Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Kama walimshindwa Caesar Manzoki kutoka Vipers kwa dau la kawaida kabisa mwaka wa jana, ndiyo wawe na uwezo wa kumsajili Stephane Aziz Kii kutoka Yanga!Kuna siri moja Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amewaachia Simba.
Kwenye ripoti yake aliyoacha amemwambia Mohammed Dewji ‘Mo’ amng’oe Aziz Ki pale Yanga.
Amekiri kumwambia mchezaji huyo ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni Yanga ni mashine na kila alipokuwa akikutana nae alikuwa roho mkononi.
“Nilimpendekeza Aziz kwa kuwa tayari yuko Tanzania ameshaanza kuzoea mazingira mazuri ni tofauti na mchezaji mpya anayefika kuja kuanza kuzoea mazingira ya hapo,” amefunguka kocha huyo.
Robertinho amesema kama angeambiwa staa mmoja wa haraka kumchukua ndani ya kikosi cha mabingwa hao basi angekuwa Aziz Ki pekee na kama kuna bahati kubwa kwa watani wao ni kuwa na mchezaji bora kama raia huyo wa Burkina Faso.
Source. MwanasportsView attachment 2815445
Na kama wana ndoto za kumsajili mwishoni mwa msimu eti "baada ya kumaliza mkataba wake"!! Ndiyo wasahau kabisa. Maana huyo Aziz Kii siyo mbumbumbu wa kutoka timu kama Yanga, na kwenda timu ya tia maji tia maji kama simba.