Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
maamuzi ya Mugabe yalikuwa na nia njema tu lakini kwakuwa aligusa maslahi ya wazungu basi wamemkomoa kwa kumuwekea vikwazo lukuki,hata kama wazawa wangeweza kuendeleza hayo mashamba wangeuza wapi?wakati wamewekewa vikwazo?nikitafakari jinsi LIBYA ilivyosambaratika naona hakuna nchi ya AFRIKA hata moja itakuja kuwa nchi tajiri na kuwa moja kati ya nchi zilizoendelea hata kuwe na rasilimali za kila aina.Maamuzi yanayoongozwa na chuki, visasi au kutafuta umaarufu wa kisiasa bila hesabu za kisayansi ni mauti!. Kama ni kweli naona mzee anaanza kuzaliwa upya kwa maisha mapya!
maamuzi ya Mugabe yalikuwa na nia njema tu lakini kwakuwa aligusa maslahi ya wazungu basi wamemkomoa kwa kumuwekea vikwazo lukuki,hata kama wazawa wangeweza kuendeleza hayo mashamba wangeuza wapi?wakati wamewekewa vikwazo?nikitafakari jinsi LIBYA ilivyosambaratika naona hakuna nchi ya AFRIKA hata moja itakuja kuwa nchi tajiri na kuwa moja kati ya nchi zilizoendelea hata kuwe na rasilimali za kila aina.
Wazungu wanaendelea kututawala kwa kigezo cha demokrasia,demokrasia siku zote inawagawa watu,siku zote kwenye demokrasia watu hawawi wamoja.Gadafi alikuwa na ubaya wake lakini kungangania madaraka haikuwa tatizo,tatizo alikuwa anatishia maslahi ya wazungu kwa kutaka AFRIKA iungane kuwe na kitu kama UNITED STATE OF AFRICA hiyo ajenda ndio iliomuua sio kitu kingine.Libya ni ushenzi wa Gadafi kung'ang'ania madaraka na wala siyo suala la nini. Ni ujinga wa viongozi kudhani uraisi ni utemi.
Mugabe alipashwa kuzijua hizo hesabu kabla hajatwanga maji. Leo hii Zanzibar watu wakianza kufa na njaa mtalaumu Wazungu? Kila maamuzi yanagharama. Zingatia uwezo wa kufika bei kabla hujatoa order.
Libya ni ushenzi wa Gadafi kung'ang'ania madaraka na wala hakuna uchawi. Hivi kama angelikuwa anatawala Libya kwa ajili ya wananchi, ni kwa nini hakukubali kufanya demokrasia? Kama angelikubali kuongoza nchi kwa utashi wa wananchi wake, kwa maana ya kufanya uchaguzi wananchi wachague raisi wanayemtaka kwa wakati walipotaka, nayeye akabaki na heshima ya uraisi mstaafu akishuhudia na kushauri mwendelezo wa Libya, yangemkuta yaliyomfika? Walibya Wangeuana? Alidhani ataishi milele? Lazima kufa angelikufa kwa namna yoyote. Je baada ya kufa kwake, Waliby awasingegombana kama ilivyoleo? Kiongozi mzuri ni yule anayetawala na kuliangalia taifa kwa vizazi vijavyo na hivyo kuandaa mfumo sahihi wa maendeleo ya uma na si yale ya faimilia au kundi dogo analotaka yeye kinyume na wenye nchi.
Ni ujinga wa viongozi kudhani uraisi ni utemi.
Mugabe alipashwa kuzijua hizo hesabu kabla hajatwanga maji. . Mugabe siyo Zimbabwe. Kama maamuzi yake yalikuw ani kwa ajili ya Wazimbabwe, kwa nini kung'anng'ani madaraka na kuua watu kwa sana eti wanampiga?
Leo hii Zanzibar watu wakianza kufa na njaa mtalaumu Wazungu? Kila maamuzi yanagharama. Zingatia uwezo wa kufika bei kabla hujatoa order. Makeke bila nguvu ni upumbavu na fedheha!. Sasa yako wapi?
Zilikuwapo njia nyingi sana za kufanya uchumi shirikishi Zimbabwe ambazo kila upande ungenufaika na hatimaye kujenga uwezo mkubwa kwa wazawa zaidi ya ubabe wa kijinga ambao haujalipeleka taifa mahala popote. Na ndiyo sababu haka kazee hakataki kuachia nchi kwa hofu ya hasira za Wazimbabwe kalikowaua kwa kisingizio cha kuwalinda.
Ulivyo na akili fupi mbona museven hawamtoi? Mda mwingine weka chuki zako pembeni ueleze ukweli
ukiiangalia ZIMBABWE hata leo hii pamoja na vikwazo vyote walivyowekewa huwezi kuifananisha na Tanzania,sisi tuna hali duni zaidi kuliko ZIMBABWE.Na bado ! huyu mzee chuki zake za kishamba zimesababisha zimbabwe irudi nyuma zaidi ya marehemu , maandiko matakatifu yanasema iko siku tutakuja kuonana na marehemu wetu .
usicheze na wazungu mkuu , wanaweza kuhamisha samaki wote kwenye bahari upande wa zanzibar na kuwapeleka mombasa na kukausha mikarafuu yote .Hahahaha poor Mugabe.....bado na Shein atawapigia magoti ngoja wakaze kamba kidogo tu utaona anavyohemea kooni