Riziki mafungu saba: Kijana muuza kashata aliyegeuka mfanyabiashara mwenye mafanikio

Riziki mafungu saba: Kijana muuza kashata aliyegeuka mfanyabiashara mwenye mafanikio

Imeandikwa Usimkatie Tamaa mwanaume anae pumua chochote utokea wakat wowote


Mkuu hawa wanasikiaga basi, yaani wao hua wanaangalia kwa wakati huo unamtongoza unaonekanaje au dinner unaeza mlipia (hata kama umekopa ili kutimiza haja zako)


Ndio maana wale waazima magari, suti na moka wanawanyandua kimasikhara sana then wakijua wanaanza kulia lia.
 
Basi nilimuuliza unaelekea wapi huku wakati ulikuwa unaishi karume? Akanambia alihama Toka mwaka Jana na kwa Sasa amepanga maeneo ya kibugumo huku akiwa anamalizia ujenzi WA nyumba yake iliyopo kisota maweni .

Na hajaoa..

Na mchango WA harusi ametoa tayari ..


Na trehe 13 naolewaaaaaaaa💃💃💃💃

Pole wewe ambaye huna hata mtu wa kukushika mkonoooo umeishiwa kuzalishwaaaaaaaa😁😁 poor you💔😂
Na uache makasiriko😁😁😁

Mwezenu naolewaaaaaa😁😁

Pyeeee 😂😂😂😂💃💃💃🤸🤸🤸
 
Tuma namba ya mchango PM nichangie hata 10 cartons of Kill Water 💦
 
Na trehe 13 naolewaaaaaaaa💃💃💃💃

Pole wewe ambaye huna hata mtu wa kukushika mkonoooo umeishiwa kuzalishwaaaaaaaa😁😁 poor you💔😂
Na uache makasiriko😁😁😁

Mwezenu naolewaaaaaa😁😁

Pyeeee 😂😂😂😂💃💃💃🤸🤸🤸
Hapa unawatambia wanawake wenzio?

Ili iweje?

Kuolewa unaona ni mafanikio makubwa sana kiasi cha kutamba hivi?

Mbona naona binti ambaye bado hajajitambua sawasawa; na kuijua thamani yake? Am I wrong?

Anyway. Ndoa zina changamoto zake; na angalia sana tambo hizi zisije kugeuka shubiri na majuto. Ingia huko ukiwa open minded kwamba unaingia kwenye mapambano.

Naomba ukawe na ndoa njema na iliyobarikiwa...
 
Me mwenyewe nimekupenda maana naona una akili za kujitambua.Kwani una elimu kwa kiwango gani?
 
Mnamo mwaka 2018, kuna kijana mstaarabu sana aliyeishia darasa la tano ambaye nilifahamiana naye kupitia mwalimu mmoja aliyekuwa amepanga nyumbani kwetu. Huyu kijana alikuwa anamletea mwalimu kashata siku za wikendi, hivyo mara nyingi alikuwa ananikuta nyumbani.

Kijana huyu alikuwa na haiba ya ucheshi na alikuwa mchangamfu mno. Baada ya kuendelea kuja pale kwa muda mrefu, tukawa tumezoeana mpaka tukabadilishana namba za simu. Alionekana kunipenda ila hakuwahi kuniambia, na hata kama angeniambia, nisingemkubalia kwa sababu tulipishana sana kielimu na hakuwa na hadhi ya kuwa na mimi.

Baada ya mwaka mmoja kupita, yule mwalimu aliyezoea kuletwa kashata alimpigia simu kijana huyo akihitaji mzigo wa kashata. Kijana yule alimwambia kwamba kwa sasa hawezi kuuza kashata kwani ameacha kazi hiyo na anauza mkaa maeneo ya Buguruni.

Tangu mwaka 2019 mpaka leo, sikuwahi kuwa na mawasiliano naye na sikuwahi kumtafuta licha ya yeye kupoteza namba yangu.

Jioni moja mida ya saa kumi na moja, nikiwa natokea mjini nimekaa kule juu kwenye pantoni nikiwa nawaangalia watu waliokuwa wanazozana chini, nilitupa jicho kwenye gari moja aina ya Toyota Lumion. Nilimuona yule kijana muuza kashata akiwa kwenye usukani. Nilishuka haraka nimuangalie vizuri kama ni yeye. Naam, ni yeye!

Tulishuka kwenye pantoni na akaniambia nimsubiri pahala ani drop nyumbani. Nilishangaa jinsi huyu muuza kashata ameweza kupata mafanikio mpaka kununua gari. Tuliongea mengi sana.

Kijana huyo aliniambia kwamba baada ya kuacha kuuza kashata, alijikita kwenye biashara ya mkaa maeneo ya Buguruni. Kwa sasa ana ofisi za mkaa kama kumi Dar es Salaam na ameajiri watu wengi! Alinambia biashara ya mkaa ina faida sana.

Nimestaajabu!
Sasa uko tayari kuolewa naye kama atakuhitaji? Akili za wanawake za ajabu sana. Unamtaka vya mwanaume siyo mwanaaume mwenyewe.
 
Back
Top Bottom