DAR si LAMU
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 2,928
- 551
...Kamuulize Mwingereza, Mfaransa na Mwitaliano kama walikuwa hawafaidiki na Libya. Hamna nchi duniani inayojitosheleza kwa kila kitu!Tukirudi kwenye mada nchi kama LIBYA wazungu walikuwa hawanufaiki nayo kwasababu walikuwa wanajitosheleza kwa kilakitu na zaidi GADDAFI akataka kuiunganisha AFRIKA jambo ambalo lilishashindwa huko nyuma kwasababu waafrika ni wabinafsi.
...Hakuna nchi ya Afrika itakaa kuunganisha raslimali. Single visa imetushinda hapa EAC. Nations have competing agendas!GADDAFI alijaribu kuwafanya waarabu wanaozalisha mafuta waungane ili wawe na sauti akasahau kuwa kuna vibaraka wa wazungu hata uarabuni ndio akaja na wazo hilo AFRIKA akiwa na maana nchi moja moja bila kujiunga tukaunganisha rasilimali tulizonazo haziwezi kujikomboa.
...Hapa nchini kuna maeneo yana njaa, wakati mengine chakula kinaharibika. Ni issue ya demand and supply, miundombinu, pamoja na sera.Tulitakiwa tuunganishe nguvu tuwe kitu kimoja,uchumi wa nchi zilizoendelea unahitaji sana rasilimali zilizopo afrika ambapo wanaichukua kwa bei ya kutupa kupitia sera zao wanazotulazimishia kama ubinafsishaji,uwekezaji n,k lakini tungejiunga tungejikuta kwanza tunajitosheleza wenyewe kwamba kuna nchi zina njaa wakati zingine mazao yanaozea shambani,tungeanzisha viwanda kwa kutegemea malighafi zinazopatikana hapahapa AFRIKA,vitu ambavyo hatuna kwa umoja wetu tungevipata hata kwa kuagiza toka nje ya afrika au kuleta wataalamu wakatengeneza hapahapa.
...Huwezi ukaamini, lakini, sera tu pekee, zinawezafanya sehemu moja chakula kikaoza wakati kwengine wanashinda njaa. Unakumbuka, vipindi ambavyo huwa ni marufuku kuuza chakula nje?
...Demokrasia haitumiki kumuweka kibaraka. Uzoefu unaonyesha waliowahi kuitwa vibaraka, hawakutawala kwa kufuata mfumo wa demokrasia. Mobutu, Banda, Omar Bongo na wengine waliitwa vibaraka.lakini haya yote yanashindikana kwasababu kwa kutumia demokrasia wazungu wanaamua nani wamuweke madarakani atakayewahakikishia maslahi yao hayatatetereka na anayeenda kinyume nao kwa vyovyote vile watamtoa.yapo mambo mengi sana ya kuyatafakari ambayo lazima tufikirishe akili zetu ili kuelewa kwanini wazungu hawakumtaka GADDAFI wala hawamtaki MUGABE.
...Mengi ya matatizo yanayoihusu Afrika hayasababishwi na wazungu, bali sisi wenyewe!