Road trip update: Dar - Chato - Dar | Kilometa 3,585 | Average Consumption ya 36 km/L, nimetumia Mafuta ya Tsh 460,000/= tu!

Road trip update: Dar - Chato - Dar | Kilometa 3,585 | Average Consumption ya 36 km/L, nimetumia Mafuta ya Tsh 460,000/= tu!

Bajeti kuu ni mafuta, kulala na kula. Vya ziada ni kulewa, Kutembelea vivution, maegesho, kutosha gari, kuonga, nk.

Mi niliweka tight budget ya 120k kwa siku. Kulala isizidi 40k, Kula 40k, na Mafuta 40k angalau.

Kuna sehemu utatumia cheaper, mfano Kuna siku usiku ulinikuta njiani nikaegesha pembeni ya matrafiki nikaamka saa 2 asubuhi.

Kuna sehemu kula cheap, unakuta msosi wa elfu 5 ni mzuri heavy.

Nilikua siendi kulala hotels kubwa, Malala lodge, sili restaurants zenye majina nakula local, natembelea vivution cheap, pia kwenye gari sikosi snacks, maji, na soda ata moja mbili.

Next time nitatafuta Yale madeli ya wauza ice cream.
Nzuri sana, umenihamasisha na mimi kufanya trip kama hiyo siku nikipunguza majukumu
 
Wakuu, kwema.

Mwezi iliopita, September, niliomba ushauri kuhusu hii njia ya Dar - Chato, kwenye Uzi huu: Wazoefu wa hii njia: Nina safari ya Dar - Kahama, sasa Nina Maswali hapa Msaada

Nilipata madini ya kutosha sana, kwenye ishu ya njia ya kupita na nini cha kuavoid. Shukrani.
View attachment 3695263

Kwa kuanza, sijakutana na Elnino Wala mvua ata kidogo katika siku 10 nilizotembea, mikoa zaidi ya 10 na miji ya kutosha.

Siku ya safari, nilianzia Shekilango kituo cha Mafuta Total, nikaset trip A 0 km, average consumption 0 km/L na average speed 0 km/h kwenye gari nilioitumia, Honda Fit.

Barabara ya Dar - Moro ni moja ya barabara za lami mbovu, maviraka, iko busy, maroli, matrafiki, yaani vurugu. Hapa sikia na vituo vingi, nilisimama tu JKT Ruvu (baada tu ya Mlandizi) kupata breakfast, then nikaendelea.

Morogoro hadi Dodoma Ina unafuu kidogo kuliko Moro-Dar, ila hii barabara ni mwendo kibati. Kuna vichaa wengi sana.
View attachment 3695256
Kwahiyo kituo kikubwa cha kupumzuka cha kwanza kikawa Dodoma. Hapo nikapoa kwa siku Mbili. Nikazitumia izo siku kulishangaa jiji la Dodoma ndani nje.

Baada ya hapo nikasogea hadi Manyoni na Itigi. Itigi napakubali sana, kwahiyo break kwa masaa kadhaa. Moja ya kamji poa sana.

Baada ya hapo jioni ilikua imeanza kuingia, mkiki mkiki hadi Tabora. Tabora niliingia usiku sana. Sikulala nikaaondoka nikaenda Nzega then Kahama.

Kwakua Nzega nilipita usiku, kituo kikubwa kikawa Kahama. Huu mji ni una vumbi sijawahi Kuona. Kila barabara inafumuliwa. Pia, nadhani moja ya mji wenye msongamano mkubwa bodaboda. Kuendesha huu mji ni kero.

Niliendelea na safari hadi Chato. Hapo njiani nilipita Kijiji flani Kuna wachimbaji wadogo wadogo, Kuna lodge za mabati, nilisimama kushangaa hapa. Watu wanapiga pesa.
View attachment 3695254
Niliendelea hadi Chato, hapa Nilipata wasaa wa Kutembelea Airport, stand za mabasi na daladala, uwanja wa mpira, fukwe, nk. Ni Mji mzuri sana.

Kutoka Chato, nikaenda Katoro, kisha Geita Mjini. Katoro is overrated kwakweli. Au nilikua na over expectations. Hii miji miwili Ina vumbi pia, ila haifikii Kahama.
View attachment 3695253
Geita, nikaja Mwanza. Ili jiji Lina heshima yake. Niliinjoy.
View attachment 3695261
Mwanza nikapita Shinyanga, Singida then Arusha kisha Moshi. Yes, Shinyanga nilipanda bodaboda za Baiskeli.

Arusha kutoka Singida nilipita barabara mbovu sana, hii ya Singida - Babati. Ilinirudisha consumption na muda.
View attachment 3695251
Nikaja Tanga. Nikastay,nilipanga kwenda Pangani ila nikaambiwa barabara mbovu kipande flani, nitaenda next time. View attachment 3695250View attachment 3695249

Baada ya Tanga nikachomoka hadi Dar, kupitia Bagamoyo road.
View attachment 3695247
Jumla ya Kilometa nilizotembea ni 3,585 hii ni kwasababu kila mkoa/wilaya niliofika nilikua sipiti tu. Naingia ndani kuzurura, au kulala na pia sometimes napark natembea na boda au baiskeli.

Average speed ni ndogo, 34 km/h. Najua ni ndogo, sana, ila me siwezagi mambio.
View attachment 3695248
Consumption ya mafuta average 36 km/L ingeweza kufika 38 km/L ila misele ya mjini imenirudisha nyuma.

Matrafiki wamekula Elfu 15 yangu (Elfu 5 na Elfu 10), kwasababu ya wrong overtake.

Matrafiki wa mikoa yote niliopita hawana shida, ila majamaa wa Pwani na Dar njaa Kali.

Company kubwa ilikua nyimbo, kama unasafiri jitahidi uwe na bank kubwa ya nyimbo, usitegemee za kustream. Njiani mtandao unaweza kua wa shida. View attachment 3695259

Huo ndio mrejesho wangu.

Shukrani za pekee ziende kwa sponsors wa hii safari, wadau wa Mshahara wa Januari vipi mbona unachelewa?

Pamoja.
Maximam speed yako ilikuwa ni ngapi?
 
Hii sasa hainifai mimi. Mimi safari zangu zote za mkoa kwa mkoa haziwi chini ya 120Km/hr, vinginevyo nitachoka kupita kiasi.

Na ninaweza na trip ya 7,000km, atleast twice a year.
Kwa hiyo speed unahitaji gari yenye balance sana. Unatumiaga Sedan, HB au SUV?
 
Vipi kuhusu mafundi wa hizi gari za Honda fit hybrid wapo? Unashauri gari Honda fit ya mwaka gani na iwe na Km ngapi kulingana na hali ya uchumi ya mtanzania wa kawaida.
Kwa sasa me Nina fundi ambae ana handle vingi sana. Kuanzia spare. Na hadi sasa sijakutana na changamoto kuu.

3rd gen kuanzia 2013 unyama, Kuhusu Kilometa, sio ishu.
 
Mkuu hongera sana.

Samahani sijajua kama umeshaongelea kwenye posts zilizopita, vipi kuhusu comfort ya hii Honda Fit hasa kwenye safari ndefu kama hii? Unaweza kuiweka sawa na gari ndogo kama ist kwenye issue ya comfort?​
 
Mkuu hongera sana.

Samahani sijajua kama umeshaongelea kwenye posts zilizopita, vipi kuhusu comfort ya hii Honda Fit hasa kwenye safari ndefu kama hii? Unaweza kuiweka sawa na gari ndogo kama ist kwenye issue ya comfort?​
Sijawahi ata ulizwa mkuu.

Comfortability ukifananisha na Magari yenye wheelbase ndefu, hii haipo poa. Ni "firm/ngumu" ila ukifananisha na grade zake kama IST (huyu kaachwa mbali sana), Vitz, Demio nk, Hawa hawamkuti.

Labda ukidaka Honda Fit Hybrid Sport ndio yenyewe iko firm kama IST.

Kuhusu seat, ziko comfortable kwa safari ndefu, hautajisikia uchovu sana. Zinajitahidi kwa grade yake.
 

Attachments

  • Screenshot_20261023-224103.png
    Screenshot_20261023-224103.png
    700.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom