniambia nimsubiri pahala ani drop nyumbani. Nilishangaa jinsi huyu muuza kashata ameweza kupata mafanikio mpaka kununua gari. Tuliongea mengi sana.

Kijana huyo aliniambia kwamba baada ya kuacha kuuza kashata, alijikita kwenye biashara ya mkaa maeneo ya Buguruni. Kwa sasa ana ofisi za mkaa kama kumi Dar es Salaam na ameajiri watu wengi! Alinambia biashara ya mkaa ina faida sana.

Nimestaajabu!
Achana Na huyo, kuna mwingine alikuwa anauza madafu tu mtaani, siku moja akaokotwa huko barabarani akaambiwa ikulu nalo ni soko zuri la kuuzia madafu. Baada ya siku chache muuza madafu akageuka Na kuwa komando mkubwa sana wa jeshi, kiasi cha kushuka Na kamba kutoka angani.

Duniani kila kitu kinawezekana
 
Back
Top Bottom